Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU UHURU, HAKI NA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU LEO TAREHE 17.09.2015

$
0
0
SISI, viongozi wa dini pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi (NEC, TAKUKURU, Polisi pamoja na Msajili wa vyama vya siasa)  tuliokutana leo tarehe 17/9/2015, tumepata nafasi ya kujadili kwa kina suala la uhuru,haki na amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 25/10/2015 na wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa uhuru,haki na amani vinalindwa kipindi hiki.Suala la uhuru haki na amani ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla na halina mjadala.Kila mmoja achukuwe nafasi yake kulinda uhuru,haki na amani na kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vya siasa.

Viongozi wa dini wamepata nafasi ya kujadili na vyombo hivi masuala ya msingi kama kuhakikisha kuwa maadili ya uchaguzi yanazingatiwa kwa wote, muda wa kutangaza matokeo ya kura unazingatiwa , haki ya wananchi kupata matokeo haraka ili kuepuka fujo wakati wa kusubiri na kutangazwa kwa matokeo. Jeshi la polisi kutokutumia nguvu kupita kiasi, wajibu wa Msajili kuhakikisha vyama vyote vinapata fursa sawa na pia tumejadili suala la kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya jukwaa la siasa.

Viongozi wa dini tumekubaliana kwa pamoja kuepuka kutumia nyumba za ibada kuonyesha ushabiki wa aina yoyote kwa chama chochote cha siasa.
Baada ya kujadili kwa kina masuala hayo viongozi wa dini wanatoa wito ufuatao;
1. Vyombo vya habari vifanye kazi kwa ueledi bila upendeleo na pia kuhakikisha kuwa inatoa taarifa ya kutosha kuelimisha umma.
2. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo  iweke utaratibu maalum wa kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha pamoja na watu wote waliojiandikisha/watakaojiandikisha waweze kupiga kura.
3. Tunaishauri  NEC    kwenye chaguzi zijazo  siku ya kupiga kura isiwe siku ya ibada.
4. NEC iendelee kutoa elimu ya uraia  kuhusu haki ya raia kupiga kura na haki yao ya  kukaa mita mia moja kusubiri matokeo yatangazwe kwa utulivu kama ambavyo NEC imehakikishia viongozi wa dini kuwa kila kituo itabandika matokeo yote (Urais,Ubunge na Udiwani)
5.  Pamoja na kutimiza wajibu wake wa msingi wa kulinda raia na mali zao Jeshi la polisi wakati huu wa uchaguzi  liendelee kutimiza wajibu wake wa kusimamia amani na taratibu kwa haki bila upendeleo.

6. Wagombea,wafuasi   na wanaowanadi,  wanaaswa waache mara moja lugha za matusi,vitisho,kejeli na kukashifiana vinavyoweza kuchochea fujo na kuleta uvunjifu wa amani wajikite kunadi sera za vyama vyao.
7.Tunawahimiza wananchi kuwa makini katika kufuatilia kampeni na sera mbalimbali za wagombea, kuzipima kwa hali ya juu sera hizo, kutokuuza kadi zao za kupigia kura, kutokununuliwa na kujitokeza kwa wingi kutumia uhuru na haki yao ya kuchagua viongozi wanao wataka kwa hiari na  amani.
 8. Viongozi wa dini wanawahimiza Watanzania wote kuendelea kuombea nchi hii kuendelea kuwa  taifa lililojengwa   katika misingi ya uhuru , haki na amani.

9. Viongozi wa dini tutabaki kuwa manabii na wahubiri wa uhuru,haki na amani wakati huu , wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
Sisi viongozi wa dini Tunawashukuru Inspekta generali wa polisi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ufafanuzi makini na wa kina juu ya nafasi na utayari wao wa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha uhuru, haki na amani vinaendelea nchini.Maelezo yao na mafafanuzi  yao tumeyasikia  na tutaendeleza kwa kuwa  hiki ni kikao cha mwanzo na tutaendelea kuwa na vikao vingine pamoja nao kuelekea uchaguzi mkuu ili kufuatilia utekelezaji na kuendeleza makubaliano yetu katika kuhakikisha uhuru,haki na amani.

MAMA WA MKE WA WAZIRI MKUU TUNU PINDA AZIKWA JIJINI DAR

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  akimfariji Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kuhosto) ambaye alifiwa na Mama yake , Hajjat Pili Mlolwa Rehani, nyumbani wa marehemu, Tanata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015. Kuliani  Mama Hasina Kawawa.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba Wapili kushoto na Mama Hasina Kawawa  waliokwenda kumfariji kufuatia kifo cha Hajjat Pili Mlolwa Rehani,Mama wa Mama Tunu , nyumbani kwa Marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015.
  Baadhi ya waomboezaji walioshiriki katika mazishi ya Hajjat Pili Mlolwa Rehani, Mama Mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, nyumbani kwa marehemu jijini Dar es salaam, Septemba 17, 2015.
 Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani   ambaye ni mama wa Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Mama Hasina Kawawa,watatu  kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.

  Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi  akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani   ambaye ni mama wa   Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015.   Kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.
  Makamu wa Rais Mohammed Bilal akishiki kubeba jeneza  lenye mwili wa Hajjat Pili  Mlolwa Rehani,mama yake Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika sala ilitofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salam Septemba 17,2015.
 Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Hajjat Pili Mlolwa Rehani,Mama wa Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda katika mazizi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es slaam Septemba 17, 2015.
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika mazishi ya Hajjat Pili Mlolwa Rehani, Mama wa mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda  wakiwa nyumbani kwa marehemu Tabta Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015.Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka , Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

