Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Diamond Motors rolls out the new Fuso FZ in ‘Ndiyo Fuso niFaida’ campaign

$
0
0
               
          Transport sector is an important component of the economy and a common tool used for development because of its intensive use of infrastructures. This is even more so in Tanzania’s economy where economic opportunities are increasingly related to the mobility of people, goods and service. It is with this factors in mind that Diamond Motors (Hansa Group) has introduceda NewFuso heavy-duty truck range of Fuso FZ which offers more benefits in terms of efficiency, operation costs and suitable for the nature of Tanzania’s infrastructures.

Diamond Motors Limitedhas been playing a major role in the transportation sector since 1980 in Tanzania by the distribution of Mitsubishi Fuso trucks and Bus Corporation.A new range of Fuso FJ and Fuso FZ encompasses exceptional functionality, durability, and comfort, giving customers an entirely new breed of trucking technology.  Fuso heavy- duty trucks delivers lower operating costs, making them the best choice for smart businesses. Trucks ideal for long distance and heavy loads with high torque engines optimized for power andmaintain being economy to provide profitable transportation facility.

The ongoing campaign of “Ndiyo Fuso niFaida” in various regions in Tanzaniaaims at bringing awareness to stakeholders of different sectors of the economy on the benefits by the use of new Fuso truck which are of latest technology, in terms of capability, reliability, economy and long distance travelling as well as characteristics from the in-built specifications which are beneficial to the user. The 170kW/810Nm engine is more fuel efficient, for better mileage and lower costs and other long-haul applications.

Diamond Motors Limited has been servicing this sector through Mitsubishi Canters and Light trucks over the past few decades. Backed with after sales and spares support, the product portfolio is amply suited and tailored to meet the requirement and demands for this sector, and become the total transport solution provider in Tanzania.


.With Fuso Value Parts, you are assured of authentic parts of the highest precision manufacturing guaranteed by Mitsubishi Fuso, without having to pay a premium. For excellent value at approachable prices, Diamond Motors Limited has made the choice easy. The availability of the required genuine parts determines the downtime of your vehicle. Turn to your Mitsubishi Fuso dealer for quick supply of the genuine parts needed to keep your truck running, reliable consultation and the quality of the service network determine how well and how long your truck performs while a trust to our trained technicians ensures high quality.

ABOUT DIAMOND MOTORS LIMITED (Hansa Group)
Diamond Motors Limited has been the exclusive distributor of Fuso trucks in the country for over 30 years. DML has set the bar in the automotive industry, working with some of the world’s best vehicle brands. Its strong partnerships with global leaders such as Mitsubishi passenger vehicles from Japan, Yokohama tires from Japan, MTU and ZF from Germany have proven to be popular, with a diverse range of customers from all across the island.

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MIAKA MIAMOJA YA SKAUTI NCHINI UGANDA

$
0
0
Rais wa Uganda Yoweri Museni akiongea na Waziri mkuu Mizengo Pinda katika sherehe ya Skauti kwakutimiza miaka miamoja nchini Uganda kulia  Waziri  wa Jinsia kazi namaendeleo ya Jamii Hajati Rukia Isanga Nakadama Waziri mkuu alimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete  Picha na Chris Mfinanga.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa anateta jambo na Makamu wa Raisi wa Sudani Kusini H.E James Wani Igga ambaye aliwakilisha nchi yake katika sherehe ya Skauti kutimiza miaka miamoja nchini Uganda kulia kwa waziri mkuu ni Naibu Mkuu wa Itafaki Bw. James Bwana .

Picha na Chris Mfinanga.

Tamasha la muziki la sauti za busara Zanzibar 2016 halitokuwepo

$
0
0
Kutokana na uhaba wa fedha, Busara Promotions inasikitika kutangaza kuwa tamasha la Sauti za Busara mwaka 2016 halitakuwepo, hii itakuwa ni mara ya kwanza ndani ya miaka kumi na tatu Zanzibar kulikosa Tamasha la kimataifa la Sauti za Busara lifanyikalo kila wiki ya pili ya mwezi Februari.

Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions, amesema leo "Uamuzi huu haukuchukuliwa kwa wepesi”. Kawaida huwa tunatangaza tarehe za tamasha mwaka mmoja kabla. Lakini baada ya kufanya tamasha lililopita kwa mafanikio, tumekuwa katika hali ya ukosefu wa fedha kwa toleo lijalo la 2016. 
 
Tulijiwekea  malengo ya kukusanya dola za kimarekani  200,000 kabla ya Julai, wakati tulipokuwa na matumaini ya kutangaza tarehe za Sauti za Busara 2016. Baada ya mikutano mingi na wadau, tulisogeza muda wetu wa kutafuta fedha hadi usiku wa Agosti 19. Kiasi ambacho tuna uhakika wa kukipata kuandaa tamasha lijayo kwa sasa kinasimamia kwenye dola za kimarekani 42,000, hivyo basi bado tuna safari ndefu mbele yetu.
 
Kawaida wakati kama huu, tunakuwa tumeshafika mbali kwenye makubaliano ya mikataba mbalimbali kama ya kukodi ukumbi, ukodishaji wa vifaa, wasanii na mameneja, tunaanza kupanga ratiba, maandalizi ya usafiri na malazi kwa wasanii mapema iwezekanavyo. Shinikizo zaidi, tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa watu mbalimbali duniani kote wakitaka kujua tarehe za tamasha ili waweze kufanya mipango yao ya safari. Mauzo ya tiketi za Sauti za Busara haijawahi kuwa tatizo, lakini hii inasaidia kulipa 30% ya gharama za tamasha ".

Yusuf ameendelea , "Matamasha yanahamasisha vijana kupenda utamaduni wao, hutoa fursa kwa wasanii na wataalamu wa muziki kukutana na kujifunza , yanashawishi uhai wa tamaduni, pia yanatoa nafasi za ajira kwa watu wa ndani na kutoa mifano ya utalii ambayo inathamini na kuheshimu utamaduni wa ndani. Hata hivyo, tangu mwaka  2004 hatuna msaada wowote wa kifedha kutoka serikali ya  Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na jitihada nyingi, msaada kutoka kwa wahisani, balozi na wafanyabiashara unazidi kupungua siku hadi siku. Busara Promotions ni shirika lisilo la kiserikali; tamasha haliko kibiashara. 
 
Wengine walipendekeza tujaribu kuomba pesa kupitia mitandao. Hata hivyo, kwa kweli ili kuwa endelevu zaidi, kipaumbele chetu kabla ya toleo la 2017  kitakuwa ni kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu na wadhamini na wafadhili ambao wanakubaliana na  mtazamo wetu. Mtu yeyote anaesoma ujumbe huu na ana nia ya kusaidia kuiweka Sauti za Busara hai, kukuza ajira nchini, wakati tunaendelea kuung’arisha muziki wetu wenye utajiri wa mila na kukuza utalii wa kiutamaduni Zanzibar na Tanzania, tafadhali awasiliana nami kupitia Busara Promotions."

Katika kipindi cha miaka kumi na mbili iliyopita, Busara imewavutia maelfu ya wageni kutoka kila pembe ya dunia  kuja Zanzibar , wakati ambayo hakuwa msimu wa wageni wengi . Ndege zote zinazokuja Zanzibar kipindi cha tamasha zinajaa, hoteli na migahawa vinajaa, maduka yaliyopo maeneo ya Mji Mkongwe yanapata wateja wengi zaidi. 
 
Hata makadirio yanaonyesha tangu mwaka 2004 tamasha limekiingizia kisiwa mapato ya kiasi dola za kimarekami milioni 70. Wakati huo huo, Shirika la utangazaji la BBC limeiweka Sauti za Busara kama moja ya "matamasha ya muziki bora na ya kuheshimika  zaidi Afrika ". Pia limeingizwa kwenye CNN "matamasha 7 ya muziki ya kiAfrika unayotakiwa kuyaona" na kileleni kwenye orodha ya AfroTourism ya "Matamasha bora ya Muziki  ”

Yusuf Mahmoud hatimaye alisema " Wakati mwingine ni muhimu kupiga hatua moja nyuma, kabla ya kusonga mbele. Bodi na uongozi wa Busara itafanya kazi kwa bidii zaidi miezi ijayo, ili kuhakikisha  kuanzia mwaka 2017 tamasha linarudi kuwa na nguvu zaid
i. Inawezekana itamaanisha kuhama  eneo, au kulifanya kila baada ya miaka miwili . Hakika vipaumbele vyetu vitakuwa kulifanya tamasha litoe nafasi zaidi kwa  wananchi  , wakati tunaelendea kuomba  kujenga ushirikiano wa muda mrefu , na sekta za umma na binafsi".

