Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 646 | 647 | (Page 648) | 649 | 650 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (aliyesimama katikati), akizungumza na maofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo y Nje, Viwanda na Biashara na Masoko, Kituo cha Uwekezaji Tanznia (TIC) na taasisi mbalimbali za serikali, walipokutana na Mtendaji huyo mkoani Mtwara jana kujadili kuhusu uzinduzi wa kiwanda hicho kikubwa cha simenti.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kushoto), akiwasikiliza kwa makini maofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje, Viwanda, Biashara na Masoko na Kituo cha Uwekezaji Tanzani (TIC), waliotembelea kiwanda cha simenti cha Dangote kinachojengwa mkoani Mtwara jana kwa ajili ya maandalizi ya kuzindua rasmi Oktoba mwaka huu.
   Mwekezaji kutoka Nigeria, Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kushoto), akiwasikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Dangote Makao Makuu, Bw. Sada Ladan Baki (kulia), Mwakilishi Mkazi wa Makampuni hayo, Bi. Esther Baruti na Kaimu Balozi wa Nigeria, Bw. S. Umaru, alipokutana nao kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha simenti mkoani Mtwara jana.


   Bendera zikipepea kwenye kiwanda hicho kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati


   Sehemu ya mitambo kiwanda hicho ambayho baadhi ujenzi wake umekamilika

  0 0

  TATIZO la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua kufuatia kuanza kupindi cha mpito cha mabasi Yaendayo Haraka (BRT) mwezi ujao kufuatia kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dar es Salaam kutoa China tayari kwa huduma ya usafiri. 

   Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki aliwaambia waandishi wa habari jana wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa mabasi hayo, kuwa wakazi wa Dar es Salaama kwa sasa wataanza kutumia usafiri wa mabasi hayo. 

   “Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito," hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili", alisema na kuongezeas kuwa kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana. 

   Alisema serikali ilifanya kazi kubwa kuwainganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDA-RT. 
   Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Tsh. 900 zilizotolewa katika mitandao ya jamii, na kusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo. 
   Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia. 

  Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit(UDA-RT),Bw,Subri Maburuki alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamlisha taratibu za bandari. 

   “Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni keli yamemekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa jumla mabasi 140", alisema Bw. Maburuki na kufafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana. 

   Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga alisema meli iliyobeba mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi ilitokea China ilikuwa imebeba magari 1700 yakiwemo mabasi ya UDA-RT. 

   “Hatua hii ni ya msingi kwa nchi yetu, itasaidia wakazi kusafiri kwa urahisi na haraka,”alisema Bw. Mhanga. UDA-RT ni kampuni iliyoundwa na wazalendo kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya DART jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki (kulia) akiwa katika bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) tayari kuanza kwa kuanza huduma ya kipindi cha mpito mwezi ujao. Kushoto ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni UDA Rapid Transit (UDA-RT),Bw. Robert Kisena ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wa pili kushoto ni Msemaji wa Kampuni hiyo,Bw, Sabri Maburuki.
   Sehemu ya  mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao
   Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito
  Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito.

  0 0

  WIKI  ya nenda kwa usalama ni muhimu katika jitihada za kuboresha masuala ya usalama barabarani ikiwa ni jambo lililo na kipaumbele katika ajenda za kitaifa nchini Tanzania. 

  Wiki hii inatoa misingi ya kufanya kazi kuelekea katika kufikia maono na matarajio ya mazingira salama na kuboresha usalama barabarani. 

  Hivi karibuni mwenyekiti wa tume ya usalama barabarani bwana Elifadhili Mgonja wakati akiongea na waandishi wa habari katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama jijini Dar es salaam yaliyo fanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mwaka 2015/16 alisema kuwa ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo kikuu cha kupoteza maisha na mali nchini Tanzania.  Ajali hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha vifo na ulemavu ambao unasababisha kudumaa kwa maendeleo ya watu kiuchumi na kuathili uchumi wa taifa kwa ujumla.

  Upigaji vita ajali za barabarani nchini limekuwa ni suala linalopewa kipaumbele kwani ajali mbaya zimekuwa zikiendelea kutokea. Pamoja na sababu nyingine, miundombinu mibovu, uchovu kwa madereva, uchakavu wa magari kama kukosa breki kutokana na kutokuwa na matengenezo imekuwa ni chanzo kikuu cha ajali mbaya nchini Tanzania.

  Kwa nyakati tofauti, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni katika ofisi za kampuni ya Diamond Motors Ltd (Hansa) iliyopo katika barabara ya Nyerere, meneja mkuu (masoko) wa kampuni hiyo Ndugu Laurian Martin aliwaasa watanzania kuweka kipaumbele katika “usalama kwanza”. 

   Aliongeza kwa kusema kuwa utumiaji wa magari yaliyoboreshwa katika teknolojia ambayo kwa sasa yanapatikana katika soko la Tanzania kama vile malori ya Fuso FZ an Fuso FJ  yanatoa nafasi kubwa ya kupunguza ajali za barabarani. 

