Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA AENDELEA NA KAMPENI ZAKE MKOANI LINDI

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo lake hilo, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakimshangilia Mgombea Ubunge wao, Salum Barwany, alipokuwa akihutubia na kukonga nyoyo zao kwa kugusa moja kwa moja changamoto zinazowakabili na namna watakavyoweza kuzitatua iwapo watapata ridhaa ya uongozi.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akifurahi jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany.
Uwanja wa Pilipili ulikuwa ni shangwe tupu, muda wote wa Mkutano.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Wananchi wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi wakionyesha furaha yao kwa ujio wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
Vinaja wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi wakiishangilia Chopa anayoitumia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, kawati ikiwasili kwenye eneo la Mkutano uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
Pipozzzzzzz........ Pawaaaaa......






Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
Wananchi wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi wakifatilia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
kadi za wanancha wa CCM zaidi ya elfu tatu (3000) wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi walioamua kuunga mkono mabadiliko ya UKAWA, zikiwekwa kwenye kiroba baada ya kukabidhiwa.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye wakionyesha kwa wananchi wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi, lundo la kadi za wanancha wa CCM zaidi ya elfu tatu (3000) walioamua kuunga mkono mabadiliko ya UKAWA, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, Mtama leo Septemba 23, 2015.







Umati wa Wananchi wa Lindi Mjini, wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili, Mkoani Lindi leo Septemba 23, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, LINDI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akimueleza Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, changamoto mbalimbali za wananchi wa Lindi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.

CHAMA CHA ACT WAZALENDO WAKUBALI MATOKEO YA UTAFITI WA TWAWEZA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa chama cha ACT Wazalendo, Nixon Tugara akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya matokeo ya  utafiti wa Twaweza na nafasi ya Mgombea wa Urais wa chama cha (ACT)Wazalendo licha ya kuonesha hali hiyo sisi (ACT) wazalendo tunafarijika na matokeo ameyasema hayo katika mkutano huo uli0fanyika katika ukumbi wa makao makuu ya chama  hicho jijini Dar es Salaam  leo kulia ni Mjumbe wa kamati ya uchaguzi, Emmanuel Mvule.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa chama cha ACT Wazalendo, Nixon Tugara leo jijini Dar es Salam .(Picha na Emmanuel Massaka)

TATHIMINI YA KUSOMA KISWAHILI, KIINGEREZA NA KUFANYA HESABU KUFANYIKA WILAYANI TARIME.

$
0
0
Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya ufadhiri wa Taasisi ya TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao umelenga kufanya kazi ya kutathimini hali ya kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda linatarajia kufanya tathimini kwa watoto (Wanafunzi na wasio wanafunzi) walio na umri kati ya miaka saba hadi 16 katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kwa lengo la kubaini hali ya kielimu na changamoto zake ilivyo wilayani humo.

Na:Binagi Media Group
Ili kufanikisha zoezi hilo, SHIMATA imetoa semina kwa wahojaji watakaofanya tathimini hiyo ambayo pia itawafikia wenyeviti wa Mitaa na Vijiji pamoja na Wanakaya pamoja na kupima kiwango cha madini joto katika kaya hizo.

Akifunga semina hiyo iliyoanza juzi Septemba 22,2015 na kutamatika jana Septemba 23,2015 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka washiriki wa semina hiyo (wahojaji) kuhakikisha wanafanya tathimini hiyo kwa ukweli na uwazi ili kupata majibu sahihi ya kiwango cha elimu katika Wilaya hiyo.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa
Mwenyekiti wa SHIMATA Joseph Magabe akizungumza katika semina hiyo.

Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina

Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Mratibu wa Twaweza Wilayani Tarime akipokea Cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
Mwenyekiti wa SHIMATA akipokea cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi
Viongozi na Wajumbe wa SHIMATA

MAGUFULI APIGWA NA BUTWAA NYOMI LA GEITA, AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

$
0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mgombea Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu, moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.

Magufuli ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya  kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha  kiwango cha  ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.

Dkt. Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania. 
Wananchi wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Kalangalala,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
 Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka. 
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea  mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
 Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.


