Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA BALOZI WA MSUMBIJI

$
0
0
unnamed (8)
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa msumbiji nchini,Dkt. Vicente Mebunia ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 3, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TAA yatoa ufafanuzi Hitilifa Uwanja wa Ndege wa Mwanza

$
0
0
download (4) Na Lorietha Laurence- Maelezo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja  Ndege nchini (TAA)  Bw Suleiman Suleiman  ametoa ufafanuzi kuhusu hitilafu ya umeme iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa imetokana na marekebisho ya kangavuke (generator) ya dhalula katika uwanja huo.
Bw. Suleiman ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii na kuongeza kuwa kila kiwanja cha ndege nchini kina generator ya dhalula.

“Viwanja vyote vya ndege nchini vina generator za dhalula, lakini kwa upande wa Mwanza hivi karibuni, generator hiyo ilipata tatizo la kiufundi na taarifa ilitolewa kwa makampuni yote ya usafirishaji wa abiria wanaotumia uwanja huo” alisema Bw. Suleiman. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, mamlaka imeshafanya utaratibu wa kununua generator mpya itakayofungwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati wowote kuanzia sasa kutatua tatizo hilo.

Aidha Mkurugenzi huyo wa TAA nchini ameeleza kuwa pamoja na tatizo la kukatika umeme katika uwanja wa ndege wa Mwanza, hali ya usalama katika uwanja huo pamoja na viwanja vingine nchini iko vizuri.

“Pamoja na tatizo hili, nawahakikishia wasafiri wanaotumia viwanja vya ndege nchini na watanzania kwa ujumla kuwa hali ya usalama katika viwanja vyetu imethibitiwa,” amesema.Tanzania ilishika nafasi ya pili mwaka 1999 ilipokaguliwa na shirika la usalama wa usafiri wa Anga Duniani ambayo hufanya ukaguzi kwa wananchama kuhakikisha kuwa nchi wanachama wanafikia vigezo. Shirika hilo linatarajia kufanya ukaguzi mwezi Septemba mwaka huu.

Hivi karibuni abiria wa kwenda Mwanza kupitia kampuni ya usafirishaji ya Fastjet walihairishiwa safari zao kutokana na hitilafu ya umeme katika viwanja vya ndege vya Mwanza ambao ulikuwa ukifanyiwa matengenezo tangu ijumaa iliyopita.

MGOMBEA MTEULE WA URAIS CCM,DKT MAGUFULI KUCHUKUA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KESHO

$
0
0
 MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. John Magufuli, kesho Jumanne, Agosti 3, 2015, atawasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Msafara wa Dk. Magufuli  kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshila Polisi.

Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombeamwenza wake, Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Dk. Magufuli alichaguliwa na Mkutnao Mku wa CCM, uliofanyika Oktoba 11,2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose Migiro na Amina Salum Ally. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifafanua jambo kwa umakini mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTOTO YATIMA

$
0
0
Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka barozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea vituo vya watoto yatima katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.

Shughuli hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto na kula nao chakula cha pamoja kilichoandaa kwaajili ya watoto hao.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa vituo hivyo ambapo alibaini changamoto balimbali zinazokabili vituo hivyo.

Yolanda ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia  jamii yake ambapo alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.

Kwa nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.

"mbali ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.

MAMAKU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA

$
0
0
me1
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ballozi mpya wa Tanzania nchini Saud Arabia, Hemed Mgaza, wakati alipofika kumuaga Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 3, 2015. Balozi Mgaza  anakwenda nchini Saud Arabia, kuanza kazi rasmi baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete. Picha na OMR

Tanzania yawa kivutio katika Maonyesho ya Afrika Mashariki yanayofanyika Nairobi Nchini Kenya

$
0
0
Ufunguzi wa maandamano ya maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama JAMFEST yaliyoanza leo katika Viunga vya Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyata uliopo jijini Nairobi Kenya.
Muongozaji wa bendi ya polisi nchini Kenya akiongoza maandamano ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo nchi zote za Afrika Mashariki zimeshiriki maonyesho hayo yanayoanza leo katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyata.
Msafara wa uzinduzi wa maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiwa unatoka katika viwanja vya Uhuru Park uliopo ndani ya jiji la Nairobi kuelekea katika Viunga vya Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyata ambapo baadhi ya wakazi wa nchi mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wakionyesha bidhaa zao.
Watanzania wakiwa na bendera ya nchi kabla ya maandamano kuanza Katika viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi.
Watanzania wakiwa na furaha ya kushiriki maonyesho ya jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoanza kufanyika katika Viwanja vya KICC Nairobi Kenya.
Watanzania wakitoa burudani katika viwanja vya Uhuru Park kabla ya Maandamo ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoanza leo katika viwanja vya KICC Nairobi Kenya.
Tanzania Kwanza mengine baadae..
Wadau wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

WAFANYABIASHARA MKOANI SHINYANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA BIASHARA KATIKA MIGODI YA ACACIA.

