Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

KIDOTI :VIJANA WA JIJI LA ARUSHA CHANGAMKIENI FURSA ZA KIJASIRIAMALI

$
0
0


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo  (kidoti) akiwa na mabalozi wake aliwapata ndani ya mkoa wa Arusha tayari kwa kwenda mtaani kutangaza bidhaa zake zake za kidoti zilizoingia jijini Arusha kwa mara ya kwanza 



 warembo wa Kidoti wakiwa wako katika pozi wameshikilia baadhi ya bidhaa za Kidoti 

 mmoja wa mabalozi wa kidoti  aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari

 Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A hii leo wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao
 mabalozi wa kidoti   wakiwa kazini.

 baadhi ya bidhaa zinazosambazwa nakidoti jijini Arusha
 hizi ndizo ndala za kidoti
 mawigi ya kidoti ndio haya

Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
Wito umetolewa kwa vijana ndani ya jiji la Arusha kujitokeza katika
kuchangamkia fursa za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza
kuwaepushia vijana na matendo maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya
jamii kukosaa thamani.
Wito huo umetolewa na Joketi Mwigelwa (kidoti) wakati akichagua vijana
wajasiriamali ndani ya jiji la Arusha katika ukumbi wa triple A jijini
hapa ambapo anatarajia kuwapata wajasiriamali vijana ambao
hatawaingiza katika fursa ya wajasiriamali kwa kupitia kampuni yake ya
kidoti.

Alisema  kuwa amevutiwa  kuja kuwekeza ndani ya jiji la Arusha  katika
nyanza za ujasiriamali kwa kuwa anaelewa kuwa vijana wa jiji la Arusha
hususa ni wasichana wana muitikio mkubwa katika swala zima la
ujasiriamali na maendeleo binafsi.

Aidha alibainisha kuwa katika  mchakato huo wanatarajia kupata
wajasiriamali wapatao 13 ambapo tofauti na kujiingizia kipato cha
ujasiriamali pia watakuwa mabalozi wa kutangaza bidhaa zilizo chini ya
kampuni ya kidoti.
“ndugu mwandishi unavyowaona hawa wote hapa ni vijana kutoka mkoa
mzima wa arusha na mikoa ya jirani tunawafanyia usaili na kupata
vijana ambao wanakithi vigezo vya kuingia katika ujasiriamali ,utakao
wapelekea wao kufanya kazi na kampuni ya kidoti pamoja na kujiajiri
binafsi” alisema kidoti

Pamoja na hayo alisema kuwa kampuni hiyo kwa mwaka huu imeamua
makusudi kusogeza huduma za  ikiwemo bidhaa zake katika mikoa ya nje
ya jiji la Dar Es Salaam ili kuwapa furusa watu wa mikoani ambao
walikuwa hawazipati huduma za kidoti.

Kwa upande wa mmoja wa washiriki waliojitokeza katika mchujo huo
Anolia Agustino  alimpomgeza kidoti kwa hatuqa aliofikia ya kuwaajiri
vijana haswa wasiochana kwani   ,jambo hili litawasaidia wanasichana
wengi kupata ajira pamoja na kujiajiri binafsi.

Aidha alisema kuwa  mbali na kupata ajira pia kampuni hii itawasidia
kujifunza ujasiriamali pamoja na kujiajiri binafsi kwani ,bidhaa za
kidoti ni za bei na fuuu na unaweza kuanza kujiajiri kwa kutumia mtaji
mdogo.
Kwa upande wa mshiriki mungine ambaye teari alikuwa amenufaika na
kampuni ya kidoti aliyejitaja kwa jina la Anjela Mushi alisema kuwa
kampuni hii imemsaidia sana kwani alikuwa anakaa nyumbani bila kazi
lakini alivyoona kwenye mtandao wa kijamii aliamua kujitafuta
mawasiliano na kuanza  na mtaji mdogo na kwasasa ivi mtaji wake
umekuwa.

“mimi nilianza kuona bidhaa za kidoti katika mitandao ya kijamii kama
intagramu  nikaamua kutafuta mawasilano kwakeli nilipata na nilikuwa
na mtaji mdogo kwani nilianza na mtaji wa shilingi laki moja na sasa
na shilingi laki nne na biashara yangu nilianza mwezi wa tano na sasa
ni mwezi wa saba  kwa hadi sasa nina mienzi mitatu nashukuru mungu
mtaji wangu umekuwa”alisema Anjela.
Alimalizia kw akumpongeza kidoti na kumsihi aendelee kuwasaidia
wasichana kwani hivi sasa kumekuwa na changamoto ya ajira kwani ajira
imekuwa ni ngumu.

MHE.DAVID KAFULILA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE TENA KATIKA JIMBO LA KIGOMA KASINI KUPITIA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI

$
0
0
 Mhe Kafulila akihutubia maelfu ya wakazi wa Nguruka mara baada ya kupokea fomu ya kugombea ubunge katika jimbo lake.aliyokabidhiwa na wazee wa jimbo hilo
 Mhe David Kafulila ikiingia katika viwanja vya shule ya msingi Nguruka kwaajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa awamu ya pili jimboni kwake.
 Mhe Kafulila akiwaaga wananchi wa Nguruka baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara.
Baadhi ya wananchi wa Nguruka waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mhe.David Kafulila na kushuhudia akikabidhiwa fomu ya ubunge

NEC YAONGEZA SIKU NNE ZA KUJIANDIKISHA KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR

$
0
0
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva .

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa imeongeza muda wa siku nne wa kuandikisha wapiga kura kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Hii inamaanisha kuwa zoezi hilo ambalo lilikuwa linaisha leo ijumaa ya julai 31, litaendelea hadi jumanne agosti 4.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi ya siku nne kwa kuwa ratiba zitaingiliana.

Aidha, Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka sasa watu zaidi ya milioni 18 wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya mfumo wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima.

