Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA WA ARUSHA,FELIX NTIBENDA AFUNGUA MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NJIRO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Kanda ya Kaskazini(Taso)Arthur Kitonga akisoma taarifa ya Taso inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambao ni wanachama wa Taso Kanda ya Kaskazini,Mh Joel Bendera akisistiza jambo kwenye mkutano wa ufunguzi uliofanyika kwenye viwanja ya Nanaenane Njiro jijini Arusha,anayesikiliza kwa makini ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(wa pili kushoto).
Meneja wa Shama la Mbegu la Serikali mkoa wa Arusha,Zawadiel Mrinji akionesha mfuko ulitengenezwa maalumu kwa lengo la kudhibiti wadudu waharibifu baada ya mavuno ili kumwezesha mkulima kunufaika na mazao yake.
Meneja wa Shama la Mbegu la Serikali(ASA) mkoa wa Arusha,Zawadiel Mrinji akizungumzia umuhimu wa zao la Ngano linalostawi kwa wingi wilaya ya Monduli na Hanang .

Viongozi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(wa tatu kulia)wakikagua bustani ya JKT ambayo imekua kivutio kwa wananchi wanaotembelea maonesho ya Nanenane Njiro mkoani Arusha.

Viongozi wa serikali wakikagua bustani ya JKT ambayo imekua kivutio kwa wananchi wanaotembelea maonesho ya Nanenane Njiro mkoani Arusha.

Bustani  ya taasisi ya Utafiti wa Kahawa(Tacri)hutembelewa na wakulima kujifunza namna bora ya kilimo cha Buni nchini.


Wananchi wakipata maelezo kutoka kwenye banda la Sementi la Simba Cement .

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki Kuu(Arusha) ambao wanashiriki kwenye maonesho  hayo wakijumuika na wananchi kusikiliza hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Felix Ntibenda. 

Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Oljoro mkoa wa Arusha wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi.

Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kujifunza mambo mbalimbali yanatolewa na Chuo hicho.
Kikundi cha burudani kutoka JKT Oljoro wakionesha ufundi wao wa ngoma kutoka Pemba.

Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com


ZAHARA ANENA BAADA YA KUSHINDWA KUPATA KURA ZA KUTOSHA TABORA

$
0
0
Baada ya kura kutotosha kumfanya apite katika kura za maoni kugombea Ubunge kwa viti vya Vijana mkoani Tabora, Zahara Muhidin Issa Michuzi (pichani) amepokea matokeo kwa moyo mkunjufu na kumpongeza mshindi Irene Uwoya na kumuahidi ushirikiano katika mambo yote mema ya kuendeleza vijana mkoani humo.
Zahara ambaye sasa ataelekeza nguvu zake katika kusaka digrii ya pili ya uchumi, amesema kwamba anawashukuru wajumbe wa mkutano wa uchaguzi, baba yake, mama walezi, kaka Mkala Fundikira wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kanda ya Magharibi na wana TBN wote wa ndani na nje ya nchi akiwemo kaka Jeff Msangi wa Canada na Mubelwa Bandio na DJ Luke wa Marekani, wanahabari wote wa makundi ya Whatsapp chini ya Francis Godwin na walimu wake pamoja  na wananchi wote kwa ujumla kwa kumpa heshima ya kumuunga mkono kwa kujitokeza kujaribu kuomba nafasi hiyo.
Amesema kushindwa kwake hakumaanishi lolote zaidi ya kwamba demokrasia imechukua mkondo wake na aliyehitajika kuendeleza mapambano amepita na yeye hana kinyongo naye na ataendelea kuutumikia mkoa wa Tabora  katika nafasi yake ya mtu ambaye si kiongozi.
Zahara ametoa mwito kwa wagombea wa nafasi zote kwamba kushindwa ni moja ya matokeo katika ushindani wowote hivyo ipo haja ya kujenga utamaduni wa kukubali matokeo bila ya hasira ama kinyongo kwani dunia i duara, na kwamba mlango mmoja ukifungwa kuna mwingine utafunguka.
Amesema hana mpango wa kuhama CCM ambayo anaiamini kuwa ni chama ambacho kitaenzi na kutunza hadhi na mustakabali wa Taifa la Tanzania kuliko chama chochote.

"Kushindwa kwangu kupata kura za kutosha sio mwisho wa dunia. Nina imani kwamba wapiga kura walijua wanachokifanya. Mimi ni nani kuwaoneshea kidole?  Maisha yaendelee kama kawaida na Mola awajaalie wote kwa yote" alisema.

UNDP PRESS RELEASE END OF JUDGES SENSITIZATION SEMINARS ON ELECTORAL DISPUTE RESOLUTION (EDR)

BODI YA USAJILI WA WAHANDISI (ERB) YAKUZA AJIRA NCHINI.

$
0
0
Picha. Na.1. Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Muhandisi Steven Mlope akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya Bodi hiyo katika kipindi cha miaka 10 hasa ukuzaji wa sekta ya ajira nchini Tanzania.

Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
BODI ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERD) imefanikiwa kutengeneza ajira 1600 kwa Watanzania kufuatia usajili wa makampuni 160 ya ushauri wa kihandisi yaliyoanzishwa nchini kote nchini katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERB) Muhandisi Steven Mlope amesema kuwa kwa kusajili makampuni 160 katika kipindi cha miaka 10 pia wamefanikiwa kusajili wahandisi wapatao 8496 ambao kwa ujumla wao wametengeneza ajira kwa Watanzania 256,480.

