Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 601 | 602 | (Page 603) | 604 | 605 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mgombea urais wa chama cha ADC,  Zanzibar, Hamad Rashid Hamad, akihutubia katika mkutano huo.
   Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha mgombea mwenza wake, Said Miraji (kulia), katika mkutano mkuu wa tatu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo. Kushoto ni mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad.
   Makamu Mwenyekiti wa ADC, Zanzibar, Faki Hamisi Silima, akizungumza katika mkutano huo.
   Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (kulia), na mgombea mwenza wake, Said Miraji, wakiwapungia mkono wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu huo.
   Katibu Mkuu wa chama hicho, Lydia Bendera akimpongeza. Said Miraji kwa kuteuliwa kuwa  mgombea mwenza.
   Makada wa chama hicho wakiwa na furaha kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea. 

  0 0

  Makamu wa Rais Wa Kenya, Mh William Rutto akifungua maonyesho ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival yajulikanayo kama JAMAFEST kwa kuwakaribisha washiriki kutoka nchi zote za Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Kenyatta uliopo jijini Nairobi, Nchini Kenya.Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta kabla ya ufunguzi wa maonyesho ya JAMAFEST 2015
   Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Makumira wakitoa burudani ya ngoma wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamadanu Festival yajulikanayo kama JAMAFEST katika ukumbi wa mikutano wa kimtaifa wa Kenyatta.
   Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya JAMAFEST 2015 kutoka nchini Burundi wakiwa katika viwanja vya KICC Nairobi Kenya.


  Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
  Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto amempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na kupelekea Wananchi wa Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki kupenda zaidi filamu za Kitanzania ambazo zimekuwa na soko kubwa sana katika nchi za Jumuiya ya Mashariki.
  Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni lijulikanalo kama JAMAFEST 2015 linalofanyika katika viwanja vya ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta uliopo katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya, Mh Rutto pia aliwapongeza marais wa nchi za Jumuiya Ya Afrika Mashariki kwa juhudi zao katika Shughuli mbalimbali za kijamii, uchumi, utamadanu na Michezo.
  Mh Rutto alitoa pongezi kwa Rais Wa Rwanda, Mh Paul Kagame kwa kutoa mchango mkubwa sana katika Michezo kwa kudhamini Michuano ya Kombe la Kagame ambapo mwaka Huu Timu ya Azam FC kutoka Nchini Tanzania iliweza kuibuka mshindi kwa kuifunga Timu yao ya Kenya Gor Mahia kwa mabao Mawili kwa sifuri. 

  Vilevile Mh Rutto aliipongeza timu ya Azam kwa kuweza kuwa mabingwa wa Kombe la Kagame kwa kuweza kuifunga timu yao ya Kenya ya Gor Mahia na kuweza kuibuka washindi wa Kombe la Kagame linalodhaminiwa na rais wa Rwanda Nh Paul Kagame.  

  Mbali na Kumpongeza rais wa Rwanda na Tanzania pia Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto aliwapongeza pia rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kuwa mstari wa mbele katika Kukuza utamaduni wa Nchi yake huku Rais wa Burundi akipongezwa Kwa Kuweza kusakata kabumbu na kusema kuwa anatamani awe rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).
  Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni (JAMAFEST) yameshirikisha nchini zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Kila Nchi mwanachama wameweza kuonyesha Bidhaa zao pamoja na utamaduni wao. Maonyesho haya ya JAMFEST hufanyika kila baada ya Miaka Miwili ambapo mwaka 2013 Maonyesho haya yalifanyika nchini Rwanda na mwaka huu yanaendelea kufanyika Nchini Kenya huku mwaka 2017 maonyesho haya yanatarijiwa Kufanyika Nchini Tanzania.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gosbert Kamugisha, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya siku tatu ya miradi na ubunifu wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi kutoka shule 120 nchini. Maonyesho hayo yatafikia kilele Ijumaa Agosti 7, 2015. (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
  Mwanzilishi Mwenza wa YST, Joseph Clowry, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii. 
  Makamu wa Rais wa kampuni ya kuchakata mafuta na gesi ya BG Tanzania, John Ulanga, akizungumzia udhamini wao katika maonyesho hayo ya YST. Kampuni hiyo imetoa kiasi cha Dola 200,000 kudhamini maonyesho ya mwaka huu. 

