Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 613 | 614 | (Page 615) | 616 | 617 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Pemba, August 19, 2015: Zantel Tanzania has today donated 10 million Tshs as a contribution to build 6 classrooms of Mkanyageni Primary School in Pemba.

  The donation aims at improving education standards to local communities through rendering support and providing school requirements such as infrastructure construction and renovations, the contribution will be used for finishing a building containing 6 class rooms covering costs of fitting windows and doors, cementing floor of 6 class rooms, plastering of 6 classrooms walls, painting of 6 classrooms walls and labor for the work.

  Zantel is keen to empower the societies we are serving, and this donation is aimed to contribute to national building by improving the lives of future leaders to have better environment to acquire education, Government alone cannot successfully fund a functional educational system, so it’s important for us to assist youths become the best in their various endeavors through education.
  Mkanyageni school head master Mr. Ramadhani Ngwali Makame, giving a speech during the handover ceremony
  that took place at Mkanyageni primary school in Pemba.


  Mr. Mohammed Mussa Zantel Government relations coordinator handing over dummy cheque to Mr. Ally Ngwali Vuai Mkanyageni school committee chairman, looking on are Zantel Acting CCO Mr. Bajwa,PembaSales Manager Farouk Ahmed and Mkanyageni pupils. 

  0 0

  Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akitoa hotuba yake wakati wa maonyesho ya sayansi kwa wanafunzi wa sekondari yanayoandaliwa na shirika la YST ambayo pia Ubalozi wake unadhamini kila mwaka.

  Na Daniel Mbega

  UBALOZI wa Ireland nchini Tanzania, umewapatia scholarship Watanzania 14 ili kusoma kozi mbalimbali za shahada ya uzamili (masters) na huku wanne kati yao wakienda kusoma vyuo vya nje ya nchi hasa University College Dublin, Dublin Institute of Technology na National University of Ireland Maynooth. 
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, scholarship hizo zimetolewa na ubalozi huo kama sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka (Fellowship Training Programme), ambapo wataalamu wanne waliobahatika kwenda ng’ambo watakwenda kusomea kozi za Maendeleo Endelevu (Sustainable Development), Kilimo na Maisha ya Vijijini (Agriculture and Rural Livelihoods), Rasilimali Watu (Human Resource Management), na Immunolojia na Afya ya Binadamu (Immunology and Human Health).

  Watanzania wengine 10 wamedhaminiwa kusomea kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya hapa nchini.Taarifa hiyo inasema, sherehe za kuwapokea wale walihitimu na kuwakabidhi scholarship wale wanaokwenda kuanza, zitafanyika kesho mchana katika ofisi za Ubalozi zilizoko Masaki, jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan, ndiye atakayetoa scholarship hizo.

  Mpango huo wa Mafunzo wa kila Mwaka, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa kiasi kikubwa unahusisha Mfuko wa Misaada wa Ireland (Irish Aid) kupitia program ya maendeleo ya Ubalozi huo nchini Tanzania. 

  Wanufaika wa mpango huo wameteuliwa na washirika wa maendeleo wa Ireland nchini Tanzania, zikiwemo wizara mbalimbali za Serikali, halmashauri za wilaya na mashirika yasiyo ya kiserikali, ambayo shughuli zao zinawiana na maeneo ya vipaumbele vya Irish Aid, hususan Kilimo, Afya, Lishe na Utawala.

  Aidha, wanufaika wote ni watendaji wa kati ambao baada ya kuhitimu masomo yao watarejea kwenye mashirika na taasisi zao kutumia ujuzi walioupata kwa manufaa ya jamii.“Kwa wanufaika watakaokwenda kusoma nchini Ireland, program inatoa fursa nzuri ya kujifunza katika hadhi ya kimataifa na kunufaika na hazina kubwa ya nyenzo za tafiti zinazotolewa kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za Teknolojia za Ireland,” imeeleza taarifa hiyo.


  Ikaongeza: “Inatarajiwa kwamba mafunzo ya wataalamu hawa yatachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania, na kuendelea kuimarisha ushirika wa kielimu baina ya Ireland na Tanzania.”

  Ireland, kupitia Mfuko wa Misaada (Irish Aid), imekuwa ikidhamini Mpango huo wa Mafunzo nchini Tanzania kwa miaka 40 sasa ambapo program hiyo imekuwa msingi wa msaada katika kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea na inaendana na mkakati wa kupunguza umaskini wa nchi washirika wa Ireland, hasa lengo likiwa kuwapatia wataalamu elimu ya juu ili waendeleze taasisi zao.


