Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal aweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya ttcl chake chake-pemba

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Julai 3,2015 Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, Wilayani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba, leo.
 Baadhi ya wawakilishi wa makampuni na Mashirika waliohudhuria hafla hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu ramani ya Jengo hilo la TTCL, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya 'Quality Buildin Contractors Ltd', Khamis Ally Shaibu,  wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Jengo jipya la Ofisi ya TTCL,  iliyofanyika leo Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.

DCB BENKI WATOA HISA KWA MAKAMPUNI MBALIMBALI

0
0
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa DCB Balozi Paul Rupia akitoa nasaha zake kwa wanahisa wa DCB benki waliohudhulia katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa  DCB benki, Edmund Mkwawa akizungumza na wadau wa hisa katika mkutano uliokutanisha wadau wa hisa ikiwa kwa kipindi chote cha miaka 13 benki hiyo imepiga hatua na kuwa na matawi 8 Dar es salaam na mawakala 113 katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaa jana.
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa DCB Balozi Paul Rupia akimpa hundi Afisa Mkufunzi na UTT management & Investor service PLC, Ligwa Temela katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

PINDA AALIKWA FUTARI YA KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI WA DAR ES SLAM NA MWANZA

0
0
tu2
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda   akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kamati za Amani za mikoa ya Dar es salaam na Mwanza walioshiki katika futari iliyoandaliwa na Kamatiya Amaniya mkoa wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Karimjee Juni 3, 2015. tu3
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda   akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kamati za Amani za mikoa ya Dar es salaam na Mwanza walioshiki katika futari iliyoandaliwa na Kamatiya Amaniya mkoa wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Karimjee Juni 3, 2015. tu1
Mke wa Waziri Mkuu , Mama   Tunu Pinda wapili kulia) akizungumza na baadhi ya wnawake walioshiriki katika  futari iliyoandaliwa na Kamatiya Amani ya mkoa wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Karimjee Juni 3, 2015. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikuwa mgeni rasmi katika futari hiyo. Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza pia walialikwa katika futari hiyo.tu4
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es slaan Julai 3, 2013ambapo mgemoi rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Viongozi wa kamati ya Amani ya mkoa wa Mwanza pia walialikwa kwenye futari hiyo. tu5
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda   akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kamati za Amani za mikoa ya Dar es salaam na Mwanza walioshiki katika futari iliyoandaliwa na Kamatiya Amaniya mkoa wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Karimjee Juni 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA

0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Ndugu Sabetha Mwambenja mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 3.7.2015.
s2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndugu Jacqueline Maleko mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya Sabasaba kwenye Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tarehe 3.7.2015.
s3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TANTRADE, Ndugu Edwin Rutageruka wakati alipowasili kwenye viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo uliofanya na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 3.5.2015.
s4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Anna Mkapa kutembelea banda la Taasisi yake ya Fursa Sawa kwa wote (EOTF) mara baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kufungua rasmi maonesho hayo tarehe 3.7.2015.
s5
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mwenyeji wake Mama Anna Mkapa wakiangalia bidhaa mbalimbali za akina mama wajasiriamali kutoka mikoa ya hapa nchini. Akina mama hao wanaratibiwa na Taasisi ya Fursa Sawa kwa Wote inayoongozwa na Mama Anna Mkapa.
s6
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwa na Mama Anna Mkapa wakifurahia bidhaa za vikapu zilizotengenezwa na akina mama wajasiriamali kutoka mkoani Singida kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika Dar es Salaam
s7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya bidhaa mbalimbali za asili wakati alipotembelea banda la Fursa Sawa Kwa Wote kwenye Maonesho ya Sabasaba tarehe 3.7.2015. Kulia kwa Mama Salma ni Mama Anna Mkapa akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema.