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Injini Philbert Rweyemamu akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao na wafanyabiashara hao kilichokuwa na lengo la kuwapatia ufahamu juu ya masuala ya manunuzi.
Bwana Nixson Mlumba – AfisaManunuzi wa ACACIA akifafanua jambo wakati wa Kikao hicho.
Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini maelezo ya kutoka kwa Uongozi wa Kampuni ya Acacia wakati wa Kikao hicho.
Mmoja wa wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga akichangia mawazo wakati wa kikao.
Wafanyabiasha wa mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya Pamoja na mkuu wa Mkoa na viongozi kutoka kampuni ya ACACIA.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa Shinyanga.

WAFANYABIASHARA wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchangamkia Fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na Mgodi wa Dhahabu Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Acacia.

Meneja mkuu wa Mgodi huo Injinia Filbert Rweyemamu ametoa wito huo katika kikao baina ya uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga ambapo alisema  mgodi wa Migodi inayomilikiwa na Acacia imejikuta ikishindwa kufanya kazi na wafanyabiashara wa mkoani humo kutokana na wengi wao kushindwa kukidhi vigezo vya taratibu za manunuzi kutokana na wengi wao kuwa na mitaji midogo hali ambayo imepelekea huduma nyingi za manunuzi kuwategemea wafanyabiashara wakubwa kutoka maeneo mengine.

“Nia ya Kampuni ya ACACIA ni kufanya kazi na wafanyabiashara wanaotuzunguka lakini kuna chanagamoto ya wengi wenu kushindwa kufikia vigezo vya manunuzi ambavyo ACACIA imejiwekea, niwaase kupitia vikao hivi ambavyo vimelenga kuwapatia uelewa mkajipange na ikiwezekana jiungeni katika vikundi ambavyo vitakuwa na mitaji mikubwa itakayowawezesha kuwa na uhakika wa kufanya kazi na migodi yetu” Alisema Injinia Rweyemamu.


Injinia Rweyemamu ameongeza kuwa kwa sasa huduma nyingi Pamoja na bidhaa vikiwemo vipuli vya magali na mitambo wamekuwa wakitegemea wasambazaji wakubwa kutoka nje, huku akisisitiza kuwa kama wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga wangeungana na kuwa na biashara hizo Migodi yetu isingelazimika kuagiza bidhaa hizo nje.

Kwaupande wake mtaalamu wa masuala ya manunuzi ya ndani na Maendeleo ya biashara wa ACACIA Bwana Nixson Mlumba akitoa taarifa za namna ambavyo wafanyabiashara wa Shinyanga wamekuwa wakishiriki kufanya biashara na ACACIA amesema takwini zinaonyesha ushiriki mdogo sana wa wafanyabiashara wa mkoa huo huku wengi wao wakishindwa kufikia vigezo vya manunuzi ya ACACIA kutokana na wengi wao kuendesha biashara kinyume cha Sheria.

“Kama alivyosema meneja wa mgodi wa Buzwagi, Fursa zipo cha msingi zingatie sharia za nchi na jiunge kwa Pamoja ili muweze kuongeza mitaji ya biashara zenu, Hatupendi kufanyabiashara na mtu ambaye baada ya kumpatia tenda atashindwa kutuhudumia kwa mujibu wa Mahitaji yetu” alisema Nixon
  
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephina Matiro alisema kuwa fursa hii ambayo inatolewa na kampuni ya ACACIA haina budi kuchangamkiwa na wafanyabiashara wote wa kanda ya Ziwa kwani itasaidia katika kuongeza pato lao Pamoja na pato la Taifa.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassor Rufunga awali alisema kuwa mgodi wa Buzwagi umekuwa kifua mbele katika suala la shughuli za maendeleo ndani ya Mkoa huo  huku ukishirikiana na wakandarasi wa ndani ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa na zahanati.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema licha ya wakandarasi wa shughuli za ujenzi kuonyesha uwezo mzuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, bado wafanya biashara wengine wameshindwa kuchangamkia fursa hizo zinazotolewa na Mgodi, hali ambayo imepekea fursa hizo kutumiwa na wafanyabiashara wa maeneo mengine ya nchi na wakati mwingine wafanyabiashara wa nje ya nchi.

