Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 598 | 599 | (Page 600) | 601 | 602 | .... | 1896 | newer

  0 0


   MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015, za Tume hya Taifa ya Uchaguzi, (NEC), kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumamosi Agosti 1, 2015. 
   
  Dovutwa amekuwa mgombea wa kwanza kuchukua fomu hizo na kazi iliyo mbele yake ni kutafuta wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Dovutwa alifuatana na mgombea mwenza wake, Hamad Mohammed UIbrahim na wanachama wachache wa chama hicho.
   MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akikabidhiwa fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, kutoka kwa afisa uchaguzi mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 1, 2015.
  Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti hicho za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
   

   Barua ya kutoka chama cha UPDP inayomtambulisha Dovutwa, (kushoto), kuwa ndiye mgombea wake wa kiti cha Rais zikikaguliwa na afisa mwandamizi wa tume hiyo, William Kitebi
   Dovutwa akitoka makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, na mkoba wenye fomu hizo baada ya kukabidhiwa.

   
   Fahmi Dovutwa, mgombea wa kiti cha Rais kupitia UPDP
  Mgombea mwenza wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UPDP, Hamad Mohammed Ibrahim
   Mtikila akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu
  Mtikila akipewa utaratibu wa kuzitumia fomu hizo
  Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti hicho za Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  Mgombea kiti cha urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, akionyesha mkoba wenye fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, baada ya kukabidhiwa

  Maxmillian Lyimo, mgombea kiti cha Rais wan Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TLP

  0 0

  Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira huku mchezaji wa timu ya Polisi akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo huo
  Kazi hiyo kuwania mpira kati ya wachezaji hawa wakiwa wameinua madaruga yao juu bila ya mafanikio kuupata mpira.
  Mshambuliaji wa timu ya Simba na kipa wa timu ya Polisi wakiwania mpira wakati wa mchezo wao huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan Simba imeshinda 2--0.
        Kipa wa timu ya Polisi akiokoa mpira golini kwake huku mchezaji wa Simba akiwa nyuma yake
  Mgeni wa rasmin katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Polisi Zanzibar Kamishna wa Polisi Zanzibar Ndg Hamdanmi kulia Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Ndg Hassan Chura na kushoto Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Taifa Hashim Salum na Kiongozi wa timu ya Polisi.wakisimama wakati ukipigwa wimbo wa Polisi na Usalama wa Raia kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan Simba imeshinda 2--0 
  Wachezaji wa timu ya Polisi na Simba wakisimama wakati wa kupigwa kwa wimbo wa Usalama wa Raia kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuaza mwezi ujao.  
  Makocha wa Simba wakifuatilia wimbo huo maalum uliopigwa wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 2--0.
  Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
  Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
  Kikosi cha timu ya Polisi Zanzibar kilichokubali kipigo cha bao 2--0 kutoka kwa timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
  Kikosi cha timu ya Simba kilichotowa kipigo cha mabao 2--0 dhidi ya timu ya Polisi Zanzibar wakati wa mchezo wao wa kujipima nguvu wa tatu kisiwani Zanzibar ikiwa imeshinda michezo yake yote

  Mchezaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Polisi wakati wa mchezo wao wa kirafiki kujipima nguvu kujiandaa na Ligi Kuu zinazotarajiwa kuaza hivi karibuni Ligi ya Tanzania Bara na ya Zanzibar.
  Mchezaji wa Simba akijiandaa kumpita beki wa timu ya Simba, wakati wa mchezo wao wa kirafiki katika mchezo huo timu ya Simba imeshinda 2--0
                         Wachezaji wa timu ya Simba na Polisi wakiwania mpira
  Mshambuliaji wa timu ya Simba akiweka majaro golini kwa timu ya Polisi 
  Picha na OthmanMapara.Blog Zanzinews,com. 

  Picha na OthmanMapara,Blog Zanzinews.com .

  0 0

  frank Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa mkoani.
  frank Kibiki akionyesha walivyo kosea jina lake.


  na mwandishi wetu,iringa


  WAKATI kura za maoni za kutafuta wagombea ubunge katika majimbo yote nchini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) zikipigwa leo, mmoja kati ya wagombea 13 wanaotafuta nafasi hiyo Jimbo la Iringa Mjini, Frank Kibiki anataka zoezi hilo jimboni humo libatilishwe.