CCM WAKUBALI MDAHARO WA WAGOMBEA URAIS JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauli Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya (CCM) January Makamba akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kufanya mambo mapya  yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaaam katika ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM.
Wanahabari wakimsikilaza Mjumbe wa Halmashauli Kuu ya Taifa na ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya (CCM) January Makamba leo katika Ofisi ndogo ya chama cha mapinduzi  jijini Dar es Salam.
(Picha na Emmanuel Mssaka)

TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.
Mwenendo wa Kampeni
Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni. Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.
Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya.
Midahalo ya Wagombea
Tumeshangazwa na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania kwamba CCM haijathibitisha kushiriki mdahalo. CCM ilipokea mwaliko wa MCT na kuijibu kwa barua ya tarehe 13 Septemba 2015 yenye kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 iliyosainiwa na Ndugu Stephen Msami, Msaidizi wa Katibu Mkuu. Barua hiyo ilipelekwa na kupokelewa kwa dispatch ambayo nakala yake tunayo. Baada ya hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba ili kutaka kujua zaidi na kutoa maoni ya CCM kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo. Katika kikao hicho, ambapo MCT iliwakilishwa na Afisa wake, Ndugu Allan Lawa, pamoja na Ndugu Tido Mhando, CCM ilithibitisha tena kushiriki mdahalo. Tatu, tarehe 16 Septemba 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo. Kauli ya Ndugu Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kuthibitisha kushiriki. Kwa msingi huu, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo, (kama vile CEO Roundtable, UDASA, Twaweza) ili kuiondolea uwezo taasisi moja, au kikundi cha watu wachache, kuhodhi na kuwa na ukiritimba kwenye jambo hili kubwa na muhimu.
CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:
1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais

2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.
3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki.

Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.
Utafiti wa TWAWEZA
CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:
1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.
2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.
3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.
4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.
5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.
Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi.
Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi.
Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu. CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.
Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki.
Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61. Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate.
Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.
Imetolewa na:
January Makamba

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
23.09.2015
BONYEZA HAPA KUSOMA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
   
CHAMA CHA MAPINDUZI
Sanduku La Posta: 50047
Dar Es Salaam, Tanzania
You received this email as part of our network.

MAGUFULI ALIVYOTIKISA MJI WA GEITA LEO.

President Kikwete meets the US Deputy Secretary of State Antony Blinken

$
0
0
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the U.S. Deputy Secretary of State Antony Blinken in Washington D.C. this morning and held bilateral talks on cementing further diplomatic and economic cooperation between the two countries. President Kikwete is in the US for a working visit whereby among other things he is expected to address the 70th session of the UN General Assembly in New York Photos by Freddy Maro

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA IDD EL HAJI KWA MAKUNDI MBALIMBALI

$
0
0

 Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Mwakilishi wa Mahabusu ya Watoto Upanga, Regina Kuname msaada wa vyakula na kitoweo cha mbuzi na mafuta ya kula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya ya Idd El Haji Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Chama cha kulea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza, Hassan Hamisi kwa ajili ya sherehe hiyo.
 Mbuzi wakiingizwa kwenye gari baada ya wahusika kukabidhiwa.
 Vyakula vilivyotolewa na Rais Jakaya Kikwete vikiwa eneo la tukio vikisubiri kuchukuliwa.

Mwakilishi wa Kituo cha Wazee na Wasiojiweza cha Nunge kilichopo Kigamboni, David Mpangala akiwa na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya kituo hicho.


Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya vyakula na kitoweo kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji ambayo inaadhimishwa duniani kote leo.

Zawadi hiyo imekabidhiwa kwa makundi hayo kwa niaba yake na Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo Dar es Salaam leo asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Fungamo alisema Rais ametoa zawadi hiyo kwa ajili ya Sikukuu ya Idd El Haji kama anavyofanya siku zote wakati wa sikukuu mbalimbali.

Fungamo alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni Mahabusu ya Watoto ya Upanga iliyopo Manispaa ya Ilala, Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nunge, Kigamboni, Chuo cha Watu wenye Ulemavu cha Yombo Temeke na Kituo cha Kulelea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza.

Alitaja vituo vingine kuwa ni Kituo cha Makao ya Watoto Yatima cha Mburahati, Ilala, Kituo cha Makao ya Watoto-Kurasini, Kituo cha Full Gospel, Temeke na Kituo cha Watoto Alsaad Children House Kurasini.

Alivitaja vituo vingine kuwa ni cha Vosa Mission cha Kongowe, Temeke na Kituo cha Kijiji cha Furaha kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Fungamo alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo ya Idd El Haji kwa upande wa Zanzibar kuwa ni Kituo cha Mabaoni kilichopo Pemba na Makazi ya Wazee Sebleni yaliyopo Unguja.


