Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 634 | 635 | (Page 636) | 637 | 638 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mwalimu Hasani Gigoro akitoa mafunzo ya Dance kwa ajili ya mazoezi ya kupunguza kitambi na kupunguza unene  mazoezi hayo ambayohufanyika kila siku ya juma tatu kuazia saa kumi na mbili jioni, mpaka saa mbili usiku  kujiunga na mazoezi hayo ya dance kiingilio ni Tsh 5000/=  mazoeo hufanyika katika viwanja vya Mzalendo Pub Kijitonyama leo Jijini Dar es Salaam.

  Mazoezi ya viungo ya kudensi yakiendelea kwa umakini wa hali ya juu.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha Omary Kwaang’ (katikati mwenye kaunda suti) akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo, akikagua lambo la maji eneo la Endesh, linalotumiwa na mifugo na binadamu, lililogharimu sh169 milioni kwa ufadhili wa shirika la World Vision. 
   Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha Omary Kwaang’ (kushoto) akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo, akikagua lambo la maji eneo la Endesh, linalotumiwa na mifugo na binadamu, lililogharimu sh169 milioni kwa ufadhili wa shirika la World Vision.
   
  WANANCHI 12,082 wa Kata ya Baray Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamekabidhiwa miradi nane ya elimu na afya ambayo imegharimu sh447.8 milioni kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la World Vision Korea.
   
  Mratibu wa mradi wa World vision Karatu John Massenza akikabidhi jana miradi hiyo kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo John Mabula alisema  itawanufaika wakazi wa vijiji vitatu vya Dumbachang, Mbuga Nyekundu na Jobaj.
   
   
  Massenza alitaja miradi hiyo kuwa ni madarasa matatu, ofisi ya walimu na choo cha wanafunzi ya shule ya msingi Mbuyuni iliyogharimu sh83 milioni na madawati 200 kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo iliyogharimu sh13 milioni.
   
  Alitaja mingine ni samani na vifaa zahanati ya Endesh sh11 milioni, madawati 100 ya shule ya msingi Mohedagew Gidamilanda sh13 milioni na vifaa vya vikundi 11 vya hisa vijiji vya Dumbecha, Jobaj na Mbuga Nyekundu sh5 milioni.
   
  “Mingine ni lambo kwa matumizi ya binadamu na wanyama sh169 milioni, zahanati na choo Endesh sh83 milioni, vitabu na vifaa vya ufundishaji 1,570 vya sh11 milioni na madarasa mawili sh53.9 Endesh,” alisema Massenza.  
   
  Alisema katika wilaya hiyo, World vision ilianza kufanya shughuli zake mwaka 2009 kwenye tarafa za Endabash na Lake Eyasi ambapo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta tofauti.
   
  “Miradi hiyo iliyotekelezwa ni ya upande wa sekta ya elimu, afya, kilimo, maji na ufadhili wa watoto kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Karatu na wana jamii wa eneo hili,” alisema Massenza.
   
  Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Karatu Omary Kwaang’ alipongeza shirika la World vision kwa kufanikisha ujenzi wa miradi hiyo ya thamani ya sh447.8 milioni ambayo itanufaisha jamii ya wafugaji na wakulima.
   
  Kwaang’ aliwataka wananchi wa kata hiyo kuhakikisha kuwa wanaitunza miradi hiyo ili iwe endelevu na kudumu kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho, kwani shirika la World vision limetumia gharama kubwa kufanikisha miradi hiyo.
   
  Alisema kwenye suala la zahanati wilaya ya Karatu imepiga hatua kwenye kutekeleza sera ya wizara ya afya inayotaka kila kijiji kiwe na zahanati kwani wamejenga zahanati kwenye vijiji 45kati vijiji 58 hivyo vimebaki vijiji 13.
   
  “Nawapongeza viongozi na wananchi wa wilaya ya Karatu kwa kupiga hatua kwenye ujenzi wa zahanati, ila tujitahidi kwenye elimu kwani vyumba vya madarasa vinahitajika 1,109 na vilivyopo ni 875,” alisema Kwaang’.
   
  Alisema kwenye ujenzi wa nyumba za walimu kuna hitajika 694 na zilizopo ni 578 na matundu ya choo yanahitajika 1,221 na pungufu ni matundu 975 hivyo wajitahidi kumalizia mapungufu yote wakishirikiana na serikali ya wilaya hiyo.

  0 0

   Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
   Mkimbizi kutoka Burundi akipata huduma ya maji katika moja ya vituo vya maji vilivyojengwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.  Huduma za maji safi na salama ni mojawapo ya mambo yanayotiliwa mkazo ili kulinda afya za wakimbizi.
  Wakimbizi kutoka nchini Burundi  walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
  PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.\

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCH
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  IDADI YA WAKIMBIZI WA BURUNDI WANAOHIFADHIWA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU YAONGEZEKA
  Idadi ya wakimbizi kutoka Burundi wanaokimbia nchi yao na kuingia nchini Tanzania imefikia 91,661 kwa takwimu za Jumanne, tarehe 08 Septemba, 2015.  Wakimbizi hawa kwa sasa wamehifadhiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

  Tangu waanze kuingia mwezi Aprili mwaka huu, Wizara ya Mambo ya Ndani  ya nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine imekuwa ikiwapokea na kuwapa hifadhi na huduma nyingine muhimu.  Huduma hizi ni pamoja na za ulinzi, chakula, maji, elimu na afya.

