Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA, YASAIDIA UBORESHAJI WA KITUO CHA FURAHINI MKOANI K'NJARO

0
0
User comments Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani na kijiji hicho.
Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
User comments 
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.
Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema wazo la kuanzishwa kwa kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
“Elimu imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na bayolojia,” alisema Isiaka na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
User comments 
Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
“Kwa kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia ya maktaba na tehama, wanafunzi wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha Kisangara.
Kijiji cha Kisangara ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
1 (11) 
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi na kuwaacha katika shule za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
User comments 
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
20151023_122610
User comments 
Mratibu wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI OKTOBA 27,2015

0
0
Magufuli azidi kungara katika matokeo ya awali katika majimbo 13. Mawaziri waanguka majimboni. Yote haya utayapata katika magazeti; 
Mzee ‘sawasawa’ ajitangaza  mshindi Zanzibar, Polisi yakamata 169 kwa kuingilia tume. Pata dondoo za habari za magazetini;  https://youtu.be/mGoDo1XC_Ts

Polisi wazima vurugu Zanzibar. Aeleza sababu ya matokeo jimbo la Ukonga kuchelewa. Pata undani wa habari hizi katika magazeti;  https://youtu.be/3jfyH1rEnjQ

Ulinzi waimarishwa Zanzibar, wasimamizi wa uchaguzi wanusurika kifo. Pitia dondoo za magazeti hapa Simu.tv;https://youtu.be/n_vmWxE0dyM

Pitia udondozi wa habari kemukemu za kisiasa zilizotawala magazeti ya leo Octoba 27.2015 hapa Simu.tv;https://youtu.be/ntk9bzkfQKE

POLISI YAZIMA VURUGU ZANZIBAR,NI BAADA YA MAALIM SHARIF HAMAD KUJITANGAZA MSHINDI WA URAIS

0
0

WAKATI wakisubiri matokeo ya uchaguzi ya rais huku Tume ya Uchaguzi ikitangaza kura za wagombea wabunge na uwakilishi katika majimbo ya uchaguzi Zanzibar, Jeshi la Polisi limelazimika kuzima fujo na vurugu kutoka kwa wafuasi wa CUF waliotanda mitaa ya Mji Mkongwe na barabara kuu ya Darajani.

Vurugu zimezuka baada ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufanya tathmini na kutangaza matokeo ya ushindi wa chama chake katika uchaguzi wa juzi kwa asilimia 52.87. 

Maalim Seif alitoa tathmini hiyo mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CUF Mtendeni mjini Unguja na kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo hayo.

Katika tathmini hiyo inaonesha kwamba mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa tiketi ya urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amepata ushindi kwa asilimia 47.13. 

Maalim Seif alidai matokeo waliyonayo yamekusanywa na mawakala waliopo katika vituo vya uchaguzi vilivyopo Unguja na Pemba kwa kufanya majumuisho. Hatua hiyo ilizusha shangwe na furaha kwa wafuasi wa CUF na kuanza kutembea barabarani huku gari zikipiga honi.

Baadhi ya mitaa ikiwemo Darajani na Mlandege, polisi waliweka vizuizi ambavyo vilisaidia kuwazuia wafuasi hao kuingia barabarani. Aidha, ofisi za Serikali zilizopo katika eneo la Mji Mkongwe pamoja na taasisi za kibenki, zilifungwa baada ya kuibuka kwa mazingira ya fujo na vurugu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha Jeshi la Polisi kudhibiti maeneo mbalimbali zaidi yaliyopo Mji Mkongwe pamoja na eneo la Darajani ambalo ni ngome ya upinzani.

“Tumefanikiwa kudhibiti vurugu za watu waliofanya fujo na vurugu katika maeneo mbali mbali ya mji wa Unguja na hali ni shwari kwa sasa,” alisema Mkadam. Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ni kosa la jinai kwa mtu yeyote au mgombea wa chama cha siasa kutangaza matokeo ya urais. Mapema, CCM Zanzibar ililaani kitendo kilichofanywa na Maalim Seif kujitangazia ushindi katika uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kitendo hicho ni sehemu ya vitendo na matukio ya uchochezi yanayotakiwa kudhibitiwa kwa ajili ya kuimarisha amani na utulivu. Vuai aliitaka ZEC kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa mgombea huyo kwa kauli zake ambazo lengo lake kuingiza nchi katika machafuko katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.




