Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 658 | 659 | (Page 660) | 661 | 662 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mchoraji wa  vibonzo maarufu nchini Tanzania, Nathan Mpangala.

  MCHORAJI  wa vibonzo maarufu nchini Tanzania, Nathan Mpangala, ameandaa mazungumzo ya wazi yatakayofanyika katika Viwanja vya Nafasi Art Space, Mikocheni, Jijini Dar es Salaam, kesho (Ijumaa) ambapo atazungumzia maisha aliyopitia katika vyombo mbalimbali vya habari akiwa kama mchoraji vibonzo.

  Ili kunogesha tukio hilo, nao wahudhuriaji watapata nafasi ya kuuliza maswali au kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali atakayogusia.

  Mazungumzo hayo yana malengo makuu matatu;

  (i)             Kueleza maisha ailiyopitia kama mchora vibonzo.
  (ii)           Kukutana ana kwa ana na ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake wa vibonzo kwa ajili ya kufahamiana zaidi.
  (iii)          Darasa huru kwa wachora vibonzo wanaochipukia kusikia maisha aliyopitia ili kuwatia moyo wafike alipofikia au kupita.

  Mazungumzo hayo ambayo hayatakuwa na kiingilio yataanza saa 10 alasiri ambapo watu mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

  Wakati huohuo, Mpangala ametoa rai kwa wachoraji vibonzo wote hasa waishio Dar es Salaam, wakongwe na chipukizi kuhakikisha wanahudhuria tukio hilo kwani ni fursa nzuri ya kubadilisha mawazo na kusemea taaluma yao.

  Kwa maelezo zaidi 0713 262 902.

  0 0

   KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florence Turuka, akihutubia wanachama wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania (TAFFA), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa TAFA kwenye ukumbi wa Karimjee .
   Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin, akiwaeleza wanachama wa Chama cha mawakala wa forodha Tanzania TAFA, juu ya hufuma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa TAFFA jijini Dar es Salaam. PSPF na TAFFA wamefungua ukurasa mpya wa mahusiano ambapo wanachama kadhaa wa TAFA walijiunga na Mfuko huo
   Viongozi wakuu wa TAFFA, wakionyesha kadi za uanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSS), baada ya kukuunga wakati wa mkutan o mkuu wa mwaka wa TAFFA. Kulia ni Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselem, Meneja Masoko, Mawasilioano na Uenezi, Costantina Martin (wapili kushoto) na meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Mwanjaa sembe
  Baadhi ya wanachama wa TAFFA wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua kwa biashara anuai.
   Alisema Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.
  Kulia ni baadhi ya wasanii maharufu wa uigizaji wakishangilia wakati Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Mwisenge.


  Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Sirari wakifikisha ujumbe wao kwa Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipohutubia wananchi katika viwanja vya Tarafa Sirari.


  Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.

  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Rashid Bugomba alipowasili Sirari kwa mkutano wa kampeni kuinadi CCM eneo hilo..

  Wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wananchi Kata ya Sirari
  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwatambulisha baadhi ya wagombea ubunge wa Wilaya ya Tarime kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Sirari.

  Ni mwendo wa 'PUSH UP' baadhi ya wananchi wakipiga 'Push Up' kwenye mkutano wa mgombea mwenza Sirari kuonesha kuwa wapo 'fit'.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.
  Wananchi wakisikiliza hotuba ya baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Musoma.


  Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.


  Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.


  Aliyekuwa mbunge wa CCM, Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mwisenge.


  Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie na wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.

  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0


  Meneja biashara wa kitengo cha  Airtel Money,  Bwn Asupya Naligingwa
  (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Airtel
  kugawa gawio la faida la zaidi ya  shilingi billion 5 kwa wateja na
  mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima.  Pichani
  ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Bi Jane Matinde

  KAMPUNI ya simu za mkononi
  ya Airtel leo imetangaza kugawa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa wateja
  na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima

  Uamuzi huo wa kutoa gawio la faida lililopo katika akaunti  ya
  udhamini ya wateja wa Airtel Money (Trust account)  litawawezesha
  wateja wa Airtel kulipwa kiwango kizuri cha gawio la faida.  Kiwango
  hiki cha pesa kitalipwa kutokana na  kiasi cha pesa mteja alichokuwa
  nacho kwenye akaunti yake ya Airtel Money kila mwisho wa siku  kuanzia
  March 2014 hadi April 2015.