KIAMA CHA MAJANGILI CHAJA, BATHAWK YAZINDUA NDEGE MAALUM KUPAMBANA NAO ​

$
0
0
Ndege aina ya Super Bat DA-50

Na Daniel Mbega, Mkomazi
Ni majira ya saa tatu asubuhi Jumatano, Septemba 16, 2015 wakati tunawasili kwenye uwanja mdogo wa ndege (air strip) katika eneo la Kisima ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi inayotenganisha mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.
Uwanja unaonekana mweupe, hakuna ndege! Nikashangaa kwa sababu wenyeji wetu kampuni ya Bathawk Recon wametuambia tunakuja kushuhudia uzinduzi wa ndege maalum zinazopambana na ujangili.
Kilichoonekana mbele yetu ni hema kubwa ambalo mbele yake kulionekana minara midogo iliyosimikwa kama fimbo. Kwenye banda kubwa ikaonekana ndege ndogo aina ya Twin otter. Nikadhani ndiyo inayozinduliwa, lakini Idrisa Jaffary, mwenyei wetu tuliyekuwa naye kwenye gari akasema, hapa siyo hiyo.
Mshangao ukanipata baada ya gari kusimama wakati nilipokiona kifaa mfano wa ndege kikiwa kimeegeshwa kwenye bomba maalum kana kwamba ndege inataka kupaa.
Kama nisingekuwa nazifahamu ndege hizi maarufu kama drones, ningeweza kusema kwamba huo ni mdoli ambao mwanangu angefurahia kama ningempelekea akauchezea.
Kwa siku za karibuni zimekuwa maarufu kwani zinatumika kupeleka misaada mbalimbali hata katika maeneo hatari ya vita ambako hakufikiki kirahisi.
“Hii ndiyo ndege yenyewe,” Idrisa akatueleza. “Hee! Ndiyo hii?” tukajiuliza kwa mshangao. Kwamba Tanzania tumeanza kuitumia teknoloia hii yanaweza kuwa maendeleo mengine mapya.
Mshangao wetu ulimalizika wakati Phil Jones, ofisa mwendeshaji wa mitambo hiyo kutoka kampuni ya MartinUAV ya Marekani iliyotengeneza ndege hiyo aina ya Super Bat DA-50 UAV, alipoanza kutuelezea namna ‘ndege’hiyo (drone) inavyofanya kazi huku akituonyesha kila sehemu na kazi yake.
“Hii ni ndege ambayo haihitaji kuwa na rubani, inaongozwa kwa kompyuta maalum, ina antenna mbili, ina kamera maalum ambazo zinaweza kupiga picha usiku na hata mchana,” akatueleza.
Akasema ndege hiyo ina uwezo wa kuruka urefu wa futi 20,000 kutoka usawa wa bahari na kwenda katika nusu kipenyo cha kilometa 35 kutoka ilipo mitambo ya kuiongoza.
Jones, ambaye baadaye alinieleza kwamba yeye rubani wa zamani wa ndege za kijeshi katika Jeshi la Uingereza aliyestaafu mwaka 2014 ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, akasema ndege hiyo inayorushwa kwa mtindo wa manati (catapult launch system), inaweza kuruka mfululizo kwa muda wa saa 10 ikiwa angani kabla ya kutua na kujazwa mafuta tena.
“Ina mfumo maalum wa kamera ambazo zina uwezo wa kupiga picha hata usiku wa manane na kutambua mienendo ya viumbe wenye damu ya moto kama hayawani na binadamu, hivyo ni rahisi kubaini kama kuna majangili,” akafafanua.
Baada ya maelezo ya takriban nusu saa, hatimaye yeye na wasaidizi wake wakaamua kuirusha ndege hiyo baada ya kuiwasha. Ilichomoka kwa kasi ya ajabu na kuelekea angani ikaanza kuzunguka.
Hapo ndipo tukasogezwa kwenye hema kubwa ambako tuliwakuta wasaidizi wake – Austin Howard na Kory Ferguson – wakiendesha kompyuta hizo na tukashuhudia mazingira halisi ya hifadhi katika eneo husika pamoja na kuona wanyama mbalimbali.
“Sasa hapa unaweza kuona kama kuna wavamizi (majangili) na inakuwa rahisi kuwasiliana na askari wa wanyama pori na kwenda kwenye eneo husika kuwakamata,” anasema Jones.
Hata ilipotua, ilikuja kama ndege za kawaida zinavyokuja, tofauti yake tu yenyewe haina magurudumu. Naam, unaweza kuwa ufumbuzi mwingine wa kupambana na ujangili nchini, tatizo ambalo haliko Tanzania tu, bali katika nchi nyingi barani Afrika.
Taasisi mbalimbali za ndani na nje zikiwemo serikali za mataifa makubwa zimekuwa zikijitahidi kusaidia mapambano hayo kama alivyofanya Rais Barack Obama wa Marekani alipoahidi kutoa Dola milioni 10 (sawa za Shs. 20 bilioni) ili kuimarisha mapambano hayo nchini.
Takwimu zinaonyesha kuwa Bara la Afrika mwaka 1930 lilikuwa na tembo 50 milioni na kwamba hadi kufikia mwaka 2013 tembo waliobakia katika bara zima ni  500,000.
Aidha, takwimu hizo zinaonyesha kwamba katika miaka ya 1960 Tanzania kulikuwa na tembo kati ya 250,000 hadi 300,000 na kwamba wanyama hao walipungua hadi kufikia 130,000 mwaka 2002 na idadi ya tembo hapa nchini imeendelea kupungua kwa kasi ambapo hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa inakadiriwa kuna tembo wasiozidi 55,000.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, wastani wa tembo 30 huuawa kijangili kila siku ikiwa ni sawa na tembo 850 kwa mwezina zaidi ya tembo 10,000 wanauawa kila mwaka,hali ambayo inatishia uwepo wa wanyama hao wakubwa zaidi duniani kwa sasa.
Kwenye Hifadhi ya Tarangire, jumla ya tembo 104 waliouawa katika kipindi cha miaka mitatu tu kutoka mwaka 2007 hadi 2009 na katika Hifadhi ya Serengeti idadi ya tembo imepongua kutoka 2,500 mwaka 1985 hadi kufikia 500 mwaka 2012 huku nyati wakipungua kutoka 70,000 hadi 40,000 ujangili huo ukiua faru wengi kutoka 1,000 waliokuwepo mwaka 1985 hadi 20 tu.
Kwenye Pori la Akiba la akiba la Selous inaelezwa kwamba hadi kufikia mwaka 2007 kulikuwa na tembo zaidi ya 70,000 lakini idadi hiyo imeshuka hadi tembo 30,000 tu kufikia mwaka 2012.
Kasi ya ujangili inayoongezeka kila mwaka inachangiwa na mambo mbalimbali yakiwemo kukua kwa uchumi wa nchi ya China na nchi nyingine za Kusini Mashariki mwa Asia kama Hong Kong, Vietnam na Philippines.  
Juhudi mbalimbali zimefanywa na wadau wa sekta ya utalii na maliasili, lakini inaoenakana tatizo hilo linazidi kuota mizizi huku taasisi za kimataifa zikiendelea kulipigia kelele bila mafanikio.
Kampuni ya Bathawk Recon Limited ya Tanzania imeitikia kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya ujangili nchini, ambapo leo hii Septemba 16, 2015 ikaamua kuzindua ndege hizo maalum zinazoweza kupambana na ujangili.
 “Haya ni majaribio ya tatu, tulifanya majaribio mara ya kwanza katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa kutumia ndege maalum aina ya DT 16, lakini hayakuonyesha matokeo mazuri,” anasema Michael Chambers, Mkurugenzi wa Mikakati na Mawasiliano wa Bathawk.
Chambers, ambaye amekuwepo nchini Tanzania kwa takriban miaka 20 sasa, anasema jaribio la pili lilifanyika katika Pori la Selous mwezi Mei 2015 kwa kutumia ndege aina ya DT 26 iliyotengenezwa Ufaransa, lakini iliharibika na haikuweza kutoa matokeo mazuri.
Anaibainisha kwamba, katika kipindi cha siku tano cha majaribio tangu Septemba 11, 2015, ndege hiyo mpya aina ya Super Bat DA-50 UAV iliyotengenezwa na kampuni ya MartinUAV ya Marekani, imeonyesha mafanikio makubwa.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi na muasisi wa kampuni hiyo, Tom Lithgow, anasema baada ya majaribio yao kuonyesha mafanikio, sasa wataandaa ripoti yao na kuiwasilisha kwenye taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) pamoja na kwenye Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili kama wataridhia, basi waweze kuona namna gani yakuanza utekelezaji kuhakikisha tembo na wanyama wengine wanalindwa.
“Tumefanya kazi kwa ushirikiano na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, hususan Tanapa na Idara ya Wanyamapori, tunaamini baada ya mafanikio haya, nao wataangalia ni kwa namna gani tunaweza kuanza kuitumia,” anasema Tom, Mtanzania ambaye ana uzoefu mkubwa wa mazingira ya porini na utalii kwa ujumla.
Hata hivyo, Mike Chambers anasema, teknolojia hiyo itakuwa ya kwanza kutumia nchini Tanzania katika suala zima la kubaini na kudhibiti ujangili na ni ya gharama nafuu zaidi kwani ndege hizo hazitumii rubani ndani yake, zinatumia mafuta kidogo na kuruka kwa muda mrefu.
“Mbali ya kupambana na ujangili, lakini pia teknolojia hii itasaidia suala zima la uhifadhi kwa kutambua hata idadi ya wanyama waliopo (scouting),” anafafanua Chambers.
Herman van Rooyen na Johnson Makere ni vijana waliohitimu stashahada ya Uhifadhi Wanyamapori katika Chuo cha Wanyamapori cha Mweka mkoani Kilimanjaro, ambao kwa sasa wameelekezwa namna ya kurusha na kuongoza ndege hizo kwa ustadi mkubwa.
Ingawa wanatakiwa kupatiwa mafunzo maalum na muhimu, lakini wanaielezea teknolojia hiyo kwamba inafaa sana katika suala zima la uhifadhi wanyamapori.
Wanasema, kutokana na tatizo la uhaba wa watumishi na vitendea kazi pamoja na miundombinu duni ndani ya hifadhi na mapori ya akiba, teknolojia hiyo inaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa ikiwa serikali itaikubali na kuitumia.
“Teknolojia hii inasaidia kuwakamata majangili wakiwa wanafanya uharamia wao ndani ya hifadhi na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo sasa kwamba majangili wanaokamatwa wanakuwa wanasingiziwa,” anasema Makere.
Makere anaongeza: “Hivi sasa utaratibu unaotumiwa ni kama wa mbwa kufuata nyayo na harufu kwani majangili mara nyingi wanakuwa wanakamatwa wakiwa majumbani mwao, lakini hapa watakamatwa humo ndani na hivyo kuukazia ushahidi kwani picha zipo na watakuwa na vidhibiti.”
Kampuni ya Bathawk Recon inajipambanua kwamba kwa kuja na teknolojia hiyo ya utambuzi inaweza kuwa suluhu ya janga la ujangili kwa kuwa inao uwezo wa kutambua majangili hata kama wakijificha, labda kama watachimbia ardhini.
“Na kama watajichimbia basi itakuwa faida zaidi, kwa sababu hawawezi kufanya lolote bila kuonekana,” anaongeza Jones, ambaye kwa zaidi ya miaka 10 amekuwa rubani wa ndege za kivita kwenye Jeshi la Kifalme (Royal Armed Forces).
Ofisa uhifadhi kutoka Hifadhi ya Tarangire, Marandu, ambaye alimwakilisha Mhifadhi katika uzinduzi huo, anasema anaamini teknolojia hiyo ni nzuri na inaweza kusaidia kuwahifadhi wanyama.
“Katika mapambano dhidi ya ujangili na ustawi wa maliasili, mbinu yoyote yenye kuleta matokeo chanya ni vizuri ikapokelewa na kujaribiwa, kama inafaa basi itakuwa msaada mkubwa kwa taifa,” anasema.
Sera ya Taifa ya Wanyamapori ya mwaka 1998 inaelekeza kuwa aina zote za viumbe hai zihifadhiwe, wanyamapori wasitumiwe kiasi cha kuifanya idadi yao ipungue na kuwa katika hatari ya kutoweka na kuhakikisha Taifa linaendelea kumiliki wanyamapori na kusimamia kwa niaba ya wananchi.

