Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WANAFUNZI WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YA SAYANSI.

$
0
0

indexaNa. Jovina Bujulu –MAELEZO.Dar es salaam.
………………………………….
Wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi kote nchini wameshauriwa  kuongeza bidii katika kujifunza masomo hayo ili kuendana na  juhudi zinazofanywa na Serikali za kuwawezesha wanafunzi hao  kujifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo.
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samweli Manyele kwenye sherehe ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia  kwa mwaka 2013 na 2014.
 
“Kama wachunguzi wa Serikali ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya Kemia na Biolojia tumeona ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa hili kupenda masomo ya Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.Amesema Zoezi la kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na Biolojia limeanzishwa  kutoakana na Wakala ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani.
 
Aidha, amesema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze kuimarisha vipaji vyao vya masomo na matumizi ya kompyuta .
 
Amefafanua kuwa Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule mbalimbali za Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali zikiwemo Fedha, Vyeti na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya Sayansi kwa upande wa wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za kufundisha masomo hayo.Kwa upande wa Wanafunzi waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za Feza, Marian, Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanoro iliyoko jijini Mwanza.
 
Sherehe za kuwazawadia na kuwapa tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi zilianzishwa mwaka 2007  chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na utoaji wa zawadi na tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Bioloji.

viingilio Tamasha la Amani hadharani

$
0
0
images
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imetangaza kiingilio kwa VIP ni shilingi 5000 kwa watakaohudhuria katika tamasha hilo.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama viti vya kawaida watalipa shilingi 3000.
Msama alisema watoto watachangia shilingi 1000 ambako alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani katika nchi yetu.
Msama alisema katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali watasindikiza maombi hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagiza maombi hayo kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.
Aidha Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu, tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.
“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.

Alisema baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba 11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora), Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).

MAGUFULI ASEMA NA WAGOMBEA UBUNGE WA KASULU

Wanachama SHIWATA kunufaika na viwanja bure

$
0
0
indexc
MAKUNDI ya wasanii, wanamichezo na waabdishi wa habari wanaendelea kumiminika kulipia nyumba za bei nafuu baada ya Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kutoa viwanja bure katika kijiji cha Wasanii Mkuranga.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana kuwa ofa hiyo inamhusu kila mwanachama ambaye atapata nusu hekari miguu (25kwa 25)kama atakuwa amelipa sh. 200,000 za kujengewa msingi wa nyumba ya chuma kimoja kutumia matofali ya saruji.

“Tumeanzisha ofa maalum kwa wanachama wetu kupata kiwanja bure kama atakuwa amelipia benki sh. 200,000 za kumjengea msingi wa nyumba yake katika kijiji chetu Mwanzega Mkuranga ambako mpaka sasa kati ya hekari 300 tulizonazo za makazi ni hekari kumi tu zimejengwa nyumba 120,.” alisema Taalib.
 
Alisema katika misingi hiyo wanaotaka kumaliza nyumba zao gharama yake jumla itakuwa sh. 850,000 kwa nyumba ya chumba kimoja, sh. 3,800.000 kwa nyumba ya vyumba viwili na sh. 6,400,000 kwa nyumba vya vyumba vitatu na sebule.
 
Mwenyekiti Taalib alisema bado nafasi iko wazi kwa wasanii wanaotaka kuwekeza kwa kujenga shule, hospitali, kumbi za starehe na viwanja vya nmichezo wanakaribishwa.Alisema makundi ya wasanii ambao bado hawajajiunga na mtandao huo watapewa ofa ya kulipa sh. 70,000 kwa mtu mmoja katika vikundi na mmoja mmoja atajiunga kwa sh. 120,000 ambapo atapewa pia katiba ya mtandao huo.
 
Alisema wanachama wanaotaka kutembelea kijijini kumeandaliwa usafiri wa kila Jumamosi kwa nauli ya kwenda na kurudi ya sh. 10,000 kwenda kujionea maendelea ya kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

MAGUFULI AZURU KABURI LA ALIYEKUWA MWALIMU WAKE WA DARASA LA KWANZA BIHARAMULO

$
0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimian na ndugu wa Marehemu Cornel Pastory,alipowasili kwenye kijiji cha Nyakantutu,wilayani Biharamulo.Dkt Magufuli amemaliza mikutano yake ya kampeni mkoani Kigoma na kuelekea nyumbani kwake wilayani Chato kwa mapumziko ya siku mbili,ambapo siku ya jumapili atawahutubia Wananchi mjini humo na kisha kuanza ziara yake mkoani Kagera.
 Marehemu Cornel Pastory enzi za uhai wake
  Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza shule ya Msingi Chato, marehemu, Cornel Pastory. 
  Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.
  Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyakanazi waliokuwa wamefunga barabara wakitaka wamuone na kumsalimia sambamba na kumueleza matatizo yao ili aweze kuyatatua iwapo atapewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano 
 Wananchi wa Nyakanazi wakimsikiliza Dkt Magufuli kwa makini 
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi  kwa  wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera leo.

 Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Biharamulo mjini mkoani Kagera.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Biharamulo ili wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka hu.
 Wananchi wa Biharamulo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini humo jioni ya leo
 Wakazi wa Biharamulo wakishangilia mara baada ya kusikiliza sera za Dkt Magufuli mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa CCM mjini humo .

  Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Biharamulo, Oscar Mkassawakati wa kampeni hizo leo.