  Baadhi ya taasisi washirika zitakazonufaika na mpango wa mwaka huu ni pamoja na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Taasisi ya Chakula na Lishe, Hospitali ya CCBRT, shirika la Sikika, Mpango wa Maendeleo wa Kinapa (Kinnapa Development Programme), shirika la CARE Tanzania na Taasisi ya Afya Ifakara (IHI).


  (Imeandaliwa na www.brotherdanny.com/Simu: 0656-331974)  HII HAPA NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:


  PRESS RELEASE  Fellowship Training Programme Awards Four Scholarships to Study in Ireland


  Four Tanzanian professionals have been awarded scholarships to pursue their post-graduate masters’ degrees in Ireland. The scholarships were awarded by the Embassy of Ireland in Tanzania as part an annual Fellowship Training Programme. The fellows will study Sustainable Development, Agriculture and Rural Livelihoods, Human Resource Management, and Immunology and Human Health. A further ten Tanzanians have also been awarded scholarships to study in Tanzania.


  The Fellowship Training Programme is closely connected with Irish Aid, the Embassy’s development programme in Tanzania. The fellows have been nominated by Ireland’s development partners in Tanzania, including Government ministries, district councils and non-governmental organisations, whose work is closely aligned with Irish Aid’s priority areas - Agriculture, Health, Nutrition and Governance.


  The fellows are all mid-career professionals who, on completion of their studies, are committed to resuming work with their organisations and putting their acquired specialist knowledge and skills into practice for the benefit of the wider community. For the fellows studying in Ireland, the programme presents a unique opportunity to study in an international setting and benefit from the research facilities provided at Ireland’s Universities and Institutes of Technology.


  It is anticipated that the training and development of these key individuals will contribute to Tanzania’s development, and continue to strengthen the educational linkages between Ireland and Tanzania.

  Notes to the Editor

  ·        *  Ireland has supported a Fellowship Training Programme for 40 years. The programme is a key element in support of capacity building in developing countries and is closely aligned with the poverty reduction strategies of Ireland’s partner countries. The objective is to strengthen capacity of partner organisations through the provision of higher education opportunities.

  ·        *  Irish Aid is the Irish Government’s programme of overseas development. Irish Aid has been providing development assistance to Tanzania since 1975.

  ·      *    Partner organisations benefiting from this year’s fellowship training programme include the Ministry of Agriculture, the Ministry of Livestock and Fisheries Development, Kigoma District Council, Muheza District Council, Ngorongoro District Council,Kondoa District Council, Missenyi District Council, Tanzania Food and Nutrition Centre, CCBRT, Sikika, Kinnapa Development Programme, CARE Tanzania and the Ifakara Health Institute.

  ·        *  The four fellows who will study in Ireland will attend University College Dublin, Dublin Institute of Technology and the National University of Ireland Maynooth respectively.
  Embassy of Ireland

  20thAugust, 2015

  For further information please contact:


  Brian Nolan, Second Secretary, Embassy of Ireland, Dar es Salaam


  Tel: (+255 22) 260 2355 │ Fax: (+255 22) 260 2362 │ Email: brian.nolan@dfa.ie

  0 0  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) akikanusha kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka Serikalini kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO.
  SERIKALI imekanusha taarifa zilizojitokeza kwenye Vyombo vya habari yakiwemo magazeti na mitandao ya kijamii kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitafanya mkutano hadhara Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe 22 Agosti, 2015.

  Akizungumza na vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema serikali haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha siasa kutumia uwanja wa taifa kwa ajili ya shughuli za kisiasa.

  Alikiri kwamba ni kweli kwamba CHADEMA waliiandikia Wizara tarehe 12 Agosti, 2015 kutaka kutumia uwanja wa taifa katika uzinduzi wa kampeni lakini ombi lao lilikataliwa kwa maelezo kwamba uwanja ule kwa mazingira ya sasa hauruhusiwi kutumika kwa ajili ya mihadhara ya vyama vya siasa.

  “kwa kipindi haturuhusu uwanja wa taifa kutumika kwa mihadhara ya kampeni za vyama vya siasa. Uamuzi huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira rafiki ya michezo na kuepuka athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na mihemuko ya kisiasa” alisema Bwana Mwambene.

  Mwambene ameeleza kuwa, Serikali imeamua uwanja huo ubaki kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za msingi za kimichezo ili kuepuka mihemuko na athari yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na hamasa za kisiasa.

  “Ni kweli kwamba tulipata barua ya Chadema kuomba Uwanja kutumika kwa ajili ya mhadhara ya kisiasa wa CHADEMA hasa kuzindua Kampeni zao kwenye Uwanja tayari tumeshawaandikia kuwaarifu kuwa Uwanja ule hauwezi kutumika kwa ajili ya shughuli zozote za kisiasa” alisema Bwana Mwambene.

