Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Vijana nchini watakiwa kujitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Dunia

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifurahia jambo na waandishi wa habari wa wa Kituo cha Redio cha TBC Taifa walipomtembelea ofisini kwake jana.Waliosimama kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa wizara hiyo Bw. James Kajugusi na wa mwisho kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi. Concilia Niyibitanga.Waandishi hao walifika ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kwaajili ya mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifanya mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani na mwandishi wa habari kutoka Redio ya Taifa TBC Taifa Bibi. Betty Tesha. Maadhimisho hayo kitaifa yanaadhimishwa tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija, WHVUM.


Na: Frank Shija, WHVUM

Vijana watakiwa kujitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kitaifa yatafanyika tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Ushiriki wa Vijana katika masuala ya Kiraia”

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.Bibi Sihaba amesema kuwa maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ikiwa ni kutambua mchango wa Vijana katika kuleta maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla kwa kuwa ndiyo kundi kubwa la nguvu kazi yenye kuleta chachu ya maendeleo kupitia ubunifu.

“Natoa wito kwa vijana wote nchini kushiriki katika kuadhimisha Siku hii muhimu kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yao, kwa wale wa Dar es Salaam ni vyema wakajitokeza na kushiriki maadhimishio hayo ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa” Alisema Sihaba.

Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwayatafikia kilele siku ya Jumatano ya tarehe 12 Agosti yatatanguliwa na Kongamano litakalofanyika mnamo tarehe 10 mwezi huu katika ukumbi wa Karimjee nakushirikisha zaidi ya Vijana 150 watakao jadiliana mada mbalimbali ikiwemo ushiriki wa vijana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Aliongeza kuwa sambamba na maadhimisho hayo siku ya kilele kutakuwa vijana watapata fursa ya kutoa na kupata burudani mbalimbali kupitia matamasha na michezo, pia siku nhiyo itatumika kwa vijana kuonyesha kazi zao zikiwemo za ubunifu.

Katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyikiwa Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika mikakati na uendelezaji wa Vijana nchini amjbapo baadhi ya wadau hao ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), AMREF,ILO, PSI, IYF, Restless Development na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na vijana.

Siku ya Kimataifa ya Vijana ilianza tangu mwaka 1991 nchini Australia ikiwa na lengo la jumuiya ya Kimataifa na jamii kwa ujumla kupata fursa ya kusherehekea na kutambua nafasi ya Vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi zao, na mwaka 1998 ilikubaliwa na jopo Mawaziri wanaoshughulikia Vijana na hatimaye Umoja wa Mataifa uliridhia rasmi kuitambua siku hiyo kuwa ya maadhimisho Kimataifa ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania walianza kuadhimsha siku hiyo muhimu.
 


dkt shein awataka wanawake nchini kuzitumia fursa zinazotolewa na serikali katka kujiletea maendeleo

$
0
0
Na Miza Kona /Khadija Khamis – Maelezo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amewataka wanawake nchini kazitumia fursa zinazotolewa na serikali katika kujiletea maendeleo na kujikwamua na umasikini.

Dkt Shein ameyasema hayo huko Kibokwa Wilaya ya Kaskazni A Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha kuwafundishia Wanawake Utengenezaji wa Vifaa vya Umeme wa Jua.

Amesema Serikali ina lengo la kuimarisha ajira kwa akinamama katika kuwaletea maendeleo na kuwaendeleza kielimu kwa kuwapa taaluma zitakazowawesha kujiendeleza na kujikwamua kwenye umasikini`.

Amesema wanawake wanapewa kipaombele katika maeneo yote nchini ili kuondokana na hali ya utegemezi kwani serikali imewapa fursa wananchi wa vijiji kujifunza mafunzo ya utengezaji wa vifaa vya umeme wa jua nchini India na kuitoa elimu hiyo kwa wengine kwa lengo la kukuza uchumi .

Wanawake hao wataweza kutoa taaluma ya matumizi ya vifaavya umeme wa jua na kusambaza huduma hiyo katika maeneo ya vijini ambayo haijafika na kutoa mchango mkubwa kwa jamii. 


Amesema katika kukuza ajira nchini serikali inafanya Tafiti mbalimbali ili kuweza kupata wa matumizi ya umeme utakaoweza kutumika nchini ikiwemo umeme wa jua, mawimbi ya bahari, umeme wa taka taka na upepo.

Akizungumzia kuhusu suala la ajira nchini Dkt Shein amewataka vijana wasihadaishwe na baadhi ya watu wasiopenda nmaendeleo kwa kuwahadaa kwa lengo la kuwapatia ajira hizo hasa katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu kwani tatizo hilo lipo duniani kote na Serikali inafanya jitihada za kupunguza tatizo hilo.

Aidha Dkt Shein ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kuongeza nafasi katika Eneo la kituo hicho ili kutoa huduma zaidi.

