Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

VALEUR YAZINDUA “VALEUR COMEDY NIGHTS” JIJINI DAR

$
0
0
 Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimaro akizungumza katika uzinduzi wa shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’ leo katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela Bw. Evans Bukuku
Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela, Bw. Evans Bukuku akizungumza jinsi shindano hilo litakavyofanyika katika manispaa 3 za Dar es Salaam uzinduzi huo uliofanyika wa shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’ leo katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Na kulia ni Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimaro
Wawakilishi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) wakiongezea kuhusiana na Valeur Comedy Nights’ wakiwa na Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela Bw. Evans Bukuku.

TANZANIA Distilleries Limited (TDL) kupitia chapa yake ya ‘Valeur Superior Brandy’, kwa kushirikiana na kampuni ya Vuvuzela Company Ltd leo hii imezindua rasmi shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’. Hili ni shindano la kusaka, kuinua na kuendeleza vipaji vya Sanaa ya ucheshi litakaloanza wiki hii jijini Dar Es Salaam.

 Vuvuzela ni kampuni inayojihusisha na Sanaa ya ucheshi, ikimiliki pia onyesho kubwa la Sanaa ya ucheshi jijini Dar Es Salaam lijulikanalo kama ‘Evans Comedy Night’.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimaro alisema. “Kauli mbiu ya chapa yetu ya Valeur Superior Brandy ni ‘Kwa story zinazonoga’. 

Watumiaji wapenzi wa Valeur hupenda sana story nzuri wakiwa katika mapumziko yao, tunaamini kwamba story nzuri na sanaa ya ucheshi vitaweza kufanya mapumziko ya wapenzi wa Valeur kuwa bora zaidi. 

Tumeungana na Vuvuzela Entertainment na tuko hapa leo kuzindua ‘Valeur Comedy Nights’. Lengo letu ni kusaka na kukuza vipaji vya Sanaa ya ucheshi hapa Tanzania, kuwafanya wasanii hawa kugundua fursa waliyo nayo kupitia sanaa hii ya ucheshi.

Bi. Warda aliendelea kusema kwamba ‘Valeur Comedy Nights’ itafanyika katika jiji la Dar Es Salaam pekee kwa sasa, lakini ina mpango wa kufika pia mikoani endapo mambo yakienda vizuri katika msimu huu wa kwanza.

 Alisema washindi 5 watakaofaulu zaidi watapata nafasi ya kujiendeleza Zaidi katika kampuni ya Vuvuzela Entertainment, na mshindi wa jumla atajipatia kitita cha shilingi 2,000,000/= taslimu. 


Aliendelea kusema kwamba wataalamu wa Vuvuzela Company Ltd ndio watahusika katika kuchuja vipaji na kusimamia shindano kwa ujumla. Bi Warda alisema pia kwamba wataalika wataalamu wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ili kusimamia mchuano uwe wa haki kwa washiriki wote.

Naye Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela Bw. Evans Bukuku alisema ‘Valeur Comedy Nights’ itafanyika kwa wiki 10 jijini Dar, ambapo kwa wiki 9 watakuwa wanasaka vipaji wilaya hadi wilaya na wiki ya kumi ni ya fainali ya mkoa kupata mshindi wa jumla.

 Aliendelea kusema usajili utafanyika siku za Alhamisi ambapo washindi 5 waliofanya vizuri watachuana katika fainali za wilaya zitakazofanyika Jumamosi hiyo. Mshindi mmoja katika kila fainali ya wilaya atapata nafasi ya kuingia katika kinyang’anyiro cha fainali za mkoa ambapo mshindi wa jumla atajipatia fedha taslimu. Bw. Evans alisisitiza kwamba kampuni yake itachukua wasanii 5 waliofanya vizuri zaidi kwa ajili ya kuwalea na kuwapa mafunzo zaidi waweze kufika mbali katika fani hii.

Bw. Evans alitaja masharti ya shindano hili kuwa ni kwa walio na umri wa miaka 18 na zaidi pekee, washiriki hawatakiwi kutoa utani juu ya mambo ya dini na siasa kwani haya hugusa hisia za watu, hawaruhusiwi kulewa wakati wa shindano nk. Alitaja pia vigezo vya ushindi kwamba ni uwezo wa kuwasilisha ujumbe katika namna ya ucheshi zaidi, uwezo wa kumiliki jukwaa vizuri, uwezo wa kuwasiliana na hadhira mbele yako nk.

Naye mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) aliipongeza sana kampuni ya TDL kupitia chapa yake ya Valeur Superior Brandy kwa kujitokeza kusaidia Sanaa hii ya ucheshi hapa Tanzania.

 Aliendelea kusema katika ulimwengu wa sasa Sanaa ya ucheshi inaweza kumfanya mtu aishi maisha mazuri sana, alitoa mifano ya mmarekani Kevin Hart na Mnigeria Basketmouth ambao wanafanya vizuri sana sasa hivi katika Sanaa hii ya ucheshi.

Alisema pia kwamba Sanaa ya ucheshi ni mpya kwa Tanzania lakini inaonyesha kukua zaidi siku za usoni na kusaidia wasanii wa Tanzania. 

Aliomba makampuni mengine yajitokeze kusaidia maeneo mbalimbali ya Sanaa ili kuwafanya vijana wengi zaidi kupata ajira katika Sanaa, pia kuwapa vijana wa Tanzania shughuli za kufanya ili wasikae vijiweni kwenye madawa ya kulevya na matatizo mengi ya dunia ya sasa.

Naye Meneja wa mauzo wa kampuni ya TDL kanda ya Dar es Salaam, Bw. Mwesige Mchuruza alielezea kwamba mashindano haya yatafanyika katika baa mbalimbali jijini Dar Es Salaam. Kwa wiki hii yakuanzia usajili utafanyika siku ya Alhamisi tar 27 July katika baa ya TCC Club Chang’ombe, na Fainali za wilaya zitafanyika siku ya Jumamosi tar 01 August katika baa hiyo hiyo na ratiba nyingine ikiwa ifutavyo;
WEEK
AUDITION OUTLET
FINAL OUTLET
LOCATION
1
TCC Club
TCC Club - Chang'ombe
Chang'ombe
2
Dar West Park
K.B Paradise - Tabata
Tabata
3
Vijana Social
Katumba Bar - Mkwajuni
Kinondoni
4
Kisuma Bar
Kisuma Bar - Mbagala
Mbagala
5
UEFA Bar
Mama Land - Ukonga
Ukonga
6
Soccer City
Mawella Bar - Sinza
Sinza
7
Brazil Pub
Brazil Pub - Tegeta
Tegeta
8
Europa Bar
Junction 98 - Buguruni
Buguruni
9
Blue Fish
Liquid Bar - Kigamboni
Kigamboni

Bi Warda alimaliza kwa kuwaalika wasanii wote wa tasnia hii ya ucheshi kujitokeza kwa wingi kuja kujisajili na kushiriki shindano hili kwani yaweza kuwa mlango wao kuelekea mafanikio makubwa ya kisanii. Aliwaalika pia wananchi wapenzi wa Valeur Superior Brand kuja kuburudika na kujionea shindano hili Jumamosi katika baa ya Tcc Club Chang’ombe jijini Dar Es Salaam. Hakuna kiingilio lakini wanaoruhusiwa ni wale tu wenye umri wa miaka 18 na zaidi.

