Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 595 | 596 | (Page 597) | 598 | 599 | .... | 1904 | newer

  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
    Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa
  shahada. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa  msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa kuanza kwa sherehe za kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
  Wasanii wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho. 

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  court_gavel
  MDAI katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali Magreth Mwangu mkazi wa Mkoani Singida dhidi ya Mkurugenzi wa Shule za sekondari za St.Mathew na St Marks Thadei Mtembei amelalamikia kitendo cha Benki ya CRDB kutoa taarifa zake za benki bila idhini yake wala ya mahakama.

  Pia ameilalamikia mahakama ya Mwanzo Kizuiani inayosikiliza kesi hiyo kwa kutumia Wakili wa kujitegemea licha ya kuwa mawakili hawaruhusiwi katika mahakama ya Mwanzo. Kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Rajab Tamaambele.

  Wakili huyo amekuwa akimwakilisha mdaiwa ambaye amekuwa hafiki mahakamani tangu kesi hiyo ifunguliwe kwa kile kilichoelezwa wamepata kibali kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali kinachoruhusu kesi hiyo kusikilizwa na wakili bila mdaiwa kuwepo. Kwa mujibu wa Mwangu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo mdaiwa amekuwa hafiki mahakamani na badala yake amekuwa akiwakilishwa na mtoto wake,Peter Mtembei ambaye ni Wakili hali iliyofanya kesi hiyo mpaka inaisha na kufungwa ushahidi mdaiwa akiwa hajasikiliza shahidi hata mmoja.

  Hata hivyo Mmiliki huyo wa St, Mathew juzi alifika mahakamani kufuatia amri ya mahakama kufuatia malalamiko ya mdai aliyokuwa akitoa mahakamani kutokana na Mtembei kushindwa kufika kwenye kesi hiyo tangu ilipofunguliwa na iliyomtaka afike mwenyewe mahakamani hapo na endapo asingefika mahakama ingehamia nyumbani kwake. Akitoa ushahidi wake, Mtembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.

  Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu. Alisema mama huyo hana hadhi ya kuwa mke wake kwani ameishia darasa la saba elimu ambayo ni ya chini sana.

  “Huyu alikuwa ni mfanya usafi tu ni nesi msaidizi kazi yake ilikuwa ni kufanya usafi na hata kufunga vidonda tu” alisema. Alisema duka hilo la dawa lilifungwa baada ya kuonekana aliyekuwa analihudumia hana elimu. Mtembei alisema mdai hana uhusiano na mali alizonazo kwani yeye ana mke wake wa ndoa na huyo alikuwa ni mwanamke tu aliyezaa naye.

  “Huyu ni mwanamke tu niliyezaa naye hana haki kwenye mali zangu” alisema.Alipohojiwa na mahakama kama alifunga ndoa na mdai alisema kuwa hajawahi kufunga naye ndoa licha ya kutoa mahari ya Ng’ombe watano. “Nilimpelekea baba yake vindama vitano tu kama zawadi” alisema.

  Alisema hajawahi kufunga ndoa ya kimila na mdai kama inavyodaiwa na mdai hana haki yoyote katika mali zake. Kwa upande mwingine mdai alihoji sababu za mdaiwa kwenda Benki ya CRDB na kutoa taarifa za fedha za akaunti yake bila kuwa na amri iliyotolewa na mahakama.

  “Mdai kwa kutumia nafasi nzuri ya kifedha aliyokuwa nayo ameweza kwenda benki ya CRDB na kupewa taarifa za fedha kwenye akaunti yangu bila ruhusa yangu au ruhusa ya mahakama jambo ambalo limeniathiri kisaikolojia’ alisema.

  Hata hivyo hakimuTamaambele alisema hafahamu ni wapi mdaiwa alitoa taarifa hiyo lakini mahakama inaipokea kuwa sehemu ya ushahidi.Kesi hiyo imepangwa kutolewa hukumu Agosti 25, mwaka huu. Katika kesi hiyo mdai anaiomba mahakama imuamuru mdaiwa kupa takala,kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.

  0 0


  Mchekeshaji maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na bendi yake ya Swahilli Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki jumamosi wiki hii.
  Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa” kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.

  Mratibu wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka Kenya na Uganda ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000/- kupata burudani za muziki wa bendi na kwa wale watakaoingia kwenye disco la kukesha ni shilingi 20,000/-, na tiketi za V.I.P zitauzwa kwa shilingi 40,000/-.

  “Wanamuziki wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi” alisema Naamala.

  Bendi ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.

