Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

SBL YAMKARIBISHA BALOZI WA IRELAND NCHINI KATIKA KIWANDA CHAKE CHA MOSHI

$
0
0

 Meneja wa kiwanda cha bia cha Serengeti Moshi Colman Hannah akitoa maelezo mafupi kwa wana habari juu ya ugeni kiwandani hapo kulia kwake ni Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan na kushoto kwake ni Msambazaji mkuu wa bidhaa za Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoani Kilimanjaro
 Balozi wa Ireland nchini  Fionnuala Gilsenan kushoto akiwa na mwenyeji wake Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Serengeti Moshi Colman Hannah akitembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki hii.
  Balozi wa Ireland nchini  Fionnuala Gilsenan akionja bia ya Guinness inayozalishwa kiwandani hapo(kulia) akiwa pamoja na katibu wake Nicholas Michael(katikati) na mwenyeji wake Meneja wa Kiwanda cha bia cha Serengeti Moshi Colman Hannah(kushoto).
    Balozi wa Ireland nchini  Fionnuala Gilsenan akipata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa maabara ya kiwanda hicho Jemima Mwambungu.
 Mpishi mkuu wa bia za Kampuni ya Bia ya Serengeti Moshi Julius Nyaki akitoa maelekezo kuhusu upikaji wa bia ya Guinness kwa Balozi
Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo.

Wizara yaahidi kuboresha ukaguzi wa shule

$
0
0


Kuongeza idadi ya wakaguzi wa shule
  • Yapiga Marufuku Walimu Kutumia Wanafunzi Kusahihisha Madaftari ya Wanafunzi Wenzao
 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema itaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha ukgauzi wa shule ili kuhakikisha ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya wanafunzi na ufundishaji shuleni. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Marystella Wassena katika mahojiano na kituo cha Redio Uhuru cha jijini Dar es salaam.

Wassena amesema chini ya utaratibu na mfumo wa sasa kila shule inatakiwa kukaguliwa mara moja kila mwaka hatua ambayo imekuwa ikitekelezwa na wakaguzi wa elimu wa kanda na wa wilaya katika kuhakikisha maendeleo ya mwanafunzi. Hata hivyo  bado kuna changamoto katika  kuzifikia shule zote.

Mkurugenzi huyo amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Wizara inakusudia kutumia mbinu na mikakati mbalimbali ili kuongeza kiwango cha ukaguzi shuleni ikiwemo kuongeza idadi ya wakaguzi.

“Kila shule inapaswa kukaguliwa mara moja kwa mwaka na tumekuwa tukifanya hivyo ingawa tumeona kwamba kuna haja ya kuongeza kiwango cha ukaguzi na kwa sasa kuna mipango inafanyika ili kuwezesha jambo hili  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.”Alisema Wassena. 

Amesema zipo nchi ambazo shule zinakaguliwa zaidi ya mara moja kwa mwaka. Alitolea mfano wa nchi ya Korea ya Kusini ambapo shule zinakaguliwa mara moja kila muhula, mfumo ambao amesema unaweza pia kutekelezwa Tanzania.

Ametaja baadhi ya juhudi ambazo Serikali inazifanya kwa hivi sasa ni kuimarisha ukaguzi wa shule kwa kushirikiana na UNICEF kutoa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule ili washiriki kikamilifu kukagua shule zao ikiwa ni pamoja na ufundishaji na kuona kuwa mazingira ya shule zao yanafaa katika kutoa Elimu bora.


“Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule watasaidia sana iwapo kila  mmoja wao atakuwa na ujuzi wa kukagua shule zao na kufahamu namna bora ya kuondoa mapungufu yanayojitokeza kwa kuwa wao wapo karibu zaidi na shule hizo,” alisema.

Wassena ameeleza zaidi kuwa kumekuwa na juhudi nyingi za kuboresha ufundishaji shuleni, juhudi ambazo zimekuwepo hata kabla ya matokeo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012 amabazo ana imani kuwa zitatoa mafanikio makubwa katika siku zijazo.

Katika hatua nyengine, Mkurugenzi huyo wa Ukagauzi wa Shule amepiga marufuku walimu kuwatumia wanafunzi kusahihisha madaftari / mitihani ya wanafunzi wenzao na amesema kazi hiyo inapaswa kufanywa na mwalimu mwenyewe ili aweze kujua kikamilifua kama somo lake limeeleweka na kutoa msaada pale inapobidi.

