Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

MISS UNIVERSE YAPATA MMILIKI MPYA

$
0
0
Mashindano ya maarufu ya urembo duniani, Miss Universe, sasa yatakuwa chini ya kampuni ya kusaka, kuendeleza vipaji na masoko ijulikanayo kwa jina la WME/IMG. 
Awali mashindano hayo yalikuwa yakiendeshwa kwa ushirika baina ya kampuni hiyo na kampuni inayojishughulisha na masuala ya habari na burudani ya NBCUniversal na mtangazaji maarufu wa vipindi vya televisheni, mwanasiasa na mfanyabiashara, Donald J Trump. 
Akizungumza jijini jana, Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamepokea taarifa kuhusiana na kampuni mpya hiyo ambayo pia inaandaa mashindano ya Miss USA na Miss Teen Usa. 
Maria ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Compass Communications alisema kuwa wamepokea mabadiliko hayo na wataendelea kufanykazi na mmiliki huyo mpya ili kuendeleza vipaji vya wasichana nchini. 
Alisema kuwa mashindano ya Miss Universe ni moja kati ya matukio makubwa ya burudani duniani ambayo usaidia wasichana kutoka nchi zaidi ya 190 zinazoshiriki kila mwaka na watu zaidi ya nusu bilioni kufuatilia mashindano hayo kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao na televisheni. 
“Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kufanya mashindano ya Miss Universe Tanzania, tunaamini kuwa mabadiliko haya yatatupa changamoto zaidi kwa lengo la kufika mbali na zaidi kuhakikisha tunatwaa taji baada ya matokeo mazuri ya Flaviana Matata ya mwaka 2007 ambapo aliingia hatua ya 10 bora,” alisema Maria. 
Afisa Mkuu wa kampuni ya WME/IMG, Mark Shapiro ameahidi kuyaendeleza mashindano hayo kufika ngazi ya juu kabisa ikiwa pamija na washindano bora. 
"Najisikia faraja kuendshs mashindano haya, tutayaendeleza kwa kiwango kikubwa na kuhakikisha umaarufu wake unaongezeka, naamini mashabiki wengi zaidi kwa sasa watafuatilia mashindano yetu kwa njia ya mbalimbali,” alisema Shapiro.
Maria Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai alizungumza katika mashindano yaliyopita.
Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard akitoa elimu ya afya kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto

MGOMBEA WA UKAWA MAULID MTULILA AZINDUA KAMPENI YA UBUNGE JIMBONI KINONDONI!

$
0
0
Mgombea ubunge wa UKAWA kupitia chama cha CUF Maulid Salum Mtulia akihutubia mamia ya watu waliohudhria uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni leo jioni.
Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA leo hii vimezindua kampeni za ubunge kwa jimbo la Kinondoni ambapo mamia ya watu walihunduria katika viwanja vya Mapilau. Ukawa wameamua kusimamisha mgombea mmoja kwa kila jimbo toka vyama vya Chadema, CUF, NCCR Mageu na NLD ambapo kwa jimbo la Kinondoni Ukawa imemsimamisha Maulid Salum Mtulia.





Bw Mtulia akimwaga sera leo hii jioni Mwananyamala katika viwanja vya Mapilau.




Meza kuu!





Baadhi ya viongozi wa vuama vinavyounda UKAWA wakiomba duaa kabla ya mkutano kuanza rasmi.
Wakati wa duaa!



Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Profesa Abdallah Safari akihutubia mamia ya watu waliohudhuria uzinduzi wa kampeni za UKAWA kwa ubunge wa jimbo la Kinondoni leo hii jioni.
Picha zote na Hassan Kachloul

READ INTERNATIONAL KUJENGA MAKTABA ZA SEKONDARI NYINGI ZAIDI NCHINI

$
0
0
  Muasisi wa Shirika lisilo la kiserikali la READ International, Rob Wilson (katikati) akizungumza katikasherehe za miaka 10 ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya wanachama wa shirika hilo la kujitolea nchini Tanzania. READ International inatimiza miaka 10 tokea kuanzishwa ikisihirikiana na Realising Education for Development pamoja na wahisani wengine imeweza kusaidia ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote.
 Mjumbe wa Bodi ya READ International, Faraja Kotta Nyalandu (kulia), mwanzilishi wa READ, Tom Wilson (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Makumbusho ya jijini Dar es Salaam wakikata keki kusherehekea miaka 10 ya shirika hilo.
  Muasisi wa Shirika lisilo la kiserikali la READ International, Rob Wilson (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho alipotembelea maktaba ya shule hiyo iliyowezeshwa kwa ufadhili wa shirika hilo kwa kushirikiana na Realising Education for Developmentpamoja na wahisani  wengine. READ International inatimiza miaka 10 tokea kuanzishwa huku ikisaidia ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote. Wengine pichani ni baadhi ya walimu wa shule hiyo.
 Mmoja wa wanachama wa kujitolea wa READ, Amani Alphonce Shayo akizungumza katika hafla hiyo jinsi mpango wa ukarabati wa maktaba ulivyoleta manufaa kwa wanafunzi wa kitanzania.  
 Mwenyekiti wa Bodi ya READ International, Hatima Karimjee akizungumza katika sherehe za miaka 10 ya shirika hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya MANTRA, Frederick Kibodya akizungumza kuhusu ufadhili wao katika katika kuisaidia READ International kwa ushirikiano na Realising Education for Development katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyenzo za elimu katika shule za sekondari nchini.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho ya jijini Dar es Salaam wakijisomea katika maktaba iliyowezeshwa na Shirika la READ International kwa kushirikiana na Realising Education for Development. READ International imetimiza miaka 10 tokea kuanzishwa ikisaidia ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote.  
ILI kukabiliana na tatizo la miundombinu katika sekta ya elimu nchini inayozikabili shule nyingi sa sekondari,  Shirika lisilo la Kiserikali la READ International kwa kushirikiana na mpango wa Realising Education for Development limetangaza mpango wa kujenga zaidi ya maktaba 500 katika kipindi cha miaka 10 ijayo ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

Akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 tokea kuanzishwa kwa shirika hilo, Muasisi wake Rob Wilson alisema jijini Dar es Salaam juzi kuwa kupitia michango ya wafadhili wao pamoja na Realising Education for Development  wanaweza kujenga japo maktaba 50 kwa kila mwaka.

 “Katika kipindi cha miaka 10 tumefanikiwa kusidia vitabu milioni 1.4 na kujenga maktaba takrabani 72. Kwa msaada wa wadau wa elimu tumefika hapa, sasa tunakusudia kufanya vizuri zaidi katika miaka 10 ijayo,” alisema bwana Wilson.

.
Muasisi huyo alisema wanajivunia mchango wanaoupata kutoka kampuni mbalimbali na kuzitaja baadhi kama Bakhresa, Simba Cement, Wentworth, Mantra, Atlas Copco, na Songas na kusema ni matumaini taasisi nyingine kwa kuona mafanikio waliyoyapata watajitokeza na kuwaunga mkono.

