Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MABADILIKO YA KAMATI NDOGO ZA TFF

$
0
0

Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichofanyika Septemba 06, mwaka huu kilifanya mabadiliko madogo ya kamati zake ndogo ndogo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Blassy Kiondo aliyekua Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni na Sakafuni (Beach Soccer and Futsal).

Amina Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake nchini (TWFA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake.


MWALIMU NYERERE KATIKA UGA WA USHAIRI

$
0
0
  RAIS wa awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  alizaliwa mwaka 1922 katika  Wilaya ya Butiama Mkoa wa  Mara, mnamo tarehe 14 Oktoba, 1999, aliaga dunia katika hospitali ya mtakatifu  Thomas  Jijini London nchini Uingereza.  

Katika uhai wake,  alikuwa ni Mmalenga.   
Aliandika barua ya Kiserikali kwa mtindo wa utenzi, pia alijibiwa barua hiyo  kwa mtindo wa utenzi na Nguli/Karii,  Hayati Saadani Abdul Kandoro aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mnamo mwaka 1964.

Nukuu ya Hayati Saadani A. Kandoro “Huu ni utenzi ulioandikwa kwa njia ya barua iliyotungwa na Muheshimiwa Mtukufu mwalimu J.K. Nyerere  President wa TANU na Serikali. Aliniletea barua hiyo ili kunizungumza jinsi ya watu wanaopenda kujisaidia katika shughuli za maendeleo na jinsi ya kuwapa moyo dhidi ya adui wa jamii katika shughuli za vijiji”.
 Picha ya Hayati Mw. J.K. Nyerere

                       SHEIKH KANDORO, SIKIA!
1.     Sheria  husaidia,
Kuijenga Tanzania,
Siyo kazi ya sheria,
     Nchi kutuharibia.

2.     Kila nchi ina nia,
Inayoikusudia,
Vile vile ina njia,
   Itakayoipitia.

3.     Tanzania tuna nia,
Ya kujenga ujamia,
Na  njia ya kupitia,
  Ni wote kusaidia.

4.     Kijiji cha turadhia,
Kisima kujipatia,
La magambo limelia,
  Watu wakahudhuria.

5.     Wakakubali kwa nia,
Kisima kujichimbia,
Aliyewakatalia,
   Kukuye wakamlia.

6.     Akenda kushtakia,
Kwa hakimu wa sheria,
Kwamba wamemuonea
    Kuku wake kalmia.

7.     Hakimu akasikia,
Akaita jumuia,
Wakaja akawambia,
    Nyinyi wavunja sheria.

8.     Basi nawahukumia,
Faini shilingi mia,
 Na sabini za fidia,
    Au jela kuingia.

9.     Hakimu wakamwambia,
Itatushinda fidia,
Hata na faini pia,
    Heri jela kuingia.

10.             Wakafungwa kwa sheria,
Na maji wakamwachia,
Mwenye kuku kuumia,
     Pamwe na Hakimu pia.

11.             Huko ni kusaidia,
Adui wa jumuia,
Nasi kazi ya sheria,
    Ila ya maharamia.

12. Kazi hasa ya sheria,
Kusaidia raia,
Sina nia kuwavunjia,
Wanapojisaidia.

“JIBU LA SHEIKH S.A. KANDORO ALIYEKUWA AREA COMMISSIONER BAGAMOYO, KWA SHAIRI LA MHESHIMIWA MWALIMU J.K.NYERERE, RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA”
“Huu ni utenzi niliandika kama barua ya kumjibu Mheshimiwa Mtukufu Mwalimu J.K. Nyerere President wa TANU kujibu utenzi wake alioniandikia juu ya wanaoharibu maendeleo ya kijiji katika kazi za jamii”.