Wakati tamasha likiwa kwenye mapumziko, Busara Promotions itaendelea na shughuli zake za kawaida za kukuza muziki wa kiAfrika, kuimarisha uelewa wa watu na kuboresha sekta ya muziki. Kwa mwaka mzima, Busara itahakikisha wasanii wa Afrika Mashariki wanapata mialiko kwenye matamasha mengine ya  kimataifa na kuwezesha kujenga ujuzi kwa wasanii wa ndani na wafanyakazi wa tamasha, kwa njia ya kubadilishana na mafunzo ya uongozi wa  sanaa, masoko, habari na ujuzi wa kiufundi . Kazi hii , ambayo inadhaniniwa na Ubalozi wa Norway , Dar es Salaam , haitotetereshwa  na uamuzi wa kufuta Sauti za Busara 2016 .

MATUKIO MBALIMBALI YAENDELEA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 70 YA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwa pamoja na  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakichanganya saruji, kokoto na mchanga ili kupata zege kwa ajili ya kuweka Jiwe la  Msingi ikiwa ni uzinduzi wa kuanza kwa ujenzi wa vyoo 22 kwenye Shule ya Msingi Kiboriloni, Mkoani Kilimanjaro. Uzinduzi huo ni tukio mojawapo kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa  Ujenzi huo umedhaminiwa na UNDP. 
Bw. Alvaro akiweka jiwe la msingi  kuzindua kuanza kwa ujenzi wa  Vyoo hivyo
Balozi Mushy naye akiweka tofali katika msingi huo 
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem naye akimpatia fundi tofali la ujenzi wa vyoo hive
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza mbele) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,kwa pamoja wakimimina zege kwenye msingi wa Vyoo vinavyojengwa katika Shule ya Msingi ya Kiboriloni
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza katika uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 vinavyojengwa katika shule ya msingi ya Kiboriloni
Juu na Chini ni Balozi Mushy akizungumza na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 katika Shule hiyo
Wanafunzi wa Shule hiyo wakionekana kuwa na furaha na matumaini baada ya uzinduzi wa Vyoo hivyo vya Shule yao.
Sehemu ya Uongozi wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni
Wananchini na waalimu wa shule hiyo wakisikiliza kwa makini 
Dkt. Kanem akizungumza kwenye uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 vya shule ya Msingi Kiboriloni
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem (kulia) akifurahia jambo na Balozi Mushy (katikati), pamoja na Bw. Alvarp
Balozi Mushy akimtambulisha Bwa. Alvaro kwa waalimu wa shule ya msingi ya kiboriloni waliojipang kumpokea  
Balozi Celestine Mushy akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Alvaro
Bwa. Alvaro (wa nne kutoka kulia) na Balozi Celestine Mushy wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi na waalimu wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni.
Picha na Reginald Philip

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika sherehe ya kumuaga mara baada ya kumaliza uongozi wake katika Serikali ya awamu ya nne.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Tom Nyanduga katika Sherehe iliyoandaliwa na Tume ya kumuaga mara baada ya kumaliza Uongozi wake.
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Tom Nyanduga akizungumza katika sherehe ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza  utawala  wake katika serikali ya  awamu ya nne ,ndani ya  ofisi za tume hiyo.
 Baadhi ya viongozi wa Serikali pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Baadhi ya wafanyakazi  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Sherehe ya kumuaga baada ya kumaliza uongozi wake katika serikali ya awamu ya nne.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora mara baada ya kuwasili katika ofisi yao.

NEC YATOA RATIBA YA KUREJESHA FORM NA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS.

AIRTEL YAPATA WASHINDI WATANO WA PROMOSHENI YA JIONGEZE NA MSHIKO

$
0
0
 Afisa huduma za ziada wa Airtel bwana Fabian Felician akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya tano ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Manyara na Bukoba walipatikana (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid (kushoto) droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam.
Afisa huduma za ziada wa Airtel, bwana Fabian Felician (kulia) akimkabidhi mshindi wa droo ya nne ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”, Daudi Ali Kingonji, Mkazi wa Dar es Salaam, shilingi million moja, kwenye makao makuu ya Airtel, Dares salaam.

JE NI WAJIBU MWANAMKE KUMTUNZA MWANAUME KISHERIA?.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.
Kisheria  ndoa inapokuwa  imefungwa   kuna  haki  za  msingi  ambazo  huibuka.  Hizi  huitwa  haki  za  moja  kwa  moja  ( automatic  right). Huitwa  haki  za  moja  kwa  moja   kwakuwa   hazina  uhiari  katika  kutekelezwa  kwake.  Kuwapo  kwa  ndoa  ndio  kuwapo  kwake  na  hivyo  haihitaji  mtu  kuziomba. Kimsingi  haki  hizi  zipo  nyingi  ambapo  tutaona  baadhi  yake hapa   huku  makala  yakijikita  katika   haki  moja ya  matunzo  kwa  wanandoa.


1.BAADHI  YA  HAKI  ZINAZOIBULIWA  NA  NDOA.

( a ) Haki  ya  tendo  la  ndoa.  Hii  ni  haki  ya  lazima  kwa  wanandoa  na  kutokuwepo  kwake  kunaweza  kubatilisha  ndoa iwapo  mmoja  wa  wanandoa ataamua  kufanya  hivyo. Ni  haki  ambayo  huchukuliwa  kama  ndio ndoa yenyewe  na  hivyo  kuifanya  kuwa  na  umuhimu wa pekee.


( b ) Haki  ya  kutumia  jina la mume. Hii   ni haki  aliyonayo  mwanamke  ambapo  anaruhusiwa kutumia  jina  la  mme  wake  badala  ya  lile  la  baba  yake. Hata  hivyo  sheria  haikueleza  iwapo  mwanaume  naye  anaweza  kutumia  jina  la  mke  wake,  au  la  baba  wa  mke  wake, au la  ukoo  wa  mke  wake.  Pia si  tu  mwanamke  ameruhusiwa  kutumia  jina  la  mme  wake  isipokuwa  hata  lile  la  ukoo  wa  mme  wake.


( c ) Haki  ya  kutumia  mali  za  familia  kwa  pamoja. Haijalishi  mali  hizo  ni  mwanamke  mwanaume  ataruhusiwa  kutumia na  haijalishi  mali  hizo ni  za  mwanaume  mwanamke  ataruhusiwa  kutumia. Isipokuwa  yawe  matumizi  ambayo  hayako  kinyume  cha  sheria.


( d ) Haki  ya  kutunza  watoto/mtoto kama  yupo. Ikiwa  familia  imebarikiwa  na  mtoto/watoto basi  wanadoa  kwa  pamoja  wanawajibika  kuwatunza  watoto  hao  kila  mtu kwa  nafasi  yake. Hii  ina  maana mwanamke  anawajibika  zaidi  kuwa  mwangalizi  mkuu wa  kila  siku  wa  watoto  huku  mwanaume  akilazimika  kutoa  matumizi   hasa  yale ya  kifedha.


( e ) Haki  ya  kugawana  mali  pindi  ndoa  inapovunjika. Hii  huhusisha  mali    zote  ambazo  huitwa  mali  za  machumo  ya  pamoja  baina  ya  mwanamke na  mwanaume.


( f ) Pia  ipo  haki  ya  kurithi  na  kurithiana  iwapo  kuna  kifo  cha  mmoja  wa  wanandoa. Mwanamke  aweza  kurithi  mali  za  mme  wake  halikadhalika  mwanaume. Hii  huenda  mpaka  kwa  watoto  waliopatikana  katika  ndoa  ambapo   huweza  kurithi  mali  za  baba, mama  au  wote  wawili.


( g ) Haki  ya  matunzo  baina  ya  wanandoa.  Hii  ndiyo  itakayojadiliwa  japo  kwa  ufupi .


2.  MWANAUME  KUMTUNZA  MWANAMKE.

Sura  ya  29  ya  Sheria  ya  ndoa  kifungu  cha  63 ( a )  kinasema  kuwa  ni  wajibu  wa  kila  mwanaume  kumtumza  mke/wake zake  kutokana  na  njia  za  kipato  chake.  Neno  njia  za kipato  chake  maana  yake  ni  namna  anavyopata   kipato  ndivyo  atavyotakiwa  kutoa  matunzo  kwa  mwanamke.  Haiwi  kuwa  mwanaume  anapata  kipato  kidogo  halafu  alazimishwe  kutoa   matunzo  makubwa.  Ushahidi  wa  namna  anavyopata  kipato  chake  ndio  utakaoainisha  kiasi  cha  matunzo  kwa  mke  wake.


Aidha kwa  mujibu  wa  kifungu  hicho  matunzo  yanayoongelewa  hapa  yanahusisha   makazi,  mavazi, chakula  na  huduma  nyingine  kama  za afya  n.k. Kitu  cha  msingi  hapa  ni  kuwa  ni  lazima  kwa  mwanaume  kutoa  vitu  hivi  kwa mke  wake.


