Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 617 | 618 | (Page 619) | 620 | 621 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Kaimu Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketansi akizungumza na wanahabari(hawako pichani) juu ya Kampeni ya uhamasishaji wa utalii wa ndani kwa wazawa itakayodumu kwa muda wa miezi sita.
  Baadhi ya Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na wanahabari (hawako pichani ) juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa ambapo katika kipindi cha miezi sita watakao tembelea zaidi ya Hifadhi nne watapata ofa ya kutembelea Serengeti ikiwa ni pamoja na kugharamiwa maradhi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano.
  Kaimu Meneja Mauzo wa TANAPA,Victor Ketansi akisisitiza jambo.
  Mkuu wa Idara ya Utali katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya akizungumza vivutio mbalimbali vunavyopatikana katika hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.


  
  Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni afisa utalii mfawidhi na mkuu wa kanda ya utalii Kaskazini,Lauriano Munishi akizungumza jambo mbele ya wanahabari(hawako pichani)juu ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha utali wa ndani.
  Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha,(ANAPA) Neema Philip akizungumzia vivutio mbalimbali vinayopatikana katika hifadhi ya Arusha.
  Afisa Utalii Mwandamizi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ,Pellagy Marandu akizungumzia vivutio mbalimbali vinavyoopatikana katika hifadhi hiyo.
  Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Catherine Mbena akiwa na mwandishi wa habari wa TBC Kilimanjaro,Sauda Shimbo wakati wa kikao cha maofisa wa TANAPA na wanahabari kuzungumzia juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa .
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini..

  0 0

  Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkoani Manyara,Mkuu wa Mkoa Mh.Joel Bendera akiwasili katika viwanja vya Halmshauri ya Mji wa Mbulu akiongozana toka kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa –Bw.Ally Uledi, Mkurugenzi wa CHF Bw.Eugene Mikongoti na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe.
  Mkurugenzi wa CHF Bw.Eugene Mikongoti akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika moja ya banda la maonyesho ambapo wananchi walipata fursa ya kupimwa afya zao, kuchangia damu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zihusuzo CHF iliyoboreshwa na NHIF.Wengine toka kushoto ni Bw.Isaya Shekifu Kaimu Meneja wa NHIF – Manyara, Bw. Ally Uledi- Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara na Dr.Heri Marwa Mkurugenzi wa Mradi wa Health Insurance – PharmAcess Tanzania.
  Mh.Mary Nagu –Waziri katika ofisi ya Raisi Mauhusiano na Uratibu na Mbunge wa Hanang akawaelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na CHF ILIYOBORESHWA katika siku ya uzinduzi .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa shirika la PharmAccess kutoka Uholanzi Bw.Sicco Van Gelder ambao ndio wafadhili wa mradi huu wakishirikiana na NHIF.
  Mgeni rasmi wa siku ya uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe kukabidhi moja ya pikipiki tano zilizotolewa kwa maafisa wa CHF iliyoboreshwa ili kuwarahisishia kazi ya uandikishaji na uhamasishaji kwa wananchi wa tarafa tano za wilaya ya Mbulu.
  Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiwasha moja ya pikipiki tano alizokabidhi kwa maafisa wanaoshughulika na CHF ILIYOBORESHWA mbele ya umati wa wananchi wa wilaya ya Mbulu katika siku ya uzinduzi wa mradi huu kimkoa.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joel Bendera akimkabidhi kadi ya CHF iliyoboreshwa mwanachama mpya aliyejiunga katika siku ya uzinduzi wa kimkoa wilayani Mbulu mkoani Manyara.
   ---
  Anna Makange, Mbulu.
  Mkuu wa mkoa wa Manyara, Mh. Joel Bendera amezindua rasmi Mfuko wa Afya ya Jamii Uliboreshwa (iCHF) mkoani Manyara.Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mh.Mary Nagu (Mbunge - Hanang) na Waziri katika ofisi ya Raisi Mahusiano na Uratibu, Wakuu wa wilaya za Hanang na Mbulu pamoja Wawakilishi wa wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, ulifanyika katika viwanja vya halmashauri ya mji wa Mbulu. Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo kwa viongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri mradi huu na kuhamasisha wananchi wajiunge kwa wingi ili kufanikisha sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote.  Pia halmshauri za wilaya mkoani Manyara zimetakiwa kuweka bajeti maalum itakayowezesha utekelezaji wa mpango endelevu wa kuziingiza kaya maskini katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kila mwaka ili kuwahakikishia huduma bora za matibabu.

  Mradi huo wa iCHF mkoani Manyara unaendeshwa kwa ushirikiano baina shirika la Pharm Access International (PIA) la Uholanzi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na Halmashauri za wilaya za Mbulu, Babati na Hanang kwa lengo la kuboresha huduma na kuhamasisha idadi kubwa ya wananchi kujiunga na mfumo wa kulipia kabla gharama za matibabu ili kuzuia vifo visivyo vya lazima katika jamii.

  Bendera alisema ili kuiwezesha serikali kufikia lengo lake la kufikisha huduma bora za afya kwa kila mtanzania kuna umuhimu wa kipekee kwa halmashauri zinazounda mkoa huo kuhakikisha wananchi wote wanajisajili katika iCHF wakiwemo maskini ili nao waweze kuhakikishiwa upatikanaji wa matibabu.

  “Kwa kutambua changamoto ya kutokuwepo rasilimali za kutosha katika vituo vya kutolea huduma ndio maana serikali iliamua kuanzisha mfumo huu wa kuchangia kidogo kila mwaka gharama za matibabu kabla ili kumwezesha kila mwananchi kupata matibabu kwa nia ya kuchangia fedha kidogo.”, alisema.

