Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

IGP MANGU AHIMIZA UCHAGUZI WA AMANI TARIME.

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na Maofisa wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi.Kushoto ni Kamanda wa Polis Kanda Maalumu Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hosteli ya Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizindua Hosteli ya Polisi katika mkoa wa Kipolis Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na wadau wa Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa  katika ziara ya kikazi mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya ambapo alitumia kikao hicho kuwaasa kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)


Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Tarime.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amewataka Viongozi wa Vyama vya Siasa katika Wilaya za Tarime na Rorya kufanya Kampeni za Kistaarabu ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu pamoja na kuimarisha Amani na Usalama Wilayani humo.
IGP Mangu aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wadau wa Polisi wakiwemo Viongozi mbalimbali, Vyama vya Siasa pamoja na Wagombea wa Viti vya Ubunge na Udiwani, wakati alipokuwa katika Ziara ya Kikazi katika Kanda Maaalum ya Polisi Tarime na Rorya.

Alisema ili uchaguzi wa mwaka huu uweze kufanyika kwa amani, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea hawana budi kuwashawishi wafuasi wao kufuata Maadili ya Uchaguzi ikiwemo kutotoleana lugha za Matusi.

IGP Mangu alisema baada ya Uchaguzi maisha yataendelea kama kawaida hilo ni jukumu la Wananchi wote wa Tarime kuondoa Uhasama wao katika mambo ya Siasa kwa kuwa Siasa siyo Uhasama.

Aidha, aliwashauri Wagombea Ubunge na Udiwani katika Majimbo ya Tarime Mjini, Vijijini, na Rorya kukutana mara kwa mara ili kujenga kuaminiana na kutatua changamoto zinazojitokeza katika kipindi hiki cha kampeni na hatimaye siku ya uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Tarime na Rorya, kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Lazaro Mambosasa, aliwahakikishia Wadau wote kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kukabiliana na vitendo vyote vya vurugu vitakavyojitokeza, pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura bila vitisho vya aina yoyote.

Naye Mgombea Ubunge katika Jimbo la Rorya kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Lameck Airo alisema katika jimbo analogombea hakuna vurugu kwa kuwa wamekuwa wakiheshimiana katika Kampeni ili kuepusha vurugu kwa Wagombea na Wafuasi wao.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa, Wafanyabiashara, Asasi zisizo za Kiserikali, Wazee wa Kimila pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tarime.

ROCK CITY MARATHON 2015 YAZINDULIWA, KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 15

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye hali ya furaha mara baada ya kuzindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (mwenye shati jeupe), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa pili kushoto), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa tatu kushoto).

 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji pamoja na wadhamini wa mbio za Rock City Marathon mara baada ya kuzindua rasmi msimu wa saba wa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni (kutoka kushoto) Katibu Mkuu wa BMT, Lihaya Henry,  Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio waratibu wa mbio hizo, Erasto Kilawe, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro , Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo pamona na Katibu Mkuu msaidizi chama cha riadha Tanzania (RT) Bi. Ombeni  Savala .
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika Novemba 15 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbio za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Bw. Malinzi alisema baraza linafuraha kuona makampuni binafsi yakijiingiza katika kuinua mchezo wa riadha nchini.
“Mchezo wa riadha una changamoto kubwa na tunatambua jitihada zinazoendelea kufanywa na kampuni ya Capital Plus katika kurudisha hadhi ya mchezo  huu nchini kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini,” alisema.

 Alisema kuwa Tanzania itarudi kileleni katika medani za michezo duniani kama wachezaji wataandaliwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
“Inashangaza kuona taifa la watu milioni 45 linawakilishwa na wanariadha wachache sana, tena katika mbio ndefu huku tukikosa wanariadha wanaoliwakilisha vyema taifa katika mbio fupi,” alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw. Erasto Kilawe alisema kuwa mbio hizo zimekuwa zikionyesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.
 “Jiji la Mwanza limebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii. Jambo hili limetusukuma kuendelea kumulika vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika ukanda wa ziwa Victoria kupitia mbio hizi,” alisema Bw. Kilawe huku akiongeza kuwa mikakati kabambe imewekwa ili kuhakikisha mbio za mwaka huu zinakuwa za mafanikio makubwa kuliko misimu iliyopita.
Alisema baadhi ya makampuni yameanza kujitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Precision Air, New Africa Hotel na Bank M huku makampuni zaidi yakionyesha nia ya kudhamini mbio hizo.
“Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na wanariadha, viongozi wa vyama vya riadha, viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wadau mbali mbali wa riadha nchini.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF , Salim Kimaro alisema kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kudhamini mbio hizo kutokana ari yao katika kukuza hali ya michezo hapa nchini.
“Kwetu suala la michezo ni moja ya vipaumbele vyetu kutokana na ukweli kuwa michezo ni afya na pia ni sehemu ya ajira kwa vijana kwa sasa…tunaahidi kuwa mstari wa mbele katika kufaanikisha mbio hizi,’’ alisema.

TASOI YAZINDUA KAMPENI YA SARATANI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO BILA MALIPO YOYOTE

$
0
0
Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo jijini Dar.
Mshauri kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Dominista Kombe ambaye akitoa takwimu ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage  akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo.
 Waandishi wa habari wakiendelea kuchuka habari.
 Mkutano ukiendelea

Na Michael Maurus, Dar es Salaam

ASASI isiyo ya kiserikali ya Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI), imezindua kampeni rasmi mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote.



Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo, alisema kuwa kampeni hiyo itatoa elimu, uhamasishaji na kutoa ushauri nasaha kwa wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).



Amesema kuwa katika kampeni hiyo, TASOI inashirikiana na wadau mbalimbali katika masuala ya afya, teknolojia na uhamasishaji wa jamii ili kutoa huduma hii muhimu bila malipo au gharama yoyote kwa watumiaji wa simu za mikononi.



