Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA MJINI IFAKARA JIONI YA LEO


Ni marufuku watoto kumiliki leseni za madini

$
0
0
 Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Masolla (aliyesimama), akifungua semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Wengine pichani ni wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Kutoka kushoto ni Placid Kabyemera, Juma Masoud, Mhandisi Nuru Shabani, Mhandisi Gabriel Senge na Tantao Tantao. 

 Sehemu ya washiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao iliyofanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Semina hiyo ni mwendelezo wa zoezi la utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchi nzima kuhusu matumizi ya huduma hiyo mpya.

 Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa Wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 5, mwaka huu mjini Singida.






 Washiriki mbalimbali wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao, wakiuliza maswali wakati wa semina hiyo. Semina ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu.

Viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mkoani Singida walioshiriki katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao. Wa tatu kutoka kulia (Waliokaa kwenye viti) ni Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati – Singida na Kulia kwake ni Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani. Semina ilifanyika Septemba 5, mwaka huu.


WANANCHI WAFUNGA BARABARA KIJIJI CHA LUPIRO-IFAKARA WAKITAKA KUMUONA MAGUFULI

WAJASILIAMALI WAHIMIZWA KUTUMIA INTERNET KUTANGAZA BIASHARA ZAO

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Zanzibar, Bw. Salim Maulidi Salim akimkabidhi picha ya mlango wa asili ya Zanzibar, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi jijini Birmingham, Bw. Prince Kateka II ikiwa ni ishara ya kukaribishwa Zanzibar.
Wafanyabiashara wamehimizwa kutumia mtandao wa internet kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa kwa kuwa njia hiyo ni nafuu na inawafikiwa watu wengi kwa haraka. Hayo yalibainishwa na Bw. Dickson Inachee, Raia wa Uganda alipokuwa anatoa mada katika kongamano la siku mbili la Watanzania wanaoishi Uingereza lililomalizika jijini Birmingham siku ya Jumamosi tarehe 05 Septemba 2015. 
Bw. Inachee alieleza kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya watu milioni 9.3 wanatumia internet nchini Tanzania. Kati ya hao watu milioni 2.4 wanatumia mtandao wa face book, hivyo ukitangaza katika face book, tangazo lako litawafakia watu wengi kuliko kutumia vyombo vilivyozoeleka kama magazeti. 
Aliendelea kueleza kuwa tangazo katika face book linatozwa Dola moja ya Marekani na kwa Tanzania litawafikia watu milioni 2.4 lakini tangazo hilo hilo ukilitoa katika gazeti linalopendwa sana nchini Tanzania utatakiwa kulipa Dola 300 na litawafikia watu elfu 50 tu. 

Bw. Inachee alimalizia mada yake kwa kusisitiza kuwa, endapo wajasiliamali nchini Tanzania wanataka kufanya biashara kwa kutumia mbinu mpya za kibiashara, basi hawana budi kutumia internet kutangaza bidhaa zao kwa kuwa njia hiyo itawaondolea mzigo wa kulipa fedha nyingi katika vyombo vilivyozoeleka sanjari na kuwafikia watu wengi zaidi.
Bw. Anthony Chaula akiwasilisha mada
Katika hatua nyingine, wanadiaspora walioshiriki kongamano hilo, wameridhishwa na hatua ya Serikali ya kuwapa hadhi maalum katika Katiba inayopendekezwa.

 Akiwasilisha mada katika kongamano hilo, Bw. Anthony, Chaula kutoka Idara ya Uhamiaji alisema kuwa Katiba inayopendekezwa itakapopitishwa, wanadiaspora watapewa hadhi maalum tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaonekana kama wageni wengine.
Wakati wa kongamano hilo, baadhi ya Watanzania wanaoishi Uingereza walitumia fursa hiyo kutangaza shughuli zao za kibunifu wanazofanya katika nchi hiyo. Bw, Ayoub Mzee alizindua rasmi progaramu yake inayoitwa AITV APP. Programu hiyo inamwezesha mteja, kwa kutumia simu ya mkononi au kifaa kingine chenye internet kuangalia vituo takriban vyote vya televisheni vya Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa gharama ya Dola za Marekani sita kwa mwezi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo yas Nje, Balozi Liberata Mulamula aksalimiana na Bw. Ayoub Mzee kabla ya kuzindua programu ya AITV APP.
Mtanzania mwingine Bw. Mediremtula ameanzisha kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa tablet. Anasema aina ya tablet anayotengeneza inafanya vizuri kibiashara katika nchi za Uingereza na Urusi na hivi sasa yupo katika mchakato wa kutengeneza aina nyingine ya tablet kwa ajili ya Tanzania.

