Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

WENGI WAJITOKEZA UZINDUZI WA AWAMU YA PILI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Kata ya Temeke, Elias Wawa akizungumza katika uzinduzi wa awamu ya pili kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni uliofanyika soko la Temeke Sterio Dar es Salaam jana. Uzinduzi huo  upo chini ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi 'Acha Lugha Chafu na Udhalilishaji Sokoni' Unaendeshwa na Shirika Equality for Growth (EfG). 
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Matumbi uliopo katika wilaya ya Temeke, Khatibu Lindi, akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Soko la Temeke Sterio, Hamad Juma Mtemi, akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Temeke, Agnes Soso, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Samora Julius (kulia), akitoa mada mbalimbali kuhusu ukatili wa jinsia masokoni wakati wa uzinduzi huo.
 Ofisa Mradi wa EfG, Susan Sitta, akielezea historia fupi ya 
shirika hilo.
 Wananchi wakiwa kwenye Uzinduzi huo.
 Mkazi wa Chamanzi, Husna Abdallah akielezea udhalilishaji wa jinsia katika masoko.

 
 Wasanii wa kundi la Machozi wakiigiza igizo la ukatili wa jinsia 
 Maofisa wa EfG wa ndani na nje ya nchi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wananchi wakifuatila matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
 Soko la Temeke Sterio ulipofanyika uzinduzi huo.
 Taswira katika uzinduzi huo.
 Msanii wa Kundi la Utamaduni la Machozi, akitoa burudani.
Burudani zikiendelea kutoka kundi la Machozi.

Na Dotto Mwaibale

 OFISA Mtendaji wa Kata ya Temeke, Elias Wawa amelipongeza Shirika la Equality for Growth (EfG), kwa jitihada zake na kupunguza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni.

Wawa alitoa pongezi hizo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na wanahabari katika  uzinduzi wa awamu ya pili ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake katika Soko la Temeke Sterio.

"Nalipongeza shirika la EfG kwa jitihada zao za kutoa elimu kwa wananchi katika masoko mbalimbali kwani imesaidia kupunguza vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa jinsia masokoni" alisema Wawa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mradi wa Shirika la EfG, Susan Sitta alisema shirika hilo lililosajiriwa Septemba 6, 2015 dhima yake ni kuinua maendeleo ya sekta isiyo rasmi Tanzania, hususani wanawake, kwa kupunguza umaskini kwa njia ya kutoa mafunzo ya sheria na haki za binadamu, kutoa msaada wa kisheria, kuwezesha kuwepo kwa fursa za biashara kwa wanawake na wanaume pamoja na kushawishi utungaji wa sera zinazoinua wanawake na kujenga uwezo sawa kwa wanawake na wanaume.

Sitta alisema shirika hilo linatekeleza mradi unaoitwa Mpe Riziki si Matusi katika masoko sita Wilayani Ilala ambayo ameyataja kuwa ni Feri, Kisutu, Mchikichini, Gezaulole, Tabata Muslimu na Temeke Sterio.

Alisema mradi huo umelenga kuwalinda wanawake katika sekta isiyo rasmi hususani wafanyabiashara masokoni dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Aliongeza kuwa mradi huo pia unaangalia wanawake wafanyabiashara katika masoko ya ya Wilaya ya Ilala na Temeke na kuhakikisha wanafanyabiashara zao katika mazingira huru yasiyo na ukatili wa matusi, kingono, kimwili, kiuchumi na kisiasa.

"Mradi huu zaidi unaangalia na kuhakikisha wanawake wanaheshiwa na kufurahi haki yao ya kiuchumi" alisema Sitta.

Sitta alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo juu ya ukatili dhidi ya wanawake masokoni unaonesha asilimia 90.32 ya wanawake katika sekta isiyo rasmi wanafanyiwa ukatili mara kwa mara wa kingono, kimwili na matusi katika maeneo yao ya kazi.  

Mkazi wa Chamanzi, Husna Abdallah alisema kufanyiwa viendo vya ukatili wa jinsia kwa wanawake wafanyabiashara masokono kwa upande mwingine kunachangiwa na wanawake wenyewe pale wateja wanapowashika katika miili yao na wao kufurahi jambo hilo bila kuchukua hatua ya kuwakalipia au kuwapeleka kwa uongozi wa soko husika.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

SINGITA SERENGETI, TANZANIA WINS PRESTIGIOUS ‘HOTEL OF THE YEAR’ AWARD FROM THE CONDÉ NAST TRAVELLER MAGAZINE UK

$
0
0
SINGITA Serengeti, Tanzania has once again affirmed its status as one of the world's leading hotels, after receiving prestigious accolades from The Condé Nast Traveller Readers’ Travel Awards, having been chosen as the “Best hotel in the world for service", taking second place in the “Best Hotels in the Middle East, Africa & Indian Ocean” category, and third place in the “Top 100 Travel Experiences in the World”.

The award is recognition for Singita Serengeti after readers and visitors voted it the best in terms of its majestic location. The outstanding service pulled together by the guides, trackers, chefs, cleaners and waiters, is what creates the magic that makes this the world's favorite place to stay for service. 

Commenting on the award, Singita Serengeti Managing Director Graham Ledger said that he and his team are humbled, honored and thrilled with winning this prestigious award from Condé Nast. 

"I am extremely proud of my team, We have been working diligently for years making sure that every facet of the business is treated with the utmost care and attention which in turn elevates the guest experience to levels that are truly world class”. 

He also adds “Tanzania will also benefit hugely as a destination on the world travel calendar as awards such as these bring a lot of positive attention and enormous credibility to the host country". 

“Being recognized as the best Hotel in the World for Service from an influential magazine like The Condé Nast Traveller is an honor and it demonstrates that Singita Serengeti is on the right track where hospitality is concerned. Having just recently launched our new campaign to brand Tanzania as one of Africa’s best tourist destinations, I am excited that Singita Serengeti are working very well to promote our tourism and hospitality industry which in turn places Tanzania at a higher position as one of the most preferred destinations in the world” explained Acting Managing Director of Tanzania Tourist Board, Devota Mdachi.

The new campaign and the two Tanzania Tourism promotional tools Mdachi is referring to were  officially launched by The President of United Republic of Tanzania, His Excellency Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. 

They consisted of a high quality television advert with the tag line of Branding Tanzania as the “The Soul of Africa” and an online Tourism Destination Portal. The new advert will be aired in CNN and BBC for six months from October this year. Before rebranding, in the world tourism markets Tanzania was known as the Land of Kilimanjaro, Zanzibar and The Serengeti.

With an estimated readership of over 1 million readers worldwide, Condé Nast Traveller UK is the foremost authority in unbiased travel and destination reporting, and is globally renowned as one of the world’s leading travel magazines.

For more information contact:
Gugu Sithole
Singita (South Africa)
Email: gugu.s@sigita.com

About Singita
Singita’s evolution from a single-lodge company to one that is now responsible for a million acres of land, operating 12 lodges and camps in five wilderness regions across three African countries – Tanzania, South Africa and Zimbabwe – has always been characterized by a pioneering spirit and a sincere desire to preserve wilderness areas for future generations. Its low-impact, high-value tourism model – fewer guests paying a premium for the privilege of experiencing vast open spaces – exists to sustain these wilderness areas and their resident wildlife, while providing an exclusive safari experience.

Singita Serengeti is comprised of Singita Explore , Singita Faru Faru Lodge, Singita Sasakwa Lodge, Singita Sabora Tented Camp,  Singita Serengeti House, and Singita Mara River Tented Camp.

DK. MAGUFULI AKIENDELEA NA KAMPENI WILAYANI BUHIGWE,MANYOVU KIGOMA LEO

$
0
0
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma leo akiowaomba wananchi hao ridhaa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Pombe Magufuli wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma leo.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Pombe Magufuli wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma leo.

HAPATOSHA JUMAMOSI HII VIWANJA VYA DON BOSCO OYSTERBAY

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na mchuano wa  nusu fainali ya shindano la  Dance 100% 2015 litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,Kundi litakaloibuka mshindi wa shindano hilo litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 5. Anayeshuhudia kushoto ni mratibu wa shindano hilo linaloandaliwa  na EATV chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania, Happy Shame.

 Moja ya kundi linaloshiriki katika kinyanganyiro cha nusu fainali ya shindano la  Dance 100% 2015 litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,Likionesha umahiri wake wa kucheza tayari kwa kukabiliana na makundi mengine kwenye kinyanganyiro hicho.Kundi litakaloibuka mshindi wa shindano hilo linaloandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 5. 
Mwandishi wetu.

·        Ni nusu fainali ya kukata na shoka ya  Dansi 100%
PATAKUWA hapatoshi katika kinyang’anyiro cha kukata na shoka cha mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa  na kituo cha televisheni cha East  Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo hapo jumamosi ijayo hatua ya robo fainali  inafanyika katika uwanja wa Don Bosco oysterbay  jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 15 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam.

Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambao yatachuana nusu fainali ni The W-T,Team Makorokocho,The W-D,Best boys kaka zao,Mad squared,Mavuno Crew,The winners crew,The heroes crew,Majoka Crew,Cute babies,Quality boys,Wazawa crew,The best,Dream team na Team ya shamba.

Mmoja wa washiriki wanaounda kundi la Cute babies ambalo ndiyo kundi pekee la wasichana Zuwena Karimu,alisema wao kama kundi la wasichana pekee kati ya makundi yote wapo ngangari kupambana na kundi lolote lile kwani wana uwezo wa hali ya juu na ndiyo maana waliingia 15 bora kwa sasa tupo kambini tunajifua ipasavyo na tupo tayari kuingia vitani alisema Karimu.

Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shamte,alisema kuwa katika kinyang’anyiro hichi cha nusu fainali  watapata makundi 10 yatakayoingia  moja kwa moja ngazi ya fainali itakayofanyika hapo baadaye.

“Huu ni mwaka wa nne East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania mwaka hadi mwaka yamekuwa yakiongezeka kupata imaarufu na kuwavutia vijana wengi nchini ambao hujitokeza kushiriki”Alisema Shame.

Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa  moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5 zitakazokabidhiwa na Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa  Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.
 

TANGAZO LA KIFO CHA MARGARETH MWAISAGA

$
0
0

Mpigapicha Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Standard Newsapapers (TSN) Limited, wachapishaji wa magazeti ya Dailynews, Sundaynews, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo, Mohamed Mambo anasikitika kutangaza kifo cha mke wake Margaret Amon Mwaisaga (pichani) kilichotokea Hospitali ya TMJ  15.09.2015. 

Msiba upo nyumbani kwa familia ya marehemu Mikocheni nyumba namba 87 barabara itokayo Clouds FM kwenda Kanisa la Mchungaji Rwakatare na mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kunzia saa sita. 

ARUSHA YAONGOZA MICHUANO YA WAZI TENISI KWA VIJANA.

$
0
0
 
Na Woinde Shizza,Arusha
Jiji la Arusha limeendelea kuwa kinara katika mchezo wa tenisi baada ya wachezaji wake kuibuka kidedea kwa kutwaa ushindi katika umri tofauti tofauti ,mashindano yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Arusha Tenisi gymkhana klabu.

Mashindano hayo yalidhaminiwa na Jubilee tyres ikiwa ni mwaka wa tatu sasa, yalishirikisha jumla ya wachezaji 90 ambao 28 kati yao ni wasichana kutoka Dar es salaam gymkhana klabu,Kijitonyama tenisi klabu kutoka Dar es salaam,Morogoro tenisi klabu, ISM –Moshi campus, AICC klabu –Arusha pamoja na Arusha tenis gymkhana klabu.

Katika umri wa miaka 6 kwa wasichana Schaefer Swantje kutoka ISM Moshi campus alifuatiwa na Suhana  Patel kutoka Arusha gymkhana klabu,huku kwa  upande wa wavulana wa umri huo Sahil Shah kutoka ISM moshi campus na kufuatiwa na Yuvraj Sidhu kutoka Arusha gymkhana klabu.

Wasichana walio na umri wa miaka 8 Asha Ali aliibuka mshindi na nafasi ya pili kumwendea Bahati Mdee wachezaji wote kutoka klabu ya AICC na kwa upande wa wavulana mika 8 Johnson Peter alibuka mshindi na kufuatiwa na Yasin Yusuph wote kutoka klabu ya AICC na kwa wasichana walio na umri wa miaka 10 Vanessa Emmanuel kutoka AICC aliibuka kidedea na kufuatiwa na Caroline Mwangata wa ISM Moshi campus, huku kwa wavulana miaka hiyo Rashid Abdallah kutoka Arusha gymkhana klabu na kufuatiwa na Abdumarik Kudra kutoka Morogoro klabu.

Kwa umri wa miaka  12 wasichana Shana Martin aliongoza na kufuatiwa na  Fei Amon wote kutoka Arusha gymkhana klabu na wavulana Damas Felex na nafasi ya pili kumwendea Benjamini Laurance wote kutoka AICC ,Huku kwa umri wa miaka 14 kwa wasichana Jackline Kayuga kutoka kijitonyama Tenisi klabu na nafsi ya pili Anikaa Aggarwal  kutoka Arusha Gymkhana klabu na kwa wavulana wa umri huo Deogratius Felex  na kufuatiwa na Yusufu Laurance wote kutoka AICC.

Jackline Kayuga kutoka  Kijitonyama Tennis klabu alishika nafasi ya kwanzana kufuatiwa Hawa Yahya kutoka Dar es salaam gymkhana klabu katika umri wa miaka 16 kwa  wasichana  na kwa  wavulana Omari Sulle Arusha Gymkhana klabu na kufuatiwa na Hassan Hamisi - AICC Club Arusha.

Kwa upande wa umri wa miaka 18 kwa wasichana hawakuwepo ,na walicheza wavulana pekee ambapo Emmanuel Mallya- Arusha Gymkhana Club alifuatiwa na -  Frank Menard -Arusha Gymkhana Club.

Nicholaus Leringa Kocha mkuu  wa klabu ya AGC alisema kuwa  mashindano hayo hufanyika kila mwaka yakiwa na lengo  la kuwaimarisha vijana katika dhana nzima ya  kunyanyua vipaji vyao.

TUZO ZA SANAA YA UCHORAJI TINGATINGA

$
0
0
 Balozi wa China nchini Tanzania Dr. Lu Younq ing akiongea na baadhi ya wasanii wa sanaa ya uchoraji  wa Tingatinga katika hafla ya utoaji wa  Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea  katika hafla ya utoaji wa  Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam.Tuzo hizo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni
 Mmoja wa wachoraji  wa sanaa ya Tingatinga akionyesha cheti chake cha ushindi katika hafla ya utoaji wa Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam,wa kwanza aliyekaa kulia ni  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga.Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimpongeza mmoja wa washindi wa uchoraji wa Sanaa ya Tingitinga katika utoaji wa Tuzo la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko. Tuzo hizo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dr. Lu Younq ing akimkabidhi mmoja wa washindi wa  uchoraji wa sanaa ya tingatinga katika utoaji wa Tuzo la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China. ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo  Prof. Hermas Mwansoko akimkabidhi  mmoja wa washindi wa  uchoraji wa sanaa ya tingatinga katika utoaji wa Tuzo la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China. ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni.
 Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Bw. Adrian Nyangamale akiongea na  baadhi ya wasanii wa sanaa ya uchoraji  wa Tingatinga katika hafla ya utoaji wa  Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China.
Mwenyekiti  wa  Tingatinga Arts Co-operation Society akiongea na  baadhi ya wasanii wa sanaa ya uchoraji  wa Tingatinga katika hafla ya utoaji wa  Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China. ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni. (Picha na Benjamin Sawe- WHVUM)

