Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

TANO ZA MAGUFULI . UADILIFU .UCHAPAKAZI .UFUATILIAJI .UTEKELEZAJI NA UTUMISHI ULIOTUKUKA

$
0
0
MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amewataka wananchi kumchagua ili awe rais wa tano ajaye wa Tanzania huku akiahidi kushughulikia masuala mbalimbali ya wananchi na hivyo kuliletea Taifa maendeleo kwa muda wote atakaokuwepo madarakani.

Akizungumza na wananchi wa mkoani Lindi katika muendelezo wa kampeni zake, Dk Magufuli alisema akichaguliwa kushika nafasi hiyo, pamoja na mambo mengine atakayoyafanya atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya Kusini, kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.

Amesema pia atatumia nafasi hiyo kutafuta namna bora ya kuwainua wakulima wa korosho, tofauti na utaratibu wa sasa wa stakabadhi ghalani, alisema umekuwa ukiwasababishia umasikini mkubwa wakulima wa zao hilo.
Akiwa Nachingwea, Ruangwa, Mtama na Lindi Mjini, Dk. Magufuli alisema tofauti na wapinzani wanaoahidi kuondoa nyumba za nyasi na tembe nchi nzima kwa siku 100 watakazokaa Ikulu, jambo alilosema ni ndoto, Serikali yake itakachofanya ni kushusha bei ya mabati, saruji, nondo, misumali na vifaa vingine vya ujenzi ili wananchi wajenge nyumba bora.


Akielezea ni vipi atawezesha hilo kufanikiwa, Dk Magufuli alisema atatumia utajiri wa rasilimali za Taifa ikiwemo gesi inayopatikanakatika Mikoa ya Kusini na Bagamoyo, Pwani ili kutoa ruzuku katika vifaa vya ujenzi.

Lakini, pia kuongeza viwanda vya bidhaa hizo ili kushusha bei kwa kiwango cha juu. Alisema dalili za kushuka kwa vifaa hivyo, zimeanza kuonekana baada ya kujengwa kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara, ambachokinatumia nishati ya gesi kwa uzalishaji, kilichowezesha kushuka kwa bei ya saruji kutoka Sh 16,000 hadi Sh 8,000 na kwamba bei hiyo itashuka zaidi atakapokuwa rais.

Alisema pia ataziba mianya yote ya rushwa serikalini ili makusanyo ya fedha hizo yatumike kuboresha maisha ya Watanzania wakiwemo wa Kusini, huku akisema ushahidi wa utendaji wake kwa watu wa Kusini ni ujenzi wa barabara za lami kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara na baadaye Tunduru na Songea.

Ili kumwezesha kuingia Ikulu, mgombea huyo aliwaomba wakaziwa Mkoa wa Lindi kufika katika vituo vya kupiga kura mapema asubuhi ya Oktoba25, huku akisema kutokana na vitisho na vurugu zilizopangwa ili kuwatishia wananchi hasa wanawake wasipige kura, kutakuwa na polisi wa kutosha ili kulinda amani.

Akizungumzia soko la korosho, Dk Magufuli alisema akiingiaIkulu atabadili mfumo wa ununuzi wa korosho ili kuwezesha wakulima wa zao hilo kwa mikoa ya Kusini, kunufaika na kuboresha maisha yao na kuachana na mfumo wasasa ambao unawafanya wakulima kukopwa fedha zao bila kulipwa na hivyo kuwa masikini.

MIAKA 53 YA MAFANIKO: AWAMU YA PILI - MWINYI (1985 - 1995)

$
0
0
Miaka 53 ya Mafaniko: Awamu ya Pili - MWINYI (1985 - 1995) 
 Miaka 53 ya Mafanikio: Awamu ya Tatu - MKAPA (1995 - 2005)

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI LINDI MJINI, NACHINGWEA NA LIWALE

$
0
0
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpilipili huko Lindi Mjini tarehe 12.10.2015.
 Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete mara baada ya kumwombea kura kwa wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili tarehe 12.10.2015. Aliyesimama kulia ni Mgombea Ubunge katika Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Mama Salma Kikwete akiwa katika kijiji cha Ngunichile kilichoko katika Wilaya ya Nachingwea kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe nchini tarehe 25.10.2015.  Katika mikutano hiyo Mama Salma alimnadi Dkt. John Magufuli kwenye urais na Ndugu Hassan Elias Masala kwenye Ubunge wa Jimbo la Nachingwea na Madiwani wote katika wilaya hiyo tarehe 13.10.2015.

RAIS JK APOKEA TUZO YA KUKUZA NA KUTHAMINI UTAFITI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia akipokea zawadi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza na kuthamini utafiti nchini, wakati wa Kongamano la 29 la Kisayansi lililoandaliwa na taasisi hiyo ili kuwasilisha na kujadili matokeo ya tafiti za tiba katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kongamano hilo linafanyika jijini Dar es Salam kwa siku tatu (Na Mpiga Wetu).

MAGAVANA WA AFRIKA WAKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA BI. CHRISTINE LAGARDE

$
0
0
Magavana wa Afrika wakutana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim kujadili namna ya kuchochea maendeleo  na kuimarisha uchumi barani Afrika.

 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile wakisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde wakati akiingia kwenye ukumbi wa mkutano.
 Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde akinukuu hoja zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo.
 Magavana wa Afrika wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim nchini Peru – Lima.

 Wa pili kulia ni Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania Dr. Joseph Masawe.
 Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye mkutano wakujadili namna ya kuimarisha uchumi na kuchoche maendeleo Barani Afrika. Kutoka kushoto ni Kamishna Idara ya Sera Bw. Bedason Shallanda, Mhasibu Mkuu Msaidizi Bw. Ishmael Kasekwa, John Mavura mchumi Wizara ya Fedha na Bw. Patrick Pima mchumi Wizara ya Fedha.

Imetolewa na

Msemaji wa Wizara ya Fedha

Bi. Ingiahedi Mduma

13/10/2015        

MAANDALIZI YA ROTARY DAR MARATHON 2015 YAKAMILIKA

$
0
0
Naibu mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso akiongea na waandishi wa habari leo hii katika ukumbi wa Hyatt Regency juu ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon 2015 ambayo huandaliwa na Rotary klabu za Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki M. Mbio na matembezi ya Dar Rotary Marathon kwa mwaka huu zitafanyika katika viwanja vya Green, Oysterbay tarehe 14 October 2015. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Rotary Bi. Sharmila Bhatt, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi. Agnes Batengas, Makamu wa Raisi wa Rotary klabu Oysterbay Bi. Anne Saels na Rais wa Rotary Klabu Dar North Bw. Masato Wassira.
baadhi ya washiriki wa Rotary Dar Marathon kutoka Malawi na Kenya wakifuatilia mkutano huo, Marathon ya mwaka huu itajumuisha wakimbiaji kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Malawi, South Africa na Ethiopia.