  Tamasha hilo limedhaminiwa na Regency Park Hotel, Vibe Magazine, Bongo5.com, Michuzi Blog, Goethe Institut, Midundo Online Radio, CEFA, Timeticket, Nafasi Art Space, Eco Sanaa Arts Space, Creative Infinity, Kenya Airways, Apex Media, Iris Media, Kumkichwa Entertainment, Santuri Safari DJs na Legendary Music.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw. Jose Castillo, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo ofisini kwake Migombani.
  Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw. Jose Castillo, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani.
  Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw. Jose Castillo, akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, baada ya mazungumzo yaliyokuwa chini ya Maalim Seif. Katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Omar Dadi Shajak.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki, pamoja na baadhi ya watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).
   ...............................................................................
                                                                                    
  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) limesema litafanya tathmini ya kina kupata njia muafaka za kuisaidia Zanzibar kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya kwa jamii.

  Hayo yamesema na Kiongozi wa ujumbe kutoka Shirika hilo, Jose Vila Del Castillo alipokutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad huko ofisini kwake Migombani na kufanya naye majadiliano.

  Del Castillo amesema kutokana na mazingira ya nchi za visiwa kama Zanzibar mikakati maalum ya kupambana na dawa na biashara za dawa za kulevya haina budi kuchukuliwa ili kuwaokoa wananchi wake na kugeuzwa njia za kusafirishia biashara hiyo haramu.

  Amesema msaada huo utalenga zaidi kuipatia Zanzibar vifaa vya kisasa, kukuza utaalamu kwa watendaji na wadau muhimu wa kupambana na dawa za kulevya, ikiwemo wendesha mashitaka, wapelelezi, watendaji wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na wanasheria.

  Alisema UNODC litaanza kufanya tathmini hiyo mwezi ujao na ikikamilika, Shirika hilo litaweza kufahamu ni hatua gani linapaswa kuanza kuzichukua kwa mashirikiano na Serikali ya Zanzibar kukabiliana na biashara hiyo na madhara yake.

  Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali inachukua hatua mbali mbali kuiepusha Zanzibar kuwa kituo cha kuingizwa na kusafirishiwa dawa za kulevya.

  Maalim Seif amesema juhudi hizo pia zinajumuisha kuwasaidia wananchi wasijiingize kwenye vitendo vya kutumia au kufanya biashara hiyo, ikiwemo kutoa miongozo kwa makundi mbali mbali ya jamii, wakiwemo wanafunzi wa skuli mbali mbali.

  Kuhusu wale ambao tayari wanatumia dawa hizo, Maalim Seif amesema Serikali kwa mashirikiano na jumuiya na watu binafsi imefungua vituo maalum kwa ajili ya kuwasaidia kubadilisha tabia, ili baadaye wawe raia wema katika jamii yao.

  Makamu wa Kwanza wa Rais amesema hivi sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imeanza ujenzi wa kituo cha kisasa cha kurekebisha tabia wananchi wanaotumia dawa hizo, ambacho jengo lake litakuwa na ghora tatu na sehemu zote muhimu kwa mahitaji yao.

  Hata hivyo, alisema zipo baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Zanzibar, ikiwemo uhaba wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na ukaguzi katika maeneo ya kuingilia na kutokea nchini.

  Changamoto nyengine alizozitaja ni mazingira ya visiwa vya Zanzibar kuwa na bandari nyingi zisizokuwa rasmi ambazo hutumiwa na baadhi ya watu kuingiza vitu vyenye madhara, zikiwemo dawa za kulevya.

  Katika mazungumzo hayo, Mshauri wa masuala ya Ukimwi wa Shirika hilo Kanda ya Afrika Mashariki, Sylvie Bertrandamesema msaada huo wa UNODC pia utajumuisha kuimarisha mazingira ya vyuo vya mafunzo, ili kuepusha maambukizi ya ukimwi na athari nyengine zitokanazo na dawa za kulevya.


  0 0

  2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) TRA, SUMATRA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, wakati  walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015.Picha na OMR
  3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa SUMATRA, TRA, na Wamiliki wa Mabasi Tanzania TABOA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Fedha, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015.

  0 0

  MU1

  Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi akiwa na kitambulisho chake mara baada ya kujiandikisha mapema Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam.
  MU2
  Mwandikishaji Msaidizi Bi. Maida Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi  fomu ambazo zimebeba taarifa zake kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam
  MU3
  Alama za vidole zikichukuliwa na Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya mara baada ya kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu ya utambulisho.
  MU4
  Jaji Mutungi akipiga picha kwa ajili ya kitambulisho
  MU5
  Mhe.Jaji  Francis Mutungi akipokea  kitambulisho cha mpiga kura kutoka kwa Mwandikishaji Bw.Ernest Moses Selelya.

