Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 575 | 576 | (Page 577) | 578 | 579 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Mgeni raism wa Mchezo wa Bonaza la Masauni Cup Khamisi Mbeto akikagua timu ya Mkunazini iliotowa kipigo kwa timu ya Kilimani mabao 2--0. mchezo uliofanyika uwanja wa malindi mnazi mmoja
  Mgeni raism wa Mchezo wa Bonaza la Masauni Cup Khamisi Mbeto akikagua timu ya Kilimani  iliyokubali kipigo cha mabao 2--0.wakati wa mchezo Bonaza unaoendelea katika viwanja vya malindi mnazi mmoja usiku.
  Kikosi cha timu ya Kilimani kinachoshiriki michezo ya Bonaza Masauni Cup inayofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja 
  Kikosi cha timu ya Mkunazini kinachotowa dozo katika michuano ya Bonaza Kombe la Masauni ambocho kimetowa dozi kwa timu ya Kilimani wakati wa mchezo wao wa pili wa Bonaza hilo ikiwa na pointi 4, baada ya kupotoka sare mchezo wao wa fungua dimba na timu ya Miembeni, Timu ya miembeni inaongoza kundi hilo ikiwa na poiti 7
  Mchezaji wa timu ya Kilimani akimpita mchezaji wa timu ya Mkunazini wakati wa mchezo wao wa Bonaza, uliofanyika uwanja wa malindi mnazi mmoja. timu ya Mkunazini imeshinda 2--0.
       Mchezaji wa timu ya Mkunazini akizuiya mpira kujiandaa kumpita mchezaji wa timu ya Kilimani.
  Mchezaji wa Kilimani akijaribu kumpiga chenga mchezaji wa timu ya Mkunazini wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Masauni Cup, linalofanyika uwanja wa Malindi Mnazi Mmoja timu ya Mkunazini imeshinda 2--0 
  Mchezaji wa timu ya Kilimani akimpita mchezaji wa timu ya Mkunazi wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Masauni Cup, linalofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja, timu ya Mkunazini imeshinda 2--0.
  Wapenzi wa mchezo wa Soka Zenj wakifuatilia Bonaza hilo linalofanyika viwabnja vya malindi mnazi mmoja 

  Mchezaji wa timu ya Mkunazini akimpita mchezaji wa timu ya Mkunazi wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Masauni Cup, linalofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja, timu ya Mkunazini imeshinda 2--0.

  0 0

  sh2
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakati wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar ilokutana kupitisha Jina la Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
  sh3
  VIONGOZI wa Meza Kuu wakiwa wamesimama baada ya kuingia katika ukumbi wa Mkutano.SH6
  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kupitisha Jina la Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM. SH7
  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali, akitoa maelezo ya kikao hicho cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar.  
  WAJUMBE wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandua kwa ajili ya kupitisha Jina la Mgombea Nafasi ya Urais wa Zanzibar Dk. Shein.SH5
  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe Kamati Maalum ya CCM Zanzibar baada ya kupitisha Jina lake kuwa  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

  0 0


  Baadhi ya wanalyalamo wakijumuika na watoto wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund.
  .

  baadhi ya wanalyamo family katika picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho, Winfrida Lubanza(mwenye miwani na blauzi nyeusi)

  WITO umetolewa kwa Watanzania nchini kujitolea kwa hali na mali usaidia watu wenye uhitaji ikiwemo watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali. Wito huo umetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo Chanika, jijini Dar es Salam, Winfrida Lubanza wakati akizungumza na wanafalia wa Lyalamo.

  Alisema jamii inapaswa kuwakumbuka na watoto wakuopo katika vituo hivyo kwani wanastahili kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu kama ilivyo kwa watoto waliopo majumbani. "watoto yatima ni watoto km wengine nao wana uhitaji sawa hivyo jamii isiwasahau na kwani nao wanapata furaja na kupata matumaini zaidi,"alisema.Aidha, aliongeza kuwa kituo chake kinakabiliwa na chsnggamoto mbalimbali ikiwemo chakula, madawa, sabuni na ada kwa wanafunzi sambamba na mtaji wa kuwezesha kuanzisha biashara ambayo itaweza kuwapatia pesa za kujikimu.

  "tunachangamoto nyingi mfano kuna mwanafunzi yupo kidato cha nne amerudishwa kituoni sababh hatujakamilisha ada,"alisema.

  Naye kiongozi wa Lyalamo family, Aziza Kibwana alisema wamefarijika kufika kituoni hapo na kuona vhangamoto hivyo watajitahidi kuchangia walichojaaliwa.Pia amesisitiza wadau kujitokeza kusaidia. " Sisi tumesoma shule ya msingi boarding tukiwa wadogo na tulikuwa na watoto kutoka katika vituo kama hivi hivyo tunaguswa sana na hali zao ndio maana tuko hapa," alisema.Aziza aliongeza kwamba kupitia umoja wao watajitahidi kadiri wawezavyo kuvifikia vituo mbambali na kutoa misaada.