  Aidha aliongeza, “Wito wangu kwenu wananchi ni jiandikisheni kwa wingi kwasababu ugonjwa haupigi hodi… kwa upande wa halmashauri hebu anzeni kuweka fedha kwa mpango mtakaokubaliana ili wale maskini nao waweze kusaidiwa kupata matibabu kama wenzao wengine wenye uwezo wa kuchangia”, alisema.

  Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugine Mikongoti akizungumza katika uzinduzi huo aliwataka watoa huduma za afya kupitia iCHF kumaliza malalamiko ya wagonjwa kwa kuhakikisha michango yote ya wananchi inatumika ipasavyo kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba ili kuwawezesha kuona thamani halisi ya fedha zao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa PIA alisema katika miezi sita kuanza kwa utekelezaji wa iCHF humo idadi ya wananchi wanaojiunga inaongezeka kwa kasi kutokana na kuongezwa kwa idadi ya vituo vya kutolea huduma, maduka ya dawa, ushirikihswaji jamii na uhamasishsaji.

  0 0

    Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Luis Benedicto (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo, kuhusu wasiona kutengwa katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Jonas Lubago na Katibu Mkuu wa (TLB), Emmanuel Simon.
   Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano  na Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.

    Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
  CHAMA cha Wasioona Tanzania (TLB)   kimesema kuwa hakitawapa kura wanasiasa ambao hawajaweka mazingira wezeshi na  rafiki  kutokana na kutoweka ilani katika  vyama vyao juu ya maslahi  na haki za watu wasioona  nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo,Mwenyekiti wa TLB,Luis Benedicto amesema wana mashaka kwa vyama vya siasa nchini kama vitakuwa vimeweka ilani zao sera au kanunizinazoelekeza utekelezwaji wa maslahi ya yanayowagusa moja kwa moja na changamoto za kimaendeleo zinazowakabili watu wasioona.

  Benedicto amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Vyama vya siasa havijawashirikisha katika mkutano wowote  juu ya wao kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni  mwa Oktoba.
   
  Amesema NEC haijainisha idadi ya watu wasioona waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na wagombea katika nafasi mbalimbali wanaotoka jamii hiyo.
   
  Hata hivyo wanataka vyama vya siasa vina mipango gani kwa siku za usoni katika kushiriki katika majukwaa ya siasa.

  Mwenyekiti wa amesema elimu ya uraia vifaa vya kupigia kura na miundombinu wezeshi juu ya kuweza kufikia vituo vya kupigia kura ni kitendawili ambavyo mpaka sasa bado havijpatiwa majibu na kufanya jamii hiyo kuwa njia panda.

  0 0

  IMG_4176

  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Mwandishi Wetu, Moshi
  MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.
  Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.Aidha aliwataka wanafunzi kuhakikisha kwamba wanajenga mshikamano mkubwa na wenye upendo kila kundi likithamini kundi jingine kwa ajili ya ustawi wa taifa .
  Alisema wasichana kwa wavulana kuheshimiana kwani katika hilo wataweza kutengeneza taifa linaloheshimiana na hivyo kulinda msingi wa maisha wa amani unaowezesha maendeleo na ustawi wa jamii.Aliwataka wanafunzi hao kushikilia ndoto zao na kusaidia kutambua kwamba wanahitajika kutunza mazingira na kujali afya zao.
  IMG_4174
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem aliyeambatana na Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Kiboriloni.
  Akimkaribisha Mratibu huyo kuzungumza na wanafunzi mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kiboriloni Salehe Msuya alisema kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1946 eneo la Msaranga na kuitwa kwa jina hilo na baadae kuhamishiwa Kiboriloni ambako kulikuwa na makazi ya Mangi mwaka 1955 inakabiliwa na ukosefu wa matundu 18 ya choo, maktaba na bwalo la chakula.
  Alisema ingawa shule ilianzishwa ikiwa na wanafunzi 12 ilipohamishiwa Kiboriloni 1955 na kupewa jina hilo mwaka 1990, sasa ina wanafunzi 613 kuanzia darasa la awali hadi la 7 na kukabiliwa na changamoto za matundu.Shule hiyo inahitaji kuwa na matundu 32 lakini yaliyopo sasa ni 14.Mwalimu huyo aliishukuru UN kwa kuwasaidia kutengeneza matundu yaliyobaki na kuwaomba pia kusaidia kuboresha mazingira ya kusomea katika kuwa na maktaba na bwalo la kulia chakula.Kwa sasa shule hiyo inatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wake na hawana mahali pa kulia.Pamoja na taaluma kuzidi kuimarika shuleni hapo, shule haina maktaba.
  IMG_4181
  Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwasili kwenye eneo la tukio ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_4625
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuweka msingi wa ujenzi wa vyoo 18 ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira bora ya kusomea sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_4602
  Sehemu ya wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni wakifurahi habari za kujengewa vyoo.
  IMG_4159
  Wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni wakinawa mikono yao kwa sababu mara baada ya kutoka msalani kama walivyokutwa na camera ya modewjiblog
  IMG_4569
  Baadhi ya vyumba vya vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni.
  IMG_4184
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) akiwapungia wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
  IMG_4192
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akiweka maji wakati wa maandalizi ya kutengeneza zege kwa ajili ya kuweka msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakisubiri kuchanganya zege.
  IMG_4198
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakianza matayarisho ya kuchanganya zege huku Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Martha Ofunguo akimwaga maji kwenye mchangayiko huo.
  IMG_4207
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege.
  IMG_4210
  Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakishiriki zoezi la kubeba maji na kokoto kwa ajili ya kuchanganya zege la msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
  IMG_4215
  IMG_4217
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati akimwaga zege waliloandaa kwenye ujenzi wa msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
  IMG_4225
  Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakishiriki zoezi la kumwaga zege katika msingi huo.
  IMG_4252
  Hapa ni kazi tu.....; Ni maneno ya Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakati akishiriki zoezi la kuchanganya zege katika shule msingi Kiboriloni. Kwa matukio zaidi Bofya hapa

  0 0

  Wahitimu wa elimu ya msingi katika shule ya kimataifa ya Shinning School  Songwe Mbeya wakiwa katika maandamano ikiwa ni sehemu ya kufurahia tukio hilo mwishoni mwa wiki mkoani hapa (Picha Jamiimojablog).  Wazazi wakiwa  katika nyuso za furaha baada ya watoto wao kuhitimu elimu ya msingi katika shule hiyo


  MKurugenzi Mtendaji wa shule ya kimataifa ya Shinning School iliyopo nje kidogo ya mji wa mbeya eneo la songwe kiwandani Amani Kajuna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya akizungumza katika hafla hiyo.