 Wadau wa Valeur Comedy Nights na Valeur Superior Brandy.
Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela, Bw. Evans Bukuku akipokea hundi ya shilingi mbili kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimar leo.
Baadhi  ya vijana wa kampuni ya  Vuvuzela wanao weza kuchekesha katika kikundi cha Comedi cha kampuni hiyo.
Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii.

DAR WATAMBA MBIO ZA MAGARI ZILIZOFANYIKA ARUSHA

$
0
0


Mwendesha magari Randeep Shingh kutoka jijini Dar es Salam ameibuka mshindi katika mashindano  ya kila mwaka ya  mbio za nyika za magari  nane-nane rally yaliyotimua vumbi katika mji wa Arusha  mwishoni mwa wiki.



Mashindano hayo yamefanykia kwa siku mbili mfululizo huku yakishuhudiwa ushindani mkali kwa madereva hao waliotoka mikoa mbalimbali na Randeep Shingh akiwa na msoma ramani guvinder singh wa gari ya mistubish lancer akiibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.



katika mashindano hayo yaliyokuwa yakitofauti mwaka huu, baada ya kufungiwa mitambo ya kisasa ya kidigitali kwa kila gari ili kuwezesha ufuatiliwaji wa kila gari na njia zitakazopitia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hakuna zengwe wala suala la madereva kuiba njia  na hata kupotea porini.



zaidi ya  madereva 20 kutoka ndani na nje ya nchi  walioshindana  zaidi ya Km 198 huku mshindi wa pili akiwa ni Raj Pal  Dhani na msoma raman Sinder Sudle  wakiwana na ghari la subaru impreza nafasi ya tatu ikiwa imeshikwa na Gurjit Singh .



huku dereva mkongwe  wa nchini tanzania Gerald Miller akiambulia nafasi  ya sita, HUKU baadhi ya madereva walioshiriki katika mashindano hayo wakisema yalikuwa magumu mwaka huu huku wengine wakizungumzia changamoto ya barabara



baadhi ya mashabiki wa mchezo waliojitokeza kwa wingi kutazama mashindano ya hayo ya  utrack nanenane rally walisema wamefurahi na kuiomba serikali kuwezesha mashindano haya kufanyika mara kwa mara

MAGIGE: TUMUUNGE MKONO DK.MAGUFULI NDIO CHAGUO LA CCM

$
0
0
SAM_4396Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza jana katika mkutano wa wagombea Ubunge 12 kupitia chama cha mapinduzi waliofanya ziara ya kujinadi kwa wananchama pamoja na wananchi kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho jana katika mtaa wa kati(CCM Mkoa),ambapo hivi karibuni Catherine aliibuka ushindi wa kishindo kwa kura 409 kati ya kura 560 huku anayemfwatia akipata kura 248 (Habari picha na Pamela Mollel)
SAM_4403Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akisalimiana na wanachama wa chama hicho jana jijini Arusha,Aliwatoa rai kwa wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi kumuunga mkono mgombea Urais Dk.John Pombe Magufuli kwani ndio chaguo la CCM,huku pia akisisitiza wanaccm kuchagua kiongozi kwanzia ngazi ya udiwani,ubunge anayekubalika ndani ya CCMna nje ya CCM.
SAM_4391Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau ambaye pia ni mratibu wa Mkoa akiteta jambo na Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha jana katika mtaa wa kati (CCM Mkoa) wakati wa ziara ya watia nia wa chama cha mapinduzi wakijitambulisha na kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama hicho katika nafasi ya Ubunge
SAM_4404Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akifurahia jambo na mwenyekiti wa wilaya ya Arusha katika ofisi za chama cha mapinduzi jijini Arusha jana wakati watia nia ubunge 12 kupitia chama hicho walipata nafasi ya kujinadi kwa wananchi na wanachama wa chama hicho
SAM_4289Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza na waandishi wa habari siku alipotangazwa kuwa mshindi

SENSA YA VIWANDA TANZANIA: SERIKALI YAONGEZA MUDA.

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kueleza uamuzi wa Serikali kuongeza muda wa Sensa ya Viwanda Tanzania Bara hadi Agosti 31,2015 na hatua zitakazochukuliwa kwa viwanda vitakavyoshindwa kutoa takwimu za uzalishaji kwenye Madodoso ya Sensa.
Kaimu Meneja wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkoa wa Dar es salaam Bw. Albert Kapala akitoa ufafanuzi wa lengo la Sensa ya Viwanda na Idadi ya viwanda vilivyotoa taarifa za Sensa hiyo jijini Dar es salaam.
NA: Veronica Kazimoto
SERIKALI imeongeza muda wa mwisho wa kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za Sensa ya viwanda kote nchini hadi Agosti 31 , 2015 kufuatia viwanda vipatavyo 366 vilivyoko jijini Dar es salaam kushindwa kuwasilisha taarifa muhimu za uzalishaji kwenye madodoso ya Sensa hiyo.

Akitoa taarifa ya kuongezwa kwa muda wa Sensa hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa Viwanda 366 ambayo ni sawa na asilimia 20 katika jijini Dar es salaam vimeshindwa kukamilisha na kurudisha madodoso ya taarifa muhimu za viwanda hivyo.


Amesema Sensa hiyo ilianza Machi 9 mwaka huu na ilitarajiwa kukamilika Juni 8, 2015 lengo likiwa kukusanya takwimu sahihi zinazohusu Sekta ya Viwanda na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Amesema Sensa hiyo pamoja na mambo mengine ililenga kupata viashiria sahihi vya uchumi pamoja na taarifa muhimu za viwanda zikiwemo orodha ya viwanda kimkoa, anuani na mahali vilipo, aina ya umiliki na utaifa wa wamiliki.

