Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

CHAGUA AMANI RAI KATIKA KURA ZA MAONI SINGIDA MJINI

$
0
0
Chagua Amani Rai Jimbo la Singida Mjini.

MKURUGENZI MTENDAJI WA 8020 FASHIONS SHAMIM MWASHA ATOA MADA NAMNA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA MANUFAA KWENYE SEMINA YATAASISI YA MANJANO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji   8020 Fashion na  Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekhar Nasser
Washiriki wakimsikiliza Kwa Makini Mentor Shamim Mwasha aliyetoa Mada kwenye semina hiyo Namna ya Kutumia Mitandao ya Kijamii kwa Manufaa ya Maisha yetu ya Kila siku na Kucha Kupoteza Muda Kwenye Mitandao ya Kijamii Bila Manufaa yoyote. 
 Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa Miradi  ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii  limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser Akimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi Mtendaji   8020 Fashion na   Shamim Mwasha  Akilezea Namna anavyoitumia Mitandao ya Kijamii kwa Manufakatika Maisha yake ya Kila siku.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser AkitoaMafunzo  kwa njia Vitendo kwa Washiriki wa Semina hiyo yenye lengo la Kumsaidia Mwanamke wa Kitanzania Kudhubutu Kujikita Kwenye Biasha ra hususani Kwa Kutumia Vipodozi Pekee  vinavyozalishwa na Shear Illusion vya Luv Touch Manjano.
 Washiriki wakiwa kwenye Picha ya Pamoja Mra Baada ya Kumaliza Mafunzo kwa njia ya Vitendo.
Washiri Wakiwa Pamoja Mra baada ya Kumaliza Mafunzo kwa Njia ya Vitendo. 
Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania



 

OLE SENDEKA AKANA KUHAMA CHAMA

WAZIRI WA UJENZI AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA TENGERU-SAKINA (KM 14.1) ITAKAYOJENGWA KWA NJIA NNE MKOANI ARUSHA

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Patandi wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya kukagua ujenzi wa barabara ya lami ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km 14.1 itakayojengwa kwa njia nne pamoja na madaraja makubwa mawili.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akizungumza na wakaazi wa Patandi, Sangis na Tengeru kuhusu ujenzi wa barabara ya lami ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km 14.1 itakayojengwa kwa njia nne pamoja na madaraja makubwa mawili.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS  Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara hiyo pamoja na Barabara ya Arusha bypass km 42.2
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akizungumza na wakazi wa Patandi mkoani Arusha kuhusu ujenzi wa barabara ya Tengeru-Sakina utakaojengwa kwa njia nne.
 Wakaazi wa Patandi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla hiyo. 
Sehemu ya barabara ya Tengeru-Sakina katika eneo la Patandi ikiwa imeanza kufanyiwa ukarabati utakaohusisha ujengwaji wa njia nne kwa kiwango cha lami.Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi

Nipitisheni nilirejeshe Jimbo la Kawe- Pijei

$
0
0
MTIA nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kawe, Jumaa Mhina 'Pijei', amewaomba wananchi wa Kawe kumpa kura ili aweze kulirejesha jimbo mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika kampeni zake za mwishoni jimboni humo, Pijei, alisema mbali ya kujitokeza makada 21 kulitaka jimbo hilo, wananchi ndiyo wenye uwezo wa kuamua nani wa kumpa nafasi hiyo.

"Wanachama sehemu zote tulizopita watakuwa tayari wamemwona anayefaa kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Kawe, nami naamini nafasi hiyo ninaiweza kwani vijana, akina mama na hata akina baba wanajua kazi zangu za maendeleo nilizozifanya jimboni kwetu," alisema.

Pijei katika kata zaidi ya tano za jimbo hilo, amekuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na jinsi alivyokuwa akijinadi katika mikutano ya kampeni ya kura za maoni.

