Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 62 | 63 | (Page 64) | 65 | 66 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Kwa yeyote mwenye sherehe unaweza kupata keki kama hii na nyinginezo za aina yoyote,wala usiwaze,usiumize kichwa,ni rahisi tu,kupiga simu namba; 0782297408 ulizia Angella Msangi na utahudumiwa fastaa.

  0 0   Welcome !

  International African Festival Tübingen, Germany 2013
  Be part of 100.000 visitors at the largest Extravanganza !
   
   African Pilgrimage to Tübingen, Germany 2013 – outdoor & Entry Free

  International African Festival Tübingen proudly announces its 2013 season today, bringing together world class African lifestyle, music, food, exciting newcomers to the international stage from 8- 11 august 2013 – African Village (Festplatz) Open-air –Down town Tübingen, Germany
  It is the fastest and largest growing Diaspora cultural event transforming the city of Tübingen in south of Germany into a pilgrim city, bringing African Diaspora worldwide irrespective of country of origin, gender and religious background , friends and well wishers of Africa together .

  More than 100.000 visitors are expected to attend International African Festival Tübingen 2013.This event promises a multi-dimensional exploration of interplay of authentic African culture and lifestyle -150 artists –live- featuring fresh sounds and voices –Ngoma Africa Band, Soweto Entsha, Wamali percussions, street arts, workshops and culinary expression. The Festival once again invites artist and audiences of all ages to experience African music, arts, culture and party, a mélange between traditional and modern Africa, bringing African hip-hop, soukouss and African movies on the international stage.

  Festival highlights will include- a grandiose opening ceremony lead by African children & youths, celebrities, African ambassadors rep. in Germany under the chairman ship of the Ghana Ambassador, program for families, panel discussion and late night events - the biggest African party in Germany, Stuttgart on Saturday night –form 22 o’clock featuring celebrities and Sunday will be special day for family – special church and Gospel day and closing ceremony
  Visual art is at the focus on our Festival and this year the African royal ballet is visiting all the way from Mali featuring Djiby & Basy Kouyate, dance styles and moves to support and build schools in Mali,   Christoffel-Blindemission project helping the blind to see in Africa, bongob trust and many more. 

  Stay updated on www.afrikafestival.net, follow and like us on facebook
  For more details you may  please contact:
  Madam Enie Muyang Tatah,CEO and Founder / Call +49-15210610374 /Email: kontakt@afrikafestival.net

  0 0


  Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Masuala ya Kisiasa nchini Somalia Balozi Dr. Augustine Mahiga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa nchi za Afrika mashariki kuichukulia Somalia kama taifa lingine lolote na kulipa ushirikiano kwani kwa sasa lina amani na utulivu tofauti na watu walivyokuwa wakilifikiria. Kulia ni Msemaji wa Ofisi ya UN inayoshughulikia suala la Somalia Nick Binback.

  0 0


  Na Maelezo Zanzibar   13/04/2013

  Watendaji wa Serikali wanaoshiriki katika kuandaa Machapisho ya Taarifa za Sensa ya Watu na Makazi wametakiwa kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa ili taarifa kamili za Sensa ya mwaka 2012 ziweze kuwafikia Wananchi kwa wakati.

  Wito huo umetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd kwenye Uwasilishaji wa Ripoti ya Idadi ya Watu kwa ngazi za Utawala katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Bwawani Mjini Zanzibar.

  Amesema kupatikana kwa Taarifa hizo mapema kutawawezesha Wananchi kutoa maoni yao juu ya Sensa na kupendekeza Mikakati ambayo Taifa linaweza kuitumia katika kukabiliana na changamoto zinazohusiana na kasi ya ongezeko la Idadi ya Watu nchini.

  Amewataka Wananchi kutosita kupeleka maoni yao kwenye Ofisi za Takwimu zilizopo katika kila Mkoa ili kuifanya Sekta ya Takwimu nchini kuwa bora zaidi.

  Balozi Seif amesema kwa vile Ripoti hiyo itagawiwa kwa Wadau wote ikiwemo Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Shehia Viongozi hao wanapaswa pia kuzingatia Takwimu husika katika kutekeleza wajibu wao.

  Ameongeza kuwa Ripoti ya Idadi ya Watu ni matokeo mazuri ya kazi kubwa iliyofanyika Agosti 26, 2012 ambayo Imebainisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina Watu Milioni 44.9  

  Kwa upande wake Waziri wa Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee amesema katika kuandaa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi kwa Mwaka 2013/2014 wanatarajia kutumia Takwimu za Ripoti hiyo.

  Aidha Waziri Mzee amewataka Wananchi wanaotumia Mitandao kupitia Tovuti ya Takwimu ili kujionea Idadi ya Wakazi katika ngazi wanazoishi.

  Amesema badala ya kusubiri Machapisho ya Takwimu kujua Idadi halisi ya Wakaazi katika maeneo husika, Wananchi wanaweza kutumia fursa ya Mtandao kujionea Idadi hiyo kupitia Tovuti ya Takwimu

  Kwa Upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab ameitaja Tovuti hiyo kuwa ni www.ocg.go.tzambapo Matokeo ya Sensa yanapatikana humo.  

  Sensa ya Watu na Makazi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilifanyika Agosti 26, 2012 ambapo Idadi ya Watu imeongezeka zaidi ya mara tatu kutoka Watu Milioni 12.3 mwaka 1967 hadi Watu Milioni 44.9 mwaka 2012

  Aidha katika Ongezeko hilo Wanawake ni wengi zaidi kwa Asilimia 51 ikilinganishwa na Wanaume ambao ni Asilimia 49 kama ilivyokuwa katika nchi nyingi za Afrika.

