Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE KUONGOZA KONGAMANO LA KUELEKEA UCHUMI WA KATI IFIKAPO 2025

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano  kongamano la kuchochea uzalishaji mali, Prof.Leonard  Mwaikambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya lengo la kongamano ni kutoa fursa kwa watanzania kwa jumla kuelewa malengo na mwelekeo wa taifa letu kufikia uchumi wa kati .
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano  Profesa,Leonard  Mwaikambo.


Na Emmanuel  Massaka ,Globu ya Jamii
RAIS Dk. Jakaya  Kikwete   anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kuchochea uzalishaji mali katika kuinua kipaato cha mtanzania  wa kawaida kufikia malengo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 litakalofanyika kesho katika Ukumbi Diamond Jubilei jijini Dar es Salaam.

Hayo ameyasema leo  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano  Prof.Leonard  Mwaikambo kongamano hilo litakuwa na watoa maada mbalimbali na wataalam katika sekta ambazo zitafanya kufikia uchumi huo.

Profesa Mwaikambo amesema kuwa wakati huu kutokana na harakati za uchumi kunahitajika wataalam ambao wamebobea kwa kuleta  maendeleo hayo ambayo watanzania  wanayoyataka kwa kukuza kipato.

 Amesema kongamano hilo linagusa nyanja zote katika sera za vyama hivyo ni muda mwafaka wa kujadili masuala ya uchumi ni ya msingi katika ukuza ji kipato kwa wananchi.

Aidha amesema  wanataaluma hao watatoa mchango wao katika maswala ya kijamii na sekta mtambuka , Utawala Bora ,na Mawasiliano ya kielektroniki kwa ukuzaji wa maendeleo watanzania ,Miundombinu ,Afya ,Maji, Elimu pamoja na ujenzi .

Majadiliano yataongozwa na Waziri Mkuu Mstaaf,Jaji Mstaafu,Joseph Sinde Warioba na neno la shukrani litatolewa na Waziri Mkuu,Mstaafu, John Malecela .

WAANGALIZI WA KIMATAIFA WA UCHAGUZI WAENDELEA KUPATA UFAFANUZI JUU YA MASUALA YANAYOHUSIANA NA VYAMA VYA SIASA NA UCHAGUZI.

$
0
0
 Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini . Jaji Francis S. K  Mutungi akizungumza na Waangalizi wa  uchaguzi Mkuu  kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jana Oktoba 21,2015.
 Baadhi ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
kushoto ni Msajili Msaidizi Usajili wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty Nyahoza akielezea utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa , kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji francis Mutungi.
Picha ya pamoja ya Jaji  Francis S.K Mutungi , Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Sababu Tisa kwanini CCM itashinda katika Uchaguzi Mkuu Jumapili hii, Oktoba 25

$
0
0
 Na January Makamba
 
Tarehe 25 mwezi huu Oktoba, Watanzania watapiga kura kumchagua rais wao wa tano, wabunge na madiwani.
 
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu umekuwa na msisimko mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka 1995. Mengi yamendikwa kuhusu uchaguzi huu, hususan kutokana na hisia kwamba safari hii Upinzani una nafasi ya kukiondoa madarakani moja ya vyama vikubwa na vyenye muundo bora barani Afrika, chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Matukio mbalimbali kuelekea uchaguzi huo yameleta shauku inayoweza kutengeneza hadithi ya kusisimua.
 
Nikiwa sehemu ya Timu ya Kampeni ya CCM,na kwa manufaa ya wote ambao wangependa kuwa na mtizamo tofauti, ninatoa sababu 9 kwanini tunaamini kuwa CCM itaibuka mshindi na kwanini Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
1.    Ugombea ‘fyongo’ (flawed) wa Edward Lowassa
 
Ilishabainika kuwa uchaguzi huu ungekuwa mgumu kwa CCM bila kujali nani angekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Upinzani. Lakini matokeo ya uchaguzi huu yalielemea upande wa CCM pale Upinzani ulipomchagua Lowassa kuwa mgombea wao. Ni rahisi kwa CCM kuchuana na Lowassa kuliko laiti mgombea wa Upinzani angekuwa Dkt Wilbrod Slaa, ambaye ndiye aliandaliwa kuwa mgombea kabla ya ‘ukusukumwa kando’ na nafasi hiyo kupewa Lowassa.
 
 Slaa alikuwa na uadilifu katika maeneo mengi, na aliaminika. Kwa Lowassa, ni vigumu na inanyima raha kuchuana na mfumo aliyoshiriki kujenga na ambao ulikuwa sehemu ya maisha yake hadi Agosti mwaka huu alipohamia Upinzani. CCM ilikuwa na nafasi ya kumpitisha Lowassa kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais. 
 
Hatukufanya hivyo kwa sababu rahisi tu kwamba ingekuwa vigumu mno kumkabidhi kwa wananchi mgombea wa matarajio ya baadaye ambaye ni kiashirio cha yale yasiyowaridhisha wananchi kuhusu CCM. Kuna wanaoamini kuwa uchaguzi huu ni mgumu kwa vile Lowassa ndiye mgombea wa Upinzani. Sisi twaamini kwamba uchaguzi huu ungekuwa mgumu mara kumi zaidi laiti Lowassa angekuwa ndiye mgombea wetu.
 
2.    Upinzani umesalimisha ajenda yake ya kupinga ufisadi
 
Kipindi cha miaka 10 iliyopita kimetawaliwa na matukio mbalimbali ya kuwabainisha mafisadi na kuwachukulia hatua. Vyombo vya habari, taasisi za kiraia na Bunge vimefanya kazi nzuri kushughulikia suala hilo. Rais Jakaya Kikwete ameweka historia kwa kuamuru ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupatikana kwa wananchi na kujadiliwa kwa uwazi Bungeni. 
 
Waziri Mkuu aliyekuwa madarakani, si mwingine bali Lowassa, alijiuzulu kwa sababu ya kashfa ya rushwa. Mawaziri kadhaa walitimuliwa kazi na manaibu waziri wawili wanatumikia vifungo jela. Huu ni uwajibikaji wa hali ya juu japokuwa kuna wanaoweza kudhani ni hatua ndogo. Umma umeamka.
 
Upinzani ulijenga hadhi yake kwa kuongelewa sana kuhusu ufisadi. Kilele cha Upinzani kilijiri mwaka 2007 katika mikutano mkubwa wa hadhara ambapo walitangaza majina 10 ya watu waliowaita mafisadi wakubwa zaidi, katika kilichokuja kufahamika kama Orodha ya Aibu (List of Shame). Lowassa alikuwa kinara kwenye orodha hiyo.
 
Ilitarajiwa kuwa Uchaguzi Mkuu huu uwe ‘hukumu’ kwa CCM kuhusu ufisadi. Upinzani ulitarajiwa kuitumia ajenda ya ufisadi ambayo inawagusa watu wengi. Lakini ghafla, kwa kumteua mwanasiasa, ambaye kwa jitihada zao wenyewe Wapinzani,  amefahamika zaidi kwa ufisadi, iliwalazimu kuzika ajenda hiyo. Kilichofuata baada ya hapo ni kituko na kichekesho. 
 
