Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 672 | 673 | (Page 674) | 675 | 676 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mahujaji wengine wawili kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia.

   Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na saba (27). Majina kamili ya mahujaji hao ni Bw. Juma Yussuf Bakula na Bw. Ahmad Awadh Namongo kutoka Kikundi cha Ahlu Dawaa.

  Hadi sasa mahujaji kumi na tatu (13) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.

  Kwa upande wa mahujaji wanne ambao walikuwa wanapatiwa matibabu kutokana na kuugua au kujeruhiwa, mmoja wao ni Bw. Mustafa Ali Mchina ambaye alikuwa amelezwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika mji wa Maddinah alifariki dunia tarehe 17 Oktoba 2015 na kuzikwa Maddinah siku hiyo hiyo. 

  Bi. Mahjabin Taslim Khan ambaye alijeruhiwa katika ajali hiyo na kusababisha kukatwa mguu wake amepata nafuu na alirejea nchini tarehe 20 Oktoba 2015. Mwingine ni Bi. Hidaya Mchomvu ambaye alijeruhiwa pia bado yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu.

   Hujaji wanne ni Bw. Ahmed Abdallah Jusab ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo alifanyiwa upasuaji wa kumuwekea kifaa cha kuongeza mapigo ya moyo tarehe 19 Oktoba 2015 na alitarajiwa kurejea nchini tarehe 21 Oktoba 2015.

  Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
  Dar es Salaam
  22 Oktoba, 2015

  0 0

   Mhe. John Lugalema  Kahyoza akila kiapo mbele ya Rais Jakaya kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam, awali mhe. Kahyoza alikuwaMsajili Mahakama Kuu ya Tanzania.
   MheKatarina Tengia Revocati akila kiapo mbele ya Rais Jakaya kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Msajili Mkuu  wa Mahakama  mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam, awali  Mhe. Katarina alikuwa Msajili wa Mahakama ya rufani.
   Waheshimiwa John Lugalema  Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati wakisubiri kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Viongozi na Wageni mbalimbali wakisubiri tukio la kuapishwa kwa waheshimiwa John Lugalema Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wanawake waliohudhuria sherehe za kuapishwa wa heshimiwa John Lugalema  Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.

  0 0

    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

   Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

   Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku  hiyo bila wasiwasi wa aina yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
  (Picha na Francis Dande)
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  0 0

   Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Airtel ilipozindua  smartifoni mpya ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10zitakazopatikata katika maduka yote ya Airtel zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  kutoa  muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita. Kulia ni bi Anethy Muga meneja masoko wa Airtel. Hafla ya uzinduzi imefanyika jana katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam
   Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Airtel ilipozindua  smartifoni mpya ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 zitakazopatikata katika maduka yote ya Airtel zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  kutoa  muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita. Kushoto ni Afisa Matukio wa Airtel Bi, Dangio Kaniki wakati wa Hafla ya uzinduzi iliyoyika jana katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam.
   Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kushoto) akiwa na  Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kulia) wakionyesha simu mpya zilizoingizwa sokoni zikiwa na ofa ya Airtel smartifonika aina ya Mgnum Bravo Z10 wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Airtel leo
  Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akijaribu kupiga picha kwa kutumia kamera ya mbele ya simu mpya aina ya Magnus Bravo Z10 inayopatikana katika maduka ya Airtel kuanzia sasa ikiwa na ofa ya Smartifonika, uzindunzi wa kuingiza sokoni simu hii yenye uwezo wa kutumia  laini mbili umefanyika jana katika makao makuu ya Airtel.

    AIRTEL  Tanzania leo imezindua smartifoni mpya na yenye ubora zaidi ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 ambapo zinapatikata sasa hivi  kwenye maduka yote ya Airtel nchini zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  inayompatia mteja muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita.

  Akiongea na waandishi wa habari Meneja masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga amesema “Airtel tumekuletea Simu mpya ya Magnus Bravo Z10 ili kukuwezesha mteja wetu kuendelea kufurahia huduma zote za Airtel na zile huduma zote za kisasa za smartifoni ukiwa mahali popote
   “Magnus Bravo Z10 toka Airtel inatumia laini mbili, ina radio, kioo (screen) kubwa ili kukupa raha zaidi kuona vyema unapokuwa unaitumia, pia imewekewa kamera zenye uwezo mkubwa mbele na nyuma za 5mp ili kukupa taswira au picha nzuri utakazopiga karibu au mbali ukiwa na ndugu, jamaa na marafiki” alielezea Bi Muga
  “Vilevile ili  uweze kufurahia huduma zote za mitandao, Airtel tumehakikisha tayari simu hii inamitandao yote ya kijamii kama facebook, Instagram, twitter na mingine mengi” . Alisema Bi Muga
  Simu hii inapatikana sasa katika maduka yote ya Airtel nchini kwa gharama nafuu kuliko zote ya sh. 75,000  tu.

