Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 659 | 660 | (Page 661) | 662 | 663 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba akiwasili Jimbo la Simanjiro na kupokelewa na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo Ndg.Ole Sendeka mapema hii leo.Mwigulu Nchemba akimnadi Ole sendeka kwa wananchi wake,Kubwa ni Ujasiri wa Ole sendeka kwenye kutetea maslahi ya taifa,Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo kama barabara zinazokwenda kujengwa kwa kiwango cha rami kuunganisha na mikoa inayopakana na SImanjiro.Ole Sendeka akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Engesbert kuhusu Ilani ya CCM na maendeleo ya Jimbo la SImanjiro.Kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Simanjiro linakwenda kujengwa barabara za Rami Zaidi ya Tatu za kutoka Arusha,Mererani na Dodoma na ile ya Babati kwenda Simanjiro.
  Mbali na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.Twende na Magufuli popote alipo.Wananchi wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka huu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya NHIF kigoma wakikabidhi msaada wa vyakula kwa uongozi wa kituo cha Silabu cha kulelea wazee wasiojiweza ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
   Meneja wa Mfuko wa bima NHIF  ya kigoma akisalimiana na wazee wanaotunzwa katika kambi ya Silabu kata ya kibirizi
  Baadhi ya wazee wasiojiweza wanaoishi na kutunzwa katika kambi ya kulea wazee ya Silabu kata ya Kibirizi Mkoani hapa.


   

  Na Editha Karlo.Kigoma
  MFUKO wa Bima ya afya (NHIF)wametoa msaada wa  vyakula kwa wazee wasiojiweza uliopo katika kituo cha silabu kata ya kibirizi mjini hapa.


  Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo wa chakula Meneja wa Mkoa wa mfuko huo Elius Odhiambo alisema kuwa mfuko unatumbua umuhimu na mchango wa wazee kwa jamii.


  "Sisi kama mfuko wa bima ya afya tuna thamini sana na kutambua mchango wenu wazee kwa jamii kwani kila mmoja wetu ni mzee mtarajiwa"alisema odhiambo


  Alisema wamekabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni moja na elfu sitini,vyakula walivyotoa ni mchele kilo 100,sukari kilo 100,unga wa ugali kilo 100,maharage kilo 100 na mafuta ya kupikia kilo 20


  Meneja huyo alisema wataendelea kusaidiana na kuwasaidia wazee hao kila inapobidi.


  Naye mkuu wa kituo hicho cha kutunzia wazee Juma Ndikamukana wasiojiweza aliushukuru mfuko wa bima ya afya kwa msaada wao huo na kuwakumbuka wazee katika siku yao leo.


  Alisema kituo hicho kina jumla ya wazee 51 wasiojiweza wanaotunzwa wanaotoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa 

  Kigoma


  0 0


  Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.

  Na Mwandishi wetu, Dodoma
  WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao. 

  Mbali na hilo, waajiri wa metakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao, kujiunga na mfuko wasio upenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza.Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.


  Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA, Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa.Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.

  0 0

  Meneja wa Wateja Binafsi wa First National Bank, Francois Botha na Meneja wa Usambazaji na Matawi wa benki hiyo wakizindua mpango maalum unaohamasisha Watanzania kujiwekea akiba na kujiwekea mustakabali salama kifedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam leo Oktoba 1, 2015.

  BENKI ya FNB Tanzania imetoa wito kwa Watanzania kujijengea mustakabali salama kifedha kwa kuendelea kuweka akiba zaidi benki kupitia fursa ya mpango mpya wa benki hiyo wa “Weka akiba na ushinde”.

  Wito huo umetolewa na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha wakati akizindua mpango huo jijini Dar es salaam ambapo alisistiza umuhimu wa kuweka akiba. Mpango huo wa Weka Akiba na Ushinde utaanza tarehe 1 Oktoba na kuendelea mpaka mwisho wa Disemba 2015.

  Ikiwa ni sehemu ya mpango huo utakaodumu kwa miezi mitatu, wateja waliopo na wateja wapya wataingizwa moja kwa kwenye droo kutokana na akiba ya kila shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao, kwahiyo watakaoweka akiba zaidi watapata nafasi ya kushinda shilingi milioni 5 ambazo zitatolewa kila mwezi kwa kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa watu wote kushiriki.

  Botha alisema, “Katika kuendeleza utamaduni wa benki hii kuwatunuku na kuwanufaisha wateja wake huku ikiendelea kutoa huduma za kisasa za kibenki, FNB inatoa fursa hii kwa wateja kuweza kujinufaisha kutokana na kuweka akiba huku wakijijengea mustakabali salama kifedha”.

  0 0

   Msikiti mpya wa Kitongoji cha Kimbangulile, Mkuranga Pwani
   Msikiti wa zamani wa Kitongoji cha Kimbangulile Wilaya ya Mkuranga mkoni Pwani.
  Tunamshukuru Mungu kwa wale wote walio tuunga mkono katika harakati hizi Mungu awabariki.

  Zaidi pia Mungu awabariki waendeshaji wa blog hii ya Jamii kwa kutuunga mkono katika kupeleka habari kwa Jamii na kutuunga mkono katika harakati zetu.

  Ndugu zangu Wapendwa Michango tuliyo kusanya toka mwanzo Program PROJECT zetu za kheri hizi ni Tshs 6,000,000 ( Milioni Sita ) .

