Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 582 | 583 | (Page 584) | 585 | 586 | .... | 1898 | newer

  0 0


  First Secretary from the Embassy of the People’s Republic of China, XU Jingchun (r) handing over a checque amounted to USD 10,000 to Newala district for the construction of a ward at Kitangari hospital in Newala district in Mtwara yesterday.

  0 0

  sn1
  Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
  sn2
  Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akivalishwa Shada la maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo.
  sn3
  Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanahabari  mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo.
  sn4
  Mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia CCM Dkt Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya Wanachama waliojitokeza kumlaki barabarani mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndenge wa Zanzibar akitokea Dodoma ambapo alithibitishwa rasmi kugombea nafasi hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

  0 0

  om1
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano wa  kumi na mbili (12) wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa nchi za Afrika Wanachama wa Jumuiya ya Madola  utakaofunguliwa leo
  om2
  Taswira ya moja ya eneo mkutano wa Wakuu wa Utumishi Barani Afrika utakapofanyika
  om3
  Katibu Wakuu na watendaji mbalimbali wakijadili wakati wa kikao: kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu . Dkt. Florens Turuka, akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimneti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhem James Meru

  0 0

  Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama
   
  MUIMBAJI wa Muziki wa Injili anayekuja kasi katika muziki huo, Danny Bulenge amesema anakidhi kuwa mmoja wa watakaomsindikiza mwenzake Bonni Mwaitege uzinduzi unaotarajia kufanyika Agosti 2 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa Bulenge anakidhi kumsindikiza Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu tatu ambazo ni moto wa kuotea mbali katika muziki huo.
  Bulenge alisema hivi sasa anaendelea na mazoezi kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu na kuahidi kusindikiza vilivyo albamu hizo tatu kwa staili ya aina yake.
   
  Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, Bulenge ni mmoja wa wataungana na Mwaitege katika uzinduzi huo.“Uzinduzi  wa  albamu tatu za Bonny Mwaitege unatakiwa kufanyika kwa maandalizi ya hali ya juu ambayo yanafanyika kwa mfumo  wa kisasa,” alisema Msama na kuongeza.
   
  “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.
   
  Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo. Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo.Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi  na raia wa eneo hilo kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia leo. 
  Viongozi wa Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, wakitembelea maeneo mbalimbali ambayo majambazi walidhuru, katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam leo.

  Na Bakari Issa
  ASKARI wa nne wa Jeshi la Polisi na raia watatu wamefariki dunia  katika tukio la ujambazi lililotokea katika kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

  Katika tukio hilo watu wapatao nane wamesadikika kuingia katika kituo hicho cha Polisi eneo la Stakishari majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo.

  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu amesema lengo la watu hao ni kutaka kuiba silaha zilizokuwa katika kituo hicho cha Stakishari.

  Aidha, amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zinazohusu uharifu kwa Jeshi la Polisi.

  Pia, kuhusu uvamizi wa Majambazi, Mangu amesema watajitahidi kuanza kuimarisha ulinzi kwa upande wao hususani katika vituo vya Polisi ndiyo baadae kwenda kuimarisha usalama wa  wananchi.

  0 0

   Picha ya 1-2 ni mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi akiwa mikononi mwa polisi baada ya kutiwa mbaroni Mnara wa Saa maeneo ya Stesheni Dar es Salaam leo mchana kwa madai ya kupora kiasi kikubwa cha fedha. Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanne.

   Kijana mwingine anayedaiwa kuwa ni jambazi akiwa amekamatwa.
   Watuhumiwa hao wanne wa  ujambazi  wakiwa ndani ya Noah kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi. Kulia ni askari Polisi.
   Askari kanzu (katikati), ndiye anadaiwa kuwadhibiti majambazi hayo kabla ya kujificha chini ya uvungu wa taxi zinazoegeshwa jirani na Mnara wa Saa katika makutano ya barabara ya Uhuru, Samora na Nkruma.
   Gari lenye namba T 976 BKK walilokuwa wakitumia majambazi hayo liondolewa eneo la tukio kupelekwa kituo kikuu cha polisi.
   Wananchi wakiwa eneo la tukio.
   Askari Polisi wakilipekua gari walilokuwa wakitumia watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi.
   Upekuzi ukiendelea.
  Maofisa wa polisi wakiteta jambo eneo la tukio baada ya kuwakamata majambazi hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

