Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49613 articles
Browse latest View live

MGOMBEA URAIS WA CCM DKT MAGUFULI APIGA KURA JIMBONI KWAKE CHATO

$
0
0
 Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kupiga kura huko kijijini kwake Chato mkoani Geita leo
  Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga kura yake
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli akikunja vizuri karatasi baada ya kupiga kura yake jimboni kwake Chato mapema leo asubuhi Oktoba 25, 2015.


MTONI KIJICHI, MBAGALA WENGI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KWA UTULIVU NA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rukia Omari (kushoto), akimsaidia kupiga kura jamaa yake Mwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho wakati wa kupiga kura katika kituo cha Mbagala Misheni Dar es Salaam leo asubuhi.
  Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shimbwe Mbagala Kuu.
 Hapa wakihakiki majina yao.
 Mkazi wa Njia ya Ng'ombe Mbagala Kuu, Sarah Simba akipiga kura katika kituo cha Shimbwe Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wake, Rais, Mbiunge na Diwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mbagala Kuu.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bwawani Mtoni Kijichi leo asubuhi.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.

 Wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Mbagala Misheni wakiwa kazini.
Msimamizi wa uchaguzi Mkuu katika kituo cha Mbagala Misheni, Yona Komba (kulia), akimpaka winoMwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho baada ya kumaliza kupiga kura katika kituo hicho Dar es Salaam  leo asubuhi. Kushoto ni binti aliyemuomba amsaidie kupiga kura  Rukia Said.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

WANANCHI WA NGORONGORO WANAKABILIWA NA UHABA WA MAJI

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha Naiyobi wilaya ya Ngorongoro wakichota maji ambayo hutumia na mifugo kijiji hicho kinakabiliwa na uhaba wa maji

Na Woinde Shizza,Arusha
WANANCHI wa Kijiji cha Nayobi  kilichopo tarafa ya Ngorongoro wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha wamelalamikia kero ya uhaba wa maji
inayowasababishia kukesha kwenye bomba la kijiji kwa takribani siku tatu
wakisubiri maji jambo linalopelekea shughuli za kijamii na kiuchumi
kusimama kwa muda mrefu na kinamama kutembea umbali mrefu wakitafuta huduma hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakiteseka kupata huduma za maji huku kinamama wajawazito wakijifungulia bombani apo baada ya kukaa kwa muda wakitafuta maji huku wengine wakilazimika kukesha na watoto wadogo.

Wanakijiji Daniel Sereki  na  Rehema Laizer  na wamesema kuwa kwa sasa
wanakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa maji pamoja na chakula na hata
pale wanapopata chakula hukosa maji ya kupikia chakula hicho na kuziacha
familia zao zikitaabika kwa njaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Naiyobi  Meleji  Sikoni amesema kuwa kwa muda wa miaka 20 wamekua wakikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji hivyo ameiomba serikali na mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  iwasaidie kutatua tatizo hilo sugu linalowaathiri  wananchi wengi.

Mgombea Ubunge Jimbo la Ngorongoro Wiliam Olenasha  ameeeleza kisikitishwa na wananchi wanaoteseka kwa kero ya maji ambayo hushirikiana na mifugo katika matumizi yake hivyo ameaidi kutatua kero hiyo pindi atakapopata ridhaa ya kuongoza wilaya hiyo.

Wilaya ya Ngorongoro inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji pamoja na chakula hasa katika kipindi hiki cha kiangazi ,juhudi zinahitajika kwa upande wa serikali na Mamlaka ya Ngorongoro ili kuweza kuwanusuru wananchi na baa la njaa pamoja na uhaba wa maji.

WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA MAENEO MBALIMBALI YA KATA YA KIJITONYAMA JIJINI DAR

$
0
0
 
Wasimamizi wa uchaguzi wakiendelea kuwahudumia wananchi waliofika katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar kwa ajili ya kupiga kura.Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog
Mmoja wa wazee akisaidiwa na mtu wake wa karibu ili kupiga kura katika kituo cha Chuo cha Ustawi wa Jamii  jijini Dar leo

Mlemavu akisaidiwa na mtu wa karibu alipofika katika kituo cha Kenton kwa ajili ya kupiga kura.
Mmoja wa wananchi akiwa kwenye sehemu ya kupigia kura katika kituo cha kupigia kura kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar.
Wananchi wakihakiki majina yao katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
 Wananchi  wakibadishana mawazo walipokuwa kwenye foleni wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
 Wananchi wakihakiki majina yao katika kituo cha Shule Kenton Mwenge jijini Dar leo
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha cha Shule ya Sinza Mapambano jijini Dar leo.
  