  Pesa hizi zimetumika katika kuwezesha kufanya Mambo Mawili katika sehemu tofauti , Sehemu ya Kwanza ni Mkoa wa Pwani , Wilaya ya mkuranga , Kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha Kimbangulile hapa tumewezesha kuubadilisha ki ujenzi Msikiti kutoka katika hali ya Nyasi kuwa hali ya bati kama mnavyo ona katika Picha.   Hii ilikuwa ni Project yetu namba Moja .

  Matumizi ya hapo tuliweza nunua Tofali 1500 katika Tofali 2000 zilizo tumika kujenga Jengo jipya.

  Pesa yote iliyo baki tuli amishia Project namba mbili ambayo ipo mbezi Salasala ambapo tulinunua pesa zote tofali na wakatokea Wahisani wengine walituongezea Tofali ambazo idadi yake zilifikia 10,000/= pamoja na Mifuko 100 ya Cement .

  Kwa Mchango huo tuliweza kufanya yafutayo:-

  1.Tumejenga Msikiti ambao mnao uona katika Picha .

  2.Madarasa Matatu .

  3.fremu 3 . 

  Na tofali zimebaki kwa ajili ya kujenga uzio.

  Mdau katika kheri kwa Michango yenu ndio tumeweza kufika hapa .

  Mungu awabariki zaidi na zaidi ili mpate kulikamilisha hili na mengine ya kheri .

   Project ya pili
  Katika Project Site namba mbili tumechimbiwa kisima na Mfadhili , kisima kina Mita 120 ametutaka katika Mita hizo tutoe Tshs Milioni Nne ambapo mpaka sasa nina Tshs 125,000/=

  Tunawakaribisha wale wote ambao wapo tayari kuchangia kwa lolote katika harakati hizi za kheri.

  Mahitajio 

  1.bati 
  2.mbao
  3.Nondo
  4.Kifusi 
  5.Madirisha na Milango 
  6.Na vifaa vyote ambavyo vinaweza kutusaidia katika Mambo ya Ujenzi .

  Nawashuru saana na saana kwa kutoa muda wako na kusoma maelezo haya , furaha yetu zaidi itakuwa pale utakapo kuwa na muda na utayari wa kututembelea site ilitupate muongozo zaidi kutoka kwako.

  NAMBA ZA MAWASILIANO YA KUTUMA MCHANGO.

  TIGO - PESA 

  +255715800772 
  +255673800772 

  AIRTEL - MONEY

  +255689604780 

  Kwa wale walio nje wanaweza tuma kupitia 

  WESTERN UNION :

  Receiver Name :- GHALIB NASSOR MONERO.

  Tafadhali naomba nijulishe mara tu utakapo tuma Mchango wako au kabla kwa Namba hizo za Simu.

  Au face book : Kijana wa Kiislam Dsm .

  0 0

  Mhe.  Mahadhi J. Maalim  Naibu Waziri, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akizungumza wakati wa Mkutano wa Nchi zilizonyuma kimaendeleo ( LDCs) wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Kundi hilo uliofanyia siku ya Alhamis hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Nyuma ya  Naibu Waziri, ni  Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa  Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan  M. Mwinyu 

  Na Mwandishi Maalum, New York
   WAKATI  kila  Nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa,  ikijianda kwa utekelezaji wa Ajenda 2030 ambayo  inajikita zaidi katika kuondoa umaskini pasipo kumwacha yeyote nyuma, sanjari na kuilinda Sayari Dunia. Tanzania imehimiza  haja na umuhimu  wa nchi ambazo  ziko  nyuma kimaendeleo ( LDCs) kuzungumza kwa kauli moja.


  Ushauri huo umetolewa  jana Alhamis na   Mhe. Mahadhi Juma Maalim ( Mb),  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa LDCs uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, sambamba na majadiliano ya  jumla ya  Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


  Katika mkutano huu wa  Mawaziri wa LDCs, Bangladesh  ilikabidhiwa uenyekiti wa  Kundi hilo kutoka kwa Benin inayomaliza muda wake. Pamoja  na Kuishukuru Benin kwa kuliongoza kundi hilo vema wakati wa  uenyekiti wake Mhe. Naibu Waziri ameiahidi Bangladesh ushirikiano  kutoka Tanzania.

  “ Kundi letu linawachama wengi, tutumie basi wingi wetu  kuhakikisha  kwamba tunasukuma mbele na kuteteta masuala  yanayotuhusu kwa  kuzungumza kwa sauti  moja wakati wa majadiliano na kuhakikisha kuwa ajenda tunazosimamia  kwa maslahi yetu  hazikwami.” Amesema Naibu Waziri

  Aidha Naibu Waziri Mahadhi, amelikumbusha kundi hilo kuwa moja  ya lengo kuu la kundi ni kuondoka katika kundi la nchi maskini na kuwa nchi zenye uchumi  wa kati.


  “ Kwa bahati nzuri  suala la kuondoa umaskini ni moja ya eneo ambalo limepewa umuhimu wa kipekee katika Ajenda 2030, hivyo ni wajibu wetu  kama LDCs, kutumia fursa hii kwa kuhakikisha kwamba, katika kipindi cha miaka 15 ijayo nchi nyingi katika kundi letu  zina-graduate na  kuwa nchi zenye uchumi wa kati”. Amesisitiza.