   Martin aliongeza kusema kuwa “Malori ya Fuso FZ yanauwezo mkubwa wa breki zenye ukubwa, upana na unene unaolingana katika magurudumu ya mbele na ya nyuma, pia ina kifaa cha kujazia upepo pamoja na matanki ya kuhifadhia yanayokuhakikishia usalama wa hali ya juu katika miundombinu ya Tanzania na masafa marefu. 

  Malori haya pia yana vifaa maalumu sehemu ya mbele kwaajili ya kuzuia gari isianguke na kubilingika  kirahisi ikiwa ni pamoja na mfumo wa matairi mpana unaoongeza ustahimilivu.  Hivi ni vipengere muhimu sana hasa katika barabara mbovu na uendeshaji wa hali iliyokithili. 

  Bwana Martin aliendelea kwa kusema kuwa uchovu kwa madereva pia unachangia katika ajali za barabarani hasa katika uendeshaji wa masafa marefu.  Malori ya Fuso FZ kutoka Diamond Motors yana kibini iliyo ninginizwa vizuri katika mihimili yake ambayo inasaidia kupunguza mtikisiko hasa katika matuta ya barabarani, haipati joto wala makerele kutoka kwenye injini, pia ina kiti ambacho kina rekebishika pamoja na usukani unaoweza kurekebishika.  Vipengele hivi vinampatia dereva unafuu wa kuendesha ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa kusababisha ajali.

  Usalama barabarani ni muhimu sana kwa watanzania na hii inadhihirishwa kwa uwepo wa wiki hii ya nenda kwa usalama nchini Tanzania ikiwa ni nia thabiti ya kupunguza ajali za barabarani. Muunganika wa sababu mbali mbali za kiusalama ukizingatiwa inaweza kupunguza ajali za barabarani. Usimamizi wa usalama barabarani  kutoka kwa washikadau wa sekta hii, mafunzo muafaka kwa madereva ikiwa ni pamoja na utumiaji wa magari yaliyoboreshwa kwa ubora kama vile Fuso FZ na Fuso FJ ambayo hayahitaji matengenezo ya mara kwa mara na yametengenezwa kwa teknolojia iliyoboreshwa katika kumpunguzia dereva uchovu na ubora wa kuhimili miundombinu ya Tanzania inaweza kuchangia katika uboreshaj wa usalama barabarani.

  FZ TRACTOR 6x4
  Kuhusu Diamond Motors Limited (Hansa Group)
  Diamond Motors Limited imekuwa wasambazaji pekee wa malori ya Fuso nchini kwa zaidi ya miaka 30. DML imeweka rekodi katika secta ya magari, kwa kufanya kazi kwa ushirikaino na makampuni ya magari yenye ubora wa hali ya juu zaidi duniani. Ushirika wao imara na makampuni yanayoongoza duniani kama vile magari ya abiria ya Mitsubishi kutoka Japani, matairi ya Yokohama kutoka Japani, MTU na ZF kutoka Ujerumani yameleta umaarufu na kutoa uwanja mpana wa wateja kutoka sehemu mbali mbali za ukanda huu. 

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (wan ne kutoka kushoto), akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa maonyesho ya siku ya bahari duniani, yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mkoani Mtwara.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (mwenye nguo ya kitenge), akiangalia meli iliyojengwa kwa kiwango, katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), leo mchana mkoani Mtwara wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya bahari duniani yanayoadhimishwa kitaifa mkoani huo.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego akimisikiliza, Meneja Bandari na huduma za Meli, kutoka Mamlaka ya Usafiri baharini Zanzibar(ZMA), Othman Said, akimweleza namna Mamlaka inavyofanya kazi hasa katika masuala ya Bahari,wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya siku ya bahari duniani,yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku mbili.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akimsikiliza Meneja Utekelezaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), Joseph Msaki,wakati akitoa maelezo ya namna mamlaka inavyofanya kazi wakati wa  wa ufunguzi wa Maonyesho ya siku ya bahari duniani ,yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akimsikiliza Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Kusini, Daudi Amoasi, wakati akitoa maelezo ya namna mamlaka ya hali ya hewa inavyofanya kazi wakati wa  wa ufunguzi wa Maonyesho ya siku ya bahari duniani , yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,akimsikiliza Meneja Mipango wa Shirika la Bandari Zanzibar (ZBC), wakati akitoa maelezo ya namna shirika hilo linavyofanya kazi wakati wa  wa ufunguzi wa Maonyesho ya siku ya bahari duniani ,yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu.

    Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (wa kwanza kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Navigation kutoka Jeshi  la Wananchi Tanzania, Meja Joseph Mjema ,wakati akitoa maelezo ya namna ramani zinavyotumika kwa watumiaji wa baharini wakati wa  wa ufunguzi wa Maonyesho ya siku ya bahari duniani ,yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu.
    Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na washiriki wa maonyesho na wananchi  leo mchana wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya siku ya bahari duniani, yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara. Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku tatu.