  Mmoja wa wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi  2015  shule ya kimataifa ya Shinning School  akionesha ushahidi  wa cheti chake mara baada ya kutunukiwa na uongozi wa shule hiyo katika mahafali hayo ambayo yamefanyika shuleni hapo.
  Wadau poleni na hekaheka za uchaguzi....pokeeni cods
  Hongera kwa kuhitimu elimu ya msingi.

  0 0

  JKRais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano  wa  Mwaka wa Wadau wa Barabara wa TAMISEMI uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto wilayni Arumeru Mkoani Arusha Agosti 24, 2015.(Picha na Freddy Maro)

  0 0

   
  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Rebecca Malope,  amepongeza wazo la kuwepo Tamasha la Amani linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Oktoba 4 mwaka huu.
   
  Mkurugenzi wa Kamati  ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema tayari wasanii mbalimbali wa kimataifa wameguswa na uwepo wa tamasha hilo.“Tumepanga kuwa na tamasha la amani Oktoba 4, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baadaye mikoa mbalimbali nchini.
   
  “Wasanii wa Injili wa ndani na nje wamepongeza wazo hilo na wameonekana kuguswa kwa kiasi kikubwa akiwemo Malope.“Amenijulisha kwamba tukimuhitaji yupo tayari wakati wowote kufanya naye kazi kwenye tamasha hilo. Bado tunajipanga na mambo yakiwa mazuri tutamualika,” alisema Msama.
   
  Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

  0 0


   Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Luis Benedicto (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu wasiona kutengwa katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Jonas Lubago na Katibu Mkuu wa TLB, Emmanuel Simon
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

  Na Dotto Mwaibale

  CHAMA cha Wasioona Tanzania (TLB), kimetishia kutompa kura mgombea urais au mwanasiasa yeyote kupitia chama chochote cha siasa ambaye hajaandaa mazingira wezeshi na rafiki kwa ajiri ya kundi hilo kupiga kura.

  Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Luis Benedicto wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu wasiona kutengwa katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

  "Ndugu wanahabari kundi la sisi watu tusioona tumetengwa katika mchakato mzima kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 wa kuchagua rais, wabunge na madiwani kuanzia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura" alisema Benedicto.

  Alisema mambo ya msingi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi mwaka huu hayajatazamwa wala kuzungumziwa ama na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) au vyama vya siasa nchini.

  Alisema zipo changamoto nyingi ambazo zinajidhihirisha hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu ambazo kwa vyovyote vile zinawanyima fursa na haki ya kupiga kura kama watu wasiona ambao ni sehemu ya jamii.

  Benedicto alisema kwamba baadhi yao walihamasishana kadri walivyoweza kujiandikisha katika daftari hilo ambapo walikumbana na changamoto luluki.

  Alitaja baadhi ya changamoto walizokumbana nazo kutokana na kutokuona kwao ni hawakutumia alama ya vidole gumba na badala yake walilazimishwa kushika kalamu na kusaidiwa kuweka sahii kwa kusaidiwa na baadhi ya waandikishaji jambo ambalo litaathiri taarifa zao nyingine zilizo katika mfumo waliouzoea wa dole gumba.

  Alisema kutokana na kutotendewa haki hiyo wao kama Chama cha Waioona Tanzania (TLB) kwa kauli moja wanatamka hawatawapa kura zao wanasiasa ambao hawajaandaa mazingira hayo wezeshi na rafiki kwa ajili ya wao kupiga kura.

  Alisema wanamashaka makubwa kama vyama vya siasa nchini vimeweka katika ilani zao sera au kanuni zinazoelekeza utekelezwaji wa maslahi yao yanayogusa moja kwa moja na changamoto za kimaendeleo wanazokabiliana nazo watu wasiona.

  Aliongeza kuwa watu wasiona wana haki ya kushiriki na kuwepo katika vyombo vya maamuzi ndio maana wanaviuliza vyama vya siasa kwamba vina mpango gani wa kuwawezesha katika kushiriki katika majukwaa ya siasa katika kipindi hiki na siku za usoni.

  "Tunasikitika kuona hata kanuni ndogo hazijatungwa ili kuwashirikisha watu wasioona katika mchakato, jambo ambalo linatengeneza mazingira ya unyanyapaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama kubwa za uchaguzi ambazo walemavu wengi hawazimudu.

  Alisema kuwa elimu ya uraia, vifaa vya kupigia kura na miundombinu wezeshi kufika vilipo vituo vya kupigia kura ni vitendawili ambavyo mpaka sasa bado havijapatiwa hivyo kujiona wapo njia panda na hawajui itakuweje.

  0 0

  Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo. Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo. Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

   BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya kuendelea na safari yake.

   Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya kuingia njia panda. 

  Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao.

   Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.
   

  Alisema yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya upatikanaji madawa. 

  "...Matatizo ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na mimi ni mzazi nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu (mgombea urais, Dk. Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri," alisema Bi. Suluhu akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia barabarani wakiomba awasalimu. Alisema kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji. 

  Aidha akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero ya uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa ajira. 

