Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

KILOMBERO WAJIVUNIA KUONGOZA UJENZI WA MAABARA KIMKOA

$
0
0
 Na John Nditi
MADIWANI wa baraza la halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro  waliohitimisha  muda wao wa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano  Julai 7, mwaka huu wamesema kutokana na kushirikiano na watendaji wa halmashauri,wilaya imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo  ikiwa na  kufikia lengo la ujenzi wa maabara .

Diwani zamani wa Kata ya Kisawasawa , Hasaan Goagoa  pamoja na Hassan Kidapa wa Kata ya Chita, kwa nyakati tofauti  walisema ushirikiano baina ya madiwani bila kujali itikati ya chama , na watendaji wa  halmashauri kupitia mkurugenzi mtendaji wake umewezesha kuibadiri wilaya iwe ya kimaendeleo katika nyanja ya kiuchumi,  kielimu na kijamii.

Madiwani wa baraza hilo walishiriki Kikao  maalumu  cha baraza kilichofanyika Julai 7, mwaka huu , mjini Ifakara , ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa , Dk Rajab Rutengwe.

Pamoja na kushiriki kikamilifu kuhamaisha ujenzi wa maabara, walisema wanajifunia kuiacha halmashauri ikiogoza kuwa na hati safi kwa muhula minne mfululizo hadi kufikia mwaka wa fedha wa 2013/2014 .

Kwa upande wake Mweyekiti wa halmashauri hiyo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Sanje, David Lugazio,alisema  kwa  ushirikiano huo uliwezesha  kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani  mwaka hadi mwaka.

“ Mapato haya yamesaidia kuongoza nguvu za wananchi kwa kutoa fedha za saruji na mabati kwa kila shule za sekondari ya kata kujenga vyumba vitatu vya maabara ya masomo ya sanyansi na wilaya imekuwa ya kwanza kukamilisha kimkoa” alisema Ligazio.

Awali, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Azimina Mbilinyi, alisema halmashauri iliendelea kujenga uwezo wa kukusanya mapato ya ndani ambapo kwa  mwaka wa fedha wa 2014/2015, imekusanya kiasi cha sh 5,013,479,000 sawa na asilimia 81 ya makisio ya kukusanya kiasi cha sh 5,473,840,000.

Hata hivyo alisema, kutokana na kuwepo kwa makusanyo mazuri na usimamizi wa matumizi sahihi ya mapato hayo, halmashauri imeweza kununua vifaa vya aina mbalimbali vya kuhudumia jamii ikiwemo na mitambo ya ujenzi wa barabara za halmashauri hiyo.
 Baadhi ya Maofisa Tarafa za halmashauri ya wilaya ya Kilombero akisikiliza jambo.
 Dereva wa Greda akionesha uwezo wake.
 Hassan Goagoa , aliyekuwa Diwani mkongwe na wamuda mrefu wa Kata ya Kisawasawa, akibadilishana mawazo na Mkuu wa mkoa, Dk Rajab Rutengwe, Julai 7, mwaka huu mjini Ifakara.
 
 Viongozi mbalimbali wangalia mitambo mipya ya ujenzi wa barabara.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( mwenyesuti) akibadilishana mawazo na baadhi ya Madiwani waliomaliza muda wao wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( suti ) akifurahia jambo pamoja na watendaji wa halmashauri ya Kilombero na madiwani waliomaliza muda wao.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( wa kwanza kulia) akiangalia onesho ya mitambo ya ujenzi wa barabara iliyonunuliwa na halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, akizundua mitambo ya ujenzi wa barabara ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( katikati walikaa) akiwa katika picha ya pamoja na madiwani waliomaliza muda wao sambamba na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

BANDA LA TAWLA KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA

$
0
0
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye banda la chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) kwenye maonesho ya kimataifa sabasaba.
 Mkurugenzi wa Programu wa TAWLA, Naseku Kisambu akitoa maelezo kwa watu waliohudhuria banda lao kwenye maonesho ya sabasaba jinsi gani Tawla inavyosaidia kisheria.
 Afisa habari wa TAWLA Goodness Mrema akitoa maelezo kwa wananchi waliohudhuria bandani kwao.
 Mkurugenzi mtendaji wa TAWLA,Tike Mwambipile akihojiwa na mwandishi wa Tbc  kwenye maonesho ya kimataifa sabasaba.