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0


  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 na kuonyesha kuwa kuna skandali kubwa sana katika akaunti ya Deni la Taifa. 
  Nanukuu
  ‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya deni ya shilingi 619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.’ (Taarifa ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158). Mwisho wa Kunukuu

  Katika Taarifa yake hiyo CAG anaendelea kuonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kukua na mwaka unaoishia mwezi Juni 2012 deni lilikuwa kwa asilimia 17 kutoka mwaka unaoishia mwezi Juni 2011.

  Kukosekana kwa maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na kupata majawabu stahiki. Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa kuna mahusiano makubwa sana kati ya Deni la Taifa la utoroshaji wa fedha kwenda kwenye mabenki ya ‘offshore’. Katika kitabu cha ‘Africa’s Odious Debts: How Foreign Loans and Capital flight bled a continent’ kilichoandikwa mabwana Leonce Ndikumana na James Boyce imeonekana kwamba Deni la Taifa huchochea utoroshwaji wa Fedha kwenda kuficha nje ya Tanzania.

  Mabilioni haya kwenye akaunti ya Deni la Taifa yanashtusha sana. Kambi ya Upinzani Bungeni kwa miaka miwili mfululizo imekuwa ikitaka ukaguzi maalumu kwenye akaunti za Deni la Taifa lakini Serikali imeshindwa kufanya hivyo. Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC pia nimemtaka CAG afanye ukaguzi huu maalumu.
  Kambi ya upinzani Bungeni ilisema hivi katika Bajeti yake kivuli 2012/13:
   
  DENI LA TAIFA
  Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inasikitika kwa serikali kuendelea kutengeneza madeni kwa Taifa kwa kuendelea kukopa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya serikali. Wakati Serikali inasisitiza kwamba Deni letu linastahmilika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaonyesha mashaka makubwa sana kutokana na kasi ya kukua kwa Deni la Taifa. 

  Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha  kuwa Deni la Taifa linazidi kuongezeka kwa asilimia 38% kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka 2009/2010 hadi shilingi trillion 14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Deni la Taifa limefikia shilingi trillion 20.3 mpaka ilipofika mwezi Machi mwaka 2012. Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia shilingi trillion 22. 

  Mheshimiwa Spika, Suala hapa sio ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikali bali ni kwamba tunakopa kufanyia nini? Bajeti ya Mwaka 2012/13 inayopendekezwa inaonyesha kwamba Serikali itakusanya shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida. Ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida. 

  Hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi. Bajeti inaonyesha kwamba Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka 2012/13.  

  Serikali ikubalikutekeleza mapendekezoya Kambi ya Upinzani ya kuimarisha ukusanyaji  wa kodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama sekta ya madini na mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza ukwepaji kodi, na kuepuka matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima.

  Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapenda kusisitiza kwamba Bunge lifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Deni la Taifa ili kuweza kubaini ukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na mikopo ambayo Serikali inachukua kama inakwenda kwenye Maendeleo na miradi ipi na kama miradi hiyo ina tija. 

  Vilevile tumependekeza kwamba Mikopo yote ambayo Serikali inachukua iwe inapata idhini ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge sharia ili kiwango cha juu cha kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. Kuiacha Serikali inaendelea kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupeleka mzigo wa kulipa madeni haya kwa kizazi kijacho. Hatuwezi kukubali Wazee wetu waishi maisha yao, waishi maisha yetu na pia wakope maisha ya watoto wetu. Mwisho wa kunukuu.

  Kambi ya Upinzani inarejea kutaka ukaguzi maalumu kuhusu akaunti za Deni la Taifa na maelezo ya kina ya Serikali kuhusu shilingi 620 bilioni ambazo hazina maelezo kwenye Deni la Taifa. Hatuwezi kukaa kimya kuona Watanzania wanabebeshwa madeni ambayo kimsingi ni madeni bandia yanayotajirisha watu wachache wenye uwezo na ujasiri mkubwa wa kuiba, kupora nakufisidi hazina ya Taifa letu.
   
  Kabwe Zuberi Zitto,Mb
  Waziri Kivuli Fedha na Uchumi

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC) na viongozi na wadau mbalimbali wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14 akisaidiana na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia baada ya kufungua rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14 akiwa na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kufungua barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14 akiwa ameongiozana na Naibu waziri wa wizara ya ujenzi, Mhe Gerson Lwenge (kulia), Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, na mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Chiku Gallawa (kushoto) Barabara ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti kama kumbukumbu yaq ufunguzi rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Kuhsorto kwake ni Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), na kulia kwake ni Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC) akipanda mti kama kumbukumbu ya uzinduzi rasmi wa barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Kulia ni Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Msafara wa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ukipita juu ya sehemu ya barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. PICHA NA IKULU

  0 0

  Wawezeshaji, wakipokea maswali kutoka kwa washiriki wa mdahalo wa kitaifa wa wanawake na kufafanua mada ya migogoro ya ARDHI na sheria zake. Wataalam hawa wakishirikiana na mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi walitoa majibu ya kina kuhusiana na migogoro ya ardhi na athari zake kwa mwanamke.
   Mshiriki akichangia kwa uchungu mada ya ardhi na jinsi kutokujua sheria ya ardhi inavyomkandamiza mwanamke wa kitanzania.


   Bi. Mbaema kutoka Loliondo akiongea kwa msisitizo kuhusu tatizo la ardhi linalowakumba wakazi wa eneo lake dhidi ya mwekezaji Mwarabu.
    Masesa Luanda, Afisa Maendeleo ya jamii kutoka mkoa wa Katavi- akisikiliza kwa makini kuhusu mada ya ardhi na haki na wanawake katika kumiliki ardhi.

   Angela Chagwa (wa kwanza kulia) kutoka Employ Yourself Tanzania ambaye alikuwa mwezeshaji wa mada zinazohusu wanawake na uchumi akiungana na washiriki wa mdahalo kusikiliza kwa makini mada ya ardhi na umiliki wa rasilimali kwa mwanamke.