   Alisema Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika vijiji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM ikipewa ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo vinawekewa umeme. Alisema anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk. Magufuli na wagombea wa CCM eneo hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani wao ndio wenye ushawishi mkubwa katika familia. Vivyo hivyo kuwataka madiwani wanaogombea kuhakikisha mgombea uraisi na wengine wanapata kura za kutosha ili kushinda uchaguzi.

   Kwa upande wake Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu aligombea na kura hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao waligombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua kuondoka ndani ya chama hicho. Alihoji kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna kushindwa na kushinda? Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na akinababa wanaoamua kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu. 

  "Nawashauri wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya vizuri, kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa hamjui kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema. Naye Mwenyekiti wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa kuamua kuanza kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza wapiga kura kwani Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha wanatwaa majimbo yote, viti vya udiwani.

  0 0

  Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) ulikamilika tarehe 04/08/2015 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
   
  Baada ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji Tume imekuwa ikichakata (processing) taarifa za Wapiga Kura ili kuweza kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura, katika maandalizi hayo mifumo imeweza kugundua kasoro mbali mbali ambazo baadhi zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi, kasoro hizo ni pamoja na Wapiga Kura Kujiandikisha zaidi ya mara moja.
  Mfumo wa BVR unao mfumo mdogo wa “Mini AFIS” unaoweza kubaini Mpiga Kura anayataka kujiandikisha zaidi ya mara moja katika kituo husika, mfumo huo ulikuwa umeandaliwa ili kuweza kubaini Wapiga Kura wanaotaka kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuzuia Uandikishaji huo katika BVR Kit yoyote.

   Hii ingewekana iwapo Mfumo wa mawasiliano ungekuwa na nguvu katika vituo vyote na kuweza kuwasiliana na mifumo iliyoko katika kituo kikuu cha maandalizi ya Daftari(Data Processing Center) kwani katika kituo hicho imewekwa mifumo ya hali ya juu inayoongoza kimataifa katika kulinganisha alama za vidole na kubaini waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
  Kwa kutokuwa na mawasiliano yenye nguvu kutoka katika kila kituo Tume ilianza kulinganisha taarifa za Wapiga Kura mara tu baada ya taarifa kufikishwa katika kituo cha maandalizi ya Daftari hivyo kwa mitambo iliyopo Tume imebaini Wapiga Kura wote waliojiandikisha Zaidi ya mara moja ambao taarifa zao zimeisha chakatwa ambao kwa sasa imefikia 52,062 Idadi hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na uchakataji wa taarifa.

  Baadhi ya vituo kutokuwa na Wapiga kura.
  Tatizo hili linasababishwa na maombi ya kuanzishwa kwa vituo wakati zoezi la Uandikishaji limeanza, baadhi ya vituo hivyo havikutumika wakati wa Uandikishaji kama ilivyokusudiwa kwa sasa Tume inafanyika kazi ya kuhamisha Wapiga Kura na kuwapeleka katika vituo hivyo ili kuwapunguzia umbali mrefu kutoka kwenye vituo walivyojiandikisha wakati wa zoezi la Uandikishaji, kazi hii Tume inaendelea kuifanya kwa kushirikiana na watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.Baadhi ya Vituo kuwa na Wapiga Kura wachache au Wengi katika Vituo vya Uandikishaji.
  Tatizo hili pia lilisababishwa na vituo kuongezwa wakati zoezi la Uandikishaji limeanza. Kabla ya kuongezwa vituo katika BVR kutokana na hamasa ya Wapiga Kura Kujiandikisha Wapiga Kura hao walianza kujiandikisha katika vituo vingine na baada ya kuongeza vituo katika BVR vituo vilivyoongezwa viliendelea kufanya Uandikishaji kwa siku mbili au tatu za mwisho hivyo kuonekana kama vina Wapiga Kura wachache, kasoro hiyo inarekebishwa pia kwa kusaidiana na watendaji wa Kata husika ili kuwahamisha Wapiga Kura waliojiandikisha katika vituo kabla ya kuongeza kwenye BVR vituo vilivyoombwa kuongezwa na kupelekwa kwenye vituo karibu na maeneo wanayoishi.

  Wapiga kura kuandikishiwa katika Mfumo wa Mafunzo.
  Katika taarifa zilizochakatwa imebainika kuwa baadhi ya Wapiga Kura waliandikishwa kwa kutumia mfumo wa mafunzo uliowekwa katika katika BVR kit iliyotakiwa kutumika wakati wa mafunzo tu, Usahihi wa taarifa za Biometric za Wapiga Kura hao kuwa sahihi lakini baadhi ya taarifa nyingine kuhitaji marekebisho kutoka katika fomu za Uandikishaji zilikizojazwa.

   Kazi hiyo inaendelea kufanyika katika kitu cha maandalizi ya Daftari kwa kuwa fomu zote za uandikishaji zimeishafika. Marekebisho hayo yalichelewesha kidogo baadhi ya taarifa katika madaftari yaliyowekwa wazi. Kazi ya Kurekebisha kasoro hizo zimeendelea kurekebishjwa na kabla ya tarehe 05/09/2015 kasoro zote zitakuwa zimerekebishwa.
  Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura kutochukuliwa taarifa zao katika BVR Kit.
  Tatizo hili lilisababisha baadhi Wapiga kura kutoonekana katika vituo walivyojiandikisha, zipo baadhi ya BVR Kit ziliibiwa na zikafanyika jitihada za kung’oa baadhi ya vifaa katika BVR kama vile Laptop na vifaa vingine.