Wale mashujaa wa mapambano dhidin ya ufisadi walijikuta wakilazimika ‘kulamba matapishi yao.’ Wengi wao waliokuwa mahiri katika mitandao ya kijamii walilazimika kufuta historia ya baadhi ya waliyoyaandika mtandaoni walipokuwa wakikemea ufisadi, lakini si kabla ya maandiko yao kunaswa kwa ‘screenshots.’ Ulikuwa ni ukweli wa kushangaza. 
 
Ni Dkt Slaa na Professa Ibrahmi Lipumba, viongozi muhimu wa Upinzani tangu miaka ya Tisini, walioamua kujiuzulu nyadhifa zao kwa kukerwa na uamuzi wa Upinzani kumpokea Lowassa.Matokeo yake, Upinzani walijikuta wakichana kadi yao turufu- ajenda dhidi ya ufisadi. Ni nadra kwao kuongelewa suala hilo, na wanapojaribu kufanya hivyo, ni kwa kujitetea tu.
 
Jioni moja mwezi Agosti, nilimwona Mbunge wa Upinzani, Peter Msigwa, katika mdahalo kwenye runinga. Aliongelea kitu ambacho kilijumuisha mtizamo wa Upinzani kwa muda huo, na kiliniacha hoi. Alisema, kabla hawajampokea Lowassa, walifanya utafiti wao, na “ufisadi sio ajenda muhimu kwa taifa letu.” Alidai kwamba wenye ushahidi kuhusu ufisadi wa Lowassa wajitokeze hadharani.Alionekana kusahau kuwa walipomtaja Lowassa katika List of Shame, walitangaza hadharani kuwa wana ushahidi. Muda si mrefu uliopita, CCM ilikuwa ikiwaomba Wapinzani kuleta ushahidi kila yalipojitokeza madai ya ufisadi dhidi ya viongozi wa chama na serikali allegations were leveled against the party and its leaders. Haikupendeza kuingiza hoja za kisheria katika masuala ya kimaadili. Upinzani sasa umeamua kwa hiari yao kuchukua ‘chembemoyo’ wakati ambapo viongozi wa CCM wanaongelea ufisadi kwa ujasiri na msisitizo.
 
Uchaguzi huu Mkuu ni muhimu sana kwa Upinzani. Kimsingi, unaweza kuwa na madhara makubwa. Endapo watashindwa hapo Jumapili, ‘watapotea’ kwa muongo mzima ujao. Ndio maana inashangaza kuona wamechukua uamuzi wa kukimbia ajenda yao kuu ya kupambana na ufisadi  ambayo iliwatambulisha na kuwaimarisha. Na kuwapa nguvu kukubalika kwa wapigakura. Kuona wanatarajia kushinda ni miujiza mkubwa.
 
3.    Mabadiliko ambayo kamwe huwezi kuyaamini
 
Ukizinguka jijini Dar es Salaam utakutana na mabango ya Upinzani yanayodaia “Ni Muda wa Mabadiliko.” Lakini ukisikiliza mikutano yao ya kampeni, ni porojo na hasira tu. Wasemaji wakuu katika mikutano hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani na kada wa muda mrefu wa CCM, Frederick Sumaye na Lowassa mwenyewe. Kwa pamoja, wamekuwa wana-CCM na katika nyadhifa  za juu serikalini kwa zaidi ya miaka 50. Kwa hiyo inasikitisha kusikiliza kauli zao – zinazokosa imani na kupalizwa na aibu – wakipambana na mfumo walioshiriki kujenga, uliojenga tabia zao za kisiasa, na ambao walikuwa wakiusifu miezi mwili tu iliyopita.
Kutokuwa wakweli na kuweka mbele maslahi binafsi kwawatuma kudai kuwa CCM haijafanya chochote katika miaka miaka 50 iliyopita. Inapotokea viongozi wawili waandamizi wa chama na serikali  kwa zaidi ya miaka 30, wote wakiwa walioshika Uwaziri Mkuu, kudai kuwa hakuna chochote kilichofanyika katika miaka 50 iliyopita, wajihukumu wenyewe. Si kwa muundo, mwonekano au ukweli, wanasiasa hao wanasimamia mabadiliko. Yayumkinikakuhitimisha kuwa mabadiliko wanayoongelea ni kuhusu kubadili chombo kilichowaingiza madarakani, mabadiliko ya sare tu za chama. Hawana habari na mabadiliko ya maisha ya wananchi wa kawaida. Wapigakura wameanza kushtukia ukweli huo.
 
4.    Migogoro na mkanganyiko ndani ya UKAWA
 
Huko nyuma, kila ulipojiri uchaguzi, Upinzani ulijaribu kuunganisha nguvu ili kuing’oa CCM madarakani.Na kila mara jitihada za ushirikiano zilishindikana. Mwaka 2014, mjadala kuhusu Katiba Mpya kuataka serikali tatu uliwapatia ajenda ya kuwaunganisha pamoja. Kisha wakaamua kutafsiri ushirikiano huo kuwa wa kisiasa, wakaafikiana kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais na kugawana majimbo.
 
Baada ya hapo kukajitokeza unafiki wa wazi. Kuonyesha kuwa matamanio yaliwekwa mbele ya kanuni zilizopatikana kwa jitihada ngumu, chama ambacho jina lake linajumuisha maneno ‘demokrasia’ na ‘maendeleo’ kilitemea mate mchakato wake chenyewe wa kidemokrasia na mshikamano kupata mgombea wake wa urais, na kukurupuka kumpitisha kada wa muda mrefu wa CCM ambaye jitihada zake kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala ziligonhga mwamba.
 
Waliamini kwamba uamuzi wa Lowassa kuhama CCM ungekiathiri chama hicho tawala, wakitarajia vigogo kadhaa wangemfuata huo Upinzani. Badala yake, ujio wake huko ukapelekea kuondoka kwa wanasiasa wawili waliokuwa nguzo muhimu kwa Upinzani, Dkt Slaa na Prof Lipumba.Kadhalika, wanachama wengine muhimu waliohama na kujiunga na chama cha ACT- Wazalendo, ambacho hakikujiunga na UKAWA.
Kana kwamba hiyo haitoshi, makubaliano ya UKAWA kusimamisha mgombea mmoja  kila jimbo yalikumbwa na mushkeli katika majimbo kadhaa na kupelekea malalamiko yaliyosababisha ugumu katika kampeni za Lowassa.
 
Huko Masasi, mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni, alilazimika kuokolewa jukwaani baada ya waliohudhuria mikutano wake wa kampeni kupiga kelele kuwa wataipigia kura CCM. Katika jimbo la Nzega, Lowassa alilazimika kuendesha ‘kura ya sauti’ kuwauliza waliohudhuria mikutano wake wa kampeni wanamhitaji mgombea gani kati ya wawili wa UKAWA waliokuwa wanachuana. Mpango mzima wa ushirikiano miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA umekwenda mrama.CCM sasa ipo katika nafasi nzuri ya kujinyakulia majimbo ambayo vinginevyo yangekwenda kwa wagombea wa Upinzani.
 
Lakini kilele cha unafiki wa UKAWA ni hiki. Umoja huo uliundwa ili kutetea Katiba Pendekezwa iliyoshauri muundo wa Muungano wa serikali tatu. Kanuni hiyo ya msingi iliwekwa kando pale UKAWA walipomchagua mgombea wao wa tiketi ya urais, Lowassa, ambaye alikuwa mtetezi mkubwa wa muundo wa Muungano wa serikali mbili. Kwa wengi wasioendeshwa na propaganda, uamuzi wa kutelekeza suala la msingi lililopelekea umoja wa vyama hivyo, kwa ajili tu ya imani ya kufikirika ya kushinda urais, yaashiria uchu wa madaraka na sio mabadiliko yanayohubiriwa kwa wananchi.
 