3.  MWANAMKE  KUMTUNZA  MWANAUME.

Kifungu  hichohicho  cha  63 ( b ) kinasema  kuwa  utakuwa  ni  wajibu  wa  kila  mwanamke  lakini  mwenye  uwezo  kutoa  matunzo  kwa   mume  wake  iwapo  mume  huyo  ana  ulemavu/hajiwezi  jumla  au  sehemu  ya  mwili  wake, kiakili  au  kimwili  na  hivyo  kutokuwa  na  uwezo  wa  kuingiza  kipato  kutokana  na  hali  hiyo.


Kwa  kifungu  hiki  tunaona  kuwa mwanamke  anao  wajibu  wa  kumtunza  mume  wake   lakini  iwapo  tu kwanza  ana  uwezo, pili mwanaume  awe  na  tatizo  ambalo  kwalo  hawezi  kuingiza  kipato  na  tatizo  hilo  liwe la  kimwili  au  kiakili. Kumbe  basi  tunaona  kuwa mwanaume  kumhudumia  mwanamke ni  lazima  hata  mwanamke  awe  mzima  wa  afya  huku   hafanyi  kazi  wakati  mwanamke  kumhudumia  mwanaume  ni  pale  tu  atapokuwa  ana  tatizo  ambalo  linamfanya  asiweze  kufanya  kazi. Lakini  pia  sheria  imesema  mwanamke  atatoa  huduma  iwapo  ana  uwezo wakati  neno  iwapo  ana  uwezo  haikuliwekwa  kwa  mwanaume.Kwa mwanaume  kutoa  ni  kutoa  tu.


MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

TCRA , MIAKA 10 YA UKUWAJI WA SEKTA YA MAWASILIANO, TANZANIA

$
0
0


TANZANIA na miaka 10 ya ukuaji wa kasi na kuimarika kwa sekta ya Mawasiliano


Na Semu Mwakyanjala, TCRA


KUMEKUWEPO na ukuaji  mkubwa na mpana wa sekta ya mawasiliano nchini Tanzania kwa upande wa miundombinu na huduma ambavo kwa pamoja vimeleta faida kwa Watanzania  katika miaka ya hivi karibuni. Sekta hii inaongozwa na Sera ya Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) ya mwaka 2003.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kwa kifupi TCRA, ni chombo huru cha Serikali kinachohusika na kusimamia sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini Tanzania na ina majukumu ya kutoa   leseni kwa makampuni ya mawasiliano, ikiwemo ya huduma za simu, utangazaji, intaneti na posta na usafirishaji wa vifurushi.


TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Na 12 ya 2003 ambayo iliziunganisha zilizokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania na Tume ya Mawasiliano Tanzania. Tangu ilipoanza kutekeleza majukumu yake 1 Novemba 2003, TCRA iomekuwa ikiwashirikisha wadau wake muhimu kupitia mashauriano kwenye masuala mbalimbali.


Ukuaji imara na wa kasi wasekta ya mawasiliano nchini ni sehemu ya matunda yanayoonekana na Serikali ya  Awamu ya Nne ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.


Sera nzuri za serikali na kufunguliwa kwa soko huria zimewezesha kuongezeka kwa wawekezaji na hivyo kuwapa watumiaji fursa ya kuchagua huduma bora wanayohitaji kwa gharama wanazomudu.


Kuanzishwa kwa mfumo wa leseni za muingiliano yaani (Convergence Licencing Framework) ambao ulianzishwa mwaka 2005 kutokana na kuendelea kukua kwa kasi kwa teknolojia kulikopelekea mwingiliano wa Teknolojia (Technological Convergence) kumechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa sekta ya mawasiliano.


Mfumo huu una aina nne za leseni ambazo ni:

—  Leseni ya Mitandao (Network Facility):

          Inajumuisha miundombinu ya setelaiti, mitandao inayotumia waya aina ya optic fibre, uwekaji wa nyaya na njia za mawasiliano, vifaa vya mawasiliano kutumia redio, milingoti ya mawasiliano ya simu za mkononi, minara na vifaa vya kurushia matangazo ya vyombo vya utangazaji;

—  Leseni ya Mtandao wa Simu (Network Services):

          Hii ni leseni inayoruhusu kutoa huduma za simu yaani sauti, picha na takwimu (voice, data, etc);


—  Leseni ya Huduma (Application Services):

          Hii ni leseni inayoruhusu mmiliki kutoa huduma kama vile internet, kupiga simu kupitia internet, takwimu kwa ajili ya biashara, na huduma za kutuma taarifa fupi;

—  Leseni ya Huduma ya Maudhui ( Content Services)


          Hii ni leseni inayoruhusu mmiliki kutoa huduma za utangazaji  wa redio na televisheni na taarifa kupitia mitandao ( online publishing) na taarifa za habari.


Leseni chini ya mfumo wa  CLF zinatolewa kwa ajili ya kutoa huduma katika ngazi nne- ngazio ya kimataifa, ya kitaifa, ya mkoa na wilaya.


Maendeleo tunayoshuhudia kwenye sekta ya mawasiliano nchini ni sehemu ya  matokeo ya mpango mkakati wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa 2006/7 hadi 2010/11 na 2011/12 hadi 2015/16 ambao ulibuniwa na kutekelezwa Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi na kuwezeshwa na kuchangiwa na juhudi  za watumishi wa Mamlaka ambao wanafanya kazi kwa bidii na weledi.


TCRA inatekeleza mpango mkakati  sambamba na dira,dhima au dhamira na lengo kuu la Mamlaka.

Dira ya TCRA ni  “Kuwa Mdhibiti mwenye hadhi ya kimataifa, kwa kuweka na kusimamia usawa katika haki na majukumu ya watoa huduma za mawasiliano na kuendeleza huduma zinazojali mazingira, na uwezo wa kiuchumi wa watumiaji.”


Dhima au dhamira ya Mamlaka ni   “Kuwa na mfumo mahsusi wa usimamizi, kuboresha utendaji wa watoa huduma, na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kutoa mchango wetu kwa uchumi jamii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”

Lengo kuu ni”  Kuendeleza ustawi wa Watanzania kupitia mfumo wa usimamizi wenye ufanisi na ambao unawezesha kupatikana kwa huduma za mawasiliano kwa wote”.


Soko la TEHAMA  limekuwa kwa idadi ya watumiaji wa huduma hizo, kwa aina mbalimbali za huduma hizo na kwa kuongezeka kwa eneo ambamo huduma mbalimbali zinapatikana; ingawaje idadi ya watumiaji wa simu za mezani imepungua. Kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 sasa ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005.  Watumiaji wa intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka 2008. Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii.


Sekta ya mawasiliano ni mojawapo ya sekta zinazoajiri watu wengi zaidi. Matumizi a simu za mkononi yamebadilisha mfumo wa maisha ya wananchi hapa nchini. Simu za mkononi siio tu kifaa cha mawasiliano 9 kwa kuongea na kutuma ujumbe mfupi au meseji0 lakini pia ni chombo cha kuimarisha watumiaji kiuchumi. Simu za mkononi zina matumizi ya aina mbalimbali ya kijitali kama vile huduma za fedha ambazo zinawawezesha watu kutuma na kupokea pesa. Watumaji wa huduma za fedha kuopitia simu za mkononi hivi sasa wanaweza kununua umeme, kulipia maji na kulipia huduma nyingine bila ya kuzalimika kwenda nje ya nyumba zao.


Watumiaji wanaweza kutoa pesa kwenye mashine za benki (ATM) na watu wengine wamejikomboa kutokana na adha ya kukaa foleni ndefu na kupoteza  muda ambao wangeutumia chini ya mfumo wa zamani wa kibenki.

Wtumiaji wa huduma za benki kupitia mtandao wanaweza kuona miamala yao ikiwa ni pamoja na  mishahara yao, wanaweza kuhamisha pesa kutoka akaunti ya benki kwenda pesa mtandao.


TCRA imefanikisha hili kwa kutopa namba fupi maalum kwa ajili ya miamala hii. Namba hizo ni ,*150*00#  (M-pesa ya Vodacom), *150*01# (tigopesa ya Tigo), *150*02#  (ezy-pesa ya Zantel),  *150*60#  (Airtel money ya airtel) na za mabenki kama vile *150*03#  (CRDB simbanking), *150*20# (Barclays), *150*55# (NBC), *150*66# (NMB) na nyingine nyingi.


