Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 651 | 652 | (Page 653) | 654 | 655 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
  VIJANA Watanzania  wameungana katika harakati za kupambana na Mabadilikio ya Tabianchi kutokana na kuwa idadi kubwa ya watu kuweza kufanya mabadiliko hayo.

  Akizungumza na wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi,Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi,Sixberty Mwanga amesema kuwa katika malengo 17 ya Maendeleo Endelevu Tanzania inatakiwa kushiriki na kukubali juu ya kuweza kupata fedha za kuweza kutekeleza malengo hayo.

  Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu unaanza kesho na washiriki viongozi juu katika nchi zilizo katika umoja ulilenga kujadili maendeleo hayo na jinsi ya uwekezaji  katika maeneo ya malengo.

  Amesema katika mkutano unaoanza kesho wa kujadili melengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kama nchi inahitaji  kuweka utashi jinsi ya kuweza kutekeleza ili isiweze kutokea kama Malengo Nane ya Millenia.
  Mwanga amesema kutekeleza malengo 17 ya Maendeleo Endelevu katika mabadiliko ya tabianchi inahitaji uwekezaji wa kutosha kama nchi pekee yake haiwezi kutekeleza.

  Aidha amaesema kuweza kutekeleza lengo moja katika SDGs  la mabadiliko ya tabia nchi kuna uwezekano wa kuweza kutekeleza malengo matano mengine kutokana na tabianchi kuwa suala mtambuka.

  Katika mkuatano huo wa wadau wameweza kuwasha mishumaa kuashiria mapambano ya mabadiliko tabianchi  yameanza kuanzia mkutano wa kesho wa Umoja wa Mataifa (UN) wa kujadili Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.
  Mkurugenzi wa Asasi ya Mazingira,Elisha Sibale amesema  kuwa vijana wanawajibu wa kuleta mabadiliko chanya katika mabadiliko ya tabianchi kutokana na kuwa sehemu ya kubwa ya kuweza kuingia katika ajenda hizo.
   Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi (CAN), Sixberty Mwanga akizungumza katika mkutano wa wadau wa mabadiliko ya Tabianchi kuelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu kwa mkutano unaonza kesho mjini New York,Marekani leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Asasi ya Mazingira, Elisha Sibale akizungumza leo katika mkutano wa wadau wa mabadiliko ya tabianchi  juu ya vijana kuweza kushiriki katika mapambano hayo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  03.Wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakiwa wamewasha mishumaa kuashilia kuanza  kwa harakati hizo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakisiliza maada kuelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu na jinsi ya uwekezaji katika mabadailiko hayo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Kikundi cha wanawake wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni sehemu yao wanawake katika mabadiliko ya Tabianchi jijini Dar es Salaam.
  05.Sehemu ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakisiliza maada kuelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu na jinsi ya uwekezaji katika mabadailiko hayo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)


  0 0

   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM,Ndugu Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,akiwaongoza baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho na wageni waalikwa kutoka Serikali ya Mkoa wa Geita kukata Ndafu  ikiwa ni sehemu ya  kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,wakati wa mapumziko ya shughuli za kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,ambapo leo alitarajia kuendelea na kampeni zake mkoani Shinyanga.

  Wakati huo huo Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dr.John Magufuli ameahirisha mikutano yake ya kampeni aliyokuwa aifanye leo Mkoani Shinyanga ili kupisha sikukuu ya Eid El Hajj,pia amewatakiwa Watanzania wote popote pale walipo sikukuu njema na yenye Baraka mbele za Mwenyezi Mungu na na kuwa tuendelee kuidumisha Amani ya Nchi yetu. 
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM,Ndugu Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,akizungumza jambo mbele ya baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho na Serikali ya Mkoa wa Geita wakati wa mapumziko ya  kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,mapema le mchana mkoani Geita
   Ndafu akiwa ameandaliwa tayari kwa kuliwa.
   Ndafu ikikatwa kwa pamoja.PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawaagiza wasanii, wamiliki na waendeshaji wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari hususan radio na runinga kuondoa na kuacha mara moja kurusha au kutangaza au kucheza nyimbo zote zenye maudhui ya kashfa, matusi, kejeli, udhalilishaji ambazo zinahatarisha kuigawa jamii ya kitanzania katika misingi yoyote hasa katika kipindi hiki Taifa linapoendelea na kampeni za kisiasa na kujiandaa na uchaguzi mkuu.

   


  Kwa mujibu wa kifungu namba 118 (a-d) cha Sheria ya Bunge namba 9 ya Mawasiliano ya Mtandao ya mwaka 2010 ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza, kuzalisha, kusambaza au kutangaza ujumbe ambao una mlengo wa matusi, dharau, uzushi au jinai kwa lengo la kutukana, kutisha, kusumbua au kushusha hadhi ya mtu mwingine.
  Aidha, Sheria ya Bunge namba 4 ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 45 (1) (a-c) kinatoa mamlaka kwa taasisi au mtu yeyote anayebaini uvunjifu wa Sheria katika mitandao kutoa notisi kwa yeyote yule anayesambaza au kutangaza ujumbe au maudhui yanayovunja sheria za nchi kuacha mara moja au vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote anayekaidi.
  Ni kwa msingi huu, BASATA linawaagiza wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii kama sound cloud, U-Tube, ITunes nk. kuondoa ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya kwanza ya taarifa hii nyimbo zote zinazokengeuka maadili na kubeba mlengo wa matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na kitaifa.

  Aidha, BASATA linawakumbusha tena Wasanii wote nchini kuacha mara moja kubuni na kutengeneza kazi za Sanaa zenye kuashiria kuigawa jamii katika misingi yoyote ya kibaguzi na zaidi kutumia Sanaa kubomoa jamii badala ya kuijenga.
  BASATA linawasisitiza wamiliki wa vyombo vya habari hususan radio na runinga pia watangazaji na Ma DJs kuhakikisha hawawi chanzo cha kusambaza maudhui yoyote ya Sanaa yenye mlengo wa kuibua chuki, matusi, kashfa na mgawanyiko wa Taifa.
  BASATA kwa mamlaka yake chini ya Sheria namba 23 ya mwaka 1984 na yale ya Sheria ya Mawasiliano ya Posta na Mitandao ya mwaka 2010 na ile ya Makosa ya mitandao ya mwaka 2015 kwa kushirikiana na vyombo vya dola halitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kinidhamu kwa wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari ambavyo vitaendelea kutangaza na kusambaza nyimbo zenye mwelekeo wa kuhatarisha usalama, umoja na mshikamano wa Taifa.
  BASATA likiwa ni msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linatambua kwamba Sanaa ikitumiwa kwa ukengeufu inaweza kuwa chanzo kikuu cha machafuko, mivurugano na kupotea kwa amani nchini. Hivyo umakini unahitajika miongoni mwa wasanii katika kuzingatia weledi, maadili, uzalendo kwa taifa na kuitumia Sanaa kama chombo cha kujenga jamii yenye kuzingatia maadili.   SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI  Godfrey L. Mngereza
  KATIBU MTENDAJI, BASATA

  0 0
 • 09/24/15--12:00: Mtoto apotea na house-girl
 • Picha ya hivi karibuni ya mtoto Loveness C. Jullu
  Familia ya Jullu ya Wazo Hill kwa Msabaha jijini Dar es Salaam inaomba msaada kutoka kwa raia wema ili kufanikisha kumpata mtoto wao Loveness Coletha Jullu aliyepotea nyumbani na msichana aliyekuwa akimlea na kusaidia shughuli za nyumbani.

  Wawili hao hawajaonekana tangu juzi Jumanne. Taarifa zimefikishwa katika kituo cha polisi na RPC wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni amekiri kupata taarifa za tukio hilo.

  Ikiwa una taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwao tafadhali zitoa kupitia namba hizi: 0715797920 na 0786977615.

  Asante.
  Binti msaidizi wa kazi za nyumbani (house-girl).
  Picha ya awali ya mtoto


  0 0
  0 0

  Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.

  Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki. 

  0 0

  Kutoka kushoto ni Professor Lyoyd Binagi (Manamba) James Binagi, Bi.Luise Binagi, Ghati Isanchu na wanandugu wengine wakiwa katika sherehe ya kifamilia iliyofanyika jana Septemba 24,2015 katika Kijiji cha Kenyamanyori ambapo Professor Binagi aliandaa sherehe hiyo kwa ajili ya kumchinjia mbuzi wa supu shemeji yake aitwae Bi.Nyamhanga Samo.

  Na:George GB Pazzo
  Kwa kabila la Wakurya sherehe ya kumchinjia mtu mbuzi kwa ajili ya supu huchukuliwa kama heshima kubwa miongoni mwa alieandaa sherehe hiyo na yule alieandaliwa sherehe ambapo ndugu, jamaa, marafiki na majirani hualikwa kwa ajili ya kushiriki pamoja katika sherehe hiyo.
  Kushoto ndie Bi.Nyamhanga Samo ambae sherehe iliandaliwa kwa ajili yake na hapa akiwa pamoja na mke mwenzie wakipata chakula
  Kushoto ni Hezekia Binagi (Maina) akipokea Supu kutoka kwa Professor Lloyd Binagi
  Bi.Luise Binagi akimpatia Supu mhusika Mkuu wa sherehe Bi.Nyamhanga Samo.
  James Binagi (Chacha) akimpatia supu Shemeji yake.

  Geban Winani akimpatia Supu Bi.Otaigo Mohabe
  Bi.Luise Binagi akimpatia Supu Bi.Sophia Binagi
  Supu hii huandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu ni inafaa kunyweka kwa wazee, mwanawake alidjifungua siku za karibuni au mgonjwa kwa kuwa huufanya mwili kuwa imara zaidi.
  Wazee wakipata supu
  Tamaduni hii ilikuwepo miaka mingi iliyopita na bado inaendelea kuenziwa na familia nyingi katika kabila la Wakurya

  Nyama huchomwa kwa ustadi mzuri pia
  Waandaaji wa Nyama
  Hapa pia Kichuri huandaliwa
  Pia vyakula mbalimbali huandaliwa
  Baada ya watu kunywa supu na kula chakula, hufuata zawadi kwa mlengwa wa sherehe  ambapo alieandaa sherehe huanza kumtuza zawadi za blanketi, vitenge na pesa yule alieandaliwa sherehe
  Mzee Maina akimtuza zawadi ya Kitenge mhusika wa sherehe ambae ni shemeji yake
  Mzee Chacha akimtuza zawadi ya Kitenge mhusika wa sherehe ambae ni shemeji yake
  Zawadi zikiendelea kutolewa
  Zawadi zikiendelea kutolewa
  Zawadi zikiendelea kutolewa
  Zawadi zikiendelea kutolewa
  Zawadi zikiendelea kutolewa
  Zawadi zikiendelea kutolewa
  Wazee katika picha ya pamoja
  Wazee wakibadilishana mawazo baada ya chakula
  Baada ya Chakula na kubadilishana mawazo
  Wanafamilia
  Wanafamilia
  Wanafamilia
  Wanandugu
  Wanafamilia
  Wanafamilia
  Wanafamilia
  Watoto nao hufurahia sherehe za kuchinja supu
  Hatimae sherehe ikafikia tamati na Muandaaji wake ambae ni Professor Lloyd Binagi akaingia ndani ya gari na safari ya kurejea nyumbani kwake Bomani Mjini Tarime kutoka Kijijini alikozaliwa Kenyamanyori ambapo sherehe ilifanyikia ikawadia

  0 0

   Injinia Mkuu wa Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Wilaya ya Musoma Suleiman Bishanga, akimuonesha Makamu wa Rais Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal ramani ya ujenzi wa msikiti huo hadi utakapokamilika wakati Makamu wa Rais alipotembelea kuangalia ujenzi huo leo Sept 24,2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Himid Jongo kwenye Baraza la eid el Hajj iliyofanyika kitaifa leo Sept 24, 1015 katika ukumbi wa MCC Musoma Mkoani Mara.
   Waumini wa Dini ya Kiislam wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akihutubia Taifa kwenye Baraza la eid el Hajj iliyofanyika leo Sept 24, 1015 katika ukumbi wa MCC Musoma Mkoani Mara.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Taifa kwenye Baraza la eid el Hajj iliyofanyika leo Sept 24, 1015 katika ukumbi wa MCC Musoma Mkoani Mara. (Picha na OMR)

  0 0

  Wasanii kutoka Rock City Mwanza wanaounda kundi la TANZANIA ONE MUSIC ambapo kushoto ni D'Maladha, Katikati ni Lady Shushu na Kulia ni Nyasa Boy.
  Na:Binagi Media Group
  Ukiwataja wasanii wanaofanya vizuri kutoka Jijini Mwanza, lazima utawataja Nyasa Boy, D'Maladha pamoja na mwanadada Lady Shushu ambao wanaunda kundi la Tanzania One Music ambalo tayari linatesa na ngoma mbili sokoni.

  Wasanii hao kupitia kundi hilo, wameweza kuliteka soko la Muziki wa Mwanza kupitia ngoma zao mbili ambazo ni Nasema Nawe (Bonyeza HAPA Kuitazama) pamoja na Thamani ya Penzi (Tazama Hapo Chini).
  Tazama Thamani ya Penzi hapa chini

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi na  kupokea Malalamiko yao Katika mkutano wa siku mbili wa tarehe 22 na 23, Septemba, 2015 katika Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi. 

  Wananchi wengi waliofika katika mkutano huo walisifu jitihada za Waziri Lukuvi katika kushughulikia Migogoro ya Ardhi ambapo tarehe 22 Septemba 2015 alipokea Malalamiko ya Wananchi kwa Manispaa ya Kinondoni na tarehe 23 Septemba 2015 alipokea Malalamiko ya Wananchi kwa Manispaa ya Temeke na Ilala.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujua jinsi alivyoshughulikia migogoro ya Ardhi nchini.
   Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi pamoja na Naibu wake Mhe. Angela kairuki wakipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam.
   Waziri wa Ardhi akimsikiliza kwa makini mwananchi mwenye malalamiko ya mgogoro wa ardhi kutoka manispaa ya kinondoni
  Baadhi ya Wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi wakiwa katika mkutano huo.

  0 0

  Vinara wa biashara Afrika walipewa tuzo mbalimbali za African Business katika picha ya pamoja. Kuanzia kushoto ni Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa, Helen Hai na Mohammed Dewji . hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika hoteli ya Four Seasons Hotel mjini New York.
  Picha na African Business. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa Albanu ya nyimbo kumi ikiwa mpaka sasa ametimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa nyia ya nyimbo hapa nchini.

   ALBAMUya OMBA YESU ANASIKIA kuzinduliwa Septemba 27 mwaka huu(Jumapili hii) katika kanisa la TAG  la upanga mkabala na chuo cha Uzumbe kwa Askofu  Mwanesongore.

   hayo yalisemwa na Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendio Nkone wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema kuwa Mungu amemuokoa katika kifo ndio maana ameona aimbe kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na mambo aliyoyapitia, pia kumshukuru Mungu wa kutimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa njia ya Nyimbo.

  Nkone alisema kuwa katika uzinduzi huo wa albamu ya OMBA YESU ANASIKIA kutakuwepo waimbaji wa nyimbo za Injili  ambao watatumbuiza katika uzinduzi wa albamu hiyo atakuwepo  Masanja mkandamizaji, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Kwaya ya Kijichi, Mather Baraka, Christina Matai, Mesi Chengula pamoja na Bendi.
    
  Pia alisema kuwa katika uzinduzi wa albamu hiyo kutakuwa na viingilio tofauti, watu wazima watalipia kiasi za shilingi elfu tano(5000) na watoto shilingi elfu mbili (2000).

  0 0

  1.Mmoja wa wanaKikundi cha Masai warriors akionesha ujanja wake wa kuendeha baiskeli ya taili moja.Mmoja wa wanakikundi cha Masai Warriors akionesha ujanja wake wa kuendeha baiskeli ya tairi moja.
  2.Watoto wakizidi kumshangaa mtaalamu huyo wa kutembelea baiskeli ya taili moja.Watoto wakimshangaa mtaalam huyo wa kutembelea baiskeli ya tairi moja.3.Masai warriors wakionesha madoidi yao kwa watoto wao.Masai Warriors wakionesha madoido kwa watoto.4.Mmoja wa wanakikundi cha Masai Warriors akionesha ujanja wa kukunja viongo vyake siku ya Idd El Hajj jana nyakati za jioni.Msanii akionesha ujanja wa kukunja viungo.5.Watoto wakizidi kupokea burudani mwanzo mwisho kwa Massai Warriors.Watoto wakizidi kufurahia burudani.6.Mtaalamu wa kuchezea baiskeli akionesha ujanja wake mbele ya watoto hao.Mchezea baiskeli akiendelea na ujanja wake.7....wakendelea kuonesha utaalamu wao.Maonyesha yakiendelea.
  WAUMINI wa dini ya Kiislam nchini kote jana waliungana na waumini wenzao duniani kote kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj.
  Katika kusherehekea sikukuu hiyo, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijiniDar es Salaam, kulikuwana tamasha lililotambulishwa kama ‘Amerudi Night’ ambapo kikundi cha Masai Warriors waliwapagawisha watoto kwa kuonesha michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi, kuchezea baiskeli na michezo mbalimbali.
  NA DENIS MTIMA/GPL

  0 0
 • 09/25/15--01:18: BEI YA MADAFU HII LEO

 • 0 0

  HABARI ZENYE LINK ZA YOUTUBE! 
  Star TV: Waumini wa Dini Ya kiislam Waungana na waislam wote nchini kusherehekea ibada ya sikukuu ya Eid El Haj na kuombea Amani Uchaguzi mkuu. https://youtu.be/DNNY-2vzKjY

  TBC: Mamlaka ya mawasiliano TCRA imewataka wamiliki wa Radio Na TV kutumia vyombo hivyo kuleta maendeleo ya Taifa na sio kufanya Uchochezi. https://youtu.be/3zkiqOOwXqI

  Star TV: Serikali yaitaja Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi kutokana na watendaji wake kushirikiana na matapeli. https://youtu.be/zz_W8emSZhU

  TBC: Mgombea Uraisi UKAWA Mhe. Edward Lowassa awaahidi wananchi wa Lindi kupitia upya mikataba ya Gesi endapo atachaguliwa kuwa raisi. https://youtu.be/ufwCxHLO4So

  Star TV: Timu Ya Arsenal The Gunners imeshinda rufaa yake dhidi ya kadi nyekundu aliyopewa mlinzi wa kati Gabriel Paulista katika mechi dhidi ya Chelsea. https://youtu.be/mZT-_cA4Rs8

  Tbc: Wakazi wa Bongwa Wilayani Bagamoyo wameitaka serikali kushughulikia tatizo la maji katika kijiji hicho baada ya visima kushindwa kukidhi mahitaji;  https://youtu.be/10cJ_0jGGg4

  STAR TV: Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kukabiliana na changamoto zinazowakabili watoto ili kulinda haki zao za msingi; HTTPS://YOUTU.BE/ID1N1N7LJ-S 

  Ch 10: TANESCO yaonya wananchi wanaofanya uhalifu katika miundombinu ya grid ya umeme wa taifa ambapo hadi sasa vipande 200 vya chuma katika grid ya umeme vimeibiwa; https://youtu.be/9WQTxyy1EWs

  AZAM TV: Balaza la habari nchini MCT yawaonya wamiliki wa vyombo vya habari kutoingilia utendaji kazi za waandishi wa habari;  https://youtu.be/DkWNWQ9BQKI

  0 0

   Mgombea Ubunge jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe.Dkt Fenella Mukangara akiwa kwenye mazungumzo na wakazi  wa jimbo la kibamba(kwa Yusuph) wakati alipotembelea vikundi vya vicoba ili kuwaskiliza kero zao ili kujua matatizo wanayowakabili kwa ujumla.
   Mkazi wa kata ya Msigani(aliyesimama) akielezea matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo ilo na kumwomba mgombea wa Jimbo ilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt Fenella Mukangara kuyatafutia ufumbuzi atakapopata nafasi ya kuwatumikia.

   Mgombea udiwani kata ya Msigani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Siraju Hassan Mwasha(aliyesimama) akiwa anazungumza na wakazi wa Maramba mawili na kunadi sera za chama chake.Bw Mwasha aliambatana na mgombea Ubunge wa jimbo la kibamba kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt Fenella Mukangara.

   Mgombea Ubunge jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe.Dkt Fenella Mukangara akiwaaga wakazi wa kwa Msigwa kata ya msigani baada ya kuzungumza na wakazi hao pamoja na vikundi vya kijasiriamali ili kujua ni kero gani zinawasibu ili kuboresha makundi hayo na maeneo yao kwa ujumla.
  Mmmoja wa wanakikundi wa Vicoba mtaa wa Temboni,Mbezi(aliyesimama) akimwuliza maswali mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(aliyekaa amesuka) Dkt Fenella Mukangara ni jinsi gani atawasaidia kuboresha vikundi vyao vya vicoba na jinsi gani atawasaidia ili wapate mafunzo ya ujasiriamali.

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  wa Tanzania na Marekani

  ·         Aiomba Serikali ya Marekani kuendelea kuiunga mkono Serikali mpya kama ilivyofanya kwake

  ·         Aishukuru kwa misaada iliyobadilisha maisha ya Watanzania katika miaka 10 ya uongozi wake


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameihakikishia Serikali ya Marekani kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili hautabadilika na kuwa utaendelea kuboreshwa zaidi hata baada ya kuingia madarakani kwa Serikali mpya Novemba mwaka huu, 2015.


  Aidha, Rais Kikwete ameiomba Serikali ya Marekani kuunga mkono utawala mpya wa Tanzania unaoingia madarakani Novemba mwaka huu kwa kiwango kile kile ambacho Serikali hiyo imeipatia Serikali yake kwa miaka 10 iliyopita.


  Vile vile, Rais Kikwete ameishukuru Serikali na wananchi wa Marekani kwa misaada mingi ambayo imechangia sana kuboreka kwa maisha ya Watanzania na kuinua kiwango cha maendeleo nchini katika miaka 10 ya uongozi wake wa Tanzania.


  Rais Kikwete ameyasema hayo , Jumanne, Septemba 22, 2015 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, Mheshimiwa Anthony Blinken kwenye Hoteli ya Ritz-Carlton mjini Washington ambako Rais Kikwete amefikia katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili kwenye mji huo mkuu wa Marekani.


  Rais Kikwete amemwambia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani: “Sioni uwezekano wowote wa msimamo wa Serikali mpya ya Tanzania kuhusu uhusiano wake na Marekani kuwa tofauti na ule ambao umekuwepo katika miaka 10 iliyopita. Dhahiri uhusiano huo hautabadilika kama Rais mpya atatoka katika chama chetu, lakini hata Rais akitokea chama kingine, sioni kama yanaweze kuwepo mabadiliko yoyote ya msingi ya sera au uhusiano kati ya Tanzania na Marekani.”


  Kuhusu ombi lake ya Serikali ya Marekani kuendelea kuunga mkono Serikali ijayo ya Tanzania, Rais Kikwete amesema: “Naiomba Serikali ya Marekani iendelee kuunga mkono Serikali yetu ijayo na wananchi wa Tanzania.”


  Ameongeza: “ Nawaombeni muendelee kuunga mkono maendeleo ya Tanzania. Matunda ya misaada yenu sasa yameanza kuonekana. Kwa mfano katika miaka 10 iliyopita Pato la Taifa limepanda mara tatu kutoka dola za Marekani bilioni 14.4 hadi kufikia dola za Marekani bilioni 50 kwa sasa.”

  Kuhusu misaada ambayo Serikali ya Marekani imeitoa kwa Tanzania katika miaka 10 ya uongozi unaomaliza muda wake, Rais Kikwete amesema: “Naishukuru sana Serikali na wananchi wa Marekani kwa misaada mingi na kila aina ambayo mmeitoa kwa nchi yetu na Serikali yangu.  Mmeacha nyanyo katika maendeleo ya nchi yetu. Tumepata ustawi usiokuwa wa kawaida katika miaka 10 iliyopita.”


  Rais Kikwete amesema kuwa Marekani kupitia mpango wake wa Pepfar, imechangia kupunguza sana makali ya magonjwa ya malaria na ukimwi. “Kwa upande wa malaria, mmesaidia kuokoa mamilioni ya maisha ya watu na vifo kutokana na ugonjwa huo sasa vimepungua kwa kiwango cha asilimia 70. Maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi yamepungua sana. 
  Matokeo yake ni kwamba wastani wa Watanzania kuishi umepanda kutoka miaka 55 hadi kufikia miaka 62 katika kipindi kifupi sana cha miaka 10 tu.”


  Baada ya hapo, Rais Kikwete ameingia katika undani wa misaada ya Marekani katika maeneo mbali mbali kuanzia kwenye kilimo na mipango inayoungwa mkono na Marekani ya Feed The Future na Alliance for Food and Nutrition Sufficiency.


  “Kutokana na misaada yenu, sasa tunajitegemea kwa chakula na hata kubakiza kiasi cha kuwauzia majirani zetu. Na hii yote ni kwa kutilia maanani kuwa wakati tunaingia madarakani tulilazimika kuwalisha kiasi cha watu 3.7 milioni kwa sababu ya ukame na ukosefu wa chakula.”


  Kwa upande wa misaada iliyotolewa chini ya Mpango wa Millenium Challenge Corporation (MCC - 1), Rais amesema kuwa misaada hiyo katika ujenzi wa barabara, usambazaji umeme na kuanzishwa kwa miradi ya kusambaza maji imechangia mno kuboresha kiwango cha maisha ya Watanzania.


  “Chini ya MCC, tumejenga kwa kiwango cha lami barabara zote za Pemba, tumejenga barabara kubwa kama ile ya Tanga-Horohoro, Tunduma-Sumbawanga, Songea-Namtumbo, tumepanua huduma za maji katika miji ya Dar es Salaam na Morogoro na tumesambaza umeme katika mamia ya vijiji katika mikoa 10 ya Tanzania Bara. Mwaka 2015, ni asilimia 10 ya vijiji vyetu vilikuwa na umeme. Sasa kwa msaada wetu, kiwango hicho kimefikia asilimia 46.”


  Katika sekta ya elimu, Marekani imesaidia upatikanaji wa vitabu vya kufundishia masomo ya hisabati na sayansi katika shule za sekondari nchini. “Msaada wetu katika eneo hili, umeanza kuboresha elimu yetu. Ubora wa elimu umepanda na viwango vinapanda.”


  Rais Kikwete pia ameishukuru Serikali ya Marekani kwa misaada yake katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na katika masuala ya usalama na vita dhidi ya ugaidi akisisitiza: “kwa sababu ya misaada yenu katika eneo hili, tuko imara zaidi hata kama matishio bado yapo.”


              Rais pia ameishukuru Serikali ya Tanzania katika ujenzi wa utawala bora yakiwemo mapambano dhidi ya rushwa. “Demokrasia yetu inaendelea kuwa bora zaidi. Tunaendelea kupambana na rushwa, hata kama mapambano yenyewe ni magumu. Kama mnavyojua, hata mawaziri wenzangu wawili sasa wako jela baada ya kupatikana na hatia za matumizi mabaya ya madaraka.”


  Rais Kikwete pia ameishukuru Serikali ya Marekani kwa mchakato wa kuanzishwa kwa Mpango wa MCC -2, akisisitiza kuwa changamoto ambazo zimejitokeza katika maandalizi ya mpango huo zitashughulikiwa ipasavyo na kwa haraka na Serikali yake.
     

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  24 Septemba, 2015

  0 0

  9Bella akicheza na waimbaji wake.5Mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo wakiserebuka.6Christian Bella akiimba wimbo wa ‘Nani Kama Mama’.7Bella akiwahamasisha mashabiki kucheza huku akiwa na taulo mkononi.8Waimbaji wa bendi ya Malaika wakiimba na kuserebuka.3Mwimbaji Msagasumu akiwapadisha mzuka mashabiki.

  4…Akionyesha umahiri wake wa kunengua.1Kadjanito akitoa burudani kwa mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live jana.2... Akiimba na kunengua.10Kadja akituzwa pesa na shabiki.

  KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’,akishirikiana na bendi yake ya Malaika Music pamoja na Msaga Sumu na Kadjanito jana katika usiku wa Idd el Hajj waliwapagawisha mashabiki vilivyo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Chipukizi watisha Katika usiku huo uliotambulika kama Usiku wa Amerudi, pazia la burudani lilifunguliwa na chipukizi ambao walionesha vipaji vya hali ya juu katika kuimba na kucheza. Chipukizi Small J, aliwavuta mashabiki wengi kwa kuingia na staili iliyofananisha na staa wa Bongo Fleva, Belle 9 na kufanya wengi wamshangilie. 

  Mbali na hapo wapo chipukizi waliofunika kama vile Bad Spence, wakali wa vinanda, na chipukizi mwenye asili ya kizungu kutoka Tongwe Records. Pazia la chipukizi lilifungwa na msanii Galaxy ambaye aliingia kwa mbwembwe na madensa wake waliofanya ukumbi wote uvutike na kushangaa shoo ambayo mashabiki wengi hawakutegemea.

   Wakali Dancer watisha kwa kucheza Kundi la kucheza la Wakali Dancer liliingia kwa mbwembwe ambapo lilianza kwa kucheza Wimbo wa Move Bit** na kufanya jukwaa lote lilipuke kwa shangwe. Msaga Sumu akinukisha Bingwa wa muziki wa Singeli asiye na mpinzani, Msaga Sumu aliingia na kufanya ukumbi wote ulipukwe upya kwa shangwe.

   Msaga Sumu alianza kwa kuwapiga nyimbo zake zote kali kama vile Rafiki wa Kweli kisha akafuatiwa na Naipenda Simba ambao ulifanya mashabiki wengi wajiachie kwa kunyoosha mikono juu kwa muda mrefu. Msaga Sumu aliendelea kukinukisha zaidi kwa kugonga vionjo vya Wimbo wa Huyo Mtoto kisha akamalizia wimbo wenyewe ambapo mashabiki wengi walimtaka asishuke jukwaani. 

  Kadjanito awasisimua mashabiki Staa kutoka Jumba la Vipaji (THT), Kadjanito naye alikuwa mmoja waliofunika ukumbini hapo. Kadja aliwaduwaza mashabiki wengi kwa muonekano wake na kwakuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kuzama katika kiwanja hicho, iliwafanya mashabiki wengi wavutike na kumshangilia kwa ikumshangaa. Staa huyo alianza kwa kuwatupia Wimbo wa Maumivu Niache ambapo ukumbi wote ulikuwa ukiimba naye. 

  Baada ya hapo aliangusha Wimbo wa Sina Maringo ambao wengi walikuwa wakicheza naye jukwaani na kisha akamalizia Wimbo wa Nzogo ambao umechanganyikana na lugha ya Kisukuma. Bella amaliza kila kitu Burudani ilihitimishwa na King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ ambapo walianza Malaika Music kwa kutoa bonge moja la sebene kisha akaingia Bella na kuanza kuimba Wimbo wa Amerudi uliofanya mashabiki wengi wapige kelele. 

  Bella aliamsha shangwe zaidi pale alipowaita wadada na kinamama wote kusogea karibu kisha kunyoosha mkono na kuanza kuimba nao Wimbo wa Nani kama Mama. Burudani iliendelea zaidi kwa Bella kwa kukamua nyimbo zake kibao kama vile Nakuhitaji, Safari Siyo Kifo kisha akawamaliza kabisa mashabiki kwa kupiga Wimbo wa Subira aliokuwa ameshirikisha na Cassim Mganga.
  STORI/PICHA: ISSA MNALLY, BONIPHACE NGUMIJE, GABRIEL NG’OSHA NA ANDREW CARLOS.

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  ·         Aunga mkono asilimia 100 staili ya Kampeni ya Magufuli

  ·         Asema Tanzania inahitaji mawazo mapya ili iweze kusonga mbele

  ·         Atamani muda wake wa kuongoza Tanzania kumalizika haraka zaidi

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya  Mrisho Kikwete amesema kuwa kama wapo watu binafsi ama taasisi yoyote mahali popote wenye matatizo na Sheria ya Takwimu mpya ama Muswada wa Habari nchini basi wawasilishe mapendekezo yake Serikalini ili yafanyiwe kazi badala ya kukaa na kulalamika pembeni ama kwenye vyombo vya habari.


  Rais Kikwete pia amesema kuwa ni jambo zuri na jema kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM anaelezea fikra na matumaini ya kuleta  mabadiliko makubwa zaidi katika uendeshaji wa Tanzania tofauti na uendeshaji huo ulivyo chini ya uongozi wake.


  Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa anatamani muda uende kwa kasi zaidi ili aweze kukabidhi madaraka ya kuongoza Tanzania kwa Rais wa Tano,  ili yeye apate muda wa kumpumzika baada ya kazi ngumu ya miaka 10 ambayo ameilezea kama mzigo mkubwa.


  Rais Kikwete ameyasema hayo, Jumanne, Septemba 22, 2015 wakati alipozungumza na wafanyakazi wa taasisi nne za Marekani  ambazo kwa namna moja ama nyingine zimefanya kazi na Serikali yake katika miaka 10 ya uongozi wake mjini Washington, D.C., ambako Rais amefanya ziara ya siku mbili ya kikazi.


  Rais Kikwete amezungumza na wafanyakazi wa taasisi za National Democratic Institute (NDI) yenye uhusiano na chama cha siasa cha Democratic, International Republican Institute (IRI) yenye uhusiano na chama cha siasa cha Republican, International Foundation for Electoral Systems (IFES) na United States Institute of Peace (USIP) kwenye makao makuu ya NDI.


  Wakati wa kipindi cha maswali na majibu na wafanyakazi wa taasisi hizo, Rais Kikwete ameulizwa swali kuhusu madai kuwa Sheria ya Takwimu na Muswada wa Habari inavuruga sifa za kidemokrasia za Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete.


  Akijibu swali hilo, Rais Kikwete amesema: “Nimelizungumza hilo huko nyuma na napenda kurudia. Sheria ya Takwimu inahusu tu takwimu rasmi za Serikali na wala si takwimu zote. Pili Sheria hii inatokana na matakwa na taratibu za Umoja wa Mataifa na Sheria yetu imetungwa kwa kutilia maanani matakwa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa. Kwa nini hili linakuwa tatizo kwa Tanzania pekee ni jambo gumu kueleza.”


  Kuhusu Muswada wa Sheria ya Habari, Rais Kikwete amesema: “Nimelisema hili huko nyuma lakini inaelekea halijaeleweka. Nilipata kusema pale Dar es Salaam na hata wakati nazungumza na wabunge wa Sweden mjini Stockholm kuwa kama mtu ana tatizo ama maoni na maudhui ya Muswada ule basi ayafikishe Serikali. Tutafanyia kazi. Hakuna tatizo na jambo hili. Ajabu ni kwamba tunachosikia ni malalamiko tu na hakuna yoyote ambaye amefikisha maoni yake kwetu.”


  Hata hivyo, Rais Kikwete ameongeza: “Jambo muhimu ambalo lazima sote tuelewane hapa ni kwamba Muswada wowote, uwe wa habari ama wa jambo jingine, ni lazima ulinde maslahi ya nchi yetu, yalinde umoja wetu, yalinde utulivu wa nchi yetu na yalinde usalama wa nchi yetu. Haya ni mambo ambayo hatuna haja ya kujadiliana na yoyote kwa sababu nchi zote duniani zinalinda kwa namna hii na zinaendeshwa namna hii.”


  Rais Kikwete pia ameunga mkono mwenendo wa mgombea urais wa CCM wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu inayoendelea nchini, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli, akisema: “Wamepata kuja watu kwangu… wakaniambia kuwa Mgombea wetu wa CCM anashutumu na kusahihisha Serikali yangu na utendaji wake kwenye mikutano ya kampeni. Niliwaambia  hivi…..analofanya Mgombea wetu ni jambo sahihi na barabara kabisa na lazima afanye hivyo.”


  Ameongeza Rais Kikwete: “Niliwaambia nchi yetu inahitaji mawazo mapya na mwelekeo mpya ulio tofauti na uongozi wangu. Niliwambia kuwa tuliporuhusu jambo hilo kufanyika, nchi yetu itabakia pale pale ambako nimeifikisha mimi. Haya yatakuwa na makosa makubwa kwa sababu nchi yetu lazima isonge mbele kwa mawazo mapya, kwa uongozi mpya na kwa staili mpya ya uongozi. Na haya ndiyo anayasema Mgombea wetu. 

  Vinginevyo ni jambo lisilokuwa na maana kubadilisha uongozi kama hatuko tayari kukubali kuwa kila kiongozi lazima awe na staili yake ya uongozi na namna yake ya kuongoza na kuendesha nchi yetu.”

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  24 Septemba, 2015
  0 0
 • 09/25/15--04:21: MJADALA KUHUSU UCHAGUZI MKUU
 • Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila azungumzia dhana ya ufisadi na aina za viongozi tunaohitaji kuwapatia Ikulu.https://youtu.be/ytmMOP7RTrE  

  Mwenyekiti wa DP Mchungaji Mtikila azungumzia umuhimu wa afya bora kwa wagombea uraisi kwani ni nafasi nyeti katika taifa.https://youtu.be/ku4Qb4R8b10   

  Mchungaji Mtikila awachambua wagombea uraisi wa CCM na Chadema na ahadi zao za kutoa elimu bure kama vipaumbele vyao.https://youtu.be/0Tr1Mt94Px0      

  Mchungaji Christopher Mtikila amkataa Lowassa asema ana mapungufu mengi yaliyowazi hivyo hamuungi mkono.https://youtu.be/KFT9QvTuwsU   

  Mwenyekiti wa DP azungumzia tafiti zilizofanywa na SYNOVATE  pamoja na TWAWEZA juu ya nani ana nafasi ya kushinda uraisi katika uchaguzi mkuu.https://youtu.be/NSk4stC7IBc   

   Mchungaji Mtikila anadi sera zake ili chama chake kiweze kupatiwa nafasi ya kuongoza nchini na kuleta mabadiliko ya kweli.https://youtu.be/KTRkmKmRIjc

older | 1 | .... | 651 | 652 | (Page 653) | 654 | 655 | .... | 1897 | newer