Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

DK SHEIN AFUTARISHA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wengine katika  futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi  jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja.
 Wananchi na Waislamu wa    Mkoa Mjini  Magharibi   wakiwa katika  futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akijumuika na wake wa Viongozi wakati wa futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja.
 Akinamama wa  Mkoa wa Mjini magharibi  wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana  katika viwanja vya Ikulu Mjini Uguja.
 Wananchi na Waislamu wa Mitaa mbali mbali katika  Mkoa Mjini  Magharibi Unguja  wakiwa katika  futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja  [Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na  Wananchi baada yafutari waliyoitayarisha jana kwa wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Wananchi wa  Mkoa wa Mjini Magharibi waliohudhuria katika futari waliyowaalika jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Ungu baada  ya kumalizikakwa futari hiyo,[Picha na Ikulu.]

KAMPUNIYA SIMU ZA MKONONI ZA HUAWEI WAZINDUA SIMU MPYA AINA YA HUAWEI P8

$
0
0
 Meneja  Mkazi wa kampuni  ya Simu za mkononi,  Peter  Zhang akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu  uzinduzi wa simu mpya ya kisasa ya Huawei P8 katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence  leo Jiji Dar es Salaam.
 Mkurungenzi wa Masoko  wa Huawei Tanzania Mamson Mjwala  akizungumza juu ya ubora wa betri ya simu hiyo aina ya Huawei P8 kwamba mfumo wa simu imezingatia matumizi ya muda mrefu mtumiaji anaweza kutumia simu kwa  siku nzima bila kuiongezea umeme huku kwa wale watumiaji wa kawaida anaweza kutumia kwa siku moja na nusu.
Meneja  Mkazi wa kampuni  ya Simu za mkononi, Peter  Zhang wa kulia  wakizinduwa simu hiyo ya Huawei P8 kushoto ni Mkurungenzi wa Masoko  wa Huawei Tanzania, Mamson Mjwala  wakionyesha simu hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence leo Jiji Dar es Salaam
 Wadau wa simu aina ya Huawei huwafurahia simu hiyo Huawei P8 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence leo Jiji Dar es Salaam.
 Baadhi ya wapiga picha wakipiga picha za uzinduzi wa Simu ya Huawei.
Mkurungenzi wa Masoko  wa Huawei Tanzania, Mamson Mjwala  kimwonyesha simu ya Huawei mwandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence leo Jiji Dar es Salaam.
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

VYUO VYATAKIWA KUTOA ELIMU KULINGANA NA MAHITAJI YA AJIRA HAPA NCHINI

$
0
0
Na Woinde Shizza, Arusha
VIJANA wengi  wanaohitimu vyuo hawapati kazi mara tu ya kuhitimu

masomo yao kutokana na kutokuwepo kwa vyanzo vya ajira vinavyokwenda
sambamba na ongezeko la wahitimu na kuchangia kuwepo kwa wimbi la
wahitimu wasiokuwa na ajira nchini.

Hayo yalisemwa    na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na
utalii ,Selestini Gesimba alipokuwa akizungumza katika mahafali ya
tano ya Chuo cha Taifa cha Utalii(NCT) ,kampasi ya Arusha ambapo jumla
la wanafunzi 55  walihitimu fani za mapishi, uokaji,mapokezi,na huduma
ya vyakula na vinywaji katika ngazi ya cheti.

Alivitaka vyuo mbalimbali kutoa elimu kulingana na mahitaji ya ajira
ili kuwezesha wanafunzi wanaohitimu kupata ajira  kwa haraka na
hatimaye kuondokana na changamoto ya wimbi kubwa la wanafunzi
wanaohitimu na kukaa mtaani bila ajira.

Gesimba alitoa rai kwa vijana wa kitanzania kujiunga na Chuo cha Taifa
cha Utalii ili wapate ujuzi ambao utatoa fursa ya kufanya kazi kwenye
sekta ya utalii na pia fursa ya kuweza kujiajiri wenyewe.

‘sekta ya utalii nchini ni ya muhimu sana na inapaswa kudhaminiwa
kwani imekuwa ikichangia asilimia 17.5 kwenye pato la Taifa na
kuifanya kuwa ya kwanza kwa kuingizia Taifa Dola bilioni mbili
ikifuatiwa na sekta ya madini ambayo imeliingizia Taifa Dola bilioni
1.7 mwaka 2004 .’alisema Gesimba.

Alisema kuwa, sekta hiyo ni miongoni mwa sekta inayokuwa kwa kasi
kubwa duniani ambapo imekuwa ikikua kwa  asilimia 4.5 hadi 5 kwa mwaka
ambapo imekuwa chachu ya kukuza na kuendeleza sekta nyingine za
kiuchumi kama kilimo, miundombinu , mawasiliano na usafiri pamoja na
kuwa kichochea kikubwa cha kupunguza umaskini katika jamii.

Naye Mtendaji Mkuu wa wakala wa chuo cha Taifa cha Utalii ,Rosada
Msoma alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutoa mafunzo na
kuwaunganisha wanafunzi wake na fursa mbalimbali za ajira ambapo kwa
mwaka huu kati ya wanafunzi hao 55 tayari wanafunzi 21 wameshapata
ajira huku wengine wakiendelea kuitwa kwenye usahili maeneo
mbalimbali.

Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake,Neema Mollel alisema
kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu
wa jenereta pindi umeme unapokatika chuoni hapo, ukosefu wa hostel
changamoto inayosababisha wanafunzi wanaosoma mbali kutoweza
kuhudhuria kozi mbalimbali chuoni hapo.