DEGE ECO - VILLAGE YAFANYA VYEMA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR

$
0
0
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village akimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.

 
 Mmoja ya Afisa Masoko wa Dege Eco - Villag.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village wakiwa katika picha ya pamoja.
Kampuni ya Hifadhi Builders iliyokuwa na mradi mkubwa nchini inayoitwa Dege Eco Village wameweza kushiriki vyema maonyesho ya maonesho 39 ya kimataifa ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo wa Dege Eco - Village, Bi. Catherine Mhina alisema kwamba Dege Eco Village wanafurahi sana kuweza kuwafikia watanzania wengi ambao walikuwa na shauku ya kujua huduma wanazo zitoa iki ni pamoja na kununua nyumba wanazojenga katika mradi wao.
"Tunashukuru Kila mmoja alikuwa akipita hapa anapenda kujua huduma zetu na pindi unapompa maelezo ya kina hasiti kujaza fomu ili aweze kununua nyumba."
Aliongezea na kusema kwamba mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Ras Dege, Kigamboni itakuwa na huduma za kijamii kama hospitali, shule aina ya chekechea, sekondari, pia kutakuwa supermarket na kadhalika.

KAMPUNI YA MABATI YA AFRICAN ALLUMIUM (ALAF), IMEZINDUA MABATI AINA YA ROYAL VERSATILE

$
0
0
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabati ya Alluminium Afrika (Alaf), Yahya Ngoza akizungumza na mmoja kati ya wateja waliotembelea banda hilo, wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa.

 Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabati ya Alluminium Afrika (Alaf), Monica Reuben akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliofika katika banda la kampuni hiyo, wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 
 Kampuni ya Mabati ya African Allumium (Alaf), imezindua mabati mapya aina ya Royal Versatile ambayo yana uwezo mkubwa wa kuhimili kutu na mazingira mengine ya hali ya hewa popote nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabati hayo, Meneja Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy alisema kuwa mabati hayo yamezinduliwa rasmi wakati wa maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, barabara ya Kilwa.
Alisema mabati hayo ambayo yana viwango vya kimataifa na yameanza kuuzwa pia nje ya nchi, yanamudu mazingira yote ikiwa ni pamoja na ukanda wa Pwani ambako hali ya hnewa yake ina kiwango kiklubwa cha chumvi.
“Maeneo mengine ni lazima ujenge na vigae na sio bati kutokana na kiwango kikubwa cha chumvi katika hewa” alisema na kuongeza kuwa hali hiyo husababisha mara nyingi kutu katika mabati hivyo kuyasababishia kuharibika katika kipindi kifupi.
Alisema utalaam na teknolojia iliyotumika katika utengenezaji wa mabati hayo unafanya  Tanzania kama Taifa kuwa na eneo la kujivunia katika sekta ya ujenzi tofauti na siku za nyuma.
“Tuna bidhaa ambayo inaweza kushindana kimataifa na pia kupanua wigo wa biashara katika nchi za Afrika Mashariki, Kat8i na Kusini” alisema Mmasy.
Kampuni hiyo ambayo asilimia kubwa ya hisa zakwe zinamilikiwa na serikali, imetoa punguzo maalum kwa wateja ambao watanunua mabati hayo wakati wa maonyesho hayo, lengo likiwa kuchangia pato la Taifa na kusaidia ujenzi wa nyumba bora nchini.

MGIMWA AWAKUNA WAZEE NYAMIHUU WAMCHANGIA TSH 100,000 YA FOMU YA UBUNGE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akishuka katika pikipiki (Boda Boda) akitoka kukagua ujenzi wa zahanati kijiji cha Nyamihuu leo.
Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akikabidhi saruji mifuko 60 kwa mwenyekiti wa kijiji cha Nyamihuu Bw Richard Mbembe  kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake.
Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimchangia pesa za fomu Mgimwa kulia.

