Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 631 | 632 | (Page 633) | 634 | 635 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  Rais Jakaya Kikwete (Pichani)ameridhishwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua iliyofikiwa ya kuweza kusajili jina la biashara kwa njia ya mtandao na kupata cheti ndani ya saa moja.

  “Hatua hii ya BRELA ni nzuri, wanastahili pongezi na wengine waige,” alisema Dkt. Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  Pongezi za Dkt. Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi.
   
  Akithibitisha maendeleo hayo mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka VIBINDO alisema hivi karibuni aliweza kufanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja tu.
   
  BRELA imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka huu.
   
  Mteja wa BRELA anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza, anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
   
  Mteja anatakiwa kuingia katika mtandao wa BRELA ambao ni www.brela.go.tz kisha ataingiza jina na baada ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.
   
  Baada ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia mchakato huo wa kimtandao.


  0 0

  Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, watu kupitia fani na kazi mbalimbali wamekuwa wakijaribu kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya maamuzi yatakayolipeleka taifa letu mbele.
  Innocent Galinoma(Pichani juu)ni msanii mkongwe wa Reggae anayefanya kazi zake nchini Tanzania.

  Naye ametunga wimbo maalum kwa ajili ya uchaguzi huu mkuu. Akisisitiza kuhusu kusikiliza na kuwahoji wagombea ili kujua fika wanalotaka kutufanyia katika kutatua kero zetu
  Karibu usikilize kibao....UCHAGUZI


  0 0


  0 0

   Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
   Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama.
   Mtoto Jamine Nibetanga(14), kutoka nchini Burundi akiandaa chakula   katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli.
   Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati), akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).
   Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda.  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina mpango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendeli na Nduta ili kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
   
   Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
   Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
   Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Ntirampeba Acquelina akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake  katika kambi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali wa  mihogo ni mojawapo ya vyakula muhimu vinavyotumika katika kambi ya Nyarugusu.
   Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira kama walivyokutwa jana na mpiga picha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Wakimbizi hao wamekua wakiingia nchini kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Burundi hivi karibuni.
   Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpiga picha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara  katika kambi hiyo.
  Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.
  (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

  0 0

  Wahitimu wa darasa la saba Fredrick Robert (kulia) na Rania Hante kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakisoma risala yao kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
   
  Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
  Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo. Waliopo meza kuu ni Wakurugenzi wa shule hiyo, kwanza kulia ni Mkurugenzi Imelda Philip akifuatiwa na Machage Kisyeri. Na wa kwanza kushoto ni Julius Rutabanja.
  Mtimu wa darasa la saba wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam Habiba Ayoub akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya shule ya msingi kutoka kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
    Mtimu wa darasa la saba wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam Deniol Msemwa akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya shule ya msingi kutoka kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
  Mwanafunzi Cuthbert Safari akimvalisha “skafu” Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema alipowasili wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam.
  Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wakionesha vyeti mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
   
  Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
  Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema (katikati mstari wa mbele walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wakionesha vyeti mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
  Baadhi ya wazazi na walezi wakifuatilia hafla ya kuwaaga Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam hivi karibuni.
  Mwalimu Evarist Runimba akipokea zawadi ya kuwa mwalimu mlezi wa darasa la saba mwaka 2015   kutoka kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema wakati wa mahafali ya nne ya wahitimu hao kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam.

  (Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
  Wanafunzi wakitumbuiza kwa michezo mbalimbali wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam.
  Mhitimu wa darasa la saba Emma Emily akiwa amepokea cheti cha kufanya vizuri katika somo la Hisabati pamoja na hati ya ufadhili wa kusomeshwa kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya sekondari ya Bright Future Girls iliyopo jijini Dar es salaam.

  0 0

  SAM_5821Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akimnadi mgombea Ubunge pamoja na madiwa katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Arusha mjini tarehe 5/9/2015 katika uwanja wa soko kuu jijini Arusha(Picha zote na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
  SAM_5835Umati wa watu uliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za ccm jimbo la Arusha mjini katika ene la soko kuu jijini Arusha,ambapo rasmi walizindua kampeni za ubunge na udiwani
  SAM_5823Mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi ccm Philemon Mollel maarufu kwa jina naMonaban akimwaga sera zake katika uzinduzi huo ambapo alikiri kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo endapo ataibuka mshindi katika uchaguzi mkuu
  SAM_5742Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi akiongea katika mkutano huo
  SAM_5804Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akisalimiana na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM jimbo la Arusha mjini tarehe 5/9/2015 katika eneo la soko kuu jijini Arusha
  SAM_5779Mjumbe wa halmashauri kuu  ya CCM Taifa kutoka Arusha mjini, Godfrey Mwalusamba akiongea katika uzinduzi huo.

