Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

WAGONJWA 100 WA UGONJWA WA MABUSHA WANAFANYIWA UPASUAJI MANISPAA YA MTWARA

$
0
0
 Mratibu wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira, akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye tatizo la ugonjwa wa mabusha Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,iliyofanyika katika hospitali  ya Mkoa ya Ligula.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) na Mwenyekiti wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Afrika Dkt. Mwele Malecela akitoa salamu kwenye uzinduzi wa kambi hiyo, ambapo alisema Matende na mabusha ni magonjwa ambayo yanatakiwa kutokomezwa ifikapo mwaka 2020 nchini Tanzania.
 Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ,wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibimayila, akipokea mfano wa hundi toka kwa mwakilishi wa Stat Oil Naomi Makota (kulia) kwa ajili ya upasuaji wa wagonjwa wapatao 100 wa Manispaa ya Mtwara.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa kambi hiyo ya upasuaji Johansen Bukweri akizungumza kwenye uzinduzi huo, alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yamekuwa yakiathiri sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wa Mtwara na kuleta mahangaiko mengi kwa wananchi ikiwemo ulemavu, hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika ujenzi wa Taifa na watoto kutoweza kuhudhuria vizuri katika masomo shuleni.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye ugonjwa wa mabusha.
 Dkt. Upendo Mwingira akiwafariji wagonjwa waliokwishafanyiwa upasuaji wa mabusha katika hospitali ya mkoa ya Ligula.Upasuaji huo ni wa siku 5. Mkoa wa Mtwara una takribani watu wapatao 2,500 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mabusha.Kambi hii itafanyika kwa watu waliojiandikisha na itatolewa bila ya malipo.

MUZIKI MNENE BANGO KINONDONI NA KAWE

$
0
0
93.7. EFM bado inaendelea na matayarisho ya tukio lao la Muziki Mnene Bar Kwa Bar ambalo litaanza kufanyika rasmi kuanziya tarehe 5/09/2015. Muziki Mnene Bango bao inaendelea na ukiwa umeweka bango la EFM kakita sehemu yako ya biashara na bwana E akipita akaona bango hilo huku ukisikiliza matangazo ya EFM utapata kifurushi chenye zawadi na tuvitu vitu kibao. 
 Mshindi wa Muziki Mnene Bango akikabidhiwa zawadi yake na bwana E mr Jimmy Jiam zikiwemo EFM t-shirt na kifurishi chenye vitu mbalimbali baada ya kuweka stika ya EFM kwenye eneo lake la biashara ndani ya soko la kinondoi, Dar es Salaam.
 Mshindi wa Muziki Mnene Bango akikabidhiwa zawadi yake na bwana E mr Jimmy Jiam zikiwemo EFM t-shirt na kifurishi chenye vitu mbalimbali baada ya kuweka stika ya EFM kwenye eneo lake la biashara ndani ya soko la kinondoi, Dares Salaam.
Bango kubwa la 93.7 EFM Muziki Mnene lililowekwa na mmoja wa mashabiki na mshindi wa EFM Muziki Mnene lilimvutia bwana E wakati anapita eneo la Kinondoni, jijini Dar-Es-Salaam.

NYUMBU KUENDELEA KUWAWEZESHA WANANCHI KUJIINUA KIUCHUMI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu miradi mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo inayodhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo utengenezaji wa matrekta madogo( power Tiller) ambayo yanalenga kumkomboa mkulima hapa nchini kwa kuondokana na matumizi ya jembe la makono.

 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) umuhimu wa kutoa habari za kuelimisha kwa jamii hasa zitakazowawezesha kuwajengea uwezo wa kimaarifa na kuwainua kichumi kupitia elimu hiyo.



Mhandisi Mkuu Msanifu Albert Wikedzi akiwaonesha waandishi wa Habari (Hawapo pichani) aina mbalimbali za sanifu zinazofanyika katika shirika hilo, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika kiwanda hicho Mjini  kibaha.

 .Mhandisi Mkuu wa Karakana kutoka Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Ayoub Mnzava akiwaonesha waandishi wa habari trekta ndogo (Power Tiller) iliyotengenezwa kwa lengo la kuongeza uwezo wa wazalishaji wa mazao ya kilimo kote nchini.

 Mkuu wa Kitengo cha Usubiaji Mhandisi Anderson Ole Zakaria akiwaeleza waandishi wa habari namna kitengo hicho kinavyofanya kazi ili kukidhi mahitaji ya kiwanda ambapo alisema kitengo hicho kinayeyusha hadi tani 2.5 za chuma zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotoka katika shirika hilo.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim akiwaonesha waandishi wa habari moja aina ya gari la kivita lililotengezezwa na shirika hilo.

.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara hiyo,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe na kushoto ni mwandishi mwandamizi wa Channel Ten.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

VODACOM NA MONEYGRAM WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

$
0
0
 Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi  wa makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram (Moneygram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kutuma fedha na kuingia moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini.Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam.
003.Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(katikati) na Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kulia)wakimshuhudia Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt(kushoto)akisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram(Monegram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(katikati) akiwashuhudia Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt(kushoto) na Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kulia)wakipongezana mara baada ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa  kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram(Moneygram M-Pesa)ambayo yatawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kushoto) na Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt,wakiteta jambo wakati  wa hafla ya Uzinduzi  wa makubaliano yaushirikiano wa  kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram (Moneygram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kutuma fedha na kuingia moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini.Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam.


  Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(kulia) akijibu maswali kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma ya za kutuma na kupokea fedha kupitia njia ya M-pesa na Moneygram(Monegram M-Pesa)kati ya Vodacom Tanzania na  Moneygram huduma hizo zitawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini leo Dar es Salaam. ,Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel na  Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt.


Makubaliano mapya yanawawezesha wateja kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti za M-Pesa nchini Tanzania.


DAR ES SALAAM (Agosti 25, 2015) —Kampuni ya MoneyGram inayotoa huduma za kutuma pesa duniani na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania zimetangaza kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M-Pesa. Kwa sasa, kuna watumiaji wa huduma ya M-Pesa zaidi ya milioni saba nchini Tanzania ambao hufanya miamala ya zaidi ya trilioni mbili kila mwezi.





Ushirikiano huo mpya utawawezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kutuma fedha moja kwa moja kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini ambao ni wateja wa M-Pesa kwa njia rahisi, inayofaa, salama na haraka zaidi. Hatua hiyo itafungua uwezekano wa kukuza utumaji pesa kwenda Tanzania, ambao kwa sasa ni umefikia dola za Marekani bilioni 1.2.


Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo pia ulihudhuriwa na Herve Chomel, Makamu wa Rais wa MoneyGram Upande wa Mauzo Kanda ya Afrika na Jacques Voogt, Ofisa Mkuu wa wa Idara ya biashara ya huduma za M-Pesa wa Vodacom Tanzania.


“Kampuni ya MoneyGram inafurahi sana kufanyakazi na Vodacom kutoa huduma ya haraka, uhakika na salama  kwa mamilioni ya wateja watakaotuma na kupokea pesa,” alisema Chomel. “Vodacom M-Pesa tayari imesaidia kuongeza huduma za utumaji pesa kwa gharama nafuu kwa mamilioni ya watu wa makundi mbalimbali nchini Tanzania na ushirikiano huu mpya utawawezesha zaidi watu walio vijijini na mijini kupokea pesa kutoka kwa marafiki na jamaa zao wanaoishi nje ya nchi.”


Aliongeza kusema, “MoneyGram inaendelea kukua Afrika yote kutokana na uhusiano mzuri ilionao na kampuni za mtandao wa simu, mabenki, ofisi za posta, watoahuduma za rejareja ili kuwapa kipaumbele zaidi wateja wetu. Kwa sasa, MoneyGram inatoa huduma zake kwa zaidi ya nchi 200 huku ikiwa na mtandao wa za mawakala zaidi ya 350,000 kote duniani ambapo 25,000 wanatoka Afrika.”


“Uhusiano huu mpya na MoneyGram unatuwezesha kuingiza nchini dola za Marekani bilioni 1.2 kwa wateja wetu kila mwaka, anasema Voogt. “Utawarahisishia zaidi na kuwezesha familia na marafiki kupokea pesa kupitia M-Pesa. Hii ni njia mojawapo tunakwenda mbali zaidi kwa ajili ya wateja wetu.”




Wateja wa M-Pesa nchini Tanzania wanaweza kupokea pesa kutoka MoneyGram moja kwa moja kwenye akaunti za simu zao kutoka kwa wateja katika nchi zaidi ya 120 kwa saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki na siku 365 kwa mwaka kulingana na mfumo uliopo. Wateja wanaoishi nchini Marekani wanaweza kutuma pesa kwenda kwenye akaunti za M-Pesa kwa haraka na usalama zaidi  kutoka kwa wakala wa MoneyGram au MoneyGram kwa njia ya mtandao.

HUKUMU YA KESI YA TALAKA NA MGAWANYO WA MALI YA MWENYE SHULE ZA ST MATHEW KESHO

$
0
0
court_gavel
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, kesho, Oktoba 25 inatarajia kutoa hukumu kwenye kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na mkazi wa Singida, Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks,Thadei Mtembei.

Katika madai yake ya Msingi, Mwangu anaomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Rajab Tamaambele.
Miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo ni pamoja na Mwangu ambaye alidai kuwa alianza kuishi na Mutembei mwaka 1995 Kongowe Mbagala ambapo mwaka 1998 alikwenda kwa wazazi wa Mwangu kijiji cha Kwaye Iguguno Singida ambapo alitoa mahali na walifunga ndoa ya kimila. 

Alisema mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1998, huku mtoto wa pili akizaliwa mwaka 2000 na mtoto wa tatu 2003
Katika ushahidi wao, watoto wa Mwangu ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma, wamedai kuwa wanasumbuliwa ada na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.

Watoto hao waliiambia mahakama kuwa, mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.
Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi kuwalipia ada na badala yake aliwapa Sh 40,000 kila mmoja, fedha ambazo aliziacha mezani.

Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.

Wakati wa ushahidi wake Mutembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.
Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.

TANGAZO LA KIFO

$
0
0
  
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA
Bodi  ya Ushauri, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wanasikitika  kutangaza kifo cha  Mwenyekiti wa Bodi  ya TAA,   Inj. Lambert W. Ndiwaita  kilichoteka  tarehe 20/08/2015  katika  Hospitali  ya Nairobi,  Kenya.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake mjini Bukoba  tarehe 25/08/2015.


Mhandisi  Lambert Ndiwaita (64)  ni mmoja wa wataalamu waliobobea katika masuala ya  usafiri wa anga  kitaifa na kimataifa, katika kipindi cha uhai wake ametoa mchango mkubwa katika  maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini na nchi  nyingine duniadi.