  0 0

    A team of 38 Heroes who reached Uhuru Peak arrived safely at the foot of Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
   Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho, addressing the media (not in picture) at the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
   13 year old Susan Elias, from Moyo wa Huruma Orphanage centre in Geita reached Uhuru Peak thus receiving her certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
   Kili Challenge Ambassador from South Africa's Rugby team Mr. Krynauw Otto reached Uhuru Peak thus receiving his certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
   13 year old Michael Lomo, from Moyo wa Huruma Orphanage centre in Geita reached Uhuru Peak thus receiving him certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.

   Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo, addressing the media (not in picture) joined by Michael Lomo (right) and Susan Elias (left) from Moyo wa Huruma, an orphanage centre that has benefited from the Kili Challenge basket of funds who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania. This is the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has raised about TZS 1.2B funds this year to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
   Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo, addressing the media (not in picture) at the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.

   The Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho celebrating the 39 Heroes from 7 different countries that is Tanzania, Mali, Egypt, Indonesia, United States, Guinea and South Africa at Mweka Gate in Moshi, that decided to undertake Kili Challenge for a good cause to demonstrate their solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS.
   Celebrating the 39 Heroes from 7 different countries that is Tanzania, Mali, Egypt, Indonesia, United States, Guinea and South Africa at Mweka Gate in Moshi, that decided to undertake Kili Challenge for a good cause to demonstrate their solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS.
  Some of the celebrated 39 Heroes from 7 different countries that is Tanzania, Mali, Egypt, Indonesia, United States, Guinea and South Africa at Mweka Gate in Moshi, that decided to undertake Kili Challenge for a good cause to demonstrate their solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS.

  0 0

  digna ft maromboso

  0 0

   Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo (kulia), akizungumza katika mkutano na wadau wa filamu na wanahabari Dar es Salaam leo jioni kuhusu tamasha la nchi za jahazi litakalofanyika kuanzia Julai 18 hadi 26 mwaka huu Ngome Kongwe mjini Zanzibar.Kutoka kushoto ni Meneja wa Tamasha, Daniel Nyalusy na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando (kushoto), akizungumza kuhusu tamasha hilo kubwa la jahazi. Kulia ni  Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo.
   Meza Kuu. Kutoka kushoto ni Mratibu John Mchaina 'Simple', Mratibu Rehema Jonas, Mjumbe wa Bodi, Mahabobo Champs, Daniel Nyalusy, Ofisa Mtendaji Mkuu, Martin Mhando na Mjumbe wa Bodi, Fatma Allo.
   Baadhi ya wasanii watakaotoa burudani siku hiyo ya tamasha.
   Wanamuziki na  wasanii wa filamu  wakiwa kwenye mkutano huo wa kutambulisha tamasha hilo.
   Mtayalishaji wa muziki, Cadrake Touch (kushoto), Msanii wa filamu Mzee Chilo na mwanamuziki Elias Barnaba wakiwa kwenye mkutano huo.

  Wanahabari na wadau wa filamu wakiwa kwenye mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