   Zipo BVR mbili (2) kati ya BVR Kit 8000 ziliibiwa na walioiba walifanya jitihada za kuiba baadhi ya vifaa katika BVR kit hizo, BVR Kit hizo zilipatikana lakini zikiwa katika hali mbaya ya Uaribifu hivyo kushidwa kuondoa taarifa za Wapiga Kura mara moja, kwa kuwa Tume iliweka vifaa mahususi inapojitokeza changamoto kama hiyo kutopoteza taarifa za Wapiga Kura, chombo hicho kinachohifadhi taarifa za Wapiga Kura mara inapotokea uaribifu mbukbwa hususan wa kompyuta kuweza kupata taarifa za Wapiga Kura bila tatizo, Tume tayari imekwisha pata vifaa vilivyokuwa vimeifadhi taarifa za Wapiga kura na tayari taarifa hizo zinaingizwa katika mfumo wa kuchakata taarifa za Wapiga Kura.
  Kata Mpya.
  Kwa mujibu wa sheria OWM ­ TAMISEMI ndiyo yenye hadhi ya kupandisha na kugawa maeneo ya kiutawala ili kuchochea maendeleo ya haraka kwa wananchi wake. Mabadiliko hayo ya mipaka ya kiutawala yanahitaji kuhuishwa na Tume katika Mifumo yake ili kuwezesha chaguzi kufanyika na hasa chaguzi za madiwani, hivyo yanafanyika marekebisho ya kuhamisha kuweka vituo na Wapiga Kura katika maeneo mapya ya kiutawala yaliyoanzishwa, ikiwa ni pamoja na:­ Vitongoji, Mitaa,Vijiji, Kata na Halmashauri.Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura taarifa zao kukosewa na BVR Kit Opereta wakati wa Uandikishaji.
  Baadhi ya Wapiga kura taarifa zao zilikosewa na BVR Opereta wakati wa Uandikishaji hivyo kuhitaji marekesho na kupatiwa kadi mpya. Tume ilipeleka BVR Kit katika Halmashauri zote wakati wa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura, ili kufanya marekebisho ya taarifa za Wapiga kura pale panapohitajika. Marekebisho yamefanyika Tume inategemea Taarifa hizo zitafika na kuingizwa katika mifumo ili kupata taarifa sahihi.
  Wapiga Kura Kujiandikishia katika maeneo tofauti na maneo wanayoishi.
  Baadhi ya Wapiga Kura walijiandikisha katika maeneo tafauti na maeneo wanyaoishi, hivyo kuhitaji kuhamisha taarifa zao, tatizo hili limebainika katika maeneo mengi ya mjini, hasa kwa Wapiga Kura kutaka kuwahi kupata kadi za Mpiga kura, kasoro hii imeendelea kurekebishwa wakati wa zoezi la kuweka wazi Daftari.
  Uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
  Uwekaji wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ni takwa la kisheria, kifungu cha 11a cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 kinaitaka Tume kuweka wazi Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uhakiki wa Taarifa na kurekebisha kasoro zozote zinalizojitokeza.
  Ili kuhakiki taarifa katika Daftari la Awali la Wapiga Kura wananchi wanatakiwa kufika katika Ofisi za kata ili kuweza kuangalia kama majina yao yapo katika Daftari, na ikiwa Taarifa zao ni sahihi mfano Jina, Jinsia, Tarehe ya kuzaliwa na Kituo chake cha kujiandikishia, Aidha, kwa Wapiga kura waliohama kata au jimbo moja kwenda kata au jimbo lingine wanatakiwa kuhamisha taarifa zao.
  Zoezi hili la uhakiki lilianza rasmi tarehe 07/08/2015 katika Mikoa mbali mbali na limekuwa likiendelea hadi sasa ili kuhakikisha kila Mpiga kura aliyeandikishwa kupiga kura anaweza kupiga kura bila usumbufu wowote.
  Katika zoezi hili Tume imeweka utaratibu wa kuwaondoa watu wote waliojiandikisha katika Daftari ambao siyo raia wa Tanzania, ambapo mchakato huo unaishia katika mahakama ya wilaya. Ili kasoro hii iweze kuondolewa Tume inahitaji kwa kiasi kikubwa Ushirikiano na wananchi wanaoishi nao ili kuwawekea pingamizi na waweze kuondolewa katika Daftari, ni ukweli kwamba iwapo wananchi watawaficha na kutowawekea pingamizi tatizo hili litakuwa gumu kwa Tume kulitatua.
  Kasoro mbalimbali zilizobainika wakati wa Uandikishaji Tume itahakikisha inazirekebisha ili kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na Daftari sahihi na la kuhaminika.
  Imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  0 0

  Bondia nyota nchini wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka atapigana na bondia wa Uingereza, Martin Murray katika pambano maalum lisilo la ubingwa la uzito wa Super Middle.Pambano hilo limepangwa kufanyika mjini Manchester Septemba 19 na maandalizi yake yamekwisha kamilika.

  Meneja mpya wa bondai huyo, Juma Ndambile alisema kuwa Cheka ataondoka hapa nchini Septemba 15 kwenda Uingereza kwa ajili ya pambano hilo la raundi 10.

  Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security alisema kuwa ameamua kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Cheka ili kuresha heshima yake katika mchezo huo na pambano la Uingereza ni la mtoano kwa ajili ya kuwania ubingwa wa Dunia.

  Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa. Alisema kuwa endapo atashinda pambano hilo, atasaini mkataba mwengine za zaidi ya dola 25,000 ili kupigana pambano la tatu.

  “Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.

  Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.Cheka alisema kuwa amefurahi sana kupata meneja mpya ambaye tayari amemtafutia pambano nje ya nchi na sasa imebakia kwake ni kufanya kazi tu. “Ndambile amenilipia kambi ya zaidi ya  Sh  milioni 2 hapa jijini, nakaa mimi na kocha wangu, naahidi kufanya vyema kwenye pambano hilo,” alisema Cheka.

  0 0


  0 0

  Na Allen Mhina na Jenikisa Ndile-Maelezo.