 Nae Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto amesema mradi huo ni mkombozi mkubwa kwa wanawake utakaowafungulia fursa nzuri wanawake wa vijijini katika kuleta maendeleo nchini.

Mapema Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Matifa Wanawake Bi Anna Collins-Falk ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi zake za kuwaunga mkono wanawake katika Mradi huo ambao utawasaidia kujiendeleza na kujikwamua na Umasikini.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Wanawake Kupanda Bi Meagan Fellon amewashukuru wanawake wa Kituo hicho kwa ushiriano wao katika utoaji wa mafunzo na kuimarisha maendeleo ya wanawake vijijini 

Kituo hicho kinafundisha mambo ya ujasiriamali kwaakinamama wa vijijini wenye umri mkubwa ambao pia hupata fursa ya kusoma na kuandika ikiwemo kushona ,ufugaji wa nyuki ushoni pamoja na biashara mbalimbali.


Mradi wa kituo hicho umegharimu zaidi ya sh. Milioni 120 ambapo Serikali ya Mapinduzi imechangia Sh.76milion na Umoja wa Mataifa wa Wanawake sh. Milioni 48  kwa ajili ya utengenazaji

MSD YAWAVUTA WANANCHI KATIKA BANDA LAO MAONYESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA MKOANI DODOMA

$
0
0


Wananchi wakisubiri kupata huduma katika banda la MSD kwenye Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Dodoma.

Ofisa Mdhibiti Ubora wa MSD, Betia Kaema, akitoa dawa kwa mgonjwa aliyefika katika banda la MSD kwenye maonyesho hayo.

Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dodoma, Sara Wangilisasi akitoa dawa kwa mgonjwa aliyefika kwenye banda la MSD kwenye maonyesho hayo.
Ofisa Mauzo, Juliana Mbogo na Ofisa Udhibiti Ubora, Betia Kaema wakiandaa dawa za kumpatia mgonjwa aliyefika katika banda la MSD.


Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wametakiwa kufika banda la Bohari ya Dawa (MSD), katika maonyesho ya Nanenane ili kujua kazi mbalimbali zinazofanywa na MSD hapa nchini.

Mwito huo umetolewa na Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dodoma, John Kisembi wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma kwenye maonyesho hayo ambayo kilele chake ni Agosti 8, mwaka huu.

Kisembi alisema kila mwaka MSD imekuwa ikishiriki  katika maonesho
hayo na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoihusu MSD.

Alisema mwaka huu MSD imeshiriki katika maonesho hayo ambayo yapo kikanda mkoani Dodoma ambapo wananchi na wadau mbalimbali wanaelimishwa kuhusu mambo mbalimbali ya kimafanikio yaliyofikiwa na MSD na yale yanayoweza kuongezea uwanda wao wa kibiashara hivyo kuongea mauzo yao.

Alitaja mambo yaliyozingatiwa katika maonesho hayo kuwa ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora kote nchini, upanuzi wa maghala hivyo kuongeza uwezo wa kuhifadhi dawa kwa wingi pamoja na usambazaji dawa na vifaa tiba kwa kutumia mfumo wa Direct Delivery (DD)

Mambo mengine ni matumizi ya mfumo mpya wa TEHAMA (Epicor 9),  Uwekaji wa nembo ya GOT katika vidonge, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ilikutofautisha dawa za serikali na za binafsi, uanzishaji wa  maduka ya dawa ya jumla karibu na wananchi (MSD 24hours Community Outlets) , pamoja kutoa elimu, sehemu maalumu ya kutolea dawa ambapo wagonjwa wanaopatiwa vipimo katika banda la Hospitali ya Mkoa wanakuja kupatiwa dawa katika banda la MSD. 







UFUNGUZI WA KITUO CHA UTENGENEZAJI VIFAA VYA UMEME WA JUA,KIBOKWA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa kituo cha kufundishia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua Bibi Meagan  Garnahan wakati aliposawasili katika uzinduzi wa kituo hicho katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Bw.Abdul Barwan Abdalla kuhusu ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa wakati alipotembelea maonesho ya kazi mbali mbali za ujasiria mali kabla ya kukifungua kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kazija Gharib Issa akiwa ni miongozi mwa wanawake waliopata mafunzo ya kutengeza vifaa ya kutumia umeme wa jua nchini India wakati alipotembelea maonesho ya kazi mbali mbali za ujasiria mali kabla ya kukifungua kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo (katikati) Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo,(kulia) makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto Nd,Ali Khamis Juma (katikati) wakati alipotembelea sehemu ya maalum ya kulia baada ya kukifungua kituo cha kutoa mafunzo kwa Wanawake jinsi ya utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa  kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja Bi Fatma Juma baada ya kifungua rasmi  leo.
 Baadhi ya wananchi walioshiriki katika ufunguzi wa kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi.
  Mtendaji Mkuu wa kituo cha kufundishia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua Bibi Meagan  Garnahan wakati alipokuwa akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa kituo kiliopo wilaya ya kaskazini A. katika kijiji cha kibokwa Mkoa wa kaskazini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  Baadhi ya Viongozi mbali mbali akiwemo Balozi wa India nchini Tanzania Satendar Kumar wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo,(kushoto) Mtendaji Mkuu wa kituo cha kufundishia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua Bibi Meagan  Garnahan na (kulia) Mkurugenzi Mkaazi wa Un Women Tanzania Anna Collins [Picha na Ikulu.]