Kipindi cha miaka 10 iliyopita kinaweza kuelezewa kuwa ni  Muongo wa Mapinduzi katika sekta ya Mawasiliano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mamlaka ya Mawasiliano imekuwa ikitekeleza kwa ufanisi Usimamizi wa Masafa ya Mawasiliano. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekuwa ikutumia kwa ufanisi mitambo minne ya kisasa iliyonunuliwa mwaka 2006/2008 ili kujiimarsiha na kujiongezea uwezo wake wa kupanga na kuthibiti matumizi ya masafa nchini. Hivi sasa kila ofisi ya Kanda ya Mamlaka ina mtambo (mobile frequency monitoring station) unaotumika kusimamia masafa katika kanda inayohusika. Kuwepo kwa mitambo hiyo kumepunguza muda wa kuchunguza na kumpangia muombaji masafa na kutambua kwa urahisi watumiaji haramu wa masafa na kuelewa mahali walipo; na kuzuia muingiliano (harmful interference) baina ya watumiaji wa masafa hivyo kuongeza ubora wa mawasiliano nchini. 
         

Aidha, Mitambo iliyoko Dar-Es-Salaam imeboreshwa kwa kuwekwa “software” mpya na hivyo kuipa mitambo hiyo uwezo mkubwa na na ubora zaidi wa kusimamia masafa.
Baadhi ya mitambo ya kusimamia masafa iliyonunuliwa na TCRA


Mafanikio mengine muhimu kwenye sekta ya mawasiliano nchini ambayo msimamizi wake ni TCRA ni  ufungaji wa mtambo wa kufuatilia mawasiliano ya simu, yaani  Telecommunications Traffic Monitoring  System, kwa kifupi TTMS.


 Mtambo huu, ambao ulizinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete February 2014 una faida kubwa tano; ambazo ni kuwa na uwezo wa kujua mapato yanayopatikana kwenye simu za kimataifa;kuongeza mapato kwa sekta ya mawasiliano kutokana na simu kutoka nje ya nchi ili kuweka uwiano ulio sawa kati ya makampuni ya Tanzania na yale ya nje ya nchi. Mtambo huu utawezesha kuwekwa kwa uwiano sawa katika kutoza gharama za simu zinazoingia kwenye nchi husika kutoka nje. Hivi sasa nchi za Afrika zina viwango vya chini vya gharama za kuingia simu kutoka nje.

 Hii imefanya makampuni ya hapa nchini kupata viwango vidogo vya mapato ukilinganisha na makampuni katika nchi nyingine. Kutokana na hili makampuni ya  nchini na serikali wamekuwa wakipata mapato kidogo tofauti na ambayo wangepata kama kungekuwa na usawa wa bei kati ya kampuni za Tanzania na za nchi za nje.


Tofauti ya gharama hizo inaingia mikononi mwa wajanja wanaopitisha simu kinyemela.


Kwa kurekebisha kasoro hii wadau wa sekta nzima ya mawasiliano, yaani makampuni ya simu na Serikali watafaidika na huu mgao mpya wa mapato. Makampuni ya simu yataona ongezeko la mapato kutoka kwenye simu za nje na serikali itanufaika na mapato ya moja kwa moja pamoja na kodi za “corporate tax” ambazo zitaongezeka kwa kuwa makampuni ya simu yamepata mapato zaidi. Mtambo utaiwezesha serikali kupata shilingi bilioni 20 kwa mwaka  kutokana na  simu za kimataifa.


Faida nyingine ya mtambo hu ni kuweza kuzuia matumizi ya simu bila leseni kwa ajili ya kuunganisha simu za kimataifa na hivyo kuikosesa Serikali na Makampuni ya simu mapato halali. Mtambo pia  utaongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya mawasiliano.

Mtambo utaiwezesha Serikali kupitia TCRA kusimamia sekta ya Mawasiliano vizuri.


 Uthibiti na ukomeshaji wa  upigaji na upokeaji wa simu kutumia mitambo ya mafichoni utaongeza  ubora wa mawasiliano ya simu hivyo kuwapa watumiaji huduma bora.


Mtambo pia  unaiwezesha Serikali kuwabaini wale wote wanaotumia mitandao ya kimataifa bila leseni hivyo kuikosesha Serikali mapato yake.

Aidha mtambo utawezesha Serikali kujua muda unaotumika kupiga simu nje ya nchi ya muda wa kupokea simu kutoka nje ya nchi. Kabla ya kufungwa kwa mtambo huu, TCRA ilikuwa inategemea takwimu kutoka kwa makampuni ya simu za mkononi.


Hata hivyo mtambo huu hausikilizi mazungumzo ya mtu yeyote. Mtambo huu unafuatilia mawasiliano ya simu ili viwango kamili viweze kulipwa na kukusanywa na Serikali iweze kupata mapato ya kuweza kuwahudumia vyema Watanzania.


TCRA pia inasimamia masuala ya usalama wa mtandao wa mawasiliano kupitia intaneti.  Mamlaka imeanzisha kituo cha usalama wa mtandao, yaani Computer Emergency Response Team (TZ-CERT). Kituo kinashirikiana na wataaalamu wa kitaifa na kimataifa kuhusiana na masuala ya usalama wa mtandao wa intaneti. Aidha, Mamlaka inafanya kazi kwa karibu na vyonmbo vya usalama wa wananchi, hususan polisi katika kufuatilia matukio ya uhalifu kupitia mitandao.


Kimataifa, Tanzania mwanachama wa Shirika la Mawasiliano Ulimwenguni, yaani  Telecommunication Union (ITU), lenye makao yake makuu Geneva, Uswisi. Vilevile kituo kinashirikiana na  chombo cha kupambana na matukio ya uhalifu wa mtandao - Multilateral Partnership Against Cyber Threats (IMPACT) cha Malaysia.

Huduma za intaneti zimeenea kwa kasi na kuwezesha watumiaji kuwa na ufanisi katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii.


Kusimikwa kwa nyaya za  mawasiliaano ya kasi ambazo zimewekwa chini ya bahari ya Hindi na kuwa na vituo Dar Es Salaam kumeiwezesha  Tanzania kuunganishwa na nchi nane majirani. Nchi hizo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, DRC  Congo, Msumbiji na Zambia.

Nyaya hizo zimewekwa na makampuini ya SEACOM, EASSy na TEAMS na zimewezesha kuwepo kwa mawasiliano ya kuaminika,  ya kasi, yenye ufanisi  na ya  gharama nafuu.


Watumiaji wa intaneti Tanzania  wameongezeka kutoka 1.6 million mwaka 2005 hadi milioni 12  ilipofika Disemba 2014.

Matumizi  ya intaneti yanafanikisha shughuli nyingi.

Mkongo wa taifa wa mawasiliano ni kama uti wa mgongo ambao utaiwezesha Tanzania kuimarisha mawasiliano na sehemu nyingine duniani.

 Mkongo huu utafanikisha utoaji wa huduma kama vuile afya mtandao, serikali mtandao, kilimo mtandao na biashara mtandao.


Optic Fibre facility


Sekta ya Utangazaji Tanzania nayo imekuwa kwa kasi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Idadi ya vituo vya televisheni  imeongezeka hadi kufikia 27. Ikumbukwe kwamba wakati Tanzania Bara inapata uhuru 1961 hapakuwa na kituo cha televisheni. Vituo vya redio vimeongezeka kutokakimoja mwaka 1961 hadi 97.


Tanznaia imekuwa nchi ya kwanza eneo la mashariki, kati na kusini mwa Afrika kuhamia kwenye mfumo wa tekinolojia wa dijitali. Vilevile imekuwa ni mojawapo ya nchi chache za Afrika ambazo zimehamia mfumo wa utangazaji wa dijitali.


Kwa kuhamia dijitali, Tanzania imeweza kufikia malengo ya yaliyokubaliwa nanchi zote duniani kuhamia mfumo huo ifikapo 17 Juni 2015.

Utangazaji wa televisheni wa dijitali una faida zifuatazo:

  • Ina ubora wa sauti na picha.

  • Vifaa vya kuhifadhi habari /vipindi (CD/DVD,MD,DVD) ni vidogo na huhifadhi  habari nyingi zaidi kuliko  vya analogue.

  • Maktaba za kuhifadhi vipindi vya digital huchukua nafasi ndogo kulinganisha na vifaa vya analogue.

  • Utumiaji wa vifaa vya digital kwenye studio ni rahisi na hutumia   muda mchache kutayarisha kipindi.

  • Kuwepo kwa huduma za ziada kwenye mtandao (network)unaotumika kwa utangazaji.Huduma hizo ni kama usafirishaji wa takwimu (data) na Interneti.

  • Mitambo ya kurushia matangazo hutumia nishati  ndogo ya umeme.Mtambo wenye nguvu ya watts elfu moja wa analogue ni sawa na mtambo wenye watts mia  mbili na hamsini wa digital.

  • Uwezekano wa kupokea matangazo ya televisheni , radio na intaneti kwa kutumia runinga za mkononi, simu za mkononi, na runinga za magari za digital.


Sababu za kwenda dijitali ni:

·         Mitandao yote ya Mawasiliano, yaani Mitandao ya simu, na mitandao ya Takwimu(internet)inatumia teknolojia ya dijitali.Ni mtandao wa utangaziji tu ndio unatumia teknolojia ya analojia. Teknolojia ya analogue imepitwa na wakati.