 
Katika masuala ya sanaa hasa ya uigizaji wa filamu, Watanzania wa Uingereza hawakuachwa nyuma. Kuna Watanzania wamecheza filamu ijulikanayo Goingbongo. Filamu hiyo imeigizwa katika viwango vya kimataifa na walioafanikiwa kuiangalia wamethibitisha kuwa ni ya kimataifa kweli.
Kongamano hilo lilifungwa rasmi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Zanzibar, Bw. Salim Maulidi Salim ambaye alisisitiza umuhimu wa wanadiaspora kuwekeza nyumbani kwa madhumuni ya kukuza uchumi na kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa jamaa zao.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe akitoa cheti cha kutambua mchasngo wa mmoja wa wadhamini wa kongamano. Na Ally Kondo, Birmingham

NI MARUFUKU WATOTO KUMILIKI LESENI ZA MADINI

$
0
0
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Masolla (aliyesimama), akifungua semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Wengine pichani ni wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Kutoka kushoto ni Placid Kabyemera, Juma Masoud, Mhandisi Nuru Shabani, Mhandisi Gabriel Senge na Tantao Tantao.
 Sehemu ya washiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao iliyofanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Semina hiyo ni mwendelezo wa zoezi la utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchi nzima kuhusu matumizi ya huduma hiyo mpya.

Na Veronica Simba - Singida
Imeelezwa kuwa ni marufuku kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa kama wabia wa umiliki wa leseni za madini za aina yoyote hapa nchini.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo wa madini mkoani Singida kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao ujulikanao kama OMCTP (Online Mining Cadastre Transactional Portal.)

 “Sheria hairuhusu kutoa leseni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kwa wale watakaobainika kutoa taarifa zisizo za kweli kwa kuwaandikisha watoto walio chini ya umri husika kama wabia wa umiliki wa leseni za madini, watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Mhandisi Shabani.

Aidha, Mhandisi Shabani aliwataka washiriki wa semina hiyo na watanzania wote kwa ujumla kufahamu kuwa ni Wizara ya Nishati na Madini pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutoa leseni za madini za aina zote hapa nchini.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya washiriki wa semina kuuliza iwapo kuna mamlaka nyingine nchini zinazoruhusiwa kisheria kutoa leseni za madini.

“Kuna baadhi ya watu au vikundi vya watu au taasisi ambazo zimekuwa zikiingilia zoezi la utoaji wa leseni za madini kwa baadhi ya waombaji nchini. Naamini wanafanya hivyo kwa kutokujua sheria, hivyo ni vyema watu wote wafahamu kuwa hakuna mamlaka nyingine hapa nchini yenye ruhusa ya kutoa leseni za madini kisheria isipokuwa Wizara ya Nishati na Madini pekee,” alisisitiza.

Mhandisi Shabani aliwataka wananchi hasa wamiliki halali wa leseni za madini wanaokumbana na matatizo ya kutotendewa haki kwa kuzuiliwa kuendesha shughuli zao katika maeneo yao kisheria, kutoa taarifa kwa ofisi za madini zilizopo karibu naoi li waweze kupatiwa msaada kwa kufuata sheria.

Pia, aliwaasa wachimbaji madini wadogo na wamiliki wa leseni pamoja na wananchi wote hususani viongozi wa vijiji, halmashauri na taasisi mbalimbali, kuisoma na kuifahamu Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ili kuepusha migogoro mbalimbali inayotokea kuhusiana na shughuli za uchimbaji wa madini.

Semina iliyofanyika Singida kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao, ni mwendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima chini ya Wizara ya Nishati na Madini kwa lengo la kuongeza uwazi na kuboresha zaidi huduma za sekta ya madini.

Washiriki mbalimbali wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao, wakiuliza maswali wakati wa semina hiyo. Semina ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu.
 Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa Wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 5, mwaka huu mjini Singida.
Viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mkoani Singida walioshiriki katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao. Wa tatu kutoka kulia (Waliokaa kwenye viti) ni Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati – Singida na Kulia kwake ni Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani. Semina ilifanyika Septemba 5, mwaka huu.

MAONESHO YA UZURI, MAVAZI, SANAA NA UREMBO.