Alianza shughuli zinazohusiana na  usafiri wa anga mwaka 19971  alipoajiriwa na iliyokuwa  Wizara ya  Ujenzi  kama  Mhandisi  Msaidizi na baadaye alipanda hadi   kufikia cheo cha  Mhandisi Mkuu  (Chief Engineer) akishughulikia masuala ya baeabara na  viwanja vya ndege.

 Mwaka 1993 alikwenda kufanya kazi katika Idara ya Usafiri wa Anga nchini Botswana kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mwaka 1994 aliajiriwa na  Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga  International Civil Aviation Organization (ICAO)  kusimamia  masuala ya  viwanja vya ndege (Aerodrome & Ground Aids) kwa eneo  la Mshariki na kusini mwa Afrika, katika ofisi za ICAO  zilizopo jijini Nairobi, Kenya.


Mhandisi Ndiwaita ni msomi aliyehitimu Shahada ya kwanza ya Uhandisi (Bsc Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1978 alihitimu  masomo Shahada ya Uzamili (Msc in Civil Engineering) katika Chuo kikuu cha Califonia, Berkley, nchini Marekani akijitikita zaidi katika masuala uhandisi wa ujenzi wa viwanja vya ndege.


Marehemu Lambert Ndiwaita atakumbukwa  na  wadau wa usafiri wa anga nchini na duniani kwa  mchango  mkubwa katika  maendeleo ya sekta hiyo  ambapo  kwa hapa nchini akiwa  Mwenyekiti wa Bodi  ya TAA  amechangia   kufanikisha ujenzi na uboreshaji wa viwanja  kadhaa  vikiwemo Mwanza, Tabora, Kigoma, Songwe,Mafia, Mpanda, Bukoba na Julius Nyerere  (JNIA).


Mungu ailaze roho marehemu  mahala pema peponi.


Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu-TAA.

24th AUGUST, 2015

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID KUHUSU HALI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari hawaponi pichani juu ya Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono Kunywa maji yaliyo safi na salama – yaliyochemshwa au kutiwa dawa Hakikisha usafi wa mazingira yako wakati wote ikiwa ni pamoja na chooni Kutokula matunda au kitu chochote bila kukisafisha kwa maji safi na salama Kuhakikisha unatumia choo kwa ufasaha na wakati wote Kuwahi mapema na toa taarifa kituo cha huduma  ya afya kilicho karibu na wewe endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au kutapika
 Katibu Mkuu wa Wizari wa Afya na Usitawi wa Jamii.Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya Usafirishaji holela wa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Ni vyema kutoa taarifa iwapo kuna abiria mwenye dalili  za ugonjwa huu ili ushauri uweze kutolewa wa namna ya kumsafirisha.
 Mwakilishi wa Shilika la Afya Duniani( WHO) Dk Rufaro Chatora akizungumza na waandishi wa habari hapo pichani juu ya  Kufungua kambi za wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa zote tatu za Dar es Salaam ambapo kwa Kinondoni kambi ipo Mburahati, Ilala, kambi ipo kituo cha Afya Buguruni  na Temeke katika Hospitali ya Temeke. Kwa Mkoa wa Morogoro kambi zimefunguliwa Sabasaba na St Thomas.
Waandishi wakimsiliza kwa makini Waziri wa Afya na Usitawi wa Jamii,Dk Seif Rashid.
Picha na Emmanuel Massaka.

IDADI YA WAGONJWA WALIYORIPOTIWA KUAMBUKIZWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU AMBAO UMELIKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM PAMOJA NA MKOA WA MOROGORO IMEFIKIA WAGONJWA 262  NA VIFO 8.
                                                                                 
Idadi ya wagonjwa waliyoripotiwa kuambukizwa na Ugonjwa wa Kipindipindu ambao umelikumba jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Morogoro imefikia wagonjwa 262,huku vifo  hadi sasa toka ugonjwa huo ugundulike Agost 15 mwaka huu vikifikia nane.


Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Daktari Seif Rashidi wakati akizungumza nawaandishib wa habari ikiwa lengo ni kutoa taarifa juu ya Ugonjwa huo hatarI ambao umeibuka kwa kasi jijini Dar es salaam pamoja na Mkoani Morogoro.




Aidha alisema kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa katika jiji la Dar es salaam walioambukizwa ni 230 na vifo saba,ambapo Manispaa ya Kinondoni ina wagonjwa 186,Manispaa ya Ilala wagonjwa 22 na Temeke 22 nakwamba wagonjwa waliyolazwa kwenye  kambi  za matibabu ni 71 ambazo ni Mburahati wagonjwa 47,kambi ya Buguruni 15 huku kambi ya Temeke ni wagonjwa 9.


Aliendelea kufafanua kuwa wagonjwa  wengi wamekuwa wakitoka katika maeneo mabalimabali ambapo katika Manispaa ya Kinondoni ni maeneo ya   makumbusho,kimara,Tandale,Manzese,Saranga,Magomeni,Mwananyamala,kibamba,kigogo,Goba,Burahati,Kinondoni na Kijitonyama.


Manispaa ya Ilala ni Buguruni,Majohe,Chanika,Ilala sharif shambana Tabata huku Katika Manispaa ya Temeke wagonjwa wengi ni kutoaka katika maeneo ya kwa Azizi Ally,Keko na Yombo Vituka.