Sehemu ya wananchi wa Chato wakimlaki Dk Magufuli.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Magufuli akiwasili katika kijiji cha Kasanda wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma,ambapo alisimamishwa na wananchi waliokuwa wamefunga barabara wakitaka kusikilizwa kero zao.Dk Magufuli amemaliza ziara ya kampeni mkoa wa Kigoma na kuelekea mapumzikoni wilayani Chato,ambapo siku ya jumapili anatarajia kuhutubia wananchi wilayani humo.
 Baadhi ya wanakijiji cha Kasanda wakisubiri kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,alipokuwa akipita kijijini hapo kuwasalimia wakati akielekea mkoani nyumbani kwake wilayani Chato kwa mapumziki ya siku mbili akitokea mkoani Kigoma.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kasanda wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma,mara baada ya kumsimamisha wakitaka pia kusikilizwa kero zao.Dk Magufuli amemaliza ziara ya kampeni mkoa wa Kigoma na kuelekea mapumzikoni nyumbani kwake wilayani Chato,ambapo siku ya jumapili anatarajia kuhutubia wananchi wilayani humo na kuanza ziara yake rasmi ya kampeni mkoa wa Kagera.
 Wananchi wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia katika uwanja wa misheni Kakonko mjini mkoani Kigoma alipokuwa njiani akielekea nyumbani kwake wilayani chato kwa mapumziko ya siku mbili.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kakonko mjini kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa misheni mkoani Kigoma mapema leo mchana.Dkt Magufuli alikuwa akimalizia mikutano yake ya kampeni mkoani Kigoma wakati akielekea mapumzikoni nyumbani kwake wilayani Chato,ambapo siku ya jumapili anatarajia kuhutubia wananchi wilayani humo na kuanza ziara yake rasmi ya kampeni mkoa wa Kagera.
  Wananchi wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia katika uwanja wa misheni Kakonko mjini mkoani Kigoma alipokuwa njiani akielekea nyumbani kwake wilayani chato kwa mapumziko ya siku mbili.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM,Mgombea Ubunge wa jimbo la Buyungu Mh.Christopher Chiza,mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kakonko mjini kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa misheni mkoani Kigoma mapema leo mchama

MAMA SAMIA ALIVYOTEKA MIKINDANI NA MAFIALEO

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni, uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini, Murji Mohammed akiomba kura baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Wasanii wakichangamsha kwa muziki katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini, Murji Mohammed wakiwapongeza wasanii baada ya kutumbuiza muziki uliosisimua wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Kada nguri wa CCM, Kijana Mtera Mwampamba, akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimpongeza Mtela Mwampamba baada ya kuhutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 
 Vijana wakiwa wameparamia ukuta wa moja ya majengo ya kale, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara leo
 Mwanamuziki wa msanii wa Bongo Movie, Snura akichangamsha mkutano kwa kuimba wimbo wa kuifangilia CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakishiriki na wananchi wengine kuselebuka muziki, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkani Mtwara
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Wasanii wa kundi la Hapa ni Kazi Tu, wakionyesha umahiri wao walipotumbuiza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mratibu wa 'Mama Sema na Mwanao' Steve Nyerere akiwa na kamarade, Ally Choky, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia akiwa na mtoto aliyepoteana na mama yake, kutokana na wingi wa watu waliofurika wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgmbea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani, kikiwemo Chadema, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mama Samia akiungana na vijana kuishangilia CCM baada ya kuwapokea walipoamua kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Kimindani mkoani Mtwara leo
"'CCM Hoyeeeee" Kijana Rashid Njechele, akipaza sauti kwa kusema hivyo, baada ya kutangaza kuhamia CCM kutoka CUF, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia (kulia), uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa CCM, wakiwa katika ndege, wakati wa safari ya Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan kutoka Mtwara kwenda Kisiwa cha Mafia kufanya mkutano wa kampeni leo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akishuka kwenye Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mafia, alipowasili kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika kisiwa hicho leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Maa Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya viongozi waliomlaki kwenye Uwanja wa Ndege wa Mafia, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika kisiwa hicho leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia akisoma baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wananchi kueleza matumaini yao kwake, wakati wa mapokezi, alipowasili katika Kisiwa cha Mafia kuhutubia mkutano wa kampeni leo. Kushoto ni Mgombea wa Ubunge katika jimbo hilo, Mbarak Dau
 Aliyekuwa Mbunge wa Mafia ambaye pia aliingia katika kinyan'ganyiro cha kuomba ridhaa ya CCm kuwania tena ubunge wa jimbo hilo, Abdulkarim Shah, akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo, Mbarak Dau, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika katika Kisiwa hicho cha Mafia
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza Kada wa CUF, Mohamed Albadawi, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. Albadawi awali alikuwa Mgombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CUF baada ya kuongoza katika kura za maoni, lakini baadaye akaenguliwa na chama hicho na kupachikwa, Shomari Kimbau ambaye alihamia CUF baada ya kushindwa katika kura za maoni za CCM
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni leo katika Jimbo la mafia mkoa wa Pwani
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la MafiaMbarak Dau katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoa wa Pwani
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto), akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani.
 PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MKUTANO WA KAMPENI YA MGOMBEA WA URAIS CCM DK ALI MOHAMED SHEIN,JIMBO LA MKOANI PEMBA.