  0 0

  Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.Ofisa Biashara wa Mkongo wa Taifa kutoka TTCL, Ian Mawala (kushoto) akifanya mazungumzo kubadilishana uzoevu na mmoja wa wadau wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, katika mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect'. Ofisa Biashara wa Mkongo wa Taifa kutoka TTCL, Ian Mawala (kushoto) akifanya mazungumzo kubadilishana uzoevu na mmoja wa wadau wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, katika mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect'.Uwasilishaji wa mada; mmoja wa washiriki katika mkutano huo akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania. Uwasilishaji wa mada; mmoja wa washiriki katika mkutano huo akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania. Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.
  Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania. Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.Uwasilishaji wa mada; Roger Blackshaw kutoka Kampuni ya Deutsche Telekom Group (kulia) akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania. Uwasilishaji wa mada; Roger Blackshaw kutoka Kampuni ya Deutsche Telekom Group (kulia) akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.Baadhi ya washiriki na wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano wakiendelea na mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect'. Baadhi ya washiriki na wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano wakiendelea na mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect'.IMG_0277Meneja Maendeleo wa China Telecom Global Limited, Li Shao Zhan (kushoto) akifanya mazungumzo na mmoja wa washiriki katika mkutano huo wa wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania. Meneja Maendeleo wa China Telecom Global Limited, Li Shao Zhan (kushoto) akifanya mazungumzo na mmoja wa washiriki katika mkutano huo wa wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini TanzaniaBaadhi ya washiriki katika mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, viongozi wa serikali wa mataifa mbalimbali ya africa, wakibadilishana uzoefu. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, viongozi wa serikali wa mataifa mbalimbali ya africa, wakibadilishana uzoefu.Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania. Mijadala mbalimbali ikiendelea ndani ya siku ya pili ya mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect' unaoshirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano unaofanyika nchini Tanzania.Baadhi ya washiriki na wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano wakiendelea na mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect'. Baadhi ya washiriki na wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa taasisi binafsi zinazotoa huduma za mawasiliano na zinazotengeneza vifaa vya mawasiliano wakiendelea na mkutano wa Kimataifa wa 'Connect 2 Connect'

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
   Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akiwasili ofisi za Makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar,akiwa ameambatana na Mh Lowassa (hayupo pichani),kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.
    Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
  Rabsha za hapa na pale zilikuwepo kama uonavyo pichani wakati Mh.Lowassa akiwasili Makao Makuu ya CHADEMA  yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
   Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
   Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  Raia wa kigeni wajaribu kujipatia vitambulisho vya kupigia kura wafikia 2040 kwa mikoa ya  mikoa ya Kagera watu 708, Mara 619, Tanga 348,Kigoma 254, Rukwa 13, Kilimanjaro 12, Ruvuma 9, Geita 6, Shinyanga 7, Mtwara 3, Pwani 2, Mbeya 1, Morogoro 1 na Dar es Salaam 65. 
  Hayo yamesemwa na Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao  jijini Dar es Salaam leo.

   Aidha Irovya amesema amewakumbusha wananchi kupiga kura ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania ana sio raia wa kigeni kujiandikisha ili apige kura kwana raia wa kigeni hana uwezo wa kupiga kura katika nchi asiko zaliwa.

  Pia Irovya amesema kuwa wananchi walio chukua paspoti za kusafiria zinapoisha muda wake ni lazima wabadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapohitaji.
    
   Irovya ameongezea kuwa wananchi wanaotafuta paspoti za kusafiria tofauti na ofisi za uhamiaji wajue huko wanapotea paspoti zote zinapatikana katika ofisi za uhamiaji tuu na sio popote pale.

  Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na wahamiaji haramu wanayo jiandikisha katika  Daftari la wapiga kura katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
  Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa uhamiaji wilaya ya Iala, Safina Muhindi,katikati ni Afisa  uhamiaji wilaya ya Temeke, Jaffari Kisesa na Afisa Mdhibiti wa Paspoti, Cripin Ngonyani wakimsikiliza Kaimu kamishina wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Da es Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya jijin Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0


  Baadhi ya wateja wakiwa ndani ya Airtel smartphone Bazaar ili
  kusmartiphonica na simu za kisasa kwa bei poa.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza offa kabambe ya
  simu za kisasa itakayopatikana katika viwanja vya nane nane kuanzia
  siku ya Ijumaa tarehe 31 julai 2015, kwa muda wa siku 10
  Akiongea kuhusu ofa hiyo Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga
  amesema, Airtel inaendelea kuwapati wateja wake mawasiliano bora na
  kuwaunganisha na simu za kisasa zilizounganishwa na vifurushi vya bure
  vya internet katika msimu huu wa nanenane".