  Kutokana na kuboreshwa kwa huduma za ulinzi, hali ya ulinzi na usalama katika kambi ya Nyarugusu na maeneo yanayoizunguka imeimarika ambapo upo usalama wa kutosha. Kazi hii inafanywa na Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi vinavyojumuisha baadhi ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hii.

  Kuhusu huduma za afya, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kama vile Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) imeimarisha huduma hizo kwa kuongeza idadi ya watendaji, vifaa na dawa.

   Kuimarishwa kwa huduma za afya kumesaidia kudhibiti magonjwa ya mlipuko na kukabiliana na magonjwa mengine yasiyo ya mlipuko.  
   


   Upatikanaji wa maji safi na salama na kutolewa kwa elimu ya usafi wa mazingira pia umesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti magonjwa ya mlipuko.
  Wakati huohuo huduma za elimu zimeimarishwa ambapo kiasi cha wanafunzi 3,889 wa elimu ya msingi na sekondari waliokuja na wazazi wao kutoka Burundi wameandikishwa na wanaendelea na masomo.

  Kabla ya kufikia idadi hii ya sasa, wengi wa wakimbizi hawa walianza kuingia kwa maelfu kupitia kijiji c,,ha Kagunga kilichopo mpakani na nchi ya Burundi ambapo idadi ilianza kupungua kidogo kidogo lakini kwa siku za hizi karibuni wakimbizi hawa wameendelea kuingilia wakiwa katika vikundi vidogovidogo kupitia katika vijiji vingine vya mpakani na nchi ya Burundi.

  Vijiji hivyo ni pamoja na Kilelema, Kitanga, Helushingo, Migongo,na Kigadie vilivyopo wilayani Kasulu na Mabamba na Katanga wilayani Kibondo na Kituo kidogo cha Uhamiaji cha Manyovu kilichopo mpakani na nchi ya Burundi.  

   Aidha wakimbizi wengine wamekuwa wakipitia vijiji vya Bugarama, Kabanga na Kasange vilivyopo wilayani Ngara mkoani Kagera.
  Wakimbizi hawa ambao wamekuwa wakipokelewa katika maeneo haya wamekuwa wakisajiliwa na hatimaye kusafirishwa hadi kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu ambapo kambi hiyo imekuwa ikipokea wastani wa wakimbizi mia mbili (200) kwa siku.

  Hata hivyo kutokana na msongamano katika kambi hiyo ya Nyarugusu ambayo awali ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kuhifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine ina mpango wa kuwahamisha wakimbizi hawa kutoka Burundi kwenda kwenye maeneo mengine.

  Maeneo hayo ambayo yameshaanza kufanyiwa maandalizi ni Mtendeli na Karago wilayani Kakonko na Nduta wilayani Kibondo. Zoezi la kuwahamisha wakimbizi hawa kutoka Burundi linatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

  Kuhamishwa kwa wakimbizi hawa kutoka Burundi kutaondoa msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu ambayo itaendelea kuhifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  IMETOLEWA NA:
  Isaac J. Nantanga
  (0754 484286)
  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Nyarugusu - KIGOMA

  0 0

   Mtoto Baraka Dombeni, akiwa na mama yake Bizimana Violet, akivishwa alama ya utambuzi muda mfupi baada ya kuwasili jana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, akitokea Wilaya ya Makamba nchini Burundi. Alama hii ni utambulisho wa kuwawezesha wakimbizi wanaofika katika kambi ya Nyarugusu kuandikishwa rasmi kabla ya kupewa hifadhi kambini hapo.
   Afisa Msajili Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi (UNHCR), Awadhi Nyanda akichukua taarifa toka kwa familia mojawapo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuingia nchini  kuomba hifadhi.  Wakimbizi hawa wanahifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kogoma.
   Mkimbizi  kutoka Burundi, Sindaye Salvatory akiwa na wenzake, akiwekewa alama yake ya utambulisho, wakati walipowasili katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu jana, wakitokea nchini Burundi kuja kuomba hifadhi nchini Tanzania kutokana na hali ya kisiasa nchini mwao.
   
   Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, Vivian Vianney akimchukua alama za vidole mkimbizi kutoka nchini Burundi Bw. Gwasa Jeremia ambaye ni mmojawapo ya raia wa Burundi wanaoendelea kuingia nchini kuomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
   Maofisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wanaohusika na usajili wa wakimbizi wanaopokelewa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarutgusu, wakiwa katika picha ya pamoja katika Kambi hiyo iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
   Mwakilishi wa Shirika la OXFAM toka nchini Ireland, Michaelo Riorpan akisaini kitabu cha wageni alipowasili na wenzake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu jana.  Shirika la OXFAM linatoa misaada mbalimbali kusaidia utoaji wa huduma za maji na utunzaji wa mazingira katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.  Aliyesimama ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B) Bw. Fredrick Nisajile ambaye aliupokea ugeni huo.