Amesema katika kipindi cha miaka 10 Bodi hiyo imefanikiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wahandisi waliosajiliwa kutoka 6868 waliokuwepo nchini Tanzania hadi 15,364 mwaka 2015.

Aidha Muhandisi Mlope amesema kuwa Fani ya Uhandisi nchini Imeendelea kukukua kutokana na uwepo wa wahandisi wa Majengo,wahandisi wa mazingira, Mifumo ya kompyuta na wahandisi wa mazingira wanaofanya kazi zao kwa kushirikiana.

Aidha, amesema kuwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa kuzingatia  sheria ya Bunge namba 15 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho, na sheria No.24 ya mwaka 2007 imepewa majukumu ya kuratibu na kusimamia mienendo na shughuli za Kihandisi zinazofanywa na wahandisi pamoja na makampuni ya ushauri wa kihandisi nchini.

Ameongeza kuwa kwa mujibu Sheria ni kosa kwa mtu binafsi,kikundi cha watu binafsi, kikundi cha watu au kampuni yoyote kutoka ndani na nje ya nchi kufanya shughuli za kihandisi bila kusajiliwa au kuwa na wahandisi wasiosajiliwa.

Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 Bodi hiyo ilitoa onyo na adhabu mbalimbali ikiwemo kufuta usajili wa wahandisi 330 waliokiuka Sheria ya Bodi ya Usajili wa wahandisi.

Kwa upande wa shughuli za kihandisi katika ngazi ya wilaya kote nchini Muhandisi Mlope amesema kuwa kufikia mwaka 2015 hali imeendelea kuimarika licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo.

Muhandisi Mlope amebainisha kuwa Bodi inaendelea kuratibu mpango wa Mafunzo (SEAP) wenye lengo la kuwajengea uwezo wahandisi wanaohitimu masomo katika  vyuo mbalimbali ili waweze kukidhi viwango kuwawezesha vya kuwawezesha kusajiliwa na Bodi hiyo.

"Mpango huu wa mafunzo unaofadhiriwa na Serikali kwa lengo la kuwajengea uzoefu wahitimu, kuwawezesha kuajiliwa na kupata uzoefu mapema umekuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu"

Ametoa wito kwa wenye viwanda na makampuni kuwapokea na kuwaajili wahandisi waliosajiliwa na wale waliokula kiapo ili kazi wanazozifanya ziweze kukidhi viwango vilivyowekwa.

Pia amesema kuwa Bodi hiyo inaendelea kuwaendeleza wahandisi wataalaam waliopo nchini kwa kuandaa mihadhara na kozi fupifupi ambazo huendeshwa na vyuo vinavyotoa mafunzo ya kozi hiyo huku wao kama bodi wakitoa ithibati  na kuandaa makongamano ya wahandisi kila mwaka.

Amefafanua kuwa Septemba 3 mwaka huu Wahandisi watakuwa na Kongamano kubwa la mwaka litakalowakutanisha wahandisi wote nchini ili kuweza kukidhi matarajio ya Wananchi kufuatia wengi wao kuongeza uelewa juu ya matumizi ya wahandisi.

"Mwamko sasa umeongezeka kutokana na Serikali kuendelea kuweka mkazo katika masomo ya Sayansi na ujenzi wa maabara ili kuzalisha wataalam wa kutosha wenye viwango" Amesema.

Kuhusu maslahi ya wahandisi nchini amesema kuwa wao kama Bodi wanaishukuru Serikali kwa kuendelea  kuboreshaji maslahi yao na kusisitiza kuwa jambo hilo linaendana na mabadiliko ya uchumi yaliyopo ili kuwawezesha wataalam hao kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuheshimiwa na jamii wanayoitumikia.

MAGUFULI ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR LEO,VIFIJO NA NDEREMO VYATAWALA

$
0
0
 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi  na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraiskupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Mhe Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Uraisi  leo agosti 4, 2015.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Uraisi leo agosti 4, 2015.
Picha ya pamoja
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Uraisi mapema leo jijini Dar. 
Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo.

WAKULIMA WATAKIWA KUFUATA USHAURI WA WATAALAMU NA KUFANYIA KAZI MAFUNZO WANAYOPEWA

$
0
0

 Afisa kilimo daraja la kwanza  wa halmashauri ya mbulu  Peter Sangawe   akiwa anaomuonyesha  Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera  jinsi ya kuifadhi  nafaka bila kutumia kemikali  .
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akiwa anakagua vitunguu vinavyolimwa na halimashauri ya mbulu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE KITAIFA LINDI

$
0
0
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua maonyesho ya Nanenane  kitaifa  kwenye uwanja wa Ngongo Lindi Agosti 4, 2015.  Kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa lindi, Mwantumu Mahiza na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mashine ya kunyonyoa kuku wakati alipotembelea banda la kampuni ya ubia kati ya watanzania na wachina ya  Poly Machinery ya Millennium Busibess Park jijijni Dares salaam, baada ya kufungua maonyesho ya Nanenane kwenye uwanja wa  Ngongo Lindi Agosti 4, 2015.
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wafanyakazi wa Bnki kuu ya Tanzania  wakatia lipotembelea banda la la Benki hiyo baada ya kufungua maonyesho ya Nanenane kwenye uwanja wa  Ngongo Lindi Agosti 4, 2015.

