Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake wafanyika Dodoma leo.

$
0
0
 Mhe. Sophia Simba akipewa maelezo na Bill Marwa kuhusiana na  tovuti rasmi iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kupaza sauti ya mwanamke (www.sautiyamwanamke.org) baada ya kuizinduwa kwenye uzinduzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika Dodoma.  Waliosimama kushoto kwa waziri ni Teresa Yates na Hilda Mashauri viongozi wa mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) waandaaji wa mdahalo huo.Tovuti hiyo itatumika kutoa taarifa za kila siku za mdahalo na kuendelea kupaza sauti ya mwanamke baada ya mdahalo kwa kuandika habari mbalimbali zinazohusu mwanamke. 
Teresa Yates, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania akikabidhi zawadi kwa Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto  na kwa Dr. Rose Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. 
 Mwanahamisi Salim, Meneja wa Kampeni, Ushawishi na Utekelezaji wa Haki za Kiuchumi kutoka shirika la Oxfam akiendesha zoezi la ufunguzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma. 
 Dr. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto kwa ajili ya kufungua rasmi mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. 
  Mshiriki kutoka Unguja akizungumza kwa niaba ya wanawake takribani 300 wanaoshiriki mdahalo wa kitaifa wa wanawake uliozinduliwa leo Dodoma na Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto. 
  Baadhi ya Wanawake wanaoshiriki Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. Mdahalo wa Kitaifa wa wanawake ni tukio linalofanyika kwa hisani ya mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) kuanzia tarehe 10-14 April, 2013 mkoani Dodoma. 


dkt.mwinyi azindua baraza la usajili wa wataalam wa afya na mazingira nchini.

$
0
0

HOTUBA YA WAZIRI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII MHE: DKT.HUSSEIN ALLY HASSAN MWINYI (MB) KWENYE UZINDUZI WA BARAZA LA USAJILI WA WATAALAM WA AFYA YA MAZINGIRA NCHINI TAREHE 10/04/2013. 
HOTUBA YA WAZIRI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII MHE: DKT.HUSSEIN ALLY HASSAN MWINYI (MB) KWENYE UZINDUZI WA BARAZA LA USAJILI WA WATAALAM WA AFYA YA MAZINGIRA NCHINI TAREHE 10/04/2013.


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga,

Mwenyekiti wa Baraza la Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira Nchini,

Msajili Baraza la Usajili wa Watalaam wa Afya ya Mazingira Nchini,

Wasajili wa mabaraza wa Kada za Afya,

Wajumbe wa Baraza la Usajili Wataalam wa Afya ya Mazingira,

Wataalam wa Afya ya Mazingira Nchini,

Wanahabari,

Wageni Waalikwa,

Mabibi na Mabwana.


Napenda kuchukua fursa hii muhimu kuwashukuru wote  kwa kufika kwenu kushuhudia kuzinduliwa Baraza hili la Wataalam wa Afya Mazingira nchini awamu ya pili. Aidha, nawapongeza sana wajumbe wote wa Baraza lililopita kwani kutokana na ushirikiano wao katika awamu ya kwanza ya Baraza hili wameweza kujenga msingi na daraja kwa Baraza la awamu ya pili ambalo tunalizindua leo. Vilevile sitakuwa mwingi wa fadhila kama sitaishukuru sekretariati ya Baraza kwa kuweza kuratibu kazi zote za Baraza lililopita na hatimaye  leo tunapokea wajumbe wapya kuendeleza yale yaliyoanzishwa katika awamu ya kwanza. ninawashukuru wote ambao mumeitikia wito kuja kuwaunga mkono wenzetu katika tukio hili la kipekee katika historia ya kada ya afya ya mazingira nchini. Nawashukuruni sana.


Ndugu Wajumbe,

Maboresho ya sekta ya afya nchini yamekuwa yakilenga mambo mbalimbali ambayo yanasaidia kudumisha huduma bora za afya kote nchini. Miongoni mwa masuala muhimu ni kuweka msingi na taratibu za kuhakikisha watoa huduma za afya wanazingatia sheria, kanuni, miiko na maadili ili waweze kutoa huduma kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu. Hivyo pamoja na mambo mengine Wizara imetunga Sheria ya kusimamia na kudhibiti utendaji wa  Wataalamu wa Afya ya Mazingira  ya mwaka 2007, na kutengeneza kanuni za Sheria zinazojulikanazo kwa jina la kiingereza “The Environmental Health Practitioners (General) Regulations 2011” Aidha kwa mujibu wa kanuni ya 3, 4 na 5  zinazungumzia suala la Usajili, kuorodheshwa na kuandikishwa kwa Wataalam wa Afya ya Mazingira Nchini.


