Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 65 | 66 | (Page 67) | 68 | 69 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Gairo,mkoa wa Morogoro kwenye mkutano wake wa ku maliza ziara yake wilayani  humo,uliofanyika uwanja wa Shule ya msingi Gairo jioni ya leo.

  Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Gairo,mkoa wa Morogoro kwenye mkutano wa kumaliza ziara wilayani humo,uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Gairo.

   Wazee wa Gairo wakimpa zawadi ya silaha za jadi Ndugu Kinana kabla ya kufanya mkutano wake wa hadhara jioni ya leo kwenye uwanja wa shule msingi Gairo,wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
   Ndugu Kinana akijaribu silaha ya jadi aliyokadbidhiwa na wazee wa Gairo.

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Chakwale,wilaya ya Gairo mapema leo mchana,alipokuwa akizindua shina jipya la wakereketwa wa chama hicho.katika uzinduzi huo Kinana aliwaasa  na kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kijitegemea badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu ikiwemo na suala la kuwapa ajira.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwapa kifuta jasho baadhi ya wazee-waasisi wa chama cha CCM,kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa shina jipya la kata yao ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema leo mchana.Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM wako ndani ya Wilaya ya Gairo katika ziara ya kuimarisha chama cha CCM mkoani Morogoro sambamba na kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.
  Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo mbele ya wakazi wa Chakwale mara baada ya shina la kata hiyo kuzinduliwa mapema leo mchana,ndani ya wilaya ya Gairo.
  Baadhi ya Wazee waasisi ndani ya CCM-Kata ya Chakwale wakionesha kadi zao za chama cha CCM walizonazo tangu kuanzishwa kwa chama hicho,kwenye shughuli fupi ya kuzindua shina la kata hiyo.
  Kijana aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA akiwa ameinyanyua kadi ya chama chake cha awali,na kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM,akiwa kama mwanachama mpya wa chama hicho cha CCM


  Baadhi ya Vijana wakiwa kwenye ajira ya kujitegemea,kama waonekanavyo pichani wakitumia mashine aina ya Trekta kupukuchua mahindi
  Baadhu ya wanachama wapya waliojiunga na chama cha CCM wakionnyesha kadi zao chama,mara baada ya shina la kata ya Kibedya kufunguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana,mapema leo wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
  Mbunge wa Jimbo la Gairo,Mh.Shabiby akizungumza jambo na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye ndani ya kata ya Kibedya,wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
  Mbunge wa Jimbo la Gairo,Mh.Shabib akifafanua jambo mbele ya wakati wa kata ya Kibedya mapema leo ndani ya wilaya ya Gairo.
  Baadhi ya wakazi wa Kata ya Chakwale,wakielekea kushuhudia uzinduzi wa shina jipya la kata hiyo..
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa mmoja wa wazee wa kata ya Chakwale,Mzee YohanaChibuya.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said sadiq akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.


  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.


  Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasibu Abdul Juma (Diamond) akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Taratibu za Mazishi zikiendelea.

  jeneza lenye mwili wa Msanii Mkongwe wa Muziki wa Mwambao (taarab) hapa nchini,Marehemu Fatma Bint Baraka (Bi Kidude) likitolewa katika msikiti wa Mwembeshauri aliposaliwa mchana wa leo,tayari kwa kwenda kwenye Mazishi.

  0 0

   Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib (kulia)'Diamond Plutnum', akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao  Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.

  0 0  0 0


  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM kwenye uwanja a shule ya Msingi Gairo B, mjini Gairo mkoani Morogoro leo hii.

  ==========  ========  ========

  NA BASHIR NKOROMO, GAIRO.


   CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi na uvunjifu wa amani yanayoanza kushamiri bungeni  na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi waliowachagua.


   Hayo yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Gairo mkoani hapa, Aprili 18, 2013, ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.