Na matukiodaimaBlog
WAZEE  wa kijiji cha Nyamihuu kata ya Nzihi wamempongeza mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kwa kumchangia Tsh 100,000 ya kuchukulia fomu tena ya ubunge baada ya kuwatumikia  vizuri kwa muda wa mwaka mmoja wa ubunge wake .

Wakitoa pongezi hizo leo wakati wa ziara ya mbunge huyo kumalizia ahadi Yake ya Bati 60 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ,walisema kuwa wamevutiwa na chapakazi wake alioonyesha katika kipindi chake kifupi cha mwaka mmoja.

Akizungumza kwa niaba ya wazee hao na wananchi wa Kijiji cha Nyamihuu Bi shekela Mvela  alisema wamelazimika kuchangishana kila mmoja kiasi cha Tsh 10,000 na kufikisha kiasi hicho cha Tsh 100,000 kama ahsante Yao kwa mbunge huyo.

Hata hivyo walisema imani kubwa ambayo wao wameionyesha kwa mbunge huyo ni wazi ni imani ya wananchi wote wa jimbo hilo ambao wamepata kushuhudia Kazi nzuri iliyofanya na mbunge huyo kijana kwa muda mfupi zaidi ukilinganisha na wabunge waliotangulia ambao walikuwa wakiahidi pasipo kutimiza

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nzihi Steven Mhapa mbali ya kumpongeza mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi zake bado alisema CCM itaendelea kushinda katika jimbo hilo kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani uliofanyika.

Kwa upande wake mbunge Mgimwa ambae alipokelewa kwa maandamano ya Boda Boda katika kijiji hicho cha Nyamihuu alisema amefarijika zaidi kwa upendo mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao wa Nyamihuu pia mchango wao wa fedha ya kuchukulia fomu

Alisema kuwa wapo ambao wanaeneza uvumi kuwa hatagombea tena ubunge jambo ambalo si kweli isipo kuwa baada ya bunge kuvunjwa atachukua fomu tena ya ubunge ili kupata kipindi chake cha miaka mitano ya kuwaletea maendeleo wananchi hao wa jimbo la Kalenga .

mbunge Mgimwa alitaja ahadi mbali mbali zilizokuwa zimebaki kata ya Nzihi na kuzitekeleza leo kuwa katika  kijiji cha kipera amekabidhi Tsh 500,000 kwa kikundi cha Umoja PTC, Kwaya ya mtakatifu Thomas Nzihi amekabidhi Tsh milioni 1, kanisa la TAG nzihi Bati 44 ,kijiji cha Nyamihuu mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji na Kidamali Tsh milioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa ghala la kijiji.

Alisema dhamila Yake ni kutimiza ahadi zake zote ndani ya siku mbili hizi ili anapogombea tena ubunge asiwe na kiporo cha ahadi.

NGOMA AFRICA BAND WAFUNGA KAZI MAMLING FESTIVAL,AUSTRIA

$
0
0

Mining,Austria

Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, siku ya Jumapili 5 Julai 2015 ilifanikiwa kutingisha jukwaa la Mamling Festival,liliofanyika kule Mining,Austria.

kikosi kazi iko cha Ngoma Africa band kilipangiwa kupanda jukwaani saa 10 na dakika 30 alhasiri,lakini maporomota walisogeza muda hadi saa 12 jioni ndio bendi hiyo ilipopanda jukwaani ,muda ulisogezwa kutoka na hali jua na joto kali lililofikia nyuzi joto 38c,ambazo sio za kawaida kwa msimu summer barani ulaya.Kikosi kazi kilipopanda jukwaani bila ya kuremba remba walianza kuporomosha muziki moto moto kama kawaida yao,kiasi cha kuwafanya waandaaji watoe mwaliko tena kwa bendi hiyo kushiriki onyesho la 2016 mungu akijalia.