Alisema Mkoani Morogoro wagonjwa waliyoripotiwa Agost 24 mwaka huu ni 32 na kifo kimoja ambapo pia wagonjwa wapatao 15 wamehifadhiwa kwenye kambi ya Matibabu ya Sabasaba Mkoani humo.


Waziri huyo wa Afya na Ustawi wa Jamii ametoa tahadhari kwa jamii kuchukua tahdhari pamoja na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo,kuzingatia usafi wa mazingira,kuchemsha maji ya kunywa,kunawa  mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula chakula,kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikoni,kuzingatia usafi wa vyoo pamoja na kula vyakula ambavyo vimeandaliwa kwenye mazingira safi na salama.


Naye mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani Daktari Rufaro Chatora amesema kuwa lazima kuwepo na hatua za haraka za kusafisha visima kwa kemikali maalumu na kuhamasisha jamii kutumia vidonge vya kusafisha maji au kuchemsha maji.


Aidha aliongeza kuwa mamlaka husika zichukue hatua za haraka na madhubuti kushugulikia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazigira katika maeneo husika nakwamba suala hilo siyo la Wizara ya Afya pekee bali ni ushirikiano na Wadau wengine ikiwemo sekta ya Uchukuzi,Mawasiliano,Maji na Elimu.


Katika hatua nyingine Wizara ya Afya imetoa namba za simu ya mkononi kwa wananchi  ambazo ni 0767300234 ambapo zitatumika kuwasiliana moja kwa moja na mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili kupata maelekezo ya kitabibu mara baada ya kuhisi dalili za maambuki ya ugonjwa huo.                                                                    

FAIDA BENKI YA EXIM YAKUA KWA ASILIMIA 69

$
0
0
 Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati)akisisitiza jambo  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kushoto) na Meneja Mwanadamizi wa utafiti na uchambuzi wa biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Mrawa (wa kwanza  kulia)
Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (wa kwanza kulia)akisisitiza jambo  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (katikati) na  Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde

Benki ya Exim Tanzania imefanikiwa kujipatia faida ya sh. bilioni 12.79 (kabla ya kodi) katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu, takwimu zinazoonyesha ongezeko la faida kwa asilimia 69 katika benki hiyo.

“Ongezeko hilo ni kubwa ikilinganishwa na faida yash.bilioni 7.56 tuliyoiopata katika robo mwaka iliyotangulia na hivyo basi tunajisikia fahari kutangaza faida hii mbele yenu,’’ alibainisha Afisa Fedha Mkuu wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Bw Ponda faida hiyo pia ni sawa ongezeko la asilimia 28 ikilinganishwa na faida ya kiasi cha sh. bilioni 13.96 katika kipindi cha miezi sita kwa mwaka uliopita.

 “Katika robo mwaka hii iliyoisha mwezi Juni, jumla ya mapato kwenye faida  itokanayo na riba ilikuwa kwa asilimia 26 hadi kufikia sh. bilioni 17.9  ongezeko lilichangiwa na gharama nafuu ya amana zetu sambamba na usimamizi bora wa fedha,’’ alibainisha.

Zaidi Bw. Ponda alisema katika kipindi hicho  faida isiyotokana na riba ilikuwa kwa asilimia 43 hadi kufikia kiasi cha sh. bilioni 12.3 kutoka sh. bilioni 8.6 iliyorekodiwa katika mwaka uliopita.

Benki hiyo pia ilikuwa na mapato mgao kutokana na uwekezaji wenye ukubwa kiasi cha sh. bilioni 2.3 ikilinganishwa na kiasi cha sh. bilioni 2 kilichorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

"Nguvu ya ukuaji wa mapato inaoyesha mafanikio ya Benki.. Tunaendelea kuboresha  ufanisi katika uendeshaji na utoaji wa huduma zetu ili kuwaridhisha zaidi wateja wetu. Kwa ripoti hii  matokeo yanaonyesha kwamba Exim tumeonyesha utendaji bora hasa kwa kuhusisha rasilimali watu na technolojia iliyo bora zaidi "aliongeza.

Rais Kikwete ashiriki mazishi ya Mtoto wa Jaji Mkuu mjini Tanga

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande wakati Rais alipokwenda Chumbageni Tanga kuhudhuria mazishi ya marehemu.
 Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman akiweka udongo katika kaburi la mwanaye Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni Tanga leo jioni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Said Mohamed Chande wakati ya mazishi yaliyofanyika katika eneo la Chumbageni Tanga leo.Marehemu Said ni Mtoto wa Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman.
 Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akiweka udongo katika kaburi la mrehemu Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika huko Chumbageni Tanga.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal,Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman wakiomba dua wakati wa mazishi ya marehemu Said Mohamed Chande ambaye ni mtoto wa jaji mkuu yaliyofanyika katika makaburi ya familia huko Chumbageni Tanga leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman(aliyesimama pembeni ya Rais) kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande mjini Tanga. Picha na Freddy Maro