Mbio na matembezi ya hisani za Dar rotary marathon yanatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 14.10.2015 hapa jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais mstaafu mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi. 

Mbio na matembezi hayo yameandaliwa na klabu sita za Rotary za hapa Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki M na kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuponya maisha, badilisha jamii” ambapo fedha zitakazochangishwa ziltaelekezwa katika ujenzi wa kituo cha afya hapa Dar es salaam. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

TASAF YAWAHIMIZA WAANIDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO HASA WAKATI HUU WA UCHAGUZI.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amewahimiza waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kuzingatia maadili ya taaluma hiyo hasa wakati huu ambapo taifa linaingia katika hatua muhimu ya kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu.

Mwamanga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kongamano hilo amewasihi waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya taaluma yao ili kuepukana upotoshaji na kuitia nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Amesema taaluma ya uandishi wa habari ina umuhimu mkubwa katika kujenga Jamii na isipotumiwa vema inaweza kuhatarisha amani na utengamano wa taifa jambo ambalo amesema halifai kufumbiwa macho.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki wa kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya PEACOCK mjini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akifunga komgamano la waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es salaam  lililojadili utekelezaji wa uhuru wa habari kwa uangalifu hususani wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano lililoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam baada ya kufunga rasmi kongamano hilo lililojadili juu ya uchaguzi huru na haki bila waandishi wa habari kuzingatia maadili ni ndoto.

DUNIA YAHIMIZWA KUWAJIBIKA KWA AJILI YA AMANI

$
0
0
IMG_5771
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. ( Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
JUMUIYA ya Kimataifa imetakiwa kuwajibika kuhakikisha kwamba wanaweza kuwepo na amani na usalama kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa duniani.
Hayo alisema Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard membe katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Hafla hiyo imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja mapema zaidi kuliko tarehe iliyopaswa ya Oktoba 24 kutokana na Tanzania kuwa katika mchakato wa uchaguzi.
Waziri Membe alisema kwamba dunia kwa sasa ipo katika changamoto kubwa ya usalama kutokana na mizozo inayoendelea katika nchi kadhaa duniani.
Alisema kumekuwepo na wimbi kubwa la mapigano ndani ya nchi mbalimbali katika nchi mashariki ya kati, Ulaya na hata Afrika, kukua kwa ugaidi na siasa za kibaguzi.
“ Sote tunafahamu shida iliyopo katika nchi kama Syria, Iraq, Somalia, Libya, Afghanistan, Yemen na jamhuri ya Afrika Kati” alisema waziri Membe na kuongeza kuwa matukio ya vita ya mara kwa mara, misimamo mikali na ugaidi vimekuwa vikisababisha vifo vingi na mateso kwa jamii.
Kutokana na hali ilivyo kwa sasa dunia haiko katika hali ya amani na hivyo juhudi zaidi zinatakiwa kufanyika ili kurejesha amani ambayo ni kiungo muhimu katika maendeleo.
Pamoja na kuzungumzia haja ya amani kutokana na dunia sasa hivi kufikia kiwango cha juu cha wakimbizi ndani na nje ya nchi zao, Waziri Membe alihimiza mabadiliko katika uendeshaji wa Umoja huo ili kuleta uwiano wa uwajibikaji kimataifa.
IMG_5783
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini huku akiwa ameambatana na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula (kushoto).
Mwaka 2005 idadi ya wakimbizi duniani ilikuwa milioni 38 lakini miaka kumi baadae takwimu zinaonesha kwamba kuna wakimbizi milioni 60 ikimaananisha kwamba katika kila watu 122 duniani, mmoja ni mkimbizi.Tanzania ina wakimbizi 169, 874.
Aidha alisema kwamba bara la Afrika linastahili kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama ili maamuzi kuhusu Afrika yawe na mamlaka ya Afrika yenyewe.
Katika hotuba yake pia alizungumzia mafanikio ya Umoja wa Mataifa ikiwamo utengenezaji wa malengo mapya 17 ya maendeleo endelevu na pia ufanisi katika utekelezaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama kitu kimoja.
Alisifu mafanikio makubwa yaliyotokana na uongozi wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez tangu alipofika nchini miezi 13 iliyopita.
Alisema utendaji wake unaozingatia ngazi za chini hadi juu na vijijini hadi mjini umeleta mafanikio makubwa kutokana na kuwa sehemu kamili ya utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo na kupiga vita umaskini.
Pia alishukuru mchango wa Umoja wa Mataifa katika kufanikisha elimu ya uchaguzi hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambao utafanyika siku 12 zijazo.
Umoja wa Mataifa na wadau wake wametoa jumla ya dola za Marekani milioni 22.5 kwa ajili ya shughuli za uchaguzi mkuu nchini na kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Naye Rais mstaafu Benjamin Mkapa akizungumza katika hafla hiyo alitaka dunia kutambua kwamba madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa bado yapo palepale na kutaka nchi wanachama kutoa michango yao kuendelea kupambana na changamoto mpya za dunia katika masuala anuia ikiwamo vita, umaskini, chakula na mabadiliko ya tabia nchini.
IMG_5777
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akisalimiana na Waziri Membe mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mataifa 51 yalikutana mjini San Francisco, Marekani baada ya vita kuu ya pili ya dunia na kuanzisha Umoja wa Mataifa. Wakati wa uanzishaji wa Umoja huo mataifa manne tu ya Afrika yalikuwepo nayo ni Liberia, Ethiopia, Misri na Afrika Kusini.
Hata hivyo rais huyo mstaafu alisema ili Umoja wa Mataifa ufanikiwe ipo haja ya kubadili mifumo yake ili iweze kuwajibika kikamilifu kwa dunia na wala si kwa matakwa ya waasisi na matajiri.
Pamoja na mabadiliko hayo nchi nyingi zinazoendelea zinataka kuwa na haki ya upigaji kura katika vyombo kadha vya Umoja wa Mataifa ikiwamo shirika la Fedha na Benki ya Dunia.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja alisema kwamba Umoja huo utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha amani na maendeleo.
 
