Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 663 | 664 | (Page 665) | 666 | 667 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari za Magazeti toka vituo mblimbali vya Televisheni Oktoba 15, 2015.
  Channel 10
  TBC 
  Hatutawavumilia watakaofanya vurugu wakati wa uchaguzi mkuu, Mwili wa waziri Kigoda kuagwa leo. Ndivyo yasemavyo magazeti ya leo;  https://youtu.be/CGjIrO7T8q0

  Azam TV
  Yanga yaipania Azam fc, Mwingereza,Mholanzi vitani . Pata kujua kile wahariri wa michezo walichokipa kipaumbele siku ya leo; https://youtu.be/31MOwWiwhnI

  MLIMANI TV 
  Sh.Bilioni 7.8 zatumika ‘kununua’ ikulu. Waratibu walipwa mil.4 kwa mwezi tangu 2013, Mfanyabiashara maarufu nchini adaiwa kuratibu dili, https://youtu.be/yeESunsrHNs

  0 0

   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimpongeza mmoja wa wakazi wa Ukonga mara baada kughani shairi lililokuwa likimsifia kuwa ana sifa zote za kuwa Rais wa Tanzania,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Ukonga jijini Dar
    Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimpongeza mmoja wa wakazi wa Ukonga mara baada kughani shairi lililokuwa likimsifia kuwa ana sifa zote za kuwa Rais wa Tanzania,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Ukonga jijini Dar
    Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Ukonga mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Dkt Magufuli amemaliza mkutano wake wa kampeni jimbo la Kisarawe,Ukonga na baadae anatarajia kuhutubia mkutano wa Kampeni Pemba na Unguja.
   Wakazi wa Ukonga wakishangilia kwenye mkutano huo wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Ukonga mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Dkt Magufuli amemaliza mkutano wake wa kampeni jimbo la Kisarawe,Ukonga na baadae anatarajia kuhutubia mkutano wa Kampeni Pemba na Unguja.
   Wakazi wa Ukonga wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe uliofanyika leo mchana kwenye uwanja wa mpira moshi bar.

   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimwombea kura mgombea Ubunge jimbo la Kisarawe Selemen Jaff mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa kampeni
    Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimwombea kura mgombea Ubunge jimbo la Kisarawe Selemen Jaff mapema leo asubuhi mbele ye Wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa kampeni
   Mgombea Urais wa CCM John Pombe Magufuli akionesha picha yake aliyokabidhiwa kama zawadi na mkazi wa Kisarawe mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akihutubia wakazi wa Ukonga mara baada ya kumsimamisha wakitaka awasalimie na wamweleze shida zao ili atakapokuwa Rais aweze kuwasaidia,Dkt Magufuli alikuwa akitokea Kisarawe kwenye mkutano wake wa kampeni.
   Katika hali isiyo ya kawaida vijana walijitokeza kuanza kufuta barabara ya vumbi ili Mgombea Urais Dkt Mafuguli aweze kupita


  0 0

  Ofisa Uchaguzi na Utawala Bora wa Halmashauri ya Kisarawe, Constantene Mnemere, akizungumza na washiriki wa mdahalo wa amani wakati wa uchaguzi kwa watendaji wa Serikali za Mitaa,Polisi na watumishi wa Halmashauri hiyo jana.
  Ofisa Habari wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Goodness Mrema, akielezea muongozo wa mdahalo wa amani kwa wenyeviti, watendaji wa serikali za mita na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani jana, wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi.
  Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Sara Kinyaga, akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Baadhi ya washiriki wakimpongeza Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) (kushoto) baada ya kuanzisha mjadala wa amani wakati wa uchaguzi mkuu, wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana.

  0 0
 • 10/15/15--03:47: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala kwa mbele ya wadau wa ujenzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mara baada ya kukutana na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) eneo la Tazara jijini Dar es Salaam mkataba uliosainiwa kati ya Tanroads na kampuni ya Sumiton Mitsui Constraction Co. LTD ya nchini Japan mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam leo.
  Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada akizungumza na wadau wa ujenzi walipokutana kusaini mkataba wa ujenzi wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale wakiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada wakisaini mkataba kwaajili ya ujenzi wa barabara ya juu (Fly over)eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wadau wa ujenzi leo jijini Dar es Salaam na kuhusiana na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) maeneo ya Tazara ambao utajengwa na kampuni ya Sumiton Mitsui Constraction Co. LTD ya nchini Japan. 