RAIS YOWERI MUSEVEN AFUNGUA MKUTANO WA MARAIS WASTAAFU KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR

$
0
0
????????????????????????????????????
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda akifungua rasmi mkutano wa Marais wastaafu wa Afrka AFRICA LEADERSHIP FORUM unaofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Mkutano huo unaojumuisha marais wastaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania , Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia, Festus Mogaye wa Botswana, Bakili Muluzi wa Malawi na Jerry Rowlings wa Ghana unajadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika bara la Afrika na Changamoto zinazokabili barahilo na umeandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin Mkapa akitoa mada katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kushoto na Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu Mstaafu wa AU na Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

VIJANA WAJASILIAMALI ZAIDI YA 650 WAKWAMLIWA KIUCHUMI NA AIRTEL FURSA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akiwakaribisha wageni katika semina ya kuhamasisha makampuni mbalimbli  kukabiriana na ukosefu wa ajira hapa nchini ili kumwezesha kijana mjasiliamali kujikwamua kiuchumi katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
 Wageni kutoka makampuni mbalimbali wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna katika mkutano wa ajira kwa vijana wajasiliamali wanaothubutu kujikwamua kiuchumi hapa nchini katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
Meneja wa huduma za jamii-Airtel Hawa Bayuni akielezea jinsi kampuni la airtel  hapa nchini linavyoendelea kukomboa vijana wajasiliamali wanathubutu kujikwamua kiuchumi hasa kwa kutumia Aitel Fursa inayoendelea kuwawezesha vijana wengi hapa nchini wa kuanzia miaka 18 hadi 24 ikiwa Aitel fursa imeshasaidia vijana wajasiliamali zaidi ya 650 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ikiwa inaendelea kwa mikoa mingine hapa nchini.katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks wakimsikilizaMeneja wa huduma za jamii-Airtel Hawa Bayuni akielezea jinsi AIRTEL FURSA ilivyokwamua changamoto mbalimbali kwa vijana wajasiliamali hapa nchini waliokua na malengo ya kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa vifaa pamoja na kuwasaidia kimasoko.






 Mwenyekiti wa kampuni ya  Roots and Shoot, Ray Kiliho akichangia maada katika mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks baada ya mtoa maada kutoka kampuni ya simu za mkononi Airtel Hawa Bayuni kuhusiana na changamoto zinazomkuta kijana mjasiliamali wakati wa kuendeleza biashara yake, katika mkutano uliofanyika katika hoteli hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Solution Bloks, Msomisi Mbenna akiuliza swali kwa Meneja huduma za jamii wa Airtel  hapa nchini ,Hawa Bayuni katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa kampuni ya Popular lines, Neserian Alexander akichangia maada mara baada ya mtoa maada kumaliza kuelezea jinsi Airtel Fursa inavyoendelea kukwamua vijana kiuchumi hapa nchini katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa hoteli ya Colossem, Tanya Visser akitoa zawadi kwa washiriki wa mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks uiofanyika jana jijini Dar es Salaam. 




Washiriki wa mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks  wakiwasikiliza watoa maada kutoka Airtel  na kampuni ya Solution Blocks  katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

SHEREHE ZA NANE NANE KANDA YA KATI KUFANYIKA VIWANJA VYA NZUGUNI MKOANI DODOMA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwasilisha taarifa ya

maandalizi ya sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati zitakazo fanyika
sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Kitaifa kuanzia Agosti
Mosi Mkoani Dodoma.


Sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati zitafanyika sanjari na Maonesho na mashindano maalum ya mifugo ya 5 Kitaifa  katika  uwanja wa Nzuguni Dodoma kuanzia tarehe 01/08 hadi 08/08/2015.





Sherehe za Nane Nane mwaka huu 2015 zinakwenda kwa Kaulimbiu inayosema “Matokeo Makubwa sasa  (BRN)– Tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya Kilimo na Ufugaji” Kaulimbiu hii imekuja wakati muafaka ambapo Taifa letu la Tanzania linaelekea katika Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba na tayari baadhi ya vyama vya siasa vimeshaanza mchakato wa kuendesha kura za maoni ili kupata wagombea wa nafasi mbalimbali.


Kaulimbiu hii inatoa msisitizo kwa wananchi na watanzania wote kuchagua viongozi bora ambao watasaidia kuleta matokeo makubwa sasa katika nyanja za Kilimo na Ufugaji kwa maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.


Kama ilivyo ada,  Sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati sanjari na Maonesho na mashindano maalum ya mifugo Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni hapa Dodoma, yameendelea  kuwa kitovu na chemchem ya elimu juu ya:  

  • Zana bora za Kilimo na Mifugo

  • Pembejeo za Kilimo na Mifugo

  • huduma za Mawasiliano ya Kibiashara

  • Usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo

  • taasisi mbalimbali za Fedha na Mabenki

  • Mafunzo na Utafiti na

  • taasisi za uzalishaji za Serikali.


Hadi kufikia sasa maandalizi muhimu kwa ajili ya kufanikisha Sherehe hizi za Nane Nane yapo katika hatua nzuri.


Maendeleo ya Vipando na Mabanda ya Mifugo kwa ujumla yapo katika hatua nzuri ingawaje hatua iliyofikiwa inatofautiana kati ya taasisi na taasisi.


Miundombinu ya Barabara Inapitika kirahisi, TASO kwa kushirikiana na Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane Kanda ya Kati  inaendelea kufanya usafi wa barabara na kuhakikisha zinakuwa katika hali nzuri wakati wote wa Maonesho.


Huduma ya Maji inategemea mtandao wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dodoma (DUWASA) ambao ndiyo unaotumiwa na wadau wengi na visima virefu (9) ambavyo vimechimbwa  na wadau kwa matumizi yao. TASO Kanda ya Kati inaendelea kushughulikia changamoto ya kiufundi na kukatika kwa umeme kwa lengo la kuhakikisha maji hayakosekani kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni.


Arena ya Mifugo imefanyiwa usafi na marekebisho madogo ili kuboresha mashindano maalum ya mifugo ya 5 Kitaifa. Kwa upande wa Mabanda ya Maonesho, Napenda kutoa wito kwa Wizara, Taasisi za Serikali, Taasisi zisizo za serikali , asasi na wadau mbalimbali kuendelea kukamilisha ujenzi wa mabanda yao ya maonesho kwenye viwanja vya Nzuguni ili kuleta ufanisi wa shughuli za Nane Nane.


Washindi wa Maonesho ya uwanjani: (Wakulima na Wafugaji bora) Kutakuwa na Majaji wasiopungua wanne (4) kutoka hapahapa Kanda ya Kati na  baadae washindi wa Maonesho watapewa zawadi kulingana na hali ya fedha, naomba nisitaje hapa  lakini niweke wazi kuwa Jukumu la kutoa zawadi ni la Kamati ya Maandalizi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.


Natumia fursa hii kuwakaribisha wakulima na wafugaji kutoka mikoa ya kanda ya kati na maeneo mengine ya Nchi, Wadau mbalimbali kuja kushiriki maonesho haya ya Nane Nane na pia nawakaribisha wananchi hususani wakulima, wafugaji, wasindikaji, wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kuja kwa wingi kutembelea Maonesho ya Nane Nane na Maonesho na Mashindano maalumu ya mifugo kwenye viwanja vya Nzuguni Manispaa ya Dodoma kuanzia tarehe 1-8 Agosti, 2015 ili waweze kujifunza.


Kwa muhtasari matukio makuu kwa mujibu wa ratiba, katika siku ya ufunguzi na Kufunga Msisitizo utakua Kaulimbiu ya Maonesho, Siku ya Pili ya Maonesho Msisitizo utakua kuona Kiwango cha teknolojia ya Uzalishaji wa bidhaa za kilimo , mifugo, maliasili na viwanda katika kukuza uchumi.