VIJANA WAASWA KUACHA UPAPARA

$
0
0
_MG_1920
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiingia katika ukumbi wa mkutano hoteli ya Double Tree by Hilton kwa ajili ya warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
Na Mwandishi wetu
VIJANA nchini Tanzania wanatakiwa kujitambua, kuacha kuwa kigeugeu na kufanya papara ya kupata fedha kama wanataka kuendelea na kufanikiwa kibinafsi na kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewea jana na Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga kwenye warsha ya wadau wa kitaifa ya kujadili suala la ajira kwa vijana Tanzania .
Kauli yake hiyo kwa vijana hao waliojumuika katika hoteli ya DoubleTree by Hilton, Dar es salaam, ilitokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini ambazo zinaonesha kwamba vijana wengi hawana msimamo wa maisha, hawana maono, hawana malengo binafsi wala kutambua matarajio.
Amesema: “ Usipojitambua, leo nikija nikakueleza habari za kuanzisha biashara ya matofali utachangamkia. Kesho akija mtu mwingine akakueleza kuhusu uchimbaji wa madini utaacha kutengeneza tofali na kukimbilia machimboni”.
Akizungumza kwa ufasaha kabisa kuhusu vijana na ajira, alisema kila mmoja ana nafasi yake katika kuleta maendeleo yake na taifa na kwamba lazima kujituma na si kubweteka na kulalamika tu.
Akizungumza kwa mfano alimzungumzia kijana mmoja Joseph ambaye alikuwa mwadilifu sana na mwenye kumwamini Mungu. Anasema Kila siku Joseph aliamka asubuhi na kumuomba Mungu amsaidie aondokane na umaskini alionao.
Alifanyakazi hivyo kwa miaka 30 lakini maombi yake hayakumsaidia kuondokana na umaskini.
Siku moja, alisema, Mungu alimuona Joseph akiwa na masikitiko makubwa akamuuliza kulikoni, Joseph akamjibu: “Mungu ni miaka 30 leo tangu nianzie kukuomba uniwezeshe nishinde bahati nasibu. Mimi nimeishi maisha yangu kwa uadilifu nawe wajua . Lakini mbona maombi hayatimii?”
_MG_1976
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifungua warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC). Kushoto ni Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga na kulia ni Kiongozi Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi wa Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) Dk. Arjan de Haan.
Naye Mungu akatabsamu akamwambia, Joseph, si ununue tiketi basi?
Dk Kiaga alisema kwa kuzingatia hadithi yake kila mmoja anatakiwa kufanya kitu na Joseph alisahau kwamba huwezi kushinda bahati nasibu bila kununua tiketi.
“Kumbuka haitoshi kuwa na elimu na ujuzi kama hutaweza kuweka elimu hiyo au ujuzi ulionao katika vitendo” alisema na kuongeza kuwa Joseph alikuwa anajua anahaitaji fedha ya kianzio lakini hakuchukua hatua ya kupata hela hiyo.
Alisema pamoja na ukweli kuwa asilimia 40 ya watu wasio na ajira duniani ni vijana, kwa maana ya kwamba kuna vijana wapatao milioni 75 duniani kote wanatafuta ajira huku vijana wa kike wakiwa na changamoto kubwa zaidi, ipo shida kubwa ya vijana kukata tamaa.
Aidha alisema kwamba hali ya kukata tamaa imewapeleka vijana kuongezeka katika soko la vijana wanaopata kazi zisizo na staha.
Alisema pamoja na sera zilizopo vijana wanatakiwa kuwa na shauku na kazi na pia kujitambua.
“Vijana wa siku hizi hawana mitazamo sahihi kuhusu ajira. Kwamba vijana hawana shauku na kazi na wana mitazamo hasi (ili mradi kazi..mkono uende kinywani?) . Matokeo yake ni kwamba vijana hawatumii ubunifu wowote katika kuboresha uwezekano wao wa kupata kazi zenye staha” alisema.
Amesema mtaji unahitaji kujiboreshea seti ya ujuzi katika kutafuta kazi ikiwa ni pamoja na uwezo, uzoefu na elimu.
_MG_2014
Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga akizungumza kwenye warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
Alisisitiza kuwa vijana waliowengi hawajitambui na kujiuliza ‘mimi ni nani’ au hawana malengo binafsi na matarajio mimi nataka kuwa nani na kusema bila kuyafanyia kazi mambo hayo mawili ya shauku ya kazi na kujitambua hakutakuwepo na mabadiliko.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida, akifungua warsha hiyo alisema pamoja na taifa kuwa mstari wa mbele kushughulikia ajira kwa vijana kwa kutunga sera zilizolenga kukidhi haja ya ajira,ikiwemo Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 na na mpango wa utekelezaji wa sera ya taifa ya ajira kwa vijana iliyo chini ya mtandao wa ajira unaofadhiliwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, changamoto bado zipo.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo wakiwemo vijana waliofanikiwa kueleza siri za fursa na kujiajiri ili kutoa mwanga kwa wenzao.
Pamoja na warsha hiyo kutoa nafasi kwa vijana kujadili namna ya kutambua na kutumia fursa za kuichumi zilizopo nchini, kutoa ujuzi kwa vijana wa namna ya kuingia katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri, kukuza ujasiriamali na kuendeleza biashara, Dk Kida aliwasihi vijana kujitafutia riziki yake na kushiriki ipasavyo katika shughuli za kiuchumi na maendeleo.
Aliwataka kujijengea uwezo wa kufanyakazi pamoja na kubaini na kuzitumia fursa za kiuchumi na kibiashara zilizopo nchini.
Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) ilikutanisha vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania na kuwezeshwa kwa sehemu kubwa na Taasisi ya tamasha ambapo Mkurugenzi wake Mtendaji Richard Mabala alikuwa Mchokozaji mkuu.
Akiwasilisha salamu kutoka IDRC, kiongozi Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo. Dk Arjan de Haan alisema kwamba taasisi hiyo ya serikali ya Canada imekuwa ikitoa ushirikiano katika tafiti zilizolenga kuangalia utatuaji wa tatizo la ajira kwa namna inavyofaa.
_MG_2200
Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole Saibul akiwasilisha mada katika semina ya vijana na ajira.
Alisema kwamba kwa kawaida taasisi yake husaidia pale inapoona utafutaji wa mbinu za kutatua tatizo unashirikisha na wahusika ili kupata suluhu endelevu ya tatizo husika.
Alisema ameridhishwa na kuona kwamba warsha hiyo imezingatia kanuni za IDRC za kutaka kutatua tatizo la ajira kwa kushirikisha vijana wenyewe, kuangalia na kushauri namna bora ya kukabili tatizo la ajira ambao kwa sasa ni changamoto kubwa duniani.
Alisema kwamba ipo haja ya kubadili baadhi ya sera kulingana na mahitaji ya sasa ili kuwezesha vijana wengi zaidi kuingia katika soko la ajira.
Wakati wa utambulisho na kuelezea kero zao katika ajira wengi wa vijana waligusia kuwapo kwa sera ambazo si rafiki zinazotengeneza urasimu mkubwa katika kusaidiwa.
Ingawa wengi walisema fursa zipo, walizungumzia kutopata ushirikiano kutoka kwa wazazi , viongozi na taasisi mbalimbali zinazodai kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Aidha vijana wengine walisema kwamba ni kweli kuna mtazamo hasi kwa vijana hasa kukata tamaa na pia kutaka maendeleo ya kasi huku wakikosa ubunifu.
Joachim Fanuel kutoka singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative Society (SYECLOS) alisema kwamba ingawa wao wanaendesha miradi ya kuku wa kienyeji na asali kama fursa zilizopo wanakabiliwa na tatizo la kukata tamaa kutokana na kuona kwamba inachukua muda mrefu kupata vitu wanavyotaka.
Aidha alisema kwamba wamekuwa hawasikilizwi na serikali na taasisi mbalimbali kwa kuwa hawana mali za kuwakilisha kama dhamana katika mambo mbalimbali.
 
_MG_2213
Johari A. Sadik kutoka kampuni inayotengeneza nguo za kitamaduni Binti Africa, akitoa ushuhuda kwamba vijana wanaweza kama watajitambua katika warsha ya siku mbili vijana na ajira inayofanyika hoteli ya DoubleTree by Hilton.
Kijana Musa Mohammed kutoka Zanzibar alisema kwamba japo wana fursa za usindikaji wa vyakula, mizizi na matunda wamekuwa na tatizo la ujuzi katika uchakataji, sera duni zisizojibu mahitaji yao na kuwalinda katika soko.
Binti mmoja kutoka Binti Africa Kampuni inayotengeneza nguo za kitamaduni alisema kwamba kuna shida ya kukata tamaa miongoni mwa vijana lakini pia hawajali kutafuta taarifa wanazohitaji wakisubiri kutafuniwa.
Vijana wengine walizungumzia ugumu wa mitaji, ukosefu wa taaluma na mfumo wa elimu kwuatengeneza kupata ajira katika serikali na taasisi zake.
Mshiriki Leticia Mango kutoka Kigoma alisema kwamba ipo shida ya vijana wenye vipaji ambao hawana elimu vijijini kudharaulika na kutothaminiwa kwa kile kinachoonekana sio wasomi.
Alisema vijana wasomi wakiunganika na wenye vipaji wanaweza kuwa mbali zaidi na kusisitiza ipo haja vijana kuwa pamoja kwa maendeleo yao.
_MG_2221
Joachim Fanuel kutoka Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative Society (SYECCOS) akionesha chupa ya asali kutoka kwa mradi wa kikundi cha vijana ambao waliamua kujiajiri katika warsha ya vijana na ajira.
_MG_2220
Joachim Fanuel kutoka Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative Society (SYECCOS) akizungumza na washiriki wa warsha ya vijana na ajira.
_MG_2178
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) akiwa na Kiongozi Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi wa Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC), Dk. Arjan de Haan wakiwa katika warsha ya vijana na ajira.
_MG_2226
Vijana wakishiriki kazi za vikundi kwenye warsha hiyo.
_MG_2229
_MG_2138
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki warsha ya vijana na ajira hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar.


PANONE FC KUFUNGUA DIMBA NA JKT OLJORO

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha
TIMU ya panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri wa mafuta ,inatarajia kuanza kutupa karata yake ya mchezo wa kwanza wa ligi daraja la kwanza(FDL) dhidi ya maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha.
Mchezo  huo utafanyika septemba 19 mwaka huu, katika uwanja wa Ushirika mjini moshi mkoani kilimanjaro,ambapo  baada ya mchezo huo pia wataikaribisha timu ya Polisi Tabora semptemba  26.
Katibu wa timu ya Panone FC  Augstino mwakatumbula alisema kuwa msimu  huu  wanaenda kuanza ligi daraja la kwanza  ambapo kila mchezo kwao ni fainali na watahakikisha wanatinga kucheza ligi kuu msimu wa 2016-2017.