  (Habari picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

  0 0

  Msimu wa Pili wa Kwetu House Unaendelea washiriki wanaendelea kuchuana vikali ndani ya Nyumba, Vipajivinaonekana na Ushabiki wa Soka wanaonekana pia. Kama unakumbuka Washiriki waliobahatika kuingia kwenye Nyumba walikuwa 30 baada ya Bootcamp kumalizika na Baada ya hapo Washiriki wameendelea kuyaaga mashindano haya kwa msimu huu wa pili na Wiki hii washiriki 18 ndio wamebaki kwenye Nyumba lakini 6 kati ya hao 18 watayaaga mashindano usiku huu. 
  Kocha ananafasi ya kumuokoa Mshiriki Moja kurudi kwenye Nyumba na kuendelea na Mshindano, Je Wiki hii Kocha atamuokoa nani kati ya washiriki 6 walioaga mashindano… Usikose Kuangalia Azam TV Jumamosi na Jumapili Saa Tatu na Nusu usiku.

  Kumpigia Kura Mshiriki unaependa  ANDIKA KH(namba ya Ushiriki) TUMA KWENDA 15522

  Unaweza Kutufuatilia kupitia Facebook/Instagram/Twitter na Kwenye Youtube Channel
  KWETU HOUSE on Social Media

  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  MKUTANO wa Nne wa Bara la Afrika wa kujadili mipango endelevu  katika eno la mafunzo kwa vijana na wataalamu  wasiojiweza na ushirikji wao katika soko la ajira, unatarajiwa kuanza kufanyika kesho Hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam.

  Mkutano huo ambao utashirikisha nchi mbalimbali tisa unatarajiwa kuhudhuriwa na wageni 50 kutoka katika nchi hizo za Afrika.

  Akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu Dar es Salaam jana kuhusu mkutano huo, Meneja Mipango wa Ofisi ya Maendeleo  Don Bosco Tanzania, Rosemarytery  Njoki alisema, mkutano huo utatoa nafasi kwa Mtandao wa Don Bosco Afrika kuchunguza njia ambazo zitaleta ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na umma ili kuleta maendeleo zaidi.

  “Mkutano unatarajiwa kutafakari juu ya mipango inayoendelea katika eneo la mafunzo ya kijamii na wataalamu vijana wasiojiweza na ushiriki wao katika soko la ajira. Kama vile namna bora ya washirika wanaweza kufanya kazi na binafsi na ya umma sekta kuelekea maendeleo endelevu,” alisema Njoki.

  Alisema mkutano huo pia utazungumzia masuala ya jinsia hasa kwa upande wa upatikanaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kuwafanya wanawake kuwa sawa na wanaume kwa kufanya kazi sawa.

  “Pia tunatafuta kubadilishana uzoefu na washirika weu wa Afrika ambao wote tunafanya kazi ili kuboresha elimu, masuala ya mafunzio ya ufundi stadi na kuwaunganisha vijana na masoko ya ajira ya dunia,” alisema.

  Alisema kwa mara ya kwanza mkutano huo unafanyika nchini kuanzia leo hadi Septemba 25, utakuwa ni kwa ajili ya ushirikiano wa sekta binafsi na umma. Alisema mkutano huo pia utawakutanisha shirikisha watu mbalimbali ikiwemo taasisi za serikali na chuo cha VETA.

  Kwa upande wake Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans alisema, mkutano huo pia utatumika kuangalia njia ambazo Don Bosco inaweza kutumia kushirikiana zaidi na sekta binafsi kama sehemu ya mipango endelevu.

  Alisema majadiliano mengine yatakuwa yanahusu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi namna ya kushirikiana ili kuboresha elimu.

  Ofisa Mwezeshaji Aira wa Don Bosco Tanzania, Oswald Manyerere alisema, lengo la mafunzo yanayotolewa na tasisi hiyo ni kuhakikisha wanawawezesha vijana wasiojiweza kupiga hatua na hatimaye kufikia malengo waliyojiwekea.

  Alisema vijana wanaopitia katika chuo hicho wamekuwa wakitafutiwa kazi baada ya kufanya mafunzo yao, ambapo kwa kipindi cha mwaka jana vijana waliomaliza walikuwa ni 322 na hadi sasa waliopatiwa kazi ni 220 huku idadi kubwa ikiwa ya wasichana sawa na asilimia 86.

  Alisema wanafunzi hao ni kutoka katika shule zilizochini ya Don Bosco, Dodoma, Iringa na  Oyterbay Dar es Salaam. 

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco,Celestine Kharkongor alisema Don Boscow ilianza hapa nchini mwaka 1996.

  Alisema tangu kuanzishwa kwa chuo cha Don Bosco kimeleta mabadiliko ya tabia kwa vijana pamoja na kuwakwamua kiuchumi.

  Mwalimu wa Don Bosco, Hellen Jackson alisema mafunzo yanayotolewa na chuo cha Don Bosco yatasaidia kutoa ajira kwa vijana na kuondoa changamoto zilizopo sasa za ukosefu wa ajira hapa nchini.

