Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SUSPECTED Designers of Fraudulent Credit and Loan Websites in Court

$
0
0
unnamedSUSPECTED Designers of  Fraudulent Credit and Loan Websites, Maxmillian Rafael Msacky (second left) and Patrick James Natala (third right) at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar Es Salaam on Friday, 11September 2015, faced with 10 charges including producing Fake Websites identified as “Jakaya Kikwete Foundation (State House), TCRA Foundation, AkibaSaccos Social Company, Social Credit and Loans Company, Ridhiwani Social Company, Hisa Tanzania, Zitto Kabwe Foundation, Vicoba Tanzania and Wekeza Fund”.The suspects who also allegedly used fake names to register SIM Cards denied all charges before Resident MagistrateEmelliusMchaulo and remanded until 24th September 2015 when the case comes up for another mention.
(Photo by Courtesy of TCRA)

Bi. Samia Suluhu Afunika Mkutano wa Kampeni Kibaha

$
0
0

WanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.

Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
WanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.
WanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.
Mmoja wa wasanii wa kugani mashairi akiwaburudisha wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, ambapo mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) alihutubia.

Mjumbe wa Kamati ya kampeni Taifa ya CCM, Anjela Kairuki, akizungumza kumnadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (hayupo pichani) kwenye mkutano wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe.

Kikundi cha akinamama wajasiliamali na utamaduni kutoka Temeke kikitoa burudani kwa umati na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais,  katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe.

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kulia) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani, Subira Mgalu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Aliyekuwa mbunge wa Nkenge na mjumbe wa kamati ya kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Bi. Asumpta Mshama (katikati) akiwagawia zawadi ya kanga wanakikundi cha akinamama wajasiriamai cha Temeke katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Vijana wakiburudisha umati wa wanaCCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu (kulia) akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Said Jafo (kulia) katikati ni mgombea udiwani, Mwishehe Mlao mkoani Pwani,
Baadhi ya wagombea nafasi za udiwani CCM Jimbo la Kisarawe, mkoani Pwani wakitambulishwa katika mkutano wa kampeni.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kulia) akipewa zawadi na baadhi ya akinamama mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kulia) akipewa zawadi na baadhi ya akinamama mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi, Samia Suluhu (kulia) akipewa zawadi na baadhi ya akinamama mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Kisarawe leo.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
Msanii Snura (katikati) akitoa burudani kwa Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni leo.
Msanii Snura (katikati) akitoa burudani kwa Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni leo.
Wema Sepetu akizungumza na Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni leo.
Chipukizi wa CCM wakitoa burudani katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis (kulia) akizungumza jambo na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais Bi. Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi ya CHADEMA toka kwa Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Bwana Nyakarungu (kulia) mara baada ya kujiunga CCM leo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis akimvalisha sare za CCM Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Bwana Nyakarungu mara baada ya kujiunga CCM leo.
Kada wa CHADEMA na Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Bwana Nyakarungu (katikati) akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa chama hicho mara baada ya kukihama chama hicho na kwenda CCM na kuvalishwa sare za CCM.
Raha ujipe mwenyewe bana..! Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis akijinasibu kwenye mkutano huo.
Kada wa CHADEMA na Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Bwana Nyakarungu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa chama hicho mara baada ya kukihama chama hicho na kwenda CCM na kuvalishwa sare za CCM.
Mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu (katikati) akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis (kulia) katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
*Picha zote/www.thehabari.com

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI USIKU HUU

$
0
0


Mtando wa haki za binadamu pamoja na waharakati mbalimbali wafungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vipengele vya sheria ya makosa ya mtandaohttps://youtu.be/8BmxxpgPmEA



Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, yawafikisha vijana wawili mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam kwa makosa ya uhalifu wa kimtandaohttps://youtu.be/CPupB76lEsA



Mgombea uraisi wa chama cha ACT  Wazalendo awaasa wagombea wenzake kuacha vijembe na kushutumiana na badala yake wajikite kunadi sera. https://youtu.be/piPuQNa1jpg



Raisi Kikwete ataembelea mahakama ya Afrika iliyoko jijini Arusha huku akiwaasa viongozi wa Afrika kuipa Mahakama hiyo Mamlaka kamili. https://youtu.be/fpueMGvuQWw



Watoto wenye maradhi ya ugonjwa wa Saratani wanaopatiwa matibabu hospitali ya taifa Muhimbili wapatiwa msaa na Vodacom Foundation. https://youtu.be/HoxL4dFceOY



Polisi mkoani Geita inamshikilia mgangawa kienyeji kwa tuhuma za kuwapa wateja wake dawa yenye sumu huku 1 akifariki na wengine kulazwahttps://youtu.be/M2wyDHLl3b4



Aliyekuwa mbunge wa Ubungo John Mnyika awataka waangalizi wa uchaguzi mwaka huu kuondoa shaka na kufanya kazi zao kwa uhuru. https://youtu.be/nez73xjrUdY



Serikali ya toa msaada wa dola milioni 4 kama msaada wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iliyoko mkoani Arusha. https://youtu.be/VDdL81VTfkM



Mgombea uraisi wa Chadema Edward Lowassa ahaidi kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama chake akichaguliwa kuwa raisi. https://youtu.be/rmPoZmwW61g



Mgombea uraisi kupitia CCM Dr.Magufuli ahaidi kufufua uchumi wa mkoa wa Mara huku akisisitiza maendeleo ya uhakikahttps://youtu.be/rLi8TVpk2AU