  0 0

   Mwenyekiti wa Afya Sacos Othman Mussa Juma akitoa hutuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ushirika huo uliofanyika Ukumbi wa Ecrotanal Mjini Zanzibar. Wajumbe wa Mkutano huo walizimia kuongeza Akiba ya shilingi elfu 30 kutoka elfu 10 kwa mwezi ili kuzidi kujikwamua na Umaskini.
   Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Madawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Ushirika wa Afya Sacos. Katika Mkutano huo aliwaomba kuzidisha mashirikiano miongoni mwao.
   Baadhi ya Wanachama wa Ushirika wa Afya Sacos wakisikiliza hutuba ya ufunguzi ya mgeni rasmi(hayupo pichani) katika Mkutano wa mwaka wa Ushirika huo.
   Katibu Mkuu wa Ushirika wa Afya Sacos Kassim Issa Kirobo akitoa nasaha zake katika Mkutano huo ambapo aliwaahidi kusimamia vyema Ushirika huo ili utimize lengo la kujikwamua na Umaskini.
  Mmoja wa wanachama wa AFYA SACOS Makame Mussa akichangia katika mkutano huo ambapo aliwasihi Viongozi wake kuwa waadilifu ili Ushirika wao uweze kuwaletea maendeleo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Shindano la Miss Kilimanjoro Ambassador 2015 limepamba moto kwa kuchukua sura mpya kwenye vyombo vya habari likiwa na mvuto wa aina yake.

  Warembo wanaowania taji hilo wako kambini kwa sasa wakinolewa vilivyo ikiwa ni maandalizi ya fainali za shindano hilo litakalofanyika julai 24 katika ukumbi Kili Home mjini Moshi.

  Habari za kuamianika toka kamati ya maandalizi imesema kuwa kamati imejipanga kisawasawa kuhakikisha wanakidhi kiu ya wapenzi wa tasnia ya urembo katika mikoa ya kaskazini  ikiwemo Arusha ,manyara na Kilimanjaro kwa ujumla.

  Pamoja na burudani toka kwa washiriki hao kutakuwa na burudani ya wasanii wa bongo flava,ngoma za asili na saplaizi amabAyo haijawahi kutokea katika mkoa wa Kilimanjaro katika anga za burudani.

  Kiingilio cha siku hiyo V.I.P(A) ni Tsh 200,000/= ikijumuisha chakula na vinywaji, V/I.P(B) ni Tsh 100,000/= pamoja na vinywaji, SILVER ni Tsh 50,000/= na REGULAR ni 30,000/=

  0 0

  Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi D-IGP, Abrahaman Kaniki(katikati) akimuangalia majeruhi wa tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi sitakishari konstebo Gaston Shadrack alipokwenda kumjulia hali jana katika hospitali ya taifa Muhimbili, askari huyo anaendelea na matibabu.
  Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi D/IGP, Abrahaman Kaniki(katikati) akimuangalia majeruhi wa tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi sitakishari konstebo Gaston Shadrack alipokwenda kumjulia hali jana katika hospitali ya taifa Muhimbili, askari huyo anaendelea na matibabu. Kushoto ni Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  Wasanii nchini wameiomba Serikali kumalizia ujenzi wa ukumbi wa Sanaa za maonesho unaojengwa kwa zaidi ya miaka minane sasa makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) eneo la Ilala sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza hilo mapema wiki hii, wasanii hao walieleza kwamba kwa sasa kuna ufinyu wa kumbi za za maonesho hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii hao kukosa maeneo ya kufanya sanaa zao hivyo kumalizika kwa ukumbi huo itakuwa ni ahueni kubwa kwao.

  “Ukumbi huu ni muhimu sana kwetu, wengi tuliutazama kama mwanzo wa ufufuaji wa Sanaa za majukwaani lakini sasa ni muda mrefu hauoneshi dalili za kumalizika. Kuna kila sababu ya ukumbi huu kukamilika ili kutusaidia katika maonesho yetu” alisema Msanii Khalid Kambau.

  Kwa upande wake msanii wa Sanaa za maigizo Christian Kauzeni ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wasanii waigizaji mkoani Dar es Salaam alisema kwamba kutokana na ukumbi huo kutazamwa kama mkombozi wa wasanii kuna kila sababu ya kuangalia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha unakamilika mapema iwezekanavyo.

  Awali akiwasilisha mada kwenye Jukwaa hilo la Sanaa iliyohusu ‘Ubora wa Filamu na Changamoto zake’ msanii na mzalishaji filamu maarufu nchini William Mtitu alisema kwamba tasnia ya filamu chini imepata umaarufu na kukua ingawa bado changamoto za uharamia, elimu na masoko zimeendelea kuiathiri.