Aidha waliomba chuo hicho kuwezeshwa zaidi na kuweza kutoa kozi
mbalimbali kwa ngazi ya diploma ili kuwawezesha wanafunzi wake kupata
elimu ya juu zaidi ambapo itawawezesha kukabiliana na changamoto ya
ajira ndani na nje ya nchi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ,Adoh  Mapunda alisema kuwa,serikali
mkoani Arusha wapo tayari kushirikiana na chuo hicho katika kuboresha
huduma mbalimbali za masomo ili kuwezesha chuo hicho kukua zaidi na
kuendelea kutoa elimu iliyo bora zaidi.

Mapunda alikitaka chuo hicho kuboresha zaidi maswala ya hoteli ili
kuwavutia wateja wengi zaidi kuweza kujiunga chuoni hapo kutokana na
elimu nzuri ,na kuwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa

kukitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi kwa ujumla.

NCHI ZAIDI ZADHAMIRIA KUJIFUNZA KWA TANZANIA KUHUSU MATOKEO MAKUBWA SASHA (BRN)

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar,Utawala Bora ,Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini akizungumza wakati akifunga mkutano wa Majadiliano ya Viongozi wa Jumuiya ya Madola ya Utawala Bora wa Afrika  uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.





Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia BRN, Bw. Omari Issa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa jumuiya ya Madola ya Utawala Bora Afrika katika Mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.






Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Omben Sefue akizungumza katika mkutano wa jumuiya ya Madola ya Utawala Bora Afrika katika Mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar,Utawala Bora, Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini  akiwa na viongozi wakuu wa Jumuiya ya Madola ya Utawala Bora Afrika  katika picha ya pamoja katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)

MIAKA miwili tangu utekelezaji wa mfumo wa BRN uanze hapa nchini na kuonesha matokeo mazuri Katika kuboresha huduma za jamii, jumuiya za kimataifa na nchi kadhaa zimeanza kutamani kuja kujifunza. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia BRN, Bw. Omari Issa, amesema kuwa inawezekana kufikia ufanisi wa juu katika utekelezaji wa huduma za jamii iwapo nchi nyingine zitauchukua mfumo wa utendaji wa BRN na kuutekeleza kwa kuzingatia uhalisia wa mazingira na mahitaji yao.


“Sisi tulijifunza kutoka mfumo wa Malaysia uitwao Matokeo Makubwa ya Haraka (Big Fast Results) lakini tuliuoanisha na vipaumbele na mazingira yetu, kwani mahitaji yetu ni tofauti na kwao,” alisema na kuongeza kuwa uwekaji wa vipaumbele, nidhamu ya utekelezaji na uwazi ni nguzo muhimu za BRN ambazo zinaweza kuigwa na kutekelezwa kwingineko duniani.


Akisisitizia kuhusu umuhimu wa uwekaji vipaumbele alisema nchi nyingi zinafanya makosa kwa kutaka kutekeleza kila kitu ili kupata mafanikio mengi kwa wakati mmoja. “Ni vyema kuanza na vipaumbele vichache na baadaye kueneza mafanikio na uzoefu huo kwa sekta nyingine,” alisema Bw. Omari akiongeza kuwa: “Ni muhimu pia kupata ushirikiano na uelewa wa watumishi wa umma kwa sababu mfumo huu unahusisha kubadili fikra na utendaji ili wajielekeze katika kupata matokeo zaidi.”


Aidha Bw. Issa alisisitiza kuhusu utayari wa PDB wa kuendelea kutoa uzoefu wake kuhusu utekelezaji wa BRN kwa nchi nyingine za Jumuiya ya Madola. “Nafahamu kuwa changamoto ya utekelezaji ipo katika nchi nyingi kwa sasa; hivyo ni muhimu kwa nchi kujifunza kwa nchi nyingine kutokana na uzoefu walioupitia. Baadhi ya nchi zimekwisha tuma watendaji wao kuja kujifunza kutoka kwetu; na siku za karibuni tumepokea maombi mengi zaidi kutoka nchi jirani na hata kutoka nje ya Bara la Africa,” alisema.

  

MICHANGO BADO YAHITAJIKA UJENZI WA MSIKITI KIJIJI CHA KIMBANGULILE MKURANGA PWANI

$
0
0
 Huu ndio msikiti wa Masjid Fisabillah ya Mlamleni uliopo Kijiji cha Kimbangulile, Wilaya ya Mkuranga , Mkoa wa Pwani. 
 Ujenzi wa Msikiti ukiwa umeanza.
Hivi ndivyo ujenzi ulipofikia katika ujenzi huo na bado fedha zinahitajika kwaajili ya kuendelea. 

TUNAMSHUKURU  Mwenyezi Mungu kwa Pumzi anayo endelea kutupa.

Ufuatao ni Mrejesho wa Michango yenu ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Fisabillah ya Mlamleni , Mkoa wa Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Kimbangulile.



Ikumbukwe kupitia Blogs na Mitandao ya Kijamii tulitoa Wito na Tangazo la watu kujitolea Vifaa vya Ujenzi wa Msikiti ambao ulikuwa katika hali ya Manyasi .



Tunashukuru M/Mungu mwitikio ulikuwa Mzuri , Ndani ya Miezi miwili tumeweza kukusanya Fedha Tshs 4,352,022/= kwa Ajili ya Ujenzi huu wa Msikiti .



Kupitia Pesa hizi tuliweza Andaa Maandalizi ya Kiwanja , tulinunua Tofali , Cement na baadhi ya Vifaa vichache vya Kuanzia Ujenzi wa Msikiti huu.



Alhamdullilah tulianza kuchimba Msingi na kulaza Tofali 2000 , na hali Mnayo iona kwa Picha ni kutokana na Juhudi zetu na Nguvu zetu .

Naomba itambulike kutokana na Gharama kubwa ambayo itatumika katika kuhitimisha Ujenzi tupo katika Mazungumzo na Moja katika Shirika la Misaada ya Kidini lipate kuhitimisha  pale tulipo fikia wakati ambao tukiwa katika hali ya  kusubiria kufanya Majukumu mengine ya Kimaendeleo .