  Alisema vyama vyovyote vitakavyoomba kutumia Uwanja ule kwa shughuli za kisiasa havitaruhusiwa.


  0 0


  Chalila Kibuda,Globu ya jamii
  UGONJWA wa kipindupindu unazidi kusambaa katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi habari leo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,Aziz Msuya watu waliofariki katika manispaa hiyo watatu.
  Amesema idadi ya wagonjwa katika manispaa imezidi kuongezeka kutoka 34 hadi kufikia 43.

  Amesema dalili za huo ni  homa kali ,kuharisha pamoja na kutapika na kuongeza kuwa mtu akifikia dalili hizo awahi katika kituo cha afya.

  Aidha amesema kujiepusha na ugonjwa huo ni kuzingatia usafi wa vyakula ,maji pamoja na kunawa mikono kwa usafi wakati wa kula.

  Msuya amesema watu waliokuwa wamelalazwa na ugonjwa huo watatu wamerusiwa.

  Katika zahanati ya Mburahati wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa ni  21.

  Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo, Nusra Kessy amesema kuwa wagonjwa hao wanaendelea kutibiwa katika zahanati hiyo.
    Usafi ukiendelea katika Zahanati ya Mburahati katika kukabiliana na Ugonjwa Kipindupindu mara baada ya Globu ya Jamii kutembelea kujionea hali halisi ya ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
   Wakati ugonjwa wa kipindupindu ukiwa umeshika kasi lakini watu bado wanakula holela kama walivyokutwa na Kamera yetu leo jijini Dar es Salaam.
  Usafi wa Mazingira katika Zahanati ya Mburahati ukiendelea kama walivyokuwa na Globu ya Jamii leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Mgombea mwenza wa ugombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho tawala Dkt John Pombe Magufuli leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
   :Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
   Meza Kuu ikimfurahia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
   Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuongea na wazee wa Dar es salaam  leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
   Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuongea na wazee wa Dar es salaam  leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
   Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuongea na wazee wa Dar es salaam  leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
  Meza Kuu ikimfurahia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam  leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

  0 0

  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam .
  Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu (mbele) wakati wa kusaini fomu za hati ya Kiapo, leo Agosti 19, 2015. Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Mabele Marando.
  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu.
  Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu. Kulia ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.

  0 0

    Ni Siku ya 16 huku Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Msimu wa nne shindano linalo endeshwa na Shirika la Oxfam kupitia Kampeni yake ya Grow,  Likiwa linaelekea Ukingoni ambapo katika siku hii tunaona Maisha ya Mama Shujaa wa Chakula  walivyo ishi kwa Siku 15, lakini kubwa zaidi ni wakazi wa Kijiji cha Kisanga hususani wale ambao ndio waliokuwa wanaishi na Akina mama hao katika Kaya zao kutoa maoni yao jinsi walivyo ishi na akina Mama hao. Pia hapa tutaona wasifu wa Washiriki wote wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo kauli mbiu ni 'Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa'
  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula katika picha ya pamoja.

  0 0

  OM1
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akifungua mkutano wa Serikali Mtandao unaowahusisha Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala,Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wakala za Serikali unaofanyika katika Ukumbi wa AICC leo jijini Arusha.
  OM2
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga akifuatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Serikali Mtandao ngazi ya Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Taasisi za Serikali unaoendelea jijini Arusha.
  OM3
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Serikali Mtandao wakifuatilia mkutano huo leo jijini Arusha.
  OM4
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu, Makatibu Tawala wa mikoa,Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Taasisisi mbalimbali za Serikali mara baada ya kufungua Mkutano wa Serikali Mtandao leo jijini Arusha.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
  …………………………………………………………………………………….
  Na Aron Msigwa -Arusha
  Serikali imezitaka Wizara,Idara,Wakala na Taasisi  mbalimbali kuanza kujiandaa na mageuzi makubwa ya matumizi ya Mfumo mmoja wa  Mawasiliano kupitia Serikali Mtandao ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuondoa urudufu wa mifumo ya TEHAMA inayofanya kazi za aina moja serikalini.
   
  Hatua hiyo ya Serikali imekuja kufuatia kuwepo kwa mifumo ya TEHAMA ya kutolea huduma kwa umma katika Taasisi mbalimbali za Serikali isiyoweza kuwasiliana na kubadilishana taarifa jambo linalosababisha usumbufu kwa wanannchi wanapotakiwa kuwasilisha taarifa za aina moja kwenye taasisi tofauti za serikali.
   