  Mkimbizi kutoka Burundi akipata huduma ya maji katika moja ya vituo vya maji vilivyojengwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.  Huduma za maji safi na salama ni mojawapo ya mambo yanayotiliwa mkazo ili kulinda afya za wakimbizi.
   (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)


  0 0

   Askali wa usalama barabarani akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya za msingi jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wakiwa navyeti walivyo tunukiwa mara baada ya kupata mafunzo ya usalama barabarani jijini Dar es Salaam.
   

  Na Tom Bishop.
  KAMPUNI  ya Mafuta ya Tatal  Tanzania imedhamini mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam.
   
  Udhamini wa mafunzo hayo yamegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 20,000 kupeleka kwenye mradi wake wa elimu ya usalama barabarani.
  Tatal   imekuwa ikidhamini mafunzo ya Usalama barabarani kila mwaka  kutokana na  kutenga  bajeti hiyo kwa ajili ya mafunzo hayo.
   
  Utengaji huo wanatumia Boksi la Usalama barabrani ambao ni mradi wa  kuendelea kwa kipindi cha miaka 10 na utakuwa ukitolewa nchi nzima, kwa maeneo yenye kiwango kikubwa cha hatari za ajali kwa wanafunzi.
   
  Mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 150,000 wamefundishwa juu ya usalama barabarani katika jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.
   
   
   Boksi la usalama barabarani lina alama za barabarani, maelekezo ya elimu ya usalama barabarani kwa mwanafunzi, maelekezo ya usalama barabarani kwa mwalimu, mfano wa barabara yenye alama na vifaa vingine kama viakisi mwanga, vyeti pamoja na kalamu.
   
  Katika mradi huo, mwaka huu Total Tanzania imefanikiwa kuzifikia shule za msingi  10 jijini Dar es Salaam.
   
  Shule zilizopata mafunzo hayo ni    Shule ya Msingi Kawe A,Shule ya Msingi Tumaini,Shule ya Msingi Hananasif,Shule ya Msingi Mkunguni, Shule ya Msingi Mwongozo, Shule ya Msingi Yombo Dovya, Shule ya Msingi Jitihada, Shule ya Msingi Mivinjeni , Shule ya Msingi Mzambarauni pamoja na Shule ya Msingi Amani.

  0 0

  SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limewatahadharisha wananchi kuepuka taarifa za uzushi zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya usambazaji maji machafu kwenye line za mabomba ya wateja wa Dawasco.

  Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco , Bi Everlasting Lyaro alisema taarifa hizo za uzushi zimesambazwa na watu wachache ili kuchafua taswira ya shirika hilo na pia  kuihusisha Dawasco moja kwa moja na mlipuko wa kipindupindu ulioingia jijini.

  “Tunawatahadharisha wateja wetu kuwa ubora wa maji unaozalisha na Dawasco unakidhi vigezo vyote kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai, hatuwezi kuzalisha maji yenye kuleta madhala kwa wananchi kwani hata haki za binadamu haziruhusu kufanya hivyo ” alisema Lyaro.

  ‘Ukweli wa maeneo yanayolalamikiwa kama vile Ilala mitaa ya Sharif shamba na Buguruni ni kuwa kuna kampuni za uchimbaji mifereji bado hatujabaini kama ni ya watu binafsi au za manispaa. 

  Wao walichimba mifereji ya majitaka karibia na mabomba ya wateja walio na line za Dawasco za majisafi hivyo kutiririsha majitaka kwenye mfumo wa majisafi. Ikapelekea maji machafu kuingia kwenye line zao na kupelekea mabomba ya maji yanapofunguliwa zinakutana na yale maji machafu yaliyokatwa kutoka kwenye mifereji” aliongezea lyaro.

  Alisema kuwa Baada ya kupokea malalamiko hayo tulichukua hatua kadhaa moja ni kuchukua sampuli za Maji hayo na kwenda kuyapima na kurudi kufunga maji hayo yasiendelee kutoka.  Na baada ya upimaji sampuli ile na kukuta sio salama tulitenga line(isolate) ya majisafi ya sharif shamba hadi hapo tatizo litakapotatuliwa na mamlaka husika.

  Tuhuma za Dawasco kusambaza Maji machafu ziliripotiwa mapema wiki hii huku zikihusishwa zaidi na athari za ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kushika kasi jijini dar.


  0 0
 • 09/09/15--04:01: NBC LAUNCHES SMS ALERT

 • PRESS RELEASE
  NATIONAL BANK OF COMMERCE
  NBC LAUNCHES SMS ALERT

  Dar es Salaam, 8thSeptember 2015
  NBC has today launched SMS alert service that enables NBC customers to receive instant SMS notifications on their registered mobile phone numbers of transactions carried out on their accounts. The SMS notifications enable NBC customers to instantly keep track of transactions happening on their accounts. 