Siku ya tatu ya Maonesho Msisitizo utakuwa Serikali za Mitaa kusimamia maendeleo vijijini; Siku ya nne msisitizo utakua juu ya sera ya mikopo kwa wakulima na wafugaji wadogo. Siku ya tano itahusisha Ufunguzi wa Maonesho na mashindano Maalumu ya tano (5) ya mifugo. Siku ya sita ya Maonesho msisitizo utakuwa kwenye umuhimu wa habari kwa maendeleo ya kilimo na mifugo. Siku ya saba msisitizo utakuwa kwenye Hifadhi ya Mazingira kwa kilimo na ufugaji endelevu.


Nawakaribisha sana wananchi na wadau mbalimbali wa kilimo na mifugo hapa Dodoma na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Maonesho ya Mwaka huu, niweke mkazo kuwa ulinzi na usalama umewekwa vizuri ili kuhakikisha Maonesho hayo yanafanyika salama kwa utulivu na amani.


Katika hatua nyingine, kila Mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine kuadhimisha ”Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani.” Maadhimisho haya yaliyoanza mwaka 1992, hufanyika kuanzia tarehe 01 – 07/08 ya kila mwaka.


Kwa mwaka huu 2015, Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi, umepewa heshima ya kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama kitaifa. Maadhimisho haya yatakwenda sanjari na Sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati na Maonesho na mashindano maalum ya mifugo ya 5 Kitaifa. Maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia  Julai 1 - 7, 2015, ufunguzi utafanyika kwenye wilaya ya Chamwino kwenye Kijiji cha Nkwenda, wakati sherehe za Kilele cha Maadhimisho hayo Kitaifa zitafanyika hapa Manispaa ya Dodoma kwenye viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Nzuguni.


Kaulimbiu ya Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama  mwaka huu ni ”UNYONYESHAJI NA KAZI: TUHAKIKISHE INAWEZEKANA” (Breastfeeding and Work Lets Make it Work). Kaulimbiu hii inalenga kuwasaidia wanawake WOTE wanaofanya kazi katika sekta rasmi na isiyo rasmi waweze kutunza watoto wao ipasavyo pamoja na kufanya kazi mathalani kuajiriwa, kujiajiri, kazi za muda mfupi au mikataba na kazi zisizo za kulipwa kwa mfano kazi za mazingira ya nyumbani, shamba, mifugo na kutunza familia.


Katika maadhimisho ya mwaka huu, pamoja na masuala mengine muhimu, kutakuwa na utoaji wa elimu ya lishe kwa njia za vyombo vya habari, elimu ya lishe kwenye vituo vya kutolea huduma na eneo la Nane Nane, elimu ya lishe na unyonyeshaji kwa makundi ya wanafunzi, viongozi na Uhamasishaji kwa njia ya gari la maonesho na semina.


Hivyo natoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kuhudhuria ufunguzi na kilele cha maadhimisho haya ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Kitaifa, halikadhalika, kutumia fursa hii adhimu kupata elimu juu ya masuala ya Unyonyeshaji na lishe ili kusaidia kumaliza tatizo la Utapiamlo baina ya wanawake walio katika umri wa kuzaa (15 – 49 yrs) halikadhalika kuondoa tatizo la utapiamlo kwa watoto wenye umri wa miezi 6 – 59.

                                             
Imetolewa na:
OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA

Julai 30, 2015.

MSHINDI WA AIRTEL TRACE NALIMI MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA KIBAO CHAKE CHA "NICE COUPLE" KWENYE CHANEL YA TRACE LEO.

$
0
0

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Nalimi Mayunga ameachia
kibao chake kipya cha " Nice Couple" video itakayorushwa kuanzia leo
katika kituo cha DSTV chanel ya Trace Urban 325

MWANZONI mwa mwezi huu, Mshindi huyo wa Airtel Trace Music star alitua
mjini Johannesburg South Afrika akitokea nchini Tanzania  ili kuanza
safari yake kujiendeleza kimuziki na kufikia ndoto zake mara baada ya
kuibuka mshindi wa mashindano makubwa yaliyoshirikisha nchi 13 barani
Afrika  yaliyofanyika tarehe 18 April 2015,

Mayunga alitangazwa mshindi na mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko ya R& B wa nchini Marekeni , Akon and kupata zawadi nono ikiwemo deli ya


 kurekodi single ambapo mayunga alishuka nchini South Afrika  na
kuredoki nyimbo yake ya "Nice Couple" katika maeneo ya Orlando East.

Nyimbo hii tayari imeshaanza kupigwa katika vyombo na sehemu



mbalimbali nchini South Afrika.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA KENYA NA MSUMBIJI IKULU DAR

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Dkt. Vicente Veloso, aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 31, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Ali Mwakwere, aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Dkt. Vicente Veloso baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam , leo Julai 31, 2015, wakati Balozi huyo alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Ali Mwakwere, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam , leo Julai 31, 2015.
Picha na OMR

MKURUGENZI WA MTENDAJI WILAYA YA HANANG' AKANUSHA TUHUMA ZA HALMASHAURI YAKE KUTAFUNA FEDHA ZAIDI YA TSH MILINIONI 500

$
0
0

Na woinde shizza.
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara,

Filex Mabula amesema taarifa zilizotolewa kuwa halmashauri hiyo imetumia

vibaya zaidi ya sh508.6 milioni fedha za shule na za kusambaza maji
vijijini, zilizotolewa na benki ya dunia, siyo za kweli.



Akizungumza na waandisi wa habari jana, Mabula alisema halmashauri hiyo

ilitoa sh225.5 milioni kwenye shule za bweni kwa ajili ya chakula kwa mwaka
2013 hadi 2014 sawa na asilimi 281.9 ya fedha zilizoidhinishwa na hazina.


Fedha zetu zinatumika kwa kufuata kanuni na taratibu ndiyo sababu mkuu wa

mkoa wetu Joel Bendera alitupongeza Hanang’ kwa kupata hati safi kwa mara
ya nne mfululizo kupitia ukaguzi wa ripoti ya CAG,” alisema Mabula.


Alisema sh283.1 milioni zilipelekwa kwenye shule za Katesh, Balang’dalalu,

Bassodesh na Gendabi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya shule na kamati ya
fedha iliidhinisha kwa kikao cha Juni 26 mwaka huu na baraza la madiwani
Julai 8. 

Alisema vijiji saba vya Getasam, Ng’alda, Gidagharbu, Simbay, Ishponga,

Garawja na Galangal, vimepatiwa miradi ya maji kupitia ufadhili wa benki ya
dunia na vijiji vya Hirbadaw, Wandela na Dajameda vitanufaika hivi
karibuni. 

