Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 649 | 650 | (Page 651) | 652 | 653 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia), Bw. Clement Mshana pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili (wa pili kulia) wakifurahia zawadi za vitambaa vilivyonakshiwa na wabunifu wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
   Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago kilichochongwa na wasanii wa Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
   Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (katikati) akifurahia jambo na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana (kulia), akikabidhiwa zawadi ya kinyago.
   Hapa ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
  Waigizaji wa filamu ya’The Young Doctor’ Zhang Yi na Zhou Fang wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.

  Na Dotto Mwaibale

  KAMPUNI ya StarTimes Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga ya Beijing wamezindua maonyesho ya mfululizo wa filamu na tamthiliya mwaka 2015 ambayo yatajumuisha filamu na tamthiliya za kusisimua za kichina barani Afrika.

  Kuendelea kwa kukua kwa muingiliano wa tamaduni baina ya watu wa Tanzania na China kumefanya filamu na tamthiliya za China kwenye luninga zijizolee umaarufu mkubwa na kuwa kichocheo kikubwa katika kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili amebainisha kuwa Tanzania itabaki kuwa mshirika wake mkubwa na wataendelea kuimarisha mahusiano yao ya kitamaduni kupitia matangazo ya maudhui ambayo yana nafasi ya kipekee kuwafikia watu wengi zaidi.

  ”Maonyesho haya ambayo kwa kawaida yatakuwa ni ya filamu na tamthiliya kutoka Beijing kwa kiasi kikubwa yataonyeshwa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa makadirio, jumla ya filamu na tamthiliya 30 za kwenye luninga zitaonyeshwa nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Dhumuni kuu ni kuimarisha muunganiko wa maingiliano ya kiutamaduni baina ya marafiki zetu wa Afrika na watu wa China.” Alisema Bi. Peili

  Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga itatoa fursa ya kipekee kwa watazamaji wa barani Afrika kama vile Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini kukutana na washiriki maarufu wa filamu ya ‘The Young Doctor’. Pia wakurugenzi wa mamlaka hiyo watakuwa na wasaa wa kuzungumza na kuyahoji makampuni ya kimataifa ya uzalishaji wa vipindi barani Afrika kwa nchi hizo tatu.

  Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ukuaji wa kasi wa tasnia ya filamu na tamthiliya kwenye luninga na kunufaisha maisha ya watu huku masoko ya tasnia hizo kwa nyumbani yakijulikana kimataifa na kuwa kiungo muhimu katika kukuza muingiliano wa kiutamaduni baina ya nchi husika.

  Kama sehemu ya chombo cha uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015, sherehe za uzinduzi zitafanyika nchini Afrika ya Kusini ambapo zitahudhuriwa na mamlaka ya bodi hiyo ya Beijing.

  “Maonyesho haya yanafuatilia tukio kama hili ambalo lilifanyika mwaka jana na kuandaliwa na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga ambapo Mr. Guo Jinlong,  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mamlaka ya Kisiasa ya CPC na Katibu wa Kamati ya Mamlaka ya Beijing alihudhuria sherehe ya aina yake alipotembelea nchini Tanzania,” alisema Bi. Peili na kumalizia, “Tamthiliya hizi za Kiingereza za kwenye luninga kama zinavyojulikana miongoni mwa watazamaji wengi zimejizolea umaarufu mkubwa burudani inayopendwa katika nchi nyingi za kiafrika na tunaamini kwa pamoja tunaweza kuziunga mkono tasnia za uzalishaji wa vipindi za nyumbani katika nchi husika ili kuweza kunufaika zaidi kwa pande zote mbili.”

  Uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015 utajumuisha vipindi vya luninga maarufu na filamu kama vile ‘The Young Doctor’, ‘The Sweet Burden’, ‘The Mi Family’s Marriage’, ‘Ordinary World’, ‘Love is Not Blind’, ’20 Once Again’, ‘A Wedding Invitation’, na ‘The Left Ear’ambazo zimepangwa kuonyeshwa nchini Tanzania ndani ya kipindi cha mwaka mzima.

  Shughuli za kukuza maonyesho haya katika nchi zingine za barani Afrika zikiwemo Kenya na Afrika ya Kusini zitafuatia kulingana na kampuni ya matangazo ya dijitali ya StarTimes ambayo ina mpango wa kuzionyesha kupitia katika ving’amuzi vyao vya antenna na madishi, na kwa uhakika itasaidia kwa kiasi kikubwa itasaidia kukuza utamaduni wa China barani Afrika. 
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0

  Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower( kushoto) akiendelea kutoa burudani ya nguvu huku msanii mwenzake Sony Masamba akiendelea kuzirundi ngoma ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar. Usikose leo siku ya Jumatano kwenye mkesha wa EID maana kuna vitu vingi vipya.
  Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha pamoja na mwenzake Kasongo Junior haya ni Majembe mapya ya bend ya Skylight yenye uwezo mkubwa wa katika uimbaji.
  Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake.
  Sam Mapenzi pamoja (kulia) akiimba pamoja na Ashura Kitenge wakiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band waliofika siku ya Jumapili kwenye kiota cha Escape One Mikocheni na leo sio ya kukosa njoo tukeshe pamoja tukifurahi na mziki mzuri kutoka katika bendi hiyo.
  Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower  akiimba huku mashabiki wa bendi hiyo wakiserebuka kwa furaha na leo sio ya kukosa njoo na mwenzako uje kuona vitu vipya kutka kwenye bendi hiyo.
  Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha akiendelea kutuoa burudani kwa mashabiki wao waliofika kwenye kiwanja cha Escape One kujionea burudani ya nguvu kutoka katika bendi hiyo.
  Msanii wa Bendi ya Skylight, Sony Masamba akiwafundisha mashabiki wao style mpya ya kucheza nyimbo za Bendi ya Skylight.
  Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (katikati) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Jumapili iliyopita katika kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
  Msanii wa Bendi ya Skylight  Ashura Kitenge akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki i wa bendi hiyo(hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar kwa kuburudika na band hii.
  Ilifika time ya Nigeria Flavour Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kushoto) pamoja na Sony Masamba.
  Ilikuwa noma sana siku ya Jumapili iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo Jumatano kwenye mkesha wa EID uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
  Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka
  Skylight Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane jumatano hii ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar kwa kuburudika na band hii.
  Mashabiki wa Bend ya Skylight wakiendelea kuserebuka na waimbaji wa bendi hiyo.
  Sakata rhumba na Skylight band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase leo kwenye mkesha wa EID njoo wewe na rafiki yako
  Mashabiki wakiendelea kuserebuka nyimbo za Skylight.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akutana na wananchi wa Dar es salaam na kupokea malalamiko ya migogoro inayohusu ardhi katika mkoa wa Dar es salaam tarehe 22 na 23, septemba, 2015 kuanzia saa 4.00 asubuhi makao makuu ya Wizara hiyo. 
  Katika siku ya jana tarehe 22 septemba 2015 Mhe. Waziri amepokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Kinondoni na leo tarehe 23 septemba 2015 atapokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Temeke na Ilala.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa Dar es salaam waliokuja kuwasilisha malalamiko yao kuhusu migogoro ya ardhi, kulia ni naibu wake Mhe. Angela Kairuki na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Methew Nhonge, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt.  Selasie Mayunga na Kamishna wa Ardhi Tanzania Dkt. Moses Kusiluka.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  naibu wake Mhe. Angela Kairuki na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Methew Nhonge, wakipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam.
   Wananchi wa manispaa ya Kinondoni wakiwa katika mkutano huo.
   Wananchi wa manispaa ya Kinondoni wakiwa katika mkutano huo.
  Wananchi wa manispaa ya Kinondoni wakiwa katika mkutano huo.

  0 0

  IMG-20150919-WA068
  UBA Tanzania staff during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015.
  IMG_0311
  UBA Tanzania staffs participate engaged in  aerobics session during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015
  IMG_0330
  UBA Tanzania staffs participate in the aerobics session during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015.
  IMG_0358
  A cross section of UBA Tanzania staff in a group selfie  after the exercises during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,  Utamaduni na Michezo, Mama Sihaba Nkinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tanzania Media Foundation - Mfuko wa Habari Tanzania - TMF) uliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. Mfuko huu unachukua nafasi ya Tanzania Media Fund 
   Mwenyekiti wa Bodi ya TMF Mama Halima Shariff akitoa neno la shukurani baada ya bodi hiyo kuzinduliwa usiku wa kuamkia leo  katika ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. .
   Mkurugenzi wa TMF Bw. Ernest Sungura akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) uliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam
   Mkurugenzi wa TMF Bw. Ernest Sungura akimpongeza Mkurugenzi wa Shirika la habari la Daraja Bw. Simon Mkina wakati wakati uzinduzi huo wa Mfuko wa Habari Tanzania 
   Mrisho Mpoto akitumbwiza wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) iliyofanyika leo katika ukumbi wa Millenium Tower jijjini Dar Es Salaam.
   Wajumbe wapya wa Bodi  ya TMF katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana  Utamaduni na Michezo Mama Sihaba Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa Bodi ya TMF na  watendaji wa mfuko huo usiku wa kuamkia  leo katika ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. 
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii 

  0 0
 • 09/22/15--22:28: KIPINDI CHA JUKWAA LANGU
 • Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Septemba 21, 2015 ambapo mbali na waongozaji Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio, pia walikuwepo Georgina Lema, NY Ibra na Dr Temba toka New York.
  Kutoka Tanzania tuliungana na Richard Kasesela
  Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 21, 2015 ambapo mbali na waongozaji Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio, pia walikuwepo Georgina Lema, NY Ibra na Dr Temba toka New York. Kutoka Tanzania tuliungana na Blogger Mr Verbs wa www.habarika24.blogspot.com, pia kulikuwa na Dr Patrick Nhigula, Hajji Khamis na Emil Mutta na Kennedy