Nawashukuru wote mlio shiriki na Mtakao penda kushiriki zaidi katika PROJECT hizi za kheri .



Nichukue fursa hii vilevile kuwatakia Kheri ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao unatuacha na pia Niwatakie Sikukuu Njema ya Eid el Fitri .



Tunakaribisha Zaidi Michango yenu kukamilika kwa hili ndio Mwanzo wa Mengine ,



Kwa Uchambuzi zaidi Ungana nami katika Mtandao wa Facebook : Kijana wa Kiislam Dsm .



WASILISHA MCHANGO WAKO KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO .



+255715800772

+255673800772

+255689604780

Hakikisha Jina kabla ya kutuma GHALIB MONERO.

+254725113783 M- pesa KENYA (Ali Hamis)

Waliopo Uingereza wawasiliane Na +447460340642



Au

WESTERN UNION : Receiver Name :- GHALIB NASSOR MONERO.

Tunawashukuru kwa Michango yenu ya hali na Mali.

Na mtumishi wenu katika kheri .



GHALIB NASSOR MONERO L AZHARY .

NATOSHA KUVAA VIATU VYA UBUNGE WA DEWJI SINGIDA MJINI- HASAN MAZALA

$
0
0
fomu
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoani Singida.
kwa nguvu
Mazala akiwaasa vijana kufanya kazi kwa nguvu katika jimbo hilo.
nimenyooka
Mkinipa nafasi ya kuwatumikia mambo yatanyooka namna hii.
ninao uwezo
tuko imara
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini Hassan Philipo Mazala akisistiza jambo kwa vijana waliomsindikiza kuchukua fomu.
pamoja
vijana
Baadhi ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na Hassan Mazala nje ya jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa singida mara baada ya kuchukua fomu.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).

Na Hillary Shoo, SINGIDA
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Singida Mjini .

Akizungumza na kundi la Vijana wa CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed Dewji aliyestaafu.
‘Nimejipima nikaona ninaweza kuvaa viatu vilivyoachwa wazi na Dewji kwani katika kipindi chote alichukuwa Mbunge nilishirikiana nae katika kuyatekeleza yale yote aliyonituma kama msaidizi wake wa karibu.” Alisema Mazala.

“Nimekuwa Kiongozi kwa muda mrefu katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye vijiji ,Kata, Wilaya, Mkoa na sasa Taifa, hivyo nina uwezo wa kutosha na nimekomaa kisiasa katika kufanya kazi hii ya Ubunge bila wasiwasi wowote pale alipoachia Dewji” Alisisitiza.

Aidha alisema anazifahamu changamoto zinazolikabili Jimbo hilo kwani ametembea kona zote na kujionea hali halisi ya wananchi wanavyojishigulisha na shughuli za kijamii.

“Nina Moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia, ninaombeni mnibebe, najua yamesemwa mengi sana juu yangu katika kipindi ambachio nimlikuwa nafanya kazi na MO, lakini yapuuzeni hayo kwani hayana ukuweli wowote ni chuki binafsi tu.” Alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana linalojiita team Mazala.

Hata hivyo Mazala ambaye ana uwezo mkubwa wa kutawa jukwaa alisema kamwe hatawaanguisha wananchi wa Jimbo hilo huku akitumia misamiati Zimwi likujualo, Usiache mbachao na mwokoto kuni porini huota moto pamoja.

Akitangaza kutogombea tena Ubunge mapema Julai 08 mwaka huu mjini Singida Dewji alimsifu Mazala kwa kusema kuwa ni mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu na ana moyo wa kujitolea kwani aliweza kusimamia kazi zake zote bila ya matatizo yoyote.

“Na pia ninapenda kumshukuru kipekee mtu mmoja ambaye bila yeye mafanikio yangu ya kiuongozi niyoyopata hapa Singida yasingeweza kufanikiwa vizuri bila ya yeye.” Alisema Dewji katika taarifa yake hivi karibuni.

MICHANGO BADO YAHITAJIKA UJENZI WA MSIKITI KIJIJI CHA KIMBANGULILE MKURANGA PWANI

$
0
0
 Huu ndio msikiti wa Masjid Fisabillah ya Mlamleni uliopo Kijiji cha Kimbangulile, Wilaya ya Mkuranga , Mkoa wa Pwani. 
 Ujenzi wa Msikiti ukiwa umeanza.
Hivi ndivyo ujenzi ulipofikia katika ujenzi huo na bado fedha zinahitajika kwaajili ya kuendelea. 
 ***********
Tunamshukuru M/Mungu kwa Pumzi anayo endelea kutupa.
Ufuatao ni Mrejesho wa Michango yenu ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Fisabillah ya Mlamleni , Mkoa wa Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Kimbangulile.

Ikumbukwe kupitia Blogs na Mitandao ya Kijamii tulitoa Wito na Tangazo la watu kujitolea Vifaa vya Ujenzi wa Msikiti ambao ulikuwa katika hali ya Manyasi .

Tunashukuru M/Mungu mwitikio ulikuwa Mzuri , Ndani ya Miezi miwili tumeweza kukusanya Fedha Tshs 4,352,022/= kwa Ajili ya Ujenzi huu wa Msikiti .

Kupitia Pesa hizi tuliweza Andaa Maandalizi ya Kiwanja , tulinunua Tofali , Cement na baadhi ya Vifaa vichache vya Kuanzia Ujenzi wa Msikiti huu.