$
0
0
 Mwandishi F Macha na msanii wa ACD Arts toka Uganda, Steve Kasamba. Picha na JJ Adamson wa Africans in London TV.
 Mohammed Juma toka Mombasa akishughulika na nyama choma, ndizi mzuzu za kuoka.
 Picha ya pamoja (selfie). Kenya na Tanzania
 Mtayarishaji wa maonesho, msanii na mwanahabari, Lydia Olet, akiwa na wacheza sarakasi toka Ghana.
 kenya Lydia Makale akiwa na mwanarapu maarufu wa London, Septimus Prime.
 
 Mwanahabari mkongwe , Deo Kamugisha (wa kwanza kulia) akiwa na Mtanzania Abdallah ( wa kwanza kushoto)  na mwenzake toka Uganda
 Fulana iliyotukuza kujifunza Kiswahili
Bango la kutangaza tamasha hilo la siku moja

ACACIA YAIDHAMINI STEND UNITED KWA KITITA CHA BILLIONI MOJA

$
0
0
Mwenyekiti wa stand united Amani Vicent (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini wa timu hiyo na Makamu wa rais wa ACACIA anaeshugulikia masuala ya Kampuni, Deo Mwanyika mara baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali na wadhamini wao kampuni ya ACACIA.
Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakiwa na baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Acacia ambao ni wadhamini wa timu hiyo muda mfupi mara baada ya kuzindua rasmi jezi za timu hiyo zitakazotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza tarehe 12.09.2015.
Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom wakati walipokuwa wakizionyesha kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(Hayupo pichani wakati wa utiaji saini wa mkataba wa timu hiyo na kampuni ya ACACIA.

 
Baadhi ya Viongozi wa Acacia kutoka kulia ni Alex Lugendo (Meneja wa Uhusiano na Serikali wa ACACIA), Elias Kastra – (Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa Bulyanhulu)na Nector Foya - (Meneja wa Mawasiliano wa ACACIA) wakifuatilia mchezo kati ya Stend United na Olympic Stars ya Burundi Mchezo uliopigwa katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Baadhi ya washabiki wa Stend United waliohudhuria wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kusherekea udhamini wao na kampuni ya Uchimbaji wa madini ya ACACIA.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi yao itakayokuwa ikitumika kwa michezo ya uwanja wa nyumbani na ile ya ugenini wakati wa msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.

RC wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akipokea jezi ya timu ya stend United kutoka kwa makamu wa rais wa ACACI, Deo Mwanyika.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mguu mkoa wa Shinyanga Benasta Lugola akipokea jezi ya timu ya stend United kutoka kwa makamu wa rais wa ACACI, Deo Mwanyika.
Mashabiki wa Stend United waliojitokeza kusherekea udhamini wa timu yao katika uwanja wa Kambarage.
Wachezaji wa Stend United wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo.
Timu za Olympic Stars yenye jezi ya bluu na timu ya Stand united yenye jezi ya rangi ya dhahabu zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo wao wa kirafiki.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na Kapteini wa timu ya Olympic Stars ya Burundi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na kapteni wa timu ya Stand United Nassoro Masoud “CHORO”
Makamu wa rais wa Acacia anaeshughulikia masuala ya Kampuni Deo Mwanyika akisalimiana na kapteni wa timu ya Stand United Nassoro Masoud “CHORO” wakati timu hiyo ilipoumana na Olympic Stars ya Burundi.
Kikosi cha Stend United Kilichoshiriki mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya Olympic Stars ya Burundi katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga. Mchezo huo uliisha kwa ushindi kwa timu ya Stend United Kushinda 1-0.
Kikosi cha Olympic Stars cha nchini Burundi kilichochuana vikali na Stend United ya Shinyanga Tanzania.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini  aliyekuwa Shinyanga.
 KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita 2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.
Udhamini wa ACACIA katika misimu hii miwili ya ligi kuu itasaidia katika kuifanya timu ya Stand United iweze kufanya vizuri katika michezo yake, pamoja na kusaidia katika kuboresha programu mbalimbali za timu na kuendeleza vipaji pamoja na masuala ya Utawala.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Makamu wa rais wa Acacia aneshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, amesema  “Kwa takriban mwaka mmoja, tumekua tukifanya kazi pamoja na Stand United. Kwa muda huo tulianzisha mchakato wa kutambua namna nzuri ya kuboresha ushirikiano wetu ili kunufaisha watu wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bwana Deo amesema Msimu uliopita uliwapatia fursa nzuri ya kushuhudia uwezo wa timu hiyo hasa ukizingatia ilikua mara yao ya kwanza kushiriki ligi kuu, “Baada ya tathmini ya kina, tunadhani huu ni muda muafaka wa sisi kusaini makubaliano au mkataba wa kuidhamini na kufanya kazi pamoja ya kuikuza timu hii ya nyumbani maarufu kama “Chama la wana”.
Hivyo, Leo, Acacia tunasaini mkataba na timu ya Stand United kwa udhamini wa misimu miwili ya ligi kuu, wenye thamani ya Shilingi bilioni moja. Udhamini huu unajuamuisha shughuli za uendeshaji wa timu, kuboresha uongozi na kukuza vipaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent, amesema udhamini huo wa miaka miwili utakuwa chachu kwa timu yake kufanya vizuri katika ligi kuu, “Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi ya nane na kipindi hicho hatukuwa na fedha ya kutosha kuendesha timu, lakini kwa udhamini tulioupata kutoka kwa ndugu zetu wa Acacia vijana wetu safari hii watafanya vizuri zaidi.
Kampuni ya Acacia ni kampuni inayoongoza kwa shughuli za uchimbaji wa madini hapa Tanzania huku ikiwa na Migodi mitatu katika kanda ya ziwa, kupitia mradi wa “Acacia Maendeleo Fund” ambao ndio pia umetoa udhamini wa timu ya Stend umekuwa pia ukitekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Jamii hapa nchi huku kampuni hiyo ikieleza kuwa dhamira yake ni kuendelea kufanya kazi na Jamii zinazowazunguka katika kuwaletea Maendeleo wenyeji.