  Naibu Balozi wa Ireland nchini, Brian Noran, akizungumzia maendeleo ya tafiti za kisayansi kwa taifa lolote duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha.
  Mkutano ukiwaunaendelea. 
  Wanahabari wakiwa kazini. 
  Wanahabari wakifuatilia kwa makini. 
  Mwalimu Geofrey Ndunguru (kulia) na mwanafunzi Yussuph Mwenda kutoka Shule ya Sekonari ya Wavulana Songea nao wanashiriki maonyesho hayo kuzungumzia Uchambuzi wa Mtazamo wa Wanafunzi Wasioona kuhusiana na Sayansi. 
  Mwanafunzi Gladness Mpelemba (kulia) wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Sumaye mjini Morogoro akielezea kuhusu utafiti wao wa 'Kutumia Njia za Asili za Kupanga Uzazi Kupunguza Madhara kwa Wanawake'. Kushoto ni mwenzake Glory Crispine. 
  Wanafunzi wakiendelea kuonyesha tafiti zao. 
  Mojawapo ya utafiti uliofanywa na wanafunzi Saada Abeid na Zaina Maliki wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara. 
  Majaji wakiwa kazini leo hii ili kuwapata washindi watakaotunukiwa zawadi mbalimbali hapo kesho ambapo Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

  Na Daniel Mbega

  MAONYESHO ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini yamfunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam leo yakiwa yanaendeshwa na kuratibiwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST).Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwenye Ukumbi wa iamond Jubilee yanashirikisha jumla ya wanafunzi 240na walimu 120 kutoka shule 120 nchini yanatarajiwa kufikia kilele keshokutwa Ijumaa ingawa kesho Alhamisi zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi zikiwemo fedha taslimu, medali, vikombe, vifaa vya maabara pamoja na maktaba.
  Dk. Gosbert Kamugisha, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa YST, amesema mgeni rasmi atakayetoa zawadi kwa washindi hapo kesho atakuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

  “Maonyesho haya ni kwa ajili ya kuonyesha ubunifu na utafiti wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi wa sekondari na katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo wanafunzi hao wataonyesha miradi mbalimbali katika maeneo tofauti ya kisayansi kama kemikali, fizikia na sayansi ya hisabati, sayansi ya kibaolojia na kiikolojia, sayansi ya kijamii na kitabia, na teknolojia,” alisema Dk. Kamugisha.

  Aliongeza kwamba, kama njia ya kutambua kazi iliyofanywa na wanafunzi hao, ndiyo maana wameandaa zawadi mbalimbali kuwamotisha ambapo mbali ya zawadi zilizotajwa, pia wanafunzi sita wanaweza kupata udhamini (scholarship) kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu kwa fani mbalimbali za sayansi na teknolojia, udhamini ambao hutolewa na taasisi binafsi ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam.

  “Maonyesho ya mwaka 2015 ya YST yanalenga kuonyesha vipaji na ubunifu wa wanafunzi wa sekondari, lakini pia ushuhuda wa umahiri wa mbinu za ufundishaji kwa walimu ambao ndio wanaowaongoza wanafunzi hao yakiwa ni matunda ya mafunzo yanayotolewa na YST kwa walimu wa sayansi katika kipindi cha miaka minne iliyopita,” aliongeza Dk. Kamugisha.

  Amewataja wadhamini wakubwa wa maonyesho ya mwaka huu kuwa ni kampuni ya BG Tanzania inayojihusisha na masuala ya utafiti wa mafuta na gesi asilia pamojana Shirika la Kimataifa la Misaada la Ireland (Irish Aid).

  Akizungumzia mafanikio ya maonyesho hayo, Dk. Kamugisha alisema mwitikio umekuwa mkubwa zaidi tofauti na walipoanza maonyesho hayo mwaka 2011.

  “Wakati tulipoanza mwaka 2011 walishiriki wanafunzi nane tu, mwaka 2012 wakawa 300 kwani zilikuwepo shule 100, mwaka 2013 walishiriki wanafunzi 200, mwaka 2014 pia walikuwepo wanafunzi 200 lakini mwaka huu wamekuwa 240 kwani hata shule zimeongezeka kutoka 100 hadi 120.

  “Tulipokea maombi ya shule 400 nchi nzima, lakini tukaamua kuzichagua hizi 120. Tulizitembelea shule zote 400 mara tatu kwa mwaka, ndipo hatimaye tukaziteua hizi zinazoshiriki ingawa tunaamini kwamba shule nyingi sasa zimehamasika na watoto wanapenda sayansi,” alisema.

  Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mwanzilishi Mwenza wa YST Joseph Clowry, alisema kwamba kuna dalili za mafanikio tangu walipopata wazo la kuanzisha taasisi hiyo mwaka 2009, kwani mwitikio umeonekana kuwa mkubwa kadiri miaka inavyokwenda.