  Wagombea wengine ni pamoja na Dk Augustino Maiga, Dk Yahaya Msigwa, Frederick Mwakalebela, Nuru Hepautwa, Michael Mlowe, Aidan Kiponda, Addo Mwasongwe, Jesca Msambatavangu, Mahamudu Mgimwa, Peter Mwanilwa na Fales Kibasa.

  Akizungumza na wanahabari hii leo, Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa mkoani hapa alisema kura hizo zinapoteza uhalali kwasababu jina lake limekosewa.

  “Mimi naitwa Frank John Kibiki, lakini kwenye karatasi ya kupigia kura ameandikwa mgombea mpya aliyetajwa kwa jina la Frank John Kibiri,” alisema.

  Alisema kwa kuwa Frank Kibiki na Frank Kibiri ni watu wawili tofauti, hawezi kukubali kutumia jina la Kibiri ili kuhalalisha mchakato huo na endapo atafanya hivyo wagombea wenzake wanaweza kukata rufani kupinga matokeo hayo.

  Kibiki alisema ameandika barua ya malalamiko yake kwa uongozi wa CCM wa Manispaa ya Iringa huku kopi ya malalamiko hayo yanayotaka uchaguzi huo ufanyike upya baada ya karatasi ya kupigia kura kusahihishwa akiipeleka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

  Akikiri kupokea barua ya mlalamikaji huyo na dosari iliyojitokeza kwenye karatasi hizo za kupigia kura, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi alisema; “suala hili tulikubaliana na mgomea huyo tulimalize kwa kusahihisha kwa peni jina hilo. Baada ya kuifanya kazi hiyo kabla ya zoezi lenyewe la upigaji kura kuanza, zoezi limeendelea kama kawaida.”

  Taarifa ya Mwampashi imepingwa na Kibiki mwenyewe aliyesema katika vituo 81 kati ya 90 vya upigaji kura alivyotembelea ni kituo kimoja tu cha Umati alichokuta jina lake limerekebishwa katika karatasi hizo.

  Huku akiahidi kuishtaki kampuni iliyopewa kazi ya kuchapisha karatasi hizo kwa kukosea jina lake, Kibiki alisema; “katika hili sitanyamaza, nitakuwa sauti ya yoyote aliyewahi kuonewa ndani ya chama  vinginevyo nitalazimika kusubiri miaka mitano ijayo ili nishriki kwenye mchakato mwingine wa haki.” Alisema.

  Wakati huo huo Katibu wa CCM wa Manispaa hiyo amezungumzia idadi ya wana CCM waliojitokeza katika mchakato huo wa kura za maoni kuwa ni ndogo ikilinganishwa na matarajio yao ya kushirikisha wanachama zaidi ya 18,000.

  0 0

    Mgombea nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.
   Mgombea nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kumpa ushirikiano mgombea wa nafasi hiyo aliyeshinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo na kukamatwa kwake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


  Na Dotto Mwaibale

  MGOMBEA nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera amesema atampa ushirikiano mgombea wa nafasi hiyo aliyeshinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhakikisha CCM inapata ushindi.

  Nawera aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa kura za maoni katika jimbo hilo na kuhusishwa na kukamatwa kwake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa.

  "Nampongeza mwenzangu aliyeongoza kura za maoni katika jimbo la Kawe na ninaahidi kushirikiana na mgombea mwenzangu atakaye teuliwa na vikao vya uteuzi vya CCM kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu na kuwa ushindi wa kishindo kwa CCM kuanzia udiwani, ubunge na urais".  alisema Nawera.

  Akizungumzia kuhusu mchakato huo na kuhusishwa na rushwa aliilalamikia Takukuru kwa kumuhusisha na tukio hilo kuwa walikuwa na nia ya kumsaidia mmoja wa wagombea nafasi hiyo na yeye kumpunguza nguvu kisiasa.

  Nawera alisema licha ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika mchakato huo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa lakini katika mazingira ambayo hakuyategemea amebambikiwa tuhuma hizo ambazo hakuwa nazo.