Jimbo la Kawe limekuwa likishikiliwa na upinzani tangu mwaka 2010, likiwa chini ya Halima Mdee,hivyo CCM wamejipanga kuhakikisha wanalirejesha mikononi mwao, lakini kama likimpitisha mtu sahihi anayependwa na wengi.

Baadhi ya waliojitokeza ni Mtiti Butiku, Yusuph Nassoro, John Mayanja, Dickson Muze, Dk. Wilson Babyebonela, Kippi Warioba, Colman Masawe, Elias Nawera, Abdallah Majura na Jerry Muro.

USIKU WA HERIETH PALLANGYO ULIVYOFANA

$
0
0
 Biharusi mtarajiwa Herieth Charles Pallangyo akiwa kwenye pozi muda mfupi kabla ya kuanza tafrija yake maalum ya kugana na familia yake kbla ya kufunga ndoa. Tafrija ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika ukumbi wa Giraffe Sunset, Mbezi Beach Dar es Salaam. Production by: MD Digital Company +255 717002303, +255 755 373999.
 Herieth akiwa katika pozi la picha na mama yake
 Wazaa chema Bwana na Bibi Charles Pallangyo wakiwa katika pozi.
 Wageni waalikwa wakiwa ukumbini hapo. PICHA ZAIDI HAPA

Simba Imeshinda katika mchezo wake wa Pili wa Mazoezi dhidi ya Timu ya Black Sailor kwa mabao 4--0

$
0
0
Kikosi cha Timu ya Black Sailor iliopanda daraja mwaka huu kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Msimu wa mwakac 2015/2016, ilikubali kupigo cha mabao 4--0 dhidi ya timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku huu katika uwanja wa amaan Zanzibar. 
Kikosi cha Simba kilichotoa kipigo kwa Timu ya Black Sailor uwanja wa Amani usiku huu Simba ikiwa Zanzibar kwa michezo ya kirafiki kuimarisha Kikosi chake kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania. 
       Jopo la Makocha wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo huo wa kirafiki na timu ya Black Sailor
Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Black Sailor, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 4--0
Mchezaji wa timu ya Black Sailor akiwapita wachezaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki.

                    Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor

Mchezaji wa timu ya Simba Abdi Banda akiifungia timu yake bao la kwanza kwa kichwa katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Simba imeshinda bao 4--0
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na mchezaji Abdi Banda kwa kichwa baada ya kupigwa krosi na Khamis Kiiza, mwenye jezi namba 5
Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor wakati wa mchezo wao wa kirafiki.
              Mshambuliaji wa timu ya Simba Khamis Kiiza akimpita beki wa timu ya Black Sailor


Mshambuliaji wa timu ya Simba na Black Sailor wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya Simba imeshinda 4--0 mchezo uliofanyika usiku huu.
Mshambuliaji wa timu ya Simba akizuiya mpira huku mabeki wa timu ya Black Sailor wakijiandaa kumzuiya.
       Kipa wa timu ya Black Sailor akidaga mpira ikiwa moja ya ulio gplini kwa timu ya Black Sailor
Mshambuliaji wa timu ya Simba akiruka kiunzi cha beki wa timu ya Black Sailor wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan Timu ya Simba imeshinda 4--0
Goli la pili la timu ya Simba lililofungwa na mshambuliaji Ibrahim Hashim katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshunda 4--0
                           Beki wa Timu ya Black Sailor akiokoa mpira galini kwake
Mchezaji wa Simba akiwa juu akipiga kichwa golini kwa timu ya Black Sailor.
Beki wa timu ya Black Sailor akioko mpira golini kwake wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Amaan Timu ya Simba imeshinda 4--0.Picha na OthmanMapara.Blog. Zanzinews.com  

MGOMBEA URAIS WA CHADEMA KUREJESHA FOMU LEO

$
0
0
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU MGOMBEA URAIS KUREJESHA FOMU

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa baada ya hatua ya kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa ndani ya chama kugombea nafasi ya urais, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa kesho (LEO) Agosti 1, 2015 atarejesha fomu yake kwa ajili ya taratibu zingine za ndani ya chama.

Shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 9.00 jioni, ambapo mgombea atakabidhi fomu  yake Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chama, Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika hadhara ikayohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali.

Mheshimiwa Lowassa atarejesha fomu hiyo akiwa mgombea pekee baada ya kuwa ametimiza taratibu za kikatiba hususan kupata wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima.

Hatua hiyo ya kurejesha fomu itafuatiwa na taratibu zingine za kikatiba, ikiwa ni pamoja na vikao vya uteuzi ambavyo vitaketi kwa mujibu wa ratiba ambayo imeshapangwa na chama.

Imetolewa leo Julai 31, 2015 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano – CHADEMA

New Music Video - NELLY Y FT MESEN SELEKTA - SINGUTA

MGOMBEA UBUNGE ARUSHA ,MUSTAFA PANJU APANDIKIZA MBEGU YA UPENDO,AMANI NA MSHIKAMANO

$
0
0
SAM_4682Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akiwaonyesha kadi ya CCM inayoonyesha imani ya mwanachamana kwa wanahabari pamoja na wadau mbalimbali jijini Arusha, pia alizungumzia kuhusu mchakato wa ndani ya chama kumpata mgombea wa Ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM siku moja baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuzunguka katika kata 25 za kuomba kura kwa wanachama wa chama hicho,aliwataka wananchi kumchagua mwanachama watakaoonyeshwa na Mungu na siyo kwa kushawishiwa kwa pesa,pia alionyesha furaha yake kwa kuweza  kupandikiza mbegu bora ya Upendo,Amani na Mshikamano kwa wagombea wenzake pamoja na Wanaarusha kwa ujumla(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4659Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali jijini Arusha ,ambapo aliwashukuru wagombea wenzake 12 wanaowania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Arusha kwa kumaliza mchakato wa kuzunguka katika kata 25 jimbo la Arusha kwa Amani,Upendo na mshikamano na pia alionyesha furaha yake kwa kupandikiza mbegu bora ya Upendo,Amani na Mshikamano
SAM_4665Sehemu ya wadau wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM .
SAM_4676
Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akisisitiza wananchi kwa ujumla kuwa na Upendo,Amani na Mshikamano na kusisitiza kuwa atamuunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na chama cha mapinduzi,kulia nia Kassim Mamboleo  katibu wa kamati ya Ushindi
SAM_4666Wadau wakifatilia hotuba kwa umakini
SAM_4692Mwenyekiti wa kamati ya Ushindi Godfrey Mhando akizungumza ambapo alisema kuwa kila mtu anahaki ya kumchagua kiongozi anayeona anafaa na siyo kurubuniwa kwa fedha
SAM_4691Kassim Mamboleo  katibu wa kamati ya ushindi akizungumza na wanahabari pamoja na wadau ambapo alitoa rai kwa Watanzania kuwa makini katika mchakato huu kuelekea uchaguzi mkuu
SAM_4677Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akisoma imani inayopatikana katika kadi yake ya CCM ,moja ya imani ni pamoja na Upendo,Amani na Ushirikiano
SAM_4686Mchambuzi wa kisiasa na Mwanahabari mkongwe hapa Nchini Abrahamu Gwandu akizungumza katika mkutano huo alisisitiza wananchi kuwa na Umoja,Upendo na kuchagua kiongozi bora kuelekea uchaguzi mkuu ili kuepusha uvunjifu wa Amani
SAM_4680Mwanahabari Mwandamizi Shaban Mdoe akifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM
SAM_4688Meza kuu
SAM_4660Taswira katika mkutano huo
SAM_4690Mdau akiongea katika mkutano huo