Alhamdullilah tulianza kuchimba Msingi na kulaza Tofali 2000 , na hali Mnayo iona kwa Picha ni kutokana na Juhudi zetu na Nguvu zetu .
Naomba itambulike kutokana na Gharama kubwa ambayo itatumika katika kuhitimisha Ujenzi tupo katika Mazungumzo na Moja katika Shirika la Misaada ya Kidini lipate kuhitimisha  pale tulipo fikia wakati ambao tukiwa katika hali ya  kusubiria kufanya Majukumu mengine ya Kimaendeleo .

Nawashukuru wote mlio shiriki na Mtakao penda kushiriki zaidi katika PROJECT hizi za kheri .

Nichukue fursa hii vilevile kuwatakia Kheri ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao unatuacha na pia Niwatakie Sikukuu Njema ya Eid el Fitri .

Tunakaribisha Zaidi Michango yenu kukamilika kwa hili ndio Mwanzo wa Mengine ,

Kwa Uchambuzi zaidi Ungana nami katika Mtandao wa Facebook : Kijana wa Kiislam Dsm .

WASILISHA MCHANGO WAKO KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO .

+255715800772
+255673800772

+255689604780

Hakikisha Jina kabla ya kutuma GHALIB MONERO.
+254725113783 M- pesa KENYA (Ali Hamis)
Waliopo Uingereza wawasiliane Na +447460340642

Au

WESTERN UNION : Receiver Name :- GHALIB NASSOR MONERO.
Tunawashukuru kwa Michango yenu ya hali na Mali.
Na mtumishi wenu katika kheri .

GHALIB NASSOR MONERO L AZHARY .

TAMKO LA SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA-CCM

$
0
0

 

SHIRIKISHO la Taifa tunawapongeza wajumbe wote wa vikao vyote vya maamuzi ndani ya chama chetu kwa kutenda haki na kumteua mgombea safi, muadilifu, mchapa kazi, mzalendo, ambaye hakuwa na kundi na hadi kwa sasa hana kundi, mwenye dhamira ya dhati na utashi wa kudumisha umoja na mshikamano ndani na nje ya chama chetu.

Shirikisho Taifa tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Mheshimiwa Daktari John Pombe Magufuli na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kuteuliwa kuwa wapeperusha bendera ya CCM 2015 katika nafasi ya Urais na Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Dr Ali Mohammed Shein kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya uraisi kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Tunapenda kuwakumbusha kuwa watanzania wana mategemeo makubwa kwao kwa fursa hii waliyoipata.  Kwa uteuzi huu, tunapenda kukipongeza chama chetu chini ya uongozi wa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara ya kwanza katika historia kwa kuwaamini na kuwapa fursa wanawake na kuwapa nafasi za juu kabisa za uongozi wa nchi yetu.


Tunapenda kuwakumbusha wanachama wenzetu waliojitokeza kuomba ridhaa ya uteuzi wa chama chetu kuwa mgombea aliyepatikana ni kwa mujibu wa taratibu na kanuni za uteuzi za chama chetu na si vinginevyo. Pia wakumbuke kuwa watia nia wote 42 walikuwa na nafasi sawa katika uteuzi lakini walitofautiana sifa za uteuzi.  Hivyo basi hakukuwa na suala la mtu kushinda au kushindwa kilichokusudiwa ni suala la chama kumteua mtia nia aliyekidhi vigezo na sifa za uteuzi, jambo ambalo limefanikiwa.


Shirikisho Taifa tunapenda kukumbusha kuwa misingi ya utawala wa kidemokrasia inatoa fursa ya kuwapa watu fursa ya kutoa maamuzi kwa pamoja.  Hii inathibitika kutoka kwenye kauli ya ya Mwl. JK. Nyerere aliowahi kuiandika kwenye maudhui yake ya dhana ya falsafa ya UHURU NA MAENDELEO: Mwalimu alisema hivi;


Tanzania ni ya Watanzania, na Watanzania ni wote. Hakuna mtu mwenye haki ya kusema ‘mimi ndiyo watu’. Wala hakuna Mtanzania, mwenye haki ya kusema, ‘Najua linalowafaa Watanzania, na wengine lazima wafuate’. Watanzania wote lazima waamue mambo ya Tanzania. Wote lazima wafanye kazi, na wote sisi lazima tuzikubali kanuni tunazojiwekea………Kanuni nyingine ni za Taifa zima, na kanuni ya namna hiyo ndiyo sheria ambayo wote tunapaswa kuitii”.


Kutokana na maandiko haya ya Muasisi wa taifa letu, Shirikisho Taifa tunapenda kurejea kauli yetu ya awali ya TAREHE 4 JULAI 2015 kuwa:

“CCM ni taasisi iliyoundwa kwa muundo wa kuongoza kwa pamoja na kutoa maamuzi kwa pamoja. Dhana hii inaonesha kuwa CHAMA chetu si mali ya Mtu binafsi au taasisi ya mtu mmoja inayotarajiwa kutoa maamuzi yanayotarajiwa kumfurahisha mtu huyo bali ni taasisi inayoweza toa maamuzi yasiyomfurahisha mtu mmoja mmoja kwa wakati wote.”


Kauli hii inathibitishwa na namna ya wanachama wa CCM walivyofanya uteuzi wa Mgombea wa Urais 2015 kwa pamoja. Kitendo cha uteuzi wa mgombea wa URAIS uliofanywa kwa pamoja unathibitisha kuwa CCM ni chama cha watanzania walio wengi, na CCM ndio Tanzania, kwani CCM ndio chama kinachotawala Tanzania.

 Hivyo basi kwa umoja wao kama watanzania, kwa kauli moja wamefanya uamuzi kupitia Mkutano Mkuu Maalum kwa kumteua mtu makini, muadilifu, mpenda haki, anayefuata sheria na taratibu tulizojiwekea, mtu ambaye ni mfuatiliaji na mtekelezaji wa maamuzi, (kwa mfano; ni mtu mwenye uwezo wa kusema hili lifanyike na kuhakikisha linafanyika).