“Kwa kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Yasiyoambukiza Wizara ya Afya, Profesa Ayoub Mgimba, ‘Hali halisi inadhihirisha kwamba magonjwa yasiyoambukiza kama saratani hivi sasa yamekuwa ni tatizo kubwa hasa katika nchi kama yetu ambapo ufahamu na mwamko ni mdogo sana juu mazingira hatarishi, viashiria, matibabu na matunzo ya wahanga wa magonjwa haya. Saratani inasababisha madhara makubwa ambayo yanaelekea kuwa majanga kwa jamii na kiuchumi kwa Taifa.”




Akielezea jinsi kampeni hiyo itakavyoendeshwa, Hellen alisema kuwa kwa muda wa miezi sita, watumiaji wa simu za mkononi za mitandao yote nchini, wataweza kupata taarifa za saratani kwa kupitia namba 15774 kwa kutuma neno CANCER au SARATANI kwenda namba hiyo na kuchagua lugha anayotaka kupokea taarifa hiyo, iwe ni Kiswahili au Kiingeza.



“Hapo utapokea ujumbe wenye elimu juu ya saratani, kati ya za viungo vya uzazi, yaani tezi dume, saratani ya matiti na shinga ya kizazi. Huduma hii itapatikana kupitia mitandao yote ya simu nchini, Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na TTCL,” alisema.



Ameongeza, “Tungependa pia kuwashirikisha wananchi wote kuchangia kwa hiyari ili tutimize malengo haya kwa pamoja. Na hii unaweza kuchangia Sh 1200 kwa mwezi au Sh 300 kwa wiki.



“Hili utaweza kulifanya kwa kukubali kupokea ujumbe mfupi kutoka kwetu ambao utakuwa na gharama ndogo ya Sh 150 tu. 

Pia unaweza kuchangia kupitia ezypesa, m-pesa, tigopesa, airtel money. Uchangiaji huu ni wa hiyari na hauzuii kupata huduma ya elimu ya saratani.”



Kwa upande wake, Daktari bingwa wa kwanza wa saratani mwanamke Tanzania, Dominista Kombe wa Ocean Road Cancer Istitute, amesema kuwa ni kweli saratani ni janga la jamii, hali halisi hapa Tanzania, saratani ni tatizo kubwa na linaongezeka kwa kasi, ni jumla ya ugonjwa wa HIV na ugonjwa wa TB, tatizo la saratani lilitakiwa kupewa kipaumbele zaidi.



“Tatizo jamii huwa haipo tayari kuweka wazi juu ya uginjwa huu kwa kuogopa aibu ya kutengwa, haya yote yakitokana na uhafamu mdogo juu ya ugonjwa huu,” amesema.



Amesema kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa huduma bure, lakini hata hivyo imejikuta ikishindwa katika kukabiliana nalo kwani tatizo ni kubwa mno, akiitaka jamii kusaidia katika vita hiyo kama walivyoamua kufanya TASOI waliokuja na mpango wao wa kampeni kupitia simu kuiwezesha jamii kujua juu ya viashiria vya janga hilo.



Amesema kuwa tatizo la saratani ni la dunia nzima, hivyo kuna ulazima wa jamii kujenga utaratibu wa kupima afya mara kwa mara kama ilivyo kwa nchi za Ulaya ambako imesaidia kupunguza ukubwa wa janga hilo kupitia chanjo.


Amesema kuwa Ocean Road hupokea wagongwa wapya 5000 kwa mwaka, kati yao asilimia 80, wanafika wakiwa katika hali mbaya kiasi kwamba hupewa tiba ya kuwaongezea siku tu, huku asilimia ndogo sana, huwahi na kupewa tiba inayowawezesha kuishi.

FRIENDS PUB YA SEGEREA NA CHECKPOINT CHANIKA BAA ZA WIKI TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI

$
0
0
 Mkazi wa Kigogo Fresh-Chanika Bi. Mazoea Kombo (katikati) akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia Serengeti kanda ya Chanika Bw. Tesha Stanslaus (Kulia) katika hafla ya kuipongeza baa ya Check Point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Bi. Mazoea aliimwagia sifa bia hiyo kuwa ni laini na haimchoshi.
 Mkazi wa Chanika Kay Christopher akipokea zawadi yake ya fulana kutoka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (Kulia) wakati wa kuipongeza baa ya Check Point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwa mara ya pili kwenye Kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli kiwanjani. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash
Mkazi wa Segerea na mteja wa bia ya Tusker Bw. Nelson Ruta akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa mwakilishi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Josephat Lukindo (kulia) katika hafla ya kuipongeza baa ya Friends ya Segerea jijini Dar es salaam ambayo ilitangazwa kuwa baa ya wiki kwenye kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo inaendeshwa kwa udhamini wa bia ya Tusker kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti.

  Mkazi wa Majohe Dotto Ramadhani akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Check point ya Chanika jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi katika baa hiyo na kuipongeza kwa kuibuka baa ya wiki kwa mara ya pili katika kipindi hiki cha Kampeni hiyo ya bia ya Tusker.
 Mkazi wa Kinyerezi na mpenzi wa bia ya Tusker Zack Ngaweleja (kulia) akiifurahia zawadi yake ya T-shirt aliyokabidhiwa na balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (katikati) wakati ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi karibu na baa yake ya mtaani “Friends Pub” iliyopo Segerea jijini Dar es salaam. Baa hiyo ilitangazwa kuwa baa ya wiki kwenye Kampeni inayoendelea ya “Tusker Fanyakweli” inayoendeshwa na bia ya Tusker kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash.
 Balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (kushoto) akikabidhi zawadi ya fulana kwa mpenzi wa bia ya Tusker aliyefahamika kwa jina la Emmy Machupa (29) (katikati) wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya “Friends” iliyopo Segerea jijini Dar es salaam ambayo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti. (kulia) ni Mshereheshaji wa promosheni hiyo na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni redio E-fm, Gadner Habash.

