Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 583 | 584 | (Page 585) | 586 | 587 | .... | 1897 | newer

  0 0


  MWIMBAJI wa Kimataifa anayeishi, Kenya Faustine Munishi anatarajia kumsindikiza mwenzake Bonny Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu tatu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
   
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, Munishi ataungana na Mwaitege, uzinduzi utakaofanyika Agosti 2 mwaka huu.Msamaalisema Munishi ni mojawapo  ya watakaomsindikiza mwimbaji huyo kwa sababu hivi sasa sambamba na Kilahiro na Kwaya ya Wakorintho wapili.
   
  “Uzinduzi  wa  albamu tatu za Bonny Mwaitege unatakiwa kufanyika kwa maandalizi ya hali ya juu ambayo yanafanyika kwa mfumo  wa kisasa,” alisema Msama na kuongeza.
   
  “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.
   
  Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo.Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo.Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.
   

  0 0

   Waziri wa Nchi Afisi ya Raisi Kazi na Utumishi wa Umma Harouna Ali Suleiman akiwahutubia Vijana aliohudhuria katika Uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Vijana Zanzibar.
   Baadhi ya Vijana waliohudhuria katika ufunguzi wa kituo cha taarifa za soko la Ajira Zanzibar huko Wizara ya Uwezeshaji Utawi wa Jamii Wanawake na Watoto iliyopo Mwanakwerekwe.
   Meneja wa Mradi wa Mfumo wa taarifa za  Soko la Ajira Zanzibar Ibrahim Mtongole akitoa maelezo akitoa maelezo kwa watu waliohudhuria katika uzinduzi wa mfumo wa taarifa za soko la ajira Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Ajira Ameir Ali Ameir akimfahamisha Waziri na Viongozi wengine mbali mbali jinsi ya mfumo wa taarifa za Soko la Ajira utakavyofanya kazi.(PICHA ZOTE NA MIZA OTHMAN- MAELEZO ZANZIBAR).

  0 0

   Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sera ,Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mathias Kabunduguru, Prof. Samuel Wangwe, Katibu Mtendaji -Tume ya Mipango Dkt. Phillip Mpango na wajumbe wengine wakifuatilia mada katika mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wanachama wa Jumuiya ya Madola barani Afrika.
   Katibu Mkuu Kiongozi wa Uganda Bw. John Mitala akiwasilisha mada katika mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaoendelea jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue na wajumbe wengine wakifuatilia mada zinazowasilishwa katika mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wanachama wa Jumuiya ya Madola barani Afrika jijini Dar es Salaam.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Kuwe Bakari na wajumbe wengine wakifuatilia mada katika mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wanachama wa Jumuiya ya Madola barani Afrika.

   Sekretariet inayohudumia mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa nchi za Afrika wanachama wa Jumuiya ya Madola.


  0 0  5
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshio la Polisi IGP Ernest Mangu wakati akiondoka leo Julai 14, 2015 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa    kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi. PICHA ZOTE NA IKULU
  4
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe Said Meck Sadick wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa   kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi. 
  1
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na makada wa CCM wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi. Makada hao walikuwa uwanjani hapo kwa mapokezi ya mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Maguful.
  23

  0 0

   Mratibu wa Burudani wa Club mpya ya 'Maisha Basement' zamani New Club Maisha, Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu uzinduzi wa Club hiyo utakaofanyika Idd Mosi katika Jengo la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la Kijitonyama ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Kulia ni Meneja Mkuu wa Club hiyo, Allan Ngugi na Meneja Uendeshaji wa Sam Kaliuki.
    Mratibu wa Burudani wa Club mpya ya 'Maisha Basement' zamani New Club Maisha, Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Matukio, Robert Salehe na Kulia ni Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla.
   Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla, akiwaonesha wanahabari ukumbi huo.
   Meneja Mkuu wa Club hiyo, Allan Ngugi (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo,Jean Claud Ciza wakati wa utambulisho wa uzinduzi huo kwa wanahabari.
   Mtaalamu wa mitambo katika Clab hiyo, Mr Dong 
  akifanya vitu vyake.
   Ukumbi huo unavyonekana kwa ndani.
  Dotto Mwaibale

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Club mpya ya 'Maisha Basement'. iliyopo katika Jengo la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam

  Hafla ya uzinduzi wa club hiyo zamani ikujulikana kama 'New maisha Club' utafanyika siku ya Idd Mosi katika ukumbi huo ambapo watu mbalimbali wamealikwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Mratibu wa Burudani wa Club hiyo, Hemed Kavu, alisema uzinduzi utafanyika kwa siku tatu tofauti ambazo ni leo, kesho na kilele ni siku siku hiyo ya Idd Mosi.