“Tulifanya usajili mzuri wa wachezaji 7  ambao wameungana na wachezaji wetu tuliokuwa nao msimu uliopita na  tunaimani wataisaidia timu hii na tuna jumla ya wachezaji 27 wanaounda kikosi cha timu pia hatukuweza kuwasajili wote waliokuwepo hapo mwanzo na  ni kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo wengine  kutokuwa na nidhamu,uwezo wao umeshuka kimchezo.”alisema Mwakatumbula .


Aliwataja wachezaji hao saba  ambao wamefanikiwa kusajiliwa na matajiri hao wa mafuta kuwa ni pamoja na Ally Mseja ambaye ni mchezaji huru na Abdallah Shauri ‘Machopa’ aliyetokea timu ya Lipuli –Iringa wote wakiwa ni washambuliaji, Florence  Haure kutoka academy ya Kitayosce ya mkoani Kilimanjaro, Frank Kijoti aliyetokea AFC Arusha Rashid Gumbo kutoka  Kinondoni Manispaa ambaao wote ni Kiungo,Maulid Khalid kutoka  Singida United ambaye ni winga,Mansoul Mansoul  kutoka Coastal Union ya Tanga ambaye ni golikipa.

Timu hiyo ya Panone FC ipo kambini miezi miwili sasa ikijiweka tayari kwa ajili ya michuano hiyo ya ligi Daraja la kwanza ambapo inatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki mapema wiki hii  na timu za  African sports,Magambo JKT na Coastal Union zote za Tanga .

Matajiri hao wa mafuta wananolewa na kocha Atuga  Manyundo akisaidiwa na msaidizi wake Azizi Nyoni .

Ligi daraja la kwanza ina shirikisha jumla ya timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu ambapo timu ya Panone ipo katika kundi ‘C’ na timu za JKT Olojro- Arusha,Polisi Mara –Mara,Rhino Rangers –Tabora,Mbao fc –Mwanza,Polisi Tabora  -Tabora,Geita Gold –

WIZARA YAKANUSHA MADAI YA ANAYEDAIWA KUUMBA MWENGE WA UHURU

$
0
0

Gazeti la Mwananchi la Tarehe 14/9/2015 toleo namba 5529 ukurasa wa 25 liliandika habari kuhusu Mwenge wa Uhuru chini ya kichwa cha Habari “Anayeumba Mwenge wa Uhuru” huyu hapa

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (WHVUM) ambayo ndiyo yenye dhamana ya Mwenge wa Uhuru inapenda kuufahamisha umma kwamba habari hiyo sio ya kweli na ni ya upotoshaji.

Mwenge wa Uhuru ni Chombo maalum na moja ya alama nyeti za Taifa la Tanzania. Mwenge wa Uhuru ni chombo chenye hadhi ya pekee na hivyo dhamana ya kukitengeneza haiwezi kupewa mtu binafsi kama alivyodai Ndugu Shaban Mwinchumu na kuandikwa kwenye gazeti la Mwananchi. Kwa sababu hiyo, kitendo cha kutengeneza au kuigiza chombo chenye dhana na falsafa ya Mwenge wa Uhuru ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ingependa kuufahamisha umma kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianzishwa rasmi mwaka 1964  na sio mwaka 1961 kama ilivyoandikwa katika toleo lililotajwa. Ieleweke kwamba, Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu kuanzishwa kwake zimekuwa zikitumika katika kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kuendelea kujenga upendo, umoja na mshikamano wa Kitaifa bila ya kubaguana kwa misingi ya kidini,rangi, jinsia, ukabila na itikadi za kisiasa.

Vilevile, Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuhamasisha na kuchochea  shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi kiuchumi na kijamii kupitia kwenye ujumbe maalum unaotolewa kila mwaka na miradi ya maendeleo inayobuniwa .

Wizara pia, inapenda kuufahamisha  umma wa Watanzania kuwa michango ya fedha inayotolewa na wananchi kwa ajili ya Mbio za Mwenge wa Uhuru si kwa ajili ya kugharamia mafuta ya Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa kama ilivyodaiwa na gazeti la Mwananchi. Fedha zinazochangwa ni kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo hubuniwa na wananchi wenyewe. Aidha,  michango hiyo hutolewa  kwa hiari kutoka kwa mwananchi mmojammoja, Vikundi, Taasisi za Umma na Binafsi, Wadau wa Maendeleo, Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya.

Kwa Taarifa hii Wizara inasisitiza kuwa madai ya Ndugu Shaban Mwinchumu ni ya upotoshaji na hayana uhusiano wowote na masuala ya Mwenge wa Uhuru. Pia, Ndugu Shaban Mwinchumu hajawahi kupewa kazi ya kutengeneza Mwenge wa Uhuru anayodai kuifanya kwa muda mrefu kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Manendeleo ya Vijana kwani hakuna Wizara hiyo kwenye orodha ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwisho kabisa Wizara inawataka waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya habari  kuandika habari kwa usahihi  zenye kujenga Umoja wa Kitaifa kwa kupata ufafanuzi wa kila upande ili habari itoe picha halisi badala ya kuegemea upande mmoja kwani kwa kuegemea upande mmoja hupotosha jamii na si maadili ya taaluma ya habari.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

NEWS ALERT: UONGOZI WA NCCR-MAGEUZI WATOFAUTIANA NA MWENENDO WA UKAWA

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI,Reticia Ghati Mosore akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam  muda huu kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu katika umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kutangaza kuendelea na mapambano nje ya umoja huo wa vyama pinzani. 
Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI, Mosena Nyambabe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatima yao ya kupambana kama wenyewe NCCR-MAGEUZI bila ya UKAWA na  kuwa  chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  kuwa inavibana  vyama vishiriki vya UKAWA  katika wagombea wa Ubunge majimboni na wagombea wa udiwani katika kata.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii .

Sintofahamu imeibuka ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi ambapo viongozi wake wamedai kuwa taratibu zilizo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zimekiukwa na kufanya chama hicho kuingia katika mgogoro wa majimbo. 

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Leticia Ghati Mosore amesema  kuwa NCCR-Mageuzi wamezidiwa idadi ya majimbo kutokana na taratibu nyingi kukiukwa kuanzia serikali ya Mtaa na sasa uchaguzi Mkuu.

 Mama Mosore amesema baada ya kuona mambo hayaendi sawa, na ingawa wataendelea kuwa UKAWA, lakini sasa wameamua kupambana wenyewe kama NCCR-Mageuzi katika kugombea viti vya ubunge pamoja na udiwani katika mgawanyo huo ambao amedai chama hicho kimepata majimbo pungufu ndani ya umoja wa vyama vinavyounda Ukawa.

Amesema kuwa ili kukamilisha ushirikishwaji kulitakiwa kuundwa kamati zitakazoendesha uchaguzi ndani ya UKAWA na mambo mengine mengi ikiwemo uwazi wa matumizi ya fedha, lakini hayajaweza kufanyika hivyo . 
“Mchakato wa kumpata mgombea Urais haukufuta utaratibu katika ushirikishwaji wa vyama vyote vitakavyoweza kutambua mgombea gani anaweza kusimama katika kupeprusha bendera ya UKAWA”, amesema Mama Mosore.

Mama Masore pia ametaka Mwenyekiti wao Mhe. James Mbatia asiwe msemaji wa CHADEMA wakati anakiacha chama chake (NCCR-Mageuzi) kinadhoofika, akidai kwamba wananchi wanashindwa kututoufautisha UKAWA na CCM na wataamua kuchagua zimwi walijualo. “Tunasisitiza upinzani wa kweli nchini hauwezi kujengwa kwa njia za hila, kwa kukiuka taratibu za kidemokrasia, tutachangishana ili tusafiri kwenye majimbo na kata za wagombea wetu na kuwasaidia” alisema. 

Mama Masore amesema”Tunamshauri Mwenyekiti James Mbatia aitishe vikao vya kikatiba haraka  ili tuweze kujadiliana kuhusu hatima ya Chama chetu.Upinzani wa kweli haujengwi kwa kuweka mbele tamaa na maslahi binafsi kuliko taifa, na kwa kutegemea propaganda. 

 “Tangu UKAWA ianze, matokeo yake yamekuwa ni mabaya kwa uhai na ustawi wa Chama chetu cha NCCR”, amesema mama Masore. 
 Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho,Bw. Mosena Nyambabe amesema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa ndio kinafanya uandaji wa masuala yote bila kuwa na ushirikiano na NCCR-Mageuzi licha kuwa na udogo katika muungano huo. 