  " Humu kuna marais, kuna mawaziri, wabunge, wanasoka, wasanii, wafanyabiashara, madaktari, wahasibu n.k sasa ni muhimu kuwakumbuka na watoto waliopo huku ili kuwajengea misingi mizuri ya kutimiza ndoto zao," aliongeza .Katika ziara yao Lyalamo family walikabidhi kituoni hapo vyakula, mafuta, dawa, madaftari, sabuni na vitu vinginevyo ambapo watoto waliopo kituoni hapo walifurahi na kushukuru.

  Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2001 kinalea watoto kati ya 150 hadi 300 wenye umri wa kuanzia 0 hadi miaka 18.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Askofu Mkuu Wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dkt.Stephen Munga wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 125 ya dayosisi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mbuyukenda mjini Tanga leo(picha na Freddy Maro)ta2
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Askofu Mkuu Wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dkt.Stephen Munga wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 125 ya dayosisi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mbuyukenda mjini Tanga leo.
  ta4
  Kukindi cha Matarumbeta kikitumhuza wakati wa maadhimisho hayo.ta5
  Ibada ya maadhimisho hayo ikiendelea wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 125 ya dayosisi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mbuyukenda mjini Tanga leo.(picha na Freddy Maro)

  0 0


  KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana ilikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea yatima ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia makundi maalumu katika jamii.

  Akikabidhi misaada hiyo katika ofisi zake zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Msama alisema misaada hiyo ni sehemu ya fedha za mauzo ya DVD za Tamasha la Pasaka la mwaka huu.

  Msama alisema kupitia mauzo ya DVD za Tamasha hilo ambalo lilifanyika April 6 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wameona ni vema kuwafariji watoto yatima.

  “Msama Promotions kama kawaida yetu, tumekuwa tukiyakumbuka makundi maalum katika jamii kama yatima, walemavu na wajane, hivyo leo hii tumewasaidia vitu mbalimbali watoto,” alisema Msama.

  Alisema kampuni yake imekuwa ikifanya hivyo sio tu kwa kutambua wajibu wake katika kusaidia jamii, pia kuguswa na mazingira ya watoto hao wanahitaji sapoti ya jamii nzima.

  “Watoto hawa ni kama wengine wanaokula, kunywa na kusaza katika familia zao, hivyo wanahitaji kusaidiwa na jamii nzima
  si jukumu la wenye vituo vya kuwalea tu,” alisisitiza Msama.

  Vituo vilivyonufaika na msaada huo wa jana, ni Chakuama, Maunga Centre, Mwandaliwa, Malaika, Honoratha, Zaidia, Mujahidin, Arahman na Almadina cha Tandale.

  Miongoni mwa vitu hivyo vilivyopokewa jana na viongozi wao, ni unga, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni na vingine vingi kwa kila kituo.

  Msama alisema mwendelezo wa msaada wa kampuni yake utafanyika pia mikoani baada ya uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji wa injili, Bonny Mwaitege utakaofanyika Agosti 2.
                       
  Alisema sehemu ya mapato ya uzinduzi huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Diambond Jubilee, jijini Dar es Salaam, yatanunua baiskeli 100 kwa ajili ya walemavu.

  Aliitaja baadhi ya mikoa itakayokumbukwa safari hii ni Iringa, Morogoro, Tabora, Dodoma, Tabora, Pwani, Mwanza, Mbeya na Singida.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula mtoto Haid Edwin (5) wa kituo cha Yatima cha Honorata cha jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula watoto wa kituo cha Yatima cha Al Madina cha jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanahabari wakijadiliana jambo kwenye tukio hilo  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijini Evarsit Kiwia akitoa maelezo binafsi mbele ya afisa wa tume alipofika kujiandikisha kupitia mfumo mpya wa BVR katika kata ya Old Moshi Magharibi.
  Kiwia akijaza moja ya fomu zinazotakiwa kujazwa wakati wa zoezi a uandikishwaji.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi Vijijini ,Evarist Kiwia akichukuliwa Taswira kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho maalumu kwa ajili ya kupigia kura.
  Kiwia akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo mpya wa BVR.

  Na Dixon Busagaga WA globu ya jamii Kanda ya Kaskazini,Moshi.

  CHAMA cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo la Moshi vijini kimeonesha kuwa na hofu kwa baadhi ya wananchi kushindwa kuandikishwa katika zoezi la uandikishaji kwa kutumia mfumo mpya wa BVR huku kikiiomba tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji kwa wakazi wa maeneo hayo.

  Ombi hilo limekuja kutoka na kuwepo kwa madai ya kuwa baadhi yam ashine hazikuweza kufanya kazi vizuri hali iliyolazimu baadhi ya wananchi kushindwa kujiandikisha.