Ndugu Wajumbe,

Kada ya Afya ya Mazingira ni miongoni wa Taaluma muhimu ulimwenguni hususan katika nchi yetu ambayo ipo Kusini mwa jangwa la Sahara. Nchi nyingi zinazoendelea hivi leo zinakabiliwa na changamoto na tekinolojia endelevu, vitendea kazi duni, mazingira duni yasiyoridhisha kiafya, hali mbaya ya uchumi, soko la ajira, uzembe na uzururaji, ushindani wa kitaaluma, mabadiliko ya tabianchi ‘kuongezeka kwa joto duniani  mabadiliko katika sekta ya viwanda na biashara, sekta ya kilimo na chakula, sekta ya nishati na madini, sekta ya elimu na pia katika sekta ya afya na ustawi wa jamii. Katika sekta ya Afya na Ustawi wa jamii kuna changamoto nyingi zikiwemo za ongezeko la milipuko ya magonjwa kutokana na uchafuzi wa mazingira. Afya ya mazingira ni suala mtambuka ambalo hushughulikiwa na wadau tofauti tofauti. Ni muhimu  utekelezaji wa majukumu haya  kuwe na ushirikishaji wa sekta wadau wa afya ya mazingira ili kutoa matokeo yenye  tija na ubora wa juu. Ni matumaini yangu kuwa tutafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kupambana na changamoto nyingi zinazotukabili hasa kuzuia maambukizi ya magonjwa.


Ndugu Wajumbe,

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo kwa matukio ya ukiukwaji wa maadili katika utoaji wa huduma za afya ya mazingira nchini, ambapo matatizo ya kitaalam hutolewa maamuzi bila ya kuzingatia taratibu na misingi ya taaluma. Hili ndilo lilipelekea kuanzishwa kwa Baraza la Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira nchini kama chombo pekee cha kusimamia na kudhibiti utendaji wa maafisa  Afya Mazingira nchini. Pamoja na mambo mengine muhimu, Baraza la awamu ya kwanza limeshaweka msingi wa utaratibu namna ya kuwasajili wataalamu mbalimbali wa fani hii, kwa kutengeneza kanuni zilizoainishwa chini ya Sheria hii, kuinua hali ya nidhamu na maadili katika taaluma ya afya ya mazingira, kukuza soko la ajira la wataalamu wa kada hii ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu, na kuwasaidia wataalamu wa afya ya mazingira kwa kuweka taratibu wezeshi katika kujiendeleza na kupanua wigo wa ufahamu wa masuala yote yanayohusu afya na usafi wa mazingira.


Ndugu Wajumbe,

Ni matarajio ya Serikali kuwa kwa kutumia  baraza hili, mambo yafuatayo yatawanufaisha wananchi;

·        Huduma ya afya ya jamii  hapa nchini itatolewa kwa viwango vinavyotakiwa na hivyo kuboresha maisha ya wananchi. Baraza litasimamia na kudhibiti utoaji wa huduma ya afya ya mazingira kwa misingi ya haki.

·        Wataalam wa kada hii watajiendeleza na kufikia kiwango cha juu cha elimu tofauti na miaka iliyopita ambapo wengi waliridhika na kubaki katika eneo moja kwa muda mrefu na kusababisha kudumaa kwa taaluma.

·        Kuendelea kutengeza kanuni, viwango na taratibu zitakazoweka taratibu sahihi za kiutendaji na ili kuendana na wakati.

·        Uwezekano mkubwa wa kupunguza ongezeko la kasi ya magonjwa. Vifo na madhara mengine katika jamii yatapungua kwa kuwa huduma ya afya ya jamii itaboreshwa.  


Sheria imeweka na kuainisha majukumu na mamlaka ya baraza kama ifuatavyo;

·        Kuweka bayana majukumu ya makundi ya wataalamu wote wanaostahili kusajiliwa na hivyo kutoa huduma ya afya ya mazingira hapa nchini chini ya Sheria hii.

·        Kuweka bayana adhabu zitakazotolewa kwa wataalamu watakaokiuka kanuni, taratibu na maadili ya kitaalamu ya wataalamu wa fani hii kwa mujibu wa Sheria.

·        Kusajili wataalamu wa afya ya mazingira kulingana na viwango vya utaalamu wao.

·        Kuweka vipengele mbalimbali vya kisheria ambavyo vitasimamia utekelezaji wa kazi za Barazan.k

·        Kuainisha vyanzo vya mapato mbalimbali ya baraza kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zote za baraza.


Ndugu Wajumbe,

Katika kuhakikisha kuwa Baraza la kusajili wataalamu wa afya ya mazingira linafanya kazi yake ipasavyo, sheria imebainisha  muhula wa utendaji kazi Baraza teule, ambayo ni miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi. Kwa kuzingatia hili ni vema Baraza likajitahidi kufanya kazi kwa bidii ikiwezekana ifikapo mwaka 2015 kuwepo na taarifa nzuri ya utendaji  kuzidi Baraza la awamu ya kwanza .


Baada ya kusema hayo machache niwaombe wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu hawa wa afya ya mazingira nchini kwa vile majukumu yao yanategemea sana na ushirikiano wenu. Aidha nawaagiza wataalamu wa afya ya mazingira nchini kufanyakazi kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma. Naagiza pia Baraza litekeleze majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya sheria na taaluma.