 
5.    Lowassa kushindwa kufanya kampeni nchi nzima
 
Lowassa anaonekana kutokuwa na uwezo wa kusafiri kwa urefu na upana wa Tanzania kufanya kampeni. Mara nyingi amekuwa akitumia usafiri wa anga kwenda mikoani ambako hufanya mikutano mikubwa kwenye makao makuu ya mikoa, kutembelea majimbo mawili au matatu ya jirani kwa helikopta, na kurejea jijini Dar es Salaam. Huko Tanga, kwa mfano, alifanya kampeni katika majimbo matatu tu kati ya tisa mkoani humo. Mkoani Ruvuma, alifanya kampeni katika majimbo matatu kati ya tisa, Kigoma majimbo mawili kati ya manane, na Kagera majimbo matatu tu.
Kinyume chake, mgombea wa CCM, Magufuli amekuwa barabarani tangu Agosti 23, huku akipumzika kwa siku tatu. Anatumia usafiri wa gari, akitembelea kijiji baada ya kijiji, na kufanya mikutano kati ya minane hadi 12 kwa siku. Aina hii ya kufanya kampeni ‘kwa rejareja’ inabaki kuwa nguzo pekee ya kujihakikishia ushindi kwenye uchaguzi mkuu nchini Tanzania, hususan katika maeneo ya vijijini ambayo usikivu na kuonekana kwa vyombo vya habari ni mdogo. Wakati Lowassa anavutia wahudhuriaji wengi katika mikutano yake katika miji mikubwa, Magufuli anajipatia wahudhuriaji wengi katika kila kona ya Tanzania. Kama idadi ya wahudhuriaji katika mikutano hiyo ya kampeni inamaanisha wingi wa kura, basi kwa hakika CCM itashinda. Lakini tofauti na Upinzani, CCM haidanganyiki na wingi huo wa wahudhuriaji katika mikutano ya kampeni. Rekodi ya mahudhurio makubwa ilikuwa ikishikiliwa na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea maarufu wa kiti cha urais kwa tiketi ya Upinzani mwaka 1995 (ambaye pia alijiunga na Upinzani akitokea CCM). Hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi huo. Sie twategemea kitu kingine.
 
6.    Mfumo imara wa CCM katika uhamasishaji kuanzia ngazi ya chini kabisa.
 
Katika Tanzania, vyama vichache mno vinavyoweza kuchuana na uwezo wa CCM kuhamasisha wananchi. Wakati Wapinzani huhadaiwa na ‘mahaba’ wakati wa kampeni za uchaguzi, mahudhurio makubwa kwenye mikutano yao ya kampeni na vichwa vya habari magazetini, CCM hutumika nguvu yake ya kimuundo na kuwasha ‘mashine zake za kisiasa,’ kuanzia ngazi ya mtaa (ujumbe wa nyumba kumi) kwa nchi nzima. Kimuundo, jumiya ya wanawake wa CCM (UWT) pekee ni kubwa kuliko Chadema, chama kikuu cha upinzani. CCM Haihitaji kusafiri ili kufanya kampeni. CCM ipo kila mahala, ikifanya kampeni katika makundi madogo, vijijini na mitaani, kila siku na mbali ya upeo wa vyombo vya habari. Kwa wanaofahamu muundo wa chama hicho, ushindi kwake si jambo la kushangaza.
 
Kwenye miaka ya 1950s, wakati wa harakati za kusaka uhuru kutoka kwa mkoloni, uwezo wa TANU kuhamasisha ulikuwa nguzo muhimu kwa Tanganyika kupata uhuru wake.CCM imerithi vinasaba vya TANU. Mwalimu Nyerere aliijenga CCM kuwa imara kwa nyakati kama hizi. Mwaka jana, huku umaarufu wake ukiwa umepungua, CCM ilimudu kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa asilimia 80 dhidi ya umoja Huohuo wa Upinzani inaokabilina nao katika uchaguzi huu Mkuu.Tofauti haipo kwenye nini kinachoonekana kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii bali jinsi gani makada wa chama hicho tawala walivyofanya uhamasishaji katika kila mtaa na kijiji. Uchaguzi huo wa serikali za mitaa, ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, hutoa dalili nzuri kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu.
 
7.    Umahiri wa Dkt Magufuli
 
Mwaka jana, baadhi ya waandishi wa habari walikiri kwamba ni vigumu mno kumshambulia na kumshinda Dkt Magufuli. Ana rekodi imara ya usafi, uchapakazi na anayetaka kuona matokeo sahihi. Hajawahi kuvutiwa na harakati za kisiasa, na ilikuwa mshangao alipotangaza kuwania urais. Na alipotangaza, hakufanya mbwembwe wala kijitangaza kwenye vyombo vya habari. Alizingatia kanuni za chama kwa ukamilifu. Dkt Magufuli analeta kumbukumbu za mgombea mwingine aliyekuwa hajulikani mwaka 1995 -  Benjamin Mkapa. Wakati umaarufu wa CCM ukiwa chini, huku ikikabiliwa na upinzani kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu aliyehama kutoka chama hicho tawala, CCM ilimchagua turufu yake ambayo ilikuwa ngumu kuikabili.Miaka 20 baadaye, ikikabiliwa na upinzani wa Waziri Mkuu maarufu wa zamani aliyehama chama hicho na kujiunga na Upinzani, CCM imefanya tena ‘vitu vyake.’ Siku zote, CCM hujua ‘kufanya pigo la haja.’
 
8.    Ufanisi wa CCM katika maeneo ya vijijini
 
Mimi ni Mbunge wa jimbo lisilo mjini, lenye idadi ya wastani ya wapigakura. Mwaka 2010, katika uchaguzi ulionekana kuwa mgumu, CCM ilishinda jimbo langu kwa asilimia 80., na kitaifa kwa asilimia 61. Hivi sasa, tunatarajia ushindi wa CCM kuwa wa asilimia 90 hivi. Tanzania ina  majimbo kadhaa yaliyo kama jimbo langu. Upinzani hupenda kuwapuuza wananchi katika majimbo yasiyo ya mijini, kama jimbo langu, kwa kudai kuwa wanaichagua CCM kutokana na ujinga wao. Wasingeweza kukosea zaidi ya hivyo.
 
Popote walipo, watu hupiga kura kulingana na mahitaji yao. Mwaka 2000, vijiji vinne tu katika jimbo langu ndivyo vilikuwa na umeme. Leo, vijiji 44 vina umeme. Japo hatujaweza kutoa huduma zote kwa kiwango cha kumfurahisha kila mtu, lakini hali halisi yaonyesha wingi wa wanafunzi mashuleni, walimu zaidi, madaktari na manesi zaidi, zahanati nyingi zaidi zimejengwa, huduma za mawasiliano ya simu zinapatikana kwa wingi, barabara nyingi za lami, nk. Porojo kuwa hakuna kilichofanyika Kwahiyo wapigakura wasiichague CCM haieleweki katika maoneo hayo ambay kimsingi ndiyo yenye wapigakura wengi. Na wagombea wa CCM wanaposema watafanya zaidi ya waliyokwishafanya, kwa kuzingatia mafanikio yaliyokwishapatikana, wananchi wanawaamini. Hotuba za kampeni ni mwonekano na mantiki.
 