  “In addition, this service will allow our customers to identify if their accounts have carried out any unauthorized transaction enabling them to take immediate action”, said Musa Jallow, the bank’s Head of Retail Banking
  The SMS notifications will be sent out for all ATM and POS transactions carried out by a customer’s debit card. This service is free of charge, and hence NBC customers will not be charged for receiving SMS notifications.
  NBC customers are not required to register for this service as SMS notifications are sent to customers’ mobile phone numbers which are registered in the NBC database. All customers with valid registered phone numbers automatically receive SMS notifications every time they carry out ATM or POS transactions with their debit card.

  “If any of our customers does not receive SMS notification, it’s mostly likely that we do not have their phone number registered in our database or the phone number registered is incorrect. If that happens, we urgently advise the customers to visit any of the nearest NBC branch to update their information and start enjoying this service”, stressed Musa Jallow

  Notes to Editors
  About NBC
  NBC is one of the most represented retail bank in the country with over 45 years experience in providing financial services. Apart from offering traditional banking services, NBC also prides itself with an expanded branch network and footprint. NBC has 52 branches, 242 Visa enabled ATMs, and over 173 Points of Sales strategically located throughout the country. NBC has employed over 1200 staff

  For more information please contact;
  Alina Maria Kimaryo, Ag. Head of Marketing and Corporate Relations
  National Bank of Commerce
  Email: Alina.MariaKimaryo@nbctz.com


  0 0

   Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino (kulia) akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita - Manzie Mangochie (kushoto) kwa niaba ya Shule za Msingi Nyamkumbu na Ukombozi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka Benki ya NMB katika hafla fupi iliyofanyika mjini Geita jana ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.
   Wanafunzi wa Shule za Msingi Nyankumbu wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 na Benki ya NMB jana wilayani Geita.NMB ilisaidia madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni 10 katika shule mbili za msingi za Nyamkumbu na Ukombozi ambapo kila shule ilipata madawati 50
  BENKI ya NMB jana ilikabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Shule za Msingi Nyankumbu na Ukombozi zilizopo mkoani Geita ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.

  Msaada huo umekabidhiwa na meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino ambapo mkuu wa wilaya ya geita alipokea madawati hayo kwa niaba ya shule hizo mbili za msingi.

  “Madawati haya tunayoyakabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema Augustino.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya jiwe lenye Madini huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aifola Investiment Co. Ltd, Zubery Mabie, kuhusu upatikanaji wa madini na utengenezaji wa Unga wa 'Lime Powder', wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Samaki wa Mapambo, Nunu Mrisho, kuhusu upatikanaji wa Samaki hao na soko lake , wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
   
   Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano hilo.
   Mwakilishi wa Umoja wa wafanyabishara wa Burundi, akizungumza.
   Waziri wa Nchi- Uwekezaji na Uwezeshaji, Eng. Christopher Chiza, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dkt. Bilal ili kufungua Kongamano hilo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Balozi waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Makatibu Wakuu waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Viongozi wa Halmashauri wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015. Picha na OMR

  0 0

  Saluti na wimbo wa Taifa kwa Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
   Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, akisaini kitabu cha wageni alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
   Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli akiwasilisha  hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015.
    Balozi mpya wa Uswisi nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, akiongea na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015.
   Balozi mpya wa Uturuki nchini Bi. Yasemin Eralp akisanini kitabu cha wageni alipofika kuwasilisha hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
   
   Balozi mpya wa  Uturuki nchini Bi. Yasemin Eralp akiwasilisha  hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015
   Balozi mpya wa  Uturuki nchini Bi. Yasemin Eralp na ujumbe wake akizungumza na Rais Kikwete baada ya kuwasilisha  hati zake za Utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2015


  0 0

   Maadhimisho ya Miaka 10 ya uanzishwaji wa MICHUZI BLOG hapa nchini chini ya Mkurugezi wake Ankal  Muhidini Issa Michuzi iliyofanyika ofisini kwake jijini Dra es Salaam leo.
   Keki  ya maadhimisho ya miaka  1o ya MICHUZI BLOG ikiwa na keki zenye majina ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
   Mr na Mrs Michuzi wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 10, wakishuhudiwa na baadhi ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
  Mkurugezi wa MICHUZI MEDIA GROUP,Ankal  Muhidini Issa Michuzi akilishwa keki na mkewe  katika hafra fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugezi wa MICHUZI MEDIA GROUP,Ankal  Muhidini Issa Michuzi akilmlisha keki mkewe.
  Mkurugezi wa MICHUZI MEDIA GROUP,Ankal  Muhidini Issa Michuzi akimlisha keki Mtangazaji na muandaaji wa kipindi cha DANGA CHEE, Shamsa Danga ndani ya Michuzi TV online katika hafla hiyo.
   Mkurugezi wa MICHUZI MEDIA GROUP,Ankal  Muhidini Issa Michuzia akiwalisha keki wafanyakazi wa MICHUZI BLOG jijini Dar es Salaam leo.
   Mpiga picha wa Michuzi Blog, Avila Kakingo akifungua shampeini katika hafra hiyo.
   Mpiga picha wa Michuzi Blog, Avila Kakingo akiwamiminia shampeini katika hafla hiyo.
   Wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA  GROUP wakiwa na keki zao.
  Baadhi ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA  GROUP wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  unnamedTume za Uchaguzi katika Jumuia ya Africa Mashariki zimetakiwa kushirikiana na kutoa ushirikiano kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanziba (ZEC) katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

  Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Africa Mashariki Bwana Charles Njoroge wakati wa ufunguzi wa mkutano wa forum ya viongozi wa Tume za Uchaguzi za Jumuia hiyo uliofanyika katika hoteli ya New Africa Hoteli jijini Dar es Salaam leo.