Alitaja vituo vingine vilivyopo mikoani vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni kituo cha The Village of Home cha Dodoma, kituo cha Moyo Mmoja cha Bagamoyo mkoani Pwani, kituo cha watoto cha Tosamaganga kilichopo mkoani Iringa na Mahabusu ya Watoto Arusha na Tanga.





Benki ya Dunia yaridhishwa na Mafanikio Mradi wa SMMRP

$
0
0
 Mchimbaji  Mdogo wa Madini kutoka kapuni ya Kidee Mining T. Ltd, Arusha, Allan Mkilatu ambaye ni moja wa wachimbaji  waliyenufaika na Utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mradi wa SMMRP kwa kupatiwa vifaa kwa ajili ya shughuli za uchimbaji akizungumza jambo wakati wa warsha ya ufunguzi wa Awamu ya Pili ya Mradi wa SMMRP.
 Kaimu  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia), akibadilishana mawazo na Mwakilishi na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP , Benki ya Dunia, Mamadou Barry (katikati) na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje wakati wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP, Awamu ya Kwanza.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Washiriki wa warsha ya Ufunguzi wa Mradi wa SMMRP, katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo. Waliokaa kutoka kulia ni  Meneja wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Katala, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Mwakilishi wa Benki ya Dunia na kiongozi wa mradi wa SMMRP, wa Benki hiyo, Mamadou Barry na mwakilishi kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).
 Sehemu ya Washiriki wa warsha ya Ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu wa Pili wakifuatilia jambo wakati wa warsha hiyo. Washiriki hao wamejumuisha Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wawakilishi wa Benki ya Dunia, Makamishna wa Madini wa Kanda, Maafisa Baadhi ya Wakaazi wa Madini, Makatibu Tawala wa Wilaya za Chunya, Geita, Kahama na Mlale na Wachimbaji Wadogo , Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), na Shirika la Madini la Taifa  (STAMICO).


 Mwakilishi na Kiongozi wa Mradi wa SMMRP  Benki ya Dunia, Mamadou Barry, akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya ufunguzi wa Mradi wa SMMRP Awamu ya Pili. Wanaomsikiliza ni baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini walioshiriki warsha hiyo.
 Meneja Mradi wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Katala akijadiliana jambo na baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya za Kahama, Geita, Chunya na Mlale wakati wa warsha ya kufungua Mradi wa SMMRP Awamu ya Pili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jilojia Tanzania (GST), Professa Abdrulkarim Mruma, akieleza jambo namna Taasisi hiyo ilivyonufaika na utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mradi na namna ilivyojipanga kutekeleza Awamu ya Pili ya Mradi huo. Wengine wanaomsikiliza kutoka kushoto ni Meneja Mradi wa SMMRP, Mhandisi Idrisa Katala, Kiongozi wa Mradi wa SMMRP, Benki ya Dunia  , Mamaduou Barry, na Mujumbe  katikakikosi cha Mradi wa SMMRP, Benki ya Dunia , Rachel Perk