EALA ROOTS FOR CONCERTED EFFORTS IN COMBATING CORRUPTION

$
0
0
 Heads of Anti-Corruption Authorities from Republic of Kenya (left), South Sudan (centre) and the Federal Republic of Ethiopia stand for the Anthem at the start of the meeting in Entebbe earlier today
 Rt Hon Daniel F. Kidega (right) Speaker of EALA, Hon Shem Bageine, Minister for EAC Affairs, Uganda and Lady Justice Irene Mulyagonja, inspector General of Uganda at the meeting earlier today.  The EALA Speaker opened the meeting
A section of delegates at the meeting in Entebbe

East African Legislative  Assembly

EALA ROOTS FOR CONCERTED EFFORTS IN COMBATING CORRUPTION
Speaker Kidega tells Anti-Corruption stakeholders Assembly keen to close ranks to fight off vice

East African Legislative Assembly,Entebbe,Uganda,29th September 2015 –  EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega wants Anti-Corruption Authorities in the EAC region to further concert efforts, establish linkages and support enactment of a regional law in their quest to rid the region of corruption. 

Consequently, the regional Assembly is set to collaborate with the anti-graft authorities under the aegis of the East African Association of the Anti-Corruption Authorities (EAAACA).  

The EALA Speaker this morning presided over the opening ceremony of the 9th EAAACA Annual General Meeting themed; Strengthening Efforts to eradicate Corruption in Entebbe, Uganda.

Rt. Hon Kidega said that EALA and the EAC were committed to combating the chronic cancer of corruption.   He said the Assembly would soon table and discuss key pieces of legislation to combat the scourge.

“On our part as an Assembly, you will be pleased to note that we are considering enacting 3 key Bills to confront corruption head-on. The envisaged Bills are the EAC Integrity and Anti-Corruption Bill, 2015, the EAC Procurement Bill, 2015 and the EAC Whistle Blowers Bill, 2015. The Laws passed by EALA supercede those of the Partner States on matters within the purview of the Community”, the Hon Speaker remarked.

He termed regional co-operation as a key component in containing corruption saying that it undermined good governance, erodes the rule of law and hampers economic growth. “If left unattended, it could spiral to uncontrollable levels given the other criminal activities such as money laundering, bribery and abuse of Office,” Rt. Hon Kidega remarked.  

The Speaker was emphatic that it was necessary for the Association to have a closer working relationship within the EAC.    “As a key institution in the eradication of corruption, it is vital and necessary for EAAACA to explore means and ways of working with EAC including been considered for Observer Status at the Community,” he remarked.

According to the Speaker, the Mbeki led Report on the High Level Panel on illicit Financial Flows released in February this year is telling. The Report narrates that illicit flows relate principally to commercial transactions, tax evasion, criminal activities such as money laundering, bribery, corruption and abuse of office, which he said promote corrupt tendencies. 

Moreover, it is reported that countries that are rich in natural resources and countries with inadequate or non-existent institutional architecture are most at risk of falling victim to illicit financial flows.  

In attendance at the two-day AGM are representatives of Anti-Corruption Authorities from Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Ethiopia and South Sudan. 

The meeting is being hosted by the Inspectorate of Government led by the Inspector General of Government of the Republic of Uganda Hon. Lady Justice Irene Mulyagonja Kakooza.   Lady Justice Kakooza maintained that ridding corruption needed political, legislative and the goodwill of all citizens.

The Minister for EAC Affairs, Hon Shem Bageine said corruption had spread its tentacles in various sectors in the region and largely manifested itself across the divide.  “Governments, Private and Public sectors must get to the bottom of and root out this evil,” Minister Bageine added.

On his part, the President of the EAAACA, Mr Clément Musangwabatware reiterated the need to embrace good governance and total fight on corruption which he termed costly to governments and businesses.

Analysts contend that promoting and facilitating co-operation among Partner States is crucial in ensuring effectiveness of measures and actions to detect, investigate, punish and eradicate corruption.
is further expected to review its activities over the year as it strategises over how to make it more effective.

The AGM is the supreme governing body of the Association and comprises of Members of Anti-Corruption Authorities of EAAACA and Honorary Members.

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI KATIKA VIWANJA CHA GARAGARA MTONI ZANZIBAR,

$
0
0
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza na Wananchi na WanaCCM katika viwanja vya garagara mtoni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na kuwatana Wananchi kumpigia kura Dk Shein, ili kuzidi kuleta maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya garagara wakihudhuria mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, 
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urai kupitia CCM katika viwanja vya garagara Mtoni Zanzibar. 
Mama Fatma Karume akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viiwanja vya Garagara mtoni Zanzibar na kuwataka siku ikifika kutia kura ya Ndio kwa Dk Ali Mohamed Shein.
Wananchi wakimshangilia Mama Fatma Karume wakati akiwahutubia katika mkutano wa Kempeni ya Mgombea ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Wasaani wa Bendi ya Moto wakitowa burudani kuhamasisha  Wanachama wa CCM wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, zilizofanyika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mambo ya Yomoto Bendi hayo katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya garagara wakimuombea Kura Dk Shein, wakati wa kampeni yake.  

Wanachama wa CCM wakifuatilia burudani hiyo wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika viwanja vya garagara mtoni akiwa katika mikutano yake ya kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar. kwa kupata ridhaa za Wananchi kuongoza Zanzibar kwa Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali na kudumisha Amani na Utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba. 

Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar na kutowa sera za CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya kipindi chake baada ya kupata ridhaa za Wananchi kumpa kura ya Ndio.katika uchaguzi mkuu mwa huu.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akifuatilia Sera za CCM wakati Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar
Wanachama wa CCM wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya garagara mtoni 

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Welezo Zanzibar kupitia CCM Saada Mkuya katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtoni Zanzibar wakati wa mkutano wa kampeni za Urais wa Zanzibar Dk Shein katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Kanali Mstaaf Khamis , wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wakati wa mkutano wa kampeni za Urais zilizofanyika katika viwanja vya garagara Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Mhe Machano Othman akizungumza kwa niaba ya wagombea wezake katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea wa Udiwani wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.


Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akiagana na Viongozi wa CCM baada ya kumalizika kwa mkutano wa Kampeni katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar 
Imetayarisha na OthmanMapara.Blogspot.

SERIKALI YAMTAKA KILA MWANAJAMII KUTAMBUA HAKI ZA WAZEE NA KUWATHAMINI

$
0
0
Na Magreth Kinabo –maelezo
30/09/2015
Serikali   imemtaka kila mwanajamii kutafakari haki ambazo wazee wanastahili na kuweka mipango ya makusudi katika kuwawezesha kuzipata haki hizo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt, Donan Mmbando (Pichani) kupitia tamko  la wizara hiyo kuhusu maadhimisho  ya siku ya kimataifa ya wazee duniani itakayofanyika kesho  Oktoba Mosi ,mwaka huu wilayani Kasulu mkoani  Kigoma.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Umuhimu  Kuwashirikisha Wazee Kwa Ustawi Endelevu Mijini”

“Uko umuhimu kwa jamii yetu kutafakari iwapo tunatambua mahitaji halisi na kuthamini michango yao kama rasilimali muhimu katika maendeleo ya taifa.

“Tunawashirikisha, tunawaheshimu na kuwaendeleza kama wananchi wengine na tunaheshimu mila na desturi nzuri za kuwaenzi wazee hao,” alisema Dkt. Mmbando.

 Ameongeza kwamba wazee katika nchi yetu wanayo nafasi kubwa katika juhudi za kuleta maendeleo. Katika maisha ya kila siku ya jamii, wazee wanakubalika kuwa ni watoa habari, ujuzi wa mila na desturi, washauri na wapatanishi. Pia wazee ni walezi wa watoto wadogo,hususan kwa watoto yatima walioachwa na wazazi wao kutokana na janga la UKIMWI.

“ Natoa  wito kwa watendaji wote kwa nafasi zao mbalimbali hususan wakurugenzi watendaji  Halimashauri za Miji/Manispaa/Wilaya na wakala mbalimbali zinazotoa huduma kwa wazee ili ziweke mipango inayozingatia haki za wazee na kuimarisha mifumo ya kinga ya jamii iliyopo ili kuboresha huduma wanayopata,” alisisitiza.

Aidha Dkt. Mmbando alisema alisema suala la wazee ni mtambuka, hivyo kila idara na asasi mbalimbali za Serikali na watu binafsi zishiriki katika  kuhakikisha  kwamba juhudi juhudi za makusudi zinafanywa ili kuboresha maisha ya wazee.

 Alisema Serikali itaendelea kutambua na kuthamini michango inayotolewa na wazee katika maendeleo ya taifa letu.

“ Hivyo nawaomba wazee waendelee kushirikiana na Serikali yao katika kuendeleza utulivu  na amani tuliyonayo na pia waendelee kuwa kielelezo bora na urithi kwa vijana wetu kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.

 Alitoa changamoto kwa vijana kuwa karibu na wazee ili kujifunza maadili mema toka kwao na kuwajibika kuwahudumia ipasavyo na kuweka taratibu za kujiwekea akiba kila wanavyopata ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kufanya maandalizi ya maisha kuelekea uzeeni.

TANGAZO LA KIFO

$
0
0

FAMILIA YA CLEMENCE KATO YA KINYEREZI KIBAGA DAR ES SALAAM INATANGAZA KIFO CHA MAMA YAO MPENDWA CORONA BITUNGWA (MAMA WAWILI) KILICHOTOKEA ALFAJIRI YA LEO TAREHE 30/09/2015 HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI,HABARI ZIWAFIKIE NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WOTE,MSIBA HUKO NYUMBANI KWA MAREHEMU KINYEREZI KIBAGA, TAARIFA YA TARATIBU ZA MAZISHI ZITATOLEWA BAADAE.
                  ..BWANA AMETOA,BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE….

SERIKALI YAKANUSHA WANYAMA KUTOROSHWA NCHINI

$
0
0

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
SERIKALI imekanusha uvumi uliozagaa katika mitandao ya jamii wiki hii kuwa wanyama aina ya twiga wanatoroshwa kutoka pori tengefu la Loliondo na kupelekwa nje ya nchi.

Katibu Mkuu wa Wizara Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru (Pichani) ameziita habari hizo kuwa za uongo, uzushi na uchochezi.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dkt. Meru alisema jambo hilo si la kweli na linalenga kuleta chuki dhidi ya serikali.

“Picha zile zimetolewa katika intaneti na kuelezwa kuwa ni za Tanzania, si kweli.  Ni picha za kughushi,” alisema Dkt Meru.

Pia alibainisha kwamba twiga wa Tanzania wanatumika kama nembo ya taifa na hawaruhusiwi kuwindwa hata kidogo, “sasa kusema wamewindwa na kusafirishwa ni uzushi na upotoshaji.”

Alisema ukweli uliopo ni kwamba Kampuni ya Ortero Business Corporation iliyosajiliwa hapa nchini iliomba kibali cha kawaida cha uwindaji na kukubaliwa.