Statment by the Director General - Tfda - Steering Committee

KUMBUKUMBU

$
0
0
Mpendwa Mama Rhoda Cleopa Msuya
Daima tutakupenda kamwe hatutokusahau.
Ni Miaka kumi tangu ulipotangulia

Tumebaki na kumbukumbu za mapenzi yako ya dhati na wema wako
Tumekukumbuka leo, jana, juzi na siku kabla yake

Tunakukumbuka moyoni na kila tunapotaja jina lako

Kumbukumbu zetu kwako haziwezi kuelezeka

Tumebaki na kumbukumbu ya tabasamu lako na picha yako

Ni kumbukumbu za upendo wako ndio zinatupa nguvu ya kuendelea mbele

Daima utabaki katika mioyo yetu

Uko Katika Ufalme wa Mungu, Tunakuombea upumzike kwa amani.


Unakumbukwa daima na mume wako Cleopa, watoto wako George,John,Joyce, Job, Naanjela.
Wakwe, Onesmo, Khadija,Mercy,Mary na Yoko, wajukuu, ndugu na marafiki.

Misa maalum ya kumbukumbu ya wapendwa wetu Mama Rhoda Cleopa Msuya na Geoffrey Cleopa Msuya itafanyika Tarehe 9 August 2015 kwenye kanisa la Azania Front Cathedral saa tatu na nusu asubuhi,
Wote mnakaribishwa.

“kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka” Mithali 10:7

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM ZANZIBAR CHATOA TAMKO JUU YA KUJITOA KWENYE CHAMA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASA.

$
0
0

 Katibu wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga akitoa taarifa ya Chama hicho kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa ndani ya Chama Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa katika mkutano uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
 
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM aKisiwandui Mjini Zanzibar. 
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Borafia Silima akitoa ufafanuzi katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wa ngazi mbali mbali za Chama na waandishi wa Habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir/Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar   

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni Chama  kikubwa chenye wafuasi  na wanachama wengi  pamoja na  Viongozi wenye hekima, busara, mapenzi na uadilifu mkubwa.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga  wakati alipokuwa akitoa taarifa  kwa Waandishi wa Habari  kuhusu kujitoa Chama cha Mapinduzi Waziri Mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowassa na kujiunga na Chama cha upinzani  huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui 

Amesema CCM ni Chama  kinacho aminiwa na kukubalika na Wananchi wengi wa Tanzania  hivyo  kujitoa kwa mwanachama mmoja ama kikundi cha wanachama haiwezi kukiathiri  chama hicho.

Nyawenga ameongeza kuwa wingi wa wanachama wa chama hicho  haujaletwa na utajiri wa vingozi wake bali umetokana na uimara wa Siasa, Sera na itikadi yake.

Alisema CCM haina hasara kumpoteza mwanacham mmoja anaetaka kubadili sera na itikadi ya Chama  kwa maslahi yake binafsi na marafiki zake hata kama utajiri  wake ni mkubwa wa kupindukia.

Ameongeza kuwa uwamuzi wa Lowassa kujiondowa ndani ya Chama hicho sijambo la kukishituwa chama, viongozi, pamoja na wanachama wake na hakiwezi kudhoofika wala kutetereka.

Alisema hii sio mara ya kwanzi kwa Chama cha Mapinduzi kuondokewa na kiongozi  mwandamizi  na kujiunga na  vyama vya upinzani na bado kinaendelea kuimarika.

“Mwaka 1989, CCM iliwafukuza uanachama viongozi waandamizi 11 akiwemo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, akafuatia Agostino Lyatonga Mrema  na mwaka jana CCM ilimfukuza uanachama aliyekua Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansour Yussf,” alikumbusha Katibu wa Chama Mkoa.

Nyawenga aliweka wazi kuwa  umaarufu alionao  Lowassa inawezekana umejengwa kutokana na CCM lakini haiwezekani umaarufu wa Chama hicho umejengwa kutokana na yeye.

