Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 594 | 595 | (Page 596) | 597 | 598 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa QAML Mwenyekiti,Yusuf Manji wa kwanza kulia, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya magari ya General Motors East Africa (GMEA) Limited, Mario Spangenberg wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Isuzu uzinduzi huo uliofanyika jiji Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya General motors (GMEA) Bi. Rita Kavashe  akisaini makubaliano ya kibiashara na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Quality automotive Vinay Upadhyay.
   Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Rita Kavashe alisema Kampuni ya General motors kuingia katika soko la Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu katika kampuni hiyo ili kuimarisha uwepo wake Afrika Mashariki. Kulia ni Rais na Mkurungenzi Mtendaji wa (GM) Africa  Mario Spangenberg.


  Wakifurahia jambo mara baada ya kukamilisha makubaliano.
  PICHA NA EMMANUEL MASSAKA


  General Motors Imerudi tena katika soko la Tanzania ikiwa imeongeza ufanisi zaidi, 

  Wenya magari Tanzania leo wana sababu ya kutabasamu maana Kampuni ya magari ya General Motors East Africa (GMEA) Limited leo wamesaini makubaliano ya kibiashara na Quality automotive mechanization limited (QAML) ambayo itashuhudia  kampuni ya magari ikiingia kwenye soko la Tanzania.

  Kupitia uuzaji mpya, wateja wa General Motors wataweza kununua bidhaa mpya aina ya Isuzu na Chevrolet kutoka katika sehemu za mauzo huku wakipata huduma za kimataifa kutoka katika eneo maalumu la magari hayo.

  Akizungumza hi leo wakati wa sherehe ya kutia saini makubaliano ya biashara, Mwenyekiti Mheshimiwa wa QAML Mwenyekiti Mheshimiwa Yusuf Manji aliahidi wateja ngazi bora ya urahisi na faraja.

   “Tumeweka uwekezaji mkubwa/muhimu kuhakikisha mafanikio ya kituo hiki na kuwezesha kupenya kwa haraka kwa bidhaa za Isuzu na Chevrolet katika soko hili lenye ushindani mkubwa”.

   Alisema
  Eneo la mauzo ya magari limetengenezwa ili kutoa/ kuwapatia wateja uzoefu na uimara kwa ujumla na bidhaa za General Motors, pamoja na kutoa huduma za mauzo na vifaa vya magari.

  Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Bi. Rita Kavashe alisema Kampuni ya General motors kuingia katika soko la Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu katika kampuni hiyo ili kuimarisha uwepo wake katika Afrika Mashariki.

  “Tanzania imejitokeza katika soko na kama General Motors tulitaka kuwa sehemu ya ukuaji huu. Sehemu hii ya mauzo itakuwa ni hatua ya kuingia kwa bidhaa zetu zenye ubora na zimetumia utaalamu mkubwa katika utengenezwaji wake  ambapo tunatanua wigo wetu katika ukanda huu. Kupitia uuzaji huu, wateja wetu watanunua aina mpya za Chevrolet na Isuzu huku wakipata huduma bora”.

  Alisema Bi. Kavashe alisema kuingia ndani ya soko la Tanzania imetokana na kukua kwa kasi kwa biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki hasa katika kuendeleza ushirikiano wa masoko ya umoja. Soko la jumuia ya Afrika Mashariki lina takribani watu milioni 140 .
  “Tanzania ni soko linalokua kwa kiwango kikubwa na imekua ni soko muhimu tunalolitazamia tunapotafuta kujikita katika soko lenye watu wengi na idadi inayokua kila kukicha. Ukuaji wa viwanda na


  kuongezeka kwa kipato ili kutengeneza ongezeko la watu wa tabaka la kati katika nchi hii ina maana kuwa kuna soko changa la bidhaa zetu, “aliongezea Kavashe.


