Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

SHULE ZA SEKONDARI NCHINI ZASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA MATUMIZI YA NISHATI ENDELEVU YA BIOGESI.

$
0
0
 Mtalaam wa masuala ya Biogesi na Majiko Sanifu wa Taasisi ya kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania ( TaTEDO) Bw.Stephen Boniface akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa mtambo wenye uwezo wa kuzalisha gesi yenye mita za ujazo 200 walioujenga katika shule  ya Sekondari Manzese iliyoko wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege.
 Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akielezea ushiriki wa DAWASA katika kufanikisha ujenzi wa Mradi wa Biogesi katika shule ya Sekondari Manzese ya jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea mradi huo jana jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege akitoa ufafanusi kwa waandishi wa habari kuhusu manufaa ya mradi wa nishati endelevu ya Biogesi utakavyowanufaisha wanafunzi wa shule hiyo.
 Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi Bw. Shima Sango kutoka Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) Akiwasha moja ya jiko la gesi liliojengwa katika shule ya Sekondari Manzese.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
 
Na.Aron Msigwa-MAELEZO
SHULE za Sekondari kote nchini zimeshauriwa kuwekeza katika matumizi ya Nishati endelevu ya Biogesi na majiko sanifu ili kulinda na kuhifadhi mazingira.

Ushauri huo umetolewa na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam  (DAWASA) Bi.Neli Msuya mara baada ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa kuzalisha Nishati endelevu ya Biogesi katika Shule ya Sekondari Manzese wilayani Kinondoni, jijini Dar es salaam.
 

Amesema kuwa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam ( DAWASA ) ikishirikiana na Taasisi ya Kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO)na  Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa UN- HABITAT wameamua kuitumia changamoto  ya uhifadhi wa Maji Taka iliyokuwa inaikabiri shule hiyo kwa kuanzisha mradi wa kuyageuza maji taka ya vyoo vya shule hiyo kuwa rasilimali ya kuzalisha nishati endelevu ya Biogesi.

Bi.Neli ameeleza kuwa TaTEDO inajenga miundombinu ya mradi huo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) na kuongeza kuwa  mradi huo unatarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi Desemba mwaka huu.

Amesema matumizi ya gesi hiyo yataimarisha utoaji wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosoma michepuo ya Sayansi kupitia maabara ya kisasa inayojengwa shuleni hapo.

"DAWASA tunauona mradi huu kama mkombozi kwa wanafunzi hawa na  mfano wa kuigwa kwa shule nyingine zilizoko ndani na nje ya jijini Dar es salaam zinazokabiliwa na uhaba wa nishati ya umeme  na gesi, natoa wito kwa shule nyingine kuanza kutumia nishati endelevu ya Biogesi ili klinda na kuuhifadhi mazingira" Amesisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Manzese Bw. Linus Mwakasege akitaja faida za mradi huo amesema utawasaidia kupunguza gharama za matumizi ya mkaa, kutunza mazingira na kuondoa harufu mbaya ya vyoo iliyokuwa ikiwasumbua wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema shule yake ina idadi ya wanafunzi 1400 hivyo matumizi ya  gesi hiyo yatawasaidia wanafunzi wanaojifunza masomo ya sayansi katika maabara iliyoko shuleni hapo ambayo imewekewa mifumo ya kusambaza gesi hiyo na kuongeza kuwa  baadhi ya shule zimeanza kwenda kujifunza  kuhusu mradi huo.

Naye Mtalaam wa masuala ya Biogesi na Majiko Sanifu wa Taasisi ya kuendeleza Nishati Asiliana Uhifadhi wa Mazingira ( TaTEDO) Bw.Stephen Boniface wasimamizi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi katika shule hiyo amesema kuwa kiwango cha gesi asilia inayozalishwa kimefikia mita za ujazo 200.

Amesema kuwa wao kama Taatedo kazi waliyoifanya ni kuunganisha mabomba katika vituo viwili vya kukusanyia taka kwa ajili ya kuanza kuzalisha gesi itakayotumika kupikia, maabara na mambo mengine.

Amesema TaTEDO wamefanya kazi bega kwa bega na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kuwezesha kiasi kikubwa cha maji taka yanayotoka katika vyoo vya shule hiyo kuzalisha gesi na wakati mwingine kutibiwa ili yaweze kutumika kwa shughuli za umwagiliaji wa bustani.

MUHIMBLI YATOA MAFUNZO YA KUZUIA KIPINDUPINDU KWA WATUMISHI WAKE, 989 WAAMBUKIZWA.

$
0
0
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili –MNH-  imetoa  mafunzo kwa watumishi wake kudhibiti  ugonjwa wa kipindupindu   ambao  umesambaa na kusababisha watu 989 kuambukizwa  ugonjwa  huo  jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo ya siku saba ambayo yanahusisha Wakurugenzi, Wakuu wa Idara , Madaktari, Wauguzi , Wafamasia pamoja na Wahudumu  yana lengo la kuwaelimisha juu ya ugonjwa huo , jinsi ya kuzuia , kumtibu mgonjwa na kumtambua mtu mwenye dalili za Kipindupindu.

Akielezea  mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura na ajali  ambaye  pia  ni Daktari Bingwa wa magonjwa  hayo  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  Dokta  JUMA   MFINANGA amesisitiza kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa Kipindupindu ni uchafu lakini pia maji  machafu yanachangia kwa asilimia kubwa kuenea  kwa ugonjwa huo.

Hivyo amewakumbusha wananchi kuzingatia usafi  kwa kunawa mikono kwa sabuni  na maji yanayotiririka , kula vyakula vya moto , kunywa maji yaliyo safi na salama kusafisha  mazingira  na kwa wale wanaosafiri wametakiwa kutokula  hovyo barabarani kwani hali  bado ni tete.

Kwa mujibu wa Dokta MFINANGA  Hospitali ya Taifa  Muhimbili imepokea wagonjwa 20 ambao wanadalili za ugonjwa huo na kisha kupelekwa katika kambi za Kipindupindu.