 Bw. Nyambabe amewataka wanachama wote wa NCCR-Mageuzi kushikamana katika uchaguzi mkuu ili kupata majimbo hayo licha ya kuwepo kwa changamoto ya kufanyiwa vurugu na Chadema. Bw. Nyambabe amehoji juu ya hatima ya NCCR-MAGEUZI baada ya uchaguzi na UKAWA wakiwa madarakani huku changamoto zikiwa bado hazijamalizika, akitolea mfano itakuwaje kwenye mgawanyo wa wakuu wa mikoa ,pamoja na wakuu wa Wilaya. 

 Amesema NCCR-Mageuzi imepoteza matumaini katika muungano huo ya kupata wabunge wengi, na kusisitiza kuwa chama hicho kitakuwa na wakati mgumu bila kutafuta ufumbuzi kukiwa bado mapema 
Mgawanyo wa majimbo ambao unaleta mkanganyiko katika UKAWA ni Chadema –Majimbo 148; CUF (Majimbo 99) ,NCCR-Mageuzi (Majimbo 12) na NLD - Majimbo matatu.

MKUTANO WA KAMPENI ZA MGOMBEA MWENZA WA UKAWA BUSANDA GEITA

$
0
0
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.

Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwasili katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita leo. (Picha na Francis Dande)
 Msafara wa mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni ukiwasili katika kata ya Katolo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwapungia mkono wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa uliofanyika katika kata ya Katolo jimbo la  Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwapungia mkono wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa uliofanyika katika kata ya Katolo jimbo la  Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
umati wa watu.

KIAMA CHA MAJANGILI CHAJA, BATHAWK YAZINDUA NDEGE MAALUM KUPAMBANA NAO ​

$
0
0
Ndege aina ya Super Bat DA-50

Na Daniel Mbega, Mkomazi

NI majira ya saa tatu asubuhi Jumatano, Septemba 16, 2015 wakati tunawasili kwenye uwanja mdogo wa ndege (air strip) katika eneo la Kisima ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi inayotenganisha mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.Uwanja unaonekana mweupe, hakuna ndege! Nikashangaa kwa sababu wenyeji wetu kampuni ya Bathawk Recon wametuambia tunakuja kushuhudia uzinduzi wa ndege maalum zinazopambana na ujangili.
Kilichoonekana mbele yetu ni hema kubwa ambalo mbele yake kulionekana minara midogo iliyosimikwa kama fimbo. Kwenye banda kubwa ikaonekana ndege ndogo aina ya Twin otter. Nikadhani ndiyo inayozinduliwa, lakini Idrisa Jaffary, mwenyei wetu tuliyekuwa naye kwenye gari akasema, hapa siyo hiyo.

Mshangao ukanipata baada ya gari kusimama wakati nilipokiona kifaa mfano wa ndege kikiwa kimeegeshwa kwenye bomba maalum kana kwamba ndege inataka kupaa.Kama nisingekuwa nazifahamu ndege hizi maarufu kama drones, ningeweza kusema kwamba huo ni mdoli ambao mwanangu angefurahia kama ningempelekea akauchezea.Kwa siku za karibuni zimekuwa maarufu kwani zinatumika kupeleka misaada mbalimbali hata katika maeneo hatari ya vita ambako hakufikiki kirahisi.

“Hii ndiyo ndege yenyewe,” Idrisa akatueleza. “Hee! Ndiyo hii?” tukajiuliza kwa mshangao. Kwamba Tanzania tumeanza kuitumia teknoloia hii yanaweza kuwa maendeleo mengine mapya.Mshangao wetu ulimalizika wakati Phil Jones, ofisa mwendeshaji wa mitambo hiyo kutoka kampuni ya MartinUAV ya Marekani iliyotengeneza ndege hiyo aina ya Super Bat DA-50 UAV, alipoanza kutuelezea namna ‘ndege’hiyo (drone) inavyofanya kazi huku akituonyesha kila sehemu na kazi yake.


“Hii ni ndege ambayo haihitaji kuwa na rubani, inaongozwa kwa kompyuta maalum, ina antenna mbili, ina kamera maalum ambazo zinaweza kupiga picha usiku na hata mchana,” akatueleza.

Akasema ndege hiyo ina uwezo wa kuruka urefu wa futi 20,000 kutoka usawa wa bahari na kwenda katika nusu kipenyo cha kilometa 35 kutoka ilipo mitambo ya kuiongoza.

Jones, ambaye baadaye alinieleza kwamba yeye rubani wa zamani wa ndege za kijeshi katika Jeshi la Uingereza aliyestaafu mwaka 2014 ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, akasema ndege hiyo inayorushwa kwa mtindo wa manati (catapult launch system), inaweza kuruka mfululizo kwa muda wa saa 10 ikiwa angani kabla ya kutua na kujazwa mafuta tena.

“Ina mfumo maalum wa kamera ambazo zina uwezo wa kupiga picha hata usiku wa manane na kutambua mienendo ya viumbe wenye damu ya moto kama hayawani na binadamu, hivyo ni rahisi kubaini kama kuna majangili,” akafafanua.

Baada ya maelezo ya takriban nusu saa, hatimaye yeye na wasaidizi wake wakaamua kuirusha ndege hiyo baada ya kuiwasha. Ilichomoka kwa kasi ya ajabu na kuelekea angani ikaanza kuzunguka.

Hapo ndipo tukasogezwa kwenye hema kubwa ambako tuliwakuta wasaidizi wake – Austin Howard na Kory Ferguson – wakiendesha kompyuta hizo na tukashuhudia mazingira halisi ya hifadhi katika eneo husika pamoja na kuona wanyama mbalimbali.

“Sasa hapa unaweza kuona kama kuna wavamizi (majangili) na inakuwa rahisi kuwasiliana na askari wa wanyama pori na kwenda kwenye eneo husika kuwakamata,” anasema Jones.

Hata ilipotua, ilikuja kama ndege za kawaida zinavyokuja, tofauti yake tu yenyewe haina magurudumu. Naam, unaweza kuwa ufumbuzi mwingine wa kupambana na ujangili nchini, tatizo ambalo haliko Tanzania tu, bali katika nchi nyingi barani Afrika.

Taasisi mbalimbali za ndani na nje zikiwemo serikali za mataifa makubwa zimekuwa zikijitahidi kusaidia mapambano hayo kama alivyofanya Rais Barack Obama wa Marekani alipoahidi kutoa Dola milioni 10 (sawa za Shs. 20 bilioni) ili kuimarisha mapambano hayo nchini.Takwimu zinaonyesha kuwa Bara la Afrika mwaka 1930 lilikuwa na tembo 50 milioni na kwamba hadi kufikia mwaka 2013 tembo waliobakia katika bara zima ni  500,000.

Aidha, takwimu hizo zinaonyesha kwamba katika miaka ya 1960 Tanzania kulikuwa na tembo kati ya 250,000 hadi 300,000 na kwamba wanyama hao walipungua hadi kufikia 130,000 mwaka 2002 na idadi ya tembo hapa nchini imeendelea kupungua kwa kasi ambapo hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa inakadiriwa kuna tembo wasiozidi 55,000.Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, wastani wa tembo 30 huuawa kijangili kila siku ikiwa ni sawa na tembo 850 kwa mwezina zaidi ya tembo 10,000 wanauawa kila mwaka,hali ambayo inatishia uwepo wa wanyama hao wakubwa zaidi duniani kwa sasa.

Kwenye Hifadhi ya Tarangire, jumla ya tembo 104 waliouawa katika kipindi cha miaka mitatu tu kutoka mwaka 2007 hadi 2009 na katika Hifadhi ya Serengeti idadi ya tembo imepongua kutoka 2,500 mwaka 1985 hadi kufikia 500 mwaka 2012 huku nyati wakipungua kutoka 70,000 hadi 40,000 ujangili huo ukiua faru wengi kutoka 1,000 waliokuwepo mwaka 1985 hadi 20 tu.

Kwenye Pori la Akiba la akiba la Selous inaelezwa kwamba hadi kufikia mwaka 2007 kulikuwa na tembo zaidi ya 70,000 lakini idadi hiyo imeshuka hadi tembo 30,000 tu kufikia mwaka 2012.

Kasi ya ujangili inayoongezeka kila mwaka inachangiwa na mambo mbalimbali yakiwemo kukua kwa uchumi wa nchi ya China na nchi nyingine za Kusini Mashariki mwa Asia kama Hong Kong, Vietnam na Philippines.  

Juhudi mbalimbali zimefanywa na wadau wa sekta ya utalii na maliasili, lakini inaoenakana tatizo hilo linazidi kuota mizizi huku taasisi za kimataifa zikiendelea kulipigia kelele bila mafanikio.