Ngoma Africa baada ya kumaliza kazi wamerudi katika maskani yao ya himaya Anunnaki,kule Ujerumani

BARAKAH DA PRINCE (TANZANIA) RELEASES NEW SINGLE “NIVUMILIE” FEATURING RUBY

BARAKAH DA PRINCE (TANZANIA) RELEASES NEW SINGLE “NIVUMILIE” FEATURING RUBY

$
0
0

2015 Kilimanjaro Tanzania Music Awards ‘Best Upcoming Artist’ Winner, BARAKAH DA PRINCE has released his new single “NIVUMILIE” (which means ‘BEAR WITH ME’) featuring Tanzanian songstress, Ruby.

“NIVUMILIE” follows the overwhelming and successful single "Siachani Nawe” released early this year; which got massive media attention and airplay in most radio and TV stations in and outside Tanzania.

“Nivumilie” is a Love song about a relationship which has been affected by financial crisis.

The love story revolves around the boyfriend (Barakah) who is not well financially to make ends meet to support his beautiful girlfriend (Ruby).

At the end of the day, his girlfriend finds herself in the hands of another rich guy, but still she doesn’t want to let go of her poor boyfriend because he is her true love.

When the  poor bf  (Barakah) found out about an affair his girlfriend  started with the new rich guy, the girl asks for  the poor bf to ‘bear with her’,  as she is only taking advantage of the rich  guy’s money, and keeps on promising to come back to him after getting what she wants.

Furthermore, the chick even suggests helping his poor boyfriend with the same money she gets from the rich guy, something which the poor boyfriend finds it to be an embarrassment.

Now, the poor bf keeps on blaming over the situation, which results into the girl giving him two options, she either let the rich dude go, so that the poor bf takes full responsibilities on her or he should be patient.

The poor boyfriend is confused because he doesn’t have money and still he doesn’t want to share her girlfriend with another man.

The song “Nivumilie”  is written by  LOLLIPOP  who also wrote Barakah’s previous single ‘Siachani Nawe’, and produced by Nusder, Lollipop and KidBoy.


'ze komiki'

WANAMUZIKI KUTOKA KONGO WAZURU JIJI LA DAR

$
0
0
Mwanamuziki wa Dance hapa  nchini ambaye anafanya shughuli zake nchini Uingereza, Said Tumba  akizungumza na  Globu ya Jamii na kuwaasa wasanii wa muziki hapa nchini  kutumia vyombo vya asili na si kutumia  vionjo vya kompyuta mara baada ya kufika hapa nchini katika hoteli ya Don Suite iliyoko Ilala, Bungoni jijini Dar es Salaam.
 
 Mwanamuziki wa Dance nchini Kongo, Fiston Lusambo (Filsa Papa) akizungumza na Globu ya Jamii juu ya ujio wao hapa nchini katika hoteli ya Don Suite iliyopo Ilala, Bungoni jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Wanamuziki kutoka Kinshasa nchini Kongo, Nzaya Nzayad akizungumza na Globu ya Jamii juu ya ujio wao hapa nchini. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika hotel ya Don Suite iliyoko Ilala,Bungoni jijini Dar es Salaam  amesema amekuja jijini Dar es Salaam kutokana na mashabiki wa muziki wa hapa nchini.
(Picha na Bakari Issa)

RAIS KIKWETE ATUA DODOMA, KUTEGUA KITENDAWILI CHA NANI MTEULE WA CCM KUWANIA URAIS WA TANZANIA WIKI HII

$
0
0
 MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015. 

Mwenyekiti huyo wa CCM amewasili na kuanza kazi mara moja ya kuongoza kikao cha kamati ya maadili ili kupokea taarifa za watia nia wa CCM, kabla ya kuanza kuwajadili na kupunguza majina kutoka 39 hadi matano, kazi itakayofanywa na Kamati Kuu ya chama hicho inayotarajiwa kukutana Alhamisi Julai 9, 2015 majira ya usiku. 