  Alisema, ili taifa lolote liendelee, ni vyema kuwekeza zaidi katika tafiti za kisayansi kwa kuanzia kwenye ngazi za chini kabisa kama wao wananvyofanya.

  “Ireland ilikuwa nyuma kimaendeleo kama zilivyokuwa nchi nyingi ulimwenguni, lakini walipoamua kuwekeza kwenye sayansi hali imebailika hivi sasa ambapo wapo wanasayansi mahiri kabisa na vijana nao wanapenda kujifunza masomo ya sayansi,” alisema Clowry.

  Kwa upande wake, Makamu Rais wa BG Tanzania anayeshughulikia Sera na Masuala ya Uhusiano, John Ulanga, alisema wameamua kujitolea kudhamini YST kwa sababu wanatambua kwamba Tanzania inahitaji kuwa na wanasayansi wengi hasa tunapozungumzia suala la mafuta na gesi ambayo yakitafitiwa yakapatikana na kuchakatwa yanaweza kuinua uchumi wa taifa kwa kiwango kikubwa.

  “Tunahitaji wanasayansi wa kutosha katika sekta hii adhimu ya mafuta na gesi, tukiwa nao wazalendo itakuwa ni bora zaidi, hivyo ni lazima tuwadhamini watu kama YST ambao wanajenga msingi imara katika kuwapata wataalamu wa kesho,” alisema Ulanga.

  Ulanga alisema kwamba, kwa mwaka huu kampuni yake imetoa Dola 200,000 (takriban Shs. 450 milioni) kwa ajili ya udhamini wa maonyesho hayo na akaahidi kwamba wataendelea kudhamini kwa kadiri ya mahitaji na hali itakavyoruhusu.

  Naye Brian Noran, Naibu Balozi wa Ireland nchini, amesema ni jambo la busara kwa serikali na jamii kuwekeza katika utafiti wa kisayansi kama kweli taifa linataka maendeleo, lakini akaahidi kwamba serikali yake itaendelea kusaidia kwani inatambua umuhimu wa kuwa na wanasayansi wabunifu.

  Aliwapongeza YST kwa hatua waliyoifikia mwaka huu na kuwahamasisha waongeze bidii zaidi ili kujenga taifa la wanasayansi kwa kuanzia ngazi ya chini.

  “Sayansi ndiyo inayoweza kuleta mabadiliko na maendeleo, hivyo ni muhimu kuendelea kuwazalisha wanasayansi ambao watakuja kuwa wabunifu wazuri hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia,” alisema Noran.

  (IMEANDALIWA NA www.brotherdanny.com. Simu 0656-331974)
  0 0

   Wanachama wa chama cha ADC wakishangilia mara baada ya kumtangaza mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
  Wanachama wa chama cha ADC wakipata urudani kutioka kwa kijana wao wa burudani katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kumtangaza mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,mgombea urais wa Zanzibar na mgombea mweza katika nafasi hiyo, katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
  Katibu mkuu wa chama cha ADC, Lidia Bendela akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ADC ambao walikuwa wanawatangaza wagombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wa Zanzibar pamoja na Mgomea mwezakatika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
  Mgombea wa Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Chifu Lutalosa Yemba akigombea nafasi ya uraiskupitia chama cha ADC akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwania nafasi hiyo leo katika mkutano wa kamati kuu wa chama cha ADC  uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa chama cha ADC na Mgombea wa urais kupitia chama cha ADC, Said Miraji Abdala akizungumza mara mbaada ya kutangazwa kugombea nafasi ya mombea mweza kupitia chama hicho leo katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
   Mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano watanzania kupitia chama cha ADC, Chifu Lutalosa Yemba na Mgombea wa urais wa Zanzibar,Hamad Rashid Mohamed wakipunga bendera za chama chao kuashiria ushindi wa kuwania nafasi za juu uongozi katika chama hicho, katika mkutano wa Kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo,Blogu ya Jamii.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza mbele ya Mabalazi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Luis Manuel Cuesta Civis.  Katika hotuba yake Mhe. Membe alimshukuru Balozi Luis kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Hispania. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Agosti, 2015.
  Balozi Luis (kulia) kwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia ni Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (wa pili kulia), Balozi wa Zimbabwe na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kushoto) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
  Balozi Luis akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo nchini.
  Sehemu ya Mabalozi na wagenui waalikwa wakimsikiliza Balozi Luis (hayupo pichani)