Manispaa  ya  Kinondoni inaongoza kwakuwa na wagonjwa 663, Ilala ina wagonjwa 246 na Temeke ina wagonjwa 80.

            Mafunzo hayo yameanza leo yatamalizika Septemba 17 mwaka huu ambapo leo waaguzi 126  tayari wamepatiwa mafunzo hayo.

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA-MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akifungua rasmi kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar uliopo mjini Dodoma, katika hotuba yake ya ufunguzi Mhe. Jaji Mkuu amewaasa Watumishi wa Mahakama kutimiza wajibu wao wa utoaji haki nchini kwa uadilifu.
 Kundi la baadhi ya Wahe. Majaji na wajumbe wengine wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi linalofanyika katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dar es Salaam.
 Mhe. Hussein A. Kattanga, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania akitoa taarifa ya Maendeleo ya Mahakama katika ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kinachofanyika mkoani Dodoma.
 Wajumbe wa Baraza wakiwa katika kikao hicho, lengo la kikao cha Baraza la Wafanyakazi ni kuwawezesha Watumishi kuainisha matatizo yanayowakabili na kutafuta njia za kutatua na kuboresha huduma za Mahakama.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikati), Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa pili kulia), Mhe. Clarensia Makuru, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Haruna Songoro, Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara (wa kwanza kushoto), Bi. Rose Tengu, Katibu Mteule wa Baraza la Wafanyakazi-Mahakama ya Tanzania (wa tatu kushoto) na Wajumbe wengine wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Wajumbe ya Kikao cha Baraza (waliosimama) wanaowakilisha mikoa mbalimbali. (Picha na Mahakama)

KIPINDI CHA JUKWAA LANGU.....SEP 7 2015 (PART ONE)

$
0
0
JUKWAA LANGU ni kipindi ambacho kitakuwa kikikujia kila Jumatatu, kujadili mambo mbalimbali yanayotokea nchini Tanzania, na zaidi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
 Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi cha Septemba 7, 2017 ambapo studioni tulitembelewa na Shamis Abdul, kuwezesha mjadala.
Pia, kulikuwa na washiriki kwa njia ya simu, toka pande mbalimbali za dunia

MAONESHO YA VITO NA USONARA MJINI BANGKOK THAILAND

$
0
0
 Tanzania  kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeshiriki katika Maonesho ya VITO na USONARA nchini Thailand Banda la Tanzania limetia fora na kuwa kivutio kikubwa.

SEMINA YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE KWA KUTUMIA VIPODOZI VYA LUV TOUCH MANJANO YAENDELEA

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shaer illusions mama Shekha Nasser  Akiwaeleza jambo washiriki wa Semina ya Ujasiriamlai ( hawapo pichani) Namna ya Kujitangaza kwa Kutumia njia mbalimbali , kuwahudumia  na kuwajali wateja wao. Semina hiyo iliyo chini ya Manjano Foundation ina lengo la kuwajengea uwezo wana wake kujikita kwenye biashara hasa kwa kutumia Vipodozi vya Luv Touch Manjano anayeshuhudia ni Mkufunzi wa Maswala ya Biashara  Ndugu Felix Maganjila.
 
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mada Mbalimbali zinazojadiliwa kwenye semina hiyo.
Mafunzo ya Ujasiriamali Phase II ya Wanawake kupitia Vipodozi vya LuvTouch Manjano yameingia siku ya tatu leo ambapo Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila ametoa mada kuhusu namna ya kutafuta wateja na njia mbalimbali za kuuza bidhaa.Washiriki walipata nafasi ya kwenda kutafuta masoko (Marketing Research) maeneo tofauti ya Jiji la Dar es salaam pamoja na kuangalia changamoto kubwa za namna ya kuuza bidhaa zao kwa wateja wa Luvtouch na namna bora ya kuwashawishi wakazi wengine kutumia kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano.
 Mkufunzi wa Maswala ya Biashara  Ndugu Felix Maganjila Akieleza jambo namna ya Kuendesha biashara kwa  washiriki hao .

 
 Waliweza kuwaelezea wateja wapya kuhusu ubora wake pia kuwa wazalendo na kuunga  kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambayo ni bidhaa ya kwanza na ya pekee ambayo ni Make-up brand ya Kitanzania inayozalishwa na Shear illusions inayomilikiwa na mzalendo mama Shekha Nasser. Baadhi ya washiriki waliopata fursa ya kufanya mauzo maeneo mbalimbali walifanikiwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.
Kwa Upande wa Afisa Mtendji Mkuu wa Shaer illusions mama Shekha Nasser amewataka washiriki wanapoanzisha biashara zao na kujikota katika tasnia ya vipodozi ni muhimi hao kujitangaza ipasavyo kwa kutumia njia mbalimbali za bei nafuu maana bila matangazo hakuna biashara.
Washiri wa semina hiyo wakifurahiya jambo.

WAZIRI MKUU ATAKA ELIMU ZAIDI YA URUTUBISHAJI WA VYAKULA ITOLEWE KWA WANANCHI

$
0
0
                                                  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema uongezaji virutubisho kwenye vyakula umeibua mguso mpya na kuleta mlipuko baina ya sekta binafsi na sekta za umma (PPP) ambazo zinasimamia masuala ya afya kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kazi kubwa zaidi inabidi ifanyike ili elimu ya kutosha iweze kufikishwa kwa mabilioni ya watu ambao milo yao ya kila siku haina virutubisho vya kutosha.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumatano, Septemba 9, 2015) wakati akizungumza na washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi 30 wanaohudhuria mkutano wa kwanza wa kimataifa wa urutubishaji vyakula ulioanza jana jijini Arusha. Mkutano huo utamalizika kesho, Septemba 11, 2015.