“Kazi ya ualimu ni kufundisha na kusahihisha ili kufanya tathmini ya kile mwalimu alichofundisha na kufahamu kama somo lake limeeleweka au la. Vilevile mwalimu ataweza kujua mwanafunzi anavyoandika, anavyoumba herufi na kuweza kutoa maelekezo ipasavyo,” alisema.

Wassena amesema walimu wanaowatumia wanafunzi kusahihisha madaftari/ mitihani ya wanafunzi wenzao wanafanya makosa ya kitaalam.

fastjet yatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima

$
0
0


Wafanyakazi wa fastjet walitoa m
saada
 wa vitabu vya shule, vinywaji na vyakula katika kituo cha watoto yatima CHAKUWAMA , Sinza Mori wakati wa pasaka, vilipokelewa na Hassan Khamis Katibu wa CHAKUWAMA
(aliyevaa buluu)

mamia ya wananchi wahudhuria maadhimisho ya karume leo Zanzibar.

$
0
0

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar.

Mamia ya Wananchi kutoka sehemu mbalimbali leo wamehudhuria katika kisomo maalum cha kumuombea dua Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume kilichofanyika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Katika kisomo hicho ambacho mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed shein kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na Mabalozi.

Awali kisomo hicho kilitanguliwa na Dua maalum iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaab. Mara baada ya Dua hiyo kilifuata kisomo cha Khitma kilichojumuisha Wanaume na Wanawake waliohudhuria katika hafla hiyo.

Akitoa Mawaidha katika Hafla hiyo Shekh wa Mkoa wa Dar es Salaam Al-had Mussa Salim aliwanasihi Waumini kufanya matendo mema kwa kuzingatia kuwa Kifo kinaweza kumtokea mtu yeyote na muda wowote. Naye Mtoto wa Muasisi huyo Balozi Ali Karume amesema njia pekee ya kumuenzi Marehemu Karume ni kuyaendeleza yale yote mazuri aliyoyaacha.

Katika hatua nyingine Vingozi wa mbali mbali Akiwemo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Kikwete waliweka Mshada ya Maua katika Kaburi la Marehemu Karume ikiwa ni ishara ya kumbukumbu.

Viongozi wengine walioweka Mashada ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Gharib Bilali, Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,Makamo wa Pili Balozi Seif Ali Idd na Marais wastaafu,Wawakilishi wa Mabalozi na Viongozi mbalimbali. 

Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alikuwa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo tarehe kama ya leo mwaka 1972 aliuwawa kwa kupigwa Risasi.
  
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR   07/04/2013

MUASISI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR MZEE ABEID AMANI KARUME AKUMBUKWA LEO

$
0
0
 Shekhe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad Mussa Salum akitoa mawaidha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein na viongozi wengine wa juu wakisoma dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013 
  Kiongozi wa Kanisa la Anglikana la Zanzibar akiomba dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013

 Kiongozi wa Kihindu  akiomba dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013 .PICHA NA IKULU
Wake za vionvgozi mbalimbali pamoja na mabalozi wakiwa katika dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAPANDA PANTONI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na watoto waliokutana nao kwenye pantoni ya MV Magogoni walipokuwa  wakitoka Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es salaam leo April 7, 2013   walikomtembelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakishuka kutoka  kwenye pantoni ya MV Magogoni walipokuwa  wakitoka Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es salaam leo April 7, 2013 walikomtembelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. PICHA NA IKULU.

NANI KUIBUKA MSHINDI JUMATANO HII KATKA MASHINDANO YA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE!

$
0
0

Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha nne cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania –bluu, Uganda- kijani na nyeusi.
=======  ======  ======  ======
TIMU NNE MPYA  KUINGIA KUCHUANA KIPINDI CHA NNE CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™


April 3, 2013, Dar es Salaam; Jumatano iliyopita  kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalionesha ni jinsi gani utulivu unavyosaidia katika mashindano ambapo timu kutoka Kenya ilifanikiwa kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka Kenya . 

Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na kufikia hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.


Kenneth na Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .


Katika Episodi ya nne ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.


Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha nne wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.


 
Timu ya blu-Tanzania:

·         Lukwesa Kanakamfunu(18) na Hamza Ziada(20), wote kutoka Dar-es-Salaam wanaojivunia kuwa marafiki japokuwa wanashabikia timu mbili adui yaani Arsenal na Manchester United. Lukwesa ni mwanafunzi na ndiye kichwa cha timu wakati Hamza ndiye atakayekua akionesha uwezo wa kuchezea mpira.


