Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 638 | 639 | (Page 640) | 641 | 642 | .... | 1897 | newer

  0 0

  1 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikiwete akiweka jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi linalomilikiwa na Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la Ngorongoro lililopo mjini Arusha jana jioni.
  unnamedMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Uhifadhi ya Bonde la Ngorongoro Balozi Mwanaidi Maajar akimkabidhi Rais Kikwete zawadi mbalimbali pamoja na pasi ya kudumu ya kuingia katika hifadhi ya Ngorongoro muda mfupi baada ya Rais Kuzindua ujenzi wa jengo la Kitega uchumi la Hifadhi hiyo mjini Arusha jana.
  e

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepokea vifaa mbalimbali vikiwemo vibanda vya kupigia kura (vituturi), masanduku ya kupigia kura, lakiri za kufungia masanduku pamoja na vifaaa vingine vitakavyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu nchini.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Ununuzina Ugavi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Eliud Njaila alipokuwa akiongea na waadishi wa habari wakati wa kupokea vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam.

   “Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha Watanzania na wadau wote wa uchaguzi kuwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu yamekamilika na vifaa vyote muhimu vya kuendeshea zoezi hilo vimekamilika” alisema Bw. Njaila.

  Akisisitiza juu ya gharama ya vifaa hivyo, Bw. Njaila alisema kuwa vifaa mbalimbali vya uchaguzi zikiwemo karatasi za kupigia kura vyote kwa ujumla vinathamani ya Sh. 41,868,045,168  bila kuweka gharama ya ununuzi wa mashine za BVR.

  Aidha, Bw. Njaila alisema kuwa vituturi vinaendelea kutengenezwa hapa nchini ambapo kila siku idadi ya vituturi 8000 vitakuwa vinakabidhiwa kwa kwa tume ya uchaguzi tayari kwa kusambazwa nchi nzima katika kila halmashauri kabla ya zoezi la kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu.

  Vifaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi vitasambazwa kwa kanda kuanzaia kanda ya Ziwa, kanda ya kati, kanda ya kusini, kanda ya magharibi, kanda ya nyanda za juu kusini, kanda ya kaskazini, kanda ya mashariki pamoja na Zanzibar kulingana na utaratibu uliowekwa na NEC na ZEC.

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli.

   Na Humphrey Pole Pole.
  Kumekuwa na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Dr. John Pombe Magufuli, kuibua na kuzungumzia mapungufu ya serikali ambayo yeye ni waziri. Baadhi ya watu wanaofuatilia kampeni zake wameenda mbali zaidi na kuhisi kuwa kwa kufanya hivyo, Magufuli anawafanyia kampeni labda bila yeye kujua wapinzani wake katika kinyang’anyiro cha Urais. 

  Bila shaka, kwa watu wenye mtizamo huo, kampeni za Magufuli zingekuwa zinatawaliwa na maneno yaliyoyajaa sifa nzuri za utendaji wa serikali na chama tawala. Kwa hiyo, kwa mtizamo huo, ni jambo la kushangaza kuona kuwa Magufuli anakosoa serikali aliyomo badala ya kuisifia na kuipamba majukwani. Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu wanasema kuwa Magufuli anazungumza kama vile anagombea kupitia vyama vya upinzani. 

  Maoni ya namna hii pia yamekuwa yakielekezwa kwa katibu mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahaman Kinana, ambaye katika shughuli zake za kisiasa za chama chake katika maeneo mbalimbali hapa nchini amesikika mara nyingi akiikosoa serikali ya chama ambacho yeye ni katibu mkuu. Watanzania watakumbuka kuwa Ndg. Kinana aliwahi kuwaita baadhi ya mawaziri wa serikali hii 'mizigo' na kutaka wawajibishwe kwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa ufanisi. Kwa baadhi ya watu Ndg.

   Kinana hakufanya vizuri kuikosoa serikali yake hadharani na hasa kwa kuongea kama mpinzani. Kitendo cha Magufuli na viongozi wa chama chake kuibua mapungufu na kuikosoa serikali yao hadharani inaonekana kama ni lugha ya wapinzani wa kisiasa. Hakika utamaduni huo ni sawa na kujikosoa mwenyewe. Hata hivyo, ili tuweze kuelewa kama kujikosoa ni jukumu pekee la vyama vya upinzani na wagombea wao, inabidi tujiruhusu kuelimishwa na maneno ya hekima aliyekuwa Rais na mpigania uhuru wa Guinea Bissau, kamarade, Amilcar Cabral ambaye alishawahi kusema kuwa kwa kiongozi au anayetaka kuwa kiongozi wa umma sharti awe na mwenendo wa kutoficha ukweli: Kwa maneno yake; "Hide nothing from the masses of our people.Tell no lies.Expose lies whenever they are told. Mask no difficulties, mistakes, failures. Claim no easy victories."

  Tafsiri yake ni kuwa, kiongozi asifiche chochote kwa wananchi. asiseme uongo, afichue uongo kila unapoibuka. Asifiche matatizo, makosa, mapungufu na kushindwa. Asijipe sifa nyepesi nyepesi.” Kutokana na hekima ya Amilcar Cabral ilivyoelezwa hapo juu, ni wazi kuwa anachofanya Magufuli ndicho haswa kinachotakiwa kufanyika. Kwa kufanya hivyo, Magufuli anaonyesha wazi kuwa anajua matatizo na mapungufu yaliyopo na badala ya kuyafunika na kuyapaka rangi anayaweka wazi. 