Hata hivyo, viongozi watendaji wa ZEC hawakuwa tayari kulizungumzia suala hilo, ambapo maofisa wote walikuwa wapo katika mchakato wa kupokea na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa majimbo. 

CCM YAIKUNG'UTA CHADEMA BILA HURUMA JIJINI MWANZA

0
0
Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM)
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.


Matokeo hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimboni humo ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya huku kukiwa na Ulinzi Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika viunga vya ofisi za Jiji hilo.


Akitakangaza matokeo hayo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Mahinya alibainisha kuwa pia CCM imeibuka kidedea kwa upande wa Madiwani ambapo kati ya Kata 18, imeshinda Kata 14 na Chadema Kata Nne.


Kwa upande wa Wagombea wengine, Chacha Okong’o (ACT Wazalendo) alipata kura 161, Faida Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad Mkangwa (NRA) kura 104, Mohamed Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan Mtoro (UDP) amepata kura 68.


Hata hivyo kabla ya matokeo hayo kutangzwa, Mgombea kutoka Chadema Ezekiel Wenje alikataa kusaini karatasi ya wagombea na kubainisha kuwa demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga matokeo hayo.


Kwa upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu awali alitarajia ushindi huo na kwamba suala la demokrasia limezingatiwa.


Katika hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabili Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujitegemea kiuchumi.
Ezekiel Wenje akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza
Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (kulia) muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

Kipindi cha Jukwaa Langu Okt 26 2015 (FULL)

0
0
Photo Credits: dw.com/sw

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Na leo, tulizungumzia Tanzania baada ya Uchaguzi wa jana Oktoba 25, 2015

TUKINGOJEA MATOKEO YA KURA ...NA HUKU TUNAPATA BURUDANI YA MUZIKI

0
0
NYIMBO ZA KUMUGA RAIS JAKAYA KIKWETE KUTOKA KWAO NGOMA AFRICA
Wakati wananchi tukiendelea kufuatilia matokeo ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa hawamu ya tano, ni vema basi kujikumbusha yale ambayo yaliyofanyika katika serikali ya hawamu ya nne ya Rais anayemaliza muda amri jeshi mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa kupitia njia ya muziki bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni chini ya uongozi wake mtunzi gwiji kamanda Ras Makunja wameshua nyimbo mbili za kumuaga Rais Jakaya KIkwete na kuyaimba baadhi ya aliyoyafanya katika hawamu ya Nne.
Pata burudani kwa kusikiliza nyimbo hizi at:

WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AIBUKA KIDEDEA UBUNGE BUKOBA MJINI.

0
0
Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yametanga usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku huu wa saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Aron T. Kagurumjuli(Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgembea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki usiku huu. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

LICHA ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika leo jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia leo hii kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na Jioni hii kuleta kasheshe na ghasia. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao ambao mpaka usiku huu walikuwa wamepandwa na jazba katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba.

Vurugu zikiwemo kurushiana mawe zilitokea. Ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri na kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa. 

Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.


Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9.
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Vingozi wa Chama cha Chadema wakiteta jambo, kushoto) ni Bw. Chief Kalumuna Mshindi wa Udiwani Kata ya Kahororo aliyeshinda kiti hicho katika Uchaguzi huu wa 2015. (Kulia) ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kahororo kupitia Chama cha Chadema katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba mjini huku wakisubiri matokeo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei (kulia) mbele akiteta na Chief Kalumuna Diwani wa kata kahororo wakibadilisha mawazo wakati wakisubiri matokeo usiku huu.Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba
Kidedea...Chif Kalumuna(kulia) wa Kata ya Kahororo akiwa amembeba mshindi bw. Wilfred Lwakatare
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa.


Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Taswira jioni hii maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.

Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 27, 2015.

0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 27, 2015.

Wakazi Wa Kata Ya Saranga jijini Dar Jana wamefanikiwa  kupiga kura ya mbunge na Raisi baada ya kuahirishwa kwa zoezi hilo Oktoba 25. 

Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Mtwara mjini Yametangazwa na msimamizi wa jimbo hilo huku kukiwa na hali ya Vurugu. https://youtu.be/CY2Y2WnYkaM

Jeshi la polisi Visiwani Zanzibar limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa CUF waliokusanyika katika ofisi za CUF. https://youtu.be/944jzWlWh6k
Mwenyekiti wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC Jaji. Damian Lubuva akemea baadhi ya watu wanaotangza Matokeo katika Mitandao ya Kijamii. https://youtu.be/Zg-spuDs1Ks

Haya ndiyo matokeo ya Uchaguzi mkuu ya Uraisi Mkoani Pwani jimbo la Chalinze ambapo mgombea Uraisi CCM akipata asilimia 69.70 na Lowassa akipata asilimia 28.53. https://youtu.be/HsdD_2j3w_8

Haya ndio Matokeo halali ya Uraisi Mkoa wa Kusini Pemba Jimbo la Chwanga visiwani Zanzibar. https://youtu.be/OKEVQQ_WZno
haya ndio matokeo halali ya Nafasi Ya Uraisi Mkoa Wa Mjini Magharibi jimbo la Chumbuni visiwani Zanzibar. https://youtu.be/u6lwnYXuBSI
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Mbeya Jimbo la Ileje kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/13vTh4vVWXQ
Oscar Rwegasira Mukasa wa CCM aibuka mshindi wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Biharamulo Magharibi. https://youtu.be/q_LAhUNBeSc

Musoma mjini jimbo lililokuwa likishikiliwa na Vicent Nyerere limetwaliwa na Ndg. Vedastus Manyinyi wa CCM kwa kishindo cha asilimia 55. https://youtu.be/oKt6jChBHSs

Zitto Zuberi Kabwe aibuka kidedea kwa ushindi wa asilimia 52 katika jimbo la Kigoma Mjini Uchaguzi mkuu. https://youtu.be/W3rx9Cw969g

Ndg. Daniel Nsanzugwanko ambwaga Moses Machali wa ACT kwa asilimia 52 na kunyakua jimbo la Kasulu mjini mkoani kigoma. https://youtu.be/zawE1FlbXfk
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Kaskazini Unguja Jimbo la Kijini kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/BT_9iEvy8tA
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Mkoa wa Tanga Jimbo la Kilindi kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/NQFWV2JWQd8

Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi Mkoa Wa Tanga Jimbo La Korogwe Mjini Tanga kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/AH3_q7X8Gi4
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi Mkoa Wa Mjini Magharibi Kwahani kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/VT8Q3C7RwZI

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC leo itaendelea kutangaza matokeo ya uraisi katika ngazi ya majimbo nchini kote kuanzia saa 3 asubuhi. https://youtu.be/AEOM3qkVvTU
Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Uliofanyika oktoba 25 yameendelea kutangazwa huku yakionesha mchuano mkali kati Chama Cha CCM na CHADEMA. https://youtu.be/UnAp-4RP9C8

Chama Cha Mapinduzi Visiwani Zanzibar kimeiomba Tume Ya Uchaguzi ZEC kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kwa kushinikizwa. https://youtu.be/Mc_E2Hlvbz8

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 27, 2015.

0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 27, 2015.

Wakazi Wa Kata Ya Saranga jijini Dar Jana wamefanikiwa  kupiga kura ya mbunge na Raisi baada ya kuahirishwa kwa zoezi hilo Oktoba 25. 

Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Mtwara mjini Yametangazwa na msimamizi wa jimbo hilo huku kukiwa na hali ya Vurugu. https://youtu.be/CY2Y2WnYkaM

Jeshi la polisi Visiwani Zanzibar limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa CUF waliokusanyika katika ofisi za CUF. https://youtu.be/944jzWlWh6k
Mwenyekiti wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC Jaji. Damian Lubuva akemea baadhi ya watu wanaotangza Matokeo katika Mitandao ya Kijamii. https://youtu.be/Zg-spuDs1Ks