“Bila kuwa na sera zinazoeleweka na jamii, bila kuwekeza zaidi na bila kuwa na timu ya wataalamu waliobobea kwenye masuala la chakula, tuko hatarini kupoteza kasi tuliyoanza nayo na tunaweza tusifanikiwe kutimiza malengo tuliyotarajia,” alionya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ambaye alifungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, alisema urutubishaji wa vyakula unaohimizwa ni uongezaji wa madini na vitamini kwenye vyakula vinavyosindikwa viwe vya mafuta au nafaka ili kupambana na udumavu na utapiamlo. Alisema hivi sasa virutubisho vinavyoongezwa kwenye vyakula ni pamoja na madini ya chuma, zinc, vitamini A na vitamini B12.

“Uongezaji wa virutubisho unaendana na kampeni ya siku 1,000 za mwanzo wa maisha ya mtoto (1,000 days of a child’s life) ambayo inaendeshwa na Serikali yetu kwa kuzingatia kuwa faida zake zinagusa ukuaji na afya ya mtoto, ukuaji wa ubongo wa mtoto, ujenzi wa kinga imara za mwili, uelewa mkubwa unaomwezesha mtoto kufanya vizuri masomoni na uhakika wa maisha marefu ambao unachangia ukuaji wa uchumi na pato la Taifa,” alisema.

Kuhusu juhudi za Serikali, Waziri Mkuu alisema Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali za Mitaa imelenga kupanua huduma za urutubishaji wa vyakula vijijini ambako asilimia 70 ya Watanzania wanaishi. “Mifumo imewekwa ili kusaidia wenye viwanda vya kusindika nafaka na mafuta waweze kuongeza virutubishi hivyo,” alisema.

Alisema Tanzania ilianza kampeni za kuongeza virutubisho kama vile madini joto (iodine) kwenye chumvi tangu miaka ya 90 na matokeo yake hivi sasa hakuna wagonjwa wa goitre kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Hivi sasa kila kaya inatumia chumvi yenye madinijoto na asilimia zaidi ya 80 ya kaya zinatumia chumvi ya aina hii. Matokeo yake ni kupungua kwa ugonjwa wa goitre  na kufikia chini ya asilimia tano kwa watoto wenye umri kati ya miaka 6-12 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kwenye miaka ya 1980,” alifafanua.

Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) wa Masuala ya Kupambana na Njaa, Mfalme Letsie III wa Lesotho alisema suala la kurutubisha vyakula lisiachwe kuwa la Serikali peke yake bali linahitaji nguvu ya pamoja kutoka kwa wadau mbalimbali na hata ikibidi Serikali zote za Bara la Afrika.

“Vyanzo vya upungufu wa virutubisho na utapiamlo na vingi na vina njia mbalimbali za kukabiliana nazo. Lakini hapa nataka nisisitize kwamba, tunahitaji utashi wa kisiasa kutoka kwa wakuu wa nchi zote duniani na siyo kwa bara la Afrika peke yake ili suala hili liweze kufanikiwa,” alisema.

“Nikiwa Balozi wa AU wa kupambana na njaa, ninazitaka nchi zote na Serikali zilizoko madarakani ziweke sheria mahsusi au sera za kitaifa ambazo zitaweka bayana suala la urutubishaji wa vyakula kama njia ya kupambana na njaa na pia kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa virutubisho vya kutosha kwenye milo ya kila siku ya watu wetu,” alisema huku akishangiliwa.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kebwe S. Kebwe alisema Serikali imelenga kuajiri maafisa lishe kwenye Halmashauri za Wilaya 157 ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa viinilishe kwenye vyakula.

Alisema kati ya mwaka 2010 na 2013 Serikali imeongeza kiasi cha fedha kutoka sh. bilioni 19/- hadi sh. bilioni 33/- ili zisaidie kusimamia masuala ya lishe na urutubishaji wa vyakula.

Mapema, akitoa taarifa kuhusu Mkutano huo wa Kwanza wa Kimataifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN), Dk. Marc Van Ameringen alisema mkutano huo unawajumuisha watendaji kutoka serikalini, taasisi binafsi, vyuo vikuu na taasisi za utafiti ili kwa pamoja waje na suluhisho la kudumu juu ya urutubishaji vya vyakula kama njia ya kupambana na njaa na udumavu.

Alisema wana maeneo matano ambayo wameyalenga yakiwemo uboreshaji wa sheria; utoaji wa elimu zaidi na ushawishi kwa jamii; haja ya kupata uwekezaji zaidi kwenye eneo hilo; haja ya kupata msukumo kutoka Serikali za nchi mbalimbali na kuhakikisha kuwa urutubishaji wa vyakula unaingizwa kwenye mikakati ya kitaifa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, SEPTEMBA 10, 2015.

MDAHALO WA VYAMA VYA SIASA VIKIJADILI MASUALA LA ELIMU NA AFYA

$
0
0
MDAHALO WA VYAMA VYA SIASA JUMAPILI 13 SEPTEMBER SAA SABA MCHANA
Tarehe: Jumapili Septemba 13 2015
Muda: 7:00 – 10:00am (Saa saba mchana hadi saa kumi jioni)
Mahali: Ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) – Posta

Midahalo hii inalenga kuvipa vyama vyote fursa ya kunadi Ilani zao na kwa wananchi kuuliza maswali muhimu yatakayo pelekea maamuzi yao katika uchaguzi. Vyama vinavyoshiriki ni vile vyenye wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na wagombea Ubunge angalau majimbo 65.

Midahalo hii itarushwa moja kwa moja na Star TV na Redio RFA.
Vyombo vya habari vinakaribishwa kushiriki lakini lazima wajiandikishe kabla ili kufanya hivyo. Tafadhali tuma barua pepe kwa rchande@twaweza.org


SHEIKH ABUBAKARY ZUBER ACHAGULIWA KUWA MUFTI WA TANZANIA

$
0
0
Wakatikati ni Mufti mpya Sheikh Abubakary Zuber ambaye amechaguliwa leo na wajumbe wa BAKWATA mkoani Dodoma kuwa Mufti wa Tanzania  akichukua nafasi  ya hayati Sheikh Issa Bin Simba.