Timu nyekunndu:

·         Ephatus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) wote kutoka Nairobi watashiriki kuona kama wanaweza kuwa timu ya tatu ya Kenya kupata nafasi ya kufuzu mashindano ya Pan Africa. Empantus meneja wa ujenzi na ndiye kichwa cha timu wakati Samuel ambaye ni mchezaji wa Nakuru Allstars FC ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.


Timu ya kijani-Uganda:

·         Andrew Mpanga(30) na Gadafi Mohammed Anguzu(18) wote kutoka Kampala,Andrew ni mshabiki wa Man.Utd wakati Gadafi ni mshabiki wa Man.City.Andrew ni daktari wa meno ambaye atakuwa kichwa cha timu.Gadafi ni mchezaji mpira hivyo ataonesha uchezaji wake.


Timu nyeusi-Uganda:
·         Badi Arorwa(25) na Dennis Bogere(30)kutoka Kampala watawakilisha Uganda katika kipindi kijacho cha mashindano.Badii atajibu maswali akiwa kama kichwa cha timu na Dennis ambaye atakayekuwa akichezea mpira kuonesha kipaji chake.
                               
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.  


Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia  ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.


Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 


*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.





UKUMBI WA MASUMBWI KUHAMIA CHALINZE

$
0
0
Bondia Martin Shekivuli kushoto akipambana na Abdull Ndosa wakati wa mpambano wao wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano huo ulitoka droo.


Bondia Amour Mzungu katikati akipambana na Josefu Marwa wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kushoto ni refarii Ibrahimu Kamwe .
Refarii Ibrahimu Kamwe akimnyoosha mkono juu Amour Mzungu kuwa mshindi wa mpambano huo dhidi ya Josefu Marwa .
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar katikati akizungumza mbele ya mabondia Issa Omari kushoto na Shabani Madilu kabla ya mpambano wao.

  
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar amesema yupo tayali kushilikiana na wadau mbalimbali ili iwezekane kupatikana ukumbi maalumu wa mchezo wa masumbwi Chalinze aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika mapambano ya ngumi yaliyopigwa katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala.

Nina tarajia kufikisha mbali mchezo huu kwa kuwa mmenishawishi kuupenda mchezo wa masumbwi mchezo unaopendwa na wengi na kukimbiwa na wadhamini wachache ata hivyo nimeandaa mpambano rasmi utakaochezwa Chalinze kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huu siku ya April 21 hivyo nawaomba wadau wote wa ngumi tuamie chalinze kwa mda hili tuweze kuhamasha mchezo huu

Ambapo siku hiyo kutakuwa na ushindani mkubwa wa mabondia kutoka Dar es salaam watacheza na mabondia wa Chalinze siku hiyo ata hivyo kwa kuonesha kwamba anajili na anathamini mchezo wa masumbwi ame aidi kutoa gari moja kwa ajili ya mashabiki na mabondia kwenda kushiriki mchezo uho wa April 21

mbali na ahadi hiyo Diwani huyo ametoa pesa taslimu shilingi 1,50000 kwa ajili ya malipo ya baadhi ya mabondia waliokuwa awajilipwa na kuanza kudai kabla ya kupanda ulingoni na kuhamua kuchukua jukumu hilo la kuwalipa mabondia hao

Mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini Ibrahimu Kamwe  amesema kuwa yupo tayali kutoa ushilikiano wa hali na mali kwa kuanzia atachukua baahi ya vijana kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo wa masumbwi uliopangwa siku hiyo hivyo tupo pamoja unajua ngumi watu wanapenda kuangalia ili galama zake ni kubwa ata hivyo naona ajabu wadhamini kushindwa kujitokeza kuzamini mchezo huu unaopendwa na vijana wengi

na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Ahmed Karama Nassar kwa kuanza kusapoti mchezo wa masumbwi sehemu uliyopo

UNIC YAWAPELEKA WANAFUNZI JIJINI DAR KILWA KISIWANI KUJIFUNZA CHIMBUKO LA BIASHARA YA UTUMWA.

$
0
0
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na mfanyakazi mwenzake Phillip Musiba, walimu waliojumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilwa katika ziara hiyo katika picha ya pamoja.