Rais Kikwete atia saini kuridhia Miswada ya Sheria mitano hadharani Ikulu, Dar es salaam

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga muhuri wake hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene baada ya kuweka saini kuridhia  Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu Waziri wa Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo Profesa Sifuni Mchome
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo Profesa Sifuni Mchome.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Profesa Sifuni Mchome baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu,jijini Dar.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya, Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa,  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi baada ya hafla ya kuweka saini na kuridhia miswada ya  Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.

PICHA NA IKULU

TAZAMA SHAMRA SHAMRA ZA MAGUFULI ALIVYOCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA CCM

Zitto Kabwe aongea na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo

$
0
0
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ATC Wazalendo Zitto Kabwe akiongea na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Urambo.  (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
 Wanachama wakimsikiliza kiongozi wao Mkuu.
 Wanachama wakimsikiliza Kionozi wao Mkuu kwa umakini mkubwa.
 Katibu Kata Urambo Kati, Mkulila Shabani akizungumza mbelea ya kiongozi Mkuu wa chama na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo
 Mwenyeti Kata ya Kiloleni Tarafa ya  Usoke, Wilaya ya Urambo Kati, Juma Kamagi akizungumza mbelea ya kiongozi Mkuu wa chama na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ATC Wazalendo Zitto Kabwe akiongea na Viongozi wa Matawi ya jimbo hayo.

MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE PETER KISUMO

$
0
0

 Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,Dk.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mwanasiasa Mkongwe nchini Mzee Peter Kisumo aliyefariki dunia jioni ya tarehe 3 Agosti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,Dk.John Pombe Magufuli akizungumza na mjane wa marehemu Pater Kisumo, Hosiana Kisumo nyumbani kwa marehemu mtaa wa Isevya ,Upanga,Dar es Salaam.(Picha na Adam Mzee) BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

DK CYRIL CHAMI KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM JIMBO LA MOSHI VIJIJINI

$
0
0
Video imepigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita. Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.

Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.

Alitolea mfano kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ( REA) nchini ambayo ilipata fedha nyingi katika miaka ya 2011 na 2012 ni miradi ya maendeleo lakini hatima yake ni kuzuia ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya nishati.

Akifafanua fedha hizo zaidi alisema kwamba Tanzania mwaka 2010 jumuiya ya kimataifa zilitoa dola za Marekani milioni 171.93, mwaka 2011 dola za Marekani milioni 225.35, mwaka 2012 dola za Marekani milioni 229.74 na mwaka 2013 Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 175.14.

Utafiti huo ambao uligharamiwa na COMESA, EAC na SADC umewasilishwa katika mkutano wa kitaifa wa uwezeshaji wa miradi ya kukabili tabia nchi kwa mfumo wa ndani ambapo pia Mwakilishi wa mtandao wa FANRPAN, Sithembile Ndema alikuwepo kuelezea maana ya mikutano ya kisera katika nchi zinazounda mtandao huo.

Mtandao huo ambao ulianzishwa mwaka 1994 baada ya mkutano wa mawaziri wa kilimo wa nchi za SADC, EAC na COMESSA na makao makuu yake kuwa nchini Zimbabwe ulianza kazi mwaka 1997 na sasa makao makuu yapo nchini Afrika Kusini.Mtandao huo umelenga kuwezesha mataifa ya Afrika kuendesha kilimo na ufugaji unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kutunza mazingira na kuongeza tija.