Ndege zilizojaribiwa

DT-18 ilijaribiwa Tarangire

Hii ilitengenezwa Ufaransa. Ni ndogo sana, inaweza kuruka kwa saa mbili tu katika nusu kipenyo cha kilometa 15 kutoka ilipo mitambo.

DT-26 ilijaribiwa Selous

Imetengenezwa Ufaransa na kampuni ya Delair Tech. Hii ni kubwa kidogo, ina uwezo mkubwa na inatumia viwango vya satelaiti za kijeshi vya mawasiliano kutumana kupokeataarifa pamoja na namna ya kuongozwa kwake.

Superbat DA 50 – Imejaribiwa Mkomazi
Imetengenezwa Marekani na kampuni ya MartinUAV. Inaitwa MLB Super-Bat DA-50. Inatumia injini yenye mapigo mawili na uwezo wa 50cc ikiwa na genereta la Watts 75 pamoja na mafuta. Urefu wake ni futi 8.5 x 5.3 x 2.25 inapokuwa imeunganishwa, lakini ikiwa bado haijaungwa ina urefu wa futi 3.5 x 1.25 x 1.5. Kasi yake ni kati ya 40 hadi 70kts, inakaa angani kwa saa 10 mfululizona inaruka kimo cha futi 15,000 hadi 20,000 bila kupoteza mawasiliano.

MWALIMU HOSEA DANIEL KUTOKA FOLUMA TUITION CENTRE AELEZA UMUHIMU WA MASOMO YA ZIADA.

$
0
0
Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.