Takwimu nyingine ni mwaka ambao viwanda hivyo vilianza uzalishaji, shughuli kuu ya viwanda husika,idadi ya wafanyakazi waliopo,gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaj na gharama za uzalishaji.

Ameeleza kuwa mwaka 2013 Serikali iliamua kuwa ifanyike Sensa ya viwanda nchi nzima ili kubaini viashiria vya uchumi vitakavyosaidia kuweka mabadiliko ya muundo wa sekta ya viwanda na mchango wake katika pato la Taifa, kuboresha Sera na Programu za kukuza ajira, utekelezaji wa Malengo ya Milenia ,Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, MKUKUTA na Mpango wa Taifa wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Aidha, ameeleza kuwa jijini Dar es salaam kazi nzuri imefanyika kwa wenye viwanda kutoa ushirikiano kwa kukamilisha ujazaji wa madodoso mafupi na marefu na tayari madodoso hayo yameshawasilishwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa uchambuzi.

Mhe. Saidi Meck Sadiki amefafanua kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kuhakikisha kuwa asilimia 8 iliyobaki ya viwanda vyote nchini inawasilisha taarifa husika kabla ya muda uliopangwa.

Amesisitiza kuwa zoezi hilo liko kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya mwaka 2012 na watakaoshindwa kutekeleza ujazaji wa madodoso hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Zoezi hili ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa taifa letu linatupa picha ya sekta ya viwanda nchini pamoja na kuongeza uwazi katika mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa, hili lazima tulisimamie, wenye viwanda lazima watii sheria" Amesema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoa wa Dar es salaam Albert Kapala amesema kuwa Zoezi hilo ni la kitaifa hivyo taarifa zote zinazokusanywa ni siri na zinatumika kwa matumizi ya kitakwimu tu.

Amesema katika Sensa hiyo iliyoanza mwezi Machi mwaka huu mkoa wa Dar es salaam ulitarajia kuwa umekusanya takwimu za viwanda 1840 ifikapo Juni 8 mwaka huu.

Ameeleza kuwa hadi sasa viwanda vilivyoshindwa kuwasilisha taarifa kwa mujibu wa Sensa hiyo jijini Dar es salaam ni 366 wakati vilivyowasilisha ni 1474.

RAIS KIKWETE AFANYA ZIARA YA KISERIKALI AUSTRALIA, ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA VITA NA KUONGEA NA JUMUIA YA WATANZANIA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Fairbairn mjini Canberra katika siku ya mwanzo ya ziara yake Rasmi ya siku nne ya Kiserikali nchini Australia.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembezwa katika jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita  - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa  kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali  katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australi. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima katika kaburi la askari wa Australia wakati alipotembelea jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali  katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanzania waishio Australia alipkutana nao na kuongea nao katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa Jumamosi, Julai 25, 2015, amewasili nchini Australia na kuanza  ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne kesho, Jumatatu, Julai 27, 2015.

Rais Kikwete anafanya ziara hiyo rasmi ya Kiserikali katika Jumuia ya Madola ya Australia (The Commonwealth of Australia) kwa mwaliko wa Mheshimiwa Jenerali Sir Peter Cosgrove AK MC (Mstaafu), Gavana Jenerali wa Jumuia ya Madola ya Australia.

Wakati wa ziara yake, Rais Kikwete ambaye mara ya mwisho alitembelea Australia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Nchi za Jumuia ya Madola mjini Perth mwaka 2011, atatembelea mji mkuu wa Australia wa Canberra na miji ya Newcastle na Sydney.

Mara baada ya kuwasili mjini Canberra kesho, Rais Kikwete atapanda Mti wa Kumbukumbu katika Bustani ya Taifa ya Miti ya Australia na kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Vita ya nchi hiyo kabla ya kukutana na Watanzania wanaoishi katika Australia.

Kesho kutwa, Jumanne, Julai 28, 2015, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Waziri Mkuu wa Australia, Mheshimiwa Tony Abbot (MB) na pia kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Gavana Jenerali Sir Peter Cosgrove ambaye alipata pia kuwa Mkuu wa Majeshi ya Australia. 

Aidha, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa GaiBrodtmann (MB), Waziri Kivuli wa Ulinzi wa Australia.

Maeneo makuu ambako mazungumzo kati ya Rais Kikwete na viongozi hao wa Australia yanatarajiwa kujikita ni katika eneo la madini na uchimbaji wake, fursa za elimu ya juu na mafunzo ya ufundi, masuala yanayohusu Bahari ya Hindi (The Indian Ocean Rim) na usalama wa Bahari hiyo, ugaidi na masuala ya usalama wa nchi za Afrika Mashariki.

Rais Kikwete pia atatumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuagana na viongozi wa Australia, nchi ambayo kwa miongoni mitano iliyopita imekuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania katika maeneo ya uchumi, ulinzi, siasa, jamii na masuala ya usalama.

Jioni ya siku hiyo, Rais Kikwete atahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo itaandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake, Gavana Jenerali Sir Peter Cosgrove na baada ya dhifa hiyo, Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka mjini Canberra kwenda Sydney, mji mkuu wa kibiashara wa Australia.

Jumatano, Julai 29, 2015, Rais Kikwete atakwenda mjini Newcastle ambako atatunukiwa Digriii ya Uzamivu ya Heshima ya Sheria (Degree of Doctors of Laws Honoriscausa – honorary LLD) na Chuo Kikuu cha Newcastle. Rais atatunukiwa digrii hiyo ya heshima kwa kutambua uongozi wake uliotukuka na mchango wake katika maendeleo ya Tanzania na Afrika na jitihada zake za kuleta amani.

Chuo Kikuu cha Newcastle ni moja ya vyuo ambavyo vimekuwa vinatoa nafasi za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania, chini ya sera ya miaka mingi ya Australia kusaidia elimu katika Tanzania. 

Wanafunzi 26 wa Tanzania tayari wamemaliza masomo katika chuo hicho na kurejea nyumbani katika maeneo ya madini, elimu ya juu, vyombo vya habari, masuala ya fedha na masuala ya serikali. Wanafunzi 45 bado wanaendelea na masomo yao katika chuo hicho.

Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka Australia asubuhi ya Alhamisi, Julai 30, 2015 kurejea nyumbani.

WIZARA YA HABARI NA ESAMI WAWAPIGA MSASA MAAFISA VIJANA.