Picha ya Hayati sheikh S. A Kandoro

1.     Labeka Mheshimiwa,
Julius msifiwa,
Kambarage muelewa,
    Bwana nakuitikia.

2.     Nakuitikia sheria,
Kwamba inasaidia,
Kuijenga Tanzania,
    Na ni nguzo ya Dunia

3.     Kutoheshimu sheria,
Huleta wingi udhia,
Amani ikapotea,
     Nchi zikaangamia.

4.     Ni msumeno sheria,
Mithali hii natia,
Haitaki kubabia,
    Pendelea liso njia.

5.     La mgambo likilia,
Watu wote hudhuria,
Kisima kujichimbia.
     Hilo lataka sheria.

6.     Kuna wavivu wa nia,
La mgambo likilia,
Nao anajikalia,
   Huendi kuhudhuria.

7.     Mfano huo hatia,
Wengine huufatia,
Na wao hujikalia,
Kazi zetu husinzia.

8.     Kimila nimesikia,
Waweza kumsikia,
Kuku wake kujilia,
Lakini sio sheria.

9.     Kwa kuwa sio sheria,
Mvivu hujishitakia,
Na walao huumia,
Pia hutozwa fidia.

10.            Twazidi kukulilia,
Ifanywe hasa sheria,
By Law kuitia,
Yaweza kusaidia.

11.            Yaweza kusaidia,
Kuku tukijilia,
Pasiwepo hata njia,
Mvivu kukimbilia.

12.            Kuku tumejilia,
Pasiwe na kuponyea,
Hakimu kumuendea,
Kwamba alipwe fidia.


13.            Mkazo twaukazia,
Bila nyuma kurudi,
Twataka kuendelea,
Kuinua Tanzania.

14.            Taifa kuitikia,
Kazi kuzishangilia,
Ndilo tunalolilia,
Ndipo tunakazania.

15.            Ndipo tuna kazania,
Na tena tuna kania,
Kuishangaza dunia,
Lengo letu kutimia.

16.            Bila nguvu kuzitia,
Mkazo wa kisheria,
Unafaa kufatia,
Kazi zitaendelea.

Utii wa Sheria bila kushurutishwa:

Nukuu ya  S .A . Kandoro , Mashairi ya Saadan,
(Jina la Ushairi ; Staharaki kwa tendo ),
  (UK. 162-166)
Mnukuu; Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo;
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni; Sehemu ya Lugha.
Hajjati  S . Kitogo na C. Mhongole

MTANDAO WA EVERJOBS TANZANIA KUWAKUTANISHA WAAJIRIWA NA WAAJIRI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs wa Ukanda wa Afrika Eric Lauer, akiwaelezea waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa jinsi mfumo wao wa tovuti ambao unaweza kuwaunganisha waajiri na waajiriwa kwa urahisi kabisa huku waajiri wakipata nafasi ya kuweza kupata taarifa zote muhimu kutoka kwa wanaoomba kazi kupitia tovuti hiyo pindi wanapokuwa wamejiunga na Kampuni ya Everjobs Tanzania.Mkutano huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es salaam.
 Mkurugenzi wa Everjobs Tanzania, Florens Roell akielezea namna ambavyo waajiri na waajiriwa wanaweza kunufaika na Kampuni ya Everjobs Tanzania ambayo inatoa nafasi kwa waajiriwa kuweza kuomba kazi kupitia tovuti yao ya www.everjobs.co.tz.
 Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Everjobs Tanzania Lucas Masson (wa pili kutoka kulia) akielezea jinsi ya waajiliwa ambavyo wanaweza kujiunga katika tovuti yao ya www.everjobs.co.tz na kuweza kuona nafasi za kazi mbalimbali zinazotangazwa kupitia tovuti hiyo na kuweza kuomba kazi hapo hapo kupitia tovuti.
Mmoja wa wageni waalikwa akiuliza swali kwa Wakurugenzi na maafisa wa Everjobs wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa uliofanyika jana
  Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs Katika Ukanda wa Afrika Eric Lauer (wa kwanza kushoto) akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano uliofanyika jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar
 Mmoja wa wageni akitoa shukrani kwa wamuluki wa kampuni ya Everjobs Tanzania kwa kuona changamoto na kuifanya kuwa fursa.
  
Baadhi ya Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo

COPA COCA COLA KUFANYIKA MWAKANI

$
0
0

MASHINDANO ya Copa Coca Cola yanayodhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Coca Cola yaliyokuwa yafanyike katikati ya mwaka huu, sasa yatafanyika mapema mwakani mwezi Februari kuanzia ngazi ya Wilaya na fainali zake kufanyika mwezi Juni na Julai 2016.

Michuano hiyo ambayo hushirikisha timu za mikoa yote Tanzania kuanzia katka ngazi ya Wilaya, hufanyika kila mwaka kwa kuwashirkisha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15).

Taarifa ya Idara ya Masoko ya Coca Cola imesema kampuni hiyo imeahirisha kufanyika kwa michuano hiyo wa mwaka huu, na sasa itafanyika mwakani ili waweze kupata nafasi ya kuandaa vizuri mashindano hayo.