   
  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akizungumza machache wakati wa hafla hiyo
  Mhe. Waziri Membe kwa pamoja na Mhe. Balozi Luis, Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Sokoine ambaye haonekani pichani
  Bi. Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza
  Balozi Luis akimweleza jambo Waziri Membe
  Maafisa Mambo ya Nje walioshiriki hafla hiyo. Kushoto ni Bi. Olivia Maboko na Bi. Tunsume Mwangolombe Mhe. Membe na Mhe. Luis wakitakiana afya njema
  Mhe. Membe akimkabidhi zawadi Balozi Luis
  Waziri Membe akizungumza na Balozi Luis
  Waziri Membe akiagana na Balozi Luis mara baada ya hafla hiyo
  Balozi Luis akiagana na Balozi Sokoin
  Picha ya pamoja

  0 0

  LIP1
  Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafuasi wa chama hicho waliojitokeza katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam,na kuwaambia kuwa CUF ni Taasisi,hivyo wanachama wote wanatakiwa kukijenga chama hicho wawe na vyeo ama wasiwe na vyeo kazi kubwa ni kukijenga chama cha CUF,Pro Lipumba aliyasema maneno hayo bila kutoa ufafanuzi wa kina.

  Profesa Lipumba alitakiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho,lakini mpaka dakika za mwisho hakufanya mkutano huo badala yake alikuwa na kikao na wazee wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa dini na wanachama,aidha wakati akiondoka katika ofisi hizo ndipo akazungumza maneno hayo hakuyafafanua zaidi.
  LIP2
  Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam
  LIP3
  Baadhi ya wanachama wa chama cha CUF wakiwa katika makao makuu ya chama hicho wakipiga kelele kuashiria kumuunga mkono mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba.
  LIP4
  Wana CUF wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika makao makuu ya chama hicho Buguruni kumsikiliza Mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba 
  LIP5
  Mpiga Picha wa Gazeti la Uhuru Emmanuel Ndege akisaidiwa na waandishi wenzake mara baada ya kujeruhiwa na feni wakati waandishi hao wakisubiri Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza nao katika makao makuu ya chama hicho Buguruni.PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG.
   
  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jami.
   
  MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),amewataka wanachama wa  chama hicho kukijenga kwa nafasi walizonazo iwe kiongozi au mwanachama wa kawaida.
   
  Lipumba ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama waliofika katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho wakitaka kauli ya yake juu ya chama na taarifa zilizopo katika mitandao juu ya kutaka kuachia nafasi yake uenyekiti wa chama hicho.
   
  Lipumba  amesema kuwa chama ni taasisi sio chama mtu mmoja anaweza kufanya kila kitu hivyo wanachama tambueni hivyo.
   
  Aidha amewataka wanachama waisome katiba ya chama hicho kwa sababu zipo ili kuweza kujua chama jinsi kinavyoendeshwa kutokana na katiba ambayo inapitishwa na wanachama.
   
  Wakati huo huo  mkutano ulitishwa na chama hicho kwa lengo la Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa,Ibrahim Lipumba umearishwa kutokana na wazee wa chama hicho kuvamia Ofisi hiyo na kwenda kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho.
   
  Akizungumza wakati kuarisha Mkutano huo Mwenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu Bara,Magdalena Sakaya amesema kuwa mkutano huo ulikuwa wa mwenyekiti Lipumba lakini wazee wa chama wamevamia hivyo hawezi kuzungumza tena.
   
  Sakaya amesema kitu ambacho alikuwa anataka kuzungumza anajua mwenyewe hivyo haiwezekani mtu mwingine azungumze kitu cha mwenyekiti.
   
  “Jamani tunaahirisha mkutano wetu ambao ulitakiwa kuzungumzwa na mwenyekiti lakini wazee wa chama wamevamia ofisi na kuwa na mazungumzo na mwenyekiti”amesema Sakaya Naibu Katibu Mkuu Bara.

  0 0

   
  Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Raymond Mapunda akitoa matokeo ya mtihani wa Utimilifu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari jijini Dar es salaam ambapo katika mtihani huo uliofanyika Mei 25 hadi Juni 12 mwaka huu shule Binafsi zimeongoza kwa ufaulu.

  Na.Aron Msigwa -MAELEZO.
  MATOKEO  ya mtihani wa Utimilifu kwa wanafunzi wanaosoma kidato cha nne katika shule za  Sekondari za jiji la Dare es  salaam yametolewa leo jijini Dar es salaam yakiwa na alama za juu  za ufaulu kwa wanafunzi wanaosoma   Katika  shule   zisizomilikiwa na Serikali.

  Akitoa matokeo hayo, Afisa Elimu wa Mkoa huo Bw.Raymond Mapunda amesema kuwa ufaulu mzuri umeonekana zaidi katika shule Binafsi kuliko za serikali kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa na walimu wa shule hizo.