   ” Mambo haya yanayofanywa na wabunge  kama ilivyotokea jana (juzi), ni dhihaka inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi waliowachagua. Baadhi ya wabunge wanafanya vituko hivi huku wakiwa wanatambua wazi kwamba heshima waliyopewa ni kwenda bungeni kujadili matatizo ya wananchi ambayo ni mengi kama migogoro ya ardhi. Hili tukio la jana ni  aibu ya mwaka”, alisema Nape.


   Alisema, muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa kuutumia wote kwa hekima busara na uwezo wao wote kujadili namna ya kuwezesha Watanzania kufikia maisha bora na siyo kuutumia muda huo kujadili tofauti zao za kisiasa au namna ya kutekeleza malengo yao binafsi ya vyama vyao.


   ”Hatua hii ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha tafrani na kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi ni ya hatari sana, hivyo wananchi wanapswa kujifunza kwamba hawa siyo watu wa kuwapa madaraka. Tazama hivi sasa bungeni wapo wachache sasa wananchi wakihadaika wakawachagua na kuwa wengi bungeni patakuwaje? Hili ni fundisho tosha”. alisema Nape.


   Alisema, hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema kulijadili suala la Mkurugenzi wa Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku wakijua kwamba ni suala ambalo lipo mahakamani, ni la kujaribu kuingilia uhuru wa mahakama kwa makusudi ili ifikie mahala mahakama itupilia mbali kesi hiyo kwa kigezo cha kuinngiliwa uhuru wake.


   ”Haya ni matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa na viongozi wao ikiwemo kuingilia uhuru wa mahakama, ili hatimaye ionekane uhuru wa mahakama umengiliwa kuhusiana na kesi hiyo na hatimaye itupiliwe mbali. Kila mwenye akili anajua kwamba  huu ni mkakati malum wa Chadema”, alisema Nape.


   Mbali na kukizungumzia bungeni suala ya Lwakatare, Chadema wamekuwa wakilisema pia mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi karibu ya Mbunge wa Singida, Tuntu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo na kwamba mbali na kutafuta kesi hiyo itupwe pia ni juhudi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama.   ”Inashangaza sana,  Lisu badala ya kutoa ushahidi wake mahakamani kuhusu suala hili anakwenda kujzungumza na wandishi wa habari ili hali anafahamu wazi kwamba kesi kuhusiana na suala hilo ipi mahakamani, tafsiri yake ni kwamba ni juhufdi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama au kushawishi mahakama kutupilia mbali kesi kwa kigezo kwamna imeingiliwa uhuru wake”, alisema na kuongeza:.


   ”Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe) pia wakati akizungumza Bungeni alitumia muda mrefu kuzungumzia suala la Lwakatare lililopo mahakamani. leo mahakama ionekane uhuru wake umeingiliwa iitupe kesi, na hata wakati wa kuchangia bajeti ya Utumishi, upande wa Chadema badala ya kuzungumzia sekta ya utumishi wa umma kurasa nne nzima zilihusu mambo ya Lwakatare”, huu ni mkakati mbaya sana  unaolenga haki isitendeke kuhusu kesi hiyo.


   Akizungumzia hatua ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutamka bungeni kwamba CCM Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete na Chama Chake  cha CCM ndiyo chanzo cha udini, aling’aka kwamba ni kauli inayotia shaka uelewa wa mambo wa mbunge huyo.


   ”Nina mashaka kama Lema ni mzima kiakili, CCM italetaje udini wakati ndiyo imeleta umoja na mshikamano kwa makabila zaidi ya 24 ya Tanzania kiasi kwamba amani na utulivu vimeshamiri? Yaani CCM ihangaike kujenga mshikamano halafu hiyo hiyo ione kicefuchefu kuilinda na kuanza kuihujumu? huu ni upuuzi wa hali ya juu sana”, alisema Nape.


   Nape alisema, vituko vyote vinavyoendelezwa na Chadema Bungeni na kwingineko ni dalili tisha kwamba wanaendelea kutekeleza ahadi waliyotangaza siku nyingi kwamba nchi haitatawalika.