Kampuni hiyo ilipata vibali vya watu wanane vya uwindaji wa wanyama wakiwemo kongoni, ngiri, pofu, na swala pamoja na aina ya ndege mbalimbali.  Kibali hakikuhusisha wanyama kama twiga, simba wala tembo.

Alisema kufuatia kibali hicho tarehe 25 Septemba, 2015 zilikuja ndege tatu aina ya CI 30 UAS, 312, na kupata kibali namba TCAA/5055/21294 ya mizigo; ndege ya abiria L6RJI iliyopata kibali namba TCAA/5055/21295 na ndege nyingine ya abiria A9HRM 767 iliyopata kibali namba TCAA/5055/21300.

Ndege hizo zilikuwa na Mohamed Sheikh Mohamed Bin Rashid, Mfalme toka Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu akiambatana na msafara wa watu 137 na kutua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Alisema ujumbe huo wa watu ulifuata taratibu za kuingia nchini na kupata vibali halali vikiwemo vya uhamiaji na baadaye walielekea Loliondo.

Miongoni mwa watu hao walikuwemo watazamaji, wafanyakazi wa ndege hizo, watoa huduma wa mfalme huyo miongoni mwa wengine.

Alisema vibali vya uwindaji huo vimeipatia serikali dola za kimarekani 41,400 sawa na Tshs milioni 85.

Kwa mujibu wa Dkt. Meru, baadhi ya watalii hao pamoja na mfalme huyo waliondoka Septemba 29, 2015 huku baadhi ya maofisa wake wakiwa bado hapa nchini kwa ajili ya kukamilisha utaratibu wa kuhakiki wanyama na ndege waliowindwa na malipo ya serikali.

Dkt. Meru alisema uwindaji huo ulisimamiwa na maofisa wa jeshi la polisi, usalama wa taifa, maofisa wa kuzuia wanyama wanaokatazwa kuwindwa, maofisa wa halmashauri ya Loliondo na maafisa wa wizara kitengo cha kuzuia ujangili.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Herman Keraryo utalii wa kuwinda ni moja ya vyanzo vikubwa vya mapato si kwa Tanzania tu bali na nchi nyingine duniani.

Kwa mwaka jana tu, utaliihuo uliingizia Wizara dola za Kimarekani milioni 18.



Alitaja faida nyingine kama kuwianisha idadi ya wanyama katika mapori na kuzuia ujangili.

WARSHA YA MAZINGIRA YAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
01
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi akifungua warsha ya siku mbili kwa wataalamu wa Mazingira juu ya kuzindua mradi wa Utafiti wa Teknolojia ya kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na usambazaji wake kwa wadau. Warsha hiyo imeshirikisha wadau kutoka Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na Mashirika yanayosimamia hifadhi na usimamizi wa Mazingira.
03
Bi Euster Kibona Mtaalamu mwelekezi akitoa mada juu ya Mabadiliko ya Tabianchi katika warsha hayo.
04
Washiriki katika vikundi mbalimbali wakijadiliana.
02
Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo, Bw. Richard Muyungi (waliokaa – kutoka kulia wa pili)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya ufunguzi wa warshahiyo.

Wadau wa sanaa waipongeza Serikali

$
0
0
 2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akiongea na wawakilishi wa Kampuni ya Haak Neel Production walipo mtembelea ofisini kwake  Septemba 29, 2015 jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuishukuru Serikali kwa ushirikiano wake katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Msanii Dunia mwaka jana.Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa Basata wamekuwa wakiaandaa maadhimisho hayo ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 12 Desemba.
1
Mratibu wa maadhimisho ya Siku ya Msanii duniani Bw. Justice Jones akifafanua jambo wakati walipotembelea ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kulia) kwa lengo la kuishukuru kuishukuru Serikali kwa ushirikiano wake katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Msanii Dunia mwaka jana.Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa Basata wamekuwa wakiaandaa maadhimisho hayo ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 12 Desemba.
3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Haak Neel Production Bw. Emmanuel Mahendeka akifafanua jambo wakati walipotembelea ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kulia) kwa lengo la kuishukuru kuishukuru Serikali kwa ushirikiano wake katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Msanii Dunia mwaka jana.Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa Basata wamekuwa wakiaandaa maadhimisho hayo ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 12 Desemba.
4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akiongea na wawakilishi wa Kampuni ya Haak Neel Production pamoja na Kamati ya maadhimisho ya Siku ya Msanii nchini Tanzania walipo mtembelea ofisini kwake jana kwa ajili ya kuishukuru Serikali kwa ushirikiano wake katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Msanii Dunia mwaka jana.Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa Basata wamekuwa wakiaandaa maadhimisho hayo ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 12 Desemba.
Picha na: Frank Shija, WHVUM

UZINDUZI WA KANUNI YAKUDHIBITI NA MATUMIZI YA MISUMENO YA MOTO WAFANYIKA ZANZIBAR.

$
0
0
1
Baadhi ya misumeno ya moto iliokamatwa katika sehemu mbalimbali ambayo ikitumika katika kukata miti ikiwa imewekwa kusubiri kuangamizwa kwa moto  katika Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.
2
Wafanyakazi wa Kilimo na mali ya Asili wakikusanya kuni kwa ajili ya kuichoma moto Misumeno ya moto iliokamatwa sehemu mbalimbali katika Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.
3
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na mali asili Zisizorejesheka Sheha Idrissa Hamdan akitia mafuta kwa ajili ya kuichoma moto  Misumeno ya moto iliokamatwa sehemu mbalimbali katika Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.
4
Waziri wa Kilimo na mali ya Asili Dk Sira Ubwa Mamboya watatu kulia akiangalia misumeno ya moto iliokamatwa sehemu mbalimbali ikichomwa moto katika Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.