    Kutoka kushoto ni Khamar Kashoro kutoka shirika la Care International na Bi Hilda Mashauri kutoka shirika la EKAMA Development wakisikiliza matatizo na vipaumbele mbalimbali vya wanawake kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania.
   Mmoja wa wanawake wa Kimasai akielezea kero yao katika mgogoro wa ardhi unao wakabili huko Loliondo.
   Mwezeshaji Akifafanua na kutoa uelewa kwa wakinamama washiriki wa mdaharo kuhusu ardhi, hifadhi au maeneo ya pembezoni mwa Mito na kuwataka wanawake watafute ardhi hata kwa kununua.
   Wanawake waliohudhulia mdaharo wa wanawake, wakiandika masomo ya mada wanazojifunza ikiwa ni kwa siku ya tatu.
   Mshiriki kutoka kijiji cha Nghaya wilaya ya Magu akielezea mgogoro wa ardhi na kuvunjiwa nyumba kwa wakazi waishio pembezoni mwa mto Simiyu.
    Kutoka Kushoto, Jane Kapongo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyehudhuria kusikia na kujibu changamoto mbalimbali za ardhi zinazowakabili Wanawake. 
  =========  ======= =======

  Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake Jana uliingia siku ya tatu ambapo mada kuu ilikuwa Haki za Wanawake katika rasilimali za asiliambapo mada ndogo ndogo kama sera ya ardhi na sheria ya ardhi ya kijiji ya Tanzania, umuhimu wa wanawake kumiliki ardhi na rasilimali nyingine pamoja na uwekezaji wa ardhi na madhara yake kwa wanawake zilijadiliwa.

  Mada ndogo nyingine zilikuwa ni pamoja na nafasi ya wanawake katika jamii yenye rasilimali pamoja na wanawake wazalishaji chakula, upatikanaji na umiliki wao wa rasilimali muhimu..

  Jopo la wataalamu wa maswala ya ardhi lilikuwepo kusikiliza na kujibu maswali mbalimbali yaliyojitokeza. Wataalamu hao walikuwa ni Bernard Baha (Mwanaharakati wa maswala ya Ardhi), Victoria Mandari ( Mwanasheria wa kujitegemea), Yifred Miyenzi (Mkurugenzi Haki Ardhi), Juvenile Rwegasira (Mwanasheria kutoka TAWLA, Lilian Loloitai (Afisa kutoka CORDS) pamoja na Enock Kijo (Mwanaharakati wa maswala ya Ardhi)

  Vilevile Jane Kapongo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alikuwepo kusikiliza na kujibu baadhi ya changamoto zilizotajwa na wanawake hao.

  Mdahalo wa Kitaifa wa wanawake ni tukio linalofanyika kwa hisani ya mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) kuanzia tarehe 10-14 April, 2013 mkoani Dodoma.

  Mdahalo huu umewaleta pamoja wanawake wapatao 300 walioko pembezoni (marginalised) kutoka katika mikoa yote ya Tanzania.


  Tunachukua fursa hii kuwasihi wananchi wote wafuatilie kwa makini mdahalo huu kupitia mitandao ya kijamii na tovuti rasmi iliyozinduliwa na Mhe. Sophia Simba (MB), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

  Twitter: www.twitter.com/SautiYaMwanamke  #MdahaloWaWanawake
  0 0


  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo Mhe. Said Mtanda akionesha nakala ya Mpango Kazi mara baada ya Kuuzindua
   Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba akiwasilisha taarifa ya namna Wizara yake itakavyotekeleza Mpango Mkakati huo kwa Kushirikiana na Wadau.
   Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Kassim Majaliwa akieleza Utekeleaji wa Wizara yake katika Mpango Mkakati hu
   Mwakilishi Mkazi wa UNICEF-Tanzania Bw. Jama Guilad akiwasilisha taarifa ya UNICEF juu ya Ukatili kwa Watoto Tanzania
   Naibu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Bibi.Anna Maembe akieleza taarifa ya awali kuhusu Uzinduzi huo
   Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dr.Seif Rashidi akieleza namna Wizara ya Afya ilivyojipanga kutekeleza Mpango huo.
   Wadau wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kutokomeza Ukatili katika Meza Kuu. kwanza Mhe.Kassim Majaliwa,akifuatiwa na Mhe.Sophia Simba,Mwakilishi Mkazi UNICEF Bw. Jama Gulaid,Mhe.Seif Rashid, Mhe.Peraira Silima
  Sehemu ya Wageni waliohudhuria Uzinduzi huo wakiongozwa na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii

  0 0


  2003 Toyota Noah... FOR SALE BY OWNER 

  0 0


  0 0

  Meneja Masoko wa kampuni ya Push Media Mobile, Rugambo Rodney akisisitiza jambo wakati wa utambulisho wa bahati nasibu ya Kigitali Zaidi.
  =====================
  Kampuni  ya Push Media Mobile imetoa ving’amuzi  91 kwa ajili ya kushindaniwa  katika promosheni ya “Kidigitali Zaidi”  ambayo lengo lake kubwa ni kuongeza idadi ya watumiaji wa mfumo wa matangaza ya televisheni ya kidigitali.
  Meneja Masoko wa Push Media Mobile, Rugambo Rodney alisema  kuwa promosheni hiyo itaanza kwanza kwa miezi mitatu ambapo kila siku mshindi mmoja atajishindia king’amuzi.
  Rugambo alisema kuwa ili kushinda king’amuzi  tuma neno “shinda” kwenda namba 15522 na mshindi anaweza kujipatia king’amuzi cha aina ya StarTimes, DiGi Tek au Zuku.
  Alisema kuwa wamesikia kilio cha watanzania kuhusiana na gharama za kupata king’amuzi na wao kuanzisha promosheni hiyo ambayo washindani watapata king’amuzi sawa na ‘bure’ na kuzishukuru kampuni za Global Publishers, Kituo cha televisheni cha DTV, Times FM, Magic FM, Maisha Club na Baakubwa kwa ushirika wao katika kampeni hiyo.
  Kwa mujibu wa Rugambo, promosheni hiyo ni endelevu na lengo lao ni kuona watanzania wanapata haki ya kupata habari kwa njia ya televisheni.
  “Tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya promosheni hii, kila siku kumekuwa na kilio cha watanzania kuhusiana na gharama za kupata king’amuzi, wengi hawana na wanakosa taarifa za kila siku ikiwa pamoja na habari za michezo, sanaa, urembo na za kisiasa,” alisema Rugambo.
  Alisema kuwa jumla ya shs  25 millioni zitatumika katika  promosheni hiyo ambapo mshindi wa siku ya 90 atapata king’amuzi na televisheni bapa ‘flat screen’ yenye thamani ya sh. 1 million.