Kampuni ya Bathawk Recon Limited ya Tanzania imeitikia kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya ujangili nchini, ambapo leo hii Septemba 16, 2015 ikaamua kuzindua ndege hizo maalum zinazoweza kupambana na ujangili.

 “Haya ni majaribio ya tatu, tulifanya majaribio mara ya kwanza katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa kutumia ndege maalum aina ya DT 16, lakini hayakuonyesha matokeo mazuri,” anasema Michael Chambers, Mkurugenzi wa Mikakati na Mawasiliano wa Bathawk.

Chambers, ambaye amekuwepo nchini Tanzania kwa takriban miaka 20 sasa, anasema jaribio la pili lilifanyika katika Pori la Selous mwezi Mei 2015 kwa kutumia ndege aina ya DT 26 iliyotengenezwa Ufaransa, lakini iliharibika na haikuweza kutoa matokeo mazuri.

Anaibainisha kwamba, katika kipindi cha siku tano cha majaribio tangu Septemba 11, 2015, ndege hiyo mpya aina ya Super Bat DA-50 UAV iliyotengenezwa na kampuni ya MartinUAV ya Marekani, imeonyesha mafanikio makubwa.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi na muasisi wa kampuni hiyo, Tom Lithgow, anasema baada ya majaribio yao kuonyesha mafanikio, sasa wataandaa ripoti yao na kuiwasilisha kwenye taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) pamoja na kwenye Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili kama wataridhia, basi waweze kuona namna gani yakuanza utekelezaji kuhakikisha tembo na wanyama wengine wanalindwa.

“Tumefanya kazi kwa ushirikiano na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, hususan Tanapa na Idara ya Wanyamapori, tunaamini baada ya mafanikio haya, nao wataangalia ni kwa namna gani tunaweza kuanza kuitumia,” anasema Tom, Mtanzania ambaye ana uzoefu mkubwa wa mazingira ya porini na utalii kwa ujumla.

Hata hivyo, Mike Chambers anasema, teknolojia hiyo itakuwa ya kwanza kutumia nchini Tanzania katika suala zima la kubaini na kudhibiti ujangili na ni ya gharama nafuu zaidi kwani ndege hizo hazitumii rubani ndani yake, zinatumia mafuta kidogo na kuruka kwa muda mrefu.

“Mbali ya kupambana na ujangili, lakini pia teknolojia hii itasaidia suala zima la uhifadhi kwa kutambua hata idadi ya wanyama waliopo (scouting),” anafafanua Chambers.

Herman van Rooyen na Johnson Makere ni vijana waliohitimu stashahada ya Uhifadhi Wanyamapori katika Chuo cha Wanyamapori cha Mweka mkoani Kilimanjaro, ambao kwa sasa wameelekezwa namna ya kurusha na kuongoza ndege hizo kwa ustadi mkubwa.

Ingawa wanatakiwa kupatiwa mafunzo maalum na muhimu, lakini wanaielezea teknolojia hiyo kwamba inafaa sana katika suala zima la uhifadhi wanyamapori.

Wanasema, kutokana na tatizo la uhaba wa watumishi na vitendea kazi pamoja na miundombinu duni ndani ya hifadhi na mapori ya akiba, teknolojia hiyo inaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa ikiwa serikali itaikubali na kuitumia.

“Teknolojia hii inasaidia kuwakamata majangili wakiwa wanafanya uharamia wao ndani ya hifadhi na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo sasa kwamba majangili wanaokamatwa wanakuwa wanasingiziwa,” anasema Makere.

Makere anaongeza: “Hivi sasa utaratibu unaotumiwa ni kama wa mbwa kufuata nyayo na harufu kwani majangili mara nyingi wanakuwa wanakamatwa wakiwa majumbani mwao, lakini hapa watakamatwa humo ndani na hivyo kuukazia ushahidi kwani picha zipo na watakuwa na vidhibiti.”

Kampuni ya Bathawk Recon inajipambanua kwamba kwa kuja na teknolojia hiyo ya utambuzi inaweza kuwa suluhu ya janga la ujangili kwa kuwa inao uwezo wa kutambua majangili hata kama wakijificha, labda kama watachimbia ardhini.

“Na kama watajichimbia basi itakuwa faida zaidi, kwa sababu hawawezi kufanya lolote bila kuonekana,” anaongeza Jones, ambaye kwa zaidi ya miaka 10 amekuwa rubani wa ndege za kivita kwenye Jeshi la Kifalme (Royal Armed Forces).

Ofisa uhifadhi kutoka Hifadhi ya Tarangire, Marandu, ambaye alimwakilisha Mhifadhi katika uzinduzi huo, anasema anaamini teknolojia hiyo ni nzuri na inaweza kusaidia kuwahifadhi wanyama.

“Katika mapambano dhidi ya ujangili na ustawi wa maliasili, mbinu yoyote yenye kuleta matokeo chanya ni vizuri ikapokelewa na kujaribiwa, kama inafaa basi itakuwa msaada mkubwa kwa taifa,” anasema.

Sera ya Taifa ya Wanyamapori ya mwaka 1998 inaelekeza kuwa aina zote za viumbe hai zihifadhiwe, wanyamapori wasitumiwe kiasi cha kuifanya idadi yao ipungue na kuwa katika hatari ya kutoweka na kuhakikisha Taifa linaendelea kumiliki wanyamapori na kusimamia kwa niaba ya wananchi.

Ndege zilizojaribiwa


DT-18 ilijaribiwa Tarangire


Hii ilitengenezwa Ufaransa. Ni ndogo sana, inaweza kuruka kwa saa mbili tu katika nusu kipenyo cha kilometa 15 kutoka ilipo mitambo.


DT-26 ilijaribiwa Selous


Imetengenezwa Ufaransa na kampuni ya Delair Tech. Hii ni kubwa kidogo, ina uwezo mkubwa na inatumia viwango vya satelaiti za kijeshi vya mawasiliano kutumana kupokeataarifa pamoja na namna ya kuongozwa kwake.


Superbat DA 50 – Imejaribiwa Mkomazi


Imetengenezwa Marekani na kampuni ya MartinUAV. Inaitwa MLB Super-Bat DA-50. Inatumia injini yenye mapigo mawili na uwezo wa 50cc ikiwa na genereta la Watts 75 pamoja na mafuta. Urefu wake ni futi 8.5 x 5.3 x 2.25 inapokuwa imeunganishwa, lakini ikiwa bado haijaungwa ina urefu wa futi 3.5 x 1.25 x 1.5. Kasi yake ni kati ya 40 hadi 70kts, inakaa angani kwa saa 10 mfululizona inaruka kimo cha futi 15,000 hadi 20,000 bila kupoteza mawasiliano.



0656-331974

LOWASSA AENDELEA NA ZIARA ZAKE ZA KAMPENI, BARIADI MKOANI SIMIYU LEO

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.

KUONA PICHA ZAIDI

TATIZO LA UHABA WA MAJI WILAYANI MKURANGA KUWA HISTORIA.

$
0
0
 Mwakilishi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania Dkt, Mohammed Akbar Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima chenye urefu wa mita 541 eneo la Mkwalia, Mkuranga, Pwani leo.Kisima hicho kinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 1.8 kwa siku.
 Maji kutoka katika kisima hicho yakitiririka kufuatia kufanyika kwa majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini.
 Kiongozi wa waendesha mitambo ya uchimbaji visima wa kampuni ya ZENTAS Bw. Sima Teodor ( kushoto) akitoa maelezo kwa wandishi wa habari kuhusu kazi ya uchimbaji wa kisima hicho katika eneo la mradi wilayani Mkuranga.

 Mtaalam wa mitambo wa Kampuni ya ZENTAS Sahtn Topal ( katikati) akifafanua teknolojia na vifaa vilivyotumika kuchimba kisima hicho.Picha na Aron Msigwa/ MAELEZO.

 
TATIZO LA UHABA WA MAJI WILAYANI MKURANGA KUWA HISTORIA.

Na.Aron Msigwa- MAELEZO
17/9/2015. Mkuranga,Pwani.

Wananchi wa wilaya ya Mkuranga,mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni  1.8  kwa siku.

Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho  mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS  kutoka Uturuki nchini Tanzania Dkt.Mohammed Akbar amesema wao kama wataalam wanaendelea na majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini  jambo ambalo limeonyesha mafanikio makubwa.

 Amesema mtambo wa kuchimba kisima hicho uliwasili eneo la mradi Julai 9 mwaka huu na kuongeza kuwa mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi kazi ya uchimbaji ilianza na kubainisha kuwa  sasa kisima hicho kinazalisha kiasi cha lita  76,000 kwa saa na lita milioni  1.8 kwa siku.

Dkt. Akbar amesema endapo maji hayo yataunganishwa kwenye miundombinu ya maji ya mji huo yatakidhi mahitaji ya maji ya mji wa Mkuranga ambayo ni lita laki  Sita na Elfu mbili  kwa siku (602,000).