   Mkutano huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana inayoendelea mkoani Morogoro, ambapo pamoja na Nape, Kinana anafuatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Seif Khatib. Ni ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani humo.  0 0  0 0  Baada ya kimya kingi katika fani ya muziki, nimeamua kuirudia fani yangu na kutoka na miondoko ya kiafrica. Kibao cha kwanza nilichoamua kuanza nacho kinaitwa "Utu uzima dawa" ft Dunga kilichoandikwa na mimi pamoja na Richie Mavoko. Na ku produciwa na Lamar wa fishcrab. 


  0 0

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga (kushoto) akikabidhiwa Kitabu chenye maelekezo mbali mbali ya Usalama Barabarani na Maneja wa Kampuni ya PUMA – Mr. Philippe Corsaletti (kulia). Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa PUMA tarehe 18/04/2013 ambapo vilikabidhiwa vitabu 4,800.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga” (kushoto) akionyesha Kitabu cha Usalama Barabarani kwa baada ya kukabidhiwa na Maneja wa Kampuni ya PUMA – Mr. Philippe Corsaletti” (kulia). Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa PUMA tarehe 18/04/2013 ambapo vilikabidhiwa vitabu 4,800.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga” na ‘’Maneja wa Kampuni ya PUMA – Mr. Philippe Corsaletti” wakijadiliana jambo wakati wa makabidhiano ya Kitabu cha Usalama Barabarani. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa PUMA tarehe 18/04/2013.
  Maneja wa Kampuni ya PUMA – Mr. Philippe Corsaletti” (katikati) akielezea mambo muhimu jinsi Kampuni yake ya PUMA itakavyokuwa inashirikiana na jeshi la Polisi katika kupambana na Ajali za Barabarani kwa vitendo. Maneja huyo alitoa maelezo hayo mbele ya Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wa makabidhiano ya Kitabu cha Usalama Barabarani. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa PUMA tarehe 18/04/2013.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga” na ‘’Maneja wa Kampuni ya PUMA – Mr. Philippe Corsaletti” wakiwa katika picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa PUMA , Maafisa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wa makabidhiano ya Kitabu cha Usalama Barabarani Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa PUMA tarehe 18/04/2013.

  0 0
 • 04/19/13--01:32: wakubwa kazini.!


 • 0 0


  Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka wilayani kasulu mkoani Kigoma,Chanzo chetu cha habari kutoka mkoani humo kinaeleza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Dani Mkanga amepata ajali mbaya eneo la Nyakanazi akielekea Mwanza na dereva wake amefariki hapo hapo.Tutazidi kupeana taarifa kadiri ya zitakavyokuwa zikiendelea kuingia.

  0 0

   Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingigwa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wapiga katika semina ya upigaji picha iliyofanyika jijini Dar Es Salaam, akifuatiwa ni Afisa uhusisano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki na Muhadhiri wa Chuo Kikuu Richard Ndunguru.
  Waandishi wa habari waliohudhuria semina ya ya upigaji picha  iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.
  =======  ======  =======
  ·       Airtel Money Yaendeleza udhamini wake katika  semina ya wapiga picha wa vyombo vya habari 15.

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya kibebki ya  Airtel Money kwa mara ya pili imedhamini semina ya wapiga picha wanahabari inayofanyika kwa muda wa siku mbili hapa jijini Da r Es Salaam kuanzia leo 18 hadi 19 Apili 2012.

  Airtel kupitia  huduma yake ya Airtel Money imedhamini kampuni ya  jijini Dar es salaam ijulikanayo kama MP5 2011 entertainment kuandaa semina maalum itakayowakutanisha wataalam na wapiga picha za habari wa muda mrefu kukutana na wanahabari wapiga picha ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi zao.

  Akiongea kwa niaba ya waandishi wapiga picha waliohudhuria semina hiyo Bw, Selemani Mpochi mpiga picha wa muda mrefu nchini alisema “hii ni sehemu muhimu sana kwetu wanahabari kujitengenezea utaratibu wakukaa pamoja na kutafakari mambo muhimu ili kuendelea kufanya kazi zetu kwa ufanisi.