Alisema wanachama wa Zanzibar  waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa katika azma  ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walifanya hivyo kwa sababu ya siasa, sera na ilani ya Chama na sasa  baada ya kuhama wameamua kujitenga  na hawako pamoja naye.

Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib Borafia Silima amesema kwamba Tanzania inaheshimika kuwa  ni  nchi yeye amani, na mshikamano na Chama cha Mapinduzi  kinafuata utaratibu wa katiba iliyowekwa.

Amesema kila Mwanachama anayo haki  na uhuru wa kuchaguwa kiongozi anayemtaka na yeye  kuchaguliwa na mtu yeyote ikiwa ni Demokrasia iliyotandikwa na Chama hicho.   

Angalia kipindi cha Nyumbani Na Diaspora cha wiki hii

TAKUKURU YAKANUSHA TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA NAPE


WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MUHIMBILI 1988 WAIKUMBUKA SHULE YAO.

$
0
0
Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, akikata utepe ili kufungua Ofisi ya walimu wa shule ya msingi Muhimbili, iliyokarabatiwa na kuweka viti 29 na meza 8 na wanafuzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo Mwaka 1988, pamoja na kiti na meza ya kisasa katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo katika hafra fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao ikiwa imehudhuliwa na walimu wa shule hiyo wa tangu mwaka 1978.
 Walimu wa Shule ya Msingi Muhimbili wakifurahia kupewa viti vipya pamoja na meza na wanafunzi wao waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo, wamekabidhiwa Samani hizo leo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muhimbili, Dafrosa Assenga akipeana mkono na Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, mara baada ya kukabidhiwa kiti na meza Mpya kutoka kwa wanafunzi waliohitimu katika shule hiyo Mwaka 1988, ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza elimu katika shule hiyo.Kutoka kulia ni Mhitimu wa shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988 na Mkurugenzi wa Galaxy Cargo, Jonatha Kasesele, Mwenyekiti wa wahitimu 1988  shule ya msingi muhimbili,Usia Nkoma
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na  Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Muhimbili, George Ntevi.
Mwalimu wa shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1986 hadi sasa, Marry Massawe akiwashukuru wanafunzi waliosoma shule hiyo kwa kuikumbuka shule yao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimmbili mwaka huu wakiwa wamehudhulia hafra fupi ya wahitimu wa shule hiyo mwaka 1988 leo jijini Dra es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

LOWASSA AREJESHA FOMU YA KUWANIA URAIS KWA CHAMA CHA CHADEMA

$
0
0

 WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, akipungia wafuasi wa CHADEMA na wananchi wengine waliofurika makao makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi Agosti 1, 2015, baada ya kurejesha fomu za kukiomba chama chake kumteua kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ndiye atakayesimama kwa niaba ya vugucugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

NA K-VIS MEDIA
WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, ambaye leo Jumamosi Agosti 1, 2015 amerejesha fomu za kuomba chama chake kipya cha CHADEMA, kimteue kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya vyama vinavyounda vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi maarufu kama UKAWA, ameanza na mtaji wa “kura”  zaidi ya Milioni 1.6, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, mafunzo na msimamizi wa Kanda 10 za chama hicho, Benson Kigaila ametangaza.
Kigaila amesema, idadi hiyo ni ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wengine ambao wamemdhamini katika fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama hicho. “Wote waliomdhamini, kwakuwa walikuwa wengi nchi nzima, tulitoa masharti kuwa kila anayetaka kufanya hivyo awe na kadi ya kupigia kura na aweke namba yake ya simu ya mkononi na wote wamefanya hivyo na hii ina maana kuwa CHADEMA, chini ya UKAWA, tuna kura za Rais milioni 1,662, 397.” Alifafanua Kigaila, wakati akielezea utaratibu uliotumika wa wana CHADEMA kumdhamini Mh. Lowassa.
Hatua hiyo ya Mh. Lowassa, ya kurejesha fomu zilizopokelewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Profesa Abdallah Safari, inasubiri hatua nyingine ya Kamati Kuu ya chama hicho ambayo inakutana Agosti 2, 2015 ili kuzipitia fomu hizo kuona kama zinakidhi matwaka ya kikatiba na kanuni za chama hicho kabla ya kupelekwa kwenye vikao vingine vya juu na hatimaye kwenye mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2015 hapa jijini Dar es Salaam.
 Wafuasi wa CHADEMA, wakimshangilia Mh. Lowassa, alipokuwa kitoka kwenye makao makuu ya chama hicho baada ya kurejesha fomu
 Mh. Lowassa, akikabidhi fomu hizo, kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Tanzania Bara), Profesa Abdallah Safari

 Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Kanda 10 za CHADEMA, Benson Kigaila, akionyesha lundo la fomu zilizomdhamini Mh. Lowassa.
 Mh. Lowassa, akipongezwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya chama hicho, Mabere Nyaucho Marando
 Wabunge wa CHADEMA na majimbo yao kwenye mabano kutoka kushoto, Godbless Lema (Arusha Mjini), Wenje (Nyamagana), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini)
 Mh. Lowassa, akiwasili makao makuu ya CHADEMA
 Mh. Lowassa, akiwa na Esther Bulaya
 Profesa Safari
 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, (Zanzibar), Salum Mwalimu
 Mtoto wa mwisho wa Mh. Lowassa, (katikati), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa CHADEMA, wakati baba yake Mh. Lowassa aliporejesha fomu
 Wabunge na viongozi wa CHADEMA
 Vijana wa 4U ambao walimuunga mkono Mh. Lowassa wakati akiwa CCM, na sasa wanaendelea kumuunga mkono akiwa CHADEMA


 Wananchi waliofurika makao makuu ya CHADEMA wakati Mh. Lowassa akirejhesha fomu


 Mh. Lowassa, akiteta jambo na Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene

UZINDUZI WA ALBAMU TATU ZA MWAITEGE NI KESHO UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE, WAIMBAJI WATAKAO MSINDIKIZA WATAMBULISHWA

$
0
0
 Mwimbaji wa nyimbo za injili, Boniface Mwaitege (katikati), akiimbaji sanjari na waimbaji wenzake wakati wakitambulishwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi. Waimbaji hao kesho watatoa burudani wakati wakimsindikiza mwimbaji mwenzao Boniface Mwaitege katika uzinduzi wa albamu zake tatu za Utanitambuaje, Mama ni mama na Tunapendwa na Mungu utakaofanyika kesho ukumbi wa Diamond Jubilee saa nane mchana kesho. Kutoka kulia ni Faustine Mnishi, Upendo Kilahiro, Jesca Magupa (BN) na Atosha Kissava.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi huo.
Msama (katikati), akiwa na waimbaji watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

MWANAMUZIKI wa Injili, Boniface Mwaitege kesho mchana anatarajiwa kuzindua albamu zake tatu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mkurugenzi wa Kapuni ya Msama Promotion alisema kuwa maandalizi yote muhimu ya tamasha hilo litakalofanyika kuanzia saa nane mchana yamekamilika, Mwaitege atatambulisha albamu hizo kwa kusindikizwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili.

Alisema mashabiki wa muziki wa Injili watarajie burudani ya nguvu kutokana na maandalizi ya nguvu na ya kipekee aliyofanya mwanamuziki huyo ikiwemo kurekodi albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Nairobi na Kenya.

"Maandalizi yote ya uzinduzi wa albamu za Mwaitege yamekamilika, mashabiki watarajie burudani ya nguvu, pamoja na ujumbe kutoka katika nyimbo hizo pamoja na mwanamuziki wengine watakamsindikiza," alisema Msama.

Alisema sehemu ya mapato katika uzinduzi huo ambao pia utafanyika katika mikoa mingine, itapelekwa kwa kwenye vitu vya watoto yatima.