Pamoja na kushukuru kwa wananchi wa Tanzania kuwa pamoja na Umoja wa Mataifa katika sherehe hizo muhimu sana Dunia nzima, alisisitiza, ushirikiano kuendelea kuwapo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wadau wa maendeleo, na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Kwa kuadhimisha siku hii ya Umoja wa Mataifa kwa pamoja, tunaimarisha ushirikiano wetu, katika masuala ya msingi, ambayo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wamekubaliana nayo. “ alisema.
Aidha alizungumzia mapatano ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na Tanzania na utekelezaji wa mipango ya maendeleo inayoichangiwa na UN nchini Tanzania chini ya UNDAP na kusema imeleta mafanikio makubwa.
Katika wiki ya Umoja wa Mataifa, wafanyakazi na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi waliwafanya shughuli mbalimbali zikiwamo za upandaji miti, usafi na miradi ya nishati mbadala.
IMG_5788
Gwaride maalum katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa likitoa heshima kwa mgeni rasmi Waziri Membe (hayupo pichani).
IMG_5795
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
IMG_5805
Waziri Membe akitoa heshima kwa bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kama ishara ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5821
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum akisoma dua kubariki sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5826
Kiongozi wa madhehebu ya Kikristo akiongoza sala katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5842
Meza kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe wakishiriki sala maalum ya kuombea amani ya nchi na Umoja wa Mataifa.
IMG_7499
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakitoa heshima kwa wimbo wa taifa.
IMG_6282
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akitoa hotuba katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_6487
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_6501
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe (kulia) akimpongeza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa kwa hotuba nzuri aliyoitoa.
IMG_6518
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza machache kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kabla ya kumkabidhi tuzo maalum Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe (wa pili kushoto) iliyoshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).
IMG_7769
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe tuzo ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa kwa kuzingatia mchango wake katika Maendeleo ya Milenia (MDGs) na Maendeleo Endelevu (SDGs) katika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo jana katika viwanja vya Mnazi mmoja.
IMG_7774
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (katikati) akimpongeza Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe mara ya kukabidhiwa na Umoja wa Mataifa kwa kutambua mchango wake katika Maendeleo ya Milenia (MDGs) na Maendeleo Endelevu (SDGs) katika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo jana katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
IMG_6303
Mshehereshaji katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ambaye pia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
IMG_7565
Meza kuu.
IMG_7573
Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wadau wa Maendeleo pamoja Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaa kuu.
IMG_6385
Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mmoja wa viongozi wa madhehebu ya dini wakifuatilia jambo kwa umakini katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_6334
Pichani juu na chini ni sehemu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja Mataifa walioshiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_5876
IMG_6351
IMG_6341
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulida Hassan na Eliet Magogo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
IMG_7610
IMG_5907
IMG_7624
IMG_6264
IMG_6331
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe hizo.
IMG_7557
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali nao walishiriki.
IMG_7529
Maafisa wa jeshi nao walishiriki.
IMG_7810
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini.
IMG_7865
Meza kuu katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini pamoja na wadau wa maendeleo.
IMG_7821
Meza kuu katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali walioshiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_7855
Meza kuu katika picha ya pamoja na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
IMG_7884
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
IMG_7906
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_8011
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshika mabango ya malengo endelevu.
IMG_7918
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
IMG_7947
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akiteta jambo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum wakati akiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OCTOBER 14, 2015

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari za Magazeti toka vituo mblimbali vya Televisheni October 14, 2015

TBC
NEC Yatumia Mfumo Mpya, ni mfumo wa kujumlisha matokeo, Dkt. Magufuli aomba kura kwenye Mabasi. Pata dondoo hizi za magazeti ya leo hapa. https://youtu.be/4I5dO8epJR8

Star TV
Magufuli Aahidi Bima Ya Afya Kwa Wananchi, Lowassa Kupigania Mikataba ya Madini, Mahujaji wengine 4 wagundulika kufariki. Habarika hapa zaidi. https://youtu.be/qqM7snXi8kM

CH 10
Lowassa ageukia Madini, JK awajia Juu Viongozi Wabovu, Lowassa na Dkt Slaa waua Katiba Mpya UKAWA, Pata uchambuzi zaidi wa magazeti hapa. https://youtu.be/lVEXj7JCT9Y

Azam TV
Tambwe Abaki Burundi, Hofu yatanda, Van Perse na Depay wazichapa mazoezini, kiiza ajitoa mechi ya mbeya City. Pata dondoo za habar za Michezo. https://youtu.be/viEey0srbBQ

MAMA SAMIA AANZA KAMPENI MKOANI KAGERA LEO, AWANADI KAGASHEKI NA MWIJAGE

$
0
0
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Buseresere, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipozunguza na waliposimamisha msafara wake katika eneo la Buseresere, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Chato kwa tiketi ya CCM, Dk. Karineli katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela akijadili jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Balozi Hamis Kagasheki wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo.
Mgombea Ubunge jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera, Charles Mwijage akiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo


Wananchi Buseresere
Mwana mama akiwa kazini wakati msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan aliposimamishwa na wananchi katika eneo la Buseresere mkoai Geita leo
Wananchi wakitazama msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, ulipopita eneo la  Chato mkoani Kagera, huku wakiwa karibu na bango la shule inayotumia jina a Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. John Magufuli
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Chato, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Chato, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo
Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasalimia katika eneo la Chato, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo
Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, alipowahutubia waliposimamisha msafara wake katika eneo la Chato mkoani Geita leo
Wananchi wakimshangilia Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan alipowahutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Chato mkoani Geita leo
Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama samia suluhu Hassan ukiendelea na safari kwenda Muleba mkoani Kagera leo
Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama samia suluhu Hassan ukiendelea na safari kwenda Muleba mkoani Kagera leo
Mama akiwa na mwanae wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera leo
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo la Muleba Kaskazini.
  Bango la kumfagilia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Jihn Magufuli katika mkutano wa kampeni jimbo la Muleba Kaskazini likiwa limeinuliwa kumfikishia ujumbe Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa kampeni jimbo la Muleba Kaskaskazini
Kazi na dawa!
Mtoto akimfuata mwenzake kumnyang'anyana kijibendera cha CCM, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama samia uliofanyika jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera leo
Kisha wakanyang'anyana kama hivi
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Meleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka.
Wagombea Udiwani jimbo la Muleba Kaskazini, wakiwasalimia wanachi walipotambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiagana na wagombea Udiwani katika jimbo la Muleba Kaskazini, baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kulia ni Mratibu wa kampeni za Mama Samia, Anhela Kizigha.
Mama Samia akiaga. wapili kushoto ni Profesa Anna Tibaijuka na watatu ni Charles Mwijage.
Kamachumu
Katerero
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akijadili jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Bukoba mjini, Balozi Hamis Kagasheki, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Kagera.
Msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Bukoba mjini mkoani Kagera leo
Watu wakiserebuka wakati wa shamrashamra kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Bukoba Mjini
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera leo
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uiofanyika leo katika jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera leo
Mgomea Ubunge jimbo la Bukoba mjini,Balozi Hamis Kagasheki akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
Mbunge wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na wadau wa kampeni za Mama Samia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera. Kushoto ni Mwanamuziki Ally Choky maarufu kwa jina na Mzee wa Farasi na Kiongozi wa kundi la Kampeni la Mama Ongea na Mwano, Steven Mengere au Steve Nyerere.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
Vijana wa Buseresere, wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samaia Suluhu Hassan, msafara wake uliposimamishwa na vijana katika eneo hilo wakati akiwa  njiani kutoka Geita kwenda Bukoba mkoani Kagera leo
 