Mikutano ya aina hiyo pia inafanyika Uganda, Ethiopia, Kenya na Zambia.
Profesa Yanda alisema kwamba pamoja na fedha hizo kuonekana nyingi kiukweli ni haba kutokana na hali halisi ilivyo sasa na hasa ikizingatiwa kwamba kunatakiwa pia fedha za mabadiliko tabia nchi yenyewe badala ya kutumia miradi ya maendeleo ambao matokeo ni kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1149
Mshehereshaji Hanif Tuwa kutoka ESRF, akitoa mwongozo wa yatakayojiri kwenye mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF.
Alisema takwimu walizopata kuhusu fedha zilizofika nchini kutoka katika jumuiya ya kimataifa zililingana na taarifa zilizopo Hazina na kuonesha kwamba fedha hizo zilienda kutumika katika makadirio yaliyokusudiwa.
“tofauti iliyopo ni tafsiri ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi. Miradi ya maendeleo, inatamkwa kama miradi ya maendeleo lakini ukiangalia mwishoni ni miradi hiyo kusaidia katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi” alisema katika mahojiano baadae na na waandishi wa habari.
Alisema kama Mkurugenzi wa Kituo cha mabadiliko ya tabia nchi anashauri serikali kuhimiza wananchi wake kuendelea kusimamia mazingira vyema huku wakulima na wafugaji wakisikiliza maofisa ugani kwa ajili ya kuwa na kilimo na ufugaji bora usioharibu mazingira..
Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo sasa hata sehemu za baridi za nyanda za juu zimeanza kuwa na magonjwa ya Malaria huku wakulima wakiwa hawajui muda wa kupanda kutokana na mabadiliko ya joto na pia unyeshaji wa mvua.
Alisema pia nyanda za juu sasa zinakabiliwa na wadudu waharibifu wa mazao vitu ambavyo awali havikuwepo.
Alisema kwamba bado taifa linahitaji kufanya tafiti nyingi zaidi na kuzitumia kuelimisha umma kuhusu nini kinatokea na nini kinastahili kufanywa kukabili mabadiliko hayo.
IMG_1174
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akihutubia mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF na kujadili taarifa ya utafiti uliofanywa kwa miaka minne kuhusiana na uwezeshaji.
Mkutano huo wa kitaifa ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Taasisi huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) Dk. Tausi Kida ambaye alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua utafiti uliofanywa na kuja na maazimio yatakayosaidia kuboresha kilimo na kuhifadhi mazingira katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliwaambia washiriki kuiangalia kwa makini tafiti ya Profesa Pius Yanda na kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa wa maudhui na kuwezesha kutoa dira ya utekelezaji katika siku za usoni.
Alisema wakati taifa linajipanga kutekeleza mpango wake wa maendeleo wa kuelekea katika uchumi wa viwanda suala la mabadiliko tabia nchi haliwezi kuachwa na hivyo wajumbe wa mkutano walitakiwa kuangalia na kuja na mapendekezo yao.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na kilimo na ufugaji wenye tija unazoingatia ufanisi katika hifadhi ya mazingira na namna uwezeshaji wa ndani unavyoweza kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni muhimu kilimo kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
ESRF ni taasisi yinayojishughulisha na tafiti mbalimbali za jiuchumi na kijamii zinazotoa mwelekeo wa utekelezaji wa sera na kanuni mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii.
Pmaoja na kuratibu mkutano huo pia ilitoa nafasi ya ukumbi wake kutumika na kutoa mwelekeo wa mkutano na umuhimu wake katika mpango wa pili wa maendeleo wa taifa ambao unatakiwa uzingatie mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1161
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba na kuwakaribisha washiriki wa mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda.
IMG_1203
Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema akielezea mradi wa COMESA wa uwezashaji wa ndani wa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano huo.
IMG_1249
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kulia) wakifuatilia ka umakini 'presentation' ya Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema (hayupo pichani).
IMG_1318
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Pius Yanda, akitoa mada ya ufadhili wa kimataifa wa uwezeshaji wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania katika mkutano huo.
IMG_1370
Pichani juu na chini washiriki wakichangia mawazo yao kuhusu namna sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi inavyopaswa kuwa katika mkutano huo.
IMG_1343
IMG_1150
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali, watafiti, na wadau wa maendeleo waliohudhuria mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1155
IMG_1231IMG_1260
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabianchi.
IMG_1256
Picha ya pamoja ya washiriki.

Mizengo Pinda:Maonesho ya Nane Nane nchini yawa shamba darasa

$
0
0
nane
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maonesho ya 22 ya Nane Nane leo katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. (Picha na Eleuteri Mangi).

Na Eleuteri Mangi-Lindi.

Maonesho ya Nane Nane nchini yamekuwa shamba darasa ambalo wananchi wanakutanishwa kujifunza masuala mbalimbali ambapo wakulima na wafugaji na wananchi kwa ujumla wanaweza kutoka na mambo kadhaa kwa manufaa ya kuongeza kipato cha kaya na taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imetolewa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda leo wakati akifungua rasmi Maonesho ya 22 ya Nane Nane kitaifa mwaka huu katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

“Nimetembelea mabanda mengi nimefarijika sana na nimevutiwa na mambo mengi ya kilimo na maandalizi mazuri yanayopamba maadhimisho haya, katika mabanda hayo nimevutiwa zaidi na banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). “Wamelima mboga mboga, mchicha, vitunguu, biringanya, mahindi, matango na nyanya. Wote mliokuja kwenye maonesho haya mkajifunze uzalishaji huo ni wa muhimu kwa kila mtu”alisema  Waziri Mkuu Pinda.

Aidha, Waziri Mkuu ameiongezea kanda ya kusini miaka miwili zaidi na kuandaa maonesho hayo kitaifa na hivyo yatafanyika miaka mitano mfululizo ambapo yanatarajiwa kujumuisha mwaka 2014 yalipoandaliwa kwa mara ya kwanza hadi 2018.

Muda huo umeongezwa ili kuendelea kufungua na kuboresha miundo mbinu ya viwanja vya Ngongo mkoani Lindi na mikoa ya kusini kwa ujumla ikiwemo huduma za jamii ndani ya mikoa hiyo na kuongeza hamasa ya ushiriki kutoka taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma pamoja na asasi mbalimbali nchini.

Kwa upande wake mkazi wa eneo la Ngongo kijiji cha Tulieni kata ya Mnazi Moja Mkoani Lindi mzee Shaibu Said Chibebedenge amesema kuwa maonesho ya mwaka huu yamaendelea kuwa bora zaidi kuliko mwaka uliopita kwa kuongezeka ubora wa miundo mbinu ikiwemo barabara ndani ya viwanja vya Maonesho.

Maonesho ya Nane Nane nchini yameanzishwa rasmi mnano mwaka 1993 ambapo hadi sasa yanaendelea kote nchini kupitia kanda saba ambazo ni Arusha, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Mwanza, Tabora na Lindi ambapo maonesho hayo yanafanyika kitaifa kwa mara ya pili mfululizo.