  0 0

  sa1
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa huduma ya Afya ya Mama, vijana  na watoto mara baada ya kufika eneo la hospitali kwa madhumuni ya kujionea namna bora yautoaji huduma.  Mama Salma yupo nchini Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchni humo.
  sa2
  Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
  sa4
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na wazazi wao.
  sa5
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole na kumtakia apone haraka binti Addison Stephen,6, aliyevunjika mguu na kufungwa PoP na hatimaye kulazwa hospitalini hapo huku akihudumiwa na baba yake Mzazi Bwana Stephen Miles (aliyesimama kulia) na aliyechuchumaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Mama Elizabeth Chatham.
  sa6
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimbeba mtoto mchanga Isabella mwenye umri wa siku moja aliyezaliwa na uzito wa kilo 3 na gramu 8 katika hospitali ya Caniberra nchini Australia huku wazazi wake Bwana Steven Fanner,34, na Bibi Tania Mras,32, wakishuhudia tarehe 28.7.2015.
  sa7
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi jarida linalochapishwa na Taasisi yake kwa Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Matendaji wa Hospitali ya wanawake, vijana na watoto ya Caniberra nchini Australia mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbaali za kutolea huduma hospitalini hapo yarehe 28.7.2015.
  sa8
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Gavana Jenerali wa Australia Mama  Cosgrove mara baada ya Rais Kikwete kukutana na Gavana Generali wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove kwenye Ikulu ya nchi hiyo tarehe 28.7.2015.
  sa9
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ikulu ya Australia  huku Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyeji wake Gavana Jenerali Peter Cosgrove na Mkewe wakishuhudia.
  PICHA NA JOHN LUKUWI.

  ……………………………………………………………………………………………
  Na Mwandishi wetu – Canberra, Australia 
   Wafanyakazi wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya  mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania ili kumuunga mkono Mke wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete katika juhudi zake za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto.

  Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia afya za wanawake, vijana na watoto wa Hospitali hiyo Liz Chatham wakati akiongea na Mhe. Mama Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Hospitali hiyo.

  Liz  alimshukuru Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kutembelea Hospitali hiyo na kujioneka kazi wanazozifanya pia alimpongeza kwa juhudi zake anazozifanya za kuhakikisha wanawake na watoto wa Tanzania wanapata huduma bora ya afya.

  Mkurugenzi huyo alisema katika Hospitali hiyo wafanyakazi wengi  wa sekta ya afya wanapenda kwenda kufanya kazi Tanzania  ili waweze kutoa huduma ya afya kwa ajili ya mama na mtoto pamoja na watu wengine  na kubadilishana ujuzi wa kazi na wenzao.

  Kwa upande wake Mhe. Mama Kikwete alisema  ni jambo la kufurahisha kuona katika Hospitali hiyo wanawake wenye afya njema wanajifungua katika mazingira mazuri na watoto ambao ni wagonjwa wanapewa matibabu na  uangalizi wa hali ya juu.

  “Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia kinamama wajawazito na watoto, kujifungua iwe sababu ya kuwa na  furaha na kusherehekea lakini siyo tofauti na hapo, nasema hivi kutokana na mazingira halisi ya kule ninakotoka”.

  Pamoja na kuwa jitihada za makusudi zinafanywa na Serikali bado wanawake na watoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika”, alisema Mama Kikwete.

  Akiwa katika Hospitali hiyo Mama Kikwete alipata nafasi ya kuongea na watoto ambao ni wagonjwa  ambao kwa wakati huo walikuwa darasani wanasoma na aliwaona  na kuwajulia hali wazazi waliojifungua Hospitalini hapo.

  Utaratibu wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary mtoto akiwa amelazwa kipindi ambacho shule hazijafungwa anafundishwa masomo ambayo wenzake wanafundishwa darasani kwani Hospitalini hapo kuna madarasa na walimu wanaofundisha watoto wagonjwa.
  Mama Kikwete ameambatana na mmewe Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Australia kwa ajili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne.

  0 0

  mad1 
  Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava , akiongea jambo wakati akifungua kikao kazi  baina ya REA taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo , Taasisi Binafsi , Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Edmund Mkwawa, katikati ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini (REA), Dr. Lutengano Mwakahesya na mjumbe wa Bodi ya REA, Dr.  Gideon Kaunda.
  mad2 
  Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao hicho.
  mad02Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijjini (REA), Dr. Lutengano Mwakahesya akiongea jambo wakati wa kikao kazi baina ya REA taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo , Taasisi Binafsi, Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme.
  mad3 
  Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao kikao kazi baina ya REA, taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo n, Taasisi Binafsi, Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme
  mad4 
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, (katikati) katika picha ya pamoja na Washirika wa Maendeleo
  mad5
  Mwenyekiti wa Bodi ya REA Edmund Mkwawa, akiongea jambo wakati wa kikao kazi baina ya REA, taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo na Taasisi Binafsi, Wizara , Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme.