  0 0


  Ndugu zangu,

  Kwanza kabisa niwashukuru kwa dhati kabisa nyote mlionitumia salaam za kunifariji kwa njia za simu, email, facebook, majukwaa ya Mabadiliko, Wanabidii na JF. 
  Nimefarijika sana kutambua kuwa kuna wengi wenye kunifuatilia na kunijali.

  Ndugu zangu,
  Kama alivyowataarifu kaka yangu Nyaroonyo Kichehere, ni kuwa, jana Jumamosi nilikuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa tano asubuhi ya jana mpaka saa tatu usiku. Ilihusu mahojiano ya Polisi na mimi kuhusiana na sakata la ndugu yetu Absalom Kibanda.

  Ukweli sikukamatwa mahali popote, bali niliitwa na Kamishna ( Upelelezi) Advocate Nyombi. Alhamisi nikiwa Iringa, tukakubaliana na kiungwana na Kamishna Nyombi kuwa nifike Makao Makuu hayo ya polisi Jumamosi saa tano. Ikawa hivyo.

  Hapo nilipokelewa na Kamishna Nyombi. Baada ya mazungumzo mafupi ndipo akawaita maofisa wengine watano wa Upepelezi kufanya mahojiano nami. 
  Niliomba niwe na Mwanasheria, nikakubaliwa. 

  Nilimpigia simu kaka yangu Nyaroonyo, naye, kwa vile ni Wakili pia wa Kibanda akanisaidia kuhakikisha napata wakili mwingine. Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, ndugu yangu Nyaroonyo Kichehere alifanya alivyoweza. Ndani ya dakika 40 hivi alifika chumba nr 704 ghorofa ya saba akiwa na Wakili Jacquiline Rweyongeza na Legal Officer Dickson Mbonde. 

  Nilimshukuru Kaka Nyaroonyo Kichehere. Na nilimuaga kwa kumwambia; “ Nenda ukaifahamishe jamii juu ya hiki kilichonitokea”.

  Nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati kabisa dada yangu Wakili Jacquiline Rweyongeza na kaka Dickson Mbonde kwa kuacha yote ya Jumamosi na kuwa tayari kuwa msaada kwangu. Jacquiline alimuacha nyumbani mtoto wake wa miezi minne kwa ajili ya suala langu. Sina namna nyingine ya kumshukuru. Na hakika, msaada wao niliuhitaji sana.

  Nawashukuru pia kwa dhati kabisa, ndugu zangu Saed Kubenea, Mbaraka Islam na wengine wote waliokuwa na utayari wa kunisaidia pale msaada wao ulipohitajika. 

  Kwa ufupi, nimetoa maelezo yangu bila shuruti wala kutishwa. Na nimeweka wazi kuwa yanaweza kutumika Mahakamani kama yatahitajika au hata kama mimi nitahitajika, kwa namna yeyote ile.

  Kesho saa mbili asubuhi nitaripoti Makao Makuu ya Polisi kupewa maelezo ya kitakachofuatia.

  Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana kwa kuwa nami katika muda wote huu.

  Maggid,

  Dar es Salaam

  0 0


  Meneja Masoko wa Kampuni ya Palray watengenezaji wa fenicha mbalimbali, Thomas Simpokolwe kulia akimkabidhi mwanafunzi wa chama cha msaraba mwekundu tawi la kisutu, Grace Raphael sehemu ya msaada wa viti kwa ajili ya kusoma masomo mbalimbali ya uokoaji kulia ni Mwenyekiti wa msalaba mwekundu tawi la kisutu Bw.Rashid Mkawa.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Palray watengenezaji wa fenicha mbalimbali, Thomas Simpokolwe kulia akisalimiana na wanafunzi wa msalaba mwekundu tawi la kisutu baada ya kuwakabidhi madawati

  Meneja Masoko wa Kampuni ya Palray watengenezaji wa fenicha mbalimbali, Thomas Simpokolwe kulia akimkabidhi mwanafunzi wa chama cha msaraba mwekundu tawi la kisutu, Grace Raphael sehemu ya msaada wa viti kwa ajili ya kusoma masomo mbalimbali ya uokoaji kulia ni Mwenyekiti wa msalaba mwekundu tawi la kisutu Bw.Rashid Mkawa.
  Wanafunzi wa Msaraba Mwekundu Tawi la kisutu wakisaidiana kubeba madawati waliyo kabidhiwa.

  Wanafunzi wa Msaraba Mwekundu Tawi la kisutu wakisaidiana kubeba madawati waliyo kabidhiwa.Picha na www.burudan.blogspot.com

  0 0


  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajia kushiriki kwenye Mkutano Mkuu wa 76 wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) unaotarajiwa kuanza kesho (Jumatatu) Sochi, Russia.
   