  Alisema wazazi wenye watoto wa kike ni fursa kwao kuwapeleka katika chuo hicho.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
   Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco Tanzania ,Celestine Kharkongor (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Don Bosco Oyterbay jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo na shughuli zinazofanywa na Don Bosco hapa nchini.
   Meneja Mipango wa Ofisi ya Maendeleo  Don Bosco Tanzania, Rosemarytery  Njoki (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco Tanzania ,Celestine Kharkongor, Mratibu wa Don Bosco, Maika Denys na Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans.
   Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
   Mratibu wa Don Bosco, Maika Denys (kulia), akichangia jambo.


   Mwalimu wa Don Bosco, Hellen Jackson (kulia), akielezea mafanikio makubwa wanayopata wanafunzi katika shule hiyo.
  Ofisa Mwezeshaji Aira wa Don Bosco Tanzania, Oswald Manyerere (kushoto), akielezea jinsi Don Bosco ilivyofanikiwa kuwatafutia ajira wanafunzi wao waliohitimu mafunzo mbalimbali.
  Mkuu wa Idara ya Utafuta wa ajira na Ofisa Masoko, Don Bosco Dar es Salaam, Nyerembe Yunus Nyampiga (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

   Mmoja wa wanafunzi wa DonBosco akielezea mafanikio wanayopata shuleni hapo.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
   Wanafunzi na walimu wao wakiwa kwenye mkutano huo.
   Wanafunzi wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
   Viongozi wa Don Bosco wakiwa meza kuu.
   Mkutano ukiendelea.
  Wanahabari na Wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

   Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
   Mhe. Wilson Masilingi   Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho  Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.  Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi, pamoja na Marystella Masilingi. Mke wa Balozi.
   Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurudi nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kukabidhi hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.

  0 0

   Mwanafunzi wa Sekondary ya Loyola akipelekwa kwenye gari kuelekea Hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo mchana, baada ya bajaj yenye namba za usajili MC 402 AWD waliokuwa wameikodi na wenzake Bandarini wakitokea Zanzibar kugongwa na Pickup Double Cabin yenye namba DFPA 826 katika makutano ya barabara ya Sokoine na Azikiwe jirani na Benki ya NBC. Katika ajali hiyo wanafuzi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali hiyo.
   Wanafunzi wa shule hiyo wakimfariji mwenzao Martha Silayo (katikati), aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
   Wananchi wakiangalia bajaj  iliyogongwa. Imeelezwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali wa bajaj hiyo ambapo pia dereva wake alijeruhiwa.
   Askari wa usalama barabarani na wananchi wakiwa eneo ilipotokea ajali hiyo.
  Bajaj iliyogongwa ikiwa eneo ilipopatia ajali 'Kweli BOGOTI imegongwa'
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

  0 0

  Maonyesho hayo yasiyo na kiingilio, yaliambatana na maadhimisho ya miaka 100 ya jeshi la maji nchini hapa.
  Maonyesho ya ndege za kivita na vifaa vingine kutoka majeshi ya Marekani, yamefanyika leo na kuhudhuriwa na maelfu ya watazamaji.
   Askari miavuli wakishuka kwa aina yake
   Mmoja wa askari wa mwavuli akishuka katika ufunguzi wa maonyesho hayo
   F-22 Raptor

   F-22 a.k.a Raptor na Mustang zikifanya onyesho la pamoja
   F-22 a.k.a Raptor ikisalimu watazamaji kwa mtindo wake
   Raptor. Ndege inayoaminika kuwa "kali" zaidi katika mashambulizi duniani
   F-22 Raptor inaaminika kuwa ndege ya thamani zaidi duniani, kila moja ikigharimu takriban dola za kiMarekani milioni 150
   F-16 Thunderbirds ambazo ndizo zilikuwa onyesho kuu kwa mwaka huu zikianza maonyesho
  C-5. Moja ya ndege kubwa za mizigo katika jesho la Marekani
   Mija ya injini za ndege zikiwa uwanjani kwa maonyesho
  Watu wakisubiri zamu yao kupata kumbukumbu kwenye "usukani" wa ndege
  Na "bodaboda" za angani nazo zilikuwepo
   F-35 Joint Strike Fighter (JSF) ni moja kati ya ndege mpya zaidi. Gharama ya kuitengeneza inakadiriwa itafikia dola za kiMarekani milioni 85 ifikapo 2018

  Kujua zaidi kuhusu ndege hizi, tazama mahojiano haya hapa chini yaliyofanyika 2011
  Picha kwa hisani ya Vijimambo na Kwanza Production 

  0 0

  Vijana wenye asili ya Kitanzania Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wameonyesha umahiri wa mchezo wa Tennis uliofanyika jana Jumamosi, September 19,2015 katika viwanja vya nyumbani kwao South East Tennis and Learning Center, South East Washington, DC.

  Briana Kagemuro alikuwa katika kinyanganyiro cha Wasichana wenye umri wa miaka 12 Singles (Girls 12 singles) ambapo alimshida Isabella De Leo 6-4,6-4; Cassi Chen 7-6,6-3,10-6 na Asha verma 6-4,6-4.

  Naye Bryan Mwombeki alipata kombe lake la ushindi la wavulana wenye umri wa miaka 10 (USTA) (Boy's 10 Singles) dhidi ya Jason De Silva 4-0,4-0, Arbert Vardimisky 4-3,4-1; Aarush Rajanala 4-1,4-2.