Mkutano huo uliofanyika katika hotel ya Submarine wilayani Kahama ulilenga kuwasaidia wafanyabiashara wa mkoa huo kupata ufahamu juu ya masuala mbalimbali ya manunuzi katika kampuni hiyo.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA TANGAMANO MJINI TANGA LEO

$
0
0
J1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya Uzinduzi wa wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani 2015 wakati wa sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga leo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni Endesha salama okoa maisha.
J2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Kamanda wa mkuu wa Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga wakati Rais alipowasili katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga kuzindua rasmi maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yenye kauli mbiu endesha Salama Okoa maisha.
J3
Baadhi ya wanafunzi wakiandamana na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu usalama barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga leo(picha na Freddy Maro).

Mh Anne Makinda ashiriki Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na WiLDAF jijini Dar es salaam

$
0
0
Maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 31 July toka tamko rasmi la Umoja wa Afrika mnamo mwaka 1962 lililotolewa jijini Dar es Salaam -Tanzania.

WiLDAF Tanzania imekuwa ikiratibu maadhimisho haya hapa nchini ikiwa pia ni siku maalumu ya kusherehekea mafanikio ya wanawake wa Afrika. Katika maadhimisho hayo WiLDAF ilizindua ripoti ya kwanza ya hali za haki za Wanawake nchini Tanzania ya mwaka 2014 iliyozinduliwa na Mh. Anne Makinda, (SPIKA wa Bunge).

Maadhimisho haya yalifanyika siku ya ijumaa tarehe 31 July 2015 katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Mh. Anne makinda akiwasili ukumbini pamoja na mwenyekiti Mh Naomi Kaihula na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya WiLDAF Edda Mariki, na mkurugenzi ?mtendanji wa WiLDAF Dkt Judith Odunga .

Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt. Judith Odunga akimshukuru Mgeni rasmi Mh. Anne Makinda katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika.

Mgeni rasmi Mh. Anne Makinda akizindua ripoti ya hali za hali za wanawake nchini Tanzania ya mwaka 2014 iliyoandaliwa na WiLDAF

Mgeni rasmi Mh Anne Makinda akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Wanawake wa Afrika iliyoandaliwa na WiLDAF

Washiriki kutoka mashirika mbalimbali wakifuatilia mada katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa afrika iliyoandaliwa na WiLDAF

Mama Laeticia Mkurasi akihamasisha wanawake kutitokeza katika uchanguzi mkuu, katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika yaliyoandaliwa na WiLDAF

Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora

$
0
0
Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
  Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupatakura 34 katiya 39 zilizopigwa.

Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkutano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? 

Waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum.
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi.
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.

Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
Team Irene wakifuatilia mchakato

SIO JAMBO LA AJABU KWA MWANACHAMA YEYOTE KUHAMA CCM-NAPE

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATINGA NDANI YA STUDIO YA KILIMANJARO

$
0
0
 Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik

 Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.

 
 Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza  Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.
 Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
  Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
 Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro,  Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

BANDA LA NSSF LAVUTIA WENGI MAONYESHO YA NANENANE

$
0
0
Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kusini, Ndandavala akipewa maelezo na Ofisa Uhusiano  Muandamizi  Salim Kimaro alipotembelea Banda la NSSF kwenye maonyesho ya Nananane.
Afisa Uendeshaji Muandamizi Bi. Kabona Kandoro akitoa Maelezo ya faida mbambali kwa mmoja wa wakazi wa Lindi waliotembelea kwenye banda la NSSF.
Mmoja wa watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakati wa maonyesho ya Nanenane mkoani Lindi.
Wakazi wa Mkoa wa Lindi wakipata maelezo kuhusu mafao yanayotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipotembelea banda la NSSF kwenye Maonyesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Lindi.

