Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE ALIKABIDHI JESHI LA POLISI MAGARI MAPYA 399 KATI YA 777 YALIYOAGIZWA

$
0
0


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe, IGP Ernest Mangu wakati akikagua sehemu ya magari mapya 399 kati ya 777 aliyokabidhi kwa jeshi la polisi leo Jumanne Oktoba 20, 2015 huko katika Chuo cha Polisi Kurasini Dar es salaam.
 PICHA NA IKULU

NYOTA NA ING'AE MAGUFULI - MSECHU

MASHALI AMDUNDA BIGRIGHT NA KUMPORA SIMU NA PESA

$
0
0

Bondia Thomas mashale wa manzese jijini Dar es salaam alifanya kitendo cha kusikitisha na kushangaza umma katika ukumbi wa friends corner uliopo Manzese ,pale alipomvamia katibu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe (bigright) kumpiga na kumpora simu na pesa. Akizungumza na vyanzo habari hizi Ibrahim kamwe alisema.”Nilikuwepo ukumbini  hapo friends corner nikishuhudia mpambano wa Jonas Segu na idd Pearali kwa kuwa watu walikuwepo ni wengi mno na pale mbele kulikuwa na fujo za ushangiliaji  nikaona ni bora nirudi nyuma kabisa ili nishuhudie kwa mbali , ghafla alitokea bondia huyo Thomas mashali akiwa na wenzake wanne akanishika mikono na wenzake kuanza kunisachi nilimputa mikono ili nizuie mifuko ndipo aliponipiga ngumi kali ya kidevuni na kichwani, watu walio karibu walipotugeukia sisi mashali na wenzake waliondoka haraka na kutokomea na simu yangu na kipochi  akiniacha na maumivu ya kidevu.

Nilichokifanya ni kuripoti polisi na kupewa PF3 na RB ili sheria ifuate mkondo wake.

Watu wengi waliokuwepo hapo ukumbini walisikitishwa na vitendo vya  bondia huyo kwa kuwa na matukio kama hayo mfululizo bila kujali anaowafanyia ni kina nani kwani hivi karibuni alimzuia kiongozi aliyekuwa akisafiri na bondia said mundi kuelekea nchini Thailand kwa kumshikia chupa na wenzake wakiwa na visu na kuwapora simu na pesa, bondia huyo wa tanga said mundi na Anthony ruta walikuwa wapole kwani tukio hilo alilifanya muda mchache kabla ya kuelekea airport.


Thomas mashali ni mwingi wa matukio kama hayo hasa maeneo ya manzese aliapa kujirekebisha kwa tabia hizo za ukabaji  lakini inaonekana amerudi kivingine sasa hata kwa watu anaowajua. Anafuatiliwa ili sheria ishike mkondo wakee 

MAOFISA WA TAASISI YA STEP1 YA KOREA WAPATA MAFUNZO YA UENDESHAJI MITAMBO TBL

$
0
0
 Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin (wa pili kushoto), akiwaonyesha Watafiti kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojkia na wageni kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea, mitambo mipya ya kuzalisha bia, walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam jana kujifunza kuhusu uendeshaji na aina ya mitambo.
 Maofisa kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wageni wao kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw Calvin Martin )wa pili kulia), walipofika kiwandani hapo Dar es Salaam jana kujifunza kuhusu uendeshaji wa kiwanda, aina ya mitambo na ushirikiano na taasisi zingine. Kulia ni Meneja Usalama wa TBL, Bw. Renatus Nyanda.
 Maofisa wa TBL, Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia na Sayansi wakiwa katika picha ya pamoja.

 Mkuu wa Kitengo cha Utafiti Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Rafael Kibunda (kulia), Mtafiti kutoka Wizara hiyo, Profesa Rogers Msuya (kushoto) na Maofisa kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea, wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin, walipotembelea kiwanda hicho Dar es Salaam jana kwa ajili ya kujifunza kuhusu uendeshaji wa mitambo. (Na Mpigapicha Wetu)
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin (aliyenyoosha mikono), akifafanua jambo, wakati akiwatembeza maofisa kutoka WIzara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Profesa Rafael Kibunda (wa pili kushoto), Mtafiti Profesa Rogers Msuya (Kulia) na Profesa Hyunho Kim (kushoto), kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea.