  Akiongea na waandishi wa habari,Meneja wa kitengo cha  Airtel Money,
  Asupya Nalingigwa, alisema wanayo furaha kutangaza mgawanyo  huu wa
  gawio la faida kwa wateja wao baada ya benki kuu ya Tanzania.
  Kuidhinisha kutoa  pesa hizi katika akaunti ya udhamini ya pesa za
  wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama trust  account.

  Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money watapata sehemu ya gawio
  lao  kulingana na salio wanalokuwa nalo kwenye akaunti zao kila siku

  "Tunaamini kiasi hiki cha pesa kitachangia kwa kiasi kikubwa katika
  kuboresha maisha ya watanzania wengi , kuwahamasisha wateja
  wasiofikiwa na huduma za kibenki kutumia mfumowa pesa kwa njia ya
  simu.Vilevile wateja wetu wa Airtel Money wataendelea kutumia huduma
  za pesa kupitia simu za mkononi, kufanya miamala yao ya kila siku na
  kutunza pesa zao ili kupata gawio lao kila watakapo weka pesa katika
  akaunti zao za Airtel Money". Aliongeza Nalingigwa

  Uamuzi huu wa kutoa gawio la faida kwa wateja ni wakuungwa mkono kwani
  unachochea na kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za
  mkononi , ukizingatia takribani asilimia 85% ya watanzania bado
  hawajafikia na huduma za kibenki

  Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kibunifu  za
  kifedha kupitia simu za mkononi ikwemo NFC huduma inayokuwezesha
  kufanya malipo kupitia kadi, Mikopo ya Timiza na huduma nyingine
  nyingi.

  Katika  maelezo yake Naligingwa aliahidi  Airtel kuendelea na dhamira
  yake ya kuzindua huduma bora na za kisasa katika mienzi ijayo ili  kuwanufaisha watanzania waishio maeneo ya mijini na vijijini.

  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during the International Conservation Caucus Foundation(ICCF) gala in New York's Harvard Club whereby he called upon advanced nations to curb the sale of illegally acquired wildlife products in their countries as a way of combating poaching and illegal wildlife trade in Africa.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks with Malawi's President Professor Peter Mutharika during the ICCF Gala held at Harvard Club in New York.
   The ICCF is an umbrella organization that works to advance conservation governance by building political support, providing on the ground solutions and applying  a natural resource  wealth management framework to sustainably develop and manage the earth's natural resources
  The Minister for Natural Resources and Tourism Hon.Lazaro Nyalandu Left and The Permanent Secretary in the Ministry Foreign Affairs and International Cooperation Ambassador Liberata Mulamula escorts President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete out of the Harvard Club in New York shortly after the President attended a gala organized by the ICCF group
  (photos by Freddy Maro)

  0 0

    Head of the German delegation Mr. Georg Rademacher and the EAC Deputy Secretary General in charge Finance and Administration, Mr. Liberat Mfumukeko signs the bilateral agreement.
  The EAC team(on the right side) led by Deputy Secretary General in charge Finance and Administration, Mr Mr. Liberat Mfumukeko and the The Federal Republic of Germany team during the negotiations.

  EAST African Community Headquarters, Arusha, 1 October, 2015The Federal Republic of Germany and the East African Community (EAC) have successfully concluded bilateral negotiations on development cooperation at the EAC Headquarters in Arusha,Tanzania. 

  The Federal Republic of Germany committed a total of 37 million euros in grants to the EAC for 2016-2018, highlightingthe strong commitment to support the integration process in East Africa.   

  ·         10 million euro in financial assistance will be invested in the establishment of a regional network of reference laboratories for communicable diseases. With this project, the German Government responds to a request for support from the EAC for the prevention and control of epidemic outbreaks in the region. 

  ·         Another 10 million euro in financial assistance will be used for Integrated Water Resource Management of Lake Victoria aiming at improving water provision and management of water resources.