Wanafunzi wakiwasili Kilwa Kisiwani.
Picha juu na chini' Tour Giude' Dullah akitoa malekezo ya ramani ya sehemu watakazotembelea wanafunzi hao ili kupata ufajamu wa jinsi Historia ya eneo hilo ilivyokuwa hadi kufikia biashara ya Utumwa na majengo yaliyokuwa yakitumika Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
Wanafunzi wakichukua maelezo muhimu kutoka kwa Mtaalamu wa masuala ya Historia ya Asali ya Kilwa Kiswani na Songo Mnara wakiwa kwenye makaburi waliyozikwa viongozi waliotawala eneo la Kilwa Kisiwani.
'Tour Giude' Dullah akiendelea kutoa ufafanuzi wa maeneo mbalimbali yaliyotumika enzi za biashara ya Utumwa ikiwemo Misikiti, Gereza na Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan ambaye alikuwa mtawala wa eneo hilo.
Wanafunzi wakielekea kwenye Gereza maarufu lililokuwa likitumiwa na kufunga watumwa.
Muonekano wa Gereza hilo kwa Nje Lango Kuu la kuingia.


Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said (mwenye shati la zambarau) akionyesha Kisima kilichokuwa kikitumiwa na wafungwa ndani ya Gereza hilo.
Wanafunzi wakiangalia Kisima kimoja wapo ndani Msikiti wakati huo.
Mmoja ya wananfunzi wa shule hizo walioitembelea maeneo hayo ya kumbukumbu akishangaa Mzinga uliodumu mpaka leo toka Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
Mafunzo yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi hao.
Moja ya Majengo ya Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan aliyeoa wanawake 77 enzi za utawala wake.
Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said katika picha ya kumbukumbu na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na Phillip Musiba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam katika siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya Utumwa.
Wanafunzi wakisindikizwa na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (mwenye kitenge) kupanda boti kurudi Bandarini baada ya kuhitimisha ziara yao Kilwa Kiswani.

Government clarifies on decision to provide huge tracks of land to Loliondo residents

Tom Cruise visits the Home of Guinness Dublin

$
0
0

GUINNESS WELCOMES HOLLYWOOD’S BIGGEST STAR TOM CRUISE
CRUISE ENJOYS A GUINNESS AHEAD OF PREMIER OF ‘OBLIVION’
  
Wednesday 3rd April 2013, GUINNESS rolled out the red carpet to welcome one of the world’s most famous actors, Tom Cruise at the GUINNESS STOREHOUSE in Dublin, IrelandCruise, joins other global stars such as American President Barrack Obama  who has been seen enjoying a GUINNESS on numerous occasions, most recently for St Patrick’s Day: http://www.whitehouse.gov/blog/2012/03/17/president-obama-dubliner-st-patricks-day
 
Cruise jetted into Dublin today, as part of his worldwide tour for his latest movie,Oblivionaccompanied by highly acclaimed Director Joseph Kosinskiand the lead lady in Oblivion, former Bond girl, Olga Kurylenkoe.


They were treated to a private tour of the Guinness Brewery where Guinness Head Brewer, Colin O’Brien demonstrated the craft behind the brewing process and even handed the reigns over to Cruisewho started his very own brew, which once complete will be specially delivered to Mr. Cruise as a keepsake of his trip to the home of Guinness.


Following the behind the scenes tour of the Brewery, Tom was whisked up to the highest viewpoint in Dublin city, the Gravity Bar at the Guinness Storehouse where Master Brewer Fergal Murray was on hand to teach him how to pour the perfect Guinness.


Cruise who was visibly excited about his surroundings, was then given a ‘windows tour of Dublin’ by Guinness archivist Eibhlin Roche highlighting key landmarks such the Phoenix Park, St. Patrick’s Cathedral, Trinity College and Croke Park

Managing Director at the Guinness Storehouse, Paul Carty said “What an exciting day for everyone in Guinness Storehouse, and indeed in Dublin, to welcome Tom Cruise through our doors. He is an absolute gentleman! We are thrilled he took the time out of his hectic schedule to join us and learn some of the craft and legacy behind Guinness”. 

Standard Bank wins EMEA Finance awards in 2013 for landmark deals

$
0
0

 Standard Bank Group, Africa’s largest bank by assets, has walked away with 11 acccolades at the 2013 EMEA Finance Achievements Awards, including being named best merger and acquisition (M&A) house, best securitisation house and best syndicated loan house in Africa.