   
  Baadhi ya wadau waliohudhulia mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Msanii wa mziki wa Hip hop wa nchini Kenya ambaye pia ni Daktari nchini humo, Francis Hamis ( a.k.a Frasha) akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA Tower na waandishi wa habari kuhusiana na kutumbuiza kesho Ijumaa ambapo baada ya kutumbuiza atatembelea vituo kadhaa vya watoto yatima hapa jijini Dar es Salaam ataanza na kituo cha Trust youth Care pia mesema kuwa kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 10 kwa kabla ya saa  sita usiku na baada  ya saa sita kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam. Nyimbo atakazo tumbuiza ni WekaWeka Kutibu pamoja na Dalia.
  Kulia ni Meneja mauzo wa kinywaji cha Johnnie worker, Francis Tibaikana akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vinjwaji vitakavyokuwepo wakati wa msanii Frasha akitumbuiza amesema kuwa chupa moja ya kinjwaji cha Johnnnie Worker itauzwa kwa shilingi laki moja na elfu idhirini badala ya shilingi  laki moja na elfu hamsini. Pia aliwaalika watanzania kuhudhulia wakati wa msanii huyo akitumbuiza na kujipatia ofa za pumbuzo la bei la kinywaji cha Johnnie Worker ikiwa msanii huyo atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

  0 0   Picha mbali mbali za wajumbe na viongozi na wataalamu (washauri) kutoka shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) pamoja na wafanyakazi wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania wakiwa katika semina ya juu ya usimamizi wa sheria na kanuni za usimamizi wa mionzi ya nyuklia Tanzania, iliyofanyika makao makuu ya Tume ya Mionzi Tanzania yaliyopo jijini Arusha. Picha na Yohana Challe.

  NA; YOHANA CHALLE ARUSHA.
  TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), imesema kuwa imejiandaa vilivyo katika usimamizi wa uchimbaji wa madini ya urani ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia John Mngodo alisema kuwa moja ya majukumu ambayo serikali inafanya ni kujiandaa juu ya kusimamia uchimbajia wa madini hayo.

  “Mkazo uliowekwa hapa ni kwamba ni lazima usalama wa mionzi upewe mkazo hivyo TAEC itahakikisha usalama unakuwepo na katika kila hatua ambayo watakuwa wanajiandaa au wanachimba na kusafirisha madini ya urani lazima ukaguzi ufanyike na kutoa kibali ili kuhakikisha usalama unakuwepo” alisema Mngodo.

  Mngodo alizungumza hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la kupitia taratibu za uendeshaji, ukaguzi na usimamzi wa nyuklia na mionzi hapa nchini, zoezi hili lilifanyika kwa siku kumi tangu Oktoba 4 hadi oktoba 14 mwaka huu katika makao makuu ya Tume hiyo mkoani hapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 10 duniani.

  “Wataalamu hawa walikuwa wakipitia taratibu na namna ya jinsi ambavyo tunavyosimamia shughuli za mionzi na nyuklia hapa nchini” alisema Mngodo.

  Wataalamu hawa wametokea katika nchi za Jordani, Irend, Ubelgiji, Sudani, Kenya,Ukreini, Argentina, Australia, Pakistani, Nigeria, Zimbabwe, Uingereza na Zambia

  Wataalamu hawa walikuja kwa mwaliko wa serikali ili kuweza kuisaidia Tume hii ili kuweza kuboresha zaidi shughuli zinazoendelea hasa elimu kwa wafanyakazi, pamoja na kupitia sheria na kanuni za usimamizi wa masuala ya Nyuklia na mionzi hapa nchini.

  Aliongeza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni jinsi ya kuwapata wataalamu wa kusimamia shughuli hizo (rasilimali watu) pamoja na fedha, japo akiipongeza serikali kwa kuendelea kujitahidi kutoa mafungu ili kuendelea kuboresha shughuli za Tume.