  Akifungua Mkutano wa Serikali Mtandao wa Makatibu Wakuu,Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wakala za Serikali leo jijini Arusha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa mabadiliko hayo ni Sehemu ya mpango wa Serikali wa kuhakikisha kuwa  inawafikishia wananchi huduma bora kwa haraka, gharama nafuu na mahali walipo.
   
  Ameeleza kuwa hatua ya Tanzania kuweka msukumo kwenye Serikali Mtandao haiepukiki kwa kuwa imelenga kuboresha utendaji wa kazi ndani ya Serikali, kuongeza tija, ufanisi na kasi ya ubadilishanaji wa taarifa ndani ya Serikali.
   
  “Jambo hili la Serikali mtandao tumeshalizungumza sana Serikalini kutokana na umuhimu wake tumekutana watoa maamuzi kwa mara ya kwanza ili kufikia malengo ya Serikali mtandao tuliyojiwekea kila mmoja achukue hatua kuhakikisha kuwa fursa zilizopo zinatumika ipasavyo,tumeshaanza hakuna kurudi nyuma katika jambo hili” 
   
  Amesema Serikali imefanya mageuzi makubwa katika uwekezaji wa miundombinu ya TEHAMA ikiwemo uanzishaji wa Mkongo wa Taifa, Kituo cha Taarifa Serikalini (National Data Centres) ili kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinapatikana kwa urahisi, haraka,uwazi,gharama nafuu,wakati wowote na mahali popote nchini.
   
  “Serikali tumefanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya TEHAMA ikiwemo Mkongo wa Taifa (NICTBB), Mtandao wa Serikali (GovNet),Vituo vya kitaifa vya Data na kutenga  Masafa ya Intaneti ya Serikali, hii yote ni kuwahakikishia wananchi huduma bora za Serikali mtandao”  Amesisitiza Balozi Sefue.
   
  Amefafanua kuwa Serikali imeendelea kuboresha Sera na sheria, kutokana kutungwa kwa Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003 na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Serikali Mtandao 2013 pamoja na sheria ya Elekroniki na Mawasiliano ya Posta (Elektonic and Postal Communicatins),Sheria ya Miamala ya Kielektroniki 2015 na Sheria ya Makaosa ya Mitandao ya mwaka 2015.
   
  Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kujenga uwezo wake wa ndani ili kuondoa utegemezi wa wakandarasi wa nje katika ujengaji wa mifumo ya TEHAMA hapa nchini ambao huigharimu serikali fedha nyingi.
   
  “Tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha tunaimarisha na kujenga uwezo wetu wa ndani ili kuondoa utegemezi kutoka nje, wataalamu sasa tunao na tutaendelea kujenga uwezo wetu wa miundombinu ya ndani ili kuwahudumia wananchi”.
   
  Ametoa wito kwa wataalam wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Tume ya Mipango na Wakala ya Serikali Mtandao kushirikiana katika kuhakikisha Serikali Mtando inaingizwa katika mpango wa taifa wa miaka mitano.
   
  Aidha, amezitaka Taasisi ambazo zina kiwango kidogo cha utekelezaji wa Serikali mtandao kushirikiana na Wakala ya Serikali Mtandao kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA yanaleta ufanisi katika kujenga Serikali Mtandao madhubuti.
   
  “Taasisi za Serikali ambazo bado zina kiwango kidogo cha utekelezaji wa Serikali Mtandao zinatakiwa kuchagua jambo moja, kukubali  kubadilika au kubadilishwa” amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali inaendelea kuzijengea uwezo taasisi hizo ziweze kuendana na mabadiliko yaliyopo.

  0 0

  Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli  akikabidhi hati ya Kiapo mapema leo mchana kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Sekieti Kihiyo (katikati). Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
   Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akisaini hati ya Kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
   Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Jaji Sekieti Kihiyo mara baada ya  kusaini hati ya kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa ndani ya moja ya chumba cha Mahakama Kuu wakirekodi tukio la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli sambamba na mgombea Mwenza,Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakisaini hati ya Kiapo mapema leo mchama Mahakamani Hapo mbele ya Jaji  Sekieti Kihiyo. 
   Mgombea urais wa chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nje ya jengo la Mahakama Kuu mara baada ya kusaini hati ya Kiapo mapema leo mchana.Hati hiyo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kituo cha Walimu Mbagala ( Teachers Resource Center ) kimezundiliwa leo na Mgeni rasmi alikuwa Ndg. Phares Magesa , Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambapo aliwaomba wadau wote wa elimu nchini kusaidia jitihada za Serikali katika kuinua kiwango Cha elimu nchini. Kituo hicho Cha Mbagala kina hudumia kata 12 zenye shule zaidi ya 48 , Mgeni rasmi alishukuru PSPF ambao walikuwepo kwenye tukio hilo kama wadau na waliahidi kusaidia kituo ili kiweze kutoa huduma bora zaidi kwa Walimu na wanafunzi .
  Mgeni rasmi akitoa nasaha
  Mgeni rasmi akipata maelezo ya kituo hicho
  Mgeni rasmi akizindua kituo
  Picha ya pamoja Walimu wa kutuo, maafisa elimu wa Wilaya ya Temeke, wadau wa elimu akiwemo mwakilishi wa PSPF na Mgeni rasmi Ndg. Magesa katikati.