  ·         17 million euros in technical assistance were committed to further support of the economic integration process, including a contribution to the EAC partnership fund. The programme is focussing on institutional strengthening of the EAC Secretariat and on supporting the implementation of the Customs Union, Common Market Protocols and Monetary Union. This includes the elimination of Non-Tariff Barriers such as tax harmonisation as well as Mutual Recognition Agreements for qualifications. At the same time Germany will support the EAC in promoting private investment especially in the pharmaceutical sector, including the establishment of a regional quality infrastructure for the pharmaceutical sector.

  Speaking during the negotiations, the  EAC Deputy Secretary General in charge of Finance and Administration, Mr. Liberat Mfumukeko, thanked the Government of the Federal Republic of Germany for its support to the EAC spanning the years since the re-establishment of the Cooperation between the three founding EAC Partner States to the present, when the Community has expanded to include the republics of Rwanda and Burundi.

  ‘’We have truly benefited from the German support which has catalyzed other development Partners to support our projects and programmes. In addition, Germany has given the EAC a permanent home by financing  the construction of the new Headquarters that today houses the Secretariat ,the Court and the Assembly under one roof thus greatly easing the EAC Organs interactions and communication’’, said Mr. Mfumukeko.


  He highlighted the successes achieved through German support in the realisation of the fully fledged Customs Union, the Common Market, and the commitments to support the realisation of the Monetary Union in the succeeding programme.

  The EAC Deputy Secretary General  noted that the development of the East African Monitoring System within the current support had resulted in a robust means of follow up of the implementation of Council and Summit directives. He further enumerated the priorities of the EAC- German cooperation for the next years.

  Mr. Georg Rademacher, Head of the German delegation, said: “Our support underlines the importance we give to the East African Community. The EAC is a role model and pace-setter in Africa and we are proud working closely with you in order to contribute to the well-being and prosperity of the citizens of this region”.

   He underlined that Germany is also supporting substantial regional infrastructure projects with promotional loans of the German development bank KfW.

  Only last week Ambassador Kochanke and Secretary General Sezibera signed a financial agreement to commit 30 million euros for live-saving vaccines in the EAC and the establishment of the EAC Regional Centre of Excellence for Health Supply Chain Management in Kigali.

  With a view to strengthen the pandemic preparedness in the EAC, Germany had announced its willingness to provide an additional 3 million euros in technical assistance for the region`s crisis response capacity (out of special funds for 2016).

  Since cooperation began in 1998 the total volume of German support to the EAC amounts to almost 213 million euro. Germany also has substantial bilateral cooperation with all five EAC member states.
  For further information, please contact:

  ·         Owora Richard Othieno, Head of Corporate Communications and Public Affairs; 


  ·         John Merikion, German Embassy, Communication Officer, Tel: +255 22 211709;  
  0 0

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  RAIS Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuendesha kikao cha 9 cha Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kesho jijini Dar es Salaam.

  Kikao hicho kitaangalia jinsi ya kutekeleza kwa haraka maazimio ya mkutano wa 8 wa baraza hilo hasa katika kuimarisha mazingira ya biashara na kujenga sekta bora zaidi ya utalii.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na TNBC, mkutano huo utahusisha mawaziri, makatibu wakuu, wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali.

  “Mkutano huu utaangalia njia na suluhisho madhubuti za kuimarisha mazingira ya biashara kama kurahisisha njia za udhibiti na kutumia intaneti kutoa huduma za kiserikali na biashara,” ilisomeka taarifa hiyo.

  Mkutano huo utazingatia mafunzo na uzoefu wa mikutano iliyopita.

  TNBC chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete ni chombo kinachotoa mwanya kwa sekta binafsi na umma kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora ya kufanya biashara na hivyo kuimarisha uchumi.

  TNBC pia inaendesha mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya nchini yanayosimamiwa na wakuu wa mikoa na wilaya husika.