  Kwa upande wake Leonard Kifanga ambaye ni Mwanasayansi mwandamizi wa nyuklia, alisema kuwa lazima Tanzania iwe na mipango mikakati ya kuboresha na kushughulikia ajali za kinyuklia zinazoweza kujitokeza, kwani itasaidia kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuepukika kwa urahisi na kwa haraka.

  “Nashauri lazima Tume na Taasisi za kusimamia majanga ziwe huru ili zifanye kazi kwa uhuru zaidi na kwa haraka ili kila mtu aweze kuwajibika katika nafasi yake na hii itasaidia kujua tatizo lilipoanzia” alisema Bwana Kifanga.

  Kifanga ni mmoja wa waatalamu kutoka nchini waliokwenda japani kwenye uchunguzi wa mlipuko wa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichotokea baada ya kutokea tetemeko la ardhi lililoharibu mfumo wa kinu cha nyuklia na hatimaye kinu kupasuka na kutokea mlipuko.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuashiria kufungua rasmi tawi la Benki kuu ya Tanzania Dodoma Oktoba 15,2015.Kushoto ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu(picha na Freddy Maro)

  0 0

  SKIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi kati ya Yanga SC dhidi ya Azam utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kiingilio vha chini kikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vyenye rangi ya bluu, Kijani na Machungwa.
  Tiketi za mchezo huo zitauzwa siku ya mchezo Jumamosi katika eneo la Uwanaj wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo kingilio cha juu kitakua ni Shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, na Shilingi Elfu Ishirini (20,000) kwa VIP B & C.
  Mwamuzi wa mchezo huo atakua Abdallah Kambuzi kutoka mkoani Shinyanga, akisaidiwa na Makame Mdogo (Shinyanga), Robert Luhemeja (Mara), mwamuzi wa akiba Frank Komba (Dsm) huku Kamisaa wa mchezo akiwa Joseph Mapunda kutoka mkoa wa Ruvuma.
  Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi ni Majimaji FC dhidi ya African Sports katika uwanja wa Majimaji mjini Songea, Ndanda FC wakiwakaribisha Toto African katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mbeya City FC watawakaribisha Simba SC kwenye dimba la uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United wakiwakaribisha Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyaga, Jijini Tanga Coastal Union watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mkwakwani.
  Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Kagera Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku wachimba Almasi wa Mwadui FC wakiwakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Mwadui Complex.

  0 0

  Mbunifu wa Mavazi nchini, Mustafa Hassanali akizungumza na  Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya umuhimu wa Amani hususani katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Mwaka huu na kusisitiza onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe Oktoba  17 Mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon uliopo Eater Point Namanga, ambalo litakaloonyesha kazi za wa wabunifu mbalimbali kama Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini taarifa iliyokuwa inatolewa na Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika,Mstafa Hassanali juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25,Mwaka huu.

  Na Bakari Issa

  Wabunifu wa Mavazi nchini Tanzania, Mustafa Hassanali,Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda wameazimia kukusanya nguvu kwa pamoja ili kuhubiri juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25,Mwaka huu.


  Wabunifu hao wamekusanya nguvu kwa pamoja kwa kuwa na onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe 17 Octoba Mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon uliopo Eater Point Namanga,ambalo litakalo onyesha kazi za ubunifu zilizofanywa na wabunifu hao watatu.


  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Saalam,Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika ,Mustafa Hassanali amesema kutokana na wimbo wetu wa Taifa “Hekima,Umoja na Amani,hizi ni Ngao zetu”kuna umuhimu kwa vijana kukuza na kulinda Uhuru,Amani na Utulivu wa nchi.


  Kwa Upande wake,Martin Kadinda amesema Uchaguzi Mkuu ni wa muhimu sana,hivyo basi vijana wa Kitanzania wahakikishe wanapiga kura kwa Amani katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25 na kukaa katikahali ya Utulivu kwa kufuatilia na kukubali matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) katika hali ya Amani.