BASATA YAMJULIA MSANII BANZA STONE ANAYEUMWA

0
0
Timu ya watendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bi. Vivian Nsao Shalua mapema jana imemtembelea Msanii na mwimbaji wa muziki wa Bendi ndugu Ramadhan Masanja ‘Banza Stone” ambaye kwa muda sasa amekuwa akiugua nyumbani kwao maeneo ya Sinza  Jijini Dar es Salaam.
Lengo la ziara hii ilikuwa kumjulia hali Msanii huyu mahiri wa Bendi na kushauriana na familia yake juu ya namna bora ya kusaidia matibabu yake na kuhakikisha anapata huduma zote stahiki kulingana na maelekezo ya daktari wake.
Katika ziara hiyo, watendaji hao wakiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment (ASET) Mama Asha Baraka walipata wasaa wa kufanya mazungumzo na familia ya mwanamuziki huyo ili kupata maendeleo ya afya yake, matibabu na mwenendo wake.
Wanafamilia hao wa Msanii Banza Stone wakiongozwa na Kaka yake Khamis Ally Masanja walieleza kwamba hali ya mgonjwa huyo imekuwa ikibadilika mara kwa mara na kwamba amekuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Sinza iliyoko Sinza Palestina jijini Dar es Salaam. Aidha amekuwa akipelekwa hospitali mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ya Mwananyamala ambayo anaendelea kutibiwa kwa sasa.
Baada ya kupata taarifa ya kina kuhusu afya ya msanii Banza Stone, watendaji wa BASATA kwa kushauriana na wanafamilia hao walifunga ziara kwenda hospitali ya Sinza ambayo pia amekuwa akitibiwa na kufanya utaratibu wa matibabu ili kuhakikisha anapewa huduma stahiki na kuhakikisha afya yake inaimarika.
Akizungumza hospitalini hapo Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bi. Shalua alitoa wito kwa wadau wa Sanaa na wasanii kwa ujumla kumwombea msanii Banza Stone na kujitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha anarejea katika hali yake ya zamani na hatimaye kurudi kwenye Majukwaa ya maonesho.
“Wadau wa Sanaaa tumwombee na kumpa msaada stahiki msanii wetu. Msanii huyu ni muhimu kwenye tasnia ya muziki wa dansi. Amechangia sana katika kukuza muziki huu ndani na nje ya nchi. Tumwombee ili arudi katika hali yake ya awali” amesisitiza Bi. Shalua.  

BALOZI WA ARGENTINA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Argentina nchini Tanzania Mhe.Bibianna Lucila Johnes ikulu jijini Dar es Salaam .ag2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiakiwa katika mazungumzo na balozi mpya wa Argentina nchini Tanzania Mhe.Bibianna Lucila Johnes baada ya kupokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi huyo  ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Freddy Maro)

JIPATIE VITABU VYA SHIGONGO SABASABA

0
0

NSSF WAIBUKA WASHINDI WA JUMLA MAONYESHO YA SABASABA

0
0
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya Biashara ya 39 ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Jacquline Maleko. 
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya Biashara ya 39 ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Jacquline Maleko. 
Picha ya Pamoja.
Maofisa wa NSSF wakifurahia tuzo walizopata baada ya kuwa washindi wa jumla katika maonyesho ya Sabasaba.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika maonyesho ya Sabasaba. 
Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho ya Sabasaba pamoja na utoaji wa tuzo kwa washindi ambapo NSSF waliibuka washindiwa jumla.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo pamoja na utoaji wa tuzo kwa washindi.
Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kulia) akiwa na baadhi ya maofisa wa NSSF wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya Sabasaba pamoja na utoaji wa tuzo kwa washindi ambapo NSSF waliibuka washindi wa jumla katika maonyesho hayo.

Angalia Kipindi Chote Cha ' Nyumbani Na Diaspora' Kwenye TBC1..