  Sababu nyingine iliyopelekea ombi hilo ni kuhusu jiografia ya jimbo hilo pamoja na shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na wakazi wa maeno hayo ambao wengi wao wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya kazi ya kilimo na ufugaji hali inayochangia kukosa muda wa kutoka kwenda kupanga foleni kwa ajili ya uandikishwaji.

  Akizungumza mara baada ya kujiandikisha Menyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini ,Ekarist Kiwia alisema kutokana na usumbufu unaotokana na mashine za BVR ni vyema tume ikatizama namna ya kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji.

  “Mimi mwenyewe nimeshindwa kujiandikisha  katika kituo cha Mande Kanisani ambapo ndiko eneo la langu ….nimeenda kitongoji kingine nikapewa ridhaa ya kujiandikisha lakini wako watu wanakosa fursa ya kujiandikisha kutokana na mashine kutofanya kazi vizuri”alisema Kiwia.

  Kiwia ambaye pia ni miongoni mwa watia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chadema ,alisema licha ya uwepo wa changamoto hizo wananchi hawana budi kujitokeza kwa wingi ili kupata kitamburisho cha kupigia kura kitakachosaidia kumpata kiongozi bora wa jimbo hilo.


  Kwa upande wao wananchi wa  kata ya old Moshi Magharibi walisema wamehamosika kujitokeza katika zoezi la uandikishaji,isipikuwa changamoto za mashine za BVR ndio zimekuwa zikiwakatisha tamaa kuendelea kungojea katika foleni.


  Elizabeth  Massawe na Alex Kiwia walisema  kuwa walitakiwa kufanya kijiandikisha katika kituo cha Mande kanisani lakini  kwa siku tatu maofisa katika kituo hicho wanadaiwa kuwajibu wananchi kuwa  mashine ni chafu za kusafisha na kwamba hawana uhakika wa kujiandikisha.

  “Mimi hata nikienda kituo cha jirani hawakubali   kuniandikisha  wanasema nijiandikishie sehmu ninayoishii sehemu ninayokaa ndio hizo mashine hazifanyi kazi mara utaambiwa ni zakusafisha huku muda wameweka kidogo ni wiki moja tuu”alisema Massawe.

  Kiwia alisema utaratibu uliowekwa na tume kuwa watu wajiandikishie shemu ambayo wanatoka  ni mbaya kutokanana kwamba mashine za BVR zinasumbua na hazitabiriki.

  Alisema wananchi wengi watakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura kutokana na kushindwa kujiandikisha na kwamba muda uliopangwa ukiisha wanondoka bila kuandikisha wananchi wote.

  0 0

  IMG_7241

  Pichani ni muonekano wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania ndani ya Karume Hall katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Pichani ni wananchi wakitembelea banda hilo na kupata taarifa mbalimbali za shughuli za Umoja huo nchini Tanzania.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  IMG_7256
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa mwananchi katika picha za viongozi mbalimbali waliowahi kuwa Makatibu wakuu wa Shirika la Umoja Mtaifa duniani ambalo hivi sasa linaongozwa na Ban Ki-Moon.
  IMG_7248
  Pichani juu na chini ni Ismael Mnikite (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
  IMG_7259
  IMG_7264
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati) akifafanua jambo kwa mdau wa Umoja wa Mataifa, Shaweji Steven (kushoto) aliyetaka kujua zaidi kuhusiana na ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika tatizo la ajira za vijana nchini. Kulia ni Emmanuel Johnson kutoka Shirika la Afya (WHO) nchini.

  IMG_7253
  Ismael Mnikite (kulia) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akitoa darasa la Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDG's) yanayotekelezwa na nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi wananchama kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda hilo lililopo Karume Hall katika maonyesho ya Sabsaba.
  IMG_7221
  Emmanuel Johnson (kulia) kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) nchini akitoa maelezo ya ripoti ya UNDAP kwa mdau wa Umoja wa Mataifa, Shaweji Steven alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba lililopo Karume Hall.
  IMG_7213
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) na Salome Mwambinga (wa pili kulia) kutoka (IAEA) wakihudumia wananchi waliotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimu vumbi jijini Dar.
  IMG_7237
  Wananchi wakisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa.
  IMG_7235
  Wananchi wakijichukulia vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu, amesema tangu Umoja huo ulipotoa fursa kwa wananchi wanaotembelea maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya sabasaba kutoa maoni kuhushu utendaji wake hapa nchini mpaka sasa zaidi ya watu 600 wameshiriki kutoa maoni yao.
  Amesema watu waliotoa maoni hapo wametumia njia tofauti ikiwemo mtandao, ujumbe mfupi wa maandishi (sms), njia ya mdomo na kwa kuandika katika fomu maalum zinazopatikana katika banda lao
  Bi. Temu amewashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano pia katika mambo mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa nchini.
  Jinsi ya kuendelea kushiriki kutoa maoni kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055 bila makato yoyote kwenye simu yako.
  Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2