  Alisema club hiyo mpya ambayo ni ya kisasa inauwezo wa kuchukua watu zaidi 700 kwa wakati mmoja na imejengwa katika kiwango cha kimataifa.

  "Katika Siku hizi zote za uzinduzi kutakuwa na burudani mbalimbali...club yetu ina vifaa vya kisasa na dance floor ya kisasa yenye uwezo wa kurusha matukio moja kwa moja kama video na mechi na ina maegesho ya magari hivyo kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa mali za wateja" alisema.

  Alisema hivi sasa wamekuja tofauti na walivyokuwa maisha club Masaki, kwani burudani zao zilikuwa zinaanza Jumatano mpaka Jumapili, lakini sasa zitaanza Jumatatu mpaka Jumatatu huku kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa siku zote.

  Akitaja ratiba zao, alisema siku ya Jumatatu watakuwa na 'Blue Monday nite' kwa ajili ya wale wanaofanya kaz mwishoni mwa wiki, Jumanne 'Meet and Greet nite' huu ni usiku wa mashabiki kukutana na mastaa mbalimbali na Jumatano ni usiku wa Figisu figisu ambapo kutakuwa na burudani zote za Kiswahili.

  "Alhamisi ni usiku wa ukae ambao tutakuwa tunapata burudani za bendi zetu za hapa nyumbani, Ijumaa 'Winngle Nite' usiku wa kupata ngoma za kisasa, RNB na East Africa Music, Jumamosi 'Ibiza Nite' kutakuwa na muziki wa kihindi na kiarabu, na Jumapili 'Bongo Swagg' ni usiku wa live performance kwa wanamuziki wetu," alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEC), Beng’ Issa, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Benjki ya Posta, Sabasaba Moshingi, (wapilia kulia), Rais wa VICOBA Endelevu Tanzania, Devota Likokola, (wapili kushoto), Mwanasheria wa Benki ya Posta Tanzania, Mystica Mapunda Ngongi, (wakwanza kulia), wakiwa wameshikana mikono baada ya benki hiyo kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya baraza na benki hiyo, katika kuwawezwesha wana VICOBA kiuchumi. Hafla hiyo ilifanyika leo Julai 14, 2015. kwenye ukumbi wa wizara ya fedha jijin I Dar es Salaam.

   BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NDC), na Benki ya Posta Tanzania, (TPB), wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuwawezesha wanachama wa VCOBA nchini.

  Akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano nhayo kwenye ukumbi wa wizara ya fedha jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2015, Katib u Mtendaji wa baraza hilo, Beng’ Issa, alisema, Katika juhudi za kuwawezesha watanzania kiuchumi kupitia upatikanaji wa mitaji na kuendeleza ujasirimali nchini, Serikali kupitia Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004, ibara ya IV, sehemu ya 16  iliagiza  uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji Mwanachi yaani ‘’Mwananchi Empowerment Fund,”.

  “Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mitaji yenye gharama nafuu kwa wajasiriamali nchini, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limesaini hati za makubaliano na Benki ya Posta Tanzania katika kusimamia udhamini wa mikopo  yenye masharti nafuu kwa makundi  mbali mbali  ya wajasiriamali nchini yanayokidhi masharti husika.” Alisema Beng’i.

  Mfuko huu utakao simamiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi katika makundi au mtu mmoja mmoja kupata mitaji ya kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi kupitia mikopo ya moja kwa moja au udhamini (direct lending   or guarantee system).