  “Uenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni nafasi nyeti na ina changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kijamii na kisiasa , ni matumaini yangu  kwamba iwapo tutaungana na kufanya kazi pamoja jumuia ya Africa Mashariki Forum na kushirikiana  kuweka nguvu katika kuendesha chaguzi kutakuwa na ufanisi , uhuru na haki katika chaguzi zetu na kufikia malengo tunayoyataka” Alisema Njoroge.

  Uchaguzi nchini Tanzania mwaka huu umekuwa na hamasa kubwa ukilinganisha na chaguzi zilizopita katika nyanja mbalimbali ikiwepo ushiriki wa wananchi na idadi ya wagombea imekuwa kubwa, hii inathihirisha kuwa wananchi wamekuwa na uelewa mkubwa na wanatambua haki zao na kuitaka serikali iwajibike kwao.Aidha Njoroge amezitaka tume za jumuia ya Africa Mashariki kufikiri kwa kina na kuweka mikakati ambayo itasaidia kupunguza gharama za Uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuandaa sera ya kusaidiana katika vifaa vya uchaguzi.


  Viongozi hao wa Tume ambao wameitembelea Tanzania chini ya Mwenyeji wao ambaye ndiye mwenyekiti wa umoja huo wa Tume za Uchaguzi za Jumuia ya Africa Mashariki na ndiye mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva walitembelea kitengo cha Daftari ambapo walijionea namna taarifa za Mpiga Kura zinavyoingizwa katika mfumo wa Daftari.

  Wakiwa katika ziara hiyo Kamishna wa Tume huru ya Uchaguzi ya KenyaBalozi Mohamed Alawi  ameipongeza Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanya kwa kuda mfupi imeweza kuandikisha wapiga Kura milioni ishirini na nne kwa kutumia BVR elfu nane (8,000) ukilinganisha na nchini mwake ambapo walikuwa na BVR 15,000 na waliweza kuandikisha wapiga Kura milioni kumi na tano kwa muda mrefu.Ikiwa ni pamoja na kuliweka wazi Daftari la awali la mpiga Kura mapema kuliko ilivyofanyika nchini kwao.

  Aidha balozi Alawi aliongeza kuwa  Uchaguzi ni zoezi kubwa katika nchi,haliwezi kuachiwa NEC pekeyake, kama inavyosemwa vita haiwezi kupiganwa na majemedali pekee, Uchaguzi ni  zoezi linalofanywa na watanzania wote kwa ujumla, kwa maana hiyo ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wao wasitoe matamshi ambayo yatajenga chuki miongoni mwa jamii/ wapiga kura, tunafahamu watanzania ni wakomavu kisiasa, ni watu watulivu waitunze amani waliyonayo kwani Tanzania ipo kabla ya Uchaguzi, wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi.

  Viongozi hao ambao wamekuja nchini kujiridhisha na maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa unaotarajia kufanyika mwezi ujao wa wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni kukemea vyama vya siasa vinavyokiuka maadili ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutoa matamshi ambayo yanaweza kujenga chuki miongoni mwa Watanzania.

  0 0

  Na Matukiodaimablog
  CHAMA Cha ACT wazalendo kimewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu waliojitokeza kuomba kuchaguliwa kupokea  nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)kwa madai kuwa hapaswi tena kupewa kura katika jimbo hilo.

  Katibu Wilaya  wa ACT wazalendo Wilaya ya  Iringa Bw Zhenepa Ally leo wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa mjini Chiku Abwao ( ACT wazalendo) kwenye kata ya Kitwiru .

  Alisema kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Msigwa wakati wa Ubunge wake awali alikuwa akipambana na ujangili kwa kupambana na wauwaji wa Tembo na kila mkutano wake alikuwa akionyesha kupiga vita ujangili ila baada ya kushikamana na Waziri Lazaro Nyalandu ( CCM ) kwa kusafiri pamoja katika Ziara za nje aligeuka ghafla na kuacha kabisa kuzungumzia ujangili.

  Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu. Waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge jimbo hilo ambalo Mchungaji Msigwa kashindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

  Aliwataja waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ya Ubunge ambao wananchi wanapaswa kuwachuja kuwa ni Chiku Abwao ( ACT wazalendo) ,Frederick Mwakalebela(CCM) na Daud Masasi (ADC)na sio kupoteza kura kwa kumpa tena mchungaji Msigwa ambae ametelekeza jimbo hilo kwa miaka yote mitano.