  “Tangu kuanza kuongoza chombo hiki kama Mwenyekiti Desemba 2005, Rais Kikwete amefanikiwa kusaidia Baraza kufikia malengo yake kwa kiwango kikubwa,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

  Kwa mujibu wa taarifa, jambo hilo limeifanya TNBC kuwa uwanja maalum nchini wa kuibua mijadala ya kisera, tafiti na ushauri kwa sekta za umma na binafsi.

  Mkutano wa mwisho wa TNBC ulifanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
   TAARIFA KWA UMMA

   Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapenda kuwataarifu  Wananchi wote kwamba kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ni Siku ya Makazi Duniani  ambayo huadhimishwa Duniani kote.

  Nchini, mwaka huu tarehe 05/10/2015  –  Jumatatu, Maadhimisho ya siku hii yanategemewa kufanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa mbili na nusu asubuhi (2:30) mpaka saa nane mchana (8:00).


  Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni; 
  “Maeneo ya Umma kwa Wote”


  Mgeni rasmi katika Maadhimisho haya anatarajiwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe.William Lukuvi.


  “Wananchi wote mnakaribishwa”


  Imetolewa na Katibu Mkuu


  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  0 0

  MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Merck Sadick anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa mwaka  wa 46 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania utakaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 octoba mwaka huu katika eneo la kitonga, Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaaM.

  Hayo yamesemwa na Amir Mbashiri Mkuu Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Sheikh Tahir amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya Islam, kukuza udugu na urafiki miongoni mwa wanajumuiya na wananchi kwa ujumla na kuhamasisha amani katika jamii.

  Ameongeza kuwa kwa muda wa miaka mitano Jumuiya imekuwa ikiandaa mikutano ya amani katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuhamasisha jamii, dini mbalimbali na asasi za kijamii kuishi kwa amani licha ya kuwepo kwa tofauti za itikadi na mitazamo.

  Kwa uapande wake Katibu Mkuu waJumuiya hiyo Seif Hassan amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, amewaasa viongozi wote wa dini tofauti kutojihusisha na mambo ya kisiasa na kushukuru ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka serikalini katika kutekeleza shughuli na kutarajia kuwa serikali na wadau wengine kujitokeza kuendelea kuwaunga mkono katika shughuli zijazo.

  Aidha Jumuiya inatoa huduma ya elimu ya sekondari katika mkoa wa Dar es salaam na shule ya msingi katika mkoa wa morogorona kupitia asasi ya Humanity First Jumuiya imetoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni pamoja na mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammogram) katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

  Takribani washiriki 3500 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, na Msumbiji watahudhuria katika mkutano huo uliobeba kauli mbiu isemayo “mapenzi kwa wote, chuki si kwa yeyote”

  0 0
 • 10/01/15--03:28: BEI YA MADAFU HII LEO

 • 0 0

   Mkurugenzi Mtendaji TPDC, Dkt. James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa miundombinu gesi asilia, Miundombinu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika eneo la Madimba Mkoani Mtwara tarehe 10 Oktoba 2015.
   Sehemu ya Kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo eneo la Madimba Mkoani Mtwara, eneo ambalo uzinduzi rasmi unatarajia kufanyika tarehe 10 Oktoba 2015.
  Sehemu ya Kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo eneo la Madimba Mkoani Mtwara, eneo ambalo uzinduzi rasmi unatarajia kufanyika tarehe 10 Oktoba 2015.

  SERIKALI ya Tanzania, kupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ilianza kuutekeleza Mradi wa Bomba la gesi asilia Kutoka Madimba Mkoani Mtwara na Songosongo mkoani Lindi mwaka 2013. 

  Mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani bilioni 1.225 ambapo asiliamia 95% ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya (China) na asilimia 5% ni pesa za ndani. Hadi kufikia mwezi Agosti miundombinu ya mradi huo ilikuwa imekamilika.