  Kwa niaba ya wenzangu wote tunawashukuru sana Airtel kupitia huduma yao ya Airtel Money kwa kutudhamini katika semina hii kwa mara ya pili sasa, tunashukuru sana kwa ushirikiano wao wa kuwa tayari kutusaidia kuendeleza taaluma yetu na kuonyesha kuwa wanatambua umuhimu wa wanahabari ncini.

  Airtel inaendelea kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi  kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hivyo semina hii ni njia nyingine itakayoweza kuinua kiwango cha mapato na uelewa wa Airtel Money kwa waandishi wa habari nchini.

  Zaidi ya wapiga picha za habari wapatao 15 toka vyombo vya habari nchini wanatarajiwa kuhudhuria semina hiyo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa msimbazi center.

  0 0


  CALAPY ENTERTAINMENT
  Contact: P.O.BOX 38457, Dar es Salaam. Tel: +255713216676,+255787216676+255656666676, email: majutoy2k@yahoo.co.uk,omajuto@gmail.com
  FOMU KUOMBA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MISS SINZA 2013
  SIFA ZA MSHIRIKI:
  ·         Awe na umri kuanzia miaka 18 mpaka 23
  ·         Awe raia wa Tanzania ambaye hajaolewa wala kuzaa
  ·         Awe na uwezo ufahamu wa kutosha kujieleza na hasiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari
  ·         Hasiwe ameshiriki mashindano yaliyochini ya Kamati ya Miss Tanzania mwaka 2012. (Maana yake hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja)
  Jina Kamili na Umri___________________________________________________________
  Tarehe ya kuzaliwa____________________________________________________________
  Kazi unaypifanya______________________________________________________________
  Anuani______________________________ simu ya mkononi_________________________
  Simu za dharula_______________________________________________________________
  Lugha unazoweza kuongea___________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
  Lugha utakayotumiwa wakati wa mashindano_________________________________________
  Kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na taratibu za mashindano haya ya Miss Tanzania, baada ya kutoa maelezo haya, kampuni itaingia mkataba na wewe ili uweze kujua haki zako wajibu wako katika mashindano haya.
   
  Sahihi ya Mshiriki____________________
  Mshiriki anaweza kudownload fomu hiyo na kuituma kwa email: majutoy2k@yahoo.co.uk, au omajuto@gmail.com. pia anaweza kutuma details zake kwa njia ya sms kwa namba za simu zilizopo hapo juu ya fomu.
  Kwa kifupi, mazoezi yataanza April 26 kwenye ukumbi wa Meeda Sinza Mori au Lufungila

  0 0

   Ujumbe wa Kampuni ya Bia Tanzania unaoongozwa na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (pili kulia) ukiingia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Mapema leo asubuhi kwa kuhudhuria Mkutano wa 11 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wengine pichani toka kulia ni Mratibu wa Ziara ya Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager,Innocent Melleck,Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania,Phocas Laswai,Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe,Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Mashariki,James Bokela pamoja na Meneja Mauzo wa TBL,Kanda ya Kati,Julius Ngaga.Ujumbe huu upo mjini Dodoma kwa azili ya kupata Baraka za wabunge na uzinduzi rasmi wa Ziara ya Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager,ambapo jioni ya leo kutakuwa na tafrija fupi ya kupongeza ushindi huo itakayofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  Wakijadiliana jambo kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Bunge ili kufatilia shunghuli mbali mbali zinazoendeshwa na Bunge.
  Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge kufatilia shunghuli mbali mbali zinazoendeshwa na Bunge.