Haya ndiyo matokeo ya Uchaguzi mkuu ya Uraisi Mkoani Pwani jimbo la Chalinze ambapo mgombea Uraisi CCM akipata asilimia 69.70 na Lowassa akipata asilimia 28.53. https://youtu.be/HsdD_2j3w_8

Haya ndio Matokeo halali ya Uraisi Mkoa wa Kusini Pemba Jimbo la Chwanga visiwani Zanzibar. https://youtu.be/OKEVQQ_WZno
haya ndio matokeo halali ya Nafasi Ya Uraisi Mkoa Wa Mjini Magharibi jimbo la Chumbuni visiwani Zanzibar. https://youtu.be/u6lwnYXuBSI
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Mbeya Jimbo la Ileje kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/13vTh4vVWXQ
Oscar Rwegasira Mukasa wa CCM aibuka mshindi wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Biharamulo Magharibi. https://youtu.be/q_LAhUNBeSc

Musoma mjini jimbo lililokuwa likishikiliwa na Vicent Nyerere limetwaliwa na Ndg. Vedastus Manyinyi wa CCM kwa kishindo cha asilimia 55. https://youtu.be/oKt6jChBHSs

Zitto Zuberi Kabwe aibuka kidedea kwa ushindi wa asilimia 52 katika jimbo la Kigoma Mjini Uchaguzi mkuu. https://youtu.be/W3rx9Cw969g

Ndg. Daniel Nsanzugwanko ambwaga Moses Machali wa ACT kwa asilimia 52 na kunyakua jimbo la Kasulu mjini mkoani kigoma. https://youtu.be/zawE1FlbXfk
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Kaskazini Unguja Jimbo la Kijini kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/BT_9iEvy8tA
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Mkoa wa Tanga Jimbo la Kilindi kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/NQFWV2JWQd8

Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi Mkoa Wa Tanga Jimbo La Korogwe Mjini Tanga kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/AH3_q7X8Gi4
Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi Mkoa Wa Mjini Magharibi Kwahani kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/VT8Q3C7RwZI

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC leo itaendelea kutangaza matokeo ya uraisi katika ngazi ya majimbo nchini kote kuanzia saa 3 asubuhi. https://youtu.be/AEOM3qkVvTU
Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Uliofanyika oktoba 25 yameendelea kutangazwa huku yakionesha mchuano mkali kati Chama Cha CCM na CHADEMA. https://youtu.be/UnAp-4RP9C8

Chama Cha Mapinduzi Visiwani Zanzibar kimeiomba Tume Ya Uchaguzi ZEC kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kwa kushinikizwa. https://youtu.be/Mc_E2Hlvbz8

VODACOM KUMKABIDHI KIIZA KITITA CHAKE

0
0
Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza.

NA MWANDISHI WETU
MSHAMBULIAJI wa Simba, Hamis Kiiza, anatarajiwa kukabidhiwa zawadi yake ya Sh milioni 1/-ya Mchezaji Bora wa Mwezi na wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, baada ya kuibuka kidedea Septemba.


Kiiza alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Septemba baada ya kufanya vema katika mwezi wa kwanza wa ligi hiyo, akiisaidia timu yake ya Simba kushinda mechi tatu mfululizo, huku Mganda huyo akifunga mabao matano, ikiwamo ‘hat-trick’ katika pambano dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, Kiiza atakabidhiwa kitita chake hicho na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao, wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Majimaji Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Alisema kuwa kampuni yao itaendelea kutoa zawadi kwa wachezaji wanaofanya vizuri kila mwezi, ikiwa ni sehemu ya mikakati na mchango wao katika kuinua kiwango cha michezo, hususan soka nchini na kubadilisha maisha ya wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu.

“Katika kuendeleza mikakati yetu ya kuinua soka hapa nchini pamoja na kuboresha maisha kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Vodacom Tanzania, itamjaza kiasi cha Sh milioni moja mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza kutokana na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa ligi hiyo kwa Septemba msimu huu,” alisema Nkurlu.

Juu ya tuzo hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ameishukuru na kuipongeza Vodacom Tanzania ubunifu huo wa kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri kwani kitendo hicho huchangia kuendeleza vipaji na kuwahamasisha wachezaji kufanya vizuri zaidi na kuzisaidia timu zao.