  Bryan Mwombeki

  Briana Kagemuro
  Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao wa mchezo huo mapema jana siku ya Jumamosi Septemba 19, 2015 baada ya kushinda makombe yao.

  0 0

    Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha  Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo mkubwa wakati akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
    Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
   Wakazi wa Chato wakishangilia kuonesha kuwa watampa kura za ushindi Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita. 
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mbele ya wakazi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita. 
   Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
   Wakazi wa Chato ilkuwa ni shangwe tu kila kona ya uwanja. 
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ,Joseph Kasheku almaarufu King Msukuma akiwaomba ridhaa wananchi wa Chato ya kumchagua Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli ili aweze kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano.
   Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia  wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
    Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
   Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
  Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
   Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano,pichani kati anaeshuhudia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli. 
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Chato mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.


   Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia  katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu. 
   Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu. 
   Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.

   Mama Janet Magufuli, mke wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia  katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.
   Sehemu ya maelfu ya wananchi   katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari  mkutano wa kampeni 
  Sehemu ya maelfu ya wananchi   katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari  mkutano wa kampeni.
  Picha na Ahmad Michuzi Jnr.

  0 0

   Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kwenye  uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka huu. 

  Mara bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari kilihemewa na simu za wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea furaha yao sio tu kwa kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini. Mama Magufuli amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani kwao Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga na bila kumung'unya maneno. 
  Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
   Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano 
  Wananchi wa Chato wakimshangilia Mama Magufuli kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato  mkoani Geita.

  0 0

  Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph).
  Na Andrew Chale, modewjiblog [Dar es Salaam] 
  CHAMA cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae.

   Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.

   Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe.

   Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia. “Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye. Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.
   Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana na bidhaa za Tumbaku.Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa mbalimbali.

  Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.

  Changamoto kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa mapato ni madogo kuliko madhara. “Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na mengine mengi. Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na madhara yanayofanana.

   Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk. Ali Mzige. Kwa upande wao wanaharakati wa kupambana na matumizi ya sigara kutoka chuo cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao ya African Fight Cancer, Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa, ni wakati wa kuepuka vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani wasipofanya hivyo wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.
  Mwalimu Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake. 

  Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho ambaye pia alikuwa mgeni katika kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu na wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao mara kwa mara ili kuwakinga na vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto wadogo.

  Mradi huo wa ’80 Children Strong’, unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) unafadhiliwa na Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation ambalo linahusiana na American Society for Clinical Oncology (ASCO) ya nchini Marekani (Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba ya saratani. 

  Hata hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila mtoto anapata haki ya kuelimishwa kujikinga na matumizi hayo mabaya ya tumbaku, ambapo kwa darasa la watoto 80, asiwepo hata mmoja atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya matumizi ya tumbaku hivyo wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali nchini. Kwa upande wa shule hizo zilizohudhuria kongamano hilo ni pamoja Shule ya Msingi Mapambano, Kijitonyama Visiwani, Victoria, Mwananyamala B, Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa, Shekilango na Mapambano. Kwa upande wa watoto hao walipata pia wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa majibu huku pia kukifanyika na masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na ngonjera zilizokuwa na jumbe mbalimbali za kupambana na matumizi ya tumbaku.
  Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku.DSC_0019
  Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.
  Kikundi cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi hatari ya Tumbaku.
  Wanafunzi wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.
  Bernard Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani
  Shairi mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
  Mwanafunzi wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango (kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.
  Wawili kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.
  Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.
  Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
  Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa vijana walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku kwani ni hatari kwa afya za binadamu
  Waandhishi wa habari wakiwa kazini.
  Afisa Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa neno kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi
  Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akisaini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Cheki.co.tz mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha Biafra jijini Dar wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya magari na bidhaa shirikishi ya Auto Fest.

  Tarehe 19 Mwezi wa septemba 2015 Mtandao wa magari unaoongoza nchini Tanzania Cheki.co.tz umetimiza mwaka mmoja wa utoaji huduma ya kipekee na iliyo salama ya biashara ya kuuza na kununua kwa njia ya mtandao pande zote za Tanzania. 

   Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa utendaji wetu, maelfu ya watu wamekuwa wakitembelea tovuti yetu kila siku na maelfu ya magari yamenunuliwa.

   Msingi wetu wa wateja umeongezeka mara 21% tangu uzinduzi . 90% ya wafanyabiashara wa magari nchini utumia mtandao cheki.co.tz kuuza magari yao na zaidi ya 50 ya majengo ya kuuzia magari nchini yana nembo ya Cheki.co.tz katika sehemu zao “Nayaweka mafanikio yetu katika mambo mawili: Kwanza, unatokana na urahisi wa kununua, kwani tumewezesha wateja kununua gari wakati wowote, na mahali popote wanapohitaji. 

  Sababu ya pili, ni mahusiano mazuri na wauzaji wa magari uliotokana na ubora wa biashara” alisema Bwana Mori Bencus, Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania.