This is the sixth consecutive year that Standard Bank has received multiple awards from EMEA Finance, which continue to recognise the group’s leading position in the African capital markets. EMEA Finance is a leading bimonthly global industry publication that reports on the major financial events and happenings initiated and influenced by the international financial industry active in Europe, Middle East, and Africa (the EMEA region).


Some of the notable transactions for which EMEA Finance recognized Standard Bank in 2013 were the group’s work on Tiger Brands’ acquisition of 63.35% of Nigeria’s Dangote Flour Mills and China’s Jinchuan Group’s US$1.3-billion acquisition of JSE listed copper miner Metorex in 2012. Standard Bank was recognized for being the best syndicated loan house in Africa largely because of facilitating the raising of a US$600-million two-year term loan on behalf of the Kenyan government.


The group was also recognised in the following categories:


·         Best sovereign syndicated loan for taking part in Kenya’s US$600-million capital raising;

·         Best supranational syndicated loan for its part in Afreximbank’s US$500-millon, five-year Eurobond issuance;

·         Best M&A deal in Africa for Tiger Brands’ acquisition of Dangote Flour Mills;      

·         Best corporate bond in Africa for facilitating JD Group’s issue;

·         Best IPO in Africa for the listing of Ugandan power distributor Umeme Limited's shares on the Nairobi Securities Exchange;

·         Best follow-on funding in Africa for Dangote Flour Mills of Nigeria, and

·         Best securitisation deal in the EMEA region for SA Home Loans’ recapitalisation


Mr David Munro, Chief Executive of Standard Bank Corporate and Investment Banking said “Standard Bank has a clear, strategic focus on Africa and these awards demonstrate  our desire to provide excellent service to our clients as we work towards the development of the continent we call home”.


Our bank’s deal-making teams across the continent have helped to structure and deliver these transactions for African companies and sovereigns. Leveraging our global footprint, expertise, experience and on-the-ground presence enables us to work with our clients to help them deliver their strategic goals.”


Over the years, Standard Bank has built strong in-country advisory capabilities in a number of key global markets, including South Africa, Nigeria, Kenya, Ghana, Mozambique, China and London, delivering a full range of corporate and investment banking services to clients across various emerging markets. The bank’s strategy is to remain committed to Africa, with a particular focus on natural resources and infrastructure.


The latest EMEA Finance Achievement awards add to Standard Bank Group’s list of accolades already received so far in 2013. These include winning: the African Deal of the Year award for Konkola Copper Mines financing in recognised in the 2013 Project Finance Deal of the Year Awards; Commercial Deal of the Year in the 2013 Trade & Forfaiting Review Deals of the Year for arranging finance for commodities trader Export Trading Group; and being named Best Trade Finance Bank in Africa by Global Finance

Fid Q, Ney Wamitego wafunika Tamasha la Airtel YATOSHA COCO Beach

$
0
0
 Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda maarufu kama Fid Q akitumbuiza wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki.
 Msanii maarufu wa kizazi kipya Sir Juma Nature akimwaga burudani katika tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.
 Msaninii maarufu wa Hip Hop Roma Mkatoliki akiwapagaisha wapenzi wake katika tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki
 Kundi la sarakasi la la jijini Dar es salaam likitoa burdani  kwa maelfu ya watanzania waliohudhuria tamasha la Airtel Yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa Majaji (JB) aliyemiliki jukwaan na msanii nguli wa bongo fleva Sir, Juma Nature  (hayupo pichani) akitoa burdani wakati tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki

 MC  shabani Rugage aka Kidevu cha kuku na MC Aloyce aka  Adam wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki
 Kundi la Kinoko lenye maskani yake Kinondoni likitoa burudani wakati wa wa Tamasha la Airtel yatosha Yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki
 Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda maarufu kama Fid Q akitumbuiza wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki.
 Umati wa watu  waliohudhuria tamasha la Airtel yatosha jijini Dar es saalam wakipata burudani huku wakishika mabango ya kuwashangilia wasanii mahiri wa kizazi kipya katika tamasha la Airtel yatosha Fid Q alionekana kung'ara zaidi
 Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi akibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki
 Msanii wa kundi la Tip top connection Tunda man  akitoa burudani  kwa wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki
Msanii wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop maarufu kama  Ney wa Mitego  akimwaga burudani kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.