  0 0

  SAM_3481
  Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha  juu ya kushuka kwa ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani duniani anayefatia ni katibu wa shirika hilo Frank Martin ,watatu ni James Mollel katibu tawi laArusha pamoja na Gabriel Simbeye mjumbe(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_3485 katibu wa shirika la Tanzania Audio Visual Works Distributors Frank Martin amebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa na mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development International ya 2011.
  SAM_3493
  Mwandishi wa habari kutoka Daily News Marc Nkwame akiuliza swali 
  SAM_3497
  Jamiiblog ilifanya jitihada za kumtafuta Msanii mkongwe wa filamu hapa Nchini, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’kuzungumzia hali halisi ya kushuka kwa soko la sanaa hapa Nnchini ambapo alisema kuwa hata kampuni za usambazaji  filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa kuwapa waandaaji malipo finyu
  SAM_3499Mmiliki wa Jamiiblog Pamela Mollel akishow love na Msanii mkongwe wa filamu, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado

  Muziki na Filamu zinazorekodiwa nchini zinadaiwa kupoteza umaarufu nchini kiasi cha kusababisha soko lake kuangukia pua, huku waandaaji na wasambazaji wake wengi wakiamua kujitoa na kutafuta shughuli zingine za kufanya.
   
  Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda, pamoja na katibu wa shirika hilo Frank Martin wamelaumu kushuka kwa ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani duniani.
   
  “Tathmini kutoka wasambazaji waliochini ya ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ ambao wanafikia 200 kwa sasa, imeonesha kupungua kwa kazi za Sanaa yaani muziki na filamu kwa asilimia Zaidi ya 50 na hii imesababishwa na kukosekana kwa masoko ya kazi hizo nchini,” alisema Katibu wa chama hicho, Frank Martini.
   
  Wakizungumza jijini hapa wakati wa kikao maalum kati ya wasambazaji na wasanii, viongozi hao wamebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa na mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development International ya 2011.
   
  “Kipindi hicho tulishihudia filamu mpya takriban 10 zikitolewa kila wiki, lakini hali ni tofauti kwa sasa ambapo tunashuhudia chini ya filamu 10 kwa mwezi mzima huku idadi hiyo kwa mwaka ikiwa ni wastani au chini ya sinema 120 tu hii ni kwa mujibu wa rekodi ya wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini kwa mwaka huu wa 2015,” aliongeza Martini.
   
  “Wasambazaji na waandaaji (producers) wa sinema na muziki wameamua kujitoa kwenye tasnia hii na kutafuta shughuli mbadala za kufanya,” alisema mwenyekiti wa taasisi hiyo Baraka Nyanda.
   
  Wakizungumzia muziki wamesema eneo hili ndilo limeathirika Zaidi kwa sababu watu hawanunui tena nyimbo zilizorekodiwa kwenye santuri za CD ambazo ndizo chanzo kikuu cha mapato kwa wasanii na wasambazaji.
   
  “Wasanii wengi wa muziki wamekuwa wakisambaza kazi zao kupitia mitandao kama You-Tube ambako mashabiki wao huzipakua bure, wengine huthubutu hata kugawa CD za nyimbo zao mpya bure kabisa mitaani alimradi kujenga jina tu huku wasambazaji wakikosa kipato,” walisema wasambazaji hao.
   
  Msanii mkongwe wa filamu, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’ amesema kuwa hata kampuni za usambazaji  filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa kuwapa waandaaji malipo finyu; “Hawa wananunua master ya sinema moja mpya kwa shilingi milioni 10 tu, ambazo utakuta ndio gharama za ktengenezea filamu sasa hapo unabaki na nini?” aliuliza.
   
  Kwa mujibu wa Rado, maadam wasambazaji wameamua kiwango cha kununua sinema mpya ni milioni 10, basi watengenezaji huamua kulipua kazi zao kwa kuwatumia waigizaji rahisi na maprodyuza kwa kuokoteza alimradi tu kupunguza gharama za uandaaji ili mwisho wa siku wapate faida.
   
  Lakini kwa mwenzake, Hussein Rajab Usichonge, tatizo ni kwamba wasanii chipukizi hawathaminiwi na matokeo yake tasnia inakosa vitu vipya; “Wao wanaangalia ma-super star tu, ingawa wengi wamechoka na wamekosa ubunifu, sisi chipukizi ndio tungeleta mabadiliko lakini tunabaniwa,” alisema.

  0 0

   Banda la Mfuko wa  Pensheni  wa LAPF liloko katika kiwanja cha Mwl. Nyerere kwenye    maonyesho ya Sabasaba 2015. LAPF ipo banda namba 22  karibu na banda CELLO na SIDO mkabala na banda la Elimu
     Mwanachama wa LAPF akifurahia kupatiwa Taarifa ya michango yake ambayo ni mmoja ya huduma utakayoipata kwenye banda la LAPF ukitembelea banda hilo

   Wanachama na wageni waliotembelea banda la LAPF wakipata fursa ya kujiandikisha kwenye mfumo wa uchangia wa hiari, kupata vitambulisho, pamoja na kupata fursa ya kuona taarifa za michango yao hapo hapo.