SMZ YAIPONGEZA UN KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KIMAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
IMG_9022
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Alisema kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.
Waziri Haroun alifahamisha kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na umoja huo imekuwa nyenzo muhimu ya kuisaidia serikali kuhudumia wananchi wake kwa ufanisi zaidi.
Alisema kutokana na misaada hiyo Zanzibar pia imekuwa mdau muhimu wa umoja huo kwani ni miongoni mwa nchi yenye urithi wa kimataifa kupitia maeneo ya Mji Mkongwe jambo ambalo ni ishara tosha ya mahusiano mema kati ya umoja huo na serikali.
IMG_9075
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar wakibadilishana mawazo wakati wa kuwasili kwa wageni waalikwa kwenye sherehe hizo.
“ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajali kwa kiasi kikubwa juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kutuunga mkono, nasi tunaendelea kutumia vizuri miradi mnayotuunga mkono.

Pia tunaendelea kukuombeni mtusaidie pale tutakapohitaji msaada wenu kwa Nyanja tofauti kwani bajeti ya serikali haitoshi kukidhi mahitaji yote ya kuendesha serikali.”, Alisema Waziri Haroun.

Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alikiri kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya umoja huo na kuahidi kuendelea kushirikiana vizuri na serikali ili kufikia dhana ya maendeleo endelevu Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

Bw. Rodriguez alibainisha kuwa umoja huo bado unaendelea kufanya tathimini na utafti juu ya masuala mbali ya kisiasa na kijamii nchini ili kuona ni kwa jinsi gani watasaidia kuunga mkono maeneo hayo kwa maendeleo ya nchi.

Alifafanua kuwa katika miradi mbali mbali iliyotekelezwa Zanzibar kupitia mashirika ya Umoja huo hasa UNDP, UN WOMEN na UNESCO miradi hiyo imeweza kufanikiwa zaidi ya asilimia 80 jambo ambalo ni faraja kwa umoja huo.
IMG_9170
Kila mtu alikuwa na tabasamu la furaha....Happy Birthday #UN70
Alieleza kuwa kupitia dhana ya maendeleo endelevu kwa mwaka 2016 umoja huo umejipanga kusaidia masuala mbali mbali ya haki za binadamu, utawala bora, uwazi na uwajibikaji, afya na vipaumbele vya kisera kwa serikali ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa ni nchi ya kupigiwa mfano kimaendeleo.

“ Tuna kila sababu za kuishukru serikali ushiriki wake katika miradi yetu kwani bila wao kutuunga mkono vizuri leo hii tusingweza kuwepo hapa kusherekea mafanikio tuliyopata ndani ya miaka 70 ya UN hivyo nasi tunaahidi kuenzi mahusiano haya kwa lengo la kujenga jamii bora.”, alisema Bw.Rodriguez.

Aidha aliishauri serikali kuhakikisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unafanyika kwa amani na kwa kuzingatia vigezo vya uwazi, uhuru na haki ili kila chama kilichoshiriki katika mchakato huo kinapata haki yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
IMG_9044
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga.


“ Tunawatakieni uchaguzi mwema na wenye mafanikio bila ya kuwepo dalili za uvunjaji wa haki za binadamu ama kiashiria chochote cha vurugu ili muendelee kulinda heshima na mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).” alisisitiza Bw. Rodriguez.

Sherehe hizo za kutimiza miaka 70 za UN zilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena Mjini Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbali mbali wa umoja huo wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Zanzibar na kutoa Tuzo na vyeti vya kumbu kumbu kwa taasisi na shule zilizoshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya umoja huo.
IMG_9494
Ofisa anayeshughulikia masuala ya ushirikiano wa WHO Zanzibar, Dkt. Ghirmay Andemichael (kushoto) akibadilishana kadi na mmoja wa wageni waalikwa (ambaye jina lake halikuweza kupatikana kirahisi).
IMG_9166
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kushoto) akifurahi jambo na Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman.
IMG_9314
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakizindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
IMG_9317
IMG_9327
Fataki zikipamba uzinduzi huo, sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_9368
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja huo.
IMG_9352
Baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Dar na Zanzibar wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakati akitoa salamu za UN katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9397
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9407
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifanya 'Toast' katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9408
IMG_9418
'Toast' hiyo iliambatana na milipuko ya Fataki kusherehesha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake. 

FAMILIA YA DK. MAGUFULI YASEMA WATANZANIA WAMEPATA KIONGOZI MCHAPA KAZI, MWENYE MSIMAMO NA MPENDA MAENDELEO

$
0
0
 
Kiongozi wa familia hiyo, Albert Michael, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita.

Na Rashid Zahor, Geita.
FAMILIA ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli imesema Watanzania watakuwa na bahati ya kumpata kiongozi mchapakazi, mwenye msimamo na anayependa maendeleo.

Imesema iwapo Dk. Magufuli atachaguliwa kuwa rais, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii, atawaletea maendeleo makubwa kwa kuwa ni mtu mwenye msimamo, asiyeyumba na anayependa maendeleo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na kiongozi wa familia hiyo, Albert Michael, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita.