Tuna uzoefu na mashindano hayo, ni vyema tukaifanya wakati wa likizo wakati vijana wakiwa mapumziko, sababu wachezaji wote wa michuano ya Copa Coca Cola ni wanafunzi hivyo ni vizuri tukaandaa mashindano hayo wakati wanafunzi wakiwa likizo.

Michuano ya Copa Coca Cola ilianza mwaka 2007 kwa kushirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U17) na baadae mwaka 2012 kubadilishwa na kuwa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15).

Baadhi ya wachezaji waliopatikana katika mashindano hayo kwa sasa wanacheza katika vilabu vikubwa vya Ligi Kuu ya Vodacom nchini na wengine wamepata naafasi ya kucheza soka nje ya nchi.

ZAIDI YA WATU 500 WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA BONANZA LA KUSHEREKEA MIAKA 17 TANGU KUANZISHWA KITUO CHA MAZOEZI CHA HOME GYM

$
0
0

ZAIDI ya watu 500 wanatarajiwa kushiriki katika bonanza la kusherehekea miaka 17 tangu kuanzishwa kituo cha mazoezi cha home gym kilichopo mwenge jijini dar es salaa litakalofanyika juma pili hii ya septemba 20 katika viwanja vya Escape One.

Andrew Mangomango ni mkurugenzi wa kityuo hicho ametanabaisha kuwa maandalizi yote yamekamalika na kusema kuwa miongoni mwa watu watakaoshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na vikundi vya Joging vya jijini DSM, vutio vya gym na yeyote atakayehitaji kushiriki katika bonanza hilo.

Miongonui mwa mambo yatakayoshamirisha bonanza hilo ni pamoja na kutembelea hospitali ya palestina  ya sinza jijini DSM na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa sanjari na kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Bonanza hilo litakalofanyika katika viwanja vya Escape One litaanza Mlimani City majira ya saa kumi na mbili asubuhi kwa washiriki kukimbia kwa mwendo wa taratibu pamoja na kutembea kwa kundi linguine.

Akitaja ratiba kwa siku hiyo amesema baada ya kuwasili katika viwanja hivyo saa mbili asubuhi itaanza AEROBICS mpaka saa nne asubuhi na mara baada ya hapo kutakuwa na michezo mbalimbali ksms vilr kuvuta Kamba, kukimbia na magunia, kukimbiza kuku kunyanyua vitu vizito , kutunisha misuli, mpira wa miguu pamoja na Burudani ya muziki,  lakini pia kutakuwa na michezo mbalimbali kwa watoto hivyo kuwataka wazazi kwenda na watoto wao ili kufurahia kwa pamoja.

Bonanza hilo limebeba kauli mbiu isemayo FANYA MAZOEZI KWA AFYA YAKO likiwa na lengo la kuwahamasisha watu wote kushiriki katika mazoezi ili kutunza afya zao.

Kituo hicho cha mazoezi kilichoanzishwa mwaka 1998  kimekuwa na mchango mkubwa katika kujenga na kulinda afya za watu wengi kupitia mazoezi.

CHART-SIKILIZA NYIMBO NA KUPATA HABARI KUPITIA POAAPP

$
0
0


“PoaApp” ni application mpya ya kitanzania itakayokujia hivi karibuni kwenye simu yako. Kama mtumiaji, utakuwa na uwezo wa kuchati na marafiki zako na ndugu, kusikiliza nyimbo uzipendazo na utaweza kupata habari za kitaifa na kimataifa;vitu hivi utavipata bure kutoka “PoaApp”.

Kwa habari zaidi kutoka “PoaApp’’ tafadhali fuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii kama;
• Facebook.com/PoaApp
• Twitter:@PoaApp
• Instagram:@PoaApp


Pia waweza kutembelea website yetu ya “www.poaapp.co.tz” ili uweze kujiandikisha punde “PoaApp” ikiwa tayari tutakutumia link ya kudownload.

“kuwa mzalendo,penda vya nyumbani”

MWENENDO WA KAMPENI ZA CCM

$
0
0
HADI jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720.
 Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.

Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. 

Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM.

Kwa upande wa kampeni zetu za Ubunge,  zaidi ya robo tatu ya wagombea Ubunge wa CCM wamekwishazindua kampeni zao na wanaendelea vizuri. Sekretarieti ya Kampeni ya CCM inaanda program maalum ya kampeni
katika majimbo yenye changamoto mahsusi.


Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wana-CCM kwamba viongozi na makada wengine wa CCM, waliopo madarakani na wastaafu watapita tena, jimbo kwa jimbo, nchi nzima katika siku 30 za mwisho katika jitihada za kuongeza ushindi wa CCM na Dr. Magufuli.

MIDAHALO YA WAGOMBEA
Wiki tatu zilizopita, CCM, na kwa hakika vyama vingine pia, ilipokea mwaliko wa Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea Urais uliondaliwa na Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kadhaa, ikiwemo Twaweza. 


Dr. Magufuli amekubali kushiriki katika mdahalo huo. Kwa msingi huo, kauli ya UKAWA iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndugu James Mbatia, kwamba UKAWA inaomba mdahalo ni njia ya kuwahadaa Watanzania tu kwa kuwa mwaliko wa mdahalo ulikwishatolewa mapema kwa vyama vyote na wanaotakiwa kushiriki ni wagombea Urais wa vyama.

CCM inafurahishwa na utamaduni wa midahalo ambao unaanza kujitokeza
katika chaguzi zetu. 
Na inaamini kwamba midahalo ya Wagombea Urais ni
sehemu muhimu ya kuwashirikisha wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi na kuwasaidia waamue nani wamchague kwa misingi ya hoja na sera na sio kwa ushabiki, kwa mihemko, na kwa propaganda. 

Mdahalo unatoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali ya moja kwa moja na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sera na ahadi zao, fursa ambayo hawaipati kwenye mikutano ya hadhara kampeni.

Hatukubaliani na kauli ya UKAWA kwamba mdahalo usiwe baina ya wagombea
bali uwe baina ya Wenyeviti wa Vyama. Tunaamini hoja hii ni kichekesho. Haijawahi kutokea popote duniani kwenye utamaduni wa midahalo, kwamba wagombea wasishiriki bali watu wengine ndio wafanye midahalo kwa niaba yao.  Tunaamini mdahalo huu unapaswa kuwa baina ya wagombea. Wao ndio wanaoomba dhamana. Wao ndio wanaopaswa kujibu maswali na kufafanua kuhusu ahadi zao.

CCM inaamini kwamba ili mdahalo huu uwe na tija, wagombea Urais wote,
hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Mdahalo hautakuwa na maana
kama mgombea mmojawapo wa vyama vikuu atatengeneza kisingizio ili asishiriki.

UCHAGUZI WA AMANI
CCM inasikitishwa na kauli zinatolewa na baadhi ya viongozi wa UKAWA zenye kuashiria fujo na vurugu. Kauli kwamba kura zitaibiwa hazina msingi wowote. Kauli hizi zinaashiria maandalizi ya kushindwa na maandalizi ya kufanya vurugu baada ya matokeo ya kushindwa.

Utaratibu wa uchaguzi wetu unajulikana na umekubalika na vyama vyote. Kura zinapigwa kituoni na kuhesabiwa kituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote, wasimamizi wa uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Baada ya kura kuhesabiwa, matokeo yanajazwa katika fomu ambayo kila wakala anasaini na kupewa nakala.

 Nakala ya matokeo hayo pia inabandikwa nje ya kituo cha kupiga kura. Kila Chama, na kila Mtanzania, kina fursa ya kujumlisha matokeo yake kwenye kila kituo na kupata jumla kuu. Matokeo ya nchi nzima yanajumlishwa mahala pamoja huku kukiwa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wawakilishi wa vyama vyote na wao wakiwa na fomu zao za kila kituo nchi nzima.

Tunapenda kuwasihi Watanzania wasikubali vishawishi vya kufanya vurugu. Mara nyingi, viongozi wanaohamasisha vurugu wanakuwa na ulinzi au walinzi au uwezo wa kukimbilia pahala penye utulivu zaidi huku wakiwaacha wafuasi wao katika wakihangaika.