  Ili kutimiza azama hiyo baraza limeamua kushirikiana na benki ya ;posta Tanzania ambayo ina mtandao mpana, kutekeleza azma hiyo ambapo wananchama wa VICOBA, watapata mikopo na mafunzo kutoka benki ya posata.

  Kwa aupande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, alisema, benki yake  ni benki ya wananchi na hivyo unayo furaha kubwa kushirikiana na NE, ili kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kupata mikopo itakayowazsaidia kuendesha shughuli zao za kiuchumi.

  “Benki ya Posta inayo furaha kubwa kushirikiana na Baraza hili ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za kifedha kwa gharama nafuu kupitia mpango huu.” Alifafanua Moshingi.

  Alisema, Benki ya Posta inaamini kuwa hii ni fursa muhimu kwa vikundi hivi visivyo rasmi  kufungua akaunti na kuweka fedha zao mahala salama. Hili litawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi, na hatimaye wataweza kupatiwa mikopo nafuu kwa ajili ya kukuza biashara zao. Hadi sasa Benki imefungua zaidi ya akaunti 340 za vikundi. Vikundi hivi vitafaidika pia na huduma ya TPB POPOTE, itakayo wawezesha kupata huduma za kifedha popote pale walipo.
   Katibu Mtendaji wa NDC, Beng'i Issa

   Mkurugenzi Mtendajin wa TPB. Sabasaba Moshingi
   Moshingi, (kulia), Beng'i(katikati) na Lokokola, wakibadilishana mawazo mwishoni mwa hafla hiyo

   Devota akishukuru Mungu, baada ya kufikiwa makubaliano hayo ambapo wanachama wake ni wafaidika wakubwa
   Picha ya pamoja, Viongozi wa TPB, NDC, na Vicoba endelevu, wakiwa katika picha ya pamoja na waliohudhuria hafla hiyo  0 0

   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala kwenye mkutano wake wa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo aliahidi kuwatumikia wananchi na kutenda haki.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kujitambulisha na kuwasalimia wakazi wa Dar es Salaam.


  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwatambulisha viongozi mbali mbali waliomsindikiza mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya mikutano vya Mbagala Zakheem.

   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za tumba pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye kwenye jukwaa la bendi ya TOT mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuhutubia  wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
  Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.

   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.

   Mgombea Mwenza wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtemvu kwenye mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Mhe. john Pombe Magufuli
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
   Ndugu, Jamaa na wafanyakazi wenzake Dk. John Pombe Magufuli wakisikiliza kwa makini hotuba kwenye mkutano huo.
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam akimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji hilo.
   Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
   Wakazi wa Mbagala wakiwa wamejipanga barabarani kumuona mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli .
   Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwasili kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala akiwa kwenye usafiri wa Boda boda.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.

   Dk. John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Idd Azzan wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Zakheem Mbagala.
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Dar es Salaam.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   
  Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari  hivi punde juu kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum jijini Dar es Salaam,Makene amesema majadiliano hayo sio urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Makene amezidi kuwataka waandishi wawe na subira kusubiri maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo. 
  Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana,Waandishi wa Habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam,wakajikuta wanaacha stendi za Camera zao na kukaa pembeni kama zionekanavyo pichani usiku huu,wakisubiri lolote litakalojiri.
  Waandishi wa Habari wakiwa wameweka kambi tangu saa saba mchana wakisubiri kupata jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam, hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa leo ndio siku rasmi ya kutangaza jina hilo lakini masaa yanazidi kwenda huku kikao chao kikiwa kinaendelea.
  Waandishi wakisubiri mtu wa kutoa taarifa juu ya jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, ambapo taarifa hizo za kuja mtu huyo ziligonga mwamba na kuambiwa kilichobaki ni makubaliano suala jinsi kuendesha uchaguzi katika majimbo.
  Waandishi wakijadiliana masuala yanayohusu tasinia ya habari baada muda mrefu kuletewa jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum ,Masaki jijini Dar es Salaam.