Baada ya kusema hayo napenda sasa nitamke kuwa Baraza la Usajili wa Wataalamu wa Afya ya Mazingira nchini leo tarehe 10 Aprili, 2013, limezinduliwa Rasmi.

  
Ahsanteni kwa kunisikiliza.




picha za muendelezo wa tamasha la pasaka mjini dodoma

$
0
0
 Bonny Mwaitege akiimba
 Upendo Kilahiro
 Anastazia Mkabwa kutoka Kenya,
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama akisalimiana na   mgeni rasmi wa tamasha hilo,Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai,kwenye muendelezo wa Tamasha la pasaka 2013  mjini Dodoma,ambapo walioimba katika tamasha hilo walikwwa ni Rose Mhando,Faraja Ntaboba Kutoka Congo,Solomon Mkubwa Kutoka Kenya,Anastazia Mkabwa kutoka Kenya,Joyers Cerebration,Upendo Kilahiro na Upendo Nkone.Picha zote na Silas Mjengi
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama akimkaribisha  mgeni rasmi  katika tamasha la muendelezo wa Pasaka,Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai.

 Faraja Ntaboba Kutoka Congo
 Upendo Nkone
 ,Solomon Mukubwa Kutoka Kenya akiimba jukwaani.
Rose Muhando akiimba

HIF YAANZISHA KAMPENI YA HUDUMA YA MATIBABU YA MADAKTARI BINGWA KWENYE MIKOA YA PEMBEZONI

$
0
0
 Mgeni rasmi Mhe.Abdallah Ulega kaimu mkuu wa mkoa wa lindi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma za matibabu ya madaktari bingwa sambamba na kupokea dawa na vifaa tiba kutoa nhif ili kufanikisha zoezi ilo wanaoshuudia kulia ni mkuu wa wilaya ya lindi Mhe. Dr Hamid Nassoro,kaimu RAS Lindi Ndg John Likango na kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya bwn.Emanuel Humba  
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF bwn. Emanuel Humba akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa utekelezaji wa mpango huo maalum uliobuniwa na mfuko kwa kutoa huduma za madaktari bingwa kwenye mikoa iliyo pembezoni,na kuzinduliwa mkoani Lindi.

 
 Mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya kilwa akisoma hotuba fupi wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa huduma za matibabu ya madaktari bingwa kwa wanachama na wananchi mkoani humo na kuwataka wajitokeze kwa wingi na kuenzi huduma hiyo kwani itaokoa maisha ya wengi,kulia ni mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Dr Hamid Nassoro,kushoto kwake ni Mkurugenzi wa NHIF wanaofatia ni mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi DR. Yusuf Sonda na Dr Frank Lekey wa NHIF

Wanachama na wananchi waliojitokeza wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani kwenye viwanja vya Hospitali ya Mkoa (Sokoine) Lindi.
==============  ==============  ============

HIF  YAANZISHA KAMPENI YA HUDUMA YA  MATIBABU YA MADAKTARI BINGWA KWENYE MIKOA YA PEMBEZONI.


Wanachama na wananchi mkoani Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutumia vyema fursa za huduma za madakatri bingwa zinazoratibiwa na mfuko wa taifa wa bima ya afya  katika hospitali ya mkoa sokoine.


Hayo  yalisemwa na mgeni rasmi  kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe: Abdallah Ulega wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa utoaji  huduma za matibabu kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili kwa magonjwa ya  akinamama,wataalam wa upasuaji na magonjwa ya  moyo,figo na shinikizo la damu  uliofanyika katika viwanja vya hospitali ya sokoine mjini lindi


Ni fursa adhimu ambayo wengi wetu hapa mkoani Lindi,hatukuwahi kukutana nayo na sababu kubwa inawezekana ni uwezo wa kugharamia safari ya kwenda huko wanakopatikana madaktari bingwa sanjari na mlolongo mrefu wa taratibu za kitabibu ili kuwafikia,lakini wenzetu,yani bodi ya wakurugenzi, menejimenti  ya Mfuko wa taifa ya bima ya afya wameiona changamoto hii na niseme wazi kuwa mpango huu utakuwa unaokoa maisha ya watu wengi ambao hawakuwahi wala kuwa na ndoto za kukutana na madaktari bingwa katika maisha yao.Ulega alisema 


Huduma hizi zimepangwa kufanyika kwa siku saba hapa hospitalini kwetu  Sokoine mkoani Lindi, hivyo nawaomba madaktari wetu tutakaoshirikiana na hawa madaktari bingwa tujifunze kwa maana ya kujiongezea ujuzi wa kitabibu ili watakapoondoka huduma hizi zisitetereke bali ziboreke zaidi,hivyo wanachama na wanachi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wafike hapa kupata matibabu bora na stahiki.alisisitiza mhe ulega 


Pia aliwataka wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) ili waweze kunufaika kwa kupata matibabu mhe ulega alisema…Maradhi hayabishi hodi wananchi hivyo kwa kuchangia CHF uhakika wa matibabu ni mkubwa na pia  utachochea maboresho ya huduma za matibabu kwenye vituo vya afya,zahanati hadi hospitali mkoa wetu…..