0
0

UMOJA WA MATAIFA WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UHABARISHAJI NA UTOAJI ELIMU KWENYE TUZO ZA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

0
0
DSC_0178
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkadhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) cheti na tuzo katika kipengele cha Uelimishaji bora kupitia Uandishi wa machapisho na mpangilio bora wa maonyesho, baada ya Umoja wa Mataifa kuibuka mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yalipozinduliwa rasmi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Abdallah Kigoda (kulia).
DSC_0179FullSizeRender_2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaohudumia banda hilo kwenye maonyesho ya Sabasaba wakisheherekea mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
UN Tanzania inawakaribisha Watanzania wote wanaotembela maonyesho sabasaba kufika katika banda lao lililopo Karume Hall na kuweza kushiriki kutoka maoni ya juu ya utendaji wa kazi za Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya mtandao wa simu yako bila kutozwa malipo yoyote ukitumia huduma hiyo, kwa wateja wote mitandao ya Airtel, Tigo na Vodacom.

Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja kupitia mtandao (Online) bofya link hii http://gpl.cc/UN2

FullSizeRender

UMITASHUMTA changamoto

0
0
 Meneja mauzo wa Isere Sports, Rasul Ndee akionesha aina ya mipira inayofaa kuchezewa katikaviwanja mbalimbali hapa nchini
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere, Abbas Ally akionesha ainaya viatu vinavyofaa katika viwanja mbalimbali nchini 

MASHINDANO ya Umoja wa Michezo na Taaluma wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) umemalizika mjini Mwanza huku ikiacha changamoto kwa Serikali kushirikisha wadau kufufua na kuendeleza vipaji.

Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally ambao ni wauzaji wa vifaa michezo nchini aliyekuwa shuhuda wa michezo hiyo Mwanza alisema Tanzania imejaa vijana wenye vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa.

Alisema mikoa mingi imetia fora katika michezo hiyo ikiwemo mkoa wa Manyara,Singida na Mara ambako kujitokeza vijana wengi kupenda mchezo wa riadha na walifanya vizuri katika michezo hiyo.

Meneja wa timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally alisema mikoa mingi ilijiandaa kwa mashindano hayo lakini kuna tatizo la waamuzi ambao walionesha upendeleo kwa timu za Kanda ya Ziwa.

Alkisema mkoa wa Dar es Salaam uliochukua ushindi wa jumla kwa kutwaa medali  26 ilijikuta inafungwa katika mchezo wa soka baada ya kupachikwa bao 1-0 na wenyeji Mwanza.

Ofisa Michezo Mkoa wa Morogoro, Neema Msita alisema kama vipaji vilivyoneshwa katika michezo ya mwaka huu vitaendelezwa Tanzania itarudisha heshima katika michezo kimataifa.

Alisema alitoa witokwa klabu zote kuanzisha timu za watotoambazozitalea vipaji kutokahatuaya shule za msingi, Sekondari na Vyuoni kwa vile Tanzania imejaliwakuwa na vipaji katika michezo yote.

Mtangazaji wa TBC Taifa, Jesse John aliyeshuhudiaufungaji wa mashindanohayo alisema kama kauli ya Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa ya kuwa wizara yake itasaidiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ukuzaji wa elimu sambamba na michezo utafanyiwa kazi hakuna timu ya taifa yaTanzania itakayotolewa katika mashindano kirahisi.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANYAKUA KOMBE KWENYE MAONESHO YA SABASABA

0
0
Washiriki katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia kombe na cheti mara baada  ya  Wizara  hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la   Wizara na Wakala wa Serikali kwa mwaka 2015 katika Maonesho ya Kimataifa ya  Sabasaba ( Dar es Slaam International Trade Fair (DITF) yanayoendelea katika viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.ni2
Washiriki katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia kombe na cheti mara baada  ya  Wizara  hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la   Wizara na Wakala wa Serikali kwa mwaka 2015 katika Maonesho ya Kimataifa ya  Sabasaba ( Dar es Slaam International Trade Fair (DITF) yanayoendelea katika viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.ni3
Washiriki katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini kutoka Mgodi wa  Dhahabu wa Geita (GGM)  wakiwa katika picha ya pamoja na kombe pamoja na cheti cha ushindi.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete Afungua kikao cha kuipitia Ilani ya Uchaguzi wa 2015, mjini Dodoma leo