   
  SAM_5786Mbunge viti maalum kundi la wanawake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza katika uzinduzi huo
  SAM_5783Mbunge viti maalum na Kada maarafu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mfuko akiongea katika uzinduzi huo
  SAM_5771Aliyekuwa dereva wa Mbunge Lema shubet akiongea jukwaani alisema hamuogopi lema kwa kuwa mbinu zake zote anazijua hivyo hawezi hata kuua mende nyumbani kwakwe licha ya kumtangazia atamtumia majambazi nyumbani kwakwe
  SAM_5793Mwigizaji maarufu wa sauti za viongozi mbalimbali Oscar Nyerere akichekesha katika uzinduzi huo
  SAM_5787Mbunge mstaafu kupitia CCM jimbo la Longido Lekule Laizer  maarufu kwa jina la "kiboko wa wapinzani" akiongea katika uzinduzi huo ,aliwataka wananchi wa Arusha kumchagua Monaban kwakuwa ni kiongozi muadilifu mwenye sifa ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo
  SAM_5812Mh.Phidesia Mwakitalima kulia anasema CCM mbele kwa mbeleeeeeeeeee!
  SAM_5749Meza kuu
  SAM_5807Mwenye miwani aliyekaa chini pamoja na wananchi Mustafa Panju ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika kura za maoni akifwatilia uzinduzi huo
  SAM_5838Mustafa Panju ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika kura za maoni akiagana na wananchi baada ya kumaliza kampeni hizo

  0 0

   Wananchi wakishuhudia mchezo ukiendelea ikiwa umedhaminiwa na Mtandao wa simu wa Smart katika viwanja vya Mkuranga mkoani pwani baadha ya mpira kumalizika ndipo Mkizi Mnene Bar  kwa Bar ulipoaaza kuchezwa mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
   Wachezaji wa timu ya EFM na Mkuranga Veteran wakiendelea kusakata kabumbu ndani ya viwanga vya Mkuranga Mkoani Pwani.
  Picha ya pamoja ya Timu  ya Mpira wa miguu ya EFM  na Mkuranga Veteraniliyo cheza katika viwanja vya Mkuranga mkoani Pwani, mashindano hayo ya  mpira wa miguu timu ya EFM iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Mkuranga Veteran. 

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman, akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa pili kutoka kulia), kabla ya kuongea na watumishi wa Serikali kutoka taasisi Mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mwishoni mwa wiki. Katibu Mkuu alikutana na Watumishi hao ili kujadili namna bora ya kufanya kazi katika Viwanja vya Ndege na kuwkumbusha wajibu wao wanapokuwa kiwanjani hapo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akiongea na watumishi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi Kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),, mwishoni mwa wiki.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa nne kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) na watuumishi wa Serikali wanaotoka kwenye ofisi mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mwishoni mwa wiki. Katibu Mkuu alikutana na Watumishi hao ili kujadili namna bora ya kufanya kazi katika Viwanja vya Ndege.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiangalia Daraja jipya la kupandia ndege “Aero Bridge” lililokamilika hivi karibuni wakati alipotembelea Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), na kukutana na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) pamoja na watumishi wanaotoka kwenye ofisi mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi kiwanjani cha Uwanja huo, mwishoni mwa wiki. Katika mkutano huo Katibu Mkuu aliwakumbusha watumishi hao kukumbuka majukumu yao na kutambua kuwa wanafanya kazi katika sehemu nyeti inayoonyesha picha ya Tanzania).
  (Habari Picha na Kitengocha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)

  0 0

   Katibu Mkuu  Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea Banda la NCC katika mkutano wa 13 wa bodi ya Wahandisi Tanzania
  Katibu Mkuu  Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ( wa kwanza kulia) akipata maelezo ya baadhi ya machapisho ya kitaalamu ya sekta ya Ujenzi yanayotolewa na Baraza la Taifa la Ujenzi kutoka kwa  Mhandisi Julius Mwita.
   Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi wakitoa maelezo ya shughuli za Baraza kwa Wahandisi waliotembelea katika banda la (NCC).  Wa kwaza kulia ni Afisa Habari Mwandamizi Robertha Makinda, Ainenyi Clement na Mhandisi Mwita Julius.