" Kwetu Haya  ni mafanikio makubwa ukizingatia mradi wenyewe haujaanza kusambaza maji kwani visima hivi vilikuwa ni kwa ajili ya utafiti, kiwango cha maji kilichopatikana ni kikubwa, kilichobakia sasa ni kwa mamlaka husika na Serikali kukamilisha mipango iliyobaki ili maji haya yawafikie wananchi" Amesema.

Ameongeza kuwa chini ya mradi huo wamechimba visima 9 na kati ya hivyo visima 7 vinafanya vizuri na  2 vimeharibika na kueleza kuwa matarajio yao  ni kuona visima vitano ambavyo sasa  vimekamilika vizuri vikizalisha  lita milioni 55.

Meneja wa Mamlaka ya Maji Mkuranga mjini (MKUWASA) Muhandisi Filbert Pius akiuzungumzia mradi huo amesema kuwa utakapokamilika utawasaidia wananchi kupata maji safi na kuondoa tatizo la muda mrefu la ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Amesema mahitaji ya maji katika mji huo ni makubwa kuliko uwezo wa sasa wa kuzalisha maji ambapo vyanzo vilivyopo vina uwezo wa kuzalisha lita 135,000 kwa siku  ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya lita 602,000 kwa siku kwa wakazi wapatao 25,847.

" Wananchi sasa watapata nafuu, tofauti kabisa na mwanzo, maji yanayozalishwa hapa ni mengi  lita 1,800,000 kwa siku hii inakidhi  mara mbili mahitaji yote ya wananchi wa mji wa Mkuranga " Amesisitiza Muhandisi Pius.

Ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu yenye urefu wa kilometa 2 inayotarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu ili Mkuranga  ambao sasa ni mji wa viwanda upate  huduma ya uhakika ya maji,

Pia amesema kukamilika kwa ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji eneo la Mkwalia ulipo mradi huo pamoja na eneo la Kurungu kutaiwezesha hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kupata huduma ya uhakika ya maji ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wagonjwa wanafika kupata huduma.

Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Bi.Nelly Msuya akifafanua kuhudsu mradi huo amesema unajengwa unatekelezwa na DAWASA kwa niaba ya Serikali na akifafanua kuwa maeneo yote yenye miundombinu ya maji katika wilaya ya Mkuranga yanatarajiwa kuanza kupata huduma hiyo ifikapo Oktoba mwaka huu.

Amesema mradi huo sasa uko katika hatua za majaribio na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wote mara  kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mabomba ya kusambazia maji , ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na kukamilika kwa  taratibu za kitaalam ili maji hayo yawafikie wananchi.

"Nachoweza kusema kwa upande wa wilayanya Mkuranga tumefika pazuri, sisi kama DAWASA watekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa niaba ya Serikali tutahakikisha kero ya maji  katika wilaya hii  na maeneo mengine inapatiwa ufumbuzi,  tumeshatoa mamlaka kwa miji na wilaya  kubuni, kusimamia  na kuendeleza miradi ya maji ili wananchi wengi zaidi wanufaike" Amesisitiza.

Aidha, amebainisha kuwa mradi wa ujenzi wa visima 8 eneo la Mkuranga umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.4 na kufafanua kuwa awamu inayofuata ni kuyapeleka maji hayo yakaunganishwe na mfumo wa kusambazia maji uliopo, ujenzi, uongezaji wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na ununuzi wa pampu ya kusukuma maji hayo kutoka kwenye chanzo.

WANAFUNZI WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha
Wanafunzi wametakiwa kuwekeza katika elimu, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha ya sasa na ya baadaye ikiwemo kufanya kazi kwa vitendo ,na mashiko vitavyowasaidia kwenye maisha yao ya sasa na baadae sanjari na kulijenga taifa lao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala na uongozi wa chuo cha Habari maalum,Mr Ernest Karata wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Full Bright college kilichopo Ngaramtoni,wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. 


Katika mahafali hayo wanafunzi  wanane walihitimu mafunzo ya ukatibu muhtasi ualimu wa shule za awali (chekechea) ambapo wote watapata ajira katika shule na vyuo mbalimbali vilivyopo ndani na nje ya nchi.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi mtendaji  wa chuo cha Full Bright College  Mr.Julius Matiko amewaasa wahitimu wajiongeze na wazidisshe bidii katika elimukwani chuo hicho kina vifaa vya kutosha vikiwemo vifaa vya kompyuta,uhazini ambavyo vipo na hotel management
.Chuo hicho kimesajiliwa na VETA ambapo pia wanatoa mafunzo ya NABE(National Business Examination)


Mku wa chuo hicho Rose Mapunda  amewasihi na kuwashauri wazazi wawalete wanafunzi chuoni hapo wajipatie elimu na maarifa ya kutosha  zikiwemo stadi za kazi mbalimbali iliwatakapotoka chuoni hapo waweze kupata ajira na kujiajiri.

.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha Full Bright Mr .Julius Matiko ameiomba serikali itoe ruzuku kwa vyuo binafsi ikiwezekana itoe usafiri pamoja na kutoa vifafa mbalimbali vya kujifunzia  na kujisomea katika chuo hicho.


Akitaja Changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa ardhi ,wa kujenga nyumba za walimu nyumba za kulala wanafunzi, maktaba za kujifunzia  na viwanja vya michezo kwa wanafunzi  na wahitimu wa chuo hicho cha Full Bright

TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU UHURU, HAKI NA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU LEO TAREHE 17.09.2015

$
0
0
Sisi, viongozi wa dini pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi (NEC, TAKUKURU, Polisi pamoja na Msajili wa vyama vya siasa)  tuliokutana leo tarehe 17/9/2015, tumepata nafasi ya kujadili kwa kina suala la uhuru,haki na amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 25/10/2015 na wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa uhuru,haki na amani vinalindwa kipindi hiki.

Suala la uhuru haki na amani ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla na halina mjadala.Kila mmoja achukuwe nafasi yake kulinda uhuru,haki na amani na kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vya siasa. 

Viongozi wa dini wamepata nafasi ya kujadili na vyombo hivi masuala ya msingi kama kuhakikisha kuwa maadili ya uchaguzi yanazingatiwa kwa wote, muda wa kutangaza matokeo ya kura unazingatiwa , haki ya wananchi kupata matokeo haraka ili kuepuka fujo wakati wa kusubiri na kutangazwa kwa matokeo. Jeshi la polisi kutokutumia nguvu kupita kiasi, wajibu wa Msajili kuhakikisha vyama vyote vinapata fursa sawa na pia tumejadili suala la kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya jukwaa la siasa.

Viongozi wa dini tumekubaliana kwa pamoja kuepuka kutumia nyumba za ibada kuonyesha ushabiki wa aina yoyote kwa chama chochote cha siasa.Baada ya kujadili kwa kina masuala hayo viongozi wa dini wanatoa wito ufuatao;


1. Vyombo vya habari vifanye kazi kwa ueledi bila upendeleo na pia kuhakikisha kuwa inatoa taarifa ya kutosha kuelimisha umma.
2. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo  iweke utaratibu maalum wa kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha pamoja na watu wote waliojiandikisha/watakaojiandikisha waweze kupiga kura.
3. Tunaishauri  NEC    kwenye chaguzi zijazo  siku ya kupiga kura isiwe siku ya ibada.
4. NEC iendelee kutoa elimu ya uraia  kuhusu haki ya raia kupiga kura na haki yao ya  kukaa mita mia moja kusubiri matokeo yatangazwe kwa utulivu kama ambavyo NEC imehakikishia viongozi wa dini kuwa kila kituo itabandika matokeo yote (Urais,Ubunge na Udiwani)
5.  Pamoja na kutimiza wajibu wake wa msingi wa kulinda raia na mali zao Jeshi la polisi wakati huu wa uchaguzi  liendelee kutimiza wajibu wake wa kusimamia amani na taratibu kwa haki bila upendeleo.
6. Wagombea,wafuasi   na wanaowanadi,  wanaaswa waache mara moja lugha za matusi,vitisho,kejeli na kukashifiana vinavyoweza kuchochea fujo na kuleta uvunjifu wa amani wajikite kunadi sera za vyama vyao.
7.Tunawahimiza wananchi kuwa makini katika kufuatilia kampeni na sera mbalimbali za wagombea, kuzipima kwa hali ya juu sera hizo, kutokuuza kadi zao za kupigia kura, kutokununuliwa na kujitokeza kwa wingi kutumia uhuru na haki yao ya kuchagua viongozi wanao wataka kwa hiari na  amani.
 8. Viongozi wa dini wanawahimiza Watanzania wote kuendelea kuombea nchi hii kuendelea kuwa  taifa lililojengwa   katika misingi ya uhuru , haki na amani.
9. Viongozi wa dini tutabaki kuwa manabii na wahubiri wa uhuru,haki na amani wakati huu , wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi..