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser (Kushoto )Akimkabidhi Cheti Mshiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali Hafla iliyofanyika Katika Ukumbi wa Parokia ya Yombo Dovya, Temeke Yalio chini ya Taasisi "Sauti ya Mama na Mtoto.".Mama Shekha Nasser ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Shuguli hiyo Kutokana na Juhudi zake za Kupambana Kama mwanamke Mzalendo wa Kiafrika na Mtanzania Pekee anayemiliki Bidhaa yake ya Vipodozi Ijulukanayo Luv Touch Manjano.Pia anahangaika usiku na Mchana kuwasaidia Wanawake wengine wa Kitanzania Kuondokana na tatizo la Ajira na kuwawezesha wanawake Kudhubutu na Kujikita kwenye biashara hasa kwa Kutumia Vipodozi Ambapo Ameweza kusidia zaidi ya wanawake 30 Kwa kuanzisha Taasisi ya Manjanio Foundation.
       Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser Akiwa kwenye Picha pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya "Sauti ya Mama na Mtoto."Ndugu  David Mwandele wa Pili kutoka Kushoto,Pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi Hiyo..Shughuli ilikuwa ni kutoa vyeti kwa kina mama 50 waliopewa mafunzo ya ujasiriamali na taasisi hiyo  ili kuwejengea uwezo wanawake hao wanaoishi katika mazingira magumu ili kuona kwamba wanapata elimu ya kuwawezesha kujikimu na mahitaji yao msingi, yaani waweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa watoto wao, kwa kupitia elimu ya ujasiriamali waliopata.
   Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali wakimpokea kwa Furaha  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser kwenye Halfa hiyo. Easter Lukindo ni mwanamke aliye Dhubutu na kuanza Biashara kwa Kupitia Vipodozi vya Luv Touch Manjano chini ya Taasisi ya Manjano Foundation akizungumza Machache kwenye halfa hiyo ambapo aliwaasa washiriki wa Mafunzo hayo Kuacha woga na kujiamini kwamba nao wanaweza,Pia aliwataka Washiriki hao nkuanza Kuchangamkia Fursa zilizopo haraka mara baada ya Kupata elimu ya Ujasiriamali.Alitumia Muda huo Pia Kumshukuru Mama Shekha Nasse Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambayo imempa nafasi ya Yeye Kuongeza Kipato kwa  kujikita kwenye Biashara,
     
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali.

  0 0

   Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya shule ya msingi Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi.Zena Tenga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha mtoto kusoma akiwa kwenye moja ya chumba chenye madawati yaliyotolewa kwa shule ya msingi Mbuyuni na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust, (kulia) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere  (kushoto) wakikata utepe kuashirikia ufunguzi wa moja ya darasa la shule ya Msingi wa Mbuyuni lililowekewa madawati mapya ambayo yametolewa kwa shule hiyo na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust.
  Walimu wa shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.
   Wanafunzi wanaosoma katika shule ya awali katika shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.

  WATOTO wa shule ya awali ya Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamenufaika na msaada wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo na Mawasiliano ya Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni 10.Pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya kusomea kwa shule hiyo ambayo pia inatoa elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili.


  Msaada huo umetolewa kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust,nayo ya jijini Dar es Salaam ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuboresha mazingira ya watoto kusomea kwa kutoa misaada ya madawati na vifaa vya kusomea mashuleni ikiwemo vitabu na tangu ianzishwe tayari imetoa misaada kwa shule mbalimbali nchini.


  Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi Mbuyuni Meneja wa Mawasiliano na matangazo wa Aggrey&Clifford  Bw.Oliver Mutere alisema kuwa msaada huo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.


  “Kampuni yetu ambayo ina mtamdao katika ukanda wa Afrika Mashariki na ikiwa imeajiri wataalamu wa Nyanja mbalimbali inajua umuhimu wa elimu bora na ndio maana tumetoa msaada huu kuwawezesha watoto hawa wasome katika mazingira mazuri ili waje kuwa wataalamu wazuri katika siku zijazo na tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu nchini”.Alisema.


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi Hassan Maajar Trust   ZenaTenga, alisema ana imani kuwa msaada huu utawanufaisha wanafunzi wengi katika shule ya Mbuyuni watakaotumia madawati haya “Mazingira bora ya kusomea ni jambo la muhimu katika kuboresha elimu nchini na huwezi kuongelea elimu bora wakati watoto wanasoma wakiwa wamekaa sakafuni”.Alisema na kutoa wito kwa makampuni na taasisi zingine kulivalia njuga tatizo la upungufu wa madawati mashuleni na kulimaliza kabisa.


  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbuyuni Dorothy Malecela alishukuru kwa msaada huo ambaye shule yake imepata na alitoa wito kwa wafadhili wengine kuendelea kujitokeza kusaidia jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika ufanikishaji wa kutoa elimu bora.