LOWASSA, DUNI WATEMBELEA MASOKO YA TANDALE NA TANDIKA JIJINI DAR

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Wazee wa Tandale, wakati alipotembelea Soko la Tandale, jijini Dar es salaam leo, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni (kushoto).PICHA ZOTE NA MTAA KWA MTAA BLOG
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni  wakipata maelezo kutoka kwa Bw.Omari Juma (kulia) ambaye ni mfanyabiashara ya kuuza Maharage katika Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015, wakati walipotembelea Soko hilo kujionea hali ya biashara masokoni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapungia wananchi wa Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kijana ambaye ni muendesha baiskeli ya miguu mitatu (guta) aliekuwa akitoka kwenye Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi Mkubwa (jina lake halikupatikana kwa haraka) aliekutana nae ndani ya Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipata kikombe cha chai ya maziwa iliyokuwa ikiuzwa na Mwanadada (jina lake halikupatikana mara moja) wakati alipotembelea soko la Tandale, Manzese, jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wananchi wa Tandale, Manzese, jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015, baada ya kutembelea Soko hilo.
Umati wa watu ukiwa umefurika nje ya Soko la Tandika, Temeke jijini Dar es salaam kutaka muwaona Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, waliotembelea Soko hilo leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakitembelea Soko la Tandika, Temeke Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Kijana Alex aliekuwa akiuza maji ya kwenye vifuko vya plastiki, akizungumza jambo na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, wakati walipotembelea Soko la Tandika, Temeke Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakikata mitaa ya Soko la Tandika, Temeke Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Vijana wa Tandika wakiwashangilia Wagombea hao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wananchi wa Tandika.

TAASISI YA BILL NA MELINDA GATE YAANGALIA UWEZEKANO WA KUSAIDIA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA KILIMO NCHINI TANZANIA.

$
0
0
x1
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates Bw. Stanley Wood akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) nchini Tanzania kuangalia uwezekano wa taasisi hiyo kusaidia miradi ya ukusanyaji wa Takwimu za kilimo nchini Tanzania.Kushoto kwake ni Mratibu wa miradi wa Taasisi hiyo Bi.Bhramar Dey.
x2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu umuhimu wa takwimu za Kilimo nchini Tanzania na mikakati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha upatikanaji wa Takwimu za kilimo nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw.Morrice Oyuke.
x4
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof.Innocent Ngalinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya chuo anachokiongoza katika kutoa elimu kwa watakwimu wa kilimo nchini Tanzania na mpango wa chuo hicho kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za  kilimo kwa kutumia wataalam wanaozalishwa.
x5
Mtakwimu mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi.Elizabeth Talbert( kulia) na Meneja wa Idara ya Viwanda na Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Joy Sawe wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wawakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates jijini Dar es salaam.Picha na Veronica Kazimoto.

…………………………………………………………………………………….
Na  Aron Msigwa
Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gate imekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)kuangalia namna ya inavyoweza kusaidia  upatikanaji wa Takwimu Bora za Kilimo nchini Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanyika kwa  mazungumzo hayo jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi wa Taasisi hiyo anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo Bw. Stanley Wood amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali Barani Afrika na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika  zilizopewa kipaumbele na kunufaika na taasisi hiyo.

Amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na matokeo chanya, taasisi hiyo inaangalia uwezekano wa kusaidia upatikanaji wa takwimu bora za kilimo.
 
” Juhudi kubwa imefanywa na Tanzania katika kufanikisha mambo mbalimbali, kwa upande wetu tumeona vipaumbele vilivyopo ili tuweze kuona namna  tunavyoweza kutoa mchango wetu kusaidia ukusanyaji wa takwimu Bora za kilimo , kikubwa ni kuendelea  kujenga ushirikiano wa kuwezesha ufanisi wa tafiti mbalimbali” Amesema.
 
Wood ameeleza kuwa taasisi ya Bill na Melinda Gates imekuwa ikichangia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Barani Afrika kupitia mashirika ya kimataifa yanayohusika na utoaji wa huduma kwa umma na kuitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika  zinazonufaika na miradi  hiyo.

Amesema taasisi ya Bill na Melinda Gate kwa kipindi kirefu imekuwa ikitoa kipaumbele kusaidia miradi ya afya hasa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi, kusaidia huduma za Afya ya mama na mtoto  pamoja na kuweka mkazo  katika kuimarisha huduma za maji safi na maji Taka Barani Afrika.

DKT MAGUFULI AZIDI KUPASUA ANGA KWA KISHINDO MKOANI RUKWA

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,Mhe. Mizengo Pinda akimtambulisha mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sumbawaga mjini mkoani Rukwa,ndani ya Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mkutano wa kampeni,pichani nyuma ni Waziri Mkuu Pinda akishuhudia tukio hilo.

   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atawatumikia kwa nguvu zake zote, na hatokuwa na simile kwa watendaji wazembe.

Wananchi wa Sumbawanga mjini wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa Nelson Mandela wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera kwa wananchi
Wananchi wa Sumbawanga mjini waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Mh.Pinda akimtambulisha Dkt Magufuli kwa wananchi wa Kata ya Majimoto,wilaya ya Mlele mkoani Katavi kwenye mkutano wa Kampeni.
Umati wa wananchi wa Kitai wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli lipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji moto wilayani Mlele mkoani Katavi.
Umati wa wananchi wa Namanyere walayani Nkasi mkoani Rukwa wakiwa wamefurika wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli lipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano huo wa Kampeni
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini tayari kuwahutubia wakazi wa mji huo.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi jukwaani anaewania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nkasi Ndugu Ali Kessy,mbele ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni. 
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mpimbwe,Dkt Pudenciana Kikwembe akimwombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi jukwaani anaewania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nkasi Ndugu Ali Kessy,mbele ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni.
 Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa mji wa Namanyere wilayani Nkasi (hawapo pichani),kabla ya kuanza kuwahutubia kwenye mkutano huo wa kampeni,kati ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,Mhe. Mizengo Pinda pamoja na anaewania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nkasi Ndugu Ali Kessy
 Moja ya bango lililobebwa na baadhi ya wafuasi wa CCM ndani ya uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga jioni ya leo.
  Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya akiwahutubia wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
 Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo.
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atawatumikia kwa nguvu zake zote, na hatokuwa na simile na watendaji wazembe.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akiwapungia wananchi alipokuwa akiwasilia katika Kata ya Maji moto alipokwenda kuwahutubia wakazi wa kata hiyo wilayani Mlele mkoa wa Katavi.kulia kwa mgombea ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Mh.Pinda
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akiwapungia wananchi alipokuwa akiwasilia katika Kata ya Maji moto alipokwenda kuwahutubia wakazi wa kata hiyo wilayani Mlele mkoa wa Katavi.kulia kwa mgombea ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Mh.Pinda
Wakifurahia jambo 
Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lunyala,wilayani Nkasi alipokuwa akielekea mjini Namanyere kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe (hayupo pichani) akiwahutubia wakazi wa kata ya Maji moto,wilayani Mlele mkoani Katavikwenye mkutano wa kampeni.

