Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MAFUNZO JUU YA UBADILISHANAJI WA TAARIFA ZA BIOANUAI YAFANYIKA ARUSHA

$
0
0
Waratibu wa Mafunzo ya siku nne kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Bw. Makuru Nyarobi (Kulia) na Bw. Selemani Kisimbo (Kushoto) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni Rasmi (hayupo Pichani). Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Silver Palm jijini Arusha na yameshirikisha wadau kutoka Wizara, Taasisi mbalimbali na Vyuo Vikuu.
ma2
Mgeni Rasmi Dkt. Julius Ningu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akifungua mafunzo ya siku nne ya Mtandao wa Ubadilishanaji Taarifa za Bioanuai kwa wadau wa mazingira.
ma3
Dkt. Julius Ningu Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne katika Hotel ya Silver Palm jijini Arusha.
ma4
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya ufunguzi.

Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA

$
0
0
Mbunge wa Mpanda Mjini Mhe. Said Arfi
akizungumza na waandishi wa habari.
Picha ya maktaba.
Akizungumza mjini Mpanda katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, jana Mhe Saidi Arfi aliwaeleza wananchi wa Mpanda kuwa uanachama wake ndani ya CHADEMA utakoma mara tu baada ya kuvunjwa Bunge Julai 9.

Pia, alitumia mkutano huu kuwaaga wananchi wa jimbo hilo akisema hatagombea tena nafasi hiyo aliyoitumikia kwa miaka kumi. 
Mhe. Arfi alifafanua kuwa hayuko tayari kugombea jimbo hilo kupitia chama chochote cha siasa na kauli hiyo imelenga kuondoa uvumi uliokuwa umeenea kwamba alikuwa na nia ya kugombea kupia ama ACT – Wazalendo au CCM.

Alisema amekuwa akishangazwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanachana na wapenzi wa CHADEMA kuwa hajafanya lolote kwenye chama hicho. Alisema kama kuna mtu anayekifahamu vizuri chama hicho ni yeye, hivyo haoni sababu za watu kumbeza. Alisema alikuwa ameamua kukaa kimya na kuwa akiamua ‘atamwaga mboga’ ili watu wafahamu upungufu ulioko ndani ya chama hicho.

Alisema hagombei katika jimbo hilo na kama kweli chama hicho kina nguvu, basi kilitetee, akisisitiza kuwa ana uhakika jimbo hilo litakwenda CCM kwa kuwa wananchi wa Mpanda Mjini walikuwa na mapenzi na mtu siyo chama.

TAREHE 11 JULAI CCM KUMTANGAZA MGOMBEA WAKE MJINI DODOMA

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti mjini Dodoma.(Picha na Adam Mzee)

…………………………………………………………………………
“Leo tarehe 7 mwezi wa saba tunaanza vikao vya mchakato wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM ambao unnategemewa pamoja na mambo mengine utapitisha ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-20 20 lakini pia utateua mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia CCM, na pia kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu ambacho kitateua jina la mgombea wa urais kwa chama cha mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, ratiba ya vikao, leo tarehe 7 kuanzia  saa tano tutakuwa na sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.


 sekretarieti hiyo ina ajenda moja kubwa kwa kupitia maandalizi ya mkutano mkuu, ina ajenda kubwa ya kupitia maandalizi ya mkutano mkuu na kuthibitisha yapo mambo mengi katika maandalizi kuna mambo ya ratiba, mambo ya malazi ya wajumbe, kuna mambo ya makablasha mbalimbali na maandalizi ya document mbalimbali zitakazotumika kwenye vikao vitakavyoendelea baada ya leo. 

Kesho tarehe 8 kunategemewa kufanyika kikao cha kamati ya usalama na maadili cha chama, ambacho kitakuwa chini ya mwenyekiti wa Taifa  Dk.Jakaya Mrisho Kikwete. 