  0 0

  PUBLIC NOTICE

  BASATA LATAKA KUONDOLEWA/KUSITISHWA MARA MOJA KUCHEZWA KWA NYIMBO ZOTE ZENYE KUKENGEUKA MAADILI, SHERIA NA TARATIBU

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawaagiza wasanii, wamiliki na waendeshaji wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari hususan radio na runinga kuondoa na kuacha mara moja kurusha au kutangaza au kucheza nyimbo zote zenye maudhui ya kashfa, matusi, kejeli, udhalilishaji ambazo zinahatarisha kuigawa jamii ya kitanzania katika misingi yoyote hasa katika kipindi hiki Taifa linapoendelea na kampeni za kisiasa na kujiandaa na uchaguzi mkuu.


  Kwa mujibu wa kifungu namba 118 (a-d) cha Sheria ya Bunge namba 9 ya Mawasiliano ya Mtandao ya mwaka 2010 ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza, kuzalisha, kusambaza au kutangaza ujumbe ambao una mlengo wa matusi, dharau, uzushi au jinai kwa lengo la kutukana, kutisha, kusumbua au kushusha hadhi ya mtu mwingine.


  Aidha, Sheria ya Bunge namba 4 ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 45 (1) (a-c) kinatoa mamlaka kwa taasisi au mtu yeyote anayebaini uvunjifu wa Sheria katika mitandao kutoa notisi kwa yeyote yule anayesambaza au kutangaza ujumbe au maudhui yanayovunja sheria za nchi kuacha mara moja au vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote anayekaidi.


  Ni kwa msingi huu, BASATA linawaagiza wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii kama sound cloud, U-Tube, ITunes nk. kuondoa ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya kwanza ya taarifa hii nyimbo zote zinazokengeuka maadili na kubeba mlengo wa matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na kitaifa.

  Aidha, BASATA linawakumbusha tena Wasanii wote nchini kuacha mara moja kubuni na kutengeneza kazi za Sanaa zenye kuashiria kuigawa jamii katika misingi yoyote ya kibaguzi na zaidi kutumia Sanaa kubomoa jamii badala ya kuijenga.


  BASATA linawasisitiza wamiliki wa vyombo vya habari hususan radio na runinga pia watangazaji na Ma DJs kuhakikisha hawawi chanzo cha kusambaza maudhui yoyote ya Sanaa yenye mlengo wa kuibua chuki, matusi, kashfa na mgawanyiko wa Taifa.


  BASATA kwa mamlaka yake chini ya Sheria namba 23 ya mwaka 1984 na yale ya Sheria ya Mawasiliano ya Posta na Mitandao ya mwaka 2010 na ile ya Makosa ya mitandao ya mwaka 2015 kwa kushirikiana na vyombo vya dola halitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kinidhamu kwa wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari ambavyo vitaendelea kutangaza na kusambaza nyimbo zenye mwelekeo wa kuhatarisha usalama, umoja na mshikamano wa Taifa.


  BASATA likiwa ni msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linatambua kwamba Sanaa ikitumiwa kwa ukengeufu inaweza kuwa chanzo kikuu cha machafuko, mivurugano na kupotea kwa amani nchini. Hivyo umakini unahitajika miongoni mwa wasanii katika kuzingatia weledi, maadili, uzalendo kwa taifa na kuitumia Sanaa kama chombo cha kujenga jamii yenye kuzingatia maadili. 

  SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI


  Godfrey L. Mngereza

  KATIBU MTENDAJI, BASATA 

  0 0

   Mkazi wa Wazo Hill, Tegeta Mary Joseph (Katikati) akipokea zawadi ya fulana toka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo, Mbezi na Tegeta Bw. Victor Mhindi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani iliyofanyika katika baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni redio E-fm, Gadner Habash.
   Mkazi wa Tegeta, Uwanja wa Upanga ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Max Richard akijiandaa kupokea zawadi ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika kiwanja cha baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo la kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo ya nchi nzima inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya.
  Mpenzi wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner Habash. 
    Mpenzi wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner Habash.
  Mkazi wa Tegeta, Uwanja wa Upanga ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Max Richard akijiandaa kupokea zawadi ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika kiwanja cha baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo la kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo ya nchi nzima inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima (kulia) akimsikiliza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi (kushoto) alipokuja kujitambulisha na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi  na Balozi mpya katika Idara hiyo ya Mashariki ya Kati. Katika mazungumzo yao waligusia masuala ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu.  
  Afisa Mambo ya Nje, Bw. Hangi Mgaka akisikiliza mazungumzo kati ya Balozi Kilima na Balozi Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi (hawapo pichani).
  Balozi Kilima (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Alsuwaidi