Mzee Albert hakuwepo Katoma juzi wakati msafara wa Dk. Magufuli uliposimama kwa muda nyumbani kwa babu yake, ambako alipata nafasi ya kuzuru kaburi lake na la bibi yake mzaa wa baba na kuwaombea dua.

"Watanzania wasiwe na wasiwasi, Magufuli ni mtu anayependa watu na maendeleo na ni mchapakazi,"alisema Mzee Albert, alipokuwa akijibu swali kuhusu sifa za mgombea huyo tangu alipokuwa mtoto.


Aidha, Mzee Albert alisema Dk. Magufuli si mpole, sio mkali sana, lakini ni mtu mwenye msimamo na asiyeyumba katika jambo analotaka kulifanya.
Mzee Albert, ambaye ndiye aliyeachiwa mji wa Katoma kwa sasa, liliko chimbuko la ukoo wa Dk Magufuli, akiwa miongoni mwa wadogo zake marehemu baba mzazi wa mgombea huyo, alisema familia yao ipo pamoja naye na inamuombea Mungu aweze kutimiza dhamira yake ya kuwa rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Ninachowahakikishia Watanzania ni kwamba Oktoba 25, watampata kiongozi bora, asiye na ubaguzi wa aina yoyote,"'alisema mzee huyo.
Akizungumzia majina ya mgombea huyo, alisema jina la Pombe alipewa na bibi yake siku alipozaliwa, kwa kuwa siku hiyo alikuwa akipika pombe. 

Alisema jina la Magufuli lilitokana na kupenda kwake michezo.
"Siku John alipozaliwa, bibi yake alipopelekewa taarifa, alisema 'huyo mume ni mume wangu aitwe pombe'," alisema mzee huyo, ambaye alifika Geita juzi usiku akitokea Chato.

Juzi, Dk. Magufuli alitembelea kwenye makaburi ya babu na bibi yake mzaa wa baba, eneo la Katoma, wilayani Geita Vijijini na kufanya ibada ndogo ya kuwaombea dua.

Dk. Magufuli alifika nyumbani kwa babu yake saa 6.30 mchana na kupokewa na baba yake mdogo, Sylvestr Magufuli, kabla ya kupelekwa kwenye makaburi hayo, ambako aliongoza ibada ndogo ya kuwaombea dua.
Akizungumza kwenye eneo hilo, baba huyo alisema makaburi hayo ni ya babu na bibi wa mgombea huyo pamoja na ndugu zake wengine, waliofariki dunia miaka mingi iliyopita.

Alisema asili ya ukoo wa Dk. Magufuli ni Katoma, ambako ndiko baba yake alikozaliwa kabla ya kuhamishia makazi yake Chato.

"Tumezoea kumuona ndugu yetu kwenye tv na kumsikiliza kwenye redio, leo tumefurahi kumuona yeye mwenyewe,"alisema na kuongeza kuwa wanamuombea dua kwa Mungu ili aweze kuchaguliwa kuwa rais.

Kwa upande wake, Dk. Magufuli alisema alifarijika kufika tena katika eneo hilo kwa sababu ndiko alikozaliwa na kukulia na pia ndiko ukoo wake ulikoanzia.

Dk. Magufuli alitumia fursa hiyo kuwatambulisha ndugu zake kwa wanahabari kabla ya kuingia kwenye nyumba ya familia, iliyoko umbali wa mita 30 kutoka barabara itokayo Kamanga kwenda Sengerema.

Mgombea huyo alisema jina la Pombe alipewa na bibi yake, aliyemtaja kwa jina la Anastazia, siku alipoivisha pombe yake.

Alisema babu yake, marehemu Michael, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 103 baada ya kumuuguza kwa muda mrefu akiwa Dar es Salaam na baadaye kumrejesha Katoma.

"Kwangu siku hii ni ya pekee. Nilipojua kwamba nitasafiri kwa kutumia njia hii, niliona ni lazima nipite hapa kwa sababu ndiko maisha yangu yalikoanzia,"alisema Dk. Magufuli na kusifu maendeleo yaliyopatikana katika kijiji hicho, ikiwemo nishati ya umeme.