Naye mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa taifa wa bima ya afya ndg Emanuel Humba alisema mpango huu maalum wa kupeleka huduma za madaktari bingwa  kwenye  mikoa ya pemebezoni , umezingatia mahitaji ya msingi na ya wakati kwani ni dhairi wapo wanachama wetu wengi waliopo vijijini,wana mahitaji makubwa ya huduma za madaktari bingwa pasipo kuzipata kwa wakati.


Tunatarajia pia kufanikiwa kwa mpango huu kutapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kubwa,hivyo kutoa fursa kwa madaktari hao kutoa huduma kwa uhakika zaidi sanjari na kuibua ukubwa wa mahitaji ya huduma za madaktari bingwa hapa mkoani lindi na nchi kwa ujumla.


Alisema Mfuko umewagharimia madaktari hao pamoja na utoaji wa dawa na vifaa tiba ,ili kufanikisha mpango huo wenye thamani zaidi ya  millioni hamsini,na  mpango huu maalum utekelezaji wake  umeanzia  mkoani Lindi na utakuwa ukitekelezwa kila baada ya miezi mitatu na wanachama wa Mfuko watapata matibabu kwa kutumia kadi zao sambamba na  wananchi watapata huduma kwa kupitia utaratibu wa kawaida ambao utakuwa na nafuu  

Alihitaja Mikoa ambayo iko kwenye mpango huu maalum ni Kigoma,Rukwa,Katavi,Mara ,Pwani na Tabora,hivyo wanachama na wananchi kwa ujumla wajitokeze ili waweze kutumia fursa hii muhimu na adimu kupata huduma za matibabu za madaktari bingwa.

Watanzania Ujerumani kusherekea miaka 49 ya Muungano,Mjini Kolon

$
0
0

Watanzania Ujerumani wapemania !
kusherehekea miaka 49 ya Muungano,Mjini Kolon,
Siku ya Jumamosi 27.04.2013.

Wasanii pia mnakaribishwa uwanjani !

umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
kufanya sherehe za miaka 49 ya muungano
wa bara na visiwani,kama linavyoonekana
tangazo hapo.

Watanzania wote na marafiki wa tanzanzania
mnaoishi ndani na nje ujerumani mnakaribishwa.

"Umoja ni Nguvu ! Utengano Ni Udhaifu"
 Chereko Chereko na mwenye mwana
 Watanzania jitokezeni kwa wingi 

kwa mawasiliano zaidi at kamati.utu@googlemail.com

Basata yawapongeza waandaaji wa Miss Universe Tanzania

$
0
0

 Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kulia) akiwakilisha tathmini ya mashindano ya Miss Universe Tanzania  mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kushoto ni  Mratibu Msaidizi wa mashindano hayo, Mwanakombo Salim . 
 Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kulia) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kushoto ni  Miss Universe 2011, Nelly Kamwelu
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (wanne kutoka kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini
============  =============== =====
Basata yawapongeza waandaaji wa Miss Universe Tanzania
Na Ripota Wetu
Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeipongeza kampuni ya Compass Communications kwa mafanikio makubwa waliyopata pamoja na kuandaa mashindano ya urembo nchini kwa muda mfupi.
Akizungumza katika kikao cha tathimini ya mashindano ya Miss Universe yaliyofanyika juzi makao makuu ya Basata,  Afisa Sanaa baraza hilo Malimi Mashili  alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.
Alisema kuwa mrembo wake, Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora, mpaka sasa anafanya vyema nje ya nchi katika sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.
Mbali na mafanikio hayo, Mashili alisema kuwa usimamizi bora wa kampuni hiyo imewafanya warembo kuwa na tabia njema na kuepukana na skendo mbali mbali ambazo zinawatokea warembo waliopitia mashindano tofauti na mashindano mengine ya urembo nchini.
“Ni mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze bidii ili kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na warembo wengi wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema Mashili.
Pia aliwataka waandaaji wa mashindano hayo kutafuta udhamini wa televisheni ambayo itaonyesha moja kwa moja ‘live’ mashindano hayo ili kupanua wigo wa wafuatiiaji wake kama ilivyo kwa mashindano mengine ya urembo.
 Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi kuongeza wigo wa washiriki kaika mashindano ya mwaka huu.
Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo alisema kuwa wameongeza mikoa saba zaidi na kufanya jumla ya mikoa 14 ambayo warembo wake watawania mataji mbali mbali mwaka huu.
Mikoa hiyo ni Katavi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Arusha, Mtwara, Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Kagera na Manyara.
Kwa mujibu wa Maria, Miss Universe Tanzania imeweka mikakati ya kuwaendeleza warembo ambao hawakufanikiwa kushinda katika mashindano hayo. Alisema kuwa mpango wao mkuu ni kuwapa msaada wa kielimu kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za hapa nchini hususani zinazoshughulika na masuala haya ya elimu.