  0 0

   Mratibu wa Kituo cha Mabinti centre cha mikocheni jijini Dar es Salaam Bi. Katia Geurts(kulia) akimwelezea jambo Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa  Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(katikati) na waandishi wa habari jinsi kazi za ushonaji zinazofanywa na baadhi ya wakina mama waliotibiwa na kupona  fistula wakati walipotembelea kituo hicho na kujionea miradi mbalimbalia inayofadhiliwa na Vodacom Foundation,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu katika Hospital ya CCBRT na kupona  ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao.
   Mmoja  wasichana  wa kituo cha Mabinti Centre cha mikocheni jijini Dar es Salaam aliyepata kutibiwa Fistula, Happiness Christopher(kushoto)akimsikiliza Mratibu wa Kituo hicho, Katia Geurts wapili toka kushoto akimuonesha nguo anayoendelea kuishona binti huyo  wakati walipotembelea kituo hicho na kujionea miradi mbalimbalia inayofadhiliwa na Vodacom Foundation,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu katika Hospital ya CCBRT na kupona  ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao.
   Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto)akichagua moja ya begi lililoshonwa na wakina mama wa kituo cha Mabinti centre kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam wakati alipowatembelea kituoni hapo  na kujionea miradi mbalimbalia inayofadhiliwa na Vodacom Foundation,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu katika Hospital ya CCBRT na kupona  ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao.Kulia ni Cherry David.


  Wanawake waliotibiwa na hatimaye kupona  fistula katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam wameamua kujikita katika sanaa ya kazi za mikono kwa lengo la kujiajiri sambamba na kujikwamua na wimbi la umasikini.


  Takribani wanawake wapatao 81, chini ya mpango madhubuti ulioratibiwa na hospitali ya CCBRT, wamekuwa wakihitimu mafunzo mbalimbali ya kazi za mikono zikiwemo sanaa za ushonaji wa batiki, nguo za aina tofauti, utengenezaji wa mabegi, kofia, ususi na kadhalika, katika Kituo kinachoendeshwa na hospitali hiyo kijulikanacho kama ‘Mabinti centre’ tangu mwaka 2007.


  Akizungumza mbele ya ujumbe wa wadhamini waliotembelea kituo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Kituo hicho, Katia Geurts, alisema kituo hicho kinatoa mafunzo mahususi kwa wakinamama waliopona baada ya kusumbuliwa na fistula.


  “Wengi wao wanatoka katika familia duni, hivyo mafunzo haya wanayoyapata baada ya kumaliza matibabu ya Fistula yanakwenda kuwasaidia kujiajiri wao wenyewe jambo linalowasaidia kupunguza ukali wa maisha,” alisema Geurts.


  Aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo kituo hicho huwapatia vyeti vya uhitimu vinavyotambulika, sanjari na vitendea kazi vinavyoendana na stadi stahiki aliyohitimu mwanafunzi kwa minajiri ya kuwarahisishia upatikanaji wa mahitaji muhimu ya maisha yao.


  Nae Mkufunzi wa Kituo hicho ambaye awali alikuwa mmoja wa waathirika wa ugonjwa wa fistula hospitalini hapo, Jane Rugalabamu, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aanze kufundisha wenzake kituoni hapo amebaini kuna idadi kubwa ya wanawake wenye matatizo ya fistula ndani ya jamii lakini waume zao wamekuwa wakiwaficha kwa dhana ya kufisha aibu.


  “Kuna haja kubwa ya kuelimisha akinababa wawaruhusu wake zao wenye matatizo waje kutibiwa. Fistula ni hali inayotibika na wala sio hali ya  kurogwa kama wengi wanavyodhani, sisi sote hapa kwenye kituo cha mabinti tulikuwa na hali hiyo na sasa tumepona kabisa wanawake jitokezeni,” alisema Rugalabamu.


  Kwa upande wake Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia,  baada ya kukagua shughuli mbalimbali za mafunzo zinazoendelea kituoni hapo, alisema kwa niaba ya wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone duniani kote, wataendelea kuwasaidia akinamama wote wanaopatwa na hali hiyo ya fistula hatua kwa hatua, sanjari na kuhakikisha wanazidisha kasi katika kampeni inayoendelea dhidi ya hali hiyo.


  “Tutaendelea kuwa karibu zaidi na waathirika wa fistula kuanzia hatua ya kuwasafirisha kutoka vijijini na mikoani kwa kuwatumia fedha kupitia huduma yetu ya M-Pesa, pia tutakuwa pamoja wakati wote wa matibabu na baada ya kupona tutawaunga mkono kwenye mafunzo kama haya ili kuwaletea ustawi ulio bora kwa maisha bora kwa ajili yao na familia zao,” alisema Mworia.  

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  VIONGOZI wa nchi wametakiwa kushiriki katika mkutano wa umoja wa Mataifa wa kujadili malengo 17 ya maendeleo endelevu utaofanyika Septemba 25 mwaka huu nchini Marekani.


  Akizungumza na waandishi  habari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mtandao wa Mabadilliko ya Tabia nchi (CAN), Sixberty Mwanga ,amesema kuwa mkutano huo ni muhimu katika kuweza kutekeleza eneo la mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kadri ya siku zinavyoongezeka hali ya ukame inazidi kuongezeka.