FANYENI KAZI KWA BIDII ILI MUWEZE KUJILETEA MABADILIKO YA KWELI KATIKA MAISHA YENU - MAMA SALMA KIKWETE

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, Liwale
14/10/2015 Wananchi wa mkoa wa Lindi wameaswa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujiletea mabadiliko ya kweli katika maisha yao kwani kuna baadhi ya watu hawapendi kufanya kazi huku wakisubiri mabadiliko.

Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa  vijiji vya Ngunichile na Mbaya vilivyopo katika majimbo ya Nachingwea na Liwale (Pichni)waliohudhuria mkutano wa kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana bila ya kufanya kazi kwani kuna baadhi ya watu hasa vijana hawafanyi kazi wakiamka asubuhi kitu wanachokifanya ni kucheza  pool huku wakisubiri mabadiliko.

“Hata katika vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na asile kwani kazi ni msingi wa maendeleo,  hata ukipiga kelele kiasi gani kama hufanyi kazi huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako”.

“Ndugu zangu Mwenyezi Mungu ametupa akili ya kutambua mema na mabaya tusikubali kudanganywa, mabadiliko ya siku hizi siyo mazuri yanaleta uvunjifu wa Amani kwani watu wamepandikizwa maneno ya chuki wanafanya vurumai na kuharibu vya kwao, wanawachukia ndugu zao imefikia hatua watu hawazikani, hawasalimiani. Lakini hao aliowapandikiza chuki kwao kuna maendeleo”, alisisitiza.

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OCTOBER 14, 2015

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Oktoba 14 2014

 Raisi Jakaya Kikwete anatarajia kuongoza shughuli ya kuzima mwenge wa uhuru mjini Dodoma ikiambatana na Maadhimisho Ya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere. 
Wafanyakazi wa Uchumi Supermarket jijini Dar wamelazimika kulala ndani ya ofisi ya kampuni hiyo kushinikiza madai yao. https://youtu.be/-B413uOYQvQ
   
Raisi Kikwete Jana amezindua mtambo wa kufua umeme wa gesi asilia eneo la kinyerezi utakaozalisha Mega Watt 150. https://youtu.be/2-YDuBMhauI

Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe asema ipo hja kubwa kwa nchi za Afrika kuwa na wajumbe wa kudumu katika baraza la usalama wa kimataifa. https://youtu.be/umszGfWpr1s

Watu wenye ulemavu wameipongeza tume ya taifa ZEC visiwani Zanzibar kwa kuweka mazingira rafiki kwa walemavu kuoiga kura https://youtu.be/ajrtbQJBxXU

Klabu ya Arsenal yasema ipo tayari kumuongeza mkataba mshambuliaji Alexis Sanchez ambaye pia ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo; https://youtu.be/2112f_J6T_o

Ligi kuu soka Tanzania Bara Inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo klabu ya Yanga na Azam Zitalaza Nyasi katika Uwanja Wa Taifa  https://youtu.be/dLEfZOuqVAg

Mgombea uraisi CCM Dkt. Magufuli atangaza kiama kwa wavuvi wanaofanya uvuvi haramu mara atakapopata ridhaa ya Wananchi. https://youtu.be/ejYDYzu8LW8

Mgombea Uraisi anbayeungwa mkono na UKAWA aahidi kusimamia wachimbaji wadogo kupata maeneo ya Uchimbaji. https://youtu.be/FSYd0_xaRZE
Kamanda Wa polisi Iringa Ramadhani Mungi awaondoa hofu wakazi wa mkoa huo na kuwahakikishia usalama wakati wa Uchaguzi. https://youtu.be/W6VU9WoJ4YU 

PRESIDENT KENYATTA ADDRESSES EALA

$
0
0

 The President signs the visitors book at the Kenya National Assembly as the EALA Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega and the Cabinet Secretary for East African Affairs, Commerce and Tourism, Hon Phyllis Kandie look on.
 The President of the Republic of Kenya, H.E. Uhuru Kenyatta addresses an attentive House.

 East African Legislative Assembly 
PRESIDENT KENYATTA ADDRESSES EALA

Lauds Assembly for improved performance, calls for more citizenry participation
East African Legislative Assembly, Nairobi, Kenya, October 14, 2015:  President Uhuru Kenyatta has today addressed EALA, calling on the Assembly to consolidate its work for the furtherance of the integration process.  President Kenyatta further said the citizens of the region were yearning to freely move, work and enjoy the tangible benefits of integration.

The President was addressing a Special Sitting of the 2nd Meeting of the 4th Session of the 3rd Assembly which commenced in Nairobi last week.

The President reiterated his commitment and that of his Government to the integration process. “I will begin by repeating my Government’s complete commitment to East African integration. I know that the future of each of us in the region is bound up with the fate of all the rest.  Leaders must create the laws, the institutions, and the framework that will help us face that future together.  Kenya will play its part in that great task”, President Kenyatta said.

The President further urged stakeholders in the integration dispensation to go the extra mile and create awareness to the citizens of the region. He remarked that citizens of the region needed to be fully aware of the integration process. He said this was a role to be undertaken by both politicians and the ordinary people as well.

“I wish to make is that we who are convinced of the imperative of integration must communicate it better to our people.Too often, the integration of East Africa is taken to be merely a political matter - a job for politicians, not ordinary people.  True, leaders must lead.  But we have failed to spark the imaginations of East Africans when it comes to integration”the President remarked.

The President maintained that the Summit of EAC Heads of State was committed to ensuring the region’s infrastructure is improved for the betterment of their lives. “Some of you will recall that several of my brothers came to the signing and witnessing of agreements for the Standard Gauge Railway, some time ago.