MASHIRIKA MATANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA(FOS) YAUNGANA KWA PAMOJA KUTOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

$
0
0
Wasemaji kutoka Mashirika Matano Kutoka kushoto ni Msemaji kutoka LHRC,OXFAM, Restless Development, BBC na VSO
  Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Oxfam Jane Foster ambao pia ndio waandaaji wa Mkutano huu na waandashi wa Habari akieleza kwa kina nia ya Mkutano huo ambao lengo kuu ni kuzungumzia maswala ya Uchaguzi kuwa kila mtu anahaki ya kupiga kura.
 Hellen Kijo Bisimba ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki  za binadamu (LHRC) (Kushoto) akiongea jinsi walivyo endesha zoezi zima la kusimamia uandikishaji wa Daftari la uandikishaji wa wapigakura la kudumu BVR na ushiriki wao kwa ujumla.
Meneja wa Programu kitengo cha Governance kutoka Oxfam Bi.  Betty Malaki  akiendelea kutoa utaratibu katika Mkutano huo.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Restless Development Bi. Rahma Bajun ambao jukumu lao limelenga sana kwa vijana , akitoa taarifa ya Jinsi walivyo washirikisha vijana katika kuwahimiza na kuwapa elimu ya uchaguzi na kupiga kura ambapo wanafanya kazi hasa katika mikoa ambayo ipo Pembezoni ambayo ipo 11 .
 Mwakilishi kutoka Shirika la Utangazaji la BBC Bi.Neema Yobu akielezea jinsi wanavyo simamia na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari nchini, kutoa elimu ya uandishi bora wa Habari za kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Innovation Skills Results Bw. Jean Van Wetter akieleza jinsi wanavyohusika kwa ukaribu kabisa hasa katika upande wa vijana wa umri wa kati kuwaelimisha juu ya umuhimu wa Uchaguzi ambapo alisisitiza kuwa vijana wanatakiwa kupewa mapema elimu hii ili wanapokuwa wafahamu umuhimu wa uchaguzi.
 Mmoja wa wasemaji kutoka VESO Bi. Lina Muro akisisitizia Jambo<!--[if gte mso 9]>
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano huo.

Umoja wa Mashirika Matano yanaounda ushirika wa Fahamu,Ongea Sikilizwa(FOS) ambayo ni Oxfam,BBC Media Auction, Legal and Human Rights Centre, Restless Development, and VSO leo wamekutana na waandishi wa Habari kwa ajili ya kuzungumzia mambo Mbalimbali yanayohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015 na kueleza malengo ya muungano huo.
Akizungumza Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Bi. Jane Foster ambao ndio waandaaji wa Mkutano huo na waandishi wa Habari alisema kuwa Lengo kubwa la Umoja huo ni kusisitiza na kuwaelimisha wananchi wote kwa ujumlan juu ya Uchaguzi mkuu 2015 ambapo Oxfam wao jukumu lao kubwa ni kuwahimiza wanawake na wasichana wadogo  kuelekea uchaguzi Mkuu kama wapiga kura, na ili kuyafikia makundi yote haya waliandaa na wanaendesha Midaharo mbalimbali, kuunda makundi ya wanawake na zaidi wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter kuwapa taarifa juu ya uchaguzi.
BBC kwa upande wao wanajukumu la kusimamia mashirika mbalimbali ya utangazaji Nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kanuni za uandishi bora wa Habari za uchaguzi Mkuu 2015 

Nao kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao walikuwa na jukumu la Kusimamia zoezi zima la uasdikishaji wa wapiga Kura ambapo walikuwa na watu 165 nchi nzima wakiangalia na kuangalia makosa yaliyojiokeza na kupeleka Maoni yao sehemu husika, na pia katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 wameandaa kitengo maalumu cha Teknolojia ambacho kitasimamia uchaguzi wote.

Wakati huo huo restless Development wamewafundisha vijana 22 ambao wamesambazwa katika mikoa 18 Nchi nzima kwa lengo kuwakusanya vijana katika makundi mbalimbali kwa nia ya kuwapa elimu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015, sambamba na hapo wamelenga kuwapa elimu viongozi wa ngazi za chini yaani Wilaya, Pia vyombo vya habari pamoja na Polisi, ambapo kwa sasa Shirika hili linaandaa ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.