  Waandishi wakiwa katika viyunga vya hoteli ya Colesseum wakisubiri jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA
  Waandishi wakiwa wamechoka na ucovu wa kusubiri jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colesseum leo jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umesema kuwa mgombea wao wa Urais watamtoa baada ya siku saba.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari usiku huu,Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi,Mh.James Mbatia amesema kuwa kuchukua muda mrefu kwa kikao hicho imetokana na kuandaa utaratibu jinsi ya kumtoa mwali wao  wa Urais kwa tiketi ya UKAWA aliye bora.Amesema kuwa mkutano huo pia umechukua muda mrefu  kutokana na mambo mengi ikiwemo mgawanyo wa majimbo.
  Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari  hivi punde juu kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum jijini Dar es Salaam,Makene amesema majadiliano hayo sio urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Makene amezidi kuwataka waandishi wawe na subira kusubiri maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo. 
  Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana,Waandishi wa Habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam,wakajikuta wanaacha stendi za Camera zao na kukaa pembeni kama zionekanavyo pichani usiku huu,wakisubiri lolote litakalojiri.
  Waandishi wa Habari wakiwa wameweka kambi tangu saa saba mchana wakisubiri kupata jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam, hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa leo ndio siku rasmi ya kutangaza jina hilo lakini masaa yanazidi kwenda huku kikao chao kikiwa kinaendelea.
  Waandishi wakisubiri mtu wa kutoa taarifa juu ya jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, ambapo taarifa hizo za kuja mtu huyo ziligonga mwamba na kuambiwa kilichobaki ni makubaliano suala jinsi kuendesha uchaguzi katika majimbo.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media group Joseph Kussaga akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited Roberto Jarrin wakati alipotembelea ofisi za Clouds zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited, Roberto Jarrin (kushoto) katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa clouds Media group Joseph Kussaga (katikati kwa waliokaa) kulia kwake ni Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba na kushoto ni Mkurugenzi wa Media wa kampuni ya Aggrey&Clifford wakati alipofanya ziara kwenye ofisi za Clouds zilizopo Mikocheni ijini Dar es Salaam.
   Ujumbe wa kampuni ya TBL ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Robert Jarrin ukipkelewa atika ofisi za ITV eneo la Mikocheni jijini Dar es Saaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya The Guardian Limited Richard Mgamba (Kushoto) akisalimana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) Roberto Jarrin (kulia) wakati alipotembelea ofisi za kampuni ya The Guardian zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  IMG_2156_1

  Ambassador of Norway, H.E Hanne-Marie Kaarstad, (left) and UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, signing agreement of USD 3.1 million for Grants to support the UN’s Refugees response, governance initiatives, and UN Partnership Building in Zanzibar as well as on Human Rights, at the ceremony which was held at the UN offices in Dar es Salaam.

  *Refugees and Governance programs among key areas of support
  The Norwegian Embassy today has signed an agreement with One UN Tanzania to release USD 3.1 million (approximately 6.9 billion Tshs).The signing ceremony was held at the UN offices in Dar es Salaam between the Ambassador of Norway H.E Hanne-Marie Kaarstad and the UN Resident Coordinator Mr. Alvaro Rodriguez. The contribution will focus on providing support to the UN’s refugee response, governance initiatives, and UN partnership building in Zanzibar as well as on human rights.

  Emphasizing on the Embassy support to the One UN, Ambassador of Norway H.E Hanne-Marie Kaarstad stated that Tanzania has set a good example of UN Agencies working together with coherence, efficiency and effectiveness. She added; “The UN has always been a vital and highly valued partner for Norway. 

  The implementation of the new Sustainable Development Goals, which we hope will be adopted by the UN General Assembly in September, will require hard work. It is not business as usual and requires concerted efforts from us all. We wish to support the UN in assisting the people and the Government of United Republic of Tanzania in their effort to achieve these goals and fulfil their international obligations, including giving a voice to the most marginalised and vulnerable.”
  IMG_2163
  Ambassador of Norway, H.E Hanne-Marie Kaarstad, (left) and UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, shake hands after affirming their signatures on the agreement.