Aliwaomba wakazi wa kijiji hicho wamuombee dua kwa Mungu ili aweze kushinda kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, unaotarajiwa kufanyika nchi nzima Jumapili.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI OKTOBA 21,2015

$
0
0
  Majimbo kumi ya kufa au kupona kati ya CCM na CHADEMA. Masha akamatwa tena.Yote haya utayapata katika magazeti ya leo;  https://youtu.be/he5sNUP8L1A

Magufuli kutikisa Dar kwa siku tatu. NEC yasema kukusanyika mita 200 ni hujuma na kwamba kutazua hofu kwa wapiga kura; https://youtu.be/1cf2IYpQLjU

Mchungaji afungwa kifungo cha maisha kwa kumbaka mwanae. Wataalam wasema ni vigumu chopa kulipuka ;  https://youtu.be/XPE-WhIy80E

Simba ,Yanga vitani leo, Kiiza mchezaji bora September. MO yaitaka Simba kwa Bil.20. Pata habari za michezo katika magazeti ;  https://youtu.be/DdCCFWuu-ow

 Mbowe anena mazito katika mazishi  wa Dr.Makaidi.Pata habari kutoka magazetini zilizopewa kipaumbele kwa siku ya leo;https://youtu.be/JgWToCo-FNo

MAHAKAMA YA WILAYA YA ILALA IMEMUHUKUMU KIFUNGO CHA MAISHA JELA MCHUNGAJI WA KANISA LA TANZANIA

$
0
0
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu kifungo cha maisha jela Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Athanas Ngomai (30), baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 15.


Pia, mahakama hiyo imetaka mchungaji huyo amlipe fidia ya Shilingi  milioni 2 mlalamikaji ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbondole iliyoko Ukonga. 

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Ngomai alianza kumbaka mtoto huyo akiwa na umri wa miaka kumi na moja, wakati huo akisoma darasa la tatu.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Ilala, Saidi Mkasiwa alisema Mahakama imemtia hatiani mchungaji huyo baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watano uliotolewa mahakamani hapo akiwamo daktari.

Alisema kutokana na ushahidi huo, upande wa mashtaka ulithibitisha shitaka hilo pasi kuacha shaka, hivyo anamtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wake. “Mahakama yangu inakutia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wako, utatumikia kifungo cha maisha jela ili liwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia mbaya kama yako, pia unatakiwa kumlipa fidia mlalamikaji ya Sh2 milioni,” alisema.

Kabla ya hukumu kutolewa, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwani alitakiwa kuwa mfano bora kwa jamii.

Hata hivyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea.
Mchungaji huyo aliiomba mahakama itende haki kwani yeye hajui sheria na kosa hilo limetengenezwa halina ukweli wowote.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani hapo, mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 21, mwaka 2008 katika eneo la Mbondole, Ukonga wilayani Ilala, Dar es Salaam.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo alianza kumbaka mtoto wake huyo akiwa na miaka kumi na moja.

UNAFAHAMU NANI ALIANZA KUFUGA MBWA NA ALIKUA AKIISHI WAPI?

$
0
0
Mbwa 
Watafiti wanakubaliana mbwa wamekuwa wakitumiwa na binadamu kwa miaka 15,000,Utafiti mpya unaonyesha kuwa Mbwa walianza kufugwa kwa mara ya kwanza katikati mwa bara Asia.


Watafiti hao walichunguza chembe za msambojeni (DNA) za aina 165 ya mbwa, kutoka mataifa 38 katika kile wanachosema ni utafiti mkubwa zaidi, kuwahi kufanyika duniani kuhusiana na uzao wa mbwa.

Utafiti huo unasema kuwa Nepal na Mongolia ni maeneo ya kwanza kabisa ambapo mbweha walianza kuwa marafiki wakubwa wa binadamu, lakini haijasema ni lini tukio hilo lilifanyika.

Kuna dhana nyingine kuwa mbwa walianza kufugwa kwa mara ya kwanza kusini mwa Uhina, bara ulaya, Siberia, au Mashariki ya Kati, yapata miaka elfu kumi na mitano iliyopita.




Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa kwenye toleo la hivi punde la jarida la Proceedings of the National Academy of Sciences, linalochapishwa nchini Marekani. 

WAJENGEENI VIJANA UWEZO WA KUJITEGEMEA-MASAJU

$
0
0
Wanafunzi wakiwa katika pozi na vyeti pamoja na vikombe walivyo zawadiwa.


WALIMU na viongozi wa shule mbalimbali nchini wamekumbushwa kutoa elimu itakayowajengea uwezo wanafunzi kujitegemea mbali na elimu ya nadharia na vitendo darasani pekee.

Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa serikali, Bw. George Masaju alipokuwa akiongea wakati wa mahafali ya 8 na maadhimisho ya miaka 10 ya shule ya Patrick Mission High School jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Bw. Masaju ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kidato cha nne, alisema elimu hiyo ya kujitegemea itawasaidia vijana kujiamini na kupambana katika soko la ajira au kujiajiri wenyewe katika shughuli halali za kuwaingizia mapato.