  0 0

  MIKOA 10 ya Tanzania bara, Inatarajia kuombea amani na utulivu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini.
  Kwa mujibu  wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mikoa hiyo itaiombea amani Tanzania kupitia muziki wa Injili kupitia waimbaji mbalimbali  wa ndani na nje ya nchi.

  Msama alisema awali kabla ya mikoa hiyo kuombea amani uchaguzi Mkuu, Tamasha la kwanza lenye dhamira hiyo litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.

  “Tumeona kuna umuhimu kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kumuomba Mungu atuongoze katika uchaguzi Mkuu ambao unatakiwa kuwa huru na haki, ili kufanikisha hayo kwa ufanisi nyimbo za kumuomba na kumtukuza Mungu zitumike ili dua na sala zisikike mbinguni,” alisema Msama.

  Msama alisema Kamati yake bado inaendelea na mchakato wa kufanikisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo litaimarisha na kudumisha amani na utulivu ulioasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.

  Aidha Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa Tanzania na nje  ambao watasaidia kufikisha ujumbe huo kwa Mungu.

  Msama alisema wananchi wajiandae kupata neno la Mungu kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili ambao watafanikisha mungu kusikia wanachohitaji wananchi.

  0 0

   Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Gregory Kibusi akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mrimia Mchomvu, akitoa hotuba ya kufunga Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
   Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
   Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Kitengo hicho katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

   Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
   Afisa kutoka Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Salome Tilumanywa, akiwasilisha mada kuhusu uchimbaji na biashara ya tanzanite katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (Wa pili kushoto – waliokaa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi. Wengine kutoka Kulia (waliokaa) ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria - Magharibi, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Mrimia Mchomvu, pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo.


  Wachimbaji madini wadogo waipongeza Serikali
  Na Veronica Simba – aliyekuwa Mwanza

  Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), limetoa pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, hususani Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Vito na Almasi (TANSORT), kwa jitihada inazofanya kuwainua wachimbaji wadogo nchini.

  Pongezi hizo zilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa FEMATA, Gregory Kibusi wakati akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika Semina ya Wathaminishaji Madini ya Vito na Almasi iliyofanyika Agosti 12 na 13, Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

  “Kwa niaba ya uongozi wa FEMATA, naipongeza Serikali hasa Kitengo cha TANSORT kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa jitihada za makusudi kabisa za kuwainua wachimbaji wadogo nchini.” 

  Akifafanua zaidi, Kibusi alisema kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi lakini kutokana na ushirikiano ambao Serikali inautoa, hakuna shaka malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yatatimia.

  Kibusi alisema, kupitia jitihada zinazofanywa na Serikali, wachimbaji wadogo wamekuwa na mwamko wa kupata taarifa za mipango na mikakati ya Serikali juu ya maendeleo yao.Pia, alisema jitihada za Serikali zimewezesha wachimbaji wadogo kushiriki maonesho ya madini ya vito na usonara ya ndani na nje ya nchi. 

  “Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo sambamba na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa mlezi wa wachimbaji wao,” alisema Kibusi.

  Kibusi alisema wachimbaji wadogo wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na uwezo mdogo wa kifedha katika kuendesha shughuli zao za uchimbaji na ukosefu wa elimu ya juu ya madini hasa ya vito.

  Alitaja changamoto nyingine kuwa ni wachimbaji wadogo wa madini kutotambuliwa na baadhi ya Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kama wadau wakubwa wa maendeleo hasa kiuchumi na kijamii.


  Akiwasilisha maombi ya FEMATA kwa Serikali, Kibusi alisema wachimbaji wadogo wanahitaji wataalamu wa madini ya vito ili wawasaidie katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua, kuthamini, kusaidia kutafuta masoko pamoja na kutoa ushauri juu ya uongezaji thamani madini na namna bora ya kufanya biashara ya madini. 