  ……………………………………………………………………..
  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
  Taasisi za Kifedha, Taasisi Binafsi na Washirika wa  Maendeleo nchini, wameshauriwa kuona fursa zilizopo katika sekta ya nishati hususani umeme kushirikiana na  serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA),  ili kuwezesha mapinduzi ya maendeleo na kuhakikisha kwamba vijiji vingi zaidi vinaunganishwa na nishati  ya umeme.

  Hayo yamebainishwa nyakati tofauti katika kikao kazi kilichoandaliwa na REA, kikijumuisha Taasisi za Kifedha, Taasisi Binafsi, Washirika wa Maendeleo Washirika katika tasnia ya nishati, wawakilishi kutoka Wizara na Taasisi za Serikali, kwa lengo la kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuhakikisha kwamba Tanzania hususan vijiji vinaunganishwa na nishati ya umeme ikiwemo  kuchochea shughuli za kiuchumi vijijini kupitia nishati hiyo.

  Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava amesema miradi ya kuviunganisha vijiji na nishati ya umeme ni eneo linalohitaji kuendelezwa kwa ushirikiano na wadau hao ili kuongeza kasi ya uunganishaji umeme.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya REA Edmund Mkwawa, ameeleza kuwa, endapo wadau hao watashirikiana na REA, mradi huo utaleta matokeo makubwa zaidi ya yaliyopatikana sasa na hivyo kuweza kuyafikia maeneo ambayo hayajafikiwa na nishati hiyo. Aliongeza kuwa, zipo fursa nyingi ambazo taasisi hizo zinaweza kuzitumia kupitia miradi mbalimbali ambayo itaziwesha kupata faida.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini (REA), Dr. Lutengano Mwakahesya alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote ambao wamewezesha Wakala huo kuunganisha miji na vijiji na nishati hiyo na kufikia asilimia 40 na kueleza kuwa, Wakala huo utaendelea kutafuta wafadhili ili kuweza kufanikisha malengo yake ya kuhakikisha kwamba taifa linaunganishwa na umeme.

  Kwa upande wake Afisa Mwandamizi anayeshughulikia nishati kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB), Stella Mandago, amezitaka taasisi hizo kufanya kazi na Wakala huo kwani zipo fursa nyingi na hivyo itawezesha taasisi hizo kupanua wigo wa shughuli zao kupitia nishati ya umeme.

  0 0
 • 07/28/15--12:47: TASWIRAZ KUTOKA BUKOBA LEO
 • Mji wa Bukoba na kwa mbali ni Kisiwa cha Msila mojawapo ya kivutio na kielelezo cha Mji wa Bukoba. Picha zote na Faustine Ruta/Bukoba
  Sehemu ya Bandari ya Bukoba

  Sehemu ya Mji wa Bukoba


  Picha zote na Faustine Ruta/Bukoba

  Mjini Bukoba

  0 0

  indexWASANII nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba katika mifuko mbalimbali ya jamii kwa kuwa kufanya hivyo kuna kumuhimu mkubwa katika maisha yao baada kuwa wamestaafu kazi zao au wanapokuwa hawana tena uwezo wa kufanya kazi.
   Hayo yalisemwa na msanii mkongwe wa maigizo hapa nchini Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala wakati akizungumza katika Jukwaa la na Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.
   Mzee Jangala alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na msanii Christian Kauzeni ambaye alitaka kujua ni kwa nini wasanii wakongwe wengi wanakuwa na maisha magumu licha ya kuwa walifanya kazi nzuri zilizo wahengea umaarufu mkubwa hapa nchini.Alisema wasanii wengi wakonge hawakuwa na utaratibu wa kuweka akiba, lakini kwa sasa kuna mifuko mingi na mifumo mingi ya kujiwekea akiba hivyo ni muhimu kwa sanii kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
   Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema huu si wakati wa msanii kupata shida baada ya kustaafu au kuzeeka kwa kuwa kuna mifuko mingi ya kuweka akiba na hata ya huduma za afya ambayo kwa mchango kidogo inatoa unafuu mkubwa wahuduma.
   “Haipendezi kwa msanii aliyekuwa na jina kubwa au umaarufu katika nchi anapokuwa amepatwa na maradhi kusubili harambee ipite ili apate matibabu, msanii akijiunga na mfumo wa bima ya Afya kwa mfano NHIF analipa fedha kidogo sana na anapata uhakika wa matibabu kwa muda mrefu wa maisha yake,” alisema Mngereza.