$
0
0
ES1
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akiongea na Maafisa Vijana waliohudhuria Mfunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu kutumia elimu na uzoefu watakaoupata katika mafunzo hayo kuwainua vijana kiuchumi kwa kutoa elimu itakayowajenga na kuwafanya vijana kujitegemea na kuwa wajasiriamali, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon Malisa.
ES2
Baadhi ya Maafisa Vijana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo
ES3
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa akiwaeleza jambo Maafisa Vijana, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute)leo Jijini Arusha.
ES4
Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon Malisa akiongea na Maafisa Vijana na kuwataka kushiriki kikamilifu katika mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yanayotolewa kwa ushirikiano wa Chuo hicho na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kuweza kuendeleza na kukuza ujasiriamali hasa kwa Vijana, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha.

ES5
Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon Malisa akiongea na Maafisa Vijana na kuwataka kushiriki kikamilifu katika mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yanayotolewa kwa ushirikiano wa Chuo hicho na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kuweza kuendeleza na kukuza ujasiriamali hasa kwa Vijana, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha.
ES6
Baadhi ya Maafisa Vijana  wakiwa katika mijadala wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari,
ES7
Baadhi ya Maafisa Vijana  wakiwa katika mijadala wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute)leo Jijini Arusha. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
…………………………………………………………………………
Maafisa Vijana Nchini wametakiwa kutumia elimu wanayopata katika kuwaendeleza vijana kiuchumi ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu.

Bw. Kajugusi alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwaendeleza vijana nchini Wizara kwa Kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) wameanzisha mradi unaolenga kuwawezesha vijana kijasiriamali nakiubunifu kwa kupitia mafunzo wanayowapa Maafisa Vijana.

“tunawaomba kushiriki kikamilifu katika mafunzo haya ya ujasiriamali na ubunifu kwa kuwasikiliza wawezeshaji kwa makini kwa dhumuni la kutumia elimu hiyo kuwainua vijana nchini kiuchumi na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujasiriamali”. Alisema Kajugusi.

Naye Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Bw. Leon Malisa alisema kuwa dhumuni la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Maafisa Vijana katika eneo la  ujasiriamali na ubunifu ili kuwawezesha kuitumia Elimu hiyo kwa vijana vijana nchini kwa kuwawezesha kujiajiri wenyewe.

Aidha Bw. Malisa ametaka vijana nchini kuunda vikundi na kubuni miradi itakayowaendeleza ili Wizara kwa kushirikiana na ESAMI waweze kuwasaidia kujiendeleza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na tatizo la Ajira Nchini.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Afisa Vijana toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliackim Mtawa alisema kuwa watatumia mafunzo haya kuwatayarisha vijana kuwa wajasiriamali wazuri na kuwasimamia katika utekelezaji wa Miradi hiyo ili kuwawezesha kushiriki katika uzalishaji mali na kukuza uchumi kupitia ujasiriamali
Mafuzno hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI)

MHE.EDWARD LOWASSA AKARIBISHWA RASMI KUJIUNGA NA UKAWA.,MGOMBEA URAIS KUTANGAZWA AGOSTI 4

$
0
0
 Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. 
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa UKAWA,uliofanyika mapema leo jijini Dar
  Mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri,Deodatusi Balile akitaka ufafanusi kuhusiana na umoja huo wa UKAWA kumkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar
 Mmoja wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar
 Viongozi wa UKAWA wakiandika maswali waliokuwa wakiulizwa na Wanahabari kwenye mkutano hou uliofanyika jijini Dar
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama hicho jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),ambapo mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana  kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kulia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi (hayupo pichani)
  Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
   Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe mara baada ya kuzungumza na Waaandishi wa Habari  makao makuu ya chama cha CUF,mapema leo mchana jijini Dar,ambapo kwa pamoja kama UKAWA wamemkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na umoja huo na kwamba watampa nafasi.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

UMOJA wa  katiba ya Wananchi  nchini (UKAWA) vinamkribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga katika  na umoja huo pamoja na watanzania wengine katika mapambano ya kuindoa CCM madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo,Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia amesema wanawalika watanzania wote kujiunga na UKAWA katika kuweza kuleta mabadiliko katika kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM)  katika kuweza kusimamia nchi.

Mbatia amesema kuwa wanamualika Waziri Mkuu  Mstaafu,Edward Lowassa kutokana na kuwa mchapakazi na mfuatilialiaji katika majukumu ambayo anayatoa na uwezo anao katika kusimamia.Amesema  akiingia Lowassa katika umoja huo watashirikiana kwa karibu kutokana na kutambua kuwa ni mhamasishaji  na  ni mtu mwenye kuthubutu.

Aidha amesema kuwa watamsimamisha mgombea  mmoja katika kila nafasi katika kupeperusha bendera  ya UKAWA katika uchuguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 25 mwaka  huu.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha  Wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba amesema tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowassa zinatokana na mfumo  uliopo. Amesema  wanatarajia kutaja jina la mgombea Urais Agosti Nne Mwaka  huu  na atapatikana kutokana na taraibu zilizowekwa na umoja huo.

Mbatia hakuweza kuweka wazi kuwa wanamkaribisha Lowassa kujiunga na chama kipi kutokana na ukawa sio chama kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa NLD,Dk.Emmanuel Makaidi amesema Lowassa akigombea Urais atamkubali na tuhuma zinazomkabili kiongozi zingekuwa za kweli angepelekwa mahakamani lakini bado yupo na wenye tuhuma wamefikishwa mahakamani .

Katika mkutano wa UKAWA masuali yalilenga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga huko na  tuhuma zake wakati vyama hivyo vilikuwa vikinadi juu ya kutokuwa na usafi na pamoja na uhusikaji katika tuhuma ya mchakato wa  umeme wa dharula kupitia kampuni ya Richmond.

Ibada ya kumuaga Balozi Liberata Mulamula Washington DC Julai 26, 2015

$
0
0

Jumapili yaJulai 26 2015, kanisa linaloabudu kwa kiswahili hapa Washington DC la The Way of the Cross Gospel Ministries lilifanya ibada maalum ya kuagana na aliyekuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula
Aliyekuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akiongea na washarika pamoja na wageni waliohudhuria ibada maaluma ya kumuaga.Picha kwa hisani ya Samuel Malonja





Aliyekuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akiongea na washarika pamoja na wageni waliohudhuria ibada maaluma ya kumuaga
Mch Ferdinand Shideko akimkabidhi cheti Mhe Balozi Mulamula kwa niaba ya kanisa

Mchungaji John mbatta akisoma kwa washarika na wageni maneno yaliyo kwenye cheti alichokabidhiwa Balozi Mulamula
Mwinjilisti Celina Lyimo akimkabidhi Balozi Mulamula zawadi

Washarika na wageni wakijumuika kumpongeza Mhe Balozi Mulamula baada ya kukabidhiwa zawadi na kanisa
Mchungaji Shideko akihubiri katika ibada hiyo
Wageni na washarika wakifuatilia mahubiri
Baada ya hapo, yalifanyika maombi maalum kwa ajili ya Balozi, yaliyofanywa na wachungaji wakishirikiana na waumini na wageni
Wachungaji toka makanisa mbalimbali hapa DMV wakiongoza maombi kwa Balozi Liberata Mulamula



Vijana watakiwa kujituma Airtel Rising Stars

$
0
0

Mbunge wa Ilala mheshimiwa Mussa Zungu leo amefungua mashindano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka vijana kucheza kwa kujituma ili kuwa wachezaji bora na hatimaye kulinusuru taifa na matokeo mabaya katika medani ya kimataifa.