  Amesema kuwa licha ya mkoa wake kuwa na idadi ya walimu wa kutosha katika shule zinazomilikiwa na Serikali bado wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hizo wamefanya vibaya ikilinganishwa na wale wanaosoma shule binafsi.

  Amesema mtihani huo ulifanyika Mei 25 hadi Juni 12,2015 mwaka huu  na ulihusisha shule 292  na kuongeza kuwa wanafunzi wapatao 40,356 walisajiliwa kufanya mtihani huo.

  Bw.Mapunda amesema kati ya hao 39,480 ambao ni sawa na asilimia 97.8 walifanya mtihani huo huku 876 ambao ni sawa na asilimia 2.2 walishindwa kufanya mtihani huo kutokana na sababu za ugonjwa na utoro.

  Ameeleza kuwa kutokana na idadi iliyosajiliwa, wanafunzi 37,560 wamefaulu mtihani huo kulingana na madaraja mbalimbali yaliyoainishwa, huku idadi kubwa ya wanafunzi wapatao 26,265 imeangukia katika daraja la mwisho la ufaulu.

  "Uchambuzi wa kina tulioufanya umeonesha shule za Serikali zilizo nyingi zinazochukua wanafunzi 28,273 hazikufanya vizuri ikilinganishwa na shule Zisizo za Serikali zenye idadi ya wanafunzi 11,207 hivyo Maafisa wa Elimu wa Manispaa waendelee kufuatilia kwa karibu hali hii" Amesisitiza.

  Aidha, amezitaja shule kumi bora za Serikali zilizofanya vizuri kimkoa  katika mtihani huo kuwa ni pamoja na Jangwani,Pugu,Kisutu,Zanaki,Chang'ombe,Azania,Dar es salaam,KIbasila,Ilala na Benjamin Mkapa.

  Kwa upande wa Binafsi amesema ni pamoja Main Green Hill,Canossa ambayo imeshika nafasi 5 mfululizo ikifuatiwa na Feza Boys nafasi 3 mfululizo na shule ya Sekondari Alpha.

   Ameongeza kuwa katika matokeo matokeo ya shule zote wasichana wameongoza kwa kuwa na ufaulu wa juu kuliko wavulana.

  "Napenda kuwafahamisha wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuwa matokeo haya yanaendelea kuchambuliwa kimasomo na kwa gredi na uchambuzi wote utawekwa kwenye tovuti ya Mkoa wa Dar es salaam ya www.dsm.go.tz ili kilia mdau ,shule,mwalimu na mwanafunzi aweze kuyatumia

  0 0

  ALIYEKUWA Mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama "Ndesa Pesa", amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko mapumzikoni, Dkt. Wilbroad Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

  Ndesamburo alifuatana na makada wenzake wa chama hicho, baadhi yao ni Meya wa Manispaa ya Moshi ambaye pia ni mgombea ubunge (mtarajiwa), wa jimbo hilo, Japhary Michael.
   
  Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya nini wamezungumza, ingawa makada hao wa CHADEMA walikuwa jijini kuhudhuria mkutano mkuu maalum wa chama hicho uliomteua Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya mwavuli wa muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA. Mgombea mwenza aliyeteuliwa ni Mh. Juma Duni Haji.  

  0 0

  SAM_4837
  MAGWIJI WA UBUNIFU WA NGUO NA WATAALAMU WA USHAURI WA NGOZI WANAPENDA KUWATAARIFU WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA KUWA TAREHE 9/8/2015 KUTAKUWA NA UZINDUZI WA TAWI LA DUKA LA VIPODOZI LA FLORA SHOW ITAKAYOFANYIKA SIKU YA JUMA MOSI KATIKA HOTELI YA KITALII YA SNOWN CREST

  KATIKA UZINDUZI HUO PIA UTAPAMBWA NA SHOW YA KUKATA NA SHOKA AMBAPO MAGWIJI WA UBUNIFU WA MAVZI WATONYESHA MAVAZI YA AINA MBALIMBALI IKIWEMO YA HARUSI ,VAZI LA HARUSI YA KIMAASAI PAMOJA NA VAZI LILILOMPA USHINDI SAIDA KESY

  MTAALAMU WA USHAURI WA NGOZI HAPA NCHINI KENEDY MLAWA ATATOA USHAURI JUU YA VIPODOZI VINAVYOENDANA NA NGOZI YAKO

  KIINGILIO NI SHILINGI 10,000/= BADALA YA SHILINGI 30,000/=IKIWA KAMA OFA YA SIKUKUU YA NANENANE.
   