 
   Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shule Kenton Mwenge jijini Dar leo
   Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Chuo cha Ustawi wa Jamii  jijini Dar leo
Umati mkubwa ukiwa kwenye foleni katika katika kituo cha kupigia kura kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar.

WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA, MADUKA YAFUNGWA KUAJILI YA UCHAGUZI

$
0
0
Wakazi wa Jiji la Mbeya Mjini wajitokeza kwa wingi kupiga kura katika Vituo mbalimbali walivyo jiandikishia kuajili ya kupiga Kura kama waonekanavyo hapo katika Picha ni baadhi ya watu wakiwa katika kituo kilichopo Mtaa wa Mkombozi Jijini Mbeya wakiwa wamepanga Foleni kuajili ya kupiga Kura.
Baadhi ya Wapiga kura wakiwa katika Foleni..

Hapa ni eneo la Mwanjelwa maharufu kwa Jina la Mtaa wa kongo likiwa Pweke kuajili ya uchaguzi hakuna alie leta Biashara yake hapa siku hii ya leo.

Baadhii ya Maduka ya Vitu vya Jumla na Lejaleja yakiwa yamefungwa Eneo la Kabwa Stendi.

Jeshi la Polisi linaendelea kuzungukia Mitaa mbalimbali kuhakikisha hali ya Usalama  jijini mbeya Inakuwa shwari katika kipindi hiki cha uchaguzi.
                           PICHA ZOTE NA FADHIRI ATICK-MR.PENGO MBEYA
                                                    PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA APIGA KURA

$
0
0
Wanannchi wakihakiki majina yao katika kituo chao cha kupigia kura.
Jaji S.K. Mutungi akipata maelekezo jinsi ya kukunja karatasi za kupigia kura kutoka kwa Bw. Franco Mololo Mwakabuta ambaye ni msimamizi Mkuu wa Kituo namba 2 cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Bunge.

Jaji Mutungi akiwa kwenye chumba cha kupiga kura.
Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji S.K. Mutungi akipiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa ngazi za ubunge na udiwani katika kituo cha kupigia kura cha shule ya Msingi Bunge mapema Asubuhi Leo Octoba 2015.
 Bw. Themistocles Justinian ambaye ni Msiamamizi  Msaidizi wa Kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Bunge akiweka alama katika kidole cha  Jaji Mutungi kushiria tayari amekwisha kupiga kura.
  Baadhi ya wananchi wakihakiki majina yao kwa ajili ya kupiga kura

MKE WA RAIS MAMA SALMA APIGA KURA KATIKA KITUO CHA MTANDA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

$
0
0
 Mama Salma Kikwete akisubiri kadi inayokaguliwa na msimamizi wa Kituo alichojiandikisha na hatimaye kupiga kura  katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mtanda Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mjini.
 Mama Salma akisubiri moja ya fomu za kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani
 Msimamizi wa kituo akiangalia picha ya Mama Salma katika dafutari la wapigakura.

 Mama Salma akiweka tiki kumchagua kiongozi BORA.
 Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Diwani.
 Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Mbunge.
 Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Rais.
 Mama Salma akiwekwa vino na msimamizi wa kituo unaotambulisha kuwa amepiga kura.
 Mama Salma akiwatakia kila la heri wananchi wanaotarajia kupiga kura kituoni hapo
 Wananchi wakiwa katika mstari tayari kuelekea kupiga kura.
 Wananchi wakiwa katika mstari tayari kuelekea kupiga kura.
 Mama Salma akiagana na baadhi ya wananchi Uwanja wa Ndege wa Kikwetu Lindi.
 Mama Salma akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Jordan Rugimbana.
Mama Salma akipanda Ndege  na kuwapungia mkono Maofisa waliopo Uwanja wa Ndege Kikwetu Lindi  tayari kuelekea Dar es Salaam baada ya kupiga kura.

WANAFUNZI 65 KUONDOKA KWA MASOMO NCHINI CHINA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya  Global Link Education imeendelea kupeleka wanafunzi kwenda kusoma vyuo vya nje vilivyo na uwezo kutoa elimu bora.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Link Education (GEL),Abdumaalik Mollel wakati akitoa mafunzo kwa wanafunzi 65 wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu.