5
Waziri wa Kilimo na Mali ya Asili Dk Sira Ubwa Mamboya akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusiana na Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.
6
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza na kunukuu taarifa inayotolewa na Waziri wa  Kilimo na Mali ya Asili Dk Sira Ubwa Mamboya katika  Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.
7
Waziri wa Kilimo na Mali ya Asili Dk,Sira Ubwa Mamboya akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari pamoja na wananchi kuhusiana na  Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.
8
Waziri wa Kilimo na Mali ya Asili Dk,Sira Ubwa Mamboya akizungumza na vyombo vya habari nje ya Ukumbi wa ASSP baada ya kutoa taarifa ya Uzinduzi wa Kanuni ya kudhibiti na matumizi ya Misumeno ya moto Maruhubi mjini Zanzibar.PICHA NA-YUSSUF SIMAI ALI -MAELEZO ZANZIBAR.

IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

$
0
0
IMG_3000Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
………………………………………….

JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

Alisema kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.

Aidha maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha mafunzo hayo.Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.
Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.

“Lengo la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa ‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,” alisema Profesa Bhalalusesa.

IMG_3089 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).

Alisema hadi kufikia wakati huu serikali imeshapiga hatua kubwa katika matumizi ya Tehama ambayo katika majaribio yake yameonesha kufanikiwa na wadau mbalimbali wa elimu wameyapongeza na kuyaunga mkono.
Profesa Bhalalusesa alisema kwa sasa wagunduzi mbalimbali wa mifumo ya Kompyuta inayoweza kutumika kufundishia ndio watakoonesha kazi zao na kutoa ufafanuzi wa kina kwa majaji wataochagua kazi chache na kuzifanyia majaribio kabla ya kuanza kutumika kufundishia.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mpango wa Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutoka Wizara ya Elimu, Agripina Habichi alisema mpango huo wa matumizi ya Tehama utasaidia wanafunzi kufahamu kusoma na kuandika kabla ya kuendelea na masomo ya darasa la tatu.
“Maonesho haya yanafanyika katika wakati muafaka ukizingatia tunataka kupiga hatua kubwa katika kuboresha elimu yetu. Washiriki wa maonesho haya wamekuja kutuonesha utawaalamu wao unaoweza kutumika kufundishia.

Lengo letu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ambapo tumeazimia kuzifikia shule zaidi ya 2000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 na hivyo tutakuwa katika kiwango bora zaidi cha utoaji wa elimu inayojitosheleza,” alisema Habichi.

MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA

$
0
0
IMG_3349
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi.

 Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.

Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
IMG_3303
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.
Akizungumza umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”
Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.
Alisema kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya kutia saini malengo hayo na hilo linaonesha ni kiasi gani serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wengine kuufuta umaskini.
Pia alisema:“Wakati huu, masuala ya uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na kuamsha upya ushirikiano wa kidunia katika maendeleo ni msingi mzuri”
Naye Kamishina wa mipango wa Zanzibar, Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba Zanzibar imekuwa sehemu ya mchakato huu...”.
IMG_3392
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema katika utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika malengo ya milenia, inaonekana namna bora ya kuuoanisha malengo ya kitaifa na ya dunia.
Ninafurahi kusema kwamba Zanzibar tuko katika mchakato wa kutengeneza mkakati wa maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia malengo ya SDGs.
Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala Gilsenan, amesema taifa lake Ireland lipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
“Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya. Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Project Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya dunia.
IMG_3397
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
“Kama benki huwa tunazungumza na umuhimu wa kuendelea kuwapo. Huu si tu msemo bali ahadi tunayoishi nayo kila siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa duniani, kutekeleza malengo 17 kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa maendeleo endelevu.
Standard Chartered inajisikia furaha ya kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu kila mtu anayeishi nchini hapa atafaidika na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
Malengo ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa Septemba 25 wakati viongozi wa dunia walipokutana pamoja mjini New York. Malengo haya yataanza kutumika Januari 1,2016.
IMG_3226
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akipozi na lengo na 17.
IMG_3280
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi rasmi wa malengo hayo nchini Tanzania.
IMG_3390
Mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama katika picha ya ukumbusho.
IMG_3789
Meza kuu katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) nchini Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
IMG_3781
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3554
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akielezea ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3580
Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3640
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
IMG_3772
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo.
IMG_3754
Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
IMG_3796
Baadhi ya wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3829
Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali meza kuu.
IMG_3868
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana (hayupo pichani).
IMG_3857
Sehemu ya wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_3851
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
IMG_3900
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3912
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3921
Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea.
IMG_3950
Fataki zikisherehesha uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3975
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali wa maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao vya malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3997
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusiana na malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_4021
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_4029
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mwanahabari mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
IMG_4097
Bendera ya Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
IMG_4078

MO KUANZISHA BENKI YA MIKOPO KWA WAFANYABISHARA WADOGO NCHINI

$
0
0
DSC_0316
CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.
Na Modewjiblog team.

Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.

Dewji maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.

Kupitia kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.Ambapo ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.
Aidha, MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.

DSC_0310
Salim Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:“Unajua na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani, benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa mtu mwenye pesa. alifafanua MO .

Katika mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya 24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.

Tuzo aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.

MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.

MAGUFULI AAHIDI KUKOMESHA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI

$
0
0
  Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu nchini Kote huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.

Akitoa hotuba yake katika moja ya mikutano  yake alioufanya katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto  mkoani Manyara.

Dkt Magufuli ameahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa  na kuunda Serikali yake,jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini mkubwa. “Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa serikali halafu Mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa wilaya yupo  na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo, wamiliki wa Ng’ombe wabaki  wanakula maisha haiwezekani,nitalala nao mbele na  Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha”,alisema Magufuli kwa msisitizo mkubwa.

Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli  zao na kukuza kipato na  uchumi wao bila kusumbuliwa. 
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wakimsiiliza Dkt Magufuli alipokuwa akinadi sera zake za kuomba kura ili kushika nafasi  ya Urais ya awamu ya tano.

  Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli kwa kuhubiri amani katika mikitano yake ya kampeni kuliko wagombea wa vyama vingine hawasisitizi kudumisha amani nchini jambo ambalo ni tunu ya taiafa
 Dkt. Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjni Dodoma leo.
  Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa mgambo.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo.
  Mawaziri wakuu wa zamani, John Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph  Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Dodoma kwenye mkutano wa kampeni. 
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akimsimamia Mgombea ubunge Jimbo la Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde aliyekuwa akifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa  akimuombea kura Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Dodoma jioni ya leo. 
 Walemavu nao wana haki ya kuwasikiliza Wagombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais,Ubunge na Udiwani
  Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa, wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt. Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Kongwa.
 Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu wa zamani Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba,mjini Kibaigwa wilayani Kongwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
 Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa wakifuatilia hotuba za Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.
  Dk Magufuli akijipigia kampeni  kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa leo.Akiwa wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa akishinda urais atahakikisha anadhibiti mapigano  kati ya wakulima na wafugaji yanayoendelea nchini na kusababisha vifo vya watu wengi 
  Dkt. Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.

MSIBA MAREKANI NA TANZANIA

$
0
0
Bettisheba Pole Ketang'enyi enzi ya uhai wake
Tunasikitika kutangaza kifo cha mama Betisheba Ketangenyi, mama yake Yvonne Matinyi, Felicia Simms, Fredderek Ketangenyi pia ni Dada yake na Rossie Musika, Neema Musika, Daudi Musika, Sijaona Musika kilichotekea 9/30/15 katika hospitali ya NIH Maryland mipango ya kusafiri mwili wa marehemu inaendelea kwa mdogo wa marehemu Daudi Musika
3819 Gateway terrace Burtonsville MD 20866
Unaweza kuwasiliana
Frederick Ketangenyi 267 809 5124
Felicia Simms 240 608 8686
Rossie Musika 240 408 2693
Neema Musika 571 991 9819
Specioser Musika 571332 2215
Sijaona Musika 202 487 8412

HABARI PICHA SHEREHE YA WAFANYAKAZI KISSA PHARMACY LTD KIJIJINI MAKANYA SAME MOSHI

$
0
0
Mgurugenzi Kissa Pharmacy Ltd Ndugu Gaspar Kilango Singo akizungumza na wafanyakazi wake katika sherehe hiyo iliyofanyika kijijini kwao Mnazi Makanya Wilayani Same Moshi Kilimanjaro


·       Wafanyakazi  Kissa Pharmacy Ltd  Pharmaceuticals Whole Sale And Retali Mbeya Tz wenye makao makuu jijini mbeya wakiserebuka katika sherehe ya wafanyakazi iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndugu Gasper Kilango Singo kijijini kwao Mnazi Makanya Kilimanjaro Moshi
 

Ndugu na jamaa wa familia ya Kilango wakijumika pamoja katika sherehe hiyo.


Wazazi wa Mkurugenzi Kissa Pharmacy Ltd




















Picha- Emanuel Madafa Jamiimojablog, Mbeya

AMRI YA KUTOUZA NYUMBA YA MKOPO HAIKATIWI RUFAA.

$
0
0
                         KUSOMA  ZAIDI  kliks  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
Na  Bashir  Yakub

Mara  kadhaa  mkopaji  anaposhindwa  kulipa  mkopo  hukimbilia  mahakamani  ili  kuona  kama  anaweza  kupata unafuu  hasa linapokuja  suala  la  wakopeshaji  wake  kutaka  kuuza    nyumba/kiwanja  alichoweka  rehani. 

Ni  ukweli  usiopingika  kuwa  hatua  hii  imewasaidia  wengi  hasa  wale  wanaowahi.  Yapo  makala   tuliwahi  kuandika kuhusu  hatua  za kuchukua  hasa  inapotokea  kuwa  nyumba  yako  inataka  kuuzwa.


 Makala  yalieleza  namna na hatua  za  kufuata ili  kuokoa  nyumba.  Kwenda  mahakamani  kuzuia  nyumba  isiuzwe  baada  ya  kushindwa  kurejesha  kiasi  cha  rejesho  sio ukorofi  isipokuwa ni  kutekeleza  lililo  ndani  ya  sheria hasa  pale panapo  sababu  za  msingi  za  kufanya  hivyo. 

 Mahakama  za  ardhi  za  wilaya  na  mahakama  kuu  hasa  ya  ardhi  ndizo  mahakama  zenye  mamlaka  katika  kutoa  mazuio  haya  kutegemeana   na thamani  ya  nyumba/kiwanja  na kiasi  cha  deni  kilichohusishwa  katika  muamala  huo. 

Swali  kwetu ni  kama  baada  ya  kuwa  umeenda  mahakamani  na  kubahatika  kupata  zuio la kutouzwa  nyumba  yako, je  upande  wa  wakopeshaji  wanaweza kukata  rufaa  kupinga  amri  hiyo na  kufanikiwa. Majibu  ya  swali  hili ndio  makala  ya  leo.


1.HAKI  YA  RUFAA.

Kifungu  cha  74   cha  sura  ya  33 Sheria  mwenendo  wa  madai kinaeleza  rufaa  katika  amri  mbalimbali  za  mahakama.  Kifungu  kilieleza  wazi  kuwa  kutakuwa  na  rufaa  kutoka  mahakama  za  wilaya  na  zile  za  hakimu  mkazi  ambapo  rufaa  hizo  zitatakiwa  kwenda  mahakama  kuu. Kwa  wasiojua  maana  ya rufaa,  hii  ni hatua  ya  kupeleka  malalamiko  mbele  zaidi  baada  ya  kuwa  hukuridhishwa  na  uamuzi  wa  mahakama   iliyoamua  shauri  lako katika  hatua  za  awali.