“Ikiwa ni sehemu ya Mpango wa Ukarabati wa Maktaba wa READ kwa kushirikiana na Realising Education for Development  na  wanachama wa shirika hili wa kujitolea hugeuza vyumba visivyotumika katika mashule na kuwa maktaba nzuri na kisha kuziwezesha kwa nyenzo muhimu kama vitabu, meza, viti na makabati,” aliongeza muasisi huyo.
  
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa READ International nchini, Montse Pejuan  alisema licha ya ujenzi huo wa maktaba lakini pia wamesaidia kufundisha wakutubi na  kusaidia shule kufundisha walimu wao wa maktaba.

“Tunafanya bidii kujenga mpango mzuri utakaowawezesha wanafunzi kupenda kujisomea na hivyo kuwawezesha kufaulu vizuri masomo yao,” alisema.

Kwa upande wake msemaji wa Kampuni ya Simba Cement Bi.Mtanga Noor alisema kampuni yao imetumia takribani shs milioni 48 kusaidia ujenzi wa maktaba tatu jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa makampuni mengine kuisaidia juhudi za READ ili kuleta mabadiliko katika ubora wa elimu nchini.
  
Mbali ya Simba Cement wadhamini wengine ni Hogan Lovells, MeTL Group, Wizara ya Elimu na Mazunzo ya Ufundi, Radar Education Ltd, KPMG, IMMMA Advocates, Nabaki Afrika, Oyster bay Group, Learning InSync, MANTRA, Wentworth Foundation, Bakhresa Group, Songas, na BG Tanzania.

Wengine ni pamoja na Karimjee Jivanjee Foundation, Better World Books,  Veolia,  klabu za Rotary za Oysterbay na Bahari, Bakhresa Group, Hogan Lovells,  Corona, Atlas Copco,  Aidan Publishing na APENET. 

KAMPUNI YA SKYLINK WATANGAZA YASHINDI WANNE WA SHINDANO LA KUNUNUA TIKETI

$
0
0
 Bw. Moustafa H. Khataw kutoka kampuni ya Skylink akiwakaribisha waandishi wa habari pamoja na wageni waliofika katika droo ya kuwapata washindi wanne leo kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Bw.Husain AlSafi kutoka Emirates ambao walikuwa ni wadhamini wa shindano akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo katika ofisi za Skylink.
Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Bw. Abdallah Hemed akizichanganya vipeperushi ili kuwapata washindi wa droo hiyo.
Mwandishi wa habari kutoka TBC akiwa ameshika moja ya kipeperushi cha mteja wa Skylink aliyeibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia gari mpya aina Hyundai ix35   katika droo iliyochezeshwa  kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Skylink Solomon Mwale akiwatangaza washindi waliopatikana kwenye droo iliyofanywa na kampuni ya Skylink leo.
Mfanyakazi wa kampuni ya Skylink wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hyundai ambao walikuwa ni wadhamini mkuu kwenye shindano hilo
Waandishi wa habari wakiwa kazini

HASSANTaliki mkazi wa  Jijini Dar es Salaam leo ameibuka mshindi na kushinda gari mpya aina Hyundai ix35   katika droo iliyochezeshwa  kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.

Mshindi huyo amepatikana kutokana na kukata tiketi ya ndege katika Kampuni hiyo hivyo ili aweze kupata zawadi hiyo ametakiwa kwenda na kipeperushi Skylink cha tiketi aliyokana na kitambulisho chake kwa maelekezo zaidi.

Washindi wengine walioshinda kwenye droo hiyo ni  Mohamed Swala ambaye  ameshinda safari ya kwenda Mahinra  kwenda na kurudi huku Issa Nassoro ambaye amekuwa mshindi wa tatu  amepata tiketi ya kwenda na kurudi Dubai ambako atapelekwa na Kampuni hiyo .

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Ofisa wa Skylink Solomon Mwale  alisema kwamba wamepanga kufanya hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao ili umma uweze kuamini kwamba hawabahatishi na droo ikichezeshwa inakuwa  ni kweli.

Droo hii ni sehemu ya motisha inayotolewa na Kampuni yetu  kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.

Droo hiyo imedhaminiwa na Skylink, Hyundai, Emirates, Exim Bank na Club Mahindra.

KATIBA NA KANUNI ZA LIGI KUU

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limebaini kuwepo kwa vitendo vyaa wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kujihusisha na masuala ya Siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo za vilabu na wadhamini wa Ligi.

Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is neutral in matters of politics and religion. Discrimination of any kind against a country, private person or group of people on account race, skin colour, ethnic, national or social origin, gender, language, religion, political opinion or any other opinion, wealth, birth or any other status is strictly prohibited and punishable by suspension or expulsion.”

Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “ Hairuhusiwi kwa mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia yeyote tangazo au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni maalum bila idhini ya TFF/TPLB”.

TFF inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa stars au za washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.

Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa.
Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya katiba za TFF na FIFA.

MKUTANO WA KILELE WA DUNIA KUHUSU CHAKULA NA LISHE WAFUNGULIWA ARUSHA

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa unahusu masuala ya Lishe na Chakula uliofanyika jijini Arusha.
Mhe. Pinda akihutubia
Mfalme wa Lesotho Mhe. Letsie III ambaye nae alihudhuria mkutano huo  akihutubia wadau mbalimbali na wageni waalikwa walioshiriki katika mkutano huo (hawapo pichani).
Balozi wa Tanzania anayeiwakilisha nchini Lesotho, Mhe. Radhia Msuya (kulia) akifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo  
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa kwanza kushoto, mwenye tai ya njano) akifuatilia kwa karibu hotuba zilizo kuwa zikitolewa katika ghafla ya ufunguzi wa Mkutano huo katika Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (katikati), Msaidizi wa Naibu Waziri wa Afya, Bw. Kurwa (wa kwanza kushoto) kwa pamoja nao wakifuatilia kwa makini Hotuba za viongozi mbalimbali katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano.
Wageni waalikwa
 Wadau mablimbali wakifuatilia hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na viongozi ho
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe naye alitoa Hotuba yake wakati wa Hafla hiyo
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau mbalimbali katika meza kuu
 Picha na Reginald philip  
Tanzania imeendelea kuunga mkono jitihada za kitaifa na kimataifa katika kuhakikisha usalama wa chakula pamoja na lishe bora yenye virutubisho muhimu hususan kwa watoto wadogo, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha inapatikana kwa maendeleo endelevu ya taifa.