  Mhe. Naibu Waziri amerejea  kwa kusisitiza kauli  iliyotolewa na  Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipolihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa, siku ya  Jumanne, Kwamba utekelezaji wa Ajenda 2030 ndiyo changamoto iliyombele yetu kwa sasa na kwamba utekelezaji wake ukikwama, LDCs ndizo zitakazo athirika zaidi.


  Ni kwa sababu hiyo juhudi za pamoja katika kuhakikisha utekelezaji wa  Ajenda  2030 ni mihimu na  za lazima.


  Kundi la   Nchi ambazo zipo nyuma kimaendeleo na kama zinavyotambuliwa na Umoja wa Mataifa zipo 48

  Ajenda 2030 ambayo ilipitishwa wakati wa mkutano wa kilele wa kisiasa uliofanyia kwa siku tatu hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  ni   Ajenda yenye malengo 17 ya maendeleo endelevu  yakichukua na nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo yanafikia  ukingoni  mwaka huu wa 2015


  Ajenda 2030 itaanza kutekelezwa mwakani ( 2016 )na utekelezaji wake ni wa miaka 15

  0 0


  0 0

  1.     Viko Mbweni  usalama  wa  taifa, vina  hati miliki, viko  karibu na  barabara  ya  lami na viko  karibu  na  beach,  vipo  Sqm  600 – 1500, bei  ni  kuanzia  milioni 35 mpaka  45.

  2.     Nyumba 3 zinauzwa, zipo Mwananyamala “A”, moja vyumba 12, nyingine vyumba  6 na  nyingine vyumba 4. Zote  zina  leseni  ya  makazi, gari  mpaka mlangoni, umeme  upo. Kila  moja  bei  milioni 65.


  3.     Nyumba yenye geti  la  gari, vyumba 4, kimoja master, umeme, sebule, dining, jiko, stoo, na  hati miliki inauzwa. Ipo Mbagala  Kuu, bei  milioni  65.


  4.     Pia  nyumba  za  milioni 65 – 70  zipo  Mbweni  na  boko.

  Mawasiliano  0784482959.

  0 0

    
  STATE HOUSE ZANZIBAR

  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

  PRESS RELEASE

  Zanzibar                                                                   2.10.2015
  MGOMBEA nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa atakapoingia madarakani katika awamu yake ya pili ya uongozi sekta ya michezo atazidi kuiimarisha.


  Dk. Shein ambaye pia, ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyasema hayo katika Mkutano wa CCM wa Kampeni za uchaguzi huko Kiwani, Mkoa wa Kusini Pemba uliohudhuriwa na maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi yakiwemo makundi ya vijana.


  Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa atahakikisha sekta ya michezo inaimarika zaidi katika kila nyanja ili Zanzibar irudi katika asili yake ambapo Zanzibar ilitambulikana ndani na nje ya bara la Afrika katika sekta hiyo.


  Dk. Shein alisema kuwa tayari kwa upande wa Serikali Idara maalum imeshaundwa kwa ajili ya kushughulikia michezo ikiwa na lengo la kuiimarisha sekta hiyo hapa nchini.


  Aidha, Dk. Shein alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha vuguvugu la michezo linaimarika sambamba na kuwapa kipaumbele wanafunzi ili nao wawe na muda wa kushiriki michezo.


  Dk. Shein alisisitiza kuwa michezo kwa vijana na watoto wa skuli ina umuhimu mkubwa katika kuwajenga kiafya, kiakili pamoja na kuwajenga watoto na vijana kujenga ushirikiano, upendo na umoja miongoni mwao.


  Kutokana na umuhimu huo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kwa kuwataka wazee kutowazuia watoto wao kushiriki michezo kutokana na umuhimu wake mkubwa katika maisha ya mwanaadamu.


  Sambamba na hayo, Dk. Shein alisema kuwa sekta ya  michezo katika kipindi cha miaka mitano ijayo itaimarishwa kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka (2015-2020) ambapo Serikali itatekeleza mambo kadhaa kwa lengo la kuiimarisha sekta hiyo.


  Katika uongozi wa Dk. Shein Serikali imetekeleza mambo mbali mbali katika kuimarisha sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na kuandaliwa kwa Sera mpya ya michezo ya Zanzibar itakayoimarisha na kuiendeleza michezo yote.


  Aidha, Serikali imeanzisha mashindano ya riadha ya Wilaya, kwa Wilaya zote kumi za Zanzibar pamoja na kutoa vifaa mbali mbali vya michezo kwa wanariadha wa Zanzibar ili kurejesha vuguvugu la michezo ya riadha ambapo bado utaratibu wa kutoa vifaa hivyo unaendelea.


  Pamoja na hayo, Serikali imewahamasisha wananchi waendeleze michezo ili wajenge afya zao kwa kufanya mazoezi ya viungo kila siku sambamba na kushiriki kwenye tamasha la mazoezi ya viungo linalofanyika tarehe 1 Januari ya kila mwaka.


  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

   E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

  0 0
 • 10/02/15--01:06: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Mwenyekiti wa Rotary Dar Marathon na mtoa maada, Sharmilla Bhatt  katika mkutano unaofanyika kila Alhamisi ya kila mwezi unaoandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jijini Dar es Salaam jana.

  JAMII ya watanzania wanatakiwa kutokutegemea misaada kutoka nje ya nchi  isipo kuwa tunatakiwa kujitolea  ili kusaidia jamii isiyojiweza  kwa jia ya harambee.

  Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Rotary Dar Marathon na mtoa maada, Sharmilla Bhatt katika mkutano unaofanyika kila Alhamisi ya kila mwezi unaoandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jijini Dar es Salaam jana.

  alisema kuwa jamii  na makampuni binafsi yatambue kua katika jamii huu hii tunayoiishi kuwa kuna watu ambao hawajiwezi katika mahitaji yao ya kila siku na hivyo makampuni yanaweza kuandaa harambee kutok vyanzo vya ndani kwaajili ya kuisaidia jamii inayo hitaji bila kutegemea misaada kutoka nje ya nchi.

  aidha alisema kuwa Oktoba 14 ambapo ni siku ya kumbukumbumbu ya Mwalimu Julius Kamabarae  Nyerere  kutakua na matembezi ambayo yatakua na uchangiaji wa jamii.
  Baadhi ya wadau waliohudhulia mkutano uliondaliwa na kampuni ya Solution Blocks wakimsikiliza mtoa maada katika hoteli ya Colesium jijini Dar es Salaam jana.
   Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Mshiriki wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana akiuliza swali kwa mtoa maada. 

  Mwanzilishi wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akiwakaribisha baadhi ya wadau mbalimbali katika mkutano wa kila Alhamisi ya kila mwezi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. 


   Wadau wakisikiliza kwa makini maada iliyokua ikijadiliwa.
    Meneja wa masoko wa Hoteli ya Colloseum akiwakaribisha wadau katika mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jana jijini Dar es Salaam.


   

  0 0

  ccvv
  Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules iliyoanguka.ccvvb
  Ramani inayoonesha eneo ambapo ndege hiyo ilipata ajali.ccvvf
  Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules imeanguka usiku wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Jalalabad nchini Afghanistan na kuua watu 12.
  Kanali wa jeshi la Marekani Brian Tribus ameiambia AFP kwamba watao kati ya waliokufa walikuwa wanajeshi wa Marekani, watano walikuwa raia wa kawaida na wawili walikuwa ni Waafghan.

  Msemaji wa kundi la wapiganaji la Taliban, Zabihullah Mujahid alisema kupitia Twitter kwamba kundi hilo lilitungua ndege hiyo, lakini mashirika ya habari yanasema hakuna ishara inayoonesha ndege hiyo kama ilishambuliwa.

  Jeshi la Marekani limesema linachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
  Ajali hiyo ya ndege imetokea huku ndege za kijeshi za Marekani zikisaidiana na wanajeshi wa Afghanistan kujaribu kukomboa mji wa Kunduz uliotekwa na wapiganaji wa Taliban.

  Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani wamo Afghanistan baada ya mpango wa kuondoa majeshi hayo asteaste kubadilishwa mapema mwaka huu.

  Rais Obama alikuwa ameahidi kuacha wanajeshi wachache sana wa Marekani nchini humo ambao wangekuwa wa kulinda ubalozi wa Marekani kufikia mwisho wa mwaka 2016.

  0 0

  nmb (1)nmb (2)
  Mkurugenzi wa NMB - Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
  nmb (3)
  Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
  nmb (4)
  Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania jana kwenye makao makuu ya NMB.
  nmb (5)
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakiangalia filamu fupi kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki ya NMB tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo yake jijini Dar es Salaam jana.
  nmb (6)
  Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akisalimiana na Mhariri na Mmiliki wa ABM FM ya Dodoma – Abdallah Majura kwenye mkutano kati ya NMB na Jukwaa la Wahariri.
  nmb (7)Mratibu wa Jukwaa la Wahariri – Prisca Kabendera akielezea kuhusu Jukwaa la wahariri na shughuli inazofanya.

  Benki ya NMB jana ilianza maadhimisho ya miaka 10 tangu kubinafsishwa huku ikiweka bayana mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwemo kuongeza matawi kutoka chini ya 100 miaka 10 iliyopita mpaka matawi 173 leo hii, kutoka kutokuwa na ATM mpaka ATM zaidi ya 600 na wateja kufikia zaidi ya milioni 2 kutoka laki 6 miaka 10 iliyopita.

  NMB pia imefanikiwa kuwa na matawi katika kila wilaya nchini. Hii inaonesha ni jinsi gani Benki imekuwa kwa kasi na kuwa benki namba moja kwa ukubwa na faida kuliko benki nyingine yoyote nchini Tanzania.

  Kwa miaka 10 pia NMB imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 7 kusaidia shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia madawati mashuleni, vifaa vya hospitali katika hospitali mbalimbali za serikali huku ikichangia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika sekta ya afya na elimu.

  NMB Pia imechangia zaidi ya Bilioni 365 ndani ya miaka 5 tu fedha ambayo imechangia sana kwenye bajeti ya serikali na hivyo kutumika kwa maendeleo ya watanzania. Huo ni mchango mkubwa kuliko benki yoyote nchini. 

  0 0

   Mwanasheria wa tume ya uchaguzi Bw.Mtibora Seleman akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
   Wanasemina wakifatilia kwa karibu mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
   Wanasemina ya masuala ya Uchaguzi kanda ya ziwa wakiwa darasani.
   Bi. Jescar Mongi kutoka tume ya uchaguzi hapa akionesha mfano wa utaratibu wa upigaji kura utakavyokuwa.