  0 0

  Simba SCAfisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Iman Kajula Akizungumza wakti wa Kuzindua Mpango wa Kuuza Vifaa vya simba Kupitia Duka la Mtandao akiwa Sambama na Rais wa Simba  Evans Aveva Pamoja na Msemaji wa Simba Sport Club.

  Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015 – 2016 kupitia duka la mtandao la Jumia www.jumia.co.tz . Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo Tanzania.
  Kupitia mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake ya michezo nchi nzima. Mkataba huu utaongeza usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba. 

  “Ukuaji kasi wa upatikanaji wa internet (mtandao) klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii ya Jumia – Simba Online Shop kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa az Simba kiurahisi na kwa bei nafuu”. Alisema Ras wa Simba Evans Aveva


  Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul aliongeza kwa kusema “uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba. Katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu 2015 – 2016 kupitia njia ya mtandao. Tunajivunia sana kwa Rais wa Simba Evans Aveva kutuchagua Jumia kwa kazi hii. Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia Jumatatu tarehe 27 – 7 – 2015 mpaka Alhamisi 31 – 7 – 2015 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa rasmi kwa rejareja”.
  “Tunawahamasisha wapenzi wa Simab popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitiawww.jumia.co.tz kuona urahisi katika kufanya manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaeza kuagiza jezi kupitia touti ya jumia na kuletewa mzigo wako mpka mlangoni. Jumia pia inatoa njia tofauti za ulipia kama ile kuweza kulipia pindi mzigo wakoutakapofika au kufanya malipo kwa njia za kipesa kupitia simu za mkononi. Kuanzia jumatatu 27 – 7 – 2015 wapenzi wa Simba watapatafursa ya kuagiza jezi kupitiawww.jumia.co.tz”. Aliongeza Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul.
  Kuzungumzia mapinduzi haya makubwa katika usambazaji wa vifaa ya michezo ya klabu ya Simba Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongezamapato yake pia kudhibiti bidhaa feki, kupitia Jumia Online Shops (duka la mtandao la Jumia) wapenzi wa Simba watanunua bidhaa za Simba kupitia washirika halali wa uuzaji wa bidhaa za Simba Tanzania.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015  katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015  katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai, 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 na kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove aliyesimama nyuma yake pamoja na Mama Salma Kikwete na Mke wa Gavana huyo Mama Cosgrove.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.PICHA NA IKULU.  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425


  Coat of Arms
  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania.

  "Nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la nadra sana Barani Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani  namna hii" Bw. Abbot amemuambia Rais Kikwete na kumueleza awe  na uhakika  kuwa " Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kukuza  uchumi"ameongeza.

  Rais Kikwete na Waziri Mkuu Abbot pia wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii.

  Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.

  Rais Kikwete amepokelewa leo asubuhi tarehe  28 katika makao  Makuu ya kiongozi  wa Australia kwa heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha mchana na baadae kupanda mti  kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya nchi hizi mbili kwa kipindi kirefu kijacho.

  Tanzania na Australia zimedumu katika ushirikiano  baina ya nchi zao tangu miaka ya sitini na sasa nchi mbili hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya  zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.

  Baadae leo jioni Rais Kikwete atakutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inaweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.

  Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo.

  Kesho tarehe 29 Julai, 2015 Rais Kikwete anatarajia kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.

  Rais Kikwete anatarajia kuondoka Australia na kurejea Tanzania baada ya shughuli ya kupokea shahada yake na ratiba yake kwa ujumla.

  Imetolewa na:
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
  Canberra-Australia
  28 Julai, 2015

   

  0 0

  Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifafanua jambo ndani ya Kilimanjaro Studio
  Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015.Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania.Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali
  Karibu

  0 0

  Mubelwa Bandio na Rose Chitallah studioni
  Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015.Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania.Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na mtangazaji Rose Chitallah,Karibu