MAMBO 10 MUHIMU ILI SHERIA YA MAKOSA YA KIMTANDAO YASIKUKAMATE.

$
0
0
Sheria ya mitandao iliyoaanza kutumika rasmi tarehe 1 septemba 2015. 
 1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao

2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao

3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)

4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii

5. Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu

6. Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu

7. Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu

8. Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu

9. Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini

10. Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu

Hukumu
Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika (au vyote!)

VIONGOZI WA TAASISI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI MTAALA WA KUFUNDISHIA ‘UJASIRIAMALI USIOATHIRI MAZINGIRA’

$
0
0
Viongozi wa taasisi za vijana kutoka kwenye nchini sita wamekutana mjini Bagamoyo kujadili na kuandaa mtaala utakaotumika kuwafundisha vijana namna ya kufanya ujasiliamali usioathiri mazingira “Green Entrepreneurship”.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO), umewashirikisha viongozi wa taasisi za vijana kutoka Slovenia, Italia, Nepal, Ureno, Argentina na wenyeji Tanzania walipata fursa ya kujifunza namna ya uzalishaji wa nishati mbadala isiyoathiri mazingira.
Shukuru Meena, Mratibu wa miradi ya nishati kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO).
 Picha ya pamoja wakati viongozi hao walipotembelea TaTEDO.
Chris Ndallo (kushoto), Mtendaji Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Vijana TYCEN akijadiliana jambo na baadhi ya watumishi wa TaTEDO.
Viongozi wa taasisi za vijana, wakitazama baadhi ya miradi inayoendeshwa na TaTEDO wakati walipotembelea ofisi za shirika hilo.

VIONGOZI WA TAASISI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI MTAALA WA KUFUNDISHIA ‘UJASIRIAMALI USIOATHIRI MAZINGIRA’

$
0
0
Viongozi wa taasisi za vijana kutoka kwenye nchini sita wamekutana mjini Bagamoyo kujadili na kuandaa mtaala utakaotumika kuwafundisha vijana namna ya kufanya ujasiliamali usioathiri mazingira “Green Entrepreneurship”.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO), umewashirikisha viongozi wa taasisi za vijana kutoka Slovenia, Italia, Nepal, Ureno, Argentina na wenyeji Tanzania walipata fursa ya kujifunza namna ya uzalishaji wa nishati mbadala isiyoathiri mazingira.
Shukuru Meena, Mratibu wa miradi ya nishati kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO).
 Picha ya pamoja wakati viongozi hao walipotembelea TaTEDO.
Chris Ndallo (kushoto), Mtendaji Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Vijana TYCEN akijadiliana jambo na baadhi ya watumishi wa TaTEDO.
Viongozi wa taasisi za vijana, wakitazama baadhi ya miradi inayoendeshwa na TaTEDO wakati walipotembelea ofisi za shirika hilo.