  " Napenda kuwajulisha watanzania wote na wakazi wa Morogoro kuwa
  Airtel   sasa tumewafikia na kusogeza huduma zetu karibu nao katika
  viwanja vya nanenane ambapo tutakuwa na offa nyingi ikiwemo simu za
  kisasa ya aina ya Airtel red itakayounganishwa na huduma za internet
  bure kwa mwaka mzima kwa gharama ya shilingi 75,000.

  Sambamba na Airtel Red pia tunazo simu za aina nyingi  ambazo ni
  pamoja na simu ya Huawei , Techno, Samsaung. Simu hizi zinamuwezesha
  mteja kuzitumia katika kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutunza
  rekodi zao, inatumika kama kamera ya kupiga picha pamoja na mambo
  mengine mengi.

  Tunatoa wito kwa wateja wetu watembelee banda la Airtel  katika
  viwanja ya Nanenane na kupata nafasi ya kununua simu hizi za kijanja
  kwa gharama nafuu "aliongeza Muga.

  Airtel Smartphone Bazaar bado pia iko jijini Dar es Salaam katika
  maduka yote ya Airtel. Khalikadhalika wateja wote bado pia wananafasi  ya kusmatiphonica kwa kutembelea maduka ya Airtel nchi nzima.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (katikati), akikata utepe kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba na (kulia kwake) ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Duka hilo, Mwanavita Chiya. 
   Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (kushoto), kuhusu bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga, baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua duka hilo jana. 
    Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba (kushoto), akifafanua jambo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (mwenye miwani), baada ya mkuu huyo kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana.
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (wa pili kushoto), akikagua Duka jipya la Airtel Tanzania baada ya kulizindua katika hafla iliyofanyika dukani hapo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana. 
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Said Magalula (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba baada ya mkuu huyo, kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana.


  KAMPUNI  ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka lake jipya
  katika mkoa wa Tanga ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha inawapatia
  wateja wake nchi nzima huduma bora na za kisasa.

  Duka hilo la kisasa,  liko katika maeneo ya tanga mjini, Barabara ya
  Uhuru, kwenye jingo la nyumbani hoteli. Huduma zinazotolewa na duka
  hilo ni pamoja na kukusanya Ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo
  ya simu hasa smartphone, Airtel money, kusajili namba pamoja na huduma
  za kimitandao.

  Akiongea wakati wa uzinduzi , Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa
  wateja wa Airtel, bi Adriana Lyamba alisema” uzinduzi wa duka hili ni
  uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kuwapatia  wateja
  wetu uzoefu toufati  katika huduma zetu.  Leo tunawawezesha wateja
  wetu na wakazi wa mkoa wa Tanga kupata hudumu muhimu kama vile za
  kifedha za Airtel Money kwa usalama zaidi pamoja na kuwaunganisha na
  simu za kisasa za smartphone na huduma zetu za intaneti”.

  “Sambamba na hilo, duka letu pia litatoa ofa kabambe za simu na vifaa
  vya aina tofauti na kuwawezesha wateja wetu kunganishwa na tecknologia
  ya simu za mkononi ya kisasa.

  Tunaamini vifaa vya kisasa ni sehemu muhimu ya mahitaji ya wateja wetu
  kwa sasa,  hivyo kupitia watoa huduma wetu waliobobea kwenye maswala
  ya tekinologia tunawewezesha wateja wetu kuchangua vifaa na simu bora
  pamoja na kuwaunganisha na huduma za intanet. Ni matumanini yangu kuwa
  wateja wetu sasa watapata suluhisho la mahitaji yao ya huduma za simu
  kwa urahisi kupitia duka hili.” Aliongeza Lyamba.

  Akizindua duka hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Magalula Said Magalula
  alisema”  Mawasiliano yanachangia kwa kiasi kikubwa katika
  kuwaunganisha watu na biashara na kukuza uchumi wa nchi. Nawapongeza
  Airtel kwa kuongeza wigo kupitia huduma kwa wateja na kuleta
  mabadiliko ya kibunifu. Tunaamini ubunifu huu utawawezesha wakazi
  waTanga kupata huduma bora wakati wote,  na kwa hilo Tunawashukuru
  sana Airtel.