·         Kutokana na mwingialiano wa teknojia (convergence of technologies)ya simu na utangazaji, mtandao wa utangazaji inabidi ubadilike.

·         Kufaidika na faida nyingi zinatokana na teknolojia hii ya digital.

·         Kwenda sambamba na makubaliano yaliyofikiwa na wanachama wa ITU – Geneva, 15/06/2006 kuwa mwaka 2015 ndiyo mwisho wa matumizi ya mfumo wa analogue kwa televisheni.
Kituo cha Mbeya FM Radio, ni kimojawapo cha vituo vya redio 115 nchini

Huduma za posta na usafikishaji wa vifurushi pia  zinasimamiwa na TCRA. Watoa huduma kwenye sekta hii wameopngezeka kutoka mtoa huduma mmoja wa posta mwaka 1961 hadi watoa huduma 50. Hawa wanatoa huduma kwenye vipengele vya soko la kimataifa, Afrika Mashariki, kati ya miji na miji, na ndani ya mji.


Mpango wa Anuani Mpya za Makazi na Postikodi

(Postcode)  ni mpango ambao utabadilisha anuani za

Watanzania kutoka sanduku la barua na kwenda namba

ya nyumba na jina la mtaa anaoishi mwananchi. Pia

maeneo wanaoishi wananchi yatapewa namba

maalumu za utalaamu wa posta (postcodes) ambayo

yataonyeshwa katika ramani za makazi ili kurahisisha

kutambulika.


Mpango huo ulizinduliwa Arusha  18 Januari 2010 na aliyekuwa

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia ambaye sasa

ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza l

Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein. Awamu ya pili ya mpango ilpitekelezwa Dodoma Desemba 2010.


Changamoto kubwa ya mradi huu ilikuwa ni  ukoswefu wa mipango miji  na kuwepo kwa maeneo ya makazi yasiyopimwa.

 Aliyekuwa Makamu wa Rais, Dr Ali Mohamed Shein katika uzinduzi wa Mradi wa Anuani ya Makazi na Misimbo ya Posta ( Post-Code Project) jijini  Arusha 18 Januari, 2010. Mradi huu ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa. Wapili kulia, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Tekinolojia (mstaafu) Mh. Prof. Peter Msolwa.

Desemba 2013 TCRA ilitekeleza kwa mafanikio mradi huu kwenye eneo  kama vile  Keko, sehemu ambayo haijapimwa.

Utoaji wa majina ya mitaa na barabara umefanyika kwenye sehemu mbalimbali wilaya za  Temeke, Ilala na Kinondoni, mkoa wa Dar Es Salaam.


Uwekaji wa Majina ya Mitaa ni muhimu kwa ajili ya anuani za Makazi. Juu Waziri wa Mawasiliani Sayansi na Tekinolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akitmbelea uwekaji wa majina ya mitaa wilayani Temeke, Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Postamasta Mkuu, Deos Khamis Mndeme , Kulia ni kurugenzi wa Masuala ya Posta Bibi Rehema Makuburi  na anayetoa maelezo (aliyenyoosha mkono) ni Meneja wa Mradi huo Bwana Haruni Lemanya.




Mafanikio mengine muhimu kwa TCRA ni chini ya uonmgozi wa Awamu ya Nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ni  pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la ghorofa 14 la makao makuu ya Mamlaka, Mawasiliano Towers barabara ya Sam Nujoma  mjini Dar Es Salaam, hivyo kuwapatia watumishi wa Mamlaka sehemu muafaka ya kufanyia kazi na pia kuweza kupangisha ofisi kwa taasisi nyingine za serikali.

TCRA imefanikiwa kufikia viwango vya utendaji vya kimataifa na ilipewa hati ya ISO 9001:2008 na taasisi ya ACM ya Uingereza tarehe 30 Juni 2014. Hati hii ni kithibitisho cha ubora wa utoaji huduma na ufanisi wa kuhudumia wateja.



Mafanikio ya TCRA: Mkrugenzi Mkuu (mstaafu) wa TCRA Prof John Nkoma akipokea cheti cha Ubora wa Kimatafia ISO 9001: 2008 Certificate kutoka kwa Mkaguzi wa Kimataifa kutoka ISO, Ndugu  Andrew Rowe kwenye jingo la Mawasiliano Towers Jijini Dar Es Salaam. 



Ufunguzi wa ofisi ya Zanzibar ya Mamlaka ya Mawasilianop eneo la Chukwani Zanzibar na ofisi nyingine tano za kanda vimeiwezesha TCRA kuwa karibu zaidi na wadau katika maeneo yote ya Tanzania.

Ofisi nyingine   ya Kanda ya Kati ambayo iko Dodoma, barabara ya   Natron, eneo la Kisasa kwenye barabara kuu ya Dodoma – Dar Es Salaam the Dar Es Salaam Ofisi ya Kanda ya Ziwa kwenye jengo la NSSF, Barabara ya Kenyatta Mwanza, Kanda ya mashariki ambayo iko Mawasiliano Towers; Nyanda za Juu kusini kwenye jengo la Century Plaza, Mbeya na Kanda ya Kaskazini kwenye jengo la Summit, barabara ya Sokoine, Arusha. 

TUZO:  Kutokana na sera na mipango ya kuiendeleza sekta ya mawasiliano, Tanzania imeweza kupata tuzo mbalimbali na kuchaguliwa kuingia katika vyombo vya kimataifa vinavyoshughulika na maendeleo.

1.           Tanznaia ilichaguliwa kuingia kwentye Baraza la Utendaji la ITU ( ITYU Council kwenye mkutano wa kila baada ya miaka mine uliofanyika Busan Korea Novemba 2014. Hii ina maana kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zinasimamia masuala ya mawasiliano duniani.

2.           Mwaka 2006 na 2009 TCRA ilitunukiwa tuzo ya Msimamizi Bora wa Mawasiliano Afrika.

3.           Umoja wa wasimamizi wa mawasiliano Afrika Mashariki ( EACO ambacho ni kifupi cha East African Communication Organisation uliichagua Tanzania kuwa nchi inayosimamia vyema zaidi mawasiliano Afrika Mashariki (“Best Regulator Country in East Africa) kwenye mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika Nairobi, Kenya Juni 2013.

4.           Tarehe 1 Novemba 2013 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilituzwa cheti na Umoja wa Posta Duniani (UPU – Universal Postal Union) kwa kuwa na mfumo wa postikodi.

Sekta ya mawasiliano ni sekta mtambuka na ni chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mawasiliano ni mhimili mkubwa wa maendeleo ya taifa na matumizi sahihi ya huduma na bidhaa za mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya nchi. 



SIMBACHAWENE AIASA KAMATI YA PAMOJA YA UENDESHAJI WA MGODI WA TANZANITEONE

$
0
0
WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameiasa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji wa Mgodi wa TanzaniteOne, “Joint Operating Committee”-JOC kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ili kuwanufaisha wadau wa Tanzanite katika uvunaji wa madini hayo, huku wakilinda maslahi ya mgodi huo kwa  Taifa.


 Simbachawene ametoa rai hiyo hivi karibuni wakati akizindua Kamati ya hiyo ya JOC, katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mirerani, katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

“Suala la kulinda maslahi mapana ya mgodi huu kwa Wabia na Taifa linawezekana, iwapo Wanakamati ya JOC mtafanya kazi kama timu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake ipasavyo. Hivyo basi ipokeeni kazi hii na kuitekeleza kwa ari, kasi na nguvu kubwa” Alisisitiza Mh. Simbachawene.


Ameigiza Kamati hiyo ya JOC kukamilisha majadiliano ya kuboresha Mkataba wa ubia uliokuwepo baina ya STAMICO na TML kwani mabadiliko ya Mkataba huo yataleta matokeo chanya katika udhibiti na uendelezaji wa mgodi na biashara nzima ya Tanzanite kwa manufaa ya wabia wote na Taifa pia.


“Baadhi  ya vipengele vinavyohitaji kuboreshwa ni pamoja na suala la kutangaza chimbuko la Tanzanite duniani kuwa ni Tanzania; kuimarisha mazingira ya mgodi kuwa kivutio cha utalii na mafunzo; kuchangia huduma za jamii zinazozunguka mgodi na kupanda miti katika maeneo ya mgodi ili kutunza mazingira” alifafanua Mh. Simbachawene.


Kamati hiyo ya JOC ina wajumbe 6 ambao  ni Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO; Bi. Asha Jumanne Ngoma, Prof. Peter Antony Kopoka kwa upande wa STAMICO na Bwana Faisal Juma Shahbhai, Bwana Hussein Omary Gong’a  na Bwana Halfan Mpenziye Hayeshi kwa upande wa Sky Associates Ltd. Kamati hii inaongozwa na Bwana Faisal Juma Shahbhai.