UCHAGUZI NA UMOJA WA KITAIFA
CCM pia inapenda kusisitiza imani yake kwamba uchaguzi haupaswi kutugawa kama taifa. Uchaguzi ni tukio la kupita. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Kuna taifa baada ya uchaguzi. Lazima taifa liendelee kubaki moja, tuendelee kubaki wamoja. Tusitoe kauli za kupitiliza zenye mrengo wa kujenga chuki katika jamii na kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

Kama Chama kilichoasisi umoja wa taifa letu, tunaendelea kuasa kwamba
wanasiasa wasijinadi kwa misingi ya udini, ukabila wala ukanda. CCM haina mpango kuendeleza mjadala wa kauli ya Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa aliyoitoa kanisani Tabora tarehe 6 September 2015kwamba nchi ilishapata viongozi Wakatoliki na kwamba sasa ni zamu ya Walutheri kuchukua nafasi hiyo. 

Tunaamini mjadala huo hauna tija. Tunaamini kwamba Watanzania wengi, wa dini na madhehebu yote, hawaamini katika siasa za namna hii. Tuliamini kwamba UKAWA ingetumia fursa ya mkutano wao na waandishi wa habari jana kuomba radhi kwa Watanzania.

 Kwakuwa hawakufanya hivyo, tunapendekeza mjadala wa jambo hili ufungwe. Itoshe tu kwamba Ndugu Lowassa amesema hivyo, Tume ya Uchaguzi imemuonya, na yeye hajajitokeza kuomba radhi wala kufafanua. Watanzania wamemjua ni kiongozi wa aina gani na watatoa hukumu yao tarehe 25 Oktoba 2015.
Imetolewa na:-

January Y. Makamba,
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI YA CCM
16/9/2015


RAIS KIKWETE AKAGUA MAENDELEO YA KITUO CHA MICHEZO KWA VIJANA CHA KIDONGO CHEKUNDU DAR ES SALAAM

$
0
0
  Kituo cha Michezo kwa vija na cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam kinavyoonekana kutoka angani.
 Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wakituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland  ya Uingereza na kampuni ya symbion.

 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wakituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland 
ya Uingereza na kampuni ya symbion
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa kocha wa vijana wa kandanda mwenyekutambulika na FIFA kutoka Uingereza  wa mradi huo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam  leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni ya symbion.
PICHA NA MICHUZI

RAIS KIKWETE AFUNGUA TERMINAL YA MBOLEA YA KAMPUNI YA YARA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi terminal ya mbole ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.   Kulia ni  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu   Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa YARA nchini Bw. Alexandre Macedo na Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwa  ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.   Kulia ni  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu   Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa YARA nchini Bw. Alexandre Macedo na Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka kukagua terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.   Kulia ni  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu   Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa YARA nchini Bw. Alexandre Macedo na Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether
 Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway akihutubua katika sherehe hizo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu  akimkaribisha Rais Kikwete kuhutubia
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati anafungua rasmi terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia sanamu ya meli aliyozawadiwa baada ya kufungua rasmi terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kushoto ni  Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka na katikati ni Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, AMOSI MAKALLA APITA OFISI ZA MICHUZI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi Makalla alipopita kusalimia katika Ofisi za MICHUZI MEDIA GROUP jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kutoka kuapishwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Watatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amosi Makalla  akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya MICHUZI MEDIA GROUP jijini Dar es Salaam leo.

LOWASSA ATIKISA CHATO, MKOANI GEITA

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnaji Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato, Dkt. Benedicto Lukanima, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.
Mh. Tundu Lissu akiwasalimia wananchi wa Jimbo la Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.

MAGUFULI APOKELEWA KAMA MFALME KIGOMA,WANANCHI WAKIRI WAZI ATOSHA KUWA RAIS

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.
 Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yake, lakini pia atawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi

Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.

Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura.
Wananchi na Mabango yao
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo mchana.
Wakazi wa Nguruka waifuatilia Mkutano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Nguruka mkoani Kigoma.

Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akiwahutubia wananchi wa Kigoma na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyka katika uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma.

Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya akina mama wakishangilia jambo
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kweny mkutano wa kampeni za Uraisi jioni ya leo.
Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalinzi,ambapo mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia aliwahutubia wananchi.
Wakazi wa mji wa Nguruka,mkoani Kigoma wakifuatilia mkutano wa hadhara
Wananchi na mabango yao
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwaomba ridhaa wakazi wa kigoma ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano wa kampeni za Urais.