  Chama cha Watu wasioona Tanzania (TLB) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka mazingira rafiki yatayowawezesha wasioona kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. 

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Luis Benedicto, amesema kuwa wakati wa kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa kieletroniki (BVR), kulikuwa na changamoto mbalimbali  zilizowakumba wasioona ikiwemo ya kushindwa kuweka sahihi kwa kutumia dolegumba.

  “ Wakati wa zoezi la kuandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu tulishindwa kuweka sahihi kwa kutumia dolegumba kama taratibu zilivyo kwa watu tusioona, badala yake ilitulazimu kuweka sahihi kwa njia ya kalamu ambayo ni nje ya taratibu zetu,” alisema Bw Benedicto.

  Aliongeza kuwa kutokana na changamoto hiyo kuna umuhimu wa tume kuweka  mikakati itakayowawezesha kushiriki katika kupiga kura kwa urahisi kwa kuwepo muongozo wa jarida la watu wasioona (TACTILE FOLDER) ili kuwawezesha kusoma maandishi kwa ufasaha.

  “Tunaiomba tume iweke utaratibu wa kuwepo na karatasi maalum za kupigia kura kwa jamii ya watu wasioona ili kuondoa uwezekano wa mtu aliyeteuliwa kupiga kura kwa niaba  na hivyo kwenda tofauti na matakwa ya mpiga kura ambaye ni mlemavu wa macho” alisema Bw.Benedicto.

  Amesema kuwa katika kulishughulikia suala hilo chama  hicho kimeishauri Tume ya kuweka wawakilishi wa walemavu wa aina mbalimbali kushiriki katika mipango yao ili kuwapa fursa  na haki watu wenye ulemavu kushiriki katika masuala ya uchaguzi.

  Chama cha walemavu wasioona kilisajiliwa mwaka 1972 kwa madhumuni ya walemavu wasioona kuungana na watanzania katika matukio mbalimbali ya kitaifa, kujishughulisha na shughuri mbalimbali za uzalishaji mali ili kutoa mchango katika jamii na pia kupata elimu katika nyanja za kiuchumi, siasa na mazingira na kuamasisha jamii ili kupunguza unyanyapaa kwa watu walemavu.


  0 0

   Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Sophia Simba katikatik) akichangia jambo wakati wa Kongamnao la Kongamano la pili la Wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika biashara ya na Maedneleo ya Kiuchumi na kijamii. 
   Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wajasiliamali wanaoshiriki Kongamano  la pili la Wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika biashara ya na Maedneleo ya Kiuchumi na kijamii.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akiangalia bidhaa za wanawake wajasiliamali katika maonesho yanayoendelea sambamba na  Kongamano la pili la Wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika biashara ya na Maedneleo ya Kiuchumi na kijamii.
   
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba anashiriki katika Kongamano la pili la Wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika biashara ya na Maendeleleo ya Kiuchumi na kijamii, nchini Kenya.

  Lengo la Kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wanawake wafanyabiashara, wa Afrika Mashariki ili waweze kubadilishana uzoefu katika biashara pamoja na kuangalia namna ya kutumia fursa zinazopatikana katika umoja wa forodha.
   
  Kongamano hilo linatarajia kuwapatia wanawake nafasi ya kubadilishana mawazo ya kibiashara na kuweka mikakati ya kuzifikia taasisi za fedha ili kujijengea  uwezo  wa kiuchumi na kibiashara.Kongamano hilo linategemewa kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 300 kutoka wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kulia) akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku mapema leo, Agosti 24, 2015 ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kulia) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku mapema leo Agosti 24, 2015 mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kulia) akimkaribisha Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku. Balozi Mseleku alimtembelea Waziri Simbachawene mapema leo (Agosti 24), ofisini kwake na kufanya nae mazungumzo.
  Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku (katikati) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (Kulia), alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam mapema leo, Agosti 24, 2015 na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini nchini, aliyeambatana na Balozi Mseleku, Bi Patiwe Mokoena.


  AFRIKA KUSINI YAVUTIWA KUWEKEZA KWENYE NISHATI NCHINI
  Na Veronica Simba.

  Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene ofisini kwake jijini Dar es Salaam mapema leo, Agosti 24, 2015 na kufanya na kueleza nia ya Serikali yake kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.

  Katika mazungumzo yao, Balozi Mseleku alitaka kufahamu kuhusu  fursa za uwekezaji nchini hususan katika sekta ya nishati na kuweka bayana kuwa Serikali yake inayo nia ya kuwekeza kwenye sekta hiyo.

  Akijibu maombi ya Balozi huyo, Simbachawene alisema kuwa bado kuna fursa za kuwekeza kwenye sekta ya nishati ikiwa ni pamoja na utafutaji wa gesi asilia.“Kama Serikali tunahitaji wabia wa kutusaidia hususan katika utafutaji wa gesi kwenye baadhi ya maeneo kama vile Msimbati,” alisema.

  Simbachawene alisema mpaka sasa gesi nyingi imeendelea kugunduliwa nchini hasa katika Mkoa wa Mtwara. “Pia kuna dalili njema za uwezekano wa kupata gesi katika maeneo ya Pwani ya Bagamoyo,” aliongeza.

  Waziri Simbachawene alisema, Serikali ya Afrika Kusini inakaribishwa kuwekeza nchini katika sekta husika na kwamba endapo watatimiza masharti na sifa husika za uwekezaji zilizowekwa na Serikali, hakutakuwa na pingamizi lolote juu yao.

  Balozi Thami Mseleku aliambatana na Afisa kutoka Ubalozi huo hapa nchini, anayeshughulikia masuala ya Siasa, Bi Patiwe Mokoena.
   


  0 0

   Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli akihutubia wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi.

  Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNICZ

   Waziri Mkuu MizengO Pinda akimtambulisha Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli mbele ya umati wa watu waliofurika jioni ya leo kwenye uwanja wa Azimio mjini MPanda mkoani Katavi wakati wa muendelezo wa kampeni za chama hicho mkoani humo leo.Chama cha CCM kimezindua kampeni zake jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama na wakereketwa wa chama hicho cha CCM
   Wananchi wakishangilia wakati  Waziri Mkuu Pinda alipokuwa akimnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa  Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi
   Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wamefurika leo katika uwanja wa Azimio mjini MPanda wakimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jonh Pombe Magufuli kupitia chama cha CCM,mkoani Katavi.
  Wananchi wa kata ya Katumba wilayani Nsimbo wakiwa wamekusanyika kwa wingi kumsikiliza Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata hiyo, wilayani Nsimbo mkoani Katavi 
  Waziri Mkuu Pinda akimuelekeza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokwenda kuwahutubia wananchi wa Mpanda mjini kwenye kutano wa kampeni  mkoani Katavi.
     Sehemu ya umati wa Wananchi wa kata ya Mishamo,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtambulisha Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya  Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.
   Mmoja wa wananchi akimshangilia Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika kijiji cha Mpandandogo,mkoani Katavi
   Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakisubiri kumisikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
    Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata yaMishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata ya Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.

     Sehemu ya umati wa Wananchi wa kata ya Mishamo,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Kata ya Mishamo mapema leo mchana wakati wa mkutano wa kampeni  wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
    Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata yaMishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
    Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata yaMishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
   Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakisubiri kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda pichani kushoto akiwa na baadhi ya wanachama cha CCM,ndani ya wilaya ya jimbo la Nsimbo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokwenda kuwahutubia wananchi hao kwenye kutano wa kampeni  mkoani Katavi.
  Wafuasi na wanachama cha CCM wakifurahia mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi.

  0 0

   Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
  wa timu ya Harmburg Queens Jamila Kassim baada ya kuwa mabingwa katika
  michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
  mkoa wa kisoka wa Ilala. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana
  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
    Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha wa timu ya Evergreen Linda Shilla baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
  mkoa wa kisoka wa Temeke. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana
  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.

  Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
  wa timu ya Wakati Ujao FC Alphonce Peter baada ya kuwa mabingwa katika
  michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
  mkoa wa kisoka wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana
  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
   Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
  wa timu ya Sylivia Mwacha baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya
  vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka
  wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana katika uwanja
  wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
   Mtendaji mkuu bodi ya ligi Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
  wa timu ya Sylivia Mwacha baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya
  vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka
  wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana katika uwanja
  wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
  Wachezaji wa timu ya Mchanganyiko FC wakishangilia baada ya kuwa 
  mabingwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel

  Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni. Hafla ya kukabidhi kombe
  ilifanyika jana katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini
  Dar-es-Salaam.

  MICHUANO ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Aitel Rising
  Stars kwa mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke jana ilifungwa
  rasmi katika uwanja wa Karume ambapo mabingwa wa mikoa husika
  walikabidhiwa zawadi zao.

  Kwa upande wa wasichana, Hamburg Queens walifanikiwa kutawazwa
  mabingwa wa mkoa wa Ilala huku Bombom wakitwaa taji la ubingwa wa mkoa huo kwa upande wa wavulana.  Katika mkoa wa Temeke upande wa wasichana, timu ya Evergreen ndio
  walitangazwa mabingwa na Wakati Ujao ndio walioibuka wababe kwa upande wa wavulana katika mkoa huo.  Kwa mkoa wa Kinondoni, timu ya wasichana ya Mburahati Queens
  walifanikiwa kuwa mabingwa wakati Mchanganyiko FC wakitangazwa
  mabingwa kwa upande wa wavulana.

  Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Meneja
  Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando, alitoa shukrani zake za
  dhati kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na vyama
  vya mikoa kwa ushirikiano wao ambao unawapa nguvu ya kuendelea
  kudhamini programu hiyo ya soka kwa vijana.

  “Mwaka huu tumeshuhudia uboreshaji mkubwa zaidi wa mashindano haya
  baada ya ujio wa timu za wasichana ambao wameongeza msisimko wa
  michuano hii. Pia naamini tutapata wavijana wenye vipaji ambao
  watasaidia kutangaza taifa letu hapo baadaye katika ngazi za
  kimataifa”, alisema Mmbando.

  “Shukrani zangu nazipeleke pia kwa Makatibu wa mikoa shiriki kwa
  kufanikisha kupata vijana bora na wenye weledi ambao ni nuru ya taifa
  letu kwa siku za usoni”, aliongeza.

  Kwa upande wake mgeni rasmi, Boniface Wambura ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, alisema anaipongeza Airtel kwa mchango wao hapa


  nchini wa kuvumbua vipaji vya vijana ambao ni manufaa kwa taifa kwa
  siku za baadaye.

  “Nimefarijika kuona vijana wakijituma na kucheza kwa ari kubwa licha
  ya umri wao mdogo, jambo ambalo litawafikisha mbali katika maisha yao
  ya soka, kitu cha msingi ni kuhakikisha hamkati tama ili kuweza
  kufikia malengo” alisema Wambura.

  “Sisi TFF, tutahakikisha michuamo yote inayohushisha vijana
  inaendeshwa kwa weledi wa hali ya juu ili kupata vijana bora
  watakaoweza kulisaidia taifa letu kuanzia timu za vijana mpaka za
  wakubwa hapo baadaye”, Wambura aliongeza.

  Wakati huo huo mikoa hiyo mitatu ya kisoka jana imeanza kutoana josha
  katika mashindano ya Airtel Rising Stars yenye lengo la kupata
  mabingwa wa mkoa wa Dar es Salaam chini ya Chama cha Mpira wa soka
  mkoani wa Dar es Salaam (DRFA).