Zungu amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuhakikiha kwamba timu zote za ligi kuu na daraja la kwanza zinakuwa na timu za vijana. “Kwa bahati nzuri, mashindano ya Airtel Rising Stars yamewapa fursa nzuri na ni vema makocha wa ligi kuu wakayatumia kupata vijana wenye vipaji na kuwaendeleza”, alisema.

Alisema mbali ya kuwa jukwaa la kubaini wachezaji wenye vipaji, Airtel Rising Stars pia yanawahamasisha vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwa na afya njema ili kukabiliana na masomo yao.

Aliwaambia vijana kwamba kwa dunia ya leo mpira ni chanzo cha kutumainiwa cha ajira kwa mamilioni ya vijana ambao wanaishi maisha mazuri kwa kuwa wanalipwa mishahara mizuri.

Aliwataka viongoizi wa soka kuchagua wachezaji watakaoshiriki fainali za taifa kwa kuzingatia uwezo na siyo upendeleo wa aina yoyote. Wakati mashindano ya mkoa yakiendelea makocha watateua vijana wenye vipaji kuwakilisha mikoa yao kwenye fainali ya taifa.

Kwa upande wake Rais wa TFF Jamal Malinzi ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kubuni programu hii ili kutumika kama jukwaa linatotumika kubaini vipaji vya wanasoka chipukizi. Alisema kuwa mashindano ya Airtel Rising stars yameifanya kazi ya TFF ya kutafuta vipaji vya soka kuwa rahisi zaidi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa IT wa Airtel Tanzania Franky Filman amewashukuru wadau wote wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili. Pia amewataka makocha kutumia mashindano hayo kuimarisha vikosi vyao.

Mashindano ya Airtel Rising yanajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke, Ilala Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha itahitimishwa kwa michuano ya taifa itakayofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21.

Mbunge wa Ilala Musa Zungu akisalimiana na wachezaji wakati akifungua rasmi mashindano ya Airtel Rising Stars. Leo Jijini Dar-es-Salaam.
Mbunge wa Ilala Musa Zungu akiongea na wachezaji wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya, Leo jijini Dar-es-Saam.
Mbunge wa Ilala Musa Zungu akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya, Leo jijini Dar-es-Saam.
Mkurugenzi wa IT wa Airtel Frank Filman akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya, Leo jijini Dar-es-Saam.

Vyama vya Siasa 21 vimesaini Maadili ya uchaguzi mkuu Tanzania

$
0
0
Vyama vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo.

Maadili hayo yanayohusisha Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema Chama cha Wananchi (CUF) hakikusaini Maadili hayo kutokana na kuwa na kazi nyingine lakini akasisitiza kuwa Chama hicho kitasaini Maadili hayo wakati wowote.

Akifafanua kuhusu Maadili hayo, Jaji Lubuva alisema Maadili yanapaswa kuanza kutumika rasmi Agosti 22 mwaka huu wakati kampeni za uchaguzi zitakapoanza, katika kipindi cha kupiga kura na wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo. 

Alisema Maadili hayo pia yatahusu wajibu wa vyama vya siasa na wagombea na mambo yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa na wagombea. 

Maadili pia yatahusu masuala yanayotakiwa kufanywa na yasiyotakiwa kufanywa wakati wa kupiga kura.Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa maadili yaliyosainiwa pia yatahusu maadili kwa Tume ya Uchaguzi yaani mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na Tume hiyo. 

Aidha, maadili hayo yatahusu mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa serikali katika kipindi chote cha uchaguzi. 

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAZINDUA MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Akitoa Mada kwenye Mradi wake aliouanzisha kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye  Ujasiriamali.Mafunzo hayo yalianza jana Chini ya Taasisi ya  Manjano Foundation.Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.
Washiriki wa Mafunzo ya Usajiriliamali yalio chini ya Manjano Foundation wakisiliza kwa Makini Mada Mbalimbali kihusu Mafunzo hayo ya kuwajengea wanawake wa Kitanzania  uwezo wa Kudhubutu Kufanya biashara ,Kujisimamia na Kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara Hususani Kupitia Bidhaa za Vipodozi vya Luv Touch Manjano.
Washiriki wa Wafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini
Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii  limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.
Mradi huu Uzinduliwa Na Mama  Tunu Pinda Ambapo  Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuzindua Mradi utakaomkomboa Mwanamke wa Kitanzania Kuondokana na Umaskini kwa Kudhubutu Kujikita kwenye Biashara hasa kwenye Bidhaa za Vipodozi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser  Akiwaeleza jambo washiriki wa Mafunzo hayo..

MAGAZETI, MAJARIDA NA VITABU VYOTE KWENYE SIMU YAKO YA MKONONI.

$
0
0

Je umekwishawahi kukwama kwenye foleni ukajutia kutobeba gazeti walau likusaidie kusogeza muda mbele? Je umekwisha wahi kutafuta chanzo cha habari za uhakika kwenye simu yako ukakikosa?

Je umekwishawahi kuambiwa kuna tangazo la kazi au tenda ila ukashindwa kuliona kwa vile lipo kwenye gazeti la siku za nyuma?
Je umeshawahi kulazimika kuchoma au kutupa magazeti ya siku za nyuma kwa sababu yamejaa sana nyumbani kwako? Au je umeshawahi kuhisi kuna umuhimu wa kuona watoto wako wanachojifunza shuleni?

Je umekwishaona maktaba inayokupa magazeti, majarida au vitabu vyote toka tulipopata uhuru, mahali popote wakati wowote ulipo?

Kama jibu la swali lolote kati ya hayo ni ndio, basi M-Paper inaweza kukupa hayo yote.