Katika uzinduzi wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Simbachawene pia aliwakumbusha wajumbe wa Kamati ya JOC kumsimamia kikamilifu mwendeshaji wa mgodi huo yaani TML ili aweze kutekeleza masharti ya mkataba wa ubia katika uzalishaji wa Tanzanite, kwa manufaa ya pande zote.


Aidha amewasisitiza wajumbe wa JOC kufanya maamuzi yenye tija katika uidhinishaji wa bajeti, kubuni mipango ya maendeleo ya mgodi; kuandaa sera za uendeshaji; kuunda kamati za ushauri kulingana na mahitaji na kuingia makubaliano ya pamoja na Kitengo cha Uangalizi na Usimamizi (Monitoring and Evaluation Unit), kuhusu mfumo wa uendeshaji mgodi, ili kuongeza uzalishaji wa tanzanite na  kukuza  soko la ndani.


Ameitaka Sky Associates kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania bila ubaguzi na kuzingatia misingi ya utawala bora  katika uendeshaji wa mgodi huo huku wakitoa maslahi bora kwa wafanyakazi wake.

Simbachawene amesema STAMICO kwa upande wake, haina budi kuwapatia Wafanyakazi wake waliopo Mirerani vitendea kazi stahili ili wasiwe na kisingizio cha kushindwa kutekeleza majukumu yao, na ameitaka Menejimenti ya Shirika hilo ipime utendaji kazi wa wafanyakazi wake mara kwa mara ili kukuza ufanisi.


Kuhusu suala la kuboresha mahusiano mazuri na Wachimbaji wadogo, Simbachawene amesema mahusiano kati ya TanzaniteOne na Wachimbaji Wadogo yaendelee kuimarishwa, na amekiri kuitambua Kamati Maalum iliyoundwa na Kamishna wa Madini, ili kuisaidia Serikali kuweka mfumo mzuri wa uchimbaji katika mgodi huo, jambo ambalo litaepusha ajali na kupunguza migogoro baina ya wadau.


“Nazitambua changamoto za wizi na utoroshaji wa madini ya Tanzanite ambazo ni matokeo ya wadau wasio waaminifu; nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Kifungu cha 6(4) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Kifungu hicho sasa kinampa Kamishna wa Madini mamlaka kamili ya kutaifisha na kupiga mnada madini yanayokamatwa yakimilikiwa kinyume cha Sheria. Hivyo, wote wenye tabia ya kufanya biashara ya madini kinyume cha Sheria wajiandae kupoteza madini yao” Aliongeza kwa msisitizo Mh. Simbachawene.


Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Deusdedith Magala amemshukuru Mh. Simbachawene kwa kuunda Kamati hiyo ya JOC na kuizindua rasmi, kwani itasaidia kulinda hisa za STAMICO, za Serikali na mali za mgodi, na pia kuuwezesha mgodi kufanya maamuzi makubwa na yenye tija.


Bwana Magala amesema tangu Juni 2013 STAMICO ilipoingia ubia wa umiliki wa mgodi wa TanzaniteOne na kampuni ya TML kwa uwiano wa 50:50 wa leseni ya uchimbaji wa Tanzanite, Bodi za Wakurugenzi za wabia hao wawili ndio zimekuwa zikifanya kazi kama Kamati ya JOC, jambo ambalo lilileta mzigo mkubwa wa kazi kwa bodi hizo.


Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kamati ya Ushirikiano ya Mgodi wa TanzaniteOne, Mh. Simbachawene na ujumbe wake pia walikagua shughuli za uchimbaji wa Tanzanite katika mgodi wa CT, zikiwemo uchorongaji, uchotaji na utoaji wa udongo na kujionea athari za kimazingira zilizosababishwa na wachimbaji wadogo kwenye kitalu C.


Hafla hiyo ya uzinduzi wa JOC ilihudhuriwa na mwakilishi wa Kamishna wa Madini Tanzania, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Wakurugenzi wa Kampuni ya Sky Associates Ltd na TML, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Kamishna Msaidizi wa Madini - Kanda ya Kaskazini, Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji (JOC) na Waandishi wa Habari.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (aliyevaa miwani) akipata maelezo kuhusu uchimbaji, ndani ya shimo la mgodi wa chini (underground mine) wa TanzaniteOne wakati alipotembelea mgodi, kabla ya kuzindua Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji mgodi huo (JOC).
 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (aliyekaa katikati) katika picha na Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji “Joint Operating Committee – (JOC) ” ya mgodi wa TanzaniteOne, baada ya kuizundua Kamati hiyo mgodini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa JOC Bwana Faisal Juma Shahbhai na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Duesdedith Magala. Wajumbe wengine waliokaa kutoka kushoto ni Asha Jumanne Ngoma, Prof. Peter Antony Kopoka (wa tano), Bwana Hussein Omary Gong’a (aliyesimama kushoto) na Bwana Halfan Mpenziye Hayeshi (aliyesimama kulia).
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (mwenye overall ya Kibluu) akipata   maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya JOC, Faisal Juma Shahbhai (aliyevaa kofia ngumu ya Kibluu) kuhusu uzalishaji wa Tanzanite katika mgodi wa TanzaniteOne. Anayemsikiliza  (mwenye overall ya Kijani) ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Duesdedith Magala.

UN YAPANDA MITI ZAIDI 2000 KUNUSURU MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
SIKILIZA kionjo cha hotuba ya Kiswahili ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez hapa chini.
  IMG_3361
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa pili kushoto) akiwasili kwenye kijiji cha Marua kata Kiruavunjo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili kupanda miti ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kupokelewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).(Pichazote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
*Sehemu ya Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa
Na Mwandishi wetu, Moshi
MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yameadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo kwa kupanda zaidi ya 2000 katika miteremko ya mlima Kilimanjaro.
Kazi ya kupanda miti ilifanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wao ikiwemo serikali ya Tanzania pamoja na wanakijiji.
Kazi ya kupanda miti iliongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishirikiana na Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge.
Shughuli hizo za kupanda miti zilifanyika katika kijiji cha Maruwa.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Waziri Mahenge alisema kwamba amefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 70 kwa kuwakumbusha washirika wao wa maendeleo suala la mazingira.
“Ni kawaida kuadhimisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa Oktoba 24 kila mwaka. Mwaka huu ni tofauti na zaidi ya tofauti umekuwa maalumu kwa namna yake kwa kuwa tunaadhimisha miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.” alisema Waziri Mahenge.
IMG_3547
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akiwasili kwenye sherehe ya kupanda miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kusalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
Hata hivyo alikumbusha kwamba wakati tunaadhimisha miaka 70 ni vyema wadau wa maendeleo wakaangalia historia na kujipanga kimkakati katika kusonga mbele kimaendeleo kwa kujali mazingira.
Alisema kwamba pamoja na hoja ya kujali mazingira pia serikali itaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumzia umuhimu wa siku hiyo ya kupanda miti, Rodriguez, alisema kauli mbiu ya wa mwaka huu ni “Sayari Moja Watu Bilioni 7: Utunzaji Mazingira ni Wajibu Wetu”, umerandana na shughuli hizo za upandaji miti.
Alisema kitendo cha upandaji miti kunaonesha wajibu wa kwanza wa kuhami mazingira ya sayari yetu kwa manufaa ya kizazi kijacho cha wanadamu.
Alisema mabadiliko ya tabia nchi si utani yapo kweli na ipo haja ya kuendelea kuwapo kwa juhudi za makusudi za wakazi wa dunia hii kulinda mazingira kwa ajili ya amani maendeleo na ustawi.
IMG_3704
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais kwenye sherehe za upandaji miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake balozi wa Ulaya alisema upandaji miti katika mteremko wa mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni alama muhimu katika mapambano ya wanadamu kulinda mazingira.
Alisema ishara hiyo muhimu inaelekeza Umoja huo na wadau wake wa maendeleo kuchukua tahadhari za kutosha kulinda mazingira na inakwenda sanjari na malengo endelevu ya milennia (SDGs) ambayo yana mada tano za kuangaliwa katika mazingira kuliko yale ya awali ambayo yalikuwa na mada moja tu.
Msemaji wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu alisema kwamba upandaji miti uliofanyika ni moja ya shughuli kadhaa zitakazofanywa na Umoja huo kuadhimisha miaka 70 toka kuanzishwa kwake.
Shughuli nyingine itakayofanywa ni kusafisha soko la Temeke, mashindano ya uchoraji kwa vijana na maadhimisho ya siku yenyewe.
IMG_3676
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe ya upandaji miti kwenye kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.
IMG_3583
Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Balozi Filiberto Sebregondi akizungumza kwenye sherehe ya upandaji miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.