FM ACADEMIA WADONDOSHA SHOW YA NGUVU JIJINI MBEYA CHINI YA UDHAMINI YA KINYWAJI CHA K-VANT GIN

$
0
0
Wanamuziki wa Bendi ya Fm Academia 'Wazee wa Ngwasuma' wakitoa burudani kwa mashabiki wao siku ya uzinduzi wa Hotel ya Mfikemo Sae jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.Picha Elvis Kimambo Jamiimojablog
Mashabiki na wadau wa Fm Academia wakiserebuka katika onyesho hilo.
Mkurugenzi wa Hotel ya Mfikemo Ndugu Lwitiko Mwandembele (katikati) Jofrey Ananiah kulia na wengine wakifurahia jambo siku ya uzinduzi wa hotel hiyo ambapo kuliambatana na onyesho la Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'

Meneja Mauzo wa K-Vant Gin Kanda za Nyanda za Juu Kusini Ndugu Lisungu Kipiga pasi akiwa tayari kutoa huduma kwa wateja wake .

 
Wadau wa burudani ,Pesi,Jofrey Ananiah ,Brand Nelson ,Kosima Patrick

ELIMU YA TANZANIA NI BORA, ASEMA JK

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete amesema madai kuwa elimu inayotolewa Tanzania ni duni ni potofu kwani wahitimu wake wanakubalika duniani.

Akihutubia Mkutano Mkuu wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema badala yake, tatizo liko kwenye kuwaandaa wahitimu kukidhi matakwa ya soko la ajira la ndani na la kimataifa.

“Elimu yetu ni bora na inakubalika popote duniani...wahitimu wanaweza kufanya kazi katika nchi yoyote, kinachotakiwa ni kuwapatia ujuzi wa kutosha kukidhi matakwa ya soko la ajira,” Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo aliwaambia wadau wa mkutano huo toka sekta ya umma na binafasi ambao hutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo.

Takwimu zinaonyesha kwamba vijana wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka nchini ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 na wanapigania nafasi za ajira zisizozidi 60,000 katika sekta ya umma na nafasi takribani 300,000 katika sekta binafsi.

Dkt. Kikwete alisema serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuvutia wawekezaji na kuomba mchango wa kila mdau kutumia fursa na raslimali zilizopo nchini kuzalisha mali na kuongeza ajira katika sekta ya umma na sekta binafsi.

Rais aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kila anayestahili kulipa kodi afanye hivyo na kusisitiza kuwa “serikali haiko tayari kuona watu wanakwepa kulipa kodi.”

Akitoa mfano alisema kama wadau wa sekta ya usafiri wa ndege wanaona kodi wanazotozwa ni kubwa ni vyema wakakaa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakubaliane lakini siyo kuchukua uamuzi wa kutolipa kodi.

Kuhusiana na mapambano ya rushwa alisema Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB) ijidhatiti vya kutosha kwa weledi na kwa mujibu wa sheria ili uwepo ushahidi wa kuiridhisha mahakama kumtia hatiani mshitakiwa.

“Mnapokwenda mahakamani mkashidwa mara kwa mara, zoezi hili la kupambana na kuzuia rushwa halitofanikiwa,” alieleza.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mali Asili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru alisema ingawa utalii unazidi kuimarika na kuchangia pato la taifa,  unakumbwa na tatizo la ujangili unaoangamiza tembo na faru.

Katika kukabiliana na tatizo hilo, alisema vifaa na askari vitaongezwa na kuwa patajengwa minara ya kuimarisha ulinzi katika mbuga za Serengeti na Ruaha.

Aliwataka wananchi kutochunga mifugo katika mbuga hizo kwani serikali haitoruhusu vurugu na uharibifu unaofanywa katika mbuga za wanyama uendelee.

DALADALA LAACHA NJIA NA KUPARAMIA GENGE NA BAJAJ MAENEO YA KITUNDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

$
0
0
 Wananchi wakiangalia ajali ya daladala lenye namba za usajili T 456 BVT lililoacha njia kutokana na mwendokasi na kuparamia genge na bajaj yenye namba MC 611 ADC, maeneo ya Kitunda relini barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam leo asubuhi. Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa daladala kukimbilia abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
 wananchi wakiangalia ajali hiyo.
 Daladala hilo likiwa ndani ya genge baada ya kuacha njia.
Bajaj namba MC 611 ADC, likiwa kanda ya daladala hilo baada ya kugongwa. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

BI. SAMIA SULUHU AHAIDI KUDHIBITI WIZI WA DAWA HOSPITALI ZA SERIKALI

$
0
0
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali.Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.

 MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema Serikali watakayoiunda endapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi watahakikisha wanadhibiti wizi wa dawa kwenye hospitali za Serikali ambazo zimekuwa zikiuziwa wananchi katika maduka ya dawa mitaani. Bi. Suluhu katoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia katika mikutano ya anuai ya hadhara Jimbo la Ilala kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo amebainisha kuwa dawa zote zitakuwa zinaingizwa katika mtandao maalum na kuzifuatilia na endapo zitatumika nje ya utaratibu itabainika na hatua kuchukuliwa. 