Pia Shirika la Voluntary service Overseas nao wameendesha mafunzo kwa viongozi wa chini, viongozi wa Dini katika mikoa Nane(8) Tanzania ambao wanashirikishwa moja kwa moja katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Mikoa hiyo ni Pamoja na Lindi, Mtwara, Kagera na Mikoa mitano Zanzibar ambayo ni Wete,Chakechake, Unguja, Makokotoni na Unguja Kaskazini. wakieleza juu ya uchaguzi Mkuu 2015.

Akizungumza na waandishi wetu mmoja wa wakurugenzi  wa mashirika hayo, Hellen Kijo Bisimba ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki  za binadamu (LHRC), alisema kuwa moja kati ya mapungufu yaliyoonekana katika uchaguzi huo ni kuwepo kwa imani potofu hasa katika kipindi cha kujiandikisha kwa kutumia mashine za BVR ambapo wananchi wengi hasa wa vijijini walikuwa na dhana kuwa mashine hizo huweza kuwapima watu Ukimwi na wengine kushikana uchawi hasa wale ambao alama zao za vidole hazikuonekana au zilipatikana kwa shida.
Katika mikoa mingine mkurugenzi huyo alisema kuwa watu walifikia mbali zaidi na kuaminishana kuwa mashine hizo ni za Freemason na makundi ya wanyonya damu mambo ambayo yalichangia wengi wao wasishiriki zoezi zima la uandishaji na kuongeza kuwa changamoto zote hizo walizibaini na kuzifikisha kwa tume.
“Kuna maeneo walihamasishana kabisa kutojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura hasa kwa njia BVR wakidai kuwa ni ya Freemason au wanyonya damu huku wengine wakishikana uchawi kwa kuwa alama zao za vidole hazisomi kwenye mashine hizo. Hizo zote ni changamoto na tumezifiksha kwenye tume,” alisema Bi Hellen na kuongeza kuwa hata hivyo muamko wa vijana mwaka huu ni mkubwa sana jambo linalotoa tafsiri kuwa uchaguzi huu utakuwa shirikishi kuliko hapo awali.


BREAKING NYUZZZZZZ.....: PROF. LIPUMBA ABWAGA MANYANGA UWENYEKITI WA CUF

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwenyekitu wa Chama cha Wananchi -CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo mbele ya Waandishi wa habari kwenye `hoteli ya Peacock, Jijini Dar es salaam leo.

Prof. Lipumba amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa Katiba ya Chama chao.

TAARIFA KAMILI 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.

Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania  katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.

Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).

Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa  kesi ya kufanya maandamano bila kibali.

Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu  pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani  pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu  ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

RAIS KIKWETE AAGA RASMI IDARA YA MAHAKAMA, YAMPA TUZO KWA MAKUBWA ALIYOFANYA KATIKA MIAKA 10

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutokana na mambo makubwa liyoifanyia idara hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi. PICHA ZOTE NA IKULU
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha  tuzo maalumu aliyoipokea kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.

  wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Sehemu ya wastaafu na viongozi wa taasisi wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
MC wa shughuli  katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Meza Kuu katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na Majaji wa  Mahakama Kuu  jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja Majaji wa  Mahakama Kuu  ya Rufani jijini  Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete katika picha ya Mwanasheria Mkuu, Mtendaji Mkuu wa Mahahama, Rais wa Tanganyika Law Society jijini  Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.















KAWAIDA

MAZISHI YA KAMISHINA MSAIDIZI WA MAGEREZA(SACP), ANNETHY LAURENT

$
0
0
 Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Magereza (SACP) Annethy Laurent.
 Mwili wa Marehemu Anneth ukiwasili katika Kanisa Katoliki Parokiani Segerea. Walio mbele ni Pamela  (mtoto wa dada yake na Marehemu) na aliyebeba picha ni mtoto wa Pamela ( Mjukuu wa Marehemu). Walioshika jeneza kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Dk.Kato Rugainunura, kulia ni Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Rajab Nyange
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati wa ibada ya kumuombea Marehemu.
 Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya akitoka salaam za Jeshi la Magereza kwa wafiwa kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa  Magereza John C. Minja.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga akitoka salaam za pole kwa wafiwa kwa niamba ya Kamati yake ambayo pia aliongozana nayo katika msiba huo (hawapo pichani)
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga(Mwenye miwani) akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. Wa pili ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akifuatiwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakhim Maswi wakitoa salaam zao za mwisho.
Mwili wa  Marehemu Anneth ukiwasili katika kanisa katoliki parokiani Segerea tayari kwa misa takatifu ya kumuombea marehemu.
PIX 8: Baada ya misa takatifu  msafara wa kuelekea makaburini ulianza ukiongozwa na Kamishina Jenerali wa Magereza (CGP) John Minja.
Picha zote na Mkaguzi wa Magereza Moses Sebastian
Makao Makuu ya Magereza.