  Kwa uteuzi huu makini uliozingatia misingi yote mikuu ya demokrasia na utawala bora, Shirikisho Taifa hatutarajii kumuona mtu yeyote au kikundi chochote ndani na nje ya chama kidhihaki au kukejeli na kukosoa maamuzi haya matukufu ya Mkutano Mkuu wa CCM 2015, isipokuwa tunatarajia kusikia na kuona kila mwana CCM na watanzania kwa ujumla wetu kuendelea kuunga mkono maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM na pia kuendelea kumuunga mkono Mgombea mwenyewe, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.


Mwisho, tunapenda kuwaambia wanachama, wapenzi, mashabiki, na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi kuwa uchaguzi au uteuzi wa mgombea kwenye ngazi ya URAIS umekwisha.

 Hivyo basi makundi yote 42 yaliyokwenda Dodoma yamevunjwa baada ya uteuzi wa Mh. Dk. John Pombe Magufuli na kubaki kundi moja tu la CCM, kwani siku zote UMOJA NI USHINDI.

 Ni busara na wajibu wetu kuungana pamoja kumnadi, kumtembeza na kumsemea Mgombea wetu pamoja na kuitangaza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa watanzania ili CCM ipate nafasi ya kushinda na kuendelea kuiongoza Tanzania. Shirikisho Taifa, tunapenda kuwaarifu wanaCCM wenzetu kuwa sisi makada wa vyuo vya elimu ya juu tutamtembeza, tutamsemea na kumnadi Dk. John Pombe Magufuli na Bi. Samia Suluhu Hassani kila kona ya Tanzania ili CCM ipate ushindi wa kishindo hapo Oktoba 2015.


Hata hivyo tunatuma salamu kwa vyama vya upinzani, tunaomba wajiandae kisaikolojia. Vijana wasomi wa CCM tutaifanya kazi yetu kwa ubora na ueledi wa hali ya juu kuhakikisha raisi anatokana na CCM, tutarudisha majimbo yaliyo shikiliwa na upinzani na hatutawapa nafasi ya wao kuupotosha umma mwaka huu. Niwatakia wale wote wanao chukua fomu za kugombea ubunge na udiwani kupitia CCM kila la heri.

 Wito wangu kwa vijana wasomi kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi ili tukisaidie chama na nchi katika kukuza uchumi wetu na kutumia taaluma na ujuzi tulio nao kuwasaidia watanzania kukabiliana na changamoto zinazo wakabili katika miaka mitano ijayo.

 Tunaamini wajumbe wa vikao vya maamuzi wamejifunza vya kutosha kupitia mchakato wa kumpata mgombea wa uraisi atakaye peperusha bendera ya CCM. Mkatuchagulie wazalendo, waadilifu, wawajibikaji wenye kukubalika ndani na nje ya chama chetu kwenye nafasi ya ubunge, uwakilishi na udiwani. Chama kwanza, mtu baadae.

 Umoja ni ushindi. Hatma ya nchi yetu ipo mikononi mwetu watanzania, ni jukumu la kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa kuwapata viongozi bora.

Ushindi ni lazima.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu Taifa (MNEC) Bi. Zainab Abdalah Issa akiongea na waandishi wa habari(Hawapo Pichani) na kutoa tamko la kuwapongeza wajumbe wote wa vikao vya maamuzi ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kutenda haki katika uteuzi wa wagombea watakaowakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu baadae mwezi kumi, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu Taifa (MNEC) Bi. Zainab Abdalah Issa wakati wa mkutano huo


Picha na Hassan Silayo

CCM ZANZIBAR WAANZA MCHAKATO WA KUTOA FOMU KWA WAGOMBEA WA UBUNGE

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhiwa Fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B “ Bibi Subira Mohammed kuomba ridhaa kwa CCM kugombea Uwakilishi Jimbo Jipya la Mahonda.
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi {CCM} Wilaya ya Kaskazini “B “ Bibi Subira Mohammed akimpatia maelezo Balozi Seif mara baada ya kumkabidhi Fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kugombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Mahonda hapo Ofisi ya CCM Wilaya hiyo Mahonda.
 Balozi Seif akimkabidhi shilingi Laki 300,000/- Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” Bibi Subira Mohammed ikiwa ni ada ya Fomu alizopewa kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Uwakilishi Jimbo la Mahonda kwa Tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu ujao.
Picha na –OMPR – ZNZ.

                                 

WAKATI Chama cha Mapinduzi kimeanza zoezi la kutoa fomu kwa ajili ya Wanachama wake wenye nia  kutaka kugombea  nafasi za Uwakilishi, Ubunge, Udiwani  na Viti Maalum vya wanawake, wazazi na Vijana mapema leo asubuhi baadhi ya wanachama wa chama hicho tayari wameshajitokeza kuchukuwa fomu hizo.

Zoezi hilo limekuwa likiendeshwa kwenye Ofisi zote za Chama cha Mapinduzi za Wilaya  hapa Nchini na linatarajiwa kuendelea hadi  Saa Nane Mchana ya Tarehe 19 mwezi huu wa Julai.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali ni miongoni mwa Wanachama hao wa CCM waliojitokeza kuchukuwa fomu hizo akijiandaa kuomba kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Jimbo Jipya la Mahonda ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

Balozi Seif Ali Iddi ni Mmoja miongoni mwa Wanachama wanane  wa CCM waliojitokeza hadi hivi sasa wenye nia ya kutaka kugombea nafasi ya Uwakilishi katika Majimbo mbali mbali ya Wilaya ya Kaskazini “B”ambao tayari wameshachukuwa Fomu hizo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” Bibi Subira Mohammed akimkabidhi Fomu hizo hapo Ofisini kwake Mahonda alimueleza Balozi Seif kwamba yuko huru kujeresha fomu hizo wakati wowote amalizapo kujaza kuanzia leo hadi Tarehe 19  Julai majira ya Mchana.