“TFF tunaamini zawadi kama hizi zinazotolewa kwa Mchezaji Bora wa Mwezi, zinaweza kuwa chachu kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu kujituma zaidi kwa faida yao, klabu zao na soka la Tanzania kwa ujumla,” alisema.


Tangu tuzo hiyo ianze kutolewa Septemba mwaka jana, ni Coastal Union pekee iliyofanikiwa kutoa wachezaji wawili walioibuka kidedea hadi sasa.




Washindi wa tuzo hiyo tangu ianzishwe mwaka jana ni Antony Matogolo wa Mbeya City (Septemba, 2014), Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr’ (Azam FC, Oktoba), Rashid Mandawa (Kagera Sugar, Novemba), Joseph Mahundi, Said Bahanunzi (Polisi Moro, Januari) na Godfrey Wambura (Coastal Union, Februari), James Mwasote (Police, Machi) na Mrisho Ngassa (Yanga, Aprili). 

MATOKEO RASMI YA WAGOMBEA URAIS TANZANIA MAJIMBO 32

BEI YA MADAFU HII LEO

0
0

TWIGA KUCHEZA NA MALAWI NOVEMBA 7

0
0
Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.
Awali Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.

Cheka ulingoni Uingereza Novemba 7

0
0
Dar es Salaam. Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
 
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo.
 
Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.Kwa mujibu wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.
 
 “Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano hilo, kuna vitu fulani fulani vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7 na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa sasa yupo Kenya kikazi.Alisema kuwa Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
 
Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa
 
 “Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.
 
Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.
Wakati huo huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku, hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuhairishwa dakika za mwisho.
 
Ndambile alisema kuwa Mwakalebela alitakiwa kupambana na bondia Craig Kennedy na pambano hilo limefutwa kutokana na sababu za kiufundi.

Dj KFLIP AACHIA MIXTAPE NYINGINE KWA YOUTUBE ISIKILIZE KWA MARA YA KWANZA.

0
0
Breakfast mix is a radio show mixed by DJ K FLIP Every Monday to Friday 7am to 10am (EAT)... Download JEMBE FM APP on GOOGLE PLAYSTORE to listen worldwide. 

Akizungumza na Gsengo Blog DJ huyo anayepiga mzigo ndani ya moja ya Hottest radio station inayo kuja kwa kasi toka pande za Rock City, amesema kuwa huo ni mwanzo wa mpango wake wa kuachia Mix Tape kila wiki kupitia Youtube na rasmi ameanza kufanya hivyo wiki hii (leo) yenye historia kwa taifa la Tanzania ambapo taifa linashuhudia kukabidhiwa hati kwa mshindi wa nafasi ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli pamoja na Makamu wake. 

"Unajua Rais anayeingia madarakani kwa awamu ya tano ni rais wa wote na kwa sababu kauli mbiu yake ni 'HAPA KAZI TU' akituhamasisha vijana tufanye kazi kwa bidii na tija, sina budi kuungana naye na kubadilika sanjari na mfumo wake mpya wa utekelezaji, hivyo nawaahidi makubwa mashabiki wangu wanaonifuatilia na wale wapya wenye kuhitaji muziki mpya mzuri" alisema  Deejay Kflip.

Gsengo Blog inaahidi kwa kila ijumaa kukushushia moja ya Mix Tape za Deejay Kflip.

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI WA URAIS WA TANZANIA AWAMU YA TANO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Urais Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Samia Hassan Suluhu.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu katika hafla hiyo.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha urais. Kutoka  kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Chief Lutalosa Yemba.
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akimpongeza Rais Mteule wa Tanzania Dk. John Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
 Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia wakati Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli alipokuwa akitoka Ukumbi wa Diamond Jubilee kukabidhiwa cheti cha urais.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Magufuli akimuonesha Rais Jakaya Kikwete cheti cha ushindi.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Makufuli akiwa katika picha ya pamoja na wagombea urais wenzake wa vyama vingine.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva kwa kusimamia vizuri uchaguzi mkuu wa 2015.
Rais Jakaya Kikwete na Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye hafla hiyo.