  0 0  0 0

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mariado na walimu iliyopo Usa River ,wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu barani Afrika katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu iliyofanyika Oktoba 21 na kudai haki za wenye ulemavu wa ngozi(Ualibino) kulindwa kama wananchi wengine

  Mwanafunzi Kelvin wa shule ya Mariado akiimba wimbo Umoja wa Afrika(AU)ambao ni maalumu wakati wa shughuli za umoja huo zinapofanyika.

  Kamishna wa Tume ya Haki Binadamu na Utawala Bora,Zanzibar ,Mohamed Khamis Hamad akizungumza katika maadhimisho hayo.


  Wanafunzi wa Shule ya Mchepuo wa kiingereza ya St.Jude ya Jijini Arusha wakiigiza athari za watoto wa kike kukeketwa.

  Wanafunzi wa Shule ya Mchepuo wa kiingereza ya St.Jude ya Jijini Arusha wakiigiza athari za watoto wa kike kukeketwa.
  0 0

  CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.

  Kufunga Kampeni
  CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo.  Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:

   1.    Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
   2.    Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
   3.    Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
   4.    Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
  5.    Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
  6.    Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
  7.    Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu  Mstaafu.
  Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.
  Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.  Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
  Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

  Tathmini ya Kampeni
  Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku.  Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
  Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69. 

  Uchaguzi wa Amani
  CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
  Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
  Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Mawakala wa vyama na Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo.  Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha fujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema.
  Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi. 
  CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwa sababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
  Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya Uchaguzi, siku ya Uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa Uchaguzi. 

  Kupokea Matokeo
  CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia Mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya Uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya Uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015. 
  Imetolewa na:                                           

  January Makamba
  MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
  MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI
  22 OKTOBA 2015

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa mgodi mara baada ya kuwasili eneo la mgodi wa urani katika mradi wa mto mkuju wilaya ya namtumbo mkoa wa ruvuma Oktoba 21,2015.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mgodi wa urani mkoani Ruvuma jana.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelekezo mara baada ya kuzindua mgodi wa urani mkoani Ruvuma jana.

  0 0

  CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya
  wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura. 

  Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais. Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais. 

  Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa. 

   Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi. 

   Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa hili. 

  Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.

  0 0

  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze,Ndugu Ridhiwani Kikwete.Dkt Magufuli amefanya mikutano ya kampeni katika jimbo la Kawe,Chalinze,Kibaha vijijini,Kibamba na Kibaha mjini.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya ccm kwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha vijijini .Ndugu Hamoud Abuu Jumaa.
   Umati wa wakazi wa jimbo la Kawe wakifuatilia mkutano wa kameni
   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa-CCM,Dkt Gharib Bilal akimuombea kura za ushindi Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Bunju jioni ya leo jijini Dar.
   Sehemu ya umati wa watu wakiwa wamekusanyika viwanja vya Bunju,kwenye mkutano wa kampeni jimbo la kawe jioni ya leo ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alijinadi na kuomba kura za ushindi ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
   Sehemu ya umati wa wakazi wa jimbo la kawe wakishangilia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Bunju jioni ya leo jijini Dar
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kawe,Keppy Warioba viwanja vya Bunju jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
  Wananchi wa jimbo la Kawe wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Bunju,jijini Dar
  Wanachama wa CCM wakishangilia kwa staili ya namna yake,kwenye mkutano wakampeni mjini Kibaha.
  Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Ndugu Silvestry Koka akijinadi mbele ya wakazi wa mji wa kibaha kwenye mkutano wa kampeni,ambapo pia Mgombea Urais wa CC Dkt Magufuli alijinadi na kuomba kura.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kawe,akijinadi viwanja vya Bunju jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
  Mmoja wa wafuasi wa CHADEMA alipojichanganya kwenye mkutano wa CCM,maara baada ya kuutiwa na sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao wananchi
  Siasa sio uhasama
   Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akijinadi kwa wakazi wa Tegeta jioni ya leo alipokuwa akielekea mjini Chalinze kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
   Staili mpya ya Kumpokea Mgeni,Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwasili viwanja vya Vunju,jimbo la Kawe kuwahutubia katika mkutano wa kampeni
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akibadilishana jambo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa-CCM,Dkt Gharib Bilal
   Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa-CCM Mama Sophia Simba akimwombea kura Dkt Magufuli ili apate ridhaa ya wananchi na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,kwa kupata kura nyingi zinazotarajiwa kupigwa oktoba 25