  UCHAGUZI MKUU MAANDALIZI KANDA YA ZIWA YAENDELEA VIZURI
  Na Atley Kuni- The Power of Media grew.
  Wasimamizi waaswa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu
  Imefahamika kwamba maandalizi muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku, waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba 25 mwaka huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi kumalizika.
  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na kuhusisha Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi, na maafisa uchaguzi kutoka katika mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Manju Msambya, amesema watumishi hao wanayo dhima ya kuhakikisha zoezi la uchaguzi linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.
  Msambya amesema nilazima dhamana waliopewa watumishi hao watambue  ni muhimu kwakua inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako taka kuelekea kwa kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais. “Ndugu wanasemina tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge uwezo katika mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha pamoja na kutangaza matokeo ya uchaguzi” hivyo suala la umakini ni muhimu sana.
  Msambya amesema, kwakutumia uzoefu walionao watumishi hao katika mazoezi mbali mbali ya kitaifa wataweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki katika zoezi kama hilo kwa mwaka 2010.
  Awali akimkaribisha kufungua semina hiyo Mratibu wa uchaguzi wa kanda ya ziwa Deogratius Nsanzugwanko alisema tayari maandalizi kadhaa kuhusiana na uchaguzi yamekwisha kamilika ikiwapo madaftari ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa tayari vimekwisha anza kusafirishwa kwenda kwenye mikoa husika.
  Kanda ya ziwa inayoundwa na mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mara, ambapo kwa mkoa wa Mwanza pekee inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,442,391 sawa na asilimia 103% ya lengo lililokuwa limewekwa hapo awali na bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya kuandikisha wapiga kura 1,403,763.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Awadh Mawenya, ambaye ni mgeni rasmi katika kongamano la saba la elimu ya juu linalofanyika jijini Arusha akiongea machache mara baada ya kumaliza kutoa mada. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
  Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.
  Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya  akiwashukuru washiriki kufika katika kongamano la saba la elimu ya juu linalofanyika jijini Arusha. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
    Prof. Ephata E. Kaaya, mwenyekiti wa Makamu wakuu wa Vyuo vikuu Tanzania akiongea machache. 
  Meza kuu.
  Prof. Sylvia Temu, Mkurugenzi - Idara ya Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiongea na vyombo vya habari juu ya mikakati na mipango ya kongamano la saba la elimu ya juu lililoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
  Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.
  Washiriki wakiwa katika picha za pamoja.

  0 0

    Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma akitoa heshima zake za mwisho kwa askari wa JKT wa kikosi cha 821 Bulombora Kigoma waliofariki jana kwa ajali ya gati.

  Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma wakitoa heshima zao za mwisho kwa askari  wa kikosi cha 821 JKT bulombora waliopata ajali ya gari jana na kufariki dunia.

  Askari kutoka vikosi na majeshi mbalimbali wakiwa mbele ya majeneza ya askari wenzao wa kikosi cha 821 JKT Bulombora waliofariki jana kwa ajali kwaajili ya kutoa heshima za mwisho.
   Askari wa majeshi yote wakishirikuana kuweka miili ya wenzao katika eneo la kutilea heshima za mwisho waliofariki jana kwa ajali ya gari.


  Na Editha Karlo,wa Blog ya jamii
  MIILI saba ya vijana wa  jeshi la kujenga Taifa(JKT)  kikosi cha 821 Bulombora waliofariki dunia  jana kwa ajali ya gari wameagwa leo na kusafirishwa makwao kwaajili ya mazishi.

  Akiongea na waombolezaji waliofika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa kigoma(Maweni)kwaajili ya kuaga miili ya marehemu Mkuu wa vikosi vya Kigoma, Kanali Msuya alisema jeshi limepoteza nguvu kazi ya Taifa .

  Alisema mpaka sasa taratibu zote za kusafirisha miili hiyo zimeshakamilika miili yote itaondoka kwa usafiri wa magari hadi mwanza na kesho watasafirishwa na ndege ya jeshi kwenda dar es salaam kwaajili ya kupelekwa kwenye mikoa yao kwa maziko.

  Kanali msuya aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MT 54407 SGT Ally Kambangwa mkazi wa mtwara,MT 108151 PTE Abeli Maisha mkazi morogoro,SM Eugini Bitati mkazi wa kibondo.

  Wengine ni AH 7190 SM Saidi Sadara mkazi wa Shinyanga,RES Bakari Kibaya mkazi wa Tanga,RES Fredrick Kahemela mkazi wa arusha.

  Msuya aliwataja majeruhi pia majina yao kuwa ni Benadicto Ndokeye,Raphael Yohana,Athanas Emanuel,Abuu Nzoge,Abubakari peter,Abubakari Msubi na Denis Manyanya.