  0 0

  Viongozi wa Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wa kuomba Dua Mkutano huo wa Baraza la Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania uliovikutanisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tamzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.wa kwanza Jaji Lubuva Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Mzirai na Msajili Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzani Mhe Ibrahim Mkwawa.
  Mmoja wa Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania akiuombea Mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. ukizungumzia maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania .
   Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiitikia dua kabla ya kuaza kwa mkutano huo kuutakia baraka 

   Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Peter Mzirai kuaza kwa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tanzania.
  Viongozi wa Vyama vya Siasa wakimsikiliza Mtoa Mada Msaidizi Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Ibrahim Mkwawa, akiwasilisha mada ya Maadili iliotiwa saini na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
  Msajili Msaini wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Ibrahim Mkwawa akiwasilisha Mada ya Maadili ya Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wote wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu mwezi huu. 
  Viongozi wa Vyama vya Siasa wakifuatilia Mkutano Huo. katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
  Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiwa makini wakifuatilia mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania ukizungumzia Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanxzania unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
  Viongozi wa Chama cha TADEA wakifuatila mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania. 
  Viongozi wa Chama cha AFP wakifuatilia mkutano huo kwa makini unaozungumzia Maadilidi ya Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot Zanzinews.com.
  Mobeli No 0777 424152 or 0715424152
  Email, othmanmaulid@gmail.com.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza na waandi wa habari wapo picha juu ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.kikao hichi kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza juu ya ujenzi huo na  Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na  Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbarimbari na Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)


   WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba kwenye maeneo ya mji huo.

  Akizungumza na wandishi wa habari badaa ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Merchants Group itakayosimamia ujenzi huo, Dk Hu Jianhao, Membe alisema katika ujenzi huo utakaochukua hekta 2400, wananchi wote watakaohuswa hawataachwa bure.


  “Mradi huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group, wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi,” alisema.

  Mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

  Mazungumzo hayo ni sehemu ya awali ya maandalizi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo, katika sherehe inayotarajiwa kuongozwana Rais Jakaya Kikwete leo.

  Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka jana, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi huo.

  Eneo hilo  litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

  Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

  Dk Turuka alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano.

  Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

  Kwa mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.
  mwaka 2008, Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

  Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.
  Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Shehe Abdullah Al Saadi.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete akiungana na wananchi wa Handeni Mkoani Tanga, katika kumzika aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Kigoda Rais akiwa na chepe ya mchanga.

  0 0  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Perera Ame Silima akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano wa Kampeni wa jimbo hilon uliofanyika katika viwanja vya mpira Bamata Kwamtipura Unguja akimuombea Kura Mbunge wa Jimbo hilo Ussi Salum Pondeza AMJADI na Mwakilishi Miraji Kwaza kwa Wananchi wa Chumbuni. 
  Viongozi wa CCM Wilaya ya Amani Unguja wakimsikiliza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Perera Ame Silima akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Chumbuni katika mkutano wa kasmpeni ya Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani. 
  Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifuatilia mkutano wa kampeni ya Wagombea wa Jimbo la Chumbuni katika viwanja vya mpira vya Bamita kwamtipura. 
  Naibu Katibu Mkuu Wazazi Zanzibar Najma Giga akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar katika mkutano wa kanmpeni wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya Bamita kwamtipura Unguja na kuwataka kukipigia kura Chama cha Maspinduzi na Wagombea wake wote. 
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Mohammed Chombo akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kabla ya kuwatambuliwa Wagombea na kuwaombea kura na kuwataka kumpigia kura ya Ndio Dk Ali Mohamed Shein, kwa maendeleo ya Zanzibar na viongozi wote wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. 
  Wagombea Uwakilishi na Ubunge wakiwa katika viwanja vya Bamiti wakati wa mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Bamita kwamtipura Unguja.
  Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Kwaza akiwahutubia Wananchi wa Jimbo hilo akitangaza Sera za CCM za Ilani ya CCM ya Uchaguzi. wakati wa mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira bamita kwamtipura. 
   Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifuatilia m,kutano wa Kampeni wa Jimbo lao.
   Viongozi wa CCM Wilaya ya Amani wakifuatilia mkutano wa Kampeni ya Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakati wa mkutano wa kampeni ya Jimbo hilo uliofanyika katika viwanja vya mpira bamati.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni akiwahutubia Wananchi katika viwanja vya Bamita Jimbo la Chumbuni Zanzibar.
  Mgombea Ubunge Jimbio la Chumbuni Ussi Salum Pondeza AMJADI akiwahutubia wananchi wa jimbo la chumbuni katika mkutanon wake wa kampeni ya kugombea Ubunge Chumbuni uliofanyika viwanja vya Bamita. 
    
   Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakisherehekea ahadi za Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Ndg Ussi Salum Pondeza AMJADI, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofabnyika katika viwanja vya bamita kwamtipura.

   Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimshangilia mgombea Ubunge wa Jimbo hilo wakati akiwahutubia na kutoa Sera za CCM katika kuliletea maendeleo Jimbo hilo.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Ndg Ussi Salum Pondeza AMJADI askisalimiwa na viwaja wa jimbo hilo la Chumbuni baada ya mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Bamita kwamtipura Unguja akiendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua.
  Imetayarishwa na Othmanmapara.Blogspot. Zanzinews.com
  Mobile No 0777424152 or 0715424152.

  0 0

  Na Mwandishi wetu Washington DC.
  Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani(ZADIA), imeunga mkono matamshiya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zaznibar Mh. Othman Massoud Othman aliyoyatoa hivi karibuni mjini Unguja.
  Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman
  Katika taarifa yake fupi kwa umma ambayo Swahilivilla imepata nakala yake, ZADIA ilimnukulu Bwana Othman akisema kuwa Katiba ya Zanzibar inampa kila Mzanzibari wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha Uhuru wa Zanzibar, Mamlaka ya Zanzibar, Ardhi ya Zanzibar na Umoja wa Zanzibar.
  "Maelezo hayo ya Mheshimwia Othman, yanakwenda sambamba na malengo makuu ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA)", ilisema taarifa hiyo, na kusisitiza "Kwa hivyo, ZADIA inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza na kumuunga mkono Mheshimiwa Othman Massoud Othman kwa kauli zake hizo za kizalendo".
  Taarifa ya ZADIA iliyosainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bwana Omar Haji Ali, imeendelea kuelezea juu ya Bwana Othman alivyowakumbusha Wazanzibari jinsi alivyotekeleza wajibu wake huo wa kikatiba kivitendo kwa kupiga kura "kama alivyopiga" kwenye Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.
  Aidha taarifa hiyo imemkariri msomi huyo wa Sheria akizifafanua kasoro zilizomo kwenye Katiba pendekezwa ya Tanzania ambayo aliielezea kuwa haina maslahi kwa Zanzibar."Kitendo hicho cha kijasiri, na maelezo hayo, vinatoa changamoto kwa Kila Mzanzibari kuiga mfano huo. 

  Nasi Wanadiaspora tumezipokea kwa moyo wote changamoto hizo na kuzifanyia kazi kama ambavyo imekuwa kawaida yetu. Na tutafanya juhudi zote na tutashirikiana na wadau wote, ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata hadhi yake na haki zake ndani ya Muungano wa Tanzania", imemalizia taarifa ya ZADIA.
  Itakumbukwa kuwa Mheshimiwa Othman Massoud Othman, alikuwa ni miongoni mwa Wazanzibari waliopiga kura za wazi za "hapana" kwenye Bunge Maalum La Katiba mjini Dodoma kupinga rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri a Muungano wa Tanzania kwa vile ilikuwa inaikandamiza Zanzibar.
  Kitendo hicho kilizingatiwa na Wazanzibari wengi kuwa ni cha kijasiri na kizalendo, lakini wachambuzi wanaona kuwa ilikuwa ndiyo sababu ya kuvuliwa wadhifa wake kama Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
  Hii ilikuwa ni mara ya mwanzo kwa Bwana Othman kuzungumza hadharani tangu kuvuliwa cheo hicho, na kumekuweko na tetesi kadhaa wa kdhaa katika mitandao ya kijamii zikimpa nyadhifa mbalimbali zikiwemo za Kimataifa.