Bibi Subira alisema Mwanachama mwenye nia ya kutaka kugombea nafasi hizo anawajibika kuzilipia  Fomu hizo kwa kiwango cha shilingi Laki 300,000/- kama ada rasmi iliyowekwa na Chama pamoja na mwanachama huyo kuchangia chama kwa kadri ya kiwango anachokimudu.

Hadi sasa tayari wanachama wa Chama cha Mapinduzi wapatao kumi wameshajitokeza kuchukua Fomu za kuomba kugombea nafasi za Ubunge na Wanachama Wanne kwa Nafasi za Udiwani Ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

Katika safari hiyo ya uchukuaji Fomu za kutaka kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba Mwaka huu wa 2015 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliambatana na wake zake wote wawili Mama Pili Seif Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi na kushuhudiwa na baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya na Jimbo la Kitope.

Rais Kikwete akutana na Koffi Annan Geneva

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungmzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan mjini Geneva leo.Watau kushoto ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Mh.Modesti Mero.Koffi Annan alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1997 na 2006. Picha na Freddy Maro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan mjini Geneva baada ya mazungumzo yao leo jijini Geneva

Article 10

Binti wa Ankal ajitosa kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Viti Maalum

$
0
0
 
 Zahara Michuzi alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.

Zahara Michuzi ni binti wa Issa Michuzi blogger na mpiga picha hodari wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamalizia muda wake sasa.

Binti wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikua wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
 Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.
 Binti huyo wa Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora
 Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.
 Zahara (kushoto) akilipia fedha halali ya form hiyo huku mama yake mlezi (katikati) akishuhudia kitendo hicho.
 Zahara sasa safari yake ya kuufukuzia ubunge wa viti maalu ndipo ikaanza huku akiipitia form yake kwa mara ya kwanza toka azaliwe
Mwasham (kushoto) akitoa baadhi ya ufafanuzi kwa baadhi ya vipengele vilivyomo katika form hiyo. Picha zote na aloyson.com TBN

Watanzania kuendelea kuula viwanja vya Bayport Vikuruti

$
0
0
Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavule.

WATANZANIA wenye nia ya kumiliki ardhi, wataendelea kuipata fursa hiyo baada ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kuwapatia nafasi  wateja wao katika mradi huo ulioanza rasmi Mei 22 mwaka huu na kuzinduliwa katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Meneja Biashara wa Taasisi hiyo, Thabit Mndeme, alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam, juu ya huduma hiyo ya viwanja vinavyotolewa kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.

Kwa mujibu wa Mndeme, wameamua kuendelea kutoa huduma hiyo ya viwanja katika eneo ya Vikuruti, baada ya kufanya tathmini kwa kuangalia umuhimu wa Watanzania kuweza kumiliki viwanja ili kujenga nyumba za kuishi, nyumba za biashara na mahitaji mengineyo wapendayo.
Mbali na huduma hiyo ya viwanja, Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa bila kusahau bima ya elimu kwa uwapendao, huku huduma zote hizo zikifanikisha maisha bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavule.

“Bayport Financial Services ni taasisi yenye kutoa huduma bora kwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, hivyo tunaamini huduma yetu ya mikopo ya viwanja kuwa endelevu ni sehemu ya kuhakikisha kwamba watu wote wanakuwa na uwezo wa kumiliki ardhi kwa ajili ya matumizi yao mbalimbali. 

 “Hii ni huduma endelevu na muhimu inayotolewa kwa watu wote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo mteja kutoka mahali popote anaweza kumiliki kiwanja hicho kwa kuchukua fomu za kuomba viwanja hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima, bila kusahau kwa wakala wetu Bank Of Africa (BOA),” alisema.


Mndeme alisema kwamba sasa wateja wao watazidi kunufaika kununua viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku wakivipata kwa njia ya mkopo au kwa fedha taslimu.

WANASAYANSI ZAIDI YA 2000 WASHIRIKI MKUTANO WA TABIANCHI, PARIS UFARANSA

$
0
0
Royal CfCC15.jpgwPichani: Baadhi ya Wanasayansi wakifuatilia mawasilisho ya wanasayansi wenzao yaliyokuwa yakiwasilishwa katika mkutani huo ulioanza Julai 7 na kumalizika Julai 10, mwaka huu katika ukumbi mkubwa wa makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa.

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris, Ufaransa] Wanasayansi zaidi ya 2500, kutoka pembe zote duniani wamekutana katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’. 

Mkutano huo ulioandaliwa katika makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa, ulikuwa wa siku nne (Julai 7-10) na ndio ulikuwa mkutano mkubwa zaidi wa wanasayansi duniani kuanda makataba ambao unatarajiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi utakaofanywa hapo Desemba, mjini Paris.

Ushiriki wa wanasayansi hao katika mkutano wao huo umefanya jiji la Paris kuwa na pilikapilika za hapa na pale hasa viunga vya makao makuu ya UNESCO na yalipokuwa yanafanyika matukio ya mkutano huo.

Miongoni mwa mada zilizowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na namna ya dunia itakavyokabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce temperature level by 2 degrees), mafuliko yanayokumba nchi mbalimbali duniani (Floods). Mada zingine ni kama vile misitu, athari za watu kuongezeka mijini, ongezeko la joto, kupungua kwa vina vya bahari, masuala ya hewa ukaa, gesi sumu na mengine mengi yanayopelekea athari za tabianchi.

Mkutano huu ulilenga jinsi ya kukabiliana na tabianchi pamoja na kubadilishana ujuzi zaidi hii ikiwa ni kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika hapa hapa Paris , Desemba mwaka huu.