Mgombea Mwenza wa uraisi kupitia Chadema Juma Duni ahaidi kuboresha huduma za afya kwenye hospitali teule kwenye wilaya ya Iringa. https://youtu.be/BBm0vuvMxVU



Katibu mkuuwa chadema John Mnyika atoa rai kwa NEC kuruhusu waangalizi wa ndani wa kutosha ili kuboresha usismamizi wa zoezi hilo. https://youtu.be/lwSr7RHVxO8



Mgombea Mwenza wa CCM Bi,Samia Suluhu atangaza neema kwa vijana baada ya kuhaidi kutoa asilimia  30 ya zabuni kwa kampuni za vijana. https://youtu.be/TiKPbetVedI



Mgombea uraisi kupitia CCM Dr.Magufuli ahaidi kuboresha mfumo mzima wa sekta ya madini ili ulete tija kwa watanzania ikiwemo ajirahttps://youtu.be/Tngdq_djA90



Baadhi ya wakazi wa kata ya Kayenze wadai watampigia kura kiongozi yeyete mwenye uwezo wa kutatua matatizo yao ikiwemo maji.https://youtu.be/kkZt4PwOW0Y



Mfuko wa uwekezaji nchini umefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 240 katika kipindi cha miaka 10 huku wananchi wengi wakiwa hawatambui umuhimu wa mfuko huo. https://youtu.be/JZqBivHNGBE



Mkuu wa majeshi ya Burundi anusurika kuuwawa wakati akielekea kazini baada ya watu wenye silaha kufanya shambulio la kushitukiza. https://youtu.be/J8yl27LEL9E



Kamati ya amani ya mkoa wa Dar es salaam yawataka wananchi kushirikiana na viongozi mbalimbali ili kuepusha vitendo mbalimbali vya uhalifu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.



Idara ya majanga na maafa ya ofisi ya waziri mkuu yakiri uwepo wa uhaba wa fedha kuendesha kitengo hicho. https://youtu.be/6Cq2ZoBngAc

MABADILIKO BORA NDIYO WANAINCHI WANAYOHITAJI NA SIO BORA MABADILIKO-DKT MAGUFULI

$
0
0
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Musoma waliojitokeza kwa wingi wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa  akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo,Dkt Magufuli aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo ambapo aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo ambapo aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo. 

 Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Tarime katika mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika mjini Tarime leo ambapo Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili aweze kuingia ikulu na kuwatumikia watanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko bora kwa watanzania na siyo bora mabadiliko.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo ambapo aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akipiga Drums Ngoma za muziki wakati alipofika Utegi wilaya ya Rolya na kufanya mkutano wa kampeni.

 Sehemu ya nyomi la watu mjini Nyamongo wilayani Tarime
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akishangiliwa na uati wa watu mara baada ya kuwahutubia wakazi hao mji wa Nyamongo,wilayani Tarime jioni ya leo
 Wananchi wa Tarime wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM
 Jaji Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba akizungumza na wananchi wa mjini Tarime wakati alipokuwa akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake mjini Tarime.
 Sehemu ya umati w Wananchi wakifuatilia sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Joseph Magufuli,alipokuwa akiomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Joseph Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarime waliofurika kwa wingi.  
 Jukwaani napo palikuwa hapatoshi
 Wazee wa kimila wa wilaya ya Tarime wakisubiri kusalimiana na mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli  akiwahutubia Wananchi wa Rorya katika uwanja wa Utegi
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia Wananchi wa Rorya katika uwanja wa Utegi 
 Mbwembwe za boda boda kama hivi zilikuwepo mjini Musoma
 Mgombea Urais wa CCM Dkt  Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Mukendo jioni ya leo,ambapo pia aliwahutubia wananchi hao 
 Kikundi cha Tot Plus kikitumbuiza jukwaani
 Wakazi wa Mji wa Musoma wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma jioni ya leo.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Makongoro Nyerere akihutubia mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi Dk. John Pombe Magufuli.
 Mabango ya wafuasi wa chama cha CCM. 
 Naibu Waziri wa  Fedha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa mji wa Musoma kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma jioni ya leo

SEHEMU YA PILI YA MAFANIKIO SIYO AJALI.

$
0
0
UNAJUA watu wengi hawajawahi kujiuliza maswali kama haya hapa... Kwa nini Mungu aliumba mito? Kwa nini Mungu aliumba Miti? Kwa nini Mungu aliumba chuma? Mungu hakukupa vitu vilivyotimia kwa sababu anajua una asili ya uumbaji ndani yako maana umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, hivyo basi hakukupa vitu vilivyokamilika ila alikupa vitu ambavyo vitakupelekea kutengeneza vitu vingine ili uendeleze ule uumbaji ambao yeye aliuanzisha ,tunajua kabisa kwamba Mungu ni asili ya uumbaji.

Nataka nikwambie hivi binadamu kawekewa uwezo wa ajabu sana ndani yake na Mwenyezi Mungu wa kutenda mambo makubwa na ya ajabu ndio maana Mungu hakukupa vitu vilivyokamilika kama magari,nyumba, ndege,umeme,meza, n.k ili aliweka ndani yako uwezo wa kutumia mito ukatengeneza madaraja juu yake na magari yakapiti lakini pia alijua kabisa unao uwezo wa kutumia mito ukatengeneza mitumbwi ikapita, lakini pia alijua unao uwezo wa kutumia maji ukatengeneza umeme na ukautumia huo umeme kwa matumizi mbalimbali kama kwenye viwandani,manyumbani,maofisini na kadhalika.