  Bahati nzuri Magufuli amekuwa akielezea namna atakavyoshughulikia hayo matatizo na mapungufu. Bahati nzuri tabia hii ya Magufuli siyo mpya. Watanzania watakumbuka kuwa hulka hii ya Magufuli ilijionyesha wakati hata alipokuwa waziri chini ya Rais Benjamin Mkapa alipoikosoa Ofisi yake hadharani kwa baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo kujimilikishia magari ya umma isivyo halali. Katika kipindi hiki cha kampeni, Magufuli amekuwa akitoa mapungufu ya serikali hata pale ambapo Rais Kikwete yupo.

  Sambamba na Amilcar Cabral, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuandika kitabu mwaka 1962 kiitwacho "Tujisahihishe" akitaka Watanzania na hasa viongozi wawe tayari muda wote kujisahihisha. Katika kitabu hicho Baba wa Taifa, alisema kuwa “makosa ni makosa bila kujali ni nani ameyafanya. Muhimu ni kuyajua makosa hayo na kujisahihisha.” Katika kitabu hicho, Mwalimu Nyerere aliendelea kusema;

  “Kujielimisha ni kujua ukweli wa mambo na kuwa na ujuzi wa sababu mbalimbali za mambo; na kama mambo hayo ni mabaya ni kujua jinsi ya kuyaondoa; na kama ni mema, jinsi ya kuyadumisha. Mpumbavu ni yule anayeyapa mambo sababu zisizo za kweli na kushauri dawa isiyo ya kweli katika kutafuta sababu za matatizo na jinsi ya kuyaondoa(Nyerere, 1962, 5).” Kwa maelezo hayo ya Baba wa Taifa, ni wazi kuwa Magufuli ameamua kuwa mkweli katika kampeni zake na ameepuka kuwa mpumbavu kama alivyobainisha Baba wa Taifa. 

  Kujikosoa anakofanya Magufuli kunadhihirisha aina ya Rais tunayemhitaji. Itakuwa ni hatari kubwa kuwa na Rais asiyetayari kujikosoa au kukosolewa. Ni janga kubwa kwa nchi kuwa na Rais ambaye anaamini kuwa yeye ni mtakatifu asiyekosea. Rais wa namna hiyo ni lazima atakuwa ni dikteta na watakodhubutu kumkosoa na kuibua makosa yake watakiona cha moto. Kama historia za nchi mbalimbali inavyoonyesha, hili likitokea, Tanzania itakuwa katika dhahama kubwa. 

  Maandiko ya vitabu vitakatifu yanatuelekeza kuwa ukamilifu wa binadamu huja kwa kusimama katika ukweli, kujikosoa na kukubali kukosolewa na kuepuka hadaa. Vivyo hivyo, ukamilifu na uhai wa taasisi zinazoundwa na binadamu kama vile vyama vya siasa na serikali lazima viwe na uthubutu wa kujikosoa na kukubali kukosolewa kama anavyofanya Magufuli.

  Kwa maelezo hayo hapo juu, ni ni wazi kuwa ukosoaji siyo jukumu pekee la vyama vya upinzani bali ni jukumu la kila mmoja hasa wale wanaotaka kuwa viongozi wetu. Hivyo, badala ya kumshangaa Magufuli kwa kubainisha makosa na mapungufu ya serikali ambayo yeye ni sehemu yake, tujielekeze katika kuwataka wagombea wengine katika nafasi mbalimbali waepuke hadaa na badala yake wafanye kampeni zao kwa kueleza ukweli. 

  Hadaa katika kampeni zitatupatia viongozi matapeli ambao bila shaka uongozi wao utakuwa wa hadaa kwa wananchi. Kinyume chake kiongozi mkweli na aliye na uthubutu wa kujikosoa anaonyesha kuwa ana uwezo wa kutafuta suluhisho la kweli la matatizo yaliyopo. 

  Kwa kuitimisha, Magufuli hajachemka katika kuikosoa serikali aliyomo bali, kwa kufanya hivyo, anaonyesha ufahamu wake wa hali halisi ilivyo. Zaidi, anaonyesha kuwa yeye ni mtu aliyetayari kusimamia ukweli jinsi ulivyo na hivyo ndivyo inapaswa kuwa.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel akitoa maelezo katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wakilipia tisheti kwa ajili ya sare ya kutambuana wakati wa safari ya kwenda katika vyuo vya China katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wanafunzi wakipata maelekekezo mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China.
  Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel akibadilisha nawazo na wazazi walifika na watoto wao wanaotarajia kwenda kusoma vyuo vya China.
  Wanafunzi wakiingia katika ofisi ya Global Education Link kupata maelezo mafunzo ya wanafaunzi wanaokwenda kusoma vyuo vya China. 
   
  Wanafunzi wakiabadilishana mawazo mara baada ya kumaliza mafunzo yao leo, yaliyoendeshwa na GEL.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link,Abdulmalik Mollel akizungumza na wafanyakazi wake mara baada ya kumaliza mafunzo ya wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China.
   (Picha na Emanuel Massaka). 