  0 0

   KAMPUNI ya ConnectMoja Technologies  Wamezindua tovuti mpya iitwayo Mavazi Store (www.mavazi.co.tz)  ambayo inajumuisha Mkusanyiko wa maduka mbalimbali ya mavazi ya aina zote mtandaoni. 

  Kwa Mujibu wa Meneja Chapa ambaye pia ni Ambasador wa Mavazi Store bwana  Steve Seducter   mfumo huu wa kisasa umelenga  Kuondoa kero ya kutafuta bidhaa mbalimbali zinazohusiana na Urembo pamoja na Mavazi, pia kuwaokolea muda wateja  kwa kuunganisha  maduka Mengi zaidi kupitia tovuti hii ya www.mavazi.co.tz .  

  Mtu yeyote mwenye simu ya kiganjani au kupitia katika kompyuta yake ataweza kutembelea Tovuti hii na kuona biashara zilizosajiliwa pamoja na Bidhaaa wanazouza. Hii itamuwezesha kuchagua  na kuwasiliana na duka husika Moja kwa moja alipo (Delivery),

  Muonekano wa Tovuti ya MavaziStore  (www.mavazi.co.tz)
  Pamoja na mengine Mtafiti wa Masoko na ukuaji wa biashara Bwana Fred Crich  alifafanua kwamba  kwa Sasa ConnectMoja Technologies imejikita kusaidia ukuaji wa biashara mbalimbali za kitanzania, na kuhakikisha kwamba Maendeleo yanayotokea katika Dunia hasa kupitia teknolojia yanaipa Manufaa pia jamii yetu ya Kitanzania.

   Crich Ameongeza kwamba  Kwa Kampuni inatoa Ofa kwa wamiliki wa maduka kutangaza katika Tovuti hii Bure kwa Mwezi Mmoja  ili kuwafikia zaidi wateja walio wengi. Ili Kutangaza Nasi Tembelea  http://mavazi.co.tz/advertise/  au Wasiliana nasi kwa Simu   0777880007  au 0714215 600  :  Office:  Oysterbay – Dar free Market Mall (GL14)

  Imetolewa na  Kitengo Cha Masoko – ConnectMoja Technologies Limited

  0 0

  Katibu wa chama hicho wilayani Lushoto, ndugu Mahanyu, akizungumza wakati wa kuzindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya Lwandai Mlalo wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, akiwa na Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha  Mapinduzi,CCM jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi  wishoni mwa wiki.
   Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha  Mapinduzi,CCM jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika viwanja vya Lwandai Mlalo, kulia ni Mgombea wa udiwani  wa kata ya Kwamshasha jimboni Mlalo, Anwari Kiwe.
  Wazee wa jimbo la Mlalo wakibadilishana mawazo baada ya kuwasili katika viwanja vya Lwandai Mlalo  kabla ya mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha  Mapinduzi,CCM jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi kufungua mkutano wa kampeni katika jimbo hilo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

  0 0

  Afisa Mtendaji  Mkuu wa kinywaji cha Trevo, Mark Stevens akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) juu umuhimu wa kinywaji na  kinywaji cha Trevo ambacho kipo nchini kwa takribani miezi tisa, na kinavyoweza kuwasaidia afya za binadamu endapo kuna mapungufu katika mwili  hasa kuimarisha afya zao.

  Pia aliongezea kuwa Kinywaji cha Trevo ni kinywaji kilichotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu kinaachuhusisha  vyakula mbalimbali nyenye kiwango kikubwa vya virutubisho na kutoka mataifa mbalimbali duniani aidhaa alisema kuwa bidhaa hiyo imethibitishwa na mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA pamoja na Shirika la Viwango nchini (TBS).
  Mkurugenzi wa Trevo Tawi la Tanzania, Michael Ajao akisisitiza jambo uwa , Kinywaji hicho kinasambazwa nchini kwa njia biashara ya Mtandao ambapo hadi sasa ni zaidi ya wanachama elfu tatu wamejiunga hapa nchini. aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Saerena jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na balozi wa India Nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 7, 2015 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Balozi wa India Nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya, baada ya mzungumzo yao yaliyofanyika  Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 7, 2015. Picha na OMR

  0 0

  Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Cement ya Twiga Simon Delens,akizungumza na wafyatua matofali wa Mkoani Mwanza juzi,kwenye semina ya mafunzo ya kutengeneza matofali imara.
  Mhandisi kutoka Kampuni ya Cement ya Twiga Emmanuel Owoya, akitoa maelezo ya umuhimu wa kuvaa viatu vya usalama wakati wa kazi,kwenye mafunzo ya matengeneza matofali wa Mkoani Mwanza juzi.
  Mhandisi kutoka Kampuni ya Cement ya Twiga Emmanuel Owoya,akimvalisha kifaa cha kuzuia vumbi puani na mdomoni mmoja wa watengeneza matofali mkoani Mwanza Issac Waitara, kwenye mafunzo ya kutengeneza matofali wa imara.
  Mhandisi kutoka Kampuni ya Cement ya Twiga Emmanuel Owoya,akionyesha nguo ya usalama (Overall)na umuhimu wa kuivaa wakati wa kazi,kwenye mafunzo ya matengeneza matofali wa Mkoani Mwanza juzi.