Na:Binagi Media Group
Mwl.Daniel anasema kuwa Masomo ya ziada ni mhimu kwa mwanafunzi kwa kuwa husaidia katika kukuza uelewa na ufahamu kwa mwanafunzi na hivyo kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi.
Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.
Kushoto ni Madam Elizabeth Daniel akiwa pamoja na Mwalimu Hosea Daniel. Wote ni kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.
Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) Foluma Tuition Centre kilichopo Bomani-Tarime Mkoani Mara ni mkombozi kwa wanafunzi wa darasa la awali pamoja na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wakati wa likizo.Kutana na Mwl.Hosea Daniel, Madam Elizabeth Daniel, Mwl.Evance Malaba pamoja na Mwl.Malima Mjinja kwa maendeleo ya mwanao kielimu.

WANAWAKE:JIVUNIE KURA YAKO NDANI YA JAMII,EPUKA MCHEPUKO.

$
0
0
 HII NAFASI YA PEKEE NA ELEWA MAANA YA MABADILIKO WITO KWA WANAWAKE WOTE [WOMEN AS WINNERBREAD] ELISERENA KIMOLO MWENYEKITI UWT DMV NCHINI MAREKANI. 1.WITO KWA WANAWAKE WOTE.

Tumepata nafasi ya pekee mwanamke kuwa Makamu wa Rais,Mama Samia anafahamu fika matatizo ya mwanamke ndani ya familia,hivyo kwa mara ya kwanza huu ni ukombozi kwa mwanamket .

Tumepata mtetezi katika ngazi ya juu kwa sababu siku zote mwanamke ndie anayehusika zaidi na mambo ya familia , huku Nchini Marekani na nchi nyingine kama China au nchi zilizoendelea, Mwanamke anajulikana kama" WOMEN AS WINNERBREAD".Kwanini tunaitwa hivyo , Kwasababu ya jitihada zetu katika jamii.

Jitihada zetu za kuhakikisha familia zetu zinasonga mbele zikiwa na maendeleo mazuri kuhakikisha hakuna mtoto atakae achwa nyuma katika maendeleo."NO CHILD LEFT BEHIND" .

Hayo yote yatafanikiwa kwa kuwa na SIASA SAFI NA UONGOZI BORA.MAENDELEO AU MABADILIKO HAYATOKEI KWA SIKU MOJA,JITIHADA ZETU TUKISHIRIKIANA NA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA Tutafika tunapotaka, Dr. Magufuli alishatutangazia kabisa katika kampeni yake kwamba mama NTILIE hatalipa tena kodi, mara atakapokuwa madarakani,hivi tunahesabu siku ifike. 

Epuka Mchepuko Mama Samia atatupigania, simama katika nafasi hiyo, tusidanganyike na sauti zetu zisikike. 

Ni heshima kubwa CCM imetupa hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kumheshimu mwanamke, kwa kuwa mwanamke ni chombo muhimu sana katika jamii.  

Mheshimiwa Rais  Mmtarajiwa alilitafakari kwa makini pamoja na uongozi wote wa CCM kuona kwamba inafaa tuangalie wanawake hu sio mwanzo ndani ya CCM wanawake tuna nafasi mbalimbali.

Lakini hii ya sasa hivi ni nafasi ya juu sana, utetezi na maamuzi mazuri tutayaona, hivyo basi acha MCHEPUKO CHAGUA MAGUFULI Siku ya mwisho utasema nilisimama katika nafasi yangu ndani ya jamii kwa kupiga kura na sasa hakuna mtoto anaeachwa nyuma kimaendeleo na matunda ndani ya jamii yanaonekana. ".WOMEN AS WINNERBREAD" CHAGUA DR. MAGUFULI CHAGU MAMA SAMIA.

TATIZO LA UHABA WA MAJI WILAYANI MKURANGA KUWA HISTORIA.

$
0
0
 Mwakilishi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania Dkt, Mohammed Akbar Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima chenye urefu wa mita 541 eneo la Mkwalia, Mkuranga, Pwani leo.Kisima hicho kinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 1.8 kwa siku.
 Maji kutoka katika kisima hicho yakitiririka kufuatia kufanyika kwa majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini.
 Kiongozi wa waendesha mitambo ya uchimbaji visima wa kampuni ya ZENTAS Bw. Sima Teodor ( kushoto) akitoa maelezo kwa wandishi wa habari kuhusu kazi ya uchimbaji wa kisima hicho katika eneo la mradi wilayani Mkuranga.
 Mtaalam wa mitambo wa Kampuni ya ZENTAS Sahtn Topal ( katikati) akifafanua teknolojia na vifaa vilivyotumika kuchimba kisima hicho.Picha na Aron Msigwa/ MAELEZO.

Na.Aron Msigwa- MAELEZO
Wananchi wa wilaya ya Mkuranga,mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni  1.8  kwa siku.

Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho  mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS  kutoka Uturuki nchini Tanzania Dkt.Mohammed Akbar amesema wao kama wataalam wanaendelea na majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini  jambo ambalo limeonyesha mafanikio makubwa.

 Amesema mtambo wa kuchimba kisima hicho uliwasili eneo la mradi Julai 9 mwaka huu na kuongeza kuwa mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi kazi ya uchimbaji ilianza na kubainisha kuwa  sasa kisima hicho kinazalisha kiasi cha lita  76,000 kwa saa na lita milioni  1.8 kwa siku.

Dkt. Akbar amesema endapo maji hayo yataunganishwa kwenye miundombinu ya maji ya mji huo yatakidhi mahitaji ya maji ya mji wa Mkuranga ambayo ni lita laki  Sita na Elfu mbili  kwa siku (602,000).

" Kwetu Haya  ni mafanikio makubwa ukizingatia mradi wenyewe haujaanza kusambaza maji kwani visima hivi vilikuwa ni kwa ajili ya utafiti, kiwango cha maji kilichopatikana ni kikubwa, kilichobakia sasa ni kwa mamlaka husika na Serikali kukamilisha mipango iliyobaki ili maji haya yawafikie wananchi" Amesema.

Ameongeza kuwa chini ya mradi huo wamechimba visima 9 na kati ya hivyo visima 7 vinafanya vizuri na  2 vimeharibika na kueleza kuwa matarajio yao  ni kuona visima vitano ambavyo sasa  vimekamilika vizuri vikizalisha  lita milioni 55.

Meneja wa Mamlaka ya Maji Mkuranga mjini (MKUWASA) Muhandisi Filbert Pius akiuzungumzia mradi huo amesema kuwa utakapokamilika utawasaidia wananchi kupata maji safi na kuondoa tatizo la muda mrefu la ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Amesema mahitaji ya maji katika mji huo ni makubwa kuliko uwezo wa sasa wa kuzalisha maji ambapo vyanzo vilivyopo vina uwezo wa kuzalisha lita 135,000 kwa siku  ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya lita 602,000 kwa siku kwa wakazi wapatao 25,847.