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Global Education Link (GEL) leo imeendesha mafunzo kwa wanafunzi wanaokwenda vyuo vya China kwa ajili ya kuanza safari na mazingira ambayo watayakuta katika vyuo hivyo. 

  Akizungumza na katika mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wanafunzi 70 jinsi ya kuanza safari ya masomo katika vyuo vya China wanaotarajia kuondoka Septemba 22 mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmaaliki Mollel amesema kuwa mafunzo hayo ni kuwaandaa wanafunzi jinsi ya kuanza safari yao kuanzia uwanja wa ndege hadi katika vyuo wanavyokwenda.

   Mollel aliwataka wazazi kuwa waangalifu na matumizi wanayopewa wakiwa vyuoni inapofikia inazidi inashawishi wanafunzi kufanya vitu visivyo na kuweza kufanya asiweze kupata elimu ambayo mzazi alikuwa anatarajia aipate huku nje.

   Katika Mafunzo hayo wanafunzi wamepewa nyaraka mbalimbali ambazo ni juu ya vyuo hivyo ambazo ni Chuo anachokwenda kuidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Taarifa za nyaraka zenye alama za vidole kutoka katika jeshi la polisi kuonyesha wanafunzi hao hawana makosa ya kijinai. 

   Amesema kuwa Global Education Link imekuwa ikifanya kwa niaba ya vyuo vya nje ambavyo vina ubora wa kutoa elimu iliyobora ambayo itakuwa na tija kwa taifa pamoja na yeye mwenyewe. 

   Hata hivyo aliwataka wazazi kuwaandaa mapema watoto wao wanaokwenda kusoma ili kuweza kuondokana na usumbufu ambao unaweza kufanya asiweze kwenda huku akiwa ameshalipa ada pamoja na tiketi ya safari. Aidha Mkuirugenzi Mtendaji amesema kuwa utaratibu wote wa kuondoka na kufika katika vyuo hivyo anafanya ikiwa ni sehemu ya kuondokana na usumbufu kutokana na wanafunzi hao baadhi ni wageni katika kusafiri na ndege. 

   Mollel amesema wanaokwenda kusoma nchini China wengi wao ni masomo ya uhandisi wa Mafuta,Ndege,Ujenzi pamoja na udakitari kwa elimu juu waliomaliza kidato cha sita.

   Amesema nafasi katika masomo ya elimu juu bado zipo wanachotakiwa ni nkufanya mchakato wa mawasiliano wa kuweza kudailiwa hili ni moja ya makundi ambapo mengine yalishaondoka. 

  Mollel amesema kuwa nafasi zipo katika vyuo vya nje kutokana kuendelea kufunguliwa kwa mawasiliano zaidi www.gel.co.tz na mawasilino ya simu ni+ 255 656 200 200. Aidha amewataka wazazi na wanafunzi kuacha kutumia baadhi ya watu walio katika nchi mbalimbali zenye vyuo kudai wao ndio wanajua ni uongo kwani Global Education Link ndio inaingia mikataba na vyuo vya nje na wengine hawajaingia mikataba.

   Kwa upande Mzazi Dk. Nicholas Eseko amsema mafunzo ni mazuri kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wakti kuanza safari pamoja na mazingira watayoyakuta katika vyuo hivyo. 

  Mwanafunzi Ismail Michael amesema kuwa mafunzo ni mazuri yanatoa mwanga wa kuanza safari ya kwenda katika vyuo hivyo vyenye ubora. “Sisi wanafunzi tunafarijika kwa kupata mwanga jinsi ya kuanza safari yetu na kujua vitu vibaya katika viwanja vya ndege ambavyo vinaweza ukafanya uwe uingie katika mikono ya dola”amesema Michael.

  0 0

  MUIMBAJI nguli wa muziki Afrika, Solly Mahlangu anatarajia kuwasha moto kwenye jukwaa la Tamasha la Amani ambalo litarajia kufanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama mwimbaji huyo ndiye atakayekoleza maombi ya amani ya Tanzania ambayo inapigiwa chapuo la kulindwa kila kukicha.
   
  Msama alisema hivi sasa Kamati yake inaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo ni chachu ya amani hasa kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 kwa nafasi za urais, Ubunge na Udiwani.
   
  Aidha Msama alisema Kamati yake inaendelea na mawasiliano na waimbaji wa nchi za Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Uingereza ambazo ni mojawapo ya nchi ambazo ni kichocheo cha  amani ya Tanzania.
   
  “Kwa kuwa tumejipanga kumpigia magoti Mungu ili kuilinda amani yetu, hatuna budi kuwashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali  sambamba na waimbaji ambao watakaoimba nyimbo ambazo zitachochea amani,” alisema Msama. 
   