  Naye Juliana Ntemo, Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz alisema, “ tuna shauku ya kuboresha zaidi huduma yetu kwa miaka ijayo kwa kuendelea kutoa huduma ya uuzaji na ununuzi kwa njia ya mtandao iliyo salama na ya kipekee kabisa”.

  Ushuhuda wa kipekee kutoka kwa wateja kwa mwaka 2015 Cheki wameturahisishia biashara, tunapata wateja kutoka nchi nzima.Wateja wanaingia moja kwa moja cheki.co.tz na kuona magari yakiwa na maelezo muhimu,na kama mtu anahitaji anawasiliana nasi- Ramadhani Makame, Planet Motors Cheki.co.tz ni duka la kimtandao, ambapo wanunuzi wa magari na wauzaji wa Kitanzania hukutana.

   Ndani ya tovuti hii magari ya kila aina yanapatikana kwa wanunuzi Tanzania nzima huku wauzaji wakipata fursa ya kuuza zaidi. Tembeleawww.Cheki.co.tz
  Mfanyakazi wa kampuni ya Cheki.co.tz akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) kuhusu ununuaji na hata kuuza gari kupitia mtandao.
  Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (kushoto) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) wakati wa ufunguzi wa maonyesho.
  DSC_0390
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akikata keki ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni ya kuuza na kununua magari ya Cheki.co.tz. Kushoto ni Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus akiwa na Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (katikati).
  DSC_0406
  Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus (kushoto) akimlisha keski mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia).
  DSC_0404
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo(kulia) akimlisha keki Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus baada ya kampuni ya Cheki.co.tz kutimiza mwaka mmoja.
  DSC_0405
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akimlisha keki Bw. Ally Nchahaga kwa niaba ya watu wote waliofika kwenye ufunguzi huo.
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo.
  Bw. Ally Nchahaga ambao ni waandaaji wa tamasha la magari Tanzania (Autofest) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar. 
  Mkurugenzi wa CW Net Tanzania, Desmond Andrew(kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo kuhusu matumizi ya modem za CW Net wakati alipitembelea banda hilo.
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kushoto) akitizama modem ya CW Net zinazotengenezwa na watanzania na kutumia laini ya mtandao wowote ndani na nje ya nchi.
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akipata maelezo kutoka kwa Bw. Zohail Hassanali (kushoto) kuhusu uzibaji wa pancha kwenye magari na vifaa gani mtu anabidi kuvitumia.
  Bw. Athman Hamis ambaye ni mwakilishi wa Auto Mobile akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo alipokuwa anatembelea mabanda hayo
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonesho hayo akipata ufafanuzi kuhusu uoshaji wa magari kutoka kwa Afisa Mauzo wa KARCHER, Josephine Scarion.
  Mfanyakazi wa Kampuni ya TFL Motor Group, Maria C. Sangiwa (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo kuhusu uuzaji wa magari na hata kufanya service ya magari yote. Katikati ni Khalid Abdallah.
  Maonesho ya uendeshaji wa magari yakiendelea katika viwanja vya Biafra jijini Dar. (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)

  0 0

  IMG_9847
  Meza kuu katika warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Kazi na Ajira kitengo cha Ajira, Joseph Nganga, Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya Kazi na Ajira, Ally M. Ahmed, Mkuu wa utafiti na machapisho Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga.
  (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Na Mwandishi wetu
  PAMOJA na kuwepo na maendeleo ya kuridhisha katika suala la ajira kwa vijana, serikali imekiri kwamba ukosefu wa ajira bado ni tatizo kubwa duniani na kwa taifa kwa ujumla.

  Kutokana na hali hiyo suala la ajira kwa vijana limebaki kuwa ajenda kuu nchini.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya kazi Ally M. Ahmed wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton.

  Alifanya ufunguzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wiza
  ra hiyo Eric Shitindi.

  Alisema Tanzania inaendelea kukabiliana na tatizo la ajira kutokana na wigo mdogo wa fursa za ajira, tatizo la utaalamu na ukosefu wa uzoefu .

  Alisema hata hivyo vijana wanaoamua kujiajiri wenyewe wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na utaalamu katika ujasiriamali utakaowawezesha kuendesha miradi wanayoibuni.

  Alisema kutokana na uwapo wa sera, mipango na miradi ya maendeleo kuhusu ajira kwa vijana inayoendeshwa kitaifa na kimataifa kumekuwepo na dalili njema za kupungua kwa ukosefu wa ajira.

  Alisema utafiti wa mwaka 2014 (ILFS) umeonesha kwamba ukosefu wa ajira umepungua kutoka asilimia 11.7 kwa mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 10.3 ka mwaka 2014 huku kwa vijana (wenye umri wa miaka 15 hadi 35) ukipungua kutoka asilimia 13.2 kwa mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 kwa mwaka 2014.
  IMG_9768
  Mkuu wa Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa hotuba ya utangulizi katika warsha ya vijana na ajira iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton. 

  Katika hotuba yake ya ufunguzi alitoa wito wa washiriki kuangalia kwa undani tatizo la ajira kwa vijana na kutoa mwelekeo utakaosaidia watunga sera kuwa na sera madhubuti kuhusu ajira kwa vijana.