  0 0

  Mkurugenzi na  mmiliki wa mitandao(BLOGU)  ya   www.matukiodaima.co.tz Bw  Francis Godwin  akimkabidhi mkuu  wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza stecker za kubandika katika magari na maeneo mbali mbali zinazohamasisha amani kuelekea  uchaguzi  mkuu utakaofanyika Octoba 25  mwaka  huu
  Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Ramadhan  Mungi akionyesha sticker za  kuhamasisha amani na  utulivu nchini kuelekea  uchaguzi  mkuu zinazotolewa na mtandao  wa www.matukiodaima.co.tz kwa mkoa wa Iringa na mikoa  mingine hapa  nchini
  Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Bi Masenza  akisoma ujumbe wa amani  uliopo katika  stecker  hizo  zilizotolewa na mtandao  wa matukiodaima ili  kusambazwa  katika wilaya  zote za mkoa  wa Iringa

  0 0

   Meneja wa Kampuni ya Business Connexion Tanzania Limited Ebenezer Massawe akitoa mafunzo juu ya kupata taarifa ya vyanzo vya mapato  kwa waandishi wahabari  wakati wa  semina iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari za kodi Tanzania  (TAWNET jijini Dar es Salaam. Kwa udhamini wa Vodacom Tanzania. 
   Afisa Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Hamisi Lupenja,akifafanua jambo  kwa waandishi wahabari (hawapo pichani ) wakati wa semina iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari za kodi Tanzania  (TAWNET ) jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo ilidhamini wa Vodacom Tanzania na  Business Connexion Tanzania Limited.Kulia ni Rose Mahendeka ,Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) 
   Afisa  kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka, akifafanua jambo    kwa waandishi wa habari wakati wa warsha iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari za kodi Tanzania  (TAWNET jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo ilidhamini wa Vodacom Tanzania.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kufungua rasmi maonesho ya Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Meneja waFast Jet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Wakala wa Shirika la Ndege la Qatar Airways, Dorah Chanafi, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko Amina Nassor.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa  IT wa Bodi ya Utalii, Rossan Mduma, kuhusu Tovuti ya Bodi hiyo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika Banda la India, alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), uliofanyika leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Saa, Mwakilishi wa Ang'ata Lodges, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Saa, Meneja waFast Jet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika Banda la Hifadhi za Taifa Tanzania, alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa ya kukuza Biashara ya Utalii yaliyopewa jina la Swahili (SITE), yaliyoanza leo Okt 01, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki na wadhamini wa maonesho. 
  Picha na OMR

  0 0

  X1
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Mkoa wa Mara wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo jana.
  (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
  X2
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho Stephen wakati walipokutana jana .IGP yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa huo kukagua utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
  X3
  Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho Stephen akizungumza katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
  X4
  Baadhi ya wadau wakichangia mawazo katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara kilichohudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
  …………………………………………………….
   
  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
  Wadau wa Amani mkoani Mara wamemhakikishia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kuendelea kuitunza amani  na kuimarisha  usalama katika mkoa huo hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
   
  Waliyasema hayo wakati walipokuwa wakitoa maoni yao wakati wa kikao kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa amani mkoani humo wakiwemo Wanasiasa, Viongozi wa Uchaguzi, Wagombea, Asasi za kiraia, Viongozi wa dini, Wazee wa kimila na Viongozi wa dini mkoani humo.
   
  Walisema mkoa huo umekuwa shwari hasa baada ya kuundwa kwa Kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime na rorya hivyo wananchi wote hawana budi kuendeleza juhudi za Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unaenda salama mkoani humo.
   
  Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ameahidi Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano wa kutosha na kusimamia vyema uchaguzi ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu bila kutishwa na wahalifu.
   
  Alisema Tume ya Uchaguzi imeweka utaratibu mzuri wa kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo hivyo hakuna haja ya wafuasi kukaa nje ya vituo vya kupigia kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kujenga mazingira ya kuleta vurugu.
   
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe,Zeletho Stephen alisema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari hivyo ni jukumu la kila mdau kuhakikisha anashiriki kwa nafasi yake kuimarisha usalama na amani hasa katika kipindi hiki.
   
  IGP Mangu yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi ambapo pia amekuwa akitumia fursa hiyo kukutana na wadau mbalimbali ili kushauriana jinsi ya kuimarisha amanai na usalama katika maeneo yao

  0 0

  Msanii vichekesho, Tausi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini humo.
   