Tarehe 9 kichama kutakuwa na shughuli kuu mbili ya kwanza asubuhi, kutafanyika uzinduzi au ufunguzi wa ukumbi mpya wa chama cha mapinduzi na ofisi zake ambao upo njia ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma bila shaka baadhi yenu mtakuwa mmeona, mwenyekiti wa chama Rais Kikwete alipokwenda kutembelea kwahiyo ufunguzi wake utafanyika tarehe 9, majira ya asubuhi kabla mheshimiwa rais hajaenda kuvunja bunge, kama ratiba itabadilika tutawaambia lakini tarehe 9 tunahiyo shughuli ya kwanza baadaye mchana kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambayo nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea mkutano mkuu. 

Tarehe 10 tunategemea kuwa na kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi ambacho kikao hichi kitafanya mambo makubwa matatu ambacho kitafanya, kwanza kitateuwa jina la mgombea urais kwa upande wa Tanzania zanzibar, halmashauri kuu ya taifa kwa mujibu wa katiba ndio inayoteua jina la mgombea urais wa Zanzibar kwahiyo hiyo itakuwa ni kazi mojawapo itakayofanywa na Halmashauri kuu ya Taifa na kazi ya pili, watapitia pia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo itakayotumika kuombea kura na ndio itakayotumika kwa kipindi cha 2015-2020, na kutoka kwao hiyo ilani itapelekwa katika mkutano mkuu kwaajili ya kuhitimishwa.

Kazi ya tatu, halmashauri kuu hii itapokea majina matano kutoka kamati kuu ambayo yatakuwa yameteuliwa na kamati kuu, tarehe 9 na hapo watafanya kazi ya kupiga kura kupata majina matatu ya wanachama wa CCM walioomba kupitishwa na chama cha mapinduzi kuwa wagombea wa nafasi ya urais kwa upande wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. 

Majina matano haya yatapigiwa kura kupata matatu na tarehe 11 ndio siku ya mkutano mkuu wa Taifa wa chama cha mapinduzi ambao una kazi kubwa mbili, moja ni kupitisha hiyo ilani ambayo itakuwa imepitishwa na halmashauri kuu ya Taifa na maandalizi ya ilani hiyo yamekamilika, tuliunda timu kama mnakumbuka tumewahi kuitangaza ipo chini ya Wasira imefanya kazi nzuri ya kutengeneza ilani nadhani safari hii tutakuwa na ilani nzuri sana ambayo itaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu zote zilizopita lakini pia itatupeleka sasa kwenye hatua kubwa zaidi ya maendeleo ya nchi yetu.

Kazi ya pili, ni kupiga kura katika majina matatu yatakayowasilishwa katika mkutano mkuu ili kupata jina moja la mwanachama wa CCM ambaye ndiye atakuwa mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi, hivyo tarehe 11, itakuwa ni siku ya mkutano mkuu na mkutano mkuu huu utakuwa wa siku moja,lakini mkutano mkuu huu utaoneshwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, tv zote zitaonesha kuanzia ufunguzi ratiba ile mpaka wakati fulani halafu baadaye wakati wa matokeo na ufungaji wa mkutano karibia masaa sita au saba hivi tutauonesha moja kwa moja. 

Ninachotaka tu ni kuwathibitishia watanzania tumejipanga vizuri chama chetu tupo wamoja tunaamini tutamaliza vikao hivi salama, na tutatoka tukiwa na ushindi, tutatoka tukiwa na nguvu, tutatoka tukiwa wamoja na bila shaka vikao hivi vitajenga msingi wa kushinda uchaguzi kwa kishindo sana mwaka huu. 


Nataka pia nichukue nafasi hii kuwathibitishia wajumbe wa vikao vyote kuwa maandalizi yao yamekamilika na tunawatakia safari njema kutoka
wanapotoka katika nchi yetu, tunawatakia afya njema na vikao vyema vya
kamati ya maandalizi na tunawakaribisha  sana Dodoma karibuni tukijenge
chama chetu na demokrasia ya nchi yetu tuendelee kuimarisha demokrasia
ya nchi yetu”.