Alisema mtandao huo utafanikiwa kukabiliana na kero ya ukosefu wa dawa katika hospitali za serikali kwani dawa hizo zimekuwa zikiibwa kwenye hospitali za Serikali na kuuzwa nje katika maduka ya dawa binafsi na hospitali binafsi. "...Tunaamini mfumo huu utatusaidia kukabiliana na wizi wa dawa na rushwa hospitalini...unakuta daktari anakuandikia dawa alafu anakuelekeza duka la kwenda kununua sasa unajiuliza huyu mtu kajuaje kama sio yeye kapeleka pale," alisema Bi. Suluhu.

 Pamoja na hayo mgombea huyo mwenza, aliwashauri wananchi kuukubali utaratibu wa kutumia mfumo wa bima ya afya kwa matibabu ambao umekuwa ukimlazimu mwananchi kuchangia kiasi kidogo cha fedha na kutibiwa mwaka mzima bure katika hospitali zote zinazotumia utaratibu huo, kwani alidai utawasaidia wengi. "...Unajua ugonjwa unampata mtu ghafla na muda wowote haijalishi una fedha za kujitibu au la, lakini kama unabima ya afya waweza kutibiwa muda wowote hata kama hauna fedha wakati huo," alisisitiza Bi. Suluhu.

 Aidha, Bi. Suluhu alisema serikali watakayoiunda itajitahidi kupima maeneo mengi ya ardhi na kuyatoa kwa wananchi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi.

 Alisema Serikali yao pia imekamilisha utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kipunguni ambao wanadai fidia na itawalipa wananchi hao kwa thamani ya sasa ya ardhi kwani 2004 hadi sasa ni muda mrefu na ardhi imepanda thamani. 

Akizungumzia kero ya foleni, alisema ili kumaliza kero hiyo na msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Serikali imepanga kujenga miji mipya maalum na ya kisasa pembezoni wa jiji hili na kwa kuanzia itajenga mjini huo eneo la Kibaha ili shughuli nyingine ziwe zikifanyika katika mji huo na Dar es Salaam kupunguza msongamano, zoezi litakaloenda sambamba na ujenzi wa barabara ndogondogo za mitaani ambao utapunguza msongamano na foleni katika barabara kubwa. 

 Aidha Bi. Suluhu alisema zitajengwa barabara za juu katika makutano ya barabara ikiwa pamoja na kuzijenga barabara ndogondogo zikiwemo za Mbezi Morogoro-Malamba Mawili-Tangi Bovu-Kimara Baruti-Goba na nyinginezo ili kupunguza msongamano katika barabara kubwa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA TUME YA UTUMISHI YA BUNGE LA NIGERIA OFISINI KWAKE LEO

$
0
0
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza.
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria na wenyeji wao kutoka Tanzania Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
 
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge  la Nigeria na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
 
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Ajira na Maendeleo ya Watumishi ya Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Salehe Pamba akifafanua baadhi ya hoja zilizokuwa zikiulizwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria (hawapo pichani) waliotembelea Bunge leo kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge. 
 Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Tume ya Utumishi ya Bunge la Nigeria Mhe. Yepwi Stephen Dako akiuliza namna ambavyo Tume ya Bunge la Tanzania husimamia Watumishi wa Bunge la Tanzania katika kuleta ufanisi kazini wakati walipokutana na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo wa tume ya Nigeria upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge  la Nigeria na wenyeji wao kutoka Bunge la Tanzania mara baada ya kukutana nao Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akielezea baadhi ya masuala ya Kiutawala katika usimamizi wa Bunge kwa  wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge  la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. 
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiagana na Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako baada ya kumaliza mazungumzo yao.

JUMA NATURE AELEZEA MSIMAMO WAKE WA KUFANYA KAMPENI

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Juma Nature leo alikua akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Ufanyaji kazi wake katika kipindi hiki cha kampeni Ambapo aliongozana na Mgombea Ubunge jimbo la Mbagala ambaye ni rafiki mkubwa na jirani wa msanii huyo Ndg Issa Mangungu. Juma nature kwa sasa amerudi kufanya kampeni na chama cha mapinduzi CCM na ameamua kuelezea nia ya kurudi CCM baada ya mashabiki kumuona katika Majukwaa mengine ya vyama vya kisiasa. Nature amesema kuwa mziki ambao anaufanya ni Biashara lakini pia anafanya kwa ajili ya Jamii yake ambayo inamzuuka na pia anaangalia sehem ambayo anakubalika ivyo akiitwa sehem yeyote kufanya kazi anaenda anafanya kazi maana mziki ndio ajira yake. Sikilize hapa Juma Nature akiongea.......