Wanasiasa msiwakatishe tamaa watendaji bila sababu ya msingi kwa kutumia

kipindi hiki cha uchaguzi kuwapotosha wananchi kwani kiongozi bora
anapatikana kwa utendaji wa kazi siyo kudanganya jamii,” alisema Mabula.


Nao, baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo walipongeza jitihada zinazofanywa na

uongozi wa halmashauri hiyo kupitia mkurugenzi huyo Mabula kwani miradi
mingi ya maendeleo imefanikiwa na jamii inanufaika nayo.

Mkazi wa Katesh, Julius Gidang’ai alisema mara nyingi wanasiasa wamekuwa

wakikwamisha miradi mingi ya maendeleo kutokana na kuzusha vitu vya uongo.

endapo baadhi ya miradi ya maendeleo itakapokuwa haijazifikia kata zao.


Hivi sasa sisi wananchi wa kata ya Endasak tumeshindwa kuendelea na mradi

wetu wa umwagiliaji kule Endagaw baada ya Mabula kusimamia zoezi vizuri
lakini wanasiasa wakakwamisha,” alisema Zainab Juma mkazi wa kijiji cha

Endagaw.

HUDUMA ZA VIBALI MAALUM VYA MATIBABU KUSOGEZWA KARIBU NA WANACHAMA

$
0
0
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WANUFAIKA WOTE KWAMBA KATIKA KUBORESHA HUDUMA KWA WANACHAMA WAKE, HUDUMA ZA VIBALI MAALUM VYA MATIBABU ZILIZOKUWA ZINATOLEWA KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA, ILIYO KURASINI BENDERA TATU HAZITATOLEWA TENA OFISI HII ISIPOKUWA KWA WAGONJWA WAPYA WANAOHITAJI VIBALI VYA DAWA ZA SARATANI  HUDUMA ZA KUSAFISHA FIGO (DIALYSIS) NA DAWA ZA KUDHIBITI NA KUONGEZA  KINGA KWA WALIOWEKEWA FIGO PANDIKIZI.


KWA WANACHAMA WALIOKWISHA ANZA KUPATA HUDUMA ZA VIBALI, WATAPATA HUDUMA HIZO KATIKA OFISI ZA NHIF ZA MIKOA NA BAADHI YA HOSPITALI KAMA IFUATAVYO:-


·      DAR ES SALAAM: HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD, BESTA, REGENCY NA TMJ, OFISI YA NHIF ILALA (JENGO LA USHIRIKA-GHOROFA NA.15), KINONDONI (JOSAM HOUSE GHOROFA YA. 4) NA TEMEKE (MKABALA NA HOSPITALI YA TEMEKE).


·      KWA MIKOA MINGINE VITUO VILIVYOWEZESHWA KUTOA HUDUMA HIZI NI KCMC (MOSHI), ALMC (ARUSHA), HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA – MBEYA. ZOEZI LINAENDELEA KUWEZESHA VITUO VINGINE NA TAARIFA ZITATOLEWA.


HUDUMA ZINAZAZOTELEWA VIBALI KATIKA VITUO HIVYO NI:-

CT SCAN, MRI, HUDUMA ZA KUSAFISHA FIGO (DIALYSIS), DAWA ZA SARATANI, VIFAA SAIDIZI, DAWA ZA KUDHIBITI NA KUONGEZA KINGA KWA WALIOWEKEWA FIGO PANDIKIZI, MIWANI YA KUSOMEA NA NYONGA AU GOTI BANDIA.


MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MABADILIKO.

UKISIKIA/KUSOMA TANGAZO HILI TAFADHALI MWARIFU NA MWENZAKO.



LIMETOLEWA NA KAIMU MKURUGENZI MKUU -NHIF.

UGANDA:MBABAZI KUWANIA URAIS NJE YA CHAMA CHA NRM

$
0
0
Waziri mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani.


Mbabazi ametangaza hilo muda mchache uliopita akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala.

''kamwe sitatoka NRM''.
''Lakini sitaweza kugombea urais katika tikiti ya chama hicho cha NRM ilihali vipengee vingi tu vya vya chama vinakiuka katiba ya nchi''.
'' sitawania urais kwa tikiti ya NRM lakini wakati wa uchaguzi nitawania urais'.

''kama mwanzilishi wa chama ,wakili na mwananchi Mzalendo,sitajiingiza katika maswala yanayokiuka sheria''NRM sharti ijipige msasa''



Tangazo hilo la Mbabazi limetokea baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kuwa atarejesha fomu zake za kuwania uwenyekiti wa chama tawala NRM leo.

Mwenyekiti wa jopo la kuchagua viongozi wa chama hicho bwana Tanga Odoi alikuwa ametanga ijumaa tarehe 31 (leo) kuwa siku ya mwisho ye kurejesha fomu za uwaniaji nyadhfa za chama hicho.

Mbabazi anasemekana kuwa alitembelea makao makuu ya chama tarehe 16 akikusudia kuwasilisha ombi lake lakini akakurupuka akidai kuwa gharama ya juu iliyowekwa kwa wagombea itawanyima maskini uwezo wa kuwania nyadhfa katika chama hicho.

Mbabazi alikuwa ameahidi kumpinga rais Museveni kama mwenyekiti wa chama na hivyo mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Mpinzani wake rais Museveni anatarajiwa kurejesha fomu zake mwendo wa saa sita adhuhuri.




katika makao makuu ya chama, wafuasi wake wamemiminika wakiwa wamevalia rangi za chama wakiimba nyimbo za kumsifu. 

BREAKING NEWSSSS !!!!!!! KESI YA IPTL DHIDI YA KAFULILA YATUPWA NJE.

$
0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi namba 301 iliyofunguliwa na Kampuni ya kufua Umeme ya IPTL, PAP pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya PAP Bw Harbinder Singh Sethi dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila kwa madai kuwa Kafulila alichafua jina kampuni hizo na muhusika huyo kwamba walichota zaidi ya 300bn kwenye akaunt ya Tegeta escrow kinyume cha sheria na taratibu.

Katika shauri hilo, Kampuni ya IPTL,PAP na Herbinder Singh Sethi walitaka Mahakama imuamulu Mhe Kafulila alipe fidia ya 310bn kwa kuchafua jina la kampuni na mkurugenzi huyo.

Katika kesi hiyo Mhe Kafulila alikuwa akitetewa na taasisi za kisheria za Legal& Human Righ Centre pamoja na kituo cha Human Righ Deffenders.