  “Natoa wito kwa wakazi wa Tanga na wateja wa Airtel kutembelea duka
  hili  na kufurahia huduma na bidhaa za kisasa ikiwemo huduma ya Airtel
  Money inayotoa suluhisho kwa mahitaji yao ya huduma za kifedha,
  kufanya malipo na kutuma pesa kirahisi  zaidi”.

  Mkuu wa Mkoa aliwahasa makampuni mengi zaidi kuiga mfano wa Airtel
  katika kutoa huduma bora na kusema Serikali iko tayari kushirikiana
  nao katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wakazi na watanzania wa
  ujumla katika maeneo mbalimbali nchini.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya moto wa la Liga utawashwa ndani ya Super Sport 3(SS3)katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika leo jijini Dar es Salaam.Kulia Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi na Afisa masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samaly.
   Meneja uendeshaji wa DST,Ronald Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari juu chanmeli mpya ya michezo katika kingamuzi cha Multchoice,katika hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi.
   Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia taarifa katika uzinduzi wa channel katika hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Picha Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  WATAZAMAJI wa Supersport watakuwa nafasi pekee kushuhudia mechi kwenye ubora wa HD pamoja na michuano ya Ligi kuu ya Uingereza (EPL),Ligi ya Hispania (La liga),Ligi ya Mabingwa wa Ulaya  (UEFA),Ligi ndogo za Ulaya (Europa),Mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu bingwa ya Dunia ,Kombe la Ujerumani ,Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) na Kombe la FA.


  Akizungumza na waandsihi wa habari leo Meneja Uhusiano wa Multchoice,Babra Kambogi amesema wateja wa DStv wateja wa DStv wakae tayari kwenye msimu wa mabingwa ulimwenguni ambapo Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine huku Manchester United wakihitaji kurudisha kiti chao cha ubingwa Uingereza.


  Amesema katika msimu huu zaidi ya mechi 900 za kimataifa zitaonyeshwa kimataifa na wateja wa DSTV Compact Plus wataweza kufurahia  baadhi ya mechi zaidi 450  live  huku wateja wa Dstv premium watazawadiwa mechi zote.


  Babra amesema wateja wa Dstv vituko vya michuano yote ya ligi kuu Uingereza vitaletwa kupitia Suparspot (SS5) kinochopaatikana katika kifurushi cha Premium na SS5 itakuwa ndio nyumba ya soka la Afrika kwa Ligi kuu ya Uingereza.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015.


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada ya kumvisha vazi hilo.
  Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Julai 30, 2015. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
    Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
    Magufuli, akikabidhiwa fimbo ya heshima ya kabila la Kimasai.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwashukuru wananchi wa zawadi ya vazi la Kimasai, baada ya kuvishwa wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR

  0 0
 • 07/30/15--08:39: Article 24
 •  


  0 0

  Nchi ya Tanzania ya bahatika tena kwa mara ya tatu kua mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya mwaka huu imekua ni Kuunganisha bara la afrika mwambao hadi mwambao. 
   
  Katika hotuba iliyotolewa siku ya kwanza katika ufunguzi wa mkutano huo ili elezea changamoto kubwa za usalama mitandao na namna unavyoweza kuleta athiri kwa kiwango kikubwa endapo usalama huu mtandao hautaangaziwa macho. Hotuba hiyo pamoja na mjadala nilio ongoza kwa siku ya kwanza unaweza kusomeka na kuonekana kwa “KUBONYEZA HAPA”.

  Mkutano huu wa mara hii uliokusanya washiriki kutoka katika mataifa 30 duniani kote  ulihusisha wafanya maamuzi ya juu, watengeneza sera na wadau wengine kadhaa ambapo Mawaziri na Manaibuwaziri  wa Nchi kadhaa wkiwa ni miongoni mwa waliopata kuongoza mijadala pamoja na kuunganisha mawazo katika maswala mbali mbali ya barani Afrika.

  Kongamano hili la mwaka huu lililoandaliwa kwa kushirikiana wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  pamoja na kampuni ya simu ya TTCL limeonyesha mafanikio makubwa sana kwa kuwezesha kauli mbiu ya mwaka huu kufikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia mijadala mbali mbali iliyo jadiliwa katia kongamano hili.