  Wengine ni Edward Nyanda,Elias Magessa,Gofrey Maliki,King Kasefu,Kamilius Agida,Stive Denis,Saidi Omary,Saidi Zuberi,Shabaani Zakari,victor John,Jackson Nyarubu na Mohamed Nyimbo

  Naye katibu tawala wa Mkoa wa kigoma eng.John Ndunguru alisema kuwa serekali ya mkoa imepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya askari hao saba na watashirukuana na wafiwa bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu

  "Serekali ya mkoa ina masikitiko makubwa kwa kupokea habari hizi za kuondokewa na askari wetu tutashikiriana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu"alisema Ndunguru.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
    Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Bw.  Frank Kanyusi akitoa maelezo kuhusu wavuti mpya ya wakala huo ambayo kuanzia sasa mteja atakuwa anajisajili yeye mwenyewe kupitia huduma hiyo ya mtandaoni
    Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
     Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi wavuti mpya ya BRELA  ambayo kuanzia sasa mteja atakuwa anajisajili yeye mwenyewe kupitia huduma hiyo ya mtandaoni.
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti  mweza wa baraza hilo wakifurahia baada ya kuzindua rasmi wavuti mpya ya BRELA  ambayo kuanzia sasa mteja atakuwa anajisajili yeye mwenyewe kupitia huduma hiyo ya mtandaoni
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akieleza kwa wanahabari juu ya mafanikio ya kikao cha tisa TNBC  hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 201
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wadau wakuu wa biashara wakati wa  kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete watendaji wakuu wakai wa kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wadau wa biashara wakipata picha wakati wa kikao  cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF)   wakati wa kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na wana TNBC  katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.

  Na Mwandishi wetu, Dodoma
  WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao. 

  Mbali na hilo, waajiri wa metakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao, kujiunga na mfuko wasio upenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza. 

  Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.

  Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA, Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa. 

  Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.

  0 0
 • 10/02/15--07:41: SHAIRI KUTOKA KWA MDAU
 • WAZALENDO – 2015

  1)    AWAMU YA TANO NDO HII, VIONGOZI KAMPENINI
  TWAMUHITAJI SAHIHI, WALA SIO WA UTANI
  HAPA HAKUNA KUWAHI, SAFARI HII TUKO MAKINI
  BIBLIA QUR’AN, VIAPIE UKO MAKINI.

  2)    SAFARI HII TUMECHOKA TWAWATOLEENI UVIVU
  SISI TUNAWAAMINI, NDO MAANA TWAWAPA SHAVU
  KURA TUKIWAPIGIA, ILI MUWE WASIKIVU
  KISHA MNATUGEUKA, KUTUONA WAPUNGAVU.

  3)    USO KWA USO TU LIVE NA IMANI ZENU POTOVU
  KWA NINI MWANG’ANG’ANIA, MPAKA MUWE VIONGOZI
  HAPO HAPO KUNA SIRI, NDO MAANA MWAOTA SHAVU
  SISI TUNADHOOFIKA, NYIE MWAZIDI KUNONA.

  4)    IMEKUWA SIKU NYINGI, WAZALENDO TWATESEKA
  WALO FAIDI KWACHACHE WENGI TUMESAHAULIKA
  RUSHWA KOTE IMETAWALA, MASIKINI HANA HAKI
  NJOO UTOE UCHAFU, TANZANIA IACHE NUKA.

  5)    NYIE WATU MMEROGWA, MWAHITAJI KUOMBEWA
  DUNIANI KUWA BINGWA, MKASAHAU AKHERA
  HAMUOGOPI ULINZWA, NCHI MLIONGOZAJE
  TAMAA MWAWEKA MBELE, UMAUTI WENU NYUMA.

  6)    SASA UMEKUWA MCHEZO, UONGOZI KUGOMBEA
  PESA MNATUMWAGIA, KISHA MNATUNYAKUA
  MIDOMO MMETUGUNGA, HATUWEZI FURUKUTA
  MWALIMU ALITUONYA, MKWEPWE KAMA UKOMA.

  7)    MWAMWAGA PESA HADHARANI, BILA HATA YA KIFICHO
  HAYA ZIMWEKURUKENI, KANA KWAMBA HATUNA MACHO
  HII SASA SI SAISA, NI YA MWENYE KUWA NACHO
  KWA MIPANGO YA MANANI, ATAPITA ALOMPANGA.
   
  8)    HATUHITAJI MAPESA KILIO CHETU USAWA
  ATACHO PEWA MENEJA NA MKULIMA IWE SAWA
  SIO MWENYE KUTUUMA-NA KUPULIZA KAMA PANYA
  KUTUACHA NA BUTWAA – JINSI ATAKANYOTUNYONYA.

  9)    TWAWAONYA WAZALENDO, WENYE AKILI TIMAMU
  TUACHENI KUPUMBAZWA – NA WAUCHU WA UONGOZI
  ANATUPIA TUKANGAA – NA AHADI ZA UONGO
  MGOMBEA WA KUHONGA – AKIFIKA IKULU NI SUMU.

  10)                       TUMKUNJENI SAMIKI, BADO ANGALI MBICHI
  WALE WEZI WA ZAMANI, SISI HATUWA SADIKI
  FISADI HUWA HASIKII, NA WIZI WAKE AACHI
  MWIZI SISI HATUMTAKI, WACHA TUMEACHE BENCHI.


  11)                       JAMANI SISI TUMECHOKA, MWENYEZI MUNGU SHAHIDI
  KIONGOZI TUNAETAKA JULETUTAE FAIDI
  WATUFANYA BURICHEKA, KWAMUOGOPI WADUDI
  WAJIONA WAMEFIKA, HWA MOLA HAWATORUDI.

  12)                       KWA MANANI TUMEOMBA TUNASUBIRI NUSURA
  YEYE PEKEE NDO MUUMBA AATAELETA NUSURA
  NA HAWA NDO KAWAUMBA INGAWA SI WATUKERA
  TUNAKUOMBA RABUKA, TUKINGE NA SHARI ZAO.