Rais Kikwete azindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo

$
0
0
 Rais Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi majengo majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mfano wa kadi yake baada ya kujiunga mfuko wa pensheni wa PSPF kwenye sherehe hizo. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Malima. Kulia kwa Rais ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF Mhe. George Yambesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka alama ya dole kwenye fomu yake ya uanmachama baada ya kujiunga mfuko wa pensheni wa PSPF kwenye sherehe hizo. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Malima. Kulia kwa Rais ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF Mhe. George Yambesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na  na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau  na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio kwenye sherehe zsa  kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.

Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika 
Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.


PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.
Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.


Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake uliofanywa na makandarasi wazalendo ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika. 

VIDEO YA SIDE NKUMBA AKIRUDI TENA CCM

Kipindi cha JUKWAA LANGU Sept 14 2015

$
0
0
Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015.Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 14, 2015
Kutoka Tanzania tuliungana na Jonathan Samiya na Nyakia, ambaye ni mmoja wa wakuu wa Itifaki wa kampeni za Dr Magufuli.Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Clare Ng'owo, Ali Badawy na Shamis Abdulla Kwenye line tulikuwa na Jeff Msangi, Dr Patrick Nhigula na Arthur

Mhe. Rais Kikwete awaapisha rasmi Balozi Mwakasege, Bundala, Kilima, Luvanda, Mbega na Shiyo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Bi. Victoria Richard Mwakasege aliyekuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. Balozi Victoria R. Mwakasege anaiwakilisha Tanzania nchini Malawi. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 16 September, 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Samweli Shelukindo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent E. Shiyo kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman, Bw. Abdallah Kilima kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda Bi. Anisa Mbega kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Bw. Baraka H. Luvanda kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Mwanza yaiadhibu Morogoro katika michuano ya Airtel Rising Stars

$
0
0
Patashika ya michuano ya vijana chini ya miaka 12 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa,
Patashika ya michuano ya vijana chini ya miaka 12 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa baina ya Mwanza na Morogoro.

Patashika ya michuano ya vijana chini ya miaka 12 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa, imeendelea kutimua vumbi katika dimba la Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam, ambapo timu za Temeke na Mwanza zilipepetana kwa upande wa wasichana huku Mwanza na Morogoro walitifuana vikali kwa upande wa wavulana. 

Kwa kuanzia na mchezo ambao ulizikutanisha timu za wavulana, Mwanza waliwasambaratisha vibaya Morogoro kwa kuwashindilia magoli 3-1. Mwanza ambao walionekana kutakata kila idara, walijipatia bao la uongozi mnamo dakika ya 30 kupitia Lazaro Richard, baada ya kuitokea pasi nzuri iliyopigwa na David Richard na kumchambua vizuri kipa wa Morogoro kisha kuukwamisha mpira huo kimiani. 


Morogoro ambao katika mchezo wa Jumatatu wiki hii, waliitandika Kinondoni mabao 2-1, waliamka kutoka usingizi na kufanya mashambulizi kadhaa ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda. Alikuwa ni David Richard ambaye aliandikia Mwanza bao la pili mnamo dakika ya 54, kutokana na krosi safi iliyochongwa kutoka mashariki mwa uwanja na kuusindikiza kwa uzuri kabisa mpira huo langoni mwa Morogoro. 

Baada ya goli hilo, Morogoro waliamka na kupeleka mashambuliza ya mara kwa mara langoni mwa Mwanza, na ndipo mshambuliaji wao hatari Evidence Kiongozi alipofunga goli dakika ya 63 na kuamsha matumaini ya walau kusawazisha na hatimaye kutafuta goli la ushindi. Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa upande wa Morogoro, baada ya David Richard kwa mara nyingine tena, kuifungia Mwanza bao la tatu na mwisho katika mchezo huo mnamo dakika ya 68 na kuhitimisha karamu ya magoli kwa upande wa timu yake. Katika mchezo mwingine, wasichana wa Temeke waliwaadabisha vikali Mwanza kwa kuwafumua magoli 3-0.

Temeke ambao katika mchezo wao wa kwanza walitaoa kipigo cha mbwa mwizi cha magoli 8-0 dhdi ya Arusha, walianza kupata bao mnamo dakika ya 11 baada ya Shamimu Khamisi kufunga goli maridhawa, baada ya kutokea rapsha langoni mwa Mwanza na kuipa timu yake goli la uongozi. Iliwachukua takribani dakika takraibani 28, Temeke wakapata bao la pili kupitia kwa Rose Mpoma baada ya kuachia shuti kali la mbali na kuzama moja kwa moja wavuni, na kumwacha mlinda mlango wa Mwanza asijue la kufanya langoni mwake. Mpaka timu hizo zinakwenda mapumzikoni, Temeke walikuwa mbele kwa magoli 2-0. 