  Msama alisema tamasha hilo litahudhuriwa na viongozi wa kada ya siasa ambao watakuwa ndio walengwa ambao wanatakiwa kutoa somo kwa vijana ambao wamejikita katika siasa bila ya kuwa na weledi wa siasa.“Tutakuwa na matukio mengi ambayo ni viashiria vya kuombea amani Tanzania ambako pia kutakuwa na tuzo maalum ambazo watakabidhiwa baadhi ya viongozi ambao mchango wao katika jamii,” alisema Msama.
  Mwisho     

  0 0

  Kikosi kazi cha Timu ya Mbeya City fc kikiongwozwa na Gorikipa mahiri Juma Kaseja katika picha waki mwomba Mwenyezi munu kabla ya kuanza Mtanange, ambapo Kagera Sugar iliibuka mshindi kwa kuitundika Mbeya City fc Gori Moja kwa bila (1,0) Dakika ya 41, Mchezaji Poul Ngaiyoma Jezi Nambari 8, Mgongoni kuipatia ushindi Timu ya Kagera Sugar katika Mechi ya Kwanza Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mtanange ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mtanange ukiendelea katika Uwanja wa Kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuri (1,0) Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.
  Juma Kaseja Jezi Nambari Moja Mgongoni akiwa makini Lango la Mbeya City katika Mtanange wa Mbeya City fc na Kagera Sugar, ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuli (1,0).
  Mashabiki wa Mbeya City fc wakishangilia katika Mtanange uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kagera moja huku Mbeya City fc Mama kajabwela Tumbo kamsokota Tumbaku Bilaaa..

  0 0

  Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka akimpatia maelekezo juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
  Vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vilivyowasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimuonyesha Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka moja ya vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kusaidia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015.
  Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni Kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw Kailima Ramadhani. 
   
  Serikali imeahidi kuipatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi fedha zote ambazo inazihitaji kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 25 mwaka huu kutoka vyanzo vyote vya mapata. Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka amesema hayo leo alipo itembelea Tume ya Tafifa ya Uchaguzi kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari. 

   "Changamoto ya kifedha ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa ikikabiliana nayo awali sasa haipo tena kwakuwa serikali imedhamiria kuipa NEC fedha zote ambazo inazihitaji katika kuhakikisha Uchaguzi mkuu unafanyika Octoba 25 mwaka huu. Fedha hizo zitatolewa kwa awamu, kutokana na ratiba ya tume ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa ambavyo vimeanza kuwasili , mafunzo kwa wasimamizi wa Uchaguzi na zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais. Vifaa vilivyo wasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na vitutuli[vibanda vya kupigia kura], mabango [yanayo onesha kituo cha kupigia kura.

  0 0


  Askari  wa usalama barabarani  wakionyesha kamera  ya  kisasa ya  kupima spidi
  Mkuu  wa mkoa Amina Masenza  kulia na Salima Asas katikati na katibu  tawala mkoa wa Iringa Ayubu Wamoja  wakitazama kifaa cha  kupima  ulevi  kwa madereva
  Bi Masenza na kamati ya  ulinzi na usalama mkoa  wakitazama gari la zima moto
  Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akijiandaa kuzima  moto
  Wahitimu wa mafunzo ya  boda  boda  wakipewa  vyeti vyao
  Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza katikati  akiwa na  viongozi  wengine wa mkoa wa Iringa 
  Maandamano  ya  askari  polisi kuelekea katika  maadhimisho  ya  wiki ya nenda kwa usalama
  Maadhimisho ya wiki ya  nenda  kwa  usalama mkoa  wa Iringa  leo
  Askari  wa FFU  wakiwa katika maadhimisho hayo  Viongozi  wa  jeshi la polisi na serikali ya mkoa  wa Iringa  pamoja na kamati ya  usalama  barabarani  wakipokea  maandamano hayo katikati ni mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
  Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza akiongoza kupokea maandamano leo
  Mkuu  wa mkoa  Amina Masenza akipata maelezo  katika banda la afya
  Mkuu wa mkoa Amina Masenza na mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani mkoa wa Iringa  Salim Asas wakitembelea banda ya askari  wa usalama barabarani


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa asisitiza jambo jana jioni  wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando na  wakipongezana mara baada ya kumaliza   jana jioni mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
  Picha namba 3367 ni Baadhi ya wanganga wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa katika  huo.

  Na Magreth Kinabo
   SERIKALI imewataka watendaji wote  afya  wa halmashauri ,mikoa wilaya  kusimamia suala la usafi wa mazingira ilikuizesha jamii kuepukana na matatizo ya milipuko ya magonjwa likiwemo suala la ugonjwa wa kipindupindu.
   
   Aidha Serikali pia imewataka watendaji hao, kuanzisha siku maalum ya usafi katika maeneo wanayotoka.
   
  Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.  
   
   
  “Ni lazima tuwe na utaratibu huu mpya kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)  vyombo vya habari ili kuweza kutatua tatizo hilo,” alisema Dkt. Mmbando.
   
   Aliongeza kwamba watendaji hao watakiwa kutoendelea kuruhusu vyakula kusafirishwa katika maeneo ya wazi, madimbwi ya maji machafu, usimamizi wa huduma za afya ufanyike ipasavyo.
   
  “ Tusimamie mpango wa utekelezaji wa elimu ya afya mashuleni, likiwemo suala la vyoo ambalo limepewa walimu maalum wa kusimamia ,hivyo zamani tulikuwa tunakaguliwa kuhusiana na usafi wa mwili mashule mafano kuoga nna kuchana nyewele pia  kuweka  yanayotunguzuka kuwa safi mazingira. Turudi katika misingi hiyo tuaondokana na matatizo ya afya,” alisisitiza.
   