VYUO VIKUU NCHINI KUNOANA KATIKA KONGAMANO LA ELIMU YA JUU 2015 JIJINI ARUSHA

$
0
0
  Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya akizungumza na waandishi habari leo kuhusu kongamano la saba la elimu ya juu 2015 linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 1-2, 2015. Pembeni ni Thea Mtau (kulia) na Cosmas Mwasoibya ambao ni wajumbe wa Kamati ya Maandalizi.
Waandsihi wakimsikiliza   Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya katika mkutano na waandsihi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii/Picha na Cathbert Kajuna.

 WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini ,Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vuo Vikuu nchini (CVCPT) imeandaa kongamano la saba la elimu. 

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya amesema wazo la kuandaa makongamano ya elimu ya juu nchini ni kubadilishana uzoefu na maarifa miongoni mwa wadau elimu katika mstakabali wa taifa. 

 Amesema katika makongamano watajadili changamoto zinazokabili sekta ya elimu ya juu kutokana na kupanuka kwa sekta hiyo kwa kuwa uazishwaji wa vyuo vikuu binafsi na ongezeko la udahili vyuoni na mabadiliko mengine.

 Profesa Mgaya amesema kongamano wanalotajia kulifanya ni la saba ambalo linatarajia kufanyika Oktoba 1 hadi 2 mwaka huu mkoani Arusha. 

 Amesema katika  kongamano hilo lina malengo ya kuangalia jukumu la Taasisi za Elimu juu nchini kusaidia maendeleo uwezo kwa kuzingatia elimu inayotolewa, Kubainisha fursa muhimu amabazo taasisi ya elimu zinaweza kutumia pamoja na mkakati wa itakayowezesha ushirikiano madhubuti baina ya sekta binafsi ya elimu ya juu,Viwanda na wadau wengine wa kuleta mabadilko katika sekta ya elimu nchini.

NITAHAMASISHA UWEKEZAJI ZAIDI MUHEZA-BALOZI ADADI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Muheza
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapiduzi (CCM), katika jimbo la Muheza mkoani Tanga, Balozi Adadi Rajabu (Kulia akipokea fomu), amesema atapigana kufa na kupona kuingiza wawekezaji wilayani humo katika nyanja ya kilimo na utalii.

Akizungumza baada ya kunadiwa na mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli, Adadi amesema mjini hapa jana kwamba ataelekeza nguvu kubwa katika kuvutia wawekezaji ili kuiinua Muheza kiuchumi.

Magufuli, aliyemnadi Adadi kwa kumuita “tunu ya Wanamuheza”, alisema akichaguliwa na kuungwa mkono  Adadi ni mtu mwenye hazina ya  uzoefu adimu na mwenye kuaminiwa na watu na taasisi nyingi ndani na nje ya Tanzania.  Kwa safi hizo ahadi zake ni rahisi kutekelezeka na kuinua   maisha ya wananchi wa Muheza..

Adadi akieleza vipaumbele vyake na mkakati wake wa kuboresha maisha ya watu kiuchumi na kijamii,  aliahidi kupigania kukuza fursa za utalii na kuwepo kwa  viwanda vya kusindika muhogo na matunda, mazao yanayopatikana kwa wingi Muheza.

 Adadi,  ambaye ni mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai mstaafu na balozi mstaafu, alitaja vivutio vya utalii kuwa misitu na viumbehai katika milima ya Amani,na kuongeza kwamba atapigania uimarishaji wa barabara kutoka Pangani hadi Muheza.

Amesema machungwa yanazalishwa kwa wingi Muheza na mengi uharibika kwa kukosa soko la ndani na nje. “Hili lazima tulifanyie kazi,” aliahidi, na kuwataka wananchi wachape kazi kwani viwanda na masoko hudumu kwa kupokea mahitaji yasiyokatizwa kwa msimu mzima.

Muhogo na mtama ni mazao ya chakula ambayo Umoja wa Mataifa unahimiza yalimwe kwa wingi na kusindikwa ili kupambana na tatizo la njaa barani Afrika.

 Adadi amewasihi wananchi wa Muheza kuilinda amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kwani pasipo amani hata uchaguzi wenyewe unaweza kuingia dosari.

Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika tarehe 25 Octoba mwaka 2015

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU KATIKA UWAZI WA BAJETI KWA NCHI ZA A.MASHARIKI

$
0
0
 Meneja wa Program wa Haki Elimu,Godfrey Bonaventura akizungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti uliofanywa na International Budget Partinership leo jijini Dar es Salaam,Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu,John Kalage
Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa utoaji wa Uwazi wa Bajeti katika utafiti uliofanywa na Interntional Budget  Partinaship iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meneja Program wa Haki Elimu, Godfrey Boneventura (picha na Chalila Kibuda Globu ya Jamii)

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TANZANIA imekuwa ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki katika uwazi bajeti kwa wananchi kwa kupata alama 46.
 
Utafiti huu umefanywa  kwenye nchi 142 ambazo zimesaini kuingia katika uwazi wa bajeti kwa wananchi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Programu wa Haki Elimu,Godfrey Bonavetura amesema kutokana na Tanzania kupata alama 46 inatakiwa kutoa taarifa za bajeti kwa wakati.
 
Nchi ya Uganda nidio inayoongoza katika uwazi wa bajeti kwa kuwa na alama  ikifuatiwa na Kenya kwa kuwa na alama 48  hali ambayo inafanya Tanzania kuongeza kasi katika uwazi wa utoaji bajeti.
 
Amesema Tanzania ni nchi ya tatu kutokana na kutoa taarifa chache za bajeti na kutoa mara kwa mara inaondoa ufisadi kwani wananchi wana kuwa uaminifu wa serikali wa serikali yao kutokana na taarifa zinazopatikana katika bajeti.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA YA BIDHAA ZA CHINA 2015, DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa (wa tano kulia), akifurahi baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara ya Bidhaa za China 2015, uliofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine na maofisa biashara wa China na wadau wa masuala ya biashara.
 Hapa Katibu Uledi Mussa akitia saini wakati wa ufunguzi wa maonyesha hayo.
 Hapa akioneshwa bidhaa mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, akizungumza na wanahabari.

Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS) limesema  bidhaa zinazotoka china zina ubora huku likitoa mwito kwa wafanyabishara kutumia fursa ya kujifunza kupitia maonesho ya bidhaa za china.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Joseph Masikitiko,Mkurugenzi wa biashara Agnes Mneney alisema haiwekani kujua kma bidhaa zina ubora au la kwa kuangalia kwa macho.

Alisema TBS ndio waliopewa dhamana na Serikali ya kukangua ubora wa bidhaa zote za ndani na za nje kisha kubainisha kwa wananchi kama bidhaa zina ubora au ni hafifu kwa maslahi ya taifa.

 

''TBS ndio imepewa dhamana ya kudhibiti bidhaa zenye ubora kwa maslahi ya taifa kwahiyo watanzania wasipende kutoa hukumu kwa njia ya kukaangali kwa macho,''alisema.

Agnes alisema mtanzania anachotakiwa kufanya ni kuhahakikisha ananunua bidhaa ambazo zina nembo ya TBS kwasababu bidhaa zote sokoni zinatakiwa kuwa na viwango vya shirika hilo.

''Bidhaa za nchini China lazima ziwe na vuwango vya ubora vinavyotolewa TBS ili kuzingatia kiwango cha ubora katika soko la Tanzania,''alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa masuala ya biashara na uchuminchini China,Lin Zhiyong alisema maoyesho ni ya siku tatu ambapo zaidi ya wafanyabishara kutoka nchina 230 wameshawasili nchini.     

Akizungumzia ubora wa bidha zao,Zhiyong alisema kupitia udhibiti waTBS wafanyabishara wa china wameanza kuondoa bidhaa ambazo ni hafifu sokoni.

''Bidhaa hafifu zimeanza kuondolewa sokoni kwa takribani miezi mitatu iliyopita ili kuimarisha ushirikiano wetu na TBS  na mkakati wa wafanyabishara wa China ni kuhakikisha tunaondoa bidhaa zote hahifu ili kulinda bora,''alisema.

Kwa upende wake Katibu Mkuu wa viwanda na bishara,Uledi Mussa alisema Tanzania imekuwa na urafiki mkubwa wa masuala ya kiuchumi na China.

Alisema kupitia urafiki huo ni imani yake China itaisaidia Tanzania kujenga viwanda na kuisaidia Tanzania kuzalisha vitu vyenye ubora na kuviuza.

Mussa alisema Tanzania inaanda mpango wa kuanzisha viwandana kwamba dhamira ya wizara husika ni kuwawesha wafanyabishara wazawa kumiliki viwanda kwa maaendeleo ya nchi.

''Tumekuwa na mambo mengi lakini dhamira ya Serikali kwa miaka mitano inayokuja ni kujenga viwanda na kuwezesha wafanyabishara wazawa kuvimiliki,''alisema. 


Maonesho hayo ni ya nne tangu kuanza kuonyeshwa nchini ambayo yanaendelea kwa siku tatu katika viwanja vya Daimond Jubilee jijini Dar es Salaam.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

WAKULIMA ZAIDI YA 12,000 KUNUFAIKA NA MBEGU BORA ZA MAHINDI NA ALIZETI MKOANI

$
0
0
Baadhi ya wakuliwa wa mkoani Shinyanga, wakiwa na maofisa wa Agrics wakati wa mafunzo na uingiaji mkataba wa makubaliano yliofanyika Kijiji cha Ishololo, Wilaya ya Shinyanga Vijijini. Warsha hiyo iliongozwa na Lazaro Japhet (aliyesimama wa tatu kushoto mstari wa mbele. Zaidi ya wakulima 12,000 wanataraji kufaidika na mbegu za mahindi na alizeti kutoka Kampuni ya Agrics.
Mahindi yaliyooteshwa kisayansi na kampuni ya Agrics kwa lengo la kuthibitisha ubora wa mbegu zinazotolewa kwa wakulima wa kanda ya ziwa. Zaidi ya wakulima 12000 watanufaika na mbegu izo msimu huu. Matokeo ya vipimo yalisadifu ubora wa kampuni ya Agrics kwa kutoa asilimia 100% ya ubora.

Kufuatia msimu mpya wa kilimo unaotarajia kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics inatarajia kuwanufaisha wakulima 12,000 wa Shinyanga vijijini, Maswa na Meatu kwa kuwapatia mbegu bora za mahindi, alizeti pamoja na mbolea ili kuhakikisha kilimo biashara kinainuliwa na kuleta tija kwa mkulima. Mbegu hizo zitatolewa hivi karibuni ili kuhakikisha mkulima anakuwa na maandalizi ya uhakika msimu huu. Kampuni ya Agrics hutoa mbegu kwa mkopo nafuu unaolenga kumnufaisha mkulima kwa mazao mengi zaidi.

Pia Agrics ikishirikiana na viongozi wa serikali huwanufaisha wakulima kwa kuwapatia mafunzo katika ngazi tofauti za ukuaji wa mazao ili kuhakikisha mavuno yanasadifu malengo ya wakulima hao. 

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya Agrics, Meneja Miradi Bw. Charles Laswai alithibitisha ubora wa mradi huo wakati akikabidhi mikataba ya uchaguzi wa mbegu kwa wakulima. ‘’ Ni miaka mitano sasa tangu Agrics ianze kutoa mbegu bora kwa mkopo kwa wakulima wetu wa kanda ya ziwa.