" Wananchi sasa watapata nafuu, tofauti kabisa na mwanzo, maji yanayozalishwa hapa ni mengi  lita 1,800,000 kwa siku hii inakidhi  mara mbili mahitaji yote ya wananchi wa mji wa Mkuranga " Amesisitiza Muhandisi Pius.

Ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu yenye urefu wa kilometa 2 inayotarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu ili Mkuranga  ambao sasa ni mji wa viwanda upate  huduma ya uhakika ya maji,

Pia amesema kukamilika kwa ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji eneo la Mkwalia ulipo mradi huo pamoja na eneo la Kurungu kutaiwezesha hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kupata huduma ya uhakika ya maji ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wagonjwa wanafika kupata huduma.

Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Bi.Nelly Msuya akifafanua kuhudsu mradi huo amesema unajengwa unatekelezwa na DAWASA kwa niaba ya Serikali na akifafanua kuwa maeneo yote yenye miundombinu ya maji katika wilaya ya Mkuranga yanatarajiwa kuanza kupata huduma hiyo ifikapo Oktoba mwaka huu.

Amesema mradi huo sasa uko katika hatua za majaribio na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wote mara  kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mabomba ya kusambazia maji , ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na kukamilika kwa  taratibu za kitaalam ili maji hayo yawafikie wananchi.

"Nachoweza kusema kwa upande wa wilayanya Mkuranga tumefika pazuri, sisi kama DAWASA watekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa niaba ya Serikali tutahakikisha kero ya maji  katika wilaya hii  na maeneo mengine inapatiwa ufumbuzi,  tumeshatoa mamlaka kwa miji na wilaya  kubuni, kusimamia  na kuendeleza miradi ya maji ili wananchi wengi zaidi wanufaike" Amesisitiza.

Aidha, amebainisha kuwa mradi wa ujenzi wa visima 8 eneo la Mkuranga umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.4 na kufafanua kuwa awamu inayofuata ni kuyapeleka maji hayo yakaunganishwe na mfumo wa kusambazia maji uliopo, ujenzi, uongezaji wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na ununuzi wa pampu ya kusukuma maji hayo kutoka kwenye chanzo.

MKUTANO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI JIMBO LA MKANYAGENI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Black wizard Chokocho jimbo la uchaguzi la Mkoani Wilaya ya Mkoani Pemba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwa Mgombea wa Urais wa kupitia CCM kwa kipindi cha pili Dk.Ali Mohamed Shein akiwatambulisha wagombea Udiwani wa Majimbo ya Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba leo katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi zilizofanyika katika uwanja wa mpira  Black wizard Chokocho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwa Mgombea wa Urais wa kupitia CCM kwa kipindi cha pili Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Ubunge Prof.MAKAME mbarawa Mnyaa Jimbo la MKANYAGENI Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba leo katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi zilizofanyika katika uwanja wa mpira  Black wizard Chokocho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwa Mgombea wa Urais wa kupitia CCM kwa kipindi cha pili Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Uwakilishi Mohamed Ijaza Jecha Jimbo la Mtambile  Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba leo katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi zilizofanyika katika uwanja wa mpira  Black wizard Chokocho.

  Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM waliohudhuria katika mkutano wa Kampeni za CCM katika Wialaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba,zilizofanyika leo katika uwanja wa Black Wizard na kuhutubiwa na  Mgombea Urais kwa kipindi cha pili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 Baadhi ya WanaCCM na wananchi na wapenda amani waliofurika katika Uwanja wa mpira wa Black Wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Jimbo la Mkanyageni Pemba wakinyanyua mikono juu kuunga mkono SERA  za CCM zilizotelewa  na Mgombea wa Urais kupitia CCM kwa kipindi cha pili  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM NEC na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho alipokuwa akiwaombea kura wagombea wa CCM katika mkutano wa hadhara wa Jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo wakati Mgombea Urais wa Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein  akitangaza sera zake wakati wa Mkutano wa Hadhara  wa Kampeni za katika jimbo hilo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwa Mgombea wa Urais wa kupitia CCM kwa kipindi cha pili Dk.Ali Mohamed Shein akionesha Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Wananchi na Wanachama wa CCM jimbo la Mkanyageni katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi zilizofanyika katika uwanja wa mpira  Black wizard leo Chokocho
[Picha na Ikulu.] 

UJUMBE WA KAMPUNI YA POLY TECHNOLOGIES, INC. YA CHINA WAMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI , MHE. MATHIAS CHIKAWE OFISINI KWAKE

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) akiongea na ujumbe wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China (haupo pichani) uliomtembelea ofisini kwake. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil na na kulia ni Katibu wa Waziri, Nelson Kaminyoge. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akimkaribisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China Bw. Huang Geming (mwenye tai) aliyeongoza ujumbe wa Kampuni yake kumtembelea Waziri ofisini kwake.
Ujumbe wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bw. Huang Geming (wa tatu toka kulia) katika mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (hayupo pichani) ulipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China uliomtembelea ofisini kwake.  Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.

CHAMA CHA MADEREVA WA SERIKALI TANZANIA CHAPATA USAJILI RASMI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST) wa kwanza kushoto mstari wa mbele Bw. Bahatisha Selemani  Mkala  akipokea  Cheti cha Usajili wa Chama hicho  kutoka kwa Afisa usajili Bw. Hashim Mwanga wakati wa. makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za msajili zilizopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).
 Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST) aliyeshika cheti cha usajili Bw. Bahatisha Selemani Mkala   akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madereva  ambao ni wanachama wa chama hicho mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho katika Ofisi za Msajili zilizopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).
(Picha na Benjamin Sawe)

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.




   PRESS RELEASE” TAREHE 18.09.2015.
·         WATU TISA WAFUASI WA CCM NA CHADEMA WAJERUHIWA KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA MAENEO YA MBATA BUCHANI JIJINI MBEYA.