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (Katikati kulia) akimfafanulia jambo Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza (wapili kushoto), pamoja na wajumbe wenzake, jinsi Tanzania ilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu utakavyokuwa wa amani. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni Rais wa Zamani wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) wakati Mkuu huyo pamoja na wajumbe wenzake walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, hata hivyo, Chikawe aliwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utakuwa wa amani. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha zote  na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


   Rais Kikwete (Kushoto) na Ridhiwan Kikwete (Kulia).

  MKAZI wa mjini Moshi, Kyefa Joachim Makundi (33), amepandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya  Kikwete.

  Mbali na shitaka hilo, mshitakiwa huyo amesomewa shitaka lingine la kumtukana Ridhiwan Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze anayemaliza muda wake.

  Mshitakiwa huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Agatha Pima.

  Wakili Pima amedai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan.

  Ingawa matusi hayo hayakuandikwa kwenye hati ya mashitaka, lakini wakili Pima amedai kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 89(1) (a) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

  Chini ya kifungu hicho, mtu yeyote anayetumia lugha ya matusi, kuudhi, au kudhalilisha dhidi ya mtu mwingine katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani anatenda kosa la jinai.

  Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na hatia katika kosa hilo ni kifungo cha miezi sita jela.

  Hata hivyo, mshitakiwa amekana shitaka hilo ambapo mahakama imesema dhamana ilikuwa wazi ikiwa mshitakiwa atakuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh1.5 milioni kila mmoja.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo.

  JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limesema halipo tayari kukipendelea chama chochote kile cha siasa katika kipindi hiki cha uchaguzi utakaofanya Oktoba 25 mwaka huu.
  Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo, wakati akizungumza na wanahabari.

  Mkumbo amesema kuwa katika kipindi hiki, jeshi halitakuwa tayari kukipendelea chama cha siasa kwani lipo kwa ajili ya kutenda haki na kulinda raia.

  Amesema kuwa wananchi wamekuwa na dhana na imani potofu ya kwamba Polisi hupendelea baadhi ya vyama vya siasa, ambavyo ndivyo sivyo na kwamba Wananchi wanapaswa kuwa na imani na Jeshi hilo.

  “Tutafanya kazi kwa kufuata sheria na pale tutakapo ona uvunjifu wa amani unatoweka hatusita kuongeza nguvu ya Polisi.

  “Kama ulivyoniuliza kwamba kuna upendeleo wa chama tawala, kitu hicho hakitakuwepo sasa hivi, hata juzi pale Nyegezi wafuasi wa Chadema na CCM walitaka kuleta fujo tulifika na kudhibiti,” amesema Mkumbo.

  Sanjali na hayo pia Mkumbo aliyaonya makundi ya watu yatakayofanya fujo siku ya uchaguzi kuacha Mara moja kwani hayatafumbiwa macho, yatachukuliwa hatua za kisheria.
  Mkumbo amesema kuna vikundi vichache vilivyoandaliwa na baadhi ya vyama vya siasa ili kuwafanyia fujo wazee na wanawake siku ya uchaguzi na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuyadhibiti mapema. 

  0 0

  Mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa akiwa katika mkutano wa hadhara
  Mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa akiwa katika mkutano wa hadhara.

  BARAZA la Wanawake la Chama Cha Demokrasia (Chadema) Taifa, Bawacha, limewataka wanawake nchi nzima kupiga kura na kukaa mita 200 ili kulinda kura zao kwani ni haki yao kisheria.
  Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Kunti Yusuph wakati wa mkutano na wanawake, uliofanyika katika ofisi za Chadema kanda ya ziwa Victoria jijini hapa.

  Kunti ambaye ni mratibu wa mikutano ya kukutana na wanawake ya mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa, amesema kuwa kupitia wanawake wa Mwanza, wanawake nchi nzima wanapaswa kupiga kura na kulinda kura zao.