  0 0

    Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.
    Mkutano na wanahabari ukiendelea.

  0 0

    Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar, Bwana Mohamed Musa akikabidhi hundi ya Shilingi millioni 10 kwa Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Mkanyageni, Bwana Ally Ngwali Vuai iliyoko visiwani Pemba kwa ajili ya kukamiIsha ujenzi wa vyumba sita vya madarasa vitakavyotumiwa na watoto zaidi ya 350. Anayeshuhudia ni Mkurugugenzi wa Mauzo Zantel, Bwana Sukhwinder Bajwa pamoja na wanafunzi na wajumbe wa kamati ya shule hiyo. 
  Mkuu wa Shule ya Msingi Mkanyageni, Bwana Ramadhani Ngwali Makame, akitoa neno la utangulizi wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 10 baina ya shule hiyo na kampuni ya Zantel kanda ya Zanzibar. Makabidhiano hayo yamefanyika leo shuleni hapo.

  Zantel yatoa msaada wa shilingi milioni kumi kwa ajili ya kukarabati madarasa sita ya shule ya Msingi Mkanyageni iliyoko Pemba.
    
  Pemba,Agosti 19,2015:Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel leo imetoa msaada wa shilingi milioni 10 kama mchango wa kujenga madarasa sita katika shule ya msingi ya Mkanyageni iliyopo Pemba.

  Kiasi hicho cha fedha kitatumika katika kumalizia ujenzi wa madarasa hayo sita kwa kuweka sakafu, madirisha na milango, kupaka rangi pamoja na gharama za kazi kiujumla, msaada ambao unatarajiwa kuboresha kiwango cha elimu katika shule hiyo.

  Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Mauzo wa kampuni ya Zantel,Bw Sukhwinder Bajwa alisema msaada huo umelenga kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule hiyo.

  ‘Kampuni ya Zantel mara zote imekuwa msitari wa mbele katika kuchangia kujenga nchi kwa kushiriki katika kuwekeza katika shughuli za kijamii hasa katika sekta ya elimu ambayo inaandaa mazingira na maisha bora ya viongozi wajao katika upatikanaji wa elimu’ alisema Bwana Bajwa.

  Akizungumza pia wakati wa makabidhiano hayo, Mkurungezi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa alisema Zantel imejikita zaidi katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora visiwani hapa.

  ‘Kama kampuni inayoongoza kwa idadi kubwa ya wateja visiwani hapa ni wajibu wetu kuhakikisha tunajitolea kwa kuwekeza katika miradi inayogusa maisha ya wananchi kama huu wa elimu ambao unaboresha miundombinu ili watoto wetu waweze kupata elimu bora’ alisema Mussa.

  Akitoa shukurani kwa kampuni ya Zantel kwa msaada, Mwenyekiti wa kamati ya shule, Bwana Ali Ngwali Vuai, alisema ni muhimu kuwekeza katika elimu kwani wanafunzi wakielimishwa watakuwa sehemu muhimu ya maendeleo  ya taifa letu.

  ‘Tunawashukuru kampuni ya Zantel kwa kutusaidia katika juhudi zetu kuhakikisha tunaboresha mazingira ya elimu kwa watoto wetu’ alisema Bwana Vuai.  

  0 0

   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akichukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Singida, Faridda Mwasumilwe katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo, juzi.
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akipokewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kinyagigi katika Jimbo la Singida Kaskazini wakati alipokwenda kuzungumza nao, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akicheza na makada wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Kinyagigi muda mfupi baada ya kuchukua fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida.
   WANANCHI wa Kijiji cha Kinyagigi katika Jimbo la Singida Kaskazini, wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya kuchukua fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida.
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati), ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida, muda mfupi baada ya kuchukua fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kinyagigi, jimboni humo juzi.

  0 0

  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma,Antony Mavunde akionesha fomu alizochukua za kugombea Ubunge katika jimbo hilo nje ya ofisi za Halmashauri ya Dodoma. 
   Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Antony Mavunde akipungia mamia ya mashabiki wakati akielekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Dodoma kwekuchukua fomu.
   Mavunde akifurahia jambo na Wafuasi wake.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi,Antony Mavunde akikabidhiwa fomu na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Elizabeth Gumbo jana Mjini Dodoma.
   
  MGOMBEA wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Anthony Mavunde amechukua fomu na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha analinda haki za wakazi wa mji wa Dodoma katika masuala ya ardhi.
   
  Akizungumza na wanachi mara baada ya kuchukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Mavunde amesema akipata nafasi ya kuwa mbunge kupitia nafasi hiyo atakuwa mjumbe wa bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA)hivyo atahakikisha mamlaka hiyo inaboresha maisha ya watu na sio kuyadidimiza.