UMEME WA GESI ASILIA KUANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUNI

$
0
0
 Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Tanesco akitembelea miradi ya umeme wa gesi alisilia iliyogunduliwa Mtwala, katika kituo lilichojengwa na Kampuni ya mafuta ya Tanzania Petrolium Development Corpolation (TPDC) hii ni sehemu iliyojengwa ni kituo kikubwa cha kutunzia gesi ya kutengenezea umeme katika kituo cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari katika katika ziara ya waziri wa nishati na madini George Simbachawene, kukagua miradi ya umeme wa gesi asilia katika kituo kikubwa cha kufikia gesi asilia kilichopo kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha kufikia gesi asilia inayotoka Mtwala ili iweze kutengeneza umeme kutokana na umeme wa maji kupungua kutokana na vyanzo vya maji vya mto Mtera na Kihansi kupungua maji kwaajili ya mabadiliko ya hali ya hewa.Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Mataragio.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Mataragio. wakielekea kwenye kituo cha kutengeneza umeme cha Tanesco kilichopo Kinyerezi jijini Dar es Salaam baada ya kukagua kituo cha gesi hii leo katika ziara ya kukagua miradi hiyo.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


 
Kituo cha gesi asilia kilichopo Kinyereza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mafundi wa kituo cha gesi asilia cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),akitoa maelekezo kwa waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene wakati wakitembelea Kituo cha Umeme wa gesi asilia cha Tanesco.  
 Meneja wa Kituo cha Umeme cha wa gesi asilia wa Tanesco, Mhandisi John Mageni akizungumza katika kituo cha umeme wa gesi asilia cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelewa na waziri wa Nishati na madini,George Simbachawene.
Mitambo ya umeme ya Kituo cha umeme wa gesi asilia kilichopo Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mafundi wa kituo cha umeme wa asilia cha Tanesco akiendelea kufanya matengenezo katika kituo cha kufua umeme wa gesi asilia cha Kinyerezi jinini Dar es Salaam.
 Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MATOKEO KURA ZA MAONI JIMBO LA MOSHI MJINI YAMPA USHINDI DAVIS MOSHA.

$
0
0
Video imepigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WASICHANA WATOANA JASHO AIRTEL RISING STARS

$
0
0
 Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Ilala Fatuma Salumu (Kushoto)
akichuana na mchezaji wa timu ya Simba Queens Mwanaidi Hamisi katika
michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0.
 Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Ilala Fatuma Salumu (Kushoto)
akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Simba Queens Asha Abdul katika
michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0.

Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Simba Queens Eva Charles
(Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Ilala Fatuma Salumu katika
michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0
 


Timu ya wasichana ya Simba Queens jana iliibuka na ushindi wa 2 – 0
dhidi ya timu ya Ilala katika michuano ya vijana ya U-17 ya Airtel
Rising Stars kwa mkoa wa kisoka wa Ilala. Mchezo huo ulipigwa katika
uwanja wa kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam jana.

Timu zilianza mchezo huo kwa kujihami na kushambuliana kwa kushtukiza.
Simba Queens walifanikiwa kupata goli la mapema baada ya Zainab
Mahmoud kuifungia timu yake katika dakika ya tano.

Timu ya Ilala ilibadilika baada ya kuwa nyuma kwa goli moja na kuanza
kushambulia kwa kasi. Lakini juhuhudi hizo hazikuzaa matunda na hadi
mapumziko timu ya Simba Queens walikua wanaongoza kwa goli moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikicheza kwa
umakini wa hali ya juu. Simba Queens waliongeza kasi na kufanikiwa
kupata goli la pili katika dakika ya 46 kupitia kwa Khadija Ally baada
ya kuachia shuti kali lililotinga wavuni moja kwa moja.

Katika kiwanja cha Tanganyika Packers, Mburahati Queens iliichakaza
Lulu Queens kwa magoli 2 -1. Wafungaji wa Mburahati Queens walikua ni
Anne Adrea dakika ya 56 na Janeth Christopher dakika ya 90. 
Wakati kwa upande wa Lulu walipata goli lao kupitia kwaOpah Clement dakika ya 46.Katika kiwanja cha Makangarawe Yombo Timu ya wavulana ya Wakati Ujaoilipata ushindi wa 2 -1 dhidi ya Dubu. 

Kwa upande wa wasichana timu za
Evergreen Queens na Temeke Queens zilienda sare ya bila kufungana.
Michuano hii ya vijana ambayo kwa jiji la Dar es Salaam imeshaanza kwa
takriban katika mikoa yake yote ya kimichezo, inafuatiliwa kwa karibu
na jopo la makocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
bila kusahau timu mbalimbali ambazo zinawanyatia kwa karibu vijana
wenye vipaji kutoka michuano hiyo.