  0 0


  0 0

  SAM_4554Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele yawananchi na wanachama wa chama hicho katika kata ya Themi viwanja vya Trans Foma jijini Arusha katika mkutano wa wagombea 12 wa chama cha mapinduzi ,kuomba kura katika kata 25 ambapo katika kura ya maoni atapatikana mmoja wa kupeperusha bendera ya CCM Arusha mjini(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_4518Kijana aliyejitokeza kusikiliza sera za wagombea 12 wa CCM akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju akimwaga sera zake kwa wananchi wa kata ya Themi viwanja vya Trans Foma jijini Arusha
  SAM_4552Wananchi  na wananchama waliojitokeza kuwasikiliza wagombea Ubunge jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi
  SAM_4512Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM akimwaga sera zake kwa wananchi na wanachama wa chama hicho kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya Ubunge.
  SAM_4517 Mtia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Thomas Munisi  a.k.a KOMANDOO akiwa anajinadi mbele ya wananchi kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM
  SAM_4542Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele yawananchi na wanachama wa chama hicho katika kata ya Lemara jijini Arusha ,mkutano huo uliudhuriwa na wagombea ubunge 12 wa chama cha mapinduzi CCM
  SAM_4644Picha ya pamoja wagombea Ubunge kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi katika ofisi ya CCM Wilaya mara baada ya kumaliza kijinadi katika kata 25 jijini hapa
  SAM_4498Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akizungumza katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi
  SAM_4492MNEC wa Arusha mjini Godfrey Mwalusamba akiongea katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM
  SAM_4510Wagombea nafasi ya udiwani kata ya Themi
  SAM_4549Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele yawananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi

  0 0

  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na tekinolojia, Selina Lyimo akimkabidhi cheti cha shukrani, Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa, wa Kampuni ya TTCL, Adin Mgendi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa ya siku mbili ya wadau wa mawasiliano wa mkongo huo iliyoanza jijini Dar es Salaam Julai 28, 2015.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na tekinolojia, Selina Lyimo akimkabidhi cheti cha shukrani, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Huwawei, Jimmy Liguo Jin wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa ya siku mbili ya wadau wa mawasiliano wa mkongo Taifa iliyoanza jijini Dar es Salaam.
  Adin Mgendi akonesha ramani ya mtandao wa Mkongo wa Taifa wakati wa mkutano jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Extensia, Tariq Malik (katikati) akifrahia jambo na wadau mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kulia ni Naibu Waziri wa ICT, Postali na Huduma Uchukuzi wa Zimbabwe, Win Mlambo na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Selina Lyimo.  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ugavi la umeme nchini (TANESCO) Mhandisi  Felchesmi Mramba akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

  Na Beatrice Lyimo-Maelezo.
  Zaidi ya Dola billioni nne za Kimarekani ikiwa sawa na Trilioni nane kwa shilingi ya Kitanzania zimewekezwa katika sekta ya umeme kwenye Miradi yote ya uzalishaji, usambazaji na usafirishaji wa umeme nchini.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ugavi la umeme nchini (TANESCO) Mhandisi  Felchesmi Mramba wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 10 (2005-2015), Serikali imeongeza uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa kutoka MW 891 hadi kufika MW 1,501.24 sawa na ongezeko la asilimia 68.5.

  “Baadhi ya miradi iliyokamilika  ni pamojaj na mtambo wa kuzalisha umeme MW 100 uliopo Ubungo, na Ujenzi wa mtambo wa kufua umeme MW 45  uliopo Tegeta jijini Dar es salaam. Miradi mingine ni mtambo wa kuanzisha umeme MW 60 Mwanza, na mradi wa umeme wa Somanga Fungu MW 7.5 Mkoani Lindi” amesema Mkurugenzi huyo.

  Kwa mujibu wa Mhandisi Mramba, kukamilika kwa Miradi hiyo kumewezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na kufanikisha kuondoa mgawo wa umeme hususani kuanzia mwaka 2012 na hivyo kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  Mtendaji huyo Mkuu wa TANESCO ameeleza kuwa kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwenye Gridi ya Taifa na nje ya Gridi ya Taifa ikiwemo utekelezaji wa Mradi wa Kinyerezi 1 (MW 150) kwa kutumia Gesi asilia, mradi wa kupeleka umeme katika miji ya Mpanda, Ngara, na Biharamulo.

  Aidha Mkurugenzi huyo ametoa ufafanuzi kuhusu kubadilisha mfumo umeme wa LUKU utakaofanyika tarehe 1/8/2015.