  Mbali na mada nyingine mbai mbali – Kwa siku zote mbili za mkutano huu mijaadala mizito ya usalama mtandao ilipata kujadiliwa kwa kina ambapo nilipata bahati ya kuongoza mjadala wa siku ya kwanza na kuhutubia kwa siku ya pili juu ya maswala ya usalama mitandao. 

  Katika hotuba yangu ya siku ya pili katika mkutano huu nilipata kuangazia hali ilivyo duniani kote na kueleza kwa kifupi kuhusiana na Mkutano mkuu wa mwaka ulioangazia maswala ya usalama mitandao jijini Johannesburg ambapo pia nilihutubia kwa niaba ya Bara la Afrika tulipo kutana wataalam wa maswala haya katika ngazi ya dunia. Zaidi niliweza kuainisha mapungufu makuu tuliyo nayo yanayo sababisha vita dhidi ya uhalifu mtandao kuenekana kutushinda kutokana na uhalifu huu mtandao kuendelea kushamiri.


  Msisitizo mkuu nilio toa mbali na kuhimiza ushirikiano na kutumia vizuri wenye ujuzi na elimu hii ya usalama mitandao, Nilipata kuainisha makundi ma nne ambayo ni Mtu binafsi, kundi la Watu ( Wana usalama mitandao), Kampuni , pamoja na serikali na kueleza kuna dhana potofu inayo dhani makundi matatu kati ya hayo manne ndio yenye dhamana ya usalama mtandao na kusahau kabisa kua lazima usalama mtandao uanzie katika ngazi ya MTU BINAFSI.

  Nikitolea hili ufafanuzi – Nilielezea mtu binafsi anakila sababu ya kuhakiki usalama wake uko vizuri kwa kuhakiki neno la siri “Password” Matumizi ya salama ya mitandao na kuhakisha kila hatua za kujilinda dhidi ya uhalifu mtandao kama ilivyo katika hali ya kawaida ya kulinda makazi yetu zina angaziwa vizuri kwani  jukumu la kulinda usalama mtandao si la kundi flani la watu pekee.

  Nikiwa na waziri wa TEHAMA - BURUNDi
  Waziri wa TEHAMA wa Burundi katika mazungumzo yake mkutanoni na baadae tulipo kutana  kwa mazungumzo baina yetu alionyesha dhahiri matumizi mabaya ya mitandao hasa hii ya kijamii ilivyo changia kuyumbia taifa la Burundi huku akiendelea kutoa wito juu ya matumizi salama ya mitandao ya kijamii ili kuweza kuchochea usalama wa taifa lolote duniani – Katika kuumunga mkono nilimpatia mifano kadhaa ya Nchi kama Misri, Libya na nyinginezo ambazo ziliyumba na kuanguka huku sababu kuu ikiwa ni mitandao ya kijamii kuchochea fujo katika nchini hizo.

  Niliwa na Waziri wa TEHAMA -  LETHOSO
  Nilifarijika kuona Nchi ya LETHOSO pamoja na NAMIBIA kuonyesha dhamira yao ya dhati ya kutaka kujifunza kutoka kwetu kwenye maswala haya ya usalama mitandao na kupongeza hatua nzuri tuliopiga hadi leo. Katika mazunungumzo yangu na Waziri wa TEHAMA wa LESOTHO alinieleza wimbi kubwa na matumizi mabaya ya mitandao nchini mwake ndio limeendelea kua kikwazo na ana mikakati ya kuandaa sera pamoja na sheria mitandao ili kuhakiki ana himili vishindo vya ukuaji wa matumizi mabaya ya mitandao.

  Aidha, Kwa upande wa NAMIBIA – Mbali na kunipongeza walionyesha dhamira ya yadhati ya kufanyia kazi ushauri niliotoa katika mkutano huu, huku wakisisitiza kua wanaamini kabisa tatizo kubwa ni upungufu wa ukuzaji wa uelewa juu ya mambo ya usalama mitandao pamoja na serikali nchini afrika kutoona Usalama mitandao ni kipa umbele na wakisahau Uhalifu mtandao unauwezo mkubwa wa kuangusha taifa lolote.