  Aliongeza kuwa wakati wa ukamatwaji wake hawakumjulisha kuwa yupo chini ya ulinzi, pia hawakujitambulisha na wala hawakumuambia anatuhumiwa kwa kosa gani na bila kumpa nafasi ya kuwasiliana na ndugu zake au mwanasheria na kumpeleka kituo cha polisi Magomeni.

  Nawera alisema si jambo zuri kwa vyombo vya dola kumkamata mwananchi na kumuhusisha na tuhuma mbalimbali hiyo si sahihi na ni matumizi yasiyofaa ya rasilimali za nchi na matumizi mabaya ya madaraka.

  Muwania ubunge huyo Julai 30, 2015 saa mbili usiku alikamatwa na maofisa wa Takukuru kwa kuhusishwa na rushwa na baada ya mahojiano alisweka rumande kwa masaa 10 na kuachiwa kwa kujidhamini mwenyewe. 
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

  0 0

  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake, Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Segerea mwisho jijini Dar es salaam, wakati akitangaza kujiondoa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Jumapili Agosti 2, 2015.

  0 0

  Wakazi wa Kata ya Kimbiji,Wilaya Temeke mkoani Dar-es-Salaam wamemchagua tena katikakura za maoni Diwani wao Mheshimiwa Muhidini Bunaya Sanya kugombea tena nafasi ya udiwani wa Kata hiyo ya Kimbiji hiliyopo wilaya Temeke.  

  Diwani wao huyo kijana Muhidini Bunaya Sanya (pichani) ameshinda kwa kura za maoni 1462 dhidi ya mpinzani wake ambaye alipata kura 68 tu,Kwa maana hii Kijana Muhidini Bunaya Sanyaamembwaga mpinzani wake kwa tofouti ya kura 1394 !Mheshimiwa Muhidini Bunaya Sanya amefanikiwa tena kukitetea kiti chake cha udiwani wa kata ya Kimbiji kuelekea katika uchaguzi mkuu 2015  kwa kupitia tiketi ya chama cha CCM.

  Diwani Muhidini Bunaya Sanya anajulikana sifa  za kuwa ni mchapa kazi,mbunifu na mpenda maendeleo mwenye uchungu na Kimbiji ambaye
  katika kipindi kilichopita alisimama kidete ufanikishaji wa ujenzi wa shule zaMsingi na sekondari katika kata ya Kimbiji,Uchimbaji wa visima vya maji nausambazaji wa umeme ambazo huduma zote hizo kwa sasa zipo kata ya Kimbijiiliyopo wilayani Temeke,mkona Dar-es-Salaam.

  Wakazi wa Kata ya Kimbiji wanawaomba wananchi wote kusimama bega kwa bega  Bwana  Muhidini Bunaya Sanya ili aweze kututumikia tena katika nafasi ya udiwani na kutuwakilisha katika baraza la madiwani la wilaya ya Temeke. Pendekezo la kata ya Kimbiji Muhidini Bunaya Sanya aka Jembe La Pini wa Chuma.

  Usikose kuungana na wanakimbiji at www.facebook.com/wanakijiji.kimbiji

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 mara baada ya kurejea kutoka  Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine waliofika kumpokea alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida  alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.

  PICHA NA IKULU


  Akiwa nchini Australia Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania.

  Rais Kikwete pia alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania ambapo walizungumzia  namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.

  Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo.

  Rais Kikwete alihitimisha ziara yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.

  0 0


  Na Jeff Msangi wa TBN Ughaibuni.
  Nyota njema huonekana asubuhi. Bila shaka umewahi kusikia msemo huu. Kwa Zahara Muhidini Issa Michuzi, nyota yake njema ni tunu ya uongozi. Tangu alipoweza kutambua maana na tofauti ya jambo jema na baya, amekuwa kiongozi.
  Muhtasari wa maisha yake unaonyesha alizaliwa mnano tarehe 2 Septemba mwaka 1987 Nzega mkoani Tabora. Amesomea katika shule zifuatazo;

  *Shule Ya Msingi Rufita, Tabora- 1995-2001

  *Shule Ya Sekondari Kazima, Tabora-2002-2005

  *Shule Ya Sekondari Ya Juu Emma, Kampala-Uganda 2007-2009

  *Chuo Kikuu Cha Dodoma, Dodoma,Tanzania 2011-2014.