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOUTIKISA MJI WA MOROGORO JIONI YA LEO,JK ASEMA MAGUFULI NDIO JIBU SAHIHI AWAMU YA TANO.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwapungia mikono wananchi huku wakiwa wameshika kofia zao. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisistiza jambo katika mkutano huo.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Jamhuti mjini Morogoro kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo Dkt Magufui aliwahutubia wananchi hao sambamba na kuzinadi sera zake
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubi maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.

Mmgombea Urais  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na saruji. Dk.Magufuli alitoa kauli hizo leo wakati anazungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Mkamba.Ruaha.Mikumi,Kilosa mjini pamoja na Morogoro mjini ikiwa ni sehemu ya kuomba ridhaa ya kuomba kichaguliwa urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Alisema kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya watanzania wote na hivyo atapunguza bei saruji na bati na hilo litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo."Serikali ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi wake.Moja ya mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.

Aliongeza kasi ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka hiyo anaiweza na anaomba wananchi wamuamini na ameomba urais kwa ajili ya kufanya kazi tu huku akieleza wapo ambao wanaosema anafanya siasa wajue yeye si mwanasiasi.''Nataka kuwa Rais wa Tanzania na si uwenyekiti .Dhamira yangu ni kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo yakiwemo ya kuwa na makazi bora.

"Natambua nchi yetu ni tajiri sana na sasa utajiri huo utumike kuleta maendeleo ya wananchi na hili linawezekana kwenye serikali ya awamu ya tano," alisema Dk.Magufuli.Alisema rasilimali za nchi hii zitumike kuleta maendeleo na ndio maana anataka nafasi hiyo kwa ajili ya kusimamia maendeleo ya wananchi wote.Wakati huo huo,Dk.Magufuli aliwataka wananchi kumchague yeye awe Rais kwa sababu hana tamaa ya fedha na ndio maana amaweza kusimamia vema fedha za wafadhili ambazo zilitumika kwenye ujenzi wa barabara.

Kwa upande mwingine alisema atasimamia amani ya nchi kwani ndio msingi wa maendeleo ya taifa letu na kuongeza shida ya watanzania si vyama vya siasa bali ni maendeleo yao.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Morogoro mjini,Mh Azizi Abbod mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.

 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akiteta jambo na Kada maarufu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na  mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro.
 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro,pichani kati ni mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akishuhuhudia tukio hilo.

 Wananchi wa kata ya Kimamba wakiwa wamekusanyka kwa wingi wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi kwao na kuomba ridhaa ya kuonza Tanzania katika awamu ya Tano
 Wanafuatilia kwa makini maneno aliyokuwa akiyazungumza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli wilayani Kilombero mapema leo mchana.
 Wananchi wa Luaha wilayani Kilombero wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hdahara

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Mikumi Ndugu Jonas Estomih Nkya.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mlimba Bw.Godwin Emmanuel Kunambi.
 Wakazi wa Mikumi wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowasili maeneo hayo alipokuwa akielekea wilayani Kilosa kuhutubia mkutano wa hadhara.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akifurahia jambo na mmto mara naada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo.
 Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wasanii wa Bongo MOvie nao walikuwepo wakiongozwa na Steve Nyerere na Wema sepetu katika kutimiza kampeni yao ya Mama ongea na Mwanao
 Wapiganaji kazini
 Kundi la Wasanii wa Filamu nchini la Mama Ongea na Mwanao likitumbuiza katika mkutano huo.
 Wema Sepetu akizungumza jambo 
 Nyomi la Watu

MAGUFULI ASISITIZA JAMBO LA AMANI KWA WAKAZI WA KIMAMBA WILAYANI KILOSA

MWIGULU NA MWAKALEBELA JANA IRINGA MJINI

$
0
0
Mwigulu Nchemba na Mwakalebela wakiwa kwenye Gari ya wazi wakielekea Uwanja wa Mwembetogwa hapa Iringa Mjini tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge.Mwigulu Nchemba akiingia na Gari la wazi kwenye Viwanja vya Mwembetogwa hapa Iringa Mjini kwaajili ya Kumnadi Mwakalebela anayepeperusha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kwenye nafasi ya Ubunge.Mwigulu Nchemba ambaye yumo kwenye kikosi cha Timu ya Ushindi ya CCM,hapa akiwasili Viwanja vya Mwembetogwa kwaajili ya kuzindua Rasmi kampeni za Ubunge Jimbo la Iringa Mjini kwa upande wa CCM
Sehemu ya Maelfu ya Wananchi wa Iringa Mjini wakifuatilia Mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za CCM Ubunge Jimbo la Iringa Mjini hii leo.Ombi la Mdahalo kati ya Wagombea Urais halikupitwa kwenye mkutano huu wa kihistoria kwa Wananchi wa Iringa.