  WADHAMINI WAKUU NI ZINDUKA MWANAMKE NA FLORA SHOW AMBAPO TIKETI ZINAPATIKA KATIKA OFISI YA ZINDUKA MWANAMKE NANE NANE,DUKA LA FLORA SHOW NANENANE,STENDI KUBWA YA MABASI JENGO LA KILUVIA KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA KWA SIMU NO,0755 950158
  MUDA SAA KUMI NA MBILI JIONI…NYOTE MNAKARIBISHWA!

  0 0

  Licha ya mtaa wa Mbweni JKT, jijini Dar es Salaam kujengwa majumba ya kifahari na kupatikana pia nyumba za viongozi mbalimbali wa serikali, miundo mbinu yake, hususan daraja linalojengwa katika eneo hilo ili kuwafanya wananchi wapite kwa urahisi kusua sua. Kwa miaka kadhaa sasa ujenzi wa daraja hilo umesimama.  Pichani ni gari la mwananchi na mkazi wa eneo hilo akipta kwenye maji ambayo mara kadhaa hujikuta wamesimama kwa saa kadhaa, hususan kama eneo hilo litajaa baada ya eneo hilo kujaa maji yanayotoka baharini.  Hali hiyo si tu inakwamisha maendeleo, pia ni hatari kwa usalama wa wananchi kwenye eneo hilo. Wananchi wengi wameonekana kuichoka hali hiyo na kuiomba serikali kulifanyia kazi daraja hilo ili kuwafanya wananchi waingie na kutoka bila usumbufu wowote kama unaotokea wakati huu.
  Kambi ya JKT Mbweni ikiwa tulii. Ujenzi wa daraja hilo umekwama. Wananchi hawajui ujenzi huo umekwamia wapi. Baadhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu walimuomba Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda na Mkurugenzi wake kuangalia namna gani mradi huo umesimama kwa miaka mitatu sasa.
  Linaloonekana nyuma ya kibao cha tangazo la Halmashauri ni daraja linalojengwa kwenye eneo la Mbweni JKT ambalo hata hivyo limesimama na kuleta adha kubwa kwa wakazi na wananchi wa eneo hilo kwa miaka mitatu sasa. Wananchi hao wameendelea kutaabika hasa sehemu hiyo inavyopokea maji mengi kutoka baharini kila wakati. Picha zote za Mpiga Picha Wetu.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo Upanga jijini Dar es salaam alipokwenda kwenye msiba wa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, aliyefariki dunia Jumatatu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu8 ya figo. Marehemu Mzee Kisumo alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa wanasiasa wakongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, aliyefariki dunia Jumatatu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu8 ya figo. Marehemu Mzee Kisumo alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.PICHA NA IKULU

  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kukamilika kwa zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu kwa kutumia mfumo wa BVR Mkoani Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani zoezi hilio limefanikiwa kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizojitokeza.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose Migiro, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi Mhe Shaaban Ally Lilla na Katibu Mkuu kiongozi katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu 13 na Jaji wa Mahakama ya Rufaa mmoja aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2015. PICHA NA IKULU

  0 0

   Meneja Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Emma Oriyo  (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam , kuhusu maandalizi ya uzinduzi Programu ya mafunzo ya kuendeleza wauzaji wadogo wadogo wa vinywaji vya TBL nchini. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Dar es Salaam, Abel Swai 
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Dar es Salaam, Abel Swai (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya uzinduzi Programu ya 
  mafunzo ya kuendeleza wauzaji wadogo wadogo wa vinywaji vya TBL nchini. Kulia ni  Meneja wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa TBL,Emma Oriyo 

  0 0

  SAM_4795Wafanyakazi wa Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,wakiwa katika banda lao la matangazo katika viwanja vya nane nane Themi njiro jijini Arusha (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_4802Mtangazaji maarufu ndani na nje ya Arusha Semio Sonyo wa kituo cha Redio 5 akirusha matangazo moja kwa moja katika maonyesho ya nane nane,kushoto Meneja masoko wa kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha, Bi.Sarah Keiya
  SAM_4789
  Taswira katika banda la kituo cha Redio 5 wakirusha matangazo yao moja kwa moja katika maonyesho ya nane nane Themi njiro jijini Arusha

  Meneja masoko wa ampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha, Bi.Sarah Keiya amesema kuwa kila wanaposhiriki maonyesho ya nane nane kila mwaka kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha wanawafikia wakulima,wafugaji na wafanyabiashara katika maonyesho hayo ya nane nane