  Thanking the government and people of the Kingdom of Norway for their continued support, the UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, stated that Norway has been a supportive and constructive partner of One UN and Tanzania for decades. “The contribution of USD 3.1 Million will be used to strengthen partnerships, enhance democratic governance interventions by UN agencies and provide urgent relief to Burundian refugees in Tanzania”. He added that the One UN looks forward to a continued collaboration with Norway in the years to come.

  Norway has been a major supporter of the UN reform agenda and the upcoming Sustainable Development Goals (SDGs) and with other development partners, is committed to the development vision of the government and the people of Tanzania.
  Ballot-box
  Ballot box.
  DSC_0170
  Nyarugusu Refugee's camp in Kigoma.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP David Misime

  Napenda kutoa taarifa fupi kuhusu tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya saa 10:00 hrs huko katika Hoteli ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa wananchi walitoa taarifa majira ya saa nne asubuhi kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa. 

  Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli. 

  Askari walithibitisha kuwa ni kweli walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina la AMIT KEVALRAMANI mwenye umri wa miaka 31, Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam   akiwa na fedha kiasi cha Tshs. 722,500,000/= ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015 alifika Dodoma kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya nafaka.

  Alipofika Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu. 

  Akiwa katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli ya St. GASPER walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa polisi. Mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa/mchakato wa uchaguzi kati ya makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho. 

  Katika tukio hili na uchunguzi tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo. 

  Aidha imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake.


  0 0

   Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (MEDO), James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kabla ya MC Pilipili kutiliana saini na taasisi hiyo ya kusaidia elimu. Kutoka kulia ni Meneja Mradi, Bertha Gama, Emmanuel Elias 'MC' Pilipili na Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin.
   MC Pilipili (katikati), akizungumza kabla ya kutia saini.
   Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akiangalia mkataba huo kabla ya kusainiwa.
   MC Pili pili (katikati), akisaini mkataba huo.
   Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akimkabidhi mkataba huo MC Pilipili. Kulia ni Meneja Mradi Medo, Bertha Gama.


  Na Dotto Mwaibale

  MSANII na mshereheshaji wa shughuli mbali mbali, Emmanuel Elias 'MC' Pili pili ameingia mkataba na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (Medo), kwa ajili ya kusaidia elimu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kabla ya kusaini mkataba wa kusaidia watoto walio katika mradi wa elimu kwa watoto unaoendeshwa na Medo, Pilipili alisema ni wakati muafaka kwa watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kusaidia shughuli za maendeleo hasa katika elimu.

  Alisema bila ya kuwa na elimu hakuna kinachoweza kufanyika katika mambo mbalimbali pamoja na uongozi hivyo kila mtu eneo alipo anapaswa kusaidia elimu kupitia taasisi hiyo ya Medo ili iweze kuwasaidia watoto wengi zaidi.

  "Napenda kuwasapoti watoto hawa waliochini ya mradi 
  unaoendeshwa na Medo kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali hivyo naomba watanzania wanisapoti wakiwemaniio wasanii wenzangu" alisema Pilipili.

  Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro, James Mbuligwe alisema taasisi yake kuingia mkataba na MC Pili pili kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao ni hatua nzuri ya mafanikio kwao.

  Alisema  taasisi hiyo imezindua kampeni maalumu ya 'Nisaidie 500 Yatosha kunipa elimu ambapo balozi wa mradi huo ni Msanii Wastara Sajuki" alisema Mbuligwe.

  Meneja wa Mradi huo, Bertha Gama alisema hadi hivi sasa kuna watoto 35 wanaopata elimu ya Sekondari katika shule za Kauzeni, Kihonda, Mwembesongwe na Mzinga na kuwa mwaka huu wanafunzi wanne waliochini ya mradi huo wanategemewa kuhitimu kidato cha nne.