  Msanii Kupa akiwa amembeba msanii wa vichekesho, Tausi huku Msanii Ndede akipunga mkono kuwasilimia wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini hapo kwa shuguli za Kampeni.
  Msanii Kajala akitoa ishara ya Gole Gumba kama alama ya CCM kwa wakazi wa mji wa Igunga alipoitwa jukwaani kuwasalimia wana Igunga.
  Msanii Ray Kigosi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Sehemu ya baadhi ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo.
  Msanii Aunt Ezekiel akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Msanii wa vichekesho, Mr Kupa akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Wasanii wa Bongo Muvi, kuanzia kushoto ni Stan Bakora, Aunt Ezekiel na Kajala wakifuatilia mkutano wa kampeni ulifanyika mjini Igunga.
  Msanii wa Bongo Muvi, Sajent akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Msanii Kitale akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Msanii Kitale akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Msanii Kajala akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Msanii vichekesho, Mboto akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  Msanii vichekesho, Mboto akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini
  Msanii Ndende akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
  hapo.
  Mboto akiwaaga wana Igunga mara baada ya mkutano kumalizika.
   
  Msanii Inspector Haarun akiwa ameongozana na Kasala wakiingia eneo la mkutano mjini Igunga.
  Picha zote na Sule Junior

  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akisoma wasifu wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais - Utumishi wakati wa Ibada ya kuuga mwili wake iliyofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu Septemba 28, 2015.
   Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma (kulia) ukiwa mbele ya wafiwa wakati wa Ibada ya kuuga iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro siku ya Jumanne Septemba 29, 2015.
   Baadhi ya waombolezaji wakishiriki ibada ya kuuaga Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro siku ya Jumanne Septemba 29, 2015.
   Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Ghalib Bilali (wa tano kutoka kulia) akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (wa nne kutoka kulia) wakishiriki ibada ya kuuaga Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro siku ya Jumanne Septemba 29, 2015.
  Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma siku ya Jumanne Septemba 29, 2015.

  0 0  0 0

   Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira akiongea na ujumbe wa wataalam wa kilimo kutoka nchini Poland ulioongozwa na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati wa mkutano uliohusu makubaliano yanalenga kuinua sekta ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa matrekta hapa nchini. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kayandabila.
   Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk (wa kwanza kulia) akiwa na zawadi aliyopokea kutoka kwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira hivi karibuni jijini Dar es salaam mara baada ya mkutano kati ya mkutano wan chi hizo mbili uliohusu makubaliano yanalenga kuinua sekta ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa matrekta hapa nchini.
  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa ujumbe wa wataalam wa kilimo kutoka nchini Poland ulioongozwa na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk hivi karibuni jijini Dar es salaam.

  0 0

  This is to announce  to  you  the  ‘Home  is  best’  Tanzania  global  diaspora  Week  UK 2015  and  the  Tanzania Diaspora  Achievement Awards to be held  from  the  3rd -6thDecember  2015 .
  We  are  showcasing  the  culture ,trade  and  investment  of  Tanzania .This  will give opportunities for Businesses to:
  •                Have access to several organisations to meet directly with various business people and foreign partners.
  •                Access to International buyers of Commodities & produce
  •                Access to Service Providers who are interested in doing business in Tanzania
  •                An opportunity for  Tanzania government and  private  sector   that  wants to  recruit  from  the  diaspora
  We  also announce  our   Tanzania  Diaspora community Leaders Gala  Dinner and  Awards  ceremony . The evening provides an opportunity for you to join us in celebrating the vital work of Tanzanians in the Diaspora   and friends of Tanzania as well as helping to deliver our mission to bring the UK and Tanzania closer together through our pioneering activities in business, policy and culture. 
  We present these annual awards to those individuals who exemplify the concept of the ‘Servant Leader’. These awards highlight the links between economic success, professional excellence accompanied by moral leadership, and service to society. By recognising individuals who embody the ‘Servant Leader’ ideal, we seek to encourage widespread recognition and adoption of these values among the global Great lakes community.

  For more information please contact
  TEL :0776888777/0715241177/00447556130219


older | 1 | .... | 658 | 659 | (Page 660) | 661 | 662 | .... | 1898 | newer