========  =========  =========
Fid Q, Ney Wamitego wafunika Tamasha la Airtel YATOSHA COCO Beach Jana, mwisho mwa wiki hii Tamasha kuhamia chalinze.Airtel Tanzania imeendeleza ahadi yake ya kuzunguka nchi nzima kutoa elimu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla ili kuifahamu huduma yao ya AIRTEL YATOSHA pamoja na faida zake

Dokezo lilitolewa na meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema "tunawashukuru sana watanzania wote waliojitokeza Coco beach nakujiunga na huduma yetu nafuu ya Airtel yatosha, wote wameikubali na wameona ukweli wa mambo kwamba kweli Airtel yatosha nyingine ya nini???

Tuwape mpya ya wiki hii ni kwamba tunahamia zetu chalinze, wateja wetu wa mkoa wa pwani sasa ni zamu yenu kupata burudani na elimu ya faida zilizopo ndani ya hii AIRTEL YATOSHA, tutapiga kambi kwa siku mbili yaani Juma mosi na Jumapili paleee kwenye viwanja vya sokoni Chalinze na wasanii kibao na zawadi kibao zitakuwepo

Ni wazi kuwa hii haina kiingilio njoo wewe na mshikaji wako upate burudani na ujifunze kutumia huduma yetu mpya ya Airtel yatosha ambayo ni rahisi kujiunga na kujipatia zawadi ofa kibao ukiunga kwa kupiga *149*99# KISHA utaweza kupata dakika za BURE, Intaneti pamoja na SMS zako za kutuma kwenda mtandao wowote nchini

Wasanii watakaotumbuiza chalinze mwishoni mwa wiki hii ni Fid Q, Juma Nature na wanaume Halisi, Madee na kundi zima la Tip top Connection, pamoja na Ney wa Mitego anaetambasana katika miondoko ya Hip Hop.

usiku wa kumbu kumbu ya Steven kanumba jijini dar

$
0
0


Pichani kushoto ni aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye siku ya kumbu kumbu ya Marehemu Steven Kanumba,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh Yusuph Mwenda akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwa niaba ya Mh Rais Jakaya Kikwete,kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanumba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.


Pichani kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko,Steven Kanumba.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanimba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power. 
Baadhi ya Filamu zilozumuhusisha Marehemu Steven Kanumba enenzi za uhai wake,zilizinduliwa hapo jana kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni Jijini dar.Filamu aliyoishiriki Marehemu kwa asilimia kubwa kabla ya kufariki kwake iliitwa Love & Power sambamba na Filamu nyingine iliyojulikana kwa jina la After Death ambazo zote zinatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni kwa mauzo. 
Pichani kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya IPP Media akipokea tuzo ya heshima kwa niaba ya kampuni hiyo kwa kutoa mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu hapa nchini,kutoka kwa Mama yake,Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho ya kumbu kumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufariki kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko.


Mwakilishi kutoka Kampuni ya Clouds Media Group,Zamaradi Mketema akipokea tuzo ya heshima kwa niaba ya kampuni hiyo iliyotoa mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu hapa nchini,kutoka kwa Mama yake,Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho ya kumbu kumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu afarikii nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko,Steven Kanumba.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama yake Marehemu Kanumba,kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwenye tasnia ya Filamu hapa nchini.
Baadhi wakati wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Kumbu kumbu ya Marehemu Steven Kanumba,ambaye alikuwa akitimiza mwaka tangu kufariki kwake.
Mmoja wa wasanii mahiri katika tasni aya filamu hapa nchini akizungumza machache kuhusiana na filamu yake alioitengeneza kwa ajili ya kumuenzi Marehemu Kanumba,iitwayo After Death iliyojumuisha wasanii mbalimbali wakiwemo chipukizi wa tasnia hiyo,kulia kwake ni mtangazaji wa Clouds TV kupitia kipindi cha Mama Land,Ben Kinyaiya aliyekuwa akiongoza ratiba nzima ya shughuli ya Kumbu kumbu ya Marehemu Kanumba iliyofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Jijini Dar.
Baadhi ya watu mbalimbali waliofika kushuhudia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri hapo jana kwenye viwanja vya Lidaz Club.
Baadhi ya Marafiki wa Marehemu Kanumba enzi za uhai wake kutoka nchini Burundi wakizungumza machache kwa namna walivyomfahamu Kanumba katika mambo mbalimbali.
Mambo yalivyokuwa yakiendelea uwanjani hapo.
Msaniii Babu Ayoub ambaye amekuwa akijizolea sifa kem kem kwa kuigiza sauti mbalimbali za watu maarufu ndani na nje ya nchi,akizungumza machache huku akiwa ameshika chupa yake ya ulabu iliyokuwa ikiwavutia wengi uwanjani hapo.
Msaniii mahiri katika anga ya uchekeshaji,aitwaye Mboto ambaye pia amekuwa akinogesha video nyingi za wanamuziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva akizungumza machache mbele ya mamia ya watu waliojitokeza kwenye kumbu kumbu ya kutimiza mwaka mmoja ya Marehemu Steven kanumba hapo jana.usiku kwenye viwanja vya Lidaz.
Jacline Wolper wakijadili jambo na Mama kanumba.
Waigizaji mahiri Ashaa Boko na Shosti yake wakionesha mbwe mbwe zao jukwaani. 