Nje  ya hilo  kifungu  cha  78  cha  sheria  hiyohiyo  kiliruhusu  pia  kufanyika kwa  marejeo  iwapo  mtu  hakuridhika  na  maamuzi  ya  amri  ya  mahakama.  Marejeo  ni  hatua  ya  mahakama   kuitisha  faili  tena  na  kupitia  kilekile  ilichoamua  ili  kujiridhisha  na  uhalali  wake.  Hii  hutokea  baada  ya  upande  wa  pili  kuomba  hilo kufanyika.  Kwahiyo  ilikuwa  ikiwezekana  kutolewa  amri  ya  kuzuia  nyumba  kuuzwa  halafu  baadae  faili  likaitishwa  tena  na  kurudiwa  na  kutolewa  amri  nyingine  ambayo  inaweza  kuwa ileile  ya kutouzwa au  ikabadilishwa  ikawa  amri  mpya  ya  kuuza.


2.   SHERIA  YA  UKOPAJI  FEDHA  NA  KUWEKA  REHANI.

Mwaka  2008  ilikuja  sheria  ambayo  iliitwa  kwa  jina  la sheria  ya  ukopaji  fedha  na  kuweka  rehani.  Sheria  hii  inazungumzia  masuala  yote  nyeti  yanayohusu   kukopeshwa  fedha  na  kuweka  rehani  mali . Ni  sheria  inayoratibu  masuala   yahusuyo  kuuzwa  kwa  mali  zilizowekwa  rehani na  kutouzwa  kwake. Inazungumzia  haki  za  mkopaji  na  mkopeshaji  halikadhalika  wajibu  wao  wote  katika  nafasi  zao.  Kutokana na  ujio  wa  sheria  hii  masuala  kadhaa  katika  sheria  ya  ardhi  ya 1999  sambamba  na  sheria  ya  mwenendo  wa  madai sura ya  33  zimelazimika  kufanyiwa  marekebisho  ili  kukidhi  malengo  kadhaa .


3.  AMRI  YA  KUTOUZA  NYUMBA  YA  MKOPO  HAIKATIWI  RUFAA.

Hapo  juu  tuliona  kuwa  awali  ilikuwa  ni  ruhusa kwa  mtu  kukata  rufaa   hata  kwa  amri  iliyotolewa  kuzuia  nyumba/kiwanja    cha   mkopo  kuuzwa.  Mahakama  ya  wilaya  ingeweza  kutoa  amri  kuwa  nyumba  fulani isiuzwe  hata  kama  mkopaji  yuko  nje  ya  makubaliano  kwasababu  kadha  wa  kadha. Hata  hivyo   ilikuwa  ni haki  ya  mkopeshaji ambaye  ndiye  hutaka  kuuza  nyumba  kukata  rufaa  na  kupinga  amri  hiyo. 

Kama  amri  hiyo  ingetolewa  mahakama  ya  wilaya  au  ya  hakimu mkazi basi  mkopeshaji  angeweza  kukata  rufaa  kwenda  mahakama  kuu.  Na  huko   ingewezekana  kutolewa  uamuzi  uleule  au  uamuzi  mpya  ambapo  pengine  amri  ya  kutouzwa  ingebatilishwa  na  kuruhusu  uuzaji  kuendelea.


Kwa sasa kutokana  na   sheria hii  ya  masuala  ya  ukopeshaji fedha  na rehani  kifungu  hiki  kimefanyiwa  marekebisho  na  sasa  ni  kuwa  amri  ya  mahakama  iwe  ya  wilaya  au  mahakama  kuu  ikishapita  na  kutoa  zuio  la  kutouzwa  nyumba  ya  mkopaji   basi   huwezi  tena  kukata  rufaa  kupinga  jambo  hilo.  Amri  hiyo  ikishatolewa  basi  inakuwa  imetolewa. Ni  kutokana  na  hilo  kichwa  cha  makala  haya kimekuwa ,  amri  ya  kutouza  nyumba  ya  mkopo  haikatiwi  rufaa.


MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

MALINZI AFUNGA KOZI YA WAAMUZI WA FIFA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo amefunga kozi ya waamuzi chipukizi wasiokuwa na beji za FIFA katika hoteli ya Holiday, ambapo jumla ya waamuzi 30 kutoka nchi 28 barani Afrika walihudhuria.
Akiongea wakati wa kufunga kozi hiyo Malinzi alitoa wito kwa wahitimu wajikite kwenye maadili kwa kuzingatia mafunzo waliyopata ili katika kipindi kifupi wote wapate beji za FIFA na waonekane kweye mashindano makubwa kama fainali za AFCON na mashindano ya Kombe la Dunia.
Kabla ya Hotuba ya Mgeni rasmi mwakilishi wa CAF Eddy aliishukuru TFF kwa maandalizi mazuri na usimamizi bora kwa kipindi chore cha kozi hii, na kuahidi kuleta kozi nyingine kubwa hapa nchini.
Naye mwakilishi wa FIFA Carlos Hendrique alitoa shukurani zake za dhati kwa TFF kwa kuwa tayari wakati wote kushirikiana na FIFA hali ambayo imefanyika TFF iaminike na itegemewe na FIFA kweye program mbalimbali
Kozi hiyo ya waamuzi imefanyika kwa mara ya kwanza hapa barani Afrika.
FIFA iliiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa kozi hii kwa nchi zinazo zungumza kiingereza. Kwa upande wa nchi zinazo zungumza kifaransa kozi ya aina hii imefanyika nchini Morocco

Washiriki 30 kutoka nchi 28 barani Afrika wamehudhuria kozi hii ilivyokuwa itafundishwa na Wakufunzi wa Sita kutoka CAF na FIFA.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images