Others – perhaps more, given that it was earlier this month – will recall that my brother President Jakaya Kikwete of United Republic of Tanzania visited Kenya to commission the Taveta-Arusha road” President Kenyatta said.

“These projects are representative of the hard work that has gone into knitting the nations of the community together by road, rail and air” he added. The President lauded the Assembly for its enhanced performance and challenged them to go the extra mile in realizing its mandate.


“A key issue if I may speak directly to the Assembly, Mr. Speaker – is on the performance.  Your mandate ends soon.  In the last few months, under the wise leadership of Speaker Kidega, you have done much: new Bills, reports, and resolutions have flowed at a steady pace.  But if I may say so myself, we would all like to see you leave a legacy: a set of measures that will be remembered as long as this Community lasts”, the President said.  

On sustainability matters, the President was emphatic that direct funding of the Assembly would strengthen the capacity for EALA to deliver its mandate. “Direct funding would strengthen the capacity of the community to deliver its mandate.  It would also hasten the day of complete integration. Now, there remains the matter of sustainability.  It has been proposed that partner states of the community show their commitment to your goals by funding you directly”President Kenyatta said.

It has my complete support, and I will be happy to consult with you to see it introduced quickly and effectively” The President added.

The President also gave a nod to the request by the EALA Speaker to change the mode of Assent of Bills from the rotational mode to be a function on the sidelines of the Summit of EAC Heads of States meeting in order to enhance efficiency.

The Head of State further lauded EAC Secretary General, Amb Dr Richard Sezibera for the role played in effective leadership of the Assembly. In his remarks, the Speaker of the EALA, Rt. Hon Daniel F. Kidega noted that East Africans were interested in seeing more tangible benefits of integration. 

The Speaker called on the Partner States to ensure its full implementation of the Customs Union and the Common Market Protocols stating that bureaucrats in governments were causing unnecessary red tape in the processes.

“Whereas there is political goodwill and commitment to strengthen integration, citizens in the region continue to demand to see the tangible benefits.   Somewhere along the way, there is always some disconnect of some form.  As politicians, we sometimes see the technocrats in Government as the persons hindering progress by instigating red tape and unnecessary bureaucracies”, Rt Hon Speaker said.

He called on government officials to follow procedures in a manner that facilitates rather than encumbers integration. The Speaker called on the Summit of EAC Heads of State to intervene to ensuring the Institutional Review of the EAC is finalized.  He lamented that the Institutional Review process was an expensive affair to taxpayers and time consuming.

“This is none other than the Institutional Review which has been on the cards for the last six years and has cost tax payers – an estimated yet astronomical figure of USD 2 Million! The process has been through a full round in circles much to the detriment of the EAC. On the one side the Secretariat and other Organs remain under-capacitated and under-funded. On the other side, the EAC is unable to realise its full potential”, Rt. Hon Speaker said.

“I appeal to you and through you to the Summit to intervene in the matter”’ he said. He reiterated the need for the mode of Assent to be enhanced by taking opportunity of the EAC Summit of Heads of State. We are of the view that the region takes advantage of the Summit sittings which can create opportune moment for the Summit Members to exercise their mandate as stipulated under Article 63.” Speaker Kidega said.  

The Speaker also called for the full autonomy of the Assembly which he said was necessary to enable it realise its mandate.  “At the moment, the Assembly has a semi-autonomous status. – the ideal scenario would be full autonomy including the direct funding by Partner States.   It is key that we sit down with the Executive in the near future to find a lasting solution to the matter”, he remarked.

The Speaker hailed the progress in Kenya as commendable.  He remarked that the country was on the verge of transformation.  He commended the Government of Kenya’s new procurement policy of allocating quotas to the youth as laudable.

“With regards to youth empowerment, the Government has supported establishment of over 20,000 youth enterprises, trained over 200,000 entrepreneurs and set aside a programme supplemented by a new policy that ensures allocation of 30 per cent of all Government procurement to enterprises owned by the youth, women and people with disability. Such drive/commitment to see the youth aspire to move out of the poverty bracket is commendable” Speaker Kidega said.

Since the Session began, we have successfully debated and enacted the EAC Electronic Transactions Bill, 2014.  This is a key Bill which paves way for the growth of e-transactions in the region by enabling the corporate world and the public sector to transact business using the digital means in a safe and secure environment.

A key Report on the Goodwill Mission of EALA to the Burundi refugees in Kigoma, Tanzania and Rwanda was also debated and passed.  Before we conclude, we hope to pass the EAC Forest Management and Protection Bill 2015 and the EAC Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2015 and to pose key questions to the Council of Ministers.

Moving the vote of thanks, Hon Martin Ngoga noted that Kenya had progressed following the leadership of President Uhuru Kenyatta.  Hon Ngoga lauded the President for reminding EALA on the obligations.   “It is important for us to walk with the people at their pace”, He said.   The member further thanked H.E. Margaret Kenyatta for her contributions towards reducing mortality of the young children in the country.

The EALA Sitting ends on Thursday, October 15th, 2015.

WATAKIWA KUCHANGIA UJENZI WODI YA AKINAMAMA

$
0
0
Mgombea Ubunge kushoto Ridhiwani Kikwete akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mgombea udiwani wa kata ya Kimange wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kata hiyo katika Kijiji cha Pongwekiona 

Na John Gagarini, Chalinze
WAKAZI wa Kijiji cha Pongwe Kiona Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo wametakiwa kushirikiana na serikali ili kukamilisha ujenzi wa wodi ya akinamama.

Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani kwenye kata ya Kimange na kusema kuwa kwa sasa hakuna wodi ya akinamama.

Ridhiwani alisema kuwa moja ya vitu ambavyo amevipa kipaumbele ni upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi ya mama na mtoto ili waweze kuhudumiwa kwa uhakika.

“Nawaombeni wananchi tuungane na serikali kwa kuchangia nguvu zetu kuhakikisha wodi ya akinamama inakamilika kwani kwa sasa hakuna hata chumba cha kujifungulia ambapo wanapojifungua wanachanganyika na wanaume jambo ambalo linasababisha kutokuwa na utu wa mwanamke,” alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa heshima ya mwanamke inapotea kutokana na kutokuwa na wodi hiyo ambayo ingewafanya akimama kuweza kujifungulia sehemu ambayo ina wastiri tofauti na ilivyo sasa hakuna stara kwa wanawake.