Serikali yasaini mkataba wa zaidi ya Sh. Bilioni 422 kuimarisha sekta ya afya nchini.

$
0
0
1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini hati ya makubaliano ya mkopo nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ili kuimarisha sekta ya afya nchini katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird.
2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo nafuu na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird (kulia) mara baada ya kusaini hati hiyo ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ili kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam.
3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird.
4
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile.

5
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa (kulia) akisisitiza jambo wakati hafla ya usatiji saini hati ya makubaliano kuimarisha sekta ya afya nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia leo jijini Dar es salaam.
6
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mipango na Sera Bernard Konga (kulia) akitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia kwa kuthamini sekta ya afya leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa.
8
Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi wa serikali na wawakilishi wa Benki ya Dunia waliohudhuria hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia katika kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam.
(Picha Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………..
Na Allen Mhina –MAELEZO
Serikali kupitia mpango wa kuimarisha afya duniani, imepokea Dola za Kimarekani milioni 200 sawa na Sh. Bilioni 422.8 toka Benki ya Dunia ili kuimarisha sekta ya afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mpango wa kuimarisha sekta ya afya nchini iliofanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa serikali na wawakilishi wa Benki ya Dunia, Dkt. Likwelile alisema kuwa dhumuni la makubaliano ya mpango huo ni kuwezesha na kuimarisha sekta ya afya na vitendea kazi vitakavyowezesha uzazi salama kwa wakina mama wakati wakujifungua na kupunguza idadi ya vifo vya watoto kutokana na mapungufu wa afya bora.
Dkt. Liwalile, aliongeza kuwa kuna umuhimu na makusudio ya dhati kuimarisha sekta hiyo kutokana na uwepo wa vifo vinavyozuilika kwa wakina mama na watoto, kama inavyodhihirisha takwimu zilizotolewa wizara ya afya kuonesha kuwa kuna kuna idadi kubwa ya watoto wanaofariki wakati wa uzazi kwa kukosekana kwa vitendea kazi na huduma bora wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuonesha juhudi za dhati kutekeleza mpango huo.
Bi Bella amesema kuwa amefurahishwa na juhudi za Serikali ya Tanzania katika kusimamia sekta ya afya ambapo alitembelea baadhi ya vituo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani na kujionea hali ilivyo na kuhaidi kushirikiana vizuri na serikali ili kukamilisha mpango huo na kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini.
Naye Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bernard Konga aliishukuru Serikali na Benki ya Dunia kwa kuthamini sekta ya afya na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kuendeleza sekta ya afya kama ilivyokusudiwa na ili kuboresha sekta ya afya ya kuleta matokeo chanya katika maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kipindi cha JUKWAA LANGU. Jumatatu Agosti 24, 2015

$
0
0
Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VYAMA VYA SIASA KUZINGATIA RATIBA YA KAMPENI YA UCHAGUZI WA RAIS KWA KUFANYA MIKUTANO KWA TAREHE, SEHEMU NA MAHALA KWA MUJIBU WA RATIBA


VYAMA VYA SIASA VYAASWA KUZINGATIA RATIBA YA KAMPENI YA UCHAGUZI WA RAIS KWA KUFANYA MIKUTANO KWA TAREHE, SEHEMU NA MAHALA KWA MUJIBU WA RATIBA.

$
0
0
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 pamoja na Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015. Kampeni za Uchaguzi huanza siku moja baada ya uteuzi na huisha siku moja kabla ya siku ya kupiga Kura. 

Kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa Kampeni zinafuata muda, Kanuni ya 39 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na Maadili ya Uchaguzi kifungu cha 2.1 (c) inaelezwa Mikutano yote ya Kampeni itaanza saa 2:00 asubuhi n kuisha saa 12:00 jioni. 

Kanuni ya 40 (1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 inasema, Mkurugenzi wa Uchaguzi kabla Kampeni za Uchaguzi wa Rais hazijaanza atavitaka vyama vya Siasa kuwasilisha mapendekezo ya ratiba za Mikutano ya Kampeni, na kanuni ndogo ya (3) inasema, lazima Chama kiwasilishe mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ikionesha tarehe, muda, Mkoa na Wilaya ambapo Mkutano utafanyika. 