UMOJA WA WASANII WA FANI MBALIMBALI WAMUGA JK,WAMTANGAZA KUWA SHUJAA WA SANAA YA MUZIKI NCHINI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo  na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia akishiriki tukio hilo.Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali  wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dk.Jakaya Kikwete.
 Baadhi ya Wadau wa muziki wakifurahia jambo wakati Rais Dkt Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wadau wa muziki nchini ndani ya ukumbi wa mlimani City usiku huu.
 Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom,Kelvin Twisa
 Dkt Kikwte akisalimiana na baadhi ya Wasanii wa muziki wa bongofleva
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick ndani ya ukumbi wa mlimani city usiku huu.
Wanauziki wakongwe pia walikuwepo kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki. 

PICHA NA MICHUZI JR.

BENKI YA NIC YATOA MADAWATI 25 SHULE YA MSINGI CHAMANZI

$
0
0
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ancent Shayo akiwa na wafanyakazi wa shule ya msingi chamanzi wakizungumza na wafanyakazi wa NIC hawapo pichani katika ofisi ya mkuu wa shule ya msingi chamanzi jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 BENKI ya NIC imetoa msaada wa madawati 25 katika shule ya msingi Chamanzi yenye thamani ya Sh.Milioni tatu kutokana na shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya madawati.

Akizungumza baada ya kukabidhi  madawati  hiyo, Mkuu wa Biashara za Kibenki,Rahim Kanjii amesema kuwa shule hiyo waliona ina umhimu wa kusaidiwa sehemu ya madawati katika kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokaa chini ardhi wakiwa darasani.

Amesema shule hiyo inatakiwa kusaidiwa kwa kila hali kwani watoto wanaoandaliwa hao ni taifa la leo hivyo wanatakiwa kuandaliwa mazingira bora ya kupata elimu.

Kanji amesema kuwa ameguswa sana na benki itaendelea kadri ya uwezo wake kusaidia shule katika kuweza kuondokana na chagamoto ya madwawati  katika kujenga mazingira bora ya kusomea watoto kwani wanaandaliwa kuja kuwa wanataaluma mbalimbali.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Ancent Shayo amesema kuwa shule ina wanafunzi 3200 lakini vyumba vya madarasa 11 na kufanya kila darasa kukaa wanafunzi 150.

Amesema madawati hayo ni kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne kutokana na upungufu wa madwati 175 ambapo NIC imepunguza imetoa madawati 25 hivyo kwa darasa hilo linahitaji madawati 150 ili waweze kukaa katika siku ya mtihani wa taifa.

Shayo amesesema hitaji katika shule licha ya madawati wanaupungufu wa vyumba vya madarasa  kutokana na idadi ya wanafunzi hao.
 Wanafunzai wa shule ya msingi Chamanzi wakiwa darasani wakiwa wamekaa chini kwa kutokuwa na madawati ya kutosha katika chumba cha darasa la tatu walipotembelewa na wafanyakazi wa Benki ya NIC leo jijini.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo akizwa na wafanyakazi wa Benki ya NIC walipowatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamanzi jijini Dar es Salaam walipotembelea chumba cha darasa la kwanza katika shule hiyo. 
Wafanyakazi wa Benki ya NIC akifungua meza na viti walivyotoa msaada katika shule ya Msingi Chamanzi ikiwa meza 25 na viti 25.
 Wafanyakazi wa Benki ya NIC waliosimama wakiwa wanafunzi wa shule ya msingi Chamanzi waliokaa baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Picha ya pamoja ya wanafunzi wa shule ya msingi Chamanzi na wafanyakazi wa Benki ya NIC baada ya kutoa msaada wa meza 25 na viti 25 vya plastiki katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Biashara za Kibenki, Rahim Kanjii akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo  mara baada ya kutoa msaada wa meza 25 na  viti 25.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chamanzi wakiwa wamekaa kwenye viti na meza walivyopewa msaada na Beni ya NIC jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFEREJI MPYA WA SUEZ

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka kwenye Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika jana Agosti 6, 2015 jijini.
 Picha na OMR

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana ameiwakilisha Tanzania katika uzinduzi wa mfereji mpya wa Suez unaounganisha mabara ya Ulaya, Afrika na Asia. Mfereji huu mpya ambao Misri inauita "zawadi mpya kwa Dunia" unalenga kukuza uchumi katika usafiri wa maji na utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa mabara haya matatu, huku Misri ambayo kijiografia iko jangwani ikitegemea kukuza uchumi wake kutokana na meli zitakazopita katika mfereji huo.