     Mwanachama akiandika maoni yake kwa jinsi alivyofurahishwa na huduma kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

  1.      Karibu katika banda la Mfuko wa Pensheni wa LAPF, mfuko bora wa Pensheni Tanzania uweze kupata elimu kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania yaani tumetoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi pamoja na huduma zinazopatikana kutoka LAPF.


  0 0

  Meya wa Ilala, Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo. Pamoja nae ni Mbunge wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa NEC wa CCM,
  Diwani wa  kata ya  Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa akihutubia wananchi katika uwanja wa shule ya msingi kitunda mwishoni mwa wiki ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na kukamilisha ahadi mbalimbali alizokuwa amezitoa.
  Mmoja wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya wenzake  kutoka kwa Meya wa Manispaa ya ilala  ambazo alikuwa amewaahidi wakati wa mkutano wa  Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
  Baadhi ya madiwani na wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya Jerry Slaa kwa kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga
   Watoto wakitoa burudani wakati wa mkutano huo
   Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba ya Meya Jerry Slaa
  Baadhi ya madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.

  0 0


  Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel akiongea na Mwanafunzi ambae aliambatana na wazazi wake (kulia) kupata huduma ya vyuo vya nje ya nchi katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Bw. Sourabh Chaudhary ambaye Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely cha nchini India na
  Afisa Masoko wa GEL, Bi. Regina Lema.  PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
  Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel akiongea na wanafunzi ambao waliambatana na wazazi wao (kulia) kupata huduma ya vyuo vya nje ya nchi katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Mejena Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely cha nchini India, Bw. Sourabh Chaudhary akitoa ufafanuzi wa kina juu ya huduma zinazotolewa na chuo chao.

   
  Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bi. Regina Lema akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Msimamizi wa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Haroun Weggoro akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bi. Jacquline Mbise akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Makungu Joseph akiwa na Mhasibu wa GEL, Bw. Ramadhani Ngereza wakiwasikiliza wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Kanda wa Chuo Kikuu cha Sharda cha nchini India, Bw. Deepak Kaushik akitoa maelezo machache kwa wateja waliotembelea ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional cha Nchini India, Bw. Gulshan Sandhu akiongea na Principal Academic Officer wa Chuo cha IFM cha jijini Dar es Salaam mara baada ya kukutana nae ndani ya ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

  Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bi. Saada Selemani akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Afisa anayeshughulikia Pasipoti na Visa kwa wanafunzi wanaosafiri nje ya nchi, Bw. Emmanuel Mbena akimsimamia mmoja ya wanafunzi kujaza fomu  kwa ajili ya maombi ya kupata pasipoti ili aweze kusafiki kwenda masomoni.
   Secretary wa GEL, Bi. Zamda Mwinyiheri akiwapokea wageni na kuwapa kitabu cha kujiandikisha wageni waliotembelea ofisi zao zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Mhasibu wa GEL, Bw. Ramadhani Ngeleza akimuelezea mteja wanavyotoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya nje katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Wageni wakitoka ndani ya ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  ---
  Wazazi na wanafunzi waliotembelea Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi wamefurahishwa na huduma zao wa kuwapatia vyuo bora vilivyokidhi viwango vya kimataifa.

  Akizungumza mmoja ya wazazi mara baada ya kufika ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wamesema wamefurahishwa na mapokezi ikiwemo vijana wenye kujituma kutoa huduma bora zinazomfanya mzazi anayefika na mtoto wake apate maelezo ya kina.

  "Nikiwa kama mzazi niliyefika GEL kujipatia huduma ya chuo kikuu cha nje ya nchi, nimefurahishwa na huduma wanazotoa kwa vile zinakidhi viwango vya kimataifa zinamfanya mzazi anapotoa atambue mwanae pindi anapomaliza shule ya sekondari asome nini," Alisema mmoja ya wazazi aliyefika.

  Mzazi huyo aliongeza kuwa wakati akifika ofisi hizo hakuwa anajua mwanae asome nini atakapomaliza shule ya sekondari ilia baada ya kufika ametoka na mawazo mapya yatakavyomjengea uwezo mwanae afanye vizuri zaidi.

  0 0

   Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Bi. Agnes Kaganda (wa kwanza kushoto) sambamba na mmoja wa maofisa wa benki hiyo wakitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki hiyo kwa mteja (aliyebeba mtoto) aliyetembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam-Saba saba mwishoni mwa juma lililopita.
  Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania (katikati)  wakifurahia moja ya zawadi kutoka benki hiyo walipotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya Biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam –Sabasaba. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Matawi ya Benki hiyo Bi. Elizabeth Mayengoh (wa kwanza kushoto).