Pia Mungu aliumba miti hakuumba meza, wala vitanda ,wala viti,wala mkaa kwa sababu anajua unao uwezo wa kubadili hivi vitu kuwa vitu vingine kwa ajili ya matumizi yako na pia ukaendeleza uumbaji wake.

Hebu angalia tena fikiri kwa kina Mungu kaumba chuma lakini hakuumba gari ila ndani yako wewe kama mwanadamu aliweka uwezo wa kutengeneza magari kwa kupitia zile chuma. Sasa swali nakuuliza katika vitu vyoote Mungu alivyotupa bure kabisa kuna ardhi,kuna maji, kuna anga,kuna hewa, kuna bahari, kuna maziwa na vingine vingi wewe umetumia kipi kuendeleza uumbaji wa Mungu hii ni changamoto kwangu na kwako.

Hebu tazama Wright Brothers waliweza kutumia anga kutengeneza ndege, Hivi unajua kwamba katika kikao cha mwisho kilichojumuisha wanasayansi 64 wote walisema kwamba haiwezekani kutengeneza ndege ikapaa hewani? Na je unajua kwamba hao wenyewe tuu ndio walibakia katika kikao kile wakisema kwamba inawezekana? Na je unajua Baba yao aliwaambia wakifa watachomwa moto kwa kuwa na wazo kwamba inawezekana kutengeneza ndege na kuirusha angani? Leo ndege zipo au hazipo?

Nafurahi hawakumsikiliza yeyote walisimamia wazo lao waliamini inawezekana na kweli mwisho wa siku waliweza Leo hii tunasafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani pasipo shida ya aina yoyote kwa sababu ya Wright Brothers, ushawahi kujiuliza kama kungekuwa hakuna ndege watu wakasafiri kwa mabasi au meli ingekuchukua mda gani kutoka hapa Tanzania kufika Marekani au Brazil au Canada au Wingereza? Bila shaka ungesafiri hata miezi miwili mitatu na bado usingefika. Mungu awapumzishe pepa peponi asante Mungu kwa kuwaumba.

Nakuja kwako wewe je una mipango mingapi umeiacha kisa watu wamekuambia haiwezekani? usiwasikilize nakwambia maana watu wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao kwa kusikiliza watu hata kama ni mzazi wako, hata kama ni rafiki,hata kama ni ndugu ivi kweli jaribu kutafakari haya maneno kwa kina kama tungefanya kama wazazi wetu walivyofanya mabadiliko yangekaa yatokee? 

Wright Brothers wangemsikiliza baba yao leo tungekuwa na ndege?anza kushughulikia mpango wako maadamu unauona katika fikra zako ina maana unaweza kuutimiliza mimi nakuhakikishia hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia kupata kile unachokitaka labda tuu uamue kujizuia mwenyewe ila kama kweli umenuia kukitafuta kwa moyo wako wote na ukafuata taratibu zote za kukitafuta utakipata tuu na sina wasiwasi katika kusema hivi.

Naomba nimalizie kwa kusema hivi kitu pekee kitakachokuzuia kupata kile unachokitaka ni wewe mwenyewe na kingine ni kuruhusu maoni ya watu wengine kutawala mawazo yako kwamba huwezi ukafanikiwa katika hilo unalotaka kufanya.
 IMEANDALIWA NA HUMPHREY MAKUNDI NA ALLARD MINJA.

VIPINDI VYA MAMA MISITU KUHUSU UZALISHAJI WA MKAA ENDELEVU KUFANYIKA KATIKA HOTELI YA NEW AFRIKAJIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa chokozi katika uzinduzi wa mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini uliofanyika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam leo asubuhi.
 Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Makamba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa UFINI ambao ni wafadhili wa mama misitu, Simo-Pekka Parviainen na Ofisa Mradi Ubalozi wa Finland, William Nambiza.
Mshauri wa Ufundi Weizara ya Maliasili na Utalii, Thomas Sellaine (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Rahima Njaidi (kushoto), akielezea shughuli zinazofanywa na mtandao huo.
Mkuu wa Mradi ya Kilimo, Kipato na Ajira wa Shirika la Maendeleo la Uswisi, Ueli Mauderli (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.

 
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
 Mkutano wa uzinduzi huo ukiendelea.
 Mwezeshaji, Faustine Ninga kutoka Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), akitoa maelekezo mbalimbali.
 Meneja Kampeni Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Balozi wa Mama Misitu, Asha Salimu (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Wasainii walioigiza namna ya utunzaji wa miti. Kulia ni Philemon Robari na Mohammed Titima.
Maofisa mbalimbali waliopo kwenye mradi huo wa Mama Misitu wakiwa katika uzinduzi huo.

Na Mwandishi wetu.
 MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.

Vipindi hivyo mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Shirika la Kuendeleza Teknolojia  za Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za vijijini na mijini.

Inakadiriwa kuwa mkaa na biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012. Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa.

Mkaa endelevu ni mkaa unaozalishwa kwa njia endelevu kutoka katika Misitu ya Hifadhi ya Jamii bila kuchangia ukataji miti na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, uzalishaji wa aina hii ya mkaa bado haujajulikana. Kampeni hii mpya ina lengo la kuleta mabadiliko kupitia ubunifu wa vipindi mfululizo vya runinga ambavyo vinazinduliwa leo.

Nishati zitokanazo na tongamotaka (biomas)  ni nishati muhimu sana nchini Tanzania itakayoendelea kutumika angalau zaidi ya miaka 20 ijayo. Kwa sasa, mkaa mwingi huzalishwa kinyume na utaratibu kutoka katika misitu ya hifadhi na misitu ya vijiji isiyo na mipango ya matumizi endelevu. Kutokana na usimamizi hafifu wa uzalishaji wa mkaa, imesababisha ukataji miti na uharibifu wa misitu kuongezeka nchini Tanzania.