IMG_3386
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye sherehe hizo.
IMG_3403
Wakufunzi kutoka chuo cha Ualimu Moshi wakitoa burudani kwenye hafla ya kupanda miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3381
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wanakijiji wa kijiji cha Marua walioshiriki sherehe za upandaji miti ikiwa ni Shamra shamra ya kusheherekea miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3384
IMG_3748
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akipanda mti katika kijiji cha Marua karibu na miteremko ya mlima Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
IMG_3774
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipanda mti katika kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, kila mti unaashiria kila mwaka ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukileta maendeleo duniani ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi. Kushoto ni Mshehereshaji Afisa Misitu wa mkoa wa Kilimanjaro, Emanuel Kiyengi.
IMG_3825
Afisa Misitu wa mkoa wa Kilimanjaro, Emanuel Kiyengi (kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi, mabalozi na viongozi wa serikali katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kupanda miti 200 zoezi lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa nchini katika kusheherekea miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3829
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_3781
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kupanda miti 2000 katika kijiji cha Marua karibu na miteremko ya mlima Kilimanjaro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto), Mkuu wa mabalozi, ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Halfan Mpango (wa nne kushoto), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan (wa tano kushoto), Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Balozi Filiberto Sebregondi (wa nne kulia), Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga ( wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ( wa pili kulia) pamoja na Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya.
IMG_3795
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akishiriki zoezi la kupanda miti katika kijiji cha Marua.
IMG_3294
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) wakati wa zoezi la upandaji miti.
IMG_3290
Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akishindilia udongo kwenye mti aliopanda katika eneo lake.
IMG_3346
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina akishiriki zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro.
IMG_3803
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akishiriki zoezi la kupanda miti lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya kusheherekea miaka 70 tangu kuanzishwa kwake duniani.
IMG_3810
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akishiriki zoezi la kupanda mti katika kijiji cha Marua.
IMG_3844
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem na Beatrice Mkiramweni kutoka ofisi za Mratibu Mkazi wa UN Tanzania wakipanda picha ya kumbukumbu kwenye mti walioshirikiana kupanda.
IMG_3864
Wakinamama wa kijiji cha Marua wakipozi miti yao wakati wakielekea kuunga mkono juhudu za Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
IMG_3275
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
IMG_3342  
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakitazama jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues wakati wa zoezi la kupanda miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro.
IMG_3577
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Umoja wa Mataifa wakijadiliana jambo na mshehereshaji wa hafla hiyo.
IMG_3883
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akikata utepe kuzindua jiwe la kumbukumbu la miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo maalum lililopandwa miti 2000 katika kijiji cha Marua, mkoani Kilimanjaro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
IMG_3886
Zoezi la uzinduzi likiendelea.
IMG_3888
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la kumbukumbu la miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
IMG_3898
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge katika picha ya pamoja na mabalozi waalikwa, viongozi wa Serikali na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
IMG_3904
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mgeni rasmi.
IMG_3847
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akipata picha ya kumbukumbu na wanakijiji wa kijiji cha Marua.

NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA, KAHAMA,SHINYANGA NA KISHAPU

$
0
0
ZIARA ya naibu waziri ilianzia kwenye chanzo ca maji kitongoji cha Ihelele, kijiji cha Nyanghomango kwa kugagua chanzo, sehemu ya kutibu maji na kusukuma maji kisha kuongea na wananchi wa kijiji cha Nysnghomango
Aidha alikagua mradi unaoendelea kujengwa wa kupeleka maji miji ya mwadui, Maganzo na Kishapu.



Mradi huu mkubwa wa maji unagharimu shilingi bilioni 254 na una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 120 kwa siku lakini mpaka sasa unazalisha maji lita milioni 80 tu kwa siku na unahudumia miji ya kahama, shinyanga, Ngudu ,vijiji 55 vilivyopitiwa na bomba.



Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa Kashwasa ambao ndiyo waendeshaji wa mradi huu injinia Laurance Wasala amesema Mradi huu ni mkubwa na maji yanatosha kufikisha maji Tabora na miji ya mwadui, mwadui, kagongwa, isaka, Tinde, Nzega na Igunga.



Akiwa kijiji cha Nyanghomango naibu waziri wa maji amewahakikishia wananchi kuwa wizara ya maji inafanya kila linalowezekana likamilishe mradi wa maji katika kijiji hicho ambacho ndiyo chanzo.



Kuhusu mradi wa maji kupeleka maji Kishapu, Mwadui na maganzo ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Kashwasa na amehaidi wizara ya maji itafuatilia fedha wizara ya fedha zilizopitishwa katika bajeti zitumwe Kashwasa kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

  Naibu waziri wa maji,  Amos Makalla akiwa katika chanzo cha maji Ihelele wilaya ya Misungwi.
 Naibu waziri wa maji,  Amos Makalla akikagua sehemu ya kutibu na kusukuma maji ihelele kulia kwake ( mwenye shati jeupe) ni kaimu mkurugenzi wa Kashwasa injinia Laurance Wasala.
 Naibu waziri wa maji, Amos Makalla Akihutubia wananchi kijiji cha Nyanghomango.
 Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akikagua mradi mradi wa Kupeleka maji Mwadui, maganzo na kishapu. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu wilson Nkambaku.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akionngea na waandishi wa habari kwenye mradi wa maji Kishapu.

Naibu waziri wa maji Amos Makalla ametembelea mradi mkubwa wa maji toka ziwa victoria na kuyapeleka miji ya Kahama, shinyanga, Ngudu, Kishapu, vijiji 55 na Tabora.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AMTEMBELEA WAZIRI MKUU WA UGANDA

$
0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda na ujumbe wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Uganda Dr Ruhakana Rugunda pamoja na viongozi wa serekalini Uganda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea jambo na Waziri Mkuu wa Uganda Dr Ruhakana Rugunda alipo mtembelea ofisini kwake kushoto ni Kaimu wa Itafaki Tanznia Bw. Jemes Bwana,  Waziri Mkuu yupo Nchini Uganda kumuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za Skauti kutimiza mika miamoja nchini Uganda.
Picha na Chris Mfinanga.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA MAFUNZO KWA MADEREVA KUPITIA CHAMA CHA TADWU.

$
0
0
WIZARA YA KAZI NA AJIRA

1.   Serikali imepata taarifa za kuwepo kwa mpango wa mafunzo kwa madereva nchini kote, ulioandaliwa na Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania-Tanzania Drivers Workers Union (TADWU) kuanzia wiki ijayo. Mpango huo umeelezwa kuwa njia mbadala ya tishio la mgomo lililotolewa na viongozi wa Chama hicho hapo awali, ili kuweza kupata suluhisho la malalamiko yao.

 Malalamiko hayo yalihusu Mkataba ya Ajira inayokidhi matakwa ya kisheria, nyongeza ya posho na viwango vya mishahara juu ya kima cha chini cha mshahara kwa sekta ya usafirishaji na kero nyinginezo za barabarani.

2. Taratibu za Chama kuendesha mafunzo na shughuli nyinginezo za kichama katika sehemu za kazi kwa mujibu wa Sheria ni kama ifuatavyo:-


(i)           Wawakilishi wa Vyama vya wafanyakazi wanayo haki ya kuwaarifu Waajiri na kuingia katika eneo la kazi ili kuandikisha wanachama, kuwasiliana na wanachama wao, kukutana na wanachama kujadili masuala yanayohusu mahusiano na Waajiri wao au kwa ajili ya kufanya chaguzi au upigaji kura kwa mujibu Katiba za Vyama vyao.


(ii)          Katika kutekeleza haki hiyo, ni lazima Wawakilishi hao wa Vyama wapate ridhaa ya Waajiri kwa kuzingatia vigezo na masharti (utaratibu) yanayolenga kulinda maisha ya watu na mali au kuzuia uvurugaji wa taratibu za kazi au utendaji kazi,  

(iii)        Vyama vya Wafanyakazi vina haki ya kutoa mafunzo katika sehemu za kazi ambazo kuna matawi yake au kuna wanachama wake wanaotambulika kisheria.


3.   Baada ya kutafakari taarifa hiyo ya viongozi wa TADWU na kuzingatia matakwa ya Sheria za Kazi nchini, Serikali imejiridhisha kwamba, taarifa iliyotolewa na uongozi wa TADWU imekiuka matakwa ya Sheria za Kazi. Taarifa hiyo haikuwasilishwa kwa Waajiri husika sehemu ya kazi, ambao TADWU ina wanachama wake inaokusudia kuwahusisha kwenye mafunzo hayo.


Taarifa hiyo haikubainisha ni wafanyakazi gani, wala idadi ya wafanyakazi hao watakaohusika na mafunzo hayo. Hakuna ratiba iliyoidhinishwa na Waajiri, inayohakikisha kuwa hakuna chombo cha usafiri kitakachosimama kufanya kazi na kuepusha usumbufu kwa watumia huduma.