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhaman Kinana akizungumza na Wakulima wa Miwa sambamba na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa,kwenye mkutano wao uliofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Honolulu,Tuliani wilayani Mvomero,Morogoro.Mkutano huo umefanyika kufuatia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero  mkoani Morogoro kukishitaki Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuwa kimekuwa kikifanya dhuluma kubwa zidi ya wakulima wa miwa huku wakimuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kufanya kila analoweza kuhakikisha mgogoro uliopo kati ya pande hizo mbili unapatiwa ufumbuzi. Aidha chama cha CCM kimetoa maelekezo ya kukukutana na Wakulima hao pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa siku ya jumatatu,kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya wakulima wa miwa na uongozi wa Kiwanda cha sukari Mtibwa kuhusiana na Mgogoro wao mkubwa uliodumu takribani kwa miaka 10 sasa,aidha Uongozi wa CCM umesikiliza pande zote mbili (Wakulima wa miwa & Uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa) na kuamua kukukutana na Wakulima hao pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa siku ya jumatatu,kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.
  Baadhi ya Wakulima wa Kiwanda cha sukari Mtibwa na Uongozi wa Kiwanda hicho wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wao na Uongozi wa juu wa CCM,mapema leo uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Honolulu,Tuliani Wilayani Mvomero .
  Mmoja wa Wakulima wa Miwa kutoka kiwanda cha sukari Mtibwa,Mzee Pascal akizungumzia tuhuma na dhuluma mbalimbali wanazofanyiwa na uongozi wa Kiwanda hicho,Aidha Mzee Pascal alisema kuwa wakulima wa miwa wamekuwa na mgogoro na kiwanda hicho uliodumu kwa miaka 10 sasa,lakini kwa bahati mbaya hakuna majibu ya suluhu hali inayofanya wananchi wajiulize maswali bila majibu. Mzee Pascal aliyataja baadhi ya matatizo makubwa yanayofanywa na kiwanda cha Mtibwa kuwa ni kucheleweshwa kwa malipo ya miwa, kiwango kidogo cha malipo pindi wanapopeleka mazao yao kuuza kiwandani, madeni sugu kwa wasataafu wa kiwanda lakini kubwa zaidi wanadai kuna dhuluma ambayo imekuwa ikifanywa na uongozi wa kiwanda hicho.  
  Mmoja wa Wastaafu wa Kiwanda cha sukari Mtibwa,akikishitaki kiwanda hicho mbele ya Uongozi Mkuu wa CCM,kuhusiana na malimbikizo ya mafao ya PPF,ambayo yamekuwa yakileta mgogoro mkubwa kati yao kutokana na kutolipwa kwa wastaafu hao.
  Mwenyekiti wa halmashauri Wilaya ya Mvomero ,Bwa.Jonas Van Zeiland akizungumza mbele ya Uongozi wa CCM,chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana uliofika Tuliani,Wilayani Mvomero  uliofika kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa Changamoto/Mgogoro uliopo kati ya Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa na wakulima wa Miwa.
  Meneja wa kanda ya Mvomero-PPF,Bwa.John Mwalisu akitoa ufafanuzi mbele ya wakulima wa Miwa-Mtibwa,kuhusiana na malimbikizo yao ya mafao ya Kustaafu kutoka kwa Mwekezaji wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa, kwamba Kiwanda hicho kimekuwa kikishindwa kuwalipa wastaafu mafao yao na hata wakienda mahakamani wanashangaa wanashindwa kesi na mwekezaji kuibuka mshindi hata katika kesi zao za msingi za madai.