Chaguzi sio kuhusu ahadi tu bali jinsi gani ahadi hizo zitaandaliwa na kutekelezwa. Jukwaa ambalo kila chama kitanadi ajenda zake za uchaguzi hujengwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama husika. Yahitaji mtu kuangalia tu uzinduzi wa kampeni za za Lowassa na Magufuli. Lowassa aliongea kwa dakika 9 tu  - akiahidi, pamoja na mambo mengine, kuwaachia huru wabakaji (sio kama ninazusha hili) wanaotumikia vifungo vyao na watuhumiwa ugaidi wanaosubiri kesi zao. Bila kujali alikuwa na malengo gani wakati anatoa ahadi hizo, makosa hayo hayastahili msamaha wa rais.  Kwa upande wake, Magufuli aliongea kwa dakika 58, akielezea kwa undani ajenda za maendeleo katika nyanja za elimu, ajira, afya, ufisadi, huduma za maji, na miundombinu. Kuanzia hapo, kwa muda wote wa kampeni, mwenendo umekuwa hivyo, kwa uzito wa ujumbe kwenye hotuba zake na muda wa kuhutubia
 
Wanaohudhuria mikutano ya Dkt Magufuli huondoka katika mikutano hiyo wakiwa na matumaini na wenye nguvu. Kwa upande mwingine, wahudhuriaji katika mikutano ya Lowassa huondoka wakiwa wamekanganywa. Siku ya kupiga kura, wapigakura wanamkumbuka jinsi mgombea alivyoonekana na alivyoongea, na jinsi walivyojisikia walipomwona jukwaani. Kwa kigezo hiki, ni bora ningekuwa upande wa Magufuli.  
 
9.    Uongo, uongo na takwimu
 
Tanzania haina utamaduni wa kura za maoni kupima nafasi za wagombea katika uchaguzi. Tuna utaratibu wa muda mrefu wa kupata maoni ya wananchi katika maamuzi makubwa ya kisera – kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa, marekebisho ya Katiba, na kadhalika. Mwaka 2005, kulifanyika kura ya maoni, iliyobashiri ushindi mkubwa kwa CCM. Na kwa hakika, CCM ilishinda kwa asilimia 80. Mwaka 2010, kura ya maoni iliyoendeshwa na kampuni ya Ipsos-Synovate iliashiria kuwa idadi ya kura za CCM ingepungua hadi kufikia asilimia 61. CCM ilipinga matokeo ya kura hiyo ya maoni ikidani kuwa yalikuwa kiasi kidogo sana. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama yalivyotabiriwa katika kura hiyo ya maoni. CCM ilipata asilimia 61 ya kura zote.
 
Hivi karibuni, kura mbili za maoni zilichapishwa. Zote zilifanywa na taasisi huru zinazoheshimika. – Twaweza and Synovate-Ipsos tena- zote zikijihusisha na utafiti wa kusaka maoni. Taasisi mbili tofauti, zilizotumia mbinu tofauti za kufanya utafiti, katika nyakati tofauti, matokeo yaleyale. CCM itashinda kwa asilimia 62 ya kura zote.
 
Inaruhusiwa, na kwa yumkini ni jambo zuri, kupingana na sababu hizi tisa za kwanini CCM itashinda. Lakini namba zina tabia ya ukandamizaji. Ndio mwelekeo wa kura huwezi kubadilika. Lakini kwa kuzingatia yote yaliyokwishaongelewa kuhusu kinachodaiwa kuwa ufuasi mkubwa kwa Upinzani, basi muda huu ingetarajiwa tuwa tunajadiliana kuhusu ufuasi wa wengi kutoka Upinzani kuelekea CCM– na sio kutarajiwa ufuasi wa wengi kutoka CCM kuelekea Upinzani. Na ndiyo, kura za maoni zaweza kukosea, na tusiwekee mkazo sana.Lakini hoja hii sasa ndiyo hupendelewa zaidi na upande unaelekea kushindwa kwenye uchaguzi.
 
January Makamba ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, na msomaji wa Kampeni za CCM

TFDA NA TAASISI YA TRADEMARK EAST AFRICA (TMEA) WAZINDUA MFUMO WA UTOAJI VIBALI KWA MFUMO WA KIELEKITRONIKI

$
0
0

 Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi (kulia), akibonyeza kituvye Dar es Salaam leo asubuhi, kuashiria uzinduzi wa mfumo wa utoaji vibali kwa njia ya kielekitroniki (e-portal) ambao utawezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuhudumia wateja wake kwa kutumia mtandao wa intaneti. Mpango huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa TFDA na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA)
 Viongozi wakiwa meza kuu wakifuatilia uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Viongozi wakiwa tayari kuzungumza na wanahabari. Kutoka kulia ni Meneja wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA), Josephat Kweka,  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo.
 Maofisa Habari kutoka Kampuni ya PR ya  PPR, wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza na wanahabari.

Na Dotto Mwaibale


MAMLAKA ya Chakula na dawa nchini (TFDA), imezindua mfumo mpya wa utoaji vibali kwa mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama 'e-portal'.

Mfumo huo uliogharimu kiasi cha sh. milioni 300 kwa ushirikiano wa taasisi ya Trademark East Afrika(TMEA) kwa kutoa dola za marekani 250,000 lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao.

Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, Dk.Mkuu wa Serikali Muhammad Kambi alisema mfumo huo uliozinduliwa umekuja wakati muafaka kwani utasaiduia kuboresha huduma katika sekta ya afya kwa kuongeza uwazi, ukweli na kwa uharaka zaidi.

"Mfumo huu uliozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kudhibiti katika utoaji wa vibali vya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje ya nchi kwa kuwa wa kuandaa vibali utafupishwa na utaongeza faida katika mamlaka hiyo,"alisema.

Alisema mfumo huo utasaidia kuhudumia wateja na katika kusajili na kufuatilia ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula,dawa, vipodozi na vifaa tiba sokoni sanjari na kuongeza kiwango cha wateja katika kuzingatia matakwa ya kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo alisema mfumo huo mpya unatumiwa na watu takribani 300 ambao wamethibitisha kuwa hauna matatizo yeyote kwani lengo la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanapunguza muda wa wateja wao katika kuomba vibali ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za huduma hiyo.

"TFDA inatambua mchango wa TMEA katika kuendeleza mfumo wa e-portal ambao utarahisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na uhifadhi wa taarifa za usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za ubora na usalama wa vyakula dawa, vipodozi, vifaa tiba nchini,"alisema.  

Mkurugenzi wa TradeMark East Afrika Tawi la Tanzania, Dk. Josephat Kweka alisema mfumo huo utasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara hasa katika kuingiza na kutoa bidhaa katika soko la ushindani.

"Portal inatarajia kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Tumewawezesha portal hiyo ili kukuza biashara ya kikanda na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za jumuia za Afrika Mashariki,"alisema.


Aidha uzinduzi huo ni hitimisho la maboresho ya mfumo huo ulioanza mwaka 2011 ambapo utawawezesha wafanya biashara kuomba na kupata vibali vyote muhimu kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika ofisi za mamlaka hiyo.