WAZIRI MKUU: WANAOHITIMU JKT WAPEWE NYENZO

$
0
0

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itapaswa itafute njia za kuwawezesha vijana wanaohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili waweze kutekeleza kwa vitendo mafunzo wanayoyapata na waweze kujiajiri.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Agosti 4, 2015), wakati akizungumza na wananchi na washiriki wa maonyesho waliohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya 22 ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) ambayo mwaka huu yanafanyika kitaifa kwenye viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.

Akizingumza mara baada ya kutembelea mabanda zaidi ya 10, Waziri Mkuu Pinda alisema kuna haja ya kuwatafutia fursa za kujiajiri vijana wanaohitimu mafunzo hayo ili wasibweteke.

“JKT ndiyo inayofundisha vijana wetu katika fani mbalimbali… tuwatafutie fursa za kujiajiri mara wanapohitimu mafunzo ili wasitoke huko na kubweteka eti hawana kazi,” alisema.

Alisema kuna haja ya kuweka mfumo maalum kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT ambao utawatambua vijana wachache wanaotoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambao hupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kama vile kutengeneza batiki, sabuni, samani, mabanda ya kuku, kufuga mbuzi, ng’ombe, samaki na kuku na kilimo cha bustani za mboga za majani.

“Mtu akishapatiwa ujuzi huu akaachwa arudi kijijini hawezi kufanya chochote… lazima atakaa kijiweni na kudai hana ajira. Tutafute mfumo wa kuwasaidia ili wapate mtaji wa kuanzia, wajiajiri kupitia kile walichofundishwa na baadaye iwe ni mfumo wa kuzungusha ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika,” alisema huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kukipongeza kituo cha utafiiti cha Naliendele kwa kuibua aina mpya 16 za mbegu za korosho ambazo zimesaidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo hadi kufikia tani 200,000 kwa mwaka ikilinganishwa na tani 16,000 miaka michache iliyopita.

“Ninawasihi ndugu zangu wa Lindi na Mtwara tusikilize wataalamu wanatuambia nini kwa sababu utafiti ndiyo mkombozi mkubwa wa kilimo cha Tanzania. Tufuate maelekezo wanayotuelekeza na hii si kwa korosho tu, iwe ni karanga, ufuta au alizeti kwani ni mazao yanayokubali vizuri katika ukanda huu wa Kusini,” alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo imekuwa ikitekeleza mipango ya Kitaifa ikiwemo shughuli za kuendeleza kilimo kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) ambayo imefikia ukomo. “Hivi sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Awamu ya Pili ya Programu hiyo yaani ASDP II. Programu hiyo  imekuwa ikitekeleza Kilimo Kwanza na miradi mbalimbali ya kilimo na imekuwa muhimili muhimu katika kuendeleza kilimo chetu nchini,” alisema.

Waziri Mkuu Pinda amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Wilaya wabadili mitazamo yao kama kweli wana nia ya kuwasaidia wananchi.

“Viongozi hatuna budi tuwe karibu na wananchi na hasa maafisa ugani. Hawa wanapaswa kujituma ili waweze kweli kubadili wananchi kwani asilimia 70 ya Watanzania ni wakulima, wafugaji na wavuvi,” alisisitiza.

Maadhimisho hayo ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) yanatarajiwa kufungwa Jumamosi, Agosti 8, mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 5, 2015.

Rais Kikwete kuzindua benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania AGOSTI 7,2015 JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Thomas Samkyi, (pichani kati) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Benki hiyo,Kinondoni kuhusu uzinduzi wa benki hiyo utakaofanyika Agosti 7, 2015,jijini Dar . Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Sera, Bwana Francis Assenga, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki, Bi Rosebud Violet Kurwijila.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bi Rosebud Violet Kurwijila akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),katika ofisi za Benki hiyo jijini Dar mapema leo kuhusu uzinduzi wa benki hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Thomas Samkyi, na Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Sera, Bwana Francis Assenga.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema asubuhi ya leo

 Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua rasmi benki ya kwanza ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, ambayo inalenga kuanzisha mtizamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbali mbali, kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake, pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda mrefu, ya kati na muda mfupi kwenye sekta ya kilimo. Benki hiyo inatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa sekta ya kilimo ambayo imeajiri zaidi ya aslimia 70 ya Watanzania.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kwa ngazi mbili: ngazi ya kwanza itahusisha uzinduzi wa Makao Makuu ya TADB jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 7 ya mwezi huu; ambapo ngazi ya pili itahusisha uzinduzi rasmi wa TADB mbele ya wadau wake wakuu ambao ni Wakulima, kwenye Maonesho ya Nane Nane Mkoani Lindi, katika kilele cha Siku Kuu ya Wakulima hapo tarehe 8 Agosti 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo yaliyoko Barabara ya Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa benki, Bwana Thomas Samkyi, alisema dhumuni kuu la uanzishaji wa benki hiyo ni kuboresha tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali ili kuwezesha uendelezaji wa miundombinu ya kilimo kama miradi ya umwagiliaji, usafirishaji, uhifadhi, mindombinu ya masoko, n.k. ambayo inachangia maendeleo ya sekta ya kilimo.