Mradi wa ujenzi wa Mfereji huu mpya umejengwa kwa mwaka mmoja licha ya kupangwa kukamilika baada ya miaka mitatu na umetumia kiasi cha dola za Marekani Bilioni Nane ambazo zimechangwa kwa njia ya Hisa na wananchi wa Misri kwa kipindi kisichozidi siku tisa. Mfereji huu ambao umezinduliwa jana, unatoa fursa kwa Meli kupita bila usumbufu tofauti na zamani ambapo ilipaswa Meli kusimama ili kupishana lakini sasa kila upande wa Meli utapita bila kuathiri upande mwingine.

Sherehe hizo za aina yake zimehudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali na kupata kuripotiwa na vyombo vyote vikubwa duniani na hivyo kutoa picha ya kuwa Afrika inapiga hatua katika kukuza uchumi wake pamoja na kuonesha dunia kuwa fursa mpya za maendeleo zipo Afrika.

Sherehe hizo za  aina yake zilipambwa na maonesho ya ndege za kivita zilizotanda anga la Mfereji mpya wa Suez huku zingine zikiruka kwa kasi na kutoa moshi ulioakisi bendera ya Misri, zingine zikipeperusha bendera ya nchi hiyo.

Katika tukio hilo la kuathimisha tukio hilo la kihistoria   serikali ya Misri ilitangaza kuwa  siku hiyo ni ya mapumziko huku ulinzi mkali ukiimarishwa katika miji yote mikuu ya nchi hiyo huku jiji la Cairo walipofikia  viongozi mbalimbali wa kimataifa likiwa chini ya uangalizi wa kijeshi kwenye maoneo yote muhimu. Barabara ya kwenda eneo la Islamelia zilikofanyika sherehe hizo ilifungwa kwa siku nzima,  walioruhusiwa kupita  ni viongiozi na wageni mbalimbali  waalikwa waliotakiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.

 Rais wa Misri Abdel  Fatah  Sisi alisema kufunguliwa kwa Mfereji  ni uthibitisho kwamba Misri inaweza na kueleza kwamba njia hiyo itaimarisha zaidi shughuli za usafirisha na kufungua fursa zaidi kwa mataifa  duniani.

Katika moja ya matukio ya  uzinduzi huo Rais Fatah na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo walisafiri katika meli za kifahari huku kiongozi huyo wa Misri akivalia mavazi maalumu ya kijeshi akiwa juu ya sehemu ya uwazi wa meli hiyo pamoja na kijana mdogo mwanafunzi wa miaka tisa aliyevalia kijeshi na kupeperusha bendera ya  Misri kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa mfereji huo.

Shughuli  ilimazika usiku  kwa  maonesho mbalimbali ya sanaa na utamaduni wa Misri  na kuhudhuriwa na viongozi na wageni wote waalikwa.

UTUMISHI YAKABIDHIWA ZAWADI YA USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA YALIYOFANYIKA CONGO BRAZAVILLE

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akipokea cheti cha ushiriki wa Tanzania kutoka kwa Mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  Barani Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akipokea zawadi ya Tanzania kutoka kwa mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akionyesha cheti cha ushiriki wa Tanzania katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni.  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto),  Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia)na mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo kutoka Wizara ya Uchukuzi Bw. William Budoya (wa kwanza kulia).

MAALIM AZINDUA UVUNAJI MATIKITI MAJI MUWANDA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua uvunaji wa matikiti maji kwa wakulima wa shehia ya Donge Muwanda.
 Mkulima wa matikiti maji na pilipili boga Bw. Salum Khamis Kiregu akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na badhi ya wakulima wa Donge Mchangani na Muwanda, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Affan Othman Maalim (wa pili kushoto). Picha na OMKR.
 
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi zinazochukuliwa na wananchi wa Donge katika kuendeleza kilimo cha matunda na mboga mboga.

Amesema iwapo kilimo hicho kitawekeza mikakati imara, kinaweza kuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima na kuweza kuweza kuongeza kipato chao.
Maalim Seif ameeleza hayo wakati akizindua uvunaji wa matikiti maji na pilipili boga katika shehia za Donge mchangani na Muwanda katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.

Amesema katika siku za hivi karibuni, kilimo hicho kimepata mafanikio makubwa na kupunguza uagiziaji wa bidhaa hizo nje ya Zanzibar kutoka asilimia 80 hadi asilimia 20.

Amefahamisha kuwa lengo la Serikali ni kuimarisha zaidi kilimo cha matunda na mboga mboga ili kuweza kukidhi soko la ndani na kuacha kuagizia bidhaa hizo kutoka nje ya Zanzibar.

Amesema kinachohitajika hivi sasa ni kwa Serikali kuongeza mashirikiano na wakulima, ili kusaidia kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji pamoja na pembejeo.

Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara ya Kilimo kupeleka mabwana na mabibi shamba wa kutosha katika shehia hizo za Mchangani na Muwanda, ili kusaidia utaalamu kwa wakulima hao na kuweza kuzalisha zaidi.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Bw. Affan Othman Maalim, amesema tayari Serikali imeanza kufanya utafiti kujua maeneo ya kuchimba visima ili kuwasaidia wakulima hao kuondokana na tatizo la upungufu wa maji.

Hata hivyo amewashauri wakulima hao kujikusanya pamoja ili kurahisisha miundombinu ya maji kuweza kuwafikia walengwa.

Kuhusu tatizo la pembejeo, Bw. Affan amesema Wizara ya Kilimo inaandaa utaratibu wa kulipeleka suala hilo katika ngazi za juu, ili kuwawezesha wakulima wa matunda na mboga mboga kuweza kupatiwa ruzuku za pembejeo za kilimo kama wanavyopatiwa wakulima wa mpunga.

Mapema mmoja kati ya wakulima hao Bw. Salum Khamis Kiregu, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa licha ya mafanikio wanayoyapata, bado wanakabiliwa na tatizo la soko la kuuzia bidhaa hizo, na kuiomba serikali kuandaa mazingira bora ya soko kwa wakulima hao.

Amesema hivi sasa wanalazimika kuuza bidhaa zao kwa bei ya chini kupitia kwa wafanyabiashara, jambo ambalo limekuwa likipunguza kipato chao licha ya kuzalisha bidhaa hizo kwa wingi.

Bw. Kiregu ameeleza matatizo mengine yanayowakabili kuwa ni pamoja wadudu waharibifu na maradhi ya mimea, na kuwaomba wataalamu wa kilimo kuwa karibu na wakulima ili kusaidia kukabiliana na changamoto.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA JANET MBENE ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIGAE CHA MKOANI MBEYA

$
0
0
 Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akizungumza, mmoja waviongozi wa kampuni ya Marmo and Garnito Mines wakati alipokuwa kwenye ziara ya viwanda mkoani mbeya hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Janet Mbene,akiangalia  baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na kampuni ya Marmo and Garnito Mines kwa ajili ya matumizi mbalimbali
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janet Mbene, akitembelea sehemu ya kiwanda cha Marmo anda Granito Mines.

TWIGA STARS YAELEKEA ZANZIBAR

$
0
0
Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars).

Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kimeodoka leo saa 6 mchana jijini Dar es salaam kuelekea kisiwani Zanzibari, ambapo kitaweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Septemba.

Msafara wa Twiga Stars umeondoka na boti ya Azam (Kilimanjaro) ukiwa na watu 32, wakiwemo wachezaji 25, benchi la ufundi 6 pamoja na kiongozi wa msafara, ambapo TFF imegharamia kambi hiyo ya mwezi mmoja

Wachezaji waliosafiri leo ni Fatuma Omari, Belina Julius, Happiness Hezron, Fatuma Hassan, Anastazia Anthony, Fatuma Bashiru, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Maimuna Hamis, Donizia Daniel, Sofia Mwasikili, Etoe Mlenzi.

Wenigine ni Amina Ally, Thereza Yonna, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Asha Rashid, Najiat Abbas, Estha Chabruma, Mwajuma Abdallah na Fatuma Mustapah.

Twiga Stars itakua kambini kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo – Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

Fainali za Michezo ya Afrika  (All Africa Games) zinatarajiwa kuanza kutivua vumbi Septemba 4 – 19 nchini Congo-Brazzavile.

TOTO AFRICAN KUCHAGUANA OKTOBA 2015
Klabu ya Toto African ya Mwanza inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi katika kamati yake ya utendaji ifikapo tarehe 11 Oktoba 2015. Katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Toto African, Katibu Mkuu wa TFF ameuagiza uongozi wa Toto African kuwasiliana na Kamati yao ya Uchaguzi ili tangazo la uchaguzi litolewe si chini ya siku sitini (60) kabla ya tarehe ya kufanyika uchaguzi.

Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano katika klabu ya Toto na suala kubwa likiwa ni kuhusu ujazaji wa nafasi zilizo wazi. Awali TFF ilipokea maombi ya wanachama na wadau wa Toto African wakitaka ufanyike uchaguzi ili kumaliza mvutano ndani ya klabu.

TFF ilishauri uchaguzi huo kusubiri klabu kukamilisha mchakato wa usajili.

Vilevile TFF imewataka wadau wote wa klabu hiyo kongwe ya mjini Mwanza kuheshimu uongozi uliopo madarakani kwani ndio unaotambulika na ndio utaendelea kuiongoza Toto African katika kipindi cha kuelekea uchaguzi uchaguzi.