Baada ya zoezi hilo la Kamati Kuu, majina hayo matano yatapelekwa kwenye Halmashauti Kuu ya CCM, nayo itakaa na kuyapunguza tena na kufikia majina matatu ambayo nayo yatapelekwa mbele hya wajumbe zaidi ya 2000 wa Mkutano Mkuu wa chama hicho hapo Julai 12 na kuchaguz jina moja ambalo ndilo litapitishwa nan kuwa mgombea wa CCM wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015. 
 Rais Kikwete, akisalimiana na viongozi wa juu wa chama hicho, makamu mwenyekiti (Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu, Abdulrahmani Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA ZAHITIMISHWA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
 Daktari Bingwa wa Watoto na magonjwa ya figo, Jacquline Shoo akitoa maelezo kwa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha kuhitimisha (Exit Meeting) la huduma za madaktari Bingwa hapa nchini.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akishuukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kikao cha kuhitimisha zoezi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey, akizungumza na timu ya madaktari Bingwa na madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, kikao cha kuhitimisha zoezi hilo.
 

 
Zoezi la huduma za madaktari bingwa liliodhaminiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili limehitimishwa mwishoni mwa wiki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
 
Katika zoezi hilo la siku tano jumla ya wagonjwa 740 wamepata huduma na wagonjwa 24 wamefanyiwa upasuaji.
 
Akizungumza katika mkutano wa madaktari na timu ya uendeshaji ya hospitali hiyo kabla ya kuhitimisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey amewashukuru madaktari Bingwa kwa uzalendo wao na kuitolea kufanya kazi katika mazingira magumu.
 
Aidha amewahimiza madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma kwa wagonjwa na kuhakikisha kuwa dawa zote muhimu zinapatikana wakati wote.
 
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Mfaume Salamu, kwa niaba ya uongozi wa Hospitali hiyo ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika hospitali hiyo na kuwapa uzoefu madaktari wake. Amesema ujuzi waliopata katika kipindi hicho cha siku tano utawasidia kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa watakaokuja kupata huduma katika hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Shinyanga.
 
Zoezi hilo sasa linahamia katika mkoa wa Simiyu kuanzia tarehe 06 hadi 10 Julai, mwaka huu.

BENKI YA DCB YAWAPA KIPAUMBELE WA WAJASIRIMALI KATIKA MAONESHO YA SABA SABA

$
0
0
Baadhi ya wateja wakiwa katika banda la wajasiriamali walionufaika na huduma za kibenki na  DCB katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
 Afisa Mauzo wa Benki ya DCB,Tatu Shija( katikati) akiwa na wajasiriamali walionufaika na huduma za kibenki na  DCB wakinyesha bidhaa zao  katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
 Afisa Mauzo wa Benki ya DCB, Rashid Ngwali (amenyosha mkono) akitoa maelezo kwa wananchi waliopita katika banda la DCB  katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
 Wakala wa Benki ya DCB Jirani,Silima Nassoro akitoa maelezo kwa wateja waliopita katika banda la DCB  katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

Mdahalo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere wataka amani, wapinga rushwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akitoa majumuisho ya jumla juu ya dhima ya mdahalo huo, ambapo aliwataka watanzania kuendelea kupiga vita rushwa na kusisitiza kutowachagua watoa rushwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 Mtoa mada Awadh Ali Said, akitoa mada kuhusu muungano na umuhimu wa kuzingatia misingi ya amani katika mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo.
 Mtoa mada Dk. Humphrey Polepole akitoa mada kuhusu kuzingatia misingi ya amani na umoja wa taifa letu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (kushoto), akiteta jambo na watoa mada katika kongamano hilo, Jaji mstaafu Joseph Warioba na Dk.Humphrey Polepole (katikati)
 Jaji mstaafu Joseph Warioba, akimuonesha Dk. Humphrey Polepole ujumbe mfupi aliotumiwa kwenye simu yake .
Jaji mstaafu Joseph Warioba akisalimiana na washiriki wa mdahalo huo baada ya kumalizika. Mdahalo huo uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
 Jaji mstaafu Joseph Warioba (kulia), akiwaaga washiriki wa mdahalo huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii. com

SHIRIKA LA GLOBAL PEACE FOUNDATION (GPF) LAANDAA KONGAMANO KUBWA LA VIJANA LA KUJADILI AMANI, KUFANYIKA ZANZIBAR KUANZIA JULAI 12, 2015

$
0
0
SHIRIKA la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha amani iliyopo ili nchi yetu isije ikakumbwa na machafuko kama nchi za jirani.