$
0
0
Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya mkutano vya Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba kwa ajili ya kampeni yake kwa wananchi wa Jimbo hilo la Mkoani.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Siasa jukwaa kuu baada ya kuwasili katikac viwanja hivyo kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya mpira Black Wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Mkutano wake wa Kampeni Jimbo la Mkoani Pemba.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM katika viwanja vya Mpira Black Wizard Chokocho Pemba ,
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, akizungumza na Wananchi wa Wilaya Mkoani Jimbo la Mkoani Pemba akiwatambulisha Viongozi waliofuatana na Dk Shein wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Pemba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Pemba Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Mberwa Hamad Mberwa akizungumza wakati wa Mkutano huo wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
WanaCCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya mpira Black Wizard Chokocho Pemba Wilaya ya Mkoani.
 Mhe Zainab Omar akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkoanni wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Chokocho, kumuombea Kura Rais wa Zanzibar Dk Shein kwa Wananchi wa Pemba ili kuendelea kupata maendeleo kupitia CCM.
Mhe Pandu Ameir Kificho akiwasalimia Wananchi wa Pemba Wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanbja vya Chokocho Mkoani Pemba.
Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Wana CCM katika mkutano wa kampeni wa CCM katika viwanja vya Black Wizard Chokocho Mkoani Pemba na kuwataka wananchi kumchagua Mgombea wa CCM Dk Shein.
Viongozi wa Jukwaa kuu wakiinua mikono wakati wa mkutano huo kuashiria kumpigia kura Mgombea wa Urais wa Zanzibar mgombea wa CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni.
Mhe Mohammed Aboud Mohammed akiwahutubia WanaCCM Kisiwani Pemba wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi kuelezea Sera za CCM na mafanikio yaliopatika katika Uongozi wa Rais Dk. Shein, na kuwataka kumchagua kwa mara ya Pili Dk. Shein kuendelea kuleta maendeleo kwa Wananchi wake katika sekta mbalimbali za Jamii Zanzibar
Viongozi wa Jukwaa kuu wakisimama wakati Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akipanda jukwaani kuwahutubia Wana CCM katika mkutano wake wa kampeni kisiwanin Pemba uliofanyika katika viwanja vya mpira vya black wizard mkoani Pemba.
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mkoani kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa Pili kisimwani Pemba kuomba ridhaa za kuchaguliwa tena kwa mara ya pili kuongoza Zanzibar kwa maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali za kijamii.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Pemba wakimshangilia Mgombea wa CCM Dk Shein wakati akiwahutubia katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba, wakati wa mkutano wake wa kampeni kisiwi humo.  
Mwanachama wa CCM akiwa katika viwanja vya kampeni akimsikiliza Mgombea wa CCM Dk Shein akiwa na picha ya mgombea Urais wa Zanzibar wakifuatilia mkutano huo.
Viongozi wa meza kuu wakifuatlia hutuba ya Mgombea wa Urais wa CCM Dk Shein wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya black wizard chokocho Mkoani Pemba.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mgombea wao wa CCM wakati akiwahutubia katika mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba katika viwanja vya black wizard chokocho Mkoani Pemba.
Viongozi wa Jukwaa kuu wakifuatilia mkutano wa kampeni wakati akihutubia Wananchi wa kisiwani Pemba katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, akiwahutubia Wananchi wa Pemba katika mkutano wake wa Kampeni kisiwani huo uliofanyika katika viwanja vya mpira black wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mkoani Pemba Profesa Makame Mbarawa,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya mpira black wizard mkoani Pemba. 
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Mtambile CCM Ndg Khamis Salum Khamis wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kiwani CCM Ndg.Rashid Abdalla,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Chambani Pemba Ndg. Mohammed Abdrahaman. Mwinyi,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mkoani Pemba. CCM Ndg Mmanga Mgengo,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mtambile Pemba. CCM Ndg. Mgaza Mohammed,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Chambani Pemba. CCM Bi.Bahati Khamis Kombo,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiwani Pemba. CCM Ndg Mussa Fumu Mussa,wakati wa mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwani katika Wilaya ya Mkoani Pemba kupitia CCM, kwa Wananchi na kuwataka kuwapigia kura ya Ndio wakati wa uchaguzi Mkuu mwezom Oktoba 2015. wakati wa  mkutano huo wa kampeni katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba
Mwanachama wa CCM akiwa na vyazi lake la kitenge la jengo la ASP wakati huo kwa sasa ni CCM akifuatlia mkutano huo, vitenge hivi vimetoka wakati wa miaka ya 70 kisiwani Zanzibar. 

Shekh akisoma dua baada ya kumalizikia kwa mkutano wa mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya black wizard chokocho
Viongozi wa jukwaa kuu wakiitikia dua baada ya kumalizikika kwa mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Wananchi wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa kampeni ya Urais kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM akisalimiana na Vijana waliohidhuria mkutano huo wa kampeni yake katika viwanja vya black wizard chokocho Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Kijiji cha Chokocho kisiwani Pemba baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni ya Urais katika Jimbo la Mkoani Pemba.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. zanzinews.com

WIZARA YA AFYA YAMTAKA MKEMIA MKUU KUFUATILIA MATUMIZI YA SIGARA YA KIKO YA MAJI (SHISHA)

$
0
0
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiagiza Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufuatilia matumizi ya sigara ya kiko ya maji (Shisha) katika kumbi za starehe  za hapa nchini kwa kuwa sigara hizo zinahusishwa na  matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya kemia na biolojia kwa mwaka 2013-2014 iliyofanyika leo Ijumaa (Septemba 18, 2015), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Dkt Donan Mmbando alisema hatua hiyo ni mkakati wa serikali wa kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Dkt Mmbando alisema  Wizara kupitia Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa mchango mkubwa wa uchunguzi wa kimaabara kuweza kutambua dawa za kulevya na pia kuwatambua waathirika wa dawa hizo.

“Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa kazi zinazofanywa na wakala wa maabara na mkemia mkuu wa serikali katika kulinda afya na usalama wa watu na mazingira pamoja na kuleta uelewano katika jamii” alisema Dkt Mmbando.

Aidha alisema serikali itaendelea kuitegemea Taasisi hususani katika utaalamu kwa utatuzi wa masuala yanayohusiana na kulinda afya na usalama wa jamii, hivyo itahakikisha inaiwezesha taasisi hiyo katika mahitaji ya rasilimalli watu na fedha.