DR. SALIM AHMED SALIM AONGOZA MAADHIMISHO YA 19 YA MAUAJI YA KIMBARI YALIYOTOKEA NCHINI RWANDA YALIYOFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0

Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mauji ya Kimbari nchini Rwanda.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.

Na pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli ni kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa maashimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.

Katika mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu zake kwa wageni waalikwa pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda wataendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine za Afrika Mashariki ili kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).


Msemaji wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw. Roland Ammousouga akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu wanaweza wakajisifu kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba imetimiza kilio cha maelefu ya waathirika na kuwa imesaidia katika kuleta upatanishi na kuijenga upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani na ulinzi katika ukanda wa Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa kuwakamata wale wote waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda kuwatafuta wahusika 6 waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na kesi zinazowakabili kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria kwamba mapambano dhidi ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi kukamatwa.
Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).
Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika ukumbi wa New World Cinema tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)

Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.


Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dr. Salim Ahmed Salim njiani kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City.

Mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto) wakisubiri kupokea maandamo ya maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar.

Dr. Salim Ahmed Salim akipokea rasmi maandamano hayo.

Watumishi wa vituo vya afya na zahanati nchini watakiwa kuwasilisha oda zao za dawa kwa waganga wakuu.

$
0
0


Na. Catherine Sungura, MOHSW.Morogoro   8/4/2013

Watumishi wa vituo vya afya na zahanati nchini, wametakiwa kuwasilisha mapema oda zao za dawa kwa waganga wakuu wa wilaya mwishoni mwa juma la kwanza la mzunguko wa ugavi shirikishi.


Hayo yamesemwa leo na KAIMU Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alipokuwa akizungumza na wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu, wafamasia pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za Mashirika ya Dini.


Mwaifwani alisema utaratibu huo utawawezesha MSD kutumia majuma nane kuchambua oda, kutengeneza Ankara za mauzo na kuzifungusha na kuzifikisha dawa moja kwa moja kituo cha afya na zahanati ifikapo juma la kumi na mbili.


“ili tuweze kuwahudumia kwa kiwango kizuri tunahitaji hospitali ziwasilishe mahitaji yake siku kumi na nne kabla ili sisi tuweze kujiandaa vya kutosha na kukamilisha oda kwa wakati”. Aidha,alisema kuwa, malalamiko mengi ya kutokuwa na dawa katika vituo vya afya nchini, yanasababishwa na watendaji wasio waaminifu ambao hawazifikishi vituoni.


Mwaifwani alisema hayo Pia alisema wengine huziuza kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi ili kujipatia utajiri wa haraka haraka. “Ili kuzuia mwanya huu, MSD itakuwa inafikisha dawa hadi ngazi ya zahanati na vituo vya afya nchini nzima kuanzia Julai mwaka huu,” alisema.


Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kunapokuwepo na shida ya utendaji au ushauri wowote kuhusu MSD inapaswa kuzitumia ofisi zao za kanda zilizopo nchini nzima, mteja asiporidhika malalamiko hayo yapelekwe katika ofisi yake.


Awali Meneja wa MSD kanda ya Kaskazini, Celestine Haule alisema kuwa, bohari kuu ya dawa nchini ilipewa agizo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii la kufikisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi hadi ngazi ya zahanati.


Alisema lengo lilikuwa ni kupunguza mlolongo mrefu uliopo kwa sasa katika ufikishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma ya afya.