  “Kwa sasa filamu zinazozalishwa zimekuwa na ubora kuliko huko nyuma. Tatizo liko kwenye elimu kwa wasanii, uharamia na masoko. Kulikuwa na maduka zaidi ya sabini na tano yanayouza kazi za wasanii wa filamu lakini kwa sasa yamebaki sita tu. Wengi wameamua kuuza kazi za nje mbazo ni nafuu. Hii ni hatari” alisisitiza Mtitu.

  Aliongeza kwamba pamoja na Serikali kuirasimisha sekta ya filamu bado kuna changamoto ya kazi zinazotoka nje kutokuwekewa stempu za mamlaka ya mapato huku kukiwa na uharamia unaotishia bei za filamu halali zenye stempu hizo.

  Jukwaa la BASATA limekuwa likifanyika kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu na wiki hii kulikuwa pia na utambulisho wa asasi ya ubalozi wa Utamaduni wa Mwafrika ambayo imeasisiwa nchini Cameroon, Afrika Magharibi mwaka 2014.
  Msanii na mzalishaji filamu nchini William Mtitu (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada iliyohusu ‘Ubora katika filamu na changamoto zake’ kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli.
  Rais na mwanzilishi wa asasi ya Mabalozi wa Utamaduni wa Mwafrika (African Culltural Embassy Association) Bwana Colpas Numfor kutoka nchini  Cameroon (Katikati) akionesha nyaraka mbalimbali za usajili wa asasi yake wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye programu ya BASATA ya Jukwaa la Sanaa. Kushoto kwake ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na Kaimu Mkurugenzi wa asasi hiyo nchini Tanzania Bw. Maganiko Charles. 


  0 0

  11752481_10101143699808225_3821973930301238449_n
  The host of the show Fatema Dewji-Jaffer, during the interview with Doctor Mwele Malecela.
  Educate, Empower and Inspire is a women’s empowerment show. The aim of this show is to put successful women in the spotlight and get a glimpse as to how they are making a difference to our society and how much hey can inspire others to do the same.
  I interviewed a girl who dreamed about being a researcher, about a passionate woman who climbed the hills of Amani in search of that dream, and the woman who is living that dream doing research and contributing to the control of a disease she has worked on all her life!
  Fatema Dewji-Jaffer conducted an interview with Doctor Mwele Malecela, Check out the full interview below:

  0 0


  0 0

   
  MWANDISHI wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” ameamua  kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyaga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
   
  Bundala ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.
   
  Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika jimbo hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu kama anavyotakiwa Mbunge Kufanya.
   
  Alisema kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wawilaya hiyo ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania
  maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wahabari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za
  wilaya.
   
  Sambamba na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi  kutokana na asilimia kubwa ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya wana ushetu kama anavyoyafahamu yeye.
   
  Aliongeza kuwa akifaniiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.
   
  Bundala alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia na kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa Ardhi,Mirathi,haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao kwa ujumla.
   
  Akizungumzia kuhusu suala la michezo katika jimbo hili Bundala amesema kuwa kupitia Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara.
   
  Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.

  Wilaya ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za
  Msalala,halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.
   
  Katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana.

  0 0

  Kukosekana kwa maadili katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla ni miongoni mwa vitu vinavyochangia ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwemo UKIMWI hasa kwa vijana

  Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mh Godbless Lema wakati akifungua warsha ya afya ya uzazi na elimu ya virusi vya ukimwi kwa vijana wadogo ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Arusha hii leo

  Mh. Lema amesema imekuwa kawaida sasa jamii hasa vijana kutokuwa na hofu ya kufanya vitendo vya ngono ambapo kutokana na sababu mbalimbali wengi wao wamekuwa wakifanya bila kutumia kinga jambo ambalo linachangia maambukizi hayo kupanda kwa rika hilo