NEW ARRIVALS @AK CLASSIC COSMETICS

$
0
0

  BAADA YA KUWA KIMYA KWA MUDA!!,WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWEE KUTOKA MAREKANI SASA WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA UHAKIKA KABISA KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUPIGA MSASA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS,NA BIDHAA ZINGINE ZA KILA AINA!!KWA HAKIKA WATU WALIOTUMIA BIDHAA ZAO WAMEJIONEA UTOFAUTI,BADO WEWE!!

 KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  
0753-482909/0713-468393.

Karibuni nyoooote!! 


MUHIMU:taarifa kwa umma kuhusu mwisho wa kubadili leseni za zamani za udereva


Barclays Bank yazindua kampeni yake mpya 'Maisha bomba na Barclays ndani ya sanduku la Dhahabu' kwa ajili ya wateja wao.

$
0
0
Baadhi ya wakuu wa Idara mbalimbali wa Barclays Bank-Tanzania kwa pamoja wakiwa wameshika Sanduku la Dhahabu,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni yao mpya kabambe ijulikanayo kama 'Maisha bomba na Barclays ndani ya sanduku la Dhahabu' kwa ajili ya wateja wao muhimu wa sasa na wale wanaolengwa baadaye iliozinduliwa leo jijini Dar.Kutoka kushoto ni Meneja Masoko Bi.Rahma Ngassa,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki ya Barclays-Tanzania,Bwa.Musa Kitoi,Ofisa Mahusiano-Barclays Bank Bi.Lilian Machera pamoja na Mkuu wa Bidhaa rejareja-Barclays Bank-Tanzania,Bwa.Samuel Mkuyu. 

Barclays itaendesha kampeni hiyo, ambayo itawapa wateja wao muhimu fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu,ukiweka pesa zako benki na ukaweza kubakisha salio lililokusudiwa,wewe ukiwa kama mteja wa benki hiyo utaweza kuingia kwenye droo hiyo, ambapo wateja 10 watajinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia shilingi milioni kumi za Kitanzania.

Promosheni hiy inaanza leo hii tarehe 11 April 2013 hadi tarehe 30 juni 2013 (miezi 3),aidha Shindano hilo litafanyika kila wiki ya kwanza ya kila mwezi  na kuzingatia  walioingia kwenye shindano mwezi uliotangulia.


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki ya Barclays-  Tanzania,Bwa.Musa Kitoi,akiongea mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni yao mpya kabambe ijulikanayo kama 'Maisha bomba na Barclays ndani ya sanduku la Dhahabu'.Bwa.Kitoi amesema kuwa shindano hilo liko wazi kwa wale wateja wapya na wa zamani wenye akaunti za binafsi ambao wanahifadhi pesa zao benki ya Barclays hata nchini kwenye akaunti ya kuweka.

 
Mkuu wa Bidhaa rejareja-Barclays Bank-Tanzania,Bwa.Samuel Mkuyu akifafanua zaidi kuhusiana na kampeni hiyo,ameeleza kuwa wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hiyo ni wale tu wenye akaunti za Hundi tano za Kitanzania (500,000 TZS), na salio hilo libakie kwenye akaunti bila kupungua ndani ya mwezi wa shindano,akaongeza kuwa wateja wote wa benki hiyo wataweza kuingia na kujishindia zaidi ya mara moja iwapo wataongeza ziadi ya shilingi laki tano (500,000TZS),ndani ya mwezi husika
 Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Barclays Bank wakiwemo na baadhi ya wanahabari mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo,iliozinduliwa mapema leo jijini Dar.

=========  ======  ======

Barclays Bank Tanzania yawaletea wateja wake kampeni kabambe ijulikanayo Kama‘Maisha bomba na Barclays ndani ya sanduku la dhahabu’



 Barclays Tanzania leo imetangaza rasmi uzinduzi wa kampeni yake ya Sanduku la Dhahabu kwa wateja wake muhimu wa sasa na wale wanaolengwa kwa baadaye.

Barclays itaendesha kampeni hii muhimu ambayo itawapa wateja wao muhimu fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3). Ukiweka pesa zako benki na ukaweza kubakisha salio lililokusudiwa, wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia kwenye droo ambapo wateja 10 watajinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya shilingi millioni kumi za kitanzania (10,000,000 TZS). Promosheni hii inaanza leo hii tarehe 11 Aprili 2013 hadi tarehe 30 iJune2013 (3 months)


Akiongea na waandishi wa habari leo hii, Kaimu Mkuu wa kitengo cha biashara cha benki ya Barclays Tanzania bwana amesemashindano hili liko wazi kwa wale wateja wapya na wa zamani wenye akaunti za binafsi ambao wanahifadhi pesa zao na benki yetu hapa tanzania kwenye akaunti ya Kuweka”.

Akiongezea wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hii ni wale tu wenye akaunti za Hundi na Akiba, na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye akaunti mpaka lifikie shilingi laki tano za kitanzania (500,000TZS), na salio hili libakie kwenye akaunti bila kupungua ndani ya mwezi wa shindano. 