MKUTANO WA WADAU KUHUSU KANUNI ZA MATUMIZI SALAMA YA BAIOTOKNOLOJIA YA KISASA

$
0
0

 Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamuwa Rais Mtaa wa Luthuli JijiniDar es Salaam.{Picha na Ali Meja]
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Kikao cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa, kikao kilihusisha wanasanyansi, wanasheria, Mtandao wa wakilishi wa wakulima na Taasisi za Mbegu.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia mjadala, katika kikao kazi kilichofanyika kwenye  Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava (Kulia) akibadilishana mawazo na Dr. Alois Kullaya kutoka Kituo cha Utafiti cha Mikocheni mara baada ya kufungua kikao cha kanuni za Matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa

==========    =========  =======

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava amewataka wadau kutoka sekta mbalimbali kujadili na kutoa maoni kuhusu utekelezaji wa kanuni za matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa ambazo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na utekelezaji wa Itifaki ya Cartagena chini ya Mkataba wa Hifadhi Bioanuai.

Akifungua kikao kazi, Eng. Mwihava amesema, Tanzania iliridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanuai mwezi machi , 1996 na kufuatiwa  na Mkutano wa wanachama ulioazimia kuandaa itifaki kuhusu  usalama wa Mazingira dhidi ya Athari za Bioteknolojia ya Kisasa.


Itifaki hiyo pamoja na mambo mengine inasisitiza nchi wanachama kuandaa Sheria na kuweka mfumo na mwongozo wa Usimamizi salama wa Mazingira na kulinda afya ya binadamu, bioanuai na wanyama.


Aidha, lengo la teknolojia ya Kisasa ni kukidhi haja ya kuimarisha ubora, kudhibiti magonjwa, kuhimili ukame na kukuza uzalishaji. Hata hivyo imebainika kuwa bado kuna wasiwasi wa athari zinazoweza kupatikana kutokana na teknolojia hiyo endapo itatumiwa bila kufuata utaratibu. “kwa hiyo tumewaita ili kujadili na kutoa maoni kuhusu utekelezaji wa Kanuni hizi ili tupate mwelekeo wa suala hili na kuishauri Serikali’. Alisisitiza Eng. Mwihava.


Akitoa maezo ya awali, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu amesema kuwa lengo la kanuni hizo si kuzuia au kukwamisha matumizi ya Bioteknojia hapa nchini bali ni kuhakikisha nchi inanufaika na matumizi hayo kwa kuzingatia usalama wa afya ya binadamu na Mazingira.


Aidha baadhi ya wadau katika kikao hicho walikuwa na maoni tofauti na kuitaka Serikali kupitia upya kanuni na kufanya tathmini ya kuondoa ama kuacha kuondoa kipengele cha Strict liability. Mkutano huo umehusisha wanasheria, wanasayansi, Mtandao wa wawakilishi wa wakulima na Taasisi za Utafiti za Mbegu, hususan Pamba na Mahindi.

Na Lulu Mussa

Afisa Habari

Ofisi ya Makamu wa Rais


Msanii wa hip hop Roma alivyoifumua coco beach ndani ya airtel yatosha wikend.

Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC ikulu jijini Dar leo,Pia apongeza walioshiriki Zoeazi la Uokozi Ajali ya Jengo la Ghorofa Dar

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC Bwana Daniel Yohannes ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akioongea na makundi mbalimbali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama vilivyoshiriki katika zoezi la uokozi wakati wa ajali ambapo jengo la ghorofa liliporomoka , kuuwa na kujeruhi watu kadhaa katikati ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibun.Hafla hiyo fupi ilifanyika katika ukumbi wa Sabasaba katik viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova kwa uendeshaji wa Zoezi la uokoaji katika ajali ya Jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kijana mlemavu Shabani Selemani Mohamed katika ukumbi Sabasaba kutoka viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa ,wakati wa hafla fupi ya kupongeza makundi mbalimbali yaliyoshiriki katika kazi ya kuokoa watu na kuopoa miili wakati wa ajali ya kuanguka kwa ghorofa katikati ya Jiji la Dar e Salaam hivi karibuni.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ walishiriki katika kazi ya kuokoa watu wakati wa ajali ya kupomoka kwa jengo katikati ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.picha na Freddy Maro.

RAIS KIKWETE AWASILI NAIROBI JIONI HII TAYARI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS WA NNE WA KENYA MHE UHURU MUIGAI KENYATTA KESHO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wakipozi na wasichana waliowazawadia mashada ya maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wamesimama pembeni na wenyeji wao. PICHA NA IKULU.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images