Article 15

MTUNGO

$
0
0
Lori halipo pichani likiwa limefunga barabara ya Morogoro na  kusababisha mtuno wa foleni  maeneo ya kibaha, Mkoa wa Pwani mapema jana jioni.

Official Video HD | Rai Classic ft. Becka Title - Lulu

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YATANGAZA MAJIMBO YA UCHAGUZI ZANZIBAR

KATIBU MKUU TAMISEMI ATEMBELEA BANDA LA LAPF MAONYESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABA SABA

$
0
0
 Katibu mkuu wa TAMISEMI Mh. Jumanne A. Sagine akisalimiana na Meneja Masoko na mawasiliano kwa Uma Bwana James Mlowe wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF . Mlowe amemweleza katibu mkuu jinsi LAPF ilivyoweza kuwa mshindi wa kwanza katika utunzaji wa kumbukumbu kwa wanachama katika sekta ya mifuko ya Pensheni na inavyolipa mafao kwa haraka. Pia kutambuliwa na Msimamizi wa mifuko hii kuwa ni mfuko unaokuwa kwa kasi kuliko mifuko yote ya pensheni tanzania

Katibu mkuu wa TAMISEMI Mh. Jumanne A. Sagine akipokea maelezo kuhusu Mfuko wa Pensheni wa LAPF kutoka kwa Meneja Masoko na mawasiliano kwa Uma Bwana James Mlowe. Mlowe amemweleza katibu mkuu jinsi LAPF ilivyoweza kuwa mshindi wa kwanza katika utunzaji wa kumbukumbu kwa wanachama katika sekta ya mifuko ya Pensheni na inavyolipa mafao kwa haraka. Pia kutambuliwa na Msimamizi wa mifuko hii kuwa ni mfuko unaokuwa kwa kasi kuliko mifuko yote ya pensheni 
 Baadhi ya tuzo za heshima  za ilizowahi kujinyakulia Mfuko wa Pensheni wa LAPF 


Kampuni ya TTCL yasaidia mifuko ya saruji kituo cha yatima

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa pili kulia) akiwakabidhi watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa pili kulia) akiwakabidhi watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiimba na kucheza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, wapopokuwa wakiwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji. Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiimba na kucheza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, wapopokuwa wakiwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa kwanza kulia walosimama) akizungumza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji. Wengine ni wafanyakazi wa TTCL na kituo hicho. Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa kwanza kulia walosimama) akizungumza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji. Wengine ni wafanyakazi wa TTCL na kituo hicho.Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipiga picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, pamoja na wasimamizi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji. Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipiga picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, pamoja na wasimamizi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.Saruji mifuko 70 ikishushwa kwenye gari mara baada ya kukabidhiwa watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma na kampuni ya TTCL. Saruji mifuko 70 ikishushwa kwenye gari mara baada ya kukabidhiwa watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma na kampuni ya TTCL.

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa mifuko ya saruji kwa kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mifuko hiyo 70 ya saruji imekabidhiwa juzi katika kituo hicho na Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo. 

Akikabidhi msaada huo, Bw. Dirisha alisema kampuni imetoa msaada huo ili kusaidia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wale wenye mahitaji maalum. Alisema msaada huo waliokabidhi utasaidia kituo hicho kuwa na majengo yake yenyewe kwani kwa sasa wamejihifadhi katika eneo dogo na ambalo sio rafiki sana kwa watoto. Kwa upande wake, Mtawa anayewalea watoto hao, Sr. Christina akipokea msaada huo alisema, anaishukuru kampuni ya TTCL kwa msaada huo; kwani umekuwa chachu ya kuamini kuwa na wao watakuwa na majengo yao na wataweza kusaidia watoto wengi zaidi. 

 Aidha ametoa wito kwa wadau wengine watakao guswa zikiwemo kampuni na taasisi mbalimbali kusaidia kituo hicho ili kiweze kukamilisha kwa wakati ujenzi wa majengo yake na hatimaye kuhudumia watoto wengi zaidi huku kukiwa na usalama wa kutosha. Hii ni mara ya pili kwa TTCL kukichangia kituo hicho mifuko ya saruji kwani mwaka jana pia ilitoa msaada wa saruji kwa kituo hicho cha watoto yatima cha Mama wa Huruma ambacho kwa sasa kina idadi ya watoto 56 ambapo wavulana ni 26 na wasichana 30.

MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA AWAFUTURISHA WAFANYAKAZI

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifuturu pamoja na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yeye mwenyewe.
Waandazi wa futari hiyo iliyofuturiwa jijini Dar es Salaam wakiendelea na maandalizi siku ya tukio.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifuturu pamoja na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yeye mwenyewe.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.

Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Chediel Msuya akionyesha umahiri namna ya kunywa maji katika dafu wakati wa futari hiyo iliyoliwa makao makuu ya NHC.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akishiriki futari kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe, Almasi Kassongo na Elias Msese wakishiriki futari kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Samweli Metilli na Adolf Kasegenya wakishiriki futari kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo

BENKI YA CRDB YARAHISISHA MAISHA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0
Mkurugezi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipeana mkono na msanii wa kughani, Mrisho Mpoto wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Mwambapa.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB inatoa huduma za kibenki katika maonyesho hayo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti kwa wateja wapya na kutoa huduma za kuweka na kutoa fedha katika tawi linalotembea iliyopo katika viwanja vya Sabasaba. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma (Na Mpiga Picha Wetu) 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki katika tawi linalotembea lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma katika Viwanja vya Sabasaba wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mteja akiweka sahihi ya dole gumba baada ya kufungua akaunti ya Benki ya CRDB.
Huduma za kibenki zikiendelea katika Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa.

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI APATA AJALI YA CHOPA JIONI YA LEO

$
0
0
 Chopa iliyokuwa ikitumiwa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassary ikiwa juu ya mti mara baada ya kup0teza mwelekeo jioni ya leo katika Kijiji cha Leguruki, Wilayani Meru Jijini Arusha. Hakuna aliepoteza maisha katika ajali hiyo, na Mbunge Nassari pamoja na Rubani wake walikimbizwa Hospitali ya Selian jijini Arusha kwa matibabu baada ya kupata majeraha kwenye ajali hiyo.

Taarifa kamili itawajia baadae kidogo.

Rais Kikwete ajiandikisha Kupiga kura kwa kutumia BVR kijijini Msoga leo, ZAIDI YA WATU MILIONI 11 WAJIANDIKISHA NCHINI

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
 Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
 Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa  kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya  kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.


JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani. 

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha. 

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo. 

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva. 

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake. 
“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva. 

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.

KAMPUNI YA MICHEZO YA BAHATI NASIBU YA GIDANI INTERNATIONAL YAJIZATITI KUINGIA NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa michezo ya Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tarimba Abbasi (kushoto) akikabidhiwa tiketi ya bahati nasibu na  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Gidani International, Clive Reynofrs wakati wa uzinduzi wa mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(Sabasaba) Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani International Profesa , Bongani Aug Khumalo na Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni hiyo Brett Smith.
Mwenyekiti wa  Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Gidani International  yenye makao yake makuu nchini Afrika ya Kusini, Profesa  Bongani Aug Khumalo akiwaelimisha wananchi waliofika kwenye banda la Michezo ya kubahatisha lililopo kwenye maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, (Sabasaba)  jinsi michezo itakayochezeshwa na kampuni hiyo itakavyoendeshwa.
Mwenyekiti wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Wiliam Mdundo (katikati) akiwahamasisha wananchi waliofika kwenye banda la bodi hiyo liliopo kwenye maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, (Sabasaba) ili waweze kushiriki katika michezo  ya   bahati nasibu  inayotarajiwa kuzinduliwa nchini mwezi Novemba na kampuni ya Gidani International.Kushoto ni Mwenyekiti wa  Kampuni hiyo Profesa , Bongani Aug Khumalo.
Mkurugenzi Mkuu wa michezo ya Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tarimba Abbasi akiteta jambo na Mwenyekiti wa michezo ya kubahatisha ya Gidan International Profesa , Bongani Aug Khumalo wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo lililopo kwenye  maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam juu ya michezo ya kubahatisha itakayozinduliwa baadaye mwaka huu.

Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Gidani International akitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo lilopo kwenye maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(Sabasaba)  juu ya elimu ya mchezo huo utakaozinduliwa mwezi Novemba ambapo washiriki watajinyakulia zawadi mbalimbali akiwemo mshindi wa zawadi kubwa ya kitita cha shilingi  bilioni 1.
Mwenyekiti wa  Kapuni ya michezo ya kubahatisha ya Gidan Intarnationa  Profesa , Bongani Aug Khumalo (mwenye shati nyeusi) akiwa katika ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya michezo ya akaubahatisha Tanzania wakati wa uzinduzi wa mchezo huu uliofanyika kwenye maonesho ya maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, (Sabasaba) Bahati na sibu yaTaifa unarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi November 2015.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TBL AENDESHA MHADHARA CHUO KIKUU CHA STEFANO MOSHI

$
0
0
 Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO),Tawi la Moshi Mjini wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na SABMiller East Africa, Roberto Jarrin alipokuwa akitoa mhadhara wa masuala ya biashara na masoko chuoni hapo, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na SABMiller East Africa, Roberto Jarrin (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi mjini, Wilfred Shangali mara baada ya kuhitimisha mhadhara wake wa masuala ya biashara na masoko kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu uliofanyika chuoni hapo juzi .
 Afisa Mipango wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi Mjini Wilfred Shangali akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa TBL Emma Urio mara baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa Biashara na Masoko uliotolewa chuoni hapo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu.
  Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Urio akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa biashara na masoko uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin katika Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi mjini kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu.


  Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Urio akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa biashara na masoko uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin katika Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi mjini kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu.

  Mkuu wa Idara ya Biashara Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO) Tawi la Moshi mjini Dk. Gasper Mpehongwa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya Mhadhara wa biashara na Masoko uliotolewa na Mkurugenzi Mtendai wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin kwa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu, pembeni yake ni Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa TBL, Emma Urio.
 Waziri wa Mahusiano wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO),Tawi la Moshi akizungumzia namna walivyonufaika na Mhadhara wa biashara na masoko uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL na SABMiler East Africa Roberto Jarrin kwa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu chuoni hapo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na SABMiller East Africa, Roberto Jarrin (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO), Tawi la Moshi mjini, Wilfred Shangali mara baada ya kuhitimisha mhadhara wake wa masuala ya biashara na masoko kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu uliofanyika chuoni hapo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Nchini (TBL) na SABMiller East Africa Roberto Jarrin akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO),Tawi la Moshi Mjini jana, Mkurugenzi huyo alikwenda kutoa Mhadhara wa masuala ya Biashara na Masoko chuoni hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Nchini (TBL) na SABMiller East Africa Roberto Jarrin akitoa Mhadhara wa mauala ya Biashara na Masoko kwa Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara na Elimu wa Mwaka wa kwanza na watatu hawapo pichani katika Chuo Kikuu cha Stefano Moshi (SMMUCO),Tawi la Moshi Mjini

Be Forwards to start importing low cost spare parts

$
0
0
Owners of imported used cars in Tanzania have something to  smile this time around after the Japanese used car exporter, Be Forward, announced the establishment of lower cost dealership of spare parts in all regions in Tanzania.

Be Forward President Hironori Yamakawa announced this in Dar es Salaam yesterday during the climax of the Dar es Salaam International Trade Fair (SabaSaba) at the Nyerere Grounds, Kilwa Road in Dar es Salaam.
Speaking during the press briefing held at the Be Forward Pavilion, Yamakawa said, initially, the company was already established branch in Arusha and will soon establish the Dar es Salaam branch.

He said owners of popular used Japanese cars including Passo, Noah and IST will benefit from the new development, as many were find more difficult to find cheaper spare parts and accessories. “We expect to start importing massive use spare parts to Tanzania at the very affordable prices,” he said.
He said they have tried to visit other dealers of used spare parts and find many were selling as a higher price as he believe that their prices will be affordable and accessible any part of the country.