  12A) MZALENDO SI MGENI NJOO MWENYEJI AHAME
  WAMEBAKIRI KAULI, NJOO MWENYEJI AHAME
  KUMUHIMISHA MWENYEJI, UKAMFADHIRI MGENI
  JAMANI HII NI DHURUMA, ISO KUWA NA MFANO.

  13)                       SIO WOTE NI WACHAFU WAPO WENGINE WASAFI
  WAO NI WAADILIFU, HAWA SIO MABEPARI
  HAWANA HATA KASIKENDO WANA SIKIKA KWA WEMA
  KURA ZETU TUWAPE LEO, KESHO NASI TUFURAHI.

  14)                       TWAHITAJI MWANDIRIFU, MWENYE MOYO WA IMANI
  ATAE ONDOSHA MACHAFU, NA KUENDELEZA MEMA
  KWA MOLA AWE NA HOFU, AJUWE WAJIU WAKE
  MWENYE ROHO SIO CHAFU, NA KUWAJALI WENZAKE.

  15)                       TWAHITAJI MWANADAMU, HAIJARISHI CHAMA GANI
  AMBAE HANA HASIRA, KUTUTIA UTATANI
  WALA SI KING’ANG’ANIZI, ASO KUBARI KUSHINDWA
  ASIYE TAKA MAKUU, AJIWEKA KAWAIDA.

  16)                       HAIJARISHI DINI GANI, ILI MRADI ANA IMANI
  IKIWA NI MCHA MUNGU, SISI TUTAPATA AMANI
  SI MBAGUZI WA DINI, KABILA AU HALI GANI
  ATAEJALI-MAENDELEO YA WANACHI NCHINI.

  17)                       TUNASISITIZA UUTU- KWA HUYU MPYA KIONGOZI
  ATAMBUE NASI WATU, ASUTIE SIMANZI
  AJUE HAPA NI KWETU, SI TU KWA AKINA FULANI
  WAZALENDO TU NYUMBANI, HAPA SIO UGENINI.

  18)                       KUMBUKA ALOKUPA CHEO, NI MWENYEWE MTUKUKA
  TUFANYIE UWADIRIFU, ASIJE KUKASIRIKA
  USIJE KUWA KINYONGA,  NA KUGEUKA KUWA NYOKA
  KAMWE HATUTOKUWEZA SHAHIDI ATAKUBUKIKA.


  19)                       TWASHITAKI KWA MUUMBA, RAIS WETU SHAHIDI
  VITUKO VYA MAFISADI, TANZANIA VIMEZIDI
  WAMEGEIZA SIASA, KITENGO CHA UFISADI
  UKIINGIA IKULU – WEKA MAGUFURI WASIRUDI.

  19A) HII DEMOKRASIA – SI NCHI YA KISURUTANI
  AWAMU HII YA TANO SIO YA KURISHANA
  TUSHAMUONA MSAFI SISI TOKEA ZAMANI
  YEYE  NDO CHAGUO LETU WALA HANA MPINZANI.

  19B) MWENYE AKILI AFIKIRIE TUSICHEZEE BAHATI
  ALOTUPAPELI AWAKI-ATUTOBOA JICHO KWA KIJITI
  MWIZI HATA ASUGULIWE KWA JIKI WALA HATAKATI
  NAMCHAGUA MSAFI, FISADI KULA YANGU HAPATI.

  20)                       ONA HAWA MAFISADI KUTUFANYA PUNGUWANI
  TANGU LINI MTU UIBE NA UFUKUZWE KAZINI
  WEWE WEWE TENA URUDI, ETI USHIKE USUKANI
  HIKI JAMANI NI KIOJA CHA KARNE DUNIYANI.
  21)                       MAFISADI MIAKA YOTE HULA WAO PEKE YAO
  SAFARI HII WATUZUGA ETI NASI TULE NAO
  HII NI DANGANYA TOTO, TUMEJUA MBINU ZAO
  TUNAMTAKA MSAFI, ALOMESH HILA ZAO.

  22)                       KUNA TOFAUTI KUBWA TAJIRI NA MASIKINI
  ZAMANI WASHAPUUZWA HAWAJUI WALA NINI
  FISADI NA MATAJIRI KULA YAO MOJA SAHANI
  HAWAHITAJI RAIYA WAO HUTEMBEA ANGANI.

  23)                       WAMESHUKA ONBA KURA TENA KWA KUHONGA PESA
  UTAJIRI WAKINADI ETI NI WANA SIASA
  HALI HII WALIPITA CHA MOTO TUTAKIONA
  MOLA ATUPISHE MBALI IKULU WASIINUSE.

  24)                       RAIS ASIINGILIWE KATIKA MAAMUZI YAKE
  TARATIBU AZIPANGE KUTIMIZA AHADI ZAKE
  AKIHITAJI USHAURI BILA SHAKA ATAKWETENI
  ILA MSIMVURUGE NA ROHO ZENU ZA KWANINI.

  25)                       UKISIKIA RAIYA, AHITAJI MSAADA
  HARAKA MTUMIZIE, UONDOE YAKE SHIDA
  MA WEWE IKIMPUUZA ATAKOSA HATA PAWENDA
  JOHN JALI MZALENDO NA SISI TUTAKUPENDA.

  26)                       USIFANYE TUJUPENDE MPENDEZE MOLA WAKO
  ALO KUPA HICHO CHEO, NA HIZO PUMZI ZAKO
  UONGOZI ALISHA TAJA, NASI TUWE NYUMA YAKO
  SASA TUFANYIE WEMA, ASIJE KUCHAPA VIBOKO.