BABA MTAKATIFU FRANSIC ZIARANI MAREKANI

$
0
0
Na Muandishi wetu Swahilivilla.Blog
Baba Mtakatifu Francis jana aliwasili nchini Marekani kuanza ziara ya kwanza kuwahi kuifanya nchini humo maishani mwake.
Pope Francis is scheduled to address Americans on the front lawn of the White House on Wednesday. Pictured above on Tuesday at the airport, being welcomed to the U.S. by President Obama  and his family
Baba Mtakatifu Papa Francis akiwa katika mapokezi chini ya  Rais Obama na familia yakeKwa kawaida marais wa Marekani huwapokea wageni rasmi Ikulu ya nchi hiyo, lakini alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kijeshi wa Andrews ulioko nje kidogo ya jiji la Washington, Baba Mtakatifu alipata heshima ya kulakiwa na Rais Obama na familia yake.
Mbali na gwaride la heshima, miongoni mwa waliokuweko kwenye mapokezi hayo rasmi ni pamoja na Makamo wa Rais wa Marekani Bwana Joe Biden na aila yake, watoto wa shule, na viongozi wa Kanisa Katoliki.Akiwa jijini Washington, Baba Francis atafanya mazungumzo na Rais Obama, kukhutubia kikao cha pamoja cha Mabaraza ya Bunge la Marekani pamoja na kuongoza Ibada mbalimbali.Ziara yake hiyo ya siku sita, pia itamfikisha kwenye miji ya New York na Philladelphia.
Akiwa jijini New York, Baba Francis ambaye ni kiongozi wa nne wa Vatican kuitembelea Marekani, atatembelea Umoja Wa Mataifa na eneo la Kituo Cha Biashara kiclichoteketezwa kwenye mashamulizi ya Septemba 11, 2001.
Kiongozi huyo wa Kanisa la Katoliki, atamalizia ziara yake katika jiji la Philladelphia, ambako anatarajiwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Familia wa Wakatoliki Duniani. 
Miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele katika mzungumzo na khotuba zake nchini humu, ni pamoja na utoaji mimba, ndoa za jinsia moja, usawa katika maswala ya kiuchumi na kijamii, mazingira na uhamiaji.
Baba Francis amewasili Marekani akitokea Cuba baada ya kukamilisha ziara yake nchini humo.
Wachambuzi wanaona kuwa kuanza ziara yake nchini Marekani akitokea nchini Cuba, kunatoa ujumbe fulani kukhuasian na kuanza tena kwa mahusiano ya Kibalozi kati ya Marekani na Cuba baada ya kuvunjika kwa muda usipungua nusu karne.
Aidha kuingia Marekani akitokea Cuba kunatoa ishara juu ya mgogoro wa wakimbizi wanaoingia Marekani wakitokea nchi za Amerika ya Kusini.
Kwa upande mwengine, ziara hiyo inakuja katika wakati ambao Kanisa Katoliki limekuwa likikabiliwa na kashfa za ngono katika miaka ya hivi karibuni.
Aidha, inakuja katika wakati ambao harakati za ndoa za jinsia moja zikiwa zimepamba moto nchini Marekani.Maswala hayo pia yamekuwa yakichukua nafasi za mbele katika kampeni za wagombea urais wa Marekani ambazo tayari zimeshamiri nchini humu.
Mbali na baraka inazotarajiwa kuletwa na Baba Mtakatifu chini humu, ziara hiyo pia itakuwa na athari zake za kiuchumi kutokana na usalama wa hali ya juu utakaokuwepo wkati wa ziara hiyo.Baadhi ya mashirika ya utumaji vifurushi na mizigo kama vile UPS na Fedex, tayari yametangaza kutotoa huduma katika baadhi ya maeneo ambayo Baba Francis atatembelea.

DKT FENELA MUKANGARA AAHIDI KUWAINUA KIUCHUMI WANANCHI WA KIBAMBA

$
0
0
Dkt Fenela Mukangara akizungumza na wana saccos wa kata ya Msigani

Sehemu ya akina mama wa Msigani wakimsikiliza Dkt Fenela Mukangara

Dkt Fenela Mukangara akiagana na akina mama wa kata ya Msigani Kibamba baada ya kuisha mkutano huo.

VUGUVUGU LA AJENDA YA WATOTO NA UCHAGUZI MKUU LAENDELEA KIBAHA

$
0
0
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Simbani, Akram-Shabani,akizungumza katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani jana.
 Baadhi ya wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani  waliohudhuria mdahalo huo.
Mratibu wa mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya mtoto kutoka Plan International, Jastin Moses akizungumza  katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani jana.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani, Ombeni Ally akizungumza  katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani jana.


JAMII imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa dhidi ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo imetolewa na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Kibaha vijijini kupitia ACT Wazalendo Dk. Rose Mkonyi alisema kuwa chama chake kinaangalia ni kwa namna gani watazingatia katika Lishe bora ya mtoto pamoja na namna gani mtoto atainuliwa Kielimu.

 Aidha Mgombea Udiwani wa kata ya maili moja kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Ramadhani Lutambi alisema chama chake kitaangalia zaidi afya ya mtoto na kuhakikisha Bohari ya dawa inakuwa na dawa za kutosha.

Hata hivyo, Watoto waliohudhuria mdahalo huo waliwataka wagombea kutimiza ahadi wanazotoa wakati wa Kampeni ili na wao waweze kufikia malengo yao. 

Watoto walipendekeza serikali ijayo iangalie namna ya kuwalinda hasa wanapoelekea mashuleni kwani wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda na kurudi shule ambako wamekuwa wakipata madhara na vishawishi vingi wanapokuwa njiani. 