  Zahara Muhidini Issa Michuzi, ambaye ni binti wa Ankal, ni mhitimu wa Shahada ya Sanaa katika masuala ya Uchumi. Mpaka kufikia hapa alipo, nyota yake ya uongozi imejidhihirisha katika sehemu mbalimbali alizopitia hususani shule.

  Amekuwa kiranja, msimamizi  wa shughuli na miradi mbalimbali shuleni na alipokuwa Chuo Kikuu Dodoma alikuwa kiongozi katika Jumuiya ya Wanafunzi- University of  Dodoma Students Organization (UDOSO) akiwa kama Mbunge wa Baraza La Wanafunzi.Mbali ya uzoefu wa kiuongozi alionao, Zahara anazo sifa zifuatazo ambazo ni nadra na tunu kubwa katika uongozi;

  Anajitambua- Zahara anajitambua vilivyo. Anatambua kwamba uongozi ni heshima na utumishi uliotukuka.

  Ana Ari Ya Kuongoza na Kujifunza- Zahara anaamini kwamba kiongozi bora lazima awe ana ari ya kuongoza na kutumikia wananchi anaowaongoza. Mbali ya kuongoza,kiongozi lazima awe tayari kujifunza kutokana na hali halisi na kukabiliana na mabadiliko ya aina yoyote yanayoweza kujitokeza.

  Ni Msikivu Na Ana uwezo Mkubwa wa Kufanya Kazi na Watu- Hili Zahara amelithibitisha katika ngazi zote za kiuongozi ambazo amepitia. Usikivu wake umekuwa chachu ya kumwezesha kutatua matatizo mbalimbali ambayo amekabiliana nayo huku yeye kama kiongozi akitarajiwa kuyatatua.

  Ana Uwezo Wa Kuongoza Mabadiliko Ya Kijamii- Zahara anaamini kwa vitendo kwamba jamii yoyote lazima isonge mbele ili kwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali ya kijamii. Anaamini kwa vitendo kwamba uongozi thabiti unahitajika ili kuleta mabadiliko chanya ambayo jamii yoyote inahitaji. Zahara Muhidini Issa Michuzi hivi sasa anagombea kuwa mwakilishi wa vijana Bungeni kupitia Viti Maalumu Vijana (Youth Seats) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)- Tabora. Anaomba Kura na Ushirikiano Wako.


   Ankal akifurahi na binti yake Zahara siku ya Maulid maalumu ya kusherehekea kuhitimu digrii ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka jana. Hii ndiyo siku ambayo Zahara aliweka nia hadharani kwamba angependa kugombea Ubunge mkoani Tabora ili kumuenzi marehemu mama yake kwa kuwatumikia wananchi wa mkoa huo kwa moyo wake wote.
  Zahara akifurahi na Mama yake mlezi
   Zahara akiwa na dada zake
   Zahara akiwa na familia yake
   Zahara akiwa na baba yake mzazi, Ankal
   Zahara akiwa na baba yake na Mama yake Mlezi ambaye ni dada wa marehemu mama yake, Bi Rehema Saidi
  Zahara akiwa na baba na wadogo zake.      


  0 0

  Mh January amepewa tena ridhaa ya kuendelea kugombea Jimbo la Bumbuli na wana CCM katika uchaguzi uliofanyika ndani ya chama na Kuibuka kinara kwa kura nyingi na zakishindo dhidi ya wagombea wenzake.
  Hivi Ndivyo Matokeo yalivyokuwa.....

  0 0
 • 08/02/15--20:30: Article 10

 • 0 0  0 0

  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano waNHC, Bi Suzan Omari akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo waliokuwa wakisimamia michezo mbalimbali wakati wa tamasha la NHC Family Day lililofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach mwishoni mwa wiki likishirikisha wafanyakazi wa shirika hilo jijini Dar es salaam na familia zao na kufahamiana ikiwani pamoja na kubadilishana mawazo.
  ????????????????????????????????????
  Wafanyakazi hao wakishindana katika mbio ufukweni.
  ????????????????????????????????????
  Mmoja wa wafanyakazi wa NHC akiwa amejishindia Jogoo katika shindano la kufukuza kuku.