Akitoa uamuzi huo mbele ya mawakili wa Human Right Defenders na Legal & Human Right Center wakiongozwa na wakili Mtobesya huku mawakili wa IPTL, PAP na Sethi wakiwa hawakufika mahakamani, Jaji Rosemary Teemba alisema Mahakama Kuu imejiridhisha kwamba kampuni ya IPTL, PAP na Mkurugenzi wao Harbinder Sethi hawakuwa na hoja za msingi kuthibitisha madai yao kama msingi wa kufungua kesi mahakama kuu na hivyo kwa kuzingatia hali hiyo Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam inatupilia mbali shauri hilo kuanzia.

TRA YAWAPIGA MSASA CTI JUU YA SHERIA MPYA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI YA MWAKA 2014

$
0
0
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiongea na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Dkt. Samuel Nyantahe akimshukuru Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa uamuzi wa kuwakutanisha wadau wa sekta ya viwanda na kuwaelimisha kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 ili kuweza kuondoa utata kwenye baadhi ya maeneo yaliyo katika sheria hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam.
 
 Wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga akimpongeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade baada ya kumaliza kuwahutubia wajumbe kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), leo Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akiwasilisha mada kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria hiyo iliyoanza kutumika Julai 1, 2015 Leo Jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakiuliza maswali kwa wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
 Makamu wa pili wa mwenyekiti kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Pankaj Kumar akiongea wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Kuhusu Sheria Hiyo
 Afisa Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Donasian Assey akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
  Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga akimueleza Jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akiwaeleza jambo baadhi ya wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO -MAELEZO

SHEIN AANDAA MIPANGO NA SERA ZA KUSAIDIA VIJANA ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mipango na sera nzuri za kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri wenyewe hasa waliojiunga katika vikundi vya ushirika na SACCOS.

Dk. Shein alisema kuwa Serikali imeanzisha Mfuko wa kuwawezesha Wananchi Kiuchumi na tayari watu kadhaa wameanza kufaidika na Mfuko huo sambamba na kuwapatia mafunzo ya kitaalamu pamoja na kuvipatia vikundi vya ushirika mbinu za kupata masoko na kuwawezesha kuwa wajasiriamali wazuri.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Dk. Shein Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum, Mhe. Haji Omar Kheir, aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Jumuiya ya Watazania Wasio na Ajira (TUEPO) huko katika ukumbi wa afisi za Jumuiya hiyo Rahaleo, mjini Zanzibar.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa katika kuwasaidia vijana walioshindwa kuendelea na masomo yao, Serikali imeyaimarisha mafunzo ya elimu ya amali katika vituo vya amali vya Mwanakwerekwe na Mkokotoni Unguja na Vitongozi huko Pemba.

Dk. Shein alisema kuwa kituo cha kuwaandaa wajasiriamali katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume imeshaanza kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kupatiwa mikopo.

Alisema kuwa katika vyuo hivyo vijana hufunzwa ujuzi wa kazi mbali mbali kama vile ufundi umeme, ufundi magari, useremala, uhunzi, kutegengeneza mafriji na amali nyengine ambapo tayari vijana wengi wameweza kunufaika na kujiajiri wenyewe.

Aidha, aliwaeleza vijana hao kuwa mafunzo wanayotoa katika taasisi yao na taasisi nyengine binafsi ni kuongeza fursa za mafunzo ya elimu ya amali kwa vijana ili waweze kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.

Dk. Shein alisema kuwa ukosefu wa ajira nji tatizo linalozikabili nchi zote duniani hivyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapindyuzi ya Zanzibar zimekuwa zikichukua jitihada mbali mbali katika kukabiliana na tatizo hilo kwa kushirikiana na jumuiya za Kimataifa, sekta binafsi na jumuiya hiyo ya TUEPO.

“Hivyo kuwepo kwenu hapa ni hatua ya juhudi za pamoja ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote huwa inazishajihisha katika kukabiliana na tatizo la ajira hasa klwa vijana wetu”,alisema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua ukubwa wa tatizo la ajira kwa vijana kutokana na uchache wa fursa za ajira serikalini na kuwepo kwa ongezeko la vijana wanaomaliza masomo katika ngazi mbali mbnali kwa kila mwaka na kutegemea ajira ziliopo.

Alisema kuwa inatia moyo kuona hivi sasa, vijana wengi wasomi wameanza kushajihishana kuanzisha vikundi vya ushirika na kujiajiri wenyewe bila ya kuendelea kusubiri ajira Serikalinini.

Dk. Shein aliwanasihi vijana hao kuhakikisha kuwa mafunzo wanayotoa yazingatie ubora na hali ya mahitaji ya soko la ajira sambamba na kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Taasisi mbali mbali za Serikali kama vile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali yenye dhamana ya kuhakikisha ubora wa elimu inayotolewa kwa wananchi.

 “Serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiya hii na taasisi zote zinazounga mkono mipango na jitihada mbali mbali za Serikali katika kuleta maendeleo na Ustawi wa wananchi wetu”,alisema Dk. Shein.

Pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kuzitumia vyema fursa zilizoandaliwa na Serikali pamoja na Taasisi binafsi katika kuwawezesha katika kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Watanzania Wasio na Ajira (TUEPO) Ussi Said Suleiman alisema kuwa lengo la Jumuiya hiyo ni kuwandaa vijana kielimu kwa kufundisha fani mbali mbali pamoja na kuwatafutia fani mbali mbali ndani na nje ya nchi, ili kuondosha tatizo la ajira.

Mwenyekiti huyo, alisema kuwa jumuiya inashirikiana na itashirikiana na taasisi za Serikali na zisizo za Serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo tayari imeanisha chuo cha Tanzania star teachers college kwa lengo lam kwuasaidia wanachama wa jumuiya hiyo.

Aidha, Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya Jumuiya hiyo pamoja na changamoto zilizopo, ambapo Waziri Kheir alichangia Tsh. milioni mbili kwa upande wake akiwa kama Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum.

Jumuiya hiyo imeenzishwa tarehe 23.4.2015 ikiwa na wanachama watano ambapo hadi sasa ina wanachama 210 .

KAGAME CUP

$
0
0
 Kikosi cha timu ya Khartoum ya Sudan kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo. Gor Mahi inaongoza kwa magoli 3-1. (Picha na Francis Dande)
 Wachezaji wa timu ya Khartoum wakishangilia bao.
 Kiungo wa Gor Mahia, Innocent Wafulawakichuana na Ahmed Adam Mahmoud. 
 Beki wa Gor Mahia, Karim Nizigiyimana akichuana na Amin IbrahimElmani.
 Mashabiki wa Gor Mahia wakishangilia timu yao.
 Ahmed Adam Mahmoudakiwatoka wachezaji wa Gor Mahia.
 Wagdi Awad Abdalla akitafuta mbinu za kumtoka Mussa Mohammed.
 Golikipa wa timu ya Gor Mahia, Boniface Oluochakiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Mashabiki wa Gor Mahia wakishangilia timu yao.