Aidha watoto pia waligusia suala la rushwa na kwa namna gani linavyorudisha nyuma maendeleo yao na kuwaomba wagombea wa ngazi zote katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa waadilifu ili watoto wapate haki zao.

Mdahalo huo ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wakishirikiana na UNICEF uligusa maeneo kumi muhimu ya uwekezaji kwa watoto ikiwemo kuwekeza kuokoa maisha ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora, kuwekeza kwenye usafi, udhibiti wa miundombinu ya maji taka na ugavi wa maji katika shule na kwenye huduma za afya pamoja na kuwekeza katika kumwendeleza mtoto akiwa bado mdogo.
Mengine ni pamoja na kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote, kuwekeza katika kuzifanya shule kuwa mahali pa usalama, kuwekeza katika kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika kupunguza mimba za utotoni, kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu, udhalilishaji na unyonyaji pamoja na kuwekeza kwa watoto wenye ulemavu. 

Vuguvugu hili la kusambaza ajenda ya watoto kupitia midahalo na wagombea wa nafasi mbalimbali linaendelea kupita mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwani tunaamini kuwekeza katika maeneo haya ya kipaumbele kunaweza kupunguza umasikini na kuwezesha kuwepo kwa taifa linalostawi na la usawa.

Unaweza kusikiliza kipindi cha redio cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org nawww.facebook.com/WalindeWatoto

Article 4

$
0
0
MILESTONE TOWARDS TANZANIA NEW CRVS SYSTEM


Veronica Kazimoto,

Dar es Salaam,



The Government of Tanzania through the Ministry Constitution and Legal Affairs together with the National Bureau of Statistics (NBS) and Registration Insolvency Trusteeship Agency (RITA) has conducted a Stakeholders Consultative Meeting on the Civil Registration and Vital statistics (CRVS) Strategy held on 22 September, 2015 in Dar es Salaam.


Speaking during the official opening of the above meeting, the Permanent Secretary, Ministry of Constitutional and Legal Affairs Ms. Maimuna Tarishi said Civil Registration plays a vital role in governance and economic development of nations where in Tanzania, it is mandatory for evidence-based development and transformation of the society which is in line with the goals of the National Strategy for Growth and Reduction of Poverty II (NSGRP II) or MKUKUTA II.


Ms. Tarishi said that the Civil Registration and Vital statistics System in Tanzania Mainland has been functioning poorly.“According to the Population and Housing Census Report of 2012, only 13.4 percent of its citizens registered hence leaving many unrecognised administratively anywhere,” She said.


She added that Death registration rate is almost negligible and causes-of-death are either wrongly reported or not reported at all making health interventions difficult. Marriages and divorces’ records are also very poor or non-existent in many cases.


Thus this Strategy is developed to overcome internal weaknesses and external threats observed as well as to maximise internal strengths and external opportunities from the assessment.


On her part, the Director General of National Bureau of Statistics (NBS) Dr. Albina Chuwa has said the major objective of the CRVS System is to establish a permanent, continuous, compulsory and universal vital events registration and vital statistics system with the view to achieving four identified outcomes by 2020/21.


These outcomes are legal rights and privileges to all; good governance and accountability; efficient CR institutional capacity; and trusted statistics.


“The overall goal of the CRVS System is to make the process simple, user-friendly, less costly and to achieve a one-stop shop at all service points which are designated health facilities, District Executive Director Offices and Ward Executive Officer offices,” she noted.


On the other hand, the acting Chief Executive Officer of Registration Insolvency Trusteeship Agency (RITA) Ms. Emmy Hudson has said that according to the current Civil Registration system, the lowest service point is at District level which to many is distance from where they live.


This and other reasons poses a challenge to many causing the service not to be easy accessible thus this situation calls for changes to the current system and RITA alone cannot be able to meet these challenges without joining forces with others hence the ongoing improvements.


The history of Civil Registration dates back in 1917 when the German Colonial power enacted a law for registration of births and deaths (Proclamation No.15 of 1917 (Civil Area).


When the British took over the administration of Tanganyika from the Germans they retained the Register of Births and Deaths established under the Germans law by saving it under the Births and Deaths Registration Ordinance, 1920 (Cap.108).


Under both colonial powers, registration of births and deaths was not compulsory for Africans. After independence, the Government took over the registration role with the existing systems which had several shortfalls with most of its population continuing being unregistered.


MKURUGENZI KINGA NA ELIMU YA AFYA ZANZIBAR ATOA TAHADHARI JUU YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.