  Benki ya Exim  yajivunia  mafaniko maonyesho ya Saba saba.
  USHIRIKI wa benki ya Exim kwenye maonyesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam umeonyesha mafanikio makubwa ambapo pamoja na fursa nyingine benki hiyo pia imefanikiwa kusogeza huduma zake karibu kwa wateja wake wanaoshiriki na kuhudhuria maonyesho hayo.

  Mbali na kutoa ushauri wa kibenki kwa washiriki na wateja wanaotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo, benki hiyo pia imeweka mashine ya ATM inayotembea jirani na banda hilo ili kuwapunguzia hadha ya kubeba kiasi kikubwa cha fedha wateja wake wanaofanya manunuzi kwenye maonyesho hayo sambamba na kujali usalama wa pesa zao.

  Akizungumza na waandishi wa habari  kwenye maonyesho hayo mwishoni mwa juma lililopita, Mkuu wa Matawi ya Benki hiyo, Bi. Agnes Kaganda alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa weledi wa hali ya juu na maofisa wa benki hiyo wanaohakikisha  kila mteja anaetembelea banda hilo anaondoka  na uelewa wa kutosha kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo.

  “Tumekuwa tukipokea wateja na wageni wengi sana wanaohitaji maelezo ya huduma zetu mbalimbali na kwa kweli pia tumefanikiwa kupata wateja wengi ambao wamefungua akaunti zao…kifupi washiriki wengi wameonyesha kuridhishwa na huduma zetu,’’ alibainisha.

  Kwa mujibu wa Bi. Kaganda mbali na huduma nyingine wateja wengi waliotembelea banda la benki hiyo wamekuwa wakipewa maelezo ya kutosha na faida kuhusu matumizi na usalama wa kadi za kutolea fedha za FAIDA zinazotolewa na benki hiyo.

  “Pia tumekuwa tukiwahamasisha wateja na washiriki wanaotutembelea hapa kuhusu umuhimu wa wao kufungua akaunti ya amana (fixed deposit account)ambapo kwa sasa tunaendelea na kampeni ya kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni kuweka akiba,’’ alibainisha Bi. Kaganda.

  0 0

  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimia na Bw. Adam Mayingu (wa tatu kutoka kushoto) na Maafisa wengine wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo katika Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
  Mheshimiwa Shaaban Lila Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akimsikiliza kwa makini Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi.Rahma Ngassa alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya 39 ya kibiashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
  Mheshimiwa Ombeni Sefue, katibu Mkuu Kiongozi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 39 ya kibiashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Magira Werema akitoa maelezo wa wateja waliotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 39 ya kibiashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
  Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF akitoa maelezo kwa wateja wateja waliotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 39 ya kibiashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais Dr Jakaya Kikwete akipata  maelezo ya  bidhaa  za Asas Daireis Ltd  kutoka kwa afisa masoko  wa kampuni  hiyo  Bw Jimy  alipotembelea  mabanda mbali mbali  katika  maonyesho ya  sikukuu ya   sabasaba yanayotaraji  kuhitimishwa kesho jijini Dar es salaam
  Rais  Dr  Kikwete  akipata  maelezo ya  bidhaa za Asas Daireis Ltd kampuni  hii  ni  ndio kampuni bora ya  usindikaji maziwa nchini Tanzania kwa miaka mitatu  mfululizo sasa
  Rais  Dr  Kikwete  akitazama  baadhi ya  bidhaa zenye ubora  za kampuni ya Asas Daireis Ltd
  Rais  Dr  Kikwete  akifurahia  baada ya  kutembelea  banda ya Asas DaireisLtd jijini Dar es Salaam
  Wananchi mbali mbali  wakitembelea  banda  ya Maziwa ya  Asas katika  viwanja  wa Sabasaba jijini Dar es Salaam
  Na MatukiodaimaBlog
  BANDA la  kampuni ya maziwa ya  Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa lililopo  limeendelea  kuwavuta  wananchi   na  viongozi mbali mbali  wanaotembelea  viwanja  wa  Saba saba jijini Dar e Salaam  kulitembelea  kupata  bidhaa  zake 
  Banda   hilo  ambalo  wiki  iliyopita  lilitembelewa na Rais Dr  Jakaya  Kikwete na  viongozio  mbali mbali  limeendelea  kuvutia  wananchi  wengi  wanaotembelea maonyesho  hayo  kupenda  kufika  kupata  bidhaa mbali mbali  .
  Baadhi ya  wananchi  waliofika katika  banda   hilo  walisema  kuwa  wamevutiwa  zaidi ya  bidhaa  zenye  ubora  zinazotengenezwa na kampuni hiyo ya  Asas Dairies  Ltd kutoka mkoani  Iringa na   hivyo kulazimika  kumiminika  zaidi  kupata  bidhaa pamoja na kupata  elimu mbali mbali ya  ubora  wa  bidhaa  hizo .
  Alisema Amina  Athuman  ambae ni mmoja wa  wateja  waliofika katika banda   hilo kupata  bidhaa  mbali mbali , kuwa yapo makampuni  mengi ya maziwa ila ubora  wa bidhaa  za maziwa  zinazotengenezwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd  ndizo  ambazo  zinawavutia  watu wengi  zaidi  kufika katika banda  hilo.
  " Mimi  nilikuwa nasikia tu juu ya ubora  wa maziwa  haya toka mkoani Iringa ila baada ya  kufika hapa  nimeshuhudia na  kuanzia  leo  sihitaji maziwa na  bidhaa nyingine kama  hizi  nje ya Asas Dairies Ltd " 
  Huku John Mwene  akieleza  kufurahishwa  zaidi na hatua  ya  Rais wa nchi Dr  Kikwete  kutembelea  mabanda  ya  wakulima mbali mbali  likiwemo  banda  hilo la Asas kwani ni ukweli  usiopingika kuwa kwa  Tanzania kampuni  hiyo ya  Asas Dairies  Ltd imeonyesha  uwezo  mkubwa wa kuzifanya bidhaa zake  kuendelea  kuwa na ubora  kwa miaka  mitatu mfululizo.
  Kwani  alisema kampuni  kuongoza  miaka mitatu  mfululizo ni jambo la  kujipongeza na kuwa  si rahisi  kwa kampuni kushikilia ubora  wake kwa miaka miwili mfulilizo ila kampuni hiyo imeweza kufanya  hivyo .
  Alisema ni jambo la nchi kupitia bodi ya maziwa  na wizara   husika kuangalia  kutoa uwezeshaji  zaidi kwa makampuni bora  ili  kuwezesha  bidhaa zake  kuingizwa katika  soko la dunia . 
  Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu pamoja na kumpongeza Rais Dr Kikwete kwa  kutembelea  banda  lao na kupongeza kwa ushiriki na ubora  wa bidhaa  zao bado  aliwashukuru  wananchi  wanaoendelea  kutembelea banda  hilo .
  Alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuonyesha  ushiriki mzuri katika maonyesho  hayo ya saba saba bado  wamekuwa  wakishiriki maonyesho mbali mbali yakiwemo yale ya nane nane kwa kushiriki katika kanda mbali mbali na  kuwataka  wananchi wa kanda  zote  nchini kujipanga kwa ajili ya kutembelea mabanda yao wakati wa nane nane mwaka  huu .
  Kuhusu kuendelea  kuongoza kwa  ubora  alisema  kuwa hivi  sasa ni  mwaka  wa tatu mfululizo bado  bidhaa  zao  nyingine  zimeendelea  kushinda medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni  hiyo katika ubora .