Sisi viongozi wa dini Tunawashukuru Inspekta generali wa polisi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ufafanuzi makini na wa kina juu ya nafasi na utayari wao wa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha uhuru, haki na amani vinaendelea nchini.Maelezo yao na mafafanuzi  yao tumeyasikia  na tutaendeleza kwa kuwa  hiki ni kikao cha mwanzo na tutaendelea kuwa na vikao vingine pamoja nao kuelekea uchaguzi mkuu ili kufuatilia utekelezaji na kuendeleza makubaliano yetu katika kuhakikisha uhuru,haki na amani.

Nchi za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali.

$
0
0

  Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate akuitoa hotuba ya ufungua wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
 Baadhi ya washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
 Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate (aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Semina hiyo.
 
Nchi za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali yanayosababishwa na virusi vya influenza ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya Dkt. Custodia Mandlhate alipokuwa akifungua semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, semina hiyo inayoendelea jijini Nairobi.

Mawasiliano ya haraka wakati wa dharura za kiafya yanahusu ngazi zote kuanzia kimataifa wakati wa hatari ni yetu sote, ni ya kimataifa, kikanda na kitaifa, hivyo basi kipaumbele cha WHO ni kuhamasisha watu, mashirika na serikali kushiriki katika kutoa taarifa na elimu juu ya namna ya kuokoa maisha ili kuchukua hatua sahihi za kuzuia,  kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa huo” alisema Dkt. Custodia.

Dkt. Custodia alisema kuwa hatua ya kupata elimu sahihi ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo inatekelezwa kwa kupitia matumizi bora ya mawasiliano ya umma juu ya afya, ushiriki wa jamii na uhamasishaji wa kijamii kwa kutumia vyombo vya habari, sera na tafiti zinazofaywa ili kuokoa maisha ya watu katika eneo husika.

Malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uwezo washiriki ambao utaimarisha mawasiliano kwa watoa maamuzi muhimu ya kitaifa na kikanda katika kuimarisha hatua za dharura katika kuzuia, kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa wa mafua makali.
 
Malengo mengine ni pamoja na washiriki kupata uelewa juu ya njia bora za kutoa taarifa wakati inapotokea hatari ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya ambayo yanahitaji dharura katika utekelezaji wake pamoja na kuimarisha mitandao ya kikanda ya watoa maamuzi na watendaji ili kubadilishana uzoefu na utaalamu kupitia nchi wanazoziwakilisha.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii TanzaniaDkt. Vida Makundi alisema kuwa semina hiyo ina manufaa makubwa kwa taifa hilo kwa kuwa nchi hiyo tayari ina viashiria vya kuapata yanayotokana na wanyama yakiwemo mafua makali ya ndege na mengine hivyo hivyo ni vema kujifunza na kuchukua tahadhari ikiwaa ni pamoja na kuelimisha jamii namna ya kujikinga majanga mbalimbali ya magonjwa na matukio yanayoathiri afya ya binadamu yanapotokea.

Dkt. Vida alisisitiza kuwa wataalamu wa afya na sekta nyingine zinzohusika na afya ya binadamu wakaelewa kuwa ili kufanikisha mawasiliano kwa jamii hawana budi kushirikiana kwa karibu na  wanahabari kutoa habari kwa jamii ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa ambapo kunahitajika kuwepo na uelewa mpana wa kisiasa, kijamii na kiutamaduni na kuzingatia eneo lililoathiriwa na ugojwa wa mlipuko.

Mkutano huo unaoendelea Nairobi nchini Kenya unaongozwa na kaulimbiu inayosema “Okoa maisha na zuia ugonjwa kuenea” unajumisha ya zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi 21 zilizopo katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo washiriki wanatoka katika Wizara za Afya, Habari na Muwakilishi mmoja wa WHO kutoka nchi anayowakilisha katika ukanda huo.

Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Uganda, Msumbiji, Malawi, Botswana, Lesotho, Sudani ya Kusini, Madagaska, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Swaziland, Rwanda, Mauritius, Eritrea, Namibia, Ethiopia, Afrika Kusini na Zimbabwe.na Kenya ambayo ni mwenyeji wa semina hiyo.

MAMA SAMIA ALIVYOTEKA MIKINDANI NA MAFIA LEO

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni, uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini, Murji Mohammed akiomba kura baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Wasanii wakichangamsha kwa muziki katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini, Murji Mohammed wakiwapongeza wasanii baada ya kutumbuiza muziki uliosisimua wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Kada nguri wa CCM, Kijana Mtera Mwampamba, akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimpongeza Mtela Mwampamba baada ya kuhutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara

 Vijana wakiwa wameparamia ukuta wa moja ya majengo ya kale, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara leo
 Mwanamuziki wa msanii wa Bongo Movie, Snura akichangamsha mkutano kwa kuimba wimbo wa kuifangilia CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakishiriki na wananchi wengine kuselebuka muziki, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkani Mtwara
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Wasanii wa kundi la Hapa ni Kazi Tu, wakionyesha umahiri wao walipotumbuiza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mratibu wa 'Mama Sema na Mwanao' Steve Nyerere akiwa na kamarade, Ally Choky, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia akiwa na mtoto aliyepoteana na mama yake, kutokana na wingi wa watu waliofurika wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgmbea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani, kikiwemo Chadema, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mama Samia akiungana na vijana kuishangilia CCM baada ya kuwapokea walipoamua kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Kimindani mkoani Mtwara leo
"'CCM Hoyeeeee" Kijana Rashid Njechele, akipaza sauti kwa kusema hivyo, baada ya kutangaza kuhamia CCM kutoka CUF, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia (kulia), uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa CCM, wakiwa katika ndege, wakati wa safari ya Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan kutoka Mtwara kwenda Kisiwa cha Mafia kufanya mkutano wa kampeni leo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akishuka kwenye Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mafia, alipowasili kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika kisiwa hicho leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Maa Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya viongozi waliomlaki kwenye Uwanja wa Ndege wa Mafia, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika kisiwa hicho leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia akisoma baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wananchi kueleza matumaini yao kwake, wakati wa mapokezi, alipowasili katika Kisiwa cha Mafia kuhutubia mkutano wa kampeni leo. Kushoto ni Mgombea wa Ubunge katika jimbo hilo, Mbarak Dau
 Aliyekuwa Mbunge wa Mafia ambaye pia aliingia katika kinyan'ganyiro cha kuomba ridhaa ya CCm kuwania tena ubunge wa jimbo hilo, Abdulkarim Shah, akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo, Mbarak Dau, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika katika Kisiwa hicho cha Mafia
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza Kada wa CUF, Mohamed Albadawi, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. Albadawi awali alikuwa Mgombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CUF baada ya kuongoza katika kura za maoni, lakini baadaye akaenguliwa na chama hicho na kupachikwa, Shomari Kimbau ambaye alihamia CUF baada ya kushindwa katika kura za maoni za CCM
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni leo katika Jimbo la mafia mkoa wa Pwani
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la MafiaMbarak Dau katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoa wa Pwani
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto), akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE NDANI YA WILAYA KASULU,BUHIGWE NA KIBONDO MKOANI KIGOMA LEO

$
0
0
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akipanda ngazi kwa kukimbia kwenda jukwaani kujinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Kibondo, Kigoma
Wananchi wa Kasulua wakifuatilia mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dk Magufuli aliwahutubia.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kibondo ndani ya uwanja wa Taifa mkoani Kigoma jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Taifa,  Kibondo, Kigoma.Akihutubia kwa nyakati tofauti, katika mikutano ya  kampeni zake mkoani Kigoma, amekuwa akihimiza kudumisha amani nchini ambapo pia aliwataka viongozi wa kisiasa  kuhubili suala hilo katika mikutano yao.
 



 Wananchi wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli huku wakiwa na matawi ya miti  katika Mji wa Munanila, Jimbo la GBuhigwe, Kigoma
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aakizungumza jambo na mgombea Ubunge jimbo la Buhigwe Albert Ntabaliba 'Obama' katika mkutano wa kampeni katika mji wa Buhigwe-Manyovu mkoani Kigoma
  Wananchi wakimsikiliza kwa makini Dk ,Magufuli alipokuwa akijinadi katika Jimbo la Buhigwe, Kigoma.
 Burudani ndani ya uwanja wa Umoja mjini Kasulu.
 Dk Magufuli akiwanadi Daniel Nsanzugwako (kulia) anayegombea ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Kasulu Mjini na Agustino Zuma Ole anayewania ubunge jimbo la Kasulu Kusini kupitia chama hicho
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma
Wananchi wa Kasulu wakimshangilia  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,kwenye mkutano wa kampeni  uliofanyika kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images