4. Hivyo, Serikali inasisitiza na kuwakumbusha viongozi wa Chama hicho cha TADWU na madereva kwa ujumla, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Sheria za Nchi na kujiepusha na vitendo vinavyohatarisha usalama wa mali na maisha ya watumia huduma. Aidha, watambue kuwa umakini wao ni muhimu katika kuepusha hatua ambazo zina uelekeo wa kudumaza shughuli za kijamii na kiuchumi nchini.


5. Kushiriki katika mafunzo yaliyoelezwa na viongozi wa TADWU kwa utaratibu walioueleza ni sawa na kuitisha au kufanya mgomo usio halali.


6. Serikali imefanya jitihada mbali mbali za kuwaelimisha na kuwaelekeza, ikiwemo semina, mafunzo, ushauri na kugawa vijarida/vipeperushi. Elimu hiyo ilihusu taratibu za majadiliano ya pamoja ya kuboresha maslahi na utendaji kazi na utatuzi wa migogoro ya kikazi kisheria ili kuepusha madhara na usumbufu usio wa lazima kwa wanachi wasio husika na utatuzi wa malalamiko yao.


7. Hitimisho: Serikali inapenda kutoa wito kwa Wamiliki wa vyombo vya usafirishaji, viongozi wa vyama vya wafanyakazi vya madereva pamoja na madereva wote nchini kutekeleza makubaliano yaliyokwishafikiwa hadi sasa katika vikao vya Kamati ya Waziri Mkuu. Aidha, Serikali pamoja na Taasisi zake itaendelea kutoa elimu pamoja na kufuatilia makubaliano yaliyofikiwa na hatua za kisheria zitachulikwa dhidi ya wale watakaokiuka utekelezaji wa makubaliano hayo.


Eric F. Shitindi

KATIBU MKUU


20/08/2015

WAZIRI MKUU: SERIKALI INATAFUTA SULUHISHO LA DIASPORA KUPIGA KURA

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda (Pichani)amesema Serikali bado inatafuta suluhisho la kudumu litakalowezesha Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) waweze kupiga kura wakiwa huko waliko.

Ametoa kauli hiyo juzi usiku (Jumatano, Agosti 19, 2015), wakati akijibu maswali ya Watanzania waishio Uganda katika kikao kilichofanyika hoteli ya Serena jijini Kampala.

“Serikali tulitamani sana mchakato huu umekamilika mwaka huu ili Watanzania waishio nje ya nchi waweze pia kushiriki uchaguzi mkuu lakini tulipoongea na wenzetu wa NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi), ilibainika kwamba isingekuwa rahisi kupeleka mashine za BVR nje ya nchi wakati huo huo zoezi la uandikishaji likiwa linaendelea hapa nchini…”, alisema.

“Walisema kuna suala la uandikishaji, likimalizika kuna suala la uhakiki wa majina ya walioandikishwa… yote haya yanataka muda na maandalizi ya kutosha,” aliongeza Waziri Mkuu.

Alisema Serikali bado haijakata tamaa na yeye binafsi anaamini jambo hilo linaweza kufanyika kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020 bila matatizo yoyote.

Akigusia kuhusu uandikishaji wapiga kura nchini, Waziri Mkuu alisema lengo la awali lilikuwa ni kuandikisha wapiga kura milioni 24 lakini kutokana na takwimu na uzoefu uliopatikana kwenye nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilishauri lengo la Serikali liwe ni kuandikisha watu milioni 22.

“Lakini kama wengi mlivyosikia, wakati hata hawajamaliza kuandikisha wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambao ulikuwa wa mwisho, tayari tulishavuka lengo la awali la kuandikisha watu milioni 24,” alisema.

Alisema hilo ni jambo la kujivunia kwa sababu tangu mwanzoni, mchakato huo ulikuwa umegubikwa na kelele nyingi na watu walihofia kwamba kwamba zoezi hilo lisingekamilika. “Sote ni mashuhuda, watu wamejiandikisha na sasa wanakamilisha taratibu za uhakiki,” aliongeza.

Waziri Mkuu Pinda aliwasili nchini Uganda Jumatano usiku kwa ziara ya siku moja akimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Maskauti cha Uganda (Uganda Scouts Association – USA). Amerejea nchini jana usiku.

Rais Yoweri Museveni ndiye mlezi wa chama hicho na alikuwa amemwalika Rais Kikwete kwenye maadhimisho hayo.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, AGOSTI 21, 2015.

NAPE AWASHUKURU WAKAZI WA MAJENGO KATA YA MTAMA

$
0
0
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Majengo wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kuwashukuru wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi kwenye mchakato wa kura za maoni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Majengo wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kuwashukuru wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi kwenye mchakato wa kura za maoni.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akiwasalimia viongozi mbali mbali wa CCM ngazi za kata na matawi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano uliofanyika Majengo .
 Wananchi wa Jimbo la Mtama wakishangilia kabla ya mkutano kuanza.
 Wananchi wa Kata ya Majengo ,Mtama wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza mbunge wao mtarajiwa Nape Nnauye .

 Mbunge wa Mchinga Mhe.Said Mtanda akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi waliompigia Katibu Mwenezi wa CCM Taifa ,Nape Nnauye uliofanyika Majengo Mtama.
 Wanancnhi wakimsindikiza Nape Nnauye kwenda jukwaani kuhutubia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Majengo,Mtama na kuwaeleza atakuwa Mbunge wa mfano kwa kutekeleza kila alichoahidi na kuwa karibu na wananchi muda wote.
 Wananchi wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndie mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM.
Mkutano huo uliofanyika sokoni Majengo ulikuwa wa kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndie mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akisisitiza jambo kwenye mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake.
 Mmoja wa wagombea waliokuwa wanagombea nafasi ya kuiwakilisha Mtama bungeni akiwasalimu wananchi na kuwahakikishia kuwa atashirikiana na Ndugu Nape Nnauye katika kufanikisha ushindi wa CCM.
 Mgombea Diwani wa kata ya Mnara Bi.Halima R. Mwambe akiwasalim wananchi kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba za shukrani.
Kikundi cha kwaya cha Majengo kikitumbuiza.

PPF YAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA NOKIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwanachama mpya wa PPF, akijaza fomu za mpango wa uchagiaji wa hiari wakati wa utoaji huduma kwa wafanyakazi wa kampuni ya NOKIA pale Mlimani City jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2015. Kulia ni Afisa wa Kanda wa PPF, Upendo Singinika Sasi
 Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanachama wa Mfuko huo, Raymond Ndambo

 Elihuruma (kushoto) na mtaalamu wa mifumo ya comuter wa PPF, (Kulia), wakiangalia jinsi wanachama wa mfuko huo wanavyopata taarifa za michangu yao kupitia simu zao
 Afisa Masoko mwandamizi wa PPF, Nelu Mwalugaja, (kulia), akimpatia maelezo ya huduma za Mfuko huo, Mwanachama wa PPF
 Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari
Msimamizi wa Kanda wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Walter Mazula, (kulia), akimkabidhi zawadi mwanachama mpya wa PPF, Raymond Ndambo, (katikati), huku Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, wakati wa siku ya wafanyakazi wa kampuni ya NOKIA





 Wataalamu wa mifumo ya computer wa PPF, wakifuatialia taarifa za Mwanachama (wapili kushoto) 
 Afisa wa Kanda wa PPF, Upendo, (kushoto), akimpatia zawadi Mwanachama wa Mfuko huo baada ya kupatiwa huduma

Msimamizi wa Kanda wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Walter Mazula, (aliyekaa), akimpatia maelezo Mwanachama wa Mfuko huo, (kushoto), wakati wa utoaji huduma kwa wafanyakazi wa NOKIA pale Mlimani City jijini Dar es Salaam

Mgombea Urais Kupitia Chadema, EDWARD LOWASSA na Mwenzake DUNI HAJI warejesha Fomu NEC

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi, Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa Kampeni, kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi kuwania nafasi hiyo,  leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.

MARAFIKI WA WAFANYE WATABASAMU WATOA MSAADA KWA WATOTO WA AMANI ORPHANAGE CENTRE, BAGAMOYO

$
0
0
Marafiki wa Wafanye Watabasamu, hivi karibuni, walitembelea kituo cha watoto yatima (Amani Orphanage Centre) kilicho katika Kijiji cha Zinga, Bagamoyo kwa ajili ya kutoa misaada mbali mbali kisha kuchora nao. Mbali na marafiki waishio nchini, pia kulikuwa na walimu sita toka Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na wawakilishi wa taasisi ya The Tanzania Norwich Association pia ya Uingereza. (Picha: Nicolas Calvin).
Msafara wa Wafanye Watabasamu ukiwasili kituoni hapo. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu.
Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Centre, Bi. Margareth Mwegalawa wa pili toka kulia aliyesimama, akitoa taarifa fupi kuhusu kituo hiko.
Mratibu wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo ITV, Nathan Mpangala akiwashukuru marafiki mbalimbali waliochangia misaada na kufanikisha ziara hiyo.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images