  Katika michezo miwili iliyochezwa jana timu ya Ilala Girls iliibuka na
  ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Temeke Girls wakati timu ya
  wavulana, Ilala Boys walipepetana na Temeke Boys ambapo Ilala Boys
  waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

  Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha
  mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha
  inatarajiwa kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa
  kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11  hadi 21.

  0 0

   Mkufunzi  na Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim akitoa  mada katika mafunzo  ya  siku tano  juu ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika  la Habari la Marekani  Internews  kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
   Mhadhiri wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akionyesha kitabu cha Sheria cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kitabu  cha Sheria cha Tanzania na cha Zanzibar  ambavyo  vinawapasa waandishi wa habari kuvisoma na kuzitumia sheria  hizo katika kuandika habari za Uchaguzi Mkuu kwa usahihi.
   Mhadhiri wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akisisitiza kitu kwa waandishi wa Habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Internews katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
   Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi kutoka vyombo mbali mbali vya Serikali na binafasi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.
   Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari katika kuripoti Uchaguzi Mkuu katika mafunzo ya waandishi wa Habari yanayofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
   Mtayarisha na Mtangazaji wa vipindi wa Redio Zenj FM Mustapha Mussa akitoa mchango katika mafunzo hayo yanayofanyika Ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Zanzibar.
   Washiriki wa mafunzo ya kuripoti Uchaguzi Mkuu wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana katika kufanikisha mafunzo hayo.
   Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Hafsa Golo akiwasilisha mada ya grop lake katika mafunzo ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika la Habari la Ineternews la Marekani katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. 
  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke alipotembelea katika ofisi za MICHUZI MEDIA GROUP (MMG), leo jijini Dar es Salaam.
  Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akifanya mahojiano na Michuzi tv online na  Michuzi Blog,Chalila Kibuda  jijini Dar es Salaam leo.
   Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi, akisalimiana na Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke jijini Dar es Salaam leo. 
  Kutoka kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi,Mpiga picha za Video, Bakari Issa Madjeshi,Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke,Mwandishi wa habari ,Chalila Kibuda, Mwandishi wa habari na Mpiga picha Avila Kakingo na Mpondela  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mahojiano na Mtangazaji wa BBC leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


   Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand EC, Cathreen Bukuku (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kongamano la wiki ya  huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkufunzi na Mratibu wa Mipango wa Kampuni hiyo, Daniel Wadelanga. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Nuebrand EC.
   Mjumbe wa Timu ya Mauzo wa Benki ya Uba United Bank for Africa, Tesha Filemon (katikati), akizungumza katika mkutano huo  kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
   Meneja wa Tawi la Kariakoo wa Benki ya The Peoples Bank of Zanzibar Ltd, Badru Idd (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu benki hiyo na matawi yake.
   Ofisa Usanifu Bidhaa na Usimamizi wa Sharia Amana Benki, Jaffari Kesowani (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu kazi mbalimbali zinazohusiana na na benki hiyo.
   Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
   Msimamizi wa Masoko wa Kampuni ya Avic Town, Daniel Kure (kulia), akielezea kadhi kadhaa zinazofanywa na kampuni hiyo katika mkutano huo. Kushoto ni maofisa wa kampuni hiyo.


   Meneja Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya  Covenant Bank, Mhina Semwenda (kulia), akizungumzia shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
   Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kifedha wakiwa 
  kwenye mkutano huo.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
   Wapiga picha wakiwa kazini. "Chezea kazi wewe"
  Mmoja wa wanufaika na makongamano hayo yanayotolewa na  Kampuni hiyo ya Nuebrand EC, Alphonce Mkubwa kutoka Mbeya akieleza faida ya makongamano hayo aliyoshiriki kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

  Na Dotto Mwaibale

  TAFITI zinaonesha asilimia kubwa ya watu hawatumii njia zilizo rasmi za kifedha kutokana na kukosa elimu ya masuala ya kifedha na uwekezaji.

  Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand, Cathreen Bukuku wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kongamano la wiki ya  huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambalo litahusisha watu wote, wawe wajasiriamali au si mjasiriamali una biashara au huna na wawekezaji wote ambapo washiriki watatoa kiingilio cha ada sh. 2000/- kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo ambapo watapata cheti cha ushiriki,"alisema Bukuku.

  Alisema lengo la kongamano hilo ni kuweka uelewa katika masuala ya kifedha kwani watanzania wengi wamekuwa hawatumii njia zilizosalama na rasmi za kifedha katika uwekaji, akiba na kutengeneza mazingira kuhusiana na huduma za kibenki pamoja na ujasiriamali.


  Bukuku alisema washiriki watapata elimu ya uelewa wa bima mbalimbali kama za maisha, afya na bima ya mali, kupata elimu ya jinsi ya kuandaa mchamganuo mzuri wa biashara, kujifunza ujuzi mbalimbali na kupata fursa ya kushiriki katika shindano la kuandaa mchanganuo wa biashara ambapo atashinda fedha itakayomsaidia kuanzisha au kuendeleza biashara yake.

   Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa,  alisema lengo lao ni kutoa elimu ya bima za maisha kwa watanzania na kujua haki zao pamoja na kujua fursa zilizopo huku mshiriki akipata huduma myimgi kwa wakati mmoja.

  Mshindi wa kongamano hilo msimu uliopita, Alphonce Mkubwa aliwataka vijana kujitokeza kushiriki ili wapate elimu ya kufanya biashara ili wapate mafanikio," Nilikuwa mshindi katika kutoa wazo la biashara ambapo nilishinda zabuni ya ukusanyaji ushuru katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya...huu ni muda wa kufanya kazi kwani huu ni ukombozi kwa kutokukaa kijiweni,"alisema Mkubwa.  
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

older | 1 | .... | 617 | 618 | (Page 619) | 620 | 621 | .... | 1898 | newer