Kwa sasa wakulima wameelewa zaidi umuhimu wa kilimo biashara. Mkulima anavuna zaidi ya asilimia arobaini kulinganisha na kabla ya kujiunga na mradi huu wa kukopeshwa mbegu na mbolea kwa ajili ya kilimo bora. Na kwa mwaka huu tunategemea mavuno mazuri zaidi kwani hali ya hewa itakuwa nzuri kutokana na vyanzo vya taarifa ya hali ya hewa nchini’’.

Wakulima wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa mikopo kwa ajili ya kilimo na ukosefu wa elimu juu ya kilimo bora chenye tija. Agrics ikiwa kama chachu ya mabadiliko kwa mkulima wa kanda ya ziwa, imekuwa ikiwakopesha mbegu na mbolea zilizothibitishwa kwa ubora, mkulima hutoa asilimia kumi wakati wa kuomba aina ya mbegu aitakayo na badae hutoa asilimia 15 wakati wa kukabidhiwa mbegu husika.

Mkulima hupewa nafasi ya kuwa huru na kusimamia kilimo chake huku akiendelea kupata mafunzo na ushauri kutoka kwa afisa miradi wa Agrics ili kuhakikisha malengo ya mkulima yanatimia na anazalisha kwa kiasi kikubwa. Mkulima humalizia asilimia 75% ya deni lake kwa awamu tatu zinazompa muda wa kutosha baada ya kuwa amevuna.

“Ni kampuni ya Agrics iliyoyabadilisha maisha yangu kufikia mafanikio haya niliyonayo. Kiujumla wamebadilisha maisha ya wakulima wa hapa kijijini na kutufanya tuuage umasikini. Nilikuwa nikivuna gunia nne katika hekari moja lakini kwa sasa navuna zaidi ya gunia kumi kulingana na muitikio wa mvua. Tangu kujiunga na Agrics nimewapeleka watoto watatu sekondari na ninamiliki pikipiki kutokana na mavuno yangu. Sijawahi kuishiwa chakula kwani huwa ninaweka SIMIYU NA SHINYANGA.

akiba ya kutosha kwa ajili ya familia yangu’’. Alieleza Bw. Steven Kanogu mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga vijijini wakati akipokea mkabataba wa mkopo wa mbegu na mbolea kwa ajili ya kilimo cha msimu huu.

Agrics Ltd ni kampuni ya kibiashara inayofanya kazi zake kwa kushirikiana na shirika la ICS. Agrics inawapa wakulima wadogo wa kanda ya ziwa nchini Tanzania na Kenya fursa ya kujipatia mbegu bora na za kisasa kwa mkopo nafuu unaolipwa kwa awamu zinazompa mkulima nafasi nzuri ya kujiendeleza. Pia Agrics inahakikisha akiba ya chakula kwa mkulima ni lazima kwa ajili ya kupunguza njaa kwa wakulima. Kwa mawasiliano Zaidi tembelea tovuti yetu www.agrics.org.

MFUMO WA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA VITUO VYA AFYA TANZANIA BARA WAZINDULIWA LEO JIJI DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donani Mmbando  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya  Mfumo unahifadhi na kutoa taarifa za zituo vya Afya kituo tangu kinapojengwa, atakikifunguliwa na hata kinapofungwa, leo Jjijini Dar es salaam.
 Wanahabari wa kimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Donani Mmbando leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donani Mmbando akifafanua jambo leo Jjijini Dar es salaam.
 
 Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Hermes Rulagirwa towa ufafanuzi kwa waandi wa habari juu ya mfumo wa kuhifadhi taarifa za vituo vya huduma za afya vya serikali na binafsi leo jijini Dar es salaam.
 SehemU ya wananchi walio hudhulia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donani Mmbando  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbail leo Jjijini Dar es salaam .
(Picha na Emmanuel Massaka)  

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imetengeneza mfumo wa kuhifadhi taarifa za vituo vya huduma za afya vya serikali na binafsi “Health Facility Registry (HFR) System”.
 
Mfumo unahifadhi na kutoa taarifa za kituo tangu kinapojengwa, ili kimejengwa, kufunguliwa na hata kinapofungwa. Zaidi tunapata taarifa ifutayo;-

Idadi ya vituo Tanzania bara, taarifa za kijiografia (yaani“Geographic coordinates), mahali kituo kilipo, kwa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Mtaa/kijiji, umiliki, hali ya utendaji kazi yaani “operation status” na huduma inayotolewa na kituo. 

Kutokana na kukamilika kwa mfumo huu, naagiza Taasisi zetu kama NHIF, MSD, NACP, TFDA pamoja na wadau wengine waanze kutumia mfumo huu.
Mfumo huu umetengnezwa kwa ufadhiri wa mfuko wa ukimwi kifua kikuu  (Global fund) CDC, RTI Intenational. Pia natambua Ushiriki wa wadau wetu, University Computing Centre, Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Aidha mfumo huu umetengenezwa kwa kushirikisha idala zote za Wizara na Taasisi zake. Hivyo ni mfumo shirikiskishi na una ownership.

Nawapongeza pia wajumbe wa kamati ya Afya za Mikoa na Wilaya, kwa kufanikisha, ukamilikaji wa mfumo huu.

Naagiza kwenu nyinyi waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kuhakikisha mnasimamia kwa kuingiza taarifa kwa wakati.

Baada ya kusema hayo, natangaza kuwa mfumo huu wa mfumo wa utunzaji wa taarifa za vituo vya afya tanzania bara, umezinduliwa rasmi.

TAARIFA KWA UMMA:MATAPELI KUTUMIA JINA LA KAMPUNI

$
0
0
 KAMPUNI YA STAMIGOLD MGODI WA BIHARAMULO
Kufuatia wimbi la Matapeli kutumia jina la kampuni wakidai kuwa wao ni wafanyakazi wa STAMIGOLD wenye uwezo wa kutoa ajira katika mgodi wa Biharamulo , kampuni ingependa kuchukua fursa hii kuutahadharisha Umma wa Watanzania kama ifuatavyo:

1. Nafasi zote za ajira zilizopo au zinazotokea katika kampuni hutangazwa kupitia magazeti ya Serikali hususani Daily news.