  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wafanyakazi wakijiandaa kushindana katika mbio za magunia.
  ????????????????????????????????????
  Wakichuana vikali katika mbio za magunia.
  ????????????????????????????????????
  Lazima kitoweo kikamatwe hapa.
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano waNHC, Bi Suzan Omari akishiriki katika kusimamia upangaji wa timu za mpira wa miguu.
  ????????????????????????????????????
  Walishiriki pia katika mchezo huu ambao niliwahi kuucheza sana nikiwa mtoto.
  ????????????????????????????????????
  Mchuano wa kuvuta kamba.
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa michezo hiyo

  0 0

  Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika mashariki na kusini Dr. Bello Moussa, akizungumza wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa ulipewa jina la Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na teknolojia kujadili changamoto za mawasiliano pamoja na ukuaji wa broadband katika nchi za Afrika. Mkutano ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano Huawei Tanzania Bw. Jimmy Nlinguo akipokea tuzo ya uongozi bora kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selina M. Lyimo kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na wizara hiyo katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam kujadili changamoto za mawasiliano pamoja na jinsi ya kuongeza ukuaji wa broadband katika nchi za Afrika.
  Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania akisema maneno machache ya shukrani kwa wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia mara baada ya kampuni yake kutunikiwa tuzo ya uongozi bora na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na wizara hiyo katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika Mashariki na kusini Dr. Bello Moussa, akijibu maswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake kwenye mkutano wa kimataifa uliondaliwa na wizara ya mawasiliano, sayansi na teknolojia uliopewa jina la “Connect to Connect (C2C)” uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kampuni yake kutunikiwa tuzo ya uongozi bora na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es salaam.

  Kampuni inayongoza katika sekta ya teknolojia na mawasiliano nchini Tanzania (Huawei) imetunikiwa tuzo ya uongozi bora kutokana na mchango wao mkubwa sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini.

  Tuzo hiyo imetolewa siku ya jana katika hoteli ya kimataifa ya Ramada jijini Dar es salaam ambapo mkutano wa kimataifa wa siku mbili unaendelea. Wizara ya mawasiliano na teknolojia huadhimisha mkutano huo kila mwaka kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.


  Mkutano huo umewaleta pamoja wadau katika sekta ya teknolojia na mawasiliano, watunga sera, wawekezaji pamoja na wafumbuzi mbalimbali kwa nia ya kujadili mbinu za kukuza teknolojia ya ‘Broadband’ kati ya nchi na nchi barani Afrika, kutoka pwani hadi pwani na uvumbuzi utakaosaidia kusukuma uchumi wa Tanzania na kukuza ubora wa huduma za jamii.

  Huawei walipokea tuzo hiyo kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia baada ya kuwa mstari wa mbele katika sekta ya teknolojia sayansi na mawasiliano pamoja na kuwa kiongozi katika utafiti na kuchangia katika ukuaji na usambazaji wa teknolojia ya broadband nchini Tanzania.

  Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika  Mashariki na Kusini, Dr. Bello Moussa alisema “ Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika katika miaka ya hivi karibuni zimeonyesha shauku kubwa kwenye kuwekeza na kukuza teknolojia ya broadband. Changamoto ni kwamba nchi hizi zipo katika hatua tofauti ya maendeleo ya teknolojia ya taarifa na mawasiliano na kwa bahati mbaya asilimia 90 ya wananchi wake bado hawajapata huduma hii ya broadband majumbani mwao na hivyo wako nyuma ukilinganisha na masoko yaliyoendelea.”

  Huawei walitumia mkutano huo pia kutambulisha mtandao wake wa LTE ambao umepewa jina la “Mkakati wa Huawei kuelekea 5G”. Wakati wa utambulisho huo, Huawei iliweka bayana mchakato mzima wa kuhama kutoka 3G kwenda 4G/4.5G hadi 5G.