Kwa wale wateja wapya wanaweza wakaweka shilingi laki tano kwenye akaunti zao bila kuzipunguza na wakaingia kwenye shindano la mwezi walioweka pesa zao. Wateja wetu wote wa sasa na wapya wataweza kuingia na kujishindia zaidi ya mara moja iwapo wataongeza ziada ya shilingi laki tano (500,000 TZS) ndani ya mwezi husika. Zawadi kubwa na ya jumla itatolewa kwenye sanduku la dhahabu, na pia washindi wote wa mwezi wa sita watapata nafasi ya kuchagua sanduku la dhahabu wanalolipenda kila mmoja na ndani yake kutakuwa na zawadi mbalimbali


  • 2 iPad mbili (2)vocha tano (5) za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shilingi laki mbili za kitanzania (TZS 200,000) kila moja, mashine za kufulia nguo mbili (2), na cinema moja (1) ya ndani.
  • 5 shopping vouchers worth TZS200,000 each.
  • 2 washing machines.
  • . Shindano hili litafanyika kila wiki ya kwanza ya kila mwezi na kuzingatia walioingia kwenye shindano mwezi uliotangulia.
  

Msafara wa mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu wapapata ajali,wawili wapoteza maisha na wengine wajeruhiwa vibaya.

$
0
0

Ajali hiyo imehusisha gari la Halmashauri ya wilaya ya Handeni ambapo watu wawili wamefariki akiwemo mwandishi wa Habari Hamis Bwanga na Afisa uhamiaji wa wilaya. 

Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 4.30 leo asubuhi katika kijiji cha Misima kweye barabara ya Handeni Korogwe wakiwa kwenye msafara wa kikazi kwenda vijijini kwaajili ya shughuli za upandaji wa miti kiwilaya. 


Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu amesema msafara huo ulikuwa na magari matatu ikiwemo ya kwake ambayo haijapata ajali.


Amesema gari hiyo ya halmashauri imepinduka baada ya kuacha njia na kwenda kama mita mia ambapo iliparamia jiwe na imeharibika vibaya. Kwa mujibu wa maelezo yake taarifa zaidi zitapatikana baadae kwani kwa sasa kinachofanyika ni kuwahudumia majeruhi ambao wanakimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro na pia kushughulikia miili ya marehemu.


Habari hii kwa hisani ya Vedasto Mwamsungu.

AIRTEL GHANA WINS TWO AWARDS AT THE 1ST PUBLIC RELATIONS EXCELLENCE AWARDS

$
0
0

Airtel Ghana has been recognized with two awards for Corporate Social Responsibility interventions. The awards, Public Relations Campaign of the year and Best Community Relations Programme of the year were handed to Airtel at the 1st Public Relations Excellence Awards Ceremony organized by the Institute of Public Relations Ghana at a ceremony in Accra over the weekend.

The first award was in recognition of Airtel’s comprehensive and widely acclaimed public relations effort before, during and after the company went to the rescue of the Odumase Krobo Presby School in Odumase.

The second award was for Airtel Ghana’s biggest social intervention programme, Touching Lives, which has already received several awards in recognition of its massive impact on a wide section of the Ghanaian society.

Airtel is committed to increase sustainability in the educations sector, reaching the grassroots of societies across Africa. Among its largest projects is the ADOPT A SCHOOL program where the most impoverished public primary schools are adopted by AIRTEL and provided with facilities including classrooms, desks text books, scholastic materials, uniforms and ICT learning facilities. Similar to Ghana, AIRTEL Tanzania has thus far implemented this project for Kiromo Primary school in Bagamoyo.

WAKENYA WAZIDI KUNG`ARA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™

$
0
0

 Washindi wa kipindi cha Nne cha Guinness Football Challenge, Enphatus Nyambura(kushoto)  na Samuel Papana(kulia) katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and Flavia Tumsiime jana baada ya ushindi.

========  ======== =========
WAKENYA WAZIDI KUNG`ARA  GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™


 Aprili 10, 2013, Dar es Salaam;  Katika sehemu ya nne jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™  yalikuwa na ushindani mkubwa  lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa. 

Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga  ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia fedha za kimarekani dola 1,500.


Enphatus na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika sehemu ya tano ya mashindano haya, yanayorushwa na vituo vya Televisheni vya ITV na Clouds TV  timu nne mpya zitaingiauwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kuendelea na mashindano hata kuingia hatua ya Pan-African. Je timu nyingine ya Kenya inaweza kushinda?


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .


Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.


UHUSIANO KATI YA PETE ZA BAHATI NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YA MWANADAMU.