Na Dotto Mwaibale

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemkabidhi cheti cha ushindi aliyekuwa mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk, John Magufuli baada ya kushinda kwa kura nyingi kuliko wenzake kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Aidha wanasiasa wamemtaka Dk. Magufuli kutekeleza mambo yote ambayo ameahidi, huku Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Anna Mghwira., akimtaka ahakikishe kuwa Katiba ya wananchi inapatikana ili kufanikisha dhana ya mabadiliko ambayo yalikuwa yanatajwa na wagombea wote.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi cheti hicho katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki huku akiwapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tofauti na mwaka 2010.

Lubuva alisema katika uchaguzi huo wagombea wa nafasi ya urais ni Anna Mghwira wa ACT, Chief Lutalosa Yemba wa ADC, Dk. Magufuli wa CCM, Edward Lowassa wa Chadema, Hashim Rugwe wa Chaumma, Malik Kasambala wa NRA, Elifatio Lyimo wa TLP na Fahmi Dovutwa wa UPDP.

Alisema, tume imemtanga Dk. Magufuli kwani amefanikiwa kupata kura nyingi kuliko wagombea wenzake ambapo  walioandikishwa ni wapigakura 23,161,440, waliopiga kura ni 15,589,639 sawa na asilimia 67,31 ya waliojiandikisha.

Alisema kura halali ni 15,193,862 sawa na asilimia 97.46, kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.58.

Jaji Lubuva alitangaza matokeo kuwa Mghwira amepata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65, ADC amepata kura 66,049 sawa na asilimia 0.43.

Dk. Magufuli amepata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 sawa na asilimia 58.46, Lowassa amepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97, Rungwe 49,256 sawa na asilimia 0.32, Kasambala amepata kura 8,028 sawa na asilimia 0.05.

Wengine ni Lyimo amepata kura 8,198 sawa na asilimia 0.05, Dovutwa amepata kura 7,785 sawa na asilimia 0.05.

Kailima

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan, alisema kura zilizopigwa zinatoka katika majimbo ya uchaguzi 264 na kata 3,957 na hakuna dosari kubwa ambayo ilitokea.

Alisema katika nafasi ya ubunge majimbo yaliyofanya uchaguzi ni 256 huku majimbo nane yakiwa hayajafanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni vifo kwa wagombea na karatasi za wagombea kuwa na mapungufu.

Kailima alisema pia kuna Kata ambazo hazijafanya uchaguzi kutokana na mapungufu mbalimbali ambapo wanatarajiwa kufanya uchaguzi mapema iwezekanovyo.

"Mchakato  wa uchaguzi umefanyika kwa kufuata sheria hivyo tume inadiriki kusema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki kwani hakuna lalamiko lolote kutoka kwa wakala," alisema.

Alisema kifungu cha 85 kinaipa mamlaka haki ya kutangaza matokeo hata kama baadhi ya wagombea watagoma kusaini matokeo husika hivyo aliyetangazwa na tume ndiye mshindi.

Mghwira

Akizungumza baada ya tume kumkabidhi mshindi cheti, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, alisema anakubaliana na matokeo na kumtaka Magufuli ahakikishe kuwa anasimamia upatikanaji wa katiba.

Mghwira alisema, iwapo anataka mabadiliko yaweze kupatikana ni jukumu lake kusimamia upatikanaji wa katiba ya wananchi kwani ndiyo inaweza kuleta mabadiliko sahihi kwa Tanzania ya leo.

Aidha, alimtaka mshindi huyo wa nafasi ya urais kusimamia suala la usawa na umoja wa kitaifa ambao utaweza kujenga nchi kufikia maendeleo sahihi pamoja na wananchi.

"Tunahitaji uchumi imara ili kurejesha fahari ya nchi na wananchi kwani hakuna shaka kuwa wananchi wamekata tamaa na taifa lao jambo ambalo sio sahihi," alisema.

Mghwira alitumia nafasi hiyo kumkabidhi Dk. Magufuli, ilani ya chama hicho kwani ina malengo ya kuibadilisha Tanzania.

Yemba

Kwa upande wake aliyekuwa mgombea urais, kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chifu Litalosa Yemba, alisema anampongeza Dk. Magufuli kwa ushindi huku akiweka bayana kuwa tangu aanze kushiriki chaguzi uchaguzi wa mwaka huu ndio uchaguzi ambao ulikuwa huru na wa haki.