 
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda alipozungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu masuala ya Chakula na Lishe uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha hivi karibuni.
Mhe. Pinda alisema kuwa jitihada hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimeelekezwa katika kuhamasisha unyonyeshaji wa watoto wachanga na kutumia vyakula vyenye virutubisho kwa watoto wa kuanzia miezi sita hadi mwaka mmoja umesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo vitokananvyo na ukosefu wa chakula bora na utapiamlo.
Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa na program mbalimbali kwa vipindi tofauti katika kupambana na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho na madini muhimu ikiwemo program ya kuongeza madini joto kwenye chumvi iliyozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi mapema mwaka 1990 ili kupambana na magonjwa yanayosababishwa na upungufu wa madini hayo mwilini ikiwemo ugonjwa wa goiter ambao ulienea nchini miaka ya 1980.
Aidha, mwaka 2013 Serikali ilizindua Program ya Kitaifa ya Uboreshaji wa Chakula ambapo virutubisho muhimu viliongezwa kwenye vyakula vinavyoliwa zaidi katika jamiii ya Watanzania ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 25 ya watu wanatumia unga wa ngano na mahindi pamoja na mafuta ya kupikia yaliyoongezwa virutubisho vyenye madini na vitamin muhimu kama chuma, zinki na Vitamini A na B12.
“Kwa upande wa Tanzania jitihada nyingi za kuhakikisha suala zima la upatikanaji wa chakula bora ili kuwawezesha wananchi kuwa na afya bora ili kuchangia katika maendeleo ya taifa lao zimefanyika. Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto wachanga, kuzinduliwa kwa Mkakati wa Taifa wa Lishe  wa miaka mitano hapo mwaka 2011 ambao lengo lake kubwa ni kuhamasisha matumizi ya vyakula vyenye virutubisho” alisema Mhe. Pinda.
Aidha, alieleza kuwa kwa sasa Serikali kupitia Mamlaka za Serikali za mitaa imeweka mkazo kuhakikisha huduma ya uboreshaji vyakula kwa kuongeza virutubisho muhimu inapelekwa katika maeneo ya vivijini ambapo zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanaishi huko.

 “Mifumo inaandaliwa ili kuhakikisha mamalaka hizi zinafanikisha uboreshaji wa vyakula ikiwemo unga wa nafaka unaozalishwa katika mashine za kawaida na mafuta ya kula yanayotengenezwa na wananchi vijijini yanaboreshwa” alisisitiza Mhe. Pinda.
Katika hatua nyingine Mhe. Pinda alisifu na kuwashukuru waandaaji wa mkutano huo kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji  kwani ni wakati muafaka ambapo kampeni hii ya dunia itasaidia kuhamasisha pia wananchi na wawekezaji katika sekta ya chakula hapa nchini na hatimaye kuleta matokeo endelevu katika lishe na usalama wa afya ya jamii kwa ujumla. 
Pia alisema kuwa kwa vile mkutano huo umewashirikisha watu kutoka Serikalini, wafanyabiashara, taasisi za kiraia, mashirika ya kimataifa, wanazuoni na washirika wa maendeleo ana imani kubwa kuwa utaainisha mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya baadaye kuhusu uboreshaji wa afya ya jamii zetu kwa maendeleo endelevu.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Mfalme Letsie III kutoka Lesotho ambaye pia ni Kiongozi wa kuhamashisha matumizi ya chakula bora na lishe wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, alisema kwamba lishe bora ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi kwa kila taifa. Kwamba kuwekeza kwenye lishe ni muhimu ili kupunguza umaskini kwa kuhakikisha kila mwanajamii anachangia kwa taifa lake.
Alieleza kuwa Mkakati wa Lishe wa Kanda ya Afrika kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015-2025 uliozinduliwa mwezi Julai mwaka huu kuwa unasisitiza ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika kuboresha lishe ikiwemo sekta binafsi ambapo alitoa tahadhari kwa wafanyabiashara kutotumia fursa hii kujitengenezea faida kubwa kwa bidhaa watakazozalisha badala ya kuangalia afya za watu kwanza. Pia mapendekezo kuhusu njia bora za uchangiaji mpango wa lishe Afrika yalijadiliwa. 
“Natoa tahadhari kwa wenzetu wa sekta binafsi kuhakikisha afya ya mtu inapewa kipaumbele na kuhakikisha ari ya kujipatia faida haihatarishi afya ya mtu yeyote”alisisitiza Mfalme Letsie III.
Pia aliongeza kuwa, Kamisheni ya Umoja wa Afrika na nchi wanachama zinatambua kwamba Serikali pekee haziwezi kutatua changamoto ya lishe duni inayolikabili Bara la Afrika bali jitihada za wadau wote muhimu zinahitajika ikiwemo sekta binafsi hususan kampuni zinazozalisha na kutengeneza vyakula, Mashirika ya Kimataifa, taasisi za kiraia na wanazuoni wanatakiwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya lishe bora kwa kila mtu. 
Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe alisma kuwa amefarijika mkutano wa kwanza kuhusu masuala ya chakula na lishe umefanyika nchini na kwamba mada zitakazojadiliwa wakati wa mkutano huo zitaziwezesha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kuangalia namna bora ya kuboresha lishe kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu uboreshaji wa Chakula na Lishe uliowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya kimataifa, serikali, wanazuoni, washirika wa maendeleo na sekta binafsi umefanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 Septemba, 2015.

UTT AMIS YAPATA TUZO YA UENDESHAJI BORA WA MIFUKO MWAKA 2015 KUTOKA KWA CAPITAL FINANCE INTERNATIONAL

$
0
0
Tuzo ya usimamizi bora wa mifuko iliyopata UTT AMIS kutoka CFI

Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Dr. Hamis Kibola akiongea na waandishi wa habari(pichani hawapo) kuhusiana na miaka 10 ya Umfuko wa Umoja na Tuzo ya Usimamizi bora wa Mifuko waliyopata kutoka CFI

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Daudi Mbaga akijibu moja ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Dr. Hamis Kibola.

Mkurugenizi wa Uwekezaji wa UTT AMIS Ms. Pamela Nchimbi akiwaelezea waandishi wa habari ufanisi wa Mfuko wa Umoja kwa kipindi cha Miaka 10 waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Dr. Hamis Kibola.

Mkurugenzi Mtendaji wa CFI, Antony Michael akitoa maelezo ya awali kwa waandishi wa habari kabla ya utoaji wa tuzo.

Mwenyekiti wa Bodi ya UTT AMIS Profesa Joseph Kuzilwa akifurahi baada ya kuzindua wovuti ya UTTAMIS. Tukio hili pia lilishuhudiwa na waandishi wa habari, bodi ya wakurungezi,menejimenti na wafanyakazi wa UTTAMIS. Pata fursa za uwekezaji sasa www.utt-tz.org

WATANZANIA WANAIPENDA TANZANIA-NCHEMBA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari juu ya Watanzania wanaoipenda Tanzania wakisha maliza kutimiza wajibu wake wawapishe waendelee kutimiza haki zao za msingi za kupiga kura, ameyasema katika Hoteli ya Serena leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkurugenzi wa (NEC) Jaji Mustafu  Hamad M. Hamid akizungumza na ziongozi mbalimbali wadini pamoja na viongozi wa Siasa juu ya zoezi la uchaguzi kuwa la amani na utulivu leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo  Dk Ayub Rioba.
 Makamu Mkurugenzi wa (NEC) Jaji Mustafu  Hamad M. Hamid akizungumza na viongozi mbalimbali wadini pamoja na viongozi wa Siasa juu ya zoezi la uchaguzi kuwa la amani na utulivu leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo  Dk Ayub Rioba.
Katibu Mkuu wa  (TLP), Nancy Mrikariaakisisitiza jambo katika mdahalo huo.
Baadhi ya viongozi Mbalimbali wakiwa katika mdahalo huo leo Jijini Dar es Salaam .
(Picha na Emmanuel Massaka)
                                       

Benki ya Exim yatoa msaada wa vitabu sekondari Mbeya.