Huu ni mwaka wa tano kwa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
kuanzisha na kudhamini michuano hiyo ya Airtel Rising Stars yenye
lengo la kutafuta na kuendeleza vipaji.

Mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka huu yanajumuisha mikoa ya
Ilala, Temeke, Kinondoni, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha ambapo
fainali za taifa za michezo hiyo zimepagwa kupigwa jijini Dar es
Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21.

LAPF YANGARISHA MAONESHO YA NANENANE –DODOMA

$
0
0
 Mwanachama akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Bi Rehema Mkamba
 Banda la Mfuko wa Pesheni wa LAPF ambalo lipo kwenye jengo la Ofisi ya waziri Mkuu, uwanja wa Nanenane, Dodoma
Wanachama wakipata maelezo kuhusu bidhaa zinatolewa na LAPF ambazo ni uwezo wa kujichangia katika mfumo wa hiari, mkopo wa elimu, mkopo wa kujikimu, mkopo wa nyumba na fao la uzazi. 

LAPF ni mfuko bora wa pensheni Tanzania pia umeshiriki Maonesho haya ya Nanenane 2015.LAPF ipo banda la ofisi za Waziri Mkuu TAMISEMI
Katika banda hilo, LAPF tunatoa huduma zote za hifadhi ya jamii,kuu zikiwa ni;Elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania yaani tumetoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi.

Tunaandikisha wanachama wapya wa hiari, wa kisheria na waajiri na kutoa vitambulisho hapohapo kwenye banda la LAPF
Wanachama wanapata fursa ya kuona michango yao na ya mwajairi na kupata nakala inayo onyesha michango yaoTunajibu maswali yawanachama, kupokea maoni ya wanachama na wananchi wote kwa ujumla.

LAPF inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kujifunza kuhusu hifadhi ya jamii, kujiunga na kujionea huduma bora zilizo pelekea  LAPF kuzawadia tuzo ya mfuko bora na msimamizi na mdhibiti wa sekta  ya hifadhi ya jamii pia kupata tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa miaka mitano kwa utunzaji bora wa mahesabu ya mfuko
Karibu sana banda la LAPF.

MGOGORO WA MAENEO YA KILIMO YA VIJIJI VYA ZANZABAR WAISHA

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Hati  ya umiliki wa eneo la Kilimo kwa Bwana Yuweni Kibwana Nzukwi  Mmoja miongoni mwa wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi  baada ya upatikanaji wa ufumbuzi wa mgogoro wa maeneo hayo.
  Mkulima Ana Nyaka Buluju wa Dole    akikabidhiwa hati ya umiliki wa eneo la kilimo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hapo Skuli ya Wazazi Dole Wilaya ya Magharibi  “A “.
Baadhi ya wakulima wa  Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi wakifuatilia zoezi la kukabidhiwa hati zao za umiliki wa maeneo ya kilimo kwenye Vijiji vyao lililafanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.



HATMA ya Mgogoro wa maeneo ya Kilimo unaowahusisha Wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke, Kijichi na Nguruweni dhidi ya baadhi ya watu wanaovamia  maeneo hayo hivi sasa umeshafikia ukingoni baada ya kurindima kwa takriban miaka 12.

Mgogoro huo ulizuka kufuatia baadhi ya watu wenye uwezo wa kifedha pamoja na marafiki na familia za maafisa wa taasisi za Kilimo kuvamia maeneo hayo wakati wakielewa kwamba wakulima wa asili wa maeneo hayo walikuwa wakiyatumia kuendeleza shughuli zao za kilimo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitekeleza Ahadi ya Serikali aliyoitoa Tarehe 14 Disemba mwaka 2012 ya kuwamilikisha Wakulima hao alikabidhi Hati za umiliki huo kwa Wakulima 145 wa Dole, Ndunduke na Kijichi hapo katika maeneo ya skuli ya Wazazi Dole.

Wakulima hao 145 ni miongoni mwa wote Mia 222 wa Vijiji hivyo ambao walipata hati hizo baada ya kuyatumia maeneo hayo ya Serikali  yaliyokuwa chini ya Wizara ya Kilimo wanayolimwa kwa kipindi kirefu cha maisha yao.