  Alisema lengo la taasisi hiyo ni kufikisha huduma zao nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza wameanzia mkoani Morogoro na kupitia chini ya mradi huo watoto 100 watanufaika na kwa awamu ya pili wanatarajia kuifanya mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

  0 0
 • 07/14/15--22:30: Kipindi cha Niambie Live
 • Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
  Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.
  Wiki hii mada ni SIKU YA KINABABA DUNIANI.
  Na mgeni mwalikwa ni Mayor Mlima
  Ni Niambie Live....
  KARIBU

  0 0


   NRDEA in collaboration with TCRA together are organizing the Cyber Defense East Africa Summit which will be held at Mlimani City Conference Hall from 11thto 13th August 2015 with the theme “PROTECTING THE INTERCONNECTED WORLD. The guest of honor will be Hon.Ambassador Ombeni Sefue the Chief Secretary to the Cabinet and head of the public service. Experienced   Speakers on Business transformation, technology and cyber security from within and outside the country will attend and   speak at the event.  

   Business leaders including CEOs’, Directors, CIOs’, CFOs’, Auditors, lawyers; information security experts from various industries in east Africa will also exchange their business knowledge and network with the rest of the participants. 

  With over 6 leading security and technology vendors/companies in the world will be available for exhibition and showcase their product with open discussion from any participants.

  To get a ticket call +255 719 253 037 / +255 222 110 895 or send an email to info@nrd.co.tz

  0 0

  Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale,Mwilu akizungumza katika mkutano  na waandishi wa habari Dar es Salaam leo ,Kuhusu mkutano mkuu wa  chama hicho uliofayika Dodoma hivi karibuni na  mchakato wa kumpata mgombea Urais na  changamoto zilizojitokeza.
  Mwanasiasa Mkongwe nchini,Kingunge Ngombale Mwilu akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) mapema leo,nyumbani kwake makumbusho,jijini Dar.
  .
   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii .

  Mwanasiasa   mkongwe nchini,Kingunge Ngombale Mwilu amesema kuwa wanachma wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ,umefika wakati muafaka sasa wa kuungana pamoja na kuzika tofauti zao zilikuwa zikijitokeza hapo awali badala yake wasimame imara kukijenga chama chao.

  Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam,Kingunge amesema CCM inatambulika kimataifa kutokana na historia yake,hivyo lazima kiwe imara wakiwemo viongozi wake wakiwashirikisha na wanachama wao .

  Amesema katika uchaguzi wa kutafuta mgombea urais uliofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma ulikiuka haki za wagombea kutokana na wagombea kushindwa kwenda katika Mkutano mkuu wa wanachama  na kujieleza.

  Kingunge amesema ,kilichotokea Dodoma sio halali na sio haki lakini chama cha CCM lazima kiendelee,alisem na kuongeza kuwa "tumepata mgombea John Magufuli yeye sio aliyefinyanga na wajumbe wa mkutano mkuu,hivyo tumuunge mkono kwa pamoja na kupata ushindi wa kishindo",alisema Kingunge.

  "Wana CCM watafute umoja wa kushikamana na kuwa Lowassa ana nafasi ndani ya CCM,hivyo  tuunde mazingira ya kutumia nguvu zilizopo CCM katika kushinda kwa ushindi wa  kishindo katika uchaguzi mkuu",amesema Kingunge.

  Amesema yaliyotokea Dodoma lazima yazungumzwe ili watu waweze kutoa duku duku zao kwa kile ambacho kimeonekana katika chama na ni changamoto kubwa ambayo inapaswa kufanyiwa kazi. 
  Mwanasiasa Mkongwe nchini na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale Mwilu (kushoto) akizungumza katika mkutano  na waandishi wa habari Dar es Salaam leo ,Kuhusu mkutano mkuu wa  chama hicho uliofayika mjini Dodoma hivi karibuni na mchakato wa kumpata mgombea Urais na  changamoto zilizojitokeza

  0 0

   Diwani wa Kata ya Vituka, Kenny Makinda (kulia), akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Mwajuma Mikorota wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ya kukabidhi kisima cha maji katika eneo la Nasizi, Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu.
   Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (katikati),  akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Haisha Juma wakati wa hafla ya TBL,  ya kukabidhi kisima cha maji katika eneo la Nasizi, Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Ali Limboa ambaye ni wa eneo la Limboa.
   Akina mama wakazi wa eneo la Kwa Limboa, Temeke,Dar es Salaam, wakiteka maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi kisima cha maji kilichojengwa na kampuni hiyo katika Nasizi, Vituka, wilayani Temeke. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika


   Mkurugenzi Mtendaji wa wa Kampuni ya Mo Resources Ltd, Onesmo Sigalla iliyojenga kisima hicho, akimuonesha Ofisa Uhusiano wa  TBL, Dorris Malulu ramani ya kisima hicho.
   Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kushoto) na Diwani wa Kata ya Vituka, Kenny Makinda wakifungulia maji kwenye bomba wakati wa hafla ya TBL kukabidhi msaada wa kisima katika Serikali ya Mtaa wa Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam
   Mama mkazi wa Yombo Vituka akifurahia baada ya kuteka maji katika kisima hicho. Kushoto ni Dorris Malulu wa TBL aliyekabidhi kisima hicho.
  Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Yombo Vituka, Mary Jailos akimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, kwa msaada wa ujenzi wa kisima uliotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mtaa huo.

  0 0

  Kada wa Chama Cha Mapinduzi Edmund Rutaraka aliyetangaza nia ya kugombea jimbo la Moshi mjini.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


  SIKU chache baada ya kumalizika mchakato wa kumpata kada atakaye peperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kinyang’anyiro cha kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ,Makada wa chama hicho sasa wamerejea majimboni na kuanza harakati za kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea Ubunge..


  Hali hiyo inajitokeza katika jimbo la Moshi mjini ,baada ya vijana wa chama hicho kuonekana kuhamasika huku wakijitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Ubunge na kutishia harakati za baadhi ya makada wakongwe ndani ya chama hicho.


  Waliojitokeza na kutangaza nia hadharani hadi sasa ,Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM na naibu kamanda wa Vijana CCM manispaa ya Moshi ,Edmund Rutaraka(37) na Mwenezi wa Chama hicho wilaya ya Moshi mjini Priscus Tarimo,diwani wa kata ya Kilimanjaro aliyemaliza muda wake.


  Rutaraka ambaye ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili,(M.BA) ya Chuo cha Uongozi ,Esami na Shahada ya Sayansi ya Chakula na teknolojia ya Chuo kikuu cha Sokoine (SUA),alisema CCM katika jimbo la Moshi mjini kwa sasa kinapaswa kumsimaisha mtu mwenye hekima,Busara na Mcha Mungu.


  “Kiongozi kwa sasa atakaye tosha kupeperusha chama chetu ni yule atakaye weza kusimamia vema rasirimali zilizopo katika jimbo letu na si yule mwenye maneno ya kulaghai wananchi”alisema Rurataka.


  Rutaraka ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi alisema baada ya kushauriwa na wazee,  kujitathmini na kupima uwezo wake ameona anatosha kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Moshi mjini .


  “Nimeshauriwa na wazee,nikajitathimini na kupima nikaona kwamba ninatosha kuwa mwakilishi mwema wa wananchi wa jimbo la Moshi mjini .hivyo basi naomba nitumie muda huu kutangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Moshi mjini.”alisema Rutaraka ambaye pia ni naibu kamanda wa vijana wa CCM manispaa ya Moshi.


  Alisema kwa namna hali ilivyo sasa  chama Cha Mapinduzi kinapaswa kuwa na viongozi vijana ambao wataweza kuliongoza taifa kwa ujumla, kwani vijana ndio wenye nguvu na ambao wanaweza kuleta mabadiliko kwa haraka zaidi.


  Rutaraka alisema kama kijana ameamua kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Moshi mjini ili kulikomboa kutoka Upinzania na kurudi Chama cha Mapinduzi huku akiwaomba vijana wenzake kumuunga mkono .


  “Kazi ya mbunge ni kuisimamia na kuishauri  serikali hivyo basi uwezi kufanya hivyo kama huna dhamira ya kweli ya kuingia kwenye bunge kwa ajili ya kufanya kazi ya wananchi.”alisema Rutaraka


  Kuhusu vipaumbele vyake Rutaraka alisema ni kuhakikisha huduma za afya zinapewa nafasi ya kwanza hasa kwa Mama wajawazito na watoto na kwamba huduma muhimu hazikosekani katika Hospitali,Zahanati na vituo vya Afya vilivyoko ndani ya jimbo la Moshi mjini.