 Temeke waliendeleza kilio kwa wapinzani wao, katika kipindi cha pili kwa kushindilia msumari wa tatu na wa mwisho mnamo dakika ya 56, baada ya Oppah Masoud kugongeana mpira vizuri na Rose Mpoma na hatimaye kuusukumiza moja kwa moja mpira kimiani. 

Baada ya kupata goli la tatu, Temeke walionekana kuridhika na kucheza kwa kijiamini huku wakisubiri kipenga cha mwisho cha mwamuzi, huku wakiwa wamejikunyajia pointi tatu kibindoni.

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITEKA KIGOMA UWANJA WA KAWAWA

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KIWANDA CHA TBL, WAFANYABIASHARA NCHINI WAPEWA WITO.

$
0
0

  Mkuu wa usalama wa mahali pa kazi wa TBL Mbeya, Godfrey Kisulilo akiwaonesha waandishi wa habari namna ya kutunza maji.
  Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na uomgozi wa tbl.
Waandishi wa habari Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara katika kiwanda cha bia cha TBL Mbeya.
WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na biashara zenye mahusiano na kiwanda hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.
Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.
 Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa hamasa hiyo alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.
Jemedari alisema bado wafannya biashara na wakulima mkoani Mbeya hawajaitumia vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua inayopelekea wenzao kutoka maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.
Alisema licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza unga kutoka Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.
“Wafanyabiashara wa Mbeya bado wamejikita katika biashara nyingine ikiwemo ya kununua nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena pasipo kuziongezea thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona kutoka mbali wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”
“Nadhani hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona kwakuwa tutakuwa tunawanytima wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji wadau wengine wa kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.
Alisema kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona kiwandani hapo ni mkubwa ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja hivyo ni fursa nzuri kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi hiyo.
Alisema TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara yeyote atakayeonesha nia ya kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha inampa mwongozo juu ya namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda inavyopaswa kutengenezwa.
Aliitaja fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida nyingine ambayo wakazi wa Mbeya hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa mkoani hapa ni wakulima wa wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda kikilazimika kununua bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Alisema licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha wakulima katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa wakulima mkoani hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko ni la uhakika.
Katika shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM David Nyembe aliibuka mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa Emmanuel Lengwa aliyeshika nafasi ya pili.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMPENI ZA MGOMBEA MWEZA SAMIA MTWARA VIJIJINI JANA

$
0
0
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, alipozungumza na walipozuia msafara wake njiani, katika eneo la Makonga wilayani Newala, wakati akieda kuhutubia mkikutano ya kampeni katika jimbo la Newala Vijijini mkoani Mtwara jana, Septemba 16, 2015.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Liwale mjini, George Mkuchika, katika mkutanowa kampeni uliofanyika jana, Septemba 16, 2015, katika jimbo hilo mkoani Mtwara.
Mgombea Ubunge jimbo la Newala Vijijini, Rashid Akbar akiomba kura baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo, jana Septemba 16, 2015
  (Picha zote na Bashir Nkoromo).
 Wagombea Udiwani katika jimbo la Newala Vijijini wakionyesha mikono walipotambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kushoto ni Mjumbe wa kampeni za mgombea mwenza wa Urais Mama Samia, Angela Kizigha.
 Kina Mama wakimpatia zawadi Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Newala Vijijini mkoani Mtwara.
 Mgobea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akizungumza na wananchi waliozuia msafara wake katika eneo la Chaume, akiwa njiani kwenda jimbo la Liwale Vijijini kuhutubia mkutano wa kampeni jana, septemba 16, 2015

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassani akihtubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Newala mjini mkoani Mtwara.
 Wananchi wakiahidi kuipigia kura CCM, Wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Newala mjini mkoani Mtwara.
 Mbunge anayesubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa katika jimbo la Nanyamba, mkoani  Mtwara, Abdallah Chikota, akimuombea Kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
 .Kijana akiwa amejinakshi kuhamasisha mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Mtwara Vijini.
 .Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, akipokea kadi za vyama vya upinzani baada ya vijana kutoka vyama hivyo kuamua kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Mtwara Vijini.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Mtwara Vijijini Hawa Ghasia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo, jana, Septemba 16, 2015. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images