Aidha, kanuni ya 41 (1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 inaeleza kuwa iwapo Chama cha Siasa kitahitaji kufanya mabadiliko ratiba au eneo la Mkutano wa Kampeni, kitawasilisha mapendekezo yakiambatishwa na sababu za kutaka kufanya mabadiliko kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambaye kabla ya kufanya marekebisho katika Ratiba husika ataitisha Mkutano wa Kamati ya Kuratibu Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi wa Rais inayojumuisha vyama vyote vyenye wagombea katika nafasi hiyo ili vikubali au kukataa mabadiliko yanayopendekezwa. 

Kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni tajwa hapo juu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivialika Vyama vya Siasa vyenye Wagombea wa kiti cha Rais kuwasilisha mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ya Rais. Mnamo tarehe 22 

1Agosti, 2015 kwenye kikao cha kwanza cha Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi, Vyama vyote vyenye Wagombea wa Kiti cha Rais vilipitia mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ya Wagombea Kiti cha Rais ambapo marekebisho yalifanyika na kwa pamoja vyama vilikubaliana kuwa Ratiba hiyo ndiyo itakayofuatwa hadi hapo kutapotokea marekebisho yatakayokubaliwa na vyama vyote vye Wagombea wa kiti cha Rais. 
Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 124A (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha Uchaguzi wa haki, uhuru na Amani, na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa na Serikali, itaandaa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi yatayoeleza maadili ya vyama vya siasa na Tume wakati wa Kampeni za uchaguzi na uchaguzi. 


Kifungu cha 124A (2) (a) na (b) kinasema Maadili hayo yatakubaliwa na kufuatwa na kila chama cha siasa na mgombea wa nafasi yoyote atapaswa kusaini Fomu namba 10 ya kukubali, kuyaheshimu na kutekeleza Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015, ambapo Wagombea wote walisaini kwani ilikuwa ni mojawapo wa kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Rais /Makamu wa Rais, Mbunge au Diwani. 

Katika Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yaliyokubaliwa na kusainiwa na vyama vyote vya Siasa tarehe 27 Julai, 2015, vyama vyote vilikubali kuheshimu na kutekeleza Maadili hayo na ukiukwaji wowote wa Maadili hayo utashughulikiwa kwa mujibu wa kipengele cha 5.11 cha Maadili hayo

Hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya vyama vya siasa kuanza kufanya mikusanyiko ya Kampeni ya Rais. Mikusanyiko hiyo yenye sura ya Kampeni haipo katika Ratiba ya Kampeni ya Urais. Mikusanyiko hiyo yenye sura ya kampeni inaweza kuingiliana na ratiba za kampeni za chama kingine katika maeneo husika na hivyo kusababisha uvunjifu wa amani. 

Iwapo Chama cha Siasa kinachotaka kufanya mikusanyiko yenye sura ya Kampeni za Uchaguzi kinapaswa kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ili aweze kuitisha Kamati ya Ratiba ya Kampeni ya Rais inayojumuisha vyama vyenye Wagombea wa Kiti cha Rais ambavyo kwamujibu wa kanuni tajwa hapo juu, vinaweza kukubali au kukataa mapendekezo hayo.Vyama vyote vya Siasa vizingatie Ratiba ya Kampeni ya Uchaguzi wa Rais na viache kufanya mikusanyiko ya aina yoyote ambayo haipo katika Ratiba ya Kampeni ya Rais. 

Chama kitakachokiuka maelezo haya kitakuwa kimekiuka kipengele cha 2.1. (a) cha Maadili ambacho kinaelekeza kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa na Wagombea kuheshimu na kutekeleza Sheria za Uchaguzi, Kanuni za Uchaguzi, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Sheria zingine za nchi katika kipindi chote cha Uchaguzi. 

Ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi adhabu zake zimefafanuliwa katika kipengele cha 5.10 na 5.12 cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.
Imetolewa na:
Tarehe 25 Agosti, 2015
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZ 

HIVI NDIVYO MAGUFULI AIIVYOUNGURUMA MJINI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

      
   “PRESS RELEASE” TAREHE 26.08.2015.

MTOTO WA MIAKA SITA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WAKIWA NA BHANGI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA SITA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGNES SHOMBE MKAZI WA CHIMBUYA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI AINA YA TOYOTA HAICE AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.08.2015 MAJIRA YA SAA 13:10 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. 

CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA AJALI. UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI DSM ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IDD MKWACHU (41) ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA YENYE NAMBA ZA USAJILI T.632 DEM  AINA YA TOYOTA R4 KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO KATIKA BARABARA YA MBALIZI/MKWAJUNI MKOANI MBEYA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 25.08.2015 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ILOLO, KIJIJI CHA NJELENJE, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBALIZI/MKWAJUNI. 
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, DEREVA WA GARI HIYO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AHIMIDIWE NGILANGWA (29) MKAZI WA JIJINI DSM NA ABIRIA WENGINE WAWILI WANAUME WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA.UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEGONGA NA KUKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.


TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ERICK SIMWANZA (18) MKAZI WA NAKONDE-ZAMBIA 2. CHARLES SILAVU (25) MKAZI WA NTINDI – NAKONDE ZAMBIA 3. GWAKISA MWAMBOMA (30) MKAZI WA MTAA WA MWAKA TUNDUMA NA 4. PRINCE CHISALA (27) MKAZI WA NTINDI –NAKONDE-ZAMBIA WAKIWA NA BHANGI KETE 575.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI MAALUM ILIYFANYIKA MNAMO TAREHE 25.08.2015 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO MPAKANI KATI YA TANZANIA MTAA WA TUKUYU [BLACK] NA NAKONDE –ZAMBIA. 