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa tamasha la kupinga na kukataa vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, lililofanyika katika viwanja vya mnara wa Mashujaa Mpwapwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Anthony Mavunde (kushoto) akizungumza jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Jacob Erasto Chimeledya wakati wa maadhimisho hayo ya kupinga na kukataa vitendo vcya ukatili kwa watoto.
   Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Anthony Mavunde akizungumza
   Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Jacob Erasto  Chimeledya akizungumza katika hadhara hiyo.
   Burudani mbalimbali zilitolewa na vikundi kwa kwaya.
   Meza kuu ikifuatilia burudani hizo.

  Watoto nao walitoa burudani.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Julai 6, 2015. Picha na OMR
  mo2
  ‘WAGOMBEA WANAPOKUTANA’,  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa Urais kupitia CCM, akizungumza jambo na mgombea mwenzake,  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount  Meru jijini Arusha. Picha na OMR
  mo3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Julai 6, 2015. Picha na OMR
  mo5
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal wakati akihutubia. Picha na OMR
  mo6
  Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kufungua Kongamano hilo. Picha na OMR
  mo7
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal wakati akihutubia. Picha na OMR
  mo8
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal wakati akihutubia. Picha na OMR
  mo9mo10
  Meza Kuu
  mo11
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya kufungua rasmi, leo jijini Arusha. Picha na OMR
  mo12
  ‘WAGOMBEA WANAPOKUTANA’ Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa Urais kupitia CCM, akifurahia jambo na mgombea mwenzake,  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount  Meru jijini Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa ARIPO, Otafiire Kahindi. Picha na OMR

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Finca, Edward Greenwood akizungumza mara baada ya kufutali mwishoni mwa wiki baada ya kujua umhimu wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani na kufuturu na waislamu waliofunga.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar  es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza mara baada ya kufutari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Finca, Edward Greenwood akizungumza na
  Sheikh wa Mkoawa Dar  es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum wakati wakifuturu mwishoni mwa wiki.
    Baadhi wa waumini wa dini ya Kiislam wakifuturu katika mwenzi Mtukufu wa Ramadhani jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki

  BENKI ya  Finca kwakutambua mchango kwa jamii wanayoihudumia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani wammeamua kufuturu na wakazi na wateja wa benki hiyo.
  Akizungumza baada yakufuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Finca, Edward Greenwood amesema wanatambua umuhimu katika mwezi huu kuwa wanawajibu kufuru na watu iliwaendelee kupata baraka yakuendelea kukua kwa benki hiyo.