  Kuhamia kwenye teknolojia ya LTE ni kuongeza ushindani. Teknolojia ya LTE inazidi kukomaa baada ya teknolojia hiyo kusambaa kwenye mitandao. Akitambulisha mtandao mpya wa 5G wakati wa warsha ya ‘Connect to Connet’ (C2C) ambayo pia ilidhaminiwa vilivyo na kampuni ya Huawei Tanzania, Makamu wa Rais wa Huawei ‘Wireless marketing’, Alex Wang alisema “Huawei wamesaidia ujenzi wa mitandao karibia 200 ya LTE dunia nzima na kujizolea uzoefu wakutosha katika mageuzi ya mitandao ya simu.

  Huawei inaendelea kuwa makini katika kulinda uwekezaji wa wateja wake na muhimu zaidi kulenga katika ukuaji na mageuzi ya mitandao ili kusaidia wateja wake kuongeza ushindani”.

  Mchango wa Huawei katika utafiti wa 5G umetambulika katika sekta nzima na ndio maana wakatunukiwa tuzo ya “Mchango bora katika maendeleo ya 5G” katika warsha ya LTE iliyofanyika Amsterdam, Uholanzi wakati wa mkutano wa dunia wa 5G tarehe 26 June 2015.

  Hii pia ni mara ya pili kwa serikali ya Tanzania kutambua mchango na jitihada za Huawei nchini ambapo licha ya tuzo ya jana ni pamoja na Huawei kutimiza makubaliano ya mkataba kati yake na serikali  juu ya  mchakato wa teknolojia na mawasiliano ili kutimiza malengo ya nchi ifikapo mwaka 2025.

  0 0


  ????????????????????????????????????
  Askofu na Dokta Mwakibolwa wa EAGT pamoja na maaskofu wenzake wakiombea albam hizo kabla ya kuzizindua rasmi kushoto ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kamuni ya Msama Promotion..
  ????????????????????????????????????
  Askofu na Dokta Mwakibolwa wa EAGT akizindua rasmi albam hizo kushoto Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
  ????????????????????????????????????
  Maaskofu na wachungaji wakiwa wameshikilia albam zao mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion.

  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya maaskofu na wachungaji waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia wakati mwimbaji huyo akiimba jukwaani.
  ????????????????????????????????????
  Mwimbaji nguli wa muziki wa injili Bonny Mwaitege akiimba katika uzinduzi wa albam zake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na maelefu ya wapenzi wa muziki wa ijini akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa muziki huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya kwaya kutoka katika baadhi ya makanisa ya jijini Dar es salaam, Bonny Mwaitege alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa ikwango kikubwa huku akiwa amevalia vazi la Kinigeria wakati akiwa jukwaani, wapenzi wa muziki waliohudhuria katika uzinduzi huo walijikuta kila mmoja akijitikisa pale alipo kutokana na kuvutiwa na nyimbo za mwimbaji huyo kutoka mkoani mbeya
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi huo.


  ????????????????????????????????????
  Mwimbaji nguli wa muziki wa injili Bonny Mwaitege akiimba katika uzinduzi wa albam zake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na maelefu ya wapenzi wa muziki wa ijini akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa muziki huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya kwaya kutoka katika baadhi ya makanisa ya jijini Dar es salaam, Bonny Mwaitege alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa ikwango kikubwa huku akiwa amevalia vazi la Kinigeria wakati akiwa jukwaani, wapenzi wa muziki waliohudhuria katika uzinduzi huo walijikuta kila mmoja akijitikisa pale alipo kutokana na kuvutiwa na nyimbo za mwimbaji huyo kutoka mkoani mbeya.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  ????????????????????????????????????
  Mwimbaji nguli wa muziki wa injili Bonny Mwaitege akitunzwa na wapenzi mbalimbali wa muziki wa injili wakati alipokuwaa akiimba jukwaani
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Msama Promotion wakishiriki katika sala.
  ????????????????????????????????????
  Sala ikiendelea kabla ya kuzinduz albam hizo.
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
  ????????????????????????????????????
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wafanyakazi wa Msama Promotion wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries linapenda kuwaalika katika siku tatu za mkutano wa uamsho utakaofanyika hapa Washington DC.
  Ni kati ya Agosti 14-16 2015

  Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ama Masanja Mkandamizaji alipohudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya Jumapili 07/07/2013 katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES

  0 0

  Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akisikiliza kwa makini taarifa fupi iliyosomwa mbele yake na Afisa mkuu wa ubalozi wa Ghana hapa Tanzania Dr. Ken Kwaku kuhusiana na utendaji kazi wa Ecobank nchini Ghana na bara la Afrika kwa ujumla na kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa kibiashara kati ya Ghana na Tanzania. (Katikati) ni Balozi wa Ghana nchini Kenya Mhe. Karim. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
  (Wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi mkuu wa Ecobank nchini Tanzania Mr. Enoch Osei-Safo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings aliyekua akiongea kuhusiana na mikakati ya kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania kupitia benki hiyo. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
  Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam
  Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakimsikiliza kwa makini Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings aliyekua akiongea na wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam
  Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania kwenye picha ya pamoja na Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings (katikati) mara baada ya kumaliza mkutano uliowakutanisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam

  0 0

  Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akipokea fomu ya kugombea urais kutoka kwa Afisa Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adam Nyando katika ofisi za NEC leo jijini Dar es Salaam.
  Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CHAUMA nje ya ofisi NEC leo jijini Dar es Salaam. (Pichana Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)  Na Chalila Kibuda, Globuya Jamii.
   MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe amechukua fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo jijini Dar es Salaam, Rungwe amesema watanzania kama wanahitaji maendeleo wachague chama hicho na sio kuchagua watu wanaotaka kutumikia matumbo yao. Amesema zoezi la kuchukua fomu za urais ziko wazi na kutufanya wagombea kuwa huru katika zoezi zima kutoka na maandalizi yalifanywa na tume ys Taifs ys Uchaguzi.

  Rungwe amesema mwaka 2015 aligombea kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi lakini kura hazikutosha na kufanikiwa kupata wabunge wawili kwa tiketi kwa chama hicho. Amesema ana uwezo wa kuwatumikia watanzania na sio kwenda Ikulu kwa ajili ya kutafuta jinsi ya kujinufaisha na kuwaacha watu walionipa ridhaa ya kuwaletea maendeleo.

  Aidha amesema nafasi ya urais sio ya mchezo kutoka na na kuwa majukumu makubwa ya kuwatumikia watu katika kuwapa maendeleo yatayotokana nafasi hiyo.

   “Nina imani watanzania wataichaugua CHAUMA katika kuperusha bendera katika kuweza kupata maendeleo kama kauli mbiu ya chama kutaka ukombozi” anasema Rungwe. Vyama vilivyochukua fomu ya urais vimefikia vinnea mbavyo ni, Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), UPDP, Chama cha Democratic Party (DP), pamoja na Chauma.

  Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli anatarajia kuchukua fomu kesho katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dar es Salaam. mwisho

  0 0

   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  Umoja wa Wanazuoni wa Kiislaam nchini umetaka kuwepo kwa amani katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Umoja huo , Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi,Suleiman Kilemile amesema nchi nyingi zimeingia katika machafuko kutokana na uchaguzi hivyo nchi yetu isiingie huku.

  Amesema kauli za viongozi  wa siasa za hivi karibu katika michakato ya kuelekea uchaguzi zinaweza kuharibu amani yetu hivyo ni wakati wa  umefika kuweza kuangalia lugha za kutumia katika kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.

  Kilemile amesema amani iliyopo lazima iendelee kulindwa katika kujiepusha na machafuko ambayo nchi zingine zimeingia kutokana na siasa.

  Amesema miaka mitano ya mwisho katika nchi ya Misri wanawinda amani ya watu kutokana na maumivu  wanayoipata ambapo nchi hiyo ilikuwa ya amani. 
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania Shehe Suleiman Kilemile akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO.
   Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi wa Umoja wa wanazuoni wa Kiislam tanzania, Ally Said Bassaleh akizungumza na waandishi katika ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania Shehe Suleiman Kilemile wakati akizungumza kuhusiana na amani ya nchi wakati wa uchaguzi mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu.  
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0
 • 08/03/15--07:36: Article 1
 • Last call to attend the
  CYBER DEFENCE EAST AFRICA 2015 SUMMIT
  “PROTECTING THE INTERCONNECTED WORLD”
  NRDEA in collaboration with TCRA together are organizing the Cyber Defense East Africa Summit which will be held at Mlimani City Conference Hall from 11th to 13thAugust 2015 with the theme “PROTECTING THE INTERCONNECTED WORLD. The guest of honor will be Hon.Ambassador Ombeni Sefue the Chief Secretary to the Cabinet and head of the public service. Experienced   Speakers on Business transformation, technology and cyber security from within and outside the country will attend and   speak at the event.  Business leaders including CEOs’, Directors, CIOs’, CFOs’, Auditors, lawyers; information security experts from various industries in east Africa will also exchange their business knowledge and network with the rest of the participants. 