Akizungumza leo jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation na Mshauri wa Amani Afrika , Arnold Kashembe alisema Shirika hilo limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC).

"Shirika la GPF limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambao utafanyika Zanzibar kuanzia Julai 21- 24," alisema Kashembe.

Kashembe alisema mkutano huo wa kipekee utawakutanisha maraisi wastaafu nane akiwemo Keneth Kaunda na Amani Karume, viongozi wa dini, wafanyabiashara na viongozi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi jirani.

Aidha Global Peace Leadership Conference (GPLC) 2015 itatoa mafunzo na nyenzo ili kuhimiza ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujaribu kupunguza tofauti na matatizo yanayowakumba.

Mada nyingine ni kuwapongeza vijana 400 kutoka Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki kuongeza nguvu katika mbinu za ujasiriamali na kuwa mfano wa wanafunzi wa wengine huko watokapo.

Kujenga mikakati imara ya kudumisha ukaribu na kusaidiana mbinu za kupambana na umaskini, tatizo la ajira, HIV, Malaria na kuwezesha na kuzindua misheni Maendeleo ya Afrika kama lengo kuu na kiini cha mabadiliko kupitia Amani, Uongozi bora, na Uimara wa maendeleo kiuchumi.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano kubwa la vijana  litakalofanyika Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mzima kuanzia Julai 12 mwaka huu. Kongamano hilo litahudhuriwa na marais wastafu na viongozi maarufu. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi na Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa
 Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi  (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga na  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
 Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga  akizungumza katika mkutano huo.
 Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa akizungumza kuhusu kongamano hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA 

IN LOVING MEMORY OF THE LATE DR KATALYEBA

$
0
0


The Late, Dr.Philbert O.Katalyeba
****** 
Our darling dad, 
Always so good,
unselfish and kind,
None on this earth your equal we will find,
Honorable and true in all your ways,
Loving and faithful to the end of your days,
Honest and liberal,
ever upright, 
Just in your judgment, 
always right.

Loved by your relatives, 
friends and all whom you knew One in a million, 
that husband was you! (5years have passed, 
our hearts still sore)  As time has passed, 
our hearts still sore As time rolls on, 
we miss you more 

A loving HUSBAND and DAD,  tender and kind What beautiful memories you left behind Still alive after 5years The love for you in the heart of  your darling wife Astridah, children, grand children, relative and friends keeps burning May heavens grant your soul eternal rest.

YANGA YAITANDIKA KMKM YA ZANZIBAR 1-0

$
0
0
 Mshambuliaji wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa KMKM ya Zanzibar, Musa Said katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0. (Picha na Francis Dande)
 Mshambuliaji wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa KMKM ya Zanzibar, Musa Said.
 Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akjimtoka beki wa KMKM, Kassim Abdulkadir.
 Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akimtoka beki wa KMKM, Kassim Abdukadir.
 Beki wa Yanga, Salum Telela akijaribu kumpiga chenga kipa wa KMKM, Nasoro Abdul.
Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akimtoka beki wa KMKM.
Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akimtoka beki wa KMKM ya Zanzibar, Khamis Ally katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 1-0. 
Timu zote mbili zikiingia uwanjani.
Wachezaji wa KMKM wakisalimiana na wenzao wa Yanga.
 Kikosi cha Yanga.
 Waamuzi wa mchezo wa Yanga na KMKM.
 Benchi la ufundi la Yanga.
 Benchi la ufundi la KMKM.
Mashabiki.

ACACIA YATANGAZA UDHAMINI MNONO KWA STAND UNITED YA SHINYANGA, NI WA MIAKA MIWILI

$
0
0
 MENEJA Mkuu wa kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, Asa Mwaipopo, (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandihi wa habari makao makuu ya kampouni hiyo barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, leo Julai 8, 2015. 

Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya kuchimba dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, imetangaza udhamini wa miaka miwili itakayotoa kwa klabnu ya soka ya Stand United ya mkoani Shinyanga. Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu iko mkoani humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent, na kushoto ni  Meneja wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia mahusiano ya kijamii, Stephene Kisakye

Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Julai 8, 2015 kuhusu kuingia mkataba wa udhamini wa klabu hiyo na kampuni ya uchimbaji madini, Acacia.Udhamini huo utakuwa wa miaka miwili, kwa mujibu wa Meneja Mkuu anayeshughulikia uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo.(katikati). Kushoto ni Meneja anayeshughulikia mahusiano ya kijamii wa kampuni ya Acacia, Stephen Kisakye.

NAIBU KATIBUuw MKUU TAMISEMI ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO NHC

$
0
0
 
Naibu Katibu mkuu Tamisemi ,Kagyabukama E.Kiliba akipata maelezo ya namna Shirika linavyofanya kazi kutoka kwa Afisa Mauzo, Vicent Ngaile katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa leo asubuhi kwenye viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. Anayeshuhudia ni Wilson Sanane.  
Naibu Katibu mkuu Tamisemi ,Kagyabukama E.Kiliba akipata maelezo ya namna Shirika linavyofanya kazi kutoka kwa Afisa Mauzo, Vicent Ngaile katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa leo asubuhi kwenye viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. Anayeshuhudia ni Wilson Sanane.
 
Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Salvatory Hinju akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. 
Umati wa watu waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa mbele ya Banda la Maonyesho la Shirka la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo langoni kuu la kuingilia kushoto kama unaingia Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea.

 
Umati wa watu wanaoingia na kutoka kwenye maonyesho ya Sabasaba Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea. 
Watu waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa ndani ya Banda la Maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 
Watu waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa ndani ya Banda la Maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 
Watu waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa ndani ya Banda la Maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakipata maelezo ya namna Shirika la Nyumba la Taifa linavyofanya kazi zake. Wateja waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa ndani ya Banda la Maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakipata maelezo ya namna Shirika la Nyumba la Taifa linavyofanya kazi zake. 
Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Rhobi Wambura akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. 
Michael Mbago wa NHC akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. 
  Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Rhobi Wambura akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.
Wateja waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa ndani ya Banda la Maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakipata maelezo ya namna Shirika la Nyumba la Taifa linavyofanya kazi zake. Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Rhobi Wambura akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. 
  Wateja waliofika kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiwa ndani ya Banda la Maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakipata maelezo ya namna Shirika la Nyumba la Taifa linavyofanya kazi zake. Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Joseph Haule akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.
Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Vincent Ngaile akitoa maelekezo kwa wateja
 
  Naibu Katibu mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akiingia katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa leo asubuhi kwenye viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. Naibu Katibu mkuu Tamisemi ,Kagyabukama E.Kiliba akipata maelezo ya namna kituo cha huduma kwa wateja kinavyofanya kazi kutoka kwa Afisa wa kitengo cha Huduma kwa Wateja, Theresia Muhondo katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa leo asubuhi kwenye viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. 
  Naibu Katibu mkuu Tamisemi ,Kagyabukama E.Kiliba akipata maelezo ya namna Shirika linavyofanya kazi kutoka kwa Afisa Mauzo, Vicent Ngaile katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa leo asubuhi kwenye viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa. Anayeshuhudia ni Wilson Sanane.  Afisa wa Mawasiliano kwa Umma wa Shirika la Nyumba, Edith Nguruwe akimkaribisha Naibu Katibu mkuu Tamisemi ,Kagyabukama E.Kiliba katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa leo asubuhi kwenye viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.