“Nawaomba mnichague ili niweze kuwa Mbunge wenu niweze kuhamasisha ujenzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo name nitahakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati ili kuondoa adha wanayopata akinamama wakati wa kujifungua,” alisema Ridhiwani.

Kwa upande wake Mgombe Udiwani Hussein Hadingoka alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anahamasisha wadau mbalimbali kuweza kuchangia ujenzi huo ambao tayari umeashaanza na uko kwenye hatua ya msingi.

Hadingoka alisema kuwa mbali ya ujenzi huo pia atahakikisha ujenzi wa zahanati za Vijiji kwenye kata hiyo unafanyika kwani baadhi ya vijiji havina zahanati hali ambayo inasababisha changamoto ya wananchi kwenda mbali kupata huduma za kiafya huku ilani ya chama ikisema kuwa kila kijiji kitakuwa na zahanati na kata kuwa na kituo cha afya.

Naye mkazi wa Kijiji hicho Asha Bakari alisema kuwa wodi hiyo ikikamilika itakuwa imewaondolea adha ya kujifungua huku wanaume nao wakiwa kwenye chumba kimoja ambapo hadhi ya mwanamke inapotea.

MABADILIKO KATIKA UPASUAJI WA UVIMBE WA SARATANI

$
0
0
Dk. Umanath Nayak, mshauri mkuu wa  magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad nchini India.

Na Mwandishi Wetu,
SEKTA ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi, njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya.

 Teknohama imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara makubwa kwa mgonjwa.

Kuna matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida, au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.

Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa ikitumika awali ya  ‘laparoscopic’. Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.

Upasuaji kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu hali mbalimbali kama vile magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja kuondoa mfuko wa uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani katika mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids uterine), saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi, fistula na viungo katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed). Utaratibu wa upasuaji na ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi kupitia teknolojia hii. Kulingana na huduma ya afya inayoitajika na umri wa mgonjwa, upasuaji kutumia Roboti pia unaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo wa kuzaa.

Kwa wagonjwa wa saratani, mara nyingi upasuaji wa aina hii huusisha upasuaji wa  kichwa, shingo, ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake, kuondoa uvimbe kwenye utumbo (colorectal surgery) na upasuaji unaohusisha nyonga.  

Mfumo huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanahitaji upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini ya shingo. Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.

Dk Umanath Nayak, mshauri mkuu wa wa magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti kutoka hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad India ameelezea faida ya upasuaji kwa kutumia Roboti. Anasema kuwa, "teknolojia ya kutumia Robot katika upasuaji itadumu sana kama tunaweza kuona faida nyingi za teknolojia hii ikilinganishwa na njia mbalimbali za zamani za upasuaji. Ni hatua ya pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu huku ukiangalia kwenye Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja ya kufanya upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi "
Anaongeza kuwa, "Upasuaji wa kutumia Robot ni njia mpya ya upasuaji ya isiyo na madhara na inajumuisha upasuaji wa kawaida (Open surgery) na Upasuaji wa kutumia skrini ya computer (laparoscopic). Kwa msaada wa Mikono maalumu ya Robot inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya upasuaji kupitia mikato midogo sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na makovu makubwa yatokanayo na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu, maumivu baada ya upasuaji na kupona kwa haraka zaidi ".
Aidha mtaalamu wa magonjwa ya saratani nchini Dk. Harrison Chuwa, anasema kuwa “upasuaji kwa njia ya roboti ni njia kuu ya kufanya upasuaji ambayo itapunguza mapungufu ya kibinadamu na hata kovu la operesheni kuwa dogo ambalo aliweze kufanya mwili wako kuonekana tofauti na ulivyokuwa awali. Faida nyingine ya upasuaji kwa njia ya roboti ni kwamba unahitaji rasimali kidogo ya binadamu ili kufanikisha kazi hii.
Teknolojia ya roboti haipatikani nchini Tanzania, lakini watanzania wengi wanasumbuliwa na saratani za kichwa na shingo na mfumo wa mkojo (mfano. kibofu), uzazi, upasuaji wa utumbo mkubwa, na matatizo mengine wamepata huduma hii mara kadhaa pale walipopata rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali za Apollo nchini India.
Ishara nyingine nyingi bado zina mjadala kwa maana njia hii ni mpya tokea upasuaji wa laparoscopic uanzishwe. Muda unavyosogea, upasuaji kwa njia ya roboti unatarajiwa kuchukua nafasi za upasuaji wa kawaida wa saratani na utakuwa ni msaada na kimbilio kwa wengi wanaoteseka na saratani na mapungufu mengine.  Inaweza tokea siku hapo baadae wakati daktari wa upasuaji amekaa ofisini kwake na anamfanyia mgonjwa operesheni au upasuaji akiwa mbali kwa msaada wa mfumo wa roboti.
Mwaka jana, Hospitali Apollo mjini Apollo Chennai na Hyderabad imefanikiwa kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna shaka kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kifaa muhimu katika masuala ya upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi zinazoendelea.

Kuhusu Hospitali ya Apollo

Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.


TASWA FC HOI KWA NSSF

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imeshindwa kutamba mbele ya timu ya soka ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi maalum ya kuadhimisha miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama, mabao ya NSSF yalifungwa na Linus  Bwegoge kwa shuti la nje ya eneo la hatari kutoka wingi ya kushoto na la pili lilifungwa kwa njia ya penati na Khalfan Waziri baada ya beki wa Taswa FC, Khatimu Nahela kumwangusha kwenye eneo la hatari msambuliaji wa NSSF, Ali Chuo.

Bao la Taswa lilifungwa na Khatimu Naheka baada ya beki wa NSSF, kumchezea rafu mbaya Shadraki Kilasi aliyekuwa anakaribia kufunga.  Katika mchezo, Taswa  Fc ingeweza kusawazisha na kama si kukosa penati kwa mshambuliaji wa Taswa FC, Saidi Seifu ambaye kipa wa NSSF aliipangua.

Penati hiyo ilitolewa baada ya beki wa kati wa NSSF kumwangusha Zahoro Mlanzi aliyecheza vizuri na mshambuliaji wa pembeni wa timu Taswa FC Angetile Osiah ambaye pia alikosa mabao mawili ya wazi baada ya kupiga mpira nje.

Mbali ya Osiah, Seif, Julius Kihampa na Mohamed Akida nao walikosa nafasi nyingi za wazi katika mechi hiyo ambayo wachezaji, Wilbert Molandi, Nurdin Mponda, Jabir Johnson na Simon walicheza vizuri sana.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa hawajaridhika na kipigo hicho cha mara ya kwanza tokea kuanza kwa mwaka huu na kujipanga upya kwa ajili ya mechi ya marudiano.