   Dkt. Mmbando alisema kanuni na miongozi ipi ya kutosha hivyo, watendaji hao wanapaswa kuongeza kasi ya utendaji kazi na kushirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na kuambukiza ili kuweza kuiwezesha sekta ya afya kupata mafanikio makubwea zaidi katika kufikia malengo ya milinea(MDG’s ).
   
    Aliongeza kwamba Mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu umetokea katika mikoa ya Dares Salaam, Morogoro na Pwani  na unatokana na tatizo la kutozingatia , misingi ya usafi wa mazingira   husasan kwenye vinywaji, vyakula na mazingira yasiyosafi.

  0 0

  lemonMo Lemon Mint imefika hadi Santorini, Greece! Umeifikisha wapi Mo soda yako kutoka hapo Dar? Tutumie picha yako 'smile emoticon' ikichaguliwa tutaiweka kwenye ukurasa wetu wa facebook.
  Na Andrew Chale, modewjiblog
  Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL GROUP), imeendelea kufanya vizuri sokoni kupitia upande wa vinywaji vyake mbalimbali vikiwemo: MO Cola, MO Portello na, MO Malt, MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).

  Kupitia ukurasa wa Facebook wa MeTL GROUP, (https://www.facebook.com/MeTLGroup) wamebainisha kuwa kampuni hiyo yenye kauli mbiu ya ‘The People’s Brand’, imeendelea kuwa karibu na wateja wao ilikuweza kushirikisha mawazo mbalimbali katika kufikia malengo ya kimaisha.

  Mbali na kushirikishana mawazo hayo na wateja wao waliopo kwenye ukurusa huo maalum wa facebook, pia imeweza kutoa elimu na namna ya hatua za kufuatwa kwa watu ikiwemo mazoezi, vyakula vinavyofaa kuliwa na mambo mengine.

  Pia kupitia ukurasa huo wa facebook, wateja wameombwa kutuma picha zao wakiwa na vinywaji kutoka MeTL GROUP, ikiwemo MO Bomba, MO Cola, MO Lemon Mint, MO Portello, Mo Embe, MO Chungwa nakisha kutuma katika ukurasa huo na 'Ku-SHARE'. Huku wakitakiwa kupiga picha na kinywaji hicho na kueleza mahala walipo!
  mo caHuwezi kujua ukiwezacho mpaka umejaribuUsikateTamaa‬

   Ndoto yako ni nini..Ndoto yako ni nini?
  mo boa
  mmo
  Vitu vya kuzingatia na kuchukua unapoenda kufanya mazoezi ya viungo...mpango mzima na MO Bomba iwepo kukuongezea nguvu na kukuweka na nguvu zaidi..
  pote
  Mchezaji bora wa Basketball MICHAEL JORDAN hakuchaguliwa kwenye timu ya basketball kwenye shule yake ya Sekondari kwasababu alikuwa mfupi kuliko wenzake. ‪#‎UsikateTamaa‬

  0 0

  Na Beatrice Lyimo – Maelezo
  12/09/2015
   SERIKALI imewataka Serikali imetoa  changamoto kwa watendaji wote  afya  wa halmashauri ,mikoa wilaya kuhakikisha wanabuni mbinu mpya na  kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kuendelea kuboresha huduma za sekta ya afya nchini.
   
  Aidha Serikali pia imewataka watendaji wa Idara ya Ustawi wa Jamii, kujumuisha suala la kutatua tatizo la watoto yatima kwa kuweka  katika mipango  ya sekta hiyo.
   
   Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.  
   
  “Kila mmoja  anapaswa kusimamia vyanzo vya mapato, misaada na bajeti ya Serikali haikidhi mahitaji kwa asilimia 100. Tunapaswa kusimamia kwa ukamini na ukamilifu suala la mapato katika vituo vya afya. Tusipotekeleza wajibu wetu ipasavyo tutawajibika kwa hili tutawajibika kwa Watanzania na hata kwa Mwenyezi Mungu,” alisema Dkt. Mmbando.
   
   Aliongeza kwamba hili kuweza kufanikiwa   vema katika masuala hayo wanapaswa kuwa makini katika kutoa maelekezo kwa kuzingatia sera, taratibu, miongozo na mikakati rasmi  ya Sera ya Afya ya mwaka 2007.
   Aliwataka watendaji hao, kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kuwasiliana na uongozi wa wizara.Pia kutumia uzoefu walioupta katika mkutano huo.  
     
  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa alisema watendaji hao kuongeza kasi ya utendaji kazi ili kuweza kukabiliana na matatizo ya sekta ya afya nchinina kufanikisha malengo ya milinea(MDG’s), mkakati wa awamu ya nne wa afya, kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na mamawajawazito, kutoa elimu juu ya masuala ya lishe kwa jamii.