Msama alizitaja albamu hizo ni pamoja na 'Tunapendwa na Mungu' yenye nyimbo za 'Tukiimba Mungu anashuka', 'Mtoto wa mwenzio ni wako', 'Safari Bado', 'Tumekuja Kukuchukua (Bibi harusi)', 'Tuko Salama', 'Moyo wa Shukrani', 'Hakuna Ridhiki', albamu nyingine ni Utanitambuaje na Mama ni Mama.

Baadhi ya wanamuziki watakaopanda jukwaani kusindikiza uzinduzi wa albamu za Mwaitege waliotambulishwa kwa waandishi wa habari na baadhi ya nyimbo zao zilizotamba katika mabano ni Upendo Kilahiro (Baba Ninakuabudu), Jesca  Magupa (Napokea), Mchungaji Faustine Munishi (Malebo) na Atosha Kisava (Umwema).

Akizungumzia utambulisho wa albamu zake tatu, Mwaitege alisema amejiandaa vizuri kwa uzinduzi huo, ambapo mashabiki wataweza kupata burudani nzuri na ujumbe, pia albamu hizo zitakuwepo ukumbini.

Aliwataka mashabiki kufika kwa wingi katika onesho hilo ili kumpa hamasa yeye na waimbaji wengine ambao watamsindikiza.

Awali wasanii wengine waliotajwa kusindikiza uzinduzi huo ni  pamoja na John Lisu, Martha Mwaipaja, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Eiphraim Sekereti, Atosha Kisava, Mess Chengula,  Eveline Kabwemela, Ambwene Mwasongwe na Joshua Mlelwa.

Onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini.


Kiingilio katika onesho hilo kitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti maalumu, sh. 5,000 na sh.2,000 kwa watoto.

 Boniface Mwaitege, atakaye zindua albamu zake tatu hapo kesho.
 Faustine Munishi, mmoja wa waimbaji wa injili atakayetoa burudani.
Upendo Kilahiro, atatumbuiza.
Jesca Maguba (BN), atatumbiza

Atosha Kissava, atatumbuiza.

 (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii

Mwigulu Nchemba Ashinda kwa 99% kura za maoni Ubunge jimbo la Iramba

$
0
0
Mwigulu Nchemba Ashinda kwa 99 % kura za maoni Ubunge jimbo la Iramba

 Masimba          
Mwigulu 88
Jairo 1
Kilimba 0
Amon 0

Mlandala
Mwigulu 50
Jairo 0
Kilimba 3
Amon
0

Mang'ole 
Mwigulu 173
Jairo 6
Kilimba 0
Amon 0

MSAI
Mwigulu 294
Jairo 35
Kilimba 59

MALUGA
Mwigulu 322
Kilimba 5
Jailo 0

 UWANZA
Mwigulu 172
Jairo 8
Kirimba 23
Amon 2

 Nganguri

Mwigulu 727
kilimba 2
jairo 2
Amon 0Mwigulu kashinda

WATANZANIA CALIFORNIA WAMUAGA BALOZI LIBERATA MULAMULA

$
0
0
 Watanzania California wakiongozwa na Balozi wa Heshima Mhe. Ahmed Issa walijumuika pamoja siku ya Ijumaa na kumuaga Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na kurudi nyumbani kwenda kulitumikia taifa kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Watanzania wa California wakipiga picha ya pamoja na Mhe. Balozi Libarata Mulamula (wapili toka kushoto) siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomuaga rasmi.
 Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi yake Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme mara tu baada ya kukabidhiwa na Watanzania California siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomualika rasmi kwa ajili ya kumuaga.
 Balozi Liberata Mulamula akicheza na kuburudika kwenye moja ya nyimbo zilizopigwa kwenye tafrija hiyo.
 Balozi Liberata akipiga makofi
Moja wa kikundi maarufu cha ngoma ya asili kikitoa burudani
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images