NB: Picha za Twiga Stars wakisafiri kuelekea Kisiwani Zanzibar zimeambatanishwa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MABONDIA RAMA SHAURI NA LULU KAYAGE WAPAA AFRIKA YA KUSINI

$
0
0
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwa na mabondia Lulu Kayage kulia na Ramadhani Shauri wakienda kupanda ndege kwenda afrika ya kusini mabondia hawo wanapanda uringoni agost 9.
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9.
Bondia Lulu Kayage.
Mabondia wakiwa na wadau mbalimbali wa masumbwi kabla ya kupaa kwenda Afrika Kusini kwaajili ya mchezo wao wa Augosti 9.
Bondia Lulu Kayage kulia  akihakiki nyalaka zake za kusafiria kushoto ni mshauri wake wa karibu Hamisi Berege kutoka kambi ya mchezo wa ngumi Ilala Lulu amenda Afrika ya kusini kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 9.
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akingia katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa julius nyerere kwa ajili ya safari pamoja na mabondia Lulu Kayage kushoto na Ramadhani Shauri mabondia
kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9.
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9.
 Picha na SUPER D BOXING NEWS.

ADC YAFANYA MKUTANO WA HADHARA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA WA URAIS KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
 Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kulia) na mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Buguruni Sheli Dar es Salaam jana. 
 Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kushoto), baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wake, Mwanaisha Lutasola.
 Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Hamad akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
  Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba, akihutubia katika mkutano huo Buguruni Sheli jana.
Wanachama wa chama hicho na wananchi wakisikiliza sera za viongozi hao watakao peperusha bendera ya ADC kwenye uchaguzi mkuu. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.

NHIF WATOA MSAADA WA MASHUKA 120 HOSPITALI YA MANISPAA YA TEMEKE

$
0
0
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa mkoa wa Temeke (NHIF),Constantine Makala akieleza jambo wakati wa kukabidhi mashuka 120 katika hospitali ya Temeke leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk.Edwin Muhondezi.
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa mkoa waTemeke (NHIF), Constantine Makala akimuwakilisha kaimu  Mkurungenzi Mkuu wa (NHIF) wa mkoa wa Temeke kumkabidhi msaada wa mashuka 120 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Edwin Muhondezi leo Jiji Dar es Salaam.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke,Dk.Edwin Muhondezi akitoa neno la shukarani baada ya hospitali yake kupata msaada wa mashuka 120 kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika hospitalini hapo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa mkoa wa Temeke (NHIF) wakiwa wameshika shuka ambayo inawasilisha msaada wa shuka 120 zilizotolewa katika hospitali ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.
(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

MSAADA ZAIDI WATOLEWA NA TBL MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Ekimu kwa Umma cha Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani,  Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Abel Swai sehemu ya fulana 3,800, kofia 2,800 na stika kwa ajili ya Maadhinisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani itakayoanza .Agosti 3 hadi 7 jijini Tanga. TBL imedhamini maadhimisho hayo kwa sh. mil 124, ambapo madereva wa masafa marefu watapimwa afya zao pamoja na kuwapatia mafunzo waendesha bodaboda 300. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Ekimu kwa Umma cha Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani,  Mrakibu Msaidizi wa Polisi, 
Abel Swai moja ya vyeti watakavyokabidhiwa madereva wa masafa marefu watakaopimwa afya zao wakati wa Maadhinisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani itakayoanza .Agosti 3 hadi 7 jijini Tanga. TBL imedhamini maadhimisho hayo kwa sh. mil 124, ambapo pia mafunzo yataendeshwa kwa bodaboda 300. Makabidhiano hayo ya stika, fulana na kofia na vyeti yalifanyika Dar es Salaam
 Dorris Malulu wa TBL akikabidhi Stika kwa Abel Swai
 Makasha yenye kofia, fulana na stika yakipakiwa kwenye gari la Polisi

TBL YAFANIKISHA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA WA MASAFA MAREFU WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Mganga kutoka kitengo cha afya makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania, Dk Issa Ndimila akimchukua damu dereva wa magari makubwa, Benedicti Samuel kwa ajili ya kumpima magonjwa katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
 Mganga kutoka kitengo cha afya makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania, Dk Issa Ndimila akimchukua damu dereva wa magari makubwa, Kanai John kwa ajili ya kumpima magonjwa katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.

 Katibu Tawala wilayaa ya Morogoro, Emmanuel Nzunda akimkabidhi zawadi ya fulana na cheti dereva wa magari makubwa baada ya kupima afya wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kitucha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, mpango ulioanzishwa na
TBL na jeshi la polisi nchini.
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Silve Massawe akijaza taarifa za dereva Edward Sanga baada ya kupima afya katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Silve Massawe akijaza taarifa za dereva Abdallah Rajabu baada ya kupima afya katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images