  “Zoezi la kubadilisha mfumo wa LUKU litachukua muda wa saa 24 kuanzia usiku wa manane wa Agosti Mosi, 2015 hadi usiku wa manane wa tarehe 2/8/2015 sio siku saba kama ilivyoenezwa katika mitandao  ya kijamii,” amesema.

  Lengo la zoezi hili ni kuongeza kasi na kuwawezesha watu wengi kuunganishwa na mfumo mpya wa LUKU utakaohudumia idadi kubwa zaidi ya watu tofauti na hali ilivyo sasa.

  0 0

  FFU-Ughaibuni wafunika katika maonyesho makubwa Ujerumani na kuwatia kiwewe    washabiki !
  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maaruka kama FFU-Ughaibuni au viumbe wa ajabu Anunnaki Alien's inayoongozwa na kamanda Ras Makunja,bendi hiyo yenye makao yake kule ujuerumani ,juzi iliuhakikishia ulimwengu tena kuwa mziki wao ni moto wa kuotea mbali! bendi hiyo ilifanikiwa kwa mara nyingine kuyafunika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival-Tübingen 2015,yaliofanyika katika viwanja vya Fest Platz,jijini Tübingen,Ujerumani.

  Bendi hiyo ilipanda jukwaani majira ya saa 4.00 usiku huku uwanja huo ukiwa umezungukwa na ulinzi mkali ! kamanda Ras Makunja akikiongoza jukwaani kikosi chake kilichoshamili vijana wa kazi akina Afande Mo Benda (Soloist) Sajent JoJo Sousa(Drumer) Kopro. Aj Nbongo (Bass) kijana Liga (Rhthym guitar) madansa Jessica Ouyah na Sarah Fina kikosi hiko kilifanya show la kukata na shoka.siku ya jumamosi 26 Julai 2015.


  0 0

  Mgeni rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment, Ndg Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure kabisa.
  Meneja bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana katika hoteli ya serena
   Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi 
  Mtangazaji wa Redio Clouds Ephraim Kibonde akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi wa Paisha wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Marquee Serena Hotel.
   Mdau akiwa pembeni ya mfano wa simu ya Iphone ambayo inaonyesha application ya Paisha.Paisha inapatikana kupitia playstore na google store bure na endapo utakuwa na application hiyo utaweza kufahamu na kupata huduma zote zitolewazo nchini huku wateja takribani Milioni 1 wameshajiunga huku watumiaji wakipata urahisi wa huduma hizo
  tukipata selfie
   Black ryhino akipata selfie na mabest zake wakati wa uzinduzi huo
   Ni mwendo wa selfie tu
   Wadau wakifuatilia uzinduzi wa application ya Paisha
  Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  Paisha ni platform ambayo inapatika katika simu za smartphone pamoja na tovuti platform hii ni kwaajili ya watoa huduma na wauzaji wa bidhaa ambao wanapenda kuwafikia wateja wao kirahisi,Paisha inapatikana kupitia google play na playstore huku watumiaji wa paisha wananufaika kufahamu sehemu ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali kama vile maduka na hata huduma nyingine sehemu ambapo watuamiaji hao sio wenyeji au wenyeji lakini hawafahamu baadhi ya bidhaa zinapatikana wapi.

  Ukiwa na application ya paisha katika simu inakusaidi kufahamu kuanzia ramani alipo mtoa huduma huyo pamoja na mawasiliano yake mfano umeenda tegeta na umepata pancha na haufahamu sehemu ilipo gereji ukiwa na paisha kwenye simu yako itakusaidia kufahamu ilipo gereji ambapo itakuonyesha jina la gereji iliyopo karibu na wewe hapo huku ikikuonyesha na ramani pamoja na mawasiliano ya gereji hiyo vilevile kwa bidhaa na huduma nyingine.

  Ni application ambayo inawalete urahisi watumiaji na watangazaji wa bidhaa hizo kupitia paisha.kufahamu zaidi kuhusu paisha unachotakiwa kufanya ni tembelea tovuti yao ya www.paisha.co.tz na vilevile unaweza kupakua application hiyo kupitia playstore na google play sasa
  Kuweza kupata faida zaidi

  0 0

  Meneja wa benki ya Exim tawi la Exim Tower, Bi. Rose Kanijo (kushoto), akikabidhi zawadi ya iPhone 6 kwa mshindi wa droo  ya kwanza ya kampeni ya Akaunti ya Malengo inayoendeshwa na benki hiyo, Bw, Prabhjot Singh, mkazi wa Dar es Salaam katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika makao makuu ya benki ya Exim jijini Dar es Salaam jana. Kampeni hiyo inayoendelea kwa miezi mitano zaidi, inalenga kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa Watanzania.