  With over 6 leading security and technology vendors/companies in the world will be available for exhibition and showcase their product with open discussion from any participants.

  To get a ticket call +255 719 253 037 / +255 222 110 895 or send an email to info@nrd.co.tz
    
  More details www.cybersecurity.co.tz


  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Alternative Communication Bw. Emmanuel John katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha bodaboda mara baada ya kusajiliwa na kukabidhiwa jezi jana kwenye ukumbu wa Princess Sinza Mapambano, Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Vodacom Stratton Mchau akizungumza na waendesha bodaboda ktk hafla hiyo.
  Waendesha boda boda wa Kanda ya Temeke wakiwa katika mkutano mkutano wa pande nne, ambao ni uongozi wa Alternative Communication, Jeshi la Polisi, Vodacom na Bodaboda wenyewe.
  Baadhi ya waendesha bodaboda waliokwisha jisajili katika mradi huo wakiwa kazini kuliendeleza libeneke huku wakiwa na uhakika wa bima pale inapotokea ajali.

  ZOEZI la kuwatambua waendesha bodaboda na kuwasajili katika mfumo maalumu wa kumbukumbu (database) liliendelea tena mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo safari hii waendesha bodaboda katika kanda ya Kijitonyama wamesajili na kupewa mafunzo muhimu katika maeneo ya usalama barabarani, ujasiriamali na bima.

  Kufanyika kwa zoezi hilo hapo jana ni mwendelezo wa mchakato unaofanywa na kampuni ya mawasiliano, masoko na matangazo ya Alternative Communication ya jijini Dar es Salaam, ikishirikiana na jeshi la polisi, lengo likiwa kuwasaidia waendesha bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.

  Hatua hiyo ina kuja kufuatia madai kuwa baadhi yawaendesha bodaboda wasio kuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu au kutumiwa na wahalifu kuvunja Amani na kupotea bila ya kutambulika.

  Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Emmanuel John Rutagonya, amesema jijini Dar es Salaam kwamba tayari kampuni hiyo imekwisha wasajili bodaboda 3,000 katika mfumo huo. Ameongeza kwamba wale waliosajiliwa pia watapata faida ya kupewa huduma ya bima ya afya, mafunzo ya usalama barabarani na  Ujasiriamali.

  Mwenyekiti huyo mtendaji alisema wale wanaosajili wa katika mfumo huo wanapewa koti (Reflectors) zilizo na namba ya usajili kifuani na nyuma ya koti. Namba hiyo ni utambulisho kamili wa mwendesha pikipiki, pia kwenye kofia zao (helmet) itabandikwa namba ya simu ya Kiongozi wa Chama cha Waendesha Bodaboda husika.

  “Mtu yoyote akiipiga namba ya chama cha waendesha bodaboda na akataja namba ya usajili wa dereva wa bodaboda, mfumo utamtambua dereva huyo mara moja.”Alisema.

  Kwa upande wake Meneja Mauzo Kanda ya Kawe wa Kampuni ya Simu ya Vodacom, ambao ni wadhamini wa mradi huu, Stratton Mchau, alisema Vodacom imeridhishwa sana na mradi huu, na kwamba mbali na mambo mengine ya kiudhamini, Vodacom pia itawateua baadhi ya madereva wa bodaboda kuwa mabalozi wa bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kubwa ya simu nchini.

  Waendesha boda boda wa Kanda ya Temeke wakiwa katika mkutano mkutano wa pande nne, ambao ni uongozi wa Alternative Communication, Jeshi la Polisi, Vodacom na Bodaboda wenyewe.


older | 1 | .... | 598 | 599 | (Page 600) | 601 | 602 | .... | 1896 | newer