  Mkutano huo wa kawaida wa mwaka ambao utashirikisha viongozi wa zaidi ya vyama vya waandishi wa habari za michezo 100 duniani, mwaka huu utaambatana na uchaguzi mkuu wa AIPS. 

  TASWA katika mkutano huo itawakilishwa na Mwenyekiti wa chama, Juma Pinto na Katibu Mkuu, Amir Mhando ambao wanatarajiwa kuondoka leo alasiri kwa ndege ya Emirates. 

  TASWA ni mwanachama hai wa muda mrefu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Duniani (AIPS) chenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi, ndiyo sababu kila mwaka tumekuwa tukishiriki mikutano hiyo kwa awamu mbalimbali za uongozi ukiwemo wa kwetu uliochaguliwa mwaka 2010.

  Mwaka 2011 tulishiriki Mkutano Mkuu wa AIPS uliofanyika Seoul Korea, Korea Kusini na tuliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti, Maulid Kitenge na mimi nikiwa Katibu Msaidizi.

  TASWA pia ilishiriki Mkutano Mkuu wa AIPS uliofanyika Innsbruck, Austria Januari mwaka jana, ambapo Katibu Mkuu, Amir Mhando alihudhuria. Tunaamini hii ni njia mojawapo ya kukutana na wadau mbalimbali kwani AIPS imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo kwa wanachama wake na semina za michezo mbalimbali.

  Ujumbe wetu katika mkutano wa mwaka huu ambao utamalizika Ijumaa wiki ijayo ni mkubwa, hivyo tunaamini utakuwa na manufaa kwa chama na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla.

  Ahsanteni. 

  George John

  Kaimu Katibu Mkuu, TASWA(0713-214724)

  14/04/2013

  0 0  Peter Mwenda

          SHIWATA imeandaa maonesho maalum kila mwezi ili kutoa nafasi kwa wasanii wa fani ya mbalimbali pamoja na wanamichezo kuonesha vipaji vyao.

   Wasanii wengi chipukizi wanakosa mahali pa kuonesha kazi zao, mara nyingi kazi za wasanii wakubwa ndizo ambazo hurushwa katika redio na luninga (TV).

   SHIWATA imeamua kuandaa maonesho haya kwa malengo makuu yafuatayo

  (1)   Kukuza vipaji

  (2)   Kuwapatia soko (underground) mahali ambapo wanaweza kuonesha vipaji vyao na kuwashawishi mapromota mbalimbali kuwaajiri.

  (3)   Kuelimisha jamii kuhusu matatizo mbalimbali kama maadili na magonjwa kama UKIMWI,malaria.

  (4)   Kuimarisha umoja kati ya wasanii na wanamichezo

   SHIWATA inawataarifu viongozi mbalimbali na makundi ya sanaa na Michezo pamoja na wasanii binafsi kutakua na mkutano Siku ya Jumatano Aprili 17 mwaka huu saa 8 mchana katika ukumbi wa Splendid,Bungoni Ilala kupanga ratiba na kupata taarifa zaidi.

  Onyesho la Kwanza litaoneshwa katika ukumbi wa Star Light Hotel, Mnazi Mmoja Dar es Salaam siku ya Jumamosi Aprili 24.

   Michezo itakayoneshwa ni pamoja na maigizo, sarakasi, ngoma, kwaya, karate, Taekwondo, Taarab, Dansi, Bongo Flava, Mavazi, Gospal na Kasida, mada kuu katika maonesho hayo ni Amani na Utulivu.

   Hii ni nafasi ya pekee kwa wasanii chipukizi (underground) kuonesha vipaji vyao.Watengenezaji wa filamu, mapromota, wamiliki wa bendi, MaDj na wanunuzi wa mbalimbali wa kazi za sanaa wanaalikwa ili waweze kuona vipaji na kununua kazi za wasanii hao chipukizi.

   Wanafunzi wenye vipaji kutoka shule za msingi, Sekondari na vyuo mbalimbali wanaalikwa kuja kuonesha vipaji vyao.  Mipango iliyofanywa ili maonesho haya yarushwe live kituo kimojawapo cha televisheni.

   Kutokuwa na chakula kwa wasanii na zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa wasanii watakaofanya vizuri katika kila onesho.

   Hii itakuwa nafasi nzuri kwa wapenzi wa burudani ya sanaa kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajui wapi wanaweza kupata burudani kama hiyo kiingilio kitakuwa bure.

   Wote mnakaribishwa

   Peter Mwenda 0715/0752- 222677

  Ofisa Habari wa SHIWATA


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Ruaha mkoani Morogoro leo, Aprili 14, 2013.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara wa CCM, uliofanyika leo Aprili 14, 2013 katika Kijiji cha Ruaha mkoani Morogoro.


   Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohamed Seif Khatib alipowasili leo eneo la Nane Nane, mjini Morogoro kuanza ziara ya kikazi ya siku nane katika wilaya zote za mkoa huo.
  Ndugu Kinana akihutubia baada ya kuwasili eneo la Nane Nane ambapo alipokelewa na wafuasi wa chama hicho,mjini Morogoro mapema leo.


   Waendesha bodaboda wakiongoza msafara wa viongozi wa CCM ulipowasili leo mjini Morogoro

   Mmoja wa wafuasi wa CCM akishangilia huku akiwa amepakiwa kwenye pikipiki zizloongoza msafara huo. PICHA KWA HISANI YA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA NA BASHIR NKOROMO.

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla ya harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

   Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba akimshukuru Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla ya harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.


    Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba,  KATIBU Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleman Lolila (wa pili kulia), Kadhi Mkuu Sheikh Abdallah Mnyasi (kulia) na Shehe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad (kushoto) wakiomba dua baada ya harambee kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla  iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika harambee ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU.