$
0
0
Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya Dkt. Mohd Dahoma akizungumza na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Wizara ya Afya juu tahadhari ya ukonjwa wa Kipindupindu hivyo amewashauri wananchi kununua chakula kilicho hifadhiwa vizuri ama chakula kimoto na kujiepusha kutumia juice zinazotengenezwa kienyeji. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar  .
  
Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya  vyakula na vinywaji  katika viwanja vya sikuu inayoanza kesho kutokana na tishio la maradhi ya kuharisha na kutapika ambayo yameanza kujitokeza  katika nchi jirani.

Akizungumza na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Wizara ya Afya, Mnazimmoja, Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya  Dkt. Mohd Dahoma amewashauri wananchi kununua chakula kilicho hifadhiwa vizuri ama chakula kimoto na kujiepusha kutumia juice zinazotengenezwa kienyeji.

Dkt. Dahoma amesema katika viwanja vya  sikukuu kunakuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu na biashara ya vyakula na vinywaji vinakuwa vingi hivyo ameshauri watu wawe waangalifu chakula cha kununua.“Chakula baridi na Juice zilizotengenezwa kwa njia za kienyeji sio busara kuzitumia katika kipindi hiki kwani hakuna uhakika wa maji yaliyotumiwa kutengeneza bidhaa hizo.”alisisitiza Dkt Dahoma.

Amewashauri wananchi kuwasimamia watoto wao wanapotaka kununua chakula katika viwanja vya sikukuu na wahakikishe chakula watakachonunua kiwe kilichohifadhiwa vizuri na kipo katika hali ya moto.

Amesema wamekuwa wakitoa elimu kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara juu ya kuchemsha maji na kujiepusha kununua chakula kilichowazi lakini bado baadhi ya wananchi wamekuwa hawatilii maanani suala hilo.

Katika kukabiliana na maradha ya kuharisha na kutapika, Dkt. Dahoma amesema wanaendelea kutoa taaluma kwa kamati za Afya za shehia na kutoa vifaa vya kutunzia usafi  kwa kamati hizo

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA (DAWASA) MNADA WA HADHARA:

$
0
0
 UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na DAWASA  watauza Magari, Photocopy mashine, na Furniture za ofisi kama zilivyoorodheshwa hapo chini kwa mnada wa hadhara  tarehe 26, September, 2015  Jumamosi saa 4.00 asubuhi. Mnada utafanyika  DAWASA makao makuu  jirani na Hospitali ya Mwananyamala .

MALI ZITAKOZOUZWA: Meza za ofisi, Viti, Book case, Cupboard, File cabinets, 
6 Photocopy m/c {Canon /Sharp} , Computer set, Printer, Scanner, A/c split unit & Window type na grili za milango nakadhalika.

MAGARI YATAKAYOUZWA:
Idadi
Muundo
Aina YA Engine
Mwaka
Ushuru
1
Toyota Hilux  D/Cabin
5L      Diesel engine
2009
Haujalipwa
1
Nissan Patrol S/Wagon
Z30    Diesel  engine
2004
Haujalipwa
2
Mitsubish P/Up double cabin  L200
4D56  Diesel engine
2005
Haujalipwa

Mali zote zinaweza kukaguliwa DAWASA jirani na Mwananyamala Hospital,  tarehe 23 mpaka 25 November,  2015 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.

MASHARTI YA MNADA:
  1. Mnunuzi atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 7 ukishindwa kulipa kwa muda huo mali itauzwa tena na dhamana haitarudishwa.
  2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo.
  3. Mnunuzi atatakiwa kuondoa mali baada ya kulipia malipo yote
       4    Ni wajibu wa Mnunuzi wa Magari kulipa Kodi zote

Kwa maelezo zaidi waone:

UNIVERSAL AUCTION CENTRE

NKRUMAH STREET MKABALA NA CO-CABS
SIMU NA:  0754-284 926, 0757 284 926               
Email : universalauction@hotamail.com
DAR ES SALAAM.