  Aidha ameahidi kuimarisha sekta ya michezo ambayo imepewa kisogo katika Mkoa wa Dodoma.Michezo hiyo ni Pamoja na Mpira wa pete,Kikapu,Mpira wa mikono na Riadha.,Mavunde alisema kama akipewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi suala la michezo kwake litakuwa ni la lazima na inapiga hatua.

  "Mimi ni muumini wa michezo hivyo tofauti na soka nitatoa nafasi pia kwa michezo mingine ambayo imekuwa ikiipa sifa mkoa wa Dodoma ili vijana waweze kujikwamua na kuondokana na tatizo la ajira, "alisema

  Alisema akipata nafasi ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi cha kwanza atakachofanya ni kukutana na viongozi wote wa vyama vya michezo mkoani hapa ili kuweka kalenda za kisasa ambazo zitaendeleza michezo.

  Mavunde alisema lengo lake lingine ni kuanzisha academic ya michezo ambayo itakuwa ikiwaandaa vijana jinsi ya kuwa wachezaji wa kulipwa katika miaka ya baadae pamoja na kuwatafutia soko la kwenda kuonyesha vipaji vyao nje ya Tanzania.

  0 0

  Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda). Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda).Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo. Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya tamasha hilo. Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya tamasha hilo.Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli). Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli).Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo. Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.Baadhi ya wasanii na makada wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari. Baadhi ya wasanii na makada wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
  Baadhi wa aandishi wa habari wakiwasikiliza wasanii hao na waratibu wa tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015. Baadhi wa aandishi wa habari wakiwasikiliza wasanii hao na waratibu wa tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015.

   WASANII ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameandaa Tamasha kubwa kuzunguka nchi nzima kwa pamoja na kukinadi chama hicho tawala pamoja na Sera zake ili kiweze kushinda Uchaguzi Mkuu onaotarajia kufanyika Oktoba Mwaka huu (2015).

   Tamasha hilo litakalojulikana kama "MAMA ONGEA NA MWANAO 2015" limeandaliwa na baadhi ya wasanii makada wa CCM wapatao 250 ambao watazunguka mikoa zaidi ya 10 kukipigia kampeni chama hicho tawala ili kiweze kupewa ridhaa tena na Wananchi ya kuendelea kuongoza nchi. 

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti Msaidizi wa tamasha hilo, Wema Sepetu alisema madhumuni ya tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume. Msanii Sepetu akiyataja masuala hayo yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi hao kuwa ni pamoja na amani na utulivu uliopo hadi sasa, maendeleo ya kijamii na kiuchumi yalioletwa hadi sasa, masuala ambayo yanastahili kuendelezwa na wala si kubezwa. 

  Tamasha hilo linajumuisha wasanii kama Odama, Davina, Wastara Juma, Keisha, Wellu Sengo (Matilda), Bi. Mwenda, Mama Lolaa, Mama Nyamayao, Herieth Chumila, Thea, Maya, Chuchu Hans, Steve Nyerere pamoja na wasanii wengine wengi. Aidha alisema kupitia tamasha hilo wasanii hao pamoja na wenzao watazunguka katika mikoa zaidi ya 10 kwa pamoja kufanya kampeni kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli, mgombea Mwenza, Samia Hassan Suluhu pamoja na viongozi wengine ngazi mbalimbali wanazogombea kupitia chama cha Mapinduzi. 

   Madhumuni ya tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume ambayo bila amani mama awezi kujifungua salama, Bila mama hakuna familia, amani inapotoweka mama hawezi kukimbia kilometa kadhaa na kuiacha familia yake, bila mama hakuna ujasiliamali, mama ni kimbilio la baba, kaka, dada na watoto...ikumbukwe kuwa mama ndio mpiga kura ndio maana tunasema mama ongea na mwanao," alisema Wema Sepetu.

   "Na leo hii kuanzia sasa tunatambulisha kampeni yetu tunayoifanya kuhamasisha vijana, kinamama, kinababa, mashabiki wetu wale wote wenye sifa za kupiga kura wapige kura kwa kumchagua kiongozi bora anayetoka Chama Cha Mapinduzi...chagua Dk. Magufuli, Samia Suluhu, wabunge na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi," alisema Sepetu. Aidha wasanii hao wamempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuongoza vizuri vikao vyote vya chama hicho hadi kupatikana kwa mgombea bora wa urais kupitia chama hicho (Dk. Magufuli), hivyo kuwataka wanaCCM wote ambao waligombea na hawakupata nafasi kuungana na kukitumikia chama. 