$
0
0
Meneja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Mbeya, Bw Iddy Mwacha(kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo kwa mmoja wa wanafunzi aliewawakilisha wanafunzi wenzie na uongozi wa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya katika kupokea msaada huo ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, uongozi wa shule pamoja na wanafunzi.
BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitabu vya masomo vyenye thamani ya sh mil. 8/- kwa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu hivyo iliyofanyika kwenye viunga vya shule hiyo mwishoni mwa juma lililopita, Meneja wa benki hiyo tawi la Mbeya Bw Iddy Mwacha alisema msaada huo ni sehemu ya uthibitisho wa namna benki hiyo imekuwa ikipambana kuhakikisha uwepo wake hapa nchini unaleta tija zaidi kwa jamii.
Alisema kipaumbele kwenye elimu ni muhimu kutokana na ukweli kwamba sekta mbalimbali ikemo ile benki ili zifanye vizuri zaidi zinategemea uwepo wa wasomi kuziendesha na jamii iliyoelimika kwa ujumla.
“Ni kutoka na kufahamu ukweli huo ndio maana siku zote tumekuwa tukihakikisha kwamba kile tunachokipata tunagawana na jamii ikiwemo kuboresha ubora wa elimu ili mwisho wa siku tupate matokeo mazuri kielimu,’’ alibainisha.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa shule hiyo Mwl Shadrack Mwakasyama licha ya kuishukuru benki ya Exim kwa msaada ilioutoa, pia aliwahikikishia viongozi wa benki hiyo kuwa yeye na walimu wote wa shule hiyo watakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vitabu hivyo vinatumiwa ipasavyo na umakini mkubwa.
“Shule yetu kiukweli bado inakabiliwa na changamoto kadhaa na ndio sababu tunawahikikishieni kwamba tutajitahidi kuhakikisha kwamba kila msaada unaolenga kupunguza changamoto hizi tunauenzi kwa nguvu zetu zote…asanteni sana!,’’ alipongeza.
Aliongeza kuwa ongezeko la vitabu shuleni hapo litakuwa kama chachu ya kutimia kwa malengo ya serikali katika kuhakikisha kwamba ubora wa elimu hapa nchini unakuwa kwa kuridhisha.
Aidha Mwl Mwakasyama alitoa wito kwa mashirika na taasisi nyingine kuiga mfano huo huku akiongeza kuwa kwa sasa serikali peke yake haiwezi kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu hivyo nguvu ya wadau mbalimbali ni muhimu.

BALOZI WA LUVTOUCH MANJANO ATEMBELEA WASHIRIKI WA SEMINA YA UJASIRIAMALI

$
0
0
  
 Balozi wa Luv touch Manjano Irene Pul Katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Semina ya ujasiriamlai ya wanawake kwa kupitia Vipodozi vya Luv Touch manjano iliyochini ya Manjano foundation.

Lengo la Mradi huo ni kuona kwamba wanawake hawa wanajisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara zao kwa lengo la kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za ukosefu wa ajira kuwa chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu mahitaji yake ya msingi, yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa kupitia ujasiriamali.Balozi huyo amewashauri Washiri hao kwanza kupenda ujasiriamali na kufanya kazi kwa bidii lazima watafanikiwa.

Pili kila mshiriki kuwa mbunifu kwenye biashara na kuja na kitu cha kipekee ambacho kitawafanya watumiaji wa luv Toch manjano pamoja na wateja wengine kushawishika kuwaunga mKono washiriki hao katika biashara yao pamoja na kuwatangaza kwa watu wengine wengi zaidi. 
 Pamoja na mafunzo ya biashara, washiriki hawa watanufaika na utaalamu (Proffessional Makeup Artist).Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea ugumu wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.

MBATIA,SELASINI NA KOMU WAPELEKA MABADILIKO JIMBO LA MOSHI VIJIJINI.

$
0
0
Viongozi wa Chadema wakiwasili katika uwanja wa Limpopo TPC kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni kwa mgombea Ubunge wa jimbo hilo,Anthony Komu.
Baaadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wakiwa katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Rombo ,Joseph Selasini ,akizunbumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni katika jimbo la Moshi vijijini.
Wananchi wakifuatolia mkutano huo.
Mgombea Ubunge jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge katika jimbo la Moshi vijijini ,Anthony Komu (Kulia).
Mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kilimanjaro,Helga Mchomvu akizungumza katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Moshi vijijini.
Mgombea Ubunge jimbo la Moshi vijijini,Anthony Komu akiteta jambo na mgombea Ubunge jimbo la Vunjo ,James Mbatia wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo,kushoto ni mgombea udiwani katika kata ya Arusha Chini ,Rojas Mmary.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,Chadema,Emanuel Mlacky akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Vitimaalumu anayemaliza muda wake,Grace Kihwelu akizungumza katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA,James Mbatia akizungumza katika mkutano huo.
Mbatia akimtamburisha mgombea udiwani katika kata ya Arusha Chini,Rojas Mmary mbele ya wapiga kura.
Mbatia akimtamburisha mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini,Anthony Komu katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika kata ya Arusha chini TPC.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini ,Anthony Komu akizungumza katika uzinduzi wa mkutano huo.
Mgombea Ubunge jimbo la Vunjo,James Mbatia  akitamburisha familia ya Anthony Komu.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini (0755659929).

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA DIMANI ZANZIBAR CHAZINDUA KAMPENI.

$
0
0
 Zuhura Seif Hassan akighani utenzi katika Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM Wilaya ya Dimani zilizofanyika uwanja wa shinyanga karibu na Baraza la Wawakilishi Chukwani nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za CCM Wilaya ya Dimani Waziri kiongozi mstaafu wa Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia wananchi waliofika kwenye Mkutano wakuwanadi wagombea wa CCM Wilaya Dimani kabla ya kuwatambulisha kwao.
 Baadhi ya wanachama wa CCM wakisikiliza Mgeni rasmin Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia katika Mkutano uliofanyika kiwanja cha shinyanga karibu na Baraza la Wawakilishi Chukwani.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Ibrahim Raza akiwatambulisha wagombea uwakilishi wa Jimbo hilo, (kulia) mgombea Uwakilishi jimbo la Chukwani Bi. Mwanasha Khamis na (kushoto) mgombea Uwakilishi jimbo la Kiembe samaki. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Waziri kiongozi mstaafu ambae ni Mgeni rasmin katika uzinduzi wa kampeni za CCM Wilaya ya Dimani Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (alievaa kofia ya kiuwa wa sita kushoto) akiwanadi wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Wilaya ya Dimani kwa wananchi.