Kampeni ya Mama Misitu na washirika wake (TFCG na MJUMITA) inalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya mkaa kutoka tatizo kuwa fursa kubwa muhimu. Hivyo, vipindi vya runinga vya Mama Misitu pamoja na jumbe muhimu za mawasiliano zitasambazwa nchini Tanzania ili kuibua mjadala wa pamoja juu ya kuboresha utawala bora wa rasilimali misitu na kuleta faida kwa watanzania.

Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano yenye lengo la kuboresha utawala bora wa misitu ya Tanzania na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu ili watu wa Tanzania wanufaike zaidi na rasilimali misitu zao.

JESHI LA POLISI LAHIMIZA AMANI NA MSHIKAMANO KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA 25.10.2015

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM LAHIMIZA AMANI NA MSHIKAMANO KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA 25.10.2015
        Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova amewakumbusha watanzania hususani wananchi wanaoishi jijini Dar es Salaam kukumbuka wajibu wao wa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi mkuu.

mchakato huo ni pamoja na wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura tarehe 25.10.2015 na baada ya kutangazwa kwa matokeo  mablimbali katika ngazi za udiwani, ubunge na urais.

Kamishna ameyasema hayo katika uwanja wa mpira wa karume jijini dsm alipoenda kukaguwa mazoezi ya pamoja yanayowashirikisha viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo Masheikh, Maaskofu, mapadre wachungaji na mabalozi wa nchi mbalimbali.

Mabalozi na wawakilishi wa Nchi zao walioshiriki mazoezi hayo ni pamoja na Ujerumani, Uholanzi, Urusi, na Denmark ambao Kamishna aliwashukuru kwa ushiriki wao ulilenga kudumisha amani ya Tanzania.

Aidha watanzania wamekumbushwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki  kuelekea uchaguzi mkuu  kwani muda huu ni mfupi sana ukilinganisha  na muda mrefu  ambapo Tanzania imekuwa na amani. Wanatakiwa washirikiane bila kujali itikadi zao au tofauti zozote zile kwa madhumini ya kudumisha amani iliyopo.

Jeshi la Polisi limejiandaa kikamilifu katika kulinda amani na usalama wa Nchi na kutoa onyo kwa wale watu wachache watakaovuruga amani na usalama kwani wakibainika watashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria.

Katika zoezi hilo hapo uwanja wa karume Kamishna Kova alikabidhi mipira mitano kwa Mwenyekiti wa timu ya Amani na mshikamano Sheikh Alhad Mussa Salum ambaye pia ni Sheilk wa Mkoa wa Dar es Salaam akisaidiwa na Mchungaji FUPE -Makamu Mwenyekiti, na Katibu wa timu PADRE JOHN SOLOMONI ili kuwapa hamasa katika kazi yao ya pamoja iliyo nzuri na muhimu kwa taifa hili. Aidha Kamishna alipata fursa ya kupuliza filimbi katikati ya uwanja ikiashiria kuanzisha mazoezi kwa madhumuni ya kuhamasisha amani na mshikamano.

Kamishna Kova amewambia watanzania kupitia shughuli hiyo kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu "kipaumbele cha kwanza ni  amani cha pili ni amani na cha tatu ni amani"

SULEIMAN H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


MKUTANO WA KILELE WA DUNIA KUHUSU CHAKULA NA LISHE WAFUNGULIWA ARUSHA

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa unahusu masuala ya Lishe na Chakula uliofanyika jijini Arusha.
Mhe. Pinda akihutubia
Mfalme wa Lesotho Mhe. Letsie III ambaye nae alihudhuria mkutano huo  akihutubia wadau mbalimbali na wageni waalikwa walioshiriki katika mkutano huo (hawapo pichani).
Balozi wa Tanzania anayeiwakilisha nchini Lesotho, Mhe. Radhia Msuya (kulia) akifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo  