‘Uanzishwaji wa benki hii unalenga kuziba mianya mikubwa ya ukopeshaji kwenye kilimo ambayo inaachwa na benki za biashara, ili kuchochea kukua kwa sekta ya kilimo, kwa kutoa mikopo na huduma nyingizezo za uwezeshaji wa kilimo kwa wakulima, ambao wengi wao hawana uwezo wa kupata huduma za kibenki’ alisema Bw. Samkyi.

Akieleza zaidi kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo, Bwana Samkyi alisema Benki ya Wakulima itakuwa msitari wa mbele katika kusukuma shughuli za kilimo pamoja na kuchagiza benki na taasisi nyingine za kifedha kushiriki katika kuwezesha shughuli za kilimo.

‘Benki hii imeundwa ili kutoa mikopo kwa masharti nafuu, pamoja na kutoa huduma nyinginezo zitakazoongeza uwezo wa wakulima kukopa na kuzalisha. Ili kufanikisha haya, benki inabidi iwe na vyanzo endelevu vya fedha za kutosha kwani nchi hii ni kubwa na wadau wa benki ni wengi sana. Lengo kuu ni kubadili kilimo cha Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara’ alisema Bw. Samkyi.

Benki hii pia inatarajiwa kuwa ni kiungo muhimu cha utekelezaji wa mageuzi ya awamu ya pili ya sekta ya kifedha, na vile vile kuboresha maendeleo ya kilimo nchini ikizingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo ya miaka mitano mitano, Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Kilimo, na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA), pamoja na sera mbali mbali za Serikali zinazohusu sekta ya kilimo.
  
Kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania

Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (katika kuanzishwa kwake) ni taasisi mpya ya kifedha iliyoanzishwa na serikali kwa madhumuni ya kuboresha huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na huduma nyinginezo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Benki hii imeanzishwa ili kufikia malengo ya taifa yaliyoafikiwa katika Tanzania Vision 2025, kusudio likiwa ni kuwezesha na kutosheleza upatikanaji wa chakula, kuchochea kilimo cha biashara, pamoja na kuleta maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umasikini.

KAMATI YA UTENDAJI YA CHAMA CHA HABARI ZA MICHEZO (TASWA) KUKUTANA AGOSTI 7 2015 JIJINI DAR

$
0
0

A; KIKAO KAMATI YA UTENDAJI

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), inatarajiwa kukutana Ijumaa Agosti 7, 2015, Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yahusiyo michezo na waandishi wa habari za michezo hapa nchini.


Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitajadili namna bora ambayo chama kinaweza kushiriki kwa kuangalia jinsi ya kuwaunganisha wanamichezo kwa namna mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa maslahi ya michezo nchini.


Moja ya madhumuni ya TASWA wakati inaanzishwa ni kuwaunganisha waandishi wa habari za michezo nchini, kushirikiana katika kukuza na kupromoti michezo na wanamichezo kwa njia ya kalamu na njia nyingine za kupashana habari.

Kwa msingi huo tunaamini kikao kitatoa muongozo mzuri, ambao unaweza ukasaidia wanamichezo hapa nchini kufahamu sera za michezo kwa wagombea mbalimbali na hivyo kufanya uamuzi sahihi wakati ukifika.


Pia kikao kinatarajiwa kufanya uteuzi wa washiriki wa semina mbili zinazotarajiwa  kufanyika hivi karibuni, zikihusisha waandishi wa habari za michezo wa kada ya kati na wale wazoefu.


Tunaamini tumetoka mbali na tunajua safari yetu ya kuchangia kukuza michezo nchini bado ni ndefu na ina mabonde, mabwawa na utelezi. Sisi hatujiulizi ,  Jee tutafika? Bali hujiambia juhudi zetu zitatufikisha tunapotaka kufika.


B; PONGEZI AZAM

Tunatoa pongezi kwa timu ya soka ya Azam FC kwa kuibuka bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ mwaka 2015.


Tunaungana na Watanzania wengine katika kufurahia ubingwa huu, baada ya Jumapili Azam kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo tunawaomba wachezaji watumie ubingwa wa Kagame kama changamoto ya kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani.


Azam wasibweteke na kuona tayari wamemaliza kazi, bali waendelee na jitihada za kutafuta mafanikio makubwa zaidi.


C: UTOAJI WA VITAMBULISHO

TASWA ilisitisha kutoa vitambulisho vipya kwa wanachama wake kwa muda kwa sababu ilikuwa ikifanya utaratibu wa kubadili vile vya awali na kuwa na vitambulisho vya kisasa zaidi, ambapo suala hilo lipo hatua za mwisho kukamilika na hivi karibuni wanachama wote wapya watapatiwa vitambulisho vyao.


Nawasilisha,

Amir Mhando,

Katibu Mkuu TASWA

05/08/2015

STAMICO KUANZISHA MTANDAO WA KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico), Zena Kangoi akizungumza na waandishi wahabari juu mafanikio ya stamico yaliyofanywa katika katika Ofisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuuwa Stamigold, Mhandisi Dennis Sibugwao akizungumza na waandishi wahabari juu Stamico inavyosimamia mgodiwa STAMIGOLD, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Stamico,jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Stamico, Rehema MwakajubeBeatrice akizungumza na waandishi wahabari juu ya mipango mikakati ya uwekezaji wa StamicoiliyofanyikaMakao Makuu ya Stamico jijini  Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Deusdedith Magala, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchongaji ,Alex Rutagwelela.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Zena Kangoi akiwa na baadhi ya wakurugenzi wakati akieleza mafanikio ya shirika hilo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika makao Makuu jijini Dar es Salaam.