JE MALI ILIYOPATIKANA KABLA YA NDOA INAHESABIKA NI YA FAMILIA ?.

$
0
0
MARA  kadhaa  linapoibuka  suala  la  kugawana  mali  pale  ndoa  inapohesabika  kushindikana   masuala  kadhaa  ya  msingi  na  yanayohitaji  uelewa  huwa  yanaibuka. Moja  ya  suala  kati  ya  masuala  ambayo  huibuka  ni  hili  la  kutenganisha  na  kufafanua  hadhi  ya  mali  za  wanandoa  ili  mgawanyo uweze  kufanyika  kwa  haki. Yawezekana  mwanandoa  akadhani  ana  haki  katika  mali  fulani  lakini  kumbe  kisheria  hana  haki  hiyo  ni mtazamo  wake  ndio  unamsukuma  kuamini  hivyo. 

Halikadhalika  yawezekana  mwanandoa  kudhani  hana  haki  katika  mali  fulani  kumbe  anayo  haki.  Ili kujua    una  haki  ipi katika  mali  ipi  na  huna  haki  katika  mali  ipi yahitajika  kujua  misingi  ya kisheria  inayotumika  kugawanya   mali  za  wanandoa.


1.KUGAWANA  MALI  ZA  WANANDOA.
Ieleweke  kuwa  tunapoongelea  wanandoa  kugawana  mali  tunaongelea  talaka. Hakuna  kugawana  mali  bila  talaka. Na  kisheria  talaka  inapotoka  tu swali linalofuata ni  habari  ya  mali  na  watoto  kama  wapo.  Mali  si  lazima  magari  na  manyumba  lakini  pia hata  vyombo  vya  ndani  vikiwemo  vitanda, makabati, sahani  n,k  nazo  ni  mali  kwa  mujibu  wa  sheria. Navyo  huhitaji mgao.


2.  JE  KUGAWANA  MALI  NI  NUSU  KWA NUSU ?.
Linapokuja  suala  la  kugawana  mali  wengi hudhani mtindo unaotumika  kugawa  ni  ule  wa    nusu  kwa  nusu.  Jambo  hili  si  kweli  kwakuwa  sheria  ya  ndoa 1971 iliyofanyiwa  marekebisho  2002  haisemi  kuwa  utaratibu  wa  kugawana  mali  ni nusu  kwa  nusu. Sheria  hii  imeweka  msingi  mkuu  wa  kugawana  mali  ambao  ndio  hutumika  katika  mahakama  zetu  katika  kutoa  maagizo  ya  kugawa  mali  za  wanandoa.  

Msingi  uliowekwa  na  sheria  ni  msingi  wa  kiwango  cha  mchango  wa  mwanandoa  katika  kupatikana  kwa mali  husika.  Kiwango  alichochangia  mwanandoa  katika  kupatikana kwa  mali hiyo  ndicho  kitakachokadiriwa  na  kiwango  hicho ndicho atakachopewa. Kwa hiyo  kama  ni  nyumba  ya  vyumba  sita  mmoja  anaweza  kupata chumba  kimoja  na mwingine  akapata  vitano kutegemea  na  mchango  wake. Na  mchango  hapa  sio  leta  ni lete. Mchango  sio  hela  tu  hata  kazi  za  nyumbani  anazofanya  mama  wa  nyumbani  ambaye  haleti  hela  nazo  huitwa  mchango  ambapo  hukadiriwa  na  kupata  kile  anachostahili.


3.  MALI  KABLA  YA  NDOA  NA  BAADA  YA  NDOA.
Katika  kutenganisha  mali  za  wanandoa   huwa  zinatenganishwa  katika  makundi  makuu  matatu. Kwanza kuna  mali ambazo  mtu  alikuwa  nazo  kabla ya  ndoa   na  wakati  anaingia  katika  ndoa  ameingia  nazo. Kwa  mfano  mwanamke  ameolewa  akamkuta  mwanaume  tayari  ana  nyumba  yake. Pili  kuna  mali  ambazo  zimepatikama  wakati  wawili  wakiwa  katika  ndoa . Kwa  mfano  ndoa  imefungwa  wawili  wakaanza  kuishi  pamoja  na  taratibu wakaanza  kujenga  na  kukamilisha. Na  tatu ni  mali  ambazo  zimepatikana  katika  ndoa  lakini zikiwa  hazina  uhusiano  wowote   wa kindoa kwa  mfano kurithi  au  kuzawadiwa mali. Tutaona hapa  chini  mazingatio  ya  sheria  ya  kila  moja  katika  haya.


4. JE  MALI  ILIYOPATIKANA  KABLA  YA NDOA  INAHESABIKA  NI  YA  FAMILIA.
Mali iliyopatikana  kabla  ya  ndoa  na  ikaendelea  kuwepo  kipindi  cha  ndoa inaendelea  kuwa  ya  huyo  mwenye  nayo bila  ushirika  wa  mwenza  wake. Kama  ni  nyumba  mwanamke  alikuwa  nayo  kabla  ya  kuolewa  au  ni  mwanaume  alikuwa  nayo  kabla  ya  kuoa  basi  inaendelea  kuwa  ya kwake  peke  yake  na  haihusiki  katika  mgao  suala  la  mgao  linapojitokeza.


Hata  hivyo  inaweza  kuingizwa  katika  mgao  ikiwa  kuna  mchango  wowote  wa  kuiendeleza uliotolewa  na  mwenza. Kwa mfano  kabla  ya  ndoa  ilikuwa na  vyumba viwili  lakini  katika  kipindi  cha  ndoa  imepanuliwa  na  kufikia  vyumba  vitano,  au  ilikuwa  haina  uzio, au  haina  madirisha  kabla  ya  ndoa  lakini  baadae  vitu  hivi  vikawepo. Katika  hali  kama  hiyo  itatakiwa  iingizwe  katika  mgao  na  kutazama kiwango cha  mchango wa  kila  mmoja  katika  uendelezaji  huo.  Ni  hapo  ambapo  mchanganuo  utafanyika ili  kila  mmoja  apate  haki  kutokana  na  kiwango  cha  mchango  wake.


Ikiwa  hakuna uendelezaji  wowote  uliofanyika  katika  mali  yaani  labda  nyumba ilivyokuwa  kabla ya  ndoa  ndivyo  hivyohivyo  ilivyoendelea  kubaki  hata  baada  ya  ndoa  basi  mali  hiyo  haitatakiwa  kuingizwa  katika  mali  za  mgao  bali  itabaki  mali  ya  mwanandoa  mmoja  pekee  ambaye  ndiye  mmiliki  wa tangu  awali.  