  Ametaja sababu hizo kuwa ni umasikini, utandawazi, ulevi kuwa ni miongoni mwa vitu vinavyochangia maambukizi kwa vijana huku akiishauri serikali kuangalia na kuchukua hatua mapema ya kupunguza urahisi wa kupatikana kwa vilevi (pombe) kwani kutokana na wingi wa maeneo na urahisi wa kupata vilevi kunachangia vijana kulewa na kufanya maamuzi yasiyosahihi katika ngono

  "Serikali yetu ipunguze ama iweke ugumu wa watu kupata pombe, siku hizi kila mahali pana grocery, pab au baa, na hapa Arusha unakuta watu wanatembeza pombe kwenye mabox wanaziuza kama pipi, hii inapelekea hata mtu aliyekuwa hana mpango wa kwenda baa kuinunua pombe kwa kuwa ipo hapo alipo, sasa tunategemea nini baada ya huyo mtu kulewa" amesema Lema

  Pamoja na mambo mengine ameishauri jamii kufuata imani za dini zao zinavyoelekeza kuhusu vitendo vya ngono, huku akiitaka serikali kupitia mamlaka zake kuhakikisha wanasimamia ipasavyo sera za nchi zinazohusu UKIMWI na kuwataka wenye mamlaka kutokuwa sehemu ya tatizo kwa kuwa hawataweza kuwakemea watu kwa vitendo

  Kwa upande wake Bi Grace Kessy Afisa vijana kutoka tume ya taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini TACAIDS amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana bado yapo juu karibia asilimia 2 kwa vijana huku akisema kila mmoja kwa nafasi yake bado ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha vijana wanakuwa na afya bora na wanapata huduma zile wanazostahili kupata

  Amesema tume imepanga mipango mikakati kwa kila mkoa nchini yenye kulenga kuwafikia vijana kwa kuwa kila mkoa maambukizi ya VVU kwa vijana kinatofautiana tofautiana baina ya mkoa mmoja na mwingine, hivyo mipango hiyo itasaidia kutambua tatizo linalochangia maambukizi hayo na namna ya kufanya kwa kila mkoa huku akiwataka wadau wanaofanya kazi na tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI( TACAIDS) waweze kuzingatia mipango mikakati hiyo iliyopo kwenye mikoa
   Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi
   Afisa Vijana TACAIDS Bi Grace Kessy akizungumza kwenye warsha hiyo
   Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha hiyo jijini Arusha
   Picha ya pamoja ya washiriki pamoja na mgeni rasmi Mh. Godbless Lema
  Mbunge Godbless Lema akiagana na mmoja kati ya wawezeshaji wa warsha hiyo mara baada ya ufunguzi (Na Edwin Moshi wa Eddy Blog)

  0 0

  Na Maryam Kidiko-Maelezo Zanzibar.
  ………………………………………..
  Jumuiya ya kuhifadhisha  qur-an ya akina Mama iliyopo Mtoni Wilaya ya magh-rib imeandaa mashindano ya kuhifadhisha qur-an kwa akina Mama watu wazima . Mashindano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Maruhubi yaliyojumuisha kinamama kutoka sehemu mbalimbali katika Wilaya ya Magharibi.

  Mwalimu mkuu Ustadh Khamis Masoud Omar kutoka Jumuiya ya Marqas amesema lengo kuu la Jumuiya hiyo kuwashajihisha kinamama kuijua Dini yao ya kiislm ili waweze kuisoma na kuielewa vizuri.

  Amesema kuwa Jumuiya hiyo haibaguwi mtu yoyote hivyo wanapokea Waislam wanawake na Watoto pia watafanya mpango wa kuanzisha kuhifadhisha qur-an waislam wa Kiume wakiwemo watu wazima ili kila muislam aweze kuhifadhi kitbu hicho.

  Hata hivyo amesema ipo haja yakuanzisha kuhifadhisha qur-ani kwa Wanaume Watu wazima na kuwapa hamasa Waislm wengine kuanzisha mfumo kama huo ili waislam waijue vizuri Dini yao. Nae mshika fedha wa Jumuiya hiyo Ukhti Latifa amesema elimu haina mwisho hivyo kila muislam anatakiwa kuisoma na kuihifadhi qur-ani tukufu Kitabu cha Mwenyezi Mungu .