Alisisitiza pia umuhimu wa kuwafundisha vijana kukua katika mila, tamaduni na maadili bora ya kitanzania kwa ajili ya kudumisha uwepo wa ustawi katika taifa.

“Wafundisheni vizuri historia ya nchi yetu na umuhimu wa kuwa wazalendo wa nchi hii,” alisema Bw. Masaju na kuongezakuwa ‘hakuna taifa lolote duniani lililowahi kuendelea na kuwa na nguvu kubwa kiuchumi na kiutawala ikiwa wananchi wake hawana uzalendo.’

Awali katika taarifa ya shule hiyo ilielezwa kuwa hadi sasa, shule imeshasomesha wanafunzi 100 ambao ni yatima na kila darasa lina yatima wawili.

Bw. Masaju aliipongeza shule hiyo kwa moyo wake wa kusomesha watoto yatima, kwani bila msaada huo, wasingepata elimu.

Miongoni mwa watu aliowashukuru kwa kutoa msaada wa elimu kwa yatima ni Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Jakaya Kikwete ambaye juhudi zake kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pia amekuwa akisaidia shule hiyo.

“Nawaomba watu wengine na taasisi mbalimbali ziendelee kuwasaidia ndugu zetu hawa,” alisema.

Katika sherehe hizo, pia palikuwa na harambee kwa ajili ya kuwasaidia yatima kuweza kupata elimu.

Akitoa ushauri kipindi hiki cha uchaguzi, alisema moja ya mambo yanayoweza kusaidia kutunza amani ya nchi ni kuzingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza uchaguzi.

“Hakuna jambo lolote la umma linalofanywa au kutekelezwa pasipo kuwekewa taratibu za kisheria,” alifafanua.

Alisema ndio maana kutokana na masharti ya sheria mbalimbali, wananchi baada ya kupiga kura wanapaswa kurejea katika makazi yao kusubiria matokeo yatakavyokuwa yanatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupitia wasimamizi wa uchaguzi au na Tume yenyewe kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi inakataza katika kifungu chake cha 104 kufanyika kwa mikutano au mikusanyiko siku ya uchaguzi au kufanya mikutano ndani ya umbali wa mita 200 kutoka katika kituo cha kupigia na kuhesabia kura.

Alitumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa viongozi wa dini kuwashauri waumini wao kuitii serikali inapokuwa inatekeleza jukumu lake la kusimamia amani, usalama na utengamano katika nchi.

Mmoja wa wazazi katika hafla hiyo, Bw. Ezekiel Marwa aliwataka watoto waliohitimu kutojiingiza katika makundi ya madawa ya kulevya na ulevi.

NHIF YAENDELEA NA MPANGO WA KIKOA.

$
0
0
????????????????????????????????????Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani wa NHIF (katikati), akizungumza na wanachama wapya wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango wa KIKOA (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo kuwakabidhi kadi ya uanachama wapatao 25 wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango mpango wa KIKOA (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi YETU MICROFINANCE PLC, Bw.Altemius Millinga, (watatu kulia) Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Bw. Eugen Mikongoti. hafla hiyo ilifanyika Yombo Dovya Oktoba 20, 2015 Jijini Da es Salaam.
????????????????????????????????????Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya YETU MICROFINANCE PLC, Bw.Altemius Millinga (kushoto), akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Wanachama wapya wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango wa KIKOA wakifuatilia mada mbalimbali wakati hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani wa NHIF akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango wa KIKOA, Mwanachama mpya, Bi. Asha Juma mkazi wa Mzizima (ILALA) Dar es Salaam.

????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani wa NHIF akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango wa KIKOA, Mwanachama mpya, Bi. Lucer Kimamba mkazi wa Mbagala.
????????????????????????????????????
Maofisa kutoka NHIF wakiwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????Wafanyakazi kutoka YETU MICROFINANCE PLC.
????????????????????????????????????
Picha ya pamoja

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 21, 2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Asubuhi Hii October 21, 2015.