2. Kampuni haina utaratibu wa kufanya usaili (Interview) kwa njia ya simu.
3. Maeneo rasmi ya kufanyia usaili (Interview) ni mgodini Biharamulo na mara chache katika ofisi zetu zilizopo katika jengo la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es salaam.

4. Kampuni haina utaratibu wa kutoza malipo yoyote kwa ajili ya usaili au kupata nafasi ya ajira.

5. Kampuni haina makubaliano na mtu au wakala wa ajira yeyote (recruitment agent) katika zoezi la kuajiri.

6. Anuani rasmi ya barua pepe itumikayo kupokea maombi ya nafasi za kazi pale zinapotangazwa ni hr.biharamulo@stamigold.co.tz
Tunawaomba Watanzania wote kuwa macho na matapeli hawa wanaopigia watu simu na kujinadi kuwa wanaweza kuwapatia ajira katika kampuni ya STAMIGOLD.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano
STAMIGOLD Biharamulo
Plot. No. 417/418 UN Road
S.L.P 78508 Dar es Salaam.
Email: info@stamigold.co.tz Website: www.stamigold.co.tz

MABALOZI MBALIMBALI WAZUNGUMZA KUHUSU MAJUKUMU YAO KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu ujao, pamoja na jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru na haki kwa vyama vyote.
Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (kushoto) wakimsikiliza Mheshimiwa Waziri.
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma, akiwatambulisha Mabalozi waliowasili nchini hivi karibuni ambao ni mara yao ya kwanza kuhudhuria Kikao cha aina hii, Wizara ya Mambo ya Nje. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye pia alikua muendeshaji wa mkutano huo Bi. Mindi Kasiga, akiratibu kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao hicho. 
Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanga Dennis Mseleku akiuliza swali katika mkutano huo.
Balozi wa Namibia hapa nchini Mhe. Japhet Isaack, akiuliza swali katika mkutano huo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akiuliza swali katika mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), akijibu Maswali ya Waheshimiwa Mabalozi, kushoto kwa Mhe. Waziri ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini Mhe. Juma Khalifan Mpango, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (kulia kwa Mhe. Waziri) na Mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.

Baadhi ya Mabalozi wakisikiliza majibu yanayotolewa na Mhe. Waziri Membe katika mkutano huo.

Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Paulo Kabale (kulia), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara hiyo Bw. Abisai Mathias (katikati), na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa wizara hiyo, Bw. Lucas Suka wakibadilishana mawazo baada ya mkutano kuisha.
 Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini Mhe. Juma Khalfan Mpango, akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, ambaye pia alikua muendeshaji wa mkutano huo.
 (pichani juu na chini) Baadhi ya  Mabalozi wakibadilishana mawazo na kusalimiana muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza. 
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi.
Waheshimiwa Mabalozi wakibadilishana mawazo.
Mkutano ukiendelea
 Mkutano ukiendelea....
Mhe. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo kumalizika.
Picha ya pamoja.
PICHA NA REUBEN MCHOME.

TANGAZO LA SHUKRANI

$
0
0
Familia ya Bwana na Bibi Charles Yanga wa Tabata Chang'ombe, Dar es salaam, wanapenda kutoa shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshirikiana nao katika mazishi ya mtoto wao mpendwa Abel Charles Yanga aliyefariki tarehe 22 July 2015 na kuzikwa tarehe 25 July 2015 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es salaam. Familia inakukaribisha kwenye Misa ya shukurani Jumamosi tarehe 12 Sep. 2015 saa  5.00 asubuhi nyumbani Tabata Chang'ombe. Baada ya Misa tutashirikiana chakula cha mchana. Karibuni sana.
Kwa mawasiliano zaidi simu namba 
0653 013 211

UNESCO WAKABIDHI KITABU CHA MAFUNZO YA TEHAMA KWA SERIKALI NCHINI

$
0
0
IMG_8554
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekabidhi rasmi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyohudhuriwa na wadau walioshiriki katika uandazi wa kitabu hicho, ikiwamo serikali ya China.

Kitabu hicho ni matokea ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
IMG_8742
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China.

Akipokea kitabu hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome, Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa ameishukuru UNESCO na serikali ya China ya kuwezesha upitiaji wa kitabu hicho kinachotoa mwelekeo wa mafunzo ili kuambatana na maagizo ya viwango yaliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Alisema kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa utekelezaji wa elimu ya Tehama kwa kuzingatia uwezo na weledi katika ufundishaji.

Kamishina huyo amesema kwamba kazi ya kuangalia viwango hivyo iliyofanywa kutokana na Mfuko wa China na Unesco kwenye moduli sita za uelewa na elimu ya teknolojia kwenye Tehama.

Alishukuru timu iliyopitia viwango hivyo na kusema serikali ya Tanzania inashukuru msaada huo wa Unesco na serikali ya China kwa kufanikisha kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.
 
IMG_8684
Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun akitoa salamu za Balozi wa China nchini kwenye hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Ni matumaini yake kwamba sasa Tanzania ina kielelezo cha kufuatia katika kufanikisha maandalizi ya walimu wenye weledi na uwezo katika kufundisha na kutumia teknolojia ya Tehama.

Naye Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza kabla ya kukabidhi kitabu hicho alisema UNESCO itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuimarisha elimu ya Tehama ili kufungua njia pana zaidi ya maendeleo.

Aidha ameikumbusha serikali ya Tanzania kutumia vyema kitabu hicho katika kuhakikisha kwamba mafunzo ya kariba ya hali ya juu yanatolewa ili kuwa na mafanikio makubwa katika sekta zote za elimu na teknolojia.

Alisema kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa hatua kwa hatua katika mafunzo ya Tehama na namna ya kufanikisha katika kumwelimisha mwanafunzi na vitu vinavyoweza kufanywa ili kuhakikisha kwamba elimu sahihi inawafikia wahusika.