 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa kwanza kushoto, mwenye tai ya njano) akifuatilia kwa karibu hotuba zilizo kuwa zikitolewa katika ghafla ya ufunguzi wa Mkutano huo katika Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (katikati), Msaidizi wa Naibu Waziri wa Afya, Bw. Kurwa (wa kwanza kushoto) kwa pamoja nao wakifuatilia kwa makini Hotuba za viongozi mbalimbali katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano.
Wageni waalikwa
 Wadau mablimbali wakifuatilia hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na viongozi ho
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe naye alitoa Hotuba yake wakati wa Hafla hiyo
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau mbalimbali katika meza kuu
Picha na Reginald philip 
TANZANIA imeendelea kuunga mkono jitihada za kitaifa na kimataifa katika kuhakikisha usalama wa chakula pamoja na lishe bora yenye virutubisho muhimu hususan kwa watoto wadogo, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha inapatikana kwa maendeleo endelevu ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda alipozungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu masuala ya Chakula na Lishe uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha hivi karibuni.
Mhe. Pinda alisema kuwa jitihada hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimeelekezwa katika kuhamasisha unyonyeshaji wa watoto wachanga na kutumia vyakula vyenye virutubisho kwa watoto wa kuanzia miezi sita hadi mwaka mmoja umesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo vitokananvyo na ukosefu wa chakula bora na utapiamlo.
Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa na program mbalimbali kwa vipindi tofauti katika kupambana na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho na madini muhimu ikiwemo program ya kuongeza madini joto kwenye chumvi iliyozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi mapema mwaka 1990 ili kupambana na magonjwa yanayosababishwa na upungufu wa madini hayo mwilini ikiwemo ugonjwa wa goiter ambao ulienea nchini miaka ya 1980.
Aidha, mwaka 2013 Serikali ilizindua Program ya Kitaifa ya Uboreshaji wa Chakula ambapo virutubisho muhimu viliongezwa kwenye vyakula vinavyoliwa zaidi katika jamiii ya Watanzania ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 25 ya watu wanatumia unga wa ngano na mahindi pamoja na mafuta ya kupikia yaliyoongezwa virutubisho vyenye madini na vitamin muhimu kama chuma, zinki na Vitamini A na B12.
“Kwa upande wa Tanzania jitihada nyingi za kuhakikisha suala zima la upatikanaji wa chakula bora ili kuwawezesha wananchi kuwa na afya bora ili kuchangia katika maendeleo ya taifa lao zimefanyika. Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto wachanga, kuzinduliwa kwa Mkakati wa Taifa wa Lishe  wa miaka mitano hapo mwaka 2011 ambao lengo lake kubwa ni kuhamasisha matumizi ya vyakula vyenye virutubisho” alisema Mhe. Pinda.
Aidha, alieleza kuwa kwa sasa Serikali kupitia Mamlaka za Serikali za mitaa imeweka mkazo kuhakikisha huduma ya uboreshaji vyakula kwa kuongeza virutubisho muhimu inapelekwa katika maeneo ya vivijini ambapo zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanaishi huko. “Mifumo inaandaliwa ili kuhakikisha mamalaka hizi zinafanikisha uboreshaji wa vyakula ikiwemo unga wa nafaka unaozalishwa katika mashine za kawaida na mafuta ya kula yanayotengenezwa na wananchi vijijini yanaboreshwa” alisisitiza Mhe. Pinda.
Katika hatua nyingine Mhe. Pinda alisifu na kuwashukuru waandaaji wa mkutano huo kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji  kwani ni wakati muafaka ambapo kampeni hii ya dunia itasaidia kuhamasisha pia wananchi na wawekezaji katika sekta ya chakula hapa nchini na hatimaye kuleta matokeo endelevu katika lishe na usalama wa afya ya jamii kwa ujumla. 
Pia alisema kuwa kwa vile mkutano huo umewashirikisha watu kutoka Serikalini, wafanyabiashara, taasisi za kiraia, mashirika ya kimataifa, wanazuoni na washirika wa maendeleo ana imani kubwa kuwa utaainisha mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya baadaye kuhusu uboreshaji wa afya ya jamii zetu kwa maendeleo endelevu.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Mfalme Letsie III kutoka Lesotho ambaye pia ni Kiongozi wa kuhamashisha matumizi ya chakula bora na lishe wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, alisema kwamba lishe bora ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi kwa kila taifa. Kwamba kuwekeza kwenye lishe ni muhimu ili kupunguza umaskini kwa kuhakikisha kila mwanajamii anachangia kwa taifa lake.
Alieleza kuwa Mkakati wa Lishe wa Kanda ya Afrika kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015-2025 uliozinduliwa mwezi Julai mwaka huu kuwa unasisitiza ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika kuboresha lishe ikiwemo sekta binafsi ambapo alitoa tahadhari kwa wafanyabiashara kutotumia fursa hii kujitengenezea faida kubwa kwa bidhaa watakazozalisha badala ya kuangalia afya za watu kwanza. Pia mapendekezo kuhusu njia bora za uchangiaji mpango wa lishe Afrika yalijadiliwa. 
“Natoa tahadhari kwa wenzetu wa sekta binafsi kuhakikisha afya ya mtu inapewa kipaumbele na kuhakikisha ari ya kujipatia faida haihatarishi afya ya mtu yeyote”alisisitiza Mfalme Letsie III.
Pia aliongeza kuwa, Kamisheni ya Umoja wa Afrika na nchi wanachama zinatambua kwamba Serikali pekee haziwezi kutatua changamoto ya lishe duni inayolikabili Bara la Afrika bali jitihada za wadau wote muhimu zinahitajika ikiwemo sekta binafsi hususan kampuni zinazozalisha na kutengeneza vyakula, Mashirika ya Kimataifa, taasisi za kiraia na wanazuoni wanatakiwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya lishe bora kwa kila mtu. 
Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe alisma kuwa amefarijika mkutano wa kwanza kuhusu masuala ya chakula na lishe umefanyika nchini na kwamba mada zitakazojadiliwa wakati wa mkutano huo zitaziwezesha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kuangalia namna bora ya kuboresha lishe kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu uboreshaji wa Chakula na Lishe uliowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya kimataifa, serikali, wanazuoni, washirika wa maendeleo na sekta binafsi umefanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 Septemba, 2015.

IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI ZANZIBAR YAANDAA MRADI WA KUBORESHA MAENEO MATANO YA WAZI YA MJI WA ZANZIBAR CHINI YA UFADHILI WA SHIRIKA LA SDC LA SWITZERLAND.