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga baada ya kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 na Mwenykiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James  Mbatia aliyechangia shilingi milioni mbili  kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

  0 0


  Stanbic Bank Tanzania today announced that it has successfully closed a USD600 million amortisation private placement on behalf of the United Republic of Tanzania.

  The Government of the United Republic Tanzania successfully raised USD600 million from the international capital markets, in what is believed to be the first ever benchmark-sized private placement transaction by a sub-Saharan sovereign. The financing took the form of an unlisted and unrated seven-year floating rate instrument, the proceeds of which will be used for infrastructure projects within the country.

  The capital raised is in support of Tanzania’s infrastructure development programme for the 2012/2013 budget. The capital will be used to roll out projects across several sectors, including energy, roads and rail equipment.

  “Despite  the Tanzanian Government being unrated, Stanbic Bank felt confident to advise the government that its aim of raising the financing for infrastructure projects which is vital to the country’s economic development could be readily fulfilled through a well-targeted private placement note issue in the offshore markets. We opted for an amortisation private placement as this means the USD600 million is paid back in installments rather than a single large amount,” says Hon. Dr.  William Mgimwa, Minister of Finance.

  “We chose the private placement route as we felt it was the quickest option for the country given that Tanzania is not yet rated and this also gave Tanzania access to a wide international investor base similar to a Eurobond,” he added.

  The private placement will be repaid in nine equal biannual amortisations commencing on the third anniversary of the issue date, with a final maturity date of 8 March, 2020.

  “This deal represents a milestone in our ability to advise the government on how to access funding from the capital markets.  It is also vital to note that these investments in key infrastructure projects, will, over the course of their economic lives, unlock benefits that will significantly enhance Tanzania’s GDP,” commented Mr. Bashir Awale, Managing Director of Stanbic Tanzania. .

  Despite the unlisted and unrated nature of the transaction and a relatively soft market backdrop the book was four times over-subscribed after price guidance was released at 6m LIBOR plus 600bp. 

  “The solution achieved given the United Republic of Tanzania’s size and timing requirements for their investment requirements in infrastructure was done in an exceptionally efficient and cost effective manner for the client. We are extremely pleased to have closed such a prestigious deal as this,” says Ms. Shose Sinare, Stanbic’s Head of Corporate and Investment Banking. .

  Stanbic Bank remains committed to supporting the United Republic of Tanzania. 

  0 0


  Salamu ndugu yangu Michuzi, pole sana na shughuli za kila kukicha. Jina langu naitwa dada Dora, natafuta mwenza wa kuishi naye hivyo nimeona nitumie blog yako labda ninaweza fanikiwa kupata mtu sahihi.

  Mtu ninayemtafuta, awe na umri kuanzia miaka 32 mpaka 44 sio mbaya, pia awe hajaoa wala hana familia kwa maana ya mke na watoto. Ni vizuri kuishi na mtu mnayeendana, hivyo ningependa awe mkristo, dhehebu lolote haijalishi mradi awe mcha Mungu na atambue uwepo wa Mungu. 

  Pia awe na elimu kuanzia degree. Mimi kwa sasa nipo nje ya Tanzania, naomba atakaye niandikia asiandike tu sababu ameona tangazo bali awe na nia ya dhati ya kuanzisha familia hivi karibuni. mwenye malengo ya maisha, mpole na asiwe mbabe. Ajue nini maana ya kuwa mme. Awe pia mwepesi wa mawasiliano, yeyote anayeona yupo busy sana na hataweza mawasiliano ya mara kwa mara tafadhali naomba asiniandikie.
  Kwa aliye tayari napatikana kwenye barua pepe:
   
   
  natanguliza shukrani kaka michuzi

  0 0


   Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni, Bwa.Mgaza Muchiwa
   Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana
  Eliakimu Kapele ni Makamu wa Shule ya Sekondari Kivesa
  ======== ======= =========
  Na Thehabari.com, Handeni

  “KESI nyingi za tuhuma za kubaka na mimba kwa wanafunzi zinazotufikia zinashindwa kufikia hukumu maana mashahidi wanashindwa kuthibitisha pasipo shaka…nyingi zinaharibika sababu hawataki kusema ukweli, hivi karibuni nililazimika kuwaweka ndani wawili (mashahidi) kwa kuwa wanadanganya. Unakuta maelezo aliyotoa polisi ni mengine na akifika huku anageuka,” anasema Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana alipofanya mahojiano na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

  Hakimu Maligana anasema licha ya takwimu zao kuonesha kesi za mimba/kubaka wanafunzi kwa sasa zinapungua bado suala la kuharibika kwa ushaidi wa kesi za mimba ni changamoto. Anasema kesi nyingi za wanafunzi zimekuwa zikishindwa kufanikiwa hadi hatua ya hukumu kutokana na mtindo wa kuvuruga ushahidi.

  Anasema awali kikwazo kikubwa kwa kesi kama hizo ilikuwa ni upande wa wazazi na walimu kutotoa ushirikiano wa kutosha kwenye mchakato wa kesi. Lakini walimu na wazazi wameacha usumbufu huo hivyo imebaki kwa wanafunzi pamoja na watuhumiwa ambao mara kadhaa wanakuwa wapenzi wao.

  Anaongeza kuwa licha ya matukio hayo kupungua changamoto bado zipo.
  Takwimu za kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2012 zinaonesha mahakama hiyo ilipokea kesi 10 za tuhuma za mimba/kubaka kwa wanafunzi, huku kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2013 ni jumla ya kesi sita tu zimepokelewa katika mahakama hiyo. Anasema kesi sita za mwisho kupokelewa zipo katika hatua anuai.

  Zuber Chembera ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni (OCD), akizungumza na mwandishi wa makala haya ofisini kwake, anakiri kupungua kwa matukio ya kesi za mimba/kubakwa kwa wanafunzi Wilaya ya Handeni kutokana na takwimu zao.