MUDA WA KUONDOKA TRENI YA DELUXE KWENDA MWANZA JUMAPILI OKTOBA 25, 2015 WASOGEZWA MBELE

$
0
0

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

 Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL unachukua fursa  hii kuwaarifu abiria wa treni ya deluxe ya Jumapili Oktoba 25, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda  Mwanza kuwa muda wa kuondoka umesogezwa mbele kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku wa  siku hiyohiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo uamuzi huo umechukuliwa maalum ili kuwapa fursa Abiria waliojiandikisha kupiga kura kutumia haki yao ya kikatiba kikamilifu.


Utaratibu huu utatumika pia kwa treni kwa siku hiyo zitakazokuwa zinaanza safari zake kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam nazo zitaanza safari hizo saa 2 usiku.


Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.


Shime kila Mtanzania ajitokeze kwenda  kutumia haki yake ya kikatiba kwa kumchagua Kiongozi mwenye sera anayoiafiki.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.


Dar es Salaam,

Oktoba 21, 2015

ZANTEL YAZINDUA OFA MPYA YA MUDA WA ZIADA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akizungumza wakati wa kuzindua ofa mpya ya Kula Tano kwa wateja wa Zantel, ambayo inawazawadia wateja wao dakika za bure kwa kupokea simu zao.
  Meneja wa Zantel, Deus Mtena akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya Kula Tano katika ofisi za Zantel, Anayetazama kushoto ni Meneja wa Huduma, Ashish Singh.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akigawa vipeperushi vya ofa ya Kula Tano baada ya kuizindua katika ofisi za Zantel.

KAMPUNI ya simu ya Zantel leo imezindua ofa mpya ya kuwazawadia wateja wake dakika za ziada kila mara wanapopokea simu kutoka mitandao yote katika simu zao za mikononi.


Ofa hiyo inampa kila mteja wa Zantel dakika moja ya bure kila akipokea simu ya zaidi ya dakika nne ya ndani ya mtandao na pia atapata dakika nne za bure akipokea simu kutoka mitandao mingine kwa zaidi ya dakika mbili.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress Chissenga alisema ofa hii imezinduliwa maalumu ili kuwapa wateja wa Zantel thamani ya fedha zao pamoja na fursa ya kufurahia zaidi huduma za mtandao huo.


‘Leo tunazindua ofa mpya na ya kipekee kabisa katika soko kwa wateja wetu wa Zantel, ambayo kila mtumiaji wa mtandao wetu atazawadiwa dakika za bure kwa kupokea tu simu yake’ alisema Chissenga.


Akielezea zaidi kuhusu ofa hiyo, Chissenga alisema hakuna mtandao uliowahi kuwazawadia wateja wake kwa kupokea tu simu, na hivyo ofa hii ni ya kwanza nchini ambayo itawapa wateja nafasi ya kufurahia dakika za bure ambazo wanazoweza kupiga kwenda mitandao yote.


‘Zantel inawajali wateja wake na itaendelea kuhakikisha inakuwa zaidi ya mtandao wa simu kwa kuwapa wateja wake fursa ya kuwasiliana zaidi iwe na ndugu zao au kibiashara’ alisema Bi Chissenga.




Mwisho Bi Chissenga alisema ofa hii itakuwa mkombozi kwa wateja wasio na kipato lakini wanatumia huduma ya Zantel kwani wataweza kujipatia dakika za bure kila mara wanapopokea simu katika simu zao za mikononi na hivyo kuwawezesha kuendelea kuwasiliana na  ndugu na jamaa zao.

WATOTO 37 WAFANYIWA UPASUAJI MUHIMBILI

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya taasisi hiyo kufanikiwa kuwafanyia upasuaji watoto 37.
 Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Godwin Shirau akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matatizo mbalimbali ya moyo.
 Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Profesa Mohamed Janabi leo katika hospitali hiyo. 

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Cardiac Institute  (JKC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi mIlioni 800 baada ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto  37 wenye matatizo ya moyo .


Operesheni hiyo imefanyika kuanzia Oktoba  10 hadi 19 mwaka huu kwa kushirikisha timu ya wataalam  18 kutoka nchini Italy na  Marekani  pamoja na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasisi hiyo.


 Kaimu Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi amewaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwamba  endapo wagonjwa hao wangetibiwa nje, kila mmoja yangegharimu kati ya Dola za Kimarekai 10,000 hadi 15,000, gharama ambazo Watanzania wengi hawawezi kuzimudu.

Kwa mujibu wa Profesa Janabi,  changamoto inayowakabili ni upatikanaji wa damu  na upungufu wa watalaam.


Alifafanua kwamba hivi sasa kuna orodha ya watu 500 ambao wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo, na kwamba desemba mwaka huu, wanatarajia  kupokea wagonjwa wenye matatizo ya moyo  kutoka nchini Zambia.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto, Dk. Edwin Shiran amesema watoto 17 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na wengine 20 wamewekewa kifaa maalum kwa ajili ya kuziba matundu na kuzibua  mishipa ambayo  imezibana  na kwamba kati ya hao watoto wawili wametokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


Tangu Januari mwaka huu tayari wamekwishafanyiwa upasuaji wa moyo watoto 122 na watu wazima 132 .

IJUE NAMNA YA KUKATA RUFAA.

$
0
0
NA  BASHIR  YAKUB -
Unaposhindwa  kesi  sio  mwisho  wa kusaka  haki. Hii  ni  kwasababu  kushindwa  kesi  kunatokana  na  sababu  nyingi . Si  kweli  kuwa  kwakuwa  umeshindwa  kesi  katika  mahakama  fulani  basi  maana  yake  ni  kuwa  ulikuwa  huna  haki. Yawezekana  kabisa  haki  ilikuwa  yako  isipokuwa  umeshindwa  tu  kutokana  na  sababu  nyingine  za  kiutaratibu na  kimbinu (procedures & technicalities).  Pia  waweza  kuwa  umeshindwa  kutokana  na  uwezo  mdogo  wa  kujieleza  na kushindwa  kugusa  nukta  muhimu  ambazo  kimsingi  ndizo  zilizokuwa zinabeba   shauri  lako. 

Lakini  pia  waweza  kuwa  umeshindwa  kwasababu  ya  hila  na  mbinu  chafu. Na  hii  wakati  mwingine  huwahusisha  hata  waamuzi yaani mahakimu  na  majaji.  Basi  ifahamike  kuwa  ni  sababu  hizi   zilizopelekea  kuwepo  utaratibu  wa  rufaa  ili  yule  anayehisi  kutotendewa  haki  aende mbele  ili  kuona  kama anaweza  kupata  haki  yake  huko.


1.RUFAA  NININI.
Rufaa  ni  hatua  ya  kisheria  ya  kupeleka  malalamiko  katika  hatua  ya  mahakama  ya  juu  zaidi  baada  ya  mmoja  wa  wahusika  katika  kesi  iliyoisha  kutoridhishwa  na  hukumu/maamuzi. Ili  ukate  rufaa  ni  lazime uwe  ulikuwa  mhusika  katika  kesi  iliyoisha  na  uwe  na sababu  za  kwanini  unadhani hukuridhishwa  na  maamuzi.  Sababu  yoyote ya  msingi  inakubalika.