  27)                       PENDELEA MASIKINI UFUKARA HAKUUOMBA
  FISADI ALIMUWAHI PESA ZOTE AKAKOMBA
  TANZANIA ITAJIRI HAIITAJI OMBA OMBA
  RAIS KILA LA KHERI NYUMA SI TWASHIRI KAMBA.

  28)                       RAIS UJITOLEE KUWEKEZA VIJIJINI
  HUKO WAMEWAPUUZA KANA KWAMBA SI NCHINI
  MASIKINI WANYAMAZA NA HAWAJUI KUNA NINI
  UKIMYA WAO SI BURE ISIJE KUWA WA LAANI.

  29)                       BARA PIA VISWANI – NI MUUNGANO WA NCHI MOJA
  WAZALENDO HAPA NCHINI, SISI NI KITU KIMOJA
  BARA TWATAKA RIDHIKA, PEMBA MPAKA UNGUJA
  RAIS WA MUUNGANO NDO HUYO TUNAMMGOJA.

  30)                       THEHEBU KUBWA NI MBILI WAKRISTO NA WAISLAM
  WOTE TUHESHIMUMIANE NA KUPEANA SALAAM
  NJE WANATUTAMANI, TUNAVYOISHI KWA SALAMA
  MFANO WA JIJI LETU, BANDARI YA SALAMA.

  31)                       ELIMU KWETU MUHIMU MAVAZI PIA MAKAZI
  TUTIBIWE KIRAHISI TUYAPATAPO MARADHI
  AJIRA ZIWE KWA WINGI, NASI TUSHIRIKI KAZI
  USALAMA UBORESHWE KUKOMESHA MAJMBAZI.

  32)                       MSAFI TUMAKUOMBA ZIDISHA ZAKO JUHUDI
  TANZANIA ISAFISHE UUTUTE UFISADI
  MAFISADI WASHATOKA, UZUIE WASIRUDI
  SIFA YETU YA ANAMI, TUUMBE MUNGU IRUDI.

  33)                       MACHAFUKO TUYAKWEPE, KWANI VITA HAINA MACHO
  MIFANO TUNAIONA, KWANI HAINA KIFICHO
  WENZETU WANAUWANA HAWANA PA KUJIFICHA
  IKIANZA IMEANZA, KAMWE HAIWEZI ACHA.

  34)                       TWAWAONYA MAJIRANI WASIO JALI AMANI
  KWAMBA TOKEA ZAMANI, TUMEITUNZA AMANI
  TUNACHOLINDA AMANI, BARA MPAKA VISIWANI
  TANZANIA YA AMANI, JADI YETU NI IMANI.

  35)                       TUNAINUA MIKONO MOLA ASISHUSHE GHARIKA
  UONEVU UKIZIDI – WOTE SI TUTADHURIKA
  YEYE PEKEE NDO ANA SIRI HUKUMU YAKE IKIFIKA
  TUSHIKANE KWA MAOMBI MUNGU ATATUITIKA.

  36)                       TUNAINUA MIKONO KUOMBA KWAKO RABUKA
  HATUNA SI KIMBILIO, ILA KWALO MTUKUKA
  RABBI ONDOA VILIO, WAZELENDO TWATESEKA
  TUTUNUKU KIONGOZI NA SISI TUPUMZIKE.

  37)                       TUMIMINIE BARAKA ISAMBAE DUNIANI
  ISITOKEE GHARIKA , KUJA KUTUANGAMIZA
  TUACHE  KUTENDA DHAMBI, TUMUOGOPE MANANI
  TUWE WATU WA UPENDO UTUKINGE NA SHETWANI.

  38)                       NIMEZALIWA TANZANIA NIMEKULIA TANZANIA
  MIMI NAJIVUNIA KUITWA MTANZANIA
  NAPIGANIA NCHI YANGU, SWEET HOME TANZANIA
  MOLA TUSHUSHIE NEEMA – TANZANIA YA WATANZANIA.

  UTENZI HUU WA WAZALENDO NI ZAWADI KWA RAIS WETU MSAFI,
  MPENDWA, MTARAJIWA. EWE MOLA WETU TUALALIE UCHAGUZI 25/10/2015 UWE WA SALAMA NA AMANI.  0 0

   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasha mshumaa baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo.
   Mama Samia akishiriki kuomba dua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
  Mama Samia akiondoka baada ya kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere. Butiama mkoani Mara. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

   Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambako alika kusalimia familia hiyo na kuzuru kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, leo, katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama, akiwa kaika ziara ya kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto wa sita wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere, alipowasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa huyo, katika Kijiji cha Mwitongo, Bitiama mkoani Mara.
   Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere
   Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
   Chifu wa Ukoo wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Japhet Wanzagi, akimkaribisha na kutoa utambulisho kwa Mgombea Mweza wa Urais Mama Samia Suluhu Hassan,
   Aliyekuwa Muomba nia ya kugombea Ubunge jimbo la Nkenge, Asupta Mshama, akipozi kwenye baadhi ya miamba ya mawe iliyopo katibu na kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, katika Kijiji cha Mwsenge, Butiama mkoani Mara.


older | 1 | .... | 659 | 660 | (Page 661) | 662 | 663 | .... | 1897 | newer