Kabla hatujaendelea, tazam video hii ya sekunde thelathini tu  https://www.youtube.com/watch?v=x00FXMqY-jg

M-Paper ni programu ya simu za mkononi, inayokuletea magazeti, majarida na vitabu vyote kwenye simu yako ya mkononi.  Programu hii ya kipekee itakufanya usome gazeti, jarida au kitabu chote kama kilivyo kwenye makaratasi na si vichwa vya habari pekee.

Kama hiyo haitoshi, watengenezeji wa programu hii watakupa shilingi 10,000 pale utakapodownload app hii ambayo utaitumia kununua magazeti, vitabu na majarida kabla hujaanza kutumia pesa zako.

Oh, jambo jingine la kipekee kuhusu program hii ni kuwa, magazeti, majarida na vitabu vyote vinauzwa kwa nusu bei. Faida mara mbili.

Unaweza kudownload app hii hapa http://www.mpaper.co.tzkisha ukaniandikia maoni yako hapa chini, umeionaje? Kumbuka unadownload BURE, unawekewa 10,000 kwenye akaunti yako hivyo huna cha kupoteza.

WAJASILIAMALI 150 WAPATIWA MAFUNZO MOSHI

$
0
0
Baadhi ya Wawezeshaji katika mafunzo yaWajasiliamali 150 yanayofanyika katika chuo cha Ufundi Veta mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki na Kusinin(ESAURP) Prof,Ted Maliyamkono akzungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajasiliamali  wadogo wa mkoa wa Kilimanjaro yanayofanyika katika chuo cha VETA Moshi.
Badhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano.
Mjumbe wa  Bodi ya Taasisi ya fedha ya FSDT ,Erick Masinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajasiliamali hao.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Lembris Kipuyo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha kurasimisha biashara zo ili wapate mkopo na kukuza Biashara.
Prof Maliyamkono akitoa neno la Shukrani.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo,wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo.
DC Kipuyo akizungumza na wanahabari mara baada ya kufungua mafunzo hayo.
DC Kipuyo akifanya mahojiano na mmoja wa wanahabari .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KAMPUNI YA BUSINESS CONNEXION YAHAMASISHA KUHUSU FURSA ZILIZOPO

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Business Connexion,Seronga Wangwe akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi mkuu mtendajiwa Kampuni ya Business Connexion, Issac Mophallene akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion,Jane Canny akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
 Mwandishi wa habari wa gazeti la The African, Jastine Amani akiuliza swali kuhusiana na utendaji kazi wa mitandao ya simu hapa nchini katika
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Gurdian, Frenk Amani.
 
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Business Connexion, Seronga Wangwe, Afisa Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion,Jane Canny na Mkurugenzi mkuu mtendajiwa Kampuni ya Business Connexion, Issac Mophallene wakijibu maswali kwa awamu katika
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wadau wa mitandao ya simu waliohudhuria katika
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
MUDA UMEFIKA WA KUPANUA BIASHARA TANZANIA
TANZANIA ina fursa nyingi ambazo bado hazijatumika. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi unategemewa kukua kwa wastani wa asilimia7.2 mwaka huu na uwekezaji wa serikali kwa kiasi kikubwa katika mkongo wa taifa unaongeza biashara na upatikanaji wa teknolojia kwa raia ili kujenga fursa za kusonga mbele kwenye teknolojia zetu. Pamoja na kuibuka kwa teknolojia nyingi zisizokuwa na mpangilio, hatua hii imewekwa kwa ajili ya kuongezeka kwa fursa nyingi. Haya ni maoni ya Jane Canny, Afisa Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion.
Kampuni ya business Connexion Tanzania imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 2000, lengo lake kubwa hasa ni kujikita katika huduma za kifedha, mawasiliano ya simu, nishati na madini na sekta ya umma. Kupitia matumizi bunifu ya teknolojia na ushirikiano wetu na UmojaSwitch Consortium, Tunatoa huduma ya upatikanaji wa miundombinu ya malipo iliyo salama katika benki 28 na mashine za ATM 200 nchini Tanzania. Miundombinu hii imeunganishwa na swichi tano za malipo ndani ya Afrika Mashariki ili kuruhusu miamala ya kimataifa, makampuni makubwa matatu ya mitandao ya simu ili kuwezesha malipo ya simu na taasisi mbalimbali za serikali katika kuwezesha makusanyo ya malipo ya kielektroniki.
Muunganiko wa vitu hivi vinavyotengeneza mtandao unabadili namna ya uendeshaji wa biashara kwa kasi kubwa," anasema Canny. "Kama wateja watakuwa wameunganishwa zaidi, mahitaji yao yanabadilika na mashirika kwani yanapaswa kubadilika kama teknolojia na namna tunavyoitumia inabadilika, au wanakutana na kile kilichoachwa nyuma na washindani wao.

Anaongeza kuwa, pia kuna miradi kadhaa inayoendelea ya kuunganisha Manispaa na hospitali nchini kote ili kuwezesha makusanyo ya malipo ya kielektroniki. ”Huu ni mfano mkubwa ambapo teknolojia imekuwa ikitumiwa kufanya maisha ya watumiaji yawe rahisi zaidi," anasema Canny. 

"Na kama teknolojia inaendelea kukua, ndivyo jinsi ambavyo wateja wataingiliana na watoa huduma wao. Kwa mfano,Katika miaka mitano ijayo kitengo cha mawasiliano cha karibu au kitengo cha teknolojia cha mawasiliano kilicho karibu kitatumika nchini kote ili kuwezesha malipo ya rejareja kupitia simu ya mkononi. Pia tunatengeneza kiunga muhimu cha kwenye simu kinachohusiana na benki katika intaneti, ambacho kitakuwa kinaratibiwa katika kituo chetu cha data hapa nchini.

Canny anasema muungano uliopendekezwa na Telkom hautarajiwi kuwa na athari yoyote juu ya uendeshaji nchini na kampuni bado linabaki likijikita katika soko la Tanzania. Bila kujali matokeo ya muungano uliopendekezwa, ni biashara kama kawaida kwetu. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kutoa suluhisho zenye ubunifu kwa wateja wetu. Tutaendelea kuwekeza katika miundombinu ya huduma za ubadilishaji wa kifedha ili kulinda nafasi yetu katika soko la huduma za kifedha, "anasema. "Kituo chetu cha data nchini,ambacho kinaratibu moja ya suluhisho kubwa za makampuni ya mawasiliano ya simu, na huduma za kufufua data pia zinaendelea kukua.
Canny anaamini muungano huu uliopendekezwa unaenda sambamba na mwenendo wa kimataifa ambapo kampuni za  mawasiliano ya simu na huduma za TEHAMA zinaungana. Inatuwezesha kuinua miundombinu ya mawasiliano ya Telkom na kutoa ufumbuzi kwa wateja wetu unaokuwa na mwisho. Wakati Telkom haijaanza uendeshaji wake nchini Tanzania, kwa sasa unasehemu kidogo nchini. Hii ni pamoja na mkakati wao wa ushirikiano wa kuunganisha na uwekezaji wa miundombinu ya mawasiliano chini ya bahari kote Afrika, bila shaka kutafaidisha wateja wetu, "anahitimisha.