FILIKUNJOMBE; MAFISADI WAMETUMA WATU WANING'OE UBUNGE NAOMBA WANANCHI WANYIMENI KURA

$
0
0
mbunge  wa Ludewa  Deo Filikunjombe kulia akiwa na mlemavu wa ngozi (ALBINO) mara  baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni za ubunge 

Na Matukiodaima Blog Ludewa
WAKATI wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM)  kesho   wanashiriki  zoezi la kupiga kura  za maoni kuwapata  madiwani na  wagombea  watakao gombea kwa CCM ,mbunge  wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewashukuru wanachama wa CCM  katika jimbo hilo kwa kuonyeha  imani kubwa kwake  ukilinganisha na wagombea  wenzake  wawili na kuwa hadi  sasa anauhakika mkubwa wa kushinda tena ila ushindi utakaompa heshima ni ule wa kupata kura zote na wenzake kuambulia patupu

Filikunjombe  aliyasema hayo   wakati wa mkutano  wa kujinadi kwa  wagombea wa nafasi ya  ubunge katioka kata ya Ludewa mjini ,kuwa hadi  sasa kutokana na mapokeo  ya wananchi na  wana CCM kote walikopata kupita kwenye kata 26 za  jimbo hilo la Ludewa wamekuwa wakitamka  bayana kuwa kura  zote kwake  hivyo  kuwaomba wana CCM kwa umoja  wao kumpa moyo zaidi wa kuwatumikia tena kwa kuhakikisha  wanampatia kura  zote za ndio.

 

Alisema kwa kauli zao wagombea wenzake wawili  waliojitokeza wanaeleza bila kuficha kuwa wametumwa na watu  ambao  aliwaondoa bungeni kutokana na vitendo vyao vya ufisadi  ili  waje Ludewa  kugombea ubunge kwa ajili ya kulipa kisasi kwa kumtoa jambo ambalo hadi sasa  limegonga mwamba kutokana na wananchi na wana CCM Ludewa kuliona hilo.

"Niliifanya kazi  ile ya  kupambana na mafisadi bungeni kwa faida ya  wananchi wa Ludewa na watanzania kwa ujumla ila nashangazwa  kuona  leo wana Ludewa wachache wanakubali  kutumika na mafisadi hao kutumwa kuja kunitoa ubunge kweli ni aibu  kubwa kwa kazi kubwa ambayo mimi nimeifanya katika  jimbo la Ludewa  sikutegemea kupata mpinzani tena ndani ya chama changu.....ila naomba sana  wana Ludewa  tuungane katika vita  hii ya maendeleo na kupinga ufisadi kwa kuwanyima kura hawa "

Alisema kuwa wilaya ya  Luudewa itajengwa na wana Ludewa kwa kushirikiana na yeye kama mbunge wao na sio wale wanaotumika  kuwadanganya wananchi wa Ludewa hata kupinga kazi kubwa iliyofanyika kwa kipindi kifupi cha miaka mitano .

Filikunjombe  alisema kuwa hawezi kusema kuwa amemaliza changamoto  zote za wilaya hiyo ya Ludewa kwani kama atasema hivyo atakuwa anawadanganya  wananchi wake na kuwa pamoja na kuwa amefanya mengi ila hajamaliza changamoto  zote za jimbo la Ludewa hivyo iwapo  watampa tena nafasi hiyo ua ubunge atahakikisha anaendelea kupunguza changamoto zilizobaki.

" nimefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimbo la Ludewa ila nitakuwa nadanganya kama nitasema nimemaliza changamoto  zote pia hata wabunge  wenzangu walifanya kulingana na wakati  ule  na kila mmoja a namchango  wake katika  maendeleo ya Ludewa .....ninachowaomba wananchi mtupime  wagombea kwa kazi  tulizofanya msitupime kwa maneneo kwangu mimi ni kazi zaidi maneno kidogo"

Hata  hivyo alisema iwapo wananchi  wa kata ya  Ludewa watamchagua kuwa mbunge kwa kura za kishindo atahakikisha kero ya maji anaanza kuitatua kabla ya  serikali kuanza kufanya hivyo kwani kati ya changamoto kubwa kwa mji wa Ludewa ni pamoja na maji .

Pia  aliwataka  wananchi kupuuza  uongo unaosambazwa na wagombea hao kuwa  vikao vya juu vya chama vimepanga  kukata  jina lake  baada ya  kushindwa na kudai kuwa huo ni upotoshaji na kuwa CCm ni chama makini na hakuna mtu wa kukatwa iwapo ametekeleza sera  vema za chama.

Huku mgombea injinia Zephania Chaula akiwaomba  wananchi hao kumchagua kuwa mbunge kwani tayari ameahidiwa na  na mwenyekiti wa DP mchungaji Christopher Mtikila na aliyekuwa mbunge wa  jimbo hilo kabla ya  kuangushwa na mbunge filikunjombe mwaka 2005 Prof Raphael Mwalyosi kuwa watamsaidia  kufanya kazi pamoja .

Chaula ambae  alipingwa vikali katika mkutano huo kiasi cha kuzomewa baada ya kudai moja kati ya kazi aliyoifanya ni kuanzisha  mfereji wa umwagiliaji kata ya  Ruhuhu baada ya mkazi wa kata  hiyo aliyekuwepo mkutanoni hapo kunyosha mkono na kumpinga kuwa hakuna mradi huo ni uongo na kuwa wao  wanamtegemea mbunge wao Filikunjombe ambae amefanya mengi kwenye kata  hiyo.

Wakagti Injinia Chaula ambae  siku za hivi karibuni aliambulia kura  11 katika nafasi ya ujumbe wa NEC akipingwa  vikali mkutanoni hapo mgombea Kepten (mstaafu) Jacob Mpangala akijikuta katika wakati mgumu kufuatia mbunge Filikunjombe kuwasilisha vielelezo sahihi mbele ya viongozi wa chama na kugawa kwa wananchi hao viinavyoonyesha mgombea  huyo anavyodanganya  wananchi  kuwa alistaafu kazi wakati kuna barua ya  kufukuzwa kwake kazi kutoka TAMISEMI.

Filikunjombe alifikia hatua  hiyo ya  kukabidhi  ushahidi huo kwa chama baada ya kauli ya  vitisho ya mgombea  huyo Mpangala kumtaka aonyeshe hadharani ushahidi unaoonyesha kufukuzwa kakwe kazi kabla ya kuchukua hatua .

ASKARI WA TANAPA ASHINDA TUZO YA ULINZI WA FARU BARANI AFRIKA

$
0
0
Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Daraja la Pili,Malale Patrick Mwita akiwa ameshika Tuzo na Cheti alivyokabidhiwa na Mwana wa Mfalme Albert wa Pili wa Monaco nchini Afrika Kusini wiki iliyopita katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tanapa jijini Arusha.
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akitangaza ushindi wa Tuzo hiyo akiwa na maafisa wa Shirika hilo  ambao wana jukumu la kuhifadhi maliasili kwaajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akitangaza ushindi wa Tuzo hiyo ambayo imeipa heshima Tanzania katika mapambano yake dhidi Ujangili nchini.