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

BENKI YA DUNIA YAIKOPESHA TANZANIA BIL 422.8

$
0
0
Mwakilishi Benki Dunia, Country Director (katikati) akisaini mkopo wa fedha kwa wizara ya Afra. Kulia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Servacius Likwelile
Mwakilishi Benki Dunia, Country Director (katikati) akisaini mkopo wa fedha kwa wizara ya Afra. Kulia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Servacius Likwelile

TANZANIA imesaini mkopo wa Sh. 422.8 Bil kutoka Benki Kuu ya Dunia ili kuimarisha huduma ya afya nchini. 
Akisaini mkopo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile amesema, mkopo huo unalenga kuimarisha huduma za awali za afya nchi inayolenga wajawazito, vichanga na watoto.

Likwelile amesema, huduma hiyo itahusisha zaidi katika usimamizi wa uratibu wa fedha kwa wagonjwa ili kuwa na mwitikio wa uwajibikaji, ufanisi na utawala.

Aidha mkopo huo utawezesha mipango iliyopangwa kuongeza uwajibikaji wa wafanyakazi wa idara ya afya, usambazaji wa uelewa kwa wafanyakazi wa huduma ya awali, hasa katika mikoa husika, kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu kwenye vifaa vya huduma ya awali, pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wajawazito, vichanga na watoto.
Hata hivyo, ameishukuru hiyo na wafanyakazi wake kwa kuwapa mkopo huo kwa wakati muafaka.

“Napenda kuwashukuru pia waliofanya bidii na kufanikisha makubaliano haya leo,” amesema Likwelile na kuongeza;
“Serikali imedhamiria mageuzi endelevu katika sekta ya afya ili kufikia malengo yaliyowekwa chini ya sekta ya afya Mpango Mkakati IV ikiwa ni pamoja matokeo makubwa sasa (BRN).

“Zaidi, pia tunataka kuwahakikishia juu ya ahadi yetu ya kuendelea katika kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Benki ya Dunia”.

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Country Director amesema mpango huo utasaidia Tanzania katika kuimarisha huduma zake za awali za afya. Director amesema zaidi ya miaka 10 Tanzania imefanikisha kupunguza vifo vya watoto na kuzidi lengo la maendeleo ya milenia kuhusu vifo vya watoto.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Bernald Konga amesema mkopo huo utachangia kutekeleza mambo mbalimbali ya afya hivyo zitatumika vizuri katika kuhudumia wajawazito, vichanga na watoto.

Amesema kuwa, maisha ya Watanzania yataimarika zaidi kutokana na sekta ya afya kuzuia vifo vilivyokuwa vikitokea mara kwa mara.




Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano na serikali. 

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LAPIGA MARUFUKU WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA KU FANYA VITENDO VINAVYOHATARISHA USALAMA.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
25/08/2015
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limegundua kwamba kuna baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa ambao wameanziasha mtindo wa kutembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kama vile vituo vya daladala, masoko mbalimbali, n.k. kwa madai ya kuyatembelea makundi ya watu wenye kipato cha hali ya chini.

Kutokana na uzoefu uliojitokeza katika ziara hizo zisizo rasmi ni kwamba imeonekana mikusanyiko mikubwa isiyotegemewa katika hali ambayo inaashiria uvunjivu wa amani. Wakati wa ziara za aina hiyo yamejitokeza makundi ya watu mbalimbali kama vile waendesha bodaboda, machinga na makundi mengine katika namna ambayo imeleta taharuki pamoja na usumbufu unaotokana na makele, msongamano au shughuli za usafiri kusimama kabisa.

Tarehe 25/08/2015 majira ya saa 12:00 mchana katika makutano ya mtaa wa SWAHILI na UHURU Kamnda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi LUCAS MKONDYA alilazimika kukutana ana kwa ana na mgombea urais wa CHADEMA Mhe. EDWARD LOWASA ili kumpa tahadhali hiyo ya kiusalama. Mgombea huyo alikuwa amezungukwa na wapanda pikipiki wasiopungua arobaini pamoja na magari mengi katika hali ambayo ilileta msongamano katika eneo hilo ya barabara za Swahili na Uhuru. Msongamano huo ulileta athari na malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine wa barabara jijini Dar es Salaam.
Aidha, imegundulika kwamba mgombea huyo alianzia kuzunguka maeneo mbalimbali ya Temeke kuanzia tarehe 24/08/2015 akitumia vyombo mbalibali vya usafiri ikiwemo mabasi ya abiria. 

Ni lazima ieleweke wazi kwamba moja ya kazi za Jeshi la Polisi ni kuthibiti makundi makubwa ya watu katika namna ambayo kiongozi yeyote wa aina ya wagombea urais anatakiwa kulindwa katika kipindi chote cha kampeni hadi siku ya uchaguzi n.k. Ni vyema wagombea mbalimbali hususani wagombea urais waonyeshe ushirikiano wa hali ya juu kwa Jeshi la Polisi ili kuzuia madhara ya aina yoyote dhidi yao. Hivyo, ni muhimu wakajihadhari kwenda katika makundi yasiyo rasmi kwa sababu za kiusalama.

Tunawashauri viongozi wa vyama pamoja na wagombea wao wafuate ratiba za kampeni za mgombea urais/mgombea mwenza kwa vyama vya siasa kama ilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuondoa hisia za kufanyika kampeni nje ya ratiba.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM



Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images