SIMUtv: Tanzania imetajwa kutofanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wazee katika Nyanja mbalimbali hususani Afya na Mazingira. https://youtu.be/cnYXI1-elnI

SIMUtv: Rais Jakaya Kikwete ameliagiza Jeshi la Polisi nchi kufanya kazi  kwa weledi ili kuhakikisha Taifa linamaliza uchaguzi Mkuu wa Amani na utulivu https://youtu.be/ktVuerobzYY

SIMUtv: Mgombea Urais CCM Dkt. John Magufuli awaondoa hofu wakulima wa zao la Pamba na kuahidi kuongeza bei ya zao hilo kwa wanunuzi. https://youtu.be/L2PB7R2F41c

SIMUtv: Serikali visiwani Zanzibar Imeyakaribisha makampuni toka mataifa Mbalimbali kuwekeza mitaji katika mji wa Fumba ili kutoa fursa za ajira kwa Vijana https://youtu.be/CJSDknBLDHk

SIMUtv: Mamlaka Ya chakula na Dawa TFDA kanda ya ziwa imeharibu bidhaa bandia za Pombe aina ya Viroba zenye thamani ya zaidi ya Mil. 80. https://youtu.be/rwz7ek0zWNk

SIMUtv: Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora awataka wakazi wa wilaya hiyo wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa Kuwa Hali ya ulinzi imeimarika. https://youtu.be/sOIK46Lp-3E

SIMUtv: Ligi kuu Tanzania bara yasimamishwa kwa muda na kupisha maandalizi ya timu ya taifa katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia;  https://youtu.be/hkGFA9Hs-e0

SIMUtv: Nyota wa kimataifa wa timu ya taifa ya Nigeria Emanuel Eminike atangaza rasmi kustaafu kuchezea timu hiyo;https://youtu.be/UMYdQynkcbQ

SIMUtv: Wakazi wa kijiji cha bendera wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Wameombwa kuweka kando tofauti zao za kisiasa katika kujadili mgogoro wa Mpaka. https://youtu.be/vepp3pVgclU

WADAU WA AMANI MKOA WA SHINYANGA WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUDUMISHA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI

$
0
0
Hapa ni katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga ambako jana Jumanne,Oktoba 20,2015,wadau mbalimbali wa amani mkoani Shinyanga wamekutana kwa ajili ya majadiliano ya ushirikiano wa kudumisha amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.Kikao hicho kimeandaliwa na uongozi wa mkoa wa Shinyanga likiwemo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Save The Children linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto.

Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa. Fuatilia matukio katika picha hapa chini-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blogMgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu siku ya uchaguzi.Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ofisi yake imepata taarifa kuwa kuna baadhi ya wagombea wanatembea na silaha za moto,mapanga,manati na kufundisha vijana mbinu za kuvunja amani siku ya uchaguzi.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisisitiza kuwa watu wote waliojiandikisha wana haki ya kupiga kura Oktoba 25,2015 na kuwataka baadhi ya watu wanaojipanga kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura kuachana na wazo hilo na badala yake waendelee tu shughuli zao na wakati muda wa kutangazwa matokeo ndiyo warudi vituoniWadau wa mkutano huo walisisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura kisha kuendelea na shughuli zao Oktoba 25,2015 badala ya kukaa mita 200/300 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura kwa vile kila chama kitakuwa na wakala wake hao ndiyo wataweza kulinda kura zao .Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus KamugishaWadau wakiwa ukumbini,kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wadau wa amani mkoani Shinyanga pia walikubaliana kukabiliana na watu wote wanaopanga kuvuruga amani ya nchi wakati wa uchaguzi. 
  
Mwakilishi wa shirika la Save the Children Herman Mbunda akizungumzia umuhimu wa kulinda watoto wakati huu wa uchaguziKushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'umbi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(kulia) 
Wadau hao walikumbushana na kuhamasishana kulinda haki za watoto,wanawake na makundi maalum katika jamii wakiwemo walemavu wakati wa uchaguziKikao kinaendeleaKikao kinaendeleaKikao hicho cha wadau wa amani walisema ni vyema katika kipindi hiki cha uchaguzi kila jambo linalofanyika basi kuwe na maslahi kwa watoto ambao asilimia kubwa wanaingizwa katika masuala ya siasaWadau wa amani wakiwa ukumbiniKatibu wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pili Misungwi(kushoto) akifuatilia kwa umakini zaidi kilichokuwa kinajiri ukumbiniMkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede(kulia)Mkutano unaendeleaKikao cha wadau kinaendelea Mkutano unaendeleaWadau wakiwa ukumbiniViongozi wa dini wakiwa ukumbiniKikao kinaendeleaWadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbiniKaimu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago(kulia)Kikao kinaendeleaKikao kinaendeleaKikao kinaendeleaKamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akiwasilisha mada ya ulinzi na usalama katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 ambapo alisisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na watu watakaovuruga amani ya nchiKikao kinaendeleaKamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka waandishi wa habari nchini kutumia vizuri kalamu zao ili kudumisha amani ya nchiWadau wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmiPicha ya pamoja washiriki wa kikao hichoWadau wakiwa katika picha ya pamoja Picha ya kumbukumbu Picha ya kumbukumbu Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BEI YA MADAFU HII LEO