BIMO MEDIA YAANDAA NYERERE CUP ARUSHA

$
0
0
SAM_5908Mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail akisoma risala katika ufunguzi wa maadhimisho ya ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015 yaliyokuwa yakitimua vumbi katika uwanja wa Stedium jijini Arushaambapo pia yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya kielimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media
SAM_5926Taswira katika ufunguzi wa Nyerere Cup katika uwanja wa stedium jijini Arusha
SAM_5928Mgeni rasmi Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat m.Ntabindi akiongea na vyombo vya habari pamoja na wanamichezo chini ya umri wa miaka 13,alisema kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.
SAM_5902Meza kuu
SAM_5939Mwandishi wa TV1 Jane Edward akichukua matukio katika ufunguzi huo
SAM_5886Mgeni rasmi ambaye Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat M.Ntabindi akisalimiana na wachezaji kabla ya mechi ya TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha na  timu ya AFC Arusha katikaufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
SAM_5893
SAM_5946Watoto wenye chini ya umri wa miaka 13 wakifanyiwa mahojiano ,aliyeshika maiki ni mmiliki wa jamiiblog Bi.Pamela Mollel
TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja lakwanza imeshindwa kuonyesha makali mbele ya wadogo zao  timu ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh AmrI Abeid ,uliiwashuhudia maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.

Vijana wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji wao Wandima Malechela baada ya kuachia  shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.

Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya BIMO Media yakiwa na kauli mbiu ‘Uchaguzi wa Amani  2015,ndio taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini’ yatazishirikisha pia timu za watoto chini ya miaka 13 ambao watachuana vikali ili kuweza kumpata mshindi ambaye atatangazwa siku ya kilele tarehe 19 mwezi huu.

Akifungua mashindano hayo Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat m.Ntabindi alieleza kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.

“Michezo hii inawakutanisha vijana hawa  wakiwa na uwezo wao tofati  ambapo pia yatawajengea urafiki  na uhusiano mzuri baina yao  vile vile   yatawasidia kuweza kuimarisha vipaji vyao  vitakavyotumika katika kuandaa taifa lililo na vijana wenye uwezo mzuri na pia yatahamasisha utalii kwani mkoa huu una vivutio vingi.”alieleza Ntabindi.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail alisema  maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya ki- elimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha.

“ Lengo ni  kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu  kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki  katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.

Timu za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na fedha.

Bi. Samia Suluhu Ahidi Neema kwa Wapiga Kura Majimbo ya Liwale na Nachingwea

$
0
0
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu kwenye Uwanja wa Nangwanda Jimbo la Liwale.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu kwenye Uwanja wa Nangwanda Jimbo la Liwale.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu kwenye Uwanja wa Nangwanda Jimbo la Liwale.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akihutubia kwenye Uwanja wa Nangwanda Jimbo la Liwale jana.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akihutubia kwenye Uwanja wa Nangwanda Jimbo la Liwale jana.
AKIZUNGUMZA na wananchi katika mikutano hiyo mgombea mwenza Bi. Samia Suluhu alisema licha ya ilaya ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuonesha kulenga kuboresha maisha ya wananchi haswa akinamama na vijana kupitia vikundi anuai, alisema Serikali itakayoundwa na CCM endapo ikifanikiwa kurudi madarakani itahakikisha inaweka utaratibu wa kupima ardhi na kuigawa kwa wananchi ili kuwaandalia hati za kawaida na zile za kimila kwa vijijini.
  Alisema utaratibu huu utawawezesha wananchi kuwa na dhamana katika mikopo na kuweza kujiendeleza kwa shughuli zao za kiuchumi. Aliongeza licha ya zoezi la upimaji na utoaji hati kuwa na manufaa kwa wananchi aliongeza kuwa litapunguza migogoro ya ardhi kati ya pande anuai na matumizi tofauti jambo ambalo lilikuwa kikwazo hapo awali.
 “…Tutapima maeneo na kutoa hati za kimila na Serikali ili wananchi waweze kutumia kama dhamana katika mikopo, hizi zitasaidia wananchi kupata fedha za kujiendeleza,” alisema. Akizungumzia soko la korosho alisema Serikali imekisikia kilio cha wananchi juu ya utaratibu wa stakabadhi ghalani hivyo kuwaahidi kulifanyia kazi suala hilo.
  Mambo mengine ambayo Bi. Samia Suluhu aliahidi kuyashughulikia ni pamoja na huduma za maji safi na salama kuzijenga barabara za kuingia na kutoka katika Wilaya hizo za Nachingwea na Liwale kwa kiwango cha lami kwa awamu na kuboresha elimu.
  Bi. Samia anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Lindi na anatarajia kuanza ziara hiyo mkoa wa Mtwara leo jioni, kuendelea kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.

Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
 
 
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Mgombea ubungea wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanaCCM na wananchi wengine katika uwanja huo.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza katika mkutano wa kampeni jana.
Meza kuu ya mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM mjini Nachingwea. Kulia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Nachingwea Hassan Elias Masala akiwa na mgombea mwenza.*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MAKAMU WA RAIS AADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MARA (MARA DAY) BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mshumaa katika Kaburi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama ishara ya Kumbukumbu wakati alipofika katika Jumba la makumbusho Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015 baadda ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) iliyofanyika Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la Maua katika Kaburi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama ishara ya Kumbukumbu wakati alipofika katika Jumba la makumbusho Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015 baadda ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) iliyofanyika Butiama. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya, Eugene Wamalwa. 
 Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika  kwenye Uwanja wa Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mbogo Futakamba (kushoto) akibadilishana mikataba na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya, Eugene Wamalwa, mara baada ya kusainiana Mkataba huo wa Maridhiano ya Mto Mara, wakati wa sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika Butiama mkoani  Mara leo Sept 15, 2015. Kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishuhudia.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mbogo Futakamba (kushoto) na Waziri  wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya, Eugene Wamalwa (katikati) wakitiliana saini mkataba wa Maridhiano ya Mto Mara wakati wa sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika Butiama mkoani  Mara leo Sept 15, 2015. Kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishuhudia.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya kushiriki maadhimisho na kutunza mazingira, Mwakilishi wa Serikali ya Jimbo la Narok nchini Kenya, Rebeccah Seenoi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika  kwenye Uwanja wa Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Eugene Muramira, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Afrika Mashariki, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika leo Sept 15, 2015 kwenye Uwanja wa Mwitongo Mkoani Mara. Picha na OMR






HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE  KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MARA (MARA DAY), BUTIAMA-MARA 
TAREHE 15 SEPTEMBA 2015

Waheshimiwa Mawaziri kutoka  Tanzania na Kenya;
Makatibu Wakuu wa Wizara;
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na  Magavana wa Majimbo;
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Wakurugenzi wa Halmashauri  pamoja na Caunt kutoka Kenya;
Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria;
Wataalam kutoka Wizara,  Taasisi mbalimbali  Kenya na Tanzania;
Wadau wa Maendeleo;
Wawakilishi wa Jumuiya za Watumiaji Maji;
Ndugu Wanahabari;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana

Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uzima na afya njema na kutuwezesha kukusanyika hapa siku ya leo kushuhudia tukio hili muhimu. Napenda nitumie nafasi hii pia kuwashukuru waandaji wa shughuli hii, kunialika kuwa Mgeni Rasmi   katika siku hii ya pekee ambayo wadau wa Bonde la Mto Mara, wanakutana katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mara (Mara Day). Nimepokea mwaliko huu kwa mikono miwili, nasema; Asanteni Sana! Nitumie fursa hii pia kuwakaribisha mkoani Mara, hususani hapa Butiama, wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania. Nasema Karibuni Sana Butima. Jisikieni mpo nyumbani. Hili ni eneo lenye historia kubwa kwa Tanzania na Bara la  Afrika kwa ujumla kwani ndipo alipozaliwa na alipolala, Baba wa Taifa letu na Mtetezi wa Wanyonge Barani Afrika na Duniani kwa ujumla, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi). Napenda pia nitumie nafasi hii kuwashukuru waandaaji wa sherehe hizi na wadau mbalimbali waliochangia kwa namna moja ama nyingine kufanikisha shughuli hii. Endeleni na moyo huo, fanyeni kila linalowezekana kuzidi kuboresha jambo hili mwaka hadi mwaka.

Ndugu Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Tukio la leo linatoa fursa kwa wadau kutoka nchi mbili,  Tanzania na Kenya zinazopitiwa na Bonde la Mto Mara, kukutana pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya uhifadhi na matumizi endelevu ya Mto Mara na kutafakari mustakabali wa  Bonde hili kwa ujumla.  
Hifadhi za Mto Mara zina umuhimu mkubwa kiuchumi kwa nchi hizi mbili kutokana na mapato yatokanayo na utalii. Wanyama waliopo katika hifadhi za Serengeti nchini Tanzania na Maasai Mara kwa upande wa Kenya, hutegemea sana maji ya Mto Mara kwa maisha yao.  Aidha siku hii inakwenda sanjari na msimu wa uhamaji wa wanyamapori jamii ya nyumbu ambapo inakadiriwa kuwa jumla ya nyumbu Milioni mbili wanahama na kurudi kutoka  mbuga za Serengeti- Tanzania na Maasai Mara nchini Kenya  kwa kipindi cha  Julai na Oktoba kila mwaka.
Kaulimbiu ya Madhimisho ya  mwaka huu ni “Mto Mara: Maisha yangu, Maendeleo yangu”. Kaulimbiu hii ni nzuri kwani inalenga kusisitiza dhamira ya dhati ya usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji na nyinginezo katika Bonde la Mto Mara. Fanyeni kila linalowezekana kuhakikisha mnabadilisha Bonde hili na kuwa mfano katika shughuli za maendeleo ikiwa pamoja na kufungua milango na fursa zaidi za uwekezaji. Ni wajibu wa wadau wote wa Bonde hili kuhakikisha chini ya Ushirikiano mzuri wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, vitega uchumi mbalimbali vinawekezwa katika Bonde hili ili kusaidia wananchi wa  nchi hizi mbili  kuondokana na umasikini .
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Mto Mara ni mto wa kimataifa unaounganisha nchi mbili za  Tanzania na Kenya. Wananchi na wadau mbalimbali  wa nchi hizi waishio katika Bonde la Mto Mara wanatumia maji na rasilimali zingine kama ardhi na misitu katika bonde hili kwa ajili ya kuendeleza maisha yao ya kijamii na kiuchumi kwa nia ya kupunguza umasikini. Hata hivyo kadri ya miaka inavyokwenda, hali ya rasilimali hizi imekuwa ikipungua kutokana na matumizi mbalimbali.
Hivi sasa tunashuhudia matumizi ya rasilimali hizi yakiongezeka kutokana na ongezeko la mahitaji ikiwa ni pamoja na ongezeko la fursa za kiuchumi. Kwa upande mwingine tunashuhudia rasilimali hizi zikipungua na kuharibika hivyo kupunguza fursa ya nchi hizi na jamii, kujikwamua kiuchumi na kupunguza umasikini. Wakazi wa Bonde hili sasa wanashuhudia kupungua kwa maji na  uchafuzi wa maji, kuzidi kupungua kwa misitu kunakosababishwa na ukataji holela wa miti, uharibifu wa ardhi na uharibifu mkubwa wa mazingira kwa ujumla unaosababishwa na shughuli za kibinadamu. Wito wangu kwenu tunapoadhimisha Siku hii ya Mara, ni wajibu wa kila mmoja wetu kutafakari juu ya changamoto za msingi zinazopaswa kuchukuliwa katika kuboresha matumizi endelevu na usimamizi wa  Bonde hili.  Sote tunafahamu kuwa Bonde la Mto Mara lina umuhimu mkubwa kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa eneo hili, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha linatunzwa na kuendelezwa ili lisadie wananchi wetu kupata maisha bora na kuondokana na umasikini.
Ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunatilia mkazo suala la utunzaji mazingira katika Bonde hili. Uharibifu wa Mazingira ni  moja ya tatizo linalotishia kwa kiasi kikubwa uhai wa Bonde hili. Tusipotilia mkazo utunzaji mazingira katika eneo hili tutaathiri kwa kiasi kikubwa rasilimali zilizomo katika Bonde hili na kukwamisha juhudi za wakazi wa eneo hili kujikwamua na umasikini. Tukiendelea kuharibu mazingira ya Bonde hili tutasababisha matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kupungua kwa kiasi kikubwa cha maji kwenye Mto Mara. Jambo hili halitaathiri wanyama tu bali linaweza hata kusababisha migogoro  ya wanaotumia maji hayo katika nchi hizi mbili. Rai yangu kwa wadau wote wa Bonde la Mto Mara ni kwamba, Maadhimisho ya Siku ya Mara kila mwaka yawe  chombo cha kuhakikisha kuwa hatufiki huko. Naamini kwamba Serikali za nchi zote mbili Tanzania na Kenya  zina sera, sheria na mikakati mizuri inayolenga kuhifadhi na kuhakikisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali mbalimbali za Mto Mara kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwa ujumla. Lazima tuwe na chombo chenye malengo ya pamoja ya kusimamia Sera na Sheria hizo.

Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu kwa mara nyingine naomba niwashukuru wadau wote mliofanyikisha Maadhimisho haya, bila kuwasahau ndugu zetu kutoka Jamhuri ya Watu Kenya kwa namna mlivyojitoa kufanikisha shughuli hii. Asanteni Sana! tuzidi kushirikiana na Karibuni tena na tena.
Baada ya kusema hayo, kwa heshima kubwa na taadhima sasa  natamka rasmi kuwa; Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mara, zimefungwa rasmi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza. 