Mollel amesema vyuo vya nje ambavyo vinashirikiana na GEL vina ubora wa elimu pamoja na kuwa na vitendea kazi vinavyoweza kufanya mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yao.

Amesema wanafunzi 500, GEL imesha wadahili katika vyuo vya nje na  wanafunzi hao wameona ubora wa vyuo hivyo na kuweza kuleta chachu ya maendeleo nchini kutokana na utaalam wataopata huko.

Mollel amesema kuwa nafasi bado zipo katika vyuo vya China hivyo wazazi wanaweza kuwasiliana na GEL kufanya usajili katika vyuo hivyo.

“Nia ya GEL ni kuona wanafunzi wanafanya vizuri katika matokea na tunafatilia tabia zao hatua kwa hatua tukiwa na lengo ya kupata wasomi wenye ujuzi kwa maendeleo ya taifa”amesema Mollel.

Aidha amesema kuwa wanafunzi wanaonyesha tabia mbaya wanawarudisha nchini katika kuweza kuokoa fedha za mzazi kuendelea kuhudumia mtoto ambaye mwishoni hatafanya vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel akizungumza na wazazi na wanafunzi wanaotarajia kuondoka Oktoba 28 kwenda kusoma masomo ya elimu ya juu yalifanyika makao Makuu ya GEL  leo jijini Dar es Salaam. 
Wazazi wakimsikiliza Abdulmaalik Mollel
Sehemu ya wazazi na wanafunzi  wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel hayupo pichani leo makao makuu GEL leo jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel ,akitoa nyaraka za taarifa za wanafunzi wanaokwenda nchini china leo jijini Dar es Salaam. 
 Wanafunzi wakiuliza swali kwa masomo wanayokwenda kusoma katika vyuo vya nje  leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel akizungumza na mzazi wa mwanafunzi wa anyekwenda kusoma nchini China,leo jijini Makao ya Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii

KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA  TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.

Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-

16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui   atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana.  uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha   usahihi wa matokeo yote   yanayotangazwa.

16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na  ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.

Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha   kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE 25/10/2015    
  

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI LEO OKTOBA 26,2015

$
0
0
 Nchi yasimama,Lowasa.Magufuli wachuana vikali.Pitia udondozi wa magazeti hapa Simu.tv;
Mgombea ubunge Arumeru mbaroni, mamilioni wajitokeza kupiga kura, amani yatawala. Pata habari kutoka magazeti ya leo;  https://youtu.be/K3MJHg68bD4

 Macho ya Afrika mashariki ni Tanzania, mshindi  kiti cha urais kutangazwa alhamis.Pata dondoo za habari hapa Simu.tv; https://youtu.be/Hn8sfh0E_dg
Yanga yaja kidigitali, N’daw aishtua Simba, Aveva aamua kuchukua hatua. Ni katika magazeti ya michezo ya leo; https://youtu.be/OxKtrvo9SaM 

Pata habari motomoto za kisiasa katika magazeti ya leo Jumatatu Octoba 25.2015 hapa Simu.tv; https://youtu.be/GwaPCQlaY7Y

Article 10

$
0
0
 Nchi yasimama,Lowasa.Magufuli wachuana vikali.Pitia udondozi wa magazeti hapa Simu.tv;
Mgombea ubunge Arumeru mbaroni, mamilioni wajitokeza kupiga kura, amani yatawala. Pata habari kutoka magazeti ya leo;  https://youtu.be/K3MJHg68bD4

 Macho ya Afrika mashariki ni Tanzania, mshindi  kiti cha urais kutangazwa alhamis.Pata dondoo za habari hapa Simu.tv; https://youtu.be/Hn8sfh0E_dg
Yanga yaja kidigitali, N’daw aishtua Simba, Aveva aamua kuchukua hatua. Ni katika magazeti ya michezo ya leo; https://youtu.be/OxKtrvo9SaM 

Pata habari motomoto za kisiasa katika magazeti ya leo Jumatatu Octoba 25.2015 hapa Simu.tv; https://youtu.be/GwaPCQlaY7Y

BEI YA MADAFU HII LEO

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 26, 2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 26, 2015.