  "...Mimi Wema Abraham Sepetu nikiwa na baadhi ya wasanii wenzangu ambao tuligombea tunasema muda bado tunao na siku tunazo kwa kukitumikia chama tukipewa ridhaa kwa njia yoyote na kwa nafasi yoyote ndio maana hatuja teteleka tupo imara kuwatumikia wananchi katika nafasi nyingine ndani ya CCM," alisema Sepetu. Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada leo jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria mkutanoni .
   Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC leo jijini Dar es salaam wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.
   Wanasekretarieti ya maandalizi ya mkutano NEC na wadau mbalimbali  na baadhi ya waandishi wakifuatilia mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akiteta jambo na mmoja  wa makamishna wa Tume hiyo Prof Amon Chaligha leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa NEC na wadau mbalimbali.
   Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi na hatua zilizofikiwa hadi sasa leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini.


  MWANDISHI WETU -MAELEZO-DAR ES SALAAM

  Tume ya Taifa ya uchaguzi  NEC  imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea  ili waweze kufanya maamuzi sahihi  wakati wa uchaguzi Mkuuu ujao.

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti   wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa uchaguzi na kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.

  Alisema kuwa  taasisi za kidini zinaaswa kama walivyo wadau wengine katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhubiri amani na kuendelea kutoa elimu kwa watanzania ili zoezi hili liishe kwa amani na kuwaacha watanzania wakiwa  na umoja na mshikamano licha ya tofauti za kiimani zilizopo miongoni mwao.

  “Tume inawataka, nyinyi  viongozi wa dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi kwa waumini wenu kuhakikisha hamuonyeshi hisia za kuwa upande wa chama chochote cha kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegema chama au mgombea fulani” amesema Jaji Lubuva.

  Mmoja wa washiriki wa mkutano huo , Askofu Philemon Phiri wa kanisa la EAGT-Mikocheni -A ameiasa Tume  hiyo  kusimama katika haki, uhuru na kuhakikisha wanatangaza washindi bila kuonyesha upendeleo  ili kuivusha nchi ikiwa  salama.

  Mshiriki mwingine kutoka Kanisa la Moravian Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa amani ndiyo tunu kwa kila mwanadamu, hatutegemei vurugu wakati  huu wa uchaguzi maana amani inapotoweka wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini wao hivyo wao kama taasisi zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili tupate viongozi kwa amani

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutano na viongozi hao na wadau wengine ikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa kampeni hapo Jumamosi ijayo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

  0 0  Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akizungumza na waandishi wa habari za masuala ya haki jinsia na uzazi katika mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam.


  Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,Siyovelwa Hussein akizungumza na waandishi wa habari wa wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR leo jijini Dar  es Salaam.
  Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akionyesha katiba ya chama hicho kuashiria uzinduzi wa chama cha TAMENET–SRHR leo jijini Dar es Salaam.
  Meneja Msaidizi wa mradi wa TMEP ,Eugnia Msasanuri akizungumza na wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR jijini Dar es Salaam leo.


  Baadhi ya wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR.
  Wadau wa  Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  SERIKALI imesema kuwa imefikia lengo la nne la millenia ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano  kwa kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000.

  Hayo ameyasema leo Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa,Dk. Koheleth Winani wakati wa uzinduzi  wa mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya  Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,amesema kuazishwa kwa mtandao kutasaidia kusukuma harakati za kupunguza vifo hivyo.

  Amesema anatambua mchango wa waandishi habari  katika mapambano dhidi ya Afya ya Uzazi na ukatili wa kijinsi  pamoja na ukatili dhidi ya watoto.

  Dk. Winani katika kuboresha afya ya uzazi ,kutokomeza ukatili wa wa kijinsia  na ukatili dhidi ya watoto katika kupunguza vifo vya vitokanavyo na uzazi  pamoja na  watoto chini ya miaka mitano.

  Aidha amesema waandishi katika  kwa kuazisha wametambua majukumu yao katika taifa  katika harakati za masuala ya afya hususani uzazi.

  Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao huo,Siyovelwa Hussein amesema kuwa kuazishwa kw amtandao huo inatokana na mafunzo mbalimbali pamoja na kujionea hali halisi  katika maeneo ambayo yako nyuma katika masuala ya afya ya uzazi.

  Siyovelwa amesema kuzinduliwa kwake na kuaza kufanya kazi katika kuweza kujiimarisha kifedha katika kuelimisha wananchi katika masuala ya afya.

older | 1 | .... | 613 | 614 | (Page 615) | 616 | 617 | .... | 1898 | newer