  Mbali na kipaumbele hicho Rutaraka pia alisema atahakikisha anawatetea walemavu wa aina zote ikiwa ni pamoja na kusaidia angalau wanapata nafasi ya kufanya kazi ambazo wanauwezo nazo.


  Pia alisema atahakikisha anasimamia miundo mbinu na kusaidia watu wanapata hati za viwanja vyao  kwani kuna baadhi ya kata  wananchi wanashida ya ardhi na viwanja havijapimwa katika manispaa.


   Kujitokeza kundi hilo la vijana kunafanya idadi ya makada wa chama hicho walioonesha nia ya kutaka kugombea Ubunge katika jimbo hilo lililoomgozwa na Philemoni Ndesamburo (Chadema) kufikia  12 hadi sasa licha ya uwepo wa baadhi yao kungojea kukamilika kwa mkutano mkuu wa Chama hicho mjini Dodoma.        0 0

  fomu

  Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoani Singida.
  vijana
  Baadhi ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na Hassan Mazala nje ya jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa singida mara baada ya kuchukua fomu.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).

  Na Hillary Shoo, SINGIDA
  MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Singida Mjini .

  Akizungumza na kundi la Vijana wa CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed Dewji aliyestaafu.
  ‘Nimejipima nikaona ninaweza kuvaa viatu vilivyoachwa wazi na Dewji kwani katika kipindi chote alichukuwa Mbunge nilishirikiana nae katika kuyatekeleza yale yote aliyonituma kama msaidizi wake wa karibu.” Alisema Mazala.

  “Nimekuwa Kiongozi kwa muda mrefu katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye vijiji ,Kata, Wilaya, Mkoa na sasa Taifa, hivyo nina uwezo wa kutosha na nimekomaa kisiasa katika kufanya kazi hii ya Ubunge bila wasiwasi wowote pale alipoachia Dewji” Alisisitiza.

  Aidha alisema anazifahamu changamoto zinazolikabili Jimbo hilo kwani ametembea kona zote na kujionea hali halisi ya wananchi wanavyojishigulisha na shughuli za kijamii.

  “Nina Moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia, ninaombeni mnibebe, najua yamesemwa mengi sana juu yangu katika kipindi ambachio nimlikuwa nafanya kazi na MO, lakini yapuuzeni hayo kwani hayana ukuweli wowote ni chuki binafsi tu.” Alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana linalojiita team Mazala.


  Hata hivyo Mazala ambaye ana uwezo mkubwa wa kutawa jukwaa alisema kamwe hatawaanguisha wananchi wa Jimbo hilo huku akitumia misamiati Zimwi likujualo, Usiache mbachao na mwokoto kuni porini huota moto pamoja.

  Akitangaza kutogombea tena Ubunge mapema Julai 08 mwaka huu mjini Singida Dewji alimsifu Mazala kwa kusema kuwa ni mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu na ana moyo wa kujitolea kwani aliweza kusimamia kazi zake zote bila ya matatizo yoyote.

  “Na pia ninapenda kumshukuru kipekee mtu mmoja ambaye bila yeye mafanikio yangu ya kiuongozi niyoyopata hapa Singida yasingeweza kufanikiwa vizuri bila ya yeye.” Alisema Dewji katika taarifa yake hivi karibuni.
  kwa nguvu
  Mazala akiwaasa vijana kufanya kazi kwa nguvu katika jimbo hilo.
  nimenyooka
  Mkinipa nafasi ya kuwatumikia mambo yatanyooka namna hii.
  ninao uwezo
  tuko imara
  Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini Hassan Philipo Mazala akisistiza jambo kwa vijana waliomsindikiza kuchukua fomu.
  pamoja


older | 1 | .... | 583 | 584 | (Page 585) | 586 | 587 | .... | 1897 | newer