  Pia alisema kwa mwaka huu kutakuwa na mashindano ya kila aina ikiwemo la shindano la kuimba,kurup,kula na kunywa,vipaji vya danadana huku akiweka wazi kuwa zawadi zipo kwa washindi wa shindano hilo
  0 0

  IMG_1853Aliyevalia shati la blue ni Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia akiondoka katika banda la kampuni yaSimba Cement mara baada ya kutembelea banda hilo katika viwanja vya nane nane Themi jijini Arusha ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kenya plant helth inspectorate service Bi.Esther Kimani(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  IMG_1863Wananchi wakipata elimu katika banda la Simba Cement katika maonyesho ya nane nane ya kandaele ya kaskazini yanayoendelea katika viwanja vya njiro Themi jijini Arusha
  IMG_1851(1)Ugeni kutoka kenya wakiongozwa na Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia wakipata maelezo katika banda la Simba Cement 
  SAM_4855Afisa masoko Mkuu wa kampuni  ya Simba Cement Leslie Massawe kushoto akitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda lao katika maonyesho ya nane nane
  SAM_4853
  Tafiti zimeonyesha kuwa baadhi ya watumiaji wa saruji hapa nchini hawafati viwango vilivyowekwa na hivyo hupelekea kupata bidhaa isiyo bora kwa watumiaji wa bidhaa hiyo

  Hayo yamebainishwa na afisa masoko Mkuu wa kampuni  ya Simba Cement ambao ni watengenezaji wa Saruji  ,Leslie Massawe wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembea banda lao katika maonyesho ya nane nane ,kanda ya kaskazini  jijini Arusha

  Massawe alisema kuwa utafiti uliofanywa na kampuni yao ya saruji inaonyesha kuwa baadhi ya wajenzi hawafuati  mchanganyiko unaokubalika baina ya saruji,mchanga,kokoto hivyo inapelekea kupata matofali yaliyochini ya kiwango 

  “Bidhaa zetu ni matokeo ya utafiti wa kina na uboreshaji makini unaofanywa na wataalumu wetu kupitia ujuzi wao wenye sifa zinazozingatia viwango vya ubora wa simenti Tanzania”alisema Massawe

  Aidha alisema kuwa wanautarabu wa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wateja wao pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya saruji ,katika ujenzi wa sekta mbalimbali sanjari na uzalishaji wa viwandani hali itakayosaidia upatikaniji wa ujenzi wa nyumba imara na miundombinu bora

  Alitoa wito kwa wananchi kupata elimu ya matumizi bora ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi kabla ya kuanza ujenzi,huku akiwataka mafundi ujenzi  na watengenezaji wa matofali kutenga muda wa kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa na kampuni za saruji


  0 0

   Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja  na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.
  

                                 Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.
   Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
  Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.

   Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta pamoja na Mkewe Agnes Mutta.
                 Mhe Balozi Liberata Mulamula akitoa  pasi yake ya kusafiria kwaajili ya kujisajili tayari kwa kuondoka.
                          Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika hatua za mwisho za usajili.
                             Mhe Balozi Liberata Mulamula tayari usajili ulipokamilika
  Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na familia zao.
  Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari anajiandaa kwa ukaguzi wa mwisho na kuelekea kwenye ndege.
   Kwa pamoja tunasema Safari Njema na Ubarikiwe Sana Balozi Mulamula daima tutakukumbuka.                    PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada katika semina hiyo leo ofisi za WLF. Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada katika semina hiyo leo ofisi za WLF.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani. Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.Waandishi wa Mitandao ya Kijamii Wapewa Elimu ya Afya na UzaziMeneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani. Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.

  BAADHI ya wanahabari wa mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam wamepewa mafunzo juu ya taarifa za uzazi na afya ya mama na mtoto ili waweze kuelimisha zaidi jamii kupitia mitandao yao dhidi ya taarifa hizo. 

  Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu alisema taasisi yake imeamua kutoa mafunzo hayo kwa wanahabari hao ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii kupitia mitandao yao juu ya umuhimu wa kupambana na vifo vya mama na mtoto vinavyoendelea kutokea kila uchao.

   Alisema kazi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto si jukumu la madaktari au hospitali pekee lakini jukumu la jamii nzima kukabiliana na huduma hiyo, alisema vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii inakilasababu za kuonesha mapungufu na kueleza changamoto katika huduma za afya zinazotolewa kwa lengo la kuboresha zaidi huduma hizo.