Mwandishi wetu,Arusha
Askari Daraja la Pili ,Malale Patrick Mwita kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti ameshinda Tuzo ya kila mwaka ya Askari Bora katikaulinzi wa Faru kwa mwaka 2015 barani Afrika inayojulikana "2015 Rhino Conservation Awards"

Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete ametangaza ushindi  huo leo katika ofisi za Makao Makuu ya Tanapa jijini Arusha.

Amesema Tuzo hiyo amekabidhiwa na Mwana wa Mfalme Albert wa Pili wa Monaco ambaye ni mlezi wa Tuzo hizo ambazo washindi walikabidhiwa Julai 27 mwaka huu nchini afrika Kusini.

Askari huyo ameibuka mshindi miongoni mwa washindani wengine kutoka nchi zote za Afrika zenye miradi ya kuendeleza Faru katika  ambapo Tuzo hizo hutolewa kila mwaka baada ya taasisi hiyo kutambua matendo ya kijasiri yaliyofanywa na askari huyo.

Baadhi ya matukio ya kijasiri yaliyofanywa na askari huyo ni askari pekee mwenye uwezo wa kuwatambua Faru zaidi ya asilimia 90  ndani ya Hifadhi ya Serengeti kwa kutumia alama za asili wakati mwaka 2007 alizuia tukio la kuuwawa kwa Faru na mwaka 2008 alishiriki kukamata silaha  5 za kivita. 

Amesema mradi wa Faru wa Moru,serengeti ndio mradi mkubwa kabisa wa faru wenye mafanikio barani Afrika unaoongoza kwa kasi ya kuzaliana ambayo ni zaidi ya asilimia 5 kwa mwaka.

Tuzo hizo huandaliwa pamoja Wizara ya Mazingira ya Afrika Kusini ambayo inahusika na Utalii.

Malale amesema Tuzo hiyo imempa hamasa ya kutambua mchango wa askari katika kukabiliana na majangiri hatari wanaotumia silaha za kivita kwaajili ya kuwinda Faru na Tembo .

"Tuzo hii ni heshima kubwa kwa Tanapa na nchi yetu kwa ujumla katika kuhakikisha tunawalinda wanyama hawa ambao wako katika hatari ya kutoweka kila mmoja wetu ni mdau muhimu kuhakikisha Faru anaishi."amesema Mwita.

BALOZI DR MAHIGA DAWA SI KUHAMA CCM ASEMA YEYE NI MKOMBOZI WA CCM IRINGA MJINI.

$
0
0
Balozi Dr Mahiga -Iringa mjini.

Na matukiodaimaBlog
ALIYEKUWA balozi wa kudumu  wa umoja  wa mataifa (UN) na mgombea urais katika mchakato  wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dr Augustono Mahiga anayeomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM amewashangaa makada  maarufu wa chama  hicho  walioshindwa katika mchakato wa ndani ya chama kwa nafasi ya urais kuhama chama hicho kuwa hao hawakuwa na mapenzi ya kuwatumikia  watanzania na kuwa watazunguka kote ila chama makini ni CCM pekee na kuwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kumpa nafasi yeye ili kuondoa masalia ya Chadema .

Balozi Dr Mahiga  alisema kuwa wana CCM hao  walioanza kuhama chama  kwa kukosa nafasi ya urais hawakuwa na mapenzi mema na CCM bali  walikuwa wawametanguliza  maslahi yao mbele na  kuacha kuangalia maslahi ya Taifa na chama hivyo ni vema watanzania  kuwatazama kwa jicho la tatu na ikiwezekana kuwachunguza japo kwa miaka 5 bila kuwachagua kuwa  viongozi  wao.


Alisema kuwa kama  suala ni uongozi kwa ajili ya  kuwatumikia  wananchi na chama kulikuwa hakuna  sababu ya kuhama chama ama kuanza kutukana chama kwa sasa ila wangeweza  kushuka chini na  kugombea nafasi za chini ukiwemo udiwani ama ubunge kama ambavyo  yeye alivyoshuka na kugombea ubunge ili kuwatumikia watanzania kwa ngazi ya ubunge.

"Kila nafasi ndani ya chama ina maana  kubwa katika kutumikia  watu hivyo kuhama chama si jambo jema na upande wa vyama lazima kuwa makini na wanachama wanaohama vyama kwa sasa ili  kupata nafasi za uongozi iwapo  watakosa nafasi hizo  bila shaka  watachukua hatua ya  kuvuruga nguvu ya vyama  hivyo ama kuhama vyama "

Balozi Dr Mahiga  aliyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa kuhusiana na mchakato mzima wa kumpata mgombea Urais wa CCM Dr  John Magufuli na mchakato wa kura  za maoni  katika ngazi ya udiwani na ubunge katika  jimbo la Iringa mjini ambako  ni mmoja kati ya  wana CCM 14  wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge .


Alisema akiwa kati ya  wana CCM 41 waliojitokeza  kuchukua fomu ya Urais hana kinyongo na uteuzi wa mgombea  Urais wa CCM Dr Magufuli kwani ni mtu  makini na safi ambae  viatu  vya Rais wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete ataweza  kuvimudu  vema kutokana na kutokuwa  mtu wa kulipisha  kisasi na hana  makuu na mtu  zaidi ya  kulitumikia Taifa  .

Hivyo alisema iwapo wana CCM  jimbo la Iringa mji watamchagua yeye  kuwa mgombea ubunge  jimbo  hilo wawe imani  ya  kulikomboa jimbo hilo asubuhi  saa 12 kutoka kwa  Chadema  chini ya aliyekuwa mbunge  wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa kwani alisema  si kweli kama Chadema Iringa mjini wananguvu kubwa kuliko  ya CCM na ukitazama idadi ya wenyeviti wa mitaa ambao CCM inao wenyeviti  104  huwezi linganisha na  wale 64 wa  Chadema kabla ya wenyeviti wake 13 kuvuliwa nafasi zao  na mahakama.

Alisema dawa ya ushindi  wa kishindo kwa CCM Iringa mjini ni moja pekee  kuvunja makundi na kuwa kundi moja la ushindi baada ya zoezi la kura za maoni kumalizika .
Dc Mwamoto  kulia akiwa na mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa ,mwamoto ni mgombea ubunge Kililo

Mkuu wa wilaya  ya Kaliuwa mkoani Tabora Bw  Venance Mwamoto ambae anawania kuteuliwa kuwa mgombea ubunge  jimbo la Kilolo mkoani Iringa amesema kuwa tishio la  kutaka kuuwawa kwake  majuzi baada ya  kufyatuliwa risasi katika gari lake  wakati akitoka katika kampeni  kata ya  Ilula bado haimtishi  katika safari yake ya  kuwatumikia  wananchi  wa jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof. Peter Msolla .