  0 0

  Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.
  Afisa Uhusiano na matukio wa wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akisikiliza (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.

  Airtel Tanzania leo imefanya droo yake ya Pili kwa wateja wake katika kampeni ijulikanayo kama “Jiongeze na Mshiko”. Kampeni hii ilianza rasmi tarehe 13 July 2015 na itaendelea hadi tarehe 10 Novemba 2015

  Akiongea na waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki amesema; “kila wiki, droo hii itawapatia wateja wawili nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni tatu za kitanzania, mmoja shillingi milioni moja kila wiki na mwingine milioni tatu kila wiki.

  Kwa wale watakaoingia katika droo ya milioni moja watajiunga na kushiriki bure na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milioni moja kila wiki na mwishoni mwa droo hii kuweza kujishindia shilling milioni 2. Na kwa wale washindi wa wa milioni tatu, mteja anaweza kuamua kuingia na kushiriki kwa tozo ya shilingi 300 kwa siku na mwisho wa promosheni mteja ataweza kujishindia milioni 50.

  Akitangaza washindi Dangio alisema" Leo tumechezesha droo ya wiki ya
  pili tangu kuzinduliwa kwa promosheni ya ”Jiongeze na Mshiko" wiki
  mbili zilizopita. Ninayo furaha kutangaza washindi hao ambao ni 
  Gabriel Fernandis(18) mwanafunzi na mkazi wa wa Mkoa wa Musoma Mara yeye amejishindi shilingi milioni 1 , na  mshindi wa pili ni Hamis Rashid(52)na mkazi wa mkoa waTabora Sikinge yeye amejishindi shilingi milioni 3.

  “Ushiriki upo wazi kwa wateja wote wa malipo ya awali. Wanachotakiwa kufanya ni kujiunga na promosheni hii  kwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), ndani ya Idara ya Habari MAELEZO,mapema leo jijini Dar kuhusiana na matokeo ya harambee ya Media Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), ndani ya Idara ya Habari MAELEZO,mapema leo jijini Dar na pia akiwa ameambatana na baadhi ya
  Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo, Athumani Hamisi na Danstan Bahai (hayupo pichani) ambapo leo wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu  yao.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari ZA Ukimwi (AJAAT), Adolf Simon Kivamwo kutokana na kusumbuliwa na Kansa ya Utumbo.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Milioni Tano kwa aliyekuwa mwandishi wa magazeti ya Habari leo na Daily News ambaye alipata ajali  na kumsababishia ulemamvu,Athman Khamis .

   
  Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo, Athumani Hamisi na Danstan Bahai wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu  yao.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson alisema kuwa fedha hizo ni matunda ya harambee ya Media Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.

  Kama tujuavyo, kwa kuanzia, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wengine waliosha magari kwenye viwanja wa Leader Club Julai 4, 2015.

  Alisema katika harambee hiyo jumla ya 31m/-, zilipatikana, ambapo kati ya fedha hizo, ndizo wagonjwa wamegawiwa.

  “Malengo yetu ya awali yalikuwa kwamba tuwachangishe fedha kwa ajili ya wenzetu wagonjwa, pia kiasi kingine kitumike kuwaingiza baadhi ya wanahabari kwenye mifuko rasmi ya Bima ya Afya. Na ndivyo tulivyofanya leo hii,” alisema.

  Bw Thompson alisema kiasi kilichosalia kitatumika kuwaingiza waandishi wa habari 100 katika mpango wa kulipia matibabu kupitia mfuko wa Bima ya Afya, yaani  NHIF.” Alisema.

  Alisema lengo la harambee hiyo ni kukusanya jumla ya 100m/- kabla ya mwezi Disemba 2015 na kazi yake kubwa itakuwa kuwahudumia wanahabari wasiojiweza kwa sababu ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.

  Pia pesa zitokanazo na harambee hiyo zitasaidia kuanzisha mkakati wa mkubwa wa kuhakikisha wanahabari wote nchini wanaingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

  “Lengo letu ni kuhakikisha wanabari wana kinga za afya zao,ili tukomeshhe huu mtindo wa kuchangiana mara kwa mara kila mmoja anapougua,”alisema na kuongeza kuwa  watakaohusika katika zoezi hilo, ni wale wasioajiriwa pamoja na wasioajiriwa lakini hawana huduma ya Bima ya Afya.