  Amesema kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa mabadiliko ya tabia ya nchi  nchi inatakiwa kutumia dola za Kimarekai bilioni 1000  kwa mwaka  na hiyo inatokana na mabadiliko katika ukame na utowekaji wa maji  pamoja na uharibifu wa miundombinu  inayotokana mafuriko.


  Aidha amesema mkutano wa maendeleo  endelevu unahitaji  utashi wa kisiasa wa kuweza kufanikisha malengo ya hayo ikiwemo suala la mabadiliko ya tabianchi  ambalo linahitaji rasilimali za kutosha.


  Mwanga amesema  mabadiliko ya tabianchi yanasababishwa na vitu vingi ambavyo vinatkiwa kuepukwa kwa kuweza kutumia vitu asili kama matumizi ya nishati mbadala.


  “Malengo 17 ya Maenndeleo Endelevu utekelezwaji wake itawezekana kama dhana ya mabadiliko ya tabianchi yatazingatiwa kwa vitendo”amesema Mwanga.


  Aliongeza kuwa kuongezeka kwa njaa ikwa ni lengo la maendeleo endelevu ambayo inatokana ukame ambao umebasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
  Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa maendeleo endelevu ya mabadiliko ya tabia ya nchi utakaofanyika nchini Marekani Septemba 25 mwaka huu. 
  Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga akizungumza na waandishi wa habari npamoja na wadau wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa jijini Dar es Salaam leo, kulia ni  Mhasibu wa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Erick Makere
   Kulia ni Afisa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Onditi Msololo na Mhasibu wa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Erick Makere wakimsikiliza Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo  wa Umoja wa Mataifa ( UNDP), Helen Clark (kushoto) akiwa na Mcheza  senema  maarufu na mwanaharakati wa Mazingira, Alec Baldwin (katikati)  na Mkewe, Hilaria Thomas wakati wa mkutano maalum na waandishi wa habari wa kutangaza washindi wa Tuzo ya Ikweta ambayo hutolewa na Umoja Mataifa kwa  NGO ambazo zinajihusisha na utunzaji wa  mazingira, ulinzi na uhifadhi wa misitu, matumizi bora na endelevu ya ardhi na mali asili na  kupiga vita umaskini. 

  Tuzo ya mwaka huu wa 2015 ambayo ni  dola  za kimarekani 10, 000 kwa kila mshindi inakwenda kwa NGO 21 ambapo  NGO ya Tanzania ijulikanayo kama Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania ( MJUMITA) ni kati ya NGO sita kutoka Afrika,  Kusini  mwa Jangwa la Sahara zilizoshinda Tuzo hiyo. 

  MTANDAO wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) ni kati ya asasi   21 ambazo mwanzoni mwa wiki hii zimetangazwa kuwa washindi wa Tuzo ya Ikweta (Equator Prize) kwa mwaka 2015.


  Tuzo hiyo hutolewa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofadhili tuzo hiyo. Kila shirika lisilo la kiserikali (NGO) iliyoshinda Tuzo hiyo inanyakua kitita cha Dola za Marekani 10,000.


  Ushindi wa Mjumita pamoja na NGO nyingine 20 kutoka maeneo mengine duniani, ulitangazwa na Mkuu wa UNDP, Helen Clark katika mkutano wake na wawakilishi wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Umoja wa Mataifa.

  Wawakilishi wa  NGO hizo   21 watapokeaTuzo zao Desemba mwaka huu, wakati wa Mkutano wa Kimataifa utakaojadili mabadiliko yaTabianchi ( COP21) utakofanyika Paris, Ufaransa.


  Mjumita ni mtandao wenye wanachama katika vijiji 450 vilivyopo katika wilaya 23 za Tanzania na hujishughulisha na utunzaji wa misitu, kuwasaidia wanavijiji kupata hati za kimila za kumiliki ardhi, kutatua migogoro ya ardhi na kubuni miradi ya matumizi sahihi ya ardhi na rasilimali za misitu.


  Taarifa iliyotumwa kwa gazeti hili ilieleza kuwa zaidi  ya watu 500,000 wamenufaika na huduma zinazotolewa na Mjumita.


  Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi hao Clark aliyefuatana na Christiana Figueres anayeshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, alisema NGO hizo zinazojihusisha na masuala ya mazingira zimedhihirisha kuwa zina jambo la kuifundisha Jumuiya za Kimataifa.


  Alisema zaidi ya washiriki 100 waliingia katika shindano hilo lakini  21 ndio walioibuka kidedea.


  Clark alisema tuzo hiyo inatolewa wakati ambao viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali wanakutana jijini New York kuzungumzia ajenda 17 za maendeleo endelevu ikiwamo namba 13 inayohusus mabadiliko ya tabia nchi.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Maimuna Tarishi akitoa hatuba ya ufunguzi rasmi wa kikao cha wadau wa Usajili na Utunzanji wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu nchini kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
   Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Emilian Karugendo, akifafanua jambo wakati wa uwasilishaji wa mada iliyohusiana na hatua za kuandaa Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu wakati wa kikao cha wadau kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
   Meneja wa Usajili kutoka RITA Angela Anatory akiwasilisha rasimu ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu katika kikao cha wadau kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Maimuna Tarishi (katikati) akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mmoja wa watoa mada wakati wa kikao cha wadau wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu kilichofanyika katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.

   Mwakilishi wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dkt. Rufaro Chatora akiongea kwa niaba ya wawakilishi wengine wa mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria kikao cha wadau wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa wadau wakati wa kikao cha kujadili rasimu ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Maimuna Tarishi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya kufunga kikao cha kujadili rasimu ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.

  Veronica Kazimoto, Dar es Salaam, 
  USAJILI wa Raia una jukumu la msingi katika kutekeleza matakwa ya utawala bora na maendeleo ya kiuchumi katika taifa lolote lile duniani.


  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba Maimuna Tarishi wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili Rasimu ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu uliofanyika jijini Dar es Salaam.


  Tarishi amesema Usajili wa Raia ni wajibu wa kisheria kwa kuwa unasaidia katika upangaji wa mipango madhubuti ya maendeleo pamoja na kuiletea maendeleo jamiii kulingana na Mkakati wa Kuondoa Umaskini na Kukuza Uchumi Tanzania (KUKUTA II).


  Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria amebainisha kuwa mfumo wa Usajili wa Raia uliopo sasa Tanzania Bara umekuwa ukifanya kazi kwa kusuasua na hivyo kusababisha baadhi ya wananchi kutotambulika katika kumbukumbu rasmi za kiutawala.


  “Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012, ni asilimia 15 tu ya watanzania ndio waliosajiliwa na kupata vyeti, hali inayowaacha wengi pasipo kutambulika popote katika kumbukumbu rasmi za kiutawala,” amesema Tarishi.


  Ameongeza kuwa usajili ya vifo ndio uko katika hali mbaya zaidi ambapo ni matukio machache ya vifo yanayoandikishwa na sababu za vifo hivyo hazibainishwi kwa usahihi au hazibainishwi kabisa hali inayosababisha ugumu katika kutekeleza majuku kwa upande wa sekta ya afya nchini.


  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ambaye ofisi yake ni mdau muhimu wa mfumo huu, amesema lengo la mkakati huu ni kuanzisha mfumo wa Usajili wa Raia ambao unakidhi vigezo vya kimataifa ambao ni wa kudumu na unaofikia watu wote katika kusajili matukio muhimu ya binadamu na kuzalisha takwimu za matukio hayo katika namna ambayo ni endelevu na ya kuaminika.


  Dkt. Chuwa amesema mfumo huu wa Usajili wa Raia ukikamilika utasaidia kupata huduma zote za usajili katika sehemu moja kwa vituo vyote vya usajili nchini.


  Nae Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) Emmy Hudson amesema mfumo uliopo sasa uko mbali na wananchi walio wengi hasa wa maeneo ya vijijini kwasababu ngazi ya chini ya usajili ni ofisi ya  Katibu Tawala wa Wilaya.


  Changamoto hii na nyingine inasababisha huduma hii ya usajili kutofika kwa urahisi kwa wananchi walio wengi hali ambayo inaleta uhitaji wa mabadiliko ambayo ili tufanikiwe, RITA inahitaji peke yake haitamudu kuzikabili changamoto za mfumo pasipo kuhusisha wadau mbalimbali katika kuboresha mfumo huu.


  Usajili wa Raia ulianzishwa na sheria ya kikoloni mnamo mwaka 1917. Kwa mujibu wa sheria hiyo usajili ulikuwa ni lazima kwa wakazi wa Tanganyika na baada ya uhuru, sheria hii ilirithiwa ambapo licha ya mabadiliko kadhaa ambayo yamekuwa yakifanyika bado wananchi wamekuwa na kasumba ya kutokuona umuhimu wa Usajili wa Raia nchini.

  0 0
 • 09/23/15--06:19: TANGAZO LA KIFO
 • Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Yakalawa Kondo – Msaidizi wa Ofisi Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Pichani) kilichotokea tarehe 21.09.2015 saa 3 usiku katika Kituo cha Afya cha Vijibweni - Kigamboni. Mazishi yalifanyika tarehe 22.09.2015 saa 10 jioni katika makaburi ya Tungi Shule – Kigamboni. 

  “Mungu ailaze  Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amen”

  0 0

   RADIO Ebony Fm yenye makao yake makuu mkoani Iringa kupitia kipindi chake cha mchana "THE SPLASH" imezindua rasmi hewani (on air launching) msimu mwingine wa kila mwaka wa tamasha maarufu kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini linalokwenda kwa jina la "MTIKISIKO" ambalo linatarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu na kupita karibu sehemu zote inaposikika redio hiyo baadhi ya picha za watangazaji wakiwa katika shangwe za uzinduzi huo.
  (PICHA zote na Denis Mlowe)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyehamishwa kutoka Tanga Mhe. Magalula Said Magalula (katikati) akisalimiana na watumishi wa ofisi yake mpya waliokusanyika kumpokea rasmi nje ya jengo la ofisi hiyo jana tarehe 22 Septemba 2015.
  Mkuu Mpya wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Magalula Said Magalula kulia na Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Smythies Pangisa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyemaliza muda wake Eng. Stella Manyanya ambaye yupo kwenye harakati za kugombea Ubunge Jimbo la Nyasa wakisaini nyaraka za makabidhiano ya ofisi mapema tarehe 22 Septemba 2015.
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa wa pili kulia kwa niaba ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya akimkabidhi rasmi nyaraka za makabidhiano ya ofisi Mkuu mpya wa Mkoa huo aliyehamishwa kutoka Tanga Mhe. Magalula Said Magalula kulia jana tarehe 22 Septemba 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Magalula Said Magalula akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi yake mpya kufuatia uhamisho wa hivi karibuni kutoka Mkoa wa Tanga. Katika salamu zake alishukuru kwa mapokezi mazuri na kuomba ushirikiano kwa viongozi na watumishi katika kutimiza majukumu ya msingi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Aliwataka viongozi pamoja na watumishi kutambua majukumu yao ya msingi ambayo ni kutoa huduma bora kwa wananchi, alisisitiza pia juu kilimo bora chenye tija kwa kuwapa wananchi huduma stahiki. Kutokana na kuwepo kwa tishio la Mvua juu wa wastani (Elnino) Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza viongozi wa halmashauri kuwapa wananchi wao tahadhari na kuhakikisha wanaoishi katika mazingira hatarishi wanaondoka na wengine kuboresha nyumba zao.
   Sehemu ya wakuu wa idara walioshiriki kikao hicho cha makabidhiano.
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Benson Kilangi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu Hamid Njovu wakishuhudia makabidhiano hayo.

  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) akimsikiliza Afisa Balozi wa China anayehusika na masuala ya Utamaduni nchini Tanzania Bw. GAO WEI (wapili kushoto) walipofika katika ofisi za Wizara kutambulisha uongozi mpya na kutoa nafasi kwa uongozi wa zamani kuaga Wizara yenye dhamana na masuala ya Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kulia) akimkabidhi Afisa Balozi wa China aliyemaliza muda wake katika masuala ya Utamaduni  nchini Tanzania Bw. LIU DONG zawadi ya picha ya Tingatinga kama ishara ya kumpongeza kwa kuhamasisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni kati ya Tanzania na China leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kulia) akiangalia vitu mbalimbali vya kiutamaduni alivyokabidhiwa na Afisa Balozi wa China aliyemaliza muda wake katika masuala ya Utamaduni nchini Tanzania Bw. LIU DONG (katikati) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Balozi wa China anayehusika na masuala ya Utamaduni nchini Tanzania Bw. GAO WEI

  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

  0 0

   Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia) na Afisa Uhusiano na
  Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha bango kwa waandishi wa
  habari jijini Dar es Salaam jana kama ishara ya kuzindua huduma mpya
  ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja  kupiga simu
  Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja
  na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi
  300 tu.
  Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa
  habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
  kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja  kupiga simu Airtel
  kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja na
  kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300
  tu. Kushoto ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.  .     Wateja kupiga  simu na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo

  ·         Piga simu bure kila siku kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi
  ·         Kwa shilingi 300 tu.
  KAMPUNI ya simu za mikononi Airtel imewapa sababu nyingine wateja wake kufurahia usiku kwa kuwapatia “Yatosha Nyts” ofa inayowawezesha kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo,pamoja na kifurushi cha internet cha  MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.

  Ofa hii ya “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima
  kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwenda
  mitandao yote kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi hadi
  siku za wikiendi.


  Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde
  alisema, “ Tunatambua wateja wetu wanamahitaji tofauti  ya huduma za
  simu. “Yatosha Nyts” ni ofa kabambe na ya kipekee inayo kidhi mahitaji
  ya wateja wetu.


   Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa  kwa kuzingatia
  mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku
  inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao. “Yatosha
  Nyts” inawawezesha wateja kuwasiliana na familia, marafiki , mpenzi na
  wafanya biashara wenzake wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.  Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni mwendelezo wa kutoa huduma za
  mawasiliano  bora zenye gharama nafuu, wateja wetu wanauwezo wa
  kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza kufurahia
  kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi. Kwa shilingi
  300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel
  kwenda Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao
  yote  na 10 MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku.


  Kujiunga na “Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya
  na moja kati ya ofa nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja
  wake chini ya huduma ya kibunifu ya  Airtel Yatosha. Airtel Yatosha
  inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia
  huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma.


  Yatosha pia inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda,


  huduma ya kibunifu na ya kwanza kutoka Airtel

older | 1 | .... | 649 | 650 | (Page 651) | 652 | 653 | .... | 1898 | newer