   Alisema tatizo la elimu ya afya ya uzazi ni kubwa nchini kwani takwimu zinaonesha kwa kila saa moja kuna mama anayepoteza maisha kutokana na matatizo ya uzaziSerikali. "...Kila siku kuna akinamama takribani 24 wanapoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi nchini," alisema Dk. Mwakatundu. 

  Awali akizungumzia hali halisi ya uzazi wa mpango nchi, Meneja Mawasiliano wa WLF, Victoria Marijani alisema kuna faida kuwa ya kuzingatia Uzazi wa Mpango kwani ni uwekezaji wenye faida na endelevu ambao unachangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 44. 

  Aliongeza kuwa uwekezaji huo wa ziada katika afya, elimu, usawa wa kijinsia na uwepo wa sera wezeshi za kiuchumi vitaiwezesha nchi kupata manufaa yatokanayo na ukuaji wa haraka wa uchumi. Alisema familia zinazotumia uzazi wa mpango zinakuwa na uwezo wa kuwatimizia watoto mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu, mavazi, huduma za afya na makazi. 

  "...Atapata muda wa kushiriki katika shughuli za jamii, Atamudu kujiwekea akiba, Atakuwa na amani na upendo kwa familia yake. Alisema kiwango kikubwa cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 (vifo 81 kwa vizazi hai 1000) Kiwango kidogo cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango (Asilimia 27). Wastani wa utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango hapa nchini bado ni mdogo. Ni asilimia 27 tu ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa ndio wanaotumia njia za kisasa za Uzazi wa Mpango. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

   Naibu Mwenyekiti Ofisi Kuu ya Hijja Tanzania (BIITHA), Yusuf Musun (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kusogezwa mbele muda wa kujisajili kwenda Hijja kutoka Juni 15 hadi Agosti 25 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Habari wa Biitha, Hamisi Tembo na Mratibu wa Biitha, Abdallah Khalid.
   Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
  Mkutano na wanahabari ukiendelea.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
  0 0

  Mhandisi Kisaka kutoka TCRA makao makuu akitoa somo kwa viongozi wa vyombo vya habari kanda ya Nyanda za juu kusini.

  Na Edwin Moshi, Mbeya
  Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuwa makini na kuripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka huu kufuata maadili na weledi wa taaluma hiyo ili kufanikisha uchaguzi huo kwa amani

  Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wakati wakiwapa semina mameneja na wamiliki wa vyombo vya habari vilivyopo kanda ya nyanda za juu kusini semina iliyofanyika jijini Mbeya

  Akizungumza katika semina hiyo wakati wa hotuba ya kufungua semina hiyo Naibu Mkurugenzi idara ya utangazaji TCRA makao makuu Bw. Fredrick Ntobi amewasisitiza waandishi wa habari kote nchini kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao ili kuepuka madhara yatakayoweza kujitokeza pindi watakapotoa taarifa potofu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu na chaguzi nyingine zitakazofuata baada ya uchaguzi huo

  "Naomba muwe makini na uandishi wenu wa habari maana ninyi ninyi ndio mtakaofikishwa mahakamani, ninyi ndio mtakaofikishwa The Heag, ajirini watu wenye professional (taaluma) ya habari, hii itasaidia kuepuka kauli za uchochezi, zitawamaliza na niwahakikishie sisi kama mamlaka tupo makini na tutafuatilia vyombo vyote vya habari" amesema Ntobi

  Kwa upande wake Mhandisi mkuu idara ya Utangazaji TCRA makao makuu Mhandisi Andrew Kisaka amewataka washiriki kuhakikisha wanazingatia usawa katika kutoa taarifa za uchaguzi na kuepuka upendeleo wa baadhi ya vyama

  "Unakuta CHADEMA mnawapa dakia mbili kujieleza halafu CUF mnawapa dakika 20 hili sio sawa, hakikisha mnatoa kipindi kilichowapa fursa sawa wagombea wote bila upendeleo

  Aidha Kisaka amewaonya waandishi wa habari kuacha kujiingiza kwenye siasa kwa kushabikia wagombea fulani na kuingiza itikadi zao katika kuripoti habari za uchaguzi kwa kuwa itasababisha kuwagawa wananchi na kuona kituo chako kina upendeleo jambo ambalo halitakiwi

  Katika semina hiyo washiriki wamepewa nafasi ya kuuliza ma swali na kutoa ushauri wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa mambo hayo katika vyombo vyao vya habari wanavyofanyia kazi.
   Semina ikiendelea
   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo
   Waandishi wa habari wakiandika vitu muhimu
  Mwandishi wa habari akichangia mada katika semina hiyo.

older | 1 | .... | 601 | 602 | (Page 603) | 604 | 605 | .... | 1898 | newer