Kuhusu Kampuni ya Business Connexion
Business Connexion ni moja ya kampuni kubwa inayotoa huduma za TEHAMA iliyo kwenye orodha ya soko la hisa la
Johannesburg (JSE) kuwepo huku kwenye  soko la hisa la JSE kulitokana na suala la mauzo, mali chini ya ushirikiano wa wasimamizi na wafanyakazi.Kampuni linabaki kuwa ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza nchini Afrika Kusini katika utoaji wa huduma za rasiliamali kupitia intaneti, likiwa na ofisi nchini Afrika Kusini, Namibia, Nigeria, Msumbiji, Tanzania, Zambia, Kenya, Botswana, Uingereza na Dubai. Kampuni imeajiri zaidi ya watu  6 800 katika bara la Afrika na inazalisha mapato ya ziada ya randi bilioni 6 kwa mwaka.

MTANZANIA ASHINDA MEDALI MBILI ZA DHAHABU SWAZILAND.

$
0
0
 Bingwa wa mita 1500, Basil John kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akimaliza mbio katika uwanja wa Mavuso mjini Mbabane Swaziland ambapo alifanikiwa kuchukua nafasi ya  katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Bingwa wa mita 1500, Basil John kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akipongezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Swaziland baada ya kumvalisha medali ya dhahabu katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)

Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland.
Mwanariadha wa Polisi Tanzania, Basil John amefanikiwa kupata medali mbili za dhahabu baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 1500 na mita 800 katika Michezo ya tisa ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) inayoendelea katika mji wa Mbabane Swaziland.

Mwanariadha huyo aliweza kuwashinda wanariadha wenzake baada ya kutumia dakika 1:49:00 katika mbio za mita 800 na katika mbio za mita 1500 aliweza kutumia dakika 3:49:02 na kuwaacha kwa mbali wanariadha kutoka nchi ya Zimbabwe na Swaziland ambao walionyesha ushindani mkubwa.

Mwanariadha mwingine kutoka Tanzania aliyeweza kupata medali ya dhahabu ni Fabian Nelson katika mbio za mita 5000, ambapo aliweza kutumia dakika 14:27:33 na hivyo kuifanya bendera ya Tanzania kupepea vyema katika michezo hiyo.

Ushindani mkubwa katika riadha upo kati ya Zimbabwe, Tanzania, Namibia na Swaziland ambapo nchi ya Swaziland imekuwa ikifanya vizuri katika mbio fupi.

Katika Michezo ya Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Wanariadha kumi na mbili ambapo mpaka sasa tayari wameshafanikiwa kuchukua medali 4 za dhahabu, mbili za fedha na moja ya shaba.

CUF CHATAKA WANANCHI KONDOA KUBADILIKA

$
0
0

CHAMA cha Wananchi (CUF) wilaya ya Kondoa kimewataka wananchi wa Wilaya hiyo kufanya mageuzi ya uongozi kwa kuchagua wagombea wa vyama vya upinzani ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuleta maendeleo.

Hayo yalisemwa na Katibu wa CUF wilaya ya Kondoa, Jafari Ganga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF Dar es Salaam jana.
Alisema kwa miaka mingi wilaya ya Kondoa imekuwa ikitawaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)katikangazi mbalimbaliza viongozi wa juu wakiwemo wabunge ambao kila mara wanatoka chama tawala.
Ganga alisema kuendelea kudidimia kwa uchumi wa wilaya hiyo kutokana na uongozi ambao hausimamii ipasavyo maendeleo ya uchumi, hivyo baada ya kuona hivyo CUF ilianza kuonesha njia kwa kusimamia mambo mbalimbali ya kiuchumi yaliyofanya chama kukubalika.
Alisema mpaka sasa katika kata zote 29 za wilaya ya Kondoa zimesimika matawi ya chama hicho na wanatarajia kutwaa viti vya madiwani na Ubunge katika majimbo mawili ya Kondoa Vijijini na Kondoa.
"CUF imeamka inayo matawi 160 katika katika Kata zote 29 za wilaya ya Kondoa, tumejiandaa kutwaa viti vya madiwani na wabunge" alisema Bw. Ganga.
Alizitaja Kata hizo kuwa ni Kondoa mjini, Chemchem, Kilimani, Kingale, Kolo, Bolisa, Serya, Suruke, Hondomairo, Changaa, Thawi, Sowera, Kikilo,Salanka, Bereko, Kisese,Kikore, Itololo,Masange, Mnenia, Itaswi, Bumbuta, Pahi, Kinyasi,Keikei, Busi, Haubi, Kwa Delo, na Kalamba.
Wilaya ya Kondoa umegawanywa na kuwa majimbo mawili ya Kondoa na Kondoa Vijijini pia kuna Jimbo la Chemba ambalo Mbunge wake aliyemaliza muda wake ni Juma Nkamia.

REA KUHUSISHA SEKTA BINAFSI PAMOJA NA BENKI NCHINI ILI KUONGEZA KASI YA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Benedict John-MAELEZO-Dar es salaam
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeadhimia kuhusisha Sekta binafsi pamoja na benki nchini ili kuongeza kasi ya usambazaji umeme Vijijini.

Hatua hiyo itasaidia kuleta maendeleo ya haraka na kufikisha umeme katika maeneo ya vijijini katika maeneo mengi hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika kikao kilichohusisha Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini.

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini , kasi ya upelekaji umeme vijijini hapa nchini imeogezeka. 

“Baada ya hiki chombo kuingia kazini kasi imeongezeka kwani kwa sasa wananchi waliofungiwa umeme ni zaidi ya asilimia 24 na wakati ule namba ya uwepo wa umeme vijijini ilikuwa asilimia 10 mwaka 2005 ambapo kwa sasa ni karibu asilimia 40 na tunatarajia kuongeza kasi hii kadri tunavyozidi kupata vyanzo vingi vya fedha kwani malengo yetu hapo baadaye ni kuweza kufikia asilimia zaidi ya 70”, alisema Mhandisi Mwihava.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Dkt. Lutengano Mwakahesya ameeleza kuwa kikao hicho kinalenga  kufafanua namna gani sekta binafsi zinavyoweza kupata faida kwa kuingia katika sekta ya nishati pamoja na kushirikia katika kuleta maendeleo ya haraka katika kufikisha umeme kwa asilimia 60 na zaidi.