·         WATU WAWILI RAIA WA KIGENI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KINYUME CHA SHERIA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MNAMO TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO LA MBATA – BUCHANI, KATA YA GHANA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CCM BW. SHAMBWE SHITAMBALA AKIWA NA WAFUASI WAKE, WAPENZI WA CHAMA HICHO ALIKUWA AKIFANYA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA ENEO HILO KWA MUJIBU WA RATIBA YAKE.
MGOMBEA HUYO AKIWA KATIKA MKUTANO HUO, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA BW. JOSEPH MBILINYI ALIKUWA AKIPITA ENEO HILO AKIWA NA MSAFARA WAKE KUELEKEA MAENEO YA NSOHO KWENYE MKUTANO WA KAMPENI. KUTOKANA NA KITENDO HICHO WAFUASI WA CCM AMBAO WALIONEKANA KUWA WENGI HADI ENEO LA BARABARA HIVYO KUPELEKEA MSAFARA WA BW. MBILINYI KUTOWEZA KUPITA ENEO HILO HALI ILIYOPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU ZILIZOPELEKEA KUJERUHIWA KWA WATU NA UHARIBIFU WA MALI.
KUTOKANA NA VURUGU HIZO, WAFUASI TISA WA VYAMA HIVYO VYA SIASA WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. ROBERT KERENGE  (58) KATIBU WA CCM WILAYA YA MBEYA 2. SALUM MWANSASU (35) MKAZI WA MAJENGO [CCM] 3. ATUPELE BROWN (39) MKAZI WA GHANA [CCM] 4. ROSE NELSON (30) MKAZI WA MAJENGO [CCM] 5. SAKINA SALUM (25) MKAZI WA GHANA [CCM] 6. MALANYINGI MATUKUTA (31) MKAZI WA FOREST [CCM] 7. AGABO MWAKATOBE (44) MKAZI WA GHANA [CHADEMA] 8. JAILOS MWAIJANDE (23) MKAZI WA ITIJI [CHADEMA] NA 9. GABRIEL MWAIJANDE, DEREVA WA MGOMBEA UBUNGE [CHADEMA].
AIDHA KATIKA VURUGU HIZO GARI LA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA BW.JODEPH MBILINYI AINA YA TOYOTA LAND CRUISER YENYE NAMBA ZA USAJILI T.161 CPP LILIHARIBIWA KIOO CHA MBELE, TAA MOJA YA NYUMA UPANDE WA KUSHOTO NA KIOO CHA UPANDE WA DEREVA KWA KUPIGWA MAWE. PIA PIKIPIKI ZENYE NAMBA ZA USAJILI T.332 CHV AINA YA T-BETTER NA T.383 CSE AINA YA SKYMARK ZILIHARIBIWA KWA KUVUNJWA SIDE MIRROR ZA UPANDE WA KUSHOTO NA ZIPO KITUO CHA POLISI KATI.
KWA MUJIBU WA RATIBA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI ILIYOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA KWA TAREHE 17.09.2015, ILIKUWA IKIONYESHA CHADEMA SAA 10:00 ASUBUHI HADI SAA 15:00 ALASIRI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA NSOHO NA SAA 15:00 ALASIRI HADI 18:00 JIONI WALITAKIWA KUFANYA MKUTANO KATA YA MAENDELEO WAKATI CCM KWA MUJIBU WA RATIBA WALITAKIWA KUFANYA KAMPENI KATA YA ITENDE SAA 08:00 ASUBUHI HADI SAA 13:00 MCHANA NA SAA 13:00 MCHANA HADI SAA 18:00 JIONI MTAA WA MBATA, KATA YA GHANA AMBAPO NIPO TUKIO HILI LILIPOTOKEA.
UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUPELEKA JALADA LA UCHUNGUZI KWA MWANASHERIA WA SERIKALI ILI WALIOHUSIKA KATIKA VURUGU HIZO WAFIKISHWE MAHAKAMANI.


KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA IDARA NYINGINE, LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI MSUMBIJI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ARQUEMIDES JOAO MAHANJANE (40) NA 2. HENRIQUES BENDITO ASSUBA (36) WOTE WAKAZI WA MAPUTO WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI VIPANDE 2 VINAVYODHANIWA KUWA NI PEMBE ZA FARU ZENYE UZITO WA KILO 5 ½, VIPANDE 4 VYA MAWE YADHANIWAYO KUWA NI MADINI YENYE UZITO WA KILO 1 ½ NA MZANI 01 [PORTABLE ELECTRONIC SCALE].

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.09.2015 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KASUMULU MPAKANI, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA WAKIWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI  ABL 860 MC AINA YA TOYOTA HILLUX VIGO D/CABIN WAKITOKEA NCHINI MALAWI KUINGIA NCHINI. NYARA HIZO PAMOJA NA VITU HIVYO VILIKUWA VIMEFICHA CHINI YA CHASES YA GARI. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAKAZI WA MAENEO YA MIPAKANI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.

Imesainiwa na
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAMA SAMIA, MIKINDANI NA MAFIA JANA.

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septemba17, 2015, katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni kwa ajili ya Jimbo la Mtwara mjini, uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara jana, Septemba 17, 2015.
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipokea Wanachama waliohamia CCM, kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakati wa mkutano wa kapnei uliofanyika jana, Septemba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.

 
 Kada wa CCM, Mtela Mwampamba akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septamba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani, Jimbo la Mtwara Mjini.

 Msanii wa Bongo Movie, Snura akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 17, 2015 katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Vijana wakiungana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kuishangilia CCM, baada ya kuwapokea kutoka vyama vya CUF na Chadema katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana, Septemba 17, 2015.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mafia mkoani Pwani, jana, Septemba 17, 2015.
 Aliyekuwa Mbunge wa Mafia ambaye pia aliingia katika kinyan'ganyiro cha kuomba ridhaa ya CCM kuwania tena ubunge wa jimbo hilo, Abdulkarim Shah, akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo, Mbarak Dau, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika katika Kisiwa hicho cha Mafia.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza Kada wa CUF, Mohamed Albadawi, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. Albadawi awali alikuwa Mgombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CUF baada ya kuongoza katika kura za maoni, lakini baadaye akaenguliwa na chama hicho na kupachikwa, Shomari Kimbau ambaye alihamia CUF baada ya kushindwa katika kura za maoni za CCM.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto), akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akihutubia katika ufunguzi rasmi wa Semina ya Ushirikiano wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency ya Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Monica Maeland, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanna-Marie Kaarstad na wadau wengine katika sekta ya biashara na uwekezaji kutoka Norway na hapa nchini.
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Maeland (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo. Kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula na katikati ni  Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Kaarstad. 
Waziri Membe akiendelea kuzungumza
Waziri wa Biasha na Viwanda nchini Norway Mhe. Monica Maeland naye alipata fursa ya kuzungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Norway, Mhe. Maeland yupo nchini kwa lengo la kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania nchini Norway. Pia wakati wa ziara hiyo Mhe. Maeland amezindua mtambo wa mbolea wa Yara ulioko kwenye Bandari ya Dar es Salaam na pia atatembelea Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.