0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha kitabu ya Rasimu ya Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakati wa Kikao cha Kamati Kuu cha kuijadili na kuipitisha Ilani hiyo kinachofanyika, leo Julai 4, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakipitia Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakati wa Kikao cha Kamati Kuu cha kuijadili na kuipitisha Ilani hiyo kinachofanyika, leo Julai 4, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza wakati akimuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua Kikao cha Kamati Kuu cha kuijadili na kuipitisha Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kinachofanyika, leo Julai 4, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma. Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg. Phillip Mangula.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa kwenye Kikao hicho.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA TANO YA KUHIFADHI QUR-AN TUKUFU YALIYOANDALIWA NA TAASISI YA ISTIQAAMA, JIJINI DAR.

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama,  iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheki ya Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu 30, wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa mashindano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama Ilala jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. SAID MECK SADICK ASHIRIKI KAMPENI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER, LEADERS CLUB LEO

0
0



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadick akizindua kampeni ya kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani ( MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Nd.Assah Mwambene akikabidhi kiasi cha fedha kwa Mmoja wa Waratibu wa MEDIA CAR WASH FOR CANCER Bwa.Benjamin Thomson,zilizochangwa na Idara hiyo kupitia chama chao cha Maofisa Habari wa Serikali ,walijitolea kuchanga kiasi cha shilingi Milioni 1,680,000=.Pichani kati anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda

Kama vile haitoshi nayo Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia walifanikisha kuchangia kiasi cha shilingi 1,350,000/= kufuatia kuguswa kwa namna moja nyingine kwa kampeni  hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani.

Mbali ya fedha hizo kupatikana pia walijitokeza watu mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER,ambalo kwa kiasi kikubwa bado linahitaji kuongeza hamasa zaidi ili wadau wazidi kujitokeza na kuchangia.

Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha,huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mh Meck  Sadick.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiendelea Kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika MEDIA CAR WASH FOR CANCER. Ikiwa ni kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari wakati wa  Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Ankali Issa Michuzi wa Libeneke la Michuzi Blog na Michuzi Media Group na Mwana TBN  akiwa Bizeee... Anaosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangie waandishi wa habari ambao wanamaradhi ya Saratani
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Assah Mwambene akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi zima la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Picha ya pamoja ya waandishi wa Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi 

Unaweza Changia pia kupitia M-Pesa 0766 970240
au Tigo Pesa 0653 155 808.


TTCL Yakuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Waziri Mkuu Atembelea Banda Lao

0
0
Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwapongeza washiriki kwa kubuni  huduma mbalimbali katika Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam Bw. Karim Bablia. Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwapongeza washiriki kwa kubuni huduma mbalimbali katika Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam Bw. Karim Bablia.Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Veronica Ngusaru (kushoto) kuhusu faida mbalimbali za kutumia mtandao wa TTCL ndani ya banda la kampuni hiyo alipotembelea Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Veronica Ngusaru (kushoto) kuhusu faida mbalimbali za kutumia mtandao wa TTCL ndani ya banda la kampuni hiyo alipotembelea Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Jotham Lujava (katikati) akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazooneshwa na kampuni hiyo. Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Jotham Lujava (katikati) akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazooneshwa na kampuni hiyo.Picha ya pamoja ya maofisa wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Picha ya pamoja ya maofisa wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services yafutulisha wadau wake

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, kushoto, akitembelea katika ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services katika futuru iliyoandaliwa na taasisi hiyo. Pichani ni wadau wengine walioalikwa katika futari hiyo.

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imefuturisha wadau wake wanaoendelea na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huku ikiwataka kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Bayport Financial Services, Evelyine Hall, katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wake mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Viongozi wa Taasisi ya Bayport Financial Services na wageni waalikwa wakijadiliana jambo katika futari ya Bayport iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mwenye koti jeusi na kofia ni Haruna Mbeyu, akifurahia jambo.