RATIBA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS/MGOMBEA MWENZA KWA VYAMA VYA SIASA (Kama ilivyorekebishwa tarehe 20/10/2015)


MAMA MWANAMWEMA SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UWT WILAYA YA MJINI UNGUJA KUMUOMBEA KURA DK SHEIN NA DK MAGUFULI

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Bi Waridi Juma akisoma risala ya Wanawake wa Mkoa wa Mjini wakati wa mkutano na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa mkutano wake na Viongozi hao uliofanyika Afisi ya CCM Mkoa Amani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa mkutano huo na kuwakaribisha Viongozi wa Ujumbe wa Kampeni ya Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja. 
Makamu Mwenyekiti wa UWT Mstaaf Balozi Amina Salum Ali akiwasalimia Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Mkoa wa Mjini katika mkutano na Mama Mwanamwema  kuwahamasisha Viongozi wa UWT Zanzibar katika kupiga kura kwa Wagombea wa CCM.  
Makamu Mwenyekiti wa Mstaaf wa UWT Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa UWT kutumia nafasi zao kuwahamasisha Wanawake kukipigia kura Chama cha Mapinduzi kwa Wagombea wao wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Wagombea wote wa CCM. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja Silima Borafya akizungumza na Viongozi wa UWT katika mkutano wao na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Muasisi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Asha Simba akiwasalimia Viongozi wa UWT na kuwaomba kukipigia kura Chama cha Mapinduzi na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, mkutanom uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania kukipigia kura ya Ndio Chama cha Mapinduzi na Wagombea wao wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.   
Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza wakati wa mkutano huo wa kuwaombea kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli. na Wagombea wote wa CCM.
Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania wakionesha mikono juu kuashiria kuwapigia Wagombea wa CCM Kura ya Ndio kwa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Mjini Unguja na kuwaomba kumpigia Kura ya Ndio Mgombea wa Urais wa CCM Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Wagombea wote wa CCM.
Mke wa Rais wa Zanzibar akiwahutubia Viongozi wa UWT wa Mkoa wa Mjini Unguja wakati wa mkutano wake wa kampeni ya kumuombea Kura ya Ndio Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. 
Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimuombea kura Dk Shein.
Umoja wa Wake wa Viongozi wa CCM Wabunge na Wawakilishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar  wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com
Mob. 0777424152 or 0715424152.
Email. othmanmaulid@gmail.com 

HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MATHIAS CHIKAWE (Mb) ALIYOTOA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 21 OKTOBA, 2015 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA WIZARA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,

Kama mnavyojua tarehe 25 ya mwezi huu wa Oktoba mwaka 2015 siku ya Jumapili katika nchi yetu kutafanyika Uchaguzi Mkuu kwa ajili ya kuchagua rais, wabunge na madiwani zoezi ambalo litawashirikisha watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura kwa mujibu wa sheria.


Zoezi hili kwa mujibu wa sheria za uchaguzi litasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaani NEC kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika chaguzi mbalimbali zilizopita ama kuwahi kufanyika katika nchi yetu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalo jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao unaimarishwa kabla, wakati na baada ya zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu katika maeneo yote ya nchi yetu, ili wananchi waweze kuwa salama na kuendelea na maisha yao ya kila siku.


Ndugu Waandishi wa habari,Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za vitisho zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na hata mitaani na watu wasio na nia njema kwa taifa letu,  zikiwataka wananchi wanunue mahitaji yao mbalimbali ikiwemo vyakula na kuvihifadhi kwa ajili ya kuja kuvitumia wakati na baada ya uchaguzi kwa ubashiri wa kuwepo kwa vurugu wakati ama baada ya uchaguzi.


Taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kwa ujumla ni taarifa potofu ambazo zinalenga kuwajengea wananchi hofu na mashaka, wasiwasi na vitisho pasipo sababu zozote zenye tija kwa taifa letu.

Ndugu zangu Waandishi wa habari,

Nitoe rai kwa Raia wote waishio hapa nchini yaani Watanzania na Wageni kupuuza taarifa zote zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kwa kuwa taarifa hizo si za kweli, na wala hazilengi kulinda amani iliyopo nchini kwetu.  


Pamoja na hayo kumekuwa na matamko kwa baadhi ya wanasiasa katika kampeni zao kudai kuwa Serikali itasitisha posho za askari mara baada ya Uchaguzi Mkuu,  Taarifa hizi si za kweli kwani Posho za Vyombo vyote vya dola   vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  ni za kudumu kama ilivyoelekezwa katika waraka wetu, hazitafutwa wala kubadilika na iwapo zitabadilika ni kwa kupandishwa na wala si kufutwa.