  Akitaja Baadhi ya Changamoto zinazoikabili Jumuiya hiyo ni pamoja na ukosefu wa Vifaa vya kusomea pamoja na uchakavu wa Banda la kusomea .

  Sambamba na hayo wameomba wale wenye uwezo wakuwasaidia wajitokeze kwani wanahitaji Uzio katika Banda lao ili kuepusha Vitendo vya uhalifu na kuweza kupata stara.Jumla ya vyuo 6 vimeshiriki katika mashindano hayo yaliyojumuisha Juzuu moja hadi juzuu ya 20.

  0 0

  Dear Africans, friends and well-wishers of Africa,

  Summer is around the corner! It’s time to relax and spend quality time with friends, family and well-wisher at the largest extravaganza African Diaspora festival taking place for the 6th time in Down-town Tübingen in Germany from the 23 to the 26h of July 2015 at the African Village (Festplatz).


   
   

  0 0

  Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman amesema kuwa ajira Zanzibar bado ni tatizo kubwa kwa vijana kitu ambacho kinaipa changamoto Serikali kulifikiria suala hilo na kulipatia ufumbuzi na namna ya kuweza kulipunguza.

   Hayo yamesemwa leo huko Mwanakwereke, Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,  Vijana Wanawake na Watoto wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa za Soko la Ajira Nchini Wizarani hapo..

  Amesema Serikali imeona ipo haja kulipunguza suala la ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuweko mfumo wa taarifa za soko la ajira nchini ili kurahisisha mawasiliano kati ya muajiri na muajiiwa.

  “Pamoja na juhudi kubwa zinazo chukuliwa na Serikali za kuimarisha Uchumi na huduma za kijamii bado hapa Zanzibar ukosefu wa Ajira kwa vijana ni tatizo,”alisema Waziri huyo.

  Aidha Waziri Haruon amesema ukosefu huo wa ajira kwa nchi zinazaendelea unachangiwa na mambo mengi ikiwemo mawasiliano kati ya muajiri na muajiriwa na kukuwa kwa teknolajia za mawasiliano duniani.


  Amesema hali hiyo imefanya nchi kuwa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa raia wake kwani kazi ambazo hufanywa na watu wengi kwa sasa hufanywa mtu mmoja.

  “Hivi sasa dunia imefikia pahala kupunguza waajiri kwa kurahisisha na kukua teknoloji,kwa mfano duniani  sasa ukienda sheli kutia mafuta unatumia kadi tu,au ule mfumo wa posta kutuma barua watu wanatumia intaneti hivyo ile nafasi ya kumuajiri mtu kwa kazi hizi zinapitiwa”,alisema Waziri.

  Hata hivyo Waziri huyo alisema ukosefu wa ajira unatokana ufinyu wa elimu na ujuzi wa kitaalamu jambo ambalo linapelekea vijana wegi kukosa sifa katika ajira.

  Nae Mkurugenzi wa ajira Ameir Ali Ameir alisema katika mwaka 2009 Serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto wakati wanaandaa Sera ya ajira na lengo kuu  la sera hiyo ni kuongeza tija na kupata ajira zenye heshima, faida na zilizo chaguliwa kwa hiari ili kupunguza ukosefu wa ajira.

  Amesema Ufunguzi wa Mfumo  niwenye manufaa kwa wananchi hasa wa Zanzibar ambao umeekewa website yake hivyo utakuwa rahisi kufuatilia ajira bila ya usumbufu.

  Mkurugenzi huyo aliwaomba wandishi wa habari kuutangaza ufumo huo mjini na vijijini ili kuweza kuenea na kupata taarifa hizo kwa jamii.

                                           IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


older | 1 | .... | 582 | 583 | (Page 584) | 585 | 586 | .... | 1898 | newer