CHIMBUKO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA MARA.
1.  Utangulizi:
Maadhimisho ya siku ya Mara hutoa taswira ya jinsi viongozi na wananchi wanchi mbili za Kenya na Tanzania wanavyoshirikiana katika kusherehekea maadhimisho ya siku hiyo. Hii ni mojawapo ya shughuli muhimu katika kuimarisha ushirikiano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kilele cha Maadhimisho hayo huwa ni tarehe 15 Septemba ya kila mwaka.
2.  Bonde la Mto Mara:
Bonde hili ni moja kati ya mabonde yenye mito inayoingiza maji katika Ziwa Victoria. Bonde hili linahusisha nchi za pande mbili ambazo ni Kenya ambayo inamiliki takribani asilimia 65 ya eneo bonde na Tanzania asilimia 35. Asili ya mto Mara ni chemichemi ya Enapuyapui iliyoko kwenye misitu ya milima ya Mau katika nchi ya Kenya na maji yake hutiririka kuelekea katika pori la akiba la hifadhi ya Taifa ya Maasai-Mara kwa upande wa Kenya, na kwa upande wa Tanzania mto Mara unapita katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kabla ya kumwaga maji yake katika Ziwa Victoria nchini Tanzania ambapo mto huo hupita katika Wilaya nne za Serengeti, Tarime, Butiama na Rorya. Ikolojia ya Bonde la mto Mara ni moja kati ya Ikolojia muhimu katika Bonde la Ziwa Victoria ambayo inachangia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii pamoja na utumiaji na uhifadhi wa uoto wa Asili.

3.  Chimbuko la Maadhimisho ya Siku ya Mara.
Maadhimisho hayo ni kufuatia maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Mawaziri wanaohusika na masuala ya Bonde la Ziwa Victoria kwenye Mkutano wa kumi uliofanyika tarehe 04 Mei, 2012 huko Kigali Rwanda. Katika Mkutano huo iliamuriwa kuwa maadhimisho hayo yafanyike kwa kupokezana baina ya nchi zote mbili za Kenya na Tanzania.
4.  Faida ya maadhimisho haya:
Siku ya Mara hutumika katika kuendelea kulitangaza na kulifuatilia tukio muhimu la wanyamapori hasa nyumbu kuhama kutoka mbuga za hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda katika pori la hifadhi ya Taifa la Maasai-Mara katika Jamhuri ya Kenya na baadaye kurudi Tanzania na mara zote mbili wanyama hao huvuka mto Mara.
Uamuzi huo wa kuadhimisha Siku ya Mara, ulitokana na kutambua umuhimu wa Ikolojia ya Bonde la mto Mara ambapo siku hiyo itatumika kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mto Mara. Aidha, maadhimisho ya siku ya Mara pia hutumika katika kufanya yafuatayo:
i.                 Kujengea jamii uwezo juu ya uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto za kijamii zinazojitokeza katika Bonde la mto Mara.
ii.                Kuwawezesha wadau kushiriki katika fursa zinazohusiana na Bonde la mto Mara
iii.              Kuitambulisha sura ya Bonde la mto Mara kama eneo muhimu la uwekezaji
iv.              Kujadili mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli zilizoratibiwa katika Bonde la mto Mara.
5.  Changamoto zinazolikabili Bonde la mto Mara
Jamii inayoishi katika Bonde la mto Mara pamoja na wadau mbalimbali wameendelea kushuhudia upungufu mkubwa wa kiwango cha maji pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli za kibinadamu, hali inayopelekea kuwa kikwazo kwa jamii inayoishi katika Bonde la mto Mara katika juhudi zao za kujiongezea kipato, kuwa na afya imara, kuwa na chakula cha uhakika pamoja na kukuza uchumi.
Changamoto hizi zinazotishia kutoweka kwa maliasili (Ikolojia) ya Bonde la mto Mara zinatokana na shughuli za kila siku za kibinadamu ambazo ni pamoja na matumizi ya ardhi yasiyo endelevu, ukataji miti holela kwa ajili ya kuchoma mkaa na ujenzi, uchimbaji holela wa madini, uchafuzi wa vyanzo vya maji, kilimo kisicho endelevu na ufugaji usio endelevu.
Shughuli zingine ni sera na sheria za nchi mbili kutofautiana, ukosefu wa elimu ya hifadhi ya mazingira kwa wakazi waishio katika Bonde la mto Mara, umaskini kwa wakazi wengi wanaoishi katika Bonde, udhaifu wa kusimamia sheria pamoja na ukosefu wa chombo shirikishi cha kusimamia rasilimali za bonde la mto Mara, hizi zikiwa ni baadhi tu ya changamoto.



MAGUFULI AENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI WILAYA YA SIKONGE,KALIUA,ULYANKULU NA URAMBO MKOANI TABORA

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa kaliua alipokuwa akiwahutubia wakazi hao katika uwanja wa Kolimba,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
  Wakazi wa mji wa Kaliua wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa jimbo la Kaliua kupitia chama cha CCM Prof.Juma Kapuya
  Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Urambo kupitia chama cha CCM,Mh.Magret Sitta,kulia kwake ni Mh.Samweli Sitta kwa pamoja wakimkaribisha Dkt Magufuli alipowasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Urambo jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Urambo jioni ya leo mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Urambo jioni ya leo mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni.
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mjini Urambo mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
Wananchi wakiwa wamekusanyika mjini Urambo kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM,Dkt Magufuli.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sikonge mapema leo mchana mjini humo,kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora,kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Sikonge ambaye alijiunga na chama cha CHADEMA mara baada ya kuondolewa kwenye kura za maoni ya chama cha CCM,Ndugu Said Nkumba abaye amerejesha kadi yake kwa Dkt Magufuli,shoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge Ndugu George Joseph.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia aliyekuwa Mbunge wa Sikonge ambaye alijiunga na chama cha CHADEMA mara baada ya kuondolewa kwenye kura za maoni ya chama cha CCM,Ndugu Said Nkumba akipeana mikono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge Ndugu George Joseph,mbele ya Wananchi wa Sikonge kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia aliyekuwa Mbunge wa Sikonge ambaye alijiunga na chama cha CHADEMA mara baada ya kuondolewa kwenye kura za maoni ya chama cha CCM,Ndugu Said Nkumba akimwombea kura Mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge Ndugu George Joseph,mbele ya Wananchi wa Sikonge kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora.
 Wananchi wa Sikonge wakishangilia walipokuwa wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia. 

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Sikonge,Ndugu George Joseph  mbele ya Wananchi wa Sikonge mapema leo mchana mjini humo,kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora 
 Mgombea Urais wa CCM,Dk Magufuli ukiwasili mapema leo kwenye uwanja wa kambi ya zamani ya Wakimbizi kutoka Burundi,Ulyankulu wilayani Kaliua kwa ajili ya kuwahutubia wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi.
 Mgombea Urais wa CCM,Dk Magufuli ukiwahutubia wakazi wa Ulyankulu mapema leo kwenye uwanja wa kambi ya zamani ya Wakimbizi kutoka Burundi,katika mkutano wa Kampeni wilayani Kaliua kwa ajili ya kuwahutubia wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi.
  Mgombea Urais wa CCM,Dk Magufuli ukiwahutubia wakazi wa Ulyankulu mapema leo kwenye uwanja wa kambi ya zamani ya Wakimbizi kutoka Burundi,katika mkutano wa Kampeni wilayani Kaliua kwa ajili ya kuwahutubia wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi.
 Wakazi wa Ulyankulu wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea wa Urais wa CCM,Dkt Magufuli mapema leo mchana.
 Wakazi wa Ulyankulu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea wa Urais wa CCM,Dkt Magufuli mapema leo mchana.
 Wananchi walipokuwa wameziba barabara wakitaka kumuona Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akipita kuelekea wilayani Kaliua kuwahutubia wananchi.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wananchi waliokuwa wameziba barabara kuuzuia msafara wa mgombea huyo awasalimie.
 Mgombea Ubunge wa CCM kupitia jimbo la Kaliua,Prof.Juma Kapuya akiwahutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba mjini Kaliuna mapema leo.
 Wakazi wa mji wa Kaliua wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.