 
Mwigulu Nchemba akizungumza na Maelfu ya Wananchi wa Iringa hii leo katika Viwanja vya Mwembetogwa wakati akifungua Kampeni za Ubunge Jimbo la Iringa Mjini ambapo CCM imemsimamisha Mwakalebela.Wananchi wakiwatayari kusikiliza sera za chama cha Mapinduzi kwa Jimbo la Iringa kuelekea miaka 5 ijayoya Ubunge.Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi wa Iringa kuwa ,Taifa letu linahitaji Kiongozi Magufuli kwasababu anasifa ya Uchapakazi,Mwadilifu,Mtanzania halisi,Sio mbaguzi na hana Urafiki kwenye kazi.Hivyo watanzania wampigie Kura magufuli ifikapo October 25 Mwaka huu.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Iringa Ndg.MwakalebelaMwigulu Nchemba akimuombea Kura mbunge Mtarajiwa wa Iringa Mjini Mh.Mwakalebela.Ndg.Mahiga ambaye ni meneja kampeni wa Mwakalebela akiwatoa hofu wananchi wa Iringa kuwa watafanya Kampeni za Amani na Utulivu na amewahakikishia wataibuka washindi mapema October 25.2015.Mwakalebela ambaye ni Mgombea Ubunge akizugumza na Wananchi wa Iringa Mjini.Kubwa amesisitiza kuwa anazijua kero za Wananchi wa Iringa Mjini hususani maji,Miundombinu na huduma za Afya,Hivyo yupotayari kuwatumikia kwa miaka 5 ijayo kama Mbunge wao.Mwigulu Nchemba akionesha alama ya "CCM ni Nambari 1"Wananchi wa Iringa wakishangilia mara baada ya Mwigulu Nchemba kumsimamisha Mbunge Mtarajiwa Ndg.Mwakalebela.Mwigulu Nchemba akiwambia Wananchi wa Iringa kuwa mambo yapo POA kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.Hisia za Wananchi kwa chama chao,Chama cha Mapinduzi.Mwigulu Nchemba (katikati),Mbunge mtarajiwa Mwakalebela(kushoto) na Kampeni Meneja wa Mwakalebela Ndg.Mahiga(Kulia) wakiwaaga wananchi wa Iringa mjini na kuwashukuru kwa Mafuriko waliyoyaleta Uwanja wa Mwembetogwa.
Picha na Sanga Festo Jr.

MGOMBEA MWENZA WA UKAWA JUMA DUNI HAJI ANGURUMA JIJINI TANGA

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema kihutubia Muheza.
 Wafuasi wa Ukawa wakifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mkinga.
 Wafuasi wa Ukawa Mkinga.
 Mgombea Mwenza akimkabidhi kadi ya CUF, Siwajibu Rajabu aliyejiunga na chama hicho wakati wa mkutano wa kampeni katika jimbo la Pangani Tanga.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Pangani, Amina Mwidau.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akihutubia mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akihutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akihutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiagana na wafuasi wa Ukawa baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
Umati wa wafuasi wa Ukawa wakifuatilia mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano.
Makamu Mwenyekitiwa Chadema, Zanzibar, Saud Issa Mohamed akimlaki Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa jijini Tanga, mgombea huyo yupo katika mikutano ya kampeni mkoani Tanga. (Picha zote na Francis Dande)
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akipokea saluti kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga (OCD), Omary Ntungu  alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Tanga kwa ajili ya mikutano ya mkoani.
Baadhi ya wafuasi wa Ukawa waliokuwa na shauku ya kutaka kumuona mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema Juma Duni Haji wakijaribu kuusimamisha msafara wa mgombea huyo alipokuwa njia kuelekea wilayani Muheza.

CCM kifo cha mende............
Mgombea Mwenza Juma Duni Haji akihutubia wakati wa jimbo la Muheza.
Muheza Tanga.

Bango.
Mfuasi wa Ukawa akiwa na bango.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images