  0 0

   Naibu Gavana wa Benki Kuu Nchini (BOT), Natu Mwamba akizungumza katika mahafali ya 17 ya Tanzania Institute of Bankers yalifanyika jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mhitimu wa Cheti ya Cha Juu katika Masuala ya Benki,Yahya Kiyabo akitunukiwa cheti na   Naibu Gavana wa Benki Kuu Nchini (BOT), Natu Mwamba  wakati mahafali ya 17 ya Tanzania Institute of Bankers yalifanyika jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Naibu Gavana wa Benki Kuu Nchini (BOT), Dk.Natu Mwamba akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kozi za juu katika masuala ya benki katika mahafali ya 17 ya Tanzania Institute of Bankers yalifanyika jana katika viwanja vaya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   (Picha na Emmanuel Massaka  Globu ya jamii)

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi ya gari Mkuu wa Majeshi wa kwanza Mzalendo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wakatiu wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi katicha chuo cha Momduli jana.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.Jenerali Sarakikya amekabidhiwa zawadi hiyo kwa kutambua mchango wake mkubwa kwa kujenga misingi imara ya jeshi la Wananchi wa Tanzania lenye weledi na nidhamu ya hali ya juu(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo Benki Kuu, Bw. Bernard Dadi (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza rasmi mabenki kufanya kazi kwa muda wa nyongeza kuwawezesha wateja wa bandari na wadau wengine kufanya malipo hadi saa 2 usiku kwa siku za kazi na saa 8 kwa siku za mwisho wa wiki na sikukuu.  Wengine ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (wa pili kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire (wa pili kulia) na Kamishna wa Forodha wa TRA, Bw. Tiagi Kabisi (kulia). Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ufanisi bandari hiyo.
   Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akielezea jambo kwa kundi la waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo kuona maendeleo ya utekelezwaji wa miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa Matokeo Makubwa Sasa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika, miradi hiyo itaongeza uwezo na ufanisi wa bandari hiyo.
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo Benki Kuu, Bw. Bernard Dadi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza rasmi mabenki kufanya kazi kwa muda wa nyongeza kuwawezesha wateja wa bandari na wadau wengine kufanya malipo hadi saa 2 usiku kwa siku za kazi na saa 8 kwa siku za mwisho wa wiki na sikukuu.  Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ufanisi bandari hiyo.

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeelezea kuridhishwa kwake na uamuzi wa serikali kuruhusu rasmi nyongeza ya muda wa kufanya kazi kwa benki hapa nchini na kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam.

  Hatua hii inakuja baada ya serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuruhusu kutumika kwa mfumo wa huduma baina ya taasisi za kibenki (TISS) hadi saa 2 usiku na hivyo kuwezesha wateja kufanya malipo na kuendelea na taratibu nyingine katika bandari hiyo bila tatizo.

  Mfumo huo umeunganishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha ili kuwezesha malipo mbalimbali kama kodi kuweza kulipwa katika muda huo wa nyongeza.

  Kaimu Meneja wa bandari hiyo, Bw. Hebel Mhango amesema jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa mfumo huo utaisaidia mamlaka hiyo na wadau wengine kwa kiwango kikubwa kwa kuwa utasaidia kuendana na mpango ulioanzishwa bandarini wa kufanya kazi kwa saa 24.  

  Aliwakumbusha watumiaji wa bandari hasa wakala wa mizigo kuwa mfumo huo mpya unalenga kuwasaidia kuokoa muda, gharama na hivyo kuongeza ufanisi katika biashara zao.

  “Tunaomba sasa wadau wengine wajitahidi kuendana na kasi ya bandari kwa kufanya pia kazi kwa muda wa saa 24. Tutaendelea kuhamasisha wadau wetu kuhusiana na mfumo huu mpya,” alisema.

  Akizungumza awali, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire alisema serikali imeamua kuongezamuda wa utendaji kazi kwa mabenki ili kuruhusu wateja na wadau kulipia kodi zao hadi saa 2 usiku.

  Alisema mbali na utekelezaji wa mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya uchukuzi, hatua hiyo pia itarahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali na huduma ya mizigo.

  Kwa mujibu wa takwimu, muda wa miezi sita ya majaribio iliyopita, mfumo huo umeonyesha mafanikio makubwa.

  “Miezi 6 ya kipindi cha majaribio ya mfumo huu, jumla ya miamala 7,727 yenye thamani ya Tshs 382 bilioni ilifanyika,” alisema.

  Alisema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya BRN katika kuifanya bandari kuwa kivutio cha nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

  “Wadau wote wa bandari watumie fursa hii kuleta ufanisi katika kazi zao,” alisema.

  Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo BoT, Bw. Bernard Dadi alisema benki hiyo imeruhusu malipo kufanyika hadi saa 2 usiku kwa siku za kazi na kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana mwisho wa wiki na siku za sikukuu.

  “Ni vyema benki zikazingatia muda huu mpya badala ya ule zamani ambapo malipo kama hayo yalirusiwa kufanyika hadi saa 7 mchana,” alisema.

  Kamishna wa Forodha wa TRA, Bw. Tiagi Kabisi alisema mamlaka hiyo inakubaliana na muda huo wa nyongeza kwani utasaidia katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.

  “TRA pia imeongeza masaa ya kuhudumia wateja wake ili kuendana na kasi ya maboresho ya bandari yanayoendelea,” alisema.

  0 0


  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mkangara leo Jumapili, Septemba 13, 2015 saa 8 kamili mchana anatarajiwa kuzindua rasmi fainali za michuano ya Airtel Rising Star katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

  Jumla ya timu sita zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambayo imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, ambapo vijana wenye vipaji huchaguliwa na kupata nafasi ya kujiunga na vituo vya michezo (Academy) za Dakara – Senegal na Doha – Qutar zinazomilikiwa na kampuni hiyo.