  Anasema kwa mwaka 2012 hadi mwezi Novemba walikuwa na jumla ya matukio ya kesi kama hizo 66, lakini kwa mwaka huu (Machi, 2013) kuna jumla ya matukio ya kesi kama hizo 14 tu yalioripotiwa.

  Anasema elimu inayotolewa na Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni imesaidia. “Kesi zinazotufikia hapa huku zikiwa na ushaidi wa kutosha tunazipeleka mahakamani, zile zinazokuwa hazina ushaidi wa kutosha tunajaribu kuzifuatilia kiuchunguzi kwa mujibu wa taratibu zetu. Lengo letu kupitia Dawati la Jinsia na Watoto ni kuhakikisha tunapunguza kama sio kumaliza kabisa vitendo hivyo.

  Anasema maranyingi ushahidi wa kesi kama hizo pia umekuwa ukiharibiwa na wahusika kabla ya kufika mahakamani, wanaweza baada ya kesi kufunguliwa wakashawishiana na kukaa nje bila ya sisi kujua na hivyo kupotea wote.


  Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama anasema idadi ya matukio ya mimba shuleni hapo inapungua kwa sasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali, lakini si kwamba matukio hayo yamekoma kabisa.

  “Matukio ya mimba kimsingi kwa sasa yanapungua…lakini si kwamba yamekwisha kabisa, tatizo kubwa ni malezi katika familia pamoja na vishawishi vingine,” anasema mwalimu huyo akizungumza shuleni Komnyang’anyo.

  Napingana kwa mtazamo mwingine kwamba umbali wa makazi kwa wanafunzi unachangia mimba…nasema hivyo kwa kuwa kwa mwaka jana mwishoni kuna mfano mzuri, shuleni kwetu yupo mwanafunzi (wa kidato cha pili ‘C’) ambaye anahudumiwa kila kitu na pia yu-karibu na shule lakini amejikuta akipewa mimba na kukatishwa masomo.

  Mwanafunzi huyu pia huwezi kumuingiza katika kundi la wanafunzi wenye mazingira magumu ya maisha katika familia zao, nasema hivyo kwa kuwa huyu analipiwa kila kitu, anapewa matumizi yote yanayoitajika na shirika moja linalosaidia wanafunzi wa kike lakini ameshindwa kuendelea baada ya kupewa mimba.

  Kesi hii tayari ipo kwenye Serikali ya kijiji kwa hatua zaidi baada ya sisi kutoa taarifa. Sasa watu wanachukulia hatua si kama ilivyokuwa hapo nyuma.Tangu amekuwa huyu Mkuu wa Wilaya mpya (Muhingo Rweyemamu) wananchi wanatoa ushirikiano kwa kesi kama hizi. Kimsingi ujenzi wa mabweni itakuwa hauweni kwa wanafunzi ambao kwa sasa wanatokea vijiji vya mbali kuja shuleni, vijiji hivyo ni pamoja na Bangu, Kwamagome na Kwakonje.

  Mazungumzo ya wanafunzi Hamad Ngomero kidato III, Salome Kalage kidato cha IV, Michael Richard kidato cha I, Mwajuma  Munga kidato cha II, Mwajabu Fungo kidato I na Farid Iddy kidato cha IV - wote kutoka Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wanakubali kwa pamoja uwepo wa matukio ya mimba, japokuwa kwa sasa ni kwa kiwango kidogo.

  Mwajuma Munga anasema matukio hayo bado yapo lakini yamepungua si kama ilivyokuwa hapo nyuma. Naye Salome Kalage anasema mfano kuanzia mwezi Januari 2013 anawajua wanafunzi watatu ambao wamepata mimba na kuachishwa shule. Anawataja wanafunzi hao ni pamoja na Kuruthumu Omar (IV), Elizabeth Hamis (IV) na Docas (III).

  Kwa upande wake mwanafunzi Hamad Ngomero anasema tamaa za starehe na hali ngumu ya maisha katika familia kaadhaa wilayani Handeni ndiyo inayowaponza wanafunzi wa kike na hata kujikuta wakitiwa mimba na kukatishwa masomo.

  Martin Mwingo ni Mwaliku Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Kileleni; ujio wa Mkuu wa Mkoa mpya Handeni umeanza kuonesha mafanikio kwa upande wa matukio ya mimba kwa wanafunzi. “DC (Mkuu wa Wilaya) wasasa anajitahidi sana kupitia kampeni yake ya “Niache Nisome” anafuatilia kesi za mimba na kuhakikisha wahusika wanapata adhabu kwa mujibu wa sheria…mfano sasa hivi tuna kesi moja tumeletewa hizi ni juhudi za Mkuu wa Wilaya,” anasema Mwingo.

  Kesi zinapungua mfano mwaka jana tulikuwa na kesi mbili za mimba lakini mwaka huu (2013) hadi sasa hatujapata kesi ya mimba…lakini pamoja na hayo malezi ya watoto kwa wazazi bado ni tatizo, mtoto ananyenyekea kea mzazi wake tu dharau kwa watu wengine-haya si malezi. Zamani mtoto anaweza kuadhibiwa na mkubwa yeyote ilimradi awe amekosa, lakini sasa sivyo.

  “Mi nashangaa kila uchao watu wanang’ang’ania haki za watoto wasiadhibiwe uweke utaratibu wa kutoa adhabu lakini nashangaa kwanini wasitaje na wajibu wa mtoto hili ni muhimu…tusing’ang’anie haki za mwananafunzi tu tuoneshe na wajibu wake pia,” anasema Mwalimu Mwingo.