Akizungumza katika futari hiyo, Evelyine alisema ni vyema Watanzania wote, hususan Waislamu kuutumia vyema mwezi huo, ikiwa ni nguzo muhimu katika Dini ya Uislamu Tanzania na duniani kwa ujumla. Alisema Bayport inaheshimu misingi ya dini zote, hivyo kwakuwa mwezi wa Ramadhan ni sehemu ya ibada kwa Waislamu, vyema wakautumia vizuri, sanjari na kulinda Amani, upendo, umoja, mshikamano, bila kusahau jamii kuishi kwa kuheshimiana ili nchi yetu iweze kupiga hatua. 
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza wa tatu kutoka kulia, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, mara baada ya kumaliza kufuturu katika futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, huku ikiandaliwa na Bayport.
Wakati wanatembelea katika ofisi ya taasisi hiyo baada ya kumaliza kupata futuru, jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega, mwenye kanzu akizungumza jambo katika futuru iliyoandaliwa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, iliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa DC ni Meneja Utawala wa Bayport, Evelyine Hall na anayemuhoji DC ni Mwandishi wa Habari, Phillip Daudi, aliyeshika kipaza sauti. Picha na Mpiga Picha Wetu.

“Bayport Financial Services inajivunia kutoa huduma kwa Watanzania wote, ambao leo baadhi yao wapo katika ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, hivyo tunaamini mwezi huu utakuwa na tija, endapo utatumiwa vyema,” alisema Evelyine. 


Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kuwa Watanzania wamekuwa wakiishi kwa kuheshimiana, hivyo wanaamini wataendelea kutoa huduma bora ya mikopo ya fedha, mikopo ya viwanja, mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile injini ya boti, vifaa vya ujenzi, ambapo huduma zote hizo zinapatikana kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz na kupitia mawakala na ofisi zao zilizoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara.

Mkuu wa Wilaya Kilwa, DC Abdallah Ulega kulia, akipiga picha na Meneja Utawala wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Evelyine Hall na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto. DC alikuwa miongoni mwa wadau walioalikwa katika tukio la futari lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mambo ya mikopo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega, aliipongeza Bayport kwa kitendo chao cha kiungwana cha kuamua kuandaa futari hiyo kwa wadau wao. “Sisi serikali tutaendelea kuwaunga mkono wadau mbalimbali wenye kuamua kuanzisha mambo mazuri kama haya, hivyo tunawapongeza kwa dhati juu ya jambo hili muhimu linalojenga kuheshimiana kwa namna moja ama nyingine,” alisema Ulega.


Bayport Financial Services ni miongoni mwa taasisi za kifedha zinazojihusisha na mambo ya mikopo, ikiwa na mchango mkubwa kwa Watanzania wote wanaoamua kukopa ili kujikwamua kiuchumi, ambapo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa wamekuwa wakinufaika kwa kiasi kikubwa tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa nchini. 

KAMPENI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR LEO.

0
0

UTT-PID YASHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA NDANI YA BANDA LA WIZARA YA FEDHA

0
0
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akiwasikiliza wateja waliotembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kushoto) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) wakiwa na nyuso za furaha na Bi. Beatrice Ngoda katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
 Afisa Masoko Bi. Mary Minja (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akimsikiliza mteja aliyetembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) ipo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yananoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Banda la UTT PID lipo jirani na kuingia katika Banda la Wizara ya Fedha upande wa kulia… karibuni sana wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi mjipatie huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo vile vya mradi wa katika Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT–PID) miji ya Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani.

Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.

Aidha Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi hiyo hapa nchini. Kwa sasa UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri katika utoaji huduma za ushauri katika maeneo ya upembuaji yakinifu wa miradi mbali mbali, uratibu wa fedha na huduma zinazohusian katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi y a zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.