Hata hivyo matarajio ya wanasayansi wengi wakiwemo kutoka nchi tofauti wameeleza kuwa, hadi kufikia mkutano wa COP 21, hiyo Desemba mataifa yataafikiana maamuzi ya kila mmoja wapo pindi watakapo wasilisha.
18898203484_c8cbf79953_kBaadhi ya wanasayansi wakiendelea na mkutano katika moja ya kumbi za mikutano katika viunga vya Makao makuu ya UNESCO, Paris Ufaransa.

19334259259_2b251d5d24_oBaadhi ya wanahabari wakifanya mahojiano na mmoja wa wanasayansi katika mkutano huo katika viunga vya Makao makuu ya UNESCO, Paris Ufaransa.
19513984222_b5e615666b_o 
Baadhi ya washiriki wakiwa nje ya mkutano huo wakiendelea na shughuli wakati wa mapumziko...
19359209648_53d8f88215_oBaadhi ya Wanasayansi wakifuatilia mkutano huo.
pasted image 0

LHRC WAZINDUA KANZIDATA YA KATIBA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Afisa KANZIDATA wa maswala ya katiba, Mr. Majaliwa Ngairo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akionyesha kwa videto juu ya utumiaji wa KANZIDATA ya KATIBA kwa mgeni rasmi Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba.
Afisa utafiti wa maswala ya katiba, Ms. Geline Fuko wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akielezea juu ya utumiaji wa KANZIDATA ya KATIBA kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa ndani ya KATIBA INFORMATION CENTRE katika ofisi za LHRC - Mbezi Upepo Avenue

Meza kuu ikiwa tayari kwa uzinduzi wa KANZIDATA ya KATIBA. Kutoka kushoto ni Dr. Khoti Kamanga, Dr. Helen Kijo-Bisimba, Mgeni rasmi Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Mwenyekiti wa bodi ya LHRC Prof. Geofrey Mmari na mkurungenzi wa idara ya Utetezi na Maboresho Wakili Harold Sungusia.


Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba, mgeni rasmi Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Mwenyekiti wa bodi ya LHRC Prof. Geofrey Mmari, Dr. Khoti Kamanga na mkurungenzi wa idara ya Utetezi na Maboresho Wakili Harold Sungusia wakifuatilia kwa umakini maelezo juu ya matumizi ya KANZIDATA (DATA BASE) ya KATIBA.



Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo akikata utepe kwa ajili ya kuizindua rasmi KATIBA INFORMATION CENTRE mapema asubui hii.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba,wakiwa katika picha ya pamoja na washiziki mbalimbali waliopata nafasi ya kuhudhuria katika uzionduzi huo uliofanyika juijini Dar es salaam mapema leo


Muonekano wa KATIBA INFORMATION CENTRE ya kisasa kabisa katika ofisi za LHRC - Mbezi Upepo Avenue ambapo ndio uzinduzi huo umefanyika leo.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba akifungua rasmi uzinduzi wa KANZIDATA ya KATIBA.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba akiongozana na mgeni rasmi Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Mwenyekiti wa bodi ya LHRC Prof. Geofrey Mmari na mkurungenzi wa idara ya Utetezi na Maboresho Wakili Harold Sungusia wakielekea kuzindua KANZIDATA (DATA BASE) ya KATIBA

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba akiwa na mgeni rasmi Mhe. Jaji mstaafu Thomas Mihayo katika zoezi la Uzinduzi rasmi wa KANZIDATA (DATA BASE) ya KATIBA. 

Wageni waalikwa wakiuliza maswali mbali mbali kuhusu KANZIDATA ya KATIBA.

Kwaya ya mwalusanya ikitoa burudani katika uzinduzi huo leo


EID SENSATION NA GROOVEBACK DEEJAYS @ RHAPSODY'S VIVA TOWERS

JUMUIYA YA KUINUA VIPAJI VYA KUHIFADHI QURAN JIMBO LA KIKWAJUNI YANDAA MASHINDANO MADOGO YA KUHIFADHI QURAN.

$
0
0
1
M.C Ustadh. Khamis Ameir akisoma utaratibu wa mashindano madoga ya kuinua vipaji ya kuhifadhi Quran ya Jimbo la Kikwajuni yaliyofanyika uwanja wa Alabama Michenzani Mjini Zanzibar.
2
Mwafunzi Ramla Khamsin Jafar wa madrasati Nurul-iman akionyesha jitihada zake katika mashindano ya kuhifadhi yaliyofanyika ya Jimbo la Kwahini. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
3
Baadhi ya washiri wa mashindano hayo wakifuatilia kwa kina mashindano hayo.
4
Jaji kiongozi Abushayth Daud Mohudhar akitoa matokeo ya mashindano hayo.
5
Mgeni rasmin Mbunge wa Kikwajuni Mh. Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi zawadi mshindi wa juzuu tano Fauzia Said Ali wa Madrasat Akhlaq, pesa taslim shiling 100000.
6
Mgeni rasmin, ambae pia ni mzamini wa Mashindano madogo ya kuinua vipaji vya kuhifandi Quran Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mh. Hamad Yussuf Masauni akitoa nasaha zake mara baada ya kushuhudia mandano ya kuhifandi Quran yaliyoshirikisha wanafunzi kutoka vyuo vinane vya jimbo la kikwajuni. (kulia) Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim (Aljazira) na kushoto ni Mwenyekiti wa mashindano hayo Khamis Said Ali
7
Mbunge wa Kikwajuni Mh. Hamad Yussuf Masauni (kulia) akiwa na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Mashinda hayo Ustahd Khamis Said Ali wakitikia dua mara baada ya kumalima mashindo hayo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

TIMU YA WATU 39 KUTOKA AFRIKA KUSINI WAPNDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA KUNUNUA TAULO MAALUMU KWA WASICHANA WALIOPO MASHULENI PINDI WAWAPO KATIKA HEDHI.