 Na ChalilaKibuda,GlobuyaJamii 
 SHIRIKA la Taifa la Madini(Stamico) limesema linatarajia kuzindua mtandao utaosaidia kupata taarifa mbalimbali za kuweza kuchimba kisasa. 

Akizungumza na waandishiwa habari jijini Dar esSalaam, Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji, Zena Kongoi amesema kuwa kuanzishwa kwa mtandao kwawachimbaji wadogo kutawafanya kuweza kukua kiuchumi kuliko ilivyosasa kwa uchimbaji duni. 

Amesema kuwa mtandao utasaidia jinsi ya kuweza kupata vifaa vya kuchimbia madini kutokana na taarifa zitazowekwa katika mtandao. 

“Lengo letu ni kuwa saidia watanzania wenzetu katika uchimbaji wamadini kuweza kwenda kisasa zaidi nasio uchimbaji duni ambao unarudisha maendeleo yao”amesema Zena. 

Amesema Stamico imeongeza mapato yake kutokana na uwekezaji wakupitia kampuni tanzu za utoaji wa huduma za kibiashara kutoka Sh.Milioni 281 kwa mwaka fedha 2014 /2015 hadi kufikia Sh.Bilioni 3.17 kwa fedha 2014 /2015. 

Zena amesema wanatarajia kuzalisha umeme wamakaa yamawe ya Kiwira ambapo watazalisha megawati 400 za umeme hali ambayo itapunguza tatizo la umeme kwashirika  licha yakuweka miradi yakusaidia wachimbaji wadogo lakini wameweza kuwekeza uchimbaji wamadini kwakushirikiana na makampuni mengine kutokana shariaziliwekwa baada ya mabaoresho ya shirika hilo. 

Amesema baadhi yamiradi ya uzalishaji wa  madini imeanza kuzalisha na kuwezasha shirika kutoka hatua moja kwenda nyingine katika utoaji huduma pamoja ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kuongeza ajira nchini kutokana na miradi ya uzalishaji wa dhahabu. 

Zena amesema kuwa shirika limeanzisha miradi kuendeleza wachimbaji wadogo kitaalamu na ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu (SMMRP) katika kuwaondoa katika uduni. 

Amesema katika mradi wa Stamigold umesafirisha na kuuza dhahabu katika nchi ya Switzerland kwa kiasi cha Wakia 12,923.35 na kuingizia shirika la Taifa la Madini (Stamico) na taifa kwa ujumla Dola za marekani Milioni 15.6. na kuaza kurejesha mrabaha wa asilimia 4.0 ya mauzo sawa na sh.1.3 milioni za serikali na Wizara ya Nishati na Madini na kulipa ushuru sh.milioni 40.

Aidha amesema shirika limeweza kuanzisha mradi wa ununuzi wa madini ghafi ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa maeneo ya vijiji vya Kabingo,Murongo ,Syndicate na Rugasha katika Wilaya Kyerw,mkoani Kagera na kuyauza madini hayo kwenye soko la nje ya nchi ikiwa na lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo . 

Zena amesema wako katika mazungumzo na Benkiya TIB kuweza kukopa Dola za Marekani700,00090000 kwaajili ya kununua mitambo hali ambayo shirika litaweza kukua katika kuendesha miradi mbalimbali. 

MOJA YA KIPAUMBELE CHETU NI KUIGEUZA TTB KUWA MAMLAKA - DK MERU

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi devota Mdachi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (Mwenye miwani) kuzungumza na wafanyakazi alipotembelea bodi hiyo jana.
Mmoja wa wafanyakazi wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano akielezea jambo kwa Katibu Mkuu alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuzungumza na wafanyakazi. 
 Baadhi ya wanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania wakimsikiliza kwa makini  Katibu Mkuu Dk Meru alipokuwa akizungumza nao.

 Na: Geofrey Tengeneza
Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kuupa kipaumbele mchakato wa kuifanya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania (TTA) kwa lengo la kuiwezesha Bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Aidha Wizara hiyo imeitaka TTB  kuangalia ni maeneo gani yanaweza kuwa ni vyanzo vya mapato vitakavyoiwezesha Bodi kujiingizia fedha.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuuwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru  alipotembelea Makao makuu ya Bodi ya Utalii yaliyoko katika jengo la IPS jijini Dar es salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bodi hiyo.
Dkt Meru ameipongeza   Bodi ya Utalii kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika mazingira yenye changamoto nyingi hasa za kifedha zinazoikabili. Amesema TTB ndiyo chombo chenye dhamana ya kutangaza vivutio vya utalii kwa ujumla wake, hivyo kinapaswa kuwezeshwa kutimiza jukumu hilo kwa niaba ya nchi badala ya kila taasisi kutangaza vivutio inavyosimamia.
“Tunawajibu wa kuwawezesha TTB mtekeleze majukumu yenu vizuri kwa kuwa ninyi ndio hasa mliokabidhiwa jukumu la kutangaza vivutio vyetu vyote vya utalii kama vile vya kihistoria, fukwe, wanyama, milima na kadhalika” alisema.
Hii ni ziara ya kwanza ya Dk Meru kutembelea Makao Makuu ya ofisi za Bodi tangu kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo. Bodi ya Utalii Tanzania ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara yake yenye jukumu la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAWASILISHA MIRADI YAO YA KILIMO NA MAZINGIRA KWA WANAKIJIJI WA KISANGA WILAYANI KISARAWE PWANI