Alisema mapungufu ambayo yanalalamikiwa na baadhi ya wagombea yanapazwa kuangaliwa kwa undani zaidi ili kuhakikisha kuwa hayarejei kutokana na ukweli kuwa mchakato huo ni muhimu kwa wananchi.

Yemba alisema, anampongeza mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, kwa kufanya kampeni za kistaarabu pamoja na matusi, kashfa na dharau ambazo zimejitokeza kwake.

"Tunaweza kusema mambo mengi ila ambaye ahataki kutambua mchango wa Lowassa katika siasa za Tanzania hasa upinzani atakuwa hajui siasa ninachoomba Chadema na vyama vya upinzani kudumisha nguvu hii kwani hatujaweza kupata kura zaidi ya milioni 2 tangu kuanza kwa vyama vyetu," alisema.

Aidha, ameweka bayana kuwa iwapo angefanya kampeni katika uchaguzi huu angeweza kuwa mshindi wa pili lakini kutokana na uhaba wa fedha walishindwa kufanya kampeni ila anawashukuru wananchi kwa kura ambazo wamepata.

Jonatha

Akizungumzia uchaguzi huo Kiongozi wa waangalizi kutoka Jumuia ya Madola, Rais mstaafu wa Nigeria, Godluck Jonathan, alisema uchaguzi ulikuwa huru na haki na kuzitaka nchi zingine kuiga Tanzania kwani imekuwa mfano bora.

Godluck alisema, uchaguzi ni jambo ambalo linakuwa na changamoto mbalimbali ambapo sio jambo rahisi kila mtu kukubaliana na matokeo lakini kwa mtazamo wao wanaamini kuwa uchaguzi huo umefanyika vizuri.

Nchemba

Mwigulu Nchemba ambaye ni mbunge mteule wa Jimbo la Iramba Magharibi, alisema amefurahishwa na ushindi huo kwani Dk. Magufuli ana vigezo vyote vinavyohitajika kwa kiongozi wa nchi.

Alisema watanzania wajiandae kwa kupata mabadiliko sahihi ambayo walikuwa wanayataka kwani kiongozi huyo ni mtu ambaye anasimamia uwajibikaji, uadilifu na mchapakazi.

"Vigezo vimetumika kumpata rais sahihi kwa maslahi ya Taifa, hivyo kilichobakia ni watu kufanya kazi ili dhana nzima ta hapa kazi tu ionekane na mabadiliko pia," alisema.

Mwijage

"Huyu ndiye chaguo sahihi kwa maslahi ya Taifa na pia naamini hata Mungu ndiye aliyetaka tumpate Magufuli naamini mabadilikio yataanza vijijini ili kuzuia watu kuja mijini kutafuta kazi," alisema.

Alisema watu wajiandae kufanya kazi kwani kasi ya kiongozi huyo mpya wa nchi itakuwa haina mzaha hivyo wale wakaa vijiweni watambue kuwa nafasi hiyo haipo kupitia Dk. Magufuli.

Madabida

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, alisema ushindi huo wameupokea kwa furaha pamoja na ukweli kuwa yalikuwa ndio matarajio yao.

"Sisi hatukuwa na shaka kuhusu ushindi huo lakini pia mgombea wetu ni mtu mzuri sana katika utendaji naamini kuwa wananchi wamemuelewa hivyo watarajie kuona mabadiliko ya kweli," alisema.

Madabida alisema vyama vya upinzani vilikuwa vinatumia nguvu ya hali ya juu kuhakikisha kuwa vinashinda lakini kutokana na mikakati yao wamefanikiwa kuibuka kidedea.

Kuhusu majimbo mengi ya mkoa wake kuchukuliwa na vyama vya upinzani alisema hayo ni maamuzi ya wananchi lakini wao kama uongozi walifanya kila linalowezekana kufanikisha ushindi.

Aidha, alikanusha taarifa za kuwa wameshindwa kutokana na yeye kumuunga mkono Lowassa wakati yupo CCM na kuwa hakufanya kampeni na kuweka bayana kuwa alikuwa anamuunga mkono wakati huo ila kwa sasa alikuwa na Magufuli.