Amesema kuwa endapo umeme nchini utaenea katika maeneo ya vijijini utaweza kuleta maendeleo makubwa hususani katika kuleta ajira kwa vijana na kuibua miradi mbalimbali kupitia viwanda vidogo vidogo jambo ambalo litapunguza tabia ya baadhi ya watu kukimbilia mijini katika kusaka ajira.

“Maendeleo makubwa yatapatikana iwapo umeme huu utafika vijijini, utasaidia kuleta viwanda vido vidogo kama vile mashine za kukoboa ili ipatikane ajira vijijini na watu waache kuhamia mjini nkutafuta maisha bora kwanbi umeme huu utasaidia wawananchi kuibua miradi mizuri ya maendeleo”. Alisema Mwakahesya.

Ameongeza kuwa, watu wengi hawawezi kulipa shilingi 27,000 hivyo Bodi hiyo inatazamia kuongea na benki za zilizopo nchini pamoja na sekta binafsi ili kuweza kupata njia bora zaidi za kufikisha umeme katika maeneo hayo ya vijijini kwa kuwapa mkopo ambao unaweza kulipwa pole pole kwa kutumia kulipia bili za umeme.

Serikali ilikamilisha mchakato wa uanzishwaji wa Taasisi ya Wakala wa Nishati Vijijini mnamo mwaka 2005 ambapo mwaka 2007 hadi hivi sasa baada ya Wakala kuingia kazini, kasi ya upelekaji ya umeme vijijini imekuwa kubwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini .
Baadhi ya wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakifuatilia ajenda wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini .
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

WAKATI UMEFIKA KWA SEKTA BINAFSI KUJENGA UTAMADUNI WA KUTOA RUZUKU ZA TAFI- DR.SHEIN

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifungua rasmi Jengo Jipya la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania { COSTECH} Ofisi ya Zanzibar liliopo ndani ya majengo ya zamani ya ilichokuwa kiwanda cha Sigara Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif wa pili kutoka Kushoto akipata maelezo kutoka kwa Wataalamu  wa Chuo cha Utafiti Kizimbani  wakiongozwa na Said Suleiman Bakari jinsi zao la viazi vitamu linavyoweza kutumiwa vyema katika utengenezaji wa Juisi.Wa kwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Majini Magharibi Mh. Abullah Mwinyi.
Watafiti na wawakilishi wa Vikundi vya wajasiri amali waliopata ufadhili kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia wakimpatia maelezo Balozi Seif wakati akiangalia maonyesha mara baada ya kulifungua Jengo la Tume hiyo.
Baadhi ya Wataalamu na wajasiri amali kutoka vikundi tofauti Nchini wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo Jipya la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia { COSTECH }.
 
Balozi Seif akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia hpo Maruhubi akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziI Dr. Ali Mohammed Shein.
 Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania { COSTECH } mara baada ya uzinduzi wa jengo la Tume hiyo hapo Maruhubi.
                                               
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema wakati umefika kwa sekta binafsi kujenga Utamaduni wa kutoa ruzuku za tafiti kwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ili ijipatie nguvu za ziada za uwezeshaji wa kuendesha shughuli zake za utafiti kama nchi nyengine Duniani zilizofanikiwa kwa kufuata mfumo huo.

Alisema kufanya utafiti kunahitaji nguvu kubwa ya fedha kiasi kwamba Serikali pekee haiwezi kumudu kugharamia bila ya kushirikisha taasisi mbali mbali za sekta binafsi za ndani na nje ya nchi.

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati wa ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia { COSTECH } liliopo Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania imeonyesha mwanga wa kusaidia jamii kwenye tafiti za kina za Kimaendeleo zitakazomkomboa Mtanzania kutoka katika dimbwi la umaskini na kuelekea kwenye maendeleo ya kweli. 

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH  Dr. Hassan Mshimba alisema ujenzi wa Ofisi ya Tume hiyo hapa Zanzibar  ni kutekekeza ahadi iliyotoa Uongozi wa Taasisi hiyo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka 2012.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa Costech alisisitiza kwamba katika azma ya kukuza ajira Nchini Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imekusudia kuungana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha vitengo vya Utafiti Zanzibar kama alivyosisitiza Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein siku ya Utafiti Tarehe 12 Disemba mwaka 2014.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Kanal Mstaafu Joseph Simba Kalia ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa ukarimu wake wa kutoa Jengo kwa ajili ya Ofisi za Tume hiyo.

Kanal Mstaafu Simba Kalia alisema kitendo hicho kilichofanywa na  SMZ ni uthibitisho wa kuthamini umuhimu wa fani ya Utafiti ambayo ndio chachu ya maendeleo ya jambo lolote lile hapa Ulimwenguni.

Ofisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojiaawali  ilizinduliwa  rasmi mnamo Tarehe 11 Juni Mwaka 2012 katika Majengo ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyopo Tunguu Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kuanza kutoa huduma zake hapa Zanzibar.

TABATA SHULE YA MSINGI YANUFAIKA NA MSAADA WA MADAWATI 100 TOKA BENKI YA KCB TANZANIA

$
0
0
 .Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta akikabidhiwa msaada wa madawati 100 na Meneja Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City, Benjamin Mgonja(kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.Benki hiyo imetoa msaada wa matawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Tabata.Wakati wa hafla ya  kukabidhiwa msaada wa madawati 100 na Benki hiyo jana.
 Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Tabata wakibeba madawati kuyapeleka madarasani baada ya kukabidhiwa msaada  wa madawati 100 na benki ya KCB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mradi wa madawati 1000 kwa shule za msingi 10 za msingi jijini Dar es Salaam.

  Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta(kushoto)akiteta jambo na Meneja Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Benjamin Mgonja wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya  msaada wa madawati 100  kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa  msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
.Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Tabata jijini Dar es Salaam, wakionyesha mshikamano na furaha baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Benki ya KCB Tanzania wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jana.

LOWASSA AJIUNGA RASMI NA UKAWA,AKABIDHIWA KADI RASMI YA UANACHAMA CHADEMA.

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
 Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
 Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
 Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA  katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images