HATIMAE BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI LAAHIRISHWA RASMI

$
0
0
1
Rais Mstaafu wa awamu ya pili , Alhaji Ally Hassan Mwinyi, akimkabidhi cheti cha utumishi uliotukuka katika baraza la madiwani Mkurugunezi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, wakati wa hafla ya kuvunja baraza la madiwani la Manispaa ya Kinondoni
5
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Alli Hassan Mwinyi, akikagua maonyesho ya kazi zinazofanywa na manispaa ya Kinondoni.
7
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na na nishani ya utumishi uliotukuka Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa sherehe zakufunga barza la manispaa hiyo
 ………………………………………………………………….
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeliahirisha rasmi Baraza la Madiwani ambapo mgeni rasmi katika kuahirisha Baraza hilo alikuwa mheshimiwa Rais mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Shughuli hizo zilianza kwa kikao cha baraza cha kawaida cha kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada ya hapo aliwasili mgeni rasmi Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kufuatiwa na tukio la kupita katika mabanda maalum yaliyoandaliwa yakionyesha shughuli za kila idara na kupata maelezo ya shughuli zinazofanywa na idara hizo pasitisha moja na mafanikio mbalimbali katika idara hizo.
Baada ya mgeni rasmi kupita katika mabanda hayo na kupata maelezo ndi[po kilianza kikao rasmi cha baraza cha kusitisha rasmi baraza hilo ambapo lilianza kwa ufunguzi wa sala na kisha utambulisho uliofanywa na Mstahiki Meya Yusuphu Mwenda kabla ya wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa kutoa neno.

Akiongea mkurugenzi wa jiji alilipongeza baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo Tanzania nzima wanaikubali ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa Manispaa hii ni mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa Tanzania nzima.
Akiongea katika kikao hicho mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa Manispaa hii ambapo ni mengi sana yaliyotekelezwa na mengine kutokana na muda bado hayakuweza kutekelezeka,lakini ameahidi kuyatimiza yale ambayo wameyabariki yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka huko mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa mtambo huo kwa msaada wa Humburg city.
Mgeni rasmi alitoa medani na vyeti kwa madiwani na kwa baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi.Katika kuitambulisha timu ya KMC-FC ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ,hali kadhalika madiwani pia walipewa jezi hizo kila mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi aliwaomba kuitangaza timu hiyo na kuisaidia kwa hali na mali .
Akiongea katika hafla hiyo Mstahiki Meya aliwashukuru wakazi wa kinondoni kwa ushirikano.kuhusiana na suala la maendeleo Meya alisema kumekuwa na ushiriki mpana wa wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa fedha za matumizi ya umma kwa kujenga mashule,barabara,mahospitali ambapo aliiongelea pia hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi,akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana kutoka bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi sasa.Akiongelea suala la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa na kupunguza msongamano na nia ni kuhakikisha vibali vya ujenzi vinapatikana ndani ya wiki moja,kuhusu usafi.
alisema Manispaa imekuwa ikishinda mfululizo katika mashindano ya usafi yanayosimamiwa na wizara ya afya pamoja na hilo aliongelea pia mpango kabambe wa alioucha katika mchakato wa utunzaji wa coco beach ili kuiboresha na kubadilishwa sura yake licha ya hayo manispaa hii pia imekuwa ikipata tuzo ya kutunza mahesabu vizuri,.Pia alimshukuru Naibu Meya Songoro Mnyonge kwa ushirikiano na ushauri mzuri ambao amekuwa akimpa na mkurugenzi kwa ubunifu na ushirikiano wake pamoja na watendaji wote kwa ujumla.
Kaimu mkuu wa mkoa akiongea alipopewa nafasi alisema haihitaji hata maelezo kuelezea Manispaa ya Kinondoni kwani juhudi zao zinaonekana kwa macho.Mgeni rasmi akiongea katika hafla hiyo aliwashukuru kwa heshima hiyo waliyompa kwani alikuwa ana hamu kubwa ya kuja kuonana na watendaji wa Manispaa hii ,alisifia kazi nzuri ya kuboresha maendeleo katika Manispaa hii na kuongeza kuwa Kinondoni ina uwezo wa kuendesha mambo vizuri kwa kuja kwake katika hafla hii amefundishika haswa.Hongera Manispaa ya Kinondoni.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images