Katika hafla hiyo ya kumkabidhi cheti cha ushindi Dk. Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan, pia Rais Jakaya Kikwete, alishiriki, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anne Makinda, Rais wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi, Mawaziri Wakuu wastaafu na viongozi wengine walihudhuria pamoja na wananchi na wanachama wa CCM.

MAGUFULI AANZA KUTEMA CHECHE LUMUMBA JIJINI DAR LEO

0
0

JANET MBENE AWASHUKURU WANANCHI WA JIMBO LA ILEJE

0
0
 MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi
wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na  Dkt. Jonh
Magufuli anayewania urais.

Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583
aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi
aliyepata kura 14,578 atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia
ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali
zinazowakalibi.

“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu,
madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh
Magufuli. Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi
sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa
kampeni,” alisema Mbene.

Mbunge huyo mteule alisema kuwa, kipaumbele chake cha kwanza  kitakuwa
mindombinu ya barabara na kuwajengea uwezo wajasiriamali  ili
kuzalisha bidhaa bora ikiwemo kuongeza thamani na mauzo.
Mbene alisema, hatua hiyo itasaidia kuondoa umaskini wa kipato na
msisitizo utakuwa kwenye ufugaji wa samaki, kuku, nyuki na mifugo ya
kisasa.

Pia alisema, kilimo nacho atakipa kipaumbele hususani cha alizeti,
kunde, choroko, dengu, mbaazi,  soya , karanga  zikiwemo njugu mawe
kwa wingi  kama mazao ya biashara.“Nitahakikisha pia kilimo cha nafaka  ambacho kitahusisha mahidi,mpunga, ulezi , mtama na kilimo cha matunda aina mbalimbali yakiwemo mananasi , maembe, maparachichi, mapera zikiwemo mbogamboga ili
kuwainua wana Ileje kupitia kilimo chenye tija,” alisema Mbene.


Mbali na hayo alisema, kwa kushirikiana na wananchi ataibua vyanzo vya
asili ambavyo ni vivutio vya watalii wilayani Ileje ili viweze
kuwavutia watalii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya
kuimarisha uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Pia alisema, atahakikisha anashirikiana na wananchi ili kuhakikisha
wanatatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na miundombinu
hatua ambayo itasaidia kuinua vipato vyao, jimbo na taifa kwa ujumla.

Wanamuziki wa WizKid wawasili tayari kwa Onesho lao usiku wa leo

0
0
Wakiingia katika basi tayari kwa msafara
Watumiaji mbalimbali wa vyombo vya muziki wa msanii Wizkid wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere tayari kwa shoo yao ya leo katika Viwanja vya Leaders.
Huyo mwenye fulana nyeusi anaitwa  Snipes ndio kiongozi wa bendi ya msanii Wizkid.

KIWIA AKANUSHA KUZIMIA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA. ASEMA ANATARAJIA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KWANI BADO HAJASAINI MATOKEO.

0
0
Highness Kiwia akionyesha moja ya karatasi yenye makosa

Na:George Binagi-GB Pazzo
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.


Kiwia ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.


Alieleza kuwa katika vituo mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale waliyojiandikishia.


Katika hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.


Kwa upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za uchaguzi.


Katika Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa na upinzani.


BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari

Kiwia akiteta jambo katika Mkutano na Wanahabari
Kutoka Kushoto ni Humphrey Mhada ambae ni Mwenyekiti Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, Highness Kiwia ambae alikuwa mgombea Jimbo la Ilemela Chadema na Hassan Haji ambae alikuwa Meneja Kampeni Jimboni Ilemela
Press Conference
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari
Wa kwanza kulia waliokaa ni Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema akiongea katika mkutano na wanahabari
Peter Kaiza ambae alikuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ibungilo Ilemela akionyesha moja ya karatasi yenye makosa
Kutoka Kushoto ni Julius Malifedha ambae ni Katibu Mwenezi Chadema Ilemela, Peter Kaiza aliekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ibungilo na Ivonne Highness ambae alikuwa Mratibu wa Kampeni za Uchaguzi
Kada wa Chama
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUJUZE JAMII
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images