  Katika uzinduzi huo wa leo, timu za mkoa wa Ilala, Kinondoni, Mbeya, Morogoro, Mwanza na Temeke zinatarajiwa kupambana kusaka mshindi kwa fainali hizo za kitaifa

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  UFAFANUZI WA TANGAZO LILILOTOLEWA TAREHE 11 SEPTEMBA, 2015
  KUHUSU VIPINDI VINAVYORUSHWA MOJA KWA MOJA WAKATI WA
  KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU

   
  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusutangazo lake lililotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 11 Septemba, 2015kuhusu vipindi vinavyorushwa moja kwa moja wakati wa kampeni za uchaguzi
  mkuu. 
   Ufafanuzi huu unatolewa kutokana na maoni mbalimbali ya wadau
  wakitaka ufafanuzi kuhusu tangazo hilo.
  Mamlaka inatoa ufafanuzi kama ifuatayo:-
  a) Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa
  Vyama vya Siasa), 2015 ni Kanuni mbayo ipo kwa mujibu wa Sheria kama
  ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi
  zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na
  uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu;
  b) Wadau wa sekta ya utangazaji walishirikishwa katika maandalizi ya Kanunihizi wakiwemo vituo vya utangazaji tarehe 28 Oktoba, 2014, Mitandao ya  kijamii tarehe 11 Novemba, 2014, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni naMichezo tarehe 19 Desemba, 2014 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe14 Aprili, 2015;
  c) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inasisitiza kuwa vyombo vinavyotoa
  huduma ya utangazaji vina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu
  uchaguzi bila ubaguzi ili wananchi wenyewe waelimike na hatimaye
  wafanye maamuzi sahihi kwa hiari yao kuchagua kiongozi anayefaa;
  d) Mamlaka inafafanua na kusisitiza kuwa vyombo vya utangazaji
  vinakumbushwa kuzingatia Kanuni za Huduma za Utangazaji
  ISO 9001:2008 CERTIFIED

  (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015,
  hususani Kanuni zifuatazo;-
  4. Kila mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba:-
  (f) haruhusu utangazaji wa jambo lolote linalohamakisha na
  kuwagawa watu katika hali ya uchochezi;
  (h) Utangazaji wa chaguzi unadhamiria kusisitiza ustahiki wa chaguzi
  na kuhimiza ushiriki wa wananchi wote katika mchakato wa uchaguzi;
  (i) wakati wa kipindi cha chaguzi habari zilenge juu ya masuala
  muhimu na yenye maslahi kwa wananchi sio tu kutangaza matukio ya
  vyama vya siasa au wagombea;
  5. Kila mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba vipindi na
  uwasilishaji wake:-
  (b) haujihusishi na kumkashifu au kumuumbua mgombea au mtu
  mwingine yeyote au kauli mbaya juu ya uadilifu wa mtu;
  (d) kipindi kisiwe na lugha ya kashfa, chuki au kufuru au lugha
  yoyote (au toni ya lugha) inayoweza kuchochea vurugu au maasi;
  (e ) kipindi kisiwe na kauli zinazoweza kumuudhi mtu yeyote kwa
  sababu ya jinsia, jinsi, mbari, rangi, tabaka, imani au mahali pa asili.
  (f) matangazo ya vyama vya siasa yatakuwa yale tu ambamo vyama
  vinajitahidi kuelezea sera, mipango na malengo yake.
  Hivyo basi, haikuwa lengo la taarifa hiyo kumzuia mtu yoyote kushiriki vipindi vyamoja kwa moja (live Programmes) iwapo Kanuni zilizotajwa hapo juu zitafuatwana kuzingatiwa.
  Vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za
  Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 nakwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazoya moja kwa moja ambayo hayatozingatia Kanuni.
  Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi yakihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa kwa maslahi ya Taifa.
  IMETOLEWA NA:
  MKURUGENZI MKUU
  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
  TAREHE 13/09/2015

  0 0

   Mufti Mkuu wa TanzaniaShekh, Abu Bakari Zuberi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya  kutokea kwa tukio la ajali ya kuanguka kwa mashine ya ujenzi na kuangukia Jengo la Msikiti wa Makka nchini Saudi Arabia na kusababisha vifo vya watu mbalimbali.
  Mufti Mkuu wa Tanzania. Shekh, Abu Bakari Zuberi (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani leo Jijini Dar es Salaam.
  ( Picha na Emmanuel Massaka)

  0 0

   Mwakilishi wa Mkurugenzi  Mkuu wa (NHIF),Mkurungenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani akizungumza na waandishi wahabari hawapo pichani juu ya wanamichezo  kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kujipatia huduma za matibabu pamoja na dawa kwa vitio vya  Afya maluumu na Maduka ya dawa Malum ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkurunge wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Eugen Mikongoti akifafanua jambo kwa wanahabar.
   Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mkurugezi wa Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii (CHF) Eugen Mikongoti, leo Jijini Dar es Salaam.
   Mwakilishi wa Mkurugenzi  Mkuu wa (NHIF), Mkurungenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani akifafanua jambo leo Jijini Dar es Salaam.
  Wanahabari wakichagia juu ya kuwahamasisha wanamichezo kujiunga na mfuko huo  katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 09/13/15--08:46: UVCCM YAMVAA MAALIM SEIF.
 • UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi umemtaka Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad kuacha kuupotosha umma na kubeza mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Rais Dk Ali Mohamed Shein.
   