Naye Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing kupitia kwa Ofisa wa Ubalozi Liu Yun aliyefika kwenye hafla hiyo, alisema kwamba serikali ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha elimu ya Tehama nchini.

Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alishawahi kusikika akisema utoaji wa mwongozo huo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa katika mradi.
IMG_8806
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akielezea maandalizi na hatua walizopitia katika uandaaji wa kitabu hicho mpaka kukamilika kwa wadau wa sekta ya elimu walioshiriki hafla hiyo.
IMG_8817
Meza kuu ikimpongeza Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (hayupo pichani).
IMG_8926
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akimkabidhi Kamishna wa Elimu, Prof.Eustella Bhalalusesa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China. Mradi huo una lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
IMG_8931
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa (walioketi kushoto) na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki kuandaa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wakati hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Mradi huo una lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
IMG_8734
Pichani juu na chini baadhi ya wadau wa sekta ya elimu na maafisa wa Shirika la UNESCO waliohudhuria halfa ya makabidhiano ya mwongozo wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye hoteli ya Protea Courtyard.
IMG_8811IMG_8743IMG_8510
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akijadiliana jambo na Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
IMG_8766
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Elimu nchini mara baada kupokea kitabu cha mwongozo wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wakati hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho kilichokabidhiwa kwa Kamishna wa Elimu nchini katika hoteli ya Protea Courtyard Hotel jijini Dar es Salaam.

MAFANIKIO SIYO AJALI SEHEMU YA KWANZA.

$
0
0
WATU wengi wanafikiri mafanikio ni kitu ambacho kinatokea tuu kama ajali lakini mafanikio sio ajali wala sio bahati mafanikio ni mipango dhahiri ambayo inapangwa na mtu anayeyataka na ayenuia kutoka katika vilindi vya moyoni mwake kwamba anataka kutoka katika sehemu moja kwenye maisha ambayo inakuwa ni duni na kwenda sehemu nyingine ambayo ni ya hadhi nzuri.

Wengi wamekuwa wakijidanganya kwamba ipo siku moja watafanikiwa (watatoboa)lakini hawana mpango wowote wa kuwawezesha kufanikiwa katika iyo siku moja na nataka niwaambie kwamba iyo siku moja haitakaa itokee kama hauna mpango dhahiri wa kupata unachokitaka katika maisha yako.

Unatakiwa kuwa na picha halisi ya kitu unachokitaka kwanza ndipo uende ukakitafute, kumbuka kumiliki kunaanzia kwenye akili kwanza acha kusema nahitaji nyumba nzuri,gari zuri,biashara nzuri, wakati hujapata picha halisi katika akili yako kile unachokihitaji unataka kiweje. Vijana wengi wamekuwa wakimaliza chuo Kikuu na kusema nipo tayari kufanya chochote huu ni ujinga na kutokuwa na maono hivi kweli kama upo tayari kufanya chochote nkikuambia ukachimbe vyoo utachimba? Be definate (unataka nini kwanza) na hicho unachokitaka hakikisha una picha yake kwenye akili yako jinsi kitakavyokuwa ndipo unaanza jitihada zote zitakazokupelekea kupata kile unachohitaji.

Jambo hili limekuwa likisumbua watu wengi sana la kukosa  picha halisi ya kile wanaachokihitaji na hivyo wamejikuta wakifanya vitu ambavyo hawavihitaji zikiwemo kazi wanazozifanya na kadhalika. Na hii pia ni mpaka kwenye kuoa/kuolewa kuwa na picha halisi ya mtu unaemtaka na sifa zake unataka aweje ndipo unapomuomba Mwenyezi Mungu sasa wewe unatafuta bila kujua unachokitafuta unataka kiweje? Weka hili katika akili yako litakusaidia sana.

Pindi utakapopata picha halisi ya kile unachokihitaji jicho lako lisiangalie nyuma, achana na hao marafiki wanaokuambia haiwezekani, maadamu akili yako imeweza kuwa na picha ya hiko kitu inamaanisha unao uwezo wa kukimiliki, watu wengi wameacha kufuata ndoto zao kwa kusikiliza maoni ya watu wengine ambao wamewakatisha tamaa na wakaacha kufanya kile walichokuwa wanataka kufanya.Hili naomba lisitokee kwako kabisa hakuna anaejua kile ambacho una uwezo wa kukifanya hata mzazi wako hajui unao uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu ni kiasi cha wewe kujiamini na kutenda tuu.

Anza kupambana fanya juhudi zote zitakazokupelekea kupata kile ulichonacho katika akili yako kama ni kuna masomo ya ziada inakubidi ukasome hakikisha unasoma hayo masomo, kama kuna watu fulani unatakiwa uwaone hakikisha unawaona hao watu kwa sababu siri ni hii huwezi kufanikiwa katika maisha haya pasipo msaada wa watu/mtu fulani, niliwahi kusema hivi na ninasema tena leo kwa mara nyingine achana na huu msemo nitafanikiwa mwenyewe (natoboa )itakuchukua muda mrefu na pia utatumia nguvu nyingi sana. 

Ili kufanikiwa inakubidi SAA zingine utafute waliofanikiwa wakushike mkono. Mfano hebu jenga taswira kwenye akili yako kuna watu wawili wote wamekaa chini kwenye sakafu ninachotaka hapa ni kwamba mmoja amuinue mwingine aliekaa nae kwa kumvuta mkono,Je hilo zoezi litawezekana wakati wote wamekaa chini? 

Bila shaka haliwezekani kadhalika na kwenye mafanikio huwezi ukainuliwa na mtu ambaye yupo sawa kiuwezo wa kufikiri,kiutendaji,na kiuchumi kama wewe tafuta aliekuzidi katika nyanja hizo au ambaye anaweza kukushauri,au ambaye tayari kashasimama ndipo atakapokunyooshea mkono na kukuvuta kisha utainuka.

IMEANDALIWA NA HUMPHREY MAKUNDI NA ALLARD MINJA
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images