 Nawaomba wananchi wote watii sheria  za nchi na zile  za Tume ya Uchaguzi zinazoongoza Uchaguzi Mkuu sambamba na kufuata Maelekezo yatakayotolewa na Tume hiyo kabla, wakati na baada ya kupiga kura jambo litakalosaidia kuilinda amani ya nchi yetu, kwani kila Mtanzania anao wajibu wa kuilinda amani kwa kufuata sheria za nchi bila kushurutishwa.


Wananchi wanapaswa kutambua kuwa baada ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu maisha ya watanzania yanapaswa kuendelea kama kawaida hivyo itikadi zao za vyama vya siasa zisiwatofautishe na kuwajengea chuki, uhasama ama uadui kwani watanzania ni wamoja na wamekuwa wakiishi kwa amani, umoja na ushirikiano katika kuendeleza taifa hili.



Ndugu waandishi wa Habari,  

Wananchi hawapaswi kuwa na hofu yoyote kwa kuwa Serikali ya awamu ya nne ambayo imeongoza na kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka kumi  inakusudia kwa dhati kukabidhi madaraka kwa serikali iyajo ya awamu ya tano katika hali ya amani na utulivu.


Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama inawahakikishia wananchi kuwa itahakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo na kuimarishwa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mpaka pale ambapo Uongozi wa  serikali ya awamu ya  tano utakapoingia madarakani.


Wananchi watoe taarifa Polisi pale watakapoona  kuna dalili za uvunjifu wa amani  kwa kupiga simu ya bure namba 112.


Nawashukuru kwa kunisikiliza, Asanteni .

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



KIJANA FIKIRIA MARA MBILI KISHA WEKA TIKI KWA MGOMBEA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO, KATIKA KITUO CHA KUTUNZIA KUMBUKUMBU CHA TAIFA (NATIONAL INTERNET DATA CENTRE) KIJITOMYAMA.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jengo jipya la Mradi wa Kituo cha Kutunzia kumbukumbu Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib, akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa mitambo ya kutunzia kumbukumbu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa za Shirika la Simu Tanzania, TTCL, Issaya Ernest, wakati Dkt Bilal, alipotembelea kituo hicho cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa (kushoto) na Mwakilishi wa Ofisi ya Uchumi na Biashara ya Serikali ya China, nchini Tanzania, Lin Zhiyong,  kwa pamoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Simu Tanzania TTCL, wakati alipotembelea kituo hicho cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa (kulia) ni Afisa Mtendaji wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura.

 Mrisho Mpoto na wasanii wa bendi yake ya Mjomba, wakitoa burudani.

 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, kuhutubia.
 Sehemu ya wafanyakazi wa Shirika la Simu Tanzania, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kutembelea mitambo hiyo, Kijitonyama.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafl ya uzinduzi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, jijini Dar es Salaam leo Okt 21, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibofya kitufye kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo Okt 21, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo Okt 21, 2015.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi huo baada ya kuzindua rasmi leo Okt. 21, 2015 Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Picha na OMR

UMMOJA WA WANANCHI WA KIBADA WAFANYA MATENGENEZO GARI LA JESHI LA ZIMAMOTO

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi iliyofanikisha upatikanaji wa Gari  la zimamoto, Mussa Bibose akitoa maelekezo kwa wananchi waliohudhuria shughuli ya kukabidhi gari hilo Kibada,Kigamboni  Jijini Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa Umoja wa wananchi wa Kibada, Kigamboni Jijini Dar es salaam Bwana Lagano Mwampetu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari moja ya zimamoto iliyopatikana kwa Juhudi za umoja huo na kukabidhi kwa  Kamishna wa Operation Jeshi La Zimamoto na uokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali.

Kamishna wa Operation Jeshi La Zimamoto na uokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali akiangumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kukabidhi Gari hilo ambapo amewapongeza wananchi wa Kibada kwa juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika maeneo yao.

Mwenyeikiti wa umoja wa wananchi wa Kibada, Kigamboni Jijini Dar es salaam Lugano Mwampeta akimpa maelekezo kamishna wa Operation jeshi la zimamoto na uaokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali wakati wa shughuli ya kumkabidhi gari moja la kuzima moto lililofanyiwa matengenezo kwa nguvu ya wananchi wa kibada kwa ajili ya kuwasaidia wakazi hao na majanga ya moto,makabidiano hayo yaliyofanyika Kigamboni Kibada Jijini Dar es salaam.

Gari la Jeshi la Polisi la zimamoto lilofanyiwa matengenezo na wananchi wa Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi wakifanya zoezi la uzimaji moto mara baada ya kukabidhiwa gari hilo.

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images