Akizungumza na Wakulima na Wananchi wa Vijiji hivyo vya Dole, Ndunduke na Kijichi Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamuwa kufanya hivyo ili kuwapa fursa ya umiliki wakulima hao waendeleze shughuli zao za Kilimo kwa utulivu zaidi akiwatanabahisha kwamba maeneo waliyopewa ni kwa ajili ya kilimo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru na kuwapongeza Wananchi na Wakulima wa Dole, Ndunduke, Nguruweni na Kijichi kwa ustahamilivu wao mkubwa waliouonyesha ambao umeipa faraja Serikali na kufikia hatua njema na ya mafanikio.

Akitoa Taarifa fupi katika mkutano  huo wa makabidhiano ya hati ya umiliki wa maeneo ya kilimo, Mwenyekkiti wa Wakulima wa Dole, na Ndunduke Dr. Daudi Silas Mukaka alisema Serikali Kuu imeonyesha nia thabiti ya kuwajali Wananchi wake.

Dr. Mukaka alisema Wananchi pamoja na Wakulima wa Dole na Ndunduke wamefarajika sana kutokana na kazi kubwa iliyochukuliwa na Serikali  Kuu chini ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kilimo na Ardhi katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hilo la mgogoro wa maeneo ya kilimo.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi  alisema licha ya Wananchi wa Vijiji hivyo kuonyesha ishara ya hasira lakini alifarajika kuona kwamba busara ilitawala katika kulishughulikia tatizo hilo.

Mheshimiwa Abdullah alisema Wananchi hao wanapaswa kuendelea kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kutokana na Uongozi wake wa busara wa kuweka ahadi na akawa makini kuitekeleza.

Migogoro ya ardhi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar hivi sasa inaonekana kuchukuwa sura mpya ya kuanza kuchukuliwa hatua za ufumbuzi kutokana na uamuzi wake wa kusajili ardhi yote ya Zanzibar.

MKUTANO MKUU WA CHADEMA WAMPITISHA MH. LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS WA TANZANIA NA DKT. JUMA HAJI DUNI MGOMBEA MWENZA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (wa nne kulia) akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) pamoja na Mgombea Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni (mwenye suti nyeusi) pamoja na wanachama wapya wa Chama hicho, wakati wakitambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais alieteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais wa CHADEMA, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

BODI YA USAJILI WA WAHANDISI (ERB) YAELEZEA MAFANIKIO YAKE NA SERIKALI YA AWAMU YA NNE KWA KIPINDI CHA MWAKA 2005-2015

$
0
0
 Msajili Mkuu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), Mhandisi Steven Mlote.
 Msajili Mkuu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Steven Mlote (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya bodi hiyo na serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha mwaka 2005-2015. Kulia ni Msajili Msaidizi wa bodi hiyo, Mhandisi Benedict Mukama na na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani wa ERB, Vicentus Vedasto..
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

BODI ya Usajili ya Wahandisi nchini (ERB) imewafutia vibali vya 
usajili wahandisi 330 baada ya kubainika kukiuka taratibu za ufanyaji kazi wa bodi hiyo.

Hayo yalibainishwa na Msajili Mkuu wa bodi hiyo Mhandisi, Steven Mlote wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya bodi hiyo na serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha mwaka 2005-2015laam jana.

Mlote alisema kufutiwa vibali vya wahandisi hao imetokana na uchunguzi wao walioufanya katika vipindi tofauti na kubaini mapungufu makubwa katika kutekeleza majukumu yao ya  sekta ya ujenzi hapa nchini.

"Hatua hiyo ilifikiwa na bodi yetu baada ya kujiridhisha na kufikia maamuzi hayo baada ya kufanya uchunguzi wa kina" alisema Mlote.

Alisema kufanyakazi za uhandisi chini ya kiwango ni hatari na ndio maana waliamua kuchukua tahadhari ya kuwafutia vibali wahandishi hao.

Mlote aliongeza kuwa mbali na hatua hiyo ERB imezifungia kampuni 32 za wahandisi kampuni, 17 ni za kizalendo na 15 ni za kigeni.

Alifafanua kuwa kwa kipindi chote hicho wamekuwa wakidhibiti mienendo shughuli za kihandisi nchini huku akiziangalia kwa 
umakini kampuni zilizopata usajili ziwe na utendaji mzuri.

Mlote alisisitiza kuwa ni marufuku kwa kikundi cha watu au mtu 
kufanya shughuli za Kihandisi bila kusajiliwa na watachukuliwa 
hatua za kisheria kwa makosa hayo.

Katika miaka ya  karibuni Ujenzi ulio chini ya kiwango umesababisha maafa mengi na chanzo kikubwa ni Ujenzi ulio chini ya kiwango.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images