2.     NI  HAKI  YAKO  KUAMUA  KUKATA  RUFAA  AU  KUACHA.
Suala  la  kukata  rufaa  halitegemei hisani  ya  mahakama. Sio  upendeleo  ambao  mtu  anapewa   ili  kuendelea  kusaka  haki. Ni  haki  ya  msingi  na  ya  kisheria  ambayo  hutumiwa  na  yule  ambaye  anahisi kutotendewa  sawa   katika  shauri  la  awali  lililoisha. Pia  ieleweke kuwa  rufaa  tunazoongelea  hapa ni  zile  rufaa  katika  mashauri  ya  madai. Rufaa  katika  mashauri  ya  madai  tunaongelea  mashauri  ya  ardhi,  ndoa,  mikataba, migogoro  ya  biashara  na  mauziano  kwa  ujumla, migogoro  ya  madeni   na  yale  yote  ambayo  sio  jinai.  Kwahiyo  katika  malalamiko  ya  namna  hiyo  ni  uamuzi  wako  ukate rufaa  kwenda  mbele  au  uache  hata  kama  umeshindwa.  Hii  ni  haki  yako  na  katu  haiondolewi  na  yoyote.


3.    HATA  ALIYESHINDA  ANAWEZA  KUKATA  RUFAA.
Hapo  juu  tumesema  rufaa  ni  kwa mtu  ambaye  hakuridhishwa  na  maamuzi   ya  mahakama.  Sio  kwa ajili  ya  aliyeshindwa  bali  ni  kwa  ajili  ya  yule ambaye  hakuridhishwa. Hii  ina  Maana  kuwa  unaweza  ukashinda  lakini  ukawa  hukuridhishwa.  Na  kama  umeshinda  lakini  hukuridhishwa  pia  waweza  kukata  rufaa. Kwa  mfano  ulifungua  kesi  ukiomba  fidia  ya  milioni 50. Hukumu  ikatoka  kuwa  umeshinda  lakini  ikasema  kuwa  utalipwa  milioni  kumi tu. Kwa  mazingira  kama  haya ni  kuwa  umeshinda lakini waweza  kukata  rufaa  kudai  zaidi. Utakata  rufaa  kwakuwa  umeshinda  lakini  hukuridhishwa   na  ushindi. Kinachotakiwa  kueleweka  hapa  ni  kuwa   rufaa  inaweza  kukatwa  hata  yule  aliyeshinda  kesi  na  si  tu  kwa  aliyeshindwa.


4.     NAMNA  YA  KUKATA  RUFAA.
Mara  tu kesi  inapoisha  hakikisha  unafuatilia  na  kupata  nakala  ya  hukumu pamoja  na  tuzo( decree). Fuatilia  kwa  karani wa  hakimu/jaji  aliyesikiliza  shauri  lako na  umwambie  nia  yako  ya  kutaka  nakala  ya  hukumu  na  tuzo  kwa  ajili  ya  kukata  rufaa. Huwezi  kukata  rufaa  bila  nakala  ya  hukumu  kwakuwa   ni  lazima  uipitie  kwa  umakini  na  kuona  ni  wapi  palikuwa  na  tatizo  ili  iwe  ndio  sababu  yako  ya  rufaa.


Ikiwa  hukumu  ilitolewa  na  mahakama  ya  mwanzo  basi  rufaa  itaenda  mahakama  ya  wilaya,  na  ikiwa  ilitolewa  na  mahakama  ya  wilaya  rufaa  itaenda  mahakama  kuu  na  ikiwa  ilitolewa  mahakama  kuu  basi  rufaa  huenda  mahakama  ya   rufaa  ambayo  ni  mahakama  ya  mwisho  kiitifaki. Pia  rufaa  zinazotoka  katika  mahakama  za  hakimu  mkazi kama  ile  ya  kisutu ambazo  baadhi  huziita  mahakama  za  mkoa,   rufaa  zake huenda  mahakama  kuu pia.


Unapokuwa  unaandaa  sababu  za  rufaa  hakikisha  unamuona  mwanasheria  kwa  ajili  ya  kupitia  hukumu  na  kukusaidia  kuandaa  sababu  za  rufaa.  Hii ni kwasababu ipo  namna  ya kisheria ya  kuandaa  sababu  hizi  kwani  haziandaliwi  kama  barua.


Muda  ni  suala  la  msingi  sana  katika  kukata  rufaa. Hakikisha  pale  tu  hukumu  inatolewa  unaandika  barua  mahakamani  ya  kuomba  nakala  ya  hukumu. Hii  itasaidia  hata zile  siku  30  au  45  za  rufaa  zikipita  kabla  hujapatiwa  nakala ya  hukumu  kujitetea  kuwa  ulichelewa kwakuwa  ulikuwa  ukisubiria  nakala  ya  hukumu ambayo  uliiomba  ndani  ya  wakati  stahiki.


MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

EWE MGOMBEA, WEKEZA KATIKA KUMWENDELEZA MTOTO AKIWA MDOGO

$
0
0
Mpango kwa ajili ya watoto wadogo ipo mstari wa mbele katika vita dhidi ya umasikini. Watoto katika jamii zilizo masikini sana wamo katika hatari kubwa za kupata maradhi na utapiamlo na hawafanyi vizuri shuleni. 

Mipango jumuishi ya watoto wadogo inayolenga watoto walio masikini sana huzisaidia familia kuwa na mwanzo mzuri wa watoto wao na husaidia kupunguza pengo kati ya masikini na matajiri. Uwekezaji kwa watoto wadogo una faida mara saba na una thamani kuliko kuwekeza kwenye mipango ya kunusuru maisha ya mtoto hapo baadaye.

Wazazi fukara wapatiwe msaada wanaohitaji ili kuhakikisha kuwa watoto wao wanakuwa na mwanzo mzuri zaidi katika maisha. Msaada kwa ajili ya miradi ya kijamii ya kulea watoto na ya maendeleo na makuzi ya awali ya watoto itasaidia katika kuhakikisha kuwa watoto wanakua wakiwa na afya, wanapata lishe bora na wametayarishwa vizuri kwenda shule.

Maendeleo ya watoto wadogo yaingizwe katika muhtasari wa mafunzo kazini ya walimu. Yaanzishwe mafunzo kazini ya kitaifa kwa wote wanaohudumia watoto wadogo. Wale wanaofanya kazi katika jamii fukara wapewe kipaumbele katika mafunzo haya.

Zianzishwe kamati za kijamii katika ngazi ya wilaya na kata ambazo zitafuatilia upatikanaji wa huduma na kusaidia uboreshaji wa vituo vya kumwendeleza mtoto akiwa mdogo.

#AjendaYaWatoto

MAMA MWANAMWEMA SHEIN AKIWA KATIKA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KUZUNGUMZA NA WANAWAKE WA UWT KUWAOMBEA KURA WAGOMBEA WA CCM,ZANZIBAR.