$
0
0
 Mkuu wa Ushirikiano wa  Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha maeneo matano ya wazi ya Mji wa Zanzibar kwa kuanzia na  Kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti utakaofadhiliwa na Shirika la SDC la nchi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akizindua  Mradi wa kuboresha maeneo ya wazi ya Mjini  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Idara ya Ardhi na Upimaji Forodhani Mjini Zanzibar, (kulia) Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Muhamad Juma
  Msaidizi  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya Landscape ya Switzerland Roland Raderschall akitoa maelezo ya  Mradi wa  mwanzo wa kuboresha  Kiwanja cha Demokrasia cha Kibandamaiti katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
 Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Zanzibar Muhamad Juma akitoa ufafanuzi kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha eneo la wazi  la Kibandamaiti., (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Ramani ya maeneo matano  ya wazi yatakayofanyiwa  uboreshaji  na Idara ya Mipango na Vijiji ambayo ni Kibandamaiti, Lumumba, Darajani, Chumbuni na Darajabovu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIIANA NA SHIRIKA LA HELPAGE INTERNATIONAL WAMEANDAA MKUTANO WA SIKU MBILI WA KUTATHMINI HUDUMA BORA ZA WAZEE ZANZIBAR KATIKA HOTELI YA OCEAN VIEW.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar ulioandaliwa na Wizara yake kwa ufadhili wa Shirika la HelpAge International katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Naibu Mkurugenzi wa Shirika la HelpAge Internalinal  Smart Daniel akizungumza na washiriki wa Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar katika Hoteli ya Ocean View Kilmani (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na kushoto Mwenyekiti wa Mkutano huo  Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Haji Makungu Mgongo. PICHA NA RAMADHANI ALI / MAELEZO ZANZIBAR.
 Washiriki wa Mkutano  huo wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana juu ya mikakati itakayofanikisha kuandaliwa mazingira bora ya maisha ya Wazee Zanzibar.
 Daktari Dhamana  Wilaya ya Wete akiwasilisha kazi za vikundi katika mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Saleh Muhammed Jidawi akifunga mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar uliofanyika katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Zanzibar, Madaktari dhamana wa Hospitali kuu za Wilaya, Jumuia ya Wazee  na Taasisi za kiraia baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya.

KAMATI ZA MAAFA MKOANI DODOMA WAFANYA TATHMINI YA MPANGO WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MAAFA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa Dodoma, LuteniMstaafu, Chiku Galawa akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
 Mjumbe wa Kamati ya Maafa wilayani Mpwampwa, Shekh, Sabah Seif akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa kujadili Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
 Wakuu wa wilya za Mkoa wa Dodoma ambao pia ni Wajumbe wa Kamati za Wilaya za Maafa wakifuatilia uwasilishaji Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015. Wakwanza ni; Shaban Kisu (Kondoa), Ramadhani Maneno (Chemba), Francis Kimoga (Bahi) na Bituni Msangi (Mpwapwa).
 
 Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Charles Msangi  akisisitiza jambo wakati akiwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wa Halmashauri ya  Chamwino, wakati wa Mkutano wa kujadili  Utekelezaji wa Mpango kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
Mkuu wa Mkoa Dodoma, Luteni. Mstaafu, Chiku Galawa (walio kaa katikati) akiwa na wajumbe wa Kamati za maafa za wilaya mkoani Dodoma mara baada kufungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa , tarehe 12 Septemba, 2015.

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la  Wasomi wa  Vyuo Vikuu Zanzibar kupitia CCM  Khamis  Ali Ameir alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar kuzungumza na Shirikisho hilo leo,
 Viongozi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Taifa CCM wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipoingia katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo kuzungumza na Shirikisho a  Wasomi wa  Vyuo Vikuu Zanzibar kupitia CCM
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa Shirikisho la Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar CCM wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar ambapo  mkutano huo ulifunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa Shirikisho la Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar CCM wakisikiliza hotuba ya ufunguzi  iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo  katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa Shirikisho la Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar CCM wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar ambapo  mkutano huo ulifunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Risala ya Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Zanzibar kupitia CCM Kassim Ali Khamis kabla ya kuufungua  wa Mkutano wa Shirikisho hilo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein Kuzungumza na Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Zanzibar kupitia CCM katika mkutano wa siku moja uliofanyika leo katika ukumbi wa   Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa Shirikisho la Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar CCM wakimsikiliza   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi  mkutano wa shirikisho hilo uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi  mkutano wa shirikisho la Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar CCM  uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

BASATA YAONYA LUGHA CHAFU, MAADILI HUSUSAN KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
KATIKA siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wasanii kuvunja maadili, kukaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi za Sanaa hususan muziki hali ambayo imezua malalamiko, masikitiko na hofu kwa jamii ambayo ni walaji wa kazi za Sanaa.

Lugha hiyo chafu ambayo inajidhihirisha kwa matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau na udhalilishaji wa kada mbalimbali za kijamii wakiwemo viongozi wa kitaifa inaonesha wazi kulenga katika kuigawa jamii na kufifisha amani, upendo, uzalendo na ustaarabu tuliokuwa nao watanzania.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa misingi ya Sanaa Duniani kote kazi zote za Sanaa zinapaswa ziwe ni zenye kuonya, kuelimisha, kuadabisha, kukosoa, kuburudisha, kuhamasisha na kuchochea maendeleo chanya katika jamii na siyo kuigawa au kuivuruga jamii.

Ndiyo maana msanii anayefanya kazi zake kwa kuzingatia misingi ya Sanaa anatambuliwa kuwa ni kioo cha jamii, kiongozi na pia ni mwalimu wa yale yote yaliyo mema katika jamii inayomzunguka.