Kwani alisema moja kati ya ahadi yake  kubwa kwa wananchi wa Kilolo ni  kuona amawatumikia kwa kasi zaidi na kumaliza kero ya maji katika mji  wa Ilula na changamoto nyingine ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kilichopita na mbunge  aliyekuwepo .

Mwamoto  alisema kuwa kazi nzuri  aliyoifanya kwa nafasi ya  ukuu  wa wilaya  kwa kipindi  kifupi ambacho  Rais Dr Jakaya kikwete alipomteua kwa  kuwa mkuu  wa wilaya ya  Kibonde na Kaliuwa ni wazi ni  kipimo tosha na heshima kubwa ya wananchi  wa Kilolo kujivunia na  wategemee makubwa zaidi  iwapo  watamchagua kuwa mbunge  wao kwa  sasa .
                                             waziri Lukuvi - Isimani

Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi amewaomba wananchi  wa jimbo  hilo hasa  wanachama wa CCM kuendelea  kujenga imani kwake na kuwa ndani ya CCM kuna Demokrasi  na kila mwanachama ana sifa ya  kugombea nafasi  yoyote ndani ya  chama japo  kipimo  cha kuchaguliwa bado kipo  kwa wananchi  wenyewe ambao  wanaweza kumpima kwa kazi alizofanya badala ya kushawishiwa kwa manenio bila vitendo.

Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kama  si wana Isimani kuonyesha ushirikiano  wao kwake na hata  kumchagua katika nafasi hiyo ya  ubunge basi heshima ambayo  ambayo  wana Iringa wameipata  kupitia  wizara yake leo  isingekuwepo .

Alisema suala la migogoro  ya ardhi  amepata  kulishughulikia kwa umaniki mkubwa na kuwa sulaa  hilo pia  lilikuwa ni kero kubwa hata kwa wananchi wake wa jimbo la Isimani ila kwa sasa kwa kiasi  limeanza kupungua na kuwa iwapo wataonyesha imani yao tena  wategemee kuona maendeleo makubwa zaidi katika jimbo hilo na kutaka baadhi ya kazi kubwa ambazo zimefanyika kuwa ni pamoja na barabara ya lami ya Iringa- Dodoma, umeme  vijini , ujenzi wa shule pamoja na ujenzi wa nyumba bora  kwa kupata bati za ruzuku .

"Tumekuwa pamoja  muda  wote katika maendeleo  na matatizo  hivyo lazima  kila  safari ina  wasindikizaji  wake na siku  zote penye maendeleo ndipo panapopendwa na wengi  ila bado kwa tathimini yetu Ismani ya  leo  sio ya jana . nimekomesha ulanguzi wa mazao kama mpunga ,alizeti  kwa kufunga mashine"
                   Godfrey Mgimwa -Kalenga

Mbunge wa jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa anayeomba kuteuliwa tena kuwa mgombea wa CCM nafasi ya ubunge  amewashukuru wananchi  wa kalenga kwa kuonyesha ushirikiano kwake na kuwa hadi  sasa amepata  kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa asilimia 99 na kuwa zipo changamoto mbali mbali ambazo  watampa tena nafasi ya ubunge atakwenda  kuzifanyia kazi .

Mgimwa ambae  amepata  kuongoza jimbo hilo kwa mwaka mmoja pekee akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki duni mwaka jana mwanzioni ,alisema zilikuwepo ahadi mbali mbali ambazo ziliachwa na mbunge aliyepita na tayari zote amezikamilisha kwa kipindi cha mwaka mmoja na kubwa anajivunia kuanzisha vikundi vya Vicoba  zaidi ya 60 ,ujenzi wa barabara , maji  vijiji ,umeme na uchangiaji wa ujenzi wa zahanati ,shule  na maabara na kuwa zaidi ya Tsh milioni 100 amepata  kutumia kwa kuchangia miradi ya maendeleo jimboni.

FOMU ZA WAGOMBEA URAIS ,UBUNGE PAMOJA NA UDIWANI KESHO-LUBUVA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juu juu ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi,Clothilde Komba.
 Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juu juu  jeshi la polisi lilivyojipanga katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia wa taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii) 
 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti 21 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva  amesema wakati wa uchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwa kuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200 katika kila mkoa na kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.

Lubuva a amesema kuwa wakati wa kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa kuchukua fomu na kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha shughuli za watu wengine.

Amesema kwa fomu za ubunge ni sh.50,000  na udiwani sh.5000 ambapo wanatakiwa kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa kistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva amesema kuwa  wanasiasa wanatakiwa  na lugha za kistaarabu katika mikutano yao katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.

Hata hivyo amesema kuna baadhi ya vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi na kutaka vyombo vya usalama kuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaouza kadi hizo.

Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa uchaguzi unaendana  na usalama hivyo jeshi limejipanga katika ulinzi katika kipindi hiki.

Kova amesema kuwa Jeshi litaendelea kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi cha uchaguzi.

SHEREHE YA KUWAKARIBISHA RASMI WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 KIJIJI CHA MAKUMBUSHO JIJINI DAR, WAINGIA RASMI KAMBINI

$
0
0
 
 Bi. Sophia Mkazi na Mwenyeji wa Kijiji cha Kasanga Wilayani Kisalawe Mkoani Pwani akiwakaribisha wageni ambao ni Washiriki wa Shindano la mama shujaa wa Chakula kijijini huko katika sherehe ya  iliyofanyika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam Jana. ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
 Bw. Godia Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam Tanzania kupitia Kampeni ya Grow Kijijini kwake.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisalawe Bw. Ellioth Phillemon akiwakaribisha washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani Kisalawe.
 Kikundi cha Burudani na sanaa cha  Rumumba Theatre wakiendelea na Burudani wakati wa sherehe hizo za ukaribisho kijiji cha Makumbusho
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu.
 Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo.
 Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi.
 Mmoja wa watoa Burudani, Mwanamke huyu akionesha kuhusu swala zima la Kilimo Endelevu.
 Stephen Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura  ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
 Wageni waalikwa katika sherehe hiyo
 
Ofisa wa Programu ya Kampeni ya Grow Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo mafupi ya Mchakato rasmi wa kumsaka Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula
 Wanao onekana Mbele ni Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa mama shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri washiriki wote wanaokwenda katika kushindana kumpata Mama Shujaa wa Chakula.
 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wakiwa wanatambulishwa Tayari kuelekea Kisalawe Kijiji cha Kisanga kwa ajili ya kumsaka mshindi ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images