  Amesema kama benki itaendelea kutoahuduma kwani imekuwa ikikua kwa kasi tangu kuanza kama taasisi yamikopo na kuweza kufikia benki ni kutokana na jamii kutambua mchango wake ambapo imetimiza miaka 18  tangu ilipoanzishwa mwaka 1998.

  “Mafanikio haya ya Finca ni kutokana na mchangowenu ,maoni na ushirikiano wenu bilahivyo tusingewezakufika hapa tulipo”amesema Greenwood.

  Nae Sheikh wa Mkoawa Dar  es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum amesema benki imetambua umuhimu katika mwezi mtukufu kwakutoa sehemu yakufuturisha kwakile wanachokipata.

  Benki ya Finca yawatu inayosikilizana kumdhamini kila mtanzania, tunawaahidi kuendelea kutoahuduma bora.

  0 0

   Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza katika mkutano wa madiwani wa manispaa ya Ilala uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Anartogolo jijini Dar es Salaam jana.
   Madiwani wa Manispaa ya Ilala wakiwa katika baraza la kuvunja baraza lao jana katika ukumbi wa mikutano wa Anartogolo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikiristo na Dini ya Kiislam wakifuatilia mkutano wa kuvunjwa kwa baraza la madiwani wa Manispaa ya ilala katika ukumbi wa mikutano wa Anartogolo jijini Dar es Salaam jana.
   Diwani wa Jimbo la Segerea wa Chama  CHADEMA, Azurly Mwambagi akizungumza katika mkutano wa kuvujwa kwa baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Anartogolo jijini Dar es Salaam jana.
  Diwani wa Jimbo la Jangwani wa chama cha CCM, Abuu Jumaa akizungumza katika mkutano wa kuvujwa kwa baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Anartogolo jijini Dar es Salaam jana.(PICHA NA AVILA KAKINGO)_

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Takwimu nchini Dr Albina Chuwa akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha katika mafunzo ya siku tano  kuhusu suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili ,Mafunzo hayo yameudhuriwa  na viongozi kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  (Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
  SAM_3677
  Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja.
  SAM_3680
  Mkuu wa kitengo cha takwimu katika Umoja wa Mataifa, Reena Shah amesema idara yake ina mkakati maalum wa kusaidia nchi hizo katika ukusanyaji wa takwimu za mazingira ambazo kwa sasa ni muhimu sana katika kuweka ajenda na mipango ya maendeleo endelevu.
  SAM_3689
  Mkurugenzi wa Takwimu Nchini Burundi Mohamed Feruz akizungumza na vyombo vya habari kuhusu takwimu katika nchi yake
  SAM_3671
  Washiriki wakifwatilia mafunzo kwa ukaribu zaidi
  SAM_3670
  Washiriki wa mafunzo ya Takwimu kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
  SAM_3672
  Meneja wa idara ya Takwimu Mkoani Arusha Margeret Mutaleba  akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha
  SAM_3669
  Prof.Innocent Ngalinda akizungumza katika mafunzo hayo.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Takwimu nchini Dr Albina Chuwa amesema kuwa suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili bado ni ngeni katika nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika na kwamba kuna umuhimu wa kutoa mafunzo maalum kwa wafanyakazi wa idara za takwimu nchini.

  Aliyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki jijini Arusha uliohudhuriwa na viongozi wa Takwimu wa nchi hizi.

  Bi.Chuwa alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia hali ya tabia nchi na mazingira huku akisisitiza kuwa Takwimu za mazingira zinahitaji watu wawe na uwezo mkubwa yaani elimu pamoja na rasilimali fedha na vifaa huku akitoa rai kwa Jumuiya ya Afrika mashariki kuangalia tasnia hiyo kwa kupewa kipaumbele kama sekta zingine.

  Naye mkuu wa kitengo cha takwimu katika Umoja wa Mataifa, Reena Shah amesema idara yake ina mkakati maalum wa kusaidia nchi hizo katika ukusanyaji wa takwimu za mazingira ambazo kwa sasa ni muhimu sana katika kuweka ajenda na mipango ya maendeleo endelevu.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Takwimu nchini Burundi Mohamed Feruz alisema kuwa katika nchi yake bado hawajaweza kuwa na vifaa vya kisasa vya kuweka kumbukumbu
  “Hatujapata mafunzo ya namna ya kufanya hizi takwimu kwa ufasaha bado ni changamoto kwetu”alisema Feruz

  0 0

  MSTAHIKI Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni. 
  Mstahiki  Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa. 
  Meya  Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya Kinondoni tu, na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao. 
  “Tumeamua kulifanya soko hili ili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda. 
   Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.
  Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akitoa maelekezo kwa  watendaji wa soko hilo  wakati akagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.
  Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hio wakikagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.

older | 1 | .... | 575 | 576 | (Page 577) | 578 | 579 | .... | 1903 | newer