DTB YAFUTARISHA WATEJA WAO ZENJI

0
0
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmeid Mazrui akizungumza wakati wa hafla ya futari ilioandaliwa na Benki ya Diamond Trust Tawi la Zanzibar kwa ajili ya Wateja wake iliofanyika hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa DTB Tanzania Ndg Sylevester Bahati akitowa maelezo ya hafla hiyo ya futari katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar. kwa ajili ya Wateja wa DTB Zanzibar hii ikiwa ni mara ya 6 kwa Benki hiyo kujumuika na Wateja wao katika futari maalumu.
Meneja wa Diamond Trust Benk Tawi la Zanzibar Ndg Othman Juhudi akizungumza na Wateja wa DTB na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya futari maalum walioandaliwa wateja wao katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Diamond Trust Mahboob Shamsi akitowa maelezo ya huduma za Benki yao kwa Watajea wao waliohudhuria hafla maalum ya futari waliowaandalia katika viwanja vya Hoteli ya Serena Shangani Zanzibar. 
Mkuu wa Idara ya Masoko wa DTB Tanzania Ndg Sylevester Bahati akitowa maelezo ya hafla hiyo ya futari katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar. kwa ajili ya Wateja wa DTB Zanzibar hii ikiwa ni mara ya 6 kwa Benki hiyo kujumuika na Wateja wao katika futari maalumu.
Mgeni rasmin na viongozi wengini na wananchi wakipata futari maalumu ilioandaliwa na DTB Tawi la Zanzibar kwa wateja wao kujumuika pamoja iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya serena shangani Zanzibar.
Meneja wa Tawi la Benki ya DTB Ndg Othman Juhudi na Mwenyekiti wa Bodi ya DTB Mahboob Shamsi. 






Wananchi waliohudhuria hafla ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wateja wao wa Zanzibar wakimskiliza Mgeni Rasmin Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui akizungumza wakati wa hafla hiyo ya futari iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Wananchi waliohudhuria hafla ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wateja wao wa Zanzibar wakimskiliza Mgeni Rasmin Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui akizungumza wakati wa hafla hiyo ya futari iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Wananchi waliohudhuria hafla ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wateja wao wa Zanzibar wakimskiliza Mgeni Rasmin Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui akizungumza wakati wa hafla hiyo ya futari iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Wananchi waliohudhuria hafla ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wateja wao wa Zanzibar wakimskiliza Mgeni Rasmin Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui akizungumza wakati wa hafla hiyo ya futari iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Kadhi wa Wilaya ya Magharibi Othman Ame Chum, akisoma dua baada ya kumalizika hafla ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wataje wake Tawi la Zanzibar iliofanyika katika hoteli ya serena Zanzibar. 
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Diamond Trust, Mahboob Shamsi wakijumuika na Wateja wa DTB wakiitikia dua ikisomwa na Kadhi wa Wilaya ya Magharibi Unguja Unguja Shekh. Othman Ame Chum.
Wananchi waliohudhuria hafla maalum ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wateja wake Zanzibar wakiitikia dua baada ya hafla hiyo
Wananchi waliohudhuria hafla maalum ya futari ilioandaliwa na DTB kwa Wateja wake Zanzibar wakiitikia dua baada ya hafla hiyo
Meneja wa DTB Tawi la Zanzibar akiwa na Mashekh wa Ofisi ya Kadhi Zanzibar baada ya hafla hiyo ya futari iliofanyika hoteli ya Serena Shangani Zanzibar. 
Meneja wa DTB Tawi la Zanzibar Othman Juhudi akiagana na Kadhi wa Wilaya ya Magharibi Unguja Shekh. Othma Ame Chum, baada ya kumalizika kwa huduma ya futari ilioandaliwa na Benki hiyo Zanzibar.
Wafanyakazi wa Benk ya DTB Tawa la Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kupata futari ilioandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya Wateja wake wa Zanzibar katika hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images