 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na mmoja wa wadau katika semina hiyo Bw. John Ulanga (kushoto) wakifuatilia Hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa na Mhe. Membe na Mhe. Maeland (hawapo pichani). 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Tunsume Mwangolombe (katikati) naye akifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo.
Sehemu ya wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo 
Semina ikiendelea
Waziri Membe (katikati) na Waziri Maeland kwa pamoja na wajumbe waliofuatana nao wakiwa kwenye mazungumzo mara baada ya kumaliza ufunguzi wa semina.
Waziri Membe (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya  faida ya semina hiyo ya wafanyabiashara wa Tanzania na Norway
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea
Picha na Reginald Philip
 TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe ameisifu Serikali ya Norway kwa kuwa mshirika wa karibu wa maendeleo wa Tanzania hususan katika sekta za biashara na uwekezaji.

Waziri Membe alitoa kauli hiyo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda wakati akifungua rasmi semina kuhusu kuimarisha ushirikiano wa Kibiashara  na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam leo.

Katika ufunguzi huo ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Monica Maeland ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi, Mhe. Membe alisema kuwa Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia kwa miaka mingi lakini sasa nchi hizi zimeamua kushirikiana zaidi katika masuala ya uwekezaji na biashara ili kukuza uchumi kwa maendeleo ya nchi zote mbili.

Aliongeza kuwa, kwa miaka mingi Tanzania imefaidika na  ushirikiano na Norway katika sekta mbalimbali ambapo nchi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuisaidia Tanzania kupambana na umaskini na kukuza uchumi. Hata hivyo alisema umefika wakati sasa nchi hizi mbili zinufaike kupitia biashara na uwekezaji ambapo nchi zote zina fursa nyingi katika maeneo hayo ikiwemo gesi na mafuta, kilimo na madini.

Mhe. Membe alisema kuwa kufanyika kwa semina hii itakayowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji itaongeza thamani katika uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo Tanzania ina mengi ya kujifunza kutoka Norway ambayo ni miongoni mwa nchi zinazosafirisha zaidi gesi asilia na mafuta duniani. Hivyo aliwaasa Watanznaia kutumia semina hiyo kujifunza ili kuimarisha sekta ya nishati ya hapa nchini. 
“Semina hii ni fursa kwa Kampuni za Tanzania na Norway kujifunza na kubadilisha uzoefu na mawazo ya namna bora ya kuboresha sekta za biashara na uwekezaji kwa manufaa ya nchi zote mbili” alisema Waziri Membe.

Akizungumzia biashara inayofanyika kati ya Tanzania na Norway, Mhe. Membe alisema kuwa Tanzania inatakiwa kuongeza biashara yake nje ya nchi ili kuimarisha uchumi wake. Alieleza kuwa kwa sasa biashara kati ya Tanzania na Norway imeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.6 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi bilioni 6.9 mwaka 2014 kwa bidhaa zilizozwa Norway kutokea Tanzania ikiwemo kahawa, chai, viungo, maua, mbogamboga, mbao na madini. 

Kwa upande wa bidhaa kutoka Norway, Tanzania imenunua kwa ongezeko la kutoka bilioni 22.3 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi bilioni 73 mwaka 2014. Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za binadamu na bidhaa za viwandani.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa Norway, Mhe. Monica aliipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika maendeleo na ukuaji wa uchumi ambao umefikia asilimia 7. Alieleza kuwa Tanzania itafikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa vile inayo dhamira ya dhati na imejipanga kupitia uvumbuzi wa gesi na mafuta, nguvukazi ya vijana na mageuzi yaliyopo katika sekta ya uchumi.

Alieleza kuwa Norway ipo tayari kuendelea kuisadia Tanzania katika sekta ya gesi na mafuta kwa vile nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika eneo hilo hususan katika masuala ya teknolojia. Aidha, aliongeza kuwa Tanzania ni mshirika wa kweli wa Norway katika maendeleo hivyo nchi yake itashirikiana kikamilifu na Tanzania.


“Kuna msemo maarufu unasema kama unataka kwenda mbio nenda peke yako, lakini kama utanaka kufika mbali nenda pamoja na mwenzako. Hivyo Norway inataka kwenda pamoja na Tanzania ili kuziwezesha nchi hizi kufika mbali kimaendeleo” alisisitiza Mhe. Monica.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne-Marie Kaarstad alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa nchi hizi mbili kukuza biashara kwa kuishirikisha sekta binafsi kikamilifu kwani ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu. 


Semina hiyo ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Norway, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) ilihudhuriwa na Makampuni 34 kutoka Norway na Tanzania na pia wadau mbalimbali wa biashara na uwekezaji.

WATAKAO HUJUMU MIUNDOMBINU YA DART KULIPA FAINI YA LAKI TATU.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mifumo Juhn Mlingi kutoka Taasisi ya Mabasi yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transport) akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo katika kituo cha Kivukoni jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakipanda  gari la Mradi  wa Mabasi yaendayo Haraka jana  jijini Dar es Salaam katika  ziara ya kukagua Miundo Mbinu ya Mradi  wa DART kabla  ya kuanza kutumika .
 Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakikagua  kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara  ambacho ujenzi wake  umekamilika  kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa  Afisa wa Tanroads akikagua kibanda cha kukatia tiketi kilichopo ndani ya kituo cha Kimara katika mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads wakiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka walipokuwa wakifanya  ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.

Na Ally Daud- MAELEZO.
Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam (DART ),Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa miundo mbinu ya mradi huo.

Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35 kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika tano.

“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza  ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART  ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.

Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.

Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.

Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.

Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden  Dragon  kutoka  Japan.

TEMEKE WATINGA FAINALI ARS.

$
0
0
 Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1
 Mchezaji wa timu ya Ilala Tumaini Michael (Kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17). Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1.
Mchezaji wa timu ya Ilala Jackline Albert (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1.

TEMEKEgirls jana walifanikiwa kutinga hatua ya fainali, baada ya kuwagaragaza majirani zao wa Ilala kwa kuwafunga mabao 2-1 katika muendelezo wa michuano ya U-17 ya Airtel Rising Stars, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Ilala ambao walionekana kuumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha kwanza walifanikiwa kuandika bao lao mnamo dakika ya 1 baada ya Tumaini Michael kuachia shuti na kutinga wavuni huku kipa wa Temeke akiwa hana la kufanya.

Alamanusra Ilala wapate baola pili manmo dakika ya 20 baada ya Tumaini Michael tena kupiga mpira wa kichwa ambao ulipaa kidogolangoni mwa Temeke.