$
0
0
Muasisi wa Umoja wa Wanawake Zanzibar Mama Fatma Karume akisalimiana na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano wa jengo la Wakorea Kibokwa Wilaya ya Kaskazini A Unguja kuhudhurika mkutano wa Mama Mwanamwema Shein na Viongozi hau wa UWT.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja.kwa ajili ya kuzungumza na Wanawake hao kuwaombea Kura Wagombea wa CCM. 
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama About Talib, akizungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja na kuwakaribisha Viongozi kuzungumza na Wanawake hao.
Makamu Mwenyekiti Mstaaf wa UWT Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, akizungumza na Viongozi wa UWT wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja na kuwataka kukipigia Kura Chama cha Mapinduzi kwa maendeleo na kudumisha amani Zanzibar kupitia Mgombea wake wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,
Kada wa CCM Bi Asha Abdalla Juma akiwasalimia Viongozi wa Umoja wa Wawanawakev Tanzania Wilaya ya Kaskazini A Unguja na kuwaomba kura kuwapigia Wagombea Ubunge Uwakilishi na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa Wanawake wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja kutumia nafasi yao kuipigia kura CCM 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Viongozi wa Umoja wa Wanawake wa UWT wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa ziara yake ya kuwaombea Kura Wagombea wa CCM. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mkorea Kibokwa Wilaya Kaskazini A Unguja. 
Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini Unguja wakimsikiliza Mama Mwanamwema Shein akitowa nasaha zake kwa Wanawake hao wakati wa mkutano wake wa kuwaombea kura Wagombea wa CCM
Viongozi wa Wanawake wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitowa nasaha zake wakati wa mkutano wake wa kuwaombea Kura Wagombea CCM na Mgombea Urais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ulioganyika katika ukumbi wa Wakorea Kibokwa Zanzibar. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI OKTOBA 22,2015

$
0
0
Kesi ya mita 200 moto, Lowasa sasa atishia kushtaki jeshi la polisi ICC. GP Hamdan awaonya waoandaa vurugu. Ni katika magaazeti ya leo Octoba 22.2015;https://youtu.be/TkIYjEUaJyw
 Yanga acha kabisa, Chipukizi Simba kutimukia Ubelgiji, Ndemla afunguka. Nyoso atafutiwa mbadala. Kwa habari hizi na nyingezo za michezo utazipata katika udondozi wa magazeti hapa Simu.tv ; https://youtu.be/yL4C4fUOPgo
 Rais Kikwete asema wanaimarisha jeshi ili kulinda mipaka ya nchi, NHIF yapania makubwa. Pata habari za kina hapa Simu.tv; https://youtu.be/eE10aUBwMHU

BALOZI MPYA WA MISRI AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kulia) akimkaribisha Balozi mpya wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf katika ofisi yake. Balozi Mpya wa Misri alikuja ofisini kwa Mhe. Waziri kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mpya wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf
Waziri Membe akishikana mkono na Balozi mpya wa Misri mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.
Waziri Membe akiangalia na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Balozi mpya wa Misri
Waziri Membe akiagana na Balozi mpya wa Misri nara baada ya zoezi la kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kukamilika

TAARIFA KUHUSU WALIOPOTEZA KADI ZAO ZA KUPIGIA KURA

$
0
0


OFISI Usambazaji na Ugavi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Eliud Njaila akiwaonyesha waandishi wa habari vizimba vya kupigia kura siku ya uchaguzi. 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote siku ya Jumapili.

Akizungumza katika mkutano wa vyama vya siasa na NEC mjini Dodoma leo, Ofisa Mwandamizi wa tume hiyo William Kitebi, amesema watu hao hawataruhusiwa hata kama majina na taarifa zao zipo kwenye Daftari la Wapiga Kura (BVR).

“Hakuna jinsi ya kuwasaidia watu waliopoteza kadi zao za kupigia kura ,”amesema Kitebi
Hata hivyo, Kitebi amesema kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye BVR  kuna baadhi ya mambo NEC wameyawekea utaratibu ili watu waweze kupiga kura.

Amesema watu ambao namba za kadi zinatofautiana na zile zilizopo kwenye BVR  lakini taarifa nyingine ni sahihi wataruhusiwa kupiga kura.

“Kuna wale ambao picha zao hazionekani kwenye daftari lakini kadi za kupiga kura wanazo, hawa wataruhusiwa kupiga kura,”amesema.
Kuhusu wale wapiga kura walioathiriwa na mipaka ya utawala, Kitebi amesema maamuzi ya tume kuwa watu hao watapiga kura kwenye kata walizopo.

“Kuna maeneo kulikuwa na mabadiliko ya mipaka ya kiutawala baada ya zoezi la uandikishaji kama Kishapu (Shinyanga) na Kaliuwa (Tabora), wao wataruhusiwa kupiga kura kwenye maeneo yao mapya,”amesema.

Kwa upande wa wapiga kura ambao wanakadi za kupigia kura lakini hawaonekani kwenye BVR, Kitebi amesema hao wamewekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura.


“Kama kule Mbarali (Mkoa wa Mbeya), kuna watu kama 6,000 ambao hawaonekani katika daftari lakini wanakadi na fomu zao zimejazwa na kuwasilishwa tume  hawa wanaruhusiwa kupiga kura,”amesema.

MAKAMU WA RAIS DKT. AGANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Saz Salula, akizungumza kutoa shukurani wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya Mhe. Makamu wa Rais kuagana na Watumishi wa Ofisi yake. Hafla hiyo ilifanyika juzi Okt 20, 2015 kwenye Makazi ya Dkt. Bilal
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Saz Salula, wakati wa hafla fupi ya kuagana na watumishi wa ofisi yake, iliyofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi Okt 20, 2015.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watumishi wa Ofisi yake (baadhi hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi Okt 20, 2015.

 Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakimsikiliza Dkt.Bilal, wakati alipokuwa akizungumza kwenye Hafla hiyo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi yake baada ya hafla hiyo.
 Picha na OMR

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewashukuru watumishi wa ofisi yake kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha miaka mitano kiasi cha kuweza kutekeleza majukumu ya msingi ya ofisi hiyo ya kudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira kwa ufanisi mkubwa.

Akizungumuza katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema kuwa, anayo furaha kufikia kipindi hiki na kwamba alifanya majukumu yake vema kutokana na kuwa na wasaidizi mahiri na waliojitoa kufanya kazi zao kwa weledi na uvumilivu mkubwa muda wote.

“Natumia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote. Walinisaidia sana katika kipindi nikifanya kazi ya kuitumikia nchi yangu. Niwashukuru ninyi wafanyakazi wa ofisi yangu, mlifanya kazi kwa kujituma sana na majukumu yetu kwa mujibu wa taratibu tuliyatekeleza kwa ufanisi,” alisema 

Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza:
“Nakutakieni kila la kheri katika utendaji wenu. Jitahidini kufanya kama mlivyofanya kwangu kwa yule atakayekuja baada yangu. Nakushukuruni kwa zawadi hasa ya vitabu maana mimi ni muumini wa kusoma, nitavisoma”.

Dkt. Bilal aliwaambia watumishi hao kuwa ushirikiano waliompa katika utendaji wa kazi umewezesha  kuzipatia ufumbuzi hoja mbali mbali za muungano na kusema hoja zilizobaki zinafanyiwa kazi na zitapatiwa ufumbuzi katika serikali ijayo.

Hoja ambazo zipo katika hatua mbalimbali za kutafutiwa ufumbuzi ni pamoja na Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na Faida ya Benki Kuu; Usajili wa vyombo vya moto, Uchimbaji na Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asili na Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya fedha.

Kwa upande wa mazingira alisema katika kipindi chake Tanzania ilipata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Masuala ya Mazingira kwa viongozi wa Bara la Afrika jambo ambalo limewezesha nchi kutoa mchango mkubwa katika suala zima la uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika Bara la Afrika.

Hata hivyo, Dkt. Bilal alionyesha wasiwasi wake katika eneo la usafi wa mazingira na kuwataka watumishi wa ofisi hiyo kushirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha usafi wa mazingira unapewa kipaumbele katika maeneo yote nchini.