Hali  ni  hiyo  hiyo  hata kwa  mali  ambayo  imepatikana  katika  ndoa  lakini  ikiwa  haina  uhusiano  na  kipato  cha  wanandoa,  kwa  mfano  mali ya urithi au  zawadi. Hii  ina  maana ikiwa  mali  hii  itaendelezwa  basi mchango  wa  uendelezaji  utatathiminiwa  na  ikiwa  haitaendelezwa  basi  itabaki  mali  ya  mrithi  au  mpewa  zawadi  pekee  na  haitahusu  mgao.


MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGWA MWILI WA MAREHEMU DKT. KIGODA KARIMJEE DAR.

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, wakati alipowasili kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kuswalia mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, aliyefariki dunia majuzi Hospitali ya Apollo nchini India, alipokuwa amelazwa akitibiwa. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Maafisa wa Bunge wakibebea Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati ulipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuagwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu, kumswalia Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati wa swala hiyo iliyoswaliwa kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Baadhi ya Wanafamilia wa marehemu Dkt. Kigoda.

Sehemu ya waombolezaji na Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo ya msiba Karimjee.
Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, akizungumza kutoa salamu kwa niaba ya Bunge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakijumuika na baadhi ya biongozi wa Kitaifa na Waombolezaji, kushiriki katika shughuli ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, iliyofanyika leo Okt. 15, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
 Picha na OMR

EVERJOBS TANZANIA CAREER REPORT.

$
0
0
In a recent World Economic Forum report, Tanzania was listed as one of the 13 fastest growing economies in the world. This comes as no surprise with GDP growing around 6-7% each year since 2009. In addition, with GDP projected to grow until 2017, many industries will continue to benefit, including the services sector. This latest edition of the everjobs Tanzania career report was assembled based on data collected from  everjobsfor the month of September 2015.



New data from the everjobs Tanzania career report shows that the services industry accounted for the largest number of available job positions in September. Job opportunities in the NGO sector are growing rapidly, followed by Financial Services, and Distribution/Logistics opportunities. Not only are these three categories providing ample employment opportunities, they also seem to be popular among job seekers, receiving almost 40% of applications made. Moreover, the Broadcasting / Music / Film industry was the most popular among job seekers, receiving, 15% of applications made in September.



The financial sector in Tanzania has expanded and become more competitive in recent years. Interestingly, foreign banks are very active in Tanzania, accounting for 48% of total assets in the industry. In addition, the increase in competition has benefited customers, as quality of financial services has increased. “With the projected economic growth, it is likely that this sector will continue to provide many opportunities for job seekers” said Tanzania Country Manager Florens Roell.



The career report also finds that most employment opportunities are located in Dar es Salaam, accounting for 77% of the total. The cities that follow include Arusha and Mwanza.



everjobs is an online job portal, already operating in Cameroon, Ivory Coast, Senegal, Uganda, and Ethiopia. Launched in March 2015, everjobs aims to become the Pan-African recruitment platform. The company is backed by the Africa Internet Group (AIG).

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA15, 2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 15, 2015.



SIMUtv: Michuano maalum ya gofu kufanyika jumamosi hii katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es Salaam kwalengo ya kuunda kikosi cha taifa; https://youtu.be/yLAoH5MvQ2U

SIMUtv: Waangalizi wa Uchaguzi kutoka SADC wawataka watanzania kuwa watulivu kwa kufuata sheria na kanuni za nchi kuelekea uchaguzi mkuu. https://youtu.be/BOGEYz5goVE

SIMUtv: Watanzania waombwa kudumisha amani, umoja na mshikamano iliyoachwa na muasisi wa taifa Hili Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. https://youtu.be/im-nOHsCoAY

SIMUtv: Raisi Jakaya Kikwete awataka watanzania kutunza shahada zao za kupigia kura ili kusiriki kikamilifu katika upigaji kura Oktoba 25.  https://youtu.be/tLHVjuI4ai8

SIMUtv: Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wamesema ili kumuenzi baba wa Taifa, viongozi na wananchi wanapaswa Kupinga ukabila na udini. https://youtu.be/ettrrIp1zi4

SIMUtv: Mwili wa aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda umewasili jana Nchini kutokea Nchini India. https://youtu.be/8EZt57Ehw-A

SIMUtv: Tume ya Taifa Ya Uchaguzi NEC imezindua kituo cha mawasiliano kitakachosaidia wadau wa uchaguzi kupata elimu ya mpiga Kura. https://youtu.be/KazdhuLzaLM
SIMUtv: Viongozi mbalimbali waungana na wananchi kumuaga aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara DR.Abdallah Kigoda  viwanja vya Karemjee https://youtu.be/A3JSkTe9HjQ

SIMUtv: Wadau wa biashara na viwanda nchini watoa salamu za rambirambi kwa familiya ya Dr.Kigoda na wananchi kwa ujumla; https://youtu.be/OyllSiz7MGk

SIMUtv: Anne Makinda aeleza mchango wa hayati Dr.Kigoda katika kamati ya uchumi na fedha pamoja na  kulinda haki za watoto https://youtu.be/JF6feNTGnDs

SIMUtv: Waziri wa mambo ya ndani  Mh.Mathias Chikawae kwa niaba ya Serikali atoa  salamu za rambirambi kwa waombolezaji https://youtu.be/cONLtPUFZcw

SIMUtv: Asha Kigoda, msemaji wa familia ya Dr.Kigoda atoa maneno ya shukrani kwa serikali na kueleza jinsi safari ugonjwa ya waziri ilivyokuwa https://youtu.be/AAjnwfWSArk

SIMUtv: Tambau mambo ya kufanya kabla na baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu ambapo zimesalia takribani siku 9 kwa uchaguzi huo kufanyika https://youtu.be/Q6SZSWJaogc

SIMUtv: Yajue mafanikio ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa mradi wa kilimo wa matrekta wa suma JKT katika kuboresha sekta ya kilimo Nchini https://youtu.be/SdPfaBfR1PE

SIMUtv: Yajue maswali ambayo huulizwa kwa wingi na wananchi kwa Dokta Mwaka kutokana na magojwa mbalimbali yakiwa na ufafanuzi wake pia https://youtu.be/qOdQy8Ho3nI

SIMUtv: Fuatilia mada inayozungumzia elimu ya mpiga kura zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25: https://youtu.be/JCuUZf32tSA
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images