   
  Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Cement ya Twiga Simon Delens,akimpongeza Nickson Cheka(kulia) baada ya kujibu vizuri maswali Mkoani  Mwanza juzi,kwenye semina ya mafunzo ya kutengeneza matofali imara.
  Baadhi ya wafyatua matofali wa Mkoani Mwanza wakiwa na wafanyakazi wa Kamuni ya saruji ya Twiga baada ya semina ya kuwafundisha mambo yahusuyo usalama, afya na kutengeneza mtofali yaliyo bora.

  0 0

   Msajili  Msaidizi wa ofisi ya msajili  wa Vyama  vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuufahamisha umma kuwa chama cha siasa Tanzania Peoples Party (TPP) kilifutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa hapa nchini na chama hicho hakipo kwenye orodha ya vyama vya siasa vilivyopo hapa nchini amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habarijijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali watu Emmanule Kayuni,.
  Wanahabari wakimsikilza kwa makini Msajili  Msaidizi wa ofisi ya msajili  wa Vyama  vya Siasa, Sisty Nyahoza leo Jiji Dar es Salaam.
   (Picha na Emmanue Massaka).
   
  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema kuwa Chama cha Tanzania People’s Party (TPP) kilifutwa, hivyo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutumia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
   
  Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema kuwa hivi karibuni kuna watu wameonekana katika chombo cha habari kimoja  sio Michuzi, wakiwajinasibu katika chama cha TPP wakati chama hicho kilishafutwa  toka 2001.
   
  Nyahoza amesema kuwa watu wanaotumia chama hicho sheria itashika mkondo wake kwa kuwachukulia hatua watu kutumia chama ambacho kilishafutiwa usajili wa kudumu kwa msajili wa vyama vya siasa.
   
  Aidha amesema kuwa vyama vilivyo katika usajili wa kudumu na vimeshiriki uchaguzi mkuu ni vyama 22 hivyo watu watambue chama cha TPP kilishafutwa kutokana na kukiuka kwa taratibu za ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
   
  Nyahoza amesema kuwa watu wote wanaotumia vyama ambavyo usajili wake ulishafutwa  kwa mamlaka ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa watatachukuliwa hatua.

  0 0

  Mr.Graham Vaas, a retired South African Hotelier, addresses a point to journalists on the sidelines of a brief ceremony organized by Diamond Motors, a Mitsubishi appointed dealer in Tanzania to bid him and his wife farewell, as they were on a 3- month round robin tour of 11 Southern and Eastern African countries by using one of the company’s brand new Mitsubishi Pajero Sports over the weekend in Dar es Salaam.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo TIB Prof. William Lyakurwa (wapili kushoto) na Msajili Hazina Bw. Lawrence Mafuru (wa pili kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kiutendaji kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mkataba huo unalenga kufungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa benki hiyo katika kuleta tija kwa taifa. Wanaoshuhudia ni pamoja na Msajili Hazina msaidizi Bw. Mwakibinga Mihalale (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtenddaji wa benki
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo TIB Prof. William Lyakurwa (kushoto) na Msajili Hazina Bw. Lawrence Mafuru (kulia) wakionyesha mikataba ya makubaliano ya kiutendaji baina yao mara baada ya kuisaini kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mkataba huo unalenga kufungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa benki hiyo katika kuleta tija kwa taifa.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo TIB Prof. William Lyakurwa (kushoto) na Msajili Hazina Bw. Lawrence Mafuru (kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kiutendaji kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mkataba huo unalenga kufungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa benki hiyo katika kuleta tija kwa taifa. 

  Na Mwandishi wetu
  BENKI ya Maendeleo TIB imesaini mkataba wa kiuetendaji na Serikali hatua inayofungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa benki hiyo katika kuleta tija kwa taifa. 

  Kusainiwa kwa mkataba huo kunaifanya benki hiyo kuwa miongoni mwa mashirika na taasisi za awali kabisa za umma zilitoa fursa kwa serikali kuzikagua na kupima ufanisi wao kiutendaji kila mwaka kupitia msajiri wa hazina.