SIMUtv: Waangalizi wa ndani wa uchaguzi ambao ni muungano wa Asasi Mbili CEMOT umetoa matokeo ya awali muda mchache baada ya kupiga kura.
SIMUtv: Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza matokeo rasmi ya majimbo 2 ya ubunge na madiwani katika majimbo ya Fuoni Na Kiembesamaki. https://youtu.be/YKGnxP4NJ2E 

SIMUtv: Timu ya Manchester City imerejea kileleni katika ligi kuu ya England baada ya Kutoka suluhu na mahasimu wao Manchester United. https://youtu.be/u171GDQ5STY

SIMUtv: Wananchi wameombwa kuchangia timu ya walemavu ya mchezo wa baisikeli ili kuwawezesha kushiriki mashindano yatakayofanyika afrika kusini; https://youtu.be/9JHWqOV6_0w

SIMUtv: Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu.https://youtu.be/yIgojd11GiM
SIMUtv: Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu Jimbo La Paje. https://youtu.be/gwVbujPU-bY

SIMUtv: Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu Jimbo La Lulindi Mtwara. https://youtu.be/7xUpGeK5LHY

MATOKEO RASMI YA MAJIMBO MATATU

$
0
0
UNGUJA-MAKUNDUCHI
KUSINI UNGUJA-PAJE
MKOA-LILUNDI 

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MANAIBU KATIBU WAKUU NA KATIBU TAWALA WA MKOA

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha manaibu katibu wawili wa wizara na Katibu Tawala wa mkoa katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Manaibu katibu walioapishwa ni pamoja Ndugu Emmanuel Kalobelo anayekuwa Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na ndugu Tixon Nzunda nayekuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emannuel Kalobelo akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda akila kiapo mbele ya Rais Kikwete leo.
Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Katavi Mhandisi Madeni Kipande akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo na kukabidhiwa miongozo ya kazi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliapishwa keo.Kushoto ni Katbu Tawala Mkoa wa Katavi Ndugu Madeni kipande, wanne kushoto ni Naibu katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emmanuel Kalobelo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mpya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda.
.(Picha na Freddy Maro).

RAIS KIKWETE AMTEUA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA TEA

$
0
0

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA).  Uteuzi huo ulianza Oktoba 18, mwaka huu, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi hiyo ya TEA na ndiye amekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015

RAIS KIKWETE AKABIDHI VITABU CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA(NATIONAL DEFENCE COLLEGE)

$
0
0
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College) katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy MRO) 

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatatu Oktoba 26, 2015, amelikabidhi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vitabu kwa ajili ya vyuo vyake na maktaba zake, ikiwa ni mara ya tano kwa Rais Kikwete kulikabidhi Jeshi hilo vitabu wakati wa uongozi wake.

Vitabu hivyo 384 vilivyokabidhiwa leo vitatumiwa na Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha National Defence College (NDC) na wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho chenye hadhi ya kimataifa.

Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amehudhuria sherehe ya makabidhiano ya vitabu hivyo ambavyo Rais Kikwete amevikabidhi kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Hiyo ni mara tano kwa Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu kukabidhi vitabu kwa JWTZ katika azma yake ya kuboresha vyuo na maktaba ya vyuo hivyo vya Jeshi. Mpaka sasa, Rais Kikwete amekwisha kabidhi vitabu 3,136 kwa Jeshi.

Rais Kikwete aliahidi kulinunulia na kulikabidhi Jeshi vitabu (titles) mbali mbali 503 na kufuatia makabidhiano ya leo, sasa vimebakia vitabu (titles) 27 ambavyo navyo tayari vimenunuliwa na vinasubiriwa kusafirishwa kuletwa nchini kutoka vilikonunuliwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015

MATOKEO YA AWALI YA URAIS MAGUFULI ANAONGOZA DHIDI YA WAGOMBEA WENZAKE

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Damian Lubuva (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari na waangalizi wa kimataifa wakati akitangaza matokeo ya awali ya urais Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.
 Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wakiwa kwenye mkutano huo wa kutangazwa matokeo ya awali.
 Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wakiwa kwenye mkutano huo wa kutangazwa matokeo ya awali.
 Jaji Lubuva akijiandaa kutangaza matokeo hayo ya awali.
 Maofisa wa NEC wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wadau wa siasa wakiwa kwenye mkutano huo.



Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

MAMIZ GRAND RESORT INAKULETEA MIAKA 18 YA FM ACADEMIA WAZEE WA NGWASUMA NA NGOMA ZAO MPYA

MATOKEO RASMI YA URAIS YA MAJIMBO 10

Viewing all 49613 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>