Kinyume na misingi hiyo ya Sanaa, baadhi ya Wasanii, studio za kurekodia na kutengenezea muziki, vyombo vya habari vya kielektroniki na mitandao ya kijamii ama kwa kutumiwa au kwa utashi wao binafsi wamekuwa wakijihusisha na Sanaa zenye viashiria vya uchochezi na kuvunja misingi ya weledi katika Sanaa hususan katika kipindi hiki cha kampeni na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Aidha, baadhi ya Wasanii wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya vyama vya Siasa au wagombea na kujikuta wakitumiwa vibaya na kuvunja misingi ya Sanaa kwa faida za kisiasa. BASATA linapenda kutoa maagizo yafuatayo:
1.    Wasanii wana haki zote za kikatiba na kidemokrasia kushiriki shughuli za Siasa lakini wanawajibika kwa kiwango cha hali ya juu kulinda misingi ya weledi,  maadili, miiko na hadhi yao kama inavyofanyika katika tasnia zingine.

2.    Wasanii wanapaswa kutambua kwamba kuna maisha na Taifa baada ya uchaguzi mkuu. Umoja wa kitaifa na umoja baina ya wasanii wa kada zote za Sanaa ndiyo utakuwa msingi mkuu wa kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla pasipo kugawanyika katika misingi ya itikadi za kisiasa

3.    Wasanii wasitumie nafasi na umaarufu wao kuligawa taifa, kukashifu viongozi wa kitaifa, kudharau mamlaka, vyama na makundi mbalimbali katika jamii kwa kile kinachoitwa ushabiki wa kisiasa. Ieleweke kuwa Serikali haitafumbia macho wale wote watakovunja sheria, kanuni na taratibu. Tukumbuke kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria. 

4.    Ijulikane kuwa wasanii kama kundi muhimu katika kipindi cha kampeni za kisiasa ni sawa na watu wengine wanaopewa kazi ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Wasanii wasitumiwe kama vyombo tofauti na watu wengine.
BASATA linatoa onyo kali kwa msanii yeyote atakayeendelea kukaidi, kuvunja maadili na kusambaza kwa njia yoyote ile kazi ya Sanaa yenye ukengeufu wa maadili. 

BASATA linawatakia wasanii wote utekelezaji mwema wa maagizo haya lakini kubwa kuliko yote kutambua kwamba tunatakiwa kujenga mshikamano, umoja wa kitaifa na kustawisha amani tuliyonayo ambapo ikitoweka itaathiri ufanisi wa Wasanii na kuirejesha itatugharimu sana.
Sanaa itumike kulinda amani, kujenga upendo, umoja wa kitaifa na mshikamano baina ya makundi mbalimbali ya kijamii.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

DRFA YAZINDUA KOZI YA WIKI MBILI YA MKOCHA WA LESENI C’

$
0
0
CHAMA cha soka mkoa wa Dar es salaam, DRFA kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF,leo imezindua rasmi kozi ya ukocha wa leseni C’ inayotambuliwa na shirikisho la kandanda barani afrika CAF.
Kozi hiyo ya wiki mbili inaendeshwa na mkufunzi, Salum Madadi ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TFF,ikiwa na jumla ya washiriki 31 wengi wao wakiwemo makocha wa vilabu vya ligi daraja la pili,daraja la kwanza na ligi kuu.
Miongoni mwa washiriki hao ni pamoja na kocha msaidizi wa Simba,Suleiman Matola,katibu mkuu wa zamani wa Simba Muhina Kaduguda,kocha wa Ruvu shooting Tom Olaba,kocha wa makipa wa Yanga Juma Pondamali,nyota wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayai na Peter Tino.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi hiyo ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Tff,Msafiri Mgoy,ambaye amewapongeza washiriki kwa uamuzi wao wa kutaka kujiongezea maarifa ya ufundishaji wa soka ,kwa kuwa tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa makocha ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepiga hatua kisoka.
Aidha amesema TFF imeweka mpango maalum wa kutunza kumbukumbu za makocha hao na wengine watakaopatikana,pamoja na kufuatilia kazi zao kwenye vilabu mbalimbali watakavyofundisha ili iwe rahisi kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao.
Naye mwenyekiti wa DRFA,Almasi Kasongo wakati akimkaribisha mgeni rasmi,amesema chama chake kinataraji pia kuendesha kozi za madaktari pamoja na kuendeleza mpango wake wa kuinua soka la vijana,ili taifa liwe na wachezaji wenye uwezo wa kushindana na mataifa mengine.
Kasongo amesema licha ya chama chake kuwa na mikakati ya kuhakikisha soka la mkoa wa Dar es salaam na nchi kwa ujumla linanyanyuka,lakini bado nguvu kumbwa inahitajika kutoka TFF pamoja na wadau wenye mapenzi mema na mpira wa nchi hii.
 
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO YA DRFA,
Omary Katanga,
Mkuu wa habari na mawasiliano DRFA.

WASANII BONGO MOVIE WANOGESHA KAMPENI ZA MGOMBEA MWENZA CCM

$
0
0
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akisalimiana na baadhi ya viongozi na wananchi baada ya kuwasili katika eneo la mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani jana.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Kibaha Vijijini, akizungumza na wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
*Imeandaliwa/www.thehabari.com

UZINDUZI WA CHEZA KWA MADOIDO WAFANA DAR LIVE!

$
0
0
1.3.
Yamoto Band wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Yamoto Band, Enock Bella (wa kwanza kushoto) akifanya yake na Aslay (kulia).
4.Msanii Ruby akiwa stejini kufanya yake.
Msanii wa Bongo Fleva, Hellen George 'Ruby' akifanya yake stejini.
9.
...Ruby akiimba wimbo wake 'Na Yule'.
5.Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
Msanii wa Bongo Fleva,  Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
6.Shetta akikonga nyoyo za mashabiki wake.
Shetta akiendelea kuwapa burudani mashabiki zake.
7.Chegge na Temba mzuka ukiwa umewapanda stejini.
Chegge na Temba wakikamua stejini.
 