  Alisema mafanikio yaliyopatikana hayaondoi ukweli kuwa kuna tatizo kubwa la ajira miongoni mwa vijana na kutokana na mazingira ya sasa ni vyema wadau wa ajira kuangalia kwa undani tatizo la ajira la sasa ili kutoa ushauri wa kukabiliana nalo kwa kipindi kifupi na kirefu.

  Shitindi alisema kwamba serikali inafurahishwa na juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kutafuta majibu ya tatizo la ajira, majibu ambayo alisema yakifanywa vyema yatasaidia sana wataalamu wa serikali kutengeneza sera na kanuni zitakazo kidhi haja.


  Alisema ipo haja kwa wachambuzi (watafiti) kuelekeza nguvu zao katika kutafiti soko la ajira ili kusaidia watengeneza sera kuona mahitaji ya soko katika miaka kadhaa ijayo.

  Alisema wakati uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka kwa miaka kumi iliyopita ajira zimekuwa haziendi sambamba na ukuaji wa uchumi na hivyo kuleta maswali mengi ya sintofahamu.

  Alisema serikali kwa sasa inataka kuhakikisha kwamba inaboresha upatikanaji wa ajira lakini hilo linawezekana kama taasisi zake zinazotengeneza sera na kuweka mipango zinatambua tatizo na kuona namna ya kuliangalia.

  Alisema watafiti wana wajibu mkubwa wa kusaidia serikali kuwezesha vijana kuwa na kazi zenye staha kama sera ya ajira ya taifa inavyotaka.
  IMG_9895
  Mkurugenzi wa kazi wizara ya kazi na ajira, Ally Msaki Ahmed, akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika warsha ya kitaifa ya ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Duble Tree by Hilton. Katika hotuba yake aliwataka washiriki kujadili kwa makini matatizo ya vijana na kutoa suluhu itakayosaidia watendaji kutunga sera na kutoa mwelekeo mpya wa kukabiliana na tatizo hilo.

  Alisema kwa kuangalia ukuaji wa kisekta, sekta ambayo sasa hivi inahitaji watu ndio ambayo haina wataalamu wa kutosha na hivyo ukuaji wa sekta hizo kama za mawasiliano hauendi sanjari na utaalamu uliopo katika soko.

  Katibu Mkuu huyo alitoa wito kwa watu binafsi na serikali kuhakikisha kwamba wanakabiliana na vikwazo vya ajira kwa kutoa elimu na taaluma ili fursa zionekane na kutumika ipasavyo.

  Alisema tija inaweza kuonekana katika ukubwa wa utaalamu, ubunifu na namna mafunzo yanavyowawezesha wanafunzi kuwa na uhakika na kazi wanazotaka.

  Alisema ipo haja kwa wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba vijana wanaingizwa katika soko la ajira na tatizo la ajira linapunguzwa.
    IMG_9829
  Kiongozi Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo, Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC), Dk. Arjan de Haan akielezea sababu za taasisi hiyo kuunga mkono tafiti kwa ajili ya kusaidia kupatikana ufumbuzi wa tatizo la ajira katika warsha ya ajira na vijana iliyofanyika Double Tree by Hilton hotel.

  Katika moja ya maazimio yaliyotolewa na washiriki vijana, walitaka kuwepo na mabadiliko makubwa katika utoaji elimu, ambapo walisema elimu itolewe kwa Kiswahili lakini pia wanafunzi waandaliwe kuwa wabunifu na kujiajiri.

  Aidha wametaka kurejeshwa kwa shule za ufundi na shule maalumu kama ilivyokuwa zamani.

  Walisema vijana Wanatakiwa kushiriki katika utengenezaji wa sera na kanuni na si kushirikishwa na kutaka matakwa yao yanastahili kuangaliwa na kuzingatiwa ili mtu ajifunze kila anachoona anaweza kukifanya vyema.
  Warsha hiyo ya ajira kwa vijana imewezeshwa na IDRC na kuratibiwa na ESRF na mada mbalimbali ziliwasilishwa ambazo zilichambua masuala ya elimu, elimu ya ufundi, changamoto na fursa za vijana katika ajira.
  Aidha kulikuwa na mada za majukumu ya serikali na sera katika kuboresha mchakato wa ajira kwa vijana.
  IMG_0011
  Mchumi na Mshauri huru Bi. Mahjabeen Haji akiwasilisha mada kuhusu hali ya ajira kwa vijana nchini katika warsha ya vijana na ajira ilyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton, katika mada yake alielezea mazingira ya ajira ambapo elimu katika sekta zinazokua kwa kasi kama Tehama ni kikwazo kikubwa katika kuwezesha ajira kwa vijana.
    IMG_9932
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene wakati warsha hiyo ikiendelea.
  IMG_0154
  Mkurugenzi wa Salama Foundation, Shadrack John Msuya akiwasilisha mapendekezo ya vijana juu ya namna ambavyo vipaji, elimu na ubunifu vinavyoweza kutengeneza ajira kwenye maeneo ya Sayansi, Teknolojia, Kilimo na Ufugaji.Moja ya azimio ni kuwa na sera mpya ya vijana yenye mpango mkakati na tafiti zinazotekelezeka katika warsha ya vijana na ajira.
  IMG_0180
  Mshauri mwelekezi katika uanzishwaji na uendelevu wa biashara na maendeleo ya jamii, Gidufana Gafufen akiwasilisha mapendekezo yaliyowasilishwa katika vikundi nini kifanyike ili vijana wapende kilimo katika warsha ya vijana na ajira iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton.
  IMG_9875
  Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau pamoja na makundi ya vijana waliohudhuria warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
  IMG_9704
  IMG_9952
  IMG_9944
  IMG_0110
  Mmoja wa washiriki akitoa maoni kwenye warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
     