$
0
0
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa katika moja ya kisima ambacho maji yake yananukia Mafuta, maji haya yanatumika zaidi katika shughuli za Kufulia Nguo.
 Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona aliyesimama (Kulia) akizungumza na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pamoja na wanakijiji katika Kijiji Cha Kisanga jana.
 Kundi la kwanza la Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Mazingira..
 Wanakijiji na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasikiliza jinsi Miradi inavyo wasilishwa.

 Kundi la pili la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora.

 Kundi la Tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora cha Mboga Mboga na Hihogo.

 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana .
 Wenyeji pamoja na  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo...
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shijaa wa chakula 2o15 linalo andaliwa na Oxfam kupitia kampeni yao ya Grow , kipindi kinachoruka kila siku ITV kuanzia Saa Kumi na mbili  Jioni na Kurudiwa saa Tano na nusu asubuhi  wakiwa katika ofisi ya Kusindika zao la Mihogo

********
Ni siku nyingine tena katika kijiji cha Kisanga, jua la saa nne asubuhi ni kali huku  mti huu mkubwa wa mkorosho uliopo eneo la makutano unatusitiri. Washiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano lililiondaliwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow, walikuwa wamesimama vikundi vikundi, bila shaka walikuwa wanahadithiana chakula walichowapikia wenyeji wao jana. 

Siku ya ilikuwa  inaanza kwa waandaaji wa shindano kutengeneza makundi matatu ya kina Mama Shujaa wa Chakula watano watano. 

Kwa muda watakaokaa hapa kijijini Kisanga, kila kundi linatakiwa kutengeneza mradi wa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kijiji cha Kisanga. Ili kufahamu fursa na changamoto zilizopo, uongozi wa kijiji unawatembeza sehemu nne. 

Upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapa ni changamoto. Kina Mama Shujaa wa Chakula wanaletwa sehemu hii yenye bwawa, wenyeji wanaiita lamboni. Inasadikika kuwa zamani kulikuwa na kisima, ila kwa sasa kimefunikwa na wingi wa maji. Pia kuna viumbe wakali kama vile chatu. 

Elimu ya msingi katika kijijini Napo inatolewa katika shule ya msingi Kisanga. Wakina Mama Shujaa wa Chakula wanaoneshwa mandhari ya shule na mwenyeji. 

Wakazi wa kijiji cha Kisanga wanapata maji ya kunywa na kupikia katika visima vilivyopo eneo hili linaloitwa Mfuru. Kufuatia msimu wa mvua ulioisha, visima vyote vinne vina maji ya kutosha, japo kisima kimoja maji yake hayatumiwi kwa kunywa kwani yana harufu inayosadikika kuwa ni ya mafuta. Hata hivyo, wakati wa kiangazi kina mama (wenyeji) wanalazimika kuamka saa tisa alfajiri kutokana na uhaba wa maji, na kibaya zaidi usalama wao wakiwa njiani ni wa mashaka kwani hawapewi msaada na waume zao (kwa walioolewa). 

Ziara ya kutembelea kijiji inafika kwenye hospitali/kituo cha afya cha Kisanga. Kina Mama shujaa wa chakula wanashangaa kuambiwa bei kubwa ya matibabu katika kituo hicho, ambacho kwa siku ya leo kimefungwa. 

Zao kuu la Kisanga ni mihogo. Ziara ya kina Mama Shujaa wa Chakula inaishia katika kituo cha kusindika mihogo. Hapa kunasagwa unga wa mihogo, pia tambi na keki za unga wa mihogo zinatengenezwa hapa. 

Naam, muda wa makundi kuwasilisha mapendekezo ya mradi wa maendeleo endelevu waliopanga mbele ya wanakijiji wa Kisanga unawadia.

KUNDI LA KWANZA 

Kutoa elimu juu ya mazingira, Kuchimba mashimo ya taka. Wafanyabiashara wanawake walio barabarani wafunike chakula ili vumbi lisiingie.Wana Kisanga wote watahitajika kufanya usafi jumamosi.  Kuanzisha shamba darasa na kutoa elimu.

KUNDI LA PILI
Biashara cha mboga na matunda kwenye bonde (karibu na bwawa) kwa kutumia mbolea asili na maji yaliyopo. Kutoa elimu kwa kupitia shamba darasa jinsi ya kutumia rasilimali za kijiji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji

KUNDI LA TATU
Mradi wa kilimo bora. Kilimo cha mbogamboga na kilimo cha mihogo na mahindi kwenye muinuko wa bonde. Wananchi kupewa elimu ya kilimo bora, kutumia wataalamu waliopo

Siku inaisha kwa waandaaji kupanga makundi matatu mapya ambayo watapewa kazi ambayo lazima iishe kesho hiyohiyo.

ILI KUMPIGIA KURA MSHIRIKI  BOFYA HAPA>>>
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images