Mapema, akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula alimshukuru Makamu wa Rais kwa uongozi wake ambao umekuwa mwongozo kwa watumishi katika utendaji wao wa kazi na kumtakia kila la heri katika kipindi cha kustaafu kwake.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam.

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 22, 2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Asubuhi Hii October 22, 2015.

SIMUtv: Fuatilia mwenendo na uchambuzi wa kampeni za vyama mbalimbali za lala salama baada ya kusalia masaa 48 kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka  huu

SIMUtv: Katibu wa chama cha madereva TADU, Rashid  saleh akizungumzia vitendo vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuwaadhibu madereva: https://youtu.be/ne2li6v5HN8

SIMUtv: Tambua namna ambayo Nchi imejiandaa kulinda amani siku ya uchaguzi zikiwa zimesalia takribani masaa 48 kuifikia siku hiyo maalumu: https://youtu.be/dK2fdWR1jS0
  
SIMUtv: Fuatalia mazungumzo na viongozi wa dini wakihamasisha amani  katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu ikiwa zimesalia siku 2: https://youtu.be/-JyP0slzlIc
  
SIMUtv: Fuatilia vipaumbele vinavyotiliwa mkazo zaidi na mgombea udiwani kata ya Mwananyamala jijini Dar es salaam kupitia chama cha ACT https://youtu.be/61OyRSbdgEI

SIMUtv: Mamlaka ya Chakula Na Dawa TFDA imezindua mfumo mpya wa utoaji na usajili wa vibali kwa njia ya kieletroniki.   https://youtu.be/EKpX7i9iUpg
   
SIMUtv: Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kesho itatoa maelekezo maalumu juu ya Madai Ya Upinzani  kukaa Mita 200 kusubiri matokeo. https://youtu.be/NniBsA0A4uA
  
SIMUtv: Mgombea Uraisi CCM Bi. Samia Suluhu awaahidi wananchi wenye ulemavu kushirikiana na serikali katika shughuli za kimaendeleo. https://youtu.be/YpieDVjInjo

 SIMUtv: Serikali imesema itaimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kabla, wakati na baada ya uchaguzi utakaofanyika oktoba 25. https://youtu.be/MIxU_FaGfQs
  
SIMUtv: Mgombea Uraisi CHADEMA Mhe. Edward Lowassa aahidi kurudia upya mchakato uliotumika kubadili matumizi ya Fedha kwa ajili ya kuboresha bandari ya Tanga. https://youtu.be/pN50aOZzqr8
  
SIMUtv: Mgombea Uraisi CCM Dkt. Magufuli amewaahidi wananchi wa Dar es Salaam kushughulikia mradi mkubwa wa maji na kuondoa kero hiyo. https://youtu.be/-Zb1ocoEOjo



SIMUtv: Siku 3 zimesalia kabla ya uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani  kufanyika  lakini kasi ya wananchi yaelekezwa katika Wagombea Uraisi pekee https://youtu.be/AGUCEprc9pc

KIJANA EDIMUND JOSEF ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

$
0
0
FAMILIA ya Josef Antoni Mloka inatangaza kupotelewa na kijana wao Edimund Josef (Pichani) mwenye umri wa miaka 23 mara ya mwisho aliondoka nyumbani  Julai 3 mwaka huu akiwa amevaa fulana ya rangi ya kijani na modo ya jinsi ya rangi ya bluu tangu siku hiyo tunamtafuta bila mafanikio.
Edimund Josef ni mrefu wa wastani kwa rangi ni maji ya kunde anaupungufu wa akili alikua anaishi Kimara Bonjokwa kwa Mashiringi mtaa wa mjumbe Ally Wila jijini Dar es Salaam. 

Amesoma shule ya Msingi Ukombozi-Mazese alimaliza shule hiyo 2007.


Kwa yeyote atakaye muona sehemu yoyote ile  (Hata kama kwa mtu kwa jirani, jalalani, au akiokota takataka au akiombaomba) tunaomba atoe taarifa kituo cha Polisi cha Urafiki, pia kituo cha Polisi cha Stakishari Ukonga,au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu nawe.

Au unaweza kuwasiliana na Baba mzazi wa kijana huyo Josef Antoni kwa simu namba 0654790019 Au kaka yake Felix Josef  kwa namba 0657536219.

TUNAOMBA USHIRIKIANO WAKO.

WAZIRI MEMBE AAGANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akifungua hafla ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe iliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akitoa muhtsari wa shughuli chache ambazo Waziri Membe alizisimamia kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 9 ya Uwazi wa Mambo ya Nje. Waliokaa ni Mhe. Membe na Balozi Mulamula ambao wanasikiliza kwa maikini shughuli zilizotekelezwa na Mhe. Waziri Membe.
Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akitangaza Tuzo na Zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kwa ajili ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri na Wenza wao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Tuzo ya Uongozi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na kukabidhiwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula
Waziri Membe akifurahia zawadi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje.
Waziri Membe akipokea zawadi kwa niaba ya Mama Membe ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo. Bi. Amisa Mwakawago, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu alikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Wizara.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Karim Taj naye akikabidhi zawadi kwa Mhe. Waziri kwa niaba ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya akipokea zawadi kwa niaba ya Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo kutokana na majukumu ya kitaifa.
Balozi Mulamula na Mama Mwakawago wakionesha zawadi ya Mama Mahadhi Juma Maalim.
Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakishuhudia zoezi la utoaji wa zawadi.
Waziri Membe akiongea na watumishi wa Wizara wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy naye akiongea machache katika hafla hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko akionekana mtu mwenye furaha katika hafla hiyo, baada ya kutangazwa kuwa ameteuliwa kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda. Wengine waliotangazwa kuwa Naibu Mabalozi ni Bi. Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Afrika Kusini na Bw. Andy Mwandembwa, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Itifaki ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Sweden.
Wakati wa maakuli. Mhe. Waziri akiwa ameshikilia sahani ya chakula na anyemfuatia ni Katibu Mkuu anayeonekana akichota chakula
Naibu Katibu Mkuu naye anajichotea chakula
Waheshimiwa Mabalozi nao wanajichotea chakula
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Idara/Vitengo
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara/Vitengo.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Waziri na Naibu Waziri.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi Wanawake.

BEI YA MADAFU HII LEO

KAMATI YA STARS YATOA NAMBA ZA UCHANGIAJI

$
0
0
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Akizungumza na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015

BENKI YA EXIM YAANDAA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KWA WATEJA WAKE MTWARA

$
0
0
 Mkuu wa Hazina Benki ya Exim Tanzania Bw. George Shumbusho (Kushoto) pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya STE BPS (COTE DIVOIRE) S.A LTD Bw. Vijayan Vetharethinam kwa pamoja wakifungua shampeni wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake Mkoani Mtwara hivi karibuni.
Mkuu wa Hazina Benki ya Exim Tanzania Bw. George Shumbusho (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na  Bw. Anoop Kumar  pamoja na  Bw  Prasoon kutoka kampuni ya Regal Holdings Ltd wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake Mkoani Mtwara hivi karibuni. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko Msaidizi wa Benki hiyo Bw.  Abdulraham Nkondo (kushoto) na Meneja Msaidizi Mauzo Hazina, Bi Glynis Stambuli (kulia).
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images