Katika kipindi cha pili, Temeke walionekana kucharuka huku wakicheza kwa kasi kubwa, na ndipo mshambuliaji wa timu hiyo, Shamimu Hamisi mnamo dakika ya 40, alipomalizia kwa umaridadi mpira uliotemwa na kipa wa Ilala na kuukwamisha moja kwa moja wavuni na kusawazisha goli.
Temeke waliofanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya 61 kupitia kwa Asia Juma na kudidimiza matumaini ya Ilala kutinga hatua ya fainali. 

Baada ya mchezo huo kocha wa Ilala Omari Bwezi alisema: “Tumekubali matokeo,wachezajiwangu walicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walionekana luchoka sana kipindi cha pili na kuwapa nafasi ya kutawala wnzetu na ndio maana tukafungwa”.

Naye kocha wa Temeke Daudi Siang’a alisema:  “Vijana wangu walifuata niliyowalekeza wakati wa mapumziko na waliporudi uwanjani walifanya nilichowaeleza na hatimaye tukapata matokeo”

BEI YA MADAFU HII LEO


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA MAUNGUMZO NA BAADHI YA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Najem wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015. 
(Picha na OMR) 

NCCR-MAGEUZI KWAFUKUTA CHINI KWA CHINI

$
0
0
 NaChalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA cha NCCR-MAGEUZI kimesema mkutano uliofanyika jana katika hoteli ya Land Mark  jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho hawajajua lengo lake kutokana na kutokwepo kwa baraka ya vikao kwa mujibu wa chama hicho.

Akizungumza leo  na waandishi habari jana Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chama hicho, Mohamed Tibanyendela amesema kuwa mkutano huo hujafanyika kwa kufuata taratibu hivyo wanaamini kuwa walikuwa wanazungumza  masuala yao wenyewe na sio masuala yanayohusiana na chama hicho.

Amesema kuwa Makamu Mwenyekiti na Katibu ndio watendaji katika uendeshaji wa vikao vya chama lakini hadi wanakwenda kuzungumza na waandishi wa habari hakuna taarifa ya maandishi katika ofisi hiyo.

Tibanyendela amesema kama kumekuwepo na manung'uniko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) suala hilo lingezungumzwa ndani ya vikao kutokana  na viongozi waliozungumza walikuwa wakishiriki katika vikao vya UKAWA.

Amesema kuwa kikao kinachotambulika kilifanyika Septemba 16 katika ofisi ya chama lakini kufuatia na kikao cha jana hakikuwepo hivyo  watakwenda tafsri katiba juu ya viongozi kuzungumza masuala ya chama bila kuwepo kwa vikao vinavyotambuliwa kikatiba.

Aidha amesema  kuwa katika harakati zozote lazima kutakuwa na milima na tambalale yote haya ni kwa ajili ya kuitoa CCM madarakani.

Kamishina wa Tanga wa Chama hicho ,Ramadhan Mnyeko ambaye alikuwa katika kikao hicho amesema kuwa yeye aliitwa na Mwenyekiti lakini alikuwa hajui anaitiwa nini katika hoteli ya Land Mark.

Amesema gharama za kuja Dar es Salaam  amejilipia mwenyewe kwani na taarifa ya kufika alipigiwa simu na sio barua.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI, Mohammed Tibanyendela akizungumza na waandishi wa habari masuala mbalimbali ikwemo viongozi wa juu kufanya kikao kinyemela leo Makao Makuu ya chama hichojijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.
 Kamishna wa Tanga wa NCCR-MAGEUZI, Ramadhan Manyeko akizungumza na waandishi wa habari juu ya kushiriki kikao cha jana cha utoaji taarifa nje ya utaratibu wa chama leo Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI,Mohammed Tibanyendela katika ofis za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
 Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AENDELEA KUPOKEA MISAADA YA VIFAA MBALIMBALI KUSAIDIA SHULE MPYA YA MSINGI KAKUNI MKOANI KATAVI

$
0
0
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda amepokea Msaada wa Vifaa vya Shule ikiwemo sare, Kompyuta pamoja na vifaa vya Michezo kutoka kampuni ya Huawei na Benki ya NMB.
 
Pinda amepokea misaada hiyo kutoka Kampuni hizo kwa lengo la kuzindua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Shule ya Msingi Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni Mkoani Katavi ni Shule aliyosoma Waziri Mkuu huyo Mhe,Mizengo Pinda.

Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukarabati madarasa ya Shule hiyo, barabara na Nyumba za Waalimu.

Meneja Uhusiano wa Huawei, Jin Liguo amesema msaada wa Kompyuta kutasaidia kuboresha Taaluma ya Wanafunzi hususani katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

Naye Afisa Mkuu wa fedha wa Benki amesema wametoa msaada huo kwa Shule alosoma Mhe,Mizengo Pinda ili kusaidia Watoto walio katika Shule hiyo katika Mavazi pamoja na vifaa vya Michezo ikiwemo Kompyuta. 
 
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu  Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa kompyuta mpakato zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni  iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi leo jijini Dar es salaam. Shule hiyo ya kisasa imeanzishwa kufuatia  wazo la Wazo la Waziri Mkuu, Mhe.Mizengo Pinda la kuwa na shule Bora na ya kisasa katika kijiji hicho na inajengwa kupitia michango na misaada ya wadau mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu  Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa Tabuleti 100 zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni  iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
 Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Bw. Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya michezi vilivyotolewa na NMB kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
 Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma Bw. Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare uliotolewa na kikundi hicho  kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni iliyopo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi .
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni hiyo kusaidia elimu katika shule mpya ya msingi Kakuni mkoani Katavi, ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 8 YA BABA MZAZI WA BLOGGER FATHER KIDEVU NA BIRTHDAY YA FATHER KIDEVU

$
0
0
Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007)
Mroki Mroki-Father Kidevu
Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika nane sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki 'Father Kidevu' alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan  pamoja na watoto wako wote, wajukuu wako na vitukuu.

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako. 

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

TPB YAKADIDHI JENGO LA KITUO CHA AFYA PEMBA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud (Wanne kushoto waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Litice Rutashobya, (watatu kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanakijiji, mbele ya jengo la Kituo Cha Afya, Ungi, Shehia ya Msuka Mashariki, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya TPB kukabidhi jengo hilo kwenye hafla iliyofanyika Sptemba 17, 2015. Kituo hicho kimekamilishwa ujenzi wake na TPB.


Waziri Abloud, akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa kituo hicho. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Letice Rutashobya, (katikati mwenye miwani) na Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya shirika wa TPB, Noves A. Moses
Waziri Aboud, (wapili kulia), Profesa Letice Rutashibya, (wapili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (kulia) na Mbunge wa jimbo la Konde, Khatib Suleiman Haji, wakibadilishana mawazo mara baada ya ufunguzi wa jengo hilo la Kituo cha Afya
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images