7
...Chege akiendeleza makamuzi.
10.Queen Dar leen akitoa burudani katika mashabiki wake.
Queen Darleen akitoa burudani kwa mashabiki wake.
8.
Makamuzi yakiendelea ndani ya Ukumbi wa Dar Live.
11.Mwimbaji wa Taarabu kutoka Bendi mpya ya Moyo Medern Taarab akiimba.
Mwimbaji wa Moyo Modern Taarab akiimba jukwaani.
12.Bebdi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.131415
Bendi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.
16.Mpiga kinanda wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
Mpiga kinanda  wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
17.Bonge la Nyau akionesha manjonjo.18.1920.
Madansa wakifanya yao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana usiku.
VIJANA wanaounda Bendi ya Yamoto, usiku wa kuamkia leo wameangusha burudani ya aina yake katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar wakati vijana hao wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido.

Kabla ya uzinduzi wa Cheza kwa Madoido, wasanii mbalimbali walipanda jukwaani kutoa burudani ikiwemo bendi mpya ya Taarab iitwayo  Moyo Modern Taarab inayomilikiwa na kiongozi wa Yamoto Band, Said Fela.
Wasanii mbalimbali wa chipukizi nao walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwa kuimba nyimbo mbalimbali ambapo wapenzi wa burudani waliburudika vya kutosha.

Katika listi ya wasani waliotumbuiza jukwaani ni pamoja na Ruby, Dulla Yeyo, Izeman huku Moyo Modern Taarab wakipagawisha na nyimbo zao kali zinazojulikana kama Haijalishi, Dongo la Gizani na Zetu Duwa.

Wengine waliokamua jukwaani ni Chegge, Temba, Queen Darleen, Shetta, Ditto na wengine kibao kisha uzinduzi wa Cheza kwa Madoido kufanyika katika ‘skrini’ kubwa kisha Yamoto Band kutumbuiza shoo kali.
(HABARI/ PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KUKAGUA NA KUKABIDHI MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA WA CHWAKA, UNGUJA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Chwaka, Unguja, wakati alipofika kutembelea kukagua na kukabidhi Mradi wa Maji safi na salama wa Chwaka, leo Sept 12, 2015.
 Msimamizi wa Mradi wa Maji safi na salama wa Chwaka, Malcom Nyanda, akizungumza kuelezea changamoto za mradi huo wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi mkuu wa Tanki la maji, Yohana Mkoloma, wakati alipotembelea kukagua Mradi wa Maji safi na Salama wa Chwaka, Unguja leo Sept 12, 2015.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka kukagua mradi wa Maji safi na salama baada ya kukabidhi mradi huo kwa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, leo Sept 12, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Chwaka baada ya kutembelea kukagua na kukabidhi mradi ya Maji safi na salama wa Chwaka, leo Sept 12, 2015 Unguja. Picha na OMR

KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA MH.LOWASSA MJINI SINGIDA LEO

$
0
0
Wananchi wa Mji wa Singida wakiishangilia Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, SINGIDA.
Wadau wa Singida wakitafuta namna ya kupata taswira ya Mgombea wao, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mabango yenye jumbe mbali mbali kwenye Mkutano huo.
Mkali wa Propaganda, Tambwe Hizza akisema yake kwenye Mkutano huo.

Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia wananchi wa mji wa Singida leo.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Lawrance Masha akionyesha Ilani ya Chama chao kwa Maelfu ya wananchi wa mji wa Singida, waliofurika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA wa Jimbo la Singida Mjini, Mgana Msindai "CRDB", katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
















































MAGUFULI AFANYA MIKUTANO YA KAMPENI WILAYA YA BUSEGA,BARIADI,ITILIMA NA MEATU MKOANI SIMIYU LEO.

$
0
0
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja wa  CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi
 Wananchi wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia
 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo
 Wananchi wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa akiwahutubia mjini Meatu jioni ya leo.Dkt Magufuli leo ametembelea wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia ya wakulima na wafugaji  hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.

Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.

"Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.

Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.

Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo.

 Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifautilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge na Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni  Mwanhunzi,mjini Meatu jioni ya leo mkoani Simiyu.
 Wakazi wa Lamadi ndani ndani ya wilaya ya Busega,Mkoani Simiyu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini humo leo.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Busega,Raphael Chegeni akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
 Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa Busega,mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.Dkt Magufuli aliwaomba wananchi hao kuitunza amani waliyonayo na kuwa kuwapuuza wale wote wenye maneno ya kuleta ufarakanishi katika nchi yetu
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkula,alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi hao akielekea Wilayani Busega kwenye mkutano wa hadhara.
 Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ndani ya uwanja wa CCM mjini Bariadi yalikuwa kama hivyo pichani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mwanhunzi,alipomaliza kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mjini Mwanhunzi,Wilayani Meatu mkoani Simiyu.

Taarifa za uongo kuhusu Rambirambi za Msiba wa Mama yake Aslay

$
0
0
Kuna mtu anatumia akaunti feki ya msanii wa Yamoto Band Enock Bella akiomba kutumiwa rambirambi ya msiba wa mama mzazi wa Aslay Isihaka Ambaye amefariki Dunia leo asubuhi.

Mtu huyo anatumia namba 0716281999 na amesajili kwa jina la Aslay Isihaka tunawaomba wadau na mashabiki wa Yamoto Band na Aslay wapuuze tariifa siyo za ukweli na hakuna utaratibu wa kutuma rambirambi katika simu.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images