JK AWAPA ZAWADI YA IDD MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA

$
0
0
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda(wa pili kulia)kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi za Idd el Hajj Meneja wa Mahabusu ya Watoto mkoa wa Arusha,Mussa Mapua leo kwa ajili ya kusherekea siku kuu hiyo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ametoa zawadi mbalimbali katika Mahabusu ya watoto walikinzana na sheria iliyopo jijini Arusha
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kikwete,Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda amesema pamoja na kuwa watoto hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujibu lakini mheshimiwa Rais anatambua haki zao za kushiriki na jamii kufurahia siku kuu hiyo ya kidini.
"Kama mnavyofahamu Rais Kikwete amekua na utamaduni wa kuwakumbuka katika siku kama hizi ili nanyi mfurahie siku kuu hii,"alisema Mapunda.
Akipokea zawadi hizo Meneja wa Mahabusu hiyo,Mussa Mapua amesema imekua ni faraja kwa kiongozi wa nchi kuwakumbuka na kuomba taasisi nyingine na watu binafsi kuiga mfano huo na kumtakia Rais Kikwete mapumziko mema anapojiandaa kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake.

MAGUFULI ALIVYOUNGURUMA MJINI GEITA

SWALA YA IDD EL HAJI ILIVYOFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya Idd El Haji katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Waislam wa Tanzania leo waliungana na wenzao duniani kote kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji.
 Sheikh Nurudin Kishki alitohotuba baada ya swala hiyo.
 Sheikh  Othman Dishi akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika swala.
 Wanawake na watoto wakiwa kwenye swala hiyo.
 Mazuria ya kuswalia yakitandikwa kabla ya kuanza ibada.
 Hapa wakitawaza kabla ya kuinza kwa swala hiyo.
Abdurahi Suleiman (kulia), akiuza mafuta na manukato mbalimbali katika viwanja hivyo.
 Ibada ya swala ya Idd El Haji ikiendelea.
 Biashara ya Balaghashia ikiendelea katika viwanja vyao.
 Swala ikiendelea katika viwanja hivyo.
 Pikipiki na baiskeli zikiwa zimewekwa kwa pamoja kwa ajili ya usalama.
 Mwanahabari akichukua picha katika ibada hiyo.
 Waumini wa kiislam wakiwa katika viwanja hivyo wakati wa ibada hiyo.
 Hapa salamu zikiendelea.
 Sheikh Othmani Dishi (kushoto), akisalimiana na Sheikh Abdu Kadri kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
 Swala ikifanyika katika viwanja hivyo.
 Swala ikifanyika kwa unyenyekevu mkubwa.
Swala ikiendelea.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

WAIMBAJI NYIMBO ZA INJILI WAAOMBA WATANZANIA KUJITOKEZA KATIKA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI

$
0
0
 Mwimbaji  wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ofisi za  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha kuombea amani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama  kuhusiana na kushiriki katika tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. Kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu akizungumza leo jijini Dar es Salaam jinsi tamasha la kuombea Amani ambapo wasanii hao watakavyo tumbuiza katika tamasha hilolitakalofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa taifa. Mwimbaji  wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) naMwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira. 
Kutoka kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili  Mathar Mwaipaja akizungumza na waandishi wa habari kuwa watu wote wajitokeze katika Tamasha hilo la kuombea amani na kuwa viingilio vyake kuwa sio vikubwa sana kwa watu wazima ni shilingi elfu tatu na watoto shilingi elfu moja pamoja na VIP  ni shilingi elfu tano.
Baadhi ya waandishi waliohudhulia katika katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam leo.

WASANII wa nyimbo za Injili wajitokeza katika  kuzungumzia Tamasha  la kuombea amani litakalofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es  Salaam Oktoba 4 Mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema wamejiandaa vizuli katika ulinzi pamoja na vyombo vya mziki vitakavyo tumika kutumbuizia siku hiyo.

Pia amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moja la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais," alisema Msama.

BARAZA LA EID EL HAJJ CHUO CHA AMALI MKOKOTONI

$
0
0
Msafara wa Gari za  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein zikiongozwa na mapikipiki wakati ukiwasili katika Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskzani A Mkoa wa kaskazini Unguja palipofanyika mkutano wa baraza la Eid EL Hajj leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa katiba na Sheria Mhe,Abubar Khamis Bakary mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo kabla ya kukagua gwaride rasmi la Sherehe hizo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya Gwaride la KIKOSI cha Polisi FFU mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo (kushoto)Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi katika ukumbi wa  Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo
 Mke wa Makamo wa Pili wa rais wa zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (mwenye miwani) pamoja na Viongozi wengine mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa  Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi katika baraza hilo akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya Viongozi wengine na Wazee na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Zanzibar katika Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini  Unguja ikiwa ni katika sherehe za Sikukuu ya Eid El Hajj,[Picha na Ikulu.] 
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images