  " Katika uchaguzi huu wananchi wa Iringa tunaomba muwapime watu watatu waliojitokeza kumpokea Ubunge Mchungaji Msigwa"

  Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo hilo la Iringa Mjini Bi  Abwao alisema jimbo la Iringa Mjini ni moja kati ya majimbo ambayo yalikuwa rahisi zaidi upinzani kuendelea kuongoza tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ila kutokana na kushindwa kwa Mchungaji Msigwa jimbo hilo wananchi wamepoteza imani na upinzani.

  Abwao aliwaomba wananchi wa jimbo la Iringa mjini kumchague yeye kuwa mbunge wao kwani sera nzuri za kuwakomboa wananchi hao

  " Mbunge  Msigwa aliahidi kuwapa nyavu kwa maana ya mitaji ila kipindi chake chote kaishia kufanya mikutano ya vurugu na kutukana wananchi wake kuwa ni wavivu wanaopenda kucheza bao wakati nae ni miongoni mwa wavivu hao na wacheza bao wazuri"

  Hivyo alitaka wananchi wa jimbo la Iringa ili kurejesha heshima ya upinzani jimbo la Iringa Mjini ni wakati wa kuchagua chama cha ACT wazalendo kuanzia Udiwani Ubunge na Urais na sio Chadema kupitia mwamvuli wao wa Ukawa ambao wamesimamisha mgombea ambae yupo katika orodha ya mafisadi.

  Akizungumzia kuhusiana na Mgombea Urais wa Ukawa Chiku ,alisema kuwa Mgombea huyo hana sifa ya kuwakomboa watanzania kwani ni genge la walanguzi linalotaka kwenda kutumia Ikulu kwa kurejesha mamilioni ya pesa waliotumia kununua Ikulu.

  Hata hivyo alisema watanzania wasidanganyike na safari ya matumaini ya Ukawa kwani safari hiyo haipo tena na hivyo ni vema kuchukua hatua kwa kukataa wagombea hao wa Ukawa.

  0 0

  Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa vilabu 16 vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TFF zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia vilabu vya Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.

  Tumekua na kilio cha muda mrefu juu ya vilabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini vilabu vilikuwa vinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.

  Naye Mkuu wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote yatakayofnayika ndani ya nchi.
  Mchezaji au kiongozi pindi atakapopata tatizo la kuumwa, basi ataweza kutibiw akatika hospitali yoyote yenye huduma ya Bima katika eneo alilopo, lengo ni kuhakikisha wanakua na afya njema kwa ajili ya kushiriki vizuri mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom.

  Lengo letu ni kuona wachezaji wanapata huduma ya afya popote wanapokuwa na kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Ligi Kuu, na kuweza kuzitumikia vyema timu zao kwenye mashindano.
  Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kwa niaba ya vilabu vya Ligi Kuu amesema wanashukuru kupata udhamini huo wa bima ya afya, uwepo wa NHIF umevipunguzia vilabu mizigo wa matibabu na sasa vilabu vitaweza kushiriki vizuri kwenye michuano ya msimu huu.

  0 0

    Mgombe Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamadi akipiga makofi kuashiri Uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi katika viwanja vya Kibanda maiti Mjini Zanzibar.
   Muimbaji Abdallah Issa akitumbuiza katika uzinduzi wa Kapeni uliofanyika Kibanda Maiti Zanzibar.
   Sehem ya Meza Kuu.

    Badhi ya wananchi wakifuatilia Mkutano huo
   Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema Mhe. Edward Lowasa akiwasalimia Wazanzibari na kuomba kura zao katika uzindizi wa kampeni uliofanyika viwanja vya kibanda maiti Mjini Zanzibar.
  Mgombe Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) 
  Mhe. Maalim Seif Sharif akiwahutubia wananchi waliofanyika kwenye uzindu wa kampeni.

  0 0

  Mkuu wa kambi ya JKT Burombola Luteni Kanali Mketo akizungumza katika sherehe ya kufunga mafunzo ya mujibu wa sheria kwa vijana waliomaliza kidato cha sita mafunzo yaliyofanyika kwenye kambi ya Burombola wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

  Baadhi ya vijana waliomaliza mafunzi ya JKT kwenye kambi ya Burombola wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
  picha na editha Karlo
     
             
     Na Editha Karlo,Kigoma
  MKUU  wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga alisema kuwa jeshi hilo litaendelea kuboresha changamoto mbalimbali zinazojitokeza ili kuwezesha vijana wote wanaomaliza masomo ya kidato cha sita kujiunga na mafunzo hayo kwa wakati mmoja.

  Muhuga alisema hayo  kwenye kambi ya JKT Burombola kikosi cha 821 katika sherehe za kumaliza mafunzo kwa vijana wa mujibu wa Taifa kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita katika mafunzo yaliyojulikana kama Operesheni Kikwete.

  Kanali hotuba iliyotolewa Kanali Chacha Wanyancha aliyekuwa akimwakilisha  Mkuu wa JKT katika mafunzo hayo alisema kuwa mafunzo baada ya kusimama kwa miaka 20 na kurudishwa tena wamegundua kuwa mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwa vijana waliopitia mafunzo ya JKT.