Be Forward is one of the popular exporters of used car globally and in Tanzania alone, according to Yamakawa, more than 20,000 used vehicle are imported to Tanzania monthly. This makes the annual used cars consignment to Tanzania to hit 240,000 cars annually. He said the plan was to increase the number to 25,000 cars monthly, making Be Forward the leading importers of used Japanese cars.

According to Yakamawa, the company was also looking to contract dealers countrywide, who will be responsible for distributing their products in Tanzania.Meanwhile, Be Forward Company has unveiled Platinum Utra Smooth Driving lubricants in Tanzania market. Speaking during the launch of the product, Hironori Yamakawa, the company President said this is the new product in the market. The new product is for both gasoline and diesel fuel cars engines.

 BeForward President Hironori Yamakawa (Left) holds the newly launched Platinum Ultra Smooth Driving lubricant product during the climax of the Dar es Salaam International Trade Fair (SabaSaba) at the Nyerere Grounds, Kilwa Road in Dar es Salaam. Others right is the company’s marketing officer, Tomohiro Nakamura and Shogo Nishimura (second right).
 Be Forward President Hironori Yamakawa (Right) speaking with journalists when announcing the company plans to open up lower cost dealership of spare parts in all regions in Tanzania, during the climax of the Dar es Salaam International Trade Fair (SabaSaba) at the Nyerere Grounds, Kilwa Road in Dar es Salaam. 

Standard Chartered Bank flops in 5.2tr/- compensation and tariff recalculation case challenged by IPTL

$
0
0

THE Tanzania High Court has dismissed the objections filed by Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited to oppose the suit challenging enforcement of a foreign decision involving recalculation of power tariffs in IPTL and for payments of about 5.3tr/- damages.

Judge Fauz Twaib decided in favour of Independent Power Tanzania Limited (IPTL) and Pan African Power Solution Limited (PAP) after concurring with counter submissions presented by advocate Joseph Makendege, for the two companies.

The judge ruled that all five grounds of objections presented by the Bank, through its counsel Gasper Nyika, were devoid of merits. In its objections, the Bank had alleged that the suit in question was filed without a board resolution from the Tanzanian companies.

Secondly, the Bank had alleged that the suit was time barred in that, it was filed beyond the required time, which is three years from 2005 when the alleged caused of action on the matter arose and that the two companies had no locus standi to institute the proceedings.

The Bank had alleged further that IPTL and PAP were barred from instituting the proceedings in Tanzania since there were others of similar nature that were pending in London. In his ruling, however, Judge Twaib rejected one by one the grounds raised by the Bank.


On board resolution, the judge ruled that the matter was a question of fact which needed to be proved and, thus it could not constitute as a ground of objection as alleged by the Bank. On the time limit, Judge Twaib resolved that the suit was filed within the required time.

Going by the plaint, he noted, there was no delay in filing the suit and that the course of action was renewed following the decision given by the London Court, the International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID).

Regarding the question on locus standi by PAP to take part in the proceedings, the judge ruled that the company has rights to defend following a decision given by the Court under Judge John Utamwa on September 5, 2013, for IPTL affaires to be handed over to PAP.

On whether the two companies were barred from filing the case in Tanzania and that the English Court was proper forum, Judge Twaib ruled that the presence of foreign proceedings does not preclude a party from filing a case of similar nature in the country.

Following the court’s decision, Judge Twaib will now proceed with the next stage in the case, including holding the first pre-trial conference on July 16. The decision which is being challenged in the case was issued by ICSID in February last year.

It is alleged in the suit that SCBH had been falsely representing being a creditor of IPTL and fraudulently procured a decision before the ICSID for, among others orders, recalculation of tariffs payable by Tanzania Electric Supply Company (TANESCO).