  Mwisho, Nitoe wito kwa serikali ya Tanzania na wadau mbali mbali kutambua athari kubwa katika Nyanja zote kuanzia kiuchumi hadi kisiasa zinazoweza kuonekana kama usalama mtandao hauta angaziwa macho ipasanyo. Wakati huu tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu lazima tujue mitandao ya kijamii inaweza kabisa kuyumbisha taifa letu hivyo hakuna budi kuwa na umakini madhubuti katika hili. Tayari nimesha lizungumzia hili mara kadhaa na zaidi unaweza kupitia Andiko linalosomeka kwa “KUBOFYAHAPA”

  0 0

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico),Zena Kangoyi akizungumza na waandishi wa habari juu mafanikio ya stamico baada ya maboresho yaliyofanywa katika shirika hilo katika Ofisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi wa  Utafiti  na Uchorongaji ,Alex Rutagwelela akizungumza na waandishi wa habari juu Stamico linavyosimamia majukumu yake katika katika kuendeleza wachuimbaji wadogo iliyofanyika leo Makao Makuu ya Stamico,jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala,Beatrice akizungumza na waandishi wa habari juu Stamico linavyoweza kusimamia miradi yake na uwezo wa Shirika hili iliyofanyika leo Makao Makuu ya Stamico jijini Dar es Salaam.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico,Zena Kangoyi akiwa na baadhi ya wakurugenzi wakati akieleza mafanikio ya shirika hilo kwa waandishi wa habari iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico)limesema kuwa kutokana na kuwepo kwa maboresho katika shirika hilo limezidi kujitanua katika utoaji wa utaalam kwa wachimbaji wadogo jinsi ya kuchimba madini kisasa na kuachana uchimbaji duni.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,Zena Kongoyi amesema kuwa shirika licha ya kuweka miradi ya kusaidia wachimbaji wadogo lakini wameweza kuwekeza uchimbaji wa madini kwa kushirikiana na kampuni zingine kutokana sharia ziliwekwa baada ya mabaoresho ya shirika hilo.

  Amesema baadhi ya miradi ya uzalishaji wa madini imeanza kuzalisha na kuweza shirika kutoka hatua moja  kwenda nyingine katika katika utaoji huduma pamoja kukuza uchumi wa nchi pamoja kuongeza ajira nchini kutokana na miradi ya uzalishaji wa dhahabu.

  Zena amesema kuwa shirika limeanzisha miradi kuendeleza wachimbaji wadogo kitaalamu na ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu (SMMRP) katika kuwaondoa katika uduni.

  Amesema katika mradi wa Stamigold umesafirisha na kuuza dhahabu katika nchi ya Switzerland kwa kiasi cha Wakia 12,923.35 na kuingizia shirika la Taifa la Madini (Stamico)na taifa kwa ujumla Dola za Kimarekani Milioni 15.6. na kuaza kurejesha mrabaha wa asilimia 4.0 ya mauzo sawa n ash.1.3 za serikali na Wizara ya Nishati na Madini na kulipa ushuru sh.milioni 40..

  Aidha amesema shirika limeweza kuanzisha mradi wa ununuzi wa madini ghafi ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa maeneo ya vijiji vya Kabingo,Murongo ,Syndicate na Rugasha katika Wilaya Kyerw,mkoani Kagera  na kuyauza madini hayo kwenye soko la nje ya nchi ikiwa na lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo .

  Zena amesema wako katika mazungumzo na Benki ya TIB kuweza kukopa Dola za Kimarekani 700,00090000  kwa ajili ya kununua mitambo hali ambayo shirika litaweza kukua katika kuendesha miradi mbalimbali.


  0 0
 • 07/30/15--09:02: PROFESA MARK MWANDOSYA ANENA
 • Na Profesa Mark Mwandosya
  Leo ni siku inayofuatia jana, siku ambayo Ndugu yangu Edward Ngoyai Lowassa aliacha rasmi uanachama wa CCM na kupewa kadi ya uanachama wa Chadema. Si yeye tu bali alisindikizwa na mke wake mpendwa Mama Regina Lowassa. 

  Nilidhani leo mitandao yote ingesheni habari hiyo kubwa. Kumbe nami nimekuwa "staa" katika mitandao ya kijamii. Kuanzia asubuhi nimekuwa nikipokea na kujibu simu mbalimbali nikiulizwa maoni yangu kuhusu tukio la jana, kuhusu mchakato wa Dodoma uliomalizika hivi karibuni, na "habari" kubwa imekuwa Mwandosya, Mwapachu na ole Medeye wahamia Chadema! 

  Kuhusu Ndugu Lowassa kuhamia Chadema nionavyo mimi ni jambo la kawaida sana katika demokrasia ya vyama vingi. 
  Wanachama hutoka na kuingia karibu kila siku. Hivyo basi tukio la jana lisingegonga vichwa vya habari kama isingekuwa kwa umaarufu wa mhusika. Jambo la msingi kwa CCM ni kutafakari, bila ghadhabu, na kwa utulivu, ni sababu zipi za msingi zilizofanya hili jambo litokee? Je tunaweza kujifunza lolote katika hili ili kukiimarisha Chama? .