  Jenerali Muhuga alisema kuwa baada ya kurudishwa kwa mafunzo hayo wamekabiliana na changamoto la ongezeko la wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita kutokana na ongezeko kubwa la shule za sekondari huku miundo mbinu ya makambi mbalimbali ya majeshi ikiwa haijaboreshwa kiasi cha kutosha kuchukua wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha sita.

  Hata hivyo alisema kuwa mkakati wa jeshi hilo kwa sasa ni kuiomba serikali kuiongezea fedha ili iweze kukabiliana na changamoto hizo na kuchukua wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha sita kwa wakati mmoja waweze kujiunga na mafunzo hayo.

  Sambamba na hayo Mkuu huyo wa JKT  ametoa wito kwa vijana wanaomaliza mafunzo kutumia stadi wanazopewa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya kujenga Taifa badala ya kurudi mtaani na kujuhusisha na ushabiki wa kisiasa na mambo ambayo hayana manufaa kwa maendeleo yao na Taifa kwa jumla.

  Akifunga mafunzo hayo MKUU wa mkoa Kigoma Issa Machibya amewataka vijana waliomaliza mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa nchini kutumia mafunzo hayo kuwafunda vijana wenzao walio mtaani kuwa na maadili mema na kujitolea katika ujenzi wa taifa badala ya kushiriki  vitendo vya uvunjifu wa maadili.

  Baada ya mafunzo hayo Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa vijana hao watakuwa askari wa akiba na siku zijazo ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama zitachukuliwa kutoka miongoni mwa vijana hao.

  “Natoa wito kwa vijana waliomaliza mafunzo kuwa chanzo cha maendeleo katika jamii kwa kuonyesha maadili mema na utendaji uliotukuka ili kuonyesha tofauti kubwa iliyopo kati yao waliopitia JKT na vijana wenzao waliomtaani ambao hawajapitia mafunzo hayo,”Alisema Mkuu huyo wa mkoa.

  Awali katika risala ya vijana hao iliyosomwa na Nashorwa George wameishukuru serikali kwa kurudisha mafunzo hayo ambapo hata hivyo walisema kuwa muda unaotumika kwa mafunzo hayo kwao ni mdogo ambao unawafanya kushindwa kufanya baadhi ya mafunzo.

  0 0

   Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kati – Magharibi, Humphrey Mmbando akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala muhimu yaliyojitokeza wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Semina hiyo imefanyika leo mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa Mafunzo yanayotolewa nchi nzima kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini. Wengine pichani (mstari wa mbele) ni baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Madini – Shinyanga.
   Baadhi ya akina mama ambao ni wachimbaji wadogo wa madini mkoani Shinyanga wakiwa katika semina kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Kutoka Kushoto ni Amina Mtoro, Hafsa Issa, Halima Mohamed, Khadija Salum na Nusura Juma. Semina hiyo imefanyika leo mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa Mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchi nzima.
   Mtaalamu kutoka Kitengo cha Leseni cha Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani, akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika leo Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga.
   Mtaalamu kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Juma Masoud akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa wakati wa Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Semina hiyo imefanyika leo Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara husika kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini kote.
   Baadhi ya Vijana ambao ni wamiliki wa leseni za madini mkoani Shinyanga wakiwa katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining cadaster Transactional Portal – OMCTP) yanayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini nchi nzima. Kutoka Kushoto ni Juma Swalehe, Steven Ngonyani, Salum Abdillah na Meshack Daniel. Mafunzo hayo kwa mkoa wa Shinyanga, yamefanyika leo Septemba 9, 2015.
   
  Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Erick Mkoma, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Madini Kanda ya kati Magharibi iliyoko mjini Shinyanga. Wengine pichani ni Juma Masoud (katikati) na Mhandisi Nuru Shabani (Kulia). Wataalam hawa leo Septemba 9, 2015 wametoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini mkoani Shinyanga kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandano (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP).

  Na Veronica Simba – Shinyanga
  Zoezi la utoaji semina kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini linaloendeshwa na wizara ya nishati na madini leo limefanyika mjini Shinyanga ambapo wachimbaji zaidi ya 60 wamepatiwa mafunzo hayo.

  Akifungua Semina hiyo mjini Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi, Humphrey Mmbando amewataka washiriki kuhakikisha wanaufahamu mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwani ni wale tu watakaosajiliwa kwenye mfumo husika ndiyo watakaotambuliwa kisheria na kupata haki zote za msingi.

  Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao mapema mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma ili kutoa huduma za haraka, kuongeza uwazi na kumuwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe.

  Ni kwa kuzingatia umuhimu wa matumizi ya mfumo huo mpya kwa wadau wa sekta ya madini nchini, Wizara kupitia Kitengo cha Usimamizi wa Leseni inaendesha zoezi nchi nzima kuwaelimisha wadau hao namna mfumo huo unavyofanya kazi.