$
0
0

Kabla  hatujafahamu   kuhusu  pete  za  bahati  ni  vyema  na haki
tukajua  kuhusu  IMMO Ring.  IMMO  Ring  ni  pete  inayo  undwa  na
madini  aina  tano  ambayo  ni  Shaba, Dhahabu, Fedha, Zinki na  Chuma
 jambo  ambalo  ni  muhimu  sana  katika  kuvuta  na  kuweka  uwiano
kati  ya  maisha  ya  mwanadamu  (  human  life  ) na  vitu  asilia
vinavyo  mzunguka  (  nature ). Hii  ni  kwa  sababu  hata  " nature"
yenyewe  inaundwa  na  vitu  vikuu  vitano  ambavyo  ni Moto, Maji,
Udongo, Hewa  na Anga. Hii  ndio  sababu  IMMO Ring  ndio  pete  ya
ajabu  inayo  leta  majibu  na  matokeo  makubwa  na  mazuri  sana
kwa  mtumiaji.

Pete  ya  IMMO  Ring  ina  nguvu  za  ajabu  sana  na  inaweza
kukusaidia  kutimiza  jambo  lolote  lile  unaloliitaji  katika
maisha  yako, ili  mradi  halipo  kinyume  na  sheria  za  nchi  yako.
Pete  hii  inaweza  kukusaidia  katika  masuala  ya  biashara,  mali,
utajiri, ndoa, kazi, mahusiano, uongozi, kujikinga  na  wachawi
nakadhalika.  Kwa  wale  wanao  hitaji  mali  na  utajiri, pete  hii
ya  maajabu  imewasaidia  maelfu  ya  walio  bahatika  kuitumia  na
inaendelea  kuwasaidia  maelfu  kwa  mamia  ya  wanao itumia.

GHARAMA  YA  PETE  HII  YA  MAAJABU: Pete  hii  hutolewa  bure  kwa
yoyote  anaye  ihitaji  na  malipo  yake  ni  baada  ya  muhusika
kufanikisha  jambo  analo  lihitaji.

KWA  MAHITAJI  YA  PETE  HII, WASILIANA  NAMI  KWA  SIMU  0656306725.

 KARIBUNI  SANA.

N.B : Matumizi  ya  pete  za  bahati  yanapaswa  kuendana  na  nyota
ya  muhusika. Ni  hatari  sana  kwa  mtu  kutumia  pete  ya  bahati
ambayo  haiendani  na  nyota  yake. Kujua  kuhusu  nyota  yako  na
aina  ya   pete  unayo  takiwa  kuitumia, tafadhali   wasiliana  nami
kwa  simu   0656306725  au  onana  na  mnajimu  yoyote aliye  karibu
nawe.

MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  DK. MUNGWA    KABILI, MNAJIMU  NA 
MTAALAMU  WA  TIBA  ZA  JADI  KUTOKA  BAGAMOYO/SHINYANGA.  ANAPATIKANA 
 KWA   NAMBA  0656306725....Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  huduma  zake,
tafadhali  tembelea  :  www. mungwakabili.blogspot.com

Mbona West Africa wameweza nasi East Africa hatutoweza?

$
0
0

wakuu, 

Nilipokuwa  Tanzania Sunday Manara alikuja kuniona na ratiba ya kuanzisha Soccer Academy kwa vijana tatizo viongozi wengi wa TTF wameelimika lakini hawana upeo wa michezo kama viongozi wa zamani wa michezo walikuwa hawana elimu ya juu, lakini walikuwa na upeo wa michezo, je wenye elimu pekee itatusaidia au tuwachanganye pamoja na wenye vipaji vya kuzaliwa na upeo wa michezo? cjuwi tutumie njia gani kuanzisha ligi kabambe ya Taifa na mfuko wa kufungua Soccer Academy kufuatana mawazo na utaalamu wa Sunday kuhusu Soccer la Tanzania?

alinishauri nishirikiane na viongozi wa wilaya ya Temeke na Ilala kuna wengi tumekuwa pamoja miaka ya 70`s kwa sasa Sunday amejenga na kuishi chang`ombe karibu na National stadium wilaya ya Temeke.
 
*Freddy Macha na wanahabari wenzio jigongeni vichwa venye fikra za uwezo mkubwa wenye busara mje na solution  tatizo la soccer la Tanzania linashuka kufuatana na mtandao wa mabloggu na vyombo vya habari haviweki mvutio mkubwa kurudisha imani ya soccer kupendwa tena kitaifa au mvutio wa ligi kubwa za ughaibuni zimewatawala vijana wetu hadi kuvunja mapenzi na soccer la ligi zetu tufahamu Brazil sasa wachezaji wengi wanatoa mchango wa ku-support kukuza ligi ya taifa na soccer na sisi hatutoweza kama tukiwawezesha vijana kwa mvutio mkubwa wa ma-blogg na vyombo vya habari?
 
 
Global advance Tanzania Network
Denmark
source: Bongo celebrity

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI WA MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME MKOANI DODOMA LEO

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes katika picha ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia huku Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes na Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lendhardt wakimponegza kwa ishsra hiyo ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes na Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lendhardt wakishuhudia uzinduzi huo wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes kwa hotuba nzuri katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes aliyemponegza kwa hotuba nzuri ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka baada ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

WARSHA YA WANAHABARI WA MKOA WA DODOMA KUHUSU UZINDUZI WA MPANGO KAZI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WATOTO

$
0
0

 Bibi Georgina Mtenga kutoka shirika la UNICEF- Tanzania akiwasilisha mada wakati wa warsha kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma kuhusu Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kutokomeza Ukatili kwa Watoto.