  Amesema endapo wanawake na watanzania kwa ujumla watapiga kura na kuondoka watakuwa wamevunja sheria ya nchi hivyo amewaomba kulinda kura zao kwani ndio maisha yao.
  Hata hivyo Regina aliwaomba wanawake na watanzania kwa ujumla kupiga kura kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kwa maendeleo ya Taifa. 

  0 0
 • 10/22/15--23:00: CHAGUA MAGUFULI

 • 0 0

  Mshambuliaji wa JKT Ruvu, Gaudence Mwaikimba akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Adrew Vicent katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka suluhu. (Picha na Francis Dande)
   Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim katika mchezowa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume. Timu hizo zilitoka suluhu.  
  Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim katika mchezowa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume. Timu hizo zilitoka suluhu.  

  0 0

  CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya
  wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura. 

   Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais.

   Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais. 

   Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa.

   Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi. 

   Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa hili. 

   Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla leo asubuhi ameshiriki chai na wafanyakazi na wateja waNMB Tawi la Moshi na kuipongeza benki ya NMB kwa kuwa benki 10 bora Afrika mashariki, benki inayoongoza kwa kuwa na matawi mengi nchini, benki inayoongoza kwa kutengeneza faida na kusaidia jamii, benki ya riba na gharama nafuu nchini na benki yenye  huduma bora kwa wateja nchini.


  Pamoja na mafanikio hayo ameishauri benki hiyo kuendelea kuwa wabunifu wa bidhaa na kuendeleza huduma bora hasa katika kipindi hiki cha ushindani.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla kushoto akipata chai asubuhi leo chai iliyoandaliwa na benki ya NMB tawi la Nelson Mandela Moshi,kulia 
  Meneja wa Tawi hilo 
  Emanuel  Kishosha.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla  akizungumza na wafanyakazi na wateja wa benki ya NMB tawi la Nelson Mandela Moshi leo mara bada ya kushiriki pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki hiyo leo katika tawi la Nelson Mandela Moshi.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla akilishwa keki na mfanyakazi wa benki ya NMB tawi la Nelson Mandela Moshi leo aliposhiriki pamoja katika kifungua kinywa.


   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki hiyo katika tawi l Nelson Mandela.

  0 0

  Description: https://pbs.twimg.com/profile_images/529573534352175104/FGz58F-d.png
  WASANII nguli wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba kutoka Tanzania na Victoria Kimani kutoka Kenya kesho Jumamosi watawasha moto katika onyesho la muziki la Coke studio linalorushwa na luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi.

  Ali Kiba ambaye anatamba na kwa vibao vyake mbalimbali katika msimu huu wa Coke Studio amefanya Kolabo matata (Mash- up) kwa kushirikiana na mwanamuziki wa kike maarufu kutoka nchini Kenya ,Victoria Kimani.

  Wasanii wengine kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu  ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na  mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, Fid Q amefanya bonge la kolabo (mash-up) na Maurice Kirya kutokana Uganda,  na wakati Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na  mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.


  Akiongea wakati wa uzinduzi wa onyesho hili hivi karibuni Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Nchini Maurice Njowoka alisema kuwa wasanii nguli kutoka Tanzania wanaungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika msimu wa tatu wa maonyesho ya  burudani ya muziki maarufu kwa jina la  Coke Studio Afrika ambalo linaendelea  kuonyeshwa katika nchi mbalimbali.

  Alisema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko lakini safari hii unatumika katika onyesho la Coke Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema

  0 0

  Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp. Mazungumzo hayo yalihusu ukimalishaji wa Makubaliano mbalimbali kati ya Tanzania na Uturuki ili yaweze kusainiwa na kuanza kutekelezwa.
  Balozi Luvanda akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp akimsikiliza kwa makini Balozi Luvanda ambaye hayupo pichani.


  Balozi wa Uturuki akibadilishana mawazo na Afisa wake wakati wa mazungumzo hayo
  Balozi wa Uturuki, Mhe. Yasemin Eralp akimkabidhi nyaraka Balozi Luvanda
  Balozi Luvanda pamoja na Afisa wake, Bw. John Pangipita wakimsikiliza Balozi wa Uturuki hayupo pichani.
  Mazungumzo yanaendelea

older | 1 | .... | 672 | 673 | (Page 674) | 675 | 676 | .... | 1898 | newer