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Bw. Haroub Soud Mzee ambaye ni  mlemavu wa miguu bajaji itakayomsaidia katika shughuli zake mbalimbali za kimasomo. Bw. Mzee  ni mwanafunzi wa Uhasibu mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kampala University jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Kikwete akisoma maelezo ya kadi ya bajaji aliyemkabidhi. Haroub Soud Mzee ambaye ni  mlemavu wa miguu bajaji itakayomsaidia katika shughuli zake mbalimbali za kimasomo. Picha na Magreth Kinabo - MAELEZO

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi na wana CCM wa Kijiji cha Mitambuuni alipofika kuwasailia akiwa katika ziara ya Kisiwa cha Pemba.
   Balozi Seif akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Kijiji cha Mitambuuni Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, kulia yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa na kushoto yake ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya Mkoa huo Omar Khamis Othman.
   Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akizungumza na wana CCM na Vijana wa Maskani ya Vumilia ya Mitambuuni Wete Pemba.
  Balozi Seif akiwapongeza Vijana wa Maskani ya CCM YA Vumilia ya Kijiji cha Mitambuuni baada ya kuamua kuuhama upinzani na kujiunga na Chama cha Mapinduzi.
  Picha na –OMPR – ZNZ. 
                      
  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba ni aibu kubwa kuona Wananchi wa Kijiji cha Mitambuuni  kiliopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wanakosa  huduma za Skuli ya Maandalizi  kwa watoto wao wakati Wawakilishi na Wabunge wao wapo.

  Alisema inasikitisha na kutia uchungu kutokana na kadhia inayowapata watoto wa Kijiji  hicho ya kufuata masomo umbali wa kilomita Sita matatizo ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi  ndani ya uwezo wa Viongozi wao wa Jimbo.

  Balozi Seif Ali Iddi alielezea masikitiko yake wakati  wa hafla fupi ya kuizindua Maskani ya CCM ya Vumilia ya Kijiji cha Mitambuuni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyoanzishwa na Vijana walioamua kuacha upinzani na kujiunga na Chama cha Mapinduzi .

  Alisema Chama cha Mapinduzi katika kipindi kijacho mara baada ya uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba kinakusudia kufanya mabadiliko zaidi ya Maendeleo katika Majimbo la Kisiwa cha Pemba kwa lengo la kupunguza kero zinazowakabili Wananchi wa Majimbo hayo.

  Balozi Seif aliwakumbusha na kuwaomba Wananchi wa Majimbo ya Kisiwa cha  Pemba  kuhakikisha kwamba wanawachagua Viongozi watakaokuwa tayari kufanya kazi nao.

  Alisema wapo viongozi wengi wa Majimbo hayo wenye tabia ya kuyahama majimbo yao mara tuu bada ya kuchaguliwa na kuazisha Familia nyengine katika maeneo ya Unguja, Dar es salaam na Dodoma  na kusahau kwamba wamebeba dhima ya kuwatumikia wananchi waliowapa kura zao.

  Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwapongeza Vijana hao wa Kijiji cha Mitambuuni kwa uamuzi wao wa kufuata sera sahihi zinazotekelezeka za Chama tawala cha Mapinduzi.

  Balozi Seif liwataka Vijana hao kwa kushirikiana na Wazazi na Viongozi wa eneo hilo kuanza maandalizi ya ujenzi wa  maskani yao ya kudumu pamoja na Skuli ya Maandalizi kwa hatua ya msingi
  Aliwahakikishia wananchi na Vijana hao wa Mitambuuni kwamba atachukuwa juhudi za makusudi katika kuunga mkono uendelezaji wa  ujenzi wa majengo yote Mawili  ili  kusaidia kuwaondoshea changamoto zinazowakabili  watoto na Vijana hao.

  Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa  alisema Mtambwe na Vitongoji vyake imebadilika kutokana na Sera sahihi za Chama cha Mapinduzi zilizokuwa zikitekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Mzee Mberwa alisema harakati za kiuchumi zimeongezeka  na kupanuka mara dufu  na kutoa fursa  pana zaidi kwa Wananchi  maeneo hayo kuendeleza vyema maisha yao  ya kila baada ya kukamilika kwa miundo mbinu bora ya mawasiliano ya bara bara.

  Akisoma Risala ya Maskani hiyo ya CCM ya Vumilia  Mitambuuni  Katibu wa Maskani hiyo Ndugu Juma Said Saleh alisema uamuzi wa vijana hao kuuhama upinzani  na kuhamia CCM unatokana na  tabia ya viongozi wanaowachaguwa kutokujali kuwatumikia.

  Nd. Said alisema dharau ZA Viongozi hao zimesababisha kuibuka kwa changamoto kadhaa zisizopaswa kutatuliwa na Serikali Kuu ambazo zimo ndani ya uwezo  kamili wa Viongozi wao wa Majimbo.

  Katibu huyo wa Maskani ya Vumilia alieleza kwamba Vijana hao katika kupambana na tabia ya Viongozi hao wameahidi kufanya kampeni ya nyumba hadi nyumba katika kuhakikisha  Wagombea Uchaguzi kupitia Chama cha Mapinduzi wanaibuka washindi ili waweze kuwatumikia kwa upendo na ushirikiano.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  9/9/2015.


  0 0
 • 09/10/15--02:12: BEI YA MADAFU HII LEO

older | 1 | .... | 634 | 635 | (Page 636) | 637 | 638 | .... | 1897 | newer