  Mratibu kutoka Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa,Bwa.Hamad yahaya akijibu tuhuma  na dhuluma mbalimbali zilizoelekezwa kwa mwekezaji wa Kiwanda hicho pamoja na uongozi mzima kutoka kwa Wakulima wa MiwaKufuatia tuhuma hizo wakulima wa miwa na wawakilishi wao walimwambia Kinana aliyeambatana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, walisema mgogoro umedumu kwa miaka 10 lakini kwa bahati mbaya hakuna majibu ya suluhu hali inayofanya wananchi wajiulize maswali bila majibu.Aidha uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa umeweka wazi kuwa kinatambua baadhi ya changamoto zilizopo baina yao na wakulima na kwamba sasa ni wakati wa kutafuta ufumbuzi wake na kuanza ukurasa mpya lakini pia wakaomba CCM kuiomba Serikali kuangalia wawekezaji wa ndani kwani kuna sukari inayotoka nje na kufanya wakose fedha.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa,Nassor Seif mara baada ya mkutano na Wakulima wa Miwa,Uongozi wa Kiwanda hicho pamoja na Uongozi wa juu wa CCM kukutana kwa pamoja na kusikiliza matatizo yaliyomo,uliofanyika mapema leo mchana kwenye ukumbi wa hotel ya Honolulu,Tuliani wilayani Mvomero,Morogoro.Mkutano huo umefanyika kufuatia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero  mkoani Morogoro kukishitaki Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuwa kimekuwa kikifanya dhuluma kubwa zidi ya wakulima wa miwa huku wakimuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kufanya kila analoweza kuhakikisha mgogoro uliopo kati ya pande hizo mbili unapatiwa ufumbuzi. 

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda la Uturuki (TUSKON) Bw. Rizanur Meral na ujumbe wake leo April 19, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazungumzo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose aliyemtembelea leo April 19, 2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Uingereza (DFID) nchini Bw. Elliot Marshall aliyeongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose (katikati) aliyemtembelea leo April 19, 2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. PICHA NA IKULU

  0 0  0 0

  Kituo cha Bomba Fm Mbeya kimetangza ajira moja katika kituo hicho, ambapo mmoja kati ya watu watakao kuwa wakiwania nafasi hiyo ya ajira watashindana moja kwa moja kupitia vipindi viwili.

  Akitangaza nafasi hiyo wakati wa kipindi cha Kali za Bomba kinachorushwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 7 ya mchana hadi saa 10 ya jioni, Meneja Mkuu wa Kituo hicho FREDY HELBERT amesema licha ya ajira hiyo kutolewa kupitia mashindano bado vigezo na taratibu za kazi zitazingatiwa.

  Mshindi wa mashindano atapatikana kwa ushirikiano mkubwa kati yake na wasilikilizaji ambao ndio watakuwa majaji wakuu……

  VIGEZO vya mshiriki:-
  1. Awe na umri wa kuanzia miaka 18.
  2. Awe raia wa Tanzania.
  3. Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha nne.
  4. Awe hana mkataba wowote na kampuni yoyote ile.
  5. Awe hajawahi kufungwa jela au kushitakiwa na kosa lolote.
  6. Awe na akili timamu.

  Fomu ya ushiriki ni shilingi 10,000/= tu ya Kitanzania.

  Kwa Waliopo nje ya Mbeya maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia simu ya mkononi.+255764 240 440

  0 0


  Bendi ya maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" imepokea kwa udhuni na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mwanamuziki mkongwe barani afrika hayati Bibi.Fatuma binti Baraka (Bi.KIDUDE) mwenyezi amrehemu.

  Ngoma Africa band inatoa mkono wa pole na rambi rambi kwa familia ya marehemu Bi.Kidude,pia kwa sisi sote wanamuziki na wasanii  pamoja na watanzania wote kuondokewa na Mkongwe wetu Bi.Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude),ambaye alikuwa ni balozi na hadhina ya utamaduni wa mwambao na waswahili, kitaifa na kimataifa.

  Marehem Bi.Kidude hakuwa msanii au mwanamuziki tu bali alikuwa mpiganaji jemedari aliyeupigania na kuulinda utamaduni wa jadi ya kiswahili na mwambao.

  Bendi ya Ngoma Africa inaungana na watanzania wote wa ndani na nje ya nchi katika kuomboleza msiba huu wa mkongwe wa sanaa barani barani Afrika hayati Bibi. Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude) .

  Ngoma Africa band itasimamisha shuguli za kutumbuiza kwa mda wa siku 10
  kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa marehemu Bi.Kidude.
  Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi Bibi.Fatima binti Baraka (Bi.Kidude).
  Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema PEPONI Bi.Kidude


older | 1 | .... | 65 | 66 | (Page 67) | 68 | 69 | .... | 1898 | newer