 Wananchi wa Urambo wakimsubiri kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa kaliua alipokuwa akiwahutubia wakazi hao katika uwanja wa Kolimba,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.

TAARIFA YA TANZIA

$
0
0
TANZIA

FAMILIA YA MAREHEMU ABDALLAH SELEMANI REHANI WA TABATA DAR ES SALAAM INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA YAO MZAZI HAJJAT PILI MLOLWA REHANI KILICHOTOKEA LEO ALFAJIRI KWENYE HOSPITALI YA MUHIMBILI.

MAZISHI YATAFANYIKA LEO SAA 10 JIONI KWENYE MAKABURI YA SEGEREA, DAR ES SALAAM.

HABARI ZIWAFIKIE:
1.  FAMILIA YA MZEE MLOLWA WA MTAA WA KAMNA, TABORA
2.  UKOO WOTE WA MLOLWA NA FUNDIKIRA WA TABORA
3.  SHEMEJI WA MAREHEMU RAJABU MBUGA WA RUKWA
4.  FAMILIA YA MHE. MIZENGO PINDA YA MPANDA NA MLELE KATAVI
5.  MDOGO WA MAREHEMU, MWL. HAMISI MLOLWA WA NDONO, TABORA
6.  FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED KAFYOME WA NG’AMBO, TABORA.
7.  FAMILIA YA MAREHEMU ABOUD JUMBE YA IGOMA, MWANZA
8.  NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

WAZIRI AWAASA VIJANA KUPAMBANA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea
wakati wa uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya karume jijini Dar
es Saalam.
 Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Prof
Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel
 Rising Stars katika ngazi ya taifa
 Mwanamuziki wa Hip Hop Nay Wa Mitego akitumbuiza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa katika Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara
amewaasa vijana wanaoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa
vijana chini ya miaka 17, kupambana kwa bidii ili kufanikisha malengo
yao.
Dr. Mukangara alisema hayo wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo katika
uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Jumapili
iliyopita.

 
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mukangara,  Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema kuwa Dr. Mukangara
amemimina pongezi za dhati kwa kampuni ya Airtel hapa nchini kwa
kuendelea kutoa sapoti kwa maendeleo ya soka hapa nchini ili
kuitangaza Tanzania kimataifa.

 
“Angalieni timu ya taifa ya wasichana- Twiga Stars. Kuna wachezaji
wengi sana ambao wametokana na michuano hii” , alisema huku akilitaka
Shirikisho la Soka nchini (TFF) na wadau wengine kutumia michuano hii
kutafuta vipaji vipya kwa maendeleo ya soka hapa nchini.

 
Alisema kuwa kwa kuweka msisitizo mkubwa kwenye soka la vijana,
Tanzania itakuja kuwa moja ya nchi zenye nguvu kubwa katika soka.
“Mataifa yote yenye nguvu katika soka duniani, yamefanikiwa kutokana
na programu hizi”, alisema.

 
“Kiwango chetu cha soka kitakapoimarika, tutakuwa na fursa nzuri sana
ya kujitangaza kimataifa hasa vivutio vyetu kama vile Mlima
Kilimanjaro ambao ndio mrefu kuliko yote duniani na hifadhi zetu za
taifa. Hii itafanya watalii wengi kuja hapa nchini hivyo kuongeza pato
la taifa”, alisema


Pia aliwashauri vijana kuongeza juhudi zaidi kwani mchezo wa soka kwa
sasa umekuwa ni moja ni sekta rasmi ambayo inatoa ajira  kwa kiasi
kikubwa, hivyo juhudi zao ndio msingi wa mafanikio yao na familia zao.

 
Akizungumza katika hafla hiyo hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel nchini, Beatrice Singano Mallya, alisisitiza kampuni yake
kuendelea kudhamini michuano hiyo huku akionesha kuridhishwa na jinsi
Wizara husika, TFF na wadau wengine wanavyotoa sapoti kubwa sana kwa
kampuni hiyo. “Tunajivunia sana mafanikio yaliyopatikana kupitia
michuano hii na tunaahidi kuendelea kutoa sapoti kama ambavyo tumekuwa
tukifanya”.

 alisema
Kwa upande wake, makamu wa rasi wa TFF Wallace Karia aliwashukuru
Airtel na kuyaomba makampuni mengine kuiga mfano huu.
Sherehe za ufunguzi zilitanguliwa na michezo miwili, ambapo
wenyeji-timu ya wasichana ya Temeke iliwatungua bila huruma Arusha kwa
magoli 8-0, kabla ya hapo baadaye Mwanza kuifunga Kinondoni kwa bao
1-0, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja huo huo wa Karume.

UKAWA WAFANYA MIKUTANO YA KAMPENI KATAVI VIJIJINI

$
0
0
 Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Zanzibar (CUF), Habib Mnyaa akihutubia mkutano wa kampeni za urais, ubunge na madiwani katika kijiji cha Katumba Wilaya ya Nsimbo, Mpanda mkoani Katavi. (Picha na Francis Dande)
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Zanzibar, Said Issa Mahamed  akihutubia mkutano wa kampeni za urais, ubunge na madiwani katika kijiji cha Katumba Wilaya ya Nsimbo, Mpanda mkoani Katavi.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Zanzibar, Said Issa Mohamed (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Nsimbo, Gerald Kitabu ambaye ni mwandishi wa habari wa The Guardian Ltd wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mnyaki, Mpanda mkoani Katavi.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Nsimbo, Gerald Kitabu ambaye ni mwandishi wa habari wa The Guardian Ltd akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnyaki, Mpanda mkoani Katavi.

WASTAAFU WA JWTZ WAKIFANYA USAJILI WA NSSF MKOANI MOROGORO

$
0
0
Kusajiliwa wastaafu wa jeshi.
 Ofisa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),mkoa wa Morogoro, Abdul Mzee ( kushoto) akichukua alama ya vidole kwa Mwanachama wa  Muungano  wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA), Luteni mstaafu, Josephat Mtema, sept 13, mwaka huu ,ili kujiunga na NSSF kwa mfumo wa kuchangia kwa hiari kwa ajili ya  kunufaika na huduma za mfuko huo ikiwa na matibabu wakati walipokuwa katika mkutano wa kawaida wa siku mbili uliofanyika Bwalo la Umwema ,mjini Morogoro.
Mwenyekiti wa MUWAWATA, Ssg Mstaafu, Asseidy Rajabbu Mayuggi, akieleza jambo.
Wastaafu wa jeshi katika picha ya pamoja.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images