  Akizungumza kwenye hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma lilipita, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Prof. William Lyakurwa alisema hatua hiyo itaisadia kuongeza msukumo zaidi kwa benki hiyo kuweza kuweza kutimiza malengo yake na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

  “Licha ya ukweli kuwa tumekuwa tukitimiza wajibu wetu siku zote kwa kuhakikisha kwamba tunatoa huduma kwa weledi na ufanisi zaidi  lakini tunaamini kuwa uwepo wa mkataba huu utasaidia kutusukuma zaidi na hatimaye si tu tufikie malengo yetu bali pia hata kupitiliza malengo tuliyojiwekea,’’ alisema.

  Aliongeza kuwa  mkataba huo pia utaongeza ari kwa waafanyakazi wa benki hiyo kwa kuwa utawajengea dhana ya uwepo wa nguvu ya ziada inayowasukuma zaidi kukamilisha majukumu yao kwa wakati na kwa ufanisi zaidi sambamba na matumizi sahihi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya uendeshaji wa benki hiyo.

  “Mkataba huu kwetu ni ushahidi kwamba tunatimiza wajibu wetu kwa uwazi na zaidi tupo tayari kupimwa kwenye hilo.Lengo ni kuwa miongoni mwa taasisi bora kabisa za fedha hapa nchini na ulimwenguni kwa ujumla,’’ alisema.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo Msajiri Hazina Bw Lawrence Mafuru alisema  mikataba ya aina hiyo inalenga kuisaidia  serikali kupunguza hasara kubwa ambayo imekuwa ikapata kutoka kwenye mashirika na taasisi za umma zinazoshindwa kujiendesha kwa ufanisi  unaotakiwa.

  Alibainisha kuwa  mashirika na taasisi za umma nyingi hapa nchini zinashindwa kujiendesha kwa ufanisi  kwa kuwa  kuna ombwe la  ufuatiliaji wa utendaji na matumizi ya pesa zinazotengwa kwa ajili ya uendeshaji wa mashirika hayo.

  Akizungumzia mikataba hiyo Bw Mafuru alisema  kuwa licha ya  utaratibu huo kuwa mgeni hapa nchini lakini unalenga  kutambua taasisi na mashirika ya umma yanayoshindwa kujiendesha kwa ufanisi sambamba na matumizi mabaya ya fedha  za umma ili kutoa fursa kwa serikali kufanya maamuzi sahihi kulingana na aina ya changamoto zinazoyakabili mashirika hayo.

  “Tunaamini huu ni mwanzo mpya kwenye usimamizi wa mashirika na taasisi hizi za umma na zote zinatakiwa ziwe na mkataba wa aina hii na tutakuwa wakali tukibaini udhaifu wowote ikiwemo kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika na udhaifu huo,’’ alisema.

  Pia alitoa wito kwa wanasiasa wakiwepo wabunge kujitoa kwenye bodi za mashirika mbalimbali ya umma ili kuondoa mgongano wa kimaslahi kwa kuwa wao wana jukumu la kukagua mashirika hayo kupitia kamati za bunge.


  0 0

   Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Adelhelm Meru akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumtambulisha Flaviana Matata  kuwa balozi wa utalii jimbo la New York City nchini Marekani.Kutoka kulia ni Flavianao Matata na kushoto Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji Bodi ya Utalii TTB Devota Mdachi.
  Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Adelhelm Meru akimkabidhi cheti   cha kumtambua kuwa balozi wa utalii jimbo la New York City nchini Marekani Flaviana Matata  katikati ni Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji Bodi ya Utalii TTB Devota Mdachi.

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Burundi hapa Nchini  Bwana Issa Ntambuka ambaye alifika ofisini kwa Waziri Mkuu leo jijini Dar es salaam kwa mazungumzo ya kikazi.
   Waziri mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza kwa makini Balozi wa Burundi hapa nchini Bwana Issa Ntambuka ambaye alifaka ofisini kwa Waziri Mkuu leo Jijini Dar es salaam kwamazungumzo ya kikazi.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akutana na Balozi wa Qatar hapa Nchini Bwana Abdullah Jassim Al Maadadi ambaye alifika ofisini kwa Waziri Mkuu leo Jijini Dar es salaa kwa mazungumzo ya kikaza
  Picha na Chris Mfinanga.

older | 1 | .... | 631 | 632 | (Page 633) | 634 | 635 | .... | 1898 | newer