  Imemtaka awe muungwana na msemakweli kuhusu mafanikio yaliyofikiwa ingawa yeye binafsi na chama chake wamekuwa wakichukia hilo.
  Pia imemtaka kutoudanganya umma kwa madai atamudu kuwapa ajira vijana Wanzibari wote katika kipindi kifupi endapo atachaguliwa kuwa Rais.

  Taarifa ya UVCCM kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka jana ilisema Seif ni kiongozi kigeugeu ambaye hupenda kuudanganya umma na kusema serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar imeshindwa kufikia yake maendeleo yake katika kipindi tangu iundwe miaka mitano iliopita.
   
  Shaka alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)  huongwazwa kwa pamoja kati ya CUF na CCM hivyo madai anayotoa Seif hivi sasa yanalenga kuupotosha umma na kuficha ukweli.
   
  “Nichukue nafasi hii kuwaeleza wananchi  Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya  Dk.  Shein huongozwa kwa pamoja  kisera  na mawaziri toka CCM na CUF seif akiwa makamu wa kwanza wa Rais. Uamuzi, ushauri na utekelezaji sera na pamoja na mikakati hupitishwa na kutekelezwa katika Baraza la Mapinduzi ambalo Seif pia hushiriki na kushauri ” alisema shaka.
   
  Kwa mujibu wa Shaka, serikali ya CCM imetekeleza majukumu yake kazi kwa Wazanzibari kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo ya kisekta ikiwemo kukuza uchumi, afya , miundombinu ,  utalii na elimu.
   
  Alisema serikali ya CCM chini ya Dk. Shein imepandisha bei ya karafuu zao ambalo ni tegemeo kubwa la kiuchumi kwa Wanzibari wengi.
   
  Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwaomba Wazanzibari kuwa makini na wanasiasa aina ya Maalim Seif kwa wamekuwa na ndimi mbili zinazomfanya ashindwe kusifu mema hata pale ukweli unapodhihiri.

  “Seif akumbuke hisani pia awe na shukran  bila  kubeza mafanikio ya  SUK  ati imeshindwa kufikia malengo yake, huo ni uongo na uzushi wa  Maalim Seif ambaye amekuwa akisaka  urais wa Zanzibar bila mafanikio tangu mwaka 1984 alipoanza  kushindana  na marehemu mzee idris abdul wakil huku kushindwa mara nne kufikia lengo lake  nje ya ccm .
   
  “Hivi kwa akili ya kawaida mtu unayeshirikiana naye katika utekelezaji na uendeshaji serikali mwenye wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais kama  Maalim Seif ndani ya SUK, anawezeje kuwa mdanganyifu na kuyapa kisogo mafanikio yaliyopatikana chini ya Dk. Shain.

  “Ikumbukwe  serilali inayoongozwa na Dk. Shein ndiyo iliyopandisha bei ya zao la karafuu, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zinanazofika hadi katika kijiji ambacho Maalim Seif anadai amezaliwa huko Mtambwe ikiwemo kuondoa tatizo la usafiri wa Pemba na Unguja baada ya serikali kununua meli ya kisiasa ambayo iko njini kufika Zanzibar wakati wowote huku uchumi ukikua kwa kasi ya asilimia 7,” alihoji Shaka.

  Mbali na hayo, Shaka alisema chini ya uongozi wa Dk. Shein serikali yake  imefanikiwa kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma mara tatu katika kipindi cha miaka mitano jambo ambalo alisema ni mafanikio makubwa katika kuimarisha huduma za maendeleo ya jamii 
  “Serikali humudu kumsafirisha Maalim Seif nje ya nchi mara tatu kwa ajili ya kupata matibabu  tangu afya yake ilipoanza kuzorota, Bila uchumi kuimarika smz  isingeweza kubeba gharama hizo” alisema  shaka.

  Aidha Uvccm  imemuonya aliyekuwa waziri katika  smz mansour Yussuf Himid kucha mara moja kutumia msamiati wa mapinduzi daima katika jukwaa la cuf kwasababu mapinduzi hayo hayana asili na cuf wala hizbu 8liokuwa ikipingana na ASP  kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka  1964.
   
  "Tunamtaka Mansour aache kutumia neno mapinduzi katika mikutano ya cuf, mapinduzi ya zbr hayana mnasaba wala uhusiano na cuf au ZNP iliongozwa na Ali Mohsin Albarwan, baba yake mansour brigedia Yussuf Himid kama ungetokea muujiza wa kufuka leo angeshangaa kumona kijana wake akishiriki katika njama za usaliti wa kutaka kufuta mapinduzi aliyoyapigania kwa nguvu zake na kujitolea  kwa nchi  yake kuleta ukombozi"alisema kaimu huyo katibu mkuu .
   
  Shaka alimtaka mansour asifikiri kama wazanzibari ni wajinga na hawajui israf na ufujaji alioifanya akiwa serikalini alipokabidhiwa dhamana ya uongozi na sasa ametajirika.

older | 1 | .... | 638 | 639 | (Page 640) | 641 | 642 | .... | 1897 | newer