  Tunaweza kuboresha nini katika taratibu na kanuni zetu? Nimeulizwa pia kitendo cha Ndugu Lowassa kuhamia Chadema kina athari gani kwa CCM? .

  Pamoja na kutotokuwa msemaji rasmi wa Chama, tukio hili lina maslahi ya umma kwa ujumla hivyo kukwepa kujibu hakusaidii. Siasa ni takwimu, hasa tunapoelekea Oktoba. Kwa mantiki hiyo mtu mmoja kukihama Chama kuna maana kura moja iliyopungua. 

  Kwa kuwa haiwezekani kuirudisha, basi changamoto ni kuwa na mkakati wa kutafuta kura ya kufidia, kuzuia kupotea kwa kura nyingine, na kuongeza idadi ya wanaoingia ili iwe kubwa kuliko ile ya wanaotoka. 
  Msaafu wa dini unasema mchungaji bora ni yule anayeweza kuwaacha kondoo wake tisini na tisa walio salama ili amtafute yule mmoja aliyepotea! Suala la kujiuliza katika mazingira ya yaliyotokea ni je tulikuwa wachungaji bora? .

  Nadhani moja ya mambo ya msingi CCM itabidi tulitafakari kuhusiana na mchakato wa kumpata mgombea wetu kwa nafasi ya urais ni je tunamtafuta mwanachama ambaye atakuwa Rais? Je tunamtafuta mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama? Au tunamtafuta mtu atakayekuwa Rais na Waziri Mkuu? 

  Vigezo vya kumtafuta mtu huyo vinapishana kama ambavyo orodha wa wenye nia au mifumo ya kumpata itapishana. Naamini tungelitafakari haya yote huenda tusingefika hapa tulipo. Lakini Taifa ni kubwa kuliko sisi watu na uhai wake ni mpaka "kiama cha wafu". 

  Tujadili masuala haya na mengine muhimu, kwa ujasiri, uwazi na ukweli. Nahitimisha kwa kujibu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na watu wengi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari kuhusu Mwandosya kuhama kwenda Chadema. 

  Misingi iliyojengwa na waasisi wa Chama, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume naendelea kuamini bado ni sahihi. Ndiyo iliyotuletea heshima kubwa kama Taifa. 
  Kama tumeyumba turudi katika misingi. Itikadi ya Chama inajengwa juu ya misingi hiyo. Hivyo basi kwangu mimi Ilihali misingi ipo, na imara, nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM ili kwa pamoja na wanachama wenzangu tuendelee kulijenga Taifa juu ya misingi hiyo, kila wakati tukikumbuka kile alichotuasa Baba wa Taifa, Tujisahihishe! Prof.

  0 0

  1
  Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa jinsi unavyofanyakazi zake kwa haraka, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
  2
  Mkurugenzi wa Shirika la John Snow Incorporated (JSI) nchini, Deo Kimera akitoa nasaha zake kwa Viongozi na Maafisa wa Afya waliopata elimu juu ya matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa wa kielektroniki walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt  Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
  8
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna kushoto akihutubia mara baada ya uzinduzi wa Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  3
  Mshauri  Mwandamizi kutoka Shirika la Misaada la Marekani USAID Kelly Hamblin akitoa shukran zake kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano yao ya kufanikisha Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa nchini,  katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel  Shangani Mjini Zanzibar.
  4
  Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akitoa shukrani zake kwa Shirika la John Snow Incorporated (JSI) kutokana na juhudi zao za kuwawezesha maafisa wa Afya wa Zanzibar kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa kwa njia ya kielektroniki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt  Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
  5
  Mfamasia kutoka Bohari Kuu Zanzibar Bi. Khadija Ali Shehe akielezea changamoto walizokumbana nazo wakati wa kutumuia mfumo wa Karatasi katika Usambazaji wa Madawa  vituoni kabla ya kuzinduliwa Mfumo mpya wa kielectroniki hii leo.
  6
  Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Gombani Pemba Abdalla Mbaruk Saleh akitoa ushuhuda wa namna Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa unavyofanya kazi zake kwa haraka na ufanisi, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika  Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
  7
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna katikati akizindua Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Kulia kwake ni Msimamizi wa taaluma  kutoka Shirika la John Snow Incorporated (JSI) Anselm Namala ,na kushoto ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman. Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.

  0 0older | 1 | .... | 595 | 596 | (Page 597) | 598 | 599 | .... | 1904 | newer