  IMG_0348

  Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
  IMG_0354
  IMG_0150
  Pichani juu na chini ni wadau kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki warsha hiyo wakibadilishana mawazo.
  IMG_0130
  Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga (kulia) akiteta jambo na baadhi ya washiriki.
  IMG_0134
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akifurahi jambo na Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole Saibul mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.

  0 0

   Washiriki wa Jogging iliyoandaliwa na kituo cha mazoezi ya viungo cha Home Gym Mwenge jijini Dar es Salaam kilichopo chini ya Andrew Mangomango (kulia) kwa lengo la kuhamasisha umuhimu wa mazoezi kwa ajili ya afya ya mwili na akili ambapo kituo hicho kimetimiza miaka 17 tangu kuanzishwa, mbio hizo zilianzia Mlimani City na kuishia ufukwe wa Escape One. (Picha na Francis Dande) 
   Washiriki wakiwa katika Jogging.

   Washiriki wakiwa katika Jogging.
  Wanachama wa kituo cha mazoezi ya viungo cha Home Gym Mwenge wakikata keki wakati wa kusherehekea mika 17 tangu kunzishwa kwa kituo hicho, hafla hiyo ilifanyika katika Ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Mazoezi ya Viungo cha Home Gym Mwenge cha jijini Dar es Salaam (kulia) akilishwa keki na mke wake wakati wa hafla ya kutimiza miaka 17 tangu kuanzishwa kwa kituo hicho.
   Watoto wakilishwa keki wakati wa hafla hiyo.
   Watoto wakilishwa keki wakati wa hafla hiyo.
  Kukata keki.
  Washiriki wa Jogging hiyo.
   Mwalimu wa mazoezi ya viungo kutoka Kituo cha Home Gym Mwenge cha jijini Dar es Salaam, Andrew Mangomango akiwapa mazoezi washiriki wa Jogging iliyofanyika leo kuanzia Mlimani City na kuishia Escape One.
   Mazoezi yakiendelea.
   Mazoezi yakiendelea.
   Mazoezi yakiendelea.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani humo leo Sept 20,2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule  wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim Pannja zilizofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu  Mkoani Mbeya.
   Wasanii wa kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenen Salim Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo Tukuyu  Mkoani Mbeya.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na kumpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa hilo Mchungaji Kenan Salim Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo Tukuyu  Mkoani Mbeya.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Kenen Salim Panja baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo Tukuyu  Mkoani Mbeya.
    (Picha na OMR)

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme kijiji cha Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani ,Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo  Mkoani humo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibonyeza kitufe   kuzindua Mradi wa  Umeme kijiji cha Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani ,Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo  Mkoani humo
   Kikundi cha ngoma kutoka Mkoa wa Kusini pemba kikitumbuiza ngoma ya Gonga wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa  Umeme kijiji cha Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani ,Mkoa wa Kusini Pemba leo uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo  Mkoani humo
   Mradi wa  Umeme katika kijiji cha Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani. Mkoa wa Kusini Pemba, ulipozinduliwa leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi katika uzinduzi wa Mradi wa  Umeme katika kijiji cha Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani ,Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo  Mkoani humo. 
  0 0

   Picha ya aliyekuwa Mgombea wa Udiwani kata ya Muleba kwa tiketi ya chama cha CCM,enzi za uhai wake,aliyefarika jana kwa ajali ya Piki Piki
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akitoa maneno ya pole kwa ndugu jamaa na marafiki leo asubuhi nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba,Marehemu Osward Peter Rwakabwa katika kijiji cha Kagabilo,Muleba mkoani Kagera. 
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba kwa chama cha CCM,Marehemu Osward Peter Rwakabwa katika kijiji cha Kagabilo,Muleba mkoani Kagera
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwapa mkono wa pole ndugu jamaa na marafiki leo asubuhi nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba,Marehemu Osward Peter Rwakabwa katika kijiji cha Kagabilo,Muleba mkoani Kagera,aliyefarika jana kwa ajali ya Piki Piki
   Baadhi ya Ndugu Jamaa na Marafiki wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu Osward Peter aliyefarika jana kwa ajali ya piki piki,Wakiomboleza kufuatia msiba huo.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

  PICHA NA MICHUZI JR-MULEBA,KAGERA.

  0 0
 • 09/21/15--01:07: BEI YA MADAFU HII LEO.


older | 1 | .... | 646 | 647 | (Page 648) | 649 | 650 | .... | 1897 | newer