In the suit, the two plaintiffs (IPTL and PAP), through legal services of Bulwark Associates Advocates and ASYLA Attorneys, have also sued a Tanzanian advocate Martha Kaveni Renju, as the second defendant for allegedly presenting herself as administrator receiver of IPTL.

Furthermore, the plaintiffs have joined Tanesco in the suit for the purpose of preventing the state owned company from enforcing the ICSID decision or any decision the ICSID may subsequently render in the matter.

The two companies are vehemently opposing the enforcement of the decision in question, which also seeks to recover the bonus amount paid to the provisional liquidator of IPTL when the company was placed under him, on grounds that SCBH procured the same fraudulently.

“Plaintiffs are suing the defendants for declaration that (they) are barred by the Tanzanian law to enforce or domesticate a foreign decision that expressly or effectually unlawfully supersedes, circumvents or varies a validly existing decision of a Tanzanian Court,” reads part of the plaint.

They claim that the impugned ICSID decision was null and void and could not be enforced as it was obtained by the  Bank fraudulently: and that it is excessive, or abusive of jurisdiction of the Tribunal for deciding on matters beyond the scope of the agreement for arbitration giving rise to it.

Such enforcement, the plaintiffs further allege, “Is abuse of the Sovereignty and Territorial Integrity of United Republic of Tanzania as well as the process, independence, powers and integrity of the Tanzanian courts.”

According to the plaint of the suit, the alleged misrepresentation by SCBH and Ms Renju have caused abortion of transactions by the plaintiffs, notably its ambitious mission of converting the Tegeta-Salasala IPTL power plant from using heavy fuel (HoF) fired to duo heavy fuel and gas fired.

In the suit, apart from the monetary damages demanded, the plaintiffs are also asking the court to declare SCHB and Ms Renju are not a creditor and administrator receiver of IPTL, respectively and have, therefore, no claim whatsoever against the plaintiffs.

Ally Nipishe - Wanapepeta ( Official Video )

UTT AMIS YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA 39 NA KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI KWENYE MIFUKO YA PAMOJA KWA WANANCHI

$
0
0
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliono. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.

Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni 237.

Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns).  Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisikiliza na kufurahia maelezo kutoka kwa Bi Martha Mashiku, Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi UTT AMIS(katikati), Kushoto ni bi Sophia Mgaya afisa mwandamizi kitengo cha Tehama na Kulia ni Bi Jesca Swai,  Mhasibu wa Mifuko inayoendeshwa na UTT AMIS

  Hapa ni rahisi tuu!!Afisa Masoko na Uhusiano msaidizi Bw. Waziri Ramadhani akimuelekeza mwekezaji jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga katika moja ya mifuko ya uwekezaji ya UTT AMIS

Tunaweza kuwasaidia kujaza fomu zenu!Bi. Pauline Kasilati na Dorice Mlenge Ofisa wasaidizi wakitoa huduma kwa wawekezaji kwa kuwasaidia kujaza fomu za kujiunga na Mfuko wa Watoto

Bw. Laurian Chokola, Afisa mwendeshaji msaidizi akiwaelekeza wawekezaji kujaza fomu za kujiunga na mifuko baada ya kuwaelimisha faida zinazopatikana kwa kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.

GLOBAL EDUCATION LINK YAVIALIKA VYUO KIKUU VYA SHARDA NA LOVELY PROFESSIONAL VYA INDIA KUSHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyuo vya nje ya nchi kutoka kushoto ni Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional cha Nchini India, Bw. Gulshan Sandh na Bw. Sourabh Chaudhary pamoja na Meneja wa Kanda wa Chuo Kikuu cha Sharda cha nchini India, Bw. Deepak Kaushik mara baada ya kuwakaribisha katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (wa pili toka kulia) akiongea na wageni wake ambao ni viongozi wa vyuo vya nje mara baada ya kuwaalika kushiriki katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Principal Academic Officer wa Chuo cha IFM cha jijini Dar es Salaam akisisitiza jambo  la kielimu wakati alipokutana na viongozi wa vyuo vya nje ya nchi ndani ya ndani ya ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja  vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. 
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>