  Anasema pamoja na juhudi hizo bado utandawazi unaathiri nidhamu za wanafunzi, umiliki wa simu za mkononi matumizi mabaya ya mitandao kama tovuti nayo yanawaharibu wanafunzi, ipo haja ya Serikali kuingilia na kupiga marufuku wanafunzi kumiliki simu shuleni maana simu inamambo mengi sasa.
  Hussen Kigoma ni mwanafunzi wa kidato cha III, katika moja ya shule za kata Wilaya ya Handeni ambazo ndizo zimezokuwa na changamoto anuai. Anasema ipo haja ya kuwa na utaratibu wa kuwapima vipimo vya ujauzito mara kwa mara wanafunzi wa kike.

  “Sasa hivi wapo ambao wanapata na kutoa mimba hizo bila uongozi wa shule kujua…sasa hivi tunawajua wanafunzi wawili ambao walipata mimba mwaka huu shuleni kwetu. Mfano Joyce Gasper na Jesca Paul wote wa kidato cha nne wamepata mimba…huenda mwaka huu mimba zikaongezeka zaidi,” anasema Hussein Kigoma.

  Eliakimu Kapele ni Makamu wa Shule ya Sekondari Kivesa; anasema linapungu tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma. Mfano mwaka jana tulikuwa na matukio mengi ya kesi za mimba kwa wanafunzi, lakini hadi muda huu kwa 2013 tunayo matukio mawili tu. Na hatu zinachukuliwa maana msukumo unaanzia kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa.

  Hii inatokana na Mkuu wa Wilaya wa sasa Muhingo Rweyemamu ametia mkazo sana masuala ya mimba kwa wanafunzi, watu wamekuwa makini na wafuatiliaji.
  “Mfano sasa mimba inapotokea kuanzia mzazi wa mtoto aliyetiwa mimba, mtoto mwenyewe na mtuhumiwa wote wanashikiliwa…mi naamini kama adhabu hizi zitaendelea kutolewa ipasavyo watu watanyooka tu,” anasema mwalimu Kapele.

  Hata hivyo mwalimu huyo anashauri mabadiliko ya sheria na kanuni za utoro shuleni, anasema maamuzi yamekuwa na mkanganyiko. Mfano kanuni za shule zinaelekeza kuwa mwanafunzi asipo hudhuria shule kwa siku 90 afukuzwe shule. Hili kwa sasa halifanyiki maana limekaa kisiasa zaidi…wanafunzi wanatoroka hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa maelekezo lakini baadaye wanarejeshwa kuja kufanya mitihani, hili ni tatizo.

  “Inatokea mwanafunzi anabeba mimba na baadaye anarudi shuleni baada ya kujifungua, mwanafunzi kama huyu ni tatizo hawezi kuwa na vurugu sana kinidhamu na wakati mwingine anawavuruga hata wenzake maana anakuwa hana maadili.”

  Shule yetu inautaratibu mzuri wa kuhakikisha muda wote unaofaa wanafunzi wanakuwa darasani kupata kilichowaleta hapa shuleni. Lakini huwezi kuamini kuna baadhi ya wanafunzi muda wote wapo huku vichochoroni wanajificha hawaji shuleni, utoro umekithiri! Lakini hawa huenda wakaruhusiwa kuja kufanya mitihani hapo baadaye.

  Kanuni za shule mara kadhaa zimewekwa pembeni na siasa kuingizwa kwenye kanuni hizo, hali hii inawapa wanafunzi kiburi na uhuru mkubwa-huwenda wanadhani kufanya hivi ni kuwasaidia lakini ukweli ni kwamba wanawaharibu.
  Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa anakiri kuwepo na mabadiliko makubwa ya utoro wa mimba ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka jana. 

  “Kimsingi huko nyuma utoro hasa wa mimba ulikithiri kwa wanafunzi wa Sekondari na Msingi, lakini hali ya sasa ni tofauti. Kuna mabadiliko kampeni ya ‘Niache Nisome’ imesaidia sana…kwa sasa wengi wanaohusika na kuwatia mimba wanafunzi wanapelekwa mahakamani,” anasema Muchiwa.

  Anasema zoezi la kamatakamata lililokwenda sambamba na kampeni ya ‘Niache Nisome’ na watu hufikishwa kwenye hatua mbalimbali limesaidia hivyo mambo yanabadilika. Kwa mantiki hiyo waweza kuona kuanzia Januari 2013 hadi sasa (Machi) sijapokea kesi hata moja ya mimba.

  Tunachokifanya sasa ni kutoa elimu zaidi kwenye mikutanyiko ya jamii kupitia viongozi wa ngazi mbalimbali za halmashauri, ili kuhakikisha tunafanikiwa zaidi tumeanza mkakati wa kuwajengea uwezo wananchi na shule. Hii ni kukabiliana na baa la njaa ambalo limekuwa likijitokeza mara kadhaa.

  “Unajua mtu anapokuwa na njaa kushawishika ni rahisi na Handeni kuna njaa sasa hali kama hii yaweza kuathiri pia sekta ya elimu, tumejipanga kuimarisha kilimo cha mazao kama mahindi na mtama shuleni ili wanafunzi wawe na uhakika wa chakula wawapo shuleni,” anasema Ofisa Elimu huyo wa Wilaya ya Handeni.
  Ofisa Elimu Taaluma, Basil Mrutu anasema kwa mwaka jana kwa mujibu wa takwimu zao walikuwa na ripoti za mimba 26 kwa Wilaya nzima, lakini tangu Oktoba 2012 hadi sasa hawajapata kesi za matukio ya mimba.

  Simon Mdaki ni Mkuu wa Idara ya Sekondari Wilaya ya Handeni; anasema kuwa “Halmashauri imeandaa matrekta 7 ambayo shule zitapewa kipaumbele cha kuyatumia ili kuweza kuendesha kilimo kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi.
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TAMWA


older | 1 | .... | 62 | 63 | (Page 64) | 65 | 66 | .... | 1898 | newer