Bw.Erasto Chingo'ro Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maendeleo ya Jamii, (aliyesimam Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bw.Benedict Missani na Kulia ni Georgina Mtenga-UNICEF.

 Bibi Rose Minja, Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto akifafanua jambo wakati wa kikao hicho


Sehemu ya Wanahabari wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa kikao kazi na wanahabari kuhusu Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kutokomeza Ukatili kwa Watoto

KING CLASS MAWE AJIANDAA KUMKABILI AMOSI MWAMAKULA MEI MOSI

$
0
0


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ally Masaga wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi dhidi ya Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba .
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde naIbrahimu Toll wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba.

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Kasimu Gamboo wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba.
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Kasimu Gamboo wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba .
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tamasha Airtel Yatosha kuhamia chalinze siku ya Kesho Jumamosi na Jumapili.

$
0
0
Tamasha la Airtel Yatosha lenye lengo la kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha linalofanyika katika mikoa mbalimbali nchini mwishoni mwa wiki hii litafanyika katika mkoa wa Pwani.

Shangwe za Airtel yatosha litajumuisha wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Ney wa Mitego, sir Juma Nature, kikundi cha Tip top connection kikiongozwa na madii,  msanii wakizazi kipya Roma Mkatoliki pamoja na burudani nyingi toka kwa wasanii chipukizi na burudani za dansi na acrobatic kutoka katika kikundi cha vinoko.

Tunawakaribisha watanzania na wakazi wa mkoa wa pwani kuhudhuria tamasha ili siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 13 na 14 mwenzi wa 4,  katika viwanja vya sokoni chalinze, kuanzia saa tatu mpaka saa kumi na mbili jioni.

Kiingilio ni BURE, njoo na kitambulisho chako usajili namba yako na kuunganishwa na huduma poa ya Airtel yatosha na kupata ofa kibao kutoka Airtel.

Airtel itaendelea na burdani hizi za shangwe katika mikoa mingine katika kuitambulisha kwa wateja wake na watanzania huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.  Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99#

RAIS KIKWETE AFUNGA SEMINA KWA MAWAZIRI YA UTEKELEZAJI WA MFUMO MPYA WA UTENDAJI SERIKALINI

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifunga semina kwa mawaziri na makatibu wakuu  walioketi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete  tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiweka saini kama wadhamini wa waraka wa  kujifunga katika utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa semina kwa mawaziri na makatibu wakuu  kujadili mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete  tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.
 Mawaziri wa  Fedha, Kilimo, Uchukuzi, Maji, Nidhati na Madini na Elimu wakiweka saini  waraka wa  kujifunga katika utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara sita  hizo sita baada ya  semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 22 Februari, 2013 na kumalizika mwezi huu wa  Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa na mawaziri na makatibu wakuu wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia Dkt Idris Jala wakti wa kuujadili  mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa PEMANDU, ambapo utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru akitoa majumuisho ya uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.PICHA NA IKULU

AFANDE SELE AFUNGUKA KUHUSIANA NA MIGOGORO YA KIDINI

$
0
0
      Mfalme  wa  Rhymes  Tanzania,  Afande  Sele  ameamua  kufunguka  kufuatia  migogoro  inayoendelea  kuibuka  nchini  juu  ya  imani  za  kidini.

   
     Afande  amefunguka  hayo  jana  jioni  nilipokutana  naye  katika  studio  za  Diggital  Vibes  za  mjini  Morogoro, anapofanyia  wimbo wake  mpya  aliomshirikisha  Belle  9. 
  
     " Ujumbe  wa  wimbo  wangu  mpya,  unahusiana  na  maswala  ya  imani  za  dini.  Leo  hii  watanzania  tumefik hatua  ya watanzania  tumeanza  kutengana  kwa  dini?  aisee  hii  ni  hatari,  tunapoelekea  siko  kabisa  ndugu  zangu, tunatengana,  

tunapigana,  tunaharibiana  mali  kisa  imani  ya  dini wakati  dini  zimekuja  na  tulikuwa  na umoja  na  watanzania  wote  ni  ndugu.  nimekuja  nawaletea  ujumbe  na  kila mmoja  ausikie  kupitia  wimbo wangu  mpya  nimeimba  na  Mdogo  wangu Belle,  lengu  ni  kuwahamasisha waanzania,  tuziache  itikadi  izo  kwani mazala  yake  ni  makubwa  sana.  tutajuta. wimbo"  

  Wimbo  huwa  wa  Afande  unazungumzia  juu  ya imani  za  kidini  na  matukio yanayoendelea  ivi  sasa  na  Afande  kiwahasa  kuachana  na  mambo  hayo  na  tuishi kama  ndugu  kama  zamani  huku  akizungumzia  hotuba  ya  hayati  Mwl  Nyerere.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images