$
0
0
Timu ya watu 39 wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kununua taulo maalumu kwa wasichana waliopo shuleni zisaidie wakati wanapokuwa kwenye siku zao za Hedhi.
Katika timu hiyo wamo wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za nchini Afrika Kusini ,watu maarufu ,watangazaji katika vituo vya Luninga,wachezaji filamu n.k. katikati hapo ni Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika kusini,Maya Makanjee.
Muigizaji maarufu wa filamu,Jack Devnarain akijulikana kama Rajesh Kumar katika tamthiliya ya Isidindo the Need akiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu Hfadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza wakati akitoa historia fupi ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo.
Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso akizungumza lengo la safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanao kama Trek4 Mandela ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuchangisha fedha zausaidia wasichana walioko mashuleni.
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Moshi ,Remida Ibrahim akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni hao kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki wa Changamoto hiyo.
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi ya taifa Mlima Kilimanjaro,Ibrahim Musa akitangaza ofa kwa mcheza filamu maarufu wa nchini Afrika Kusini Jack Devnarain (Rajesh ) kuja nchini kucheza sehemu ya filamu zake katika moja ya hifadhi za Tanzania.
Mcheza filamu maarufu nchini Afrika Kusini,Jack Devnrain(kulia) akituma picha mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Washiriki wa changamoto hiyo.
Jack Devnarain maarufu kama Rajesh Kumar wa kwenye tamthiliya ya Isidingo the Need akifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Ofisa Uhusiano wa nje wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika Kusini ,Maya Makanjee akifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Ofisa Uhusinao wa nje wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ,Maya Makanjee akizungumza jambo katika hafla hiyo kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki.
Washiriki wa Changamoto hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania,Allan Kijazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Allan Kijazi akiwa na Mkurugenzi wa Utalii wa shirika hilo,Ibrahimu Musa wakiongozwa na Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya kuelkea eneo maalumu kwa ajili ya kuanzisha safari ya kupanda mlima Kilimanjaro. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi bendera za taifa la Tanzania na Afrika Kusini kwa kiongozi wa timu hiyo Richard Mabaso ikiwa ni ishara ya kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wageni hao wakipia "Serfie"kabla ya kuanza kupanda Mlima.
Safari ya kupanda Mlima ndio imeanza.
Rajesh wa Isidingo the Need akiwa miongoni mwao.
Ofisa Uhusiano wa nje waKampuni ya Mawasiliano ya Vodacom,Maya Makanjee ni miongoni pia mwa wapandaji hao hapa akiianza safari"Pole pole"

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mtoto Sophia Said wa kituo cha Yatima cha Maunga cha Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitr.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwakabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali watoto, Gatson Edward na Bonny Mayanga wa kituo cha Yatima cha Tuwakomboe cha Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitir. Jumla ya vituo 10 vilinufaika na msaadahuo ambao umetokana na mapato ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu.
Sehemu ya misaada hiyo ikishushwa


KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana iligawa misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi mil 9.5 kwa vituo 10 vya kulea yatima vya jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo kwa viongozi na wawakilishi wa vituo hivyo, Msama mwasisi wa matamasha ya Injili nchini tangu mwaka 2000, alisema ametoa vitu hivyo kuwapa faraja watoto wa vituo hivyo.

Msama ambaye hivi karibuni alitoa msaada kama huo wenye thamani ya shilingi mil 7.5, alisema msaada huo wa jana ni kuwapa faraja watoto hao kufurahia sikukuu ya Idd el Fitr inayoweza kuangukia kati ya Julai 18 au 19.

“Nimeguswa kuendelea kusaidia watoto hawa, najisikia faraja na amani ya moyo ninapofanya hivi nikikumbuka mbali mno, ikiwemo hata maisha niliyowahi kuishi na kuyapitia, hivyo si kutaka sifa wala umaarufu,” alisema.

Msama ametoa wito kwa jamii kutambua watoto wanaolelewa katika vituo hivyo si kupenda kwao, bali ni kutokana na changamoto za kimaisha zilizowapata hadi ku kila mtoto angependa kulelewa na wazazi wake.

Vituo vilivyopewa msaada wa vitu mbalimbali kama unga, mchele, sukari, sabuni na juisi, ni Honoratha, Mwana, Umra, Mujahidina, Zaidi, Hairat, Sifa, Mwandaliwa na Chakuwama.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Alhaji Mzee ambaye ni mmoja wa watoto wa kituo cha Alhaji Mzee wa kituo cha Mwandaliwa, alisema ni furaha kubwa kwao kupata msaada huo kuelekea sikukuu hiyo.

Msama alisema fedha zilizotumika kununua vitu hivyo ni kutoka katika mfuko wa Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2000 chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.

Msama ni mtu aliyejipambanua kama mdau mkubwa katika kusaidia jamii kupitia makundi maalumu kama yatima, walemavu na wajane kwa lengo la kuwapa faraja ya kufurahia maisha kama wengine.

Mbali ya kutoa misaada mbalimbali kwa makundi hayo kabla au baada ya tamasha la Pasaka kila mwaka, Msama amewahi kusaidia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, mwaka 2011

IN LOVING MEMORY

$
0
0
ANDREW MINANI FATUKUBONYE

It is 10 years now since you departed. Your untimely departure clouded our hearts with untold sadness and grief. As we pray for you on this day for eternal peace and comfort, you are fondly remembered by your beloved wife, daughters, grandchildren, relatives and your friends.
John 5:28-29, “Rest in God’s loving Embrace”
Memorial services will be held at his residence Buhororo- Ngara on 18th July 2015 at 1400hrs.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images