  Ili kuendeleza mchakakato wa kufikia lengo kuu, wanahabari Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na wenzao wa Jijini Dar es Salaam, Agost 15 mwaka huu, wataosha magari kwenye viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.

  Tunaomba wadau mbalimbali waungane nasi kwenye hili,ikiwemo kulipia gharama mbalimbali ukiwemo usafiri kwenda na kurudi Mwanza,hoteli, matangazo ya radio na mabango.

  Wakati huo huo Bw Thompson amesema kutakuwa mkutano wa wadau habari Jumamosi Agost 1, mwaka huu utakaofanyika Msimbazi Centre Jijini Dar es Salaam kwa jili ya kuanzisha mchakato wa usajili wa rasmi wa kampeni hii.

  “Tunaomba wanahabari wote nchini watakaoweza kuhudhuria wasikose kufika, maana hapa ndipo juhudi za ukombozi wa kiafya kwa wanahabari zitakapoanzishwa rasmi,” alisema.

  Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema kuwa Kamati yake imewashirikisha wahariri wote nchini katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kwamba viongozi hao wa vyumba vya habari ndio waliotoa majina hayo kwa kamati.


  0 0

   
   Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis 'Gadafi' akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa na Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis 'Gadafi' alipozungumza nao mapema leo mchana  kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.
   

  Chama Cha Mapinduzi  mkoa wa  Dar es Salaam kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi  alisema anawashukuru waandishi kwa ushirikiano waliounesha  kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa urais  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.
  Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani na Ubunge .Katika mkutano huo ambao waandishi wengi walionekana kuwa na  shauku ya kutaka kujua maoni ya  CCM juu ya kuondoka kwa Edward  Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”.

  0 0

  Afisa Madini Mkazi- Ofisi ya Madini Handeni, Frank Makyao (kulia) akifungua mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyokutanisha wachimbaji wa madini kanda ya mashariki mjini Handeni. Kutoka kushoto ni wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Pendo Elisha na Charles Gombe.
  Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Charles Gombe (kushoto) akisisitiza jambo katika mafunzo hayo. Kulia ni Afisa Madini Mkazi- Ofisi ya Madini Handeni, Frank Makyao.

  Na Greyson Mwase, Handeni-Tanga

  Wachimbaji wa madini nchini wametakiwa kuendana na teknolojia inayokua kila kukicha ili kuwezesha sekta ya madini kuwa na mchango zaidi katika pato la taifa.

  Rai hiyo ilitolewa na Afisa Madini Mkazi kutoka Ofisi ya Madini- Handeni mkoani Tanga, Frank Makyao kwenye ufunguzi wa mafunzo juu ya matumizi ya huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyokutanisha wachimbaji wa madini katika kanda ya mashariki yanayoendelea mjini Handeni.

  Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wa matumzi ya huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao ijulikanayo kama online mining cadastre transactional portal.

  Makyao alisema kuwa ni vyema wamiliki wa leseni za madini wakaachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika huduma za leseni kwani mfumo wa kisasa wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao utawawezesha kupata leseni kwa wakati na uwazi zaidi.

  “ Kwa mfano kuanzia sasa mtaweza kufanya malipo ya leseni zenu kwa njia ya M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa hali itakayowezesha ofisi za madini kupata mapato zaidi.” Alisisitiza Makyao

  Makyao aliendelea kusema kuwa wachimbaji wa madini wanatakiwa kuchangamkia mafunzo yanayotolewa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na kuanza kutumia huduma hiyo mara moja ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.

  Alisema biashara katika nchi nyingi duniani imekuwa ikifanyika kwa njia ya mtandao na kuwataka wachimbaji wa madini kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kuendana na ushindani wa biashara ya madini duniani.

  Aidha aliwataka wachimbaji wa madini kufuata sheria za madini katika uombaji na umiliki wa leseni za madini pamoja na kushirikiana na serikali kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali kama Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 inavyowataka ili sekta hiyo iwe na mchango zaidi katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.


older | 1 | .... | 594 | 595 | (Page 596) | 597 | 598 | .... | 1903 | newer