  0 0

   Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri.
   *************
  Onyesho la muziki la Coke Studio ambalo linajumuisha Kolabo ya wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wan je limeanza kurushwa nchini Jumamosi nchini kupitia luninga ya Clouds ikiwajumuisha wanamuziki Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao wanashirikiana na wanamuziki Wangechi,Maurice Kirya,Victoria Kimani na 2Face.
  Baada ya uzinduzi huo zilifanyika party za kukata na shoka katika viwanja vya maraha sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha zilzowajumuisha vijana kucheza muziki,kuimba na kufurahi na kujishindia zawadi mbalimbali za Coca Cola.
   Wadau mbalimbali ndani ya Coce Studio Party
   Baadhi ya mayanki waliohudhuria Coke Studio party wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
   Ilikuwa ni burudani kubwa vijana wakicheza muziki kwa furaha ndani ya Maisha Club.
   Vijana wakishiriki kuimba Coke Studio Party mkoani Mwanza
   zawadi mbalimbali zilitolewa katika party ya Mwanza kama anavyoonekana Masai akijichukulia zawadi katika party ya Mwanza
   Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri
  Watu wa rika mbalimbali walifika CokeStdi party kupata burudani kama wanavyoonekana baadhi yao pichani mjini mwanza

  0 0

  IMG_8357

  Cake maalum iliyoandaliwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
  IMG_8408
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakifanya 'cheers' ya kutakiana afya njema na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  IMG_8411
  Tunywe kwa afya.
  IMG_8432
  Fataki zikipamba mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8427IMG_8449
  Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi (kulia) na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues wakibadilishana mawazo na baadhi ya waalikwa kwenye mnuso huo.

  IMG_8548
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
  IMG_8579
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakikata cake ya birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8587
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akiendelea na zoezi la kukata vipande vya cake huku baadhi ya wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia zoezi hilo.
  IMG_8598
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifurahia picha pale camera ya Modewjiblog ilipommulika.
  IMG_8612
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akifurahi jambo na viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
  IMG_8487
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo, Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoyam pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem.
  IMG_8402
  Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.
  IMG_8457
  Kiongozi wa Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali Tanzania Balozi Juma Mpango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo.
  IMG_8662
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Bi.Tonia Kandiero kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8474
  Waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiendelea kupata viburudisho katika mnuso wa kukata na shoka wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8476
  Usia Nkhoma Ledama na Naibu Mkurugenzi Mkazi-Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina wakifurahi kwenye mnuso huo.
  IMG_8652
  Musa Haji wa YUNA na Phillip Musiba wa UNIC Dar es Salaam kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8490
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) akipozi kwa picha na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo.
  IMG_8636
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi.
  IMG_8469
  Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo na kuendelea kuburudika kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8648
  IMG_8452
  Wageni waalikwa wakiendelea kubadilishana mawazo.
  IMG_8732
  Hoyce Temu (wa pili kulia) na Usia Nkhoma Ledama (kushoto) wakipata picha ya ukumbusho na wadau wa MISA-TAN pamoja na UTPC.
  IMG_8742
  Dada Petra Karamagi na Zoe Glorious wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania wakipata picha ya ukumbusho.
  IMG_8761
  Pichani juu na chini Vijana wa YUNA katika picha ya kumbukumbu.
  IMG_8782
  IMG_8670
  Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa East Africa Radio Nasser Kingu (kulia) na Isaac Lukando (katikati).
  IMG_8787
  Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka kushoto ni Petra Karamagi, Laurean Kiiza na Beatrice Mkiramweni wakipata ukodak.
  IMG_8659
  IMG_8617
  Mshauri wa masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitralekha Massey, Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka pamoja na Mwandishi wa Habari mkongwe Mama Eda Sanga wakipozi kwa picha kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.
  IMG_8673
  Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulida Hassan (kulia). akipozi na familia ya Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia)
  IMG_8680
  Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakipozi na Familia ya Usia Nkhoma Ledama.
  IMG_8697
  Kutoka kushoto ni Mzee Mushi na Petra Karamagi (katikati) wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.
  IMG_8831
  Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.
  IMG_8844
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wnahabari.
  IMG_8700
  Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika picha.
  IMG_8711
  Kutoka kushoto ni Prosper Makene, Hoyce Temu, John Badi na Lauren Kiiza wakipata Ukodak.
  IMG_8050
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipokea wageni nyumbani kwake kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  IMG_8060
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (katikati) akimtambulisha mmoja wa wageni waalikwa kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kulia).
  IMG_8109
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini, Joyce Mends-Cole (kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kushoto) wakati wa zoezi la kupokea wageni waalikwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania. Katikati ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
  IMG_8121
  Wageni mbalimbali wakiendelea kuwasili na kupokelewa na wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8163
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim mara tu alipowasili kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
  IMG_8144
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kulia) akifurahi jambo na mmoja wa wageni waalikwa. Katikati ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
  IMG_8326
  Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy pamoja na Katibu wa Dkt. Mahadhi wakiwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8315
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
  IMG_8347
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania, nyuma yake ni wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
  IMG_8350
  Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakitazama moja ya 'Documetary' ya Malengo Endelevu ya dunia katika mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8387
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akitoa salamu za Serikali ya Tanzania kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nyuma yake ni baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo.
  IMG_8401
  Msaidizi wa Mh. Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Hoyce Temu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Waziri huyo.
  IMG_8353
  Sehemu ya wageni waalikwa, wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mabalozi, viongozi wa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo waliohudhuria mnuso huo.

  IMG_8492
  Burudani mbalimbali zikiendelea kusherehesha birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_8527
  IMG_8646
  Baadhi ya waandishi wa habari katika picha ya pamoja.

  0 0

   Ofisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu (wa tatu kushoto), akipata maelezo kuhusu bidhaa za kampuni mpya ya simu za mkononi ya Halotel katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania wamiliki wa Halotel,  Nguyen Thanh Quang na wageni wengine waalikwa.
   Ofisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu (kushoto), na Mkurugenzi  wa kampuni mpya ya simu za mkononi wa Halotel  Mkoa wa Kinondoni, Alex Thiem (kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo nchini jijini Dar es Salaam leo. Katikati Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania wamiliki wa Halotel,  Nguyen Thanh Quang .
   Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Viettel Tanzania wamiliki wa Halotel,  Nguyen Thanh Quang akizungumza katika hafla hiyo.

   Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu akizungumza akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo aliyetarajiwa kuwa mgebni rasmi.
   Ofisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Ananias Kamundu (kushoto), akiagana na  Mkurugenzi  wa kampuni mpya ya simu za mkononi wa Halotel  Mkoa wa Kinondoni, Alex Thiem mara baada ya kumalizika kwa shughulia za uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo. 
   Wasanii wa kikundi cha Mama Afrika wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

  0 0

  Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Elizabeth Buwimba, akichangia mada ya wajibu wa mwanamke kushiriki kwenye uchaguzi na umuhimu wakufanya hivyo wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati na baada ya uchaguzi, uliofanyika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.


   Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Edna Kamaleki, akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, kwa watendaji wa serikali za mitaa jimbo la Ukonga na watendaji wa Halmashauri ya wilaya na Jeshi la Polisi. 

   Baadhi ya Watendaji wa Tawla wakiandika baadhi ya maoni ya washiriki wa mdahalo huo.
   Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pugu jijini Dar es Salaam Jamila Jackson, akichangia hoja ya mjadala huo
   Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala, Victor Mukiza, akichangia mada ya amani wakati wa mdahalo ulioandaliwa na chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwa watendaji wa Serikali za Mitaa,Polisi na watumishi wa Halmashauri hiyo jana.


  .picha na Emmanuel Massaka


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akiwasili kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akihutubia wakazi wa mji wa Tunduma kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma ambapo aliwaelezea wananchi hao kuwa mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuibadilisha Tanzania,kubadili mfumo wa chama na atakuwa na Baraza la Mawaziri dogo, atapunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali lakini pia ataondoa kodi ndogo ndogo zinazowapa kero na kurahisisha njia za kufanya biashara kwa wananchi wa mipakani.
  wakazi wa mji wa Tunduma wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mku wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma ambapo aliwaelezea wananchi hao kuwa mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuibadilisha Tanzania,kubadili mfumo wa chama na atakuwa na Baraza la Mawaziri dogo, atapunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali lakini pia ataondoa kodi ndogo ndogo zinazowapa kero na kurahisisha njia za kufanya biashara kwa wananchi wa mipakani.

  Wakazi wa Mji wa Tunduma na vitongoji vyake wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwenye mkutano wa kampeni.

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akisisitiza jambo mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tunduma kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma.

older | 1 | .... | 663 | 664 | (Page 665) | 666 | 667 | .... | 1897 | newer