Aidha Dkt Mmbando aliwapongeza walimu na wanafunzi wote waliofanya vyema katika mitihani yao na kuwakumbusha juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo yanaweza kufuta ndoto ya kuwa nguvu kazi ya taifa.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAKABIDHIWA PIKIPIKI TANO

$
0
0
 Mwakilishi  wa washirika la kuhudumia watoto Zanzibar (Save the children)  Mali Lisson akitoa maelezo kabla  ya kukabidhi pikipiki za wakuu wa vitengo vya mkono kwa mkono  katika hafla iliyofanyika  wizara ya  afya  mnazimmoja mjini zaznibar.
 Mwakilishi  wa Shirika la kuhudumia watoto Zanzibar (Save the children)  Mali lisson akimkabidhi funguo za pikipiki tano, Naibu waziri  wa  Afya  Mahmoud Thabit Kombo  kwa ajili ya wakuu wa vitengo vya mkono kwa mkono  wa wilaya katika hafla  iliyofanyika  wizara ya Afya  mnazimmoja  mjini Zanzibar.
 Naibu waziri wa Afya Mahmoud Thabit  Kombo akitia saini  baada ya kupokea pikipiki tano kwa ajili ya kuwarahisishia kazi  wakuu wa vitengo vya   huduma ya mkono kwa mkono wa wilaya.
 Naibu waziri  wa Afya  mahmoud Thabit Komba akizungumza na  wafanyakazi na wakuu wa vitengo vya mkono kwa mkono waliokabidhiwa pikipiki hizo.

picha zote na Miza Othman –maelezo zanzibar.
Pikipiki walizo kabidhiwa wakuu wa vitengo  vya mkono kwa mkono kwa ajili ya kuwasaidia shughuli za kufuatilia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto.

CHIKU ABWAO: HERI YA MONICA MBEGA WA CCM KULIKO MCHUNGAJI MSIGWA WA CHADEMA NAOMBA NICHAGUENI MIMI SAFARI HII

$
0
0
MGOMBEA  Ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia ACT Wazalendo Bi Chiku Abwao(pichani) amesema heri ya miaka mitano ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mobica Mbega ( CCM) kuliko miaka mitano ya Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)hivyo ametawa mwaka huu wananchi kumchagua yeye

Akizungumza katika mkutano wake wa kampeni za Ubunge jana  kata ya Kihesa alisema iwapo atakuwa mbunge wao atahakikisha anakuwa mbunge wa mfano wa kuwaletea maendeleo sahihi.

Kwani alisema kuwa historia ya jimbo hilo mwaka 1995 walichagua NCCR mageuzi ambapo Bw Mfalamagoha Kibasa kuwa mbunge ila baada ya kushindwa kutekeleza ahadi zake mwaka 2000 walimchagua Monica Mbega ( CCM) ambae kipindi cha kwanza alifanya Kazi vizuri na mwaka 2005 wananchi walimchagua tena ila hakuweza kufanya Kazi ndipo walipomchagua Mchungaji Peter Msigwa( Chadema) ambae hajafanya Kazi yoyote.

Hivyo  alisema  kwa  sasa imani yake  juu ya  wanaume  kuwa  wabunge  katika   jimbo  hilo haipo  tena kwani hawana nia ya  kweli ya  kuwatumikia  wananchi na  kudai kuwa  iwapo  mbunge  aliyemaliza  muda  wake mchungaji Msigwa angetekeleza ahadi  zake vema  leo asingesimama kugombea  ubunge bali  angemuunga  mkono mbunge   huyo ili  aendelee  kwa  kipindi  cha  pili  ila kwa  kuwa hakuna jipya  alilolifanya hana imani nae na  hivyo ni  wakati wa  wananchi wa  jimbo  hilo  kuwapima wagombea  wengine waliojitokeza nje  ya mbunge  huyo .

Alisema ahadi  za  mbunge  aliyemaliza muda  wake  zilikuwa zaidi ya 14  ikiwemo ya  kuwawezesha wananchi  waliojiunga katika  vikundi  kupatiwa  mitaji ya  kuanzisha  biashara  kwa  wakati  huo  alisema  yeye  si mbunge  wa  kutoa pesa bali atawawezesha  kiuchumi kwa  kuwapa nyavu  (mitaji) ila baada ya  kuwa mbunge alianza  kuwasema  vibaya  wananchi kwa kudai yeye  si mbunge wa  kutoa  pesa (ATM)pia  aliahidi  ujenzi  wa  soko la kisasa  Kihesa  na  kumweka mwanasheria  katika  ofisi  yake  ila hadi  sasa hakuna alichofanya na  akikumbushwa  hukimbilia  kujenga  chuki na  kila mtu .

Bi  Abwao  ambae  amepata  kuwa  mjumbe wa kamati  kuu ya Chadema  Taifa na  mbunge  wa viti maalum  mkoa  wa Iringa  kupitia Chadema  alisema  kuwa hali ya chadema na UKAWA  kwa  sasa  imepoteza mwelekeo na  chadema kugeuka ni  chama  cha kutetea  mafisadi   tofauti na  iliyokuwa awali kuwa chama cha  kupinga  ufisadi .

Hivyo  alisema  sababu ya  kukihama  chama  hicho na  kujiunga na ACT  wazalendo ni kutafuta  chama cha  upinzani makini ambacho atawatumikia wananchi  bila ya kuwajengea maswali kama  ilivyo  hivi  sasa kwa  mgombea  wa Chadema Iringa mjini mhungaji Msigwa ambae alikuwa mbele  kupinga ufisadi na hata  kusema  wanaomuunga mkono aliyekuwa  waziri  mkuu Edward  Lowassa ambae ni mgombea wa Chadema kwa  sasa wakapimwe akili  zao .

Alisema Chadema  kwa  sasa  imekuwa ni  chama  cha kupiga  dili akiwemo  aliyekuwa  mbunge wa  jimbo hilo Mchungaji Msigwa ambae leo kati ya maswali magumu ambayo anahojiwa  na  wapiga  kura  wake ni  juu ya kauli  yake  dhidi ya wale  wanaomuunga mkono  LOwasa  kutakiwa  kupimwa akili  zao.

Akielezea  kuhusu  sera  zake  kwa  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini iwapo  watamchagua  kuwa mbunge  wa  jimbo  hilo atahakikisha anautumia  vema  mfuko  wa  jimbo kwa  kuwasaidia  wazee ,vijana na  wanawake  kuwa na  vikundi  vya kiuchumi tofauti na  ilivyokuwa awali miaka  mitano iliyopita  kwa  mfuko  huo kushindwa  kufanya kazi  yoyote.

Pia  kuhakikisha  anaibana  serikali  ili vijana  kupewa mikopo  nafuu na  kuzuia posho kwa  watumishi  wa umma ambazo  zimekuwa  zikikwamisha maendeleo katika  jimbo  hilo .

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro yaipiga jeki taswa katika tuzo za Wanamichezo Bora

$
0
0
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA),  imetoa Sh. 10, 486,000 kwa ajili ya kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. 

Tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA zinatarajiwa kufanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo pia TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa sekta ya michezo katika uongozi wake. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo, alisema wameamua kusaidiana na TASWA kwa sababu Rais Kikwete ni mdau mkubwa wa michezo na pia wa masuala ya utalii. 

‘’Dk. Kikwete ni mdau mkubwa  wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani kwa kipindi chote ambacho amekuwa Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ametembelea hifadhi hii  mara nyingi zaidi kuliko viongozi wengine wote wa Taifa letu waliomtangulia. 

‘’Pia amekuwa mdau muhimu na wa mstari wa mbele wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika  kutangaza vyema vivutio vya watalii vya hifadhi ya Ngorongoro katika mataifa mbalimbali duniani alikokwenda kwa ziara za kikazi. 

‘’Jambo hili limeleta watalii wengi nchini kutoka mataifa  mbalimbali dunini. Vile vile ziara zake za mapumziko hifadhini wakati wa sikukuu mbalimbali zimewahamasisha sana  Watanzania walio  wengi kutembelea  hifadhi hii kutoka kote nchini na hata nchi jirani,’’ alisema Akyoo. 
Pia alisema waandishi wa habari ni wadau wakubwa na muhimu katika harakati za utalii na ndiyo sababu wameamua kuisaidia TASWA ifanikishe shughuli yake. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru mamlaka ya hifadhi hiyo na kusema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuomba wadau wengine waungane nao kufanikisha jambo hilo. 
‘’Kama tulivyosema bajeti yetu ni Sh milioni 130, juzi (Jumatano) tulipata watu wa GSM Foundation waliotupa Sh. Milioni 50, tunaomba na wengine tushirikiane nao katika hili,’’ alisema Mhando. 

Alisema TASWA imeamua kuandaa hafla ya wanamichezo kumuaga Rais na pia kumpa tuzo kwa vile wakati wa uongozi wake amefanya mambo makubwa katika sekta ya michezo. 
Kwa mujibu wa Mhando, wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na TASWA kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, mwaka huu.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WA AFRIKA KUSINI SIPHO MWAKABANE KUSHIRIKI TAMASHA LA KUOMBEA AMANI OKTOBA 4 MWAKA HUU.

$
0
0
 Mwenyekiti wa  kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusina na Msanii wa Afrika Kusini,Sipho Mwakabane ambaye atatumbuiza katika tamasha  Oktoba 4 mwaka huu. Pia amesema kuwa msanii huyo wa nyimbo za Injili wa kimataifa. Na kulia ni Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga.
Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salam amesema kuwa watanzania wote bila kujali kabila, rangi na dini zote wajitokeze katika tamasha hilo la kuombea amani ambapo viingilio ni sawa na bure kabisa watu wazima kwa nafasi ya VIP wataingia kwa shilingi elfu tano (5000), kawaida elfu tatu (3000) na watoto ni shilingi elfu moja(1000)
Baadhi ya waandishi wa habari wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mwenyekiti wa  kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama leo jijini Dar es Salaam.
 
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Afrika kusini, Sipho Mwakabane kuwa atashiriki tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili uwe wa amani na utulivu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama.
 
 
Msama alisema watoto watachangia shilingi 1000 ambako alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani katika nchi yetu.
Msama alisema katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali watasindikiza maombi hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagia maombi hayo aidha Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu, tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.
 
"Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais," alisema Msama.

Alisema baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba 11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora), Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).

BENKI YA DCB YAKUTANISHA VIONGOZI WA SACCOS JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BENKI ya DCB imekutanisha viongozi wa  mifuko ya kuweka na Kukopa (SACCOS) kuweza kuwapa fursa mbalimbali zilizopo katika benki hiyo.
Akizungumza na viongozi wa SACCOS,Meneja Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa,Haika Machaku,amesema benki ya DCB iko karibu na SACCOS katika kupata fursa za utuzaji wa Amaana na huduma mbalimbali kwa gharama  nafuu.

Amesema wataendelea kushirikiana  na SACCOs kuangalia watavyoweza kusaidiana katika kuimarisha saccos pamoja na wanachama kunufaika na mikopo katika benki hiyo.

Aidha amesema kuwa  nia ya benki kuahakikisha wanachama wananufaika na benki  katika kuendeleza maisha kupitia fursa ambazo benki imeanisha kuinua wajasiriamali  pamoja na ushirika ikiwemo SACCOS.

Benki imewataka viongozi wa SACCOs  kufungua akaunti katika benki hiyo katika kuweza kuanza kufanya kazi  kwa ushirikiano na fursa zao ziweze kuwafikia wanachama.
 Meneja wa Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB,Machaku,akizungumza na viongozi mbalimbali wa Saccos juu  ya fursa zinazopatikana katika benki ya DCB leo Makao Makuu ya DCB jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko wa Benki ya DCB, Boyd Mwaisame akizungumza na viongozi wa SACCCOs  jinsi watavyoshirikiana katika kuinua SACCOs,leo Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa SACCOS ya Wafanyakazi wa TRL,Gwammy Mwakangale Akichangia maada katika mkutano wa DCB  juu ya faida zinaziopatikana katika benki hususani mikopo ya nyumba leo Makao Makuu ya DCB,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki  ya viongozi wa SACCOs wakiwa katika mkutano ulioitishwa na benki ya DCB kuwapa fursa zinazopatikana katika benki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

BARAZA LA VYUO VIKUU AFRIKA MASHARIK(IUCEA)KUWA NA MAONESHO YA VYUO VIKUU UGANDA

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(IUCEA)Profesa Mayunga Nkunya akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha jana kuhusu hali ya wahitimu katika nchi za Afrika Mashariki na ushirikiano wa Baraza la Wafanyabiashara Afrika Mashariki(EABC) kuwajengea uwezo wahitimu ili kumudu soko la ajira .Taasisi hiyo itakuwa na maonesho ya vyuo katika nchi za EAC  Kampala ,Uganda mwezi Oktoba ,2015.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki(EABC)Lilian Awinja akizungumza katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini kwaajili kuuhabarisha umma.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

MBOWE ATAKA KAMPENI ZA KIISTARABU

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kila chama kifanye  kampeni za kistaarabu ili kila mtu aende Ikulu  pasipo kuvuruga amani.

Mbowe ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuelezea masuala ya kampeni zinazoendelea kwa vyama vyote vya siasa, pia amesema kuwa kuna kauli za viongozi wa baadhi ya vyama ambazo haziridhishi katika kupiga kwao kampeni.

Mbowe amasema kauli ya watu hao ni ya kichochezi na haiwezi kuvumilika lakini chama husika hakikuweza kufuta kauli hiyo.

Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekaa kimya kwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyama kuwa hawawezi kuachia watu wakatawale Ikulu.

Amesema kumekuwa na changamoto katika umoja wa katiba ya wananchi lakini hadi sasa mgogoro wa majimbo hauzidi 10 ambapo ni hatua nzuri kwa umoja huo nia yao ni kwenda Ikulu na sio kuwagwana majimbo kama sadaka.

Mbowe amesema tatizo la viongozi waandamizi  NCCR-MAGEUZI, inatokana na kutaka majimbo wasimame licha kutambua mtu anapewa kugombea  kutokana na sifa alizonazo  pamoja na uwezo wa mtu kushinda katika uchaguzi mkuu.
 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani)juu hali ya kampeni inayoendelea kwa baadhi ya vyama kushindwa kufanya kampeni za kiistarabu leo Ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Afisa Habari wa Chama hicho,Tumaini Makene.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Freeman Mbowe leo makao makuu ya ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo.

KONGAMANO LA WAJASIRIAMALI WANAWAKE NCHINI LAFANA

$
0
0
 Meneja wa Mpango wa  Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (katikati) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi katika Kongamano la Wajasiriamali Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi wa Mfuko huo Bi Matilda Nyallu. 
 Meneja wa Mpango wa  Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (katikati) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi katika Kongamano la Wajasiriamali Wanawake nchini  kabla ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa katika Banda la Mfuko huo wakati katika Kongamano la Wajasiriamali Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana), wa kwanza kulia ni Meneja wa Mpango wa  Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe.

 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi akizindua Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini lililofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida Waziri
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi akimlisha keki Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida Waziri katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini mara baada ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania. (Picha na Benjamin Sawe)

MGOMBEA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU (CCM) YUSUF MANJI AZINDUA KAMPENI ZAKE DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

 Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia (kulia), akimtambulisha Yusuf Manji katika uzinduzi huo.
 Mgombea nafasi ya udiwani Kata ya Mbagala Kuu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Manji (kushoto), akihutubia wananchi na makada wa chama hicho katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika eneo la Kichemuchemu Kaskazini Dar es Salaam leo jioni.
  Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia, akihutubia katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Umati ukimsikiliza Yusuf Manji.
 Mchumi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Urio akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Kada wa CCM, Godbertha Kinyondo akisalimia wananchi kwenye uzinduzi huo.
 Makada wa CCM wakiserebuka
 Vijana wa hamasa wa CCM wakiwa kazini.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Michango mbalimbali ikitolewa.
 Mkazi wa eneo hilo, Sharifa Ali akimueleza Manji kuhusu kero ya kutokuwa na soko.
 Dogo akihubia kwenye uzinduzi huo. Dogo huyo alisema wana CCM wanapaswa kumchagua Magufuli kuwa Rais, Mbunge Mangungu na Diwani Manji.
 Chipukizi wakifanya vitu vyao.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Yusuf Manji (kulia) akifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo. 

MKUTANO WA KAMPENI ZA URAIS ZA UKAWA MJINI BUKOBA LEO.

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mmoja wa wadau wa Mabadiliko, Prof. Azaveli Rwaitama, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Aliekuwa Meya Mji wa Bukoba, Anatory Amani akizungumza kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.








Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza na baadhi ya vingozi, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi, Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Wananchi wa Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera wakimshangilia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye eneo la Mkutano.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Nkenye, Misenyi Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Bw. Simon Andrew (55) ambaye ni Mlemavu wa miguu, mkazi wa Kijiji cha Kilimilile, Kyaka Wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera leo Septemba 19, 2015.

 Umati wa Wananchi wa Mji wa Bukoba ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Aghakhan kuhudhulia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi Bukoba waliofika kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi baadhi ya wagombea wa Udiwani wa vyama vinavyouda UKAWA, kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza, Mh. Ezeckiel Wenje akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mke wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, akimuombea Mumewe Kura kwa Wananchi wa Mji wa Bukoba, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimpongeza Mke wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Bukoba.

Diamond motors yaboresha usafiri wa masafa kwa matumizi ya Fuso.

$
0
0


Wiki ya nenda kwa usalama ni muhimu katika jitihada za kuboresha masuala ya usalama barabarani ikiwa ni jambo lililo na kipaumbele katika ajenda za kitaifa nchini Tanzania. Wiki hii inatoa misingi ya kufanya kazi kuelekea katika kufikia maono na matarajio ya mazingira salama na kuboresha usalama barabarani. 

Hivi karibuni mwenyekiti wa tume ya usalama barabarani bwana Elifadhili Mgonja wakati akiongea na waandishi wa habari katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama jijini Dar es salaam yaliyo fanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mwaka 2015/16 alisema kuwa ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo kikuu cha kupoteza maisha na mali nchini Tanzania.  Ajali hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha vifo na ulemavu ambao unasababisha kudumaa kwa maendeleo ya watu kiuchumi na kuathili uchumi wa taifa kwa ujumla. 
Upigaji vita ajali za barabarani nchini limekuwa ni suala linalopewa kipaumbele kwani ajali mbaya zimekuwa zikiendelea kutokea. Pamoja na sababu nyingine, miundombinu mibovu, uchovu kwa madereva, uchakavu wa magari kama kukosa breki kutokana na kutokuwa na matengenezo imekuwa ni chanzo kikuu cha ajali mbaya nchini Tanzania. 
Kwa nyakati tofauti, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni katika ofisi za kampuni ya Diamond Motors Ltd (Hansa) iliyopo katika barabara ya Nyerere, meneja mkuu (masoko) wa kampuni hiyo Ndugu Laurian Martin aliwaasa watanzania kuweka kipaumbele katika “usalama kwanza”.  Aliongeza kwa kusema kuwa utumiaji wa magari yaliyoboreshwa katika teknolojia ambayo kwa sasa yanapatikana katika soko la Tanzania kama vile malori ya Fuso FZ an Fuso FJ  yanatoa nafasi kubwa ya kupunguza ajali za barabarani.  

Martin aliongeza kusema kuwa “Malori ya Fuso FZ yanauwezo mkubwa wa breki zenye ukubwa, upana na unene unaolingana katika magurudumu ya mbele na ya nyuma, pia ina kifaa cha kujazia upepo pamoja na matanki ya kuhifadhia yanayokuhakikishia usalama wa hali ya juu katika miundombinu ya Tanzania na masafa marefu. Malori haya pia yana vifaa maalumu sehemu ya mbele kwaajili ya kuzuia gari isianguke na kubilingika  kirahisi ikiwa ni pamoja na mfumo wa matairi mpana unaoongeza ustahimilivu.  Hivi ni vipengere muhimu sana hasa katika barabara mbovu na uendeshaji wa hali iliyokithili. 

Bwana Martin aliendelea kwa kusema kuwa uchovu kwa madereva pia unachangia katika ajali za barabarani hasa katika uendeshaji wa masafa marefu.  Malori ya Fuso FZ kutoka Diamond Motors yana kibini iliyo ninginizwa vizuri katika mihimili yake ambayo inasaidia kupunguza mtikisiko hasa katika matuta ya barabarani, haipati joto wala makerele kutoka kwenye injini, pia ina kiti ambacho kina rekebishika pamoja na usukani unaoweza kurekebishika.  Vipengele hivi vinampatia dereva unafuu wa kuendesha ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa kusababisha ajali.
Usalama barabarani ni muhimu sana kwa watanzania na hii inadhihirishwa kwa uwepo wa wiki hii ya nenda kwa usalama nchini Tanzania ikiwa ni nia thabiti ya kupunguza ajali za barabarani. Muunganika wa sababu mbali mbali za kiusalama ukizingatiwa inaweza kupunguza ajali za barabarani. Usimamizi wa usalama barabarani  kutoka kwa washikadau wa sekta hii, mafunzo muafaka kwa madereva ikiwa ni pamoja na utumiaji wa magari yaliyoboreshwa kwa ubora kama vile Fuso FZ na Fuso FJ ambayo hayahitaji matengenezo ya mara kwa mara na yametengenezwa kwa teknolojia iliyoboreshwa katika kumpunguzia dereva uchovu na ubora wa kuhimili miundombinu ya Tanzania inaweza kuchangia katika uboreshaj wa usalama barabarani.

FZ TRACTOR 6x4

Kuhusu Diamond Motors Limited (Hansa Group)
Diamond Motors Limited imekuwa wasambazaji pekee wa malori ya Fuso nchini kwa zaidi ya miaka 30. DML imeweka rekodi katika secta ya magari, kwa kufanya kazi kwa ushirikaino na makampuni ya magari yenye ubora wa hali ya juu zaidi duniani. Ushirika wao imara na makampuni yanayoongoza duniani kama vile magari ya abiria ya Mitsubishi kutoka Japani, matairi ya Yokohama kutoka Japani, MTU na ZF kutoka Ujerumani yameleta umaarufu na kutoa uwanja mpana wa wateja kutoka sehemu mbali mbali za ukanda huu. 

<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Diamond Motors rolls out the new Fuso FZ in ‘Ndiyo Fuso ni Faida’ campaign

Transport sector is an important component of the economy and a common tool used for development because of its intensive use of infrastructures. This is even more so in Tanzania’s economy where economic opportunities are increasingly related to the mobility of people, goods and service. It is with this factors in mind that Diamond Motors (Hansa Group) has introduced a New Fuso heavy-duty truck range of Fuso FZ which offers more benefits in terms of efficiency, operation costs and suitable for the nature of Tanzania’s infrastructures.

Diamond Motors Limited has been playing a major role in the transportation sector since 1980 in Tanzania by the distribution of Mitsubishi Fuso trucks and Bus Corporation.A new range of Fuso FJ and Fuso FZ encompasses exceptional functionality, durability, and comfort, giving customers an entirely new breed of trucking technology.  Fuso heavy- duty trucks delivers lower operating costs, making them the best choice for smart businesses. Trucks ideal for long distance and heavy loads with high torque engines optimized for power and maintain being economy to provide profitable transportation facility.

The ongoing campaign of “Ndiyo Fuso ni Faida” in various regions in Tanzania aims at bringing awareness to stakeholders of different sectors of the economy on the benefits by the use of new Fuso truck which are of latest technology, in terms of capability, reliability, economy and long distance travelling as well as characteristics from the in-built specifications which are beneficial to the user. The 170kW/810Nm engine is more fuel efficient, for better mileage and lower costs and other long-haul applications.

Diamond Motors Limited has been servicing this sector through Mitsubishi Canters and Light trucks over the past few decades. Backed with after sales and spares support, the product portfolio is amply suited and tailored to meet the requirement and demands for this sector, and become the total transport solution provider in Tanzania.

      FZ

.

With Fuso Value Parts, you are assured of authentic parts of the highest precision manufacturing guaranteed by Mitsubishi Fuso, without having to pay a premium. For excellent value at approachable prices, Diamond Motors Limited has made the choice easy. The availability of the required genuine parts determines the downtime of your vehicle. Turn to your Mitsubishi Fuso dealer for quick supply of the genuine parts needed to keep your truck running, reliable consultation and the quality of the service network determine how well and how long your truck performs while a trust to our trained technicians ensures high quality.

ABOUT DIAMOND MOTORS LIMITED (Hansa Group)
Diamond Motors Limited has been the exclusive distributor of Fuso trucks in the country for over 30 years. DML has set the bar in the automotive industry, working with some of the world’s best vehicle brands. Its strong partnerships with global leaders such as Mitsubishi passenger vehicles from Japan, Yokohama tires from Japan, MTU and ZF from Germany have proven to be popular, with a diverse range of customers from all across the island.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Sipho Makhabane kulipamba tamasha la Amani Tanzania

$
0
0
 Mwenyekiti wa tamasha la kuliombea Taifa Aman pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo wakatio wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 19 kuhusu maandalizi ya tamasha hilo. Kulia ni Mratibu wa tamasha hilo, Hudson Kamoga. (Picha na Francis Dande)
Mratibu wa Tamasha la kuombea amani nchin na uchaguzi mkuu, Hudson Kamoga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo, litakalofanyika Oktoba 4 Uwanja wa Taifa jijini. Kushoto ni Mkurugenzi Msama Promotions, Alex Msama. 


BAADA ya kumtangaza Mchungaji Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini kuimba kwenye tamasha la kihistoria la kuliombea Taifa la Tanzania Kampuni ya Msama Promotions imemtangaza mwimbaji mwingine wa nchi hiyo, Sipho Makhabane kumsindikiza mwenzake katika tamasha hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa mwimbaji huyo amethibitisha kujumuika na waimbaji kutoka nchi mbalimbali katika tukio hilo muhimu la kuliombea taifa la Tanzania.

Msama alisema kuwa kutokana na ukaribu na uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili Tanzania iliisaidia nchi hiyo kupata uhuru miaka ya nyuma hivyo wameona wawaalike waimbaji hao mahiri.

Tamasha hilo la kusifu na kuiombea Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, inatarajia kushirikisha waimbaji kutoka nchi za Zambia, Kenya, Uingereza, Afrika Kusini na Rwanda.
Msama alisema kuwa tamasha hilo linatarajia kufanyika mikoa 10 ambako alifafanua kuwa kutokana na tamasha hilo kutokuwa na wadhamini wameweka viingilio kwa VIP ni Sh. 5000, kawaida Sh. 3000  na watoto Sh.1000.


Mkurugenzi huyo alisema watanzania watambue kuwa baada ya uchaguzi kuna maisha mengine hivyo kutokana na kipindi hiki kigumu Watanzania kuunganisha nguvu ya pamoja na kujitokeza kwenye tamasha hilo ili waiombee nchi yao amani iliyopo iendelee kudumu hata baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.

“Maandalizi ya Tamasha la kusifu kuombea nchi amani yanaendelea vizuri, waimbaji wengi watakuwepo kutoka nchi mbalimbali wote kwa pamoja wataimba wimbo mmoja ukiwa ni kwa ajili ya kuiombea nchi yetu amani,” alisema Msama.

Msama aliwataja waimbaji wengine ambao waliothibitisha kuimba katika tamasha hilo ni pamoja na Sarah K  na Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Ifeanyi Kelechi (Uingereza) huku kwa upande wa Tanzania ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu, Rose Muhando, Christopher  Mwahangila, Bonny Mwaitege, Danny Bulenge, Atosha Kissava na Jesca BM.

Naye mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Hudson Kamoga alitoa wito kwa watanzania kujitokeza huku akisisitiza kuwa uchaguzi unaotarajia kufanyika ni msingi wa kuwaleta pamoja watanzania.
Alisema kuwa kamati imejiandaa vizuri pia kutakuwa na nyimbo za kumsifu